SIRI
PART 1: SEASON 4
MTUNZI: PATRICK CK
Eneo lote la kuzunguka
kitalu 7 kulikuwa na giza
lililosababishwa na kukatika
kwa umeme baada ya nguzo
kulipuliwa na mlipuko.Kaiza na
watu wake waliacha gari lao
umbali wa mita mia mbili
wakatembea kwa miguu
wakiwa katika tahadhari
kubwa.Kila alipojaribu kupiga
simu kwa watu wake
waliokuwa wakilinda nyumba
ile hazikuwa zikipokelewa hii
ikazidi kumpa hofu.Walifika
katika geti la kuingilia ndani ya
ile nyumba na kukuta mtu wa
kwanza akiwa amelala chini
amekwisha kufa.Wakamgeuza
wakamtazama alikuwa
amepigwa risasi katika paji la
uso.
“Damn !! Kaiza akasema
kwa hasira
Waliendelea kuzunguka
ukuta uliozunguka ile nyumba
na kukuta miili ya watu kumi na
tatu.
“Hii ni mara ya kwanza
tukio kama hili linatokea katika
idara yetu.Nani kawaua watu
hawa wote? akajiuliza Kaiza na
kumpigia simu Zakaria
akamtaka afike pale kitalu 7
kwani wao tayati walikwisha
fika.Haraka haraka
akawaelekeza watu aliokwenda
nao waingize miili yote ndani
kisha akawasiliana na Devotha
kumjulisha kile alichokikuta
“Devotha ni hali ya
kusikitisha sana iliyoko hapa.P3
Unit imekwisha.Watu kumi na
tatu wote wameuawa
isipokuwa Zakaria peke
yake.Kitu cha kushangaza
karibu wote wamepigwa risasi
za kichwa.Inaonekana wauaji
walikuwa wanawalenga
vichwani bila wao kuwa na
taarifa ndiyo maana wameweza
kuua timu nzima”akasema
Kaiza
“Kaiza hili unaloniambia
limenipa mstuko
mkubwa.Haijawahi kutokea
toka idara hii ianzishwe
kupoteza watu wengi kiasi
hicho.Haraka sana mili yote ya
waliouawa iondolewe hapo na
kuletwa hapa kitalu 2
tuihifadhi.Vipi hapo maeneo ya
karibu hakuna taharuki
yoyote?Hakuna wananchi
wanaoishi maeneo ya karibu
ambao wamefika eneo la tukio
baada ya kusikia milio ya risasi?
“Eneo liko kimya kabisa
Devotha na inaonekana
majirani wa eneo hili
hawafahamu
kilichotokea.Ninahisi wauaji
walitumia bunduki zenye
viwambo vya kuzuia sauti na
kuua watu wetu kimya
kimya”akajibu Kaiza
“Sawa Kaiza hakikisha miili
hiyo inaondolewa haraka sana
eneo hilo” akasema Devotha na
kukata simu
“Haya ni majabu.Hadi
nitakapoiona miili ya watu wetu
ndipo nitakapoamini kama hii
ninachoambiwa na Kaiza ni kitu
cha kweli.P3 Unit ni kikosi
tegemezi kabisa katika idara
yetu na kina watu waliopata
mafunzo ya hali ya juu nje ya
nchi.Ni watu ambao tumekuwa
tunawatumia katika operesheni
mbalimbali na hawajawahi
kushindwa au kuuawa hata
mmoja wao.Imetokeaje leo
wakauawa wengi kiasi
hicho?.Huyu MathewMulumbi
ni kiumbe wa aina gani
anayeweza kuwaua watu wote
hao kirahisi namna
hii?akajiuliza Devotha
“Nilitegemea suala hili
lingekuwa dogo na kumalizika
bila matatizo lakini sasa tayari
limechukua sura mpya na
limekuwa kubwa.Ameingia
MathewMulumbi na kuharibu
mchezo wote.Ngoja nimjulishe
rais hiki kilichotokea” akawaza
Devotha na kumpigia simu Dr
Evans
“Devotha habari za usiku
huu.Mambo yanakwendaje
hapo.Kila kitu kimekwenda
vizuri?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais mambo
yanakwenda
vyema.Tumefanikiwa
kumuhamisha Olivia na kumleta
hapa kitalu 2 kama
ulivyoelekeza.Vile vile tayari
tumempata Agrey Themba na
hivi tuongeavyo yuko njiani
analetwa hapa kitalu 2”
akasema Devotha
“Very good.Vipi kuhusu
MathewMulumbi?Uliweka
kikosi cha kumsubiri pale kitalu
7?akauliza Dr Evans
“Mheshimia rais tumepata
mafanikio katika sehemu zote
lakini kuna tatizo kidogo katika
upande wa Mathew”
“Kuna tatizo gani
Devotha?Mmeshindwa kumpata
Mathew?Hajafika kitalu
7?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais hivi sasa
Kaiza na timu ndogo
nimewatuma waende kitalu 7
baada ya kupokea taarifa
kutoka kwa mmoja wa watu
wetu aliye ndani ya P3 unit
kwamba kumetokea wamavizi
na wameua watu wetu.Kaiza
amefika hapo na taarifa
aliyonipa ni mbaya sana.Watu
kumi na tatu wameuawa
isipokuwa mmoja tu” akasema
Devotha na kumstua Dr Evans
“Kikosi kizima kimeuawa?
Imewezekanaje wakauawa
wote?akauliza
“Amesalia mmoja tu
mheshimiwa rais”
“Kusalia mtu mmoja si
hoja.Ninachotaka kufahamu ni
namna hawa watu
walivyouawa.P3 Unit ni kikosi
maalum katika idara yetu
chenye mafunzo ya hali ya juu
na ndicho kikosi
tegemeo.Wamefanya
operesheni nyingi na hakuna
opereseni hata moa waliyowahi
kumpoteza mtu.Nini kimetokea
hadi wauawe wote?Una hakika
ulipeleka P3 unit kweli?
“Ndiyo mheshimiwa rais
kikosi kilichokwenda kulinda
pale kitalu 7 ni P3 unit”akajibu
Devotha
“MathewMulumbi
!!Mathew!!!..akasema Dr Evans
huku akisikika akigonga meza
kwa hasira
“Ni kiumbe wa aina gani
huyu?akauliza Dr Evans na
ukapita ukimya
“Devotha huyu mtu tayari
amevuka mpaka na kama
tusipokuwa waangalifu
atavuruga kila kitu.Hiki
alichokifanya leo ni tangazo la
vita hivyo tunapaswa kumsaka
kwa kila uwezo tulio nao na
kuhakikisha anapatikana.Bila
kumpata MathewMulumbi
tumekwisha.Nataka mpaka
kufikia kesho asubuhi nipate
mikakati yako namna ya
kumpata Mathew.Kama hauna
mikakati au uwezo wa kumpata
nieleze ukweli ili niweze
kutumia vyombo vingine
kumpata lakini nina imani na
idara yako kuwa hamuwezi
kushindwa kumpata Mathew.”
akasema Dr Evans
“Sawa mheshimiwa rais
tutafanya hivyo.”akasema
Devotha
“Devotha kwa sasa baada
ya kumpata Agrey Themba
hakikisha unamfungua
Olivia.Nina uhakika mkubwa
kwamba kwa kumumia baba
yake lazima atafunguka kila
kitu.Hakikisha kabla ya
mapambazuko uwe tayari
umefahamu kila kitu kuhusu
Olivia na IS” akasema Dr Evans
na kukata simu
PART 1: SEASON 4
MTUNZI: PATRICK CK
Eneo lote la kuzunguka
kitalu 7 kulikuwa na giza
lililosababishwa na kukatika
kwa umeme baada ya nguzo
kulipuliwa na mlipuko.Kaiza na
watu wake waliacha gari lao
umbali wa mita mia mbili
wakatembea kwa miguu
wakiwa katika tahadhari
kubwa.Kila alipojaribu kupiga
simu kwa watu wake
waliokuwa wakilinda nyumba
ile hazikuwa zikipokelewa hii
ikazidi kumpa hofu.Walifika
katika geti la kuingilia ndani ya
ile nyumba na kukuta mtu wa
kwanza akiwa amelala chini
amekwisha kufa.Wakamgeuza
wakamtazama alikuwa
amepigwa risasi katika paji la
uso.
“Damn !! Kaiza akasema
kwa hasira
Waliendelea kuzunguka
ukuta uliozunguka ile nyumba
na kukuta miili ya watu kumi na
tatu.
“Hii ni mara ya kwanza
tukio kama hili linatokea katika
idara yetu.Nani kawaua watu
hawa wote? akajiuliza Kaiza na
kumpigia simu Zakaria
akamtaka afike pale kitalu 7
kwani wao tayati walikwisha
fika.Haraka haraka
akawaelekeza watu aliokwenda
nao waingize miili yote ndani
kisha akawasiliana na Devotha
kumjulisha kile alichokikuta
“Devotha ni hali ya
kusikitisha sana iliyoko hapa.P3
Unit imekwisha.Watu kumi na
tatu wote wameuawa
isipokuwa Zakaria peke
yake.Kitu cha kushangaza
karibu wote wamepigwa risasi
za kichwa.Inaonekana wauaji
walikuwa wanawalenga
vichwani bila wao kuwa na
taarifa ndiyo maana wameweza
kuua timu nzima”akasema
Kaiza
“Kaiza hili unaloniambia
limenipa mstuko
mkubwa.Haijawahi kutokea
toka idara hii ianzishwe
kupoteza watu wengi kiasi
hicho.Haraka sana mili yote ya
waliouawa iondolewe hapo na
kuletwa hapa kitalu 2
tuihifadhi.Vipi hapo maeneo ya
karibu hakuna taharuki
yoyote?Hakuna wananchi
wanaoishi maeneo ya karibu
ambao wamefika eneo la tukio
baada ya kusikia milio ya risasi?
“Eneo liko kimya kabisa
Devotha na inaonekana
majirani wa eneo hili
hawafahamu
kilichotokea.Ninahisi wauaji
walitumia bunduki zenye
viwambo vya kuzuia sauti na
kuua watu wetu kimya
kimya”akajibu Kaiza
“Sawa Kaiza hakikisha miili
hiyo inaondolewa haraka sana
eneo hilo” akasema Devotha na
kukata simu
“Haya ni majabu.Hadi
nitakapoiona miili ya watu wetu
ndipo nitakapoamini kama hii
ninachoambiwa na Kaiza ni kitu
cha kweli.P3 Unit ni kikosi
tegemezi kabisa katika idara
yetu na kina watu waliopata
mafunzo ya hali ya juu nje ya
nchi.Ni watu ambao tumekuwa
tunawatumia katika operesheni
mbalimbali na hawajawahi
kushindwa au kuuawa hata
mmoja wao.Imetokeaje leo
wakauawa wengi kiasi
hicho?.Huyu MathewMulumbi
ni kiumbe wa aina gani
anayeweza kuwaua watu wote
hao kirahisi namna
hii?akajiuliza Devotha
“Nilitegemea suala hili
lingekuwa dogo na kumalizika
bila matatizo lakini sasa tayari
limechukua sura mpya na
limekuwa kubwa.Ameingia
MathewMulumbi na kuharibu
mchezo wote.Ngoja nimjulishe
rais hiki kilichotokea” akawaza
Devotha na kumpigia simu Dr
Evans
“Devotha habari za usiku
huu.Mambo yanakwendaje
hapo.Kila kitu kimekwenda
vizuri?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais mambo
yanakwenda
vyema.Tumefanikiwa
kumuhamisha Olivia na kumleta
hapa kitalu 2 kama
ulivyoelekeza.Vile vile tayari
tumempata Agrey Themba na
hivi tuongeavyo yuko njiani
analetwa hapa kitalu 2”
akasema Devotha
“Very good.Vipi kuhusu
MathewMulumbi?Uliweka
kikosi cha kumsubiri pale kitalu
7?akauliza Dr Evans
“Mheshimia rais tumepata
mafanikio katika sehemu zote
lakini kuna tatizo kidogo katika
upande wa Mathew”
“Kuna tatizo gani
Devotha?Mmeshindwa kumpata
Mathew?Hajafika kitalu
7?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais hivi sasa
Kaiza na timu ndogo
nimewatuma waende kitalu 7
baada ya kupokea taarifa
kutoka kwa mmoja wa watu
wetu aliye ndani ya P3 unit
kwamba kumetokea wamavizi
na wameua watu wetu.Kaiza
amefika hapo na taarifa
aliyonipa ni mbaya sana.Watu
kumi na tatu wameuawa
isipokuwa mmoja tu” akasema
Devotha na kumstua Dr Evans
“Kikosi kizima kimeuawa?
Imewezekanaje wakauawa
wote?akauliza
“Amesalia mmoja tu
mheshimiwa rais”
“Kusalia mtu mmoja si
hoja.Ninachotaka kufahamu ni
namna hawa watu
walivyouawa.P3 Unit ni kikosi
maalum katika idara yetu
chenye mafunzo ya hali ya juu
na ndicho kikosi
tegemeo.Wamefanya
operesheni nyingi na hakuna
opereseni hata moa waliyowahi
kumpoteza mtu.Nini kimetokea
hadi wauawe wote?Una hakika
ulipeleka P3 unit kweli?
“Ndiyo mheshimiwa rais
kikosi kilichokwenda kulinda
pale kitalu 7 ni P3 unit”akajibu
Devotha
“MathewMulumbi
!!Mathew!!!..akasema Dr Evans
huku akisikika akigonga meza
kwa hasira
“Ni kiumbe wa aina gani
huyu?akauliza Dr Evans na
ukapita ukimya
“Devotha huyu mtu tayari
amevuka mpaka na kama
tusipokuwa waangalifu
atavuruga kila kitu.Hiki
alichokifanya leo ni tangazo la
vita hivyo tunapaswa kumsaka
kwa kila uwezo tulio nao na
kuhakikisha anapatikana.Bila
kumpata MathewMulumbi
tumekwisha.Nataka mpaka
kufikia kesho asubuhi nipate
mikakati yako namna ya
kumpata Mathew.Kama hauna
mikakati au uwezo wa kumpata
nieleze ukweli ili niweze
kutumia vyombo vingine
kumpata lakini nina imani na
idara yako kuwa hamuwezi
kushindwa kumpata Mathew.”
akasema Dr Evans
“Sawa mheshimiwa rais
tutafanya hivyo.”akasema
Devotha
“Devotha kwa sasa baada
ya kumpata Agrey Themba
hakikisha unamfungua
Olivia.Nina uhakika mkubwa
kwamba kwa kumumia baba
yake lazima atafunguka kila
kitu.Hakikisha kabla ya
mapambazuko uwe tayari
umefahamu kila kitu kuhusu
Olivia na IS” akasema Dr Evans
na kukata simu