SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 2: EPISODE 8
Katika makazi ya
Ammar Nazari sherehe
kubwa ilikuwa
inaendelea.wafuasi wake
walikuwa wakicheza ngoma
na kufurahi.Msafara wa
magari uliwasili na furaha
ikazidi.Ammar akashushwa
garini na kuingizwa ndani
akasalimiana na mke wake
na watoto.
“Abu kutanana familia
yangu.Nina watoto tisa na
wake wawili” akasema
Ammar na kumtambulisha
Mathew kwa wake zake na
watoto.
“Huyu anaitwa Abu Al
zalawi ni mwenzetu katika
mapambano dhidi ya Israel
na ndiye aliyefanikisha mimi
kuwepo hapa leo.Ni mtu
muhimu sana kwangu na
nina deni kubwa kwake”
akasema Ammar na
kuelekezwa Mathew apewe
chumba maalum katika
makazi yake na ahudumiwe
kwa kila kitu.Mke mdogo wa
Ammar akamchukua
Mathew na kumpeleka
katika chumba cha wageni
muhimu katika jumbe lile la
Ammar
“Karibu jisikie
nyumbani.Naitwa Nawal.Ni
mke mdogo wa Ammar”
akasema Nawal na kumtaka
Mathew akaoge.
“Mathew Mulumbi
karibu katika ulimwengu wa
magaidi.Mpaka hapa
naamini Ammar ameniamini
vya kutosha kwani
nimefanikiwa leo hii
amewasili nyumbani
kwake.Uhakika wa kumpata
Habiba Jawad ni mkubwa
sana” akawaza Mathew
akiwa bafuni akajitazama
katika kioo
“Ninatisha.I look like
hell.Hata Peniela
akinitazama leo anaweza
akanipotea.Tazama mwili
wangu ulivyokuwa na
makovu na vidonda kila
mahali.Sijawahi pitia kipindi
kigumu katika maisha yangu
na katika kazi yangu ya
ujasusi hadi sasa.Nimeteseka
mno na kama nikifanikiwa
kutoka salama katika sakata
hili sintajishughulisha tena
na mambo haya.It’s
over.Nataka nitulie na
familia yangu” Mathew
alipokumbuka familia yake
akajikuta akipandwa na
hasira za ghafla.
“Peniela anaamni tayari
nimekwisha fariki na
ameamua kuendelea na
maisha yake akaanzisha
mahusiano na na Yule mtu
wa Mossad.Inaniuma sana
kwa mke wangu
ninayempenda kuchezewa
kiasi hiki.Mossad
wanamtumia kwa ajili ya
kunitaka nifanye
wakitakacho.Siwezi
kumlaumu sana kwani haya
yote nimeyataka mimi
mwenyewe.Lakini naapa
kama nikifanikiwa kutoka
salama na kumkuta Yule
jamaa anaendelea na
mahusiano na Peniela
nitamnyonga kwa mikono
yangu nimalize hasira zangu
zote nilizonazo” akawaza
Mathew na kuoga maji
alipotoka akakuta kuna nguo
zimewekwa kitandani
akavaa halafu akakaa
kitandani
“Najaribu kuwaza ni vipi
kama wakigundua mimi
nimetumwa na
Mossad?Hakutakuwa na
kingine zaidi ya
kuuawa.Natakiwa kuwa
makini sana kuhakikisha
sifanyi kosa hata dogo kwani
kosa dogo sana linaweza
kuniletea matatizo
makubwa”
Mlango ukagongwa
akaenda kuufungua
akakutana na Nawal
akamkaribisha seheu ya
chakula ambako alikuwepo
Ammar na watu wengine
watano waliokuwa na ndevu
nyingi.Wale jamaa
walimuangalia Mathew kwa
makini sana akawasalimu
halafu akaketi katika mkeka
pamoja nao.Ammar
akamtambulisha Mathew
kwa wale jamaa ambao ni
viongozi wa juu wa kundi la
Ammar Nazari Brigades
“Ndugu zangu viongozi
wenzangu huyu anaitwa Abu
Al Zalawi ni raia wa Kenya
lakini mwenye asili ya
Misri.Amekuwa akiendesha
mapambano dhidi ya
waisrael nchini Kenya na
amefanikiwa kumuua mkuu
wa Mossad Afrika mashariki
aliitwa ..” akasema Ammar
na kumtazama Mathew
“Aliitwa Avi Abramson”
akasema Mathew.
“Vile vile aliua watu
wengine wawili wa Mossad
hadi alipokamatwa na
kuletwa katika gereza
nililokuwa nimefungwa.Kwa
bahati nzuri mimi nay eye
tulielewana na kuwa
marafiki na yeye ndiye
aliyefanikisha mimi kuwepo
hapa muda huu.Yeye ndiye
aliyenisaidia hadi
kunifikisha hapa.Nilipigwa
risasi na kushindwa
kutembea angeweza
kuniacha na kuendelea
kutoroka lakini hakuniacha
alinibeba na kuhakikisha
tunatoka wote
gerezani.Ndugu zangu huyu
ni mgeni muhimu sana
kwetu na tuna deni kubwa
kwake.Baada ya kutoka
gerezani hatarejea tena chini
kwake kwani tayari taarifa
za kutoroka kwake zitakuwa
zimesambaa hivyo atabaki
hapa ataungana na sisi
katika mapambano” akasema
Ammar na watu wale
wakamkaribisha Mathew
kwa furaha.Baada ya kupata
chakula Ammar akaelekeza
Mathew apelekwe
akapumzike
Baada ya Mathew
kuondoka Ammar akawa na
kikao kizito na wasaidizi
wake wakampa kwa
muhtasari yale yote
yaliyofanyika wakati akiwa
gerezani akawapongeza kwa
kuendeleza mapambano hata
wakati akiwa
amefungwa.Baada ya
maongezi marefu
yaliyochukua saa tatu Habib
msaidizi mkuu wa Ammar
akasema
“Ammar sote
tunashukuru sana kwamba
umerejea salama kutoka
gerezani.Lakini kuna kitu
kinanipa wasiwasi sana”
“Nini kinakupa wasi
wasi?
“Huyu jamaa uliyekuja
naye.Una uhakika gani kweli
ni mpiganaji?Hudhani
kwamba anaweza kuwa ni
pandikizi la waisrael
wakitaka kutuchuguza na
kupata taarifa zetu?akauliza
Habib
“Msiwe na wasi wasi
ndugu zangu.Abu Zalawi ni
mtu mzuri na si
pandikizi.Haikuwa rahisi
kwangu kumuamini lakini
baada ya kumchunguza
nikamuamini ni
mwenzetu.Ameteswa kwa
miaka mitatu na hata
mngebahatika kumona
mgongo wake wote umejaa
vidonda.Msiwe na shaka
naye hata kidogo” akasema
Ammar
“Ammar wewe ni
kiongozi wetu na hata siku
oja hatuwezi kukupinga kwa
kila ukisemacho lakini
binafsi bado nina mashaka
na huyu mtu.Kama
mtakubaliana name kabla ya
kumuingiza katika jeshi letu
tumchunguze na kumjua ni
nani na tumpime kwa kumpa
jaribio kama kweli anaweza
kuwa ni muaminifu kwetu”
akasema Habib na ukimya
ukatawala mle chumba
baada ya muda Ammar
akauliza
“Kwa nini mnakuwa na
wasi wasi kuhu huu
mtu?Kwa mambo
aliyonifabnyia hatustahili
hata kumchunguza kwani ni
mtu safi na hana tatizo.Huyu
ni mwenzetu anastahili
heshima kubwa” akasema
Ammar akionekana
kukereka na maneno yale ya
Habib
“Ammar utanisamehe
kama maneno yale
yalionyesha utovu wa
nidhamu lakini ni kanuni ya
jeshi letu kabla ya
kumuingiza mtu yeyote
lazima kwanza tumchunguze
na tujiridhishe kama kweli ni
mtu safi na anaweza
akatufaa.Hata huyu pia
lazima tumchunguze tumjue
ni nani na katokea
wapi.Naomba unipe ruhusa
nimchunguze huu mtu na
kama nikikuta kuna chembe
ya kasoro basi nitakupa
taarifa”
“Sawa hakuna tatizo
fanya hivyo” akasema ammar
na kikao kikaishia hapo
kwani hakuonyesha
kufurahishwa na kitendo kile
cha kutaka kumchunguza
Mathew
Habib hakutaka kusubiri
hadi asubuhi akawachukua
vijana wawili wakiwa na
kifaa Fulani wakaenda
katika chumba cha Mathew
wakagonga akaamka na
kufungua mlango wakaingia
ndani.
“Abu Zalawi
unajisikiaje?akauliza Habib
“Ninajisikia maumivu
mwili mzima” akasema
Mathew
“Pole sana.Mimi naitwa
Habib ni kamanda mkuu wa
vikosi vyote vya Ammar
Nazari Brigades.Ammar
amenipa maelekezo ya
kukujumuisha katika jeshi
letu hivyo basi kabla ya
kukuingiza rasmi jeshini
kuna mchakato ambao
lazima uupitie” akasema
Habib na kuwapa ishara
wale vijana aliokuwa nao
wafaye ukaguzi.Kifaa kile
walichokuwa nacho
kikawashwa na kuanza
kupitishwa katika mwili wa
Mathew lakini hawakukuta
kuna kitu chochote ambacho
Mathew alikuwa
amepandikizwa mwilini ili
kuwajulisha Mossad mahala
alipo.Habib akaagiza
warudie tena lakini
hakukuwa na kitu
chochote.Akaelekeza nguo
zote alizokuja nazo Mathew
zichunguzwe lakini
hakukuwa na kifaa chochote
“Uko safi sasa tunaomba
tuongozane”akasema Habib
na Mathew akainuka
akaongozana na wale jamaa
“Nilijua mambo kama
haya yanaweza kutokea
ndiyo maana nilikataa
kufungwa kifaa chochote cha
kuwajulisha Mossad mahala
nilipo.Kama ningekuwa na
kifaa kile hivi sasa
yangekuwa ni mambo
mengine.” Akawaza Mathew
Waliingia katika chumba
kimoja kikubwa chenye
mitambona vifaa vingi vya
mawasilano
“Watu hawa
wameendelea sana.Ofisi hii
ni kubwa utadhani ofisiya
Mossad” akawaza Mathew na
kuingizwa katika chumba
kidogo chenye meza na viti
viwili.Akakaa mle na baada
ya muda akaingia kijana
mmoja aliyevaa kanzu ya
rangi ya kijivu.Alikuwa
amevaa miwani na hakuwa
na ndevu nyingi kama
wenzake.Mkononi alikuwa
na faili akaliweka mezani.
Habib na wenzake
walikuwa wanafuatilia
mahojiano yale ya Mathew
na Yule kijana kupitia
runinga kubwa katika
chumba kingine
“Naitwa
Mustapha.Nimekuja hapa
nataka kuchukua taarifa
zako hivyo naomba unipe
taarifa za kweli ili tuweze
kukufahamu na kukuingiza
katika mfumo wetu”akasema
Mustapha.
“Nafurahi kukufahamu
Mustapha.Natumai
tutafanya kazi
pamoja”akajibu Mathew
huku akitabasamu
“Nataka kufahamu jina
lako nani?akauliza Mustapha
“Naitwa Abu Al Zalawi”
“Unaweza ukatupa
historia yako kwa ufupi
umetokea wapi hadi ukafika
hapa?akauliza Mustapha
“Kama nilivyosema
naitwa Abu Al zalawi,raia wa
Kenya mwenye asili ya
Misri.Baba yangu aliitwa
Khalid Al Zalawi.Alikuwa ni
mmoja wa viongozi wa kundi
la Abu Hafs al-Masri
Brigades.Baba yangu Khalid
aliuawa na majeshi ya Israel
na hapo ndipo nilipoapa
kuendeleza mapambano na
Israel.Mama yangu alitokea
Kenya hivyo haikuwa kazi
kwangu kupata uraia wa
Kenya.Nikiwa Kenya
nilimuua Avi Abramson
mkuu wa Mossad Afrika
Mashariki pamoja na
majasusi wengine wawili
ndipo nilipoanza kutafutwa
na serikali ya Israel”
Wakati Mathew
akimuelezea Mustapha
historia yake katika chumba
kile walichokuwemo akina
Habib vijana walikuwa na
kasi ya aina yake na mara tu
alipotaja jina lake
wakalitafuta na sura na
picha yake vikaonekana
Runingani.Abu Zalawi
alikuwa ni mmoja wa watu
waliokuwa wanatafutwa
sana na serikali ya Israel.
“Anachokisema ndicho
kilichoandikwa na Israel”
akawaza Habib
Mathew aliulizwa
maswali mengi kuhusu
maisha yake na hadi namna
walivyofanikisha kutoroka.
“Majibu yake
yanaridhisha kabisa na
yanashawishi kumuamini
lakini bado nafsi yangu
inakuwa nzito kumuamini
moja kwa moja.lazima nimpe
mtihani kesho” akawaza
Habib na kumrejesha
Mathew chumbani kwake.
“Nashukuru Mossad
wameweza kufanya kama
walivyoelekeza.Taarifa zote
nilizowapa ziko mtandaoni
na wameridhika mimi ni Abu
Zalawi lakini huyujamaa
Habib bado haonyeshi
kunikubali.Amesema
tutaonana asubuhi.Sijui
anataka afanye nini tena”
akawaza Mathew na kujilaza
kitandani alikuwa amechoka
sana
Saa kumi na mbili za
asubuhi mlango wa chumba
alimolala Mathew
ukagongwa akaingia Habib.
“Abu kumekucha kazi
inaanza.Sisi hatuna muda
wa kupumzika” akasema
Habib na Mathew bila hata
kunawa uso akatoka
wakaingia katika gari na
kuondoka.Ulikuwa ni
mwendo mrefu hadi ilipofika
saa nne za asubuhi
wakasimamisha gari sehemu
na Habib akasema
“Abu wewe ni mtu
shujaa.Tunakushukuru sana
kwa kumuokoa mkuu wetu
na kuamua kuungana nasi
katika mapambano dhidi ya
waisrael.Jana ulinieleza
hasira ulizo nazo kuhusu
Israel na uliapa kulipiza
kisasi kwa kitendo cha
kumuua baba yako.Kilometa
chache kutoka hapa kuna
soko kubwa la samaki na
watu wengi kutoka upande
wa Israel huja kununua
samaki.Ulinieleza kwamba
umeteswa kwa miaka zaidi
ya mitatu gerezani.Ni wakati
wa kulipa
kisasi.Tunakwenda kuondoa
maisha ya waisrael” akasema
Habib na kufungua sanduku
lililokuwa nyuma
likaonekana bomu kubwa.
“Jesus Christ ! akawaza
Mathew baada ya kuliona
bomu lile.
“Abuu nadhani mpaka
hapa umekwisha fahamu
ninachokimaanisha”
“Nimekuelewa Habib”
akasema Mathew huku
akijitahidi kutokuonyesha
woga wowote.
Walikwenda hadi katika
soko kubwa la
samaki.Magari kadhaa
yalikuwa yamejipanga
yakiuza samaki wabichi.Gari
walilopanda akina Mathew
likapenya na kuingia kati
kati ya magari yale ya kuuza
samaki.
“Abu tumefika.Muda
utakapowadia utabonyeza
kitufe hiki bomu litalipuka
na damu ya waisrael
itamwagika.Wewe ni
mpambanaji nadhani
unafahamu thamani ya hiki
unachokwenda kukifanya”
“Ninafahamu Habib”
akasema Mathew.Habib
akamfanyia dua halafu
akabonyeza saa iliyokuwa
mbele halafu akashuka
akafungua mlango.
“Mathew dunia
itakukumbuka kwa ushujaa
huu wa leo na sote
tutakutana ahera” akasema
Habib na kushuka garini
akamuacha Mathew
“Nimenusurika mara
nyingi kupoteza maisha hadi
watu wananiambia nina
maisha marefu kama paka
lakini leo hii nadhani maisha
yangu yamefika
ukingoni.Hakuna namna
nitakavyoweza kupona.Bomu
litalipuka na kuua watu
wengi na mimi
nikiwemo.Najuta
kilichonileta huku.Bora
ningebaki gerezani Israel
kuliko kuja kufa kigaidi
huku nikiua watu wengine
wasio na hatia” akawaza
Mathew huku uso wake
ukiwa umeloa jasho
akitazama sekunde
zinavyozidi kukimbia kwa
kasi
“Mathew Mulumbi leo
ninakufa kifo cha kijinga
sana.Ile sifa yangu yote ya
mtu shujaa lakini leo
inafutika na kufa kama
gaidi.Nadhani muda huu
uliobaki wa dakika mbili
niutumie kwa maombi”
akawaza Mathew na
kufumba macho
“Ee Mungu ni wewe
pekee mwenye kuona hadi
ndani ya mioyo yetu na kujua
dhamira zetu nadhani
unanitazama hivi sasa
dhamira yangu si kuua watu
wako wasio na
hatia.Nimefika hapa
kutokana na mapenzi
makubwa niliyo nayo kwa
nchi yangu na lengo langu ni
kuhakikisha ninapambana
na magaidi hawa wasio na
huruma hata chembe lakini
nimejikuta mikononi mwao
na wananilazimisha kujiua
na mimi kuua
wengine.Nimekukosea
mambo mengi ee Mungu
wangu naomba unisameheme
yale yote niliyokukosea
makubwa na madogo.Mungu
wangu,Musa aliwaondoa
waisrael utumwani Misri
lakini hakuweza kufika nchi
ya ahadi,ninaomba baada
yangu umuinue mtu
mwingine aweze kuiendeleza
hapa nilipofika na
kuutokomeza kabisa
ugaidiNinakufa nikiwa na
mapenzi makubwa na nchi
yangu Tanzania na ndilo
neno langu la mwisho
kulitamka.Nakupenda
Tanzania” akafumbua macho
na kutazama saa zilibaki
sekunde tano.
“It’s time” akawaza na
kutazama nje halafu
akatazama saa sekunde
zilibadilika tatu ,mbili moja
“Allahu akbar ! akasema
Mathew na kubonyeza kitufe
alichoelekezwa
MPENZI MSOMAJI
USIACHE KUFUATILIA
SIMULIZI HIIKATIKA
SEHEMU IJAYO……..