SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 8
EPISODE 5
Kijua kilikwisha
chomoza wakati gari mbili
zilipofunga breki katika geti
la nyumba ya Mathew.Hawa
walikuwa ni watu
waliotumwa na Rais.Mathew
akawapokea na
kuwakaribisha ndani
akapewa maelekezo ya Rais.
“Gosu Gosu utaongozana
na hawa jamaa wawili mimi
natakiwa kuwahi ikulu sasa
hivi kuonana na
Rais.Nitakapotoka huko
nitakuja moja kwa moja
kuungana nanyi.Gari langu
utaondoka nalo” Mathew
akampa maelekezo kisha
akaingia katika mojawapo ya
zile gari mbili akaondoka
akiwaacha akina Gosu Gosu
wakijiandaa kuondoka
kuhamia katika makazi
mapya.
Hakukuwa na
mazungumzo katika gari ile
alilopanda Mathew hadi
walipofika ikulu akapelekwa
moja kwa moja kuonana na
Rais
“Mathew karibu sana
nimefurahi kukutana nawe
tena.Pole kwa kazi kubwa
uliyoifanya usiku wa
leo”akasema Dr Evanbs
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais” akasema
Mathew na Rais
akamuelekeza kiti aketi
“Mathew leo ni siku
itakayokuwa ndefu sana
kwangu,ratiba yangu
inaonyesha nitakuwa na
mfululizo wa vikao ndiyo
maana nimeona nizungumze
nawe kwanza kabla ya
mambo mengine
yoyote.Kabla hatujaendelea
una hakika kila kitu
kimekwenda kama
tulivyokubaliana? akauliza
Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
tumejitahidi sana
kuhakikisha kila kitu
kinakwenda sawa.Nakutoa
hofu mheshimiwa Rais
hakuna tatizo litakalotokea”
“Yule balozi una uhakika
naye hataweza kuwaeleza
watu wake kile kilichotokea?
“Hapana mzee hataweza
kwani mke wake
tunamshikilia sisi na
nimekwisha muonya kama
akifanya ujinga wa aina
yoyote ile hatamuona tena
mke wake.Kingine ambacho
kitamlazimisha asiweze
kutamka chochote ni woga
hataki Israel wagundue
kwamba yeye ndiye aliyetupa
siri zote kuhusiana na Edger
Kaka.Usiwe na hofu na
balozi mheshimiwa Rais
lazima atatupa ushirikiano
wa kutosha”
“Sawa Mathew kama una
uhakika hakutakuwa na
tatizo lolote ninakuamini”
akasema Dr Evans
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais”
“Sasa tujielekeze katika
jambo hili
linalotukabili.Nimekuachia
wewe kila kitu ukiendeshe
katika suala hili nataka
kusikia namna ulivyojipanga
kulimaliza hili suala na
hatimaye mwanangu na
Olivia wapatikane” akasema
Dr Evans
“Mheshimiwa Rais kama
nilivyokueleza usiku kwamba
ili kulimaliza suala hili
tunatakiwa kumpata Edger
Kaka ambaye amefichwa
katika ubalozi wa Israel jijini
Nairobi”
“Mathew suala hili bado
linanipa ukakasi
mkubwa.Ninataka kumpata
Edger Kaka lakini si kwa
kuvamia ubalozi wa
Israel.Hili ni suala zito
Mathew na ninasita hata
kulikubali lifanyike kwani
endapo ikijulikana basi
kutakuwa na mzozo mkubwa
wa kidiplomasia na
tutakuwa tumepoteza rafiki
mzuri sana wa nchi
yetu.Hicho kinanipa hofu
sana Mathew” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais Israel
wanamshikilia Edger Kaka
kwa sababu wanaamini ana
mahusiano na kikundi cha IS
na ndiyo maana walifanya
operesheni ile kubwa ya siri
na kumchukua wakaenda
kumficha Nairobi katika
ubalozi wao.Waliomteka
Coletha ni mtandao huu wa
akina Edger Kaka na tayari
wanafahamu kuwa Edger
Kaka yuko hai.Ili kuwapata
Coletha na Olivia lazima
tumpate Edger Kaka na
hakuna namna nyingine ya
kumpata Edger zaidi ya
kuvamia ubalozi wa
Israel.Hili ni suala kubwa
mheshimiwa Rais ni sawa na
kuvamia nchi lakini hatuna
namna nyingine ya kufanya
lazima tumpate Edger Kaka
kwa gharama zozote zile.Ni
mtu muhimu sana kwetu na
kuna maswali mengi ambayo
anapaswa
kuyajibu.”akasema Mathew
“Mathew hicho
ulichokisema ni kitu
ambacho kimenistua sana
hata mimi kusikia kwamba
Edger Kaka ana mahusiano
na magaidi.Hakuna
anayeweza kuamini jambo
hili kwani Edger alikuwa
mmoja wa wanasiasa vijana
aliyejizolea umaarufu
mkubwa sana hasa katika
mapambano ya
ufisadi.Alikuwa mstari wa
mbele katika kuanika ufisadi
na aliwataja mafisadi bila
woga wowote.Inashangaza
mno kusikia kwamba mtu
kama huyu ambaye
alionekana kama mkombozi
wa taifa kumbe
anashirikiana na magaidi.Ni
kweli kuna mambo mengi
ambayo tunahitaji
kuyafahamu kutoka kwa
Edger Kaka.” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa Rais
nadhani umeona umuhimu
wa kumpata Edger Kaka
kwa gharama zozote”
akasema Mathew
“Nakubaliana nawe
Mathew kwamba Edger ni
mtu muhimu sana lakini njia
ambayo umependekeza
kuitumia kumpata ndiyo
inayonipa hofu”
“Mheshimiwa Rais kuna
njia yoyote nyingine ambayo
unadhani inaweza
kutusaidia kumpata Edger
Kaka?akauliza Mathew.Dr
Evans akafikiri kidogo na
kusema
“Njia nyingine ya
kufanya kumpata Edger ni
kwa kufanya majadiliano na
serikali ya Israel” akasema
Dr Evans
“Hapana mheshimiwa
Rais hatuwezi kufanya
hivyo.Israel hawapaswi
kabisa kujua kama tayari
tunafahamu Edger yuko hai
ndiyo maana nashauri
tufanye operesheni ya kimya
kimya bila wao
kujua.Mheshimiwa Rais
operesheni hii si operesheni
rahisi lakini lazima tuifanye
na ninakuhakikishia
nitaiongoza mimi mwenyewe
na tutarejea hapa nchini
tukiwa n Edger
Kaka.Ninachohitaji ni
ruhusa yako mheshimiwa
Rais”
“Mathew ninaomba
nikueleze ukweli kijana
wangu ninatamani sana
kuruhusu operesheni hii
ifanyike lakini bado ninahofu
kubwa.Kwanza tunavamia
ubalozi wa nchi nyingine
ndani ya nchi ya jirani..Dah !
Dr Evans akashika kichwa
“Mheshimiwa Rais muda
unakwenda na mwenye
maamuzi ya mwisho ni
wewe.Mimi sina namna
nyingine ya kuweza kumpata
Edger Kaka na ninaomba
ufahamu kuwa bila kumpata
Edger Kaka itakuwa vigumu
sana kwetu kuwapata
Coletha na Olivia Themba”
akasema Mathew na kumpa
nafasi Dr Evans akatafakari
halafu akasema
“Mathew let us do it”
akasema Dr Evans lakini
bado macho yake yalionyesha
woga
“Ahsante mheshimiwa
Rais najua haya ni maamuzi
magumu umeyafanya lakini
yana faida kubwa kwa nchi”
“Tell me how’re you going
to do it?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa Rais
operesheni hii ni kubwa
mimi na watu wangu
hatuwezi kuifanya peke
yetu.Tunahitaji kuongezewa
nguvu”
“Nguvu ya namna gani
unaihitaji?
“Nahitaji watu mahiri”
“Watu wa aina gani
unawahitaji
Mathew?akauliza Dr Evans
“Ninahitaji watu wenye
mafunzo ya hali ya juu na
uwezo wa kupambana kwani
hii ni vita hivyo lazima watu
wanaokwenda kufanya
operesheni hii wawe na ujuzi
mkubwa katika mapambano”
“Nitakupa kikosi maalum
cha wanajeshi ambao
hutumiwa katika operesheni
maalum.Unadhani watu
wangapi watatosha katika
operesheni hii?akauliza Dr
Evans
“Naomba niongezewe
watu kumi ukijumisha na
watu wangu nilionao jumla
tutakuwa watu kumi na
nne.Tunatosha kabisa
kuvamia ubalozi wa Israel na
kumchukua Edger
Kaka.Operesheni itakuwa
namna hii.Tutatanguliza
kwanza majasusi kwenda
nchini Kenya kufanya
uchunguzi namna jengo lile
la ubalozi wa Israel
lilivyo,namna tunavyoweza
kuingia ndani na mahala
alipo Edger Kaka.Tukipata
ramani nzima ya jengo hilo
na tukifahamau namna
ulinzi ulivyo basi tutafanya
mazoezi namna ya kuweza
kuingia ndani ya hilo jengo
na kumchukua
Edger.Tutahitaji helkopta
mbili za kijeshi ambazo
hazitoi mlio na hazionekani
katika rada na zoezi la
uvamizi litafanyika usiku wa
manane” akasema Mathew
na kunyamaza baada ya
simu ya Rais kuita akaitoa
mfukoni na kuipokea
akazungumza halafu
akamgeukia Mathew
“Mathew nimetaarifiwa
kuwa nina wageni ambao
napaswa kuonana nao muda
huu.Mpango wako
nimeusikia ni mzuri na mimi
niko tayari kutoa kila aina ya
msaada unaohitajika.Kwa
kuwa bado maandalizi
yanaendelea nitakuomba
tukutane tena jioni hapa
hapa ikulu ili tuwe na
mazungumzo mapana zaidi
na unijuze mahala
mlikofikia.Nafahamu
operesheni hii inahitaji fedha
hivyo basi nimeandaa kiasi
Fulani cha fedha kwa ajili ya
kuanzia kazi” akainuka
akafungua kabati na kutoa
sanduku jeusi
“Humu kuna milioni mia
mbili thelathini na tatu.Hizi
ni kwa ajili ya kugharamia
operesheni hii hivyo basi
sehemu yoyote inayohitaji
kutumia fedha msisite
kutumia fedha na kama
ikimalizika mniambie nitatoa
nyingine.Mathew
ninakukabidhi kila kitu na
ninaamini kwamba mambo
yote yatakwenda vyema na
mwisho wa operesheni hii
nataka Coletha na Olivia
wapatikane.Naomba
nisikucheleweshe nenda sasa
hivi mkaanze maandalizi
kwa ajili ya operesheni
hii.Jioni tutakutana hapa
nataka uje na taarifa ya vifaa
vyote utakavyovihitaji ili
nivifanyie maandalizi”
akasema Dr Evans na
kuagana na Mathew
wakatoka ndani ya kile
chumba cha mazungumzo ya
faragha.Moja kwa moja
Mathew akaelekea katika
gari lililomleta na kuondoka.
“Nadhani hii itakuwa ni
moja kati ya operesheni
zangu kubwa kabisa kuwahi
kufanya tangu nimeanza
kazi hii ya ujasusi” akawaza
Mathew
“Katika operesheni hii
namuhitaji vile vile Tino.”
akaendelea kuwaza Mathew
na kumuelekeza dereva wa
lile gari sehemu ya kwenda
halafu akatoa simu na
kumpigia Tino
“Mathew kuna habari
gani?akauliza Tino
“Tino ninakuja hapo
nyumbani kwako
kukuchukua”
“Kuna nini
Mathew?akauliza Tino kwa
wasi wasi
“Usiogope Tino muda si
mrefu nitafika hapo ni kwa
ajili ya ile kazi imekuwa
kubwa zaidi kidogo” akasema
Mathew na kukata simu.
Kwa maelekezo ya
Mathew dereva wa lile gari
alifika hadi nyumbani kwa
Tino Mathew akashuka na
kuingia ndani
“Karibu sana
Mathew.Kuna tatizo
gani?akauliza Tino akiwa
amesimama akionekna kuwa
na wasiwasi
“Usihofu Tino hakuna
tatizo lolote lakini kuna
operesheni nyingine
imejitokeza ambayo
ninakuhitaji uwepo”
“Unanihitaji mimi?
“Ndiyo Tino.Nakuhitaji
sana katika operesheni hiyo”
“Inahusiana na nini hiyo
operesheni?
“Sitaki kuzungumzia
hapa lakini kwa ufupi tu ni
kuhusiana na kwenda
kumchukua Edger Kaka
kutoka katika ubalozi wa
Israel jijini Nairobi” akasema
Mathew na kumtazama Tino
“Tino hii ni operesheni
nzito na ya hatari sana hivyo
nahitaji sana msaada
wako.We need to do this for
our country”
“Mathe……”
“Tino please don’t say no!
I need you in this brother !
Tino akafikiri kidogo na
kusema
“Fine ! akaenda
chumbani kwake akavaa
shati na kutoka wakaingia
katika gari wakaondoka.
Mathew na Tino
walipelekwa moja kwa moja
katika nyumba ya
mapumziko ya Rais iliyoko
nje kidogo ya jiji.Tayari
akina Gosu Gosu walikwisha
fika.Kulikuwa na wahudumu
wawili wa kike na mmoja wa
kiume na tayari daktari
alikwisha wasili alikuwa
anawahudumia Ruby na mke
wa balozi
“Karibuni” akasema
Gosu Gosu wakaelekea ndani
“Kila kitu kiko vizuri
mahala hapa? Akauliza
Mathew
“Nimekagua kila kitu
kiko safi.Kuna watumishi
watatu hapa ndani kwa ajili
ya kutuhudumia na vyumba
vipo vya kutosha.Kuna ofisi
mbili ambazo tunaweza
kuzitumia zenye vifaa vya
kutosha ambazo huzitumia
Rais.Vile vile kuna chumba
cha tiba hapa ndani chenye
vifaa vingi ambacho unaweza
kukiita ni hospitali ndogo hii
ni kwa ajili ya Rais endapo
atapatwa na ugonjwa wakati
akiwa hapa.Humo ndimo
wanamohudumiwa akina
Ruby hivi sasa kwa ujumla
naweza kusema kwamba
nyumba hii imekamilika ina
kila kitu ambacho
kitatuwezesha kufanya kazi
zetu bila wasi wasi” akasema
Gosu Gosu na kumzungusha
Mathew kwa haraka haraka
katika nyumba ile halafu
wakarejea sebuleni Mathew
akamtaka Gosu Gosu awaite
watumishi wa ile nyumba
wakafika mara moja
“Ndugu zangu samahani
kwa kuwatoa katika kazi
zenu lakini nimewaiteni
hapa kwa ajili ya
kufahamiana.Yawezekana
mkawa mnajiuliza maswali
mengi kuhusiana na sisi ni
akina nani.Mimi naitwa
Mathew Mulumbi huyu
mwenzangu hapa anaitwa
Papii Gosu Gosu na huyu
hapa anaitwa Tino.Tuko
hapa kwa ajili ya kazi
maalum tuliyotumwa na Rais
na tutakuwepo hapa kwa
muda wa siku kadhaa kisha
tutaondoka.Naomba
kuwajulisha kwamba kuna
zoezi litakuwa linaendeshwa
hapa kwa siku hizo chache
tutakazokaa hapa hivyo
msiwe na wasi wasi pale
mtakapoona watu wakiingia
na kutoka humu ndani
ambao hamuwajui,msiwe na
wasi wasi mkisikia mtu
anapiga kelele za maumivu
au mkiona mtu akipigwa au
hata mkisikia mlio wa
risasi.Mko salama na
msihofu kitu.Endeleeni na
shughuli zenu kama
kawaida.Kama kutakuwa na
lolote la kuwajulisha
tutawajulisheni lakini
ninawaomba jambo
moja.Usiri.Chochote kile
mtakachokiona ndani ya
nyumba hii hakipaswi
kutoka nje.Naamini tayari
mnalifahamu hilo” akasema
Mathew na kuwataka wale
watumishi wakaendelee na
majukumu yao kisha
akawachukua akina Gosu
Gosu wakaenda katika moja
ya ofisi ya Rais
“Ni muhimu kuwaweka
sawa watumishi hawa ili
wafahamu kile
kinachoendelea na wasistuke
siku wakiona mtu anakatwa
kichwa humu
ndani.Tuachane na hayo
tuendelee na mambo
yetu.Nimetoka kuonana na
Rais tumezungumza japo si
kwa urefu sana kwani ratiba
yake kwa siku ya leo
imembana mno.Kitu
kikubwa ambacho Rais
alitaka kusikia kutoka
kwangu ni namna
tulivyojipanga kuhakikisha
tunawaokoa mwanae na
Olivia kutoka katika mikono
ya magaidi wanaowashikilia
hivi sasa.Nilimuweka wazi
Rais kwamba njia pekee ya
kuwapata watu hao ni
kwanza tumpate Edger Kaka
ambaye ana mahusiano na
watu hao na kumpata Edger
Kaka lazima tuvamie ubalozi
wa Israel nchini Kenya
ambako ndiko
amefichwa.Ndugu zangu
kuvamia ubalozi wa nchi
nyingine tena ndani ya nchi
nyingine ni jambo ambalo
lina athari kubwa sana
kidiplomasia lakini hatuna
namna nyingine ya kufanya
kumpata Edger Kaka zaidi
ya kuvamia ubalozi
huo.Baada ya
majadiliano,Rais akakubali
tufanye operesheni hiyo
lakini akatoa angalizo
kwamba tujitahidi kuifanya
kwa umakini mkubwa sana
na yeye yuko tayari kutoa
kila aina ya ushirikiano
kuhakikisha operesheni hii
inafanikiwa.Ameahidi
kutupatia makomandoo wa
kikosi maalum cha jeshi
ambao hutumiwa katika
operesheni maalum hivyo
tutakuwa na nguvu ya
kutosha.Tutakuwa jumla
watu kumi na nne kwani
Ruby naye ameomba
ajumuishwe katika
operesheni hii lakini yeye
atakuwa na kazi yake
maalum kama mnavyojua
yeye ni mtaalamu wa
kompyuta kwa hiyo atakaa
katika idara ya
mawasiliano.Tutatumia
helkopta za kikosi cha jeshi
kinachohusika na operesheni
maalum ambazo ni za kisasa
hazina mlio wala haziwezi
kuonekana katika rada”
akanyamaza kidogo
“Kitu kikubwa cha
kwanza ambacho tunatakiwa
kufanya ni kulifahamu
vyema jengo hilo la ubalozi
namna lilivyo ili tuweze
kujipanga namna ya kuingia
na kumchukua
Edger.Tunatakiwa kuipata
ramani ya jengo
zima,kufahamu mfumo
mzima wa ulinzi ulivyo ndani
na nje ya jengo na jambo la
tatu kubwa ni kufahamu
mahala alipofichwa Edger
Kaka.Hii ndiyo kazi kubwa
ya kwanza tunayotakiwa
kuifanya ambayo itatupa
urahisi wa kuweza kuingia
ndani ya jengo hilo” akasema
Mathew
“Uko sahihi Mathew
operesheni nzima
inategemea sana kama
tutafaulu kulifahamu jengo
hilo namna lilivyokaa na
mpangilio wote wa ulinzi”
akasema Tino.
“Kufuatia nchi ya Kenya
kuandamwa na mfululizo wa
matukio ya kigaidi mara kwa
mara ulinzi katika balozi
mbali mbali hasa za nchi
ambazo zimekuwa
zikipambana na vikundi vya
kigadi kwa muda mrefu
kama Marekani na Israel
umeimarishwa sana.Naamini
jengo hilo litakuwa na
teknolojia ya hali ya juu sana
ya ulinzi hivyo ili tuufahamu
mfumo mzima wa ulinzi
hatuwezi kuwakwepa
Mossad.Lazima tupate mtu
ndani ya Mossad ambaye
anaweza akatusaidia kutupa
taarifa zote za mfumo mzima
wa ulinzi ulivyo katika
ubalozi huo” akasema Tino
“Tino jambo unalolisema
ni sahihi na ninakubaliana
nalo lakini upo ugumu wa
kumpata mtu ndani ya
Mossad ambaye anaweza
akatusaidia kupata taarifa
nyeti kama hiyo.Ukumbuke
Edger amehifadhiwa pale
hivyo ni sehemu ambayo
wanaitazama kwa macho
matano” akasema Mathew
“Kwa nini tusipandikize
mtu ndani ya Mossad
ambaye atatumika kama
kirusi cha kuchota taarifa?
akauliza Gosu Gosu.
“Hilo nalo ni wazo
zuri.Kama hatuwezi
kumpata mtu ndani ya
Mossad basi tupandikize wa
kwetu” akasema Tino
“It’s not that simple guys
na inahitaji muda wa
kutosha hadi mtu huyo
kufanikiwa kumpandikiza
mtu huyo ndani ya Mossad
na sisi hatuna muda huo”
akasema Mathew
“Mathew nadhani
nimepata jibu.Devotha”
akasema Gosu Gosu
“What?! Akauliza
Mathew kwa ukali kidogo
“Mathew najua hili
halipenyi vyema katika
masikio yako lakini tunaye
mtu ambaye tunaweza
kumtumia katika operesheni
hii na akatusaidia sana
ambaye ni Devotha” akasema
Gosu Gosu.Mathew akatoa
kicheko kidogo
“Gosu Gosu umetoa wapi
wazo kama hilo?Yaani
tumshirikishe tena Devotha
katika mipango yetu?That
woman is a devil.She shot
Ruby three times,she nearly
killed her nitawezaje
kumsamehe mtu kama
huyu?Nitawezaje tena
kumjumuisha mtu kama
huyu katika timu
yangu?Hakuna namna
ninayoweza kufanya naye
kazi tena na nimeweka kiapo
popote nitakapomuona
Devotha I’ll kill her !
akasema Mathew
“Mathew wewe ni kaka
yangu ni kiongozi wangu na
ninakuheshimu
sana.Sijawahi kukupinga
katika jambo lolote,kila
ulichonielekeza
nimekifanya.Nafahamu unao
ujuzi mkubwa sana katika
mambo haya zaidi
yangu.Mimi ni mwanajeshi
tu na kazi yangu ni kupigana
vita lakini kwa mara ya
kwanza naomba unikubalie
na mimi hiki ninachokisema
ambacho ninaamini
kinaweza kuleta mchango
mkubwa katika operesheni
hii.Nafahamu alichokifanya
Devotha kinaumiza sana na
hata mimi nina hasira naye
lakini tunaweza kuweka
pembeni tofauti zetu kwa
muda na tukaungana
kufanya kazi pamoja kwa
manufaa ya nchi na baada ya
kumaliza kazi ndipo
tukaendelea na mambo yetu
binafsi.Samahani Mathew
kama nitakuwa
nimekukwaza kwa mawazo
haya” akasema Gosu Gosu
“Nadhani Papii amesema
kitu cha msingi sana.Kama
mwanamke huyo
anayemzungumzia anaweza
akawa na msaada katika
operesheni hii basi nashauri
ajumuishwe kama
itaonekana inafaa.Hii
operesheni ni kubwa sana na
kila ambaye anaweza kuwa
na msaada hata wa kupeleka
karatasi muhimu sehemu
Fulani basi atumike.Mathew
naungana na Papii
kukuomba kama utaona
inafaa mwanamke huyo
ajumuishwe katika
operesheni hii” akasema Tino
“Kwa nini alitaka
kumuua Ruby?Alimkosea
nini?Hili jambo limeniumiza
sana na kumfanya Devotha
awe ni adui yangu
mkubwa.Ruby hakustahili
kufanyiwa ukatili mkubwa
kama ule” akasema Mathew
“Mathew ninayafahamu
haya yote na unayo haki ya
kuwa na hasira na Devotha
hata mimi nina hasira naye
sana lakini kwa sasa lazima
tukubali kwamba
tunamuhitaji sana.”
Akasema Gosu Gosu na
Mathew akamtazama kwa
macho makali
“Gosu Gosu kwa nini
unadhani tunamuhitaji
Devotha katika operesheni
hii?akauliza Mathew
“Devotha ni wakala wa
Mossad hivyo itakuwa rahisi
kwake kuweza kuchota
taarifa za mfumo wa ulinzi
ulivyo katika ubalozi wa
Israel pamoja na mahala
alipo Edger Kaka ndani ya
ubalozi huo.Hivi ndivyo
tutakavyomtumia.Tutamtum
a Devotha kwenda
Nairobi.Akiwa kule Devotha
ataomba kuonana na mkuu
wa Mossad pale Kenya na
hapo ndipo atakapotumia
ujuzi na uzoefu wake kuchota
taarifa zile
tunazozihitaji.Simfahamu
vyema Devotha lakini kwa
namna nilivyofanya naye
operesheni ile ya kuja
kukukomboa ni mwanamke
mwenye uwezo mkubwa
sana” akasema Gosu
Gosu.Ilimchukua Mathew
zaidi ya dakika mbili
akitafakari halafu akasema
“Sawa nimekuelewa
Gosu Gosu.Japo moyo wangu
haufurahii jambo hili lakini
inabidi tulifanye kwa
manufaa ya taifa.Kama
tukitaka kumpata Devotha
lazima tumtumie balozi Dr
Yonathan.Yeye amekuwa
akiwasiliana naye kwa
kutumia mfumo wao wa
mawasiliano.Baadae saa nne
ninakwenda kukutana na
balozi Samawati beach
hotel.Pale pametulia sana na
ninafahamika ni hoteli ya
mmoja wa marafiki
zangu.Nitamuelekeza balozi
amjulishe Devotha naye afike
hapo hotelini kabla yeye
hajafika hapo na akishafika
tutamalizana naye.Tino
wewe utakwenda
kushughulikia tiketi tatu za
ndege ya saa saba mchana
inayoelekea
Nairobi.Mtasafiri nyote
watatu wewe,Gosu Gosu na
Devotha” akasema Mathew
“Hakuna tatizo katika
hilo” akajibu Tino.Mathew
akachukua simu na kupigia
Samawati beach hotel
akaweka oda ya chumba
akapewa chumba namba 98
halafu akampigia balozi Dr
Yonathan
“Hallow Mathew”
akasema Dr Yonathan baada
ya kupokea simu
“Dr Yonathan
nimekupigia kukukumbusha
kwamba saa nne za asubuhi
natakiwa kukutana nawe
Samawati beach hotel”
“Ninakumbuka Mathew
kwamba nina miadi ya
kuonana nawe mida hiyo”
“Vizuri sana kama
unakumbuka.Jambo lingine
ninamuhitaji Devotha”
akasema Mathew
“Devotha? Dr Yonathan
akauliza kwa mshangao
“Ndiyo namuhitaji
Devotha.Nataka utumie njia
zako mnazotumia
kuwasiliana na umtake afike
Samawati beach hotel
chumba namba 98 saa tatu
na nusu mwambie una
mazungumzo naye”
“Sawa Mathew nitafanya
hivyo.Vipi mke wangu
anaendeleaje?
“Usihofu anaendelea
vyema kabisa hana tatizo
lolote anapatiwa huduma
nzuri” akajibu Mathew na
kukata simu.
“Tino wewe utakwenda
kushughulikia hizo tiketi
mimi na Gosu Gosu
tutakwenda Samawati beach
hotel kuonana na balozi na
Devotha.Utatumia gari
langu,sisi tutatumia gari la
hawa wasaidizi wa Rais”
akasema Mathew na kwenda
katika chumba walimo Ruby
na mke wa balozi.Kilikuwa
ni chumba kikubwa ambacho
kilionekana kama hospitali
ndogokwani kulisheheni
vifaa vya kila aina vya
matibabu
“Ruby” akasema Mathew
akitabasamu baada ya
kumkuta Ruby akiwa
amekaa kitandani.Mathew
akasalimiana na Daktari
Yule aliyekuwa
anawahudumia akina
Ruby.Mke wa Dr Yonathan
alipomuona Mathew
alipatwa na mstuko mkubwa
akashindwa kujizuia kuanza
kulia.Mathew hakumjali
akamfuata Ruby
“Unaendeleaje
Ruby?akauliza
“Ninaendelea vizuri
Mathew kama unavyoniona”
“Sawa Ruby endelea
kupumzika ninatoka kidogo
nitakaporejea nitakuwa na
mazungumzo marefu nawe”
akasema Mathew
“Mathew unakwenda
wapi?Hapa ni wapi
tulipoletwa?
“Hapa ni sehemu salama
sana kwa wakati huu Ruby
usiwe na hofu yoyote hata
nisipokuwepo” akasema
Mathew
“Mathew tayari
umempata Yule
shetani?akauliza Ruby
“Usihofu Ruby mambo
yanakwenda vyema
nitakaporejea nitakuw na
mengi ya kukueleza”
akasema Mathew akambusu
Ruby katika paji la uso
akamuaga na kutoka mle
chumbani akimuacha mke
wa balozi
akitetemeka.Mathew
akazungumza na walinzi
akawataka wahakikishe
hakuna mtu yeyote kati ya
Ruby au mke wa balozi
anatoka ndani ya nyumba
ile.Wakaingia garini na
kuondoka
“Hili wazo la
kumshirikisha Devotha
katika operesheni hii
litamuumiza sana Ruby hata
hivyo kama Devotha
ataonekana kuwa na msaada
kwetu hakuna ubaya
tunaweza kumtumia halafu
mimi na yeye tutamalizana
baada ya operesheni hii
kumalizika” akawaza
Mathew wakiwa garini.
******************
Boti tatu ndogo za
mwendo kasi zilikaribia jiji la
Mombasa.Tayari ilikaribia
saa tatu za asubuhi.Boti hizi
zilikuwa zinatokea Pemba
nchini Tanzania ambako
walikwenda kwa ajili ya kazi
maalum.Hiki kilikuwa ni
kikosi kilichotumwa kwenda
Tanzania kuwachukua Olivia
Themba na
Coletha.Mawasiliano
yalikuwa makubwa kati ya
wale jamaa waliokuwa
katika zile boti na wenzao
waliokuwa wanawasubiri
sehemu Fulani kabla ya
kufika jiji la
Mombasa.Sehemu Fulani nje
ya bahari walikuwepo watu
kadhaa wakiwasubir wenzao
waliokuwa wakija na zile
boti.Kwa kufuata maelekezo
waliyokuwa wanapewa na
wenzao watu wale
waliziongoza boti zao
kuelekea ufukweni halafu
boti zikasimama wakashuka
watu na kuwashusha
wanawake wawili waliokuwa
wamefunikwa mifuko
kichwani.Wakawatoa nje
wakawakabidhi wanawake
wale kwa wale jamaa
waliokuwa nje wakiwasubiri
na bila kupoteza muda
wanawake wale wakaingizwa
katika helkopta iliyokuwa
mita chache kutoka
ufukweni.Watu wawili
kutoka katika zile boti nao
wakaingia katika helkopta
ile ikapaa na kuondoka
kuelekea Nairobi
TANZANIA
Gosu Gosu aliyekuwa
amejibanza sehemu fulani
katika hoteli ya Samawati
aliyaelekeza macho yake
katika maegesho alimuona
mwanamke mmoja mwenye
umbo lenye la kumtoa
udenda rijali yeyote akishuka
kutoka ndani ya gari na
kuanza kuelekea katika
jengo la hoteli.Haraka
haraka akachukua simu na
kumpigia Mathew
“Gosu kuna chochote
huko?akauliza Mathew
“Devotha amefika tayari
na anapanda huko juu”
“Good” akajibu Mathew
Devotha aliingia katika
lifti na kuelekea ghorofa ya
nne kilipo chumba namba
98.Gosu Gosu naye akatoka
katika mahala alipokuwa
amejificha akaenda kupanda
lifti nyingine naye akaelekea
ghorofa ya nne alipo Mathew.
Milango ya lifti
ikafunguka ghorofa ya nne
na Devotha akashuka kisha
akaanza kutembea huku
akiangalia namba za vyumba
akikitafuta chumba namba
98.Siku hii alikuwa amevaa
sketi ya jeans rangi nyeupe
iliyomkaa vyema na fulana
nyepesi ya rangi nyeupe
iliyoubana mwili wake na
kukifanya kifua chake kizuri
kionekane vyema.Alikuwa
amependeza sana.Alifika
hadi chumba 98 akabonyeza
kengele.Mathew aliyekuwa
ndani ya chumba
akachungulia katika kitundu
kidogo kilichopo mlangoni
akamuona Devotha.Mwili
wote ukafura kwa
hasira.Kwa kasi ya umeme
akaufungua mlango na
kumvuta ndani Devotha
ambaye hakuwa amejiandaa
kwa lolote akiamini kwamba
anakwenda kukutana na Dr
Yonathan,Mathew akaupiga
mlango teke ukajifunga
halafu akamkaba shingo
Devotha akamgandamiza
ukutani.
“Hatimaye nimekupata
shetani wewe !! akasema
Mathew kwa hasira akiwa
ameiweka bastora kichwani
kwa Devotha ambaye mwili
wote ulikuwa unamtetemeka.
“Mathew ! akaita Gosu
Gosu baada ya kuingia mle
ndani na kumkuta Mathew
akiwa amembana Devotha
ukutani huku bastora ikiwa
kichwani
“Mathew please brother !
akasema Gosu Gosu
“I promised to kill this
witch and I have to fulfill my
promise !! akasema Mathew
akiwa ameuma meno kwa
hasira.Gosu Gosu aliingiwa
na hofu kubwa kwa hasira
alizokuwa nazo Mathew.
“Mathew ukimuua
tutakosa kila kitu.We need
her so much.Please don’t kill
her ! akaomba Gosu
Gosu.Mathew akamtazama
halafu akamuachia Devotha
akainama akikohoa
mfululizo.Gosu Gosu
akamfuata
“Take a deep breath !!
akamwambia Devotha
ambaye alivuta pumzi ndefu
haraka haraka.Bado Mathew
alikuwa amesimama kati
kati ya kile chumba akiwa na
hasira.
“Take a sit ! Gosu Gosu
akamuelekeza Devotha aketi
halafu akamsogelea Mathew
“Mathew nadhani
tungemalizana kwanza na
Devotha kabla ya balozi
hajafika” akasema Gosu
Gosu kwa adabu.Mathew
aliyekuwa amegeukia
dirishani akageuka na
kumtazama Devotha kwa
hasira
“Ulifikiria nini Devotha
kumpiga risasi Ruby
?Alikukosea nini? Ulifikiri
sintakupata? Devotha
nakuhakikishia njia pekee ya
kunikwepa mimi ni
kufa.Kama uko hai ndani ya
dunia hii nikiamua kukusaka
ni lazima nikupate.Anyway
tuyaweke pembeni hayo
kwanza tuzungumze mambo
ya msingi.” Akasema
Mathew na kuiweka bastora
yake pembeni.
“Sifahamu nianzie wapi”
akasema Mathew na
kumtazama Devotha
ilionyesha wazi kwamba
hakuwa ameridhika
kumuacha Devotha bila
kumfanya chochote.
“Edger Kaka ni kweli
yuko hai” akasema Mathew
na mstuko ukaonekana usoni
kwa Devotha
“Yuko hai?akauliza
“Ndiy😵livia alikuwa
sahihi kabisa.Edger Kaka
yuko hai”akasema Mathew
huku hasira zikionekana
kuanza kupungua
“Hata mimi nilihisi
hivyo.Msisitizo aliouonyesha
Olivia ni mkubwa.Yuko wapi
Edger?Tayari mnafahamu
mahala alipo?akauliza
Devotha
“Ndiyo tunafahamu
mahala alipo” akajibu
Mathew
“Good.Sasa sikiliza
Mathew.Nilizungumza na
Olivia na akanihakikishia
kwamba ana siri kubwa
ambayo atanieleza endapo
nitampa taarifa za mahala
alipo Edger Kaka nadhani
sasa ni wakati wa kuifahamu
siri hiyo kubwa”akasema
Devotha
“I’m sorry Devotha
unaonekana uko nyuma ya
wakati sana.We don’t have
Olivia”akasema Mathew
“Olivia alichukuliwa na
Rais jana usiku na tuk…”
“Olivia hayuko kwa Rais”
akasmea Mathew na
kumkatisha Devotha
“What do you
mean?akauliza Devotha
“Nadhani unafahamu
jana usiku magaidi walifanya
shambulio katika hospitali
ya Mtodora.Mlengwa mkuu
wa shambulio lile alikuwa ni
Coletha mtoto wa Rais
ambaye walifanikiwa
kumchukua na kuondoka
naye.Rais alipigiwa simu
akajulishwa juu ya jambo lile
na akaonywa afuate kila
atakachoelekezwa ama sivyo
mwanae atapoteza
maisha.Kitu cha kwanza
walichokihitaji magaidi wale
ni Olivia Themba.Rais kwa
kuwa alihitaji kumpata
mwanae akalazimika
kuwapatia kile
walichokihitaji hivyo Olivia
Themba yuko katika mikono
ya magaidi hivi
tunavyozungumza na hatujui
yuko wapi”
“Bastard !! akasema
Devotha kwa hasira
“Kwa nini Rais akafanya
jambo kama hilo?Kwa nini
akawakubalia magadi kile
wanachokitaka?akauliza kwa
ukali
“Hakuwa na namna
nyingine ya
kufanya.Anahitaji kumuokoa
mwanae na mtu yeyote
angekuwa mahala pake
angefanya kama vile
alivyofanya Rais” akasema
Mathew
“So what’s going on
now?akauliza Devotha
“Devotha nataka kwanza
utambue tayari tunafahamu
kuwa wewe ni wakala wa
Mossad hapa nchini”akasema
Mathew
Uso wa Devotha
ulionyesha mstuko mkubwa
sana
“Mmef..fah…Oh my God !
Devotha akababaika
“Jana usiku ulikwenda
kuonana na balozi wa Israel
Dr Yonathan Cohen katika
ubalozi wa Israel hapa nchini
na kikubwa kilichokupeleka
kule ni kwenda kukutana na
majasusi wawili wa Mossad
waliotumwa Tanzania kwa
kazi maalum ya kuandaa
operesheni ya kumtafuta
Olivia na wewe kama wakala
wao wanakutumia katika
kuwasaidia kuandaa
operesheni hiyo” akasema
Mathew bado sura ya
Devotha ilikuwa katika
mshangao.Hakutegemea
kama akina Mathew
wangeweza kufahamu jambo
lile.
“It’s not true ! akasema
Devotha.
“BRAVO 15E 361 A ndiyo
namba yako ya
utambulisho.Devotha we
know everything about
you.Hakuna siri
tena.Naomba tusipoteze
muda kubishana jambo
hilo.Ninachotaka unieleze ni
je majasusi wale walikueleza
sababu ya kumtafuta Olivia
Themba?akauliza
Mathew.Zilipita sekunde
kadhaa Olivia akasema kwa
sauti ndogo
“Hapana
hawakunieleza.Niliwahoji
sababu za kumtafuta Olivia
lakini hawakutaka kuniweka
wazi kwa nini wanamtafuta”
akasema Devotha
“Sawa.Hawakutakakuku
weka wazi kwa sababu
anayemuhitaji Olivia ni
Edger Kaka”
“What? Sijakuelewa una
maanisha nini Mathew”
“Japokuwa wewe ni
wakala wa Mossad lakini
hulifahamu jambo hili.Akiwa
katika matibabu nchini
Israel Edger Kaka
alitembelewa na watu wawili
ambao wanatafutwa na
Mossad kwa muda mrefu
kwa kufadhili kundi la IS na
vikundi vingine vinavyofanya
mashambulizi katika ardhi
ya Israel na kuua
watu.Mossad ndio
waliotengeneza ajali ile
ambayo ilituaminisha
kwamba Edger amefariki
dunia lakini kumbe bado
yuko hai” akasema Mathew
“Oh my God ! akasema
Devotha akionekana
kushangazwa sana na taarifa
zile
“Baada ya kumchukua
Edger Kaka usiku ule
walimpeleka kumuhifadhi
katika ubalozi wa Israel
nchini Kenya ambako yuko
hadi hivi sasa.Kufuatia
mfululizo wa matukio ya
kurusha maroketi
yanayofanywa na vikundi
vya wanamgambo wa
kipalestina katika ardhi ya
Israel ambayo
yamesababisha vifo vya
wanafunzi kadhaa na
walimu,walitumwa majasusi
wawili kwenda nchini Kenya
kumuhoji Edger kwani
wamemuweka pale kwa
muda wa miaka mitatu bila
kumuhoji chochote.Katika
mahojiano hayo Edger Kaka
alikuwa tayari kuwaeleza
Mossad kila kitu
wanachokihitaji kwa sharti
la kuhakikisha wanampata
Olivia.Anadai kwamba
anampenda Olivia na ndiye
mwanamke anayetaka kuishi
naye.Hiyo ndiyo sababu ya
Mossad kuja kumtafuta
Olivia nchini
Tanzania”akasema Mathew
“Binafsi sikuwa tayari
kuwasaidia Mossad kumpata
Olivia kwani ninafahamu
umuhimu wake kwetu na
hata taarifa nilizowapa
hazikuwa za
kweli.Niliwaahidi
kuwasaidia lakini sina
mpango huo wa kuwasaidia
badala yake ninatafuta
namna ya kufanya ili
mpango wao huo usifanyike
hapa nchini”akasema
Devotha
“Huna haja ya kuwa na
wasiwasi nao tena.They’re
gone” akasema Mathew
“Gone?Where?akauliza
Devotha
“Dead.We killed them”
“Jesus Christ ! You killed
them?
“Yes we did” akajibu
Mathew
“Ahsanteni sana kwa
jambo hilo kubwa
mlilolifanya ila hili ni
tangazo la vita.Mossad
watawawinda usiku na
mchana hadi wahakikishe
wamewapata watu
waliowaua majasusi
wao.Mathew mmeingia
katika hatari kubwa
sana”akasema Devotha
“Tunajua,lakini
hawatafahamu chochote
kuhusiana na suala hilo
kwani tayari limekwisha
shughulikiwa kikamilifu”
“Mathew samahani
naomba nipewe nafasi ya
kuuliza swali.Mmewezaje
kufahamu mambo haya yote
hadi kuwaua wale
majasusi?Ni vipi mtafanya ili
Mossad wasiweze kugundua
kama majasusi wao
wameuawa? Ninauliza hivyo
kwa sababu mimi kama
wakala wao lazima
nitaulizwa mahala walipo
Fishel na Ehud.Moja kwa
moja tayari na mimi
nimekwisha ingia katika hili
jambo japo sikufanya mauaji
hayo” akasema Devotha
“Devotha hayo mambo
mengine hayana umuhimu
mkubwa.Akili na nguvu zetu
zote tuapaswa kuvielekeza
katika kuwatafuta Olivia na
Coletha ambao hatujui
mahala walipo hadi hivi
sasa.Ili kuwapata akina
Olivia lazima kwanza
tuhakikishe tumempata
Edger Kaka.Kuna njia moja
tu ya kumpata Edger Kaka
nayo ni kwa kuvamia ubalozi
wa Israel nchini Kenya
ambako ndiko amefichwa”
“Mathew mnataka
kuanzisha vita ! akasema
Devotha
“Thay started this
war.Tunachokifanya sisi ni
muendelezo wa kile
walichokianzisha
wao.Waliingia katika ardhi
yetu wakaua na kuteka raia
wetu wakiamini jambo hili
litabaki siri na
hatutalifahamu.Edger Kaka
ni raia wetu ambaye
ametekwa hivyo kila aina ya
mbinu itatumika kumrejesha
nyumbani na mbinu pekee
ambayo inatakiwa kutumika
kwa sasa ni kuvamia ubalozi
wa Israel nchini Kenya na
kumchukua na hapo ndipo
wewe unaingia” akanyamaza
Mathew akamtazama
Devotha kisha akaendelea
“Tunaandaa kikosi
kabambe kitakachofanya
operesheni ya aina yake ya
kumchukua Edger.Kitu
kikubwa kabla ya yote
ambacho kitatuwezesha sisi
kufanikisha operesheni hiyo
ni kupata ramani ya jengo
hilo lilivyo na vile vile
kufahamu mfumo mzima wa
ulinziulivyo na tatu
tunatakiwa kufahamu alipo
Edger Kaka ndani ya ubalozi
huo.Tulihitaji kupandikiza
mtu ndani ya Mossad lakini
muda tulio nao ni mfupi sana
ndiyo maana tukaamua
kukutumia wewe ambaye
tayari una mahusiano na
Mossad” akasema Mathew.
“Nini mnataka
nikifanye?akauliza Devotha
“Unakwenda
Nairobi.Nataka ukatafute
ramani ya jengo la ubalozi
wa Israel nchini
Kenya,mfumo wote wa ulinzi
wa ubalozi huo na mahal
alipofichwa
Edger.Tumekuchagua wewe
kwa kuwa tayari ni mtu wao
wa karibu unawasiliana nao
hivyo ni rahisi kuweza
kuingia kati kati yao na
kupata taarifa
tunazozihitaji.Naomba
ufahamu Devotha kwamba
katika operesheni hii
tunakutegemea
sana.Ukishindwa kufanikiwa
utakuwa umetuangusha
sisi,umemuangusha Rais na
umewaangusha pia
watanzania kwani
operesheni hii tunaifanya
kwa ajili ya Tanzania hivyo
nakuomba ufanye kila
unaloweza kulifanya ili
kupata taarifa hizo.Naomba
utambue vile vile kwamba
Rais Dr Evans ndiye aliyetoa
kibali cha kufanyika kwa
operesheni hii hivyo utaona
namna ilivyo muhimu.Rais
yuko pamoja nasi na
ametutuma tuifanye kazi hii
kwa niaba ya watanzania”
akasema Mathew
“Ni kweli mimi nina
ukaribu na Israel kupitia
shirika lao la ujasusi la
Mossad na ninawaahidi
kufanya kila linalowezekana
kuhakikisha ninazipata
taarifa hizo.Makao makuu ya
Mossad kwa ukanda huu wa
Afrika Mashariki yapo katika
ubalozi wao nchini Kenya na
ninafahamiana sana na Avi
mkuu wa Mossad kwa
ukanda huu.Nimekuwa
nikiwasiliana naye mara kwa
mara.Ninaamini kupitia
kwake tutaweza kupata kila
kitu tunachokihitaji.Mawazo
yangu bado ni kwa wale
majasusi wawili
mliowaua.Nina wasiwasi
kukosekana kwao kunaweza
kuharibu kila kitu ninaweza
kuulizwa maswali kuhusu
wao nikashindwa
kujibu”akasema Devotha
“Usihofu Devotha.Balozi
wa Israel Dr Yonathan
Cohen yuko na sisi katika
operesheni hii”
“Yuko nasi?Kivipi?
“Ni hadithi ndefu lakini
fahamu kwamba yuko
upande wetu.Yeye ndiye
atakayesimamia suala la
wale majasusi wawili kila
taarifa zao
zitakapotakiwa.Wewe
ukiulizwa utasema kwamba
kuna tetesi kwamba Olivia
baada ya kutekwa
amepelekwa jijini Arusha
hivyo basi majasusi hao nao
wamekwenda jijini Arusha
kufanya uchunguzi.Balozi Dr
Yonathan yeye ataendelea
kuwahakikishia Mossad
kwamba ana mawasiliano ya
mara kwa mara na majasusi
hao wakiwa jijini Arusha
hadi pale tutakapomaliza
operesheni yetu ambapo
balozi atadai kuwa
mawasiliano yamekatika
ghafla na hajui kama
majasusi hao wako salama”
“Mmewezaje kumuingiza
balozi Dr Yonathan katika
suala hili?akauliza Devotha
“Utafahamu hapo baadae
lakini kwa sasa kama
nilivyokueleza awali kwamba
tujielekeze katika
kuhakikisha operesheni hii
inafanikiwa” akasema
Mathew.
“Sawa Mathew mimi niko
tayari.Lini ninatakiwa
kwenda huko Nairobi?
“Unaondoka baadae
leo.Utaambatana na Gosu
Gosu na Tino”
“Tino?Who is he?
“Utamfahamu
baadae.Kwa pamoja
mtaunda timu ambayo
mtahakikisha mnafanikiwa
kuipata ramani hiyo ya jengo
la ubalozi wa Israel na
mtakuwa mkiwasiliana nasi
huku Dar es salaam kwa kila
mnachokifanya.Tino ni
mtaalamu sana wa
mawasiliano na
atatuunganisha sisi na ninyi
huko Nairobi” akanyamaza
Mathew baada ya simu yake
kuita.Alikuwa ni balozi Dr
Yonathan
“Hallo balozi”
“Mathew tayari nikefika
hapa hotelini uliponielekeza
tuonane” akasema Dr
Yonathan
“Njoo moja kwa moja
chumba namba 98 ghorofa ya
nne” akaelekeza Mathew
“Devotha kabla sijasahu
naihitaji ile kompyuta
ambayo uliichukua kutoka
kwa Ruby” akasema Mathew.
“Guys I don’t know how
to say this but I’m
sorry.Nilichokifanya ni kitu
kibaya na hata mimi
mwenyewe
ninakijutia.Sifahamu akili
yangu ilikuwa inawaza nini
hadi nikafanya kitendo
kile.Naombeni sana
mnisamehe” akasema na
kumtazama Mathew
“Is she….”
“She’s not
dead.Tumepambana kwa kila
tulivyoweza na Mungu
amesikia maombi yetu na
kumrejeshea uhai ila tayari
alikwisha chungulia kaburi”
“Please forgive me
Mathew”
“Sifahamu nitaanzia
wapi kukusamehe Devotha
kwa hiki
ulichokifanya.Umeniumiza
sana.Hujui ni kwa namna
gani Ruby alivyo mtu wangu
wa muhimu.Lakini hayo yote
tuyaweke pembeni kwanza
naomba ukafanye kazi
niliyokuag…………” Mlango
ukagongwa na Mathew
akanyamaza.Gosu Gopsu
akainuka kwenda
kuufungua,alikuwa ni balozi
Dr Yonathan.Devotha
akatazamana na Dr
Yonathan
“Huyu Mathew ni mtu
wa kuogopwa
sana.Amewezaje kumdhibiti
balozi na kumfanya afanye
kila
anachomuamuru?Sikutegem
ea kabisa kama angeweza
kugundua jambo kama hili la
mimi kuwa wakala wa
Mossad lakini tayari
anafahamu kila kitu hadi
namba yangu ya
utambulisho.Licha ya hilo
ameweza vile vile kuwaua
Ehud na Fishel.Huyu si mtu
wa kawaida napaswa
kumuogopa sana.Tayari
amekwisha niandika kwa
kalamu nyekundu hivyo
napaswa kuwa makini sana
kufuata maelekezo yake
vinginevyo he’s going to kill
me ! akawaza Devotha
“Balozi karibu
sana.Ahsante umefika kwa
wakati
tuliokubaliana.Nataka
kufahamu huko utokako nini
ninaendelea?Kuna tatizo
lolote kuhusiana na kile
kilichotokea jana? akauliza
Mathew
“Mpaka sasa kila kitu ni
shwari kabisa.Hakuna tatizo
lolote.Nimewasiliana na
mamlaka za juu na
kuwajulisha kwamba huku
kila kitu kinakwenda
vyema”akajibu balozi
“Vipi kuhusu wale
majasusi wawili?akauliza
Mathew
“Ehud na Fishel
walipofika hapa nchini
walifikia katika hoteli na
baadae ndipo wakaja
ubalozini ambako tuliwapa
nyumba inayotumiwa na
wageni wanaofika ubalozini
hapo hivyo hawakuwa
wamerudisha vyumba
vyao.Wakati ninakuja huku
nimepita katika hoteli
walikofikia kuwafahamisha
kwamba wageni wale
hawatarejea tena pale
hotelini na nikalipa kiasi
chote cha fedha walichokuwa
wanadaiwa.Viongozi wa
Mossad niliwasiliana nao
asubuhi ya leo nikawajulisha
kwamba watu wao
wanaendelea na maandalizi
ya operesheni na
wameelekea Arusha”
akasema Dr Yonathan
“Vizuri.Nafurahi kama
mambo yamekwenda vyema”
akasema Mathew
“Vipi mke wangu
anaendeleaje? Akauliza
balozi
“Yuko vizuri usihofu”
akajibu Mathew
“Balozi nimekuita hapa
kuna mambo ambayo
tunataka utusaidie”akasema
Mathew na kumtazama
balozi halafu akaendelea
“Israel kwa kutumia
shirika lao la ujasusi la
Mossad walivamia ardhi yetu
wakaua na kuteka raia wetu
wakampeleka
mafichoni.Walifanya kitendo
kibaya sana na kama
haitoshi wanajiandaa tena
kuvamia ardhi yetu na
kufanya operesheni nyingine
ya kumteka raia mwingine
wa Tanzania na kumtorosha
na hatujui katika operesheni
hiyo watanzania wangapi
watapoteza maisha
yao.Israel ni marafiki zetu
lakini kwa hiki
walichokifanya
hatukubaliani nacho hata
kidogo.Mheshimiwa balozi
tunamuhitaji mtu wetu
aliyetekwa na Israel na
kwenda kufichwa katika
ubalozi wenu nchini
Kenya.Hatuhitaji
majadiliano yoyote kwani
wao wakati wakimchukua
hawakujadiliana nasi hivyo
na sisi tunataka kumchukua
kama wao walivyomchukua
yaani kimya kimya”
akanyamaza akamtazama
balozi aliyekuwa kimya
akimsikiliza halafu
akandelea
“Nafahamu umuhimu wa
Edger Kaka kwa Israel lakini
huyu ni raia wa Tanzania na
tunamuhitaji vilevile hasa
kwa wakati huu hivyo basi
tunaandaa operesheni ya
kwenda kumchukua mahala
alikohifadhiwa jijini Nairobi
katika ubalozi wenu na
tunahitaji msaada wako”
Dr Yonathan alijitahidi
kuficha woga alioupata lakini
vidole vyake vilikuwa
vinatetemeka.Mathew
aliligundua hilo lakini
hakumjali
“Devotha ambaye ni
wakala wa Mossad
anakwenda jijini Nairobi
ambako atakutana na mkuu
wa Mossad katika ukanda
huu wa Afrika Mashariki na
kati ndugu Avi.Tunamtuma
Devotha kwa kazi maalum
katika ubalozi huo hivyo
atahitaji msaada wako pale
atakapohitaji”akanyamaza
tena akamtazama balozi
“Devotha atamjulisha Avi
kwamba majasusi wale
wawili wa Mossad wako jijini
Arusha na Avi akikuuliza
utamthibitishia hivyo
kwamba kweli wako
Arusha.Ukumbuke bado
tunakufuatilia Dr Yonathan
na kosa moja utakalolifanya
litagharimu uhai wa mke
wako na wewe pia.Hii ni
operesheni ya kitaifa na
lazima ifanikiwe kwa
gharama zozote zile na
kumrejesha Edger Kaka
Nyumbani.Umenielewa?
akasema Mathew
“Kwa upande wangu nina
wasiwasi mkubwa na hicho
mnachotaka
kukifanya.Ninawashauri
msikifanye kwani ni hatari
kubwa na kitazidi kuyaweka
mahusiano ya nchi zetu mbili
katika mashaka
makubwa.Serikali ya Israel
wakigundua hiki
mlichokifanya mtajiletea
matatizo makubwa ninyi na
taifa lenu.Nawahakikishia
kwamba hakuna
atakayeshiriki katika jambo
hili atakayebaki salama”
akasema Dr Yonathan
“Dr Yonathan naomba
ufahamu kwamba
tunachokifanya sisi ni
muendelezo wa kile
walichokianzisha
Israel.Walivamia ardhi yetu
wakaua na kumteka raia
wetu,tunachokitaka sisi ni
kumkomboa Raia wetu
ambaye walimteka hivyo huu
si uvamizi bali tunakwenda
kumchukua raia wetu ka
kutumia njia ile ile
waliyoitumia wao”akasema
Mathew
“Edger Kaka ni mtu
muhimu sana kwa nchi
yangu.Ni yeye ambaye
tunamtegemea atuonyeshe
mahala walipo wafadhili
wakuu wa vikundi vya ugaid
ambavyo vinaendelea kuua
waisrael”
“Tunajua umuhimu wake
kwa nchi yako lakini ukweli
unabaki pale pale kwamba
huyu bado ni raia wetu na
kama Israel inamuhitaji basi
wanatakiwa kufuata taratibu
kwa kuwasiliana na
mamlaka zetu husika.Edger
Kaka ni mtu muhimu sana
kwetu pia hivyo lazima
tumrejeshe nyumbani”
akasema Mathew
“Siwashauri mfanye hivi
jamani.Mtaibua jambo zito
amb……….”
“Dr Yonathan hauna
uwezo wowote wa kutuzuia
kufanya
chochote.Tunakwenda Kenya
kumchukua Edger Kaka na
kumrejesha nyumbani na
hakuna wa kutuzuia si wewe
wala taifa lako la
Israel.Ninataka utoe
ushirikiano kila pale
utakapotakiwa ufanye
hivyo.Umenielewa Dr
Yonathan? Akauliza Mathew
“Sawa nimekuelewa
lakini msije laumu huko
mbeleni kwamba
sikuwaonya” akasema Dr
Yonathan
Majadiliano yaliendelea
kisha Dr Yonathan
akaondoka zake.
“Nadhani hakuna tena
cha ziada kila kitu tayari
kimewekwa wazi ni wakati
wa kwenda kujiandaa kwa
safari” akasema Mathew
“Vipi kuhusu
silaha.Hatujui huko
tuendako tutakutana na
hatari gani hivyo lazima
tujihami
kw……………”akasema
Devotha lakini Mathew
akamkatisha
“Usihofu kuhusu
hilo.Tino atashughulikia kila
kitu na silaha zitapatikana”
akajibu Mathew.
“Kuna lingine unataka
kulifahamu?akauliza
“Mathew we have a
problem” akasema Devotha
“What problem?
“Rais aliniamini akanipa
idara niingoze lakini jana
nilifanya mambo
yaliyonifanya nikawa adui
yake mkubwa.Nilidukua
simu yake na vile vile
kusababisha mauaji
makubwa ya watu wa idara
ya niliyokuwa
naiongoza.Rais ametoa amri
popote pale nitakaponekana
nipigwe risasi.Itakuaje pale
atakaposikia kwamba
nimejumuishwa katika
operesheni hii?Sina hakika
kama atakubali niwepo”
“Usihofu kuhusu
Rais.Leave that to me I can
handle it.Kuna lingine”
akauliza Mathew
“Hakuna” akajibu
Devotha
“Kama hakuna basi
tumemaliza hapa
kinachofuata ni kwenda
kuanza maandalizi” akasema
Mathew wote wakatoka
“Devotha tunakwenda
nyumbani kwako kuchukua
kompyuta ya
Ruby.Inahitajika sana katika
operesheni hii ” akasema
Mathew
Kutoka Samawati beach
hotel walielekea moja kwa
moja hadi nyumbani kwa
Devotha.Gosu Gosu
akamtaka Mathew abaki
garini yeye akashuka na
kumfuata Devotha ndani.
“Gosu Gosu thank
you.Uliniokoa sana pale
ulipoingia mle
ndani.Nilimuona Mathew
machoni alikuwa
amedhamiria kuniua na
kama si wewe angenitoa
uhai.Yule mtu ni hatari
sana.Sikuwa nimetegemea
kabisa kama ningeweza
kumkuta mle
chumbani.Halafu namna
alivyoweza kunikamata na
kuniingiza mle chumbani
mpaka sasa ninajiuliza
alifanyaje kwani kufumba na
kufumbua nilijikuta nikiwa
ndani” akasema Devotha
“Don’t mess with him
again.Mathew ni mtu mzuri
lakini ni mbaya mno pale
unapomkorofisha” akasema
Gosu Gosu
“Hata sasa bado naona
hana imani na mimi.Nina
wasi wasi nini kitatokea
huko mbeleni”
“Usihofu.Unachotakiwa
kukifanya ni kufuata
maelekezo yake na kufanya
kile anachokuelekeza”
“Nitafanya hivyo”
akasema Devotha na
kumpatia Gosu Gosu ile
kompyuta ya Ruby
“Vipi kuhusu
Ruby,atanisamehe kweli kwa
kile nilichokifanya?akauliza
Devotha
“I don’t know.Kwa sasa
tujielekeze katika operesheni
yetu na hayo mengine
yatakuja baadae” akasema
Gosu Gosu akabaki
amesimama akimtazama
Devotha
“Mbona unaniangalia
hivyo?akauliza Devotha
“Nothing.Anza
kujiandaa.Kumbuka hili ni
jambo la siri kubwa
sana.Funga mdomo wako
usimwambie yeyote.We’re
watching you”akasema Gosu
Gosu na kuondoka
“Siku zote nimekuwa
nikiamini kwamba mimi ni
mmoja wa watu mahiri sana
katika mambo haya ya
upelelezi lakini leo
nimethibisha kwamba bado
kiwango changu ni kidogo
mno.Kuna watu ambao wako
juu mno katika taaluma
hii.Sikuwahi kuwaza kama
Mathew angeweza kugundua
siri yangu kubwa ambayo
sikutaka watu wa hapa
nchini waijue lakini tayari
imejulikana.Kikubwa hapa
ni kujaribu kujenga
mahusiano mazuri na
Mathew ili amani kati yangu
naye iwepo.Anaonekana ni
mtu mbaya na mkatili
anayeweza kutoa uhai wa
mtu kufumba na
kufumbua.Sitakiwi
kumfanyia masihara
kabisa.Mathew amekuwa
mwanaume wa kwanza
kumuogopa” akawaza
Devotha
NAIROBI – KENYA
Helkopta iliyowabeba
Olivia na Coletha ilianza
kushuka taratibu na kutua
katika sehemu maalum ya
kutulia helkpota iliyokuwa
na herufi H ndani ya jumba
moja kubwa la ghorofa tatu
lililokuwa na uwanja
mkubwa uliopandwa majani
mazuri yenye ukijani
uliokolea.Ndege na wanyama
wa aina mbali mbali kama
vile Farasi na Punda milia
walionekana kwa
mbali.Magari ya kifahari
yalikuwa yamejipanga na hii
ilikuwa ishara tosha kwamba
aliyekuwa akiishi ndani ya
jumba hili alikuwa ni mtu
tajiri sana.
Watu sita waliovalia suti
nzuri nyeusi wakaisogelea
helkopta ile na mlango
ukafunguliwa akashushwa
Olivia halafu Coletha
wakawachukua na
kuwapeleka ndani na kila
mmoja akawekwa katika
chumba chake.Fahad ambaye
naye alikuwamo katika ile
helkopta akashuka na
kuongozwa na mmoja wa
jamaa aliyevaa suti nyeusi
hadi ndani ya jumba lile
akapelekwa ghorofa ya
pili.Mtu mmoja aliyekuwa
ndani ya ofisi nzuri
akawakaribisha wakaingia.
“Fahad karibu sana
Nairobi.Nimefurahi
kukuona” akasema Yule
jamaa mnene
“Nimefurahi kukutana
nawe pia Rashid” akasema
Fahad na Rashid
akamchukua wakaenda
katika sebule nzuri
“Vipi safari yenu
haikuwa na tatizo lolote?
Akauliza Rashid
“Hakukuwa na tatizo
lolote tumesafiri salama
kabisa”
“Nashukuru kusikia
hivyo.Poleni kwa safari”
“Tunashukuru sana”
“Nilipokea maelekezo
kutoka kwa viongozi wa juu
kwamba kila kitu
kitaendeshwa kutokea hapa
na maandalizi yote
yamekwisha fanyika”
“Nilielekezwa hivyo mimi
pia.Kwa ujumla kila kitu
kinakwenda vyema.Rais wa
Tanzania anaendelea
kutekeleza kila
tutakachomuamuru na hivi
sasa anasubiri kwa hamu
kubwa tumuambie kitu gani
kingine tunachokihitaji ili
kumuachia mwanae.Kabla ya
kumwambia kwamba
tunamuhitaji Edger Kaka
tunatakiwa kwanza kumtesa
kihisia.Tutamuacha kwa
muda bila kumpigia simu ili
kuendelea kumpa hofu
zaidi.Hatuna cha kuhofia
kwani hakuna anayejua
kama Olivia na mtoto wa
Rais hawako tena
Tanzania.Lilikuwa ni wazo
zuri sana kuamua kuwaleta
huku Kenya.Kwa kuwa
hatuna haraka na Rais
tunachotakiwa kukifanya
kwa sasa ni kumuhoji
Olivia.Maelekezo
yaliyotolewa na mama
Habiba kuna wasiwasi
kwamba Olivia anatumiwa
na serikali ya Tanzania
kuchota siri zetu na kutekwa
kwake ulikuwa ni mpango
wa serikali baada ya kupata
taarifa za kutosha kuhusu
sisi hivyo wakaamua
kumteka Olivia kumficha
wakati wanaendelea
kujiandaa kutushughulikia”
akasema Fahad.
“Fahad naomba nikuulize
kitu kimoja samahani lakini”
“Uliza Rashid usihofu”
“Una hakika kweli Olivia
alikuwa anatumiwa na
serikali ya Tanzania?
“Sina uhakika sana na
hilo lakini linawezekana”
akajibu Fahad
“Binafsi ninaingiwa na
mashaka kwa sababu kama
kweli angekuwa anatumiwa
na serikali kupata taarifa
zetu kwa muda huu wote
tayari tungekwisha ona
hatua kadhaa zikichukuliwa
na serikali ya Tanzania
katika kuwatafuta lakini
mpaka sasa hakuna hatua
zozote zilizowahi
kuchukuliwa na serikali ya
Tanzania kupambana nanyi
hii ina maana kwamba
Serikali ya Tanzania hawana
uhakika au hawajui kama IS
wana mtandao wao
Tanzania” akasema Rashid
“Nadhani wanajua ndiyo
maana wakamteka Edger
Kaka na kuidanganya dunia
kwamba amefariki katika
ajali.Nina uhakika mkubwa
wanamfahamu Edger ni nani
na hivi sasa watakuwa
wanausaka mtandao
wake.Haya yote
tutayafahamu kwa kumuhoji
Olivia” akasema Fahad.
Rashid akamchukua
Fahad hadi katika chumba
ambacho kiliandaliwa
maalum kwa ajili ya
mahojiano.Kulikuwa na kiti
ambacho nyuma yake
kulikuwa na kitambaa cheusi
chenye maandishi meupe
yalioandikwa kwa lugha ya
kiarabu.Kulikuwa na taa nne
zenye mwangaza mkali vile
vile kulikuwa na kamera
tatu.
“Maandalizi mazuri
sana.Habiba anapaswa
kufuatilia mubashara
tunavyomuhoji Olivia”
akasemaFahad na Rashid
akachukua simu yake
akampigia Habiba Jawad
“Hallo Rashid” akasema
Habiba baada ya kupokea
simu
“Mama Habiba habari za
huko?
“Huku kwema habari za
Nairobi?
“Huku salama
kabisa.Nimekupigia
kukujulisha kwamba timu ya
Dar es salaam imekwisha
wasili hapa Nairobi muda
mfupi uliopita,wote wako
salama kabisa”
“Vizuri sana.Olivia na
Yule mtoto wa Rais nao wako
salama?akauliza Habiba
“Wote wako salama”
“Ahsante kwa taarifa
hizo Rashid.Naweza
kuzungumza na
Fahad?akauliza Habiba
“Ndiyo,huyu hapa
zungumza naye” akasema
Rashid na kumpatia simu
Fahad
“Mama Habiba”akasema
Fahad
“Fahad nakupeni
hongera nyingi kwa kazi
kubwa mliyoifanya vile vile
poleni kwa safari”
“Tunashukuru
mama.Tuliondoka Dar es
salaam salama tukaenda
hadi Pemba ambako
tuliwakuta wenzetu kutoka
Mombasa wanatusubiri
tukaingia katika boti na
safari ya kuja huku
ikaanza.Tunashukuru
tumefika salama kabisa”
“Baada ya kufika Kenya
nini mipango yenu?
“Kwa kuwa tumetoka nje
ya Tanzania hatuna cha
kuhofia tena hivyo tunataka
kumtesa kwanza Rais
kihisia.Hatutampigia simu
kwa haraka na kwa muda
huu tunataka kumfanyia
mahojiano Olivia kama
ulivyoelekeza” akasema
Fahad
“Vizuri sana.Itakuwa
vyema kufahamu kama kweli
alikuwa anatumiwa na
serikali ya Tanzania kuchota
siri zetu”
“Kila kitu kiko tayari
mama na tutakuunganisha
moja kwa moja ushuhudie
kile kinachoendelea hapa”
“Nitafurahi sana”
akasema Habiba na vijana
waliokuwa katika chumba
kingine kilichokuwa na
mitambo na kompyuta
kadhaa wakaelekezwa
kumuunganisha Habiba ili
aweze kushuhudia Olivia
akihojiwa.Baada ya kila kitu
kukamilika Fahad akaagiza
Olivia aletwe katika kile
chumba cha
mahojiano.Akawekwa katika
kiti na mikono ikafungwa
mfuko ukatolewa
kichwani.Alikuwa dhaifu
mwili wake ulikuwa
umevimba kutokana na
kupigwa na mateso makali
aliyoyapata kutoka kwa
akina Kaiza.Kamera
zikawashwa na Fahad
akachukua kiti akamsogelea
Olivia.
“Olivia pole
sana.Unajisikiaje
sasa?akauliza Fahad
“I’m fine” akajibu Olivia
kwa sauti ndogo
“Olivia unaweza
kufahamu hapa uko
wapi?akauliza Fahad Olivia
akatikisa kichwa ishara
kwamba hafahamu chochote
“Can you guess?akauliza
Fahad
“I can’t” akajibu Olivia
“Olivia japokuwa hali
yako bado dhaifu lakini kuna
mambo ambayo tunataka
kuyafahamu kutoka kwako
ndiyo maana uko hapa
kuhojiwa”
“Nini mnataka
kukifahamu? Akauliza Olivia
“Tunataka kufahamu
namna ulivyotekwa na kile
kilichotokea baada ya
kutekwa” Akauliza fahad.
“What is the meaning of
this?Kwa nini mnanirekodi?
Niko kwenye
hukumu?akauliza Olivia
“Olivia just answer the
question! Akasema Fahad.
“Nilitekwa wakati
ninarejea nyumbani kutokea
Kinshasa kuonana na Seif
Almuhsin.Walioniteka ni
idara ya serikali
inayojulikana kama idara ya
siri ya mambo ya ndani ya
nchi.Walipata taarifa kuwa
nimekwenda Kinshasa
kukutana na Seif na
wakaanza
kunifuatilia.Kikubwa
walichotaka kukifahamu
kutoka kwangu ni
mahusiano yangu na IS
kwani katika kompyuta
yangu walikuta barua pepe
nilizokuwa ninawasiliana na
Sayid Omar” akasema Olivia
“Hii idara ya siri ya
serikali walifahamuje
kuhusu wewe kukutana na
Seif Almushin?
“Idara ya usalama wa
taifa ya jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo
walipewa taarifa kwamba
Almuhsin anakwenda nchini
Congo na wakaanza
kumfuatilia na kugundua
nilikuwa na mazungumzo
naye wakaitaarifu serikali ya
Tanzania na ndipo
wakajiandaa na kuniteka”
“Nini kiliendelea baada
ya kukuteka?akauliza Fahad
“Kama nilivyowaeleza
kwamba walitaka kufahamu
mahusiano yangu na IS na
kwa kuwa walikuta
mawasiliano yangu na Sayid
Omar waliamini lazima
nitakuwa na mahusiano
nao.Ninaye rafiki yangu
anaitwa Mathew Mulumbi
huyu alinipa namba Fulani
za siri nimpigie pale
nitakapokuwa na matatizo
na nikawapa namba hizo
wapige nikiwadanganya
kwamba ni namba za Sayid
Omar walipopiga namba hizo
mifumo yao yote ikazima”
“Mifumo yao
ikazima?Kivipi?
“Idara hii ina mifumo
yake ya mawasiliano ambayo
yote ilijifunga baada ya
kutumia simu yao kupiga
namba zile”
“Huyo Mathew ni nani?
“Ni mpenzi wangu”
“Anafanya kazi gani?
“Ni mfanya
biashara.Anao mfumo wqa
ulinzi kwa ajili ya familia
yake na mimi akaniunga na
mfumo huo”
“Endelea”
“Walinitaka nifungue
mfumo wao na mimi sikujua
namna ya kuufungua
nikawaambia wakitaka
niwafungulie mfumo wao
ninataka kuzungumza na
Rais wakakubali na kumleta
Rais,nikamueleza kwamba
mwanae amechomwa
sindano yenye virusi na
atakufa kama hatatimiza
kile
ninachokitaka.Nilimuweka
wazi ili mwanae apone
anapaswa kunipa taarifa zote
za mahala alipo Edger
Kaka.Rais alikana kufahamu
chochote kuhusiana na Edger
Kaka.Nilianza kupewa
mateso makali nikitakiwa
kueleza kila kitu kuhusiana
na mahusiano yangu na
IS.Wamenitesa sana lakini
sikufumbua mdomo wangu
kusema chochote hadi
niliporejea tena katika
mikono yenu.Ahsanteni kwa
kuniokoa” akasema Olivia
“Olivia nakupa pole sana
kwa mateso
uliyoyapata.Pamoja na hayo
kuna jambo nataka
kukueleza.Baada ya kutekwa
tumefanya uchunguzi wetu
na tumegundua kwamba huu
ulikuwa ni mchezo
umechezwa kati yako na
serikali ili ionekane
umetekwa lakini ukweli ni
kwamba wewe unatumiwa
na serikali katika
kutuchunguza na kuwapa
taarifa zetu” akasema Fahad
na mstuko mkubwa
ukaonekana usoni kwa Olivia
“Sijakuelewa hicho
ulichokisema Fahad”
“Olivia tumegundua
kwamba unashirikiana na
serikali na hata kutekwa
kwako ulikuwa ni mchezo
maalum ili kutuvuruga na
kuwapa serikali nafasi ya
kushughulikia taarifa zile
ulizowapa” akasema Fahad
“Are you crazy?Nani
kawapa habari hizo zisizo na
ukweli wowote?Kitu gani
kimewafanya muhisi
kwamba ninashirikiana na
serikali kuwahujumu?
Akauliza Olivia
“Olivia tunataka majibu
ni mambo gani ambayo
umewaeleza serikali kuhusu
sisi? Olivia hili si suala la
mchezo na kama hautakuwa
mkweli basi huu utakuwa ni
mwisho wako.Tuambie
ukweli wote na ninakuahidi
tutakusamehe lakini kama
utaendelea kuficha wakati
tunafahamu kila kitu
utajiweka katika mazingira
mabaya sana ” akasema
Fahad.Olivia akamuangalia
kwa macho yaliyojaa hasira
“Sikujua kama ninyi
watu mko namna hii”
akasema Devotha na kuvuta
pumzi ndefu
“Nilimsaidia mtu wenu
Edger Kaka alipotaka
kuuawa kwa sumu.Baadae
mkanifuata na kuniambia
Edger Kaka yuko hai na
mkanitaka niwasaidie
kufanya uchunguzi wa suala
hilo.Nilikubali kuacha kazi
yangu niliyokuwa naifanya
kwa ajili ya kuwasaidia
kuufahamu
ukweli.Mliniingiza katika
mtandao wenu bila mimi
kutaka lakini bado
niliendelea kushirikiana
nanyi na hadi ukweli
ukabainika kwamba Edger
yuko hai.Kama haitoshi
nimetengeneza hadi kirusi
ambacho ameambukizwa
mtoto wa Rais ambaye ni
sawa na mdogo wangu.Ni
moja ya jambo gumu sana
ambalo nimewahi kulifanya
katika maisha yangu
kumuambukiza Coletha
virusi vile lakini nimefanya
kwa ajili ya kuwasaidia
kumpata Edger Kaka.Pamoja
na hayo yote niliyowafanyia
bado mnasema nashirikiana
na serikali?Kama ningekuwa
nashirikiana na serikali
ningekubali kuteseka namna
hii?Nimeteswa mateso
makali,nimechomwa na
umeme na kila aina ya
mateso ili kutoa taarifa za
kuhusiana nanyi lakini
sikufumbua mdomo wangu
kusema chochote
nimevumilia haya yote kwa
ajili ya kuhakikisha Edger
Kaka anapatikana.Kwa haya
yote niliyoyafanya hivi
ndivyo mnavyonilipa?
Sikujua kama ninyi ni watu
msio na shukran kiasi hiki”
akasema Olivia akionekana
kukasirika sana
“Olivia nataka ufahamu
kwamba hakuna kitu kibaya
katika mtandao wetu kama
usaliti.Kila tunapogundua
msaliti ndani ya kundi letu
adhabu yake ni kukatwa
kichwa.Tunafahamu msaada
wako mkubwa uliotusaidia
lakini yote uliyoyafanya
yameharibiwa na huu usaliti
uliofanya na umegeuka adui
yetu.Lakini kwa kuuthamini
mchango wako kwetu
tunakupa nafasi ya kukiri
kosa lako na ukitueleza
ukweli tutakusamehe ila
ukiendelea kutudanganya
utatulazimisha tuendelee na
adhabu unayoistahili”
akasema Fahad
“Ninafahamu mambo
mengi kuhusu ninyi na kama
ningekuwa nashirikiana na
serikali kama mnavyodai
nyote msingekuwepo hapa
muda huu.Kama ningekuwa
msaliti msingeupata ukweli
kuhusu Edger Kaka lakini
kama mnaamini mimi ni
msaliti nawapa uhuru wa
kufanya kile
mkitakacho.Kama ni kuniua
I’m ready.Fikisheni salamu
zangu kwa Habiba Jawad
mwambieni ninashukuru
kwa malipo aliyonilipa baada
ya kuhangaika kumtafuta
mwanae” akasema Olivia
“Olivia tueleze ukweli
tafadhali.Nakuhakikishia
tutak…………….” Akasema
Fahad na Olivi akamkatisha.
“Niueni!! akasema Olivia
Fahad akaenda katika
pembe ya chumba akachukua
panga kali akamsogelea
Olivia
“Olivia nafasi yako ya
mwisho”
“Sina cha
kuwaeleza.Nimewasaidia
kwa kila mlichokihitaji lakini
mmeamua kunilipa kwa
namna hii.Kill me! Akasema
Olivia na kufumba
macho.Fahad akaliinua
panga
“Fahad stop.Hana
mashirikiano yoyote na
serikali.Imetosha mfungueni
mpelekeni akapumzike”
akasema Habiba na Fahad
akalishusha chini panga
alilokuwa amelishika.
“Open your eyes
Olivia.It’s over” akasema
Fahad na Olivia akafumbua
macho akashangaa baada ya
kumuona Fahad
akitabasamu.Mtu mmoja
akaenda kumfungua mikono
“Mmeahirisha
kuniua?akauliza Olivia
“Olivia lile lilikuwa ni
zoezi la kupima uaminifu
wako.Tumejiridhisha wewe
ni muaminifu”
“Mmenisikitisha sana
kwa kushindwa kuniamini
hata baada ya kuwafanyia
mambo
mengi.Nimesikitishwa sana”
akasema Olivia
“Olivia usihofu.Ni
utamaduni wetu kila pale
tunapofanikiwa kumkomboa
mwenzetu ambaye alikuwa
ametekwa kumfanyia
mahojiano kufahamu
kilichotokewa wakati akiwa
ametekwa.Kwa sasa
utakwenda kupumzika”
akasema Fahad na kuwataka
watu wawili waliokuwamo
mle ndani wamchukue Olivia
na kumpeleka katika
chumba chake
alichoandaliwa akapumzike
“Mama Habiba
umeshuhudia mwenyewe
mahojiano” akasema Fahad
baada ya Olivia kutolewa mle
chumbani
“Olivia hana
mashirikiano yoyote na
serikali.Endeleeni na
mipango mingine ya
kumtafuta Seif.Mtoto wa
Rais anaendeleaje?
“Anaendelea
vyema.Olivia alimtibu jana
kabla ya kuanza safari ya
kuja huku na sasa
anaendelea vizuri”
“Vizuri sana.Lini
umepanga kumpigia simu
Rais kumpa maelekezo
kuhusu Seif?
“Nitampigia simu
kesho.Siku ya leo
ninamuacha ateseke kwa
mawazo” akasema Fahad.
DAR ES SALAAM
Mathew na Gosu Gosu
waliwasili katika nyumba ya
Rais waliyopewa waweke
makazi ya muda.Aliposhuka
garini akamfuata Ruby
chumbani kwake na
kumkuta amekaa kitandani
“Ruby unaendeleaje?
“Maendeleo yangu ni
mazuri sana” akajibu Ruby
“Namshukuru sana
Mungu kwa maendelo haya
mazuri.Ninakuhitaji sana”
akasema Mathew
“Mathew uliniahidi
kunieleza kile
kinachoendelea”
“Nitakueleza Ruby lakini
kwanza naomba nikurejeshee
kompyuta yako ambayo
Devotha aliichukua”
“Oh Thank you
Mathew.Tell me you’ve killed
her ! akasema Ruby
“Kuna mambo mengi
yanaendelea Ruby
nitakueleza kila kitu”
akasema Mathew na kuanza
kumsimulia Ruby kile
kilichotokea katika usiku wa
jana.
Machozi yalimtiririka
Ruby baada ya kusikia
namna Mathew na Gosu
Gosu walivyohangaika
kuyaokoa maisha
yake.Mathew akashindwa
kuendelea akaanza
kumbembeleza Ruby
“Nyamaza kulia Ruby”
“Mathew mimi ni nani
hadi ukanifanyia haya?
Akauliza Ruby
“Ruby wewe ni mtu wa
muhimu sana kwangu na
ndiyo maana nilikuwa tayari
kufanya kila lililo ndani ya
uwezo wangu kuhakikisha
unapata matibabu”
“You killed for me
Mathew.Oh my God !
Nitakulipa nini kwa hiki
ulichonifanyia? Akauliza
Ruby
“Ruby toka
tulipofahamiana ni mimi
ambaye nimekuwa na deni
kubwa kwako na kwa mambo
ambayo umekuwa
unanifanyia mpaka leo sina
cha kukulipa.Nilichokifanya
ni kidogo sana ukilinganisha
na mambo ambayo umekuwa
unanifanyia.Ni mimi ndiye
mwenye deni kubwa kwako
ambalo hata nikitumia
utajiri wangu wote sintaweza
kulilipa”
“Mathew sifahamu
niseme nini kwa hiki
ulichonifanyia” akasema
Ruby na kuushika mkono wa
Mathew akaubusu.
“Naomba niendelee
kukueleza kile kilichotokea
jana usiku kwani bado
sijamaliza” akasema Mathew
“Endelea tafadhali”
akasema Ruby huku akifuta
machozi
“Baada ya kuhakikisha
umepata matibabu tulianza
kumsaka Devotha na kitu
cha kwanza tulichokigundua
alikuwa amewasiliana na Dr
Yonathan Cohen balozi wa
Israel hapa nchini na
wakaenda kukutana katika
ubalozi wa Israel.Baada ya
kuligundua hilo kiguu na
njia tukavamia makazi ya
balozi na kuwateka yeye na
mke wake ambaye yuko nasi
hapa.Balozi akatueleza
sababu ya kukutana na
Devotha usiku wa leo na
akatueleza kitu ambacho
hatukuwa
tunakifahamu.Kumbe
Devotha ni wakala wa
shirika la ujasusi la
Israel.Mossad wametuma
watu wao kuja kuandaa
operesheni ya kumtafuta
Olivia” Mathew akamueleza
Ruby kila kitu kuhusiana na
Devotha,Edger Kaka na
mipango ya Mossad
“Sikufikiria kama jambo
hili ni kubwa kiasi hiki”
akasema Ruby baada ya
Mathew kumaliza kumpa
maelezo ya kina kuhusiana
na kile walichokuwa
wamekigundua.
“Baada ya kugundua
hayo yote ikalazimu kwenda
kuonana na Rais” Mathew
akaendelea
“Jitihada zilifanywa
nikafanikiwa kukutana na
Rais nikamueleza mambo
haya yote na tofauti zetu za
awali zikamalizika
tukaungana na kuwa kitu
kimoja.Hivi sasa
tunawasiliana moja kwa
moja na Rais” akasema
Mathew
“Hilo ni jambo kubwa
sana umelifanya Mathew
hongera.Nini mlikipanga
baada ya kukutana na Rais?
“Kama utakumbuka jana
usiku lilifanyika shambulio
la kigaidi katika hospitali ya
Mtodora na shambulio hilo
lilimlenga mtoto wa Rais na
magaidi walifanikiwa
kumteka wakaondoka naye
kisha wakampigia simu Rais
wakamjulisha na kumtaka
awapatie Olivia.Rais hakuwa
na namna ya kufanya
akawapatia Olivia.Rais
aliniomba sana nimsaidie
kuwakomboa Olivia na
Coletha.Ili kuwakomboa
Olivia na Coletha lazima
kwanza kumpata Edger
Kaka ambaye anashikiliwa
katika ubalozi wa Israel
nchini Kenya.Kuna namna
moja tu ya kuweza kumpata
Edger Kaka nayo ni kuvamia
ubalozi huo na
kumchukua.Rais amekwisha
toa ruhusu jambo hilo
lifanyike na hivi sasa tuko
katika maandalizi ya awali
ya operesheni hiyo ya
kwenda kumuokoa Edger
Kaka.Ili tuweze kuingia
ndani ya ubalozi huo
tunahitaji kupata ramani ya
namna jengo lilivyo na
taarifa za kiusalama hivyo
basi tunatanguliza timu ya
watu watatu kwenda Nairobi
mchana huu kuanza
kuifanya kazi hiyo.Wakiwa
kule watakuwa
wakiwasiliana nasi huku
Tanzania kutujulisha kila
kinachoendelea hivyo
nakuhitaji sana katika
operesheni hiyo.Tunahitaji
kuwa na mawasiliano kati ya
ofisi ya Dar es salaam na
watu wa Nairobi” akasema
Mathew
“Mathew hakuna tatizo
katika hilo.Mimi niko zaidi
ya tayari” akasema Ruby
“Ahsante sana Ruby
nafahamu muda wowote uko
tayari lakini kuna tatizo
kidogo” akasema Mathew
“Kuna tatizo gani
Mathew? Akauliza Ruby
“Timu inayokwenda
Nairobi mchana huu ni Gosu
Gosu,rafiki yangu mwingine
anaitwa Tino na ……”
Mathew akasita
“Mbona unasita
Mathew?akauliza Ruby
“Ruby kuna jambo
limefanyika ambalo naamini
halitakupendeza lakini
imebidi lifanyike”
“Jambo gani hilo Mathew
nieleze tafadhali” akasema
Ruby
“Ili kuweza kupata
ramani ya jengo na taarifa
zote za ulinzi inatubidi
tupandikize mtu ndani ya
Mossad jambo ambalo ni
gumu na linahitaji muda
mrefu ambao sisi hatuna
hivyo tumeamua kumtumia
mtu ambaye tayari ana
ukaribu na Mossad ili asaidie
katika kupata taarifa hizo.”
Mathew akanyamaza kidogo
halafu akasema
“Tumemshirikisha pia
Devotha katika operesheni
hii”
Ruby akamtazama
Mathew kwa mshangao
mkubwa
“Mathew naomba
usinitanie tafadhali”
akasema Ruby
“Ruby haikuwa rahisi
kwangu kufanya maamuzi
haya niliyoyafanya lakini ni
kwa ajili ya operesheni hii”
akasema Mathew
“Mathew that witch shot
me three times.She’s
supposed to be in hell right
now.Unathubutuje
kumrejesha ashirikiane nasi
tena? Akauliza Ruby
“Ruby imelazimu iwe
hivyo kwani tunahitaji mtu
ambaye anaweza kuingia
ndani ya Mossad akatusaidia
kupata taarifa muhimu za
kutuwezesha kufanikisha
operesheni yetu.Hata mimi
nafsi yangu haitaki jambo
hili lakini imebidi iwe
hivyo.Nakuomba Ruby
ukubali Devotha ashirikiane
nasi na baada ya operesheni
kumalizika nitajua adhabu
ya kumpa lakini kwa sasa ni
mtu wa muhimu sana”
akasema Mathew.
“Mathew sina cha
kusema kwa sababu wewe
ndiye kiongozi na ndiye
mwenye kauli ya mwisho
kama umeamua
kumshirikisha mtu aliyetaka
kuniua katika timu yetu sina
cha kupinga lakini Mungu
atanilipia” akasema Ruby
“Ruby my dear do you
trust me?
“With all my life” akajibu
Ruby
“Ahsante kwa kuniamini
Ruby”
“Mathew nimekuwa
ninakuamini toka siku ya
kwanza nilipofahamiana
nawe”
“Ruby nakuomba
uniamini pia katika
hili.Niliumizwa na kitendo
alichokifanya Devotha na
adhabu niliyokuwa naifikiria
kichwani kwangu ni kumuua
lakini mwanamke huyu ana
maisha marefu kama paka
kwani nimejikuta sina
namna zaidi ya kukubali
kumtumia tena kutokana na
umuhimu wake lakini this
isn’t over yet.Mimi na yeye
tutamalizana baada ya
operesheni hii kumalizika”
akasema Mathew
“Mathew sina chochote
ninachoweza
kukupinga.Kauli yako ni ya
mwisho na lazima
niiheshimu hata kama moyo
wangu hautaki”akasema
Ruby na Mathew
akamtazama kisha akauliza
“Ruby kutakuwa na
tatizo lolote kufanya kazi na
Devotha?
Ruby akafikiri kidogo
halafu akasema
“Hakuna tatizo lolote.I
trust you”
“Thank you my Ruby”
akasema Mathew akambusu
Ruby katika paji la uso na
kutoka akamfuata Gosu
Gosu
“Nimezungumza na Ruby
kuhusu Devotha” akasema
Mathew
“Amesemaje?akauliza
Gosu Gosu akionekana kuwa
na shauku ya kutaka kujua
maamuzi ya Ruby
“Haikuwa rahisi
kumshawishi akubali
kufanya kazi tena na
Devotha lakini amekubali
Devotha ashiriki katika
operesheni hii na amekubali
kufanya naye kazi.Najua
amekubali kwa kuniridhisha
mimi ila moyoni bado ana
kinyongo”
“Ahsante sana kwa
kumshawishi Ruby.Nini
kinafuata?Umewasiliana na
Tino?akauliza Gosu Gosu
“Kabla ya kuwasiliana na
Tino natakiwa kwanza
kuwasiliana na Rais na
kumjulisha hatua tuliyofikia”
akasema Mathew na
kuchukua simu akampigia
Dr Evans
“Mathew nimelazimika
kusimamisha kikao kwa
muda ili kupokea simu yako
kwani ni ya muhimu sana
kwa sasa.Nini kinaendelea
huko?
“Mheshimiwa Rais
samahani kwa usumbufu
huu”akasema Mathew
“Mathew nimekupa
uhuru wa kupiga simu yangu
muda wowote ambao
utakuwa na jambo la
kuniambia usione kama ni
usumbufu tafadhali”
“Ahsante mheshimiwa
Rais kwa heshima
hiyo.Nimekupigia
kukujulisha kwamba mchana
huu timu ya watu watatu
itaondoka hapa Dar es
salaam kuelekea Nairobi kwa
ajili ya kuanza maandalizi ya
ile operesheni.Kila kitu
tayari kimewekwa sawa”
“Safi sana Mathew.Hilo
ni jambo zuri.Lini mmepanga
kufanya operesheni?
“Mheshimiwa Rais
operesheni inategemea na
uhodari wa timu yetu
inayokwenda Nairobi namna
watakavyotekeleza yale
tunayowatuma wakayafanye
yaani kutafuta ramani ya
jengo la ubalozi wa Israel
nchini Kenya na mahala
alipofichwa Edger.Kama
wakiweza kuyakamilisha
haya mchana huu basi hata
usiku wa leo tunaweza
kufanya operesheni
yetu”akasema Mathew
“Mathew kwa nini
usiongozane na hao jamaa
wanaokwenda Nairobi ili
kuhakikisha kwamba mambo
yanakwenda haraka na kwa
mafanikio?akauliza Rais
“Usihofu mheshimiwa
Rais watu ninaowatuma
huko ninawaamini
wanaweza wakaifanya kazi
kwa haraka na kwa
ufanisi.Hata hivyo
mawasiliano kati yetu ni
makubwa na nitakuwa
nikifuatilia kila kitu
wanachokifanya kule nikiwa
hapa hapa Dar es
salaam.Mheshimiwa Rais
kuna jambo nataka
ulifahamu pia kuhusu timu
ninayoituma Nairobi”
“Ndiyo nakusikiliza
Mathew” akasema Dr Evans
“Katika timu hiyo ya
watu watatu yupo pia
Devotha Adolph” akasema
Mathew na ukimya wa
sekunde kadhaa ukapita
“Mheshimiwa Rais”
akaita Mathew
“Nimestuka sana
nilipolisikia jina la
Devotha.Huyo mwanamke
sihitaji kabisa kumuona
mbele ya macho
yangu.Nilimuamini sana
lakini kwa aliyoyafanya
hastahili kuendelea kuwa hai
na sitaki ashiriki tena suala
lolote linalohusiana na nchi
yetu.Ni msaliti na atatuuza!
akasema Dr Evans kwa ukali
“Mheshimiwa Rais
nafahamu kila kitu kuhusu
Devotha na hata mimi
nilikuwa namtafuta mno
nimuadhibu kwa kitendo
alichokifanya cha kutaka
kumuua mmoja wa watu
wangu wa karibu lakini
mheshimiwa Rais kwa sasa
Devotha ana umuhimu
mkubwa sana katika
operesheni yetu.Ni yeye
ambaye tutamtanguliza
mbele kutafuta ramani ya
jengo la ubalozi tunalotaka
kuvamia.Ni kwa umuhimu
huo ndio maana nimeamua
kumjumuisha katika kikosi
hiki”
“Mathew I real don’t like
this ! akasema Dr Evans
“Nafahamu mheshimiwa
Rais na hata mimi sikutaka
lakini imenilazimu.Naomba
uniamini mheshimiwa Rais”
Dr Evans akafikiri
kidogo halafu akasema
“Mathew kama unaona
ana umuhimu wa kushiriki
katika operesheni hiyo sawa
mjumuishe lakini kwa sharti
moja” akasema Dr Evans na
kunyamaza kimya kwa
sekunde kadhaa
“Nakusikiliza
mheshimiwa Rais” akasema
Mathew
“Baada ya operesheni
kumalizika kill her !
Ilipita dakika moja ya
ukimya Dr Evans akasema
“Mathew umenisikia
nilichokwambia?
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais”
“Good.Akishamaliza kile
ambacho umemtuma
akifanye nataka auawe”
akasema Dr Evans
“Nitafanya hivyo
mheshimiwa Rais”
“Ahsante.Ninawatakia
kila la heri katika
maandalizi yenu kama kuna
chochote mtakihitaji msisite
kuniambia”
“Ahsante mheshimiwa
Rais kwa sasa ni hilo tu
nililotaka kukufahamisha”
“Keep me posted !
akasema Dr Evans na
kukata simu
“Rais
amesemaje?akauliza Gosu
Gosu.Mathew akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Rais amekubali
tumjumuishe Devotha lakini
ameagiza baada ya kumaliza
kazi tuliyomtuma tumuue”
Gosu Gosu alistushwa na
maagizo yale akamtazama
Mathew kwa sekunde
kadhaa na kuuliza
“Mathew are you real
going to kill her?akauliza
Gosu Gosu
“I don’t know yet” akajibu
Mathew
“Mathew please don’t kill
her.She’s an asset.Kuna
mambo mengi ambayo
tutaendelea
kumuhitaji.Mathew hatuna
sababu ya kumuua Devotha
badala yake tunapaswa
kumsaidia kumuondoa
katika hatari hii ya
kuuawa.This is a win win
situation.Anatusaidia na sisi
tunapaswa kumsaidia”
akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu naomba
tusiliongelee suala hili kwa
sasa.Tujielekeze katika
safari ya Nairobi” akasema
Mathew na kumpigia simu
Tino ambaye alimjulisha
kwamba anakaribia kufika
pale nyumbani.
“Mathew wakati
tukimsubiri Tino nataka
tumalize lile suala la
Devotha” akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu Rais
amekwisha toa maelekezo
ambayo hatuna budi
kuyafuata na isitoshe hata
mimi bado nina hasira naye
sana kwa alichomfanyia
Ruby”
“Mathew kama
unakubaliana na
alichokiagiza Rais kwamba
tumuue Devotha basi tufanye
hivyo kabla hajaenda
Nairobi.Haitakuwa busara
tumtume kazi atufanyie
halafu tumuue.Mathew
hatuna sababu ya kumuua
Devotha.Nakubali amefanya
kosa kubwa na hata mimi
sikufurahia kitendo
alichokifanya lakini Devotha
bado ana msaada mkubwa
kwetu.Atatusaidia mno”
akasema Gosu Gosu Mathew
akamkazia macho
“Gosu Gosu unaonekana
kumtetea sana
Devotha,why?Mathew
akauliza
“The truth is,I don’t want
her to die” akasema Gosu
Gosu na mlango ukagongwa
Gosu Gosu akaufungua
alikuwa ni Tino amerejea.
“Karibu Tino” akasema
Mathew.
“Ahsanteni
sana.Nimerejea na huko
nilikotoka nimefanikiwa
kupata tiketi tatu katika
ndege ya shirika la ndege la
Tanzania inayoondoka saa
saba mchana kuelekea
Nairobi.Nimekata daraja la
kwanza” akasema Tino
“Safi sana” akasema
Mathew
“Vipi kwa upande wenu
mambo yamekwenda
vizuri?Tino akauliza
“Kwa upande wetu kila
kitu kimekwenda
vyema.Tumekutana na balozi
na Devotha na mambo yote
yamewekwa sawa kilichobaki
kwa sasa ni kujiandaa kwa
safari ila kuna jambo moja
ambalo nataka utusaidie
Tino kama litakuwa ndani ya
uwezo wako”
“Jambo gani Mathew?
“Mkiwa Nairobi mtahitaji
vifaa vya mawasiliano
kuhusu hilo hakuna tatizo
kwani fedha zipo mtanunua
lakini zitahitajika silaha kwa
ajili ya kujilinda kabla ya
operesheni.Unaweza
ukatusaidia kwa hilo?
“Mathew usiwe na hofu
yoyote kuhusu silaha.Hilo ni
jambo dogo sana
kwangu.Ninao mtandao
mkubwa wa watu Afrika
Mashariki na Kenya ninao
watu wangu ambao
watanipatia hizo silaha”
“Good.Pamoja na silaha
kuna jambo lingine vile vile
ambalo ninataka ukiwa
Nairobi uanze
kulishughulikia.Siku
tutakayofanya operesheni
tutalazimika kukata umeme
eneo lote la karibu na ubalozi
wa Israel.Tunatakiwa
kuifanya operesheni yetu
gizani hivyo basi kwa kuwa
tayari unao mtandao wako
jijini Nairobi anza kulifanyia
kazi hilo suala” akasema
Mathew
“Hesabu hilo nalo
limekwisha.Mtandao wangu
unao watu wazito na hilo
suala nitalifanikisha”
akasema Tino.
“Sawa ndugu zangu
naona yale yote yalipangwa
kufanyika asubuhi ya leo
yamekamilika kinachofuata
kwa sasa ni kujiandaa kwa
ajili ya safari”
Mathew,Gosu Gosu na
Tino wakaingia katika gari la
Mathew wakaondoka
kuelekea nyumbani kwa
Mathew ambako Gosu Gosu
alikuwa ameacha sanduku
lake halafu wakaelekea
nyumbani kwa Tino naye
akachukua vitu vichache
alivyovihitaji wakatoka na
kuelekea nyumbani kwa
Devotha ambaye tayari
alikwisha jiandaa
wakamchukua na kuelekea
uwanja wa ndege
“Guys this is
it.Nawatakia kila la heri
katika safari yenu hii mfike
salama na mtekeleze jukumu
mlilotumwa.Ninawategemea
sana ndugu zangu na nchi
inawategemea
pia.Kumbukeni hamtarejea
tena Tanzania hadi
operesheni itakapokamilika
hakikisheni mnakuwa
salama” akasema Mathew na
kuwaaga akina Gosu Gosu
ambao waliingia ndani
sehemu ya kusubiri
ndege.Mathew hakuondoka
hadi pale alipohakikisha
ndege waliyopanda akina
Tino imepaa
“Mungu awatangulie
tutakutana Nairobi” Mathew
akasema kwa sauti ndogo
akawasha gari lake na
kuondoka akarejea katika
makazi yao ya muda moja
kwa moja akaelekea katika
chumba cha Ruby.
“Ruby akina Gosu Gosu
tayari wameondoka kuelekea
Nairobi.Tunahitaji
kuwasiliana nao pindi tu
wakifika hivyo basi
tunapaswa kuanza kuandaa
ofisi kwa ajili ya
mawasiliano.Dar es salaam
hadi Nairobi kwa ndege ni
mwendo wa saa moja na
nusu hivi hivyo maandalizi
yanatakiwa yaanze mara
moja” akasema
Mathew.Ruby akamtazama
akamshika mkono na
kusema
“Mathew moyo wangu
hauko tayari kufanya kazi na
mtu aliyetaka kuniua lakini
nitafanya kwa ajili yako.You
want to know why?akauliza
Ruby
“Ndiyo Ruby ningependa
kujua”akasema
Mathew.Ruby akamtazama
Mathew machoni akafumbua
midomo yake laini akasema
‘It’s because I love you
Mathew”
Mathew akatabasamu
kidogo halafu akasema
“I love you too Ruby”
“Mathew naelewa
unanipenda kama rafiki
yako,kama mtu wako wa
karibu lakini mimi ni tofauti
kidogo.Nakupenda Mathew
like I..ouh gosh I don’t know
how to say it” akasema Ruby
“Niambie Ruby chochote
unachotaka kuniambia”
akasema Mathew.Ilimlazimu
Ruby kuvuta pumzi halafu
akasema
“Mathew nilikupenda
sekunde ya kwanza
nilipokutia
machoni.Niliamini wewe
ndiye mwanaume pekee
ambaye ninastahili kuwa
naye maishani.Mathew I
know you have a wife and
beautiful kids na hiyo ndiyo
sababu iliyonifanya niishi na
mzigo huu mzito moyoni
mwangu kwa muda mrefu
lakini siwezi kuendelea tena
kubeba zigo
hili.Nimechungulia kaburi na
kwa hiki kilichonitokea ni
kama vile nimekumbushwa
kwamba maisha haya ni
mafupi sana na uhai
unaweza ukakutoka sekunde
yoyote ile hivyo tunatakiwa
kuyaishi maisha tuliyonayo
sasa.Hakuna anayeijua
kesho yake.Kama una kitu
cha kumwambia mtu
mwambie sasa na usisubiri
hadi kesho kwani hujui kama
utaiona hiyo kesho.Kwa
nafasi hii niliyoipata baada
ya kunusurika kifo ninataka
nikueleze Mathew kwamba
wewe ndiye mwanaume wa
maisha yangu.Nakuhitaji
Mathew katika dunia
yangu.Milango ya himaya
yangu nimekwisha ifungua
kwako muda mrefu sana ila
bado hujaingia.Mathew
nakutaka uwe mpenzi
wangu” akasema
Ruby.Mathew alibaki
anamtazama Ruby
akashindwa aseme nini
“Ruby sijui niseme nin…”
“Usiseme chochote
Mathew kwani nafahamu
utakachokisema na
kitanivunja moyo wangu
sana lakini naomba
unisikilize.Najua una mke
lakini niko tayari kuwa
mpenzi wakjo wa siri bila
mke wako kujua.Niko tayari
kuzaa nawe mtoto.Kama
uliweza kuwa na Olivia bila
mkeo kujua naomba uwe na
mimi pia.Sijali una
wanawake wangapi pembeni
ya mke wako lakini
ninachohitaji ni penzi lako
Mathew” akasema Ruby kwa
hisia kali na kwa mbali
macho yake yalilengwa
machozi.
“Look at me Mathew”
akasema
“I’m very pretty may be
than your wife and your
Olivia but….” Akashindwa
kuendelea akamwaga
machozi
“Ruby
nimekuelewa.Nyamaza
kulia.Nimekuelewa yote
uliyoniambia” akasema
Mathew
“Umenielewa?
“Ndiyo nimekuelewa
lakini ninaomba
tuyazungumze baada ya
operesheni yetu
kumalizika.Tushike suala
moja tulimalize kwanza
halafu tutaingia tena katika
suala lingine.Jambo hilo
linazungumzika”
“Mathew nataka
tulimalize suala hili hapa
hapa.Nina hofu kubwa baada
ya kunusurika kifo”
“Ruby wewe
unanifahamu mimi vizuri
pengine kuliko mtu yeyote,
nikisema tutalizungumza
jambo hili amini
hivyo.Nakuahidi Ruby mara
tu operesheni hii
itakapomalizika mimi na
wewe tutakwenda mahala
mbali na Dar es salaam
tukiwa peke yetu tupumzike
na tutazungumza mengi
likiwamo suala hili.”
akasema Mathew na kwa
mbali tabasamu likaonekana
usoni kwa Ruby.Mathew
akamsaidia kusimama
akamshika mkono
wakatembea hadi katika ofisi
akaketi kitini na kuanza
kumpa Mathew maelekezo ya
kufanya.
“Sikutegemea kabisa
kama Ruby angeweza
kunitaka niwe mpenzi
wake.Mimi na yeye
tunaheshimiana sana na
ninamchukulia kama mdogo
wangu lakini kumbe
mwenzangu amebeba mzigo
mzito moyoni mwake.Ngoja
kwanza nijielekeze katika
operesheni nzito na baadae
tutazungumza kwani hili si
jambo dogo”akawaza Mathew
akiendelea kuuganisha vifaa
huku akielekezwa na Ruby
aliyekuwa ameketi kitini