RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

“Noooo, Khajat!! Huyu aliyejulikana kama Joan alipiga kelele baada ya kuona Khajat ametuwa chini kama mzigo baada ya kuwa amerushwa juu. Wakati anataka kukimbilia pale alipokuwa ameangukia Khajat, Joan alishikwa na mshangao alipomwona mzee mmoja wa makamu akienda pale alipoangukia Khajat na kumchukua. Ilikuwa ni kitendo cha kasi na wepesi sana. Ilikuwa kama vile Mwewe amchukuavyo kifaranga. Yule mzee alitoweka kwenye majengo yaliyokuwa jirani. Kuona hivyo Joan akakimbilia sehemu ambayo mzee yule alikuwa ameingia na Khajat. Vilikuwa ni vitendo vya haraka, hivyo wakati Joan na yeyé akiwa anapotelea kwenye lile jengo ndipo gari la jeshi la FRPI lilipopiga breki kwa fujo eneo hilo. Wanajeshi kadhaa walishuka na kuanza kukimbilia alipokuwa ameelekea Joan.
“Shiiiiiiii! Yule mzee alisema mara baada ya Joan kutokezea kwenye chumba ambacho alikuwa amemlaza Khajat na kuanza kumpa huduma ya kwanza.
“Mzee Kasheba! Joan alisema
“Kaa hapo Joan, huyu anahitaji huduma ya haraka kama kweli tunataka aendelee kuishi! Alisema mzee Kasheba.
“Wako wanakuja huko nje! Joan alisema. Punde kidogo wakasikia mlango wa jengo hilo ukigongwa kwa nguvu.
“Oooooh shiiit! Mzee Kasheba alisema kwa mshituko.

* * *

“Wote wako hapa sipokuwa watu wawili tu ndiyo wanakosekana! Alisema askari huyu mwenye cheo cha juu jeshini huku jicho lake moja la kushoto likiwa na bandeji nyeupe iliyochafuka damu.
“Umeshajua ni nani wanakosekana, unajua inatakiwa tukamilishe kazi hii ndani ya masaa machache yajayo??!! Alisema Joseph Katanga. Ambaye alikuwa amechafuka sana, mavazi yake ya kijeshi yakiwa na matone na michirizi mingi ya damu.
“Kwa orodha iliyokuwa imetolewa mwezi wa nne siku chache kabla operesheni hii haijaanza wanaokosekana hapa ni Khajat na Joan! Alisema huyu mwanajeshi mwenye jicho lenye bandeji
“Watafutwe, hii ni sumu ambayo hapo baadae itatuathiri. Halafu Nataka kujua kwa nini wao hawakuwa na watu wa kuwachukua wakati mambo yalipoanza? Alisema Joseph Katanga. Wakati wakiongea hayo mara kaingia mtu mwingine aliyekuwa amevaa kiraia, wote wakampigia saluti. Hakujisumbua kuitikia saluti zao. Alikuwa jamaa mrefu, mzungu, mwenye kipara kinachong’aa. Aliwaangalia kwa muda bila kusema neno, halafu akatoa tabasamu la dhihaka. Hapo meno yake yaliyoungua na jino moja la dhahabu pembeni vilionekana.
“Nasikia kuna wasichana wawili wamekosekana, jitahidi watafutwe haraka. Nataka hili jambo limalizike ndani ya muda mfupi ujao ili tumiliki mambo kama tulivyopanga” Alisema huyo mtu mwenye meno machafu kwa ghadhabu.
“Tayari tumeshawaombea hifadhi Tanzania, hivyo tunangoja hao wawili wapatikane ili malengo yetu yatimie. Nawapa masaa kumi na mbili muwe mmekamilisha” Alisema huyo mzungu aliyejulikana kwa jina la KK na kutoka nje ya chumba kile huku nyuma akiwaacha Joseph Katanga na askari mwingine.
“Tumeua zaidi yawatu 200 usiku wa kuamkia leo, hebu hivi vitoto visituharibie kazi. Huyo Joan ni mjuu wa mzee Kasheba. Hebu nenda kaangalie, kama wako kwake muue yeyé halafu walete. Sitojali ukweli kuwa nirafiki yangu lakini kama hafuati nisemacho sheria hufuata mkondo wake. Fanya haraka nataka kufunga kazi hii haraka iwezekanvyo, halafu nianze kuangalia kwenye TV jinsi suala hili litakavyoongelewa! Katanga alisema huku macho yake yakionekana kuwa machovu na mekundu. Hii ni kutokana na kazi aliyokuwa ameifanya usiku kucha. Kazi ya kuongoza jeshi la FRPI kuwauwa watu wote wa jamii ya Hema na kuhakikisha hakuna mfugaji anabaki eneo hilo. Lilikuwa ni zoezi kubwa na gumu, waliua kadiri walivyoweza na kwa namna yoyote ile.
Yule askari alipiga saluti na kuondoka na vijana wengine kumi, walielekea nyumbani kwa Mzee Kasheba kuona kama wanaweza kuwapata Joan na Khajat.

*****************

Goma, DRC – 2017

Alhamisi, Saa 4:30 usiku

NDEGE maalum iliyokuwa imebeba makomandoo watano, ilikuwa ikipita juu ya anga la Goma - Congo DRC. Anga lililokuwa limefunikwa na mawingu mazito, meusi ambayo mra kwa mara yalikuwa yakimulikwa na mwanga wa radi. Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya abiria sita pamoja na rubani, japo ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria kumi na mmoja. Makomandoo wote walikuwa na vifaa vyao tayari kwa kuruka toka kwenye ndege hiyo hadi kwenye kambi maalum ya jeshi la serikali ambayo ilikuwa eneo hilo la Kivu Kaskazini.
Ilipofika eneo fulani, ndege hiyo maalum ilitoa mlio maalum, hivyo makomandoo wote wakajua walikuwa wamefika sehemu waliyotakiwa kudondoshwa. Kila mtu akaanza kuweka sawa begi lake wakati ndege hiyo ilipokaribia sehemu ambayo makomandoo hao wangedondoshwa kwa miavuli.
“Haya makamanda tuko eneo husika. Nitahesabu hadi tano, kisha nitafyatua mlango nanyi mtaruka. Mlango utakuwa wazi kwa sekunde thelathini halafu nitaufunga. Kila la kheri makamanda!” Kapteni Ambrose ambaye ndiye alikuwa rubani wa ndege hiyo alisema kwa sauti ya juu.
Makomandoo walikuwa kimya kila mmoja akiwa tayari kwa tukio.
“Moja…mbiliii…tatuuu…nnneeee… Tano twendeeee!”
Mlango ulifyatuka makomandoo wakajiachia hewani.
Ilitokea kama sadfa tu neno “shiiiiiit!” likasikika.
“Nini tena?” Kapteni Ambrose alihoji kwa hamaki baada ya kusikia komandoo mmoja akisema shiiiit!
“Limechanika, anyway ngoja niende. See you Kapteni!” alisema komandoo huyo aliyekuwa amesema shiit hapo awali, baada ya kubaini kuwa parachuti lake lilikuwa limechanika sehemu ya katikati
“High risk (ni hatari sana), ngoja kidogo!” Kapteni Ambrose alipiga kelele kumzuia yule komandoo asiruke. Lakini alikuwa ameshachelewa, yule komandoo alikuwa ameshajiachia angani!

* * *

Alhamisi, Saa 5:15 usiku

Komandoo wa kwanza alitua kwa kukimbia kwenye shamba kubwa la kahawa, zao ambalo ni maarufu eneo hilo. Dakika tano baadaye makomandoo wote isipokuwa mmoja tu walikuwa wameshafika sehemu waliyokuwa wakitarajiwa kutua. Hapo walipokelewa na wanajeshi watatu wenye vyeo vya juu wa jeshi. Makomandoo waliopokelewa ni Twaha Mchopa, Musa Buti, Mark Muga na Emily Otieno.
“Poleni kwa safari!” alisema ofisa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Meja Jean Francis Kabananga.
“Asante. Ila tuna wasiwasi na mwenzetu sijui amepatwa na madhila gani!
“Nilitaka kuuliza, maana tuliambiwa mko watano!? Meja Kabananga alisema
“Tulimsikia akilalamika akiwa angani, inaonyesha alipata changamoto ndogo, ila yeyé ni mhitimu bila shaka atafika tu,” Luteni Musa Buti mmoja wa wale makomandoo alisema. Yeye ndiye kiongozi wa wenzie kwenye misheni hii.
“Kwani hapatikani kwenye mawasiliano?” Meja Kabananga alihoji wakati wakielekea kwenye magari matatu ya kijeshi yaliyokuwa yamepaki eneo hilo.
“Dakika tatu baada ya kutua tulikuwa na mawasiliano naye. Akatuambia kwa sababu ya kuharibika parachuti lake amedondokea mbali na sehemu iliyokusudiwa. Na kama unavyoona hali hii ya upepo mkali na mvua hizi bila shaka unaweza kuelewa mtu akikutwa na ajali ya kuharibikiwa parachuti angani!” alisema Luteni Musa Buti.
“Okay, maadam ana ramani tutamngoja hapo kambini, ni kilomita kumi toka hapa. Twendeni maana mnasubiriwa kwa hamu kubwa sana na mkuu!” Meja Kabananga alisema kwa Kiswahili chake cha Kikongo. Mvua nzito ilikuwa bado ikiendelea kunyesha. Milio ya bunduki na risasi vilisikika kwa mbali, kitu kilichowaambia wale makomandoo kuwa walikuwa wameingia kwenye uwanja wa vita.
“Nasikia milio ya mashine huko! Mchoppa alisema
“Nakwambia hapa limeshakuwa swala la kawaida. Wakati wote ni wakati wa mapambano. Hali iliyofanya raia na askari wazoee tu sasa! Alisema afisa mmoja wa jeshi. Ardhi ilikuwa imelowa chepechepe!

Alhamisi, Saa 5:15 usiku.

Kilomita nane toka mahali ambapo Meja Kabananga alikuwa anawapokea wale makomandoo, huyu naye alikuwa amepokelewa kwa namna yake. Baada tu ya kutua chini, Komandoo Pablo Mahene alishtukia anamulikwa na mwanga mkali sana usoni. Wakati bado anahangaika namna ya kujitoa kwenye parachuti alishtukia anachomwa na kitu kama sindano shingoni. Fahamu zikamtoka.
“Ndiyo mkuu, kama tulivyotarajia, aliangukia eneo lilelile,” alisema jamaa mmoja mrefu sana, mweusi sana, mwenye jicho moja bovu. Wakati huu walikuwa kwenye gari moja la jeshi lililokuwa likiendeshwa kwa kasi sana kama wako kwenye barabara ya lami.
“Vema, kazi nzuri! Sasa watajua kuwa Jose Katanga karudi. Watafidia muda wote ambao nilikuwa nje ya uwanja!” Ulisema upande mwingine kwenye redio ile ya mawasiliano.
“Haya ndiyo mambo tulikuwa tunayakosa bosi, huu msisimko umerejea tena!” Alisema yule jamaa mrefu, mweusi, mwenye jicho bovu.
“Mwiteni mzee Kasheba amuhoji huyo jamaa!” Joseph Katanga alisema
 
Nisingependa kupoe hapa hivyo naombeni niweke simulizi kwa siku hizi tunazongojea season two

Bogoro – Buni, DRC

Msichana wa miaka 15 hivi, akiwa na majeraha mazito mwilini alizidi kujilazimisha kupiga hatua kwenye mtaa uliojaa maiti. Majeraha yake yaliyokuwa bado mapya yalifanya ausikie mwili wake kuwa kama ganda la kidonda kilichooza ambacho kilikuwa kikingoja mkasi kutumbuliwa ili kirushe usaa mzito. Kwa hali ilivyokuwa hakuwa na wakati wala namna ya kuyapooza majeraha yake hayo.
Kila kitu kilikuwa kimeharibika.
Nafsi yake ilikuwa imechafuka.
Akili yake ilikuwa imevurugwa vibaya.
Uwezo wake wa kufanya maamuzi ulishakufa ganzi.
Hali yake ya utu ilikuwa imeng’olewa kwa vile alivyokuwa amelazimika kuua bila kujali ili kupigania maisha yake. Maana maisha huwa na thamani kubwa sana mtu anapokuwa kwenye mdomo wa mauti. Ndiyo maana hata mgonjwa aliye dhoofu sana utashangaa anapata wapi nguvu anazotumia kupigania pumzi ya mwisho. Ni wakati mtu anapotakiwa kutoa pumzi ya mwisho ndipo huwa tayari kufanya chochote ili pumzi hizo zisimtoke!
Hakuwa akijali kitu sasa, bunduki aina ya SMG ikiwa inaning’inia begani kwake alishitushwa na mlio mkali wa ndege aina ya tai aliyekuwa akiruka wenye anga la eneo alilokuwepo.

Ndege huyu aina ya Tai alikuwa amefungua mabawa yake na kuyaachia yamiliki anga lililo juu ya kijiji kidogo kilichoko kwenye vilima ya Ituri, kijiji hicho kinaitwa Bogoro. Kiko kama kilomita 25 hivi toka mji wa Buni, Congo DRC. Tokea angani, macho yake makali yalikuwa yakiangalia juu ya barabara za mitaa ya mji huo, maiti kadhaa zilionekana zikiwa zimetapakaa mitaani. Ndege huyo fundi na mbabe wa anga, alitikisa mkia wake kwa furaha huku akitoa ukelele wa kusheherekea hali aliyoiona mitaani. Maiti zilizotapaa, hari ya baridi na unyevunyevu kufuatia mvua iliyokuwa imekatika punde, ilileta upweke kwenye mitaa hiyo ya Bogoro.

Kwa kawaida mji wa Ituri ufunikwa na mvua kubwa tangu mwezi wa pili hadi mwezi Juni. Mji huu ambao una lile pori kubwa na maarufu lenye mvua nyingi sana lijulikanalo kama msitu wa Ituri huwa wa kijani kibichi muda wote wa mwaka. Ndege walikuwa wenye furaha. Mijibwa ya mitahani ilikuwa imetulizana huku ikiwa imeshiba. Mlio wa maji yaliyokuwa yakitiririka baada ya mvua kubwa ulisikika. Hali ilikuwa kimya kabisa huku magari kadhaa-machache sana ya jeshi yalionekana kuzunguka kila baada ya dakika kadhaa. Magari hayo yalikuwa yameandikwa FRPI kifupi cha Patriotic Resistance Force in Ituri. Kwa ujumla hali ilikuwa ukiwa sana. Katikati ya hali hiyo Tai huyo aligeuza kichwa chake kumtazama binti mdogo aliyekuwa akikatiza kwenye mitaa pweke ya eneo hilo. Mitaa iliyokuwa imejaa maiti nyingi, zilizokuwa ama na majeraha mabaya ya risasi au visu. Hii ilikuwa ni masaa machache tangu yalipohitimishwa yale mauaji ya kikabila ya Bogoro ambayo wenzetu waliyabatiza jina Bogoro Massacre. Msichana huyu, alitembea taratibu huku akitetemeka kutokana na jinsi hali ilivyokuwa. Alitembea hivyo huku akijificha ficha. Tai yule alijikuta akimshangaa binti huyo, hivyo akawa akiruka anga hilo na kutoa milio ya kipekee huku macho yake makali yakimdhihaki.
Binti mwenyewe alimwangalia yule Tai kwa jicho baya, alitamani angekuwa na uwezo wa kumnyamazisha lakini alijua hilo lilikuwa nje ya uwezo wake. Alizidi kwenda kwa kujificha ficha huku akijitahidi kujificha kwenye macho ya yule Tai. Kutokana na uzoefu wake binti huyo, Tai huyo alikuwa wa hatari kama kama ambavyo magari ya wanajeshi yaliyokuwa yakipita yalivyokuwa ya hatari. Akiwa na umri wa miaka 15, tayari alikuwa amefunzwa vema kama mwanajeshi kamili, alikuwa na uwezo huo japo hakuwa na mwonekano huo. Akiwa anatokea kwenye kabila la Lendu, kabiloa ambalo hujishuhulisha na kilimo kwenye eneo hilo la Ituri, kufunzwa vita ilikuwa sehemu ya lazima kwenye jamii. Hii iliwawezesha kuwa tayari kwa vita ya kikabila kati ya kabila lake yaani Lendu na ile ya Hema. Makabila yote haya mawili yalikuwa yakipatikana kwenye jimbo hilo la Ituri huku Lendu wakijihusisha zaidi na kilimo na kabila la Hema wao wakifanya zaidi ufugaji. Ufugaji na ukulima ndiyo ilikuwa chanzo kikubwa cha kupigana kwao. Hawa wakitaka sehemu za malisho na hawa wakitaka sehemu za kulima.
Yeye akiwa kati ya watoto waliokuwa wamekamatwa kwa nguvu na kufundishwa mapigano na kundi la kijeshi la FRPI lilikuwa likiongozwa na Joseph Katanga. Ilikuwa dhahiri kichwani mwake kuwa mlio wa yule Tai, ungetuma ujumbe tosha kwa mwanajeshi yeyote kuwa eneo lile kulikuwa na mtu aliyeonekana wa ajabu ajabu. Ndiyo maana hakupenda kuona yule tai akiendelea kuzunguka eneo lile na kutoa aina ya mlio alioakuwa akitoa. Baridi kali, ubichi-ubichi, maiti za watu, upweke, majeraha aliyokuwa nayo na njaa vilifanya aonekane kiumbe wa ajabu katikati ya uwanja wa mauti.
Huku akiwa anachechemea, mara hii akaingiza mkono wake tena kuelekea sehemu za siri. Alipoutoa bado aliweza kuona damu mbichi kabisa ikiwepo. Alisimama, akavua chupi aliyokuwa amevaa. Aliiangalia ile chupi jinsi ilivyokuwa imechanwa kwa fujo na mtu aliyekuwa katika zoezi la kumbaka. Hapo machozi yakaanza kumtoka kwa mara nyingine tena. Aliitupa chini ile chupi na kuendelea kutembea tarataibu huku akichechemea kufuatia majeraha mwilini, baridi lakini pia kitendo cha kubakwa na mtu aliyekuwa amemwamini sana, Joseph Katanga. Hakutegemea kuwa siku mmoja kiongozi wao wa kundi la kijeshi, mtu aliyekuwa akihubiri kuwa alikuwa anapigania na kutafuta haki ya kabila la Lendu na jamii ya wakulima kwa ujumla angembaka kinyama namna ile. Khajat, huku silaha yake aina ya SMG ikiwa begani, silaha ambayo ilionekana kumzidi umri, alikuwa akikatisha upande mmoja wa barabara kwenda mwingine wakati aliposikia muungurumo wa gari ukija. Wakati huo huo yule Tai alizidi kupiga kelele. Alikimbia na kwenda kujibanda nyuma ya kibanda fulani kilichokuwa cha mbao. Ni wakati akiwa na hakika kuwa amejificha vema ndipo aliposikia sauti upande mwingine ikisema ‘Khajat, not safe, run this way! (Khajat, siyo salama, kimbilia huku). Ilikuwa ni sauti ya mtu aliyemjua, lakini hakuwa ni sauti ya mtu aliyetegemea kukutana naye. Aliangalia kule ilikotokea ile sauti, akamwona mtu aliyemwita, alimwangalia jinsi alivyokuwa taabani. Akajikuta anashawishika kwenda kumsaidia, wakati anakwenda akasahau kuwa alikuwa amesikia mlio wa gari hapo kabla. Kutokana na ukaribu wa yule mtu aliyemwita na jinsi alivyokuwa amejeruhiwa akakimbia tena kuvuka barabara. Wakati huo huo akasikia mvumo wa gari ukiwa jirani kabisa na alipokuwa, lakini kabla gari ile haijamfikia, ulitokea mlipuko mkubwa toka kwenye kile kibanda alichokuwa amejibanza. Mlipuko uliomrusha hewani. Akiwa hewani, msichana yule alitoa ukelele mkubwa wa hofu na maumivu “Jooooaaan!!

“Noooo, Khajat!! Huyu aliyejulikana kama Joan alipiga kelele baada ya kuona Khajat ametuwa chini kama mzigo baada ya kuwa amerushwa juu. Wakati anataka kukimbilia pale alipokuwa ameangukia Khajat, Joan alishikwa na mshangao alipomwona mzee mmoja wa makamu akienda pale alipoangukia Khajat na kumchukua. Ilikuwa ni kitendo cha kasi na wepesi sana. Ilikuwa kama vile Mwewe amchukuavyo kifaranga. Yule mzee alitoweka kwenye majengo yaliyokuwa jirani. Kuona hivyo Joan akakimbilia sehemu ambayo mzee yule alikuwa ameingia na Khajat. Vilikuwa ni vitendo vya haraka, hivyo wakati Joan na yeyé akiwa anapotelea kwenye lile jengo ndipo gari la jeshi la FRPI lilipopiga breki kwa fujo eneo hilo. Wanajeshi kadhaa walishuka na kuanza kukimbilia alipokuwa ameelekea Joan.
“Shiiiiiiii! Yule mzee alisema mara baada ya Joan kutokezea kwenye chumba ambacho alikuwa amemlaza Khajat na kuanza kumpa huduma ya kwanza.
“Mzee Kasheba! Joan alisema
“Kaa hapo Joan, huyu anahitaji huduma ya haraka kama kweli tunataka aendelee kuishi! Alisema mzee Kasheba.
“Wako wanakuja huko nje! Joan alisema. Punde kidogo wakasikia mlango wa jengo hilo ukigongwa kwa nguvu.
“Oooooh shiiit! Mzee Kasheba alisema kwa mshituko
haya ndo maneno shemeji yangu wa ukwel
 
Kilomita nane toka mahali ambapo Meja Kabananga alikuwa anawapokea wale makomandoo, huyu naye alikuwa amepokelewa kwa namna yake. Baada tu ya kutua chini, Komandoo Pablo Mahene alishtukia anamulikwa na mwanga mkali sana usoni. Wakati bado anahangaika namna ya kujitoa kwenye parachuti alishtukia anachomwa na kitu kama sindano shingoni. Fahamu zikamtoka.
“Ndiyo mkuu, kama tulivyotarajia, aliangukia eneo lilelile,” alisema jamaa mmoja mrefu sana, mweusi sana, mwenye jicho moja bovu. Wakati huu walikuwa kwenye gari moja la jeshi lililokuwa likiendeshwa kwa kasi sana kama wako kwenye barabara ya lami.
“Vema, kazi nzuri! Sasa watajua kuwa Jose Katanga karudi. Watafidia muda wote ambao nilikuwa nje ya uwanja!” Ulisema upande mwingine kwenye redio ile ya mawasiliano.
“Haya ndiyo mambo tulikuwa tunayakosa bosi, huu msisimko umerejea tena!” Alisema yule jamaa mrefu, mweusi, mwenye jicho bovu.
“Mwiteni mzee Kasheba amuhoji huyo jamaa!” Joseph Katanga alisema

*******************

SAA kumi kamili asubuhi, kikao cha dharura kilikuwa kimeanza eneo la Pugu jijini Dar es Salaam. Mada ilikuwa moja tu; kujadili hatua za kuchukua kutokana na taarifa zilizopatikana usiku kuhusu timu yao maalum waliyoituma Goma kwa kazi maalum!
“Makamanda, bila shaka mmeshtushwa na taarifa kuwa makomandoo wetu watano wako Congo DRC,” alisema Meja Jenerali Obed Mahenda, huku nyuso za makamanda waliokuwa kikaoni hapo zikionyesha ubaridi uliotokana na hali halisi kuzunguka suala lenyewe. Hapo akajua kuwa kwanza alikuwa na kazi kubwa ya kuwatuliza wajumbe wale na kuwashawishi wakubaliene na kilichofanyika hadi sasa kabla ya kutaka maoni yao juu ya nini kifanyike zaidi.
“Uamuzi wa kupeleka makomandoo hawa ulifanyika kwa ombi toka ngazi za juu, na ulifanywa na watu wachache sana kwa upande wa ndani. Hivyo itanilazimu kuelezea kwa kifupi kwa nini viongozi walituomba sisi kupeleka makomandoo watano, halafu ndiyo nitawaeleza kile ambacho inatakiwa tukifanyie uamuzi baada ya taarifa za usiku huu.”
Akazungusha kichwa kuwaangalia wajumbe tisa waliokuwa wamehudhuria kikao hiki. Mmoja kati ya wajumbe hao ni Kapteni Ambrose, rubani aliyekuwa ametumika kuwapeleka wale makomandoo. Watu wote walikuwa kimya kabisa.
“Iko hivi,” aliendelea, “nchi kadhaa zenye mapenzi mema na nchi ya DRC zilifanya kikao cha dharura. Hii ilitokana na hali iliyokuwa imejitokeza katika wiki za hivi karibuni. Kama mjuavyo kiongozi wa nchi hiyo kwa kushauriana na nchi hizo aliridhia kuitisha uchaguzi mkuu. Pamoja na Tume ya Uchaguzi, Jumatatu wiki ijayo anatarajiwa kutoa tangazo la tarehe za uchaguzi. Kila kitu kilikuwa kimepangwa vyema hadi pale ambapo ICC walipotangaza ghafla kuwa wameamua kumwachia Joseph Katanga siku kumi zilizopita.
Bila shaka wote mlizipata taarifa hizi. Katanga alitumikia kifungo chake cha muda mrefu na sasa alikuwa amebakiza miaka michache ili kumaliza. Lakini kwa maelezo kuwa amejutia na kusikitikia vitendo vyake, ICC imeamua kumwacha huru na kumrejesha DRC. Lakini pia, ICC inadai kuwa amebadilika sana kitabia. Taarifa hii ilikuwa ya kushangaza na kuchanganya. Kiufundi, kwa muda ulivyo na mazingira, Katanga akishasikia tangazo hili bila shaka atatangaza kugombea. Taarifa za kijasusi zinadai kuwa Katanga ameshaanza kufufua lile kundi lake la waasi na anakusudia kulifanya kuwa chama cha siasa. Kurudi kwa Katanga kumeharibu zaidi hali ya usalama huko Goma. Taarifa tulizonazo ni kuwa watu wengi sana wameuawa Goma na kupelekea kuenea kwa magonjwa ya mlipuko eneo hilo hasa kwa vile maiti zimetapakaa mitaani na mvua kubwa bado inaendelea kunyesha. Hivyo ili kuweka hali ya usalama na kuhakikisha uchaguzi huu hauingiliwi na Ktanga, kazi yetu ikawa ni ‘kumnyamazisha’!
Wenzetu wa DRC hawakutaka kuhusika kwa namna yoyote na huyo Bwana Katanga. Hivyo wakaomba msaada, ikiwa kama sehemu ya kutafuta amani ya DRC. Adui wa rafiki yako ni adui yako na adui wa adui yako ni rafiki yako. Tunaunga mkono serikali halali, ndiyo maana tumepeleka nguvu yetu kule kukabiliana na waasi. Hivyo hii nayo ni sehemu ya kukabiliana na waasi.
Lakini tukiachana na ombi la serikali, mtakumbuka kuwa kwenye mafaili yetu tuna faili lililo wazi dhidi ya mtu huyu. Yaani Joseph Katanga. Mnakumbuka ile kashfa ‘Mapandikizi’ ambayo yeyé alikuwa mhusika mkuu! Hivyo ili kufunga faili lile hatakiwi kuendelea kuishi!
Sasa ni kwamba, makomandoo wanne wamefika salama na tayari wako kwa ajili ya kazi. Ila komandoo wetu mmoja inawezekana akawa amekamatwa na waasi wa Goma. Hii ina maana kazi imeongezeka na kuwa kubwa kuliko ilivyotarajiwa. Kazi imekuwa kubwa kwa namna hii; Moja tunatakiwa tuendelee na operesheni yetu ya awali, yaani ‘kumfuta’ Katanga. Pili, inabidi kufanya utaratibu wa kumwokoa komandoo wetu ambaye inaaminika yuko kwenye mikono ya waasi hao ambao wanaongozwa na Joseph Katanga hapohapo Goma. Tatu, ni kufanya uchunguzi wa ndani kujua ilikuwaje parachuti likawa limetoboka kabla ya kutumiwa.
Kwa mujibu wa Kapteni Ambrose ambaye ndiye aliyeongoza ndege na kuwadondosha wale makomandoo kwenye anga ya Goma, komandoo aliyetoweka alilalamika kuhusu parachuti lake kuwa na ubovu, hata kabla hajatoka kwenye ndege. Ina maana kulikuwa na parachuti bovu, jambo ambalo si la kawaida, hasa ukizingatia namna utaratibu wetu wa manunuzi ya vifaa vya jeshi ulivyo madhubuti na umakini mkubwa. Haliwezi kuwa kosa tu, siamini kuwa ni bahati mbaya. Hivyo nataka kujua undani wa jambo hili kwani inaonyesha kuwa mpango wa kukamatwa kwa komandoo wetu ulipangwa tokea hapa. Hiyo itamaanisha kuwa kuna ‘pandikizi’ mwingine wa Katanga, na hii inathibitisha ni jinsi gani mtu huyu alivyo wa hatari sana.”
Meja Jenerali Obed Mahenda alipofika hapo alishusha pumzi ndefu kuashiria kuwa alikuwa amehitimisha maelezo yake ya awali. Hapo ukafuata mjadala mkali sana toka kwa wajumbe wa kikao. Ilipofika saa kumi na moja na robo Meja Jenerali Obed Mahenda alipiga makofi kusitisha mjadala mkali.
“Nikiwasikiliza wajumbe wote naona kimsingi tunakubaliana kufanya haya mambo matatu,” alisema.
“Nimeona watu mmekwenda mbali zaidi namna ya kuyatekeleza. Mawazo ya awali yanaonyesha kuwa ile timu ya makomandoo walioko Goma igawanywe.
Wawili wamtafute Luteni Pablo Mahene, komandoo wetu aliyetoweka.
Wawili wamtafute Katanga.
Leo ni Ijumaa asubuhi, Tangazo kuhusu uchaguzi linatakiwa kutolewa Jumatatu. Ina maana wana saa 72 tu za kukamilisha kazi zote mbili! Au niseme tuna saa 72 tu za kufanya kazi hii. Nitawafikishia ujumbe huu ili asubuhi hii ya leo waanze operesheni zao. Tunakubaliana hapo?”
Wote waliafiki.
“Sasa kazi ya ndani, mnadhani tufanyeje ili kuchunguza suala hili? Tupate mtu wa ndani au?”
Hapo tena ukazuka mjadala mkubwa sana. Wengine wakisema mpelelezi wa ndani hatakuwa huru hasa ikitokea anawachunguza waliomzidi cheo. Wengine walisema sheria za ndani haziruhusu mambo kwenda nje!
 
kumi na moja na robo Meja Jenerali Obed Mahenda alipiga makofi kusitisha mjadala mkali.
“Nikiwasikiliza wajumbe wote naona kimsingi tunakubaliana kufanya haya mambo matatu,” alisema.
“Nimeona watu mmekwenda mbali zaidi namna ya kuyatekeleza. Mawazo ya awali yanaonyesha kuwa ile timu ya makomandoo walioko Goma igawanywe.
Wawili wamtafute Luteni Pablo Mahene, komandoo wetu aliyetoweka.
Wawili wamtafute Katanga.
Leo ni Ijumaa asubuhi, Tangazo kuhusu uchaguzi linatakiwa kutolewa Jumatatu. Ina maana wana saa 72 tu za kukamilisha kazi zote mbili! Au niseme tuna saa 72 tu za kufanya kazi hii. Nitawafikishia ujumbe huu ili asubuhi hii ya leo waanze operesheni zao. Tunakubaliana hapo?”
Wote waliafiki.
“Sasa kazi ya ndani, mnadhani tufanyeje ili kuchunguza suala hili? Tupate mtu wa ndani au?”
Hapo tena ukazuka mjadala mkubwa sana. Wengine wakisema mpelelezi wa ndani hatakuwa huru hasa ikitokea anawachunguza waliomzidi cheo. Wengine walisema sheria za ndani haziruhusu mambo kwenda nje!

* * *

Jabir Omari Makame alikuwa jikoni wakati aliposikia simu ya mezani kwake ikilia sebuleni. Si kawaida yake kuamka asubuhi sana na kwenda jikoni, ila kwa ombi la mpenzi wake aitwaye Juliana Owima ilibidi aende jikoni. Mpenzi wake huyo alikuwa mjamzito, ujauzito mkubwa tu. Hivyo alimkurupusha asubuhi na kumwomba amtengenezee mayai ya kukaanga.
Hivyo wakati simu ile inaunguruma, yeye alikuwa jikoni. Aliondoka haraka kuelekea sebuleni. Hata kabla hajaipokea alishajua kuwa simu ile ingekuwa inatokea ofisini. Ni ofisini pekee ndiyo humpigia simu ile ya mezani wanapokuwa na hakika kuwa yuko nyumbani. Lakini marafiki ndugu na jamaa hutumia zaidi simu ya mkononi.
“Jabir hapa,” alisema baada ya kuweka sikioni kiwambo cha kusikilizia.
“Bila shaka hujambo Jabir, ninakuhitaji haraka iwezekanavyo!” sauti ya mwanamke wa makamo ilisikika.
“Duuh, ofisini siyo?” Jabir Omari Makame aliuliza.
“Hapana, nitakueleza ukiwa njiani unakuja!” ilisema ile sauti ya kike.
“Tuonane hapo ndani ya dakika arobaini zijazo! Jabir Makame alisema na kuibamiza simu kwenye sahani yake.

* * *
Dakika arobaini baadaye, mpelelezi Jabir Omari Makame alikuwa kwenye gari na Mkurugenzi wa Ofisi Fukuzi, Bi. Anita.
“Kwa mujibu wa Meja Jenerali Obed Mahenda, hali siyo ya kuaminika sana huko ndani, Bi. Anita alisema. “Hivyo hakuona ni salama kama akionana na sisi. Ameridhia kuwa miye nikwambie kile ambacho nilitaka ukipate toka kwake. Nadhani umeelewa picha halisi. Swali ni fupi tu, kwa nini yule komandoo alikuwa na parachuti lililotoboka?”
Wakati huo, Bi. Anita alikuwa analizungusha gari kwenye mitaa ya Jiji la Dar es Salaam. Hawakuwa na mahali maalum pa kwenda, bali ilikuwa ni njia ya kuhakikisha kikao chao kinamalizikia kwenye gari halafu amrudishe Jabir Makame mahali alipokuwa ameacha gari lake.
Bi. Anita ni mkurugenzi wa kitengo maalum kinachojishughulisha na upelelezi na ujasusi kwa pamoja. Hutegemea tu nini kinahitajiwa kwa wakati mwafaka. Kitengo hiki ni cha siri sana na hufahamika na watu wachache sana serikalini. Ni kitengo kilichosheheni vijana makini katika fani hiyo.
“Mbona sioni kama suala hili lina uzito wa kufanya lije kwetu?” Jabir aliuliza.
“Come on Jabir, ni wewe au miye ninayeweza jua hili ni zito au jepesi kushughulikiwa na ofisi yangu?” Bi. Anita alifoka.
“Okay, suala hili ni zito sana kutokana na kuunganishwa na lile faili liitwalo “Pandikizi”. Kuwepo kwa mkongomani Jose Katanga, na ile ishu ya kupandikiza watu aliyoifanya kunafanya iwe ni kazi inayotakiwa kufanyika kwa makini na kupewa uzito mkubwa sana!” Bi. Anita alisema.
Halafu akaongeza, “Hili faili lina taarifa zote namna hayo maparachuti yalivyonunuliwa hadi kukabidhiwa kwa Kapteni Ambrose ili yatumiwe na wale makomandoo watano. Jabir, una saa zisizozidi sabini na mbili kuleta ufumbuzi wa suala hili. Mpango ni kuwa Rais wa Congo aendelee na mpango wa kutangaza siku ya uchaguzi. Fanya kila unaloweza ukweli upatikane ndani ya muda huo. Hiki hapa ni kibali maalum ambacho kinakuwezesha kufanya mambo ambayo katika hali ya kawaida usingeyafanya hasa kwa sababu ya aina ya watu unaoweza kukabiliana nao katika kazi hii!”
Akazungusha usukani kushika barabara ambayo inaelekea Upanga, sehemu ambayo walikuwa wameliacha gari la mpelelezi Jabir Omari Makame! Jabir alilichomeka lile faili kwenye koti lake!
Ilikuwa inagonga saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano asubuhi wakati Jabir alipotoka kwenye gari la Bi. Anita kwenda kwenye gari lake.

* * *

Wakati mpelelezi Jabir Makame akiwa anaingia kwenye gari lake, ni wakati huohuo hawa walikuwa kwenye maongezi kwa simu.
“Kama yeyé ndiye amepewa kazi ya kupeleleza kisa hiki basi nakupa saa ishirini na nne kuhakikisha kuwa Jabir anakuwa Kinshasa!” Sauti ya Joseph Katanga ilisema kwenye simu.

**************

ALIPOWASILI nyumbani kwake maeneo ya Makongo Juu, tayari ilikuwa saa moja na dakika tatu asubuhi. Ukweli ni kuwa, pamoja na kuelezwa na kusisitizwa na Bi. Anita, lakini bado mpelelezi Jabir hakuwa ameipa uzito mkubwa ile kazi aliyokuwa amepewa. Aliona kuwa walikuwa wanajiingiza kufanya kazi za kihisia zaidi. Alishindwa kumkatalia bosi wake. Alipofika nyumbani kwake alipitiliza chumbani ambako alimkuta mpenzi wake akiwa bado amelala.
“Vipi Jabir?” Juliana alimuuliza kama aliyekuwa akitarajia habari fulani.
Tangu amjue Jabir, sasa huu mwaka wa tatu. Japo hawajaoana, lakini wamekuwa wakiishi kama mke na mume. Alishajua kuwa simu ikipigwa kwa ile simu ya mezani basi itakuwa inatokea ofisini. Pia kwa kuzingatia muda ambao simu hiyo imepigwa, ilikuwa wazi kuwa kulikuwa na jambo la muhimu sana, ndiyo maana mpigaji alishindwa kusubiri Jabir aende kazini muda wa kawaida wa kazi.
“Safi, kuna kazi tu kidogo!” Jabir alisema.
“Hausafiri?”
“Hapana, nipo hapahapa. Ni kazi za ndani tu!” Jabir alisema huku akibwaga lile faili kwenye meza ndogo iliyokuwa pembeni mwa kitanda. Akambusu Juliana halafu akasimama akiwa anavua shati.
“Umependa mayai niliyokuandalia?” Jabir alimuuliza wakati akielekea bafuni.
“Ndiyo, asante! Julian alisema kwa sauti ya chini kiasi.
_________________

Saa 1:30, Goma DRC

Meja Kabananga, maofisa wengine wa jeshi pamoja na wale makomandoo wanne walikuwa kwenye kikao kizito. Ilikuwa kikao cha mkakati wa operesheni maalum.
“Ngome kuu ya hawa waasi iko hii sehemu ambayo wao wameibatiza jina Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga,” Meja Kabananga aliwaambia wanakikao wenzake. “Iko eneo la mpakani kati ya Congo na Rwanda. Kambi hii ilijengwa na Wabelgiji wakati wakiwa wanatawala iliyokuwa Zaire. Tumeshafanya mashambulio mara kadhaa kwa miaka mingi lakini imekuwa ngumu sana kuwamaliza kabisa waasi hawa maana wengi wao hukimbilia Rwanda pale wanapoona mashambulizi yamekuwa magumu.
“Hivyo basi, njia pekee iliyobaki kuwamaliza waasi hawa ni kuua viongozi wao wote waandamizi. Hilo nalo limekuwa gumu sana maana imekuwa ngumu sana kuwapata wote na wamekuwa wakitumia majina na sura za bandia. Ila vyanzo vyetu vya habari vinasema Jose Katanga kaitisha kikao cha siri ambapo makundi mbalimbali ya waasi wa Congo yanatarajiwa kukutana eneo hilo liitwalo Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga. Viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria ni hawa hapa.”
Akaweka picha zipatazo kumi na moja kwenye meza ya duara ambayo wajumbe wa kikao hicho walikuwa wamekaa kuizunguka. Wajumbe walianza kuziangalia zile picha. Mwishoni zilibaki kwenye mikono ya wale makomandoo wanne.
“Hapa ndiyo Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga,” Meja Kabananga alisema huku akiwa amesimama na kuonyesha ramani ya eneo hilo lililo Mashariki mwa Kivu kaskazini. “Inadhaniwa kuwa eneo hili kuna handaki kubwa sana limejengwa hapa kwenye hili jengo linaloitwa THE ROCK. Ni ndani ya jengo hili liitwalo The Rock ndipo inadhaniwa kuwa Joseph Katanga hupenda kukaa. Wengi wamejaribu kwenda hapa lakini imeshindikana. Na sababu kuu ya kushindikana ni jinsi ambavyo kimahesabu inakuwa ngumu sana. Unaona hivi vilima sita ambavyo viko pembezoni mwa kambi hii. Kutoka kwenye kila kilima kwenda ilipo The Rock ni mita 500. Juu ya kila kilima inaaminika kuwa kuna wadunguaji wasiopunguwa watatu ambao wana kazi kuu tatu. Mdunguaji mmoja wa kila kilima muda huwa ana kazi ya kumwangalia Joseph Katanga. Hivyo ikitokea jambo lolote la kuhatarisha maisha yake, risasi ya mdunguaji huyo huchukua maisha ya chochote ambacho kinahatarisha maisha ya bwana wao huyo wa vita. Nadhani mnaelewa naposema wadunguaji, yaani, snipers! Bunduki zao za kisasa zenye darubini za kisasa zinauwezo mkubwa wa kuona mbali na kushukua shabaha ya mbali. Hii ina maana wadunguaji sita wako macho muda kumwangalia Katanga.
Mdunguaji wa pili aliyeko kwenye kila kilima, hii inamaana wadunguaji sita, wao kazi yao ni kufuatilia milango mitatu ya kuingilia kambi hiyo na kufuatilia wageni wote. Hivyo unapokuwa mgeni jua kuwa kuna mdunguaji anakufuatilia kwa mbali.
Mdunguaji wa tatu aliyeko kwenye kila kilima huwa hana kazi maalum. Hivyo yeyé huwa tayari kwa dharula yoyote itakayojitokeza. Lengo ni kuona kuwa wale wadunguaji wawili wa awali hawaachi kufanya kazi zao muhimu.
Katanga siyo mtu wa ratiba maalum, inadhaniwa kuwa ana marafiki wachache sana anaowaamini. Marafiki hao hawajulikani hadi sasa. Katanga ni mtu aliyekamilika katika kutumia silaha yoyote. Ana uwezo wa juu katika kutumia mwili wake kujikinga na kushambulia. Anaogopwa na kupendwa sana na watu wake hasa jamii ya wakulima ya kabila la Lendu. Inadhaniwa kuwa wazee walioko vijiji vya jirani hupewa zawadi na vitu mbalimbali na Katanga ili wawe wanampa taarifa yoyote ambayo wanadhani ni hatari kwake.

Njia pekee ya kwenda huku ni hii hapa, lakini njia hii inalindwa kuliko kitu chochote kile. Upande huu kuna ziwa na upande huu kuna mpaka na Rwanda ambapo jeshi la nchi hiyo lina kituo chake kikubwa eneo hili…” alizidi kufafanua Meja Kabananga.
“Kamanda, tumeshafanya upembuzi wa kutosha kabla ya kuja hapa. Na njia pekee ambayo tunaweza kufanikisha misheni hii ni kwa sisi kukamatwa halafu tutajua cha kufanya tukishafika huko. Hakuna namna nyingine ya kuingia na kuwafanya kitu mbaya bila siye kuwa mateka kwanza!” alisema Kamanda Twaha Mchopa ambaye licha ya kuwa komandoo pia ni mtaalamu sana kwenye mambo ya mikakati.
“Sawa, sasa mtafanikishaje hilo maana mtu anaweza kuamua kukuua badala ya kukuteka? Tutahakikishajekuwa mnatekwa badala ya kuuawa?” ofisa mwingine wa Jeshi la Congo alihoji.
 
Kamanda, tumeshafanya upembuzi wa kutosha kabla ya kuja hapa. Na njia pekee ambayo tunaweza kufanikisha misheni hii ni kwa sisi kukamatwa halafu tutajua cha kufanya tukishafika huko. Hakuna namna nyingine ya kuingia na kuwafanya kitu mbaya bila siye kuwa mateka kwanza!” alisema Kamanda Twaha Mchopa ambaye licha ya kuwa komandoo pia ni mtaalamu sana kwenye mambo ya mikakati.
“Sawa, sasa mtafanikishaje hilo maana mtu anaweza kuamua kukuua badala ya kukuteka? Tutahakikishajekuwa mnatekwa badala ya kuuawa?” ofisa mwingine wa Jeshi la Congo alihoji.

“Hilo tuachieni sisi! Kwa sasa tunahitaji saa nne za kujiandaa. Mbili za kulala halafu mbili nyingine za kupanga mkakati na kuondoka hapa!” alisema Musa Buti huku akiwaangalia wenzie wanne
“Mtahitaji gari ili liandaliwe?” alihoji Meja Kabananga ambaye alishajua kuwa alikuwa akiongea na makomandoo hivyo kuuliza maswali madogomadogo lisingekuwa tatizo.
“Ndiyo, nimesikia wale waasi wanatumia Spartan 4 x 4, je, mnazo aina hiyo?” Musa alihoji.
“Tunazo, hata walizonazo walipora kwetu,” alijibu meja Kabananga.
“Tunaihitaji hiyo. Iwe tayari muda wowote kuanzia sasa!” Musa Buti alisema.
“Halafu chumba mlichonipa kuna shida, kuna bomba linadondosha matone ya maji, kutokana na aina ya ile sakafu yale matone yanakuwa kama yanadondokea kwenye sufuria tupu. Imenifanya nisilale vema. Huu muda wa kuikusanya akili na utayari wa kifikra kwa kazi ngumu iliyoko mbele yetu nitahitaji suala hilo lishughulikiwe. Sitaki ule mlio!” Mark Muga mmoja wa wale makomandoo, alisema.
“Nitatafuta mwingine maana fundi wetu wa kawaida alikutwa ameuawa usiku wa kuamkia jana,” alisema Meja Jean Francis Kabananga.
“Hapahapa kambini?” alihoji kamanda Emily Otieno, mmoja wa wale makomandoo ambaye alikuwa kimya muda mrefu. Kwa asili yeyé ni mkimya sana.
“Ndiyo, inaaminika ameuawa na mmoja wetu kwa sababu ya wivu wa mapenzi. Wajua tuna wanawake sita tu hapa kambini na tuko wanaume zaidi ya mia na hamsini. Nadhani unaweza kuelewa hali hii,” alisema Meja Jean Francis Kabananga.
“Ukata! Hahahaha!” kamanda Musa Buti alisema huku akichukua ile ramani ambayo Kabananga alikuwa akiitumia kuwaelekeza juu ya Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga, akimkabidhi Mark Muga.

* * *

Saa mbili za kwanza za mapumziko, wote walikuwa kwenye vyumba vyao vidogo sana vilivyokuwa kwenye moja ya majengo yaliyokuwa kwenye kambi hiyo, Kambi hiyo ilizungukwa na msitu mnene. Vyumba hivyo vilikuwa na giza sana, halafu kwa sababu za kiusalama hakukuwa na milango kwenda vyumbani. Hapakutofautiana na pango. Kuta nene sana, imara, vitanda vya mbao tu hakuna godoro, taa hafifu sana kiasi ulihitaji kuwa nauono mzuri kuweza kumwona mtu, vilikuwa maalum kwa ajili ya mapumziko. Kulikuwa na choo ndani ya kila chumba na bomba la maji pembeni yake. Ni bomba hilo ambalo walikuwa wamelilalamikia!
Tayari zilipita dakika ishirini tangu pale walipopeana saa mbili za kupumzika na kukusanya akili zao pamoja. Inaaminika kuwa makomandoo kabla hawajaanza operesheni ngumu huhitaji muda kama huo kwa ajili ya zile sala zao na kuweka akili na hisia katika kiwango kinachotakiwa. Kwa hivyo hutumia muda huo kwa ajili ya kutafakari.
‘Ta’
‘Taa’
‘Taaa’
‘Taaaa’
“Mxccchyuuuuuu’ Emily Otieno alisonya kutokana na kero iliyoletwa na mlio huo wa matone ya maji yaliyokuwa yakidondoka sakafuni. Alisimama akaenda kujaribu kulifunga tena lile bomba, lakini hakufanikiwa. Akaamua kuukaribisha ule mlio kwenye ubongo wake na kuupa nafasi kisha afanye alichotaka. Akafanikiwa. Mlio uliendelea kuwepo lakini hakuuona kama kero tena kwa vile alishaukubali na kuupa nafasi kwenye mfumo wake wa kufikiri.
Saa moja ilipopita wote walikuwa wamezama kabisa kwenye fikira zao huku wakijaribu kutembea kifikira. Wakifikiria kila aina ya hatari ambayo wanaweza kukutana nayo, wakati huohuo walitumia fikira zao kujikumbusha uwezo wao na jinsi walivyo wa kipekee. Kila mmoja alijiambia kuwa ilikuwa kazi ya hatari sana waliyokuwa wakienda kuifanya. Lakini wakajikumbusha kuwa ndiyo maana walipewa mafunzo ili kufanya kazi ya hatari iwe sehemu ya maisha yao.
Kila mmoja alikuwa kwenye chumba chake. Vyumba vyao havikuwa karibu kwa sababu maalum pia. Komandoo Muga alikuwa kitandani amelala chali huku macho yamefumbwa. Komandoo Otieno alikuwa amelalia ubavu wa kulia huku uso unatazama ukuta. Komandoo Mchopa alikuwa ametumbua macho, akiliangalia lile bomba lililokuwa likidondosha maji. Japo macho yalikuwa wazi, yamemtoka, lakini hayakuwa timamu kwani akili ilikuwa kwingine.
‘Ta’
‘Taa’
‘Taaati’
‘Taaaatii’
Ni Twaha Mchopa peke yake aliyeweza kuhisi utofauti kwenye mlio huo wa matone. Ile ‘ti’ ya mwisho ilimrejeshea umakini kuelekea kwenye lile bomba. Macho yakarejeshewa mawasiliano. Japo hakujitingisha lakini ilimshangaza, kama kila kitu kiko kama ilivyokuwa awali kwa nini mlio umebadilika japo ilikuwa mabadiliko madogo sana.
Ilipopiga ‘taaaati’ nyingine ndipo macho yake yalipobaini kuwa ile ‘ti’ ilikuja na mwonekano wa buti ya jeshi iliyokuwa imejitokesa kwenye ukuta mmoja wa mlango kwa nje! Aliangalia eneo lile, alikuwa na hakika kuna mtu alikuwa amenyata hadi kufika pale. Na sasa akajua nini kilikuwa kinafuata, yule mtu alikuwa anasubiri tone jingine ili sasa apige hatua nyingine na kusababisha ‘ti’ nyingine ambayo ingemfikisha mtu huyo katikati ya ule mlango.
Komandoo Twaha Mchopa hakufanya purukushani, alichomoa kisu toka kwenye buti yake. Kitendo hicho alikifanya kwa namna ambayo hata angekuwa mgongoni kwako usingesikia. Sasa akawa anasubiri tone lije.
Ghafla akaona mguu uko hewani unasogezwa katikati ya mlango. Hii ikamjulisha kuwa mtu aliyekuwa hapo alikuwa ameshasoma muda uliotumika kati ya tone moja hadi jingine. Hivyo alinyanyua mguu akiwa anasubiri ashushe pamoja na tone la maji! Kitendo hiki kilimshangaza sana Twaha Mchopa. Hakuwa amefikiri kuwa maji yale yalikuwa yamefanywa vile kwa kusudi ili mtu akinyata asisikiwe. Akawa tayari anasubiri na kisu chake.

Wale mliokuwa mmeweka oda vitabu tayari

Arusha vitabu vinapatikana tayari 0757690302

Morogoro vinapatikana tayari jioni hii 0621075891

Dodoma kesho asubuhi viko kwa huyu hapa ‭0715368220‬

Mbeya kesho asubuhiiiiiii nitakuwekeannamba ya mwenye navyo

Dar kesho asubuhi posta vitakuwa kwa huyu ‭0755454152‬

Kuweka oda ya kitabu hiki tuma neno ODA SAA 72 kuja namba 0762204166
 
Hii ni hadithi moja ile ya kwanza au hii nyingine?kwanini usianzishe Uzi mwingine kuliko kutuchanganya mkuu Kudo?
 
S A A 72 ndani ya GOMA-CONGO DRC

Hadi alipofika kwenye ule mzunguko maarufu sana mjini Goma, yaani, roundabout, mzunguko wenye sanamu ya mtu akiwa anaendesha baiskeli. Wenyewe wanauita Chikudu Tshukudu. Komandoo Mchoppa aliiangalia ile sanamu wakati akiwa anauzunguka huo mzunguko. Alipoumaliza akaingia kulia kwake na sasa akawa kama anatoka nje ya mji. Aliendesha lile gari kwa mwendo wa wastani hadi alipotoka nje kidogo ya mji. Sasa akawa ameingia kwenye mitaa ya vigogo kwenye eneo maarufu lijulikanalo kama Kanyamuhanga, sehemu inayodhaniwa kuwa na usalama kiasi kulinganisha na maeneo mengine ya Goma ambayo yako ovyo kiusalama. Eneo hili la Kanyamuhanga ndilo ambalo kuna mahoteli ya maana na ofisi za huduma kubwa kubwa muhimu kama mabenki na mawasiliano. Alipofika eneo hilo akaendesha hadi alipoona kibao kilichoandikwa Boulevard Kanyamuhanga et Avenue Butembo. Hapo akaanza kuangalia nyumba kubwa kubwa za kifahari zilizokuwa kwenye mtaa huu wa Butembo. Mtaa ulikuwa kimya kabisa huku nyumba nyingi zikionekana kuwa na vifaa vya kisasa vya usalama. Aliendesha taratibu hadi pale macho yake yalipoona kibao cha nyumba P-1 Butembo 309. Aliangalia kwa makini sana wakati akiipita nyumba hiyo. Aliweza kukiona kibao kilichochoka cha kampuni ya ulinzi kilichoandikwa Eagle Eye Security Company. Halafu katikati ya lango kuu la kuingilia kwenye ua wa nyumba hiyo kulikuwa na plastik imebandikwa yenye maneno HOUSEFORRENT–CALL0980x980. Twaha Mchoppa alimeza mate, akaliendesha Spartan 4x4 kwa mwendo ule ule. Hadi alipopita kabisa mtaa huo. Alikwenda hadi alipofika mtaa wa mbele ambapo kulikuwa na uwanja wa michezo, hapo akaona magari kadhaa ya kifahari yakiwa yameegesha. Bila kusita na yeyé akaegesha gari lake na kutoka. Hatua ndefu, imara za haraka alitembea kuelekea alikoiacha ile nyumba.

Ilikuwa inagonga saa saba kasoro dakika kumi mchana wakati komandoo Twaha Mchoppa anawasili kwenye nyumba P-1 Butembo 309. Kati ya nyumba hii na nyumba ya jirani yake kulikuwa na uchochoro mdogo ambao ulifanya kijinjia ambacho mtu angeweza kutokea mtaa wa pili. Ilionekana kuwa ni njia ambayo inatumika. Hivyo alichukua kijinjia hicho. Wakati huo huo aliweza kusikia muungurumo wa radi na mawingu mazito yalionekana kujikusanya. Hii ilimwambia kuwa muda mfupi ujao angetakiwa kuendelea na kazi yake kwenye mvua. Goma ni mji wa mvua nyingi, hilo analijua na akili yake ilishakubali hilo. Wakati akitembea kwa chati sana alikuwa akiziangalia camera za CCTV jinsi zilivyokuwa zimekaa. Alikuwa amevaa magwanda ya kaki, halafu kwa juu alikuwa amevaa koti moja lefu la kitambaa lililomfunika tokea juu hadi kwenye ugoko. Koti hili lilisaidia kuficha magwanda yake ambayo hata hivyo hayakuonyesha yeyé alikuwa wa upande upi. Kilichosaidia tu ni kutoonekana kwa zana zake za kazi ambazo alikuwa amezipaki kwenye magwanda. Japo koti lenyewe lilikuwa refu lakini vifungo vyake vilifunga hadi usawa wa mkanda wa kiuno, hivyo kuendelea chini lilikuwa likipepea tu kama mkia wa farasi. Alipofika sehemu ambayo mahesabu yake yalimwambia kuwa camera ya upande huu na upande ule zisingempata aliruka kama nyani na kuparamia ukuta. Gloves ama kwa kiswahili tungesema mifuko ya mikono aliyokuwa amevaa ilimsaidia kuweza kunata vizuri kwenye ule ukuta mrefu aliokuwa ameupanda na kudumbukia kwa ndani ya ukuta. Huku akiwa anacheza na camera za CCTV alifanya mindoko yake kwa namna ambayo asingedakwa na camera zile zilizokuwa zimefichwa vema. Kwa mtu wa kawaida asingeweza kujua kuwa kulikuwa na camera za CCTV, zilikuwa zimewekwa kwa uficho kwenye dari la upande wa nje kuzunguka nyumba. Zilionekana kama taa ndogo za mapambo zilizokuwa ndogo kama vifungo vya koti na zenye mwonekano kama macho ya panzi.

Wakati anapiga hatua ya nne toka ukutani, aliangalia vema hatua zake. Akarudisha hatua yake nyuma.
“Was***e hawa! Mchoppa alitukana kwa kuwahusudu waliokuwa wameweka ulinzi kwenye hiyo nyumba. Bila shaka yeyote aliyekuwa ameweka ulinzi alishajua kuwa eneo hilo lisingekuwa chini ya CCTV camera, hivyo kwa chini kwenye majani, majani yakawa yamekatwa kwa mtindo wa umbo la madini ya almasi, yaani diamond style, na macho pekuzi ya Mchoppa yakawa yameona pini moja iliyokuwa imejificha kwenye majani hayo yaliyokatwa vema. Ilikuwa pini ya kulipulia bomu, ina maana hatua ya tatu ingempeleka mtembeaji, ambaye angekuwa anakwepa CCTV camera akanyage ile pini. Ndiyo maana Mchoppa akarejesha mguu wake wakati anataka kumalizia hatua ya tatu.
Mchoppa akatabasamu, huku moyo wake unapiga kwa kasi.
Aliyeweka anajua hesabu, alishapima hatua ya tatu itakuwa hapa. Alishajua wapiganaji wengi ni warefu na hupenda kupiga hatua ndefu wanaponyata. Mchoppa aliwaza na kumsifia mtu aliyeweka ulinzi.
Unapokutana na fundi namna hii inatakiwa kufanya kinyume na matarajio. Mchoppa akajikumbusha. Hivyo akapiga nusu hatu, ikawa hatua yake ya tatu, halafu robo tatu hatua ikawa ahtua yake ya nne. Alipoufikia ukuta akataka kusimama jirani na ukuta akasita. Fanya kinyume na matarajio. Hivyo nusu hatua toka ukutani, akasimama pale pale. Kaaangalia namna ambavyo anaweza kuingia ndani. Mara akaona kwa juu yake kulikuwa na dirisha. Dirisha la kioo. Kwa haraka akajua kuwa yeyote ambaye alikuwa amefanya ufundi wa kutega vitu eneo lile angekuwa ameona ule mwanya. Hivyo akafuta huo uwezekano. Kwa juu kabisa ya ukuta kulikuwa na ile sehemu ambayo wajenzi huweka kwa ajili ya kuingizia hewa. Huwa ndogo kwa ukubwa wa msaafu mkubwa! Hapo akili yake ikaamua kufanya kitu ambacho alikuwa na hakika kuwa yeyote aliyeweka ulinzi asingefikiria. Aliingiza mkono kwenye moja ya mifuko ya gwanda lake. Hapo akatoa kitu kama zile kamba maalum za kufanyia mazoezi ya kuruka. Alikielekeza kwenye dari la kwenye paa juu kabisa, akabonyeza kitufe fulani. Kitu kama waya chenye kitu kama mshale kwa mbele kikafyatuka na kwenda juu na kujichomeka kwenye mbao ya darini kwa upande wa nje. Mchoppa akafanya kama anajivuta hivi ule waya ukaanza kumvutia juu. Hivyo akawa amekwea hadi juu kabisa. Alipofika kwenye ile sehemu ya kuingizia hewa ndani akapabomoa na kuondoa tofali moja zaidi. Alikuwa na vifaa vya kutosha kufanya kazi hiyo bila kelele. Hapo akawa ametumbukia ndani. Alipoangala kwenye dirisha alilosita kulitumia aliona waya maalum ukiwa umetandazwa kwenye lile dirisha ambao ulikwenda hadi kwenye bomu lililokuwa pembeni ya chumba kile.
“Damn it! Alisema kwa kujigamba.
Hakukuwa na kitu kingine chochote chumbani mule. Alianza kuzungukia chumba kimoja baada ya kingine. Nyumba ilikuwa kubwa yenye vyumba vingi. Wakati akitembea kwenye kijinjia kimojawapo alisikia kama mashine ya faksi iko inafanya kazi. Hapo alinyata kwenda kwenye hicho chumba. Aliweka kifaa chake maalum kwenye mlango halafu akasikiliza. Akajihakikishia kuwa hakukuwa na mtu. Hivyo akafanya maarifa kuufungua mlango wa kile chumba ambao ulikuwa umefungwa. Baada ya dakika kadhaa alifanikiwa kuufungua mlango ule ambao kufungua kwake na kufunga kwake kulihitaji namba maalum.

Alipoingia tu ndani akakalibishwa na mashine iliyosema
“Welcome please provide your passcode within two minutes” (Karibu, tafadhali unatakiwa kutoa nywila ndani ya dakika mbili).
Duuuh, hapo sasa!
Mchoppa akachachawa, akajua ilimaanisha nini kama angeshindwa kutoa nywila kama alivyotakiwa. Akili yake ikazunguka haraka haraka huku kijasho chembamba kikimtoka kwenye paji lake la uso. Hakutegemea angekutana na hali kama hii.
“Was**ge hawa! Mchoppa alitukana kwa sauti ya kunong’ona. Dakika ya kwanza ikakatika. Wakati anafikiria cha kufanya mashine ikamkumbusha.
“You have only one minute to provide your passcode before it is too late!(Una dakika moja tu imebaki ya kutoa Nywila kabla hujachelewa)
“Shiiit! Mchoppa alisema sasa akiwa anahisi hewa inaanza kwisha kwenye kile chumba. Nguvu zikaanza kumwishia.

kitabu hiki kinapatikana kwenye mikoa yote nchini kwa sh7,000 tu. Hebu angalia mkoa wako ili ununue nakala yako kabla havijakwisha

MOSHI MJINI vitabu vimefika
‭065 424 1700‬

TABORA - 0719694989

MERERANI (mgodini) -‭ 0763646465‬

KAHAMA - ‭0655618385‬

SIMIYU - BARIADI

SONGEA - 0684302723

SUMBAWANGA - 0719551771

TUNDUMA - 0764123845

TARIME - ‭0759142940‬

NZEGA - 0788080401

NYAMONGO (mgodini) - 0753255516

KIGOMA MJINI - ‭‬ ‭0715 218 237‬

KASULU - 0759635615

SHINYANGA MJINI vitabu vimefika
‭0766048469‬

GEITA - 0712735331

MBEYA 0756772070 NA 0765819181, WANAPATIKANA MBEYA RETCO KITUO CHA DALADALA

DAR
Posta kuu 0755454152‬
Kinondoni
‭0766000663‬

MWANZA vimefika jioni hii pale VICTORIA BOOKSHOP
0768937634

DODOMA kitabu kimefika
‭0715 368 220‬

IRINGA MJINI Kitabu kimefika
0763500396

MOROGORO
Mjini sasa kinapatikana 0621075891
 
Mkuu kudo900 ulituambia season two ungeirusha jumatano , leo hii ni jumapili mkuu tufanyie wepesi
 
Mkuu kudo900 ulituambia season two ungeirusha jumatano , leo hii ni jumapili mkuu tufanyie wepesi

Majukumu yalibana naomba tukutane hapa jumamosi mapema kabisa lakini pia wale wasiopenda kungoja tuwasiliane kupitia namba zilizoko hapo juu uupate mzigo wote hadi mwisho yani mwisho kabisa

Karibuni
 
Majukumu yalibana naomba tukutane hapa jumamosi mapema kabisa lakini pia wale wasiopenda kungoja tuwasiliane kupitia namba zilizoko hapo juu uupate mzigo wote hadi mwisho yani mwisho kabisa

Karibuni
Mkuu Kudo900 ulituahidi jumamosi leo hii jumapili, tukumbuke kwenye huu ufalme wako wa ikisikika tyuuuuu.......
 
Riwaya.Sauti Ya mtutu
Season two

RIO DE JENEIRO
Ndege tuliokuwamo mimi na kisuti ilikuwa ikibalizi juu ya anga la mji ule mkubwa ndani ya nchi brazil.
Lengo la rubani halikuwa kutua juu ya uwanja wowote wa kiserikali na sijui kwa nini haikuwa hivyo.
***
• Baada ya kukaa kwa muda kidogo juu ya anga la nchi ile hatimae ile rubani wa ndege tuliokuwamo akaishusha taratibu kwenye uwanja wa vumbi uliokuwa umejengwa nje kidogo ya jiji lile la Rio de jeneiro.
Baada ya kutua rubani alituomba tushuke kwenye ndege ile.
Tuliposhuka nikapata kushuhudia uwanja ule ulikuwa ndani ya majengo yalioonesha kama ni hospital kubwa iliokuwa eneo lile na katika kiwanja kile kidogo hapakuwa na ndege nyingine ,zaidi tuliona tu majengo mengi yakiwa yamekizunguka kiwanja kile na kwa mbali tuliona watu wakiwa wamevalia mavazi kama matabibu wakizurura huku na huko.
Kisuti alinipa ishara ya kuelekea kuliko jengo moja liliokuwa umbali wa kama nusu kilomita hivi kutoka pale uwanjani.
Nilikuwa nipo nyuma ya kisuti aliekuwa akitembea eneo lile bila wasiwasi wowote na bila Shaka alikuwa mzoefu wa eneo lile.
Tulifika hadi mlangoni mwa jengo lile na hapo nikamwona kisuti akijipapasa mifuko yake na kutoka na kikadi kidogo mfano wa zile kadi za bank na alipokwisha kuitoa akaielekeza karibu na kitasa cha mlango ule na eneo zima lilikuwa kimya kabisa na hapakuwa na pilikapilika za watu Kama nilivyoona kwenye majengo mengine.
Mlango ulifunguka na bila kusema kitu kisuti akaanza kuingia ndani nami nikafuata nyuma .
Tofauti na nilivyotegemea baada tu ya kuingia ndani ya jengo lile tukakuta pembeni ya mlango ule kuna askari wakiwa na bunduki zao fupi aina ya SR.
Askari mmoja akaja kwa kasi na kumfikia kisuti kisha kwa haraka bila kuongea akatoa kifaa kidogo mfano wa saa ya mkononi na kuanza kupitisha juu ya mwili wa kisuti.
Askari yule alipokwisha kumkagua akamruhusu apite kisha akanifuata na mimi na kufanya vile alivyomfanyia kisuti kisha akaniruhusu nipite.
Tuliingia ndani ya kabisa ya jengo lile lakini ajabu jengo halikuwa na chumba hata kimoja yaani lilikuwa na uwazi mkubwa na mle ndani hapakuwa na chochote kitu.
Macho yangu yakawa na kazi ya kukagua kila pahali lakini sikuambulia kitu zaidi ya macho yangu kugota ukutani tu.
Kisuti kila mara alikuwa akiiangalia saa yake alilokuwa kaivaa mkononi na hakuwa na habari kabisa na mimi Kama vile hakuwa anajua nipo nyuma yake.
Baada ya kama dakika nne za kukaa pale, mara nikaanza kuhisi Kama tetemeko hivi likitokea chini ya ardhi,na kila nilivyozidi kumakinika na mtetemo ule nao ukazidi kuongezeka mara dufu na punde ukakoma hapo nikahamishia macho yangu kwa kisuti nae alikuwa akimtizama huku akitabasamu.
Hatua kama nne kutoka tulipokuwa tumesimama,nikasikia sauti ya kama mlango kufunguka kutokea chini na nilipotizama nikaona kuna pahali panajiachia na kuwa na uwazi wa kama mlango wa kisima.
Kwenye uwazi ule nikaona anatokea mtu akiwa na vikofia kama vya madaktari wawapo kwenye chumba cha upasuaji.
Alipotoka mtu yule alikuwa nae kashika bunduki mkononi na kibegi mgongoni hakutusemesha zaidi alivua kile kibegi na kutoa koti mbili za kitabibu na kutupatia tuzivae na kisha akatupa vikofia na masks za kuziba pua na mdomo.
Tulipokwisha kuzivaa akatuonesha ishara tumfute kuelekea kule alikotokea.
Nilikuwa wa mwisho kuelekea kufika kwenye himaya iliokuwa chini ya ardhi.
Kulikuwa na watu wengi wakiwa bize na shughuli zao huku wote wakiwa na mavazi kama tuliokuwa tumevaa na kulikuwa na baadhi ya Walinzi waliokuwa bize kuhakikisha usalama ndani ya eneo lile.
Tuliendelea kusonga huku tukiviacha vyumba kadhaa vilivyokuwa vimejengwa kwa vioo hivyo kunifanya niweze kuwaona watu walivyokuwa bize kufanya kazi zinazowahusu.
Nilipata kushuhudia baadhi ya watu wakipaki maboksi makubwa kwa madogo ambayo sikujua yamebeba kitu gani.
Tulifika pahali ambapo peke yake ndo palijengwa kwa zege na milango yake ikiwa ya vioo vyeusi na yule mtu aliekuwa akituongoza akasimama na kuichia bunduki yake kisha akapeleka kiganja cha mkono wake ukutani na alipotoa nikaona mlango ule ukifunguka wenyewe na kutufanya tupite na kuzama ndani zaidi.
Tofauti ya huku ni kuwa kukionekana kama ni maabara hivi na vyumba vyake vilikuwa vimetengenezwa kwa vioo vyeupe hivyo kutufanya tuone yaliomo.
Kulikuwa na majokofu makubwa yaliokuwa yanabarafu huku kukiwa kama na watu au maiti za watu na baadhi ya majokofu yalikuwa na viumbe kama nyoka na panya wengi sana sikujua lengo la maabara ile.
Tulizidi kusonga mbele na hapo nikakadiria tutakuwa tumetembea zaidi ya dakika kumi tangu tuingie kwenye himaya ile na bado tulikuwa hatujafika tuendako na kila tulipopita tuliacha askar kadhaa wakiwa wamesimama na hakutusemesha.
******
Tuliingia kwenye chumba kimoja kilichokuwa kimezungukwa na mashine nyingi za kitabibu hasa hadubini kubwakubwa na baadhi ya chupa kadhaa zilizokuwa na kemikali ambazo sikujua ni za nini.
Mle ndani kulikuwa na walinzi kama kumi na tano hivi wakiwa wamevizunguka vifaa vile vilivyokuwa vikihudumiwa na watu watatu tu waliokuwa bize na kazi yao.
Askari yule alietupeleka akatuonesha pahali pa kusimama kisha akatuacha na kuingia kwene chumba kingine kilichokuwa kipo ndani ya maabara ile na punde akarudi na kutuita nasi tukaingia ndani yake.
Kilikuwa chumba kipana kilichokuwa na samani za kisasa kabisa na kulikuwa na meza kubwa ya kioo huku nyuma ya ile meza kukiwa na mtu mnene mfupi aliekuwa kafuga nywele zake ndefu na kuzitia brichi huku shingo yake ikiwa imezungushiwa skafu nyeupe na hapo nikajua tupo kwa washirika wa akina Kisuti.
Mtu yule baada ya kutuona akasimama na kwa furaha akampa mkono kisuti kisha wakaongea lugha ambayo sikuielewa na kisha wakacheka kwa sauti kubwa kuonesha furaha yao baada ya kukutana.
Walipokwisha kusalimiana bwana yule akanigeukia na kunisabahi kwa lugha ya kiingereza kibovu chenye lafudhi ya kibrazili na baada ya kumisalimiana akatukaribisha kwenye viti vilivyokuwa ndani ya ile ofisi yake.
Tulikaa huku mimi nikiwa kimya kabisa na kuwaacha wao wazungumze yanayowahusu.
****
Ilikuwa imepita kama masaa mawili hivi tangu kisuti na bwana yule waondoke pale ofisini na kuniacha nikiwa nimekaa pasipo kujua ni nini kinafuata na ni wapi nitaanzia mpango ule wa mauaji na kuiba huo mkoba ambao sikujua una nini ndani yake.
Lakini hilo kwangu halikuwa shida shida yangu ilikuwa ni kukamilisha mission na kuondoka kisha kumpa uhuru wa mzee Niyonzima na kamanda malebo.
Niliendelea kutizama mandhari za mle ndani huku nikiwashuhudia wale madaktari wakiwa bize na kazi zao na hata nilipowatizama askari wanaolinda pale ndani nao walikuwa makini na kila hatua ya wale madaktari na hapo nikashindwa kuelewa kwa nini mambo yale yapo vile ila ya ngoswe mwachie ngoswe.
Yule mbrazili alirudi mle ofisini akiwa peke yake na kisuti sikujua aliko.
“Defarando is ma name” alijitambulisha hivyo huku akikaa kwenye kiti chake na kuanza kukaguakagua karatasi kadhaa zilizokuwepo juu ya ile meza yake.
Alipopata kile alichokuwa akikitafuta kwenye karatasi zake akasimama kisha akanambia nimfuate nami nikachukua kibegi changu na kutoka nyuma yake huku muda wote huo nikiwa sijamwona kisuti.
Tuliingia kwenye lift iliotupeleka juu ya handaki lile na punde tujakuta tukitokea kwenye chumba kizuri sana na hapo nikapata kuona mandhari ya nje kwa kutumia Vioo vya madirisha ya kile kichumba tulimofikia japo niliona nje lakini kulikuwa bado ni usiku ni taa tu zilikuwa zikimulika nje.
Alibonyeza kitufe chekundu ukutani na punde mlango wa kile chumba ukafunguka na tukatoka nje ya kabisa ya jengo lile huko akaniongoza had kwenye nyumba nyingine iliokuwa na gorofa moja na kisha tukaingia ndani.
Tifauti na nilivyotegemea humo kulikuwa na starehe za watu yaani watu walikuwa wanakula na kunywa huku mziki ukiwa unapiga na baadhi ya wanaume walikuwa wamezungukwa na wasichana warembo kifupi ulikuwa ni ukumbi wa starehe za kila aina lakini hata hapa ukumbini kulikuwa kumejaa askari waliokuwa wamevalia nguo nyeusi na silaha mkononi huku wakiwa makini na ulinzi kuzunguka mle ukumbini.
Defarando alinigeukia na kunitizama kisha akanambia ni wakati wa kubadilisha mavazi yaani ilitakiwa nivue ile nguo nilokuwa nimevaa kutoka kule maabara na akanielekeza nielekee upande wa kushoto wa ukumbi ule huku yeye akikakaa kwenye moja ya viti vilivyokuwa mle ukumbini.
Nilizipita korido kadhaa zilizokuwa mle ndani na huku macho yangu yakiwa makini kukitafuta chumba namba kumi nilichoelekezwa na Defa.
Niliiingia kwenye kile chumba na kuvua zile nguo nilizokuwa nazo mwilini kisha nikaenda maliwatoni kuoga na nilipotoka nikavaa nguo nyingine na kutoka mle chumbani la sikupiga hata hatua mbili baada ya kufunga mlango nikakutana na wanaume wawili wakiwa na fimbo mkononi wamesimama mbele yangu.
Nilifanya jitihada za kuwakwepa ili nipite lakini walinizuia na hapo nikamshuhudia mmoja akinijia kwa kasi huku akiwa kanyanua fimbo yake na haraka nikainama akapita hivyo nikabaki nimesimama Kati kati ya na kibegi changu mgongoni.
Aliekuwa mbele yangu akanitupia ile fimbo ila nikawahi kuiona na kuikwepa ikapita na kwenda kumpiga yule aliekuwa nyuma yangu kisha kwa haraka nikamfuata na kumrushia ngumi ila akaikwepa kiustadi sana hapo nikajua napambana na mjuvi wa mambo hivyo ilinipasa kutulia ili nimalize zoezi.
Yule aliepigwa na fimbo akaja tena kwa kasi lakini nikafanya hesabu za akili tu aliponifikia nikajirusha juu na mguu mmoja ukagota ukutani hivyo nikamkwepa kisha Wakati natua ngumi yangu ilikuwa mbele na hivyo ikampata aliekuwa kasimama na kumpeleka chini lakini sikutaka anyanyuke haraka nikamziba teke la ubavu na haraka nikageuka ili nimkabili niliemkwepa na hapo nikaona akija mzima nikafanya kupiga msamba chini na akapita juu yangu na kwenda kujibwaga chini na haraka nikasimama na sikutaka mapamabno tena nikawapita na kukimbia kwenda kule nilikomwacha Defa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom