Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 8
EPISODE 9
Saa kumi na moja na
dakika ishirini na nane
mkurugenzi wa Mossad
ukanda wa Afrika Mashariki
Avi Abramson akawasili
Sadena hotel.Ndani ya gari
alikuwa na dereva pamoja na
mlinzi wake mmoja ambao
aliwataka wabaki garini yeye
akashuka na kuelekea ndani
ya hoteli akapanda lifti hadi
ghorofa ya tano akakitafuta
chumba 204 akagonga kama
alivyoelekezwa.Mlango
ukafunguliwa na Devotha
aliyekuwa amevaa gauni
jepesi ambalo liliweza
kuyaonyesha hadi mavaziya
ndani.Kwa sekunde kadhaa
Avi alibaki amesimama
mlangoni akimshangaa
Devotha.Hakuwa ametarajia
kumkuta akiwa katika hali
ile
“Avi karibu ndani ”
akasema Devotha
“Devotha..” akasema Avi
akionekana kuendelea
kumshangaa
“Samahani nilikuwa
ninajiandaa kwenda kuoga
sikutegemea kama ungeweza
kuja mida hii.Umewahi
sana”
“Tulikubaliana tukutane
saa kumi na moja jioni na
nilipotoka kazini nimekuja
moja kwa moja hapa”
akasema Avi
“Karibu naomba
unisubiri nikaoge
kwanza.Utatumia kinywaji
gani? Akauliza Devotha huku
akilitikisa umbo lake na
kuzidi kumpagawisha Avi
“Kitu chochote
ulichonacho humu ndani
nitatumia malaika wangu”
akasema Avi Devotha
akaenda katika kabati
akachukua chupa ya mvinyo
akaiweka mezani na
kumuwekea David katika
glasi.
“Devotha U mrembo
sana” akasema Avi akiwa na
tabasamu pana sana.Devotha
naye akatabasamu
“Devotha hakuna ubaya
wowote tukiendelea
kuzungumza ukiwa katika
mavazi hayo.Ninafurahi sana
kuliona umbo lako
zuri.Mungu amekujalia uzuri
wa kipekee
kabisa.Ninamshukuru na
kumsifu kwa uumbaji huu
uliotukuka” akasema Avi
akiwa katika tabasamu pana
sana
“Ouh Avi” akasema
Devotha akiilegeza sauti
yake na kuwa laini sana
“Kweli kabisa
Devotha.Uzuri wako si wa
kawaida” akasema Avi na
Devotha akabaki amesimama
akitabasamu
“Ahsante sana
Avi.Nisubiri dakika mbili
nikaoge” akasema Devotha
na kuanza kupiga hatua
kuelekea katika mlango wa
chumba cha kulala na mara
tu alipokishika kitasa
akageuka na kumtazama Avi
ambaye bado alikuwa
anamtazama kwa uchu.
“Ungependa kuoga nami
Avi?akauliza huku kidole
kimoja akiwa amekiweka
mdomoni.Avi akatabasamu
na kubabaika
“Ninakutania Avi”
akasema Devotha akitoa
kicheko kidogo
“Hakuna tatizo
Devotha.Kuna mtu yeyote
unayemtegemea hapa kuja
mida hii?akauliza Avi
“Hakuna
ninayemtegemea.Hapa
Nairobi nimekuja kuonana
nawe pekee sina miadi na
mtu mwingine” akasema
Devotha na Avi akasimama
akavua koti
“Basi hakuna tatizo
nitajumuika nawe.Hakuna
mwanaume anayeweza
kukataa ombi la kuoga na
malaika kama wewe”
akasema Avi huku akivua
shati haraka haraka na
kulitupa katika sofa
akaufungua mkanda wa
suruali lakini akasita halafu
akapiga hatua kuelekea
mlangoni akaufunga mlango
kwa funguo halafu akavua
suruali na kubakiwa na nguo
ya ndani
“Niko tayari malaika
wangu” akasema Avi na
kumfuata Devotha
bafuni.Devotha akafungua
mkanda wa ile nguo laini
aliyokuwa ameivaa akaiachia
ikaanguka chini akabaki
amevaa mavazi ya
ndani.Kitendo kile kilileta
vurugu ikulu kwa Avi
ambako kulichachamaa na
kufura kwa hasira.Devotha
huku akitabasamu akamtaka
Avi amsaidie kuifungua
sidiria yake kwa
nyuma.Wakati Avi
akimfungua akayagusisha
makalio yake kwa makusudi
ikulu kwa Avi.
“Kwisha habari
yake.Nikiwaambia viumbe
hawa ni wadhaifu
wanakasirika lakini huo ndio
ukweli angalia macho
yanavyomtoka Avi mwili
wote unamchemka kama
ningekuwa na nia ya
kumuua ningemtoa roho
yake sasa hivi” akawaza
Devotha halafu akamshika
mkono Avi wakaingia bafuni
wakakaa katika beseni
kubwa la kuogea.
“Tunahitaji mvinyo”
akasema Devotha akitaka
kuinuka
“Usiinuke Devotha
nielekeze nikachukue”
akasema Avi na kutoka
ndani ya maji akaenda
kuchukua chupa ya mvinyo
wakaendelea kuoga huku
wakipata mvinyo.Mkono wa
kulia wa Devotha ulikuwa
ukiisugua sugua ikulu ya Avi
ambaye alifumba macho kwa
raha alizohisi.Mara
akakumbuka kitu
“Devotha karibu sana
Nairobi.Nimefurahi kukuona
japo ujio wako umekuwa wa
ghafla sana”
“Hata mimi sikuwa
nimetarajia kama ningekuja
Nairobi lakini imenilazimu
kuja kwa dharura”
“Nini hasa sababu ya
kuja Nairobi?Kuna tatizo
gani?
“Usihofu Avi nitakueleza
kila kitu lakini kwanza tu…”
akasema Devotha huku
akiinuka na Avi akajua
alichokitaka
Devotha.Hakumpa nafasi na
kumaliza sentensi yake
akamkamata sawa sawa na
mtanange ukaanza bafuni.
Tino na Gosu Gosu
walikuwa wakishuhudia kila
kinachoendelea katika
chumba cha Devotha kupitia
kamera wakiwa chumbani
kwao.Akina Mathew Dar es
salaam nao pia walikuwa
wanashuhudia pia
kinachoendelea Nairobi
“Ni muda wa kuingia
kuichukua kadi” akaelekeza
Mathew baada ya kuona
Devotha na Avi wakiwa
wamezama mapenzini.Tino
akatoka ndani ya chumba
chao akatazama pande zote
kulikuwa kimya akaenda
katika mlango akaingiza vitu
Fulani katika kitasa akaanza
kukichokonoa na ndani ya
muda mfupi akafanikiwa
kufungua kitasa
akakinyonga na taratibu
akaingia ndani.Moja kwa
moja akaenda katika mavazi
ya Avi yaliyokuwa sofani
akalichukua koti akaanza
kulipekua na katika mfuko
wa ndani wa koti akaikuta
kadi waliyokuwa
wanaitafuta.
“Hiyo ndiyo kadi
tunayoitafuta” akasema
Ruby ambaye naye alikuwa
akishuhudia kila kitu akiwa
na Mathew Dar es
salaam.Taratibu Tino
akatoka ndani ya kile
chumba cha Devotha
akarejea katika chumba chao
“Good job Tino” akasema
Mathew
Katika kamera bado
mtanange ulikuwa
unaendelea bafuni.Devotha
aliendelea kumpeleka Avi
vilivyo.
Baada ya kuipata ile kadi
kazi ikaanza na usukani
akaushika Ruby akiwa Dar
es salaam.Tino akaanza
kufuata maelekezo aliyopewa
na Ruby akaingiza kadi ile
katika kifaa Fulani
kilichounganishwa na
kompyuta ambacho
kilimuwezesha Ruby kuweza
kupata taarifa alizozihitaji
kutoka katika ile kadi.Baada
ya dakika saba akamtaka
Tino aitoe kadi ile.
“Guys kazi yetu
tumeimaliza nimepata
taarifa zote ninazozihitaji
katika hiyo kadi sasa
mnaweza kuirejesha”
akasema Ruby.Tino
akichukua kadi ile na
kuirejesha katika chumba
cha Devotha,baada ya kutoka
akagonga mlango mara mbili
kama alivyokuwa
ameelekeza Devotha halafu
akaelekea chumbani
kwake.Akiwa bafuni Devotha
alisikia mlango ukigongwa
kama alivyokuwa
ameelekeza mara moja
akajua kazi imekwisha
“Avi
imetosha.Tutaendelea
baadae kama ukitaka”
akasema Devotha
“Devotha mbona
unaniacha kati
kati?Tuendelee malaika
wangu” akasema Avi huku
akitweta
“Usijali Avi tutaendelea
hata baadae lakini kwanza
nataka tuzungumze kile
kilichonileta hapa Nairobi”
akasema Devotha na kutoka
ndani ya lile beseni la kuogea
akajifuta maji.Avi alibaki
anashangaa lakini Devotha
akamtaka atoke ndani ya
maji
“Sawa Devotha
tuzungumze kile
kilichokuleta Kenya.Kuna
tatizo gani? Kwa nini
umetaka kuniona?akauliza
Avi huku akivaa mavazi yake
“Avi usiku wa jana
nilikutana na watu wako
wawili uliowatuma Tanzania
Fishel na Ehud.Walinieleza
kile kilichowaleta Tanzania
kwamba ni kuandaa
operesheni ya kumtafuta
Olivia ambaye ametekwa na
watu wasiojulikana na
mpaka sasa bado vyombo
vyote vinaendelea kumsaka
ikiwemo na idara yangu
lakini bado hatujampata.Ili
niweze kuwasaidia kuandaa
operesheni yao nilitaka
kwanza kufahamu sababu ya
Mossad kumtafuta
Olivia.Fishel na Ehud
walilazimika kunieleza
sababu ya kumtafuta
Olivia.Walinipa siri kubwa
ambayo sikuwa nikiifahamu
kuwa Edger Kaka ambaye
aliwahi kuwa mbunge wa
bunge la jamhuri ya
muungano wa Tanzani
ambaye sisi sote tunaamini
alifariki dunia katika
ajali,yuko hai” akasema
Devotha na sura ya Avi
ikaonyesha mshangao
mkubwa
“Najua hili ni suala la
siri kubwa lakini mimi kama
mtu wenu ambaye
mnanitumia katika masuala
yenu mbali mbali sikupaswa
kuwekwa gizani hadi
ninakuja kufahamu hivi
sasa”akasema Devotha
“Devotha hukupaswa
kufahamu jambo hili na hata
hao waliokueleza wamefanya
makosa makubwa mno
kukupa taarifa hizi za siri”
akasema Avi
“Avi tayari nimekwisha
fahamu siri hii na
usiwalaumu sana watu wako
kwani hawakuwa na namna
nyingine zaidi ya kunieleza
ukweli ili niwasaidie nami
nitawasaidia kumpata Olivia
na ndiyo maana nimekuja
hapa.Kikubwa kilichonileta
kwako ninataka kuonana na
Edger Kaka.Nataka
nizungumze naye” akasema
Devotha
“Hilo haliwezekani
Devotha.Edger yuko mahala
pa siri na wanaoruhusiwa
kuonana naye ni watu
wachache tena maalum
tu.Wewe hauko katika kundi
hilo la watu wanaoweza
kuonana na Edger
Kaka”akasema Avi
“Avi nafahamu Edger
anazo taarifa nyeti sana
mnazozitafuta na ili awape
taarifa hizo lazima mumpate
Olivia.Ili kumpata Olivia
lazima nifanye mahojiano na
Edger Kaka yeye anafahamu
mahala alipo
Olivia,anafahamu
waliomteka”
“Olivia ametekwa na
IS?akauliza Avi
“Tunahisi hivyo ndiyo
maana ninataka kuhojiana
naye.Edger anampenda
Olivia na lazima atanipa
ushirikiano wa kujua mahala
alipo.Avi naomba unipe
dakika tano tu nizungumze
na Edger na ninakuahidi
Olivia atapatikana” akasema
Devotha na Avi akazama
mawazoni huku akiendelea
kumtazama Devotha
“Avi nisingeweza kuja
hapa kama sina uhakika wa
hiki
ninachokuomba.Tafadhali
naomba unipe dakika tano tu
za kuzungumza na Edger
Kaka na ninakuhakikishia
zitakuwa na msaada
mkubwa sana” akasema
Devotha lakini Avi
alionekana kuwa na wasi
wasi na kumuangalia
Devotha kwa macho makali.
“Huyu jamaa tayari
ameonyesha wasiwasi.Kuna
kitu amekihisi kuhusu
Devotha.Guys we need to get
in there fast.Tukichelewa
Devotha atakuwa katika
hatari kubwa! akasema Gosu
Gosu
“Wait ! akasema Mathew
“Mathew Devotha yuko
katika hatar…”
“Ninasema subiri Gosu
Gosu.She knows what she’s
doing” akasema Mathew
“Devotha nataka
uniambie ukweli nani
aliyekupa taarifa za Edger
Kaka?akauliza Avi
“Nimekwambia Avi
taarifa hizo nimezipata
kutoka kwa watu
uliowatuma kwangu
niwasaidie kumpata Olivia
Fishel na Ehud”akajibu
Devotha
“Hapana si kweli.Fishel
na Ehud ni majasusi
wakubwa sana na
wanafahamu umuhimu wa
siri hii ambayo hata watu
wengi ndani ya Mossad
hawaifahamu na majasusi
wetu wamekula kiapo cha
kutokutoa siri zozote.Nataka
uniambie ukweli aliyekupa
taarifa hizi” akasema Avi
Devotha akawa kimya
akimtazama
“Nijibu Devotha,nani
amekupa siri hii? Akauliza
Avi
“Avi najua unawaamini
sana watu wako lakini ni
mimi ndiye niliyewafanya
hadi wakavunja kiapo chao
na kunipa siri hii kwani
sikuwa tayari kuwasaidia
kumpata Olivia kama
wasingenieleza sababu ya
kumtafuta.Kama ni lawama
mimi ndiye ninastahili.Avi
kwa nini usinipeleke mara
moja nikaonana na Edger
Kaka halafu tutakuja
kuendelea pale
tulipoishia?akasema Devotha
na kumfuata Avi akaanza
kuchezea maeneo ya ikulu
“Devotha una uhakika
kwamba Edger anaweza
kuwa na msaada katika
kumtafuta Olivia?akauliza
“Nisingeweza kuja hapa
Nairobi kama nisingekuwa
na uhakika Avi.Naomba
dakika tano tu na nitakuwa
na jibu mahala alipo
Olivia.Edger anafahamu kila
kitu” akasema Devotha
“Lakini Edger amekaa
ndani kwa miaka mitatu
sasa hafahamu chochote
kinachoendelea huko nje na
kikubwa zaidi hafahamu
chochote kuhusu kutekwa
kwa Olivia Themba”
akasema Avi
“Avi niamini
ninachokwambia.Nisingewez
a kupoteza nauli yangu
kutoka Dar es salaam kuja
hapa Nairobi kama
nisingekuwa na uhakika
kwamba Edger anaweza
akasaidia kupatikana kwa
Olivia” akasema Devotha
“Devotha vipi kuhusu
serikali yako,una hakika
hawataweza kugundua kama
tunamtafuta Olivia?
“Usihofu hawataweza
kufahamu chochote” akajibu
Devotha.Avi akamtazama
kwa makini halafu akasema
“Sawa nitakupa dakika
tano tu za kuzungumza naye
lakini hii ni siri kubwa na
ninaomba upate majibu ya
mahala alipo Olivia.Jambo
lingine ni kwamba hii ni siri
kubwa na asifahamu mtu
mwingine jambo
hili.Tukigundua kwamba
umetoa siri
tutakuua.Umenielewa?
akauliza Avi na kusimama
“Ahsante sana Avi”
akasema Devotha
“Tusipoteze muda twende
mara moja” akasema Avi
wakatoka mle ndani.Devotha
alikuwa amevaa suti ya
kijivu na kifuani upande wa
kushoto aliweka ua jekundu
ambalo kati kati yake
kulikuwa na kamera ndogo
ambayo ingewawezesha
wenzake kufuatilia kile
kinachoendelea ndani ya
ubalozi wa Israel
MPENZI MSOMAJI
- DEVOTHA
ATAFANIKIWA
KUONANA NA EDGER
KAKA?
- OPERESHENI YA
KUVAMIA UBALOZI
WA ISRAEL
ITAFINIKIWA?
- NINI HATIMA YA
OLIVIA NA COLETHA?
ENDELEA KUFUATILIA
SIMULIZI HII
Mkuu mbona umeotea?? Tuwekee hata kamoja
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 1
Gari la Avi Abramson
mkuu wa Mossad ukanda wa
Afrika Mashariki lilikaribia
kufika katika ubalozi wa
Israel jijini Nairobi akatoa
simu na kupiga
akazungumza na mtu simuni
akamtaka azime kamera zote
za ulinzi ubalozini hapo kwa
muda wa dakika kumi na
tano.
Gari lilifika getini na
kwa haraka walinzi
wakafungua geti na kuingia
ndani ya jengo la
ubalozi.Mlinzi wa Avi
akawahi kushuka garini na
kuangaza pande zote kama
kuna hatari yoyote halafu
akamfungulia mkuu wake
mlango wa gari Avi
akashuka.Bila kuonekana
Devotha akabonyeza ile
kamera aliyoivaa katika koti
lake naye akafunguliwa
mlango akashuka.
Mara tu Devotha
alipobonyeza kamera,akina
Gosu Gosu waliokuwa ndani
ya chumba cha hoteli Sadena
wakaanza kupata picha.
“She’s in”akasema Tino
na kuwajulisha akina
Mathew Dar es salaam
waliokuwa wanafuatilia kila
kinachoendelea Nairobi
“Good job” akasema
Mathew
Baada ya kushuka garini
Avi akamuita Devotha
pembeni
“Nimeelekeza kamera
zote zizimwe kwa muda wa
dakika kumi na tano ili
uweze kuonana na
Edger.Sitaki mtu yeyote
afahamu kama nimekuleta
hapa ukaonana
naye.Naomba tusipoteze
muda twe….” Akasema Avi
“Avi kabla hatujaenda
huko una hakika mtu
uliyemuelekeza azime
kamera kweli amezima
kamera zote? Akauliza
“Nina uhakika
amezima.Kwa nini umeuliza?
“Yawezekana akajiuliza
maswali mengi kwa nini
kamera zote katika jengo hili
zizimwe? Anaweza akapata
ushawishi wa kuacha baadhi
ya kamera ili ajue
kinachoendelea.Nakushauri
ufanye uhakiki kama kweli
kamera zote zimezimwa ili
yasije kutokea matatizo kwa
upande wako baada ya mimi
kuondoka” akasema Devotha
“Ninawaamini watu
wangu lakini ulilolisema lina
msingi yawezekana kweli
mtu niliyemuelekeza azime
kamera akataka kuchunguza
kujua nini kinaendelea”
akasema Avi na kumtaka
Devotha amfuate wakaelekea
ofisini kwake akawasha
kompyuta yake.Kulikuwa na
sehemu ya kuweka namba za
siri na Devotha akaielekeza
kamera yake makusudi
katika kompyuta ya Avi ili
wenzake wanaoendelea
kumfuatilia wazione namba
zile za siri atakazoandika
Avi.Huu ulikuwa ni ujanja
wa Devotha kumleta Avi
ofisini kwake ili waweze
kuipata namba ya siri
anayoitumia kuingia katika
mtandao wao.Avi akabonyeza
kompyuta yake na
kujiridhisha kamera zote
zilikuwa zimezimwa.
“Kamera zote zimezima”
akasema Avi huku akizima
kompyuta yake
“Ni vyema
umejiridhisha” akasema
Devotha wakatoka na
kuelekea mahala aliko Edger
kaka
Timu ya akina Mathew
waliokuwa wakimfuatilia
Devotha walikuwa na kazi
kubwa ya kuhakikisha
wanaipata vyema ramani ya
njia ya kupita kuelekea
mahala alikofichwa Edger
Kaka.
Avi alitumia kadi yake
kufungulia mlango mkubwa
wakaanza kushuka ngazi
kuelekea chini ya jengo hadi
walipofika katika lango
lingine kubwa akalifungua
kwa kutumia kadi ile ile
wakatokea katika sebule
nzuri yenye sofa za kuvutia.
“Hapa ndipo anapoishi
Edger Kaka” akasema Avi na
kwenda kuufungua mlango
mwingine akaingia Devotha
akamfuata.Ndani ya chumba
kile kulikuwa na kitanda
kikubwa ambacho alikuwa
amelala mtu mmoja
aliyedhoofu sana.
“Edger
unaendeleaje?akauliza Avi
“Naendelea vyema.Kuna
taarifa zozote
umeniletea?Olivia
amepatikana?akauliza Edger
“Nimekuletea
mgeni.Atajitambulisha yeye
ni nani na kwa nini yuko
hapa” akasema Avi na
kumgeukia Devotha
akamnong’oneza sikioni
“Una dakika tano tu za
kuzungumza
naye,usithubutu kufanya
kitu chochote cha kijinga”
akasema Avi na kutoka
akaufunga mlango.Devotha
akachukua kiti
akaketi.Edger alikuwa
anamshangaa hakuwahi
kumuona hapo kabla
“Edger kaka”akasema
Devotha
“Wewe ni nani?Unataka
nini?akauliza Edger ambaye
bado sauti yake ilikuwa
dhaifu
“Naitwa Devotha
ninatokea Tanzania”akasema
Devotha na kumstua Edger
“Tanzania?akauliza
“Ndiyo” akajibu Devotha
na woga mkubwa ulionekana
machoni pa Edger
“Umefahamuje kama
niko hapa?akauliza Edger
“Ninafanya kazi na
Mossad hivyo ninafahamu
kila kinachoendelea na kwa
nini uko hapa.Nimepewa
dakika tano tu za
kuzungumza nawe hivyo
nataka kujielekeza moja kwa
moja katika suala la msingi
lililonileta kwako” akasema
Devotha na kumkazia macho
Edger
“Hivi sasa nchini
Tanzania shirika la ujasusi
la Israel Mossad,wanaandaa
operesheni kubwa ya
kumtafuta Dr Olivia Themba
ambaye ametekwa na watu
wasiojulikana.Ili uweze
kuwapa Mossad taarifa za
muhimu wanazozitafuta
kuhusu mtandao wenu wa
IS,umeelekeza wahakikishe
wanamtafuta na kumpata
Olivia.Mimi ndiye wakala wa
Mossad nchini Tanzania na
operesheni nzima ya
kumtafuta Olivia
inaniegemea mimi.Katika
uchunguzi wetu wa awali
tumebaini kwamba Olivia
ametekwa na watu wa
mtandao wako wa IS hivyo
nimekuja kwako kukuomba
utoe ushirikiano ili tuweze
kumpata Olivia” akasema
Devotha
“Olivia ametekwa na
watu wa IS?akauliza Edger
“Ndiyo ametekwa na
IS.Kama ulimaanisha
ulichokisema kuwa Olivia ni
mwanamke pekee
unayempenda ,huu ni wakati
wako wa kutoa ushirikiano
mkubwa ili tuweze
kumuokoa kutoka katika
mikono ya IS” akasema
Devotha
“Kwa nini IS wamteke
Olivia Themba?akauliza
Edger
“Mimi siwezi kuwa na
jibu lakini wewe unafahamu
kila kitu kwa nini wamteke
Olivia”
“Sifahamu chochote dada
yangu.Nimekaa mahala hapa
ambapo sijui ni wapi kwa
muda wa miaka mitatu na
sielewi chochote
kinachoendelea huko
nje.Siwezi kujua sababu ya
IS kumteka Olivia”
“Edger umekuwa hapa
kwa muda wa miaka mitatu
na katika muda huo wote
watu wako wa IS hawajui
kama uko hai hivyo hakuna
yeyote
atakayekusaidia.Unapaswa
kuyapigania maisha yako
wewe mwenyewe.Umeanza
vyema kwa kuahidi kueleza
kila kitu japo umetoa
masharti ya kupata Olivia
ninakuahidi tutampata
lakini nataka utupe
ushirikiano mkubwa katika
hilo kwani Olivia kama
nilivyokuelea anashikiliwa
na watu wa mtandao
wako.Nataka unipe orodha
ya watu walio katika
mtandao wa IS nchini
Tanzania ambao unamini
wanaweza kuwa wanahusika
na kutekwa kwa Olivia
Themba” akasema Devotha
“Sifahamu mtu yeyote wa
IS Dar es salaam” akajibu
Edger
“Edger ulikiri mwenyewe
kwamba unampenda
Olivia,huu ni wakati wako
wa kulithibitisha hilo kwa
kutoa taarifa ambazo
zitasaidia
kumpata.Waliomteka ni
wenzako wa IS na
yawezekana lengo lao ni
kumuua.Kama kweli
unampenda Olivia nipe
majina ya watu walio katika
mtandao wa IS nchini
Tanzania ili tuweze
kumuokoa Olivia” akasema
Devotha
“Dada yangu sifahamu
mtu yeyote ambaye
anashirikiana na IS nchini
Tanzania” akajibu Edger na
Devotha akamtazama kwa
hasira
“Edger unaonyesha wazi
kwamba maneno yale
uliyoyasema kwamba
unampenda Olivia si maneno
ya kweli bali ulikuwa ni
uongo.Huna mapenzi yoyote
kwa Olivia kwani kama
ungekuwa unampenda
ungedhihirisha hilo kwa
kutoa taarifa ambazo
zingesaidia kumuokoa
kutoka katika mikono ya
watu ambao hatujui lengo lao
ni nini kwake.Edger Olivia
alikuokoa pale ulipowekewa
sumu kwa sasa yuko
matatizoni ni wakati wako
na wewe kuhakikisha
unamsaidia kuyaokoa
maisha yake kama
alivyofanya kwako” akasema
Devotha.Edger hakujibu kitu
aliendelea kumtazama
Devotha
“Edger muda wangu
unakwisha tafadhali naomba
unijibu ili tuweze kumuokoa
Olivia ambaye hastahili
kupitia mateso kama haya
anayoyapitia hivi sasa”
akasema Devotha lakini bado
Edger aliendelea kuwa
kimya.Mlango ukagongwa.
“Edger muda wangu
umekwisha.Nitakapotoa
mguu wangu ndani ya
chumba hiki bila kupata jibu
lako naomba ufahamu kuwa
hakutakuwa na uwezekano
tena wa kumpata Olivia.IS
are going to kill her !!
akasema Devotha.Bado
Edger aliendelea kuwa
kimya.Devotha akainuka
“Edger nina sekunde
chache zimebaki nieleze
tafadhali! Akasema Devotha
“Sifahamu mtu yeyote”
akajibu Edger.Devotha
akamtazama kwa hasira na
kumfuata pale kitandani
akamshika na kumuinua
lakini kabla hajafanya
chochote Avi akaingia
“Devotha !! akasema Avi
na Devotha akamuachia
Edger
“Muda
umekwisha.Twende
tuondoke” akasema Avi
“Olivia akifariki dunia
damu yake itakuwa juu
yako” akasema Devotha kwa
ukali na kutoka ndani ya kile
chumba
“Muda nilioelekeza
kamera kuzimwa umekaribia
kumalizika hivyo unapaswa
kuwa tayari umetoka ndani
ya jengo pale kamera
zitakapowashwa” akasema
Avi huku wakitembea
haraka haraka kutoka ndani
ya jengo wakaingia katika
gari la Avi na kuondoka
katika ubalozi wa Israel.
Hakukuwa na
mazungumzo garini baada ya
kuondoka katika ubalozi wa
Israel hadi walipofika
Sadena hotel.Avi na Devotha
wakashuka garini
wakaelekea chumbani.
“Umepata ulichokuwa
unakitafuta kwa Edger
Kaka?akauliza Avi
“Hapana sikufanikiwa
kupata chochote muda
ulionipa wa kuzungumza
naye ni mdogo sana”
akasema Devotha
“Nafahamu ni muda
mfupi lakini ulipaswa
kuutumia kikamilifu na
kuweza kupata taarifa
kutoka kwa Edger.Devotha
hata kama ningekupa masaa
manne ya kuzungumza naye
Edger asingeweza kukueleza
chochote.Kama ameweza
kukaa kwa muda wa miaka
mitatu bila kuzungumza
chochote usingeweza kupata
chochote kutoka kwake kwa
muda wa dakika tano”
akasema Avi
“Edger alikuwa karibu
sana kufunguka.Kwa ajili ya
Olivia yuko tayari kueleza
kitu chochote.Ungenipa
muda zaidi wa kuzungumza
naye nakuhakikishia
ningeweza kupata kile
nilichokuwa nakitafuta
kwake”
“Devotha unapaswa
ushukuru kwa hata dakika
zile chache nilizokupatia
ukaweza kuonana na Edger
Kaka.Kuna watu wako ndani
ya ubalozi wetu hawafahamu
kama kuna mtu anaitwa
Edger ameishi pale ndani
kwa miaka mitatu”
“Ninalifahamu hilo Avi
lakini kama ningeweza
kupata nafasi nyingine ya
kuzungumza naye nina
uhakika mkubwa wa kuweza
kupata kile ninachokitafuta”
“Devotha hakutakuwa na
nafasi nyingine tena ya
kuonana na Edger kaka na
ninaomba hiki tulichokifanya
kibaki kuwa siri kwani
ikijulikana ni mimi nitakuwa
katika matatizo
makubwa.Naomba uitunze
siri hii” akaomba Avi
“Usijali Avi.Ninafahamu
umuhimu wa siri hii kubwa
na ninakuhakikishia
nitakwenda nayo kaburini”
akasema Devotha
“Kwa sasa baada ya
kukosa taarifa kutoka kwa
Edger nini mipango yako ya
kumpata Olivia? Akauliza
Avi
“Bado yapo matumaini
makubwa.Kuna taarifa
fulani tunazifuatilia jijini
Arusha ambako niliwaacha
Fishel na Ehud.Nikitoka
hapa ninakwenda kuungana
nao.Nina uhakika taarifa
hizo zinaweza kutupa
mwanga.Usihofu Avi lazima
tutampata Olivia” akasema
Devotha na kwenda
kumkalia Avi mapajani
“Avi nimemaliza kile
kilichonileta Nairobi japo
sijafanikiwa lakini
nimejaribu.Unataka
tuendelee pale
tulipoishia?akauliza Devotha
huku akikuna kidevu cha Avi
na kumfanya atabasamu
halafu akaanza kumfungua
tai yake akamuinamia na
kumbusu.
“Unasemaje Avi
tuendelee?akauliza Devotha
akiendelea kumbusu Avi
“Mhh ! Avi akaguna
“Unasemaje
Avi?Unahitaji tuendelee pale
tulipoishia?Nataka
nikuonyeshe namna
wanawake wa kiafrika
wanavyoyafahamu mapenzi”
akasema Devotha akiendelea
kumfanyia uchokozi Avi
ambaye tayari damu ilikuwa
inamchemka.Akamvua koti
na kulitupa pembeni
akaanza kumvua shati.Avi
mashetani yake yakampanda
akajikuta akiufungua
mkanda wa suruali yake
akaivua na kuitupa
sakafuni.Akamvuta Devotha
na kuanza kumbusu
akamfungua vifungo vya
koti,Devotha akainuka
akamshika mkono Avi
akamuongoza hadi katika
chumba cha kulala na
kumlaza kitandani akamvua
nguo ya ndani na kuanza
kufanya utundu mkubwa
ikulu kwa Avi kwa kutumia
ulimi wake halafu akambusu
Avi na kusema
“Avi ninahitaji kupata
vinywaji nisubiri dakika
mbili nikachukue kinywaji
nikipendacho halafu
nitarejea” akasema Devptha
“Kwa nini usiwapigie
simu walete kinywaji hicho
hapa hapa chumbani?HUna
haja ya kwenda wewe
mwenyewe” akasema Avi
“Ngoja nikachukue
mwenyewe nirudi
haraka.Wahudumu
wanaweza wakachelewa kuja
na mimi huwa ninapata
starehe sana nikinywa
kinywaji nikipendacho.Nipe
dakika mbili tu” akasema
Devotha na kumbusu Avi
kisha akatoka na kwa
haraka akaingia katika
chumba cha akina Gosu Gosu
“Mambo yanakwendaje
huku? Mmefuatilia kila
kitu?akauliza Devotha
“Devotha umefanya kazi
nzuri.Tumekufuatilia kila
ulichokifanya” akasema Gosu
Gosu na mara katika picha
za kamera Avi akaonekana
akiishika simu yake
“Guys Avi ameishika
simu yake kuweni makini
kufuatilia kile
anachokizungumza” akasema
Mathew na wote wakageukia
runinga kumtazama Avi
“Ongeza sauti tusikie kile
anachokizungumza” akasema
Mathew na Tino akaongeza
sauti
“Hallow Nabil” akasema
Avi baada ya mtu
aliyempigia kupokea
simu.Baada ya sekunde
chache akasema
“Nabil kuna kazi ambayo
nataka uifanye usiku wa
leo.Kuna mwanamke mmoja
ametoka Tanzania nataka
kumkata pumzi usiku wa
leo.Nitakupa maelekezo
baadae kidogo anza
kujiandaa” akasema Avi na
kukata simu.
“Guys Avi
hajafurahishwa na kitendo
cha Devotha kufahamu siri
yao na kuonana na Edger
Kaka na sasa anasuka
mpango wa kumuua.Siri hii
ya Edger Kaka kuwepokatika
ubalozi wao hawataki
ijulikane.Devotha umefanya
kazi nzuri sana.Kwa sasa
wote tuna uhakika Edger
Kaka yuko hai na
tumethibitisha hilo.Baada ya
kufahamu mpango wa Avi
kumuua Devotha kuna
mambo mawili ambayo
lazima tuyafanye”
akanyamaza kidogo na
kusema.
“Tunatakiwa
kuhakikisha Avi,mlinzi na
dereva wake hawatoki
salama ndani ya
hoteli.Tunatakiwa kuwaua
wote.Devotha utarejea ndani
ya chumba chako na
kumtaka Avi awapigie simu
watu wake aliowaacha ndani
ya gari ambao ni dereva na
mlinzi wake ili waweze
kupata kinywaji wakati
wewe ukiendelea
kumstarehesha.Akiwapigia
utawafuata utawachukua na
kuwapeleka katika chumba
cha akina Gosu
Gosu.Wakiingia humo
waueni wote na atabaki Avi
peke yake hiyo itakuwa ni
kazi ya Devotha
kummaliza.Kabla ya saa tatu
usiku wa leo watu hao wawe
wameuawa.Gosu Gosu
unajua namna ya kufanya
baada ya kuwaua watu
hao.Tino ni mwenyeji hapo
Nairobi atakusaidia namna
ya kuihifadhi miili ya watu
hao isionekane” akasema
Mathew
“Sawa Mathew
nimekuelewa”akasema Gosu
Gosu
“Jambo la pili,baada ya
kuwaua hao jamaa,Tino
utachukua gari la Avi na
utakwenda katika ubalozi wa
Israel.Wanalifahamu gari la
Avi wakiliona watakuruhusu
kupita getini na kama
kutakuwa na tatizo lolote
waambie wapige simu ya Avi
ambayo itaunganishwa na
mfumo wetu na Ruby
ataipokea na kuzungumza na
hao jamaa kwa kutumia
sauti ya Avi ambayo
imerekodiwa.Ukivuka geti
tutakuongoza kuelekea
katika ofisi ya Avi kwani
tayari tumeipata ramani
muda ule alipokuwa na
Devotha.Tunataka kuingia
katika mtandao wa Mossad
ili tuweze kupata taarifa zote
za muhimu
zitakazotuwezesha
kufanikisha operesheni
yetu.Ukishaingia katika ofisi
hiyo Ruby atakupa
maelekezo nini cha
kufanya.Nadhani
mmenielewa” akasema
Mathew.
“Tumekuelewa
Mathew,hakuna muda wa
kupoteza mimi ngoja nirejee
chumbani nikamshawishi ili
awapigie simu watu wake
kule garini” akasema
Devotha
“Devotha kuwa makini
sana ili Avi asigundue
kwamba tayari tunafahamu
kile anachotaka kukifanya”
akasema Mathew
“Niko makini usihofu”
akasema Devotha kisha
akatoka katika kile chumba
na kurejea tena chumbani
kwake akamfuata Avi pale
kitandani ambaye alikuwa
mtupu akambusu
“Mbona umerejea bila
vinywaji?akauliza Avi huku
akiuchezea uume wake
“Avi kuna kitu
kimenirudisha”
“Kitu gani?akauliza Avi
“Umewaacha ndani ya
gari mlinzi na dereva wako
wanakusubiri na hawajui
utatoka humu ndani saa
ngapi.Haipendezi wakati sisi
tunastarehe wao waendelee
kupigwa na baridi ndani ya
gari.Itapendeza kama
tukiwatafutia sehemu nao
waweze kupata nafasi ya
kupumzika wakati sisi
tunaendelea na mambo
yetu”akasema Devotha
“Usihofu Devotha
watanisubiri hata kama
nikitoka saa tisa usiku,ni
kazi yao” akasema Avi
“Avi nakubali ni kazi yao
lakini wakati mwingine tuwe
na ubinadamu.Kuna ubaya
gani wakati sisi tukistarehe
wao wakiendelea kupata
kinywaji na chakula cha
jioni?Yawezekana ukatoka
humu saa nne za usiku.Muda
huo wote watakuwa garini
wanakusubiri?Wapigie simu
tafadhali wajulishe kwamba
ninakwenda kuwachukua ili
wapate kinywaji kidogo
wakati sisi tunastarehe.Avi
unajua kunikuna na
ninataka nikupe vitu adimu
sana leo hadi umsahau mke
wako”akasema Devotha na
kumbusu Avi akamletea
simu yake.Avi akaweka dole
gumba simu ikafunguka
akampigia mlinzi wake
akamjulisha kwamba kuna
mtu anakwenda kuwachukua
ili wapate kinywaji kwani
yeye atachelewa kidogo
“Ahsante Avi.Umefanya
jambo jema ninawafuata
sasa hivi ili nao waendelee
kuburudika kwa vinywaji”
akasema Devotha na kutoka
akashuka chini hadi katika
maegesho ya magari
akagonga mlango wa gari
kioo kikashushwa
“Amewapigia simu Avi?
Twendeni mkapumzike
kidogo mpate chakula na
vinywaji kuna sehemu
mmeandaliwa.Avi
atachelewa kidogo” akasema
Devotha wale jamaa
hawakuwa na wasiwasi
kwani wamekwisha pewa
ruhusa na mkuu wao
wakashuka garini na
kumfuata Devotha
wakaelekea ndani.Moja kwa
moja akawapeleka hadi
katika chumba cha akina
Gosu Gosu akakiminya
kitasa na kuufungua mlango
“Karibuni
ndani”akasema Devotha
David Kioko dereva wa
Avi ndiye aliyekuwa wa
kwanza kuingia ndani ya kile
chumba ambamo aliwakuta
Gosu Gosu na Tino
“Karibu kaka” akasema
Tino na kulazimisha
tabasamu usoni.Mlinzi wa
Avi naye akapiga hatua
kuingia ndani ya kile
chumba lakini
alipochunghulia ndani
akasita kuingia.Devotha
aliyekuwa nyuma yake kwa
kasi ya umeme akamrukia
teke kali la mgongo Yule
jamaa akaangukia
ndani.Gosu Gosu aliyekuwa
karibu na mlango alimpokea
Yule mlinzi wa Avi kwa
ngumi nzito iliyompeleka
chini kisha akamtandika
tena teke zito la uso na Yule
jamaa akaanza kutoa damu
mdomoni.Gosu Gosu akatoa
bastora iliyofungwa kiwambo
cha sauti
“Msiniue jamani !
akasema dereva aliyekuwa
akitetemeka lakini Gosu
Gosu hakupoteza muda
akaizinga bastora yake na
kuachia risasi tatu
akimlenga kifuani Yule
mlinzi wa Avi.
“Ndugu zangu msiniue
nawaomba sana” akaomba
Yule dereva lakini masikio
ya Gosu Gosu yalikuwa
yameziba akaachia risasi
kadhaa na Yule dereva
akaanguka sakafuni.Gosu
Gosu akawavuta
akawaingiza chooni
akawapekua na kuchukua
simu zao zote akazizima
kabisa kisha akafuta damu
iliyosambaa pale sebuleni.
“Kazi nzuri Gosu
Gosu,Devotha usichukue
muda mrefu nenda kaendelee
na sehemu yako.Tino jiandae
uelekee katika ubalozi wa
Israel hapo muachie Gosu
Gosu ataendelea kumlinda
Devotha”akaelekeza Mathew.
Devotha akatoka na
kurejea katika chumba chake
“Tayari wanapata
chakula na kinywaji.Sisi
tuendelee”akasema Devotha
akivua koti lake
“Ahsante Devotha una
roho nzuri sana.Ngoja
niwakumbushe wasinywe
kupitiliza sintakawia sana
hapa” akasema Avi na
kuchukua simu yake lakini
Devotha akamshika mkono
na kuichukua simu akaitupa
pembeni.
“Usiwasumbue Avi wale
ni watu wazima wanafahamu
wanachotakiwa
kukifanya.Waache nao
waburudike kidogo” akasema
Devotha na kuanza
kumporomoshea mabusu
mfululizo na taratibu Avi
akazidiwa na kipute
kikaanza.
Tino alitoka chumbani
kwao akaufungua taratibu
mlango wa chumba cha
Devotha na kuingia sebuleni
akapekua mavazi ya Avi
akachukua kadi ya Avi ya
kufungulia milango halafu
akatoka na kurejea
chumbani kwao akachukua
funguo za gari akaenda
maegesho akalitafuta gari la
Avi akaingia na kuondoka
kuelekea katika ubalozi wa
Marekani akiwa ameweka
kifaa cha mawasiliano sikioni
ili aweze kuwasiliana na
akina Mathew
“I’m on move” akasema
Tino
“Tunakufuatilia Tino”
akasema Mathew.Tayari kiza
kilikwisha ingia
Hotelini chumbani kwa
Devotha kipute kilikiwa
kinaendelea na Devotha
alimpeleka Avi vilivyo.Hadi
mzunguko mmoja
ulipomalizika Avi alikuwa
hoi akihema kama mkimbiaji
wa mbio ndefu.Devotha
akamuacha pale chumbani
amelala kitandani akaenda
sebuleni akatazama
kamera.Hii ilikuwa ni ishara
kwa akina Gosu Gosu
“Gosu Gosu hakuna
kupoteza muda ni wakatiwa
kummaliza Avi ” akaelekeza
Mathew na Gosu Gosu
ambaye sura yake ilikuwa
imejikunja kwa hasira
akaificha bastora yake
kiunoni akachungulia nje
hakukuwa na mtu akaenda
katika mlango wa chumba
cha Devotha akakiminya
kitasa taratibu na mlango
ukafunguka akamkuta
Devotha sebuleni akichomoa
bastora yake akanyata na
kuingia chumbani akamkuta
Avi amelala kitandani
hoi.Kijiusingizi kilianza
kumpitia
“Hey ! Gosu Gosu
akamstua
Avi alistuka akainua
kichwa akajikuta
akitazamana na
bastora.Alitaka kuinuka
lakini alichelewa kwani
kidole cha Gosu Gosu tayari
kilikwisha izinga bastora na
risasi zikatoka na kuzama
kifuani kwa Avi.Gosu Gosu
aliyeonekana kuwa na hasira
kali alimchakaza Avi kwa
risasi hadi zilipomalizika
katika bastora.
“Papii imetosha,tayari
amekufa ! akasema Devotha
aliyekuwa amesimama
mlangoni akishuhudia Gosu
Gosu akifanya mauaji yale
“Mfiche bafuni
tutamuondoa baadae”
akasema Gosu Gosu na
kutoka mle chumbani
“Ama kweli safari hii
nimekutana na watu wa aina
yake.Gosu Gosu ni muuaji
hata macho yake
yanaonyesha kwake kutoa
roho ya mtu ni kitu chepesi
mno.Ilitosha kumuua Avi
kwa risasi mbili lakini
amemimina risasi zote
katika bastora yake.Kuna
nyakati hata mimi ninaogopa
sana kuwa karibuna watu
hawa?akawaza Devotha
akamvuta Avi toka kitandani
akampeleka bafuni
akampekua na kuchukua
kila kitu alichokuwa nacho
kisha akatoka na kwenda
chumbani kwa Gosu Gosu.
“Kazi nzuri Devotha.Kwa
sasa tunasubiri Tino aingie
ndani ya ubalozi.Anafanya
jambo la hatari tumuombee
arejee salama”akasema
Mathew aliyekuwa
akishuhudia kila kitu
“Tino tupe mrejesho
tafadhali” akasema Devotha
“Ninakaribia kufika
ubalozini nimechelewa njiani
msongamano mkubwa sana
jioni hii hapa
Nairobi.Nitawajulisha
kitakachoendelea” akasema
Tino
Alikaribia kufika katika
geti la kuingilia ndani ya
balozi akapewa ishara na
walinzi ya kusimama
akapunguza mwendo lakini
walipogundua ni gari la Avi
haraka haraka wakakimbia
kufungua geti.Lilikuwa na
vioo vyeusi hivyo
hawakuweza kuona
aliyekuwa ndani ya gari ni
nani.
“Guys I’m in.Nimepita
getini bila taabu wakidhani
ni Avi.Nahitaji maelekezo ya
kufika katika ofisi ya Avi”
akasema Tino
“Safi sana Tino.Katika
mzunguko fuata njia ya
kushoto halafu utapinda
kulia utaona kibao
kimeandikwa VIP
parking.Huko ndiko
alikoegesha gari Avi wakati
nimekwenda naye” akasema
Devotha na Tino akafuata
maelekezo aliyopewa akafika
katika maegesho
aliyoelekezwa
“Tayari nimefika
maegesho” akasema Tino
“Shuka garini nenda
katika mlango mkubwa
utapitisha kadi mlango
utafunguka utaingia ndania”
akaelekeza Devotha.
Tino akavuta pumzi
ndefu nakusema
“Pray for me guys”
Akashuka garini na
kuangaza pande zote
kulikuwa kimya na ofisi
chache zilikuwa zinawaka
taa.Alipohakikisha hakuna
tatizo lolote akatembea kwa
kujiamini kuelekea katika
mlango mkubwa akatoa kadi
ya Avi akaipitisha na mlango
ukafunguka akaingia ndani
akakuta kuna lifti nne
“Tayari nimeingia kuna
lifti nne ninaziona” akasema
Tino
“Kuelekea ofisini kwake
panda lifti ya kushoto kwako
hadi ghorofa ya sita ndiko
ziliko ofisi za
Mossad.Ukishuka kwenye
lifti fuata korido hadi
chumba cha mwisho kabisa
kwenye kona hiyo ndiyo ofisi
ya Avi” akasema Devotha na
Tino akaingia ndani ya lifti
hadi ghorofa ya sita
akashuka na kuanza
kutembea kuelekea katika
chumba cha mwisho kama
alivyoelekezwa.Wakati
akielekea katika ofiosi ya Avi
mara mlango wa ofisi moja
ukafunguliwa wakatoka
jamaa wawili lakini Tino
hakuwajali akajiamini na
kupishana nao.Jamaa wale
nao hawakumjali kabisa
waliamini Tino ni mmoja wao
kwani asingeweza kuingia
katika ghorofa ile kama si
muhusika wa Mossad.
Alifika chumba cha
mwisho ambacho ndicho ofisi
ya Avi kwa mujibu wa
maelekezo ya Devotha
akapitisha kadi ile mlango
ukafunguka akaingia ndani.
Mara tu Tino alipoingia
ndani ya ofisi ya Avi,katika
chumba walimo Gosu Gosu
na Devotha simu ya Avi
ikaanza kutoa mlio.
“Tino hebu jaribu kutoka
ndani ya hicho chumba”
akasema Devotha na Tino
akatoka ndani ya kile
chumba
Mara tu Tino alipotoka
ndani ya kile chumba ule
mlio katika simu ya Avi
ukakoma
“Nadhani kuna
muunganiko kati ya ofisi na
simu ya Avi.Ulipofungua tu
mlango simu ikaanza kutoa
mlio ulipotoka ikaacha”
akasema Devotha
“Kuna kitu hata mimi
nimekigundua ambacho si
kawaida katika ofisi
hii.Hakuna hewa na hakuna
kitu chochote kinachowaka
hata taa ya ndani haiwaki”
“Ofisi hiyo” akasema
Ruby akiwa Dar es salaam
“Ina mfumo maalum
ambao unamtambua Avi
pekee na ndiyo maana
wakati ule alipoingia na
Devotha hakukuwa na tatizo
lolote.Akiwa nje ya ofisi na
mlango wa ofisi yake
ukafunguliwa atajulishwa
kwa kutumia simu yake ya
mkononi iliyounganishwa na
mfumo huo.Lazima iko
namna ya kuweza kuufungua
mfumo huo kwa kutumia
simu ya Avi.Tino ingia tena
katika hiyo ofisi na mlio
ukianza katika simu ya Avi
ichukue na ujaribu
kuifungua uizime kengele ”
akasema Ruby
“Sawa nimekusikia
Ruby” akasema Tino na
kufungua tena mlango wa
ofisi ya Avi akaingia ndani
na simu ya Avi ikaanza tena
kutoa mlio.
“Devotha ichunguze simu
hiyo ya Avi kwa haraka
lazima kuna namna ya
kuweza kuufungua mfumo”
akasema Ruby na Devotha
akaichunguza simu ile
akakuta mahala kuna alama
ya kuweka dole gumba Gosu
Gosu akatoka mbio akaenda
chumbani kwa Devotha na
kukata dole gumba la Avi
kisha akaliweka katika ile
sehemu inayohitaji dole
gumba la Avi na mara simu
ikafunguka na Devotha
akapekua akaipata sehemu
iliyoandikwa unlock the
system akaibonyeza na
ofisini kwa Avi taa zikawaka.
“Tino nini kimetokea
hapo?akauliza Devotha
“Taa zimewaka” akasema
Tino
“Good sasa nataka uende
katika kompyuta ya Avi
uiwashe” akaelekeza
Devotha na kwa haraka Tino
akaenda katika kompyuta ya
Avi akaiwasha na kukutana
na sehemu inayomtaka
aingize namba za siri.Ruby
tayari alikuwa na namba za
siri za kufungulia kompyuta
ile ya Avi akamtajia Tino
akaziingiza namba zile na
kompyuta ya Avi ikafunguka.
“Elekeza kamera yako
katika kompyuta ya Avi”
akasema Ruby na Tino
akaelekeza kamera katika
kompyuta ya Avi akaanza
kumuelekeza namna ya
kuiunganisha na kompyuta
ndogo aliyokuwa nayo
Tino.Haraka haraka Ruby
akaanza kazi yake akiwa Dar
es salaam huku
akimuelekeza Tino kufanya
mambo kadhaa katika
kompyuta ile ya Avi.Baada
ya muda wa dakika kadhaa
mafaili yakaanza
kuhamishwa kutoka katika
kompyuta ya Avi kuingia
katika kompyua ya
Tino.Asilimia zilihesabu
haraka haraka namna
mafaili yalivyokuwa
yakihama kutoka katika
kompyuta ya Avi.Ilipofika
asilimia mia moja Tino
akaelekezwa kitu cha
kufanya halafu akaizima ile
kompyuta ya Avi akatoka
ndani ya ile ofisi na
kuufunga mlango akaanza
kutembea kwa tahadhari
hadi katika lifti akashuka na
kuelekea maegesho alikoacha
gari la Avi akaingia na
kuondoka,akafunguliwa geti
bila kuulizwa chochote
walinzi wakidhani ni Avi
ndiye aliyekuwamo ndani ya
gari.
“Nimetoka salama”
akasema Tino
“Kazi nzuri sana sasa
rejea hotelini” akasema
Mathew.
Kabla ya kurejea hotelini
Tino akapita kuchukua
baadhi ya vifaa ambavyo
aliagizwa na Gosu Gosu
kisha akarejea hotelini.
“Mathew tayari nimefika
hotelini salama” Tino
akawajulisha akina Mathew\
“Tino kazi nzuri
sana.Sasa ni wakati wako
Gosu Gosu unajua nini cha
kufanya wakati Ruby
akiendelea kupitia kile
ambacho tumekipata kutoka
katika kompyuta ya Avi.”
akasema Mathew.Gosu Gosu
akachukua vifaa alivyokuja
navyo Tino ambavyo ni shoka
dogo kali,panga na kisu
kikubwa kikali na bila
huruma akaanza kuikata
kata miili ya dereva na
mlinzi wa Avi ikafungwa
vizuri katika mifuko ya
nailoni na kuingizwa ndani
ya masanduku makubwa
akaenda pia chumbani kwa
Devotha na kufanya hivyo
pia kwa Avi halafu usafi
mkubwa ukafanyika kabla ya
miili ile iliyokuwa ndani ya
masanduku kuondolewa mle
hotelini.Gosu Gosu Anita
wakayakokota masanduku
yale matatu hadi katika lifti
wakashuka chini wakatoka
nje ya hoteli hadi katika gari
la Avi.Tino alibaki nyuma ili
kuhakiki usalama wa
wenzake.Baada ya
kuhakikisha wenzake
wameingia garini na yale
masanduku Tino naye
akawafuata akaingia garini
wakaondoka.Walielekea
mtaa Fulani ambako Tino
akawataka Gosu Gosu na
Devotha wabaki garini yeye
akashuka baada ya dakika
kama kumi hivi akarejea
akiwa na watu wengine
wawili wakaingia garini na
safari ikaanza wakaingia
katika kiwanda kikubwa
haraka haraka masanduku
yale matatu yakashushwa
kutoka garini watu wale
wawili wakiongozana na Tino
wakaingia ndani ya nyumba
Fulani Gosu Gosu na
Devotha wakabaki
garini.Dakika ishirini
zikapita Tino akarejea na
wale jamaa wawili wakaingia
garini na kuondoka pale
kiwandani.Safari ilikuwa ya
kimya kimya kurejea
hotelini.
DAR ES SALAAM
“Mathew kupitia haya
mafaili ambayo Tino
ameyachukua katika
kompyuta ya Avi
tumefanikiwa kupata mambo
mengi ya Mossad kwa
ukanda huu wa Afrika
Mashariki.Siri zao nyingi
sasa tunazo.Tunayo orodha
ya majasusi wote wa Mossad
walioko eneo la Afrika
Mashariki na kati na
kusini.Orodha ya operesheni
zao zote ,watu
wanaowafuatilia na mambo
mengine mengi lakini
kikubwa ni kuipata ramani
ya jengo zima la ubalozi na
Israel nchini Kenya ambayo
inaonyesha kila kitu kuanzia
mfumo wote wa ulinzi,njia za
dharura za kujiokoa endapo
kumetokea
shambulio,mahala
zinapohifadhiwa silaha na
mambo mengine mengi”
akasema Ruby baada ya
kumaliza kuyapitia mafaili
ambayo waliyapata kutoka
katika ofisi ya Avi.
“Good job Ruby.Vijana
wamefanya kazi kubwa sana
kule Nairobi.Ramani hii
ndiyo ambayo tulikuwa
tunaitafuta sana na
hatukujua kama tungeweza
kuipata mapema namna hii
hivyo basi usiku wa leo
tunakwenda Nairobi
kumchukua Edger Kaka”
akasema Mathew
“Usiku wa leo?akauliza
Ruby
“Ndiyo.Kila kitu
kitamalizika usiku wa
leo.Hatuna tena muda wa
kuendelea
kusubiri.Avi,dereva wake na
mlinzi wote wameuawa na
siku ya kesho wataanza
kutafutwa na
wasipopatikana tayari
wataanza kuhisi wameuawa
na kufanya operesheni yetu
kuwa ngumu hivyo lazima
tuhakikishe kila kitu
kinamalizika usiku wa
leo.Kikosi cha jeshi cha
operesheni maalum ambacho
tutashirikiana nacho kipo
tayari muda wowote kwa
kazi hivyo sioni sababu ya
kuendelea
kusubiri.Everything ends
tonight and we’ll bring Edger
Kaka home” akasema
Mathew.
“Mathew una hakika
hakuhitajiki maandalizi zaidi
kabla ya kuvamia ubalozi
huo?akauliza Ruby
“Ruby usihofu.Kikosi
ambacho utashirikiana nacho
ni kikosi hatari kabisa na
wao muda wotewapo tayari
kwa kazi hawahitaji
maandalizi.Kikubwa kwao ni
kujua wapi wanakwenda na
kufanya nini.Tunayo ramani
ambayo inatuongoza katika
kila kitu hivyo hakuna haja
ya kupoteza muda kufanya
maandalizi.Tukitaka kuvuta
muda zaidi tutatengeneza
mazingira magumu.Avi ni
mtu mkubwa na shughuli
nyingi za Mossad
zinamtegemea yeye,simu
yake tumeizima na
itakapofika asubuhi bado
hapatikani simuni na
hajulikani alipo wataanza
kuingiwa na wasi wasi na
juhudi za kumtafuta zitaanza
mara moja na wasipompata
hadi kufika kesho mchana
wataamini amepatwa na
jambo baya hivyo basi
tahadhari kubwa
itachukuliwa na kuifanya
kazi ya kumchukua Edger
kaka iwe ngumu ndiyo
maana ninataka usiku wa leo
operesheni hiyo
imalizike.Sisi tuko
tayari,kikosi kiko
tayari,hakuna cha kusubiri”
akasema Mathew na
kuchukua simu akampigia
Dr Evans
“Mathew habari yako
kijana wangu.Umekuwa
kimya sana nini
kinaendelea?akauliza Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais kabla
sijasema chochote nataka
kufahamu kama wale jamaa
wamekupigia simu siku ya
leo” akasema Mathew
“Hawajanipigia simu na
hata mimi nashangaa kwa
ukimya wao.Waliniahidi
kunipigia simu kunipa
maelekezo mengine ya nini
wanakitaka lakini
nashangaa mpaka sasa
hawajawasiliana nami na
hapa nilipo
nimechanganyikiwa sijui hali
ya mwanangu
ikoje.Nimejaribu kupiga
namba zile walizotumia
kunipigia
hazipatikani.Nifanye nini
Mathew? Akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais usiwe
na hofu mwanao atakuwa
salama.Hawatakubali
mwanao afe watahakikisha
kwa kila namna anakuwa
mzima ili waweze kumtumia
katika mabadilishano na
Edger Kaka.Bado wanaamini
kwamba wewe unafahamu
mahala alipo Edger na ndiyo
maana wanamshikilia
mwanao hivyo basi
watahakikisha kwa namna
yoyote ile mwanao anakuwa
salama na ndiyo maana
wakamtaka kwanza Olivia ili
aweze kumtibu virusi vile
alivyomuambukiza” akasema
Mathew
“Mathew ahsante sana
kwa kunipa moyo lakini yule
ni mwanangu lazima niwe na
wasi wasi.Ukimya wao
unanipa mashaka sana
kwamba yawezekana
wanashindwa kuwasiliana
nami kwa kuwa mwanangu
tayari amefariki”
“Tusiombe hayo yatokee
mheshimiwa Rais,nina
uhakika mkubwa kwamba
mwanao atakuwa mzima
kabisa.Nina uzoefu na hawa
magaidi namna
wanavyofanya operesheni
zao na Coletha watakuwa
wanamchunga sana kwa kila
namna wawezavyo.”
“Tuachane na hayo
nataka kufahamu mmefikia
wapi katika maandalizi
yenu?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
nimekupigia kukujulisha
kwamba timu niliyoituma
kwenda Nairobi kufanya
maandalizi ya
operesheni,imefanya kazi
nzuri na tayari tumefanikiwa
kuipata ramani ya jengo la
ubalozi na tayari
tumefahamu mahala alipo
fichwa Edger kaka na
kikubwa zaidi sote
tumefanikiwa kumuona na
kuthibitisha kuwa ni yeye
japo amedhoofu
mno”akasema Mathew
“Hongera sana Mathew
na timu yako kwa kupiga
hatua hiyo kubwa ndani
muda mfupi.Sikutegemea
kabisa kama mngeweza
kulifanikisha jambo hilo
mapema namna hii” akasema
Dr Evans
“Mheshimiwa
Rais,katika kuifanikisha kazi
waliyotumwa watu wetu
wamelazimika kutoa uhai wa
watu watatu akiwemo mkuu
wa Mossad Afrika mashariki
na kati dereva wake na
mlinzi.Mhshimiwa Rais
naamini tumeupanua zaidi
mgogoro huu lakini
hakukuwa na namna
nyingine ililazimu watu hao
wauawe ili tupate
tunachokihitaji”
“Ni kweli Mathew hiki
kilichofanyika kinaongeza
mafuta kwenye moto lakini
kama ilikuwa lazima watu
hao wauawe ili tupate
tunachokihitaji mimi sina
tatizo.Kwa hiyo nini mipango
yenu baada ya kupata
mlichokuwa mnakihitaji?
“Mheshimiwa Rais
operesheni yetu ya
kumchukua Edger Kaka
inakwenda kufanyika usiku
wa leo”
“Usiku wa leo?akauliza
Dr Evans kwa mshangao
kidogo
“Ndiyo mheshimiwa Rais
lazima tuifanye usiku wa
leo.Aliyeuawa ni mkuu wa
Mossad Afrika Masjhariki
hivyo asipopatikana hasi
asubuhi ya kesho wataamini
ameuawa hivyo kuifanyakazi
ya kwenda kumchukua
Edger kuwa ngumu ndiyo
maana ninataka kila kitu
kimalizike usiku wa leo”
akasema Mathew
“Mathew hatuwezi
kuzungumza suala hili
simuni nataka ufike hapa
ikulu mara moja.Mmoja wa
wasaidizi wangu ambaye
nimemuweka hapo awasaidie
atakuleta hapa ikulu mara
moja” akasema Dr Evans
“Sawa mheshimiwa Rais”
akajibu Mathew na Dr Evans
akakata simu.Mathew
akampigia Tino Nairobi
“Tino mnaendeleaje
huko?
“Tunaendelea vyema
Mathew.Tumetoka kumalizia
kuiteketeza miili ya wale
jamaa”
“Good.Avi ni mtu
muhimu sana kwa Mossad
na lazima atatafutwa,mna
hakika hawataweza
kupatikana na kugundulika
wameuawa?akauliza Mathew
“Haitakuwa rahisi
kupatikana kwani miili yao
imetupiwa katika tanuru
kubwa la moto na hivi
tunavyoongea imekwisha
kuwa majivu.Hakuna hat
mfupa utakaoonekana”
“Good.Tino nataka
kuwapa mrejesho wa kile
ambacho tumefanikiwa
kukigundua kutoka katika
yale mafaili tuliyoyachukua
ofisini kwa
Avi.Tumefanikiwa kupata
siri nyingi za Mossad afrika
mashariki lakini kikubwa
tumefanikiwa kupata ramani
ya jengo la ubalozi yenye
kuonyesha kila kitu.Baada
ya kuipata hiyo ramani
hatuna tena muda wa
kuendelea kusubiri hivyo
basi tunakwenda kumchukua
Edger Kaka usiku wa leo”
“Usiku wa leo?akauliza
Tino
“Ndiyo Tino,usiku wa leo
tutamaliza kila kitu na
kuondoka
Nairobi.Hamtakiwi kuwepo
hapo Nairobi hadi kufika
kesho asubuhi kwani Avi
ataanza na ninyi ndiyowatu
wa mwisho kuonekana naye
hivyo mtakuwa katika hatari
kubwa.Kila kitu kinakwenda
kufanyika usiku wa leo kabla
Avi hajaanza kutafutwa”
akasema Mathew na
kunyamaza baada ya mlango
kufunguliwa akaingia mmoja
wa wasaidizi wa Rais
Mathew akamfanyia ishara
asubiri dakika mbili
“Tino ninakwenda
kuonana na Rais muda si
mrefu ili kupanga namna
tutakavyotekeleza
operesheni hii na baada ya
kutoka huko nitawapa
taarifa nini kinaendelea
lakini kwa muda huu anzeni
kujiandaa na hakikisheni
mkiondoka hapo hotelini
mnaacha kila kitu kiko
salama.Kama kuna kamera
za usalama hapo hotelini
fanyeni kila namna
mnayoweza kufuta
kumbukumbu zote.Tino
wewe unao utaalamu huo”
akasema Mathew
“Sawa Mathew tunaanza
kujiandaa na utakapokuwa
tayari utatujulisha mambo
yanavyokwenda” akasema
Tino na Mathew akakata
simu akamuaga Ruby
ambaye aliendelea kupitia
mafaili yale waliyoyapata
kutoka katika ofisi ya Avi
akaingia katika gari na
kupelekwa ikulu.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 2
Mathew alifika ikulu
akapokewa na kupelekwa
mahala aliko Rais ambaye
alikuwa na mtu mmoja
aliyevaa sare maalum za
jeshi.
“Karibu sana Mathew
Mulumbi” akasema Dr Evans
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais”akajibu
Mathew
“Mathew kutana na
mkuu wa kikosi cha
operesheni maalum anaitwa
Austin January”Dr Evans
akafanya utambulisho
Mathew akaonyesha
mshangao kidogo
“Austin
January?akauliza
“Ndiyo.Mbona
umeshangaa?
“Jina na sura hii si vigeni
kwangu lakini sina kumbu
kumbu tumewahi kuonana
mahali.Nikumbushe
tafadhali kama tumewahi
kuonana sehemu Fulani”
akasema Mathew
“Hata mimi jina na sura
yako si vigeni kwangu lakini
kama ilivyo kwako hata mimi
nahisi kukufahamu japo sijui
tumewahi kuonana wapi”
akasema Austin
“Mtakumbushana baadae
ni wapi mmewahi kukutana
lakini kwa sasa tujielekeze
katika kile kitu cha muhimu
kilichotukutanisha hapa ila
kwa kukusaidia Mathew ni
kwamba Austin January
amewahi kufanya kazi
katika idara ya ujasusi ya
Taifa na alikuwa anaishi na
kuendesha biashara zake
nchini Afrika kusini lakini
alipata misuko suko
mikubwa kule alivamiwa
shamba lake likachomwa
mke na watoto wake kuuawa
na ndipo serikali kwa
kushirikiana na ubalozi wetu
Afrika kusini wakamsaidia
akarejea nyumbani salama
ambako alianza upya maisha
yake na kwa kuwa
anafahamika sana kwa
umahiri wake nililetewa
mapendekezo ya kumjumisha
katika kikosi cha jeshi
kinachoshughulika na
operesheni maalum na kwa
sasa ndiye kiongozi wa kikosi
hicho.Ninyi nyote mmewahi
kufanya kazi idara moja
ndiyo maana imekuwa rahisi
kile mmoja kumkumbuka
mwenzake.Mtaendelea
kukumbushana taratibu”
akasema DrEvans
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais kwa
kusaidia kunipa picha hii
ndogo itanisaidia
kukumbuka ni wapi mimi na
Austin tumewahi kukutana”
akasema Mathew
“Austin,Mathew
Mulumbi ana historia kama
yako kwani naye aliwahi
kupatwa na matatizo kama
yaliyokupata ya kupoteza
familia yake yote na ndipo
alipoamua kuacha kabisa
kazi ya ujasusi na kuanza
kufanya biashara kwa sasa
ni mfanya biashara mkubwa
ni mmoja wa mabilionea
wakubwa tulio nao hapa
nchini lakini pamoja na hayo
bado anaendelea kulitumikia
taifa kila pale
anapolazimika.Kwa ujumla
ninafurahi kuwa na nchi
yenye hazina kubwa ya
vijana kama ninyi ambao
wanaweza wakafanya kazi
kubwa ya kulilinda taifa lao”
akasema Dr Evans
“Ninashukuru pia
kukutana na Mathew
Mulumbi.” akasema Austin
“Mathew nimemuita
Austin hapa na ninashukuru
amefika kwa haraka kwani
kikosi chake ndicho
tutakachokitumia katika
operesheni hii.Toka jana
nilikwisha mpa maelekezo ya
kuandaa kikosi cha watu
kumi kwa ajili ya kufanya
operesheni maalum lakini
sikuwa nimemueleza kwa
undani ni operesheni gani na
inakwenda kufanyika
wapi.Ninataka utumie nafasi
hii kumpa picha pana kabisa
ya kile kinachokwenda
kufanyika na kwa nini
tunahitaji kikosi chake”
akasema Dr Evans.
Mathew akaanza
kumueleza Austin toka
mwanzo wa sakata lile la
kutekwa Olivia
“Muda hautoshi kueleza
kila kitu lakini kikubwa ni
kwamba tulifanikiwa
kufahamu kuwa Edger Kaka
ambaye aliwahi kuwa
mbunge wa bunge la jamhuri
ya muungano wa Tanzania
na ambaye alifariki katika
ajali na kuzikwa miaka
mitatu iliyopita,yuko
hai.Israel wakitumia shirika
lao la ujasusi la Mossad
walitengeneza ajali ile na
kutuaminisha Edger
amefariki lakini kumbe ni
mzima wamemficha Nairobi
wakimuhoji kutaka kupata
taarifa za mtandao wa IS
.Inasadikiwa Edger Kaka
ana mahusiano na kikundi
cha IS”
“Nimekuelewa vizuri
Mathew.Ninapenda
kuchukua nafasi hii
kukupongeza sana kwa
jitihada zote ulizofanya hadi
kulifikisha hapa hili
jambo.Kama alivyoagiza Rais
tayari kikosi cha watu kumi
kimekwisha andaliwa na
kiko tayari kwa kazi muda
wowote tutakapopata
maelekezo”akasema Austin
“Ahsante Austin.Kwa
sasa Edger amefichwa katika
ubalozi wa Israel jijini
Nairobi na operesheni yetu
tunayoiandaa ni kwenda
kumchukua hapo
ubalozini.Tukifanikiwa
kumpata yeye tutaweza
kuwapata Olivia na Coletha
na vile vile tutapata taarifa
za mtandao wa IS hapa
nchini”
“Mathew mimi na vijana
wangu tuko tayari hata sasa
kwa kazi tunahitaji
maelekezo tu”akasema
Austin
“Ili kuweza kumchukua
Edger Kaka ubalozini hapo
ililazimu kwanza kuipata
ramani ya jengo lote la
ubalozi na kufahamu mfumo
wote wa ulinzi
ulivyo.Nilituma timu
kwenda Nairobi kufanya kazi
hiyo na tayari
wameikamilisha kazi
niliyowatuma.Tumeipata
ramani ya jengo la ubalozi
wa Israel nchini Kenya hivyo
basi kilichobaki ni kuvamia
ubalozini hapo usiku wa
manane leo hii na
kumchukua Edger Kaka
kumrejesha nyumbani”
akasema Mathew
“Austin nadhani
umemsikia Mathew na
kumuelewa.Ninaamini vijana
wako wamekwisha jiandaa
kwa operesheni hii na mimi
ninatoa ruhusa kwamba
operesheni hiyo
ifanyike.Ninataka Mathew
na Austin sasa mkakae na
mjadili kwa kina namna
mtakavyoiendesha
operesheni hii.Kama kuna
kitu chochote ambacho
mnadhani mtakihitaji
kwangu mnijulishe haraka
sana” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais kwa
upande wangu kila kitu
kutuwezesha kufanya
operesheni hiyo
tunacho”akasema Austin
“Sawa Austin.Mathew
tusiendelee kupoteza muda
nataka niwaache wewe na
Austin mkajadili namna ya
kufanya operesheni hii.Mimi
nitaendelea kuwasiliana
nanyi mara kwa mara kujua
maendeleo yenu” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais
ninakushukuru sana kwa
kutupa ruhusa kuifanya
operesheni hii.Nitaendelea
kuwasiliana nawe
kukujulisha kila hatua
tunayopiga.Ninakuhakikishi
a kwamba tutarejea hapa
nyumbani tukiwa na Edger
Kaka.Kama wale jamaa
watakupigia simu jitahidi
kuvuta muda hadi pale
tutakapokuwa
tumerejea”akasema Mathew
“Mathew hili
mnalokwenda kulifanya ni
jambo ambalo linaweza
kuibua mgogoro mkubwa
sana kwanza na majirani
zetu Kenya na pili kwa
marafiki zetu Israel endapo
itagundulika kama ni
sisi,hivyo nawaomba
mjitahidi kufanya kila
linalowezekana kuhakikisha
hakuna chochote
kitakachoweza
kututambulisha kwamba ni
sisi ndio tuliofanya tukio
hilo”akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
ninakuomba ondoa hofu
kabisa kuhusu suala
hili.Tayari tumekwisha
chukua kila tahadhari
kuhakikisha hatujulikani
kama sisi ndio tuliovamia
ubalozi na kumchukua Edger
Kaka.Tunafanya hivi kwa
ajili ya kujilinda sisi
wenyewe na kuilinda nchi
yetu” akasema Mathew
“Kitu kingine ambacho
tunatakiwa kukifanya ni
kujiepusha kuua watu wengi
bila sababu.Kama
inawezekana tujitahidi
kusiwe na idadi kubwa ya
vifo” akasema Dr Evans
“Tutajitahidi mzee
kufuata maelekezo
yako”akajibu Mathew
“Sawa vijana wangu
ninawaachia kila kitu na
ninaamini mtafanya
operesheni hii kizalendo kwa
maslahi mapana ya nchi yetu
na vile vile kusaidia
kuwaokoa watu wetu wawili
Coletha na Olivia.Ninawapa
Baraka zangu na
ninawatakia kila la heri”
akasema Dr Evans na
kusimama akapeana mikono
na akina Mathew wakatoka.
“Mathew tunaelekea
katika kambi yetu ambako
safari itaanzia hapo”
akasema Austin wakaingia
katika gari lake wakaondoka
“Sikujua kama kuna
viongozi ambao wanakuwa
na sura mbili.Machoni
wanaonekana wazalendo
lakini kumbe ndani ni chui
wakali.Nimesikitika sana
kwa taarifa hii niliyoipata leo
kuhusiana na Edger Kaka
kujihusisha na kikundi cha
kigaidi cha IS” akasema
Austin
“Mungu alifanya jambo
kubwa sana la kutuficha
kufahamu mawazo ya
mwenzako vinginevyo
tungekwisha
malizana.Hakuna
aliyetegemea kama Edger
kaka angeweza kujihusisha
na magaidi.Mpaka sasa bado
hatujapata jibu nini hasa
lilikuwa lengo la kuungana
na magaidi hawa?Ni
kujipatia fedha? Majibu haya
yote tutayapata pale
tutakapomtia mikononi”
akasema Mathew na safari
ikaendelea hadi walipofika
katika kambi ya kikosi cha
jeshi kinachoshughulika na
operesheni maalum.Ilikuwa
ni mara ya kwanza Mathew
kuingia katika kambi hii
nzuri.Austin akamuongoza
wakaenda hadi katika
chumba cha mipango ambako
kulikuwa na watu sita,wote
walisimama na kutoa
heshima kwa mkuu wao
halafu wakakaa. Kuta za
chumba hiki zilijazwa
runinga kubwa zenye
kuonyesha picha mbali
mbali.Kulikuwa na
kompyuta nyingi na mitambo
mbali mbali
“Gentlemen tumepata
mgeni lakini huyu si mgeni
wa kawaida ni mgeni
maalum kabisa anaitwa
Mathew Mulumbi.Huyu ni
mmoja kati ya majasusi nguli
kabisa kuwahi kutokea hapa
nchini kwetu na yuko hapa
kwa sababu maalum hivyo
msishangae kwa mara ya
kwanza mtu ambaye si
mwanajeshi kuingia katika
chumba hiki.Huyu ni
mwenzetu katika ulinzi wa
taifa” akasema Austin na
kumtambulisha Mathew
wale makamanda
waliokuwemo mle ndani.
“Nilipigiwa simu na Rais
jana usiku akanipa
maelekezo niandae kikosi
cha watu kumi kwa ajili ya
operesheni ambayo
atanifahamisha pale muda
utakapofika.Nilifanya kama
alivyonielekeza na usiku huu
ameniita ikulu na
kunifahamisha kwamba ile
operesheni ambayo alinitaka
niandae kikosi inakwenda
kufanyika usiku huu.Mathew
Mulumbi ambaye ndiye
kiongozi wa operesheni hiyo
maalum atawafafanulia
zaidi.Karibu Mathew”
akasema Austin
“Ahsante Austin.Miaka
mitatu iliyopita Israel kwa
kutumia shirika lake la
ujasusi la Mossad walifanya
operesheni ya siri hapa
nchini wakafanya mauaji na
kumteka raia wetu ambaye
alikuwa mbunge wa bunge la
jamhuri ya muungano wa
Tanzania anayeitwa Edger
Kaka.Walitengeneza ajali
ambayo ilituaminisha wote
kwamba Edger kaka
amefariki dunia lakini
kumbe haikuwa kweli.Edger
Kaka yuko hai na amefichwa
katika ubalozi wa Israel
nchini Kenya.Baada ya
kupata taarifa hizo za Edger
kaka kuwa hai tulifanya
uchunguzi wa kutosha
kujiridhisha kama taarifa
hizo ni za kweli na mapema
usiku huu wa leo timu
ambayo niliitanguliza
Nairobi kufanya uchunguzi
wa jambo hilo imepata
majibu”akasema Mathew na
kuiwasha kompyuta yake
ambayo ikaunganishwa na
picha za video ambazo
walizipata Devotha
alipoingia ndani ya ubalozi
wa Israel jijini Nairobi
kuonana na Edger Kaka
zikaanza kuonekana katika
runinga kubwa ukutani.
“Mmoja wa watu wangu
walioko Nairobi alifanikiwa
kuingia ndani ya ubalozi wa
Israel jijini Nairobi akiwa
amevaa kamera ya siri na
hizi ndizo picha tulizozipata
kutoka katika kamera
hiyo.Huyo anayeonekana
pichani ndiye Edger Kaka
raia wa Tanzania
anayeshikiliwa mateka na
Israel katika ubalozi wake
nchini Kenya” akasema
Mathew na baada ya wale
makamanda kuitazama video
ile mmoja wao akauliza
“Kwa nini Israel
wakamteka nyara mbunge
wetu na kwenda kumficha
Kenya?
“Kuna maelezo marefu
kidogo hapo lakini kwa ufupi
tu kuokoa muda ni kwamba
Edger Kaka ana mahusiano
na watu ambao wanafadhili
kikundi cha kigaidi cha IS na
vikundi vingine vya
wanamgambo wa kipalestina
ambavyo vimeendelea
kufanya mashambulizi
katika ardhi ya Israel na
kuua watu.Walimteka Edger
ili awasaidie kuwapa taarifa
za namna ya kuwapata watu
hao lakini mpaka leo hii
Edger hajafunguka chochote”
akajibu Mathew
“Hii ni taarifa ya
kushangaza sana.Mbunge wa
Tanzania anajihusisha na
kundi la kigaidi.Kwa nini
vyombo husika vya
uchunguzi havikuweza
kumbaini?akauliza mwingine
“Hilo ndilo swali ambalo
tunalitafutia majibu lakini
inaonekana hayuko peke
yake kuna mtandao wao
hapa nchini na inaonekana
kuna watu wapo hadi ndani
ya serikali ndiyo maana
imekuwa vigumu kwa Edger
kaka kujulikana”akajibu
Mathew
“Misheni yetu ni nini
hasa?akauliza mwingine
“Misheni yetu
tunakwenda Nairobi
kumchukua raia wetu Edger
kaka anayeshikiliwa mateka
katika ubalozi wa Israel
nchini Kenya”
“Wow ! It’s more than a
mission.It’s a war” akasema
mmoja wao
“They started this
war.Waliingia nchini kwetu
wakaua raia na kuteka hivyo
tunachofanya sisi ni kwenda
kumkomboa raia wetu
anayeshikiliwa mateka na
njia pekee ya kumkomboa
raia wetu ni kwa kuvamia
ubalozi huo.Makamanda hii
ni operesheni ya siri sana na
mpaka sasa hivi serikali ya
Israel haifahamu chochote
kuhusiana na operesheni hii
tunayokwenda kuifanya na
wala hawajui kama tayari
tunafahamu kuwa Edger
Kaka yuko hai na
anashikiliwa katika ubalozi
wao.Jambo hili ni kubwa
ndugu zangu lakini naomba
nisitumie muda mwingi
kuwaeleza kwani kweni ninyi
kubwa ni operesheni
inayokwenda kufanyika
usiku wa leo.Tayari tunayo
ramani ya jengo hilo lilivyo
na mfumo wote wa ulinzi
tunaufahamu hivyo
operesheni yetu haiutakuwa
ngumu” akasema Mathew na
kuwafungulia ramani ya
jengo la ubalozi wakaitazama
kimya kimya
“Hiyo ndiyo ramani ya
jengo la ubalozi wa Israel
nchini Kenya lakini Edger
Kaka yuko chini ya jengo
hili” akasema Mathew
“Kwa namna jengo hili
lilivyokaa” akasema Austin
“Tunahitaji kujigawa
katika timu mbili.Timu ya
kwanza ambayo itakuwa ni
Oscar team wataingia kwa
juu na kulidhibiti jengo
kutokea juu na timu ya pili
ambayo itajulikana kama
Mike team wao wataingia
kwa kupitia lango kuu na
kuidhibiti sehemu yote ya nje
ili kuwapa nafasi Oscar team
watakaopitia juu ya jengo
kuweza kuigia ndani na
kumchukua mateka
wetu.Mathew una timu ya
watu wangapi kule
Nairobi?akauliza Austin
“Ninao watu
watatu”akajibu Mathew
“Ni
wapiganaji?Wanaweza
wakaungana na timu yetu
itakayopita upande wa
chini?akauliza Austin
“Wawili ni
wanajeshi.Mmoja alikuwa
komandoo wa jeshi na
mwingine amepigana vita
vya msituni nchini Congo
kwa muda mrefu wa mwisho
ni mwanamke ambaye ndiye
tuliyemtumia ku….”
Akasema Mathew lakini
Austin akamkatisha
“I’m sorry Mathew we
don’t include women in our
missions.Si kwamba ni
ubaguzi lakini ni kutokana
na aina ya mafunzo
tunayoyapitia ambayo kwa
mwanamke inakuwa ngumu
hivyo tutawajumuisha katika
Mike team hao wanajeshi
wawili lakini huyo
mwanamke
hatutamjumuisha” akasema
Austin
“Austin this woman is
not just a woman ni
mpiganaji hatari.Anatakiwa
kujumuishwa katika kikosi
na baada ya operesheni
kukamilika wote wanarejea
nyumbani hakuna
atakayebaki nyuma hivyo
basi kwa mara ya kwanza
itawalazimu kwenda nje ya
taratibu zenu na
kumjumuisha mwanamke
katika misheni.Msiwe na
hofu ninamuamini Devotha”
akasema Mathew
“If you trust her it’s fine
lakini sisi tuna taratibu moja
tuwapo katika misheni kama
kuna mmoja kati yetu
ambaye anaonekana kutaka
kuwa mzigo na kuharibu
misheni tunamuua hapo
hapo na kama huyo
mwanamke ataonekana
kuwa mzigo kwetu nasikitika
kwamba hatutakuwa na
namna nyingine zaidi ya
kumuua” akasema Austin.
“Hakuna tatizo sina
shaka kabisa na Devotha”
akasema Mathew
“Good.Oscar team ambao
watapitia juu watakuwa
watu saba na Mike team
ambao itawajumuisha pia na
watu wako walioko Nairobi
itakuwa na watu nane jumla
tutakuwa watu kumi na
tano.Mathew naomba
ufahamu kwamba watu
wangu wana mafunzo ya hali
ya juu mno na usiwe na wasi
wasi wowote.Nitaongoza
Mike team na wewe
utaongoza Oscar
team.Tutatumia helkopta
tatu zinazotumia teknolojia
ya hali ya juu sana ambazo
hazina mlio kama helkopta
nyingine na sifa yake
nyingine haziwezi kuonekana
katika rada.Lakini kuna
jambo linatakiwa
lifanyike.Umeme unatakiwa
kukatika katika eneo lote la
kuzunguka jengo la ubalozi
ili ndege zetu zisionekane
wakati zikitua.Tutakuwa
tumevaa miwani ya kuonea
gizani na mavazi ambayo
yatatufanya tusionekane kwa
urahisi” akasema Austin
“Hilo la umeme tayari
nimekwisha litolea
maelekezo na mmoja kati ya
watu wangu walioko Nairobi
analishughulikia hilo.Swali
la kujiuliza hapa ni vipi
watakuwa na jenereta la
dharura wakaliwasha?
akasema Mathew
“Tutakapokuwa tayari
tumekaribia jengo
tutamjulisha huyo mtu wako
na umeme ukikatika
helkopta ya Oscar team
itatua juu ya jengo na kama
kutakuwa na jenereta la
dharura basi kazi ya kwanza
itakayofanyika itakuwa ni
kuliharibu ili kulifanya eneo
liendelee kuwa na giza na
kuwapa Mike team nafasi ya
kutua.Hii haitachukua
dakika tano.Watu wako
watakao ambatana na Mike
team wanapaswa kuandaa
sehemu ya wenzao
kutua.Baada ya kutua
itarushwa angani kamera
ambayo itakuwa
inalizunguka jengo lote na
watu wa Dar es salaam
wataweza kuangalia kila kitu
kinachoendelea nje ya jengo
kupitia kamera hiyo na
watatujulisha kama kuna
hatari yoyote inakaribia eneo
hilo.Mike team
tutahakikisha tunalidhibiti
eneo la nje ka haraka sana ili
ninyi muweze kupata nafasi
nzuri ya kumchukua Edger
Kaka.Unauonaje huo
mpango?akauliza Austin
“Mpango ni mzuri hata
mimi nilikuwa ninafikiria
hivyo hvyo kama
ulivyopanga” akasema
Mathew kisha wakaendelea
kuchambua ramani ile na
kuweka mikakati zaidi
namna watakavyoweza
kutekeleza operesheni yao.
“Mathew nafahamu
wewe na timu yako mnayo
ofisi yenu na pamoja na
taratibu zenu za kufanya
operesheni mbali mbali
lakini hii ni operesheni ya
kijeshi hivyo inapaswa
kuongozwa kutokea hapa na
tukishaikamilisha
tutawakabidhi mtu wenu
nanyi mtaendelea na
taratibu zenu
wenyewe.Nadhani
hakutakuwa na tatizo katika
hilo”akasema Austin
“Hakuna tatizo
Austin.Haijalishi operesheni
inaongozwa kutoka wapi
kikubwa ni
kuikamilisha.Hata hivyo
kuna mtu wangu mmoja
ningeomba aje kuungana
nanyi hapa katika kuongoza
operesheni hiyo” akasema
Mathew
“Mathew utanisamehe
ndugu yangu kwa taratibu
zetu hapa mtu ambaye si
mwanajeshi au hahusiki kwa
namna yoyote na kikosi hiki
haruhusiwi kuingia katika
chumba hiki hata wewe
mwenyewe uko hapa kwa
agizo la Rais vinginevyo
usingekuwa eneo hili.Hii ni
sehemu nyeti sana kuna
mambo mengi yanayofanyika
ya kiulinzi ndani ya chumba
hiki ambayo tunaopaswa
kuyafahamu ni sisi pekee
wahusika” akasema Austin
“Ninalifahamu hilo
Austin lakini ninakuomba
umkubali huyo mwanadada
ninayekwambia.Anaitwa
Ruby ninamuita mchawi wa
kompyuta na mambo yote ya
kielektroniki.Ni mtu ambaye
naamini tunamuhitaji sana
awepo katika chumba cha
kuongozea operesheni kwa
usiku huu” akasema Mathew
“Mathew..” Austin
akataka kusema kitu lakini
Mathew akamkatisha
“Austin tafadhali ndugu
yangu,Ruby ninamuamini
sana na ninakuhakikishia
kwamba msaada wake ni
mkubwa.Vile vile ninataka
awepo hapa kwa ajili ya
usalama wake amenusurika
kuuawa kwa risasi na siwezi
kukubali tena akauawa.Ni
mtu mtu muhimu sana
kwangu” akasema Mathew
.Austin akafikiri kidogo
halafu akasema
“Sawa hakuna tatizo
tutaruhusu aje hapa lakini
hatajihusisha na kitu
chochote hadi pale msaada
wake utakapohitajika.Ninayo
timu ya kutosha yenye ujuzi
mkubwa wa mambo haya na
wamekuwa wakiongoza
operesheni mbali mbali kwa
miaka mingi.”
“Ahsante sana
Austin.Kabla ya kwenda
kuzungumza na makamanda
wako nataka tuzungumze na
timu iliyoko Nairobi
kuwajulisha kuhusu mipango
ya operesheni na kitu
wanachotakiwa kukifanya”
akasema Mathew na kupewa
simu maalum ili aweze
kuwasiliana na watu wake
kwani ukiwa eneo lile
huruhusiwi kutmia simu za
kawaida za mkooni bali zipo
simu maalum.Mathew
akaandika namba na
kumpigia Tino
“Hallow” akasema Tino
baada ya kupokea simu
akiwa hajui nani aliyempigia
“Tino it’s me
Mathew.Mnaendeleaje hapo?
“Tunaendelea
vyema.Tayari tumekwisha
rejea hotelini tumejianda
tunasubiri maelekezo yako”
akasema Tino
“Kama nilivyowaeleza
kwamba operesheni
itafanyika usiku wa
leo.Nimetoka ikulu
kujadiliana na Rais kuhusu
operesheni ya usiku wa leo
ametoa baraka zake ifanyike
na amenikabidhi kwa mkuu
wa kikosi cha jeshi
kinachohusika na operesheni
maalum ambaye amenileta
katika kambi yao tumejadili
kwa mapana namna
tutakavyotekeleza
operesheni yetu”akasema
Mathew na kumpa Tino
maelekezo yote
wanayotakiwa kuyafanya
“Upande wa timu ya
Nairobi hakuna tatizo sasa
tukazungumze na vijana
wako” akasema Mathew
wakaelekea katika chumba
cha mikutano ambako
waliwakuta watu kumi na
mbili wote wakasimama
baada ya kumuona mkuu
wao,akawataka waketi
“Toka jana niliwataka
mfanye mazoezi makali kwa
ajili ya operesheni
maalum.Namini tayari
mmekwisha jiandaa vya
kutosha.Usiku wa leo
tutakuwa na operesheni
maalum.Kabla sijawaeleza
kile tunachokwenda
kukifanya usiku wa leo
nataka niwatambulishe
kwenu mgeni niliyekuja naye
anaitwa Mathew Mulumbi ni
mmoja kati ya majasusi nguli
kabisa kuwahi kutokea hapa
nchini.Yeye ndiye kiongozi
wa operesheni hii na
nitamuomba awafafanulie
kwa ufupi umuhimu wa
operesheni ya usiku wa leo”
akasema Austin na bila
kupoteza muda Mathew
akasema
“Miaka mitatu iliyopita
Israel kupitia shirika lake la
ujasusi la Mossad walifanya
operesheni ya siri hapa
nchini na kuua watu kadhaa
kisha wakamchukua mateka
mbunge wa bunge la jamhuri
ya muuungano wa Tanzania
na kutuaminisha kwamba
mbunge huyo aliyejulikana
kama Edger Kaka amefariki
katika ajali
waliyoitengeneza.Jambo hili
limekuwa siri kubwa hadi
hivi majuzi tulipogundua
kwamba Edger Kaka raia
wetu aliyetekwa yuko hai na
amefichwa katika ubalozi wa
Israel nchini Kenya.Edger
Kaka anatajwa kuwa na
mahusiano na wafadhili
wakuu wa vikundi vha
kigaidi kama vile IS na
vikundi vingine vya
wanamgambo ambavyo
vinaendesha mashambulizi
na kuua watu katika ardhi
ya Israel na hii ndiyo sababu
ambayo Israel walimteka ili
aweze kuwapa taarifa
zitakazosaidia kuwapata
wafadhili hao wa ugaidi
ambao wamekuwa
wakitafutwa kwa miaka
mingi.Japokuwa ana
mahusiano na magaidi lakini
bado ni raia wetu ambaye
ametekwa hivyo basi
tunakwenda usiku wa leo
kumchukua Edger Kaka na
kumrejesha nyumbani.Ni
operesheni ya siri ambayo
tunataka baada ya
kuikamilisha serikali ya
Kenya wala Israel
wasigundue kama ni sisi ndio
tuliofanya uvamizi huo
katika ubalozi wa
Israel.Maandalizi ya kutosha
yamekwisha fanyika
kutuwezesha kuikamilisha
operesheni hii. Mimi na
mkuu wenu Austin
tumejipanga vyema
kuhakikisha kwamba
tunawalinda nyote na
mnarejea nyumbani
salama.Hakuna atakayebaki
nyuma awe
mzima,amejeruhiwa au
amekufa.” akasema Mathew
na kumuachia Austin
aendelee kutoa maelekezo
“Nadhani mmesikia
tunachokwenda kukifanya
usiku wa leo.Tutajigawa
katika timu mbili timu Oscar
na timu Mike.Timu Oscar
itaongozwa na Mathew na
timu Mike itaongozwa na
mimi.Oscar team wataingia
ndani ya jengo kwa kupitia
upande wa juu na Mike team
tutaingia kwa kutumia lango
kuu ili tuweze kulidhibiti
jengo kwa nje” akasema
Austin na kutoa maelekezo
ya kile kinachotakiwa
kufanywa usike ule katika
operesheni.Baada ya kutoa
maelekezo Mathew
akalazimika kuondoka
kwenda kumchukua Ruby
“Mambo yamekwendaje
huko?akauliza Ruby mara tu
Mathew aliporejea katika
makazi waliypopewa na Rais
“Mambo yamekwenda
vizuri.Kila kitu tayari
kimeandaliwa nimekuja
kukuchukua unahitajika
sehemu Fulani” akasema
Mathew na kumfafanulia
Ruby kila kitu.Ruby hakuwa
na tatizo akakubali
kuongozana na Mathew
kwenda katika kambi ya
kikosi cha operesheni
maalum.
Saa saba na dakika moja
za usiku helkopta ya kwanza
iliyowabeba wanajeshi wa
kikosi maalum ikapaa na
kuondoka kuelekea
Nairobi.Hawa walikuwa
Oscar team wakiongozwa na
Mathew Mulumbi ambaye
usiku huu naye alikuwa
amevaa sare za kikosi hiki na
mkononi akiwa na bunduki
kubwa.Baada ya dakika tatu
helkopta ya pili iliyobeba
team Mike wakiongozwa na
Austin nayo ikapaa ikaelekea
Nairobi.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 3
Simu ya Rais iliyokuwa
katika mfuko wa koti lake
ilianza kutetema kuashiria
kuna mtu anapiga.Alikuwa
amepumzika sebuleni kwake
akiwa mchovu na mwenye
mawazo mengi.Akaitoa simu
ile na kutazama mpigaji
akahisi mwili wote
unaingiwa baridi.Aliogopa
kuipokea.Zilikuwa ni zile
namba zinzotumiwa na wale
magaidi waliomteka
mwanae.Aliitazama simu
ikiita na kukatika
“Ni wenyewe
wanapiga,naogopa hata
kuipokea simu yao” akawaza
Dr Evans na mara simu ile
ikaanza kuita tena.Kabla
hajaipokea akachukua simu
nyingine akapiga namba za
Mathew lakini simu yake
haikuwa ikipatikana
“Ngoja niipokee nisikie
wanachokitaka” akawaza Dr
Evans na kuipokea ile simu
“Hallow” akasema
“Mheshimiwa Rais
habari za usiku huu.Ni mimi
Yule rafiki yako nimekupigia
tena ili tuzungumze”
“Kabla ya yote nataka
kuhakikisha kama
mwanangu yuko salama”
akasema Dr Evans
“Mwanao ni mzima hana
tatizo lolote anaendelea
vyema” akajibu Yule jamaa
“Ili mimi na ninyi tuweze
kuzungumza nataka
unihakikishie kwanza kama
mwanangu yuko hai na
anaendelea vyema kwa
sababu mlimchukua akiwa
mgonjwa” akasema Dr Evans
“Naomba dakika mbili”
akasema Yule jamaa na
kukata simu.Dr Evans
akavuta pumzi ndefu na
kuchukua kitambaa akafuta
jasho
“Hawa jamaa
wamenitikisa sana.Hakuna
kitu kinachoniumiza kama
wanavyocheza na uhai wa
mwanangu.Ngoja niwe
mvumilivu kama
alivyoshauri Mathew”
akawaza Dr Evans na simu
ikaita tena akaipokea na
kumshuhudia mwanae
Coletha akiwa kitandani
amekaa anasoma
kitabu.Afya yake ilionekana
kuimarika
“Coletha my queen
nitatumia kila njia
kuhakikisha ninakutoa
katika mikono ya hao
magaidi.Ninaamini
hawataweza kukuua kama
alivyosema Mathew”akawaza
Dr Evans kwa sauti ndogo na
video ile ikakatwa baada ya
sekunde kadhaa simu y
akaaida ikapigwa akaipokea
“Mheshimiwa Rais
naamini sasa umepata
uhakika kuwa mwanao yuko
hai na yuko salama hivyo
tunamuhudumia vizuri
sana.Sasa tunaweza
kuendelea na maongezi yetu”
akasema Yule jamaa
“Nini mnakitaka
tena?Nimekwisha wapatia
Olivia mnataka nini kingine?
Akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais kuna
kitu kingine tunakitaka
kutoka kwako”
“Sema mnataka nini?
“Tunamtaka Edger
Kaka” akasema Yule gaidi na
Dr Evans akatoa kicheko
kidogo
“Mheshimiwa Rais
usicheke tafadhali hili ni
jambo zito
sana.Tunamuomba Edger
Kaka na sisi tutakurejeshea
mwanao”
“Niwaambie lugha gani
mnielewe ninyi watu? Edger
Kaka hayuko hai amekwisha
fariki miaka mitatu iliyopita
na mimi si Mungu sina
uwezo wa kumfufua na
kuwakabidhi”
“Mheshimiwa Rais
tunafahamu kuwa Edger
kaka hajafariki dunia bali
wewe na watu wako
mlitengeneza ajali ili
kudanganya wananchi
kwamba Edger amefariki
dunia kumbe yuko mahala
amefichwa.Tunamuomba
tafadhali.Ukitukabidhi
tunakuhakikishia
mheshimiwa Rais kwamba
tutakurejeshea
mwanao”akasema Yule gaidi
“Edger Kaka amekufa na
hakuna namna ya
kumrejesha tena duniani na
hata kama angekuwa hai
nisingeweza kumkabidhi
kwenu kwani ni msaliti kwa
taifa na angestahili adhabu
kali sana kwa kitendo cha
kushirikiana na magaidi !
akasema Dr Evans kwa ukali
kidogo
“Mheshimiwa Rais
nakuomba tafadhali
utekeleze hilo tunalokutaka
na tunatoa muda hadi kesho
saa mbili za asubuhi uwe
umemuandaa Edger
Kaka.Nitakupigia simu saa
mbili kamili za asubuhi na
kukupa maelekezo zaidi
mahala pa kumpeleka na
namna utakavyompata
mwanao” akasema Yule
jamaa
“Naombeni mnisikilize
vizuri nyie watu na fikisha
ujumbe huu kwa wakubwa
zako kwamba sintafanya
tena makubaliano yoyote na
ninyi.Tanzania haifanyi
majadiliano na magaidi na
ninakuhakikishia kwamba
nitawasaka kokote mliko na
kumchukua mwanangu !!
akasema Dr Evans kwa
ukali.Ukapita ukimya wa
sekunde kadhaa Yule mtu
simuni akasema
“Rudia tena kauli yako
mheshimiwa Rais sijakusikia
vizuri !
“Ninaomba unisikie
vizuri.Nimesema sintafanya
majadiliano tena na
ninyi.Tanzania hatufanyi
majadiliano na magaidi bali
tunawafyekelea mbali.Damu
mliyomwaga ya watu wasio
na hatia inatosha na sasa
inafuata zamu
yenu.Ninatangaza vita na
ninyi na ninawahakikishia
kwamba nitampata
mwanangu akiwa mzima na
kitakachowatokea kitakuwa
ni historia kwenu na kwa
vizazi vyenu.Umenipa hadi
saa mbili za asubuhi niwe
nimemrejesha Edger Kaka
na mimi ninawapa hadi
muda huo muwe
mumemrejesha mwanangu
ama sivyo nitawachapa
kichapo kitakatifu” akasema
Dr Evans kwa ukali
“Mheshimiwa Rais
kwanza kabisa nataka
kukusahihisha kwamba
hatujamwaga damu
Tanzania.Bado hakuna damu
iliyomwagika.Umekosea sana
kwa hiki ulichokitamka
kwamba unatangaza vita na
sisi.Kwa kauli hiyo
umetulazimsha tufanye kile
ambacho hatukuwa
tumetaka kukifanya.Kwa
kuwa umekuwa
kiburi,hatuna budi
kukulazimisha ufanye kile
tunachokutaka ukifanye na
hapo ndipo utakapoiona
damu halisi
ikimwagika.Mheshimiwa
Rais vita yetu ni vita takatifu
ya vizazi hadi vizazi na
ninarudia tena umekosea
sana kutangaza vita na sisi”
Dr Evans akiwa amefura
kwa hasira akasema
“Mnadhani ninaogopa
hata mkitishia kumuua
mwanangu? Fanyeni kile
mnachotaka kukifanya lakini
mjue kwamba siku zenu
zinahesabika.Mpaka saa
mbili asubuhi kesho nataka
unipigie simu unijulishe
alipo mwanangu ama
vinginevyo mjiandae!
Akasema Dr Evans na
kukata simu
“I need my pills.Naona
hali imebadilika” akawaza
Dr Evans na kuchukua kopo
dogo lenye dawa akatoa mbili
akameza
“Nimetangaza vita na
magaidi na kwa kufanya hivi
nimeyaweka mashakani
maisha ya mwanangu
Coletha.Sifahamu magaidi
hawa watamfanya nini lakini
sina hakika kama wataweza
kumuua.Hata hivyo
nimefanya vyema kuonyesha
msimamo vinginevyo kama
ningewakubalia kila kitu
wanachokisema wangeweza
kunitaka hata niachie
urais.Mathew amenifanya
niwe jasiri sana kabla
sijakutana naye sikuwa na
ujasiri wa kuweza
kuzungumza na magaidi na
kuwatisha kama nilivyofanya
leo.Naamini muda huu
watakuwa angani wakielekea
Nairobi kumchukua Edger
kaka nawaombea wafanikiwe
kumpata” akawaza Dr Evans
na kujifuta jasho usoni
“Kinachofuata sasa ni
kuhakikisha ulinzi
unaimarishwa kila sehemu
zenye mikusanyiko mikubwa
ya watu kwani magaidi hawa
wanaweza wakafanya
shambulio sehemu yoyote ile
hasa zenye mikusanyiko
mikubwa ya watu” akawaza
Dr Evans na kumpigia simu
waziri wa mambo ya ndani
Deus Mkuza
“Deus nimekupigia simu
usiku huu kuna maelekezo
ninataka yafanyiwe kazi
haraka sana”
“Nakusikiliza
mheshimiwa Rais” akasema
waziri Deus Mkuza
“Kuna vitisho vya
kutokea kwa mashambulio
zaidi ya kigaidi hapa nchini
vikifanywa na wale wale
waliofanya shambulio la
Mtodora.Ninataka kuanzia
sasa ulinzi uimarishwe
katika sehemu zote zenye
mkusanyiko mkubwa wa
watu katika vituo vya
mabasi,mahoteli,maduka
makubwa,misikiti ,makanisa
na kokote kule ambako idadi
kubwa ya watu
wanakusanyika kwa wakati
moja.Sitaki shambulio
lingine litokee wakati tayari
vipo viashiria vya kuonyesha
kwamba kuna shambulio
lingine linapangwa.Nataka
maelekezo haya yafanyiwe
kazi haraka sana kuanzia
usiku huu”akasema Dr
Evans
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais ninatoa
maelekezo hayo kwa jeshi la
polisi sasa hivi” akasema
waziri Deus
“Ahsante Deus.Usiku
mwema” akasema Dr Evans
na kukata simu
“Lazima kila jitihada
ifanyike kuhakikisha
kwamba IS wanadhibitiwa
wasifanye shambulio lingine
hapa nchini.Nilifanya
makosa makubwa kutekeleza
takwa lao la kuwapa Olivia
kama si Mathew kutokea na
unifumbua macho
wangeniendesha sana
washenzi wale.Kwa sasa sina
hofu tena nitakabiliana nao
kwa kila nguvu
niliyonayo.Naamini akina
Mathew watakuwa
wamerejea kabla ya saa mbili
za asubuhi kesho,tutakaa na
kujadiliana namna ya
kufanya kukabiliana na
hawa magaidi.Hii vita lazima
tushinde” akawaza Dr Evans
Jijini Nairobi,Fahad
ambaye alikuwa
anawasiliana na Rais Dr
Evans alipandwa na hasira
kali baada ya Dr Evans
kukata simu.
“Nadhil ! akafoka Fahad
“Kuna nini Fahad mbona
umebadilika hivyo?akauliza
Rashid
“Rais amebadilika
ghafla.Sikutegemea kama
angeweza kubadilika namna
hii.Rais niliyezungumza naye
sasa hivi si Yule ambaye
nilizungumza naye awali
ambaye alikuwa na sauti
yenye woga akiwa tayari
kutekeleza kila
tutakachomuamuru,lakini
usiku huu amekuwa na sauti
yenye ujasiri ,ukali na
haonyeshi kuogopa kitu
tena.Amediriki hata
kutamka kwamba
anatangaza vita na sisi na
ametupa hadi kesho saa
mbili za asubuhi tuwe
tumemrejesha mwanae ama
sivyo atatufyekelea mbali”
akasema Fahad na Rashid
akalazimika kutoa kicheko
kidogo
“Ni Rais wa Tanzania Dr
Evans ndiye aliyetamka
maneno hayo au kuna mtu
mwingine aliyejifanya Rais?
“Ni yeye mwenyewe.Hata
mimi nimeshangaaa
sana.Ametoa wapi ujasiri wa
kutamka maneno kama
haya?akauliza Fahad
“Nilijaribu kumsihi
asitamke maneno kama yale
kwani yatakuwa na athari
kubwa sana kwa nchi yake
lakini hakutaka kunisikia na
badala yake akatoa vitisho
na kikubwa zaidi haonyeshi
kujali tena kuhusu mtoto
wake kutekwa” akasema
Fahad
“Nini maamuzi yako
baada ya kauli yake? Tuvute
subira labda atabadili
mawazo?akauliza Rashid
“Hatabadili mawazo
badala yake ataendelea na
juhudi za kutusaka kama
alivyoahidi”
“Nini basi unashauri
kifanyike?Rashid akauliza
“yurid alharb ,
falanuqatil alharb”akasema
Fahad kwa lugha ya kiarabu
akimaanisha “ametaka vita
twendeni tukapigane”
“Twendeni
tukamuonyeshe kwamba IS
tupo Tanzania na tunao
uwezo wa kufanya chochote
tukiamua.Ametulazimisha
yeye mwenyewe tumwage
damu na sasa damu
inakwenda kumwagika”
akasema Fahad ambaye
alikuwa na hasira kali
“Nini unakifikiria Fahad
kitakachomfanya Rais atii
maelekezo yetu?akauliza
Rashid.Fahad akafungua
sehemu anakohifadhi majina
katika simu yake akatoka nje
akazungumza na mtu Fulani
kwa zaidi ya dakika kumi
halafu akarejea ndani
akitabasamu
“Tayari nimepata
suluhisho.Kuna shule moja
ya wasichana iko nje kidogo
ya jiji inamilikiwa na kanisa
inaitwa St Getrude
secondary school.Ni moja
kati ya shule bora kabisa
Tanzania.Tunavamia shule
hiyo usiku wa leo na
kuwachukua mateka baadhi
ya wasichana na kuwapeleka
mafichoni halafu
tutazungumza tena na Rais
tuone kama ataendelea kuwa
kiburi.Tutampa Rais muda
wa kutekeleza maelekezo
yetu na kama akipuuza
tutaanza kuua mwanafunzi
mmoja baada ya mwingine
huku wananchi
wakishuhudia kupitia simu
zao na hiyo itasaidia sana
kumpa Rais shinikizo aweze
kutekeleza kile
tunachokitaka.Wananchi
lazima watashikwa na hasira
wakiona watoto wao
wanachinjwa kama kuku
hawatakaa kimya lazima
wataitaka serikali kufanya
kila wawezalo kuwakomboa
watoto na Rais atakuwa
ndani ya shinikizo kubwa
hivyo lazima atatekeleza kile
tunachokitaka.Kwa njia hii
tutaua ndege wawili kwa
jiwe moja,tutampata Edger
Kaka na tutamuondoa Rais
madarakani kwani
tutahamasisha maandamano
yasiyokwisha ya kumtaka
Rais aachie madaraka na
kisha tutamuweka
madarakani mtu wetu”
akasema Fahad
“Fahad hili ni suala zuri
lakini linahitaji maandalizi
ya kutosha ili
kulitekeleza”akasema Rashid
“Hatuna muda wa
kujiandaa Rashid.Tunao
vijana ambao wako tayari
kwa kazi muda wowote
watakapopewa maelekezo na
hii ndiyo faida ya
kutengeneza
mtandao.Tunayo timu ya
kutosha Dar es salaam
ambao wanatosha kabisa
kuifanya kazi hii usiku wa
leo.Hakuna mtu
anayetegemea tukio kama
hilo kutokea na
tutawastukiza usiku wa
manane wakiwa wamelala
tutavamia na kuchukua
wasichana na kuondoka
nao.Huu utatumika kama
moja ya mpango wa
kumuweka mtu wetu
madarakani.Tulishindwa
kwa Edger Kaka lakini safari
hii hatuwezi kushindwa
tena”akasema Fahad
“Kuna ulazima wa
kumjulisha mama Habiba
kabla hatujafanya jambo
hilo?akauliza Rashid
“Habiba alitukabidhi sisi
kazi tuhakikishe tunafanya
kila tunaloweza kumpata
Edger Kaka hivyo hakuna
ulazima wa kupata Baraka
zake kwa kila
tunachokifanya.” akasema
Fahad.
NAIROBI – KENYA
Helkopta ya kwanza
iliyowabeba Oscar team
wakiongozwa na Mathew
Mulumbi ilivuka anga la
Tanzania na kuingia anga la
Kenya.Ilipata saa tisa na
dakika kumi za usiku.Kwa
kuwa helkopta hizi
zilitengenezwa kwa
teknolojia ya hali ya juu ya
kutoonekana kwenye rada
haikuweza kugundulika
ilipoingia katika anga la
Kenya. “Tino tayari
tumeingia katika anga la
Kenya” Mathew akamjulisha
Tino
“Sisi huku tunawasubiri
mtakapofika jijini Nairobi
mtatujulisha ili kazi ianze
mara moja” akasema Tino.
Baada ya kufika katika
jiji la Nairobi Mathew
akampigia simu Tino
akamjulisha kwamba tayari
wamekwisha fika katika jiji
la Nairobi na walikuwa
tayari kuelekea katika jengo
la ubalozi wa Israel
Mara tu Tino alipopokea
taarifa kutoka kwa Mathew
kuwa wamekwisha fika
katika jiji la Nairobi Tino
akapiga namba Fulani katika
simu yake na dakika mbili
baadae umeme ukazima
katika jiji zima la Nairobi
.Wakiwa angani akina
Mathew waliweza
kushuhudia namna umeme
ulivyokatika
“Kila kitu kimekwenda
kama tulivyotaka sasa kazi
inaanza” akasema Mathew
na helkopta ile ikaelekezwa
katika jengo la ubalozi wa
Israel.Kulikuwa giza lakini
helkopta ile ilikuwa na
teknolojia ya hali ya juu mno
ya kumuwezesha Rubani
kuona na kutua salama
sehemu anakotakiwa
kutua.Wakati helkopta ya
team Oscar ikikaribia kutua
juu ya jengo la ubalozi wa
Israel,helkopta iliyowabeba
team Mike ilijiandaa kutua
katika sehemu ya nje ya
ubalozi huo na Tino
akatakiwa kutoa
ishara.Akavua shati na
kulichoma moto na ishara ile
ikaonekana kisha moto ule
ukazimwa na helkopta ile
ikaanza kushuka na
ilipokaribia chini Austin na
kundi lake wakashuka kwa
kutumia kamba kisha
helkopta ikapaa.
Bado jiji zima la Nairobi
lilikuwa giza.Mike team
walijipanga na kulikaribia
geti kuu la kuingilia ndani ya
ubalozi.Wote walikuwa na
miwani maalum ya
kuwasaidia kuona kwenye
giza.Katika geti kuu walinzi
wawili walikuwa wamekaa
katika viti wakizungumza
mmoja akivuta sigara huku
bunduki zao wakiwa
wameziweka
mapajani.Wawili
walionekana wakiwa
wamelaza vichwa vyao
katika meza na kofia zao
zikiwa pembeni hawakuwa
na habari kama kulikuwa na
watu wakiwatazama bila wao
kuwaona.Ilikuwa ni
operesheni inayokwenda kwa
muda maalum hivyo
hakukuwa na muda wa
kupoteza.Tayari walinzi wale
wote walikwisha lengwa na
bunduki kubwa za team
Mike zilizofungwa viwambo
vya kuzuia risasi.Austin
akatoa ishara na risasi
mfululizo kutoka katika
bunduki zao zikawakata uhai
walinzi wale ambao
hawakuwa na habari yoyote
kama wamevamiwa.Haraka
haraka Austin na timu yake
wakaenda katika geti kuu
“Mathew tayari
tumelidhibiti geti kuu”
akasema Austin kisha
akamtaka mmoja wa watu
wake aliyebeba ndege ndogo
yenye kamera aiwashe na
kuirusha ili kuwawezesha
watu walioko Dar es salaam
kuweza kufuatilia kila
kinachoendelea pale nje ya
jengo kujua kama kuna
hatari yoyote.
“Dar es salaa tayari
tumerusha kamera
angani,mnaweza kutuona
sasa” akasema Austin
“Tayari tumeiona na
tunapata picha
nzuri.Tunaizungusha jengo
zima kujua kuna walinzi
wangapi” akasema kamanda
aliyeko Dar es salaam katika
chumba cha kuongozea
operesheni ile.
Mathew na kundi lake la
Oscar walifanikiwa kuingia
ndani ya ubalozi kwa kupitia
sehemu ya juu ya ghorofa.Ni
usiku mwingi tayari ofisi
nyingi hazikuwa na watu
hivyo walishuka bila vikwazo
vyovyote hadi walipofika
katika ghorofa ya sita
ambako ndiko kuna ofisi za
Mossad.Katika ghorofa hii
kulisikika milio ya betri za
kutunza umeme wa
kompyuta na ilionyesha
kulikuwa na watu
wanafanya kazi wakihifadhi
data zaso kabla ya kompyuta
kuzima.Mathew na timu
yake wakaanza kunyata
kuelekea katika chumba mlio
ule wa betri ulitokea.Mlango
mmoja ulikuwa wazi na kwa
kuwa walikuwa na miwani
ile ya kuwawezesha kuona
katika giza waliweza
kuwaona watu sita
wakijitahidi kuhifadhi
mafaili katika kompyuta
kabla hazijazima.
“Hii ndiyo adha ya
Afrika,hakuna umeme wa
uhakika bado.Nini sababu ya
kukatika umeme usiku
huu?Kuna matengenezo gani
usiku hu...!” Mmoja wao
akasikika akilalama lakini
hakumaliza sentensi yake
kwani alipigwa risasi ya
kichwa kutoka katika
bunduki yenye kiwambo cha
sauti akaanguka
chini.Hakuna aliyebaki hai
ndani ya kile chumba baada
ya kuhakikisha wamewaua
wote wakatoka na kuendelea
kushuka
chini.Hawakukutana na
kikwazo chochote.
“Mike one,tayari
tumefika jengo la chini
kabisa.Vipi huko
nje?akasema Mathew
akiwasiliana na Austin
“Tumedhibiti eneo lote la
nje”
“Good.Oscar team
tunaelekea mahala aliko
Edger Kaka.” akasema
Mathew na kuelekea katika
mlango mkubwa ulioonekana
kama mlango wa lifti
kukabandikwa kifaa Fulani
kilichounganishwa na waya
mrefu na kisha akina
Mathew wakakaa mbali
kidogo baada ya sekunde
chache kifaa kile kikalipuka
na mlango
ukasambaratishwa,haraka
haraka wakafuata ujia
ulioelekea chini wakaukuta
mlango mwingine ambao nao
waliulipua kama
walivyofanya ule wa
kwanza.Kabla ya kukifikia
chumba alimo Edger Kaka
wakaukuta mlango wa
chuma ambao iliwalazimu
waweke kifaa kikubwa zaidi
na kishindo kikatokea
kikubwa wakapata nafasi ya
kupita hadi katika chumba
alimo Edger Kaka ambaye
alikutwa amekaa kitandani
jasho likimtoka kutokana na
woga baada ya kusikia
kishindo kile
kikubwa.Alimulikwa na tochi
kubwa yenye mwanga mkali
“Edger kaka? akaita
Mathew lakini Edger
alikuwa anatetemeka mwili
wote kwa woga baada ya
kuliona kundi la watu
wakiwa na silaha nzito
wakiingia mle ndani.
“Mike team we have
Edger Kaka” akasema
Mathew
“Are you sure it’s
him?akauliza Austin
“100% it’s him” akasema
Mathew
“Good job Oscar team”
akasema Austin.
“Who are you?Where are
you taking me?akauliza
Edger Kaka
“Edger Kaka we’re here
to rescue you.We’re taking
you home”
“Home? Where?akauliza
Edger bado alikuwa
anatetemeka
“Tanzania” akasema
Mathew
“No ! please don’t take
me there ! please kill me
right here don’t take me
there” akasema Edger Kaka
“Wewe ni Raia wa
Tanzania ambaye
unashikiliwa mateka na
tumekuja kukukomboa
kukurejesha nyumbani.Can
you walk?akauliza Mathew
lakini Edger alionekana
kuchanganyikiwa.Mathew
akaelekeza afungwe pingu na
abebebwe.Akachukua
karatasi na kalamu
akaandika maneno kwa
lugha ya kiarabu
“aqad khadhna rajlna.
hadhih harb muqadasat
walan tantahi abdaan.
hadhih hi albidayat faqat
alkthyr min al'umur hataa
tati 'iilaa 'ard falistina. la
'iilah 'iilaa allah
” Akimaanisha
“tumemchukua mtu
wetu.Hii ni vita takatifu na
isiyokoma.Huu ni mwanzo tu
bado kuna mengi yanakuja
hadi pale mtakaporejesha
ardhi ya
wapalestina.Hakuna Mungu
zaidi ya Allah”
Ujumbe ule akauweka
juu ya meza kisha akaamuru
Edger abebwe na kutolewa
mle ndani kwa kuwa hakuwa
na uwezo wa kutembea
“Mike team,tunatoka
sasa” akasema Mathew
akiwa ametangulia mbele
mkononi akiwa na bunduki
kubwa.Bado Edger kaka
alikuwa analalama akitaka
asipelekwe Tanzania
ikawalazimu kumziba
mdomo kwa gundi ya plastiki
ili asipige kelele.Bado jengo
lilikuwa giza umeme
haukuwa
umerudi.Walipanda hadi
ghorofa ya juu na kuikuta
helkopta yao tayari imetua
ikiwasubiri.Edger kaka ndiye
aliyekuwa wa kwanza
kuingizwa ndani ya
Helkopta.Mathew
alihakikisha watu wake wote
wameingia ndani ya
Helkopta na yeye akawa wa
mwisho
“Mike Team,Oscar team
tuko tayari kwa
kuondoka.Kuna tatizo
lolote?akauliza Mathew
“Hakuna tatizo
lolote,Mike team wote wako
salama na wamekwisha ingia
ndani ya helkopta tayari kwa
kuondoka”
“Good job guys now we
can go back home” akasema
Mathew na helkopta ikapaa
halafu akabonyeza kitufe
chekundu katika kifaa
Fulani alichokuwa nacho na
bomu walilokuwa wamelitega
katika chumba kikubwa
walimowakuta watu wa
Mossad likalipuka na
kusambaratisha kila
kitu.haukuwa mlipuko
mkubwa lakini ulitosha
kusambaratishakila kitu
ndani ya kile chumba.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Saa kumi na mbili na
dakika ishirini na moja
helkopta ya kwanza
iliyowabeba Oscar team
ikatua katika kambi ya jeshi
ya kikosi cha operesheni
maalum,Mathew Mulumbi
akawa wa kwanza kushuka
kisha Edger Kaka
akashushwa na kwenda
kuhifadhiwa katika chumba
maalum.Helkopta ya pili
ikatua na Mike team
wakiongozwa na Austin
January wakashuka.Austin
akamfuata Mathew
“Mathew Mulumbi
hongera sana kwa
kufanikisha vyema
operesheni yetu” akasema
Austin
“Hongera nawe Austin
na timu yako.Kila mmoja
amesimama katika nafasi
yake vyema
kabisa.Ninashukuru kwa
kuwa hakukuwa na majeruhi
wala hatujampoteza mtu
yeyote” akasema Mathew
“Operesheni imekuwa
nyepesi sana zaidi ya
nilivyotegemea”
“Hawakuwa
wamejiandaa na hawakujua
kama wangeweza
kuvamiwa.Ilikuwa ni
operesheni ya siri sana na
itawawia vigumu kujua
kama ni sisi ndio tuliofanya
uvamizi ule kwani mle ndani
ya chumba cha Edger
niliacha ujumbe ambao
unaonyesha IS ndio
waliofanya uvamizi ule na
kumchukua mtu wao”
akasema Mathew
“Mathew kwa upande
wetu nadhani tumemaliza
kazi yetu na tunawaachia
ninyi muendelee na taratibu
zenu”akasema Austin
“Ahsante
Austin.Ninataka
kuwashukuru wote
walioshiriki katika
operesheni hii.Baada ya hapa
mimi na timu yangu
tutaendelea na taratibu zetu
lakini nitaomba Edger
aendelee kukaa hapa hadi
hapo tutakapokuwa
tumepata sehemu muafaka
ya kumuhifadhi”akasema
Mathew
“Hakuna tatizo Mathew
hapa ni sehemu salama
sana” akasema Austin na
kumuongoza Mathew hadi
katika chumba cha mikutano
ambako wote walioshiriki
katika operesheni ile
walikuwa
wamekusanyika.Autin na
Mathew walipoingia wote
wakasimama
“Gentlemen poleni kwa
uchovu.Mathew hapa ana
neno la kusema” akasema
Austin na kumpa nafasi
Mathew
“Sina maneno mengi ya
kusema lakini kubwa
ninataka kuwashukuruni
sana kwa namna mlivyojitoa
kuhakikisha operesheni hii
inafanikiwa.Kila mmoja
alisimama vyema katika
nafasi yake ndiyo maana
operesheni imekwenda vizuri
na imeonekana nyepesi
kuliko wengi
mlivyotarajia.Hakuna
aliyeumia au kupoteza
maisha na wote tumerejea
nyumbani salama.Ahsanteni
sana” akasema Mathew
kisha akawapa wote mikono
wakaagana.Austin
akampeleka Mathew katika
chumba cha kuongozea
operesheni.Mara tu
alipoingia Ruby ambaye
alionekana kuwa na
tabasamu kubwa usoni
akainuka katika kiti na
kwenda kumkumbatia
Mathew
“Ahsante Mungu
umerejea salama
Mathew”akasema Ruby
“Ahsante sana
Ruby.Sote tumerejea salama”
akasema Mathew na
kuwageukia makamanda
waliokesha wakiwaongoza
katika operesheni ile.
“Gentlemen sina neno
zuri la kuwashukuru kwa
kazi kubwa mliyoifanya
usiku wa leo ya kutuongoza
tumekwenda salama na
kurejea salama.Operesheni
yetu imefanikiwa na
tumemrejesha nyumbani raia
wetu aliyekuwa anashikiliwa
mateka nchini
Kenya.Ahsanteni sana”
akasema Mathew na kuanza
kuwapa mikono
kuwapongeza kwa kazi
kubwa waliyoifanya.
“Mathew Mulumbi”
akasema kamanda mmoja
ambaye umri wake ulikuwa
mkubwa kidogo
“Nimefurahi sana
nimefanya kazi nawe lakini
nina ombi moja kwako kama
utakuwa
tayari.Tunamuhitaji sana
Ruby.Amekuwa na msaada
mkubwa sana kwetu kiasi
ambacho hatukuwa
tumetegemea.Uwezo wake ni
mkubwa na wa kushangaza
kabisa.Tunamuhitaji katika
chumba hiki” akasema Yule
kamanda na Mathew
akatabasamu na kumtazama
Austin
“Kwa bahati mbaya
Ruby haishi hapa nchini
makazi yake ni Uingereza
vile vile hii ni operesheni
yake ya mwisho
kushiriki.Amenursurika
kuuawa hivyo hatashirii tena
katika shughuli hizi atafanya
kazi nyingine” akasema
Mathew na kumtaka Ruby
akae katika kiti ili
amsukume watoke lakini
Ruby akagoma akataka
kutembea.
“I’m okay now Mathew”
akasema Ruby kisha
wakatoka ndani ya kile
chumba wakaenda katika
ofisi ya Austin ambako
Mathew alitaka kuwasiliana
na Rais Dr Evans.Akampigia
simu kwa kutumia simu
maalum ya Austin
“Austin” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais”
“Niliisubiri sana simu
hii.Naamini tayari
mmekwisha rejea”
“Ndiyo mzee tumerejea
saa kumi na mbili za
asubuhi”
“Ahsante
Mungu.Mmefanikisha
salama operesheni yenu?
“Mheshimiwa Rais yuko
hapa Mathew Mulumbi
ambaye atakueleza kila kitu”
“Mzee shikamoo”
“Marahaba Mathew
poleni sana kwa kazi
kubwa.Ninashukuru
mmerejea salama.Nyote mu
wazima?
“Mzee tunashukuru kila
kitu kimekwenda
vizuri.Operesheni
imemalizika salama na kwa
mafanikio makubwa
tumempata Edger Kaka na
kumrejesha nyumbani kwa
hivi sasa amehifadhiwa hapa
katika kambi hii hadi hapo
utakapotoa maelekezo
mengine”
“Dah ! Mathew sijui
niwashukuruje kwa kazi hii
kubwa mliyoifanya”
“Mheshimiwa Rais wale
jamaa wamekupigia tena
simu?akauliza Mathew
“Mathew naomba
tuwasiliane kwa kutumia
simu yako” akasema
DrEvans
“Sawa mzee nitakupigia
baada ya muda mfupi”
akasema Mathew kisha
akamuaga Austin wakapewa
gari na dereva kwa ajili ya
kuwarejesha katika makazi
yao.Mathew na Ruby
walikuwa wa kwanza
kuingia garini kisha
wakafuata Tino,Gosu Gosu
na Devotha ambaye alisita
kuingia ndani ya gari baada
ya kumuona Ruby
“Devotha get in !
akasema Mathew kwa sauti
kali na Devotha akaingia
garini wakaondoka.
Baada ya kuondoka
katika kambi ile Mathew
akachukua simu yake
akaiwasha na kumpigia
DrEvans ambaye alipokea
haraka
“Mathew nimefurahi
sana nyote mmerejea
nyumbani salama
salimini.Hizi ni taarifa njema
kabisa” akasema DrEvans
“Mheshimiwa Rais
tunashukuru Mungu sote
tumerejea salama kabisa
hakuna hata mmoja wetu
aliyepata jeraha au kupoteza
maisha ilikuwa ni operesheni
yenye mafanikio makubwa
na kama nilivyokujulisha
awali kwamba tumefanikiwa
kumpata Edger kaka ambaye
amehifadhiwa katika kambi
ile ya kijeshi tukisubiri hatua
nyingine” akasema Mathew
“Kazi nzuri sana
Mathew
mmeifanya.Hakukuwa na
tatizo lolote ambalo linaweza
kupelekea tukagundulika
kuwa ni sisi ndio tuliofanya
uvamizi huo?
“Tumejtahidi sana
mheshimiwa Rais kuwa
makini mno ili kutoacha
alama yoyote ya
kuwawezesha Israel na
serikali ya Kenya kujua
kama ni sisi ndio tuliofanya
uvamizi ule”akajibu Mathew
“Ahsante sana Mathew
kwa uhakika huo japo
tunatakiwa kuendelea kuwa
makini sana kufuatilia
taarifa za tukio hili”
“Tutafanya hivyo
mheshimiwa Rais.Hata hivyo
kuna suala lingine nilikuwa
nalifikiria” akasema Mathew
“Suala gani Mathew?
“Dr Yonathan Cohen
anafahamu kile kilichotokea
na sina uhakika sana kama
ataendelea kuificha siri hii
kwa miaka yote bila kuiweka
wazi.Yawezekaa kwa sasa
akawa kimya lakini nina
wasi wasi yawezekana hapo
baadae akaamua kuiweka
wazi siri hii na kuibua
mgogoro”
“Unashauri nini kuhusu
huyo mtu Mathew?
“Kwa sasa sishauri
tumfanye chochote lakini upo
ulazima wa kumuweka
katika uangalizi mkubwa”
“Hakuna tatizo
utaratibu kila kitu
unachoona kinafaa Mathew
nimekupa ruhusa hiyo.Si kila
jambo lazima uniambie mimi
ili kupata ruhusa
yangu,kama kuna jambo
unaona lina umuhimu
lifanye haraka na
utanijulisha baadae”
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais” akasema
Mathew
“Mathew mmerejea
asubuhi hii na yawezekana
bado hamjasikia kilichotokea
usiku wa kuamkia leo”
“Hatujapata taarifa
zozote mheshimiwa Rais nini
kimetokea?akauliza Mathew
“Usiku wa kuamkia leo
yapata saa tisa kuelekea saa
kumi za usiku watu
wasiojulikana wamevamia
shule ya sekondari ya
wasichana ya St Getrude
wameua walinzi na
kuwateka wanafunzi
wapatao sitini na sita na
walimu wao watatu.Msako
mkali umekwisha anza
kuwatafuta wanafunzi
hao.Mathew nakuhitaji hapa
ikulu kwa ajili ya maongezi
muhimu ya faragha”
akasema Dr Evans
“Sawa mheshimiwa Rais
nitafika hapo” akasema
Mathew
“Ninakusubiri asubuhi
hii” akasema Dr Evans na
kukata simu Mathew
akashusha pumzi
“Vipi Mathew kuna
tatizo?akauliza Gosu Gosu
“Wakati tukiwa katika
operesheni yetu kule
Nairobi,hapa nyumbani
kumefanyika tukio la
utekaji.Watu wasiojulikana
wamevamia shule ya
sekondari ya wasichana ya St
Getrude na kuteka
wasichana wapatao sitini na
sita na mpaka sasa
hawajulikani walipo”
“Nani wanaoweza
wakafanya tukio kama
hilo?akauliza Ruby
“Hakuna wengine
wanaoweza kufanya tukio
kama hili zaidi ya
magaidi.Wamekuwa
wakifanya utekaji ili
kushinikiza serikali
kuwatekekelezea mambo yao
wanayoyataka.Tuliona
mwaka 2014,wanafunzi wa
kike 276 walitekwa kutoka
katika shule ya sekondari ya
serikali katika mji wa Chibok
jimbo la Borno nchini
Nigeria.Ninaamini hata hapa
nyumbani waliofanya tukio
hilo la kuteka wasichana ni
magaidi ambao bado hatujui
ni kikundi gani cha kigaidi
na nini lengo lao” akasema
Mathew
“Another
mission?akauliza Tino
“Bado hatujafahamu
nani waliofanya tukio hilo na
kwa nini hata hivyo vipo
vyombo vya kushughulikia
suala hilo hivyo sisi
hatutajihusisha” akajibu
Mathew
“Mathew naomba
niliweke wazi hili
mapema.Sihitaji tena
kushirikishwa katika
operesheni nyingine kama
itajitokeza.Nimetoa msaada
katika operesheni hii na
imefanikiwa hivyo nahitaji
sasa kuendelea na shughuli
zangu kama kuna kitu
utahitaji kutoka kwangu you
know where to find me”
akasema Tino.
“Tino nakushukuru
sana kwa msaada wako
mkubwa ulioutoa katika
operesheni hii.Ninakwenda
kuonana na Rais muda mfupi
ujao na nitamueleza kuhusu
mchango wako mkubwa
katika operesheni
hii.Tafadhali naomba
usifunge milango kila pale
tutakapokuwa na shida na
kuhitaji msaada wako au
hata ushauri”
“Mathew milango iko
wazi na unakaribishwa muda
wowote” akasema Tino
Walifika katika makazi
yao ya muda Mathew
hakupoteza muda akamtaka
mmoja wa wasaidizi
waliopewa na Rais ampeleke
ikulu lakini kabla
hajaondoka akamfuata Ruby
katika chumba alimokuwa
anatibiwa akamuomba
daktari dakika mbili
azungumze na Ruby daktari
akatoka nje
“Ruby ninaelekea ikulu
kuonana na Rais amenitaka
nikaonane naye asubuhi
hii.Nitapata muda baadae wa
kukushukuru kwa kazi
kubwa uliyoifanya licha ya
kuumwa na kutuwezesha
kufanikisha kumpata Edger
lakini kuna kitu nataka
nikuombe” Akasema Mathew
na kumtazama Ruby
“Najua hauna amani
kumuona Devotha hapa
lakini nakuomba
uvumilie.She’s part of
us.Amekuwa na mchango
mkubwa sana naye katika
operesheni hii lakini kama
haujisikii vizuri I can let her
go” akasema Mathew
“Mathew siwezi kuwa
muongo kwamba kila kitu
kiko sawa kuhusu mimi na
Devotha.Alitaka kuyaondoa
maisha yangu na kila
ninapomuona ninapata
mstuko lakini kama
ulivyosema amekuwa na
mchango mkubwa sana
katika operesheni hii na kwa
ajili ya hilo nitajitahidi
kuweka kando kile
kilichotokea baina yetu.I’ll
try to act like nothing
happened”
“Thank you
Ruby.Aliyekupa jina hili
hakukosea kabisa wewe u
mwanamke wa kipekee
kabisa.Nitakaporejea tutajua
nini kinachoendelea”
akasema Mathew na
kumbusu Ruby shavuni
halafu akatoka akaenda
katika chumba alimokuwa
Devotha akamkuta amejilaza
kitandani
“Hello
Devotha”akasema Mathew
Devotha akainuka na kukaa
“Mathew nimemaliza
kile mlichotaka nikifanye,can
I go home now?akauliza
Devotha
“Usiwe na hofu Devotha
nyumbani utakwenda lakini
bado hatujamaliza
operesheni yetu.Kumpata
Edger Kaka si mwisho bado
kuna mambo mengi
tutahitaji kuyafahamu
kutoka kwake.Suala hili ni
pana zaidi hivyo utaendelea
kubaki nasi
hapa.Ninakwenda kuonana
na Rais na yawezekana
nikarudi na maelekezo
mapya hivyo kwa sasa siwezi
kusema chochote hadi
nitakaporejea.Kuna kitu
kimoja nataka
kukuomba,najua wewe na
Ruby bado hamuangaliani
usoni lakini naomba uwe
mvumilivu.Kitendo kile
ulichokifanya hawezi
kukisahau kwa haraka
naomba mpe muda.Kwa sasa
usizungumze naye kitu
chochote hadi nitakaporejea”
akasema Mathew
“Mathew do you think
she’s okay for me to be
here?akauliza Devotha
“Ruby hana tatizo
isipokuwa bado kuna kitu
kimemkaba kooni na
hakiwezi kuondoka kwa
urahisi kama
nilivyokueleza.She needs
time”
“Unadhani ataweza
kusahau tukio lile?Unadhani
anaweza
akanisamehe?akauliza
Devotha
“I don’t know yet but
she’ll try.Devotha
tutazungumza baadae
nitakaporejea” akasema
Mathew na kuanza kupiga
hatua kuelekea mlangoni
halafu akageuka
“Hongera ulifanya kazi
nzuri sana Nairobi” akasema
Mathew na Devotha
akatabasamu
“Thank you” akajibu na
Mathew akatoka akamfuata
Gosu Gosu
“Gosu Gosu ninakwenda
kuonana na Rais.Kuna jambo
ambalo hakuweza kunieleza
katika simu ndiyo maana
akanitaka nimfuate ikulu
ninadhani linahusiana na
tukio la kutekwa kwa wale
wasichana.Kuwa macho sana
na hawa wanawake wawili
Ruby bado ana hasira na
Devotha japokuwa
nimejaribu kumtuliza na
amenielewa lakini viumbe
hawa si wa kuwaamini sana
anaweza akabadilika
sekunde.Najua umechoka
lakini jitahidi kuwachunga”
“Usijali Mathew hakuna
kibaya kitakachotokea
wakiwa chini ya uangalizi
wangu.Nenda tafadhali
usichelewe” akasema Gosu
Gosu na Mathew akatoka
akaingia katika gari ambalo
lilikuwa linamsubiri
akaelekea Ikulu kuonana na
Rais.
“Naamini lipo jambo
kubwa ambalo Rais
ameshindwa kunieleza
katika simu ndiyo maana
akanitaka nikaonane naye
tuzungumze faragha.Hata
hivyo ninashukuru kwa
operesheni yetu imekwenda
vyema na sasa tunaye Edger
Kaka na hapa ndipo mchezo
unaponoga kati yetu na
IS.Lazima kwa kila namna
Olivia na Coletha
wapatikane.Sijawahi
kupambana na magaidi hawa
nikashindwa na hata sasa
hawatanishinda labda
wawahi kuniua lakini kama
bado niko hai nitapambana
bao kwa kila uwezo nilio nao
kuhakikisha ninawakomboa
Olivia na Coletha” akawaza
Mathew akiwa garini na kwa
mbali akahisi macho
yanakuwa mazito hakuwa
amepata usingizi kwa siku
ya pili
“Nahisi macho
yameanza kuwa mazito ngoja
kwa dakika hizi chache kabla
ya kufika ikulu nisinzie
kidogo kwani sifahamu
nitakalolikuta huko kwa
Rais” akawaza Mathew na
kulaza kiti akasinzia
NAIROBI – KENYA
Taarifa kuu iliyoliamsha
taifa la Kenya ni tukio la
kuvamiwa kwa ubalozi wa
Israel jijini
Nairobi.Iligundulika kuwa
ubalozi wa Israel
umevamiwa na watu wote
waliokuwemo ndani
kuuawa.Waliogundua jambo
hilo ni walinzi waliokuwa
wakiingia zamu ya asubuhi
kuchukua nafasi za wale
waliokuwa zamu ya usiki
kukuta wenzao wote
wameuawa.Kenya ni moja
wapo ya nchi ambayo
mashirika mengi makubwa
ya habari duniani yalikuwa
na ofisi zake hivyo taarifa za
kilichotokea katika ubalozi
wa Israel zilisambaa kwa
haraka duniani kote
“Kumetokea tukio la
uvamizi katika ubalozi wa
Israel usiku wa kuamkia leo”
kiliripoti chombo kimoja
kikubwa cha habari chenye
makao yake makuu nchini
Uingereza katika taarifa
yake ya habari ya
asubuhi.Taarifa hiyo
iliendelea
“Watu
wasiofahamika,wamevamia
jengo la ubalozi wa Israel
jijini Nairobi Kenya usiku wa
kuamkia leo na inadaiwa
watu wote waliokuwamo
ndani ya jengo usiku huo
wameuawa.Hakuna taarifa
rasmi iliyotolewa hadi sasa
kuhusiana na nani
waliofanya uvamizi huo wala
sababu ya kuvami aubalozi
huo lakini taarifa za awali
zinaonyesha kwamba hilo ni
tukio la ugaidi.Tutaendelea
kuwaletea taarifa zaidi
kuhusiana na tukio hilo
katika taarifa zetu mbali
mbali za habari” taarifa hiyo
ilimalizia
Vyombo vingi viliripoti
kwa ufupi kuhusiana na
tukio lile wakati wakisubiri
taarifa rasmi kutoka kwa
mamlaka zinazohusika ili
kujua nini hasa
kilichotokea.Lilikuwa ni
tukio lililoleta mshangao
mkubwa kwa wakazi wa jiji
la Nairobi hasa namna
wavamizi hao walivyoweza
kuingia ndani ya Jengo hilo
na wengi walijiuliza sababu
ya kuvamia ubalozi huo
Balozi wa Israel nchini
Kenya alifika kwa haraka
sana baada ya kupata taarifa
ya ofisi yake
kuvamiwa.Alikuta tayari
askari wa kikosi maalum cha
kupambana na ugaidi nchini
Kenya wamekwisha wasili na
kuimarisha ulinzi kuzunguka
jengo lote akazungushwa
kuona namna wavamizi wale
walivyofanya mauaji na
kuingia ndani.Walikwenda
hadi katika ofisi yake lakini
haikuwa imeguswa.Katika
ghorofa yenye ofisi za Mossad
kulifanyika uharibifu
mkubwa katika mojawapo ya
ofisi na watu
waliuawa.Balozi
akakumbuka kitu na
kupatwa na mstuko mkubwa
sana akawataka askari wale
wasiendelee na chochote na
watoke kwanza nje ya jengo
waachie wenyewe kwanza
wafanye uchunguzi
wao.Askari wale walitii
maelekezo ya balozi na
kuendelea na zoezi la
kuimarisha ulinzi nje ya
jengo na balozi akarejea
ofisini kwake akihema
akawaita ofisini kwake
baadhi ya maofisa wa
Mossad ambao tayari
walikuwa wamewasili pale
ubalozini.
“Kabla ya yote nataka
kujua Edger Kaka yuko
salama?akauliza na hakuna
aliyekuwa na jibu balozi
akawataka waelekee chini
mahala alikokuwa
amefungwa Edger.Walistuka
baada ya kukuta mlango
mkubwa wa kuelekea chini
mahala aliko Edger ukiwa
umesambaratishwa na
mlipuko wakatazamana na
kisha wakashuka chini
wakakuta milango kadhaa
yote ikiwa
imelipuliwa.Mlango wa
chumba alimokuwa Edger
Kaka ulikuwa chini baada ya
kulipuliwa na mlipuko .Wote
walihisi kuishiwa nguvu
kwani tayari jibu walikuwa
nalo.Waliingia ndani ya kile
chumba lakini kilikuwa
kitupu Edger Kaka
hakuwemo.Balozi
alichanganyikiwa alikosa cha
kuzungumza.Mmoja wa
maafisa akamletea karatasi
iliyokuwa mezani
akaichukua akaisoma
akahisi mwili wote
unaingiwa baridi.Yalikuwa
ni yale maandishi
aliyoandika Mathew kwa
lugha ya kiarabu na
kuyaacha mezani.Balozi
alijaribu kumpigia simu
mkuu wa Mossad Afrika
Mashariki Avi Abramson
lakini simu yake haikuwa
ikipatikana balozi akazidi
kuchanganyikiwa akarejea
ofisini kwake
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 4 & 5
“Mathew Mulumbi
karibu sana kijana wangu”
akasema Dr Evans baada ya
Mathew kuwasili ikulu
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais” akasema
Mathew
“Kwa kukutazama tu
unaonekana umechoka na
una usingizi.Pole sana”
“Ahsante mzee.Kwa
siku ya pili mfululizo
hatujafunga ukope
tumekuwa kazini hivyo
lazima mwili uchoke”
“Pole sana Mathew na
timu yako kwa kazi kubwa
ambayo
mnaifanya.Natamani
ningekufahamu toka awali
kabla sijafuata maelekezo ya
washenzi wale na kuwapa
Olivia naamini hivi sasa
tungekuwa katika sehemu
nzuri sana ya kumpata
mwanangu”
“Usijali mzee mimi na
wenzangu tutafanya kila
lililo ndani ya uwezo wetu
kuhakikisha tunawapata
Olivia na Coletha”kasema
Mathew
“Nalifahamu hilo
Mathew na ninaamini
mtawapata lakini kama
mzazi ninaumia sana kila
ninapowaza mwanangu yuko
katika mikono ya wale
makatili ambao wanaweza
wakamuua muda
wowote.Anyway tuweke
pembeni hayo.Nataka
kuwapeni pongezi nyingi kwa
kazi kubwa mliyoifanya.Kwa
dhati kabisa ninasema
mnastahili tuzo ya kipekee
kwa namna mnavyojitoa kwa
taifa lenu.Nawaomba
msichoke kwani bado tunayo
kazi ya kufanya kusafisha
nchi na kuwaondoa hawa
magaidi ambao wameanza
kuleta hofu nchini.Mafanikio
mliyoyapata usiku wa leo ni
makubwa na ya kupongezwa
sana,Edger Kaka
amerejeshwa nchini na
ninaamini kupitia kwake
tutafahamu mambo
mengi.Nimetazama taarifa
za habari za mashirika mbali
mbali makubwa ya habari
duniani na habari kuu
iliyopewa kipaumbele kile
kilichotokea jijini Nairobi
katika ubalozi wa
Israel.Wengi wametoa
taarifa kwa ufupi sana
wakiahidi kutoa taarifa zaidi
baadae.Kazi nzuri sana
mmeifanya lakini kama
nilivyosema tuendelee
kutega masikio kusikia kile
kinachoendelea huko
Nairobi” akasema Dr Evans
“Usiwe na hofu mzee
tumejitahidi sana
kuhakikisha kwamba
tunaifanya operesheni kwa
umakini mkubwa bila
kuacha nyayo yoyote nyuma
inayoweza kusababisha watu
wakafuatilia na kugundua ni
sisi.Imekuwa ni operesheni
ya siri kama walivyofanya
Mossad katika ardhi yetu”
akasema Mathew na Dr
Evans akainama akavuta
pumzi ndefu na kusema
“Jana usiku mida ya saa
saba hivi nilipigiwa simu na
wale jamaa na kama
tulivyokuwa tumehisi ni
kweli walitaka niwapatie
Edger kaka ili waweze
kumuachia
mwanangu.Niliwaeleza
ukweli kwamba hatutafanya
makubaliano tena na
magaidi.Walinipa hadi saa
mbili za asubuhi ya leo niwe
nimemuandaa Edger Kaka
na watanipigia kunipa
maelekezo
zaidi.Sikuwaogopa nami
nikawaeleza kwamba
itakapofika muda huo huo
wawe wamemrejesha
mwanangu kwani nitatumia
kila nguvu niliyo nayo
kuhakikisha ninawafyeka
wote.Mazungumzo yale
yalikuwa ni kama tamko la
vita.Usiku mida ya saa tisa
kuelekea saa kumi nilipigiwa
simu na mkuu wa jeshi la
polisi akinijulisha kwamba
kumetokea tukio baya katika
shule ya sekondari ya
wasichana ya St Getrude
ambako watu wasiojulikana
wamevamia wakaua walinzi
na kisha kuwateka
wasichana sitini na sita a
walimu wao watatu.Usiku
huo huo jeshi la polisi
lilianzisha msako mkali sana
kuwatafuta watekaji hao na
hadi kumepambazuka bado
hakuna taarifa zozote za
kuwapata watekaji wala
wasichana.Saa kumi na moja
na nusu za asubuhi
nilipigiwa simu tena na wale
jamaa wakanijulisha
kwamba wao ndio
waliowateka wasichana wale
na wakanitaka niwapatie
Edger kaka ama wasichana
wote
watauawa.Wameendelea
kusisitiza kwamba ikifika
saa mbili kamili za asubuhi
watapiga simu kujua kama
tayari nimemuandaa Edger
Kaka na kama sintakuwa
nimemuandaa basi
wataanzia hapo kuua
msichana mmoja baada ya
mwingine hadi pale
nitakapotekeleza ombi
lao.Mathew
nimechanganyikiwa na sijui
nifanye nini kibaya zaidi
mmoja wa wasichana
waliotekwa katika shule hiyo
ni mtoto wa waziri mkuu”
akasema Dr Evans na
kutulia kidogo.
“Katika matukio yote
yalitotokea ndani ya kipindi
hiki kifupi nimekuwa kimya
na sijamueleza mtu jambo
lolote kama ninafahamu
watu wanaoyatekeleza
imekuwa ni siri kubwa.Hata
alipotekwa mwanangu
sijamweleza mtu yeyote
kama ametekwa na magaidi
bali nimekuwa nikiwaeleza
kwamba mwanangu yuko
sehemu salama.Nilikuwa
nataka kulimaliza suala hili
kimya kimya kwani
nikiliweka wazi mambo
mengi ya siri yataibuka
ambayo sitaki yajulikane na
kubwa zaidi ni hii idara ya
siri ya mambo ya ndani ya
nchi ambayo wengi
hawaifahamu kama ipo.Idara
hii inanisaidia sana mimi
binafsi katika kutekeleza
majukumu yangu.Mathew
sitaki watu wafahamu
kwanza kuhusu idara ile ya
siri,pili kuhusu Edger Kaka
kuwa hai na vile vile kuhusu
kutekwa kwa Olivia,Agrey
themba na Coletha.Sitaki
watu wajue kama nimekuwa
nikiwasiliana na magaidi
kwa siri na kujadiliana nao
kuwapa kile wanachokitaka
ili wamrejeshe
mwanangu.Kinachonipa hofu
ni kwamba magaidi wale
wanaweza wakaanza kuwaua
watoto waliowatea kama
walivyoahidi ili
kunishinikiza kuwapa Edger
Kaka.Siko tayari na siwezi
kuwapa kile wanachokitaka
na kichwa changu
kinapouma.Nishauri Mathew
nini tukifanye? akasema Dr
Evans
“Mzee kwanza kabisa
pole sana kwa huu mtikisiko
unaoendelea ninachoweza
kukushauri ni kwamba
usilegeze msimamo
wako.Kama umeamua jambo
hili liwe siri basi liendelee
kuwa siri wakati
tukilitafutia ufumbuzi.Kuna
mambo mengi yanaambatana
na jambo hili ambayo
hayatakiwi kujulikana”
“Mathew nina wasiwasi
sana na hili jambo ndiyo
maana nimekuwa kimya
nikisubiri kwanza urejee ili
unishauri nini cha
kufanya.Sitaki jambo hili la
siri lijulikane ndiyo maana
nataka unishauri nini cha
kufanya.Mathew kuna
wakati ninajikuta ninawaza
kwa nini jambo hili
sikuliweka wazi mapema?
Yawezekana ningeliweka
wazi na kuwakabidhi vyombo
husika hivi sasa tayari
magaidi hawa wangekuwa
wamekwisha dhibitiwa na
mateka wote
wameokolewa.Nina wasi
wasi mwingi Mathew nini
kitatokea itakapofika saa
mbili za asubuhi? Je
nivitaarifu vyombo vya
uchunguzi jambo hili?
Ninawaza hadi nahisi kichwa
kinataka kupasuka”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais japo
suala hili linazidi kuchukua
sura mpya lakini nakuomba
usikate tamaa.Bado tunao
uwezo wa kupambana na
hawa magaidi na
kuwakomboa watu wetu
kimya kimya bila mambo
yale ya siri
kujulikana.Tunaye mtu wao
muhimu sana
wanayemtafuta na ambaye
tunaweza kumtumia
kuwapata watu
wetu.Naomba kibali cha
kukumhoji Edger kaka na
kupata taarifa za muhimu
kutoka kwake kuhusiana na
mtandao wao na namna ya
kuweza uwapata Olivia na
Coletha.Mheshimiwa Rais
endelea kulifanya suala hili
kuwa siri kwani endapo
utaamua kuliweka wazi
litafumua mambo mengi
yaliyofichika.Ukiamua
kuliweka wazi fahamu
kwamba hakutakuwa tena
na idara ya siri ya usalama
wa ndani ya nchi ambayo ni
muhimu na inafanya kazi
nzuri,uvamizi wetu katika
ubalozi wa Israel lazima
utajulikana na maisha yangu
na watu wangu tuliofanya
uvamizi huo yatakuwa
shakani Mossad
watatuandama sisi na
familia zetu hadi
wahakikishe wamelipa
kisasi.Mheshimiwa Rais kwa
namna yoyote ile suala hili
halipaswi kujulikana
linapaswa kuendelea kuwa
siri kwani ndani yake kuna
mkusanyiko wa mambo
mengi” akasema Mathew
“Mathew si kwamba na
mimi ninapenda iwe hivyo
lakini hawa magaidi
wananilazimisha nifanye
hivyo.Hawa watu ni wakatili
kuliko wanyama wa mwituni
na kwao kutoa uhai wa mtu
ni kitu chepesi sana hivyo
basi hawatasita kutoa uhai
wa watoto wale kama
walivyoahidi kwa lengo la
kumpata mtu wao.Hapo
ndipo akili yangu
inapokwama nifanye nini
kuwanusuru watoto wale
wasio na hatia yoyote
wasiuawe?Je niendelee
kulifanya siri jambo hili na
kuyaweka hatarini maisha
ya watoto wale ambao
hawafahamu chochote? Je
niliweke wazi hili jambo na
kukubali kifo changu cha
kisiasa?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais mimi
ushauri wangu ni jambo hili
liendelee kuwa siri.Endapo
itajulikana kwamba ulikuwa
unafahamu kilichotokea na
umekuwa na mawasiliano na
magaidi na mkafanya
majadiliano bila kuhusisha
vyombo husika vyenye
dhamana na ulinzi wa taifa
kitakuwa ni kifo chako
kisiasa kama ulivyosema
lakini si wewe tu bali sisi
sote,watu wote wanaofanya
kazi katika idara ya siri ya
usalama wa ndani wa nchi
ambao wamekuwa
wakiendesha mambo yao
kimya kimya bila
kujulikana.Hatutabaki
salama mheshimiwa
Rais.Bado ninaamini
kwamba tunao uwezo wa
kuwadhibiti magaidi hawa
na kuwakomboa mabinti zetu
waliotekwa pamoja na akina
Olivia.Ninaomba jambo hili
utuachie mimi na timu
yangu tuendelee
kulishughulikia hadi mwisho
wake.Nina uhakika mkubwa
kwamba tutalifikisha
mwisho na kuwakomboa
watu wetu.Ninaposema hivi
simaanishi kwamba vyombo
vingine vya ulinzi na
usalama havina uwezo wa
kulishughulikia hili jambo
lakini ni kwa ajili ya
kukulinda wewe
mheshimiwa Rais na sisi pia
ambao tumeshirikiana nawe
katika hili jambo”
“Mathew nakuamini
sana kijana wangu kila pale
ninapokuwa nimekata tamaa
unanipa moyo na tumaini la
kusonga mbele.Ninauchukua
ushauri wako na kuendelea
kuufumba mdomo wangu
kama vile sifahamu chochote
kuhusiana na suala
hili.Ninachokutaka Mathew
japo umechoka lakini wewe
na timu yako mnapaswa
kuendelea na hili jukumu
mtapumzika pale kazi hii
itakapokuwa
imekamilika.Nataka umuhoji
Edger Kaka.Make him
talk.Sifahamu wala sijali njia
utakazotumia ninachohitaji
mimi ni Edger kaka
afunguke taarifa za muhimu
zitakazotusaidia kuweza
kuwapata wasichana
waliotekwa pamoja na akina
Olivia.Wewe ni mzoefu
katika mambo hayo
unafahamu njia nyingi za
kumfungua mtu kama
huyu.Nataka kabla ya kufika
saa mbili za asubuhi muda
ambao hawa jamaa
wanataka wampate
Edger,uwe umefanikiwa
kupata chochote cha
kutusaidia kuwapata watoto
wetu.Nimeitisha kikao cha
dharura cha baraza kuu la
usalama wa taifa saa mbili
na nusu za asubuhi hivyo
nataka hadi kufika muda
huo tayari muwe mmepata
taarifa kutoka kwa Edger
Kaka ambazo zitatuwezesha
kujua mahala walipo
watekaji.Nataka tuufahamu
mtandao wao wote.Mathew
naomba kazi hii kubwa
tuliyoifanya isiende bure”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais kwa
mara nyingine tena
ninakutoa hofu na kukuahidi
kwamba mimi na wenzangu
tutafanya kila tuwezalo
kuhakikisha kwamba
tunapata taarifa muhimu za
kutusaidia kuwapata watu
wetu waliotekwa na IS.Vile
vile bado naendelea
kukusisitiza kuendelea
kuliweka jambo hili siri”
“Nitafanya hivyo
Mathew.Nawategemea sana
ninyi katika hili suala
vinginevyo hali itakuwa
mbaya sana kwa upande
wangu.Endapo watapiga
tena simu hawa jamaa
nitakujulisha” akasema
DrEvans
“Nashukuru
mheshimiwa Rais mimi ngoja
nikaendelee na kazi”
akasema Mathew kisha
wakaagana akaondoka.
“Magaidi ni watu wenye
roho mbaya kuliko hata
Simba na bila kufanya
juhudi watoto wetu
watachinjwa ili kumshinikiza
Rais aweze kuwapatia
wanachokihitaji.Kwa namna
yoyote ile Edger Kaka
hataweza kuingia katika
mikono yao.Yule ndiye
atakayetusaidia sisi
kuwafahamu magaidi hao na
mtandao wao.” akawaza
Mathew
Alirejea katika makazi
yao na kuwaita Devotha na
Gosu Gosu.Ruby alikuwa
chumbani kwake akipumzika
“Nimetoka kuonana na
Rais na mambo niliyoyakuta
huko ni makubwa.Ndugu
zangu bado tunayo kazi
kubwa mbele yetu.Magaidi
wa IS ndio waliowateka
wasichana usiku wa leo na
wanataka kuwatumia
wasichana hao kumshinikiza
Rais aweze kuwapatia kile
wanachokitaka yaani Edger
Kaka.Rais yuko katika
wakati mgumu sana hivyo
tunapaswa kumsaidia.Kwa
nini ninasema hivyo ni kwa
sababu hili suala lina mambo
mengine mengi ndani yake
ambayo hayapaswi
kujulikana ndiyo maana Rais
amekuwa kimya kuanzia
kutekwa kwa Olivia hadi
kutekwa kwa wasichana
usiku wa kuamkia
leo.Magaidi wale wameahidi
kumpigia simu Rais leo saa
mbili asubuhi kujua kama
tayari amemuandaa Edger
Kaka na kamabado basi
wataanza kuua wasichana
waliowateka. Ndugu zangu
najua mmechoka sana lakini
kazi bado inaendelea na
hatuna muda wa kupumzika
hadi tuhakikishe
tumewakomboa wasichana
wote waliotekwa,Olivia na
Coletha hivyo tunarejea tena
katika ile kambi ya jeshi
tulikomuhifadhi Edger kaka
na kuanza mahojiano naye
Rasmi.Leo lazima
atafunguka” akasema
Mathew
“Nilidhani kwa kumpata
Edger tutakuwa tumekaribia
kulimaliza hili suala lakini
kumbe mchezo umeanza
upya” akasema Devotha
“Mathew usiwe na hofu
kama ulivyosema
tutapumzika pale
tutakapokuwa tumelimaliza
hili jambo”akasema Gosu
Gosu
“Ahsanteni sana”
akasema Mathew na kwenda
kumuaga Ruby wakaondoka.
***************
Gari aina ya fuso
lililowabeba wasichana
waliotekwa kutoka shule ya
sekondari ya St Getrude
huku likisindikizwa na gari
nyingine mbili lilikatisha
katika viunga vya jiji la Dar
es salaam bila kutiliwa
shaka yoyote hadi lilipofika
katika nyumba moja kubwa
eneo la magetini
iliyozungushiwa uzio
mkubwa na kilichoweza
kuonekana ukiwa nje ni bati
la kijani.Miti mbali mbali ya
kivuli na minazi viliizungka
ile nyumba.Geti la nyumba
ile likafunguliwa na gari zile
zikaingia ndani.Lile gari
kubwa aina ya Fuso ambamo
ndimo wanafunzi wote
walikuwa wamepanda
likafunguliwa mlango
mkubwa wa nyuma na watu
nane wakashuka wakiwa na
silaha.Nazil Jalib kiongozi
wa opereseheni ile naye
akashuka kutoka kutoka
katika gari dogo na
kuwafuata wale jamaa
akaanza kuwapongeza
“eamal jayid !!(kazi
nzuri) ndiyo maneno
aliyokuwa akiyasema Nazil
kwa lugha ya kiarabu kila
alipokuwa anampongeza
mmoja wa watu wale
waliofanikisha kuwateka
wale wasichana.Baada ya
kumaliza kuwapongeza,wote
wakasimama kimya
kumsikiliza
‘ana saeid lilghayat
alyawm bima faealtaha. ma
faealtuh alyawm hu bidayat
alharb alty la tantahi dida
alwilayat almutahidat
al'amrikiati. 'uqsim biaism
allah 'anahum sayadfaeun
thmnaan bahzaan jdaan
likuli ma faealuh lana. ma
faealtuh alyawm hu 'iieadat
tashkil jil 'iilaa jilin.(
“Nimefurahi leo kwa yale
mliyoyafanya.Mlichokifanya
leo ni mwanzo wa vita vya
kudumu dhidi ya maadui
zetu.Naapa kwa jina la
Mwenyezi Mungu,watalipa
kwa gharama kubwa sana
kwa kila kitu ambacho
wametufanyia.Kwa
mlichokifanya leo
mtakumbukwa na vizazi hadi
vizazi”)
Baada ya maneno yale
aliyoyatamka Nazil watu
wake wakainua bunduki zao
juu kuonyesha ishara ya utii
halafu Nazil akasema
“Haraka sana
washusheni wasichana wote
wapelekwe katika chumba
kilichoandaliwa halafu hao
walezi wao wapelekwe katika
chumba kingine
wakafungiwe” akaelekeza
Nazil na kwa haraka
wasichana wale wakaanza
kushushwa kutoka katika
lile gari walimokuwamo aina
ya Fuso wakaingizwa ndani
huku wakihesabiwa.Jumla
walikuwa wanafunzi sitini na
sita.
Ndani ya lile jumba
kubwa kulikuwa na chumba
kikubwa ambacho hutumiwa
kwa ajili ya ibada na
wanafunzi wale wote
wakawekwa ndani ya
chumba kile,walimu wao
watatu wakafungiwa ndani
ya chumba kingine.
“Msiogope mabinti.Sisi si
watu wabaya lakini serikali
yenu ndiyo
mbaya.Tumewaleteni hapa
kwa muda ili kuishinikiza
serikali yenu kutupa kile
tunachokitaka na
wakishatupatia tunachohitaji
tutawaacha huru lakini
kama hawatakuwa tayari
kutupa kile tunachohitaji
tutawauweni mmoja baada
ya mwingine” akasema Nazil
Jalib na wasichana wale
wakaanza kulia
“Quiety ! akafoka na
wasichana wale wakatulia
“Sijawaambia kwamba
tunaanza kuwaua bali
tunasubiri kwanza
utekelezaji wa serikali yenu
kwa kile tunachokitaka na
kama wakitekeleza
tunavyotaka sisi basi
tutawaachia huru” akasema
Abdul na kuagiza wanafunzi
wale wapewe maji ya
kunywa.Maboksi ya chupa za
maji yakaingizwa wakaanza
kupewa maji ya kunywa
Nazil alienda katika
chumba kimoja chenye vifaa
mbali mbali ya mawasiliano
akampigia simu Fahad
“Mambo yanakwendaje
Nazil?Akauliza Fahad akiwa
nchini Kenya
“Fahad kila kitu
kimekamilika tayari
wasichana wamefikishwa
hapa kwako wote wako
salama tumewahifadhi
tukisubiri maelekezo yako”
akasema Nazil
“Kazi nzuri sana Nazil.
Ni wakati wa kumuonyesha
Rais wa Tanzania kwamba
sisi hatuna mchezo hata
kidogo.Tukisema kitu
tunakimaanisha.Kwa sasa
endeleeni kuwachunga hao
wasichana mimi nitaondoka
hapa Nairobi kwa ndege ya
saa kumi na mbili za asubuhi
nitafika Dar es salaam saa
moja na nusu .Saa mbili
kamili za asubuhi nitampigia
simu Rais kumuuliza kama
tayari anaye Edger Kaka na
kama akiendelea kuwa
kiburi basi tutaanza zoezi la
kuua wanafunzi mmoja
mmoja hadi pale
atakapoamua kutekeleza kile
tunachokitaka.Tutawaua
mubashara huku watu
wakishuhudia hivyo anzeni
maandalizi ya tukio hilo
kubwa ambalo watanzania
hawajawahi kulishuhudia
nchini kwao” akasema Fahad
akiwa jijini Nairobi.
“Sikufikiria kumwaga
damu ya watanzania hasa
watoto ambao hawana kosa
lolote lakini yote haya
ameyataka Rais wao kwa
kutaka kushindana
nasi.Nitamuonyesha nguvu
yetu pale nitakapoanza kutoa
uhai wa msichana mmoja
baada ya mwingine” akawaza
Fahad.
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 6
Rais wa Zanzibar akiwa
ameongozana na makamu wa
pili wa Rais wa serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar
waliwasili ikulu jijini Dar es
salaam tayari kuhudhuria
kikao maalum cha dharura
cha baraza la usalama la
taifa kilichoitishwa na Rais
kujadili hali ya usalama wa
taifa kufuatia mfululizo wa
matukio ya kigaidi.Baraza
hili la usalama la taifa
hujumuisha Rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania
kama mwenyekiti,makamu
wa Rais wa Tanzania,Rais
wa Zanzibar,makamu wa
Rais wa serikali ya
mapinduzi Zanzibar na
waziri mkuu wa Tanzania
kama katibu.Viongozi
wengine walioalikwa katika
kikao hicho ni wakuu wa
vyombo vyote vya ulinzi na
usalama vilivyopo nchini.
Mara tu baada ya Rais
wa Zanzibar kuwasili kikao
kikaanza bila kuchelewa.
“Ndugu wajumbe wa
baraza hili na wengine
waalikwa karibuni
sana.Nimelazimika kuitisha
kikao hiki cha dharura
kufuatia mfululizo wa
matukio ambayo
yanahatarisha amani na
usalama wa nchi.Ndani ya
kipindi kifupi sana
kumetokea matukio ambayo
yameleta hofu kubwa kwa
raia wetu.Tukio la kwanza
lilikuwa ni kutekwa kwa
Olivia Themba na baba yake
Agrey Themba.Mpaka leo hii
hawajapatikana.Lilitokea
tena tukio lingine la
shambulio katika hospitali
ya Mtodora na watu kadhaa
kuuawa.Kabla tukio hilo
halijapoa wametekwa tena
wasichana wengine sitini na
sita.Matukio haya yote
yametokea ndani ya wiki
moja tu,vyombo vyetu vya
ulinzi wa taifa viko
wapi?Kwa nini mpaka sasa
matukio haya yanaendelea
kutokea nchini? Akina nani
wanaofanya matukio
haya?Mmefikia wapi hadi
sasa katika kuwabaini na
kuwatia nguvuni? Kuna
maswali mengi sana
yanayoibuka kufuatia
matukio haya ambayo
yanahitaji majibu.Tuanzie
kwanza na tukio lililotokea
usiku wa leo la kutekwa kwa
wasichana sitini na sita
katika shule ya sekondari ya
St Getrude.Jeshi la polisi
hebu tupeni picha halisi nini
hasa kimetokea huko?Watoto
hawa wametekwa katika
mazingira gani? Hatua gani
mmepiga hadi sasa katika
kufahamu mahala walipo na
nani waliowateka?akauliza
Dr Evans kana kwamba
hafahamu chochote.
“Mheshimiwa Rais”
akasema mkuu wa jeshi la
polisi
“Mida ya saa kumi
alfajiri ya leo nilipigiwa simu
na kamanda wa polisi kanda
maalum ya Dar es salaam
akanijulisha kuwa amepata
taarifa za kutokea kwa
uvamizi katika shule ya
sekondari ya St Getrude na
wakati ananipigia simu
alikuwa njiani akielekea
huko akiwa na kikosi ha
askari waliojihami silaha
kali kwenda kuthibitisha
taarifa hizo.Walipofika huko
walikuta ni kwelli tukio hilo
limetokea na wanafunzi
sitini na sita wakiwa
wametekwa pamoja na
walimu wao watatu huku
walinzi wanne wakiwa
wameuawa kwa kupigwa
risasi.Taarifa za awali
ambazo jeshi la polisi tunazo
zinaonyesha kwamba watu
hao walifika shuleni hapo
mida ya saa tisa usiku
kuelekea saa kumi na
kufanya tukio hilo ovu.Jeshi
la polisi tayari tumekwisha
anza uchunguzi wa awali wa
tukio hilo tukifuatilia picha
za kamera za barabarani
ambako tunahisi watu hao
walipita baada ya kuwateka
watoto.Kimeundwa kikosi
maalum kwa ajili ya
kulishughulikia suala hili
mheshimiwa Rais na wako
kazini.Kuhusu matukio yale
mengine ya nyuma..”
akasema mkuu wa jeshi la
polisi lakini Rais
akamkatisha
“Jeshi la polisi
tumechoka na chunguzi
zisileta majibu.Tunataka
matokeo ya haraka,tunataka
kujua watoto wako wapi na
waliowateka ni akina
nani.Tunataka kufahamu
wapi alipo Olivia Themba na
baba yake Agrey
Themba,tunataka kujua nani
waliofanya shambulio katika
hospitali ya Mtodora na
kusababisha vifo vya watu
wasio na hatia.Nataka
kusikia mipango inayoweza
kutupa majibu ya haraka
kuwafahamu watu hao ni
akina nani hasa katika suala
hili la wanafunzi kutekwa
nyara.Hatujui lengo la watu
hao ni nini kwa kuwateka
hao wanafunzi.Hili jambo
lipewe uzito mkubwa sana”
“Mheshimiwa Rais toka
yalipoanza matukio haya
jeshi la polisi hatujalala tuko
macho saa ishirini na nne
tukichunguza na
tunaendelea
vizuri.Mheshimiwa Rais
watu hawa wanaotekeleza
haya matukio ni watu
waliojiandaa vyema na
wanafanya kitaalamu sana
wakijihadhari kutokuacha
nyayo zozote nyuma
zinazoweza kusababisha
wakagundulika ndiyo maana
uchunguzi umechukua muda
lakini tuko pazuri”akasema
mkuu wa jeshi la polisi
“Idara ya kudhibiti na
kupambana na ugaidi nini
kinaendelea kwa upande
wenu?Mko kimya sana na
matukio ya ugaidi
yanaendelea kufululiza hapa
nchini,jukumu lenu kubwa ni
kupambana na kudhibiti
ugaidi lakini hamuonekani
kutekeleza jukumu lenu na
kuwaachia magaidi uwanja
mpana wa kutawala na
kufanya kile
watakacho.N…..” Dr Evans
akanyamaza baada ya
kusikia mtetemo katika koti
lake,akaitoa simu kutazama
mpigaji akahisi
kuchanganyikiwa akatazama
saa ukutani ilikuwa ni saa
mbili kamili za
asubuhi.Akaitazama simu ile
ikiita na kukata.Wote mle
ndani ya chumba walikuwa
kimya wakimtazama
Rais,simu ikaanza kuita tena
akashindwa kuipokea.
“Tuendelee.Nataka
kupata taarifa kutoka kwa
idara ya kupambana na
kudhibiti ugaidi.Katika
matukio haya yote
yaliyotokea ninyi mmepiga
hatua gani katika kuwabaini
waliotekeleza….”akanyamaz
a Rais baada ya simu yake
kuita tena.Akaomba radhi
akatoka nje ili aweze
kupokea.Alikuwa na hasira
nyingi zilizochanganyika na
woga,akawataka walinzi
wake wasogee mbali kidogo
wampe nafasi kisha
akaipokea ile simu
“Nilikupa hadi saa mbili
kamili uwe umemrejesha
mwanangu umefanya hivyo
tayari?akauliza Dr Evans
kwa ukali
“Mheshimiwa Rais
nataka unisikilize
vizuri.Ulitangaza vita na sisi
na tayari vita hiyo
imeanza.Kama
nilivyokujulisha kwamba
tayari tunawashikilia
wasichana sitini na sita na
walimu wao watatu.Hatima
ya maisha yao iko mikononi
mwako.Utaamua kama
unataka kuwaokoa au kama
unataka
kuwaangamiza.Kuwaokoa
wasichana hao tunataka
utupatie Edger Kaka na kwa
kuwa umekuwa kiburi na
kutaka kupambana nasi
tutafanya majadiliano
mengine kuhusu mwanao
Coletha”
“Bastard ! akasema Dr
Evans kwa hasira
“Mheshimiwa Rais
hatuhitaji kuwafanya kitu
chochote hawa wasichana
wasio na kosa hivyo basi
ninakuongezea saa moja hadi
saa tatu kamili.Nitakupigia
tena simu na wakati huo
nataka tayari uwe na Edger
Kaka kisha nitakupa
maelekezo wape apelekwe na
wapi pa kwenda kuwachukua
wasichana wenu.Baada ya
hapo tutaanza majadiliano
kuhusu mwanao.Endapo
utashindwa kutekeleza
maelekezo hayo hadi kufika
saa tatu kamili za asubuhi
tutaanza kuua msichana
mmoja kila baada ya dakika
thelathini kwa kumchinja
shingo na kitendo hicho
kitafanyika huku watanzania
wakishuhudia mubashara
kupitia simu zao.Nakuonya
tena mheshimiwa Rais
usijaribu kupambana
nasi.Sisi ni jeshi kubwa na
tumesambaa hapa nchini na
ukijaribu kupambana na sisi
Tanzania itageuka nyekundu
kwa damu nyingi
itakayomwagika.Tutazungu
mza tena saa tatu kamili”
akasema Yule jamaa na
kukata simu.Dr Evans
alijikuta akihisi baridi na
kushindwa kutamka
chochote.Akaitazama simu
yake kwa sekunde kadhaa
halafu akazitafuta namba za
Mathew akampigia lakini
simu ya Mathew haikuwa
ikipatikana akazidi
kuchanganyikiwa akarejea
tena katika chumba cha
mikutano kuendelea na
kikao kile na wajumbe wa
baraza la usalama la taifa
 
Hatari sana

Hadi wakati huu bado sijaliona kosa la raisi. .kuamua kumshikilia Olivia na mzee agrey. ..

Hata kama mimi ningekuwa ndiye raisi ninge fanya kama alivyo fanya raisi. ... story nzuri sana

Ila Kuna baadhi ya vipande kwa namna fulani vinahusiana na simulizi ya peniela
Iyo simulizi ya Paniela I wapi mkuu nikajinonoe nayo pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom