RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

Haukupita muda mrefu ule mlango ukafunguka na akaingia wmtu mmoja mrefu na mwembamba akiwa na bunduki ya kivita akaja kusimama karibu na mahali nilipokuwa.
Haukupita muda tena wakaingia watu wengine wawili na walipofika wakasimama kwa kufuatana huku wakiwa makini na silha zao walizoshika mikononi mwao.
Walikuwa kimya bila kusema kitu huku mlango ukiwa bado upo wazi na punde nikaona ukiwa umetangulia mguu ukiwa na kiatu cha raizoni,kisha ukafuatia mguu wa pili na kiwiliwili kizima,alikuwa ni kisuti.
Kisuti alifika hadi mahali nilipo kisha kabla hajesema lolote akacheka kwa kile kicheko chake chembamba cha kupandisha mabega juu huku vidole vyake vikiiziba pua yake ndefu.
Siku hii tena alikuwa amevaa ile suti yake ila hii ilikuwa ni suti nyeusi lakini pia haikumtosha ilikuwa fupi kuliko urefu wake.
Akanisogelea karibu zaidi kisha akawapa ishara ya kujichekesha vijana wake na bila kutarajia nikajikuta nanyanyuliwa mzegamzega na safari ya kwenda nje ikaanza
------------------------------
Nilifikishwa kwenye ukumbi mpana na uliokuwa na tv kadhaa ukutani na humo ndani nilikjutana na wanajeshi wawili wa jeshi la Burundi na miongoni mwao alikuwemo luteni E.Musaza.
Wale walionileta wakaondoka ila alibaki Kisuti tu punde wakaongezeka watu wengine sita na watatu kati yao walikuwa ni wazungu.
Waliketi kwenye viti vilivokuwa mle ukumbini na punde kisuti akajichekesha tena na hapo nikaona wanakuja watu wengine sita wakiwa na bunduki mikononi mwao na walipofika wakaenda kusimama nyuma ya wale watu waliokuwa wamekaa kwenye viti vilivyokuwa ukumbini pale.
Kisuti alinishika mkono na kuniongoza nisimame mbele yao wale watu,sikutaka kuwa mbishi maana nilijua mazingira niliokuwa niliamini kabisa hayakuwa rafiki kwangu kufanya ukorofi wowote kwa wakati huo.
Ulipita muda wa kama dakika kumi huku kila mtu akijaribu kunitathimini anavyoweza na hauna aliemsemesha mwenzie na hata kisuti alikuwa kimya kabisa nyuma yangu.
-----------------------
Alianza luteni Musaza kuzungumza.
“hatuhitaji kutumia tena nguvu kubwa ili uzungumze usioyajua,ila kubwa tunakuomba uache yote yaliokuleta hapa Bunjumbura maana yatakuweka kubaya” alisema kisha akawatazama wengine mle ukumbini kisha akaendelea.
“walikuleta hapa wapo mikononi mwetu hivyo kuendelea kuwatafuta unajiweka katika wakati mgumu sana ikizingatia wewe ni mmoja tu na sisi tupo zaidi ya mia moja hivi kila nchi hivyo hutaweza,lakini kabla hatujaendelea mbele naomba nikuoneshe kitu”
Hapo akasimama kisha akelekea uapande wa kulia wa ukumbi ule na kuwasha umeme uliotumika kuziwasha tv zile na hapo nikaona tukio gumu kuamini ila ndivyo ilivyokuwa.
Niliwaona watu wawili wakiwa katika kipindi kigumu cha mateso,walikuwa wamedhoofu miili yao na walikuwa ni wagonjwa kwa kuwatazama.
Niliwatambua watu wale alikuwa ni kamanda malebo na mzee niyonzima hii ilidhihirisha wako kwenye mikono ya watu hawa nisiojua lengo lao hadi sasa.
Luteni E.Musaza alizima tv zile na kunigeukia na pasipo kusema kitu akapiga ngeta na punde akaletwa mtu mbele yetu,mtu huyu alikuwa ni sawa na wale watu waliokuwa wahusika wakuu kwenye filamu ya Avatar,alikuwa mrefu na rangi ya ngozi yake ilikuwa imekuwa kama kijani hivi na kupauka sana,mtu yule alionekana anaumia sana hasa upande wa tumbo lake maana hata alipoachiwa hakuweza kusimama wima zaidi alijiinamia na kujishika tumbo lake huku akilia lakini pia alikuwa akitoa mate kama motto mdogo.
Luteni Musaza aliamuru mtu yule aondolewe pale lakini kuna kitu kilinijia katika akili yangu mtu huyu namfahamu haraka nikapiga hatua kumfikia bwana yule na kumtanga mbele yake nikamtazama usoni.
Lahaula!! Nilijikuta nikitamka hivyo huyu alikuwa ni waziri wa Afya mstaafu na alikuwa na urafiki wa karibu sana na bwana Malebo na kila mara alikuwa akija nyumbani na walikuwa wakizungumza kwa usiri sana na hakutaka mtu mwingine ajue wanachozungumza.
Alinitizama nay eye na akataka kusema jambo ila mdomo wake ulikuwa mzito a hakuweza kusema kitu chochote wakati huo zaidi ni udenda mwingi ulitoka mdomoni mwake.
Nilikabwa na koo kwa hasira kwa nini watu hawa wanatesa hivi watu,nikawageukia watu wale huku sas kamanda musaza alikuwa amerudi kukaa pale alipokuwa amekaa awali.
‘hiyo ni virus ya kisasa inaua kwa mateso sana ndani ya mwezi mmoja,huyo mtu ana siku nne tu za kuishi lakini pia babu yako na baba yako nao wanstahili adhabu hii na wanasiku ishiri na nane za kuishi na hatimayao ipo mikononi mwako ili wapate antdote.unapaswa kutufanyia kazi moja kubwa na tunaamini utaiweza kazi hiyo kwa sababu ulimuua kijana wetu Frankoo kwa dakika chache tu”
Nikakumbuka kitu kilichotokea miezi michache tu hapo nyuma,na swali lilibaki kumbe hawa watu wanahusian na frankoo! Ama hakika watu hawa ni hatari sana.
Yule askari mwingine aliekuwa kakaa karibu na luteni Musaza alinyanyuka na karatasi kadhaa kononi mwake na kunipa zile karatasi ili nizisome name nikafanya hivyo.
---------------------------------
Zile karatasi zilikuwa na ramani tu ilionesha mji wa Rio De Jeneiro wa nchini Brazil.nilikuwa nikizipekuwa kwa ndani zile karatasi zilizotimia sita kwa idadi yake na mabli ya ramani ile lakini pia kulikuwa na maandishi yalioandikwa kwa lugha ya kibrazil na bila tafsiri yake.
Kulikuwa na picha katikati ya karatasi zile na picha ile ilikuwa na mtu mmoja alikuwa na asili ya kibrazil na pembeni yake alikuwa amezungukwa na wadada watatu waliooneka kuwa kama walinzi wake waliokuwa wamevalia kinadhifu suti zao za rangi ya samawati.
Nikazirudisha zile karatasi kwa yule askari alienipa.
“unapaswa umuue huyo mtu kisha uchukue mkoba wake alionao mkoba huo ukishauchukua unapaswa kumpa mtu utakae elekezwa kwake ndani ya hilo jiji” ilikuwa ni sati ya kisuti ikiongea nyuma yangu alikuwa na sauti nzito tofauti na kicheko chake na kikubwa alinambia nikishamuu a huyo mtu na kupata huo mkoba ndio nitaruhusiwa kuwachukua wazee wangu na watapata tiba ya kile kirusi walichowekewa mwilini kwao.
‘mzungu mmoja alisimama na kunisogelea kisha akageuka kule waliko wenzie na kuuliza
‘’huyu ndie alimuua frankoo?” hakuna aliemjibu lakini akaoneka akutikisa kichwa chake kwa masikitiko na kisha akasema kwa sauti ya chini kabisa
“usifungue huo mkoba ukishaupata’” alipomaliza kusema hivyo akaondoka kuelekea kule alikokuwa amekaa mwanzo.
Kisuti alinishika tena mkono na kuniongoza kutoka ndani ya ukumbi ule na kuelekea nje na hapo ndipo nikapata kushudia ile kambi kubwa kama ya jeshi ilikuwa na kila kitu kinachotumiwa na jeshi,ilikuwa na ndege mbili za kivita zilizokuwa zimepaki kwenye uwazi pale kambini lakini pia kulikuwanamagari mengi ya jeshi.
Kilichonivutia ni vileulinzi ulivyokuwa pahali hapa kila kona kulikuwa nawalinzi zaidi ya kumi wakiwa wameweka skafu zao kuzungushia shingo zao.
Kisuti alikuwa akinitizama tu na bila kusema kitu akanivuta kwa nguvu ili nimfuate na mimi nikafanya hivyo.
-------------------------
Tuliingia sehemu moja iliokuwa ni kama sehemu ya kuhifadia silaha na kulikuwa na watu sita kuilinda sehemu hiyo,tuliwapita watu wale na kuingia ndani zaidi huku tukivipita vyumba kadhaa amabavyo sikujua vina kazi gani.
Safari yetu ilikomea kwenye chumba kikubwa kilichokuwa na vifaa vya mazoezi yaani gym.
Kisuti aliniacha pale na kuniachia maagizo machache tu yakuwa nikimaliza kujiweka fiti atakuja dokta kunitibu majeraha yangu na kunifanyia vipimo kadhaa mwilini kwangu kisha akaenda zake kwenye vyumba vingine vilivokuwa mle ndani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom