Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 093

Hakutaka kuchelewa kumtafuta mzee Raymond kwa kuuhofia usalama wake. Kanuni ya kundi la mafia zilikuwa ngumu sana kitu ambacho alikiogopa sana. Ilikuwa ni lazima Aifanye Hiyo kazi. Ilikuwa ni lazima ampate Mzee Raymond. Kuchelewa kulifanya hilo na kusababisha kutumwa kwa wengine ni wazi kuwa hatakuwa na maisha marefu. Akatembea usiku ule katika giza. Njia moja ndiyo aliyoiamini kuwa ingemfikisha mahala alipotaka kufika. Nguo zake nyeusi Zilimfanya afanane na giza. Hakuweza kuonekana kwa Urahisi. Alitembea huku bastola ikiwa mkononi, alitembea kidole kikiwa tayari tayari kwa kutuhusu Risasi. Muda wote alikuwa akiliwaza hili, muda wote alikuwa akiwaza mwanzo wa mission. Hakutambua kama kungekuwa na ugumu ule. Wakati anakuja hakujua kuwa angekutana na kizingiti hiki. Hakujua kuwa hapakuwa na utani. Kwa mara hii alikuwa akiuona ugumu katika hili. Aliihitaji betri kuliko hata masimba. Alimhitaji Mzee Raymond Kuliko Hata Yasser na France. Alitamani kuipata betri ili aweze kutoweka katika Dunia hii. Alitambua ukaribu aliyoujenga kwa Masimba hautasababisha Chochote kile. Alijua mpaka sasa Masimba alikuwa akimuamini. Alitaka kuitumia nafasi Hiyo kuipata Betri ambayo Tayari ilikuwa mikononi mwa Rais. Mtu pekee ambaye aliona anaweza kuifanya kazi yake ya Kuipata Betri kuwa ngumu ni Mwanaharamu. Ni Binadamu Yule aliyelaaniwa. Binadamu ambaye ana matendo ya Hatari. Huyu Pekee ndiye ambaye angemletea Tabu. Huyu pekee ndiye alijua atamtatiza katika hili. Ilikuwa lazima Mtu Huyu afe. Lazima mtu huyu aondolewe Hapa chini Ya Jua. Ni lazima Bastard aondoke kabisa. Alipomfikiria Zaidi Akaiona Hofu moyoni. Moyo wake Ulikuwa Ukimdunda Sana. Akaona Ulikuwa ni wakati wa kuuhitaji Msaada. MSAADA kutoka FSB na Hata Mafia. Ilikuwa nilazima apate watu wa kumuondoa Mwanaharamu. Akatembea huku sasa akianza kuuona mwanga kwa mbali. Mwanga ambao ulionyeshakuwa palikuwa na makazi ya Binadamu. Makazi ambayo yalikuwa ni Maalum. Bado akaendelea kusogea na kusogea. Wakati akikikaribia kichaka fulani akaisikia sauti, sauti ambayo ilimwambia kuwa sehemu hiyo palikuwa na watu. Wakati akiendelea kunyata kusogea hapo, akaisikia Harufu ya Moshi. Moshi kutoka kwenye sigara ngumu. Ulikuwa ni moshi wa bangi. Moshi ambao ulikuwa ukipulizwa na watu. Akauona wakati wa mapambano ukiwa umefika. Wakati wa safari ya kuipata Betri. Akatembea kwa hatua za Panya, hatuA za kuiogopa Ardhi. Muda mfupi alikuwa akimuona mtu mmoja akiwa pembeni akiipuliza. Mtu huyu alikuwa ameuegemea mtu akiendelea kuipata ladha. Hilo likamfanya Asite kwanza. Ni muda huu tu ambao alikuwa akizisikia sauti za Watu Wawili. Lakini muda huu alikuwa akimuona mmoja. Akimuona peke yake. Wakati akiendelea kuwaangalia watu hawa ambao kwa wakati huu akagundua kuwa walibeba bunduki. Akamuona mtu wa pili akiongezeka. Huyu alikuwa akitokea kichakani kuonyesha kuwa alikwenda kufanya kitu. Baada ya mtu wa Pili kurudi, Veronica Akaanza kuipiga hatua za Taratibu kuelekea pale.

Akafanikiwa kufika karibu kabisa na watu hawa. Kuwafikia kulikofuatana na Mluzi kutoka kwa Veronica. Mluzi ambao ulizifanya shingo za watu hawa kugeuka. Ulikuwa ni kama mchezo wa Kuigiza. Mchezo ambao haukutarajia. Risasi mbili zikapita katika vichwa vya watu hawa. Hakuna hata mmoja ambaye aliomba maji. Wote wakatambarajika chini wakiwa maiti. Baada ya kuwamaliza watu hawa wawili, Veronica akawapekuwa haraka haraka.. mifukoni hakuona chochote kile cha maana Zaidi Ya Misokoto ya Bangi. Alichokifanya ni kuiokota Bundiki moja na kuipachika begani. Hapo akaendelea kutembea safari hii akiwa makini zaidi. Alikuwa akitizama kila upande, alikuwa akitizama kwa umakini. Baada ya kutembea kwa muda wa dakika kama Kumi, akakiona kizuizi mbele yake. Walinzi wasiopungua kumi wenye Silaha nzito walikuwa wakizunguka huku na huko wakionyesha kuwa makini. Kuliona hilo kukamfanya atulie kwanza Ilikuona ni Jinsi gani ataweza kupambana na watu wale. Aliwaangalia walivyokaa, akawaangalia walivyokuwa wakizunguka na kuziba kila mahali. Hapo akauona Ugumu Wa kuingia ndani ya eneo lile kwa Urahisi. Ilikuwa ni lazima apambane, ilikuwa ni lazima Aingie hapo kuwaokoa watu hawa hasa Mzee Raymond. Akauona ulikuwa wakati wa kubadilisha njia, na pili ilikuwa ni lazima aingie ndani kwa njia yoyote. Muda huu alikuwa akiirudisha bastola mahala pake huku akiikamatia SMG Mikononi safari ya kuingia msituni Ikiendelea.

*******

Wakati Veronica akiwa katika eneo lile la msitu nje kidogo ya Jiji la DSM. Masimba ndio kwanza alikuwa anashuka pembezoni mwa nyumba moja ambayo ameambiwa kuna mtu anataarifa za kumpa. Baada ya kushuka tu, akachapuka akiuendea mtaa wa pili amba0 ndipo ilipo nyumba aliyoambiwa kuna mtu anaweza kumsaidia. Simu alizowapigia marafiki zake ambao bado walikuwa ndani ya Idara ndiyo iliomfikisha hapo. Alihitaji kulimaliza hili mapema. Alihitaji kulimaliza ili aweze kuianza safari ya kumtafuta Teddy. Muda wote alihitaji kumuweka mtu Huyu katika mikono yake. Alihitaji kumuua Teddy kwa ubaya alioutenda kwake. Hakukuwa na huruma Hata chembechembe za upendo. Akaufikia mtaa ule. Kufika hapo akaanza kutembea kwa hatua za Tahadhali. Taarifa aliyopewa ni kwamba hii ilikuwa nyumba ya Mhariri na mmiliki wa Gazeti la Jamii Forums Leo. Bwana MAX MERO. Mhariri ambaye Gazeti lake ndio lililoripoti kwa Kina kuhusu kile ambacho kinaendelea Hapa Nchini. Akaendelea kutembea akiubadilisha uelekeo wake. Safari hii aliamua kuizunguka nyuma ili kuweza kuingia kwa nyuma. Alitambua kutokana na habari iliyoandikwa kwenye Gazeti lake, lazima Atakuwa akiangalia na Macho fulani kutoka mahali fulani. Wakati akiukaribia uchochoro ambao ulikuwa ukitenganisha Nyumba ya Bwana MERO na nyumba ya mtu mwingine. Akakisikia kishindo kikitokea mbele yake. Akasita kutembea kwanza ili kuangalia Nini ambacho kimesababisha kishindo. Kusimama hapo kukafanikisha kuwaona watu wakiruka na kutua kwa ndani. Akawaangalia watu wale kwa umakini mkubwa. Hawa walikuwa watu kutoka Sehemu nyeti. Akaiona Hatari kwa Bwana MERO. Akasogea taratibu mpaka usawa wa ukuta wa Nyumba. Kufika Hapo akatulia kwanza akiitafuta namna ya kufanikisha kuingia pasipo kuonekana. Ilikuwa lazima awahi kuhofia hatari itakayomkuta Mhariri Huyo. Sekunde hii alikuwa akiliwaza hili, lakini sekunde iliyofuata Alikuwa ameuruka ukuta na kutua ndani bila kutoa mchakato wa Chochote kile. Ukimya ulikuwa umetawala eneo lote. Ukimya kanakwamba hapakuwa na mtu sehemu ile. Hilo halikumshangaza kutokana na watu aliyo waona wakiingia muda ule Ukimya ndani ya nyumba ni kitu ambacho hakukiwaza. Watu walikuwa wameingia muda huu , sasa mbona Nyumba yote ipo kimya? Lilikuwa swali ambalo hakutaka kulijibu kwa maneno. Hakutaka kukisumbua kichwa chake. Alihitaji kwenda kujipa majibu kwa Vitendo. Akatembea huku bastola yake ikiwa imetangulia mbele. Akakivuka kijumba ambacho kilionekana kama kilikuwa cha mbwa. Akipopiga hatua mbili mbele akakutana na kitu kilichomshtua. Mbwa watatu walikuwa wamelala chini huku kila mmoja akivuja Damu. Hapo akatambua kuwa Mhariri na Mmiliki wa Gazeti Alikuwa katika Hatari. Akawaangalia mbwa wale kwa muda wa sekunde kama tano hivi. Sekunde ya Sita alikuwa ameufikia mlango wa kuingilia nyumba kubwa. Akaupeleka mkono ili kukinyonga kitasa, lakini Sauti ya Mwanamke kutoka ndani akionyesha kupiga kelele, ndiyo iliyomzuia Kushika kitasa. Akaurudisha mkono safari hii akifikiria kipi cha kufanya. Alitakiwa kuitafuta njia ya kuwasaidia watu hawa. Akiwa bado yupo hapo akiwaza nini afanye, akausikia mlio wa bastola. Mlio ambao ulijirudia kama mara tano. Hilo halikumfanya Masimba Ashangae. Muda mfupi alikuwa yupo ndani akiangaliana na sebule iliyotapakaa damu sambamba na miili ya binadamu. Lakini katika watu hawa hakuwepo Mhariri wala familia yake. Bali waliouawa walikuwa hawa hawa watu aliowaona wakiingia. Na kingine ni kutokuiona familia na hata mtu huyu aliyefanya hiki kilichofanywa hapa sebuleni. Hapakuwa na mtu, hata mwanamke aliyekuwa akipiga mayowe hakuwepo. Hilo likausisimua mwili wake. Hilo likamfanya atabasamu. Alijua kuna mtu ndiye amemuwahi kuifanya kazi hiyo. Lakini atakuwa nani Huyu? Hilo lilikuwa swali ambalo lilimkuta akiwa nje ya jumba lile. Akatembea usiku kurudi alipotoka huku akikikosa kile ambacho alitakiwa kwenda kukifuata sehemu ile. Alitamani kumjua na kumtambua akiyewapukutisha watu wale na kuondoka na Mhariri sambamba na familia yake. Hapakuwa na mtu yeyote yule ambaye alitambua ama kujua kama yeye atakuwa hapo. Kufanywa kwa tukio lile katika muda mfupi kama ule ni dalili kuwa alikuwa akimulikwa na kutizamwa na kufuatiliwa kila kona. Haikuwa dalili nzuri katika namna ile ya Kijasusi. Japo haikuwa nzuri lakini kwa nini mtu aliyefanya hivi akaondoka pasipo kumsubiri? Lilikuwa swali jingine ambalo hakutaka kutafuta majibu kwa wakati huo. Kwa kuwa ulikuwa muda wa mapambano, alitambua majibu angeyapata kila pale muda utakapokuwa ukisonga.

********

Ilikuwa lazima apitie njia nyingine, ilikuwa ni lazima atafute Njia mbadala ya kufika ndani ya majengo yale pasipokupitia Getini. Akaianza safari ya msituni. Safari ya kufa na kupona. SMG ilikuwa imetangulia mbele tayari kwa kumuondoa mtu yoyote yule. Akafanikiwa kuipata Njia fulani ambayo alianza kuifuata kwa umakini. Akaipiga hatua ya kwanza na ya pili. Hatua ya Tatu akauhisi mchakato. Mchakato wa Majani. Kabla hajajua ni kitu gani akausikia Tena mvumo. Mvumo ambao kwa safarii aliutambua na kutambua kuwa haukuwa wa kawaida. Wakati anataka kugeuka ili kuondoka katika namna ya kuukwepa ule mvumo. Alijikuta akitandikwa mateke manne mfululizo ambayo yalimtupa mpaka Chini mithili ya Mzigo. Akasimama Haraka ili kumkabili mtu huyu. Akajikuta Akitizamana na Teddy Akiwa amesimama mbele yake akimtizama kwa macho ya Dharau. KARIBU KUZIMU.. AKATAMKA TEDDY AKIINUA BUNDUKI KUMLENGA VERONICA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom