Riwaya: See Me (Nione)

SEE ME

SEHEMU YA 40/50



Nikamtizama Tyalat nakumuona akitizama kule ambako mimi nipo ambapo nilikuwa nachungulia kupitia tundu la ufunguo wa mlango, akakaza macho na kuanza kuja kule nilipo mimi lakini ni kama alikuwa anashangaa kwa juu, yaani juu ya mlango, sasa nikakaa vizuri kwa ajali ya kumnasa ndege wangu huku nikiwa makini nisijetambulika nikatoa bastola yangu kiunoni na kuikoki vizuri ilitoa sauti ndogo maana ilikuwa ya kisasa zaidi na toleo jipya kwa ajili ya kazi kama hizo za siri, sasa nikamuona akitabasamu na kisha akageuka na kunipa mgongo, sikutaka kujiuliza mara mbili mbili kwa haraka nikabinya kitasa na kufungua mlango huo na nikamuona akishtuka na kutaka kugeuka ila tayari nilikuwa nishamkwida shingoni akawa anajaribu kujivuta vuta ila na kutaka kujinasaua ila mdomo wa bunduki nikaweka kichwani pake na akatulia tuli mithili ya maji ya mtungini,nikamkokota na kumuingiza ndani ya choo kile cha kisasa kisha na kifunga mlango, akaonekana kushangaa sana baada ya kuingia humo ndani, akaona shimo kubwa likiwa wazi ambalo ndipo nilipopita akataka kuzungumza kitu ila nikamuwahi kwa kumsonteshea kidole kuwa anyamaze na akatii huku akitetemeka, macho yake yalikuwa ya rangi ya Brown alikuwa mwembamba na mwenye nywele ndefu kama wazungu wengine sema yeye tu alikuwa na ngozi nyeusi yenye mvuto wa kuvutia kama wanawake wengine warembo wa afrika.
Nikamsonteshea bastola kuwa ashuke chini huku nikimulika kule chini na tochi, nikamuona akitetemeka huku akijitahidi kuficha maungo yake ya mwili maana alikuwa na chupi na sidiria kifuani, akatingisha kichwa kuwa hawezi kushuka ila nikamkazia macho na kukunja ndita kiasi kilichofanya mpaka aogope na taratibu akasogelea shimo lilo na kutanguliza mguu mpaka kwenye makanyigio ya ngazi, uso wake ulihisi kinyaa kila aliponitizama na yeye mwenyewe kuna muda alitaka kutapika, akaanza kwenda chini taratibu huku nikijitahidi kumulika mwanga wa tochi ili akanyage sehemu sahihi, akashuka mpaka umbali haliopo diana na nikaona diana akimvuta kwenda katika lile bomba la pili,
“ Madam”. Nikasikia sauti zikitoka kule upande wa pili kile chumba alichokuwepo tylat kwa umakini nikasikia sauti wakija kule nilipo kwa haraka nikajificha nyuma ya mlango na kuweka silaha yangu vizuri, nikasikia wakitembea kama kwa kunyata na kitasa cha mlango kikaguswa ili kufunguliwa, na ukafunguliwa mlango taratibu huku nikiona buti ya kike ikitangulia, kwa haraka nikajitokeza na kumbana mikono yake na kufanya bastola aloishika kuanguka chini niliweza kutambua ana bastola baada ya kuiona kupitia kivuli cha ukutani, alikuwa ni mwanamke wa kizungu, akafurukuta na kujitoa kwa nguvu kisha akarusha ngumi kwa haraka ila nikainama chini na ikapita na akaacha sehemu zake za mbavu wazi, sikufanya hajuza nikashusha ngumi kwenye ubavu wake wa kushoto ila ni kama nilipiga kitu kigumu mithili ya mgomba, akatabasamu na kuleta shambulizi lake la pili, nalo nikalikwepa na mara hii ngumi ya ubavu ikatua kisawa sawa na akagugumia kwa sauti ya kike yenye maumivu, kitu nilichogundua alikuwa anaacha sana mbavu zake wazi anaonekana hakuwa professional sana wa kupigana akatizama bastola yake iliyoko chini, lilikuwa kosa kwani tayari nilikwisha muangusha chini na kuanza kumfunga na mkanda wake ambaoa hajuhi ni saa ngapi nimeutoa kiunoni, akaanza kupiga kelele ila nikampiga kichwani na akazima, kisha nikafunga mlango na kumsogeza mlangoni, nikaanza sikia sauti za watu wakija, kwa haraka nikarudi kule kwenye lile shimo na kuanza kushuka haraka haraka kupitia zile ngazi, nikawa nasikia kwa mbali wakizungumza kizungu hiyo ni baada ya kufungua mlango ule uliochukua kama sekunde 30 kufunguka maana nililaza mwili wa yule mwanamke pale,
Nikafika kule chini na kuanza kukimbia kuelekea kule tulipotokea na kwa vile diana alikwisha tangulia na yule mwanamke sikuwa na kitu cha kupoteza zaidi ya kukimbia kutoka eneo lile, nikawakuta njiani wakimalizia kushuka bomba la mwisho ili kutoka na kupanda ngazi kwenda juu ya lile tank
“ Tuna sekunde kama 120 kufika kwenye zile ngazi ni kama dakika mbili au tatu”. Nikazungumza huku nikimtizama mwanamke yule ambaye tayari alikwisha tapika siku nyingi.
“ okay dear twende”. Diana akazungumza na tukaanza kwenda huki nikimkokota yule mwanamke au binti wa kizungu,
“ Ongeza mwendo kuna panya wanatoka huko tulipopotoka kwa fujo inaonekana wapo nyuma”. Nikazungumza na kuwatanguliza mbele diana na tylat na wakatembea haraka mpaka kwenye bomba ambalo lina ngazi ambazo zinatufikisha mpaka kule juu, akaanza kupanda diana kwa harka haraka kisha akafata yule binti wa kizungu mwenye asili ya kiiafrika yani mzungu mweusi, na yeye akapanda,kisha nikafata na mimi ile napanda tu na mwanga mkali wa tochi ukamulika pale nilipokuwa nikawasikia wakiteta kwa kizungu kuwa wapo huku.
Nikaongeza kasi na kupanda mpaka juu ya tank kisha kurudisha mfuniko ule wa chuma na kufunga na nyororo zake, milio ya risasi ikaanza kusikika na risasi zikawa zinapiga ndani ya ule mfuniko, nikashuka mpaka chini na tukaingia mpaka ndani ya gari ambalo yule dereva alikuwa akitusubiri,....
Alikuwa alishaliwasha ile naingia tu naye akaliondoa kwa kasi kutoka eneo lile ambalo tupo..
“ ooh sheet kuna gari linakuja”. Diana akazungumza nikageuka nyuma na kuona gari likija kwa kasi kutufata kule tulipo.
“ Mkague ana cheap”. Nikazungumza na diana akaanza kumkagua binti binti yule bila mafanikio yeyote.
“ Mtoe hereni zake”. Nikazungumza na diana akataka kufanya ivyo ila akashindwa baada ya mlio wa risasi kusikika na kuvunja kioo cha nyuma.
“ oooh shit”. Nikazungumza na kuona gari mara hii zikiwa mbili tena jamaa wale wakionekana hawana mchezo kabisa na sisi.
“ Ongeza mwendo”. Nikazungumza huku tukiwa tumeinama na mpenzi wangu chini na pia tumemuinamisha yule msanii chini ili asidhulike maana waokoaji wake walionekana hawana mchezo kabisa,
Milio ya risasi ikazidi kusikika na kutufanya tuwe makini zaidi maana kama ungeinua kichwa basi mwisho wako ungekuwa hapo, ghafla gari ikaanza kupepesuka hiyo ni baada ya gari moja kutugonga ubavuni mwa gari yetu, na kufanya dereva aanze kukosa mwelekeo vizuri wa barabara hiyo ambayo hipo kabisa nje ya mji na makazi ya watu ni machache, sasa zikawa gari mbili moja imetubana kulia nyengine kushoto, nikajikuta nikimtukama dereva wetu kimoyo moyo kwani aliishiwa ujuzi kabisa wa kufanya, jamaa wakaanza kuligonga kwa kupokezana.
“ kumteka huyu binti ni sawa na kumteka raisi wa umoja wa mataifa”. Nikazungumza baada ya kuona kazi imekuwa ngumu sasa nikagundua ndiyo maana wale jamaa walitutumia sisi, na siyo askari wao ili kulinda siri zao kama wakikamatwa, kwahiyo wakatutumia sisi maana siri zao hatuzijuhi ata tukishikwa.
Tukawa tunajigonga kwenye siti huku yule binti akiwa katikati yetu, nikaanza kuona gari ikizidi kujigonga na sisi wa ubavuni uwenda tungevunjika kabisa.
Dereva wetu akapigwa shaba ya kichwa na kuegemea usukani, kitendo kilichofanya miguu yake kufunga breki ya ghafla, na kichwa chake kutua kwenye usukani na kufanya honi ianze kulia tayari alikuwa amekwishafariki. Gari ikasimama katikati ya barabara, nikatoa bastolo na kutizama risasi zilikuwa kwa hesbu ya harka haraka kama 12 na hivi.
Wale jamaa wakashuka maana niliwasikia wakishuka baada ya milango ya magari yao kufunguliwa, nikamshika yule binti mkono kisha nikamtizama diana ambaye naye yupo kwenye hali mbaya, paji lake la uso lilikuwa likivuja damu.
“ Nakupenda sana randy”. Akazungumza na kunitizama
“ unataka kufanya nini?” Nikazungumza baada ya kumuona akishika kitasa cha mlango na kutaka kukifungua, nikachungulia na kuona wale jamaa wakizunguka lile gari letu tuliokuwemo huku wakinyata
“ Niache kwa sasa”.
“ Hapana”.
“ Fanya hivyo randy”. Akazungumza na kwa harka akafungua kitasa cha mlango na kutoka nje kisha kubamiza mlango kwa nguvu kiasi kwamba mpka ukajilock maana ulikuwa ushaharibika kwahiyo ukajilock, nikamuona akinyanyua mikono juu, kwa harka nikamgusa yule binti shingo kwenye mishipa yake ya fahamu na akazima, wakati wale wakimtizama diana nikatumia fursa hiyo kuwahi kusogea mpaka kule mbele alipo dereva, sikufanikiwa kukaa nilikuwa nimeinama kwa chini.. nikapangua gia kwa haraka na gari ikawaka huku nikimsukuma yule dereva kushoto na kumtoa kichwa chake kwenye usukani wale jamaa wakaanza kushambulia kule nilipo na risasi mbili zikanipata kwnye bega langu la kushoto ila tayari nilikuwa nishakanyaga mafuta, lilikuwa ni tukio la sekunde chache sana na la uhatari zaidi lenye kuondoa hata maisha yangu kupita sitemillor nikamuona diana akiwa kapiga magoti huku mikono yake ikiwa nyuma ya kichwa, wale jamaa wakambeba na wengine kupanda kwenye gari haraka, sikuwahi fika afrika kusini kwhiyo nikawa naendesha tu gari hiyo ambayo muda huo ilikuwa ikitoka moshi na muda wowote ule ingezimika au kulipuka, nikaona wale jamaa wakizidi kuja na gari zao kwa kasi ya ajabu, moyo wangu uliuma sana diana kwa kitendo kile alichokifanya, tukafika kwenye daraja kubwa ambalo chini yake kuna mto mkubwa ambao nina uhakika kuna mamba wa kutosha, lile gari likawa sasa linaenda kuzima, sikujishauri nikahama njia na gari lile kupiga kuta za daraja hilo na gari ikaanza kushuka chini kwa kasi huku nikijipiga piga na kupasuka pasuka kichwani, gari ikatumbukia mtoni.


SEE MEE
 
Swez watupa hii kitu inaisha na zote znaisha hii jumapili inaisha ya kesho kutwa
 
SEHEMU YA 41/50…..



Gari ikatumbukia mtoni na kuanza kushuka kwenda chini ya maji ambayo yalionekana yana kina kirefu mno, taa za gari zikaanza kuwaka na kuzima, huku mimi nikijitoa mguu ulokuwa umebana kwenye siti, nikawa najivuta huku pumzi nikiwa nimeibana maana maji yalikuwa yashajaa ndani ya gari, nikamuona yule binti akitapa tapa huku naye mguu akiwa anataka kuunasua uliposhika,nikafanikiwa kujitoa baada ya kunyanyua kwa nguvu ile sehemu ya kukalia, nikatoa mguu wangu na kwenda nyuma ya gari nikamtoa yule binti kisha nikataka kufungua mlango ila ukashindikana, nikachukua fire extinguisher na kupiga kile kioo cha nyuma ambacho tayari kulikuwa kishavunjika ila nilikiongezea ukubwa tu wa sisi kupita maana risasi ilikivunja vunja, kikawa kikubwa nikamshika mikono yule binti na kuanza kumvuta kutoka ndani ya gari, nikamuona akikata pumzi taratibu,nikajitahidi kuogelea kwa haraka kutoka eneo lile ambalo lina giza kubwa, nikajitahidi kumtoa mpaka nchi kavu, alikuwa tayari alikwisha zimia maana mapigo yake ya moyo yalidunda kwa kasi sana, nikamtoa macho maji tumboni, huku mara kadhaa nikimpulizia pumzi mdomoni mwake akashtuka na kunitizama huku akitapika maji na kuhema juu juu, nikatizama juu ya daraja sikuona kitu maana ukiwa chini huwezi ona chochote juu ni kutokana na ukubwa wa daraja hilo, yule binti akawa anatetemeka kwa baridi maana mpaka hapo alikuwa na chupi yake na sidiria pekee, nikamshika mkono wake na kumnyanyua kisha tukaanza kutembea kuelekea porini huku nikiwa sijuhi naelekea wapi.

“ We nani?”. Akaniuliza kwa kingereza huku akikata mkono wangu na ikaachana, alipata ujasiri wa ghafla.

“ Unataka nini kwangu?”. Akaniuliza kwa kingereza niliweza kuielewa lugha ya kingereza maana kila kitu nilisoma japani lugha ambayo sikuhisoma ni kiarabu pekee.

“ Naomba twende”. Nikazungumza kwa kingereza na nikamuona akitingisha kichwa kukataa, ghafla mchakacho kwenye majani ukasikika, nikamwambia atulie ila akatingisha kichwa kuwa hataki,

“ Nipo huku”. Akazungumza kwa sauti kwa lugha kingereza na kufanya kule kwenye majani kutulie, nikatizama kwa umakini kupita mwanga wa mbaramwezi nikafanikiwa kuona nyoka mkubwa akisogea kuja kule tulipo, na binti alikuwa ananitizamana na mimi huku joka ilo likiwa linakuja nyuma yake.

“ Ushawai ona nyoka mkubwa”?. Nikazungumza na kauli yangu ikamfanya kwa haraka anirukie juu na kunikumbatia kwa nguvu huku akijikunyata na kufurukuta furukuta, nikaanza rudi nyuma taratibu maana joka lile lilikuwa lina tutizama sasa, nikawa natizama kwa umakini huku nikirudi nyuma kwa umakini na binti yule kutokana na mwili wake kuwa mwepesi hakunipa uzito wowote ule,nikageuka kwa haraka na kuanza toka nduki huku nikiwa nimembana vizuri yule binti, na nyuma huku tukisikia michakacho ya majani kuonyesha joka lile linakuja.

“ Nikamate vizuri”. Nikazungumza huku nikiongeza kasi na kutoka eneo la majani,na kufata njia yenye vumbi vumbi lakini haikuwa ndefu sana kwani kwenye pori lile nyasi zilijaa na miti ya kutosha, sikutaka kugeuka nyuma kabisa zaidi ya kuongeza mbio, mlio wa risasi ukasikika na kufanya kwa haraka nibane kwenye mti.nikajificha bila ya kuona chochote kile wala kisikia michakacho ya majani,bega langu lilikuwa linazidi kutiririka damu za kutosha na jeraha kuzidi kuuma maana risasi mbili zilikuwa kwenye bega.nikamshusha yule binti ambaye alikuwa hataki kabisa kushuka nikaanza sikia sauti za kiarabu nikajua ni wale watu walonipa kazi wamekuja kunifata ila nikataka kupata uhakika zaidi, na inaonekana walimshambulia yule joka mkubwa, hakuwa joka mdogo .

“ Randy”. Nikaanza sikia wakiniita huku miale ya tochi ikimurika huku na kule, nikataka kujitokeza ila nikashindwa nikakumbuka kuwa sina Diana na kama nikijitokeza hawa jamaa watamchukua huyu binti na diana wangu sitompata kabisa na huenda nikampoteza kabisa

“ siwezi wapa”. Nikajisemea kimoyo moyo na kumshika yule binti mkono sasa kazi ikawa imebadirika ni kumrudisha mateka wangu kwa watu wake ili wanipe mke wnagu.

“ Tunajua umempata na unaye uko wapi?”. Sauti ya yule mtu mfupi ikasikika yule aliyenipokea na diana uwanja wa ndege. Nikajinyanyua taratibu na kumshika yule mwanamke mkono wake vizuri na tukaanza kutembea taratibu kutoka eneo hilo, huku nikijitahidi miale ya mwanga isitufikie.

“ nifate mimi nakurudisha”. Nikazungumza ili kufanya binti huyo awe pamoja na mimi,tukaendelea kutembea mwendo kama wa dakika 30 hivi, huku nikiwa nishaanza kuishiwa nguvu, kwa mbele tukaona kijiji kikubwa kilichojaa nyumba nyingi za nyasi na za udongo huku nyumba chache sana zikiwa za kisasa na zenye umeme.Mwili ukaanza kuishiwa nguvu nikaanza kupoteza nguvu ya kuona kwa mbali sana nikaona wanaume wawili wa kimasai wakiwa na mikuki mikononi na mishale, huku yule dada msanii akiwa amenikamata kwa nguvu huku akitetemeka kwani walituzunguka nikajikuta nazimia na giza zito kutua machoni mwangu…….

*************** *******************



SOMALIA


Mage hakutaka kusubiri mara mbilimbili akazidi kutembea kwa umakini mkubwa huku kila mara akitizama kulia na kushoto ili asiweze kukamatika kirahisi, akafanikiwa kufika mpaka kwenye yale mapipa makubwa ambayo uwa yanatolewa ndani ya kambi hiyo na kuperekwa kwenye boat au feli ambazo zinabeba mizigo hiyo na kuitoa na kuipereka sehemu asiyoijua hakuwa tayari kubaki hapo,akafika mpaka kwenye mapipa hayi na kufungua mfuniko mmoja, harufu kali ikamfanya afunge, ilikuwa ni mafuta ya petrol, akasogelea pipa la pili na kufungua lilikuwa na oil, akafungua na jengine na kukuta napo kuna mafuta,

“ uuh”. Akaguna kwani akiingia kwenye mafuta kwa kukosa hewa na harufu mbaya na pia mafuta ni sumu angekufa. Akafungua pipa jengine na kuona barafu akajishauri akashika shika zile barafu na roho ya kijasiri ikamwambia aingie katika barafu zile.

“ hapana”. Akaongea baada ya kuona gari ikija kubeba mizigo ile akatoka na kujibanza sehemu yenye giza kumbuka ni msichana aliyepitia mafunzo makubwa ya kijeshi, kwa haraka akatoka na kijiburuza chini na kuingia chini ya uvungu wa gari kisha akajificha, na kutulia tuli. Wale jamaa wakaanza kubeba mizigo ile na kuipakia kwanye gari walipomaliza wakafunga gari ile na wakarudi ndani ya gari, mage akajishikiria kwenye machuma ya gari lile kubwa huku akiwa makini asishike sehemu isiyokuwa sahihi, alipata maumivu makali ambayo hakuwahi kuyapata alihisi mpaka mimba yange changa uenda ingetoka, gari ikawashwa na kuanza kutoka eneo ilo.


******************
 
Reactions: ram
SEHEMU YA 42/50……




AFRIKA KUSINI


Macho yangu yakaanza kufunguka taratibu huku nikitizama sehemu niliyokuwepo sikuweza kujua niko wapi ila niliona nipo ndani ya nyumba ya udongo, na iliyokuwa na vitu vya jadi pembeni yangu kulikuwa na mwanamake mdogo mdogo niliweza kumtambua ni yule mwanamke wa kizungu ambaye ana asili ya kiafrika lakini muonekano wake kila mtu angejua tu ni mzungu kutokana na asili ya macho yake na nywele zake.

Alikuwa kavaa lubega la kimasai nilipomtizama sasa nikapata fahamu kamili kuhusu mimi maisha ya mateso nayopitia mpaka sasa, yule dada aliponiona akanifaa huku uso wake ukionyesha kutokuwa na amani kabisa

“ Umeamka”. Akazungumza kwa kingerereza nikatingisha kichwa kukubali, nikakumbuka mara ya mwisho niliona wanaume wa kimasai na ndipo nilipopoteza fahamu nazinduka ndiyo najikuta katika chumba icho,nikatizama bega langu na kuona likiwa limepakwa dawa za mitishamba amabazo zina harufu kali ambayo moja kwa moja ilipenya kwenye tundu za pua yangu. Bado maumivu niliyasikia kwenye bega langu ambayo ni sawa na kitu chenye ncha kali kunikata bila ya ganzi.

“ wale jamaa ndiyo wamenisaidia”. Nikazungumza kwa kingereza na akatingisha kichwa nikamtizama na kuona zile heleni zake za masikio zikiwaka.

“ Oooh sheet hawako mbali na hapa”. Nikazungumza kimoyo moyo baada ya kugundua heleni zile siyo za kawaida ni zinamuonyesha binti kokote kule anapokwenda na kuwaka waka vile ni ishara ya kuwa wanaomtaka binti huyo hawako mbali wapo karibu na eneo hili na huenda zilipoteza mawasiliano na ndio maana zikawaka hivyo baada ya mawasiliano kurejea.

“ Tuondoke”. Nikazungumza na kumtizama kwa kumkazia macho.

“ nilihitaji kutoroka lakini huku panatisha sana nambie kwanini uniteke”. Akazungumza

“ kama una shida na pesa nambiye nahitaji unitoe eneo hili”.

“ kama uliteka kwa ajili ya pesa nambye pia nitakupa kiasi chochote kila unachotaka”.

Wakati akizungumza ghafla tukasikia milio ya risasi nje na kufanya kwa haraka ninyanyuke kitandani huku nikijitonesha kidonda changu cha begani ambacho kinaonekana kilishaanza kukauka na uwenda nimelala kitandani hapo siku tatu au mbili nikiwa sijitambui kutokana na dalili ya kidonda navyokiona.

Nikachukua shati yangu kitandani na kumuomba tylat kwa ishara anivishe na akanisaidia ivyo, sikuwa na suruali zaidi ya kufungwa kanga ya kimasai kiunoni.

“ suruali yangu iko wapi?”.

“ waliifua iko nje”.

“ tuondoke na nionyeshe ilipo”. Nikazungumza na kuchungulia nje kupitia dirisha nikawaona wale jamaa wakisomali waliyonipa kazi wakiwa wamewaweka chini ya ulinza baadhi ya watu waamasai katika kijiji hicho ambacho kilionekana ni cha wamasai watupu, nikaona wale jamaa wakitizama huku tulipo baada ya masai mmoja kusontesha huku kidole chake, kilichotusaidia kulikuwa na zizi la ng’ombe ambalo lilijengwa kwa miti mingi iliyozunguka kwahiyo haikuwa rahisi kuniona dirishani bila kupepesa pepesa macho yake,tylat akaniletea suruali yangu kwa haraka na kunivisha kisha akashika raba zangu ambazo nilimwambia hazishike kwani muda wa kuvaa raba haukuwepo,tukatoka nje na kuzunguka nyumba ya nyumba yani ni kama bahati kwani tuanatoka tu wale jamaa nikawasikia ndani wanazungumza.

“ wako nyuma”.

Sauti yao ikafanya tuzidi kukimbia kutokomea ndani ndani ya mazizi ya ng’ombe na nyumba za matope ya mji ule wa kimasai nilijitahidi sana na kujikaza ili nisiweze kamatwa na hao watu kwani kwa sasa nahitaji kumrudisha huyu binti ili nimpate mpenzi wangu diana.sikuwa tayari kuwakabidhi mikononi mwao kwani nisingempata mpenzi wangu.

“ wale kina nani?”.

“Hao ndiyo waonipa kazi nikuteke”. Nikazungumza

“ mbona unawakimbia”. Akazungumza kwa upole

“ mpenzi wangu yupo kwa walinzi wako bila wewe kuwa hai au kukurudisha siwezi mpata”. Nikazungumza huku tukiingia kwenye vichaka

“ siwezi endelea kukimbia maana mguu wangu unasumbua uliteguka kwenye gari hawa wamasai wamenisaidia kunitibu ndiyo maana nakimbia hivi ila nahisi nautonyesha tena na utavunjika sasa”. Akazungumza huku akisimama na kuhema kama mtu anayetaka kufa ndani ya kina kirefu cha maji.

“ Jitahidi”. Nikazungumza

“ siwezi”

“ tuna siku ngapi hapa”.

“ tatu”. Akanijibu na ghafla tukasika mchakacho wawatu wakija kule tulipo,nikamshika mkono na tukaanza kukimbia tena kutoka eneo lile tukajitahidi kadiri ya uwezo wetu kutoka eneo lile la msitu na kutokomea kusikojulikana maana sikuhifahamu kabisa afrika ya kusini.

“ Vua heleni zako” nikazungumza

“ hapana walinzi wangu ndiyo wanafat hizi”.

“ vipi kama walinzi wako wakiwa wameuwawa na hao jamaa afu wakachukua hiyo simu inayoonyesha tulipo”. Nikazungumza na akatafakari

“ Nikivua hawatotupata kabisa nitapotea”. Akazungumza

“ watakupata nitajua nini nafanya”.

“ hivi unajua baba yangu ni nani eeh utanyongwa nakwambya”. Akazungumza kwa kisirani na kuvua heleni zake, miguu yake ilikuwa imeanza kuchubuka na kutoa damu, miguu yake ilijaa mikwaruzo na kuchubuka vibaya vibaya nikamuonea huruma.

“ vaa hizo raba”.

“ mmmh sihitaji”. Akazungumza na ghafla tukasikia muungurumo wa gari ikipaki nikamwambia atulie nikanyata kidogo na kuchungulia ndipo nikagundua tushafika barabarani, yani ilikuwa ni kuvuka tu kichaka na kukanyaga kwenye barabara ile ya vumbi.Nikatizama na kumuona akishuka mzee mmoja kisha akatizama kulia na kushoto na nikamuona akiingia kichaka cha pili, nikatoka kwenye kichaka na kwenda kuchungulia nikamuona akiwa akitokomea kwenye pori kisha akachuchumaa kumbe alikuwa anajisaidia huwenda ametoka mbali na tumbo limemvuluga, nikachungulia ndani ya gari sikuona mtu wala funguo, alikua ameondoka nayo na gari yake ilikuwa imechoka tena ya zamani, nikamuita yule msichana wa kizungu akaja na nikafungua mlango taratibu na tukaingia ndani ya gari lile, kisha nikakata nyaya zilizoko chini ya usukani na kuzimenya kisha nikaanza kuzigusanisha kama mtu anavyowasha kiberiti au kugonganisha mawe mawili, nikafanya bila chochote kile kutokea, yule mzee akaanza kuja nikaendelea kujitahidi kugonganisja nyaya zile na mungu akasaidia cheche zikatoka na gari ikawaka kitendo kilichofanya yule mzee ashtuke na kuanza kuja kwa kasi.

“ Am sorry”. Nikajisemea na kupangua gia kisha kukanyaga mafuta na kuondoka eneo lile kwa kasi huku nikimuona mzee yule akishika kichwa kwa mikono yake miwili na kupiga kelele.

Nikaanza kunyoosha njia kwenda tu mbele nisipopajua



*SEE ME



KAZI JAMENI…MNISAMEHE ILA NAIMALIZA KABISA H
 
SEE ME




SEHEMU YA 43/50……



Akazinduka toka kwenye usingizi mzito aliokuwa nao, alihisi kichwa chake ni kizito kama amebeba dunia hii yenye kila aina ya uovu ndani yake, alikuwa ndani ya kontena kubwa lisilokuwa na kitu chochote kile zaidi yake mwenyewe akashangaa yupo eneo gani la dunia na kafikaje eneo hilo, kumbukumbu zake kabla hazijarudi kamili mlango wa kontena lile ukafunguliwa na mwanga mkali kuingia ndani, ya kontena lile, mbele yake akaona kundi kubwa la watu wenye asili kama yeye yaana waafrika.

“ Amezinduka mtoeni nje”. Sauti ikasikika na kumfanya azidi kushangaa, wanaume wawili mbavu wakaingia na kumshika mabega mmoja kulia na mwengine kushoto, wakatoka mpaka nje na mtu huyo akashangaa mazingira hayo ila asiweze tambua chochote zaidi ya kuona kundi kubwa la watu walochanganyikana wakiwa wanaingiza kwenye roli kubwa, na yeye pia akaingizwa kwenye roli hilo lenye watu mchanganyiko mkubwa wa watu yaani watu toka mabara mbalimbali ya dunia hii,kisha gari ilo ikatolewa eneo hilo taratibu huku ikifungwa milango yake ya nyuma na minyororo mikubwa.

Akatizama na kuona watu wakilia wengine wakiwa wameshajikatia tamaa kabisa nyusoni mwao,ghafla akamuona mwanamke anayemjua na kumtambua akiwa amelala chini tena akionekana amezimia na pia tumbo lake lilikuwa kubwa, mapigo ya moyo wake yakaenda mbio alipomtizam kwa umakini na kugundua ni mke wake MAGE.



“ mage??”. Akamuita huku akimsogelea na kumtingisha tingisha, watu wote wakamtizama bila ya kumsemesha kitu, mage akafumbua macho taratibu na akakutana na sura ya mwanamume huyo.

“Jearadi?”. Akazungumza kwa sauti ya upole na ya chini sana iloyojaa uchovu mwingi, ni wazi alikuwa amechoka.

“ Unafanya nini huku”?. Jeradi akamuuliza huku akimnyanyua na kumpakata na machozi kumtoka, kichwa chake kikaanza kupata kumbukumbu kuwa mzee don john alimpigia simu na kumwambia kuwa mage amepatikana lakini akajikuta akizimwa baada ya kwenda eneo aliloelekezwa, anazinduka na kujikuta kwenye kontena na anabebwa na kuwekwa ndani ya roli kubwa yeye na baadhi ya watu, mage akajinyanyua na kumtingisha jeradi tumboni na kumfanya apige kelele za maumivu kitu kilichomshtua mage na kumtizama kwa mshangao, maumivu makali yakampata jeradi tumboni alihisi ni kama amekatwa na kisu, akashangaa amekuwaje akafunua shati lake na kujikuta akishtuka baada ya kuona bandeji upande wake wa kushoto, mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi, kijasho chembamba kikamtoka na kushangaa kawaje mpaka avishwe bandeji tumboni, kwa haraka akamfunua mage na kumkuta akiwa sawa, akamtizama jirani yake aliyekuwa amejikatia tamaa ya kuishi akamfunua shati lake na akashtuka baada ya kumuona na yeye akiwa na bandeji tumboni mwake, akajikuta akimgeukia mwengine na kumfunua huyo alimuona akiwa na nyuzi tumboni mwake upande wa kulia.

“ FIGO SINA”. Akazungumza na akachanganyikiwa akili yake kwani tayari alishatambua hakuwa na figo, akawatizama watu wote walokuwa mule, watu toka, asia, na afrika walikuwa wengi zaidi.

“ Nini kinaendelea”. Mage akamuuliza jeradi huku akiwa na wasiwasi.

“ Tunauzwa viungo”. Jeradi akazungumza huku machozi yakimtoka akajikuta akimkumbatia mage kwa nguvu na kuanza kulia kwa uchungu.

“ DON JOHN”. akazungumza kwa chuki huku akikunja ngumi na kuuma meno kwa hasira, kwa wakati huo alikuwa hajui wanaenda wapi.

“ umefikaje huku”.

“ story ndefu sana jeradi”. Mage akazungumza huku akilia kwani alijua bado yeye kutolewa chochote mwilini mwake.



***************


GARI ilo kubwa likafika sehemu isiyojulikana na mlango ukafunguliwa ilikuwa tayari ishafika usiku usiojulikana ni saa ngapi kwa mateka wale.

“ Watu weusi kushoto”. Mtu aliyevaa kinyago akazungumza huku akiwa na bunduki kubwa mkononi mwake na waafrika wakafanya hivyo, wakabaki ambao hawajuhi kiswahili ambapo walielewa baada ya kuona ngozi nyeupe ikijitenga na ngozi nyeusi. Nao wakafata msafara wakaenda kushoto.

“ mkuu wamefika”. Jamaa huyo akazungumza kwa kingereza alikuwa ni mtu mweusi na alizungumza kupitia simu,

“ sawa mkuu”. Akazungumza na wakaja wenzake na kuwachukua wale watu weusi kisha kuwafunga kamba ngumu na wakaingia kwenye jengo kubwa ambalo lipo mafichoni, eneo ilo ambalo halitambuliki ni wapi,jeradi akamuona don john akivaa kinyago ili asitambulike alimuona baada ya kushuka kwenye gari na akavishwa kinyago,

“ Don john”. Jeradi akazungumza kwa sauti na kufanya watu wote kushtuka na kumshangaa akiwemo don john mwenyewe.

“ Nimekutambua hii ndiyo biashara yenu”. Jeradi akazungumza kwa sauti kubwa, mlinzi akataka kumpiga ila don john akamzuia kwa ishara kuwa asifanye chochote.

“ Nitakuuuuuuuua”. Jeradi akazungumza na ghafla moyo wake ukashtuka baada ya kumuona mke wa baba yake aliyekuwa akilala naye kwa siri Juliana akiwa pamoja na mzee huyo.

“ Juliana”. Akazungumza na kumfanya mage na yeye ashtuke kumuona mama yake eneo hilo akatoa macho kwa msahangao na kumtizama mama yake akiwa na yeye anapewa kinyago avae usoni mwake, watu wote walikwishafanikiwa kuona sura zao ila sheria ilisema ni lazima wafiche sura zao kwa maboss watakaokuja kununua mali hizo kama figo mpaka moyo.

“ Mama”. Mage akaita kwa nguvu na kufanya juliana kuvua kinyago chake usoni na kutoa macho kwa mshangao na kumtizama mage huku moyo wake hukiwa kama huamaini anachokiona….


SEE ME
 
Mnisamehe trhe 28 nachukua likizo ya mwezi mmoja ndo zamu yangu imeanz nimepta likizo ndo tamalizia kazi maan kipnd napost vile nilivyoanza kwa moto nililuwa likiz ko hii likiz tunazimaliza hii likiz nisipomaliz basi mnitukane mtakavyo ndugu zangu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…