Cephalocauda
Member
- Jul 31, 2015
- 62
- 14
Mzaramo, umetusahau nduguzo
Mkuuuu leta nyingineee aseee Sie wenginee MB zina takaa kuishaaa Mkuu letaaa mambooooSEHEMU YA ISHIRINI
WALA hakuwa amedanganya jina lake, ni kweli aliitwa
Eric Mlewa, akaelezea kuwa kazi yake ya awali ilikuwa
ni udalali jijini Mwanza, kazi ambayo haikuwa ikimlipa
vizuri lakini katu hakuwahi kulala njaa.
Siku moja alikutana na bahati ya mtende pale
alipopata mteja anayetaka nyumba nzima, na mkononi
Eric tayari alikuwa na nyumba hiyo. Akamtajia bei
kisha akampeleka nkatika nyumba hiyo!!
Kama ilivyo kawaida ya madalali sio wakimya,
huzungumza sana mithiri ya dereva taksi.
Eric alizungumza mengi na yule mteja ambaye alikuwa
amempakia katika gari lake wakielekea huko nyumba
ilipokuwa inapatikana, Eric alizungumza mengi sana
na kuonyesha ni kiasi gani anaujua ule mji mzima.
Maongezi yale yakamvutia yule mteja,hata baada ya
kumfanikishia kupata nyumba yule bwana akamtafuta
Eric kwa mara nyingine na hapa akamtangazia kazi
iliyokuwa na manufaa makubwa, ilikuwa kama udalali
lakini huu ni udalali wa kutafuta watu.
Wasichana wenye umri usiozidi miaka kumi na tano
wasiokuwa na kile chochote na ikiwa vyema wawe na
ule mvuto wa kike.
Eric aliona kazi hiyo ni ndogo sana kwake, akapewa
maelekezo na kuanza mara moja.
Ni katika kazi hiyo maisha yake yalibadilika na
hakuwahi kujiuliza kuna nini kimejificha nyuma ya
pazia.
Aliishia kuambiwa kuwa hao wasichana wanakwenda
kufanya kazi nzuri kabisa nchini Oman na huko Dubai.
Alipowauliza wao wananufaika nini, akajibiwa kuwa
asilimia ishirini ya mshahara wa hao mabinti ndo posho
yao.
Neema zikamuangukia Eric Mlewa, kwa juma moja
alipata hadi wasichana wawili, anawakabidhi kwa huyo
mkuu wake wa kadhi na analipwa chake.
Baadaye kwa sababu ya uchapakazi wake akapandishwa
cheo na kuongezewa kazi na posho, alitakiwa kutafuta
msichana kisha yeye ndiye anamshughulikia masuala ya
pasi ya kusafiria.
Eric akajenga nyumba kubwa jijini Mwanza,
pembezoni kidogo maeneo ya Shamaliwa.
Maisha yakabadilika!
Baadaye akahamishiwa ofisi za Dar Es salaam.
Alipofika huku alikuta mzozo uliojitokeza juu ya
mfanyakazi aliyetoroka nchini Oman na kurejea
Tanzania huku akiwa na siri nzito.
Siri ambayo kamwe Eric hakuwahi kuifahamu.
“Kwa kweli nilianza kuhisi kuwa kuna mchezo mchafu
unaendelea huko Oman dhidi ya hawa mabinti lakini
sikuwa na namna ya kufanya, tayari nilikuwa katika
huu mtandao….. siku kadhaa baadaye nikamwona huyo
binti. Nilimuona katika picha, na hapo nikawaona
vijana watatu waliopewa juikumu la kumrejesha
kazini.
Siku kadhaa baadaye katika gazeti nikaona taarifa ya
huyo binti kukutwa ameuwawa…. Niliona gazetini.”
Alisita Eric kusimulia kisha akaendelea na hapo mbele
yake walikuwepo watu watatu, IGP, Sajini Pilipili na
Geza asiyekuwa na cheo.
“Nilifadhaika sana na kuhisi kuwa wale akina dada
wote niliowashawishi kwa maneno matamu ya kidalali
kisha wakaenda Oman wapo katika mateso, nakiri
kuwa sikuwahi kushtaki popote hadi leo hii nipo
mikononi mwenu wakuu. Ila sijui lolote kuhusu
mtandao huu…. Nimejikuta tu ndani yake.” Alimaliza
kusimulia Eric Mlewa.
Geza alikuwa hamtazami machoni, alipomtazama kwa
mara ya kwanza alikuwa na swali kwake.
“Kwanini ulitaka kukimbia mpaka nikatumia teke
kukurudisha ndani ikiwa hujui lolote…”
Eric hakutarajia swali lile, akaomba msamaha!
Hakujua anayemuomba msamaha ni mtu wa ainja gani.
Geza aliwageukia Sajenti na IGP kisha kwa upole
kabisa akawaambia.
“Mmemsikia wenyewe ananitukania mama yangu….
Mmemsikia kwa hiyo msije kusema mimi mkorofi” na
mara ghafla akajirusha na kumfikia Eric akamtandika
ngumi moja kali sana katika sikio lake na hapohapo
akamuuliza.
”Unasikia kitu gani sikioni kwako?”
Eric alikuwa hasikii chochote bali miluzi mikali kabisa.
Geza alijua kuwa hasikii, akamwacha kwa sekunde
kadhaa.
“Geza muache usije kumuua bwana… tunahitaji
kumsikia.” IGP alimuonya Geza.
Geza akasusa, akasimama atoke nje!
IGP kamfuata nyuma.
“Mkuu unamuoneaje huruma huyu mpumbavu? Hebu
nenda ukamuulize kama wakuu wake walijiuliza wakati
wanaikunja shingo ya Hajrati hadi akapoteza maisha,
huyo ni mmoja ambaye tunamfahamu, unadhani
wameua wangapi?? Je? Kuna hata mmoja wao
amewahi kusimama akasema, ‘mwache huyo binti
utamuua?........ Geza alihoji bila kugeuka nyuma.
IGP akakiri kimya kimya kuwa Geza anajua
anachokifanya na wala hakurupuki!
Kimoyomoyo akatamani kama siku moja Geza
angejiunga na jeshi la polisi avikwe vyeo afanye kazi
kihalali kabisa.
Lakini hiyo haikuwahi kuwa ndoto ya Geza Ulole.
“Nenda ukazungumze naye Geza… we nawe kidogo tu
unataka utukimbie… au umeshawakumbuka wale
mademu zako.” IGP kamtania Geza.
Na kwa mara ya kwanza katika maisha yake akayaona
meno ya Geza akiwa anacheka!
Mkuu wa jeshi la polisi akajifunza kitu!
Geza akamwendea Eric Mlewa ambaye sasa alikuwa
anaweza kusikia tena vizuri.
“We dogo! Niliwahi kuwa mpumbavu kama wewe, wakuu
wangu wa kazi wanafanya ujinga kisha wananijaza
ujinga eti siku nikikamatwa nisiseme lolote…. Usiwe
mjinga kama nilivyokuwa mimi dogo. Nitakuua vibaya
mno….na nikiamua kukuua siui kwa dakika moja,
nitatumia masaa mawili na nusu hivi ili ukasimulie huko
motoni inauma kiasi gani kutolewa roho na Geza.”
Maneno haya yakamwingia Eric, akaanza kuimba
mengine anayoyajua kuhusu ule mkakati.
Akataja kuwa mkakati ule unahusisha mtu mzito
nchini ambaye hajawahi kulijua jina lake lakini kuna
siku alisikia wakimtaja kama kamanda, akaelezea
kuwa ni mradi endelevu wa kurithishana na ni mradi
ulioanzia Zanzibar koloni la zamani la waarabu wa
Oman.
Mradi wa kupeleka wasichana Oman kufanya kazi huku
wakilipwa kiduchu, lakini kuhusu kuwanyanyasa
wasichana alikata kata kata hajawahi kusikia juu ya
hilo.
Geza akamtazama na wala hakumpiga tena,
akawavuta IGP na Sajenti Pilipili kando kisha
akawaeleza kwa ufupi.
“Huyu kijana ametapika hadi nyongo”
Wote wakaduwaa, IGP akalalamika, “ndo maana
nilikwambia usimpige utaua!!”
Geza akatabasamu akatambua walikuwa hawajaelewa
maana yake, “Amesema kila kitu anachokijua….” Geza
akafafanua kwa utulivu.
“Umemuaminije?”
“Nimemuuliza vizuri sana kwakweli.” Aliwajibu na
kisha akamwachia Sajenti Pilipili jukumu la kuwahoji
wale wawili waliobakia.
“Sasa unaenda wapi Geza?” Sajenti alimuuliza.
“Kule uliponitoa siku ile, wale mademu wamenitumia
meseji wanalalamika eti sikulipa bili siku ile
wamekamatiwa simu zao pale baa…. Naenda kusafisha
jina mara moja!!” alijibu Geza huku akiondoka zake.
IGP na Sajenti walibaki na mzigo wa matabasamu
bandia katika nyuso zao!
Geza alitoweka!!
Ni kama kuondoka kwa Geza kulizua balaa ama labda
kuondoka kwa Geza alilikwepa balaa jipya!
______
NCHINI OMAN
Rama anasimulia!
Nilikiona kifo kikiwa kinaunda urafiki na mimi
waziwazi kabisa, na sikuwa tena na silaha.
“Brother… help me… take me out with you” niliisikia
sauti ikinisihi, ilikuwa ni sauti ya kike. Hapo hofu
ikapungua ya kudhani ninakabiliwa na maadui ama
kiumbe hatarishi.
Nikamuuliza kiingereza yeye ni nani akanijibu kuwa
tulikuwa wote kule chimboni. Nikamuuliza maswali
mawili matatu yaliyonijengea imani, kwa kupapasa
nikaipata silaha yangu na hapo nikamsihi asogee
nilipokuwa, akafanikiwa kunifikia, nikamgusa na
kumwambia atulie palepale alipokuwa nitafute namna
ya kutoka katika lile tanki ola maji.
Nilipapasa huku na kule hadi nikafanikiwa kuipata
ngazi, nikaijaribu uimara wake kisha nikapanda hadi
juu. Nikachungulia.
Hapakuwa na mtu yeyote yule!
Nikashuka hadi chini na kumweleza yule binti anifuate,
tukapanda ngazi hadi kutoka nje kwa uangalifu
mkubwa sana.
Eneo lote lilikuwa kimya kabisa, tukapita hadi
tukafikia sehemu ambayo tulikutawatu wamelala,
walikuwa wawwili.
Nikamzuia yule binti asiendelee kwenda mbele bali mimi
mwenye silaha.
Nikajirusha upesi na kutua karibu na watu wale
wawili.
Bunduki yangu mkononi, nikatarajia watainuka na
kufikia mikononi mwangu.
La! Hawakuinuka, nikajaribu kumtikisa mmoja, lakini
alikuwa wa baridi sana.
Maiti! Nikajisemea na nilipomgusa yule wa pili hali
ilikuwa ileile.
Nikiwa bado palepale kwa mbali kabisa nikasikia sauti
zikizungumza kwa luha ya kiingereza, kwa sababu ya
mwangwi kuwa mkubwa sikuweza kusikia jambo lolote
lakini mara nikawa nasikia neno Tanzania likirudiwa
mara kwa mara, nikatega sikio nisikie walau nini
kinajiri Tanzania lakini mwangwi uliniathiri na ninakiri
kuwa si mwangwi pekee uliokuwa kikwazo hata lugha
ya kiingereza kwangu haikuwa nyepesi hasaha mtu
akizungumza upesiupesi.
Hapa nikabaki katika mkanganyiko wa aina yake!
Mara baada ya mazunguzo yale kengele ikagongwa
kwa nguvu sana, na hapo nikaona taa zikianza
kuwashwa.
Nikakimbia upesi sana na kumfikia yule dada
niliyemuacha nyuma.
Nikamshika na kumlaza chini, jirani kabisa na zile
maiti!!
“Usikubali kutikisika… usitikisike hata kidogo
watatuua….” Nilimsihi huku nikikiri mbele yake kuwa
tuna asilimia tano tu za kutoka hai ndani ya chimbo lile
na tuna asilimia 95 za kupoteza maisha.
Kengele ikapigwa tena!! Sasa kila sehemu mwanga
ulitanda……
Yule binti akajikojolea, nikamwonea huruma kuliko
nilivyokuwa najionea mimi.
Kuja kushtuka nami mkono ulikuwa umepenya, kitu
ambacho sina uhakika ni nani alikuwa wa kwanza
kujikojolea kati yangu na yule binti!
ukinitumia hela ya bando utakuwa umenisaidia pia ahaaa ahaaaHahahahahahah hakika hii story ni kaleeee balaaaa Safiii mzaramooo yani mfano ukaishia hapo na ukatoaa kitabu chenye mwisho wake itabidi ninunue maana hakuna namnaa tenaaa eeehh
Tunasubiri next episode kakatuko pamoja mkuu