Riwaya: Siri

Wakuu Samahani Sana nilibanwa sana ....Ndo naelekea home sina hakika kama naweza tupia ila kesho asubuhi ya kuanzia saa mbili tyu nitatupia....Nitajitahid tupige Season 3 hiyo kesho asubuhi moja mchana moja na jioni moja ...Tuombe Mungu Majukumu ya Kikaz yasinibane had nikose Muda...Tupo Pamoja
 
Hainaga kwere
 
Saa mbil tyar mkuu
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 5
EPISODE 1
Jumba la bilionea Agrey
Themba lilikuwa na mfumo wa
kisasa kabisa wa
ulinzi.Kulikuwa na kamera za
siri katika sehemu mbali mbali
za jumba lile ambazo
zilimuwezesha mtu aliyeko
ndani ya chumba kikubwa
kulala cha Agrey kufuatilia kila
kinachoendelea kuzunguka
jumba lake.Lucy Themba
alikuwa ameketi kitini
chumbani kwake akimfuatilia
Mathew Mulumbi katika
kamera toka alivyoingia
sebuleni na hadi alipovamiwa
ghafla na kuchukuliwa.
“Nilifanya kosa kubwa sana
kumuamini huyu kijana.Akili
yangu haikuwa sawa ndiyo
maana aliponiaminisha tu kuwa
yeye ni mpelelezi na anafahamu
mahala alipo Olivia
nikamuamini haraka na
kumtuma akamtafute
mwanangu sikujua kumbe
ninamtuma chui kwenda
kuniletea kondoo
wangu.Naamini baada ya
kumkamata leo ufumbuzi wa
wapi walipo mwanangu Olivia
na mume wangu Agrey
utapatikana.Huyu kijana
anafahamu kila kitu na lazima
ataeleza” akawaza Lucy
Themba huku akishuhudia
Mathew akivishwa mfuko
kichwani na kutolewa
sebuleni,akahamia katika
kamera nyingine akashuhudia
akipakiwa garini na magari
yakaondoka.
“Huyu kijana ni hatari
sana.Alitumia akili sana
kumteka mume wangu na hata
mimi nimenusurika pale
alipotaka kunihamisha
kunipeleka sehemu anakodai ni
sehemu salama.Nilifanya vyema
kukataa kwani na mimi hivi
sasa ningekwisha ungana na
akina Olivia huko waliko.Kuna
nini anakitafuta kwetu?
Anahitaji fedha?Kama ni fedha
kwa nini hataki kuwa wazi
tumpatie kuliko kuendelea
kututesa namna hii? Au kuna
watu wanamtumia ili kututesa
namna hii? Lakni leo kila kitu
kitajulikana baada ya kuhojiwa”
Akawaza Lucy na kuchukua
simu akampigia Dr Evans
“Lucy nipe mrejesho
mambo
yamekwendaje?akauliza Dr
Evans
“Dr Evans mambo
yamekwenda vizuri kama
tulivyopanga.Nimempigia simu
Mathew na kumtaka afike hapa
nyumbani na akafika bila
kuchelewa.Wale watu
uliowatuma walijipanga vyema
na kumvamia akashindwa
afanye nini wakamfunga pingu
na hivi tunavyoongea
wameondoka naye”akasema
Lucy
Dr Evans akashusha pumzi
baada ya kupewa taarifa ile.
“Lucy nakushukuru sana
kwa kusaidia huyu jamaa
amepatikana.Ni mtu muhimu
sana ambaye ninaamini atatupa
maelezo yote kuhusiana na
kutekwa kwa Olivia na
Agrey.Nina uhakika mkubwa
kwamba huyu jamaa
anashirikiana na watekaji na
anazo taarifa zote za
kinachoendelea hivyo atahojiwa
na ataeleza kila
kitu.Ninachokuomba Lucy
endelea kuwa mvumilivu kwa
wakati huu ambao tunaendelea
kushughulikia suala
hili.Nitawasiliana na mkuu wa
jeshi la polisi na kumjulisha
kuhusu kupotea kwa Agrey
Themba.Watakuja hapo
nyumbani askari polisi kukuhoji
lakini usiwaeleze kitu chochote
kuhusiana na Mathew
Mulumbi.Waeleze kwamba
Agrey alikuaga usiku wa jana
kuwa anakwenda kuonana na
mtu Fulani lakini hakukueleza
ni wapi anakwenda na
hakurejea nyumbani hadi
kulipopambazuka na simu yake
haipatikani ndipo uliponipigia
mimi simu kunijulisha kupotea
kwake.Narudia kukusisitiza
Lucy usitamke lolote kuhusu
Mathew Mulumbi.Kuna tatesi
nimezipata ambazo ninazifanyia
kazi kuwa watekaji wana watu
wao ndani ya jeshi la polisi
ndiyo maana sijataka
kuwashirikisha suala hili la
Mathew.Wale waliomchukua ni
walinzi wangu na watamuhoji
ataeleza kila kitu.Tukijua
mahala alipo Olivia na baba
yake ndipo tutawataarifu polisi
wakawachukue lakini kwa hili
la Mathew litaendelea kubaki
siri.Nadhani umenielewa
Lucy”akasema Dr Evans
“Dr Evans nimekuelewa
usiwe na wasiwasi.Nitatoa
maelezo kama
ulivyonielekeza.Nashukuru
sana kwa namna ulivyojitolea
kuisaidia familia yangu.Naomba
ufanye kila linalowezekana leo
hii Agrey na Olivia wapatikane”
akasema Lucy Themba
“Ninakuahisi Lucy,huyu
jamaa lazima atahojiwa na
ataeleza kila kitu.Nina uhakika
mkubwa sana wa kuwapata
Olivia na Agrey siku ya leo”
“Jambo lingine Dr Evans
naomba atakachowaeleza huyu
jamaa na mimi
nikifahamu.Naamini hayuko
peke yake,kuna watu nyuma
yake anaomtuma afanye haya
anayoyafanya hivyo nataka
kuwajua watu hao ni akina nani
wanaotuandama kiasi hiki.”
akasema Lucy
“Hilo ni moja wapo ya
mambo tutakayomuhoji huyu
jamaa.Hata mimi naamini
hayuko peke yake hivyo
tutamtaka atueleze watu
anaoshirikiana
nao.Tutaufahamu mtandao
wake wote na
nitakujulisha.Lucy kwa mara ya
mwisho ninarudia tena
kukusisitiza kwamba
usimweleze mtu yeyote yule
kuhusu Mathew
Mulumbi”akasisitiza Dr Evans
“Usihofu Dr Evans siwezi
kumweleza mtu yeyote”
“Ahsante
Lucy.Nitawasiliana nawe tena
baadae kukupa mrejesho wa
mahala tulikofikia”
“Nitashukuru sana Dr
Evans” akasema Lucy na kukata
simu
Wakati Lucy na Dr Evans
wakiwa katika
mazungumzo,gari lililomchukua
Mathew lilikuwa katika
mwendo mkali.Mathew alikuwa
amelazwa chini amefungwa
barabara na mitutu minne ya
bunduki ikiwa
imemuelekea.Wale jamaa
hawakutaka kufanya kosa hata
dogo kwani walikwisha onywa
yule ni mtu hatari
“Hiki kilichonitokea ni
kweli au niko ndotoni? Siamini
kama kweli nimetekwa”
akawaza Mathew na kurudisha
kumbu kumbu namna tukio lile
lilivyotokea.Akauma meno kwa
hasira
“Sikuwa na mawazo yoyote
kama tukio hili lingetokea.Ruby
alikwisha hisi kitu Fulani
kufuatia mwito ule wa Lucy
Themba lakini mimi sikuwa na
wasi wasi wowote.Nilimuamini
Lucy na sikuwa na shaka naye
hata kidogo ndiyo maana
niliitika wito wake haraka sana
aliponiita.Nilifanya makosa
kutostuka kuwa ule ulikua ni
mtego ule ambao naamini hata
Lucy Themba ameshiriki
kuuandaa.Niliwatazama hawa
jamaa walioniteka naamini ni
kikundi kimoja na wale
niliowaua kule Kigamboni jana
usiku ambao kwa mujibu wa
Ruby ni idara ya siri ya usalama
wa ndani wa nchi.Hawa ndio
wamemteka Olivia na ninaamini
hata Agrey Themba ametekwa
na wao pia.Bado ninaendelea
kuamini lazima yupo mtu
ambaye ana mahusiano na idara
hii ya siri na vile vile ana
ukaribu mkubwa na familia ya
akina Olivia kiasi kwamba
anafahamu kila
kinachoendelea.Naamini mtu
huyo ndiye aliyesuka mpango
huu wa mimi kukamatwa baada
ya kupata taarifa zangu kuwa
tayari ninafahamu mahala alipo
Olivia.Ninachojiuliza kwa nini
Lucy Themba akakubali
kutumiwa na huyo mtu na
kushiriki katika kuandaa mtego
huu ili nikamatwe wakati
nimejitolea kumtafuta mwanae
na mume wake?Ninashindwa
kuelewa je alifanya hivi kwa
shinikizo? Je na yeye pia
ametekwa na hawa watu
wakamlazimisha anipigie simu?
Mathew akaendelea kujiuliza
maswali
“Kadiri muda
unavyokwenda suala hili nalo
linaendelea kuwa
kubwa.Ninajiuliza nini sababu
ya hii inayoitwa idara ya siri ya
usalama wa ndani ya nchi
kuiandama familia ya Agrey
Themba? Walianza kumteka
Olivia,akafuata baba yake Agrey
na sasa wamenipata mimi
ambaye tayari ninafahamu nani
waliomteka Olivia.Ninaanza
kupata picha kwamba kuna siri
kubwa imejificha katika suala
hili.Si rahisi Olivia na baba yake
wakatekwa na idara ya serikali
kama hakuna jambo kubwa
lazima ipo sababu ambayo
natakiwa
kuifahamu.Yawezekana labda
Agrey Themba anajihusisha na
mambo haramu na ndiyo maana
wamemteka ili kumfanyia
mahojiano.Kama si sababu hiyo
basi ipo sababu nyingine kubwa
iliyopelekea Agrey na mwanae
Olivia watekwe.Ili kufahamu
siri iliyojificha katika sakata hili
lazima nitafute namna ya
kujiokoa kutoka katika mikono
ya hawa jamaa.Vile vile
natakiwa kumuokoa Olivia na
familia yake na hapo ndipo
nitakapoupata ukweli.Hawa
jamaa wamekwisha elezwa
mimi ni mtu hatari ndiyo maana
wananilinda namna hii na
ninaamini huko
wanakonipeleka watanihoji na
kunitesa sana lakini nikipata
nafasi hata ndogo lazima
niitumie kikamilifu
kujiokoa”akawaza Mathew
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…