Riwaya: Pumbazo

mzaramo

JF-Expert Member
Sep 4, 2006
6,371
5,183
NA: George Iron Mosenya

SEHEMU YA KWANZA

ILIKUWA yapata majira ya saa tatu na dakika zipatazo
kumi na mbili kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi.
Nilikuwa nimegida chupa za pombe zipatazo tatu na
hapo nilikuwa nikikisikia kichwa changu walau kwa
kiasi fulani kikiwa kimechangamka na ule mzigo wa
mawazo ukiwa umepungua.
Ilikuwa ni kawaida yangu kila ninapotingwa sana na
kazi ofisini basi hata kabla sijafika nyumbani ilikuwa ni
kanuni moja lazima nipite baa kwa ajili ya kujiweka
sawa. Si kwamba nilikuwa nikiiamini sana pombe la!
Ulikuwa utaratibu tu....
Wahudumu wa pale walikuwa hawanichangamkii sana
kwa sababu sikuwa aina ya yule mwanaume ambaye
wao walitaka niwe, mwanaume wa kuwatongoza ama
kama sitawatongoza basi niwe nawapa ofa ya kunywa
bia walau moja moja. Au kama sifanyi yote hayo basi
walau niwabughudhi kwa kuwashika maziwa na makalio
yao ambayo yamenona.
Mimi sikuwa na ukaribu huo kwao hivyo hata katika
meza yangu sikuwa nimezungukwa na wahudumu,
nilikuwa nipo peke yangu. Na wala sikutarajia mgeni
yoyote yule katika meza yangu……
Nikiwa katika kuianza chupa ya nne mara nikasikia
sauti ya kike ikisema nyuma yangu, ilikuwa ikiniomba
kuwa kama sitajali basi aketi pamoja nami.
Huyu hanijui vizuri! Niliwaza kimyakimya
Nikaitazama chupa yangu, na nilikuwa najikubali sana
linapokuja suala la kunywa bia upesi. Nikaona si tatizo
akiketi kwa sababu baada ya dakika tano ama sita
hatakuwa na mimi tena bali yeye na chupa tupu
nitakazoziacha pale.
Nikamkaribisha akaketi!
Akanisalimia nami nikamjibu huku nikipata muda wa
kumtazama uso wake uliojawa na simanzi.
Sikujali lolote na wala sikumuuliza…..
Nikaendelea kugida pombe yangu hadi ilipokaribia
kuisha… yeye alikuwa ana pombe yake lakini hakuwa
ameinywa hata kidogo, alikuwa amejiinamia tu muda
wote.
Anazuga! Nikajisemea huku nikichekea mbavuni
Nikazungusha macho yangu kiwiziwizi na kugundua
kuwa licha ya kuinama binti yule alikuwa katika kilio.
Nikatamani kumuuliza lakini nikajizuia kwa sababu
kwa kitendo cha kumuuliza basi sikuwa na namna
nyingine zaidi ya kuyasubiri majibu yake.
Nikaitazama saa yangu ya mkononi tena, muda
ulikuwa unakimbia haswa. Nikamkumbuka mama Jose.
Huyu alikuwa ni mke wangu, kati ya wanawake wote
niliowahi kukutana nao kabla sijaoa hadi kuja
kukutana na mama Jose na kuzaa naye mtoto mmoja.
Sikuwahi hata siku moja kushuhudia siku ambayo
mwanamama huyu alinizoea na kupunguza wivu.
Alikuwa na wivu mkali sana.
Ili kuepusha shari nikaona kuwa ni heri niende
nyumbani. Nikamuita muhudumu na kumuulizia juu ya
baki yangu katika ile pesa niliyokuwa nimempatia.
Muhudumu yule akauvuta mdomo wake kwa ghadhabu
huku akionekana waziwazi kutawaliwa na chuki…
Labda alitaka niisahau ile pesa ili iwe baraka kwake.
Lakini ubaya mimi sikuwa mtu wa kusahau!!
Baada ya kupewa baki yangu, nikasimama niweze
kuondoka. Nikamuaga yule dada ambaye muda wote
alikuwa ameinama akilia kwa uchungu.
Hakunijibu badala yake alinyanyua uso wake na
kunitazama.
Uso wake ulikuwa umevimba bila shaka ni kwa sababu
ya kulia kwa muda mrefu, nilimtazama kwa uchache
lakini nilimwona kama mtu aliyetingwa na jambo
kubwa sana ambalo halipoozeki kwa kunywa bia za idadi
yoyote ile.
Kuna mguso niliupata lakini hapohapo nikamkumbuka
tena mama Jose. Nikaamua kuondoka.
Nyumbani hapakuwa mbali sana, ni kama mita mia tatu
na nukta kadhaa hivyo nilitembea kwa miguu.
Nilifika getini na kuanza kubisha hodi lakini hakuna
aliyekuja kufungua.
Nikabisha tena hodi bado mlango haukufunguliwa,
nikatoa simu yangu ili niweze kumpigia mama Jose
lakini nikakumbuka kuwa sikuwa na salio la kuweza
kupiga simu.
Ni nini kimemlaza fofofo hivyo mama Jose……
Nikatambua kuwa sina namna nyingine zaidi ya
kufanya zaidi ya kurejea nilipotoka ninunue muda wa
maongezi na kisha kuwasiliana na mama Jose
anifungulie geti.
Moyoni nilikuwa nimeghadhabika huku nikijiapiza kuwa
kama mama Jose ameacha kunifungulia geti kwa
sababu ya hasira zake za kipuuzi basi kwa mara ya
kwanza ataijuwa ladha ya kupigwa na mumewe.
Wakati natafakari namna ambavyo nitamnyoosha
mama Jose mara nikashtushwa na sauti ya kilio kwa
mbali, bila shaka kilikuwa ni kilio cha mwanamke na
alikuwa katika kuomba msaada.
Nikasikiliza kwa sekunde kadhaa ile sauti ikasikika
tena….
Nikaipuuzia lakini nikakumbuka kuwa kabla sijawa na
kazi yangu hii ya sasa iliyokuwa ikinipa msongo wa
mawazo kila kukicha niliwahi kulitumikia jeshi la polisi.
Nikajisikia kuguswa sana na kilio kile lakini hapohapo
nikihofia usalama wangu kwa sababu sikuwa polisi
tena.
Nikapuuzia na kuendelea mbele kurejea kule baa
ambapo kuna duka linalochelewa sana kufungwa. Hapo
ningeweza kununua muda wa maongezi na kuwasiliana
na mke wangu.
Wakati naendelea kupiga hatua mara nikasikia
vishindo. Nikasita na kutulia tuli huku uoga nao
ukiniingia kwa sababu sikuwa na silaha yoyote pale.
Ghafla mbele yangu akatokea mwanamke akiwa yu
uchi wa mnyama, akaanza kukimbilia kuja upande
niliokuwa hapa sasa nikataka kutimua mbio lakini
nikajikaza. Akafika na kutaka kunikumbatia….
Nikapiga hatua kadhaa nyuma akaanguka chini huku
akinililia kuwa nimsaidie.
Alipomaliza kunisihi vile hapohapo wakatokea wanaume
wawili waliokuwa wanamkimbiza, hawakuonekana
kuwa na silaha.
Wakasimama wakinitazama, wakaniambia niwaachie
yule binti kwani ni dada yao anafanya umalaya
wanataka kumrudisha nyumbani.
“Kaka usiwasikilize hao mimi sio dada yao… siwajui
wanataka kuniua wanataka kuniua..” Alinisihi kwa
sauti ya chini huku akiwa bado anahema juu juu.
“Mjomba eeh!Hili jambo halikuhusu tafadhali usinunue
kesi usiyoijua haumjui huyo dada wala sisi hautujui…
ila sisi kwa sisi tunajuana huyo ni dada yetu
tunamuomba…..” sasa alizungumza mmoja aliyekuwa
mrefu huku akinisogelea.
Hadi wakati huo sikuwa na uhakika kama nahitaji
kumsaidia yule dada ama la.
“Kaka… nimekaa meza moja na wewe baa… sikuwa
nafanya umalaya pale usiwaamini nakuomba
wataniua….” Alizungumza tena kwa sauti ileile. Hapa
sasa akanifanya nimtupie jicho mara moja na
kugundua ni mwanadada yuleyule tuliyeketi naye pale
baa….
Hapa sasa nikahisi anahitaji msaada…..
Nikiwa sijajua nitaondoka naye vipi, tayari mtu mrefu
alinifikia na kunisukuma.
Pombe ilikuwa imenilegeza kidogo nikayumba lakini
sikuanguka.
Nikamtazama bwana yule na kutambua kuwa mwili
wake ni wa hovyo tu, mwili mkubwa lakini hana mbinu
ambazo mimi nimepitia nikiwa jeshini.
Hapohapo nikaamua kukumbushia enzi nikafyatuka
teke moja kali likamkumba katika mbavu zake
akatokwa na mayowe makubwa.
Sikumpa nafasi ya kufikiria nikaokota jiwe na
kumrushia yule aliyekuwa anakuja kutoa msaada
likampata barabara kifuani.
Nafsini nilikuwa namlaumu sana mama Jose kwa
kuacha kunifungulia mlango maana nilijiuliza ikiwa
kweli wale ni kaka wa dada yule ni kesi gani hiyo
nilikuwa nimeinunua…..
Licha ya hayo sikuacha kupambana… nikamfyatua
tena yule mtu mrefu teke la ubavu wa pili.
Kisha upesi nikatoa kitambulisho changu cha kupigia
kura kisha nikawatetemesha kwa kuwaonyesha kile
kitambulisho ambacho niliamini kabisa kuwa
hawatapata ujasiri wa kunilazimisha wakisome.
Nikajitambulisha kama mwanajeshi na kuwasihi
waondoke pale mara moja kabla hawajalala pabaya.
Wakatimua mbio bila kusema neno lolote lile
wakamwacha yule dada akiwa yu uchi wa mnyama
mbele yangu.
“A….A….sa….nte…” maneno haya yakamtoka
yakiwa ya mwisho kabisa kabla hajapoteza fahamu
zake.
Hapa sasa nikajikuta katika kuchanganyikiwa.
Nitafanya nini na mwili wa mwanamke aliye uchi wa
mnyama halafu hana fahamu zake na usiku ulikuwa
umeenda.
Ilikuwa tayari saa tano kasoro dakika chache sana.
“Ramadhani mimi nimejinunulia kesi mbaya kabisa
hapa….” Nilijisemea huku nikiwa sijapitisha maamuzi
ya aina yoyote ile……
 
SEHEMU YA PILI

Mbeya,Tanzania

Nilibaki katika sintofahamu katika giza lile lisilotisha
sana lakini lilibaki kuwa giza lililomaanisha ule ulikuwa
usiku.
Nikawa najiuliza ni maamuzi yapi sahihi natakiwa
kuyachukua.
Nikafikiria kumwacha pale yule binti aliye uchi wa
mnyama nami niondoke zangu kwa sababu hata jina
lake tu nilikuwa silifahamu.
Nikamtazama jinsi uso wake ulivyotazamika bada ya
kupoteza fahamu, alinihitaji haswa kwa wakati ule.
Nikajiuliza ni vita kubwa kiasi gani nitaiibua nikisema
nimbebe binti yule eti niende naye nyumbani kwa mama
Jose mke wangu kisha nimueleze eti yule mwanamke
asiyekuwa na mavazi nimemuokota huko na sasa
nimekuja kumuhifadhi.
Walah! Mama Jose aidha angejiua ama la kesho yake
angefungasha virago vyake na kuondoka.
Kuhusu hili la kumpeleka binti yule nyumbani nikalifuta
kabisa katika kichwa changu.
Nikiwa bado katika kufikiria mara binti yule
akachezesha mguu kisha akafumbua macho…..
Baada ya muda mchache alikuwa wima akijaribu
kujificha kwa sababu alikuwa yu uchi wa mnyama.
Nikavua shati langu upesi na kumpatia akajifunga
kiunoni halafu nikavua na fulana yangu ya ndani
nikampatia akajistiri juu.
Nikaongozana naye huku nikimuuliza ni wapi nyumbani
kwao ili nimpeleke, akakataa katakata akasema ni
kweli ana kwao lakini hawezi kwenda kwa usiku ule na
kwa siku inayofuata pia hataweza kwenda.
Nilitamani sana kumuuliza nini tatizo hadi ashindwe
kwenda nyumbani kwao lakini nikaona huo haukuwa
wakati muafaka.
“Nisikilize binti, chukua hii pesa nenda ukalale nyumba
ile pale ya kulala wageni. Lipia siku mbili…. Huo ndo
msaada wangu pekee kwa sasa, nimeoa na ninajua
wakati huu mke wangu atakuwa ana mashaka
makubwa sana, sijawahi kuchelewa kurudi nyumbani
kwa kuchelewa kiasi hiki…..” nilimsihi huku
nikimkabidhi kiasi kile cha pesa.
Alizipokea huku akinishukuru sana kwa kumwepusha na
balaa lile la kubakwa na wale vijana wabaya.
Sikutaka kurefusha maongezi zaidi nikaondoka katika
uelekeo wa kuelekea nyumbani kwangu, tayari nikiwa
nimesahau kuwa kilichokuwa kinanipeleka kule
nilipokutana na yule binti ni safari ya kwenda kununua
muda wa maongezi niweze kumpigia mama Jose.
Nikaitazama saa yangu, muda ulikuwa umeenda haswa
nadhani hata lile duka nililojiaminisha kuwa lilikuwa
linachelewa sana kufungwa lingekuwa limefungwa
tayari.
Nikaamua kuelekea nyumbani kwangu nikiwa kifua
wazi.
Nilitembea upesiupesi huku uoga ukiniingia, niliwahofia
wale wanaume huenda wameenda kukusanya wenzao
na kisha kunivizia wanifanyie lolote la kunidhuru.
Baada ya kuitazama saa yangu niliificha simu katika
pensi yangu niliyokuwa nimeivaa kwa ndani.
Sasa nilitembea upesiupesi sana huku kila mara
nikigeuka nyuma…. Hadi nilipofika mlangoni kwangu.
Safari hii niligonga mara moja tu nikazisikia hatua
zikisogea kuja mlangoni, sikuhitaji kufanya uhakiki
nilishatambua kuwa zilikuwa hatua za mama Jose.
Aliuliza nikajitambulisha, akanifungulia mlango.
Nikataka kuingia mara akajitanda mlangoni ili nisipite
bila hiari yake.
“Mbona umechelewa sana kurudi?Mbona upo kifua
wazi?Mbona unahema juu juu mume wangu?”aliniuliza
maswali mfululizo.
Nikamsihi twende ndani, akanishika mkono tukaelekea
ndani wakati huo nikijipanga nini cha kumweleza ili
anielewe vizuri pasi na kutia mashaka yoyote yale.
Tulifika sebuleni, nikataka kuyumbisha maneno
nikajikumbusha kuwa gharama ya kuutunza uongo ni
kubwa sana.
Nikamfikiria mke wangu alivyokuwa mtu wa kukuza
mambo, jambo dogo kulifanya kuwa kubwa kupita
maelezo. Nikajipangia majibu ambayo anaweza
kuyatoa, jibu la kwanza atakalotoa kwa maelezo
yangu ni kwamba nimefumaniwa na mwanamke
nimekimbia kutoka nyumba ya kulala wageni ndo maana
sina shati.
Jibu la pili ambalo angefikiria ni kwamba nilikuwa na
Malaya ama changudoa ambaye tulielewana bei lakini
sikumpa sawa na alichohitaji hivyo tumeishia katika
mgogoro mkubwa na akaamua kubaki na shati langu
kama fidia.
Kwa mantiki ile nikapima katika mzani na kuona ni heri
uongo utakaomuacha salama mke wangu huku nami
nikiwa na amani kuliko ukweli ambao utazua mengi
mabaya yanayokera.
Nikamweleza mke wangu kuwa nilikabwa na vibaka,
nikatumia uzoefu wangu wa jeshi kuwatoroka.
Mama Jose akanipa pole lukuki huku akinipooza.
Akaniandalia maji bafuni nikaoga kisha tukala pamoja
chakula.
Usiku huo ukapita.
Japokuwa nilikuwa nimechoka sikuwa mvivu katika
kuamka, niliamka kwa wakati nikafanya mazoezi ya
kukimbia kama ilivyokuwa kawaida yangu.
Niliporejea ndani nilitarajia kukuta mke wangu
ameniwekea maji bafuni, kwa sababu hayo ndiyo
yalikuwa maisha yetu ya kila siku nikimaliza kufanya
mazoezi.
Ajabu haikuwa vile nikamkuta ameketi sebuleni akiwa
yu katika utulivu wa hali ya juu sana katika maungo
yake yote kasoro mdomo wake tu.
Mama Jose alikuwa amenuna na alikuwa ameuvuta
mdomo wake kwa kiasi kikubwa!
Balaa! Nikajisemea, lakini nikajifanya kama
sijaitambua hali ile ya mabadiliko ya ghafla kwa mke
wangu.
Nikataka kumpita niendelee na utaratibu mwingine.
Mama Jose akaninyooshea mkono huku akinipatia simu
yake ya mkononi.
“Ongea na Malaya wako.” Aliniambia.
Nikajisikia mapigo yangu ya moyo yakipiga kwa nguvu
haswa, ndugu msikilizaji ni heri niwe wazi kuwa
japokuwa nilikuwa nimemuoa mama Jose ndoa ya
bomani na nilikuwa napendana naye haswa lakini kuna
masalia kadhaa bado yalikuwa yameniganda.
Nikajiuliza atakuwa ni nani huyu aliyeisaka namba ya
mke wangu na kumpigia simu.
“Malaya wangu….aah! Malaya wa nani?... hiyo simu
nani kapiga….” Nilihoji huku nikiingiwa na kigugumizi
kikali.
Mama Jose akanikata jicho la chuki, nikajikuta
naipokea simu ile.
Kutazama sio kwamba kuna mtu alinipigia simu bali
kuna ujumbe ulikuwa umetumwa.
Nikausoma kwa makini kabisa.
“SIJUI HATA NISEME NINI LAKINI ASANTE SANA KWA
SIKU YA JANA, NIPO GESTI ILEILE ULIYONIACHA.SII
KUMBUKI HATA SURA YAKO LAKINI NINAPOTAZAMA
SHATI LAKO NI KAMA NAKUONA. NIMETAMANI
KUKUPIGIA SIMU LAKINI NIMEHOFIA KUWALETEA
USUMBUFU USIKU HUU…. SIMU HII SIO YANGU
NIMEAZIMA NITOE SHUKRANI.”
Niliingiwa na ubaridi baada ya kuusoma ujumbe ule,
kwa maana halisi kabisa iliyotokea jana ulikuwa
ujumbe safi kabisa kutoka kwa mwanadada
anayetambua mana ya fadhila. Lakini kwa mazingira
yale ya ujumbe kutumwa katika simu ya mke wangu
nay eye kuwa wa kwanza kuusoma ilihali jana yake
nilimwongopea kuwa nilikabwaa, hapo ndipo utata
ulipoanzia.
Nilijikuta najutia ule uongo wangu wa siku iliyopita,
laity kama ningeusema ukweli nadhani ujumbe huu
ungezidi kuiimarisha kweli yangu.
Ubaya ni kwamba neno ninge huja wakati ule wa
majuto.
“Rama….. yaani Rama…. Rama umempa mwanamke
mwingine namba yangu ili aniumize hivi… Rama!!”
Mama Jose alianza kulalamika huku akitetemeka sana
na sekunde hiyohiyo akaanza kutokwa machozi.
Na kama ilivyokuwa kawaida yake akaanza kulalamika
huku akikumbushia ni jinsi gani wazazi na ndugu zake
walimtenga kwa sababu ya kuolewa na mtu asiyekuwa
wa dini yake, japokuwa hakuna aliyebadili imani yake
lakini hata ndugu zangu mimi hawakuridhika.
Lakini ile nguvu ya mapenzi nikamuoa Aneti ndoa ya
bomani tukapata mtoto wa kwanza tukamuita Jose.
Na sasa Aneti anaitwa mama Jose.
Mama Jose aliugulia pale kilio cha kwikwi na kila
alipojaribu kuzungumza alikuwa akiishia kulia kwa
sauti ya juu… niliumia sana kumtazama katika hali ile
lakini nilimtambua vyema pale asingeweza kunisikiliza
vyema.
Nikaketi katika kochi nikaanza kujipanga namna ya
kumtuliza.
Lakini kabla akili aijapata mbinu za kumtuliza mara
nikashambuliwa ghafla nawazo.
“Namba ya simu ya mke wangu yule binti ameitoa
wapi?”
Nikasimama wima mdomo wazi mikono kiunoni.
Nikajikuta katika pumbaziko la namna yake!!
Nikatambua kuwa sio mke wangu tu aliyekuwa katika
matatizo hata mimi nilikuwa katika tatizo jipya la
kutafuta jawabu.
 
SEHEMU YA TATU

KUKAA kimya wakati mke wangu analia juu yangu
ilikuwa kuhalalisha hisia zake kuwa ni kweli mimi
nimempatia mtu namba yake kwa ajili ya kumuumiza
jambo ambalo si kweli kabisa.
Nikajikaza kisabuni hatimaye nikazungumza.
“Aneth mke wangu…..nisikilize.sikiliza sasa nikueleze
ukweli ulivyo na ninaomba unisamehe sana kwa sababu
jana nilikuongopea. Sikujua kama yatakuwa makubwa
kiasi hiki…” nilianzia pale na sikumpa nafasi ya
kuzungunmza nikaelezea tukio lote lilivyokuwa kwa
msisitizo mkubwa sana.
Lakini mke wangu alinitazama kwa jicho la dharau
iliyochanganyika na chuki. Ni kama hakuelewa wala
kuamini nilichokuwa namueleza.
“Yaani wanaume… sijui mkoje yaani….eti alikuwa
uchi wa mnyama ukampa shati lako. Rama nenda
ukawadanganye mahawara zako huko sio
mimi….kumbuka nimekuzalia mtoto Rama. Nimekataa
kuwasikiliza wazazi wangu Rama...” Alinijibu mama
Jose kwa malalamiko.
Sikuwa tayari kuona ndoa yangu ikiharibika mapema
kiasi hiki, najua hili lingekuwa doa kubwa sana…. Kwa
upande wangu baba aliyesema kuwa nimerukwa akili
yaani sijaona wasichana warembo wa dini yangu
nikamrukia Aneti, sasa angethibitisha kuwa kweli
nilikuwa nimerukwa akili iwapo tungeachana. Kwa
upande wa Aneti ingekuwa hali ngumu zaidi kwa
sababu kwao walikuwa wamemtenga, sasa chuki
ingezidi na wangemsimanga.
Ya nini ayapate haya mtoto wa watu?
Nilijiuliza na kuona kuwa bado ninayo nafasi.
“Mama Jose nakuomba simama…. Twende wote, shika
simu zangu sipigi simu wala sifanyi kitu chochote
naomba twende alipo huyo mwanamke mwenye nguo
zangu…. Mama Jose simjui hata jina huyo dada…
simjui na utakuwa shahidi… nilimsaidia tu.” Nilimsihi
sasa mama Jose, lakini akakataa katakata akasema
hayupo tayari kudhalilika mbele ya kadamnasi pale yule
mwanamke wangu atakapoanza kumtukana na
kumrushia makonde.
Maneno yale ya mke wangu yaliniumiza sana, na laiti
kama ningesema niende peke yangu basi ningemwacha
katika maumivu makali sana.
Hapo sasa nikalazimika kutumia amri, nikavaa fulana
yangu bila hata kuoga. Nikamwambia mama Jose kuwa
tunaenda kwa yule mwanamke ikiwa ni amri na si ombi.
Akatii amri japo kishingo upande!
Akajitanda upande wa kanga kustiri nywele zake,
tukaondoka.
Kimya kilitanda njia nzima hakuna aliyemsemesha
mwenzake. Hatua kwa hatua mimi nikiwa kiongozi hadi
tukaifikia ile nyumba ya kulala wageni niliyomuelekeza
aingie kulala pale.
Wakati tunataka kuingia niliwaona kwa mbali vijana
watatu, mmoja kati yao sura yake haikuwa ngeni hata
kidogo.
Nikamsemesha mke wangu kwa mara ya kwanza,
nikimwambia kuwa wale vijana mmojawapo
namfananisha kama wale waliotaka kumbaka binti yule
usiku.
Mke wangu akanitazama kisha akatikisa kichwa kwa
masikitiko ni kama alikuwa akiona namlaghai
waziwazi.
Hali hiyo iliniumiza sana, ila sikuwa na la kufanya ili
kumuaminisha.
Tukaingia ndani ya ile nyumba ya kulala wageni, hapo
sasa ikawa mshikemshike nitauliza jina gani na
muhudumu anielewe, maana wenye nyumba hizi kwa
kutunza siri hawajambo. Mwanao wa kike anaweza
akahifadhiwa na bwana ndani ya nyumba zao kwa siku
tatu mfululizo, wanajua wazi ni mwanao lakini
hawasemi kitu.
Wana roho ngumu! Nilijisemea.
Lakini sikuwalau maana kasheshe la fumanizi nilikuwa
nalijua waziwazi, mafumanizi husababisha vurugu na
kisha uharibifu wa mali.
Tulienda hadi mapokezi nikiwa bega kwa bega na mke
wangu, nikajitambulisha pale mapokezi na kisha
kumtambulisha mke wangu.
Na hapo nikaelezea juu ya ujio wa mwanadada
aliyejifunga shati na kuvaa fulana nyeupe usiku
uliokwishapita.
Ili kumfanya yule bwana aamini zaidi nikamweleza
kuwa yule dada nilimpatia pesa mimi alipie siku mbili.
Hapo akatikisa kichwa kukubaliana na nilichosema.
Lakini hakuniruhusu kwenda kumwona badala yake
akaniuliza ikiwa kuna mtu mwingine ambaye alitakiwa
kuonana na yule dada tofauti na mimi.
Hapo sikuwa na jibu, nikamweleza bayana kuwa yule
dada hata jina simjui bali nilimsaidia tu na
hatujawasiliana hadi alipotuma ujumbe kwa mke
wangu.
Nikamweleza yule muhudumu juu ya tatizo lililozuka na
nimekuja hapo na mke wangu ili tu aamini kuwa mimi
huyo binti simfahamu kabisa balini msaada tu ambao
umenitokea puani mimi.
Maneno yangu yalimuingia lakini alikuwa anashindwa
kusema jambo fulani ambalo sikulijua hata.
Baada ya muda akatueleza kuwa anaenda kumuuliza
iwapo yupo tayari ili waingie.
“Aah! Nimwambie nani amekuja?” aliniuliza.Nika
mwambia amweleze kuwa yule kaka aliyemsaidia usiku.
Yule bwana akaondoka zake akituacha pale na mke
wangu.
Kwa jicho la kuibiaibia nikamwona mke wangu kidogo
akianza kupata tumaini jipya kuwa nilichomwambia ni
kweli tupu. Lakini hakuwa na imani ya asilimia mia.
Baada ya muda yule muhudumu alirejea, alikuwa
mwenye mashaka kidogo.
Akatueleza kuwa anajaribu kugonga kile chumba na
hakuna majibu lakini ndani kuna mtu. Hapo sasa
akatueleza kuwa kuna mwanaume amekuja hapa
akidai yeye ni mume wa yule binti na wana miadi ya
kuonana, hivyo aliingia ndani na kutoka baada ya muda
mchache akidai kuwa anaenda dukani kununua
kinga.Tangu hapo hakurudi tena.
Muhudumu akashauri twende kuufungua mlango kwa
kutumia funguo za ziada yumkini kuna tatizo.
Hapa sasa badala ya kuvuta mdomo, niliiona hofu
machoni mwa mke wangu. Labda alihisi ninamzuga ama
aliwaza lolote alilowaza la kumletea mashaka.
Muhudumu akatuongoza hadi katika kile chumba.
Tukajihakikishia wenyewe kwa kugonga kile chumba….
Kweli hapakuwa na majibu kabisa. Zaidi ya kusikia
miguno ya kimahaba chumba cha jirani mwanamke
akilalamika hapakuwa na sauti nyingine iliyojibu!
Hapo sasa muhudumu akaingiza funguo wa ziada na
kuufungua mlango.
Lahaula!
Kitandani hapakuwa na mtu bali mashuka tupu….
Tukaangaza huku na kule na hapo muhudumu akabaini
kuwa kuna mtu alitoka kwa njia ya dirishani.
Kwanini apitie dirishani wakati alikuwa hadaiwi
chochote?
“Rama usitake kunichezea Rama, kama umenichoka
Rama naomba uniache hata bila talaka hiki
unachonionyesha ni talaka tosha.” Gatimaye mama
Jose alizungumza kwa uchungu huku midomo yake
ikitetema kwa hasira.
Muhudumu upesi akakagua mali zake, alikagua hadi
kipande cha sabuni kilichokuwa bafuni.
Vyote vilikuwepo hakuna kitu kilichoondolewa.
Watu bwana! Yaani anajali mali zake kuliko usalama
wa mteja mwenyewe.
“Mh! Labda ameondoka na kandambili maana aliingia
bila viatu..” muhudumu akajisemea huku akiinama
uvunguni mwa kitanda kutazama iwapo kandambili zipo
ama la.
Alipoinama uvunguni, ghafla akaruka na kujibamiza
ukutani.
Mke wangu akatokwa na yowe kubwa la uoga huku
akinikumbatia….hii ni baada ya Yule muhudumu
kumbabatiza aliporuka.
Macho yalikuwa yamemtoka pima muhudumu. Alizidi
kujibanza ukutani huku akitetemeka sana.
Alitaka kusema neno lakini aliishia kuunguruma tu na
kupepesa macho.
Hapo sasa niliingiwa na hofu pia.
Nikaamua kwa ujasiri na mimi niiname nione
alichokiona muhudumu hadi kujikuta katika hali ile.
 
SEHEMU YA 4

Mbeya,Tanzania

HAIKUWA mara yangu ya kwanza kuona tukio ama lile
wakati nilipokuwa kazini kabla ya kuamua rasmi
kuyavua magwanda na kuendelea na maisha nikiwa
kama raia wa kawaida.
Lakini kwa wakati ule sikuwa natishika sana kwa
sababu nilikuwa kazini...
Sasa sipo kazini!
Nilishuhudia mwili ukiwa umekunjwa katika namna
ambayo mwanadamu wa kawaida ukikunjwa basi tamati
yake ni mauti hata pasipo kuhesabu dakika tano.
Shingo yake iligeukia mgongoni huku miguu ikiwa
imevunjwa!
Hivyo hata kwa kiumbe kile mvunguni mwa kitanda
hapakuwa na haja ya kuusaka ushahidi wa kitabibu
kuthibitisha kuwa mwili ule hauna uhai pale ulipo.
MSIMULIZI ANASIMULIA
Hili la kukosa uhai kiwiliwili kile hakukumwogopesha
sana Rama. Kilichomwogopesha zaidi ni kwamba
aliyeuwawa ni yule mwanadada ambaye usiku uliopita
tu alitoka kumsaidia kwa kumpigania asibakwe na
kisha kumpatia pesa ambazo zingemtosha kabisa kulala
pale kwa siku mbili kabla hajaamua ni wapi aelekee.
Wivu wa mama Jose ulikuwa umetimka mbio na nafasi
yake kuchukuliwa na na hofu kuu!
Hofu ya kuishi chumba kimoja na maiti.
Rama alijua hila za maafisa wa polisi, ikiwa
watakutwa eneo lile basi watakamatwa kwa ajili ya
kulisaidia jeshi la polisi upelelezi......
Upelelezi kwa kesi ya mauaji, ungeweza hata
kuwagharimu mwezi mzima bila kuipata dhamana!
Rama akakikamata kiganja cha mkono cha mkewe na
kisha akamvuta watoke nje... wakimwacha muhudumu
akihaha kupiga simu popote alipojua!!
****
Rama na mkewe wakiwa wanashindana kutembea kwa
kasi kubwa walielekea hadi lilipokuwa gari la abiria
lililoelekea walipohitaji wao, mama Jose akapanda wa
kwanza akifuatiwa na mumewe.
Ikawa bahati mbaya hawakuketi siti moja.
Hata hivyo hakuna aliyejishughulisha na hilo.
Safari ikaanza kwa ukimya wa hali ya juu kati ya
wawili hawa.....
Baada ya vituo viwili gari lilisimama na abiria wengine
wakapanda, hawa wa sasa hawakupata nafasi za
kukaa.
Mama Jose alikuwa amejiinamia muda wote akiombea
gari lifike waendapo amsikilize mumewe ataamua nini
juu ya hili.
Sasa hakukumbuka kuwa wakati akiwa na wivu
hakutaka hata kidogo kumwamini mumewe lakini sasa
anahitaji kumwamini na kumtegemea kwa asilimia
zote!!
Wanawake bwana!
Mama Jose kila alipoyafumba macho yake aliiona
taswira ya kiumbe kile kilichonyongwa katika mtindo
wa kutisha sana hadi kilipopoteaza maisha. Hali hii
ikamfanya asitamani kufumba macho yake bali
kuyaacha wazi kila muda.
Baada ya kuinama kwa muda mrefu, gari lilisimama
tena kituo kingine, akaisikia sauti ya kondakta
ikiamrisha abiria mwenye mtoto akalie siti ambayo
kuna abiria mmoja alitakiwa kushuka.
Kweli gari liliposimama akashuka abiria akiacha pengo
katika nafasi aliyokuwa amekaa Mama Jose.
Abiria wakampisha mama mtoto huyo akajibanabana
hadi akafika eneo aliloachiwa wazi akaketi,
akamsabahi mama Jose.
Mama Jose akajibu huku akiwa bado ameinama......
Mawazo yake hayakuwa hapo kabisa!!!
Gari lilipoanza kuondoka yule mama mtoto akamuomba
mama Jose amshikie mtoto ili aweze kutoa nauli
kabisa...... hapa sasa mama Jose aligeuka kumtazama
yule abiria na hapa ndipo kilipozuka kizaazaa!!
*****
RAMA ANASIMULIA
Licha ya kujifanya kuwa sijatetemeshwa na tukio
lililotokea lakini hakika nilikuwa katika hofu kuu, ila
sikutaka mama Jose atambue kabisa kuwa nimeogopa.
Niliingia garini na kuketi huku nikishukuru kuwa
sikukaa siti moja na mke wangu, nilimjua vyema mama
J. Hana subira yule hata kidogo....
Angeanza kuniuliza maswali kedekede palepale garini
na kunilazimisha nimjibu kama anavyotaka yeye,
sikutaka jambo hilo litokee.
Kweli hatukukaa siti moja!
Nikiwa katika siti yangu, nilikuwa namuona vyema
mama Jose. Nilimwona alivyokuwa akiumizwa na
mawazo, alikuwa amejiinamia muda wote wa safari
ile.... niliamini kuwa kuna haja ya kulisawazisha
jambo hili mapema sana.
Nikafikiria pia juu ya ile maiti katika nyumba ile ya
kulala wageni, nilijiuliza ni kitu gani kimemsibu dada
yule hadi kujikuta katika dhahama ya kuuwawa kifo
cha namna ile ya kutisha.
Hakika sikupata majibu, badala yake kichwa kikaanza
kuniuma na mimi nikajiinamia kama mama Jose wangu.
Hazikupita hata dakika tano tangu niiname niliposikia
makelele makubwa sana kutoka ndani ya ile gari,
nikajikuta katika taharuki. Hapohapo nikaunyanyua
uso wangu ili nijue ni kipi kinatoke.
La! Haula.....
Alikuwa ni mama J akipiga mayowe huku akimwachia
mtoto aliyechukuliwa na mwanamke ambaye nilikuwa
namwona mgongoni pekee.
Nikajiuliza kulikoni, huenda kila abiria alijiuliza
kulikoni kama mimi.
“Baba Joseeee jiniiiiii....mzimuuuuuu!” sasa alinipigia
kelele, sekunde moja akinigeukia huku sekunde
nyingine akimtazama yule mwanamke aliyebeba
mtoto......
Kelele za mama Jose ziliwatisha sana abiria na hadi
dereva akalazimika kusimamisha gari na kuiweka
kando.
Kitendo cha mama Jose kuniita kwa sauti kuu vile, hii
ikasababisha yule mwanamke kugeuka na kutazama ni
nani hasa huyo baba Jose.
Mungu wangu!!
Nikakutanisha macho yangu ana kwa ana na sura ya
mwanamke ambaye alikuwa uvunguni mwa kitanda
akiwa amenyongwa vibaya mno hadi kupoteza uhai
wake kisha kutelekezwa palepale bila msaada wowote
hadi tulipokuja kumgundua na sisi tukaondoka
kimyakimya kuepuka kujiingiza katika mambo
yasiyotuhusu.
Mapigo yangu ya moyo yalipiga kwa nguvu sana macho
yetu yalipogongana... nilijiona nikitazamana na maiti
aliyefumbua macho ghafla wakati anasafishwa tayari
kwa kuzikwa.
Miguu ikaingiwa ganzi kali kisha nikawa natetemeka
waziwazi.
Nilikuwa nayasikia tu haya mambo ya kishirikina hapo
kabla, kwa mara ya kwanza niliyashuhudia kazini
kwangu baada ya mfungwa mmoja kupotea katika
mazingira ya kutatanisha yaliyoambatanisha nguvu za
giza na kusababisha polisi watatu waliokuwa lindo
kutupwa gerezani.
Hii ilikuwa sababu moja kuu sana iliyosababisha
nifanye harakati za kuiacha kazi ile.
Sasa ninakutana na mkasa huu wa kutisha.... yaani
dakika kadhaa nyuma niliona maiti sasa maiti hii
inanitazama.
Mkojo ukabisha hodi, nikaugomea usipenye na
kunidhalilisha!!!
Abiria wakaanza kuingiwa na mashaka sasa...na wao
wakaingiwa na PUMBAZO
Ikazuka tafarani ya aina yake isiyosemekanika!
 
SEHEMU YA TANO

MKE wangu alizidi kupiga mayowe ya hofu huku
akinisihi nimsaidie, sasa aliniita kwa majina yote
aliyoweza na baada ya kuona msaada wa upesi
haupatikaniki akaanza kumuita mama yake na Mungu
wake kwa juhudu zote.
Yule mama mwenye mtoto alistaajabu, hakuonyesha
dalili yoyote kuwa alikuwa na nia mbaya nasi.
Tatizo ni moja tu!
Inawezekana vipi maiti atokee ghafla ndani ya gari
huku akiwa na mtoto halafu moja kwa moja akaenda
kuketi pamoja na mke wangu.
“Nipisheni.... nipisheni...” nilianza kujitapa. Kisha
nikajipuuza baada ya kugundua njia ya kwenda
alipokuwa mke wangu ilikuwa wazi kabisa hapakuwa na
haja ya mtu yeyote kunipisha, wakati huo wote abiria
wengine walikuwa wameanza kuteremka garini kwa
kugombea mlango wa kutoke.
Wanawake walisikika wakilia kwa hofu huku
waklisemezana kuwa mzuka ulikuwa umevamia garini,
wanaume nao hawakusogea karibu na lile
songombingo!
Nilipiga hatua kadhaa na kumfikia yule mama mwenye
mtoto. Hapa tena tukagonganisha macho.
E walaa!
Alikuwa ni yuleyule binti tuliyeonana siku iliyopita
kisha nikamsaidia.
“Unataka nini we mwanamke?” nilimuuliza bila
kujipanga vizuri.
“Niwaulize ninyi, mnataka nini kwangu? Maana
siwaelewi asilani..” alijibu huku akionekana
kustaajabu.
Kitendo cha kunigeukia kwa sekunde kadhaa, hapohapo
mama Jose alipanda juu ya siti na kisha akaparamia
kioo kabla hajarukia dirishani na kutua nje na kisha
kilio kikuu kikasikika.
Kilio cha maumivu!
“Mna nini nyie?” aliniuliza yule mama akiwa na mtoto
wake ambaye sasa alikuwa akilia kwa juhudi sana
baada ya songombingo ile ya aina yake, watu
barabarani walikimbilia mahali ambapo bila shaka ni
Mama Jose alikuwa ametua baada ya kutokea
dirishani.
Kitendo kile kikanivuta na mimi kutoka nje kwa sababu
nilijua tayari mambo si mambo, nikampita yule
mwanamke wa ajabu na kushuka chini.
Mama Jose alikuwa ametulia tuli akiwa ameikumbatia
barabara ya lami.
Nikauchekecha umati ule hadi nikamfikia mama Jose.
“Mama Jose... we mama Jose..... Anetiii...Aneti hebu
amka...” nilimsihi lakini alibaki katika utulivu uleule.
Nikiwa nazidi kupagawa mara nikasikia sauti za
kinamama zikinipigia kelele, sikuwa nasikia
walichokuwa wanasema badala yake niligeuka na
kuona kuna mahali walikuwa wananyoosha vidole.
“Nyuma yako linakuja jiniiii...” mama mmoja alipaza
sauti zaidi.
Ebwana ee! Ile nageuka nakutana na yule mama akiwa
amebeba mtoto wake. Alikuwa anapiga hatua kujongea
nilipokuwa nimeinama.
Upesi nikasimama wima, nilijidanganya kuwa
nimesimama kiujasiri sana lakini haikuwa hivyo
nilikuwa natetemeka sana.
“Samahani kaka yangu.... samahani sana nakuomba
nizungumze nawe dakika moja tu!” alizungumza kwa
utulivu huku akionekana pia kupagawa.
“Nini? Nani? Uzungumze na nani?” niliuliza kibwege.
“Kaka yangu sijui ni nini kimetokea hadi inakuwa hivi
ilivyo.... naomba unieleze huenda kuna jambo mimi na
wewe hatulijui!” alinisihi.
Kauli zake thabiti sana na bila kupepesa macho
zilinifanya nikaanza kumuamini.
“Wewe ni nani?” nilimuuliza.
“Naitwa Nasra... Nasra binti Kombo. Mwanangu
anaitwa Nusrati... naitwa mama Nusrati.” Alinijibu
kwa kirefu... wakati huo tayari watu walikuwa
wametuzunguka.
“Jana tulikuwa wote baa... baadaye ukakabwa na
majambazi nikakufadhili nguo zangu na pesa...
umenizushia kesi kubwa sana kwa mke wangu na
asubuhi hii..... asubuhi hii dakika chache zilizopita.....
” nilishindwa kusema neon nililotaka kumalizia kwa
sababu halikuwa jambo jepesi.... kusema kuwa
nilimkuta amepoteza uhai ilikuwa ni sawa na
kujiopeleka polisi na kusaidia upelelezi wa kesi hiyo.
“Kaka yangu, si mimi niliyekuwa nawe, sinywi pombe
wala si mtembezi wa usiku nitamuacha nani na
mwanangu..... huenda umeonana na Hajrati”
“Hajrati... Hajrati ni nani?”
“Hata simfahamu...” alinijibu huku akionekana
kupagawa, jibu lake likasababisha raia waanze kupiga
kelele kumzonga kuwa ni mwongo.
“Hajrati.... Hajrati niliambiwa kuwa nilizaliwa pacha
na kisha katika mazingira ambayo siyaelewi vizuri
niliporejea kutoka Oman ambapo nilipelekwa tangu
utoto wangu sijabahatika kumuona huyo Hajrati.”
Alijibu kwa kirefu.
“Na niliambiwa kuwa tofauti kubwa kati yetu ni hiki
kidoti puani, yeye hana mimi ninacho...” alimalizia
utetezi wake huku akiwa bado mwenye hofu.
Kwa utetezi huo nilifumba macho mara moja na
kutambua kuwa ni kweli kabisa nilikuwa nazungumza
na mtu mwingine kabisa.
Bila shaka hata yeye alinisoma macho yangu na
kugundua hilo.
“Kaka umemuona wapi Hajrati, nina shida naye sana
tafadhali nakuomba unielekeze ulipomuona huyo ndugu
yangu wa pekee katika ulimwengu huu.” Alinisihi. Sasa
sikuwa na hofu kwa asilimia kubwa kama ilivyokuwa
hapo awali.
Sikuwa na cha kumjibu kwa wakati ule, bali zilifuata
hekaheka za kumsaidia mke wangu kumpandisha katika
teksi tayari kwa kumpeleka hospitali.
MSIMULIZI ANAINGIA
ILE hali ya kusikia kuwa Ramadhani na mkewe
wamewahi kwa namna moja ama nyingine kuonana na
Hajrati kilimtie kimuhemuhe Nasra, kuna kitu kikubwa
kilikuwa katika moyo wake. Hakutaka kumwacha Rama
kwa sekunde. Alivunja ratiba zilizokuwa mbele yake na
kuamua kuandamana na Rama kuelekea hospitali
ambapo mkewe alipatiwa huduma ya kwanza, alikuwa
ameteguka mguu wake hivyo walimchua kwa madawa
mbalimbali kabla hajaruhusiwa kuondoka.
Rama hakumruhusu Nasra aonane na Aneth kwanza
hadi hapo atakapokuwa ameuleza ni kitu gani
kilichokuwa kinaendelea.
Kweli baada ya Rama kumweleza ukweli mama Jose,
sasa aliweza kuonana na Nasra bila hofu kubwa.
Nasra alijiona kama mwenye donge zito haswa
kifuani, alitamani kujua juu ya jambo ambalo aliliona
kuwa ni la muhimu sana juu ya pacha wake.
Rama alishindwa kumweleza bayana kuwa Hajrati ni
maiti katika chumba kimojawapo katika nyumba za
kulala wageni. Alijizungusha na kumweleza kuwa
alikutana na binti huyo katika baa na baadaye katika
hekaheka za kumwokoa asibakwe....
“Atakuwa Vonso huyo... ni Vonso tu...” Nasra alisema
kwa uchungu.
Rama akauliza Vonso ni nani... Nasra hakujibu badala
yake alibaki kupambana na mawazo yake mwenyewe.
“Yaani inamaana haijatosha tu au?” alisema kama
anayezungumza peke yake huku akijifuta machozi kwa
kutumia kiganja cha mkono wake.
Rama alikuwa mchovu na aliyetawaliwa na mawazo
sana juu ya vitu vilivyopita ndani ya muda mfupi, hata
usikivu wake haukuwa mzuri sana kwa nasra.
Akaghairisha mazungumzo yale kwa kumpatia nambari
za simu ili waweze kuwasiliana siku iliyofuata.
Nasra akaipokea huku akiwa na majonzi ya waziwazui,
kuna kumbukumbu mbaya ilikuwa imetawala kichwa
chake.
Si yeye tu hata Rama alitawaliwa na kumbukumbu ya
kumwona pacha wa Nasra akiwa mfu. Ukweli ambao
hakutaka kumshirikisha Nasra kwa kuhofia kuzua
tafrani kubwa sana.
Wakaagana, Rama akiondoka na mkewe na Nasra naye
kivyake!
________
MAMA JOSE alilala fofofo sana, lakini Rama
hakukumbwa lau na lepe la usingizi. Alikuwa anawaza
sana juu ya kila kitu ambacho kimetokea, awali
alidhani kuwa ataweza kuikimbia kesi hii kwa
kuwakimbia polisi upesi baada ya kumshika kiganja
mkewe na kutoroka naye, lakini sasa amekutana na
pacha wa marehemu.....
“Sina ujanja hapa hii kesi inazaa na mimi wazi
wazi...” alijisemea kwa sauti ya juu kiasi iliyomfanya
mkewe ageuke na kuendelea kufurahia usingizi wake.
Akajaribu kuutafuta usingizi lakini ikawa ngumu,
akakiona kitanda kichungu. Akainuka na kuketi katika
kochi lililokuwa pale ndani.
Dakika hazikupita sana akasikia hatua zikisogea
kuelekea katika nyumba aliyokuwa anaishi. Akatega
sikio vizuri hatua zikazidi kusogea.
Hatimaye mlango wake ukagongwa....
Ilikuwa yapata saa sita usiku.....
Rama akasikilizia kwa muda kama waliogonga hodi
alikuwa anawafahamu, siko likaipokea sauti na ubongo
ukamnong’oneza Rama kuwa aliyekuwa anagonga
mlango ni bosi wake.
Usiku huu anataka nini? Alijiuliza hukua akisimama
kuujongea mlango. Jibu la k2wanza alilojiwekea ni
kwamba bosi wake amesikia juu ya majanga
yaliyompata na sasa ameona usiku usipite bila kumpa
pole.
Lakini upande wa pili aliikataa dhana ile, bosi wake
hakuwa mtu anqayejali wafanyakazi wake kiasi kile.
“Nani?” aliuliza kibabe huku akiigiza kuwa anatokea
usingizini.
“Rama eeh Martin hapa..... Martin wa ofisini.”
“Mkurugenzi nini tena usiku huu....”
“Aaah! Fungua bwana tuzungumze unataka niliwe mbu
nje bwana...” alijibu kimzaha.
Rama akaufungua mlango, mlangoni hakuwa
mkurugenzi peke yake, bali palikuwa na watu wanne,
wawili kati ya hao aliwatambua kuwa mmoja ni bosi
wake na yule wa pili alikuwa ni Nasra!
Pacha wa marehemu!
Sura yake ilijenga chuki kubwa sana na hakuwa na
dalili yoyote ya kutabasamu wala kuunda urafiki na
Rama.
“Dada unao uhakika kuwa ni huyu?” bwana mmoja
alimuuliza Nasra, Nasra akatikisa kichwa kuthibitisha
kuwa ni yeye.
“Bwana Ramadhani Said, una dakika tano za kujiandaa
tunaondoka wote kuelekea kituo cha polisi, kuna
jambo nyeti la kujadili nawe....” alizungumza yule
bwana huku akitoa kitambulisho chake na kumpatia
Rama.
Rama alipagawa!
 
SEHEMU YA 6

“Nani?” aliuliza kibabe huku akiigiza kuwa anatokea
usingizini.
“Rama eeh Martin hapa..... Martin wa ofisini.”
“Mkurugenzi nini tena usiku huu....”
“Aaah! Fungua bwana tuzungumze unataka niliwe mbu
nje bwana...” alijibu kimzaha.
Rama akaufungua mlango, mlangoni hakuwa
mkurugenzi peke yake, bali palikuwa na watu wanne,
wawili kati ya hao aliwatambua kuwa mmoja ni bosi
wake na yule wa pili alikuwa ni Nasra!
Pacha wa marehemu!
Sura yake ilijenga chuki kubwa sana na hakuwa na
dalili yoyote ya kutabasamu wala kuunda urafiki na
Rama.
“Dada unao uhakika kuwa ni huyu?” bwana mmoja
alimuuliza Nasra, Nasra akatikisa kichwa kuthibitisha
kuwa ni yeye.
“Bwana Ramadhani Said, una dakika tano za kujiandaa
tunaondoka wote kuelekea kituo cha polisi, kuna
jambo nyeti la kujadili nawe....” alizungumza yule
bwana huku akitoa kitambulisho chake na kumpatia
Rama.
Rama alipagawa!
“Dakika nne zimesalia afande!” askari mwingine
alimwambia Rama kwa sanifu.
Rama akaingia ndani na kuvaa suruali yake, kisha
akabaki katika sintofahamu.
Alimjua vyema mama Jose!
Akisikia jambo kama hilo usingizi utapaa moja kwa
moja huku akipagawa na kupiga simu kwa kila ndugu
amjuaye usiku huo.....
Rama akajiuliza kuwa itakuwaje ikiwa jambo lenyewe
litakuwa ni dogo la kumalizika usiku huohuo, Mama
Jose aende kuhangaisha watu na kuwafanya
wapagawe?
Pili, itakuwaje ikiwa mama Jose atadamka na kukuta
kitanda kikiwa cheupe na yeye Rama hayupo, huo
utakuwa mwanzo wa kumuhisi vibaya kuwa ameenda
kwa kimada.
Rama alichanganyikiwa na dakika alizopewa zilikuwa
zinayoyoma, akaamua kuchukua kalamu na karatasi
akaandika ujumbe mfupi na kuuacha pale mezani.
Kisha akatoweka na wale maaskari, mkurugenzi wake
pamoja na Nasra pacha wa marehemu.
“Yaani Rama umeichafua sana kampuni yetu.... kumbe
uzushi mtupu ulivyotoa vigezo vya kuacha uaskari nasi
tukakuamini...” mkurugenzi alikuwa wa kwanza
kuvunja ukimya huu. Wale askari wakatikisa vichwa,
Rama hakujua kama wanamsikitikia yeye ama
wanamsikitikia anayetoa kauli hizo.
“Na utanilipa kwa kuniita mimi jinni mbele za
watu....” Nasra naye akazungumza. Wale maaskari
wakatikisa vichwa tena, rama akashindwa kuelewa
wanamuunga mkono yule binti ama wanamsikitikia
yeye.
“Jamani lakini....”
“Hakuna cha lakini Rama ni heri ukaendelea kuwa
kimya kuliko kuzungumza utazua mengine...’ askari
alimkatisha kwa ghadhabu.
“Sawa lakini...” akataka tena kuzungumza, sasa
alikutana na kibao kikali shavuni. Kisha akashikwa
mikono yake hna kufungwa pingu!
Ama! Rama alikuwa amekamatika pabaya, mbaya zaidi
hakuijua sababu ya yote haya kutokea.
Gari ilisimama mbele ya kituo cha polisi, askari
wasiopungua wanne wakiwa na mitutu walikuja
kumpokea Rama huku wakimzonga huku na kule kana
kwam,ba anaweza kutoroka muda wowote ule.
Rama alikosa la kusema hadi pale alipohifadhiwa katika
chumba cha mahabusu, huku akiwa peke yake.
______

RAMA ANASIMULIA KILICHOJIRI.

SIKUTAMBUA nini maana ya tukio lile, ulikuwa ni
mfululizo wa matukio mengi ndani ya masaa machache,
mfululizo wa visa ambavyo sikuujua muunganiko wake.
Kwanza kukyrtana na mwanamke baa akiwa ameketi
na chupa yakle ya bia ikiwa imejaa na asiinywe hata
kidogo badala yake akitokwa machozi tu, pili kukutana
na mwanamke huyuhuyu akiwa anakimbia uchi huku
akidai kuwa kuna watu wanataka kumuua,
nikapambana nao na kumsaidia kisha nikampatia shati
na fulana yangu.....
Kitendo hicho sikukiweka wazi mbele ya mke wangu,
palipokucha nikaamkia katika lawama baada ya ujumbe
kutoka nyumba ile ya kulala wageni... ujumbe ule
ukazua kizaazaa na ili kutetea ndoa yangu ya bomani
nikalazimika kuondoka na mke wangu hadi katika
nyumba ile na hapo tukakutana na mwili ukiwa
umekunjwa vibaya sana na kupoteza uhai.
Nikamshika kiganja mke wangu ili kuukimbia ule
ushahidi... katika gari kama filamu vile tunakutana na
kizaazaa. Kabla siku haijaisha vizri hata usingizi
sijaupata vyema nakutana na hili la kudakwa
nyumbani kwangu na kisha kulala mahabusu!
Hakika ulikuwa mlolongo usosemekana!
Chozi likanitoka!
Nikisema nililala mahabusu nitakuwa nimekosea kwa
sababu hata sikulala, baada ya masaa kama mawili
nikafunguliwa milango na kuchukuliwa kupelekwa
katika chumba kilichotawaliwa na giza na mbu wakali
walioikosa damu ya mwanadamu kwa muda mrefu.
Nilidhani kuwa nipo peke yangu katika chumba kile
ambacho hata mbele sikuweza kuona.
Lakini mara nikasikia sauti ya mtu akijikohoza. Na
kisha akazungumza.
“Rama yu wapi Vonso.... tupatie jibu upesi ili
tukuache uende kulala na mkeo ama chelewa kujibu na
uendelee kuwapa mbu hawa faida.”
Kulisikia jina Vonso kukanikumbusha kauli ya Nasra.
Lakini hii ilikuwa mara ya pili kulisikia jina hili, hakuna
mahali nimewahi kulikiskia zaidi ya hapa na hapo kabla
kwa Nasra.
Sauti ile ilitulia kimya kabisa bila kunisisitiza kujibu.
“Simjui Vonso... sijawahi kulisikia jina hilo zaidi ya
leo aliponiambia Nasra.” Nilijibu kwa kujiamini.
“Nasra ambaye muda si mrefu ulimuua dada yake ili
asitoe siri zenu!” sauti ile ilinieleza kwa kejeli.
Hapo sasa niliusikia mwili wangu ukiingiwa ubaridi
mkali, hata yale maumivu ya kung’atwa na mbu
sikuyahisi tena.
“Sijaua na kamwe sijawahi kuua mkuu....” nilijikaza
kiujasiri ili nisionyeshe namna yoyote ya kutetereka.
Hapohapo nikasikia mjeledi ukitambaa katika mgongo
wangu. Maumivu yakasafiri katika mwili mzima na
kujikuta nikipiga magoti bila kupenda.
“Rama utamtaja tu Vonso alipo na mtalipa madhambi
yenu....” sauti ilinisihi kwa sauti ile ile iliyojaa
fedheha.
Ndugu msikilizaji hapo sikuwa najua lolote la
kufikirika wala lenye uhalisia. Nilikuwa katika
pumbazo gizani!
Ile kauli ya rama utamtaja tu Vonso hakika
ilinichanganya na nilijua maana ya kauli ile kwa jeshi
la polisi, ikifikia hatua afisa anakueleza vile maana
yake yupo tayari kutumia njia zozote zile ilimradi tu
useme kile ulichokificha katika moyo wako.
Nilijua vyema kwa sababu hata mimi nilifundishwa
namna ya kumuhoji muharifu.
Mwili wangu ukaingiwa hofu nikiwa bado katika giza
lile nene la kutisha lililo chini ya utawala wa mbu
wenye kiu ya damu kiasi cha kung’ata kana kwamba
wanaondoka na nyama kabisa.
Baada ya hapo nikasikia hatua zikisogea kisha
zikatulia, nikawa najiuliza mtu anayenihoji yu upande
gani wa mwili wangu.
Hapohapo ghafla taa zenye mwanga mkali zikawashwa
na kunimulika machoni.
Ile najaribu kujiziba macho yangu hapohapo nikawa
nimefanya kosa kubwa kuuacha mgongo wangu wazi.
Mjeledi ukapenya!
Nikapiga mayowe makubwa sana ya uchungu, mayowe
yale yakawa kama yameuzima ule mwanga mkali.
Giza likarejea na mbu nao wakachukua utawala wao
wa kunishambulia bila kupeana zamu ya kung’ata.
“Silijui jina hilo afande!” nililia huku nikimsihi mtu
nisiyemuona.
Kwa sauti ya utaratibu kabisa kana kwamba hakuna
kilichotokea mtu yule alinijibu.
“Rama... mimi sijakuuliza iwapo unalijua jina ama
la... maana hata majambazi huwa hawajuani kwa
majina bali matendo yao. Nahitaji tu unieleze ni wapi
tutampata huyo shetwain muuaji mwenzako”
alizungumzan huku akimalizia kwa kupiga kite cha
ghadhabu.
Alipotaja jina ‘Shetwain’ akili yangu ikafanya kazi
upesi na hapo nikagundua kuwa aliyekuwa akinihoji ni
mtu niliyekuwa namfahamu.
Nasem,a nilikuwa namfahamu ila si kwamba tulikuwa
tunafahamiana.
Huyu alikuwa ni mpelelezi ambaye alikuwa akihusika na
kesi nzito nztito.
Ukisikia kesi imefikia hatua ya kukabidhiwa kwake basi
utambue wazi kuwa muhusika akikamatwa ni lazima
huyu bwana amalize hasira zake kwanza ndipo mambo
mengine yaendelee.
Usoni alionekana mpole sana lakini hakuwa na utu
katu!
Kwa muonekano wake huu maafande wenye vyeo vya
kawaida wakambatiza jina lililoanza kimasihara
akalikataa lakini baadaye akalikubali.
Walimuita sajini PILIPILI!
Wakimaanisha kuwa anawasha na kuumiza lakini haui!
Nilikuwa mikononi mwa sajini Pilipili!
Moyo wangu ulipiga kwa nguvu sana huku mwili
ukiingiwa ubaridi!
 
SEHEMU YA SABA

Makambako,Iringa,Tanzania


Baada ya hapo nikasikia hatua zikisogea kisha
zikatulia, nikawa najiuliza mtu anayenihoji yu upande
gani wa mwili wangu.
Hapohapo ghafla taa zenye mwanga mkali zikawashwa
na kunimulika machoni.
Ile najaribu kujiziba macho yangu hapohapo nikawa
nimefanya kosa kubwa kuuacha mgongo wangu wazi.
Mjeledi ukapenya!
Nikapiga mayowe makubwa sana ya uchungu, mayowe
yale yakawa kama yameuzima ule mwanga mkali.
Giza likarejea na mbu nao wakachukua utawala wao
wa kunishambulia bila kupeana zamu ya kung’ata.
“Silijui jina hilo afande!” nililia huku nikimsihi mtu
nisiyemuona.
Kwa sauti ya utaratibu kabisa kana kwamba hakuna
kilichotokea mtu yule alinijibu.
“Rama... mimi sijakuuliza iwapo unalijua jina ama
la... maana hata majambazi huwa hawajuani kwa
majina bali matendo yao. Nahitaji tu unieleze ni wapi
tutampata huyo shetwain muuaji mwenzako”
alizungumzan huku akimalizia kwa kupiga kite cha
ghadhabu.
Alipotaja jina ‘Shetwain’ akili yangu ikafanya kazi
upesi na hapo nikagundua kuwa aliyekuwa akinihoji ni
mtu niliyekuwa namfahamu.
Nasema nilikuwa namfahamu ila si kwamba tulikuwa
tunafahamiana.
Huyu alikuwa ni mpelelezi ambaye alikuwa akihusika na
kesi nzito nztito.
Ukisikia kesi imefikia hatua ya kukabidhiwa kwake basi
utambue wazi kuwa muhusika akikamatwa ni lazima
huyu bwana amalize hasira zake kwanza ndipo mambo
mengine yaendelee.
Usoni alionekana mpole sana lakini hakuwa na utu
katu!
Kwa muonekano wake huu maafande wenye vyeo vya
kawaida wakambatiza jina lililoanza kimasihara
akalikataa lakini baadaye akalikubali.
Walimuita sajini PILIPILI!
Wakimaanisha kuwa anawasha na kuumiza lakini haui!
Nilikuwa mikononi mwa sajini Pilipili!
Moyo wangu ulipiga kwa nguvu sana huku mwili
ukiingiwa ubaridi!
Nikiwa bado katika hali ileile ya ubaridi na hofu kuu
ikiwa imenitawala nikifahamu fika kuwa yule bwana wa
kuitwa pilipili anakwenda kunisulubisha. Nilikuwa
katika majuto makubwa sana nikijiuliza ilikuwaje hadi
nikamkaribisha yule binti ambaye sasa ni marehemu
katika meza yangu.
Laiti kama nisingemkaribisha basi nisingekubwa na
balaa hili ambalo nipo nalo sasa.
Kimya kilitanda bila kumsikia Sajini Pilipili wala kiumbe
chochote pale ndani.
Ukimya ule ukazidi kuniweka katika mashaka nikijiuliza
amepanga kunifanya nini bwana yule katili.
Lakini hakuna kilichotokea baada ya hapo… ukimya
uliendelea kutanda huku mbu pekee wakipiga kelele za
kushangilia chakula kilichokuwa mbele yao.
Niling’atwa na mbu kwa kiasi kikubwa sana… hadi
mwanga ulipoonekana tena nilikuwa nimewazoea.
Nilichukuliwa na kupelekwa mbele ya sajini Pilipili. Sasa
niliweza kuonana naye ana kwa ana.
Alikuwa anatabasamu kama kawaida yake, huwezi
kujua tabasamu lake lina maana gani.
Neno la kwanza alilosema kwangu ni kunipa pole kwa
usiku uliopita, hakusubiri nijibu pole yake badala yake
akaendelea kuzungumza huku akifanya juhudi ya
kukikuna kidevu chake kisichokuwa na ndevu.
“Umekataa kumtaja Vonso anapopatikana sivyo?”
aliniuliza… sasa alisubiri jibu langu.
Nikamueleza kwa kuapa mbele ya Mungu kuwa katu
sijawahi kukutana na mtu huyo, na hapo upesi
nikauunganisha mkasa wa mimi kukutana na yule binti
ambaye ni marehemu kwa sasa.
“Kwa hiyo zile alama za vidole mikononi, mabegani na
shingoni zimejiweka zenyewe ama?” alinisanifu.
Nikarejea maelezo yangu na kumweleza kuwa ni kweli
nilimgusa binti yule wakati wa kumsaidia.
“Wakati wa kumsaidia kuutoa uhai wake ama?”
alinisanifu tena huku akiacha kukikuna kidevu chake.
“Sajini… hakuna ninachokuficha naomba tu uniamini
lakini kama wewe hautaniamini basi sina jingine la
kufanya lakini nilichosema ni kweli tupu….” Sasa
niliamua kumjibu kwa jazba tu kwa sababu sikuona
dalili yoyote ya kunielewa na nilijihisi kukata tamaa.
“Ramadhani… huna haja ya kupaniki….. unatakiwa
utulie kuna jambo zito katika mkasa wako huu… na
ukileta ujuaji na kujifanya una hasira na mihemko ya
kipuuzi itakugharimu tena sana….”
Alisita na kisha akapiga simu yake na kuzungumza
maneno machache, halafu kimya kikatanda hadi pale
askari wawili wasiovaa sare walipofika wakiwa pamoja
na Nasra pacha wa marehemu.
“Keti” sajini alimuelekeza kwa ishara ya mkono naye
akatii.
Kimya kikatanda nikamtazama Nasra usoni.
Ama! Alikuwa anatisha haswa, uso wake ulikuwa
umewiva kwa hasira kali na chuki ya waziwazi dhidi
yangu.
“Nilijaribu kumwokoa dada yako laki…” nilimweleza
lakini kabla sijamaliza alinigeukia na kunitandika kibao
kikali usoni kisha akaendelea kumtazama Sajini.
Sajini akatokwa na tabasamu hafifu.
“Rama…” aliniita bila kuzungumzia lile tukio la mimi
kuchapwa kibao na yule binti.
Niliitika akaendelea kuzungumza.
“Mtashirikiana na Nasra….” Akapiga kimya kisha
akaendelea.
“Mtashirikiana kuanzia sasa ninavyozungumza nawe.”
Akasita tena.
“Majibu ya ushirikiano wenu ndo hatma ya mkeo…..
mkeo yupo salama lakini ukifanya ujanja wowote ule
wa kujioana unajua sana hautawaona mke na mtoto
wako tena maishani mwako.” Alisita na kunikazia
macho akinitazama jinsi nilivyokodoa macho yangu.
Nilitaka kusema neno lakini akanipungia mkono kuwa
ninyamaze.
“Mtaondoka hapa pamoja, mtazungumza kila
kinachotakiwa kuzungumza. Mkihitaji msaada wangu
nitakuwepo kwa ajili ya kuwasaidia… tafadhali
msiwasiliane na mtu mwingine tofauti na mimi….
Sababu nazijua mimi.” Akatoa kadi yake na kumpatia
Nasra.
Mara simu yake ikaita, akapokea na kuzungumza huku
akiondoka… tukamsindikiza kwa macho. Akageuka na
kusema neno la mwisho kwa siku ile.
“Huyo sio aliyemuua pacha wako….. zungumza naye.
Atamtaja muuaji"
Akatoweka akituacha mafahali wawili tukishindwa
namna ya kutazamana.
Sasa sikiwa namuwaza tena Nasra bali nilikuwa
nawaza juu ya mke na mtoto wangu.
Nilifikiria kwa muda kiasi na kisha machozi yakaanza
kunitoka kwa kasi, nilikuwa najenga picha jinsi
nitakavyokuwa ikiwa tu mke na mtoto wangu
sitawatia tena machoni.
Baada ya kilio cha dakika kadhaa nilinyanyau macho
yangu na kumtazama Nasra.
“Dada Nasra, mke na mtoto wangu wakiuwawa na
damu yao iwe juu yako…. Sijawahi kuua… sijawahi
hata kufikiria juu ya hilo umeamua kunishtaki kuwa
mimi ni muuaji wa pacha wako? Ukweli wangu kwako
umenilipa haya? Kwanini lakini… eeh kwanini Nasra…
ni kweli nastahili haya…. Nitazame ngozi yangu…
nimechapwa mijeledi nimeliwa na mbu wenye dhiki kuu
ya damu… nimeishi maisha ya hofu. Lakini sikumuua
wala kumjeruhi dada yako… nilimwokoa…” hapo sasa
sikuweza kuendelea kuzungumza nikajikuta katika
kilio tena.
Ule mwonekano wa chuki ukageuka kuwa wa huruma
na hapo akanifikia akanishika mkono tukaondoka.
Huu ulikuwa mwanzo wa safari ndefu ambayo
sikuitarajia kamwe.
 
Back
Top Bottom