Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

Mamy relux,
Kuna sehemu tena sio zaidi ya Mara moja ibra87 amekuwa akisema wewe ni fake I'd yangu.
Sasa sielewi ametumia nini kulidhibitisha hilo.
Ila IBRA labla nikwambie tuu I'd yangu ni cute b , tabia za


kulazimisha I'd za watu ziwe zangu sipendi.

Utakuwa umenielewa

Sijawahi kulazimisha fulani kuwa Fulani na siwezi kufananisha. Hembu tafuta kingine cha Kusema Hapa. Hayo mengine sio Mambo Yangu
 
Jamani Mnamshughulisha Sana Ibra
Mgeacha hayo mazozo yenu tusofaidika nayo
Ili Ibra atushushie vitu badala ya kukaa anazozana nanyi
Aaarrrghhhhhhhhb
Mnaboa
 
Jamani Mnamshughulisha Sana Ibra
Mgeacha hayo mazozo yenu tusofaidika nayo
Ili Ibra atushushie vitu badala ya kukaa anazozana nanyi
Aaarrrghhhhhhhhb
Mnaboa
Hawaijui Akili Ninayoitumia kwenye kuandika. Mimi Huwa Si Copy wala Ku paste. Comment za kipuuzi huwa zinanitoa kwenye njia.

Ujinga uwe na Mipaka
 
Mamy relux,
Kuna sehemu tena sio zaidi ya Mara moja ibra87 amekuwa akisema wewe ni fake I'd yangu.
Sasa sielewi ametumia nini kulidhibitisha hilo.
Ila IBRA labla nikwambie tuu I'd yangu ni cute b , tabia za kulazimisha I'd za watu ziwe zangu sipendi.
Utakuwa umenielewa
Sidhani kama ilikua sahihi sana kulisemea hapa,ingependeza ukaenda pm ukamwambia angeelewa zaidi,huenda kwasababu yako watu wakalala na arosto ya hadithi hii
 
[06-27, 19:38] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 092

Wakati akiukaribia Mlango, akausikia ukigongwa. Akatulia huku mkono wake ukishuka mahala alipohifadhi Bastola. Bado mgongaji alikuwa akiendelea kugonga zaidi na zaidi. Bado hakuitika na bado hakusogea. Mgongaji naye akaongeza ugongaji katika Namna ambayo ilianza kuamsha kengele za Hatari Kwenye Kichwa Cha Masimba. Akautoa mkono pekee pasipo na Bastola,kisha akausogelea Mlango na kutaka kuufungua. Lengo lake halikukamilika.. ni muda ule ule mlango ulipopigwa kikumbo watu wanne wenye bastola wakiingia ndani. Hawakuujua wepesi wa mtu huyu, hawakuujua Wepesi wa Masimba. Kilikuwa kitendo cha kufumba na kufumbua tayari bastola ilikuwa mkononi na wakati Huo huo Bastola akiruhusu kutoa cheche. Watu wanne Walikuwa Chini Wamelaliana. Meneja wa Hoteli aliyefuatana na watu hawa alipoona Kilichokuwa kikifanywa. Akataka kukimbia, kukimbia ajiokoe na Hata kukimbia Kwenda kuitoa Taarifa. Hakujua kitendo Hicho kingempa Tiketi na Nauli yake. Ni kweli Hakufika Hatua mbili kutokana na uzito wa Mwili wake. Risasi zikakifumua kisogo na kuuruhusu Ubongo kuruka na kuichafua Korido yote. Kwa kuwa Bastola ilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti.. Tukio lile halikufika popote kwenye Masikio ya Watu. Masimba akaondoka hapo kama mtu wa kawaida. Alirudi mpaka mapokezi na kuukabidhi Ufunguo. Akaondoka Taratibu Akitabasamu na kutamani kucheka. Wana Usalama waliokuwepo nje hawakumuona kwa kuwa kutoka kwake ndani ya hoteli kukafuatiwa na kitendo cha kusimama kwa gari miguuni mwake. Kioo kikashushwa huku sura ya binadamu aliyelaaniwa ikitamalaki. Masimba hakuuliza. Akajipakia Kwa Haraka na Muda ule ule gari ikaondoshwa kwa mwendo wa kawaida. "Vipi Kiongozi umepona? Akauliza Mwanaharamu huku akiendelea kuendesha.

"Nimekufa ndio maana Unaniona Hapa. " akajibu Masimba na kusababisha wote waangue kicheko. "Yuko Wapi Veronica? Aliuliza Masimba huku akijitahidi kutizama kwa Dirishani kuangalia kama Wanafuatiliwa. "Anafuatilia Sehemu waliopelekwa watoto sambamba na Mzee Raymond. Kuna fununu kuwa CHIEF yupo mahala salama sambamba na watoto." Akajibu Mwanaharamu.

"Kwahiyo Chief, Mzee Raymond na Watoto wapo sehemu moja?" Akauliza Masimba akionyesha uso wake kubadilika. "Tunahisi hivyo, isitoshe leo nimemsoma Chief kwenye Gazeti la JAMIIFORUMS LEO." Akajibu mwanaharamu akiendelea kutabasamu. "Hata mimi nimemsoma na kumuelewa. Naomba nipeleke Tabata. Kuna sehemu lazima nifike kwa wakati huu. Pia Itabidi ukitoka kunipeleka huku nakuomba nenda kwenye mazishi ya Meja Jenerali Luois Chomboko. Unaweza kunusa ama kupata cha kutusaidia. " akajibu Masimba.

"Ahsante Mkuu nimekuelewa. Ila ningekushauri upumzike Mpaka kesho ndipo uianze hii kazi." Akajibu Mwanaharamu na kutoa Ushauri.

"Bastard umenisahau leo?" Akauliza Masimba akimtizama usoni.

"Hakuna Jasusi yoyote asiyekufahamu wewe. Kila mmoja anakujua kwa sifa kedekede. Najua kilichokichwani kwako ni Kumuondoa Teddy. Nakuruhusu kulifanya hilo. Lakini nasikitika kusema kuwa Veronica Amekusaidia kumuondoa mmoja. Jimmy Yupo Safarini kuelekea kuzimu." Aliongea Bastard katika Mzaha Ambao ulipokelewa na Masimba katika namna ya kutabasamu. Ni kweli alikuwa ameshangazwa na Veronica. Kitendo cha kumuua Jimmy Hakukitarajia kabisa. Masimba akageuza macho tena kumtizama Mwanaharamu. Lakini akamkuta mwanaharamu akikitizama kitu, kitu ambacho kilimfanya atizame kule. Masimba naye akapeleka macho sehemu hiyo. Gari moja aina ya Noah Ilikuwa ikitembea Taratibu sambamba na wao. Ilikuwa ikionyesha kuwa wanafuatiliwa kwa nyuma. Hilo halikumpa Hofu Masimba na hata Mashaka katika uso Wa Mwanaharamu. Muda wote binadamu huyu aliyelaaniwa alikuwa akitabasamu kuonyesha kufurahishwa na kile alichokuwa akikitizama. Walipofika maeneo ya Ubungo mataa wakaacha barabara ya Mandela, wakaingia Barabara ya Morogoro. Walipoiangalia ile Toyota Noah Bado ilikuwa nyuma ikiwafuatilia kwa mbali. Kufika Maeneo Ya kimara Bucha. MASIMBA AKAMWAMBIA MWANAHARAMU achepuke kwenye barabara kubwa, aingie Barabara ya Vumbi. Bastard akafanya hivyo.. Wakati wakiingia Hapo kwa mbele yao kukawa kuna gari kubwa lililobeba Kontena lilikuwa likitaka kupita. Bastard akaliwahi kabla halijaingia barabarani. Wakapita huku nyuma wakilianya gari ile Ikiziba barabara na Kusababisha Noah Ile Kushindwa kupita. "Simamisha Gari hapo Gereji." Aliongea Masimba. Mwanaharamu Akaingia Upande Wa Kushoto Wenye Gereji na kuisimamisha gari.

Wakati mwanaharamu Akiiweka gari Vizuri Masimba alikuwa tayari yupo Chini akitembea taratibu kurudi kule nyuma. Bastard hakujiuliza Mara mbili. Hata yeye Alijua nini ambacho Masimba alihitaji kwenda kufanya. Hakuchelewa kushuka. Muda huu alikuwa sambamba na Masimba lakini kila mmoja akionyesha kutokumfahamu mwenzake. Walitembea sawa lakini pasipo kuongeleshana wala kuonyesha kuwa walikuwa wakijuana.

Macho ya Masimba yalikuwa yakitizama pembeni kiasi, huku macho ya mwanaharamu yakiwatizama mafundi gereji waliokuwa hapo wakihangaika na kutengeneza magari. Wakati mwanaharamu akibadili uelekeo kuelekea pembeni kidogo mwa barabara waliotokea. Akaiona Ile Noah kwa mbali ikiwa imesimama pembezoni mwa barabara huku mtu mmoja akiwa ameinama akitizama kitu. Wakati huyu wa Pili alisimama akionyesha kuongea na yule aliyeinama. Wakati mwanaharamu Akiendelea kuwaangalia watu wale waliokuja na Noah. Mara akamuona Masimba akitokea Nyuma ya Ile Noah. Hilo kwanza halikutegemewa na Mwanaharamu. Akasimama kwanza kutizama kile ambacho kingeendelea Hapo. Alimuangalia masimba alipokuwa akitembea. Akipiga hatua kuelekea mahala hapo. Mahala ambapo walisimama hawa watu Wawili. Akasogea kana kwamba alikwisha zoeana na Watu hawa. Hata alipowafikia na kusalimiana nao, bado watu hawa walikuwa wakimtizama, walikuwa wakimwangalia katika namna ya mshtuko na Fadhaa. Wakati hawajajiandaa katika hilo, Wakamuona mtu wa pili akisogea hapo. Huyu alikuwa Mwanaharamu. Huyu alikuwa mtu mwingine kichaa kuliko wengine.
********
[06-27, 19:40] Ibrahim Masimba: Alikuwa mwanaharamu aliyelaaniwa. Huyu alikuja kama mtazamaji mahala hapa. Sio utizamaji wa macho tu. Ni utizamaji wa kutumia mdomo sahihi wa Bastola. Kuwaacha watu hawa ulikuwa ni mwiko kwao. Safari hii watu hawa walikuwa wakitizamana na watu hawa wengine. Sura ya masimba na sura ya Bastard hazikuwa sura ngeni kwao. Hazikuwa sura wasizozijua. Licha ya kuwajua huko lakini haikuondoa Sheria kufuata mkondo Wake. Bastola kutoka sehemu fulani ya Mwili wa Mwanaharamu, ulikuwa imeshikwa sambamba na koti kuwafanya watu wasishuhudie kilichokuwa kikiendelea. Lakini pia hawakuujua wepesi kutoka kwa watu hawa. Ni muda huo ikaonekana bastola ya mwanaharamu ikipaa angani baada ya kupigwa teke la mkono na mmoja kati ya watu hawa wawili. Hilo halikuonyesha kumchuuza Mwanaharamu. Bado alitulia na kuyadhibiti mapigo kazaa kutoka kwa mtu huyu. Wakati hili likiendelea tayari yule mmoja alikuwa chali akivuja damu sakafuni baada ya kupigwa Dhoruba kadhaa na Masimba. Ulikuwa ni mchezo uliochezwa kwa Dakika moja na nusu. Mchezo ambao hapakuwa na mpita njia yeyote aliyeng'amua kilichokuwa kikiendelea. Baada ya Tukio hilo wakaondoka hapo na kurudi ndani ya gari.

*****

Giza halikumpa ruhusa ya kukiona kile kilicho mbele ama kinachokuja mahala hapo. Alikuwa ndani ya Endeo ambalo alihisi hapo ndipo alipo Mzee Raymond sambamba na watoto wa Masimba. Ulikuwa msitu mzito na wenye wanyama wakali sana. Mingurumo yao Mikali ingeweza kumuogopesha mtu yoyote. Lakini kwa Veronica ulikuwa ni kama Wimbo Masikio. Tena wimbo mtamu ulioimbwa na Celine Dion ama Shania Twain. Hakuogopa hilo na hakuogopa kilichokuwa kikitoka hapo msituni. Alichohitaji ilikuwa ni kurudi Na watu hao. Alihitaji kurudi na wote ambao angewakuta huko. Mkononi alikuwa amekamatia Bastola macho yake yakijaribu kupambana na Giza. Giza ambalo halikuhitaji kumpa hata ule mwanga. Akainuka hapo akielekea huko, akitembea katika namna fulani hivi ya kuogopa kutoa kishindo. Akatembea akikifuata kinjia kimoja kati ya vinjia vingi ndani ya msitu huo. Mzee Raymond alikuwa ni mtu muhimu sana katika ili. Ilikuwa ni lazima ampate. Ilikuwa ni lazima Amrudishe pale alipokuwa akiishi. Ilikuwa ni lazima afanye hivyo kabla ya Kundi la Mafia Kutuma watu wengine ambao kama Wangekuja. Basi wangeanza kumuua Yeye kabla ya kumtafuta Mzee Raymond.
 
Daaa mkuu umetuacha na arosto kali ila shukrani asiye shukuru kwa kidogo hata kikubwa hawezi kufanya hivyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom