RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

Samahani ndugu zanguni lakini inabidi tu iwe hivi

Riwaya hii hapa chini inauzika na ipo mwanzo mwisho bila kuwa na season kwa sababu kitabu chake kinatoka tareh tano mei
Kwa garama ya Tsh 8000/=

Lakini kuna watu wanaeza wasipate Hardcopy kwa sababu ni chache hivyo yule atakaeihitaji softy copy yake tuwasiliane bei ni Tsh 4000/=
0758573660 kimesajiliwa ni marufuku kusambaza bila idhini ya mwandishi

Kionjo

Wakati huu ambapo wadunguaji walikuwa
wakijaribu kila namna ili wafanikishe kuwaona na
kuwapiga adui zao,ghafla ilisikika sauti ya helkopta
mahali hapo. Risasi kutoka helkopta mbili ambazo
zilitokea kusikojulikana zilianza kushambulia
msafara wa magari hayo.Hapo magari ya
kusafirisha pesa yakafunguliwa milango kisha
askari kadhaa waliovalia gwanda nyeusi,kofia
ngumu pamoja na fulana nzito maalum kwa kuzuia
risasi , walitoka kutoka ndani ya magari haya.Hawa
walikuwa ni askari wa weledi kutoka katika kikosi
maalum cha United States Marine Corps Forces
Special Operations Command(MARSOC ).Askari
hawa walianza kuzishambulia helkopta zile kwa
kutumia bunduki zao za kisasa kabisa aina ya HK
MP7.Lakini hawakufua dafu japo walitumia bunduki
za kisasa sana ambazo hutumiwa na Kikosi
maalum kingine maarufu sana cha makomando
kutoka katika taifa lao kijulikanacho kama Navy
Seal DEVGRU. Pengine ni kwa sababu katika
mapambano ni rahisi sana kwa aliye juu
kumuangamiza aliye chini kuliko aliye chini
kumuangamiza aliye juu. Adui waliokuwa katika
helkopta waliendelea kumwaga risasi nzito nzito
kama njugu bila kuwapa upenyo askari hawa
maalum kulenga shabaha.Vikosi vyote yaani askari
wa kitanzania na wale wa Marekani waliendelea
kupambana lakini kazi ilikuwa bado ni nzito sana.
Wakati mapambano makali yakiendelea , helkopta
nyingine ya tatu ikatokea upande wa mashariki.Hii
ilikuwa ya tofauti na hizi helkopta nyingine kiumbo
na ilikuja kwa lengo tofauti kabisa.
Helkopta hii ilikuwaimetundikwa ndoano kubwa
sana ambayo ilichomekwa minyororo minene na
imara sana minne.Minyororo hii kwa pamoja
iliunganishiwa sumaku kubwa sana iliyokuwa na
umbo la mche mraba iliyokuwa kama mita mbili za
mraba kila upande.Helkopta hii ilienda hadi juu ya
gari mojawapo kati ya yale magari yanayotumika
kusafirisha pesa, kisha ikagusisha lile sumaku juu
ya paa la bodi la gari hilo kisha ikaanza kupaa
tena.Kadri helikopta ile ilivyopaa ndivyo gari lile
lilivyoanza kunyanyuliwa polepole.Mwisho gari
lilinyanyuliwa juu zaidi na zaidi kisha kutokomea
angani.
Wakati huu ndipo adui wengine walijitokeza
kutokea porini na kuanza kushambulia.Map
ambano yakawa makali zaidi na kufanya eneo lote
kuwa kama eneo la vita kwa kelele za risasi.Askari
wa weledi wa idara ya C.T.I na wenzao wa kikosi
cha MARSOC waliendelea kupambana na adui
hawa waliokuwa wengi sana na waliopigana kwa
ari ya juu sana.Hata adui waliouawa kwa wingi
bado waliendelea kupambana kwa ari ya juu sana
kitu kilichosababisha vita kuwa ngumu zaidi na
zaidi. Kiongozi wa kikosi cha askari hawa wa
weledi wa kitanzania Kapteni Joshua na yule wa
kikosi cha Marekani cha MARSOC kamanda Lucas
Bradock waliongoza vyema vikosi vyao na
kuonesha uwezo wa hali ya juu kimapambano
.Lakini kutokana na ari na uwingi wa adui, vikosi
hivi vilianza kuzidiwa nguvu.
"We are out numbered,sergent John request for
backup". Kamanda wa kikosi cha MARSOC alitoa
maelekezo kwa askari wake kwamba afanye
mawasiliano kuomba usaidizi. "Okey Cover
me".Alijibu sajenti John akitaka kulindwa wakati
akifanya mawasiliano. Kwa kutumia kifaa maalum
cha mawasiliano alichokivaa katika sikio lake la
kushoto na kuanza kuwasiliana na makao makuu
ya muda kuomba usaidizi. Makao makuu haya ya
muda yaliweka kambi ndani. Huku makao makuu
helkopta tatu za kisasa ziendazo kasi aina ya
'Chinook' zilikuwa ziko tayari na makomando tisa
kutoka vikosi vya Navy SeAL Marekani pamoja na
makomando kutoka JWTZ Tanzania. Kikosi hiki
cha Navy Seal kilikuwepo Tanzania tangu miezi
mitatu iliyopita kwa ajili ya kufanya mazoezi ya
pamoja na vikosi vya makomando vya JWTZ ili
kuwaongezea uzoefu makomando hawa wa
Tanzania.
Kikosi hiki kilichojumuisha watanzania na
wamarekani kilikuwa tayari kutoa usaidizi tangu
walipopata taarifa za kiintelijensia kuwa msafara
ule umevamiwa.Walikuwa wanasubiri amri ya
kwenda kutoa usaidizi tu.Mara tu walipopata
mawasiliano, makomando hawa (Navy Seal na
JWTZ) walipaa na helkopta zao muda huo huo.
Uwanja wa mapambano kulikuwa na kelele za
risasi kutoka katika bunduki za wanausalama na
adui.Majibizano ya risasi yaliendelea huku idadi za
majeruhi na maiti zikiendelea kuongezeka kila
upande.Upande wa kikosi cha ' MARSOC' tayari
askari wawili walipoteza maisha na wanne
kujeruhiwa huku Tanzania ikipoteza askari wa
weledi wanne na mmoja kujeruhiwa. Upande wa
adui, walipoteza askari wengi zaidi kwa idadi
isiyojulikana. "Cease fire and take cover". Amri
nyingine ilisikika kutoka kwa kiongozi wa kikosi
cha 'MARSOC' na ambaye ndiye alikuwa mkuu wa
msafara huu kamanda Bradock.Amri hiibiliwataka
askari wote kuacha kupambana bali
wajifiche.Wakati huu ndipo kundi kubwa la adui
likajitokeza kutokea msituni na kuanza
kuyasogelea magari ya wanauslama wale kutoka
pande zote.Sura zao zilionesha kuwa ni watu walio
na asili ya somalia. Wengi kati yao walionekana
kuwa wachafu sana na wengine wadhoofu wa miili.
Lakini ni hawahawa walionekana kuvipa shida
vikosi hivi kwa muda wa saa moja na dakika
thelathini sasa.
Adui walizidi kuyasogelea magari ambayo
yaliwaficha wanausalama wale ndani yake.
Walionekana kuwa na uchu kama fisi mwenye njaa
aliyeona mzoga mahali.Sasa walizidi kusogelea
magari yale huku wakipiga kelele na kunyoosha
bunduki zao mbele.Wakiwa karibu sana na magari
yale,walisikia kelele za helkopta zaidi ya
moja.Kadri sekunde zilivyosogea ,mvumo ule wa
helkopta uliongezeka kuonesha kuwa pengine
helkopta ilikuwa inaelekea upande ule waliokuwapo
wao. Mara wakaanza kuziona helkopta zile
zikiwaelekea na wakati huo huo risasi zikaanza
kurushwa kuwaelekea adui wale . Adui walianza
kuanguka mmoja baada ya mwingine kwa kasi
kubwa.Vikosi vya uokozi vilikuwa vimefika tayari.
Bunduki aina ya FN Minimi 7.62 zilizofungwa
katika helcopter zilifanya kazi yake ipasavyo.
Makomandoo walioshuka kwa miamvuli mita
chache kabla ya kufika uwanja wa mapambano,
nao wakaanzisha mashambulizi ya ardhini na
kufanya adui kuzidiwa nguvu. Vikosi vya usalama
vilivyojificha ndani ya magari navyo vikaendeleza
mashambulizi kama mwanzo.Maadui wakaanza
kuzidiwa nguvu na kuamua kukimbilia msituni
huku wakibeba maiti za wenzao.
Hadi kufika saa kumi na mbili jioni,hakukuwa na
mapambano tena wala sauti ya risasi. Eneo
palipotokea mapambano , lilizungushiwa utepe
maalum na jeshi la polisi ili mtu yeyote asipite na
kuharibu upelelezi. Kisha askari kadhaa wakaletwa
kulilinda eneo hilo.
*********************************************
****************************************************
Mtaalamu wa teknolojia ya kompyuta ambaye pia
alikuwa mtaalamu wa kuvunjavunja ' password'
bwana Abdallah Yusoof,alifanya kila jitihada
kuhakikisha anafungua loki iliyofunga mlango wa
nyuma wa gari lile. Ni lile gari lililobebwa na
helkopta kule katika uwanja wa mapambano.
Alikwisha wahi kufungua loki nyingi sana lakini hii
ya leo ilihitaji umakini wa hali ya juu zaidi. Loki hii
ilitengenezwa kwa mfumo maalum ambapo
mfunguaji alipewa nafasi mbili za kuifungua.
Kukosea mara ya kwanza kungempa mfunguaji
nafasi ya pili.Kukosea mara ya pili kungesababisha
mlipuko kama wa bomu ambao ungeteketeza gari
pamoja na watu ambao wapo karibu na gari.
Abdallah au kama alivyozoeleka kwa ubini wake
Yusoof,alichukua waya fulani wa 'USB'
akauchomeka katika simu yake iliyokuwa na
programu maalum kisha upande wa pili wa waya
huo akauchomeka mahala fulani pembeni ya
kidubwasha kilichobeba vitufe vilivyo na namba
sifuri hadi tisa.Kidubwasha hiki kilifanana na mita
za umeme wa LUKU za TANESCO. Mara
alipochomeka waya huo, namba fulani zilionekana
zikipita na kubadilika kwa kasi katika kioo cha
simu yake kisha zikajitokeza tarakimu sita. Yusoof
akazibonyeza tarakimu zile katika kidubwasha
kile.Ukasikika mlio 'krack'. Loki ilikuwa
imefunguka.
Yusoof akafungua milango ya gari lile ,ndani ya
gari lile akaonekana mtu mwenye ndevu nyingi na
ndefu sana huku akiwa na upara wa haja. Mtu huyu
alikuwa amesheheni pingu madhubuti sana
zilizofungwa mikononi na miguuni. Yusoof
alizitawanyisha pingu hizi kwa risasi kutoka katika
bastola yake.Yule bwana akashuka kutoka katika
gari.
Naam.Labda ni kimo cha gari like kilichomfanya
atoke akiwa kainama kilichangia kumfanya
aonekane kuwa mtu wa kimo cha kawaida
tu.Aliposhuka kutoka katika gari lile alionekana
sasa kuwa mtu mwenye tambo kubwa na mrefu
sana. Japo alikuwa katika vazi kubwa la asili kama
yale yanayovaliwa na 'Wanigeria', lakini haikusaidia
kuficha kuonekana kwa misuli mikubwa
iliyojengeka katika mwili wake ule.Usoni
alionekana kama mtu aliye na umri wa miaka
mwishoni mwa arobaini au mwanzoni mwa miaka
hamsini.
Mara mtu huyu alipokanyaga ardhi,watu kadhaa
waliokuwepo mahali hapo wakiwa webeba bunduki
zao, walipiga goti moja chini na kukunja mkono wa
kulia mbele huku wakiinamisha ichwa chini usawa
wa mkono uliokunjwa kama ishara ya heshima
kubwa.Kwa kuwaangalia tu, ilionekana huyu
aliyekuwa mbele yao alikuwa mtu mkubwa na
mwenye kuheshimiwa sana na watu hawa.
Bwana yule akawataka watu wale
wasimame,akawakumbatia kila mmoja na
kuwabusu katika paji la uso huku akizungumza nao
kwa lugha ya kiarabu.Wakati huo huo helkopta
nyingine ikawasili eneo hilo.Hii ilikuwa na chapa
ya shirika la utangazaji la CNN. Bwana mkubwa
yule akaongozwa na watu wake hadi katika
helkopta ile na baada ya kupanda ikapaa na
kutokomea kutoka katika eneo hilo. Sekunde
chache baada ya helkopta ile kupaa, ile helkopta
iliyotumika kubeba gari, ililipuka na kuteketea
kabisa.
*********************************************
*****************************************************
"Breaking news".Ndivyo vioo vya luninga
vilivyosomeka siku hiyo.Vituo mbali mbali vya
televisheni vilikatisha matangazo ya kawaida na
kurusha habari hizi mpya zilizokuwa na msisimko
kuliko habari nyingine.Vituo vikubwa vya
televisheni na radio viliripoti moja kwa moja
kutoka eneo la tukio.Makamanda waliohusika
kuongoza msafara ule walihojiwa nao wakatoa
ushirikiano wa kutosha. Vyombo vya habari vya
kimataifa kama BBC,CNN,ALJAZEERA na Sky News
navyo viliripoti kupitia wawakilishi wake.Dunia
nzima ilipata habari hizi za kuogofya moja kwa
moja kwamba yule gaidi aliyeisumbua dunia kwa
uhusika wake katika matukio mbalimbali bwana
'Omar Al-Mahmood' ametoroka tena kutoka katika
ulinzi mkali sana.
Usiku ulipita,siku mpya ikaanza kwa mchaka
mchaka wa hali ya juu.Jua lilichomoza wakati
makachero wa polisi na wanausalama wa vitengo
na idara mbali mbali wakiwa wamemwagwa kila
kona ya nchi. Wanausalama walipewa maagizo ya
kuacha kazi nyingine zote zisizo na uhitaji wa
haraka na kipaumbele chao kiwe ni kesi hii
iliyokuwa mbele yao. Kesi ya kutoroshwa kwa
gaidi aliyesemwa kuwa ni hatari sana zaidi ya
magaidi waliowahi kutokea katika historia ya bara
la Africa.
Baadhi ya wananchi walisikika wakitoa sifa kwa
kituo cha habari cha CNN kwa kuwahi kuelekea
eneo la tukio kabla hata mapambano hayajapoa
vizuri. Watu wengine walienda mbali zaidi kwa
kusema kuwa vyombo vya habari vya Tanzania
vimelala sana.Wapelelezi waliomwagwa kila kona
ya nchi walisikia habari ya helkopta ya shirika la
habari la ' CNN' kuonekana ikielekea eneo la tukio
kabla hata watu hawajajua ni nini kinaendelea.Lak
ini haikuchukua muda kwa wapelelezi kujua kuwa
ilikuwa ni helkopta ya 'CNN feki'. Magazeti nayo
hayakuwa nyuma kiripoti habari hii.
Gazeti la 'MTANZANIA MZAWA' liliandika " Gaidi wa
kimataifa aliyekamatwa na vyombo vya usalama
vya marekani kwa kushirikiana na Tanzania
ametoroshwa kutoka chini ya ulinzi mkali
alipokuwa anasafirishwa mara baada ya kutokea
mapambano makali sana.Gaidi huyo alikamatwa
katika mpaka wa Tunduma mkoani Mbeya wakati
alipokuwa akitaka kutorokea nchini
Zambia.Mapambano haya yalitokea baada ya
msafara huo kuvamiwa na kundi kubwa la watu
wanaodaiwa kuwa ni magaidi kutoka nchini
Somalia. Aidha maswali ambalo watu wengi
wanajiuliza sasa ni kuwa inawezekana vipi kundi
kubwa la magaidi kuvuka mipaka yetu na kuingia
nchini kwetu bila vyombo vya usalama kung'amua?
Na ni vipi watu hawa wavushe silaha nyingi kiasi
kike bila vyombo vya usalama kuona?"
 
J.K.T MAFINGA
Saa kumi na mbili na nusu jioni.
Ndani ya moja kati ya ofisi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),mlango uligongwa gongwa na mtu aliye nje.Sauti nzito ya mtu aliyekuwa ndani ilisikika ikisema "karibu".Mlango ulifunguliwa kisha ajenti Mick-reuben akiwa amevaa suti nyeusi iliyomkaa vyema ikisindikizwa na shati jeupe na tai nyeusi huku sikioni akiwa amevaa kifaa maalum cha mawasiliano kinachoitwa 'Tube Coiled Earpiece'.Kijana huyu alifunga mlango nyuma yake baada ya kuingia kisha akakaa katika kiti kilichokuwa mbele ya meza huku akitazamana na yule aliyekaa nyuma ya meza, mtu mzima mmoja ambaye alionekana kama mwenye umri kati ya miaka 50 hadi 55 hivi.
"Naitwa Mick-reuben kutoka C.T.I, nadhani ulipata ujumbe kuhusu ujio wangu".Aliongea kwa nidhamu kijana huyu huku akiwa katika hali ya utulivu wa hali ya juu.
"Ok, nimepata habari kutoka makao makuu na ndiyo maana niko ofisini hadi sasa.Mimi naitwa Aloyce Mwasambili.Ni mkuu wa kambi hili la Hapa mafinga.Nimepewa maagizo nikupe ushirikiano kwa kila utakachokitaka.Sijui nikusaidie nini kijana wangu."Aliongea kwa nidhamu pia mzee huyu ambaye mabegani alichafuka kwa nyota kadhaa.Alionekana kuwa mtu kwenye cheo cha juu.
"Kubwa hapa ni kuhusu tukio lililotokea na ambalo bado ni la moto kwa taifa letu na mataifa mengine.Tukio la kutoroka kwa gaidi wa kimataifa Omar al-Mahmood. Namna pekee ya kujua aliko kirahisi ni kwa kuwatambua baadhi ya watu wanaotuhumiwa kusaidia kutoroka kwake. Moja ya watu wanaotuhumiwa kuhusiana na tukio hili ni mtu ambaye hapo mwanzo alidhaniwa kuwa ji marehemu tangu mwaka 1998.Lakini katika upelelezi imegundulika kuwa yupo hai na anahusishwa moja kwa koja kwa kuhusika na tukio hili kwa namna moja au nyingine.Tumemtambua mtu huyu,kwa jina anaitwa John Karobota.Kwa kuwa hakufariki, ninaweza kusema kuwa alipotea akiwa na cheo cha luteni katika jeshi la wananchi,yaani JWTZ."Alianza kujieleza Mick kisha akaacha kwa muda kidogo kumuacha mwenyeji wake ayatafakari haya kabla hajaendelea kumueleza kwa kina.
"Sasa picha iliyopatikana inayotushuhudia kuwa mtu huyu yupo hai , imerekodiwa na kamera za kambi hii kwa hiyo tunaamini mtu huyu alikuwapo ndani ya kambi hii aidha kwa muda mrefu au kwa muda mfupi.Picha yenyewe ya mtu huyo ni hii hapa,sijui kama unaweza kuitambua".Alimaliza kueleza Mick huku akitoa 'Tablet' kutoka katika mfuko wa suruali aliyoivaa, kisha akapapasa kioo hapa na pale kisha picha waliyoipata ya John Karobota ikaonekana vizuri kabisa.Ni picha ya muda mrefu,lakini mkuu wa kambi hii bwana Aloyce alionekana kuitambua mara baada ya kuiangalia kwa sekunde chache tu.
"Picha hii siyo ngeni kwangu......Ahaa....Nadhani nimekumbuka kitu.Miezi kama mitatu hivi iliyopita,nilipigiwa simu kutoka makao makuu ofisi ya C.D.F(Mkuu wa Majeshi Tanzania). Simu hii ilipigwa na katibu muhtasi wa C.D.F, ambaye alinipa maagizo kuhusiana na ujio wa mtu huyu, kwamba atakuja katika kambi hii kwa muda mfupi kwa sababu ya kazi maalum anayoifanya katika mipaka ya nchi upande huu wa nyanda za juu kusini,yaani katika mkoa wa Mbeya kisha ataondoka.Kwamba hapa ndiyo itakua kituo chake kikuu wakati wote atakaokuwa akifanya kazi hiyo. "Alijieleza kwa maelezo ya mwanzo mkuu huyu wa kambi kisha akanyamaza kidogo akionekana kufikilia jambo fulani kwa kina kabla hajaendelea.
"Nilitambulishwa jina lake.Anaitwaaaaaaaa (huku akitafuta kitu katika makabrasha mengi yaliyokuwa katika droo za meza yake na kisha kutoa bahasha moja ya ukubwa wa 'A4'.akaifungua haraka na kutoa karatasi mbili zilizounganishwa kisha akaiangalia kwa haraka), yes....Anaitwa Jeremiah Mwakibinga.Cheochake ni Luteni. Lakini hiyo picha uliyonionesha haina utofauti sana na sura yake.Labda tu hiyo picha naweza kusema inamuonesha akiwa kijana zaidi ya alivyokuja hapa, au labda kama ni ndugu yake aliyefanana kwa asilimia mia."
"Na hii ni barua yake aliyokuja nayo na pia nilitumiwa ' email' kwa anwani ya makao makuu ya jeshi( huku akibonyeza hapa na pale katika keyboard ya kompyuta iliyo mezani pake) ambayo ni hii hapa".Alimaliza kuongea mkuu huyu wa kambi huku akimgeuzia Mick kompyuta yake ili aweze kuona barua pepe ile.
"Wewe umewahi kuzungumza na katibu muhtasi wa C.D.F kabla"Alihoji Mick Reuben.
"Ndiyo nimewahi kuzungumza naye zaidi ya mara ya tatu na hii ilikuwa ni ya nne.Tena kwa namba hiihii tangu nilipoteuliwa kuwa mkuu wa kambi hii miaka mitano iliyopita."Alijibu mkuu huyu wa kambi hii ya JKT.
Kisha mara tu alipojibu akaonekana kukumbuka kitu kwa ghafla ambacho ni kama kilimshitua kidogo.
"Lakini, kuna kitu nimekumbuka ambacho sijawahi kukifikiria hapo mwanzo.Nilipoongea naye mara ya mwisho,sauti yake ilikuwa kama inakwaruza hivi, siyo ile niliyowahi kuisikia kabla.Na siku ile alikuwa akiongea kama mtu aliyechangamka sana tena kirafiki kuliko kawaida ya siku zingine ambapo huwa anazungumza akiwa yupo siriasi , tena kwa sauti kama ya ki-amri amri hivi."Alimalizia kuongea mkuu huyu wa kambi,Aloyce Mwasambili.
Kengere ya hatari ikalia katika kichwa cha Mick.Tayari alikwishaunganisha maelezo haya na mambo ambayo yeye alikuwa akiyahisi, na kung'amua jambo katika kichwa chake.
"Ahsante.Ila kwa kukumbushana tu nadhani unafahamubkuwa tuliyoongea hapa ni siri kubwa na hakuna mtu anatakiwa kufahamu.Nikikuhitaji tena nitakutafuta.Naomba niondoke na barua hii kwa upelelezi zaidi pia naomba unitumie barua pepe hiyo uliyotumiwa katika anwani hii( huku akimuandikia anuani ile)." Akamaliza kuongea Mick.
"Haina shida.Nafurahi tu kama maelezo yameweza kukusaidia kwa lolote.Wakati wowote utakaponihitajiunakaribishwa sana".Aliongea mkuu wa kambi kisha wakapeana mikono na Mick.Mick akaondoka huku akionekana kufikiria mambo kadhaa kichwani.
******;********************************************************************************************
"Nimefanyia utafiti ile barua uliyokuja nayo pamoja na barua pepe.Nikianza na barua.Imefanana na barua za makao makuu ya jeshi kwa asilimia kubwa sana.Asilimia chache zilizobaki kufika asilimia mia iko katika muhuri uliopigwa katika barua hii.Kama unavyoona, muhuri wa jeshi uko katika umbo la duara.Lakini nikifananisha na barua nyingine kutoka makao makuu ya jeshi, zinatofautiana kidogo katika kipenyo kwa milimita moja na nusu.Pia umbali kati ya herufi na herufi umetofautiana kwa umbali ambao haiwezekani kutambua kwa macho ya kawaida.Mimi mwenyewe nimeng'amua hayo baada ya kui'scan' katika kompyuta na kutumia programu maalum ya kompyuta inayoweza kupima vitu hivyo."
"Nimeitafiti barua pepe ambayo ilitumwa kwa mkuu wa kambi ya jeshi Mafinga.Nimetafiti pia na namba ya simu ambayo mkuu wa kambi ya JKT Mafinga anadai kuwa ilipigwa kutoka makao makuu ofisi ya C.D.F na katibu wake.Vyote hivyo,yaani barua pepe na simu vilitumika kuwasiliana kutokea eneo la ofisi za mamlaka ya mapato (TRA) Mbeya. Ninadhani mpigaji simu na mtumaji wa barua pepe hiyo alikuwa mtaalamu au aliwezeshwa na mtaalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano na inawezekana alitumia programu maalum kufanya mawasiliano hayo.Programu hiyo inamsaidia mtumiaji kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine,na hivyo nadhani mawasiliano ya ofisi ya C.D.F yaliingiliwa. Nathubutu kusema mtaalam wa teknolojia aliyehusika kufanya haya yawezekana ni mtaalamu wa hali ya juu sana kuweza ku-'hack' hata mawasiliano ya taasisi kubwa kama ofisi ya mkuu wa majeshi".
"Kwa sababu hiyo ninaweza kuhitimisha kuwa mawasiliano hayo pamoja na barua ile ni feki na wala hazihusiani na ofisi ya C.D.F."Alimaliza kuongea Clara.Wasikilizaji wake walikuwa ni ajenti Mick,mkurugenzi wa C.T.I, Maajenti wengine watatu wa C.T.I pamoja na mtu mmoja aliyekuja pamoja na mkurugenzi wa C.T.I ambaye wengine walikuwa bado hawajamfahamu.
"Kwanza naomba niwatambulishe mgeni wetu huyu. Kutokana na majukumu kuwa mengi, raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa George Katumba amemteua Josephat Moses kutoka idara ya usalama kitengo cha ulinzi wa rais,kuwa makamu mkurugenzi wa idara ya C.T.I. Sahani kwa kuwa mpaka wakati huu amekwisha kuhudhuria kikao chake cha kwanza ndani ya idara bila nyinyi kumgundua.Hii ni kwa sababu rais ameagiza aanze kazi mara moja."Aliongea mkurugenzi wa C.T.I na wanaidara waliokuwemo katika kikao hiki wakapiga makofi kama ishara ya kumkaribisha mgeni huyu.
"Lakini pia ,kutokana na alichokigundua Mick pamoja na maelezo haya ya ajenti Clara, basi ninadhani kuna umuhimu wa ajenti Mick na ajenti Clara kwenda kwenda huko Mbeya ofisi za mamlaka ya mapato TRA mkaanzie hapo.Wengine tutaendelea kutoa usaidizi kutokea hapahapa ofisini. Mtapata usaidizi wote mtakaouhitaji."Alimaliza kuongea mkurugenzi wa C.T.I.
Dakika ishirini baadaye,Ajenti Mick pamoja na Ajenti Clara walikuwa ndani ya helkopta iliyo na chapa ya polisi wakielekea Mbeya .
***************************************
 
Nilibaki kwenye kile chumba nikikitizma huku nikijaribu kukagua kila pahali na sikuchelea kugundua kuna kamera zimefungwa mle ndani.
“vua nguo zote’ ilisikika sauti kutoka kwenye zile spika zilizokuwa zimefungwa mle ndani.
Nikavua bila ubishi na punde nikasikia tena sauti ikiniamuru nielekee upande ilipokuwa spika kubwa na hapo nitapata traksuit nyeusi na nikaamuriwa kuivaa.
Mziki ulianza kusikika kutoka kwenye zile spika na mimi nikajua sina tena muda wa kukaa inabidi nifanye mazoezi ili nitoke salama ninakotakiwa kwenda ili wazee wangu wapate kuishi salama.
Nilifnya mazoezi makali bila kupumzika na sasa nikawa nipo kwenye panchingbag nikijaribu kutupa mitupo kadhaa ya ngumi huku akili yangu ikiwa mbali na jambo lolote ndani ya chumba kile hata muziki sikuusikia kabisa ilikuwa ni mimi najasho langu.
“pah pah…’ nilisikia makofi yakipigwa tokea nyuma yangu na nikageuka na kukutana na Kisuti akiwa na wale wazungu wakitabasmu na hapo kisuti akanambia jambo lililonifanya nikatae kwa mara ya kwanz tangu niingie pale ndani.
Alinambia wale wazungu wamependekeza nifanyiwe uapasuaji wa sura yanguili nifanane na wazungu kabisa,nikakataa katakata hilo jambo sikutaka kwenda kinyume na uumbaji wa mungu alieniumba hivi nilivyo.
-----------------------
Baada ya malumbano ya hapa na pale hatimae walikubaliana na mimi na wakaamua kuondoka na kuniacha na kisuti alienielekeza pahali pa kuoga na huko maliwatoni nikakutana na nguo nilizopaswa kuzivaa ilikuwa ni suti nyeusi.
Nilipotoka maliwatoni nikkutana na Kisuti akinisubiri mlangoni na aliponiona akaonesha ishara nimfuate akaniongoza hadi kulipokuwa na ukumbi wa chakula na huko nikakutana na watu wengine ambao walikuwa ni wale wazungu na wanajeshi lakini alikuwa ameongezeka mtu mmoja alikua amevalia kibandiko cha chuichui kichwani na aikuwa na koti refu jeusi,uso wake ulionesha ni katili sana mtu yule.
Chakula kililetwa mezani na kila mtu akaanza kula lakini mimi nikabaki nikijiliza juu ya mtu yule alieonekana kama ndie mkubwa pale na hpo sura yake ikanijia vyema alikuwa anafanana na raisi wa Zaire mika ile bwana Mobutu sese seko.
Nikanyanyua uso wangu ili nimtizame vyema mtu yule ni kweli walifnana na hpo nikajua ndo sababu ya yeye kuvaa kile kikofia alichopenda kukivaa mobutu enzi ya uhai wake.
Sikupata jibu kwanini yako hivi mambo haya ila sikutaka yanipe uzito katika akili yangu kubwa sasa ni kuhusu uhai wa wazee wale basi mengine sitaki kuyaingilia kama mimi kufanya kazi yao ndo uhuru wao hakuna shida.
Tulimaliza kula na hapo kisuti akanipeleka sehemu nyingine ya jengo lile na huko nikakutana hospitali kubwa ya kisasa na manesi kadhaa walikuwa wako bize kuwahudumia watu kadhaa ambao sikujua wamepaytwa na kadhia gani.
Tuliongoza hadi ndani kabisa ya hospitali ile na huko nikawekwa kwenye chumba Fulani hivi na kufungiwa humo kisha kisuti akaniacha na kwenda zake.
Nikiwa nimekaa kwenye kitanda kilichokuwa mle ndani akaingia dada mmoja aliekuwa kavalia mavazi ya rangi ya bahari na vifaa kadhaa vya utababibu kwenye kisinia.
Alipoviweka kwenye kimeza kilichokuwa mle ndani akaniamuru nilale juu ya kile kitanda lakini kabla sijalala nikamuuliza kuhusu kile kimshono kilichokuwa karibu na kwapa langu.
Akanitazama bila kusema neon kisha kachukua simu yake na kuniandikia neno “traking” hapo nikatambua nimewekewa chip ya kufuatilia mwenendo wangu na kila nikifanyacho.
Dokta yule alifanya anavyojua juu ya mwili wangu kisha akaniruhusu nisimame na niliposimama akanionesha chumba Fulani mle ndani na kuniruhusu nikalale kwa masaa mawili tu nami nikaenda kulala ndani ya kile chumba.
Kilikuwa chumba kizuri sana nikalala chali na kutazama paa la nyumba ile usingizi haukuja kabisa na hapo nikapitisha kumbukumbu za miaka kadhaa nyuma.
---------------------------
DODOMA 1999
Alikuwa mbele name nilikuwa nikimfuata kwa nyuma huku mgongoni nikiwa na begi kubwa lilokuwa na uzito wa kilo kama kumi na tano hivi huku yeye akiwa na begi lenye kilo hamsini.
Tulikuwa tumekwisha kukibia zaidi ya kilometa sabini tangu kupopambazuka na tayari kilometa hizo tulikuwa tunazimalizia kwa kuingia ndani ya uzio wa nyumba yetu.
“kila unachokifanya hakikisha unakuwa na kiba nacho hivyo hata sasa ulipaswa kuwa na akiba ya pumzi”alinambia kamanda Malebo.
Tuliingia kwenye chumba cha mazoezi na tuliendelea kkufanya mazoezi kwa ajili ya kuweka sawa miili yetu ili misuli isipate shida baada ya mwendo mrefu wa kukimbia.
Tulimaliza mazoezi na kuelekea bafuni huko tulioga nakurudi mezani na kukutna na kifungua kinywa kilichokuwa tayari na kilikuwa kimeandaliwa na mfanyakazi pale nyumbani.
Jioni ilikuwa ni ratiba ya kwenda uwanjani kwa ajili ya kulenga shabaha.
Usiku ni muda wa mazoezi hadi saa sita ndo muda wa kulala na tulilala masaa matatu tu kisha kuamkia mazoezini.
Hiyo ndio ilikuwa ratiba yetu kila siku hadi huo mwaka unaisha.
--------------------------------
2005
Tayari nilikuwa nimeiva kila idara na hata mapambano ya aina yoyote nilikuwa fiti bila tatizo nahata baadhi ya wanafunzi wenzangu walikuwa wameonja joto la jiwe pindi waliponileta dharau.
2006
Kamanda malebo aliondoka kwenda nchini sudani kwa jaili ya kutuliza amani akiwa ni mmoja viongozi wakubwa na alikuwa anakaribia kustaafu jeshi baada ya kulitumikia kwa zaidi ya miaka thelathini ila huko ndiko yaliko mkuta masihibu yote na hakurudi tena nchini na hivyo mimi niliishi bila yeye zaidi ya miaka miwili.
2008
Niliamua tu kuingia chumbani kwake na kufungua email zake zilizokuwa kwenye kompyuta yake mle ndani na hapo ndipo nilipokutana na jambo la ajabu.
Yeye mwenyewe alikuwa amejiiemail lakini ni kama alitka mimi nipate taaarifa maana alikuwa amenieleza umuhimu wa mimi kuelekea Burundi kuonana na mzee niyonzima na kisha akaambatanisha ramani nzima ya kuweza kufika kwenye makazi yam zee yule.
Lakini kulikuwa na utata kwenye kuamua kuondoka maana muda huo nilikuwa kwenye harakati za kujiingiza kwenye jeshi la kujenga taifa.
Hapo ndipo nikakumbuka jindi harakati zile zilivyokuja kunibadilisha kabisa.
Nikakumbuka
--------------------
Ilikuwa ni ahsubuhi tulivu kabisa niliamka na kuelekea kwenye kambi ya jeshi makutupora na huko nikaenda kuonana na luteni kanali Mazengo lengo likiwa ni kuomba anisaidie nipate kujiunga na jeshi la kujenga taifa.
‘huoni kama huna sifa za kuwa mwanajeshi?” ndilo lilikuwa swali la kwanza na hivyo kunifanya nikose chakumjibu ni kweli nilikuwa nina mapungufu kwenye ngozi yangu na kanuni na taratibu hazikuruhu mimi kuruhusiwa kujiunga.
Nilirudi nyumbani huku mawazo yakiwa mengi kichwani na nilishindwa kujua kwanini nafanyiwa vile na watu hawa na kwanini sheria hairuhusu alibino kujiunga na jeshi?
 
Sikulala usiku huo na kulipopambazuka ikabidi niende tena kule jeshini na nilipofika nikakuta watu wengi wanafanyiwa usaili na mimi nikajiunga kwenye mstari lakini sikudumu sana akaja Mp MMOJA NA KUNIONDOA KWA KEJELI NYINGI
Nikasimama pembeni huku sasa machozi yakiwa wazi usoni pangu na nilikuwa nimesimama juani.
Usaili ulikuwa upo ukingoni ndipo katokea luteni kanali Mazengo na kuniona akanitazama kisha kwa upole akaniita,nilipofika kwake akanisihi sana nibadilishe maamuz yangu na kaniahidi niwe kiongozi kwene kampuni yake ya ulinzi lakini nilikataa hiyo haikuwa kichwani pangu kabisa.
Baada ya miezi miwili ilibidi vijana wote walipita kwenye usaili waripoti kambini na mimi nikaenda huku nikiwa na nguo tatu tu kwenye mfuko a Rambo.
Vijana wote walikuwa wamenyoa nywele hata mimi pia nilinyoa nywele zangu zote.
Vijana kadhaa walikuwa wanakagua vijana wenzao wanajiunga na jeshi nailipofika zamu yangu nilitolewa pembeni huku wao wakiendelea na utaratibu wao.
Vijana wote waliruhusiwa kuingia kambini ila mimi nilikataliwa huku wale vijana wadogo waliokuwa wamevaaa sare zao mpya wakianza kunizonga zonga ili nitoke eneo lilelakini ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa ili acheze.
Mzozo wetu ulidumu kwa dakika kadhaa huku vijana wale wa JW wakianza kunishambulia bila mafanikio maana nilikuwa nikijitahidi kuwakwepa kila walipojaribu.
Walikuja ma MP wawili na kuwaondoa vijana wale kisha wakabaki na mimi na hapo wakaanza kunirukisha kichura,tofauti na walivyotegemea walinikuta nipo fiti kioa idara hatawalipojaribu kunipiga push up mia zote nilizimaliza na kuwaacha wakiwa wanashangaa tu,wakaona haitoshi wakaanza kukimbia na mimi kuzunguka uwanja uliokuwa pale kambini bado nilianikiwa kuwaacha nakuwazunguka bila taabu yoyote.
Yale yote wakati yakiendelea luteni kanali Mazengo alikua anashudia kutoka kwenye ofisi yake iliokuwa karibu na uwanja ule alitoka na kuja hadi pale kiwanjani na kunisimamisha hukuwale askai wakimpigia saluti mkubwa wao.
Alinitizama na kutikisa kichwa kisha akaniita ofisini kwake,hakusema kitu akachukua simu iliokuwa pale ofisini kwake na kupiga pahali na katika mazungumzo yao nilisikia wakitaja neno usalama wa taifa na alipokwisha kumaliza maongezi akanigeukia na kunambia niende nje kuna mtu ataniongoza kwenda kwenye bweni na huko nitapewa maelekezo mengine.
--------------------
Tulikuwa tupo kwenye mazoezi makali ya wiki za mwanzo huku kila kitu kwangu kikiwa kama marudio tu na hapo nikawa nikiwafurahisha wakufunzi wangu ambao walikubali uwezo wangu lakini hawakuwa na la kusema zaidi ya kutikisa tu vichwa vyao.
Ilikuwa imepitazaidi ya miezi mitatu tangu tuwe kambini na tayari uwezo wangu wa kutumia silaha ulikuwa upo wazi na kila mtu alitambua hakuna zaidi yangu.
Ilikuwa kama masihara ila sasa niliona jambo lile linakuja kuwa kubwa zaidi ilikuwa ni ombi nililopata kutoka kwa mkufunzi wetu alikuwa anataka niue wanafunzi wenzangu tukiwa kambini,sikujua kwa nini anataka iwe hivyo ila kila mara niliktaa kufanya hivyo na kaanza kunitisha na kunipa adhabu nyingi kila mara.
Waliongezeka wawili waliotaka niue angalau mmoja ili malengo yao yatimie na sikujua ni malengo gani.
Ilikuwa imebaki mwezi mmoja ili tuhitimu mafunzo huku sifa zangu zikiwa zimetapaka kwa kila mtu juu ya uwezo wangu wa kule mafunzoni.
Ilikuwa usiku mnene tulikuwa tumelala nje ya kambi kwa ajili ya zoezi maalumu na tulikuwa tumepewa lisaa limoja tu ili kupumzika na mimi niliamua kujitenga kidogo na wenzangu hasa kundi nililokuwepo walikuwa hawanipendi huku kila mara wakiiniita mnoko kwa kuwa nilikuwa nafanya mazuri kila siku kambini.
Kulikuwa na mvua kubwa usiku ule hivyo hata usingizi haukuwa mzuri sana kwenye yale mahema tuliokuwamo,nilishangaa nikiwa napewa hema klangu peke yangu huku wengine wakiwa wamelala watanowatano.
Yale matone ya mvua yalikuwa yanasikika vizuri masikioni pangu lakini sikio langu lilinasa sauti nzito ya kitu tofauti na matone yale,nikatega sikio vizuri na kweli ndivyo ilikuwa kulikuwa na kishindo kikubwa zaidi na nilifikiria ni kishindo cha kiatu cha miguu ya mtu,lakini hakuwa akitembea kawaida alikuwa ananyata.
Nilikaa kitako huku mwili wangu ukianza kusisimuka na hapo nikajua kuna tatizo huko je lakini ni vile tu hatukuruhusiwa kutoka nje kabla ya muda wa filimbi ya kuamshwa.
Mojngeo ule sasa ukahamia karibu na mlango wa kuingilia kwenye hema lile.
Nikasimama nikiwa nimevaa viatu vynguvyema huku nikiwa tayari kwa lolote.
Nikiwa nimesimama nikashuhudia watu wane wakiingia kwa kasi mle ndani huku wakiwa na rungu za kutenegeneza porini ama rungu za kuwindia.
Nikajipanga kuwakabili,mmoja kati yao kaja hadi karibu na mimi ili ashambulie lakini nikawahi kujua hil yake hivyo nikawahi kumpiga kwenye magoti na kisha nikaruka na kumpiga mwingine kifuani akadondoka chini na wakabaki wawili wakiwa wamesimama na sikutaka wapange hila yoyote nikawahi kumpiga mmoja teke ubavuni mwake na akaenda chini naliekuwa amebaki akakimbia nje.
Zile purukshani ziliwaamsha walikuwa hema la pili nao wkatoka kwa kasi na kuja mle huku wakiwa na tochi na walipokwisha kuingia wakawazingira wavamizi wale na hivyo nikapata kupumua.
Ahsubuhi kambi nzima ilikuwa ina taarifa ya wanafunzi wenzangu kunivamia lakini tulikuwa tumepewa onyo na wakufunzi hakuna kusema kilichotokea…………………….
-------------------------------
Nilisikia mtu akigonga kwenye chumba nilipokuwa na hivyokukatisha kumbukumbu zangu na mimi nikanyanyuka na kwenda kufungua nikakutana na Kisuti akiwa amesimama mlangoni huku akiwa na komputa mpakato na alinipa kisha akaingia kwenye kile chumba.
Alinionesha jinsi mtu yule alivyokuwa na ulinzi na siku ya kumuua ni siku gani na kiu gani nitahitaji ili kukamilisha zoezi hilo.
Alinipa maelekezo mengi na kuninesha video nyingi pia sasa alipohakikisha nimeelewa akaniomba nimfuate.
Tuliekea sehemu iliokuwa na chumba ha silaha na mimi nikachagua silaha chache tu kwa ajili ya kukamilisha kazi yangu huko brazil.
Nikaletewa kibegi kilichokuwa na hati zote za kusafiria na uhalali wa kuishi brazil,lakin pia kulikuwa na nguo chache za kuvaa,kisha nikapelekwa kwenye ndege ndogo iliokuwa kwenye viwanja vya kambi ile lakini sikuwa peke yangu nilikuwa naongozana na Kisuti.
Tulipanda ndege ile ndogo na safari ikaanza sikujua huko mbele mabo yatakuwaje na laity ningejua nisingelikubali mtego ule ila yote yanakuja tu kwa sababu ya ningejua………..


MWISHO WA SEASON ONE

ITAENDELEA JUMATANO HAPAHAPA
MNIKUMBUSHE SIKU IKIFIKA
 
Sikulala usiku huo na kulipopambazuka ikabidi niende tena kule jeshini na nilipofika nikakuta watu wengi wanafanyiwa usaili na mimi nikajiunga kwenye mstari lakini sikudumu sana akaja Mp MMOJA NA KUNIONDOA KWA KEJELI NYINGI
Nikasimama pembeni huku sasa machozi yakiwa wazi usoni pangu na nilikuwa nimesimama juani.
Usaili ulikuwa upo ukingoni ndipo katokea luteni kanali Mazengo na kuniona akanitazama kisha kwa upole akaniita,nilipofika kwake akanisihi sana nibadilishe maamuz yangu na kaniahidi niwe kiongozi kwene kampuni yake ya ulinzi lakini nilikataa hiyo haikuwa kichwani pangu kabisa.
Baada ya miezi miwili ilibidi vijana wote walipita kwenye usaili waripoti kambini na mimi nikaenda huku nikiwa na nguo tatu tu kwenye mfuko a Rambo.
Vijana wote walikuwa wamenyoa nywele hata mimi pia nilinyoa nywele zangu zote.
Vijana kadhaa walikuwa wanakagua vijana wenzao wanajiunga na jeshi nailipofika zamu yangu nilitolewa pembeni huku wao wakiendelea na utaratibu wao.
Vijana wote waliruhusiwa kuingia kambini ila mimi nilikataliwa huku wale vijana wadogo waliokuwa wamevaaa sare zao mpya wakianza kunizonga zonga ili nitoke eneo lilelakini ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa ili acheze.
Mzozo wetu ulidumu kwa dakika kadhaa huku vijana wale wa JW wakianza kunishambulia bila mafanikio maana nilikuwa nikijitahidi kuwakwepa kila walipojaribu.
Walikuja ma MP wawili na kuwaondoa vijana wale kisha wakabaki na mimi na hapo wakaanza kunirukisha kichura,tofauti na walivyotegemea walinikuta nipo fiti kioa idara hatawalipojaribu kunipiga push up mia zote nilizimaliza na kuwaacha wakiwa wanashangaa tu,wakaona haitoshi wakaanza kukimbia na mimi kuzunguka uwanja uliokuwa pale kambini bado nilianikiwa kuwaacha nakuwazunguka bila taabu yoyote.
Yale yote wakati yakiendelea luteni kanali Mazengo alikua anashudia kutoka kwenye ofisi yake iliokuwa karibu na uwanja ule alitoka na kuja hadi pale kiwanjani na kunisimamisha hukuwale askai wakimpigia saluti mkubwa wao.
Alinitizama na kutikisa kichwa kisha akaniita ofisini kwake,hakusema kitu akachukua simu iliokuwa pale ofisini kwake na kupiga pahali na katika mazungumzo yao nilisikia wakitaja neno usalama wa taifa na alipokwisha kumaliza maongezi akanigeukia na kunambia niende nje kuna mtu ataniongoza kwenda kwenye bweni na huko nitapewa maelekezo mengine.
--------------------
Tulikuwa tupo kwenye mazoezi makali ya wiki za mwanzo huku kila kitu kwangu kikiwa kama marudio tu na hapo nikawa nikiwafurahisha wakufunzi wangu ambao walikubali uwezo wangu lakini hawakuwa na la kusema zaidi ya kutikisa tu vichwa vyao.
Ilikuwa imepitazaidi ya miezi mitatu tangu tuwe kambini na tayari uwezo wangu wa kutumia silaha ulikuwa upo wazi na kila mtu alitambua hakuna zaidi yangu.
Ilikuwa kama masihara ila sasa niliona jambo lile linakuja kuwa kubwa zaidi ilikuwa ni ombi nililopata kutoka kwa mkufunzi wetu alikuwa anataka niue wanafunzi wenzangu tukiwa kambini,sikujua kwa nini anataka iwe hivyo ila kila mara niliktaa kufanya hivyo na kaanza kunitisha na kunipa adhabu nyingi kila mara.
Waliongezeka wawili waliotaka niue angalau mmoja ili malengo yao yatimie na sikujua ni malengo gani.
Ilikuwa imebaki mwezi mmoja ili tuhitimu mafunzo huku sifa zangu zikiwa zimetapaka kwa kila mtu juu ya uwezo wangu wa kule mafunzoni.
Ilikuwa usiku mnene tulikuwa tumelala nje ya kambi kwa ajili ya zoezi maalumu na tulikuwa tumepewa lisaa limoja tu ili kupumzika na mimi niliamua kujitenga kidogo na wenzangu hasa kundi nililokuwepo walikuwa hawanipendi huku kila mara wakiiniita mnoko kwa kuwa nilikuwa nafanya mazuri kila siku kambini.
Kulikuwa na mvua kubwa usiku ule hivyo hata usingizi haukuwa mzuri sana kwenye yale mahema tuliokuwamo,nilishangaa nikiwa napewa hema klangu peke yangu huku wengine wakiwa wamelala watanowatano.
Yale matone ya mvua yalikuwa yanasikika vizuri masikioni pangu lakini sikio langu lilinasa sauti nzito ya kitu tofauti na matone yale,nikatega sikio vizuri na kweli ndivyo ilikuwa kulikuwa na kishindo kikubwa zaidi na nilifikiria ni kishindo cha kiatu cha miguu ya mtu,lakini hakuwa akitembea kawaida alikuwa ananyata.
Nilikaa kitako huku mwili wangu ukianza kusisimuka na hapo nikajua kuna tatizo huko je lakini ni vile tu hatukuruhusiwa kutoka nje kabla ya muda wa filimbi ya kuamshwa.
Mojngeo ule sasa ukahamia karibu na mlango wa kuingilia kwenye hema lile.
Nikasimama nikiwa nimevaa viatu vynguvyema huku nikiwa tayari kwa lolote.
Nikiwa nimesimama nikashuhudia watu wane wakiingia kwa kasi mle ndani huku wakiwa na rungu za kutenegeneza porini ama rungu za kuwindia.
Nikajipanga kuwakabili,mmoja kati yao kaja hadi karibu na mimi ili ashambulie lakini nikawahi kujua hil yake hivyo nikawahi kumpiga kwenye magoti na kisha nikaruka na kumpiga mwingine kifuani akadondoka chini na wakabaki wawili wakiwa wamesimama na sikutaka wapange hila yoyote nikawahi kumpiga mmoja teke ubavuni mwake na akaenda chini naliekuwa amebaki akakimbia nje.
Zile purukshani ziliwaamsha walikuwa hema la pili nao wkatoka kwa kasi na kuja mle huku wakiwa na tochi na walipokwisha kuingia wakawazingira wavamizi wale na hivyo nikapata kupumua.
Ahsubuhi kambi nzima ilikuwa ina taarifa ya wanafunzi wenzangu kunivamia lakini tulikuwa tumepewa onyo na wakufunzi hakuna kusema kilichotokea…………………….
-------------------------------
Nilisikia mtu akigonga kwenye chumba nilipokuwa na hivyokukatisha kumbukumbu zangu na mimi nikanyanyuka na kwenda kufungua nikakutana na Kisuti akiwa amesimama mlangoni huku akiwa na komputa mpakato na alinipa kisha akaingia kwenye kile chumba.
Alinionesha jinsi mtu yule alivyokuwa na ulinzi na siku ya kumuua ni siku gani na kiu gani nitahitaji ili kukamilisha zoezi hilo.
Alinipa maelekezo mengi na kuninesha video nyingi pia sasa alipohakikisha nimeelewa akaniomba nimfuate.
Tuliekea sehemu iliokuwa na chumba ha silaha na mimi nikachagua silaha chache tu kwa ajili ya kukamilisha kazi yangu huko brazil.
Nikaletewa kibegi kilichokuwa na hati zote za kusafiria na uhalali wa kuishi brazil,lakin pia kulikuwa na nguo chache za kuvaa,kisha nikapelekwa kwenye ndege ndogo iliokuwa kwenye viwanja vya kambi ile lakini sikuwa peke yangu nilikuwa naongozana na Kisuti.
Tulipanda ndege ile ndogo na safari ikaanza sikujua huko mbele mabo yatakuwaje na laity ningejua nisingelikubali mtego ule ila yote yanakuja tu kwa sababu ya ningejua………..


MWISHO WA SEASON ONE

ITAENDELEA JUMATANO HAPAHAPA
MNIKUMBUSHE SIKU IKIFIKA
Mmh shemela jumatano mbali
 
Nisingependa kupoe hapa hivyo naombeni niweke simulizi kwa siku hizi tunazongojea season two

Bogoro – Buni, DRC

Msichana wa miaka 15 hivi, akiwa na majeraha mazito mwilini alizidi kujilazimisha kupiga hatua kwenye mtaa uliojaa maiti. Majeraha yake yaliyokuwa bado mapya yalifanya ausikie mwili wake kuwa kama ganda la kidonda kilichooza ambacho kilikuwa kikingoja mkasi kutumbuliwa ili kirushe usaa mzito. Kwa hali ilivyokuwa hakuwa na wakati wala namna ya kuyapooza majeraha yake hayo.
Kila kitu kilikuwa kimeharibika.
Nafsi yake ilikuwa imechafuka.
Akili yake ilikuwa imevurugwa vibaya.
Uwezo wake wa kufanya maamuzi ulishakufa ganzi.
Hali yake ya utu ilikuwa imeng’olewa kwa vile alivyokuwa amelazimika kuua bila kujali ili kupigania maisha yake. Maana maisha huwa na thamani kubwa sana mtu anapokuwa kwenye mdomo wa mauti. Ndiyo maana hata mgonjwa aliye dhoofu sana utashangaa anapata wapi nguvu anazotumia kupigania pumzi ya mwisho. Ni wakati mtu anapotakiwa kutoa pumzi ya mwisho ndipo huwa tayari kufanya chochote ili pumzi hizo zisimtoke!
Hakuwa akijali kitu sasa, bunduki aina ya SMG ikiwa inaning’inia begani kwake alishitushwa na mlio mkali wa ndege aina ya tai aliyekuwa akiruka wenye anga la eneo alilokuwepo.

Ndege huyu aina ya Tai alikuwa amefungua mabawa yake na kuyaachia yamiliki anga lililo juu ya kijiji kidogo kilichoko kwenye vilima ya Ituri, kijiji hicho kinaitwa Bogoro. Kiko kama kilomita 25 hivi toka mji wa Buni, Congo DRC. Tokea angani, macho yake makali yalikuwa yakiangalia juu ya barabara za mitaa ya mji huo, maiti kadhaa zilionekana zikiwa zimetapakaa mitaani. Ndege huyo fundi na mbabe wa anga, alitikisa mkia wake kwa furaha huku akitoa ukelele wa kusheherekea hali aliyoiona mitaani. Maiti zilizotapaa, hari ya baridi na unyevunyevu kufuatia mvua iliyokuwa imekatika punde, ilileta upweke kwenye mitaa hiyo ya Bogoro.

Kwa kawaida mji wa Ituri ufunikwa na mvua kubwa tangu mwezi wa pili hadi mwezi Juni. Mji huu ambao una lile pori kubwa na maarufu lenye mvua nyingi sana lijulikanalo kama msitu wa Ituri huwa wa kijani kibichi muda wote wa mwaka. Ndege walikuwa wenye furaha. Mijibwa ya mitahani ilikuwa imetulizana huku ikiwa imeshiba. Mlio wa maji yaliyokuwa yakitiririka baada ya mvua kubwa ulisikika. Hali ilikuwa kimya kabisa huku magari kadhaa-machache sana ya jeshi yalionekana kuzunguka kila baada ya dakika kadhaa. Magari hayo yalikuwa yameandikwa FRPI kifupi cha Patriotic Resistance Force in Ituri. Kwa ujumla hali ilikuwa ukiwa sana. Katikati ya hali hiyo Tai huyo aligeuza kichwa chake kumtazama binti mdogo aliyekuwa akikatiza kwenye mitaa pweke ya eneo hilo. Mitaa iliyokuwa imejaa maiti nyingi, zilizokuwa ama na majeraha mabaya ya risasi au visu. Hii ilikuwa ni masaa machache tangu yalipohitimishwa yale mauaji ya kikabila ya Bogoro ambayo wenzetu waliyabatiza jina Bogoro Massacre. Msichana huyu, alitembea taratibu huku akitetemeka kutokana na jinsi hali ilivyokuwa. Alitembea hivyo huku akijificha ficha. Tai yule alijikuta akimshangaa binti huyo, hivyo akawa akiruka anga hilo na kutoa milio ya kipekee huku macho yake makali yakimdhihaki.
Binti mwenyewe alimwangalia yule Tai kwa jicho baya, alitamani angekuwa na uwezo wa kumnyamazisha lakini alijua hilo lilikuwa nje ya uwezo wake. Alizidi kwenda kwa kujificha ficha huku akijitahidi kujificha kwenye macho ya yule Tai. Kutokana na uzoefu wake binti huyo, Tai huyo alikuwa wa hatari kama kama ambavyo magari ya wanajeshi yaliyokuwa yakipita yalivyokuwa ya hatari. Akiwa na umri wa miaka 15, tayari alikuwa amefunzwa vema kama mwanajeshi kamili, alikuwa na uwezo huo japo hakuwa na mwonekano huo. Akiwa anatokea kwenye kabila la Lendu, kabiloa ambalo hujishuhulisha na kilimo kwenye eneo hilo la Ituri, kufunzwa vita ilikuwa sehemu ya lazima kwenye jamii. Hii iliwawezesha kuwa tayari kwa vita ya kikabila kati ya kabila lake yaani Lendu na ile ya Hema. Makabila yote haya mawili yalikuwa yakipatikana kwenye jimbo hilo la Ituri huku Lendu wakijihusisha zaidi na kilimo na kabila la Hema wao wakifanya zaidi ufugaji. Ufugaji na ukulima ndiyo ilikuwa chanzo kikubwa cha kupigana kwao. Hawa wakitaka sehemu za malisho na hawa wakitaka sehemu za kulima.
Yeye akiwa kati ya watoto waliokuwa wamekamatwa kwa nguvu na kufundishwa mapigano na kundi la kijeshi la FRPI lilikuwa likiongozwa na Joseph Katanga. Ilikuwa dhahiri kichwani mwake kuwa mlio wa yule Tai, ungetuma ujumbe tosha kwa mwanajeshi yeyote kuwa eneo lile kulikuwa na mtu aliyeonekana wa ajabu ajabu. Ndiyo maana hakupenda kuona yule tai akiendelea kuzunguka eneo lile na kutoa aina ya mlio alioakuwa akitoa. Baridi kali, ubichi-ubichi, maiti za watu, upweke, majeraha aliyokuwa nayo na njaa vilifanya aonekane kiumbe wa ajabu katikati ya uwanja wa mauti.
Huku akiwa anachechemea, mara hii akaingiza mkono wake tena kuelekea sehemu za siri. Alipoutoa bado aliweza kuona damu mbichi kabisa ikiwepo. Alisimama, akavua chupi aliyokuwa amevaa. Aliiangalia ile chupi jinsi ilivyokuwa imechanwa kwa fujo na mtu aliyekuwa katika zoezi la kumbaka. Hapo machozi yakaanza kumtoka kwa mara nyingine tena. Aliitupa chini ile chupi na kuendelea kutembea tarataibu huku akichechemea kufuatia majeraha mwilini, baridi lakini pia kitendo cha kubakwa na mtu aliyekuwa amemwamini sana, Joseph Katanga. Hakutegemea kuwa siku mmoja kiongozi wao wa kundi la kijeshi, mtu aliyekuwa akihubiri kuwa alikuwa anapigania na kutafuta haki ya kabila la Lendu na jamii ya wakulima kwa ujumla angembaka kinyama namna ile. Khajat, huku silaha yake aina ya SMG ikiwa begani, silaha ambayo ilionekana kumzidi umri, alikuwa akikatisha upande mmoja wa barabara kwenda mwingine wakati aliposikia muungurumo wa gari ukija. Wakati huo huo yule Tai alizidi kupiga kelele. Alikimbia na kwenda kujibanda nyuma ya kibanda fulani kilichokuwa cha mbao. Ni wakati akiwa na hakika kuwa amejificha vema ndipo aliposikia sauti upande mwingine ikisema ‘Khajat, not safe, run this way! (Khajat, siyo salama, kimbilia huku). Ilikuwa ni sauti ya mtu aliyemjua, lakini hakuwa ni sauti ya mtu aliyetegemea kukutana naye. Aliangalia kule ilikotokea ile sauti, akamwona mtu aliyemwita, alimwangalia jinsi alivyokuwa taabani. Akajikuta anashawishika kwenda kumsaidia, wakati anakwenda akasahau kuwa alikuwa amesikia mlio wa gari hapo kabla. Kutokana na ukaribu wa yule mtu aliyemwita na jinsi alivyokuwa amejeruhiwa akakimbia tena kuvuka barabara. Wakati huo huo akasikia mvumo wa gari ukiwa jirani kabisa na alipokuwa, lakini kabla gari ile haijamfikia, ulitokea mlipuko mkubwa toka kwenye kile kibanda alichokuwa amejibanza. Mlipuko uliomrusha hewani. Akiwa hewani, msichana yule alitoa ukelele mkubwa wa hofu na maumivu “Jooooaaan!!

“Noooo, Khajat!! Huyu aliyejulikana kama Joan alipiga kelele baada ya kuona Khajat ametuwa chini kama mzigo baada ya kuwa amerushwa juu. Wakati anataka kukimbilia pale alipokuwa ameangukia Khajat, Joan alishikwa na mshangao alipomwona mzee mmoja wa makamu akienda pale alipoangukia Khajat na kumchukua. Ilikuwa ni kitendo cha kasi na wepesi sana. Ilikuwa kama vile Mwewe amchukuavyo kifaranga. Yule mzee alitoweka kwenye majengo yaliyokuwa jirani. Kuona hivyo Joan akakimbilia sehemu ambayo mzee yule alikuwa ameingia na Khajat. Vilikuwa ni vitendo vya haraka, hivyo wakati Joan na yeyé akiwa anapotelea kwenye lile jengo ndipo gari la jeshi la FRPI lilipopiga breki kwa fujo eneo hilo. Wanajeshi kadhaa walishuka na kuanza kukimbilia alipokuwa ameelekea Joan.
“Shiiiiiiii! Yule mzee alisema mara baada ya Joan kutokezea kwenye chumba ambacho alikuwa amemlaza Khajat na kuanza kumpa huduma ya kwanza.
“Mzee Kasheba! Joan alisema
“Kaa hapo Joan, huyu anahitaji huduma ya haraka kama kweli tunataka aendelee kuishi! Alisema mzee Kasheba.
“Wako wanakuja huko nje! Joan alisema. Punde kidogo wakasikia mlango wa jengo hilo ukigongwa kwa nguvu.
“Oooooh shiiit! Mzee Kasheba alisema kwa mshituko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom