Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 054

Mwili wa mhudumu aliyemuacha sekunde dakika moja iliyopita, alimkuta akiwa mfu amelala katikati ya dimbwi la damu huku kisu kubwa imesimama katikati ya tumbo. Utumbo ulikuwa nje ukining'inia kwa pembeni. Bado mwili ulikuwa wa moto na damu ilikuwa ndio kwanza inatembea. Kengele za hatari zikagonga kichwani kwa masimba. Aliujua uhatari wa kupambana na mtu wa aina hii. Mtu aliyetumia sekunde kufanya mauaji ya aina hii. Hilo pekee lilimpa ujumbe kuwa ndani ya hoteli ile kulikuwa na mtu hatari sana. Mtu ambaye hatakiwi kuachwa. Akarudi nyuma na kuuacha mwili wa mhudumu yule ukiwa bado umelala katikati ya damu. Akairuhusu miguu yake itembee katika namna ya utayari , mikono ilikuwa tayari hata pale alipokuwa akipanda ngazi. Akanyoosha kuelekea pale kwenye chumba alichokisoma kwenye daftari la wateja. Chumba alichohisi kuwa atakuwa ameingia Salha na mwanaume Yule aitwaye marlon. Masikio yakinasa huku pua zikiinusa harufu ya damu. Harufu ambayo bado ilikuwa ikisumbua katika matundu ya puA zake. Hatua ishirini mbele akauona mlango wa chumba kile. Mlango ambao hakuonyesha kufungwa bali kuegeshwa tu. Akaongeza umakini mkono wake ukiwa umenyooshwa kwa mbele kuilekeza bastola pale. Hata alipoangalia chini matone ya damu kutoka ndani ya chumba kile yalimrejesha katika utambuzi yakinifu katika medani ile. Sasa alikuwa ameuweka mwili katika aina yoyote ya mapambano. Akageuka na kuelekea pale. Masikio yakinasa kushoto, kulia na hata kisogoni kusikia chochote kitu. Bado damu ilikuwa ikitembea taratibu. Mlango uko wazi na kisha damu. Kuna nini? Ama ni mtego? Lilikuwa swali lisiliteguliwa kwa wakati ule. Mguu wake wa kushoto ukausukuma mlango huku bastola imetangulia. Baada ya mlango kumpa nafasi ya kuangalia ndani, akatupa macho kwa haraka.. hakukiona kitu zaidi ya damu.. Hilo likamfanya aingie ndani kabisa.. Kuingia ndani akajikuta akitizama na kitu ambacho hakukitegemea, tukio ambalo lilimfanya ahisi kwanba anaitizama picha za video zisizopendeza machoni mwake. Alihisi kile anachokitizama hakikuwa kitu cha kweli. Ni punde alikuwa akimtizama akiingia akiwa hai. Lakini sasa alikuwa akimtizama akiwa maiti. Akimtizama akiwa amechinjwa shingo na kutenganishwa. Hakuwa anamtizama mtu mwingine, hakuwa akimtizama mnyama ama picha za video. Bali alikuwa akimtizama Salha akiwa uchi wa mnyama huku kichwa na kiwiliwili vikiwa vimetenganishwa. Hakukiamini kitu hicho, hakuamini kama Salha ameuawa katika namna ile. Akarudi nyuma na kuiacha ile hoteli akiwa amechanganyikiwa. Akiwa amefura kwa Hasira. Aliamua kuwarudia vijana wale kule kigogo. Akatembea katika namna ya kuonyesha kutokuwa makini. Hakupita hatua hata nne akaisikia sauti ikitokea nyuma yake.. sauti ya mwanaume asiye na utani.. mwanaume shupavu. "Tupa Bastola yako chini na usigeuke." Masimba akatii akijiona mpumbavu. Akauona mwisho wake, akajua kwanza safari hii hawezi kupona. Akaituma bastola chini kisha kuinyanyua mikono juu. Akakisikia kidole cha mtu wa nyuma yake kikiitoa risasi katika chemba cha usalama. Sasa alikuwa akilipuliwa. Lakini kabla ya hilo akahisi umajimaji ukimmwagikia katika mavazi yake. Maji maji ambayo yalimfanya ageuke kuangalia nyuma. Hapo akakutana na tukio jingine la kushangaza. Maiti ya mtu ilikuwa nyuma yake, maiti ya mtu ikiwa haitazamiki kwa Risasi. Kichwa kikiwa kimefumuliwa. Yalikuwa matukio yaliyotokea katika kipindi kifupi sana. Ndani ya sekunde thelathini. Nani amemuokoa katika hili? Nani amemuua huyu mtu..? Akiwa anajiuliza akamuona mtu akitokea, mtu ambaye aliiduwaza akili yake kwa sekunde tano. Teddy Harry alikuwa akitokea taratibu akitembea kuelekea pale aliposimama yeye. Teddy mwanamke wa maisha yake. Teddy mzuri na hata teddy mtamu. Mkononi alikuwa ameishikilia bastola ya kirusi Special colt 38. Alikuwa akitembea kwa madaha yote. Alikuwa akinataka katika mwendo wake wa twiga.

Alifanana na Nuru wa Joram kiango, akifanana na Yule Veronica wa Willy gamba. Alikuwa mfano wa Regina wa Sudi. Alinata na kunata. Alipofika aliposimama Masimba teddy akajitupa kifuani huku akimgonga Masimba Mgongoni. "Kuwa makini Baba ningekupoteza mpenzi wangu. Aliongea teddy akiendelea kujilaza kifuani kwa masimba. Kwa mara ya kwanza masimba akaamini Teddy alikuwa amebadilika. Teddy alikuwa amerudi katika uaminifu wale. "Nimeamini mpenzi, nimekuamini kutoka moyoni. Huu niwakati wa kuondoka." Aliongea masimba wakitoka Ndani ya Hotel. Walitoka kama kawaida pasipokutiliwa shaka. Wakatoweka katika namna ambayo hakukuwa na mtu aliyewaona au kuwatilia shaka

*******
Wakati Masimba akielekea masaki nyumbani kwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi, teddy alikuwa akielekea kigogo baada ya kupewa maelezo na Masimba kuhusu kushuka kwa vijana wale ambao anahisi watakuwa na maelezo kuhusu aliyemuua Salha. Alisaidiwa na giza usiku ule kutembea bila kuonekana mpaka kigogo. Akapokelewa na sauti za mbwa waliokuwa wakibweka. Teddy akatulia gizani kwa muda akiichunguza nyumba aliyoambiwa. Ilikuwa nyumba nzuri pekee katika Nyumba zote zilizolizunguka eneo lile. Licha ya uzuri huo lakini pia ilizungushiwa miti ya michongoma ambayo iliifanya nyumba hiyo ionekane kama kichaka. Upande wa nyuma wa nyumba ile kulikuwa na migomba mingi ambayo ndani yake palionekana uwepo wa kinjia kilichopita katikati ya migomba. Teddy akahama pale nakuzunguka upande mwingine wa Jengo lile. Akakutana hata upande ulijengwa na kupandwa migomba kama Upande aliopita. Akaangaza macho huku na huko alipoona kuna utulivu wa kutosha Teddy alijibunua na kuchupa kisha kutua ndani katika sekunde ile ile. Utuaji wake ulikuwa mfano wa paka anayenyatia panya. Baada ya kutua hapo akapokewa na giza nene na totoro. Taa zisizo na mwanga ndizo zilizokuwa zikiwaka ndani ya Nyumba ile. Wimbo wa Shania Twain still the one ndio pekee uliosikika ukihanikiza katika nyumba ile. Wimbo ulioonyesha uburudishaji wa miili ya mtu kutoka mahala fulani. Akaachana na hilo sasa akawa anatafuta nafasi ya kuingilia ndani ya nyumba ile. Hakutaka kufanya haraka kutokana na kutokiamini sehemu ile. Aliogopa na kuogopa kugutukiwa mapema. Aliamini kwa mazingira yale hapakosi mtu anayetizama usalama. Kutoka pale alipo akaokota kupo ambalo lilikuwa pembeni yake na kulitupa upande mwingine tofauti na alipo, nia ikiwa ni kujua kama kuna mtu au lah.

Hazikupita hata dakika akamuona mtu akitokea katikati ya migomba. Mtu huyu alikuwa amevaa mavazi meusi ambayo yalifanana kabisa na giza la sehemu ile. Mtu yule mkononi alikuwa amekamatia bunduki aina ya Sub Machine Gun. Akazunguka akiutizama kila upande. Teddy akaanza kutambaa mfano wa nyoka kuelekea pale aliposimama yule mlinzi. Alikuwa mfano wa kiza na mfano wa kivuli cha migomba. Hata alimfikia karibu mlinzi yule hakumuona. Teddy akafyatuka mfano wa mshale na kumtia kabari na kuanguka naye chini. Kufika chini akamshika shingo na kuivunja. Yule mtu akakata roho pale pale. Baada ya kummaliza akamburuza mpaka katikati ya Migomba. Akamuacha hapo yeye akaanza kusonga kuelekea ndani ya Nyumba ile. Alitembea kwa umakini wa hali ya juu. Alitembea kwa umakini mpaka pembozini mwa nyumba. Hapo akatulia kusikiliza sauti. Bado sauti ya wimbo wa shania ilikuwa ikipenya masikioni mwake. Akaongeza hatua nyingine mpaka mlangoni. Akausukuma kidogo, akauona mlango ukifunguka. Akagundua haukuwa umefungwa.. Akausukuma tena kidogo, akajikuta yupo ndani ya korido moja ndefu. Akasogea haraka ili kuipita ile korido. Akiwa anakaribia kuimaliza, mlango wa mbele yake Ukafunguliwa...
 
Wadau tukazane kuchanga,Namna hii tunamvunja moyo muandishi,yaan tunakuwa na style za kizamani sana za kupenda vya dezo,Kama kitu unakipenda,kinakufurahisha changia tu ili kiendelee kuwepo.tukichanga japo elfu 5 tu kila mmoja wetu mwandishi atapata nguvu ya kuendelea kuifanya kazi vema na kuendelea kutufariji na kutupunguzia stress.
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 055

Wakati anaimaliza korido mlango wa mbele yake ukafunguliwa, akamuona mwanaume akitokea, kilikuwa kitendo cha sekunde Teddy kumuondoa mtu yule kwa kumpiga Risasi ya kichwa. Baada ya mtu yule kukata roho Teddy akampekua mifukoni. Humo akakuta mtu yule akiwa hana kitu cha maana. Baada ya hapo teddy akaongoza na kuingia ndani ya chumba alichotoka yule mwanaume. Baada ya kuingia akapokewa na manukato sambamba na mtiririko wa maji kutokea bafuni. Akaufunga mlango kwa ndani huku Bastola mkononi. Akapiga hatua akielekea kule maji yanaposikika kumwagika. Wakati anataka kuufikia mlango wa bafuni akasikia mchakato kama wa kitasa cha mlango ukifunguliwa. Akageuka kuangalia nyuma.. ni kweli ilikuwa hivyo.. kitasa kilikuwa kikitingishwa kuonyesha kulikuwa na mtu kwa nje. Teddy akarudi na kufanya kama anaufungua mlango.. kitendo bila kuchelewa akamuona mwanaume akiingia mkononi akiwa na bastola akionyesha kuwa na wasiwasi sana. Kwa kuwa hakujua kama ndani kuna mtu, ilikuwa ni Rahisi sana Teddy kufanya kile alichotarijia. Pigo Moja la kareti lilitosha kumpeleka chini mtu yule. Hata baada ya kuanguka chini Teddy alimfuata na kumnyonga shingo. Baada ya hapo akamburuza mpaka mwisho mwa chumba kile na kumfunika. Baada ya hapo akakaa hapo chumbani kumsubiri mtu aliyekuwa akioga bafuni. Huyu alihisi ni mwanamke, alijua huyu ndiye atakayesema nani aliondoka na marehemu Salha. Baada ya kukaa kwa dakika kama tano hivi, akausikia mchakato wa miguu ya mtu akitembea taratibu kuja pale sebuleni. Punde akamuona mwanadada mwenye asili ya kisomali akiingia pale chumbani akiwa amejifunga Taulo lililoishia juu ya magoti na kuyafanya mapaja yake yawe wazi. Alikuwa mzuri na mrembo sana.. alikuwa mrefu mithili ya Twiga. Aliingia akitembea katika aina ya mwendo wa kinyongo. Ukiachana na hilo mwanamke huyu hakushtuka pale alipomuona Teddy pale Chumbani. Hakushtuka kwa mwili na hata macho. Macho yake hayakuionyesha hofu, hofu ya kuhofia na hata kuogopa. Tabasamu la kifedhuli liliipamba sura yake. Tabasamu lakinyama lilitawala katika uso wake. Akapita na kwenda kukaa sehemu fulani. Akimuangalia teddy katika macho fulani yenye maswali. Maswali ambayo hayakuwa na majibu. Alijiukiza kutembelewa na Mwanamke mwenzie. Mwanamke ambaye amejikaribisha chumbani kwake pasipo taarifa. Mwanamke huyu ni nani? Ameingiaje hapa chunbani kwangu? Amewapitaje walinzi hadi kuingia humu? Alijiuliza mwanamke yule huku sasa akiyaruhusu macho yake yamtizame Teddy. Ya mtizame mwanamke huyu ambaye hakuwa na mashaka. Wakatizamana!! Naam! Walitizamana na kutizamani. Nuru ya utambuzi ikang'ara mithili ya mbalamwezi isiyo na kizuizi cha mawingu. Nuru iliyomulika mpaka katika undani wa viumbe hawa. Walijuana na kutambuana katika aina moja na aina nyingine zote. Mwanamke yule akatambua kuwa amekuwa ametembelewa na Teddy Harry, mwanamke ambaye hakuonyesha masihara. Mwanamke ambaye alikuwa akizisikia sifa zake duniani kote. Leo alikuwa naye ndani ya chumba chake. Mwanzo wakati anaingia hakuwa anamuogopa. Lakini hapa sasa alikuwa na hofu. Hofu juu ya kifo. Kufika hapo ndipo alipoangaza pembeni kuangalia msaada. Mwili wa mlinzi ulikuwa umetambalajika sakafuni ukiwa hauna uhai. Hilo likaonyesha kumshangaza mwanamke yule. Ni katika mshangao huo akainuka kwa kasi ya ajabu akielekea pale alipokaa Teddy. Alikuwa akipiga mapigo mfululizo. Yote yalikuwa yakipita patupu. Yote yalipita hewani na wakati huo huo akaisikia ngumi nzito ikitua usoni. Ilikuwa ngumi iliyomtupa chini mithili ya fulushi la mihogo. Hakuchelewa kuchupa akipiga mapigo mengine, safari hii alibadili mapigo.. alikuwa akichanganya Kung Fu na Hata Karate. Hakujua Teddy ni waaina gani.

Ni ndani ya sekunde ile ile akajikuta yupo chini baada ya kupigwa mapigo mawili yaliomungia sahihi mwilini. Alipotaka kuinuka akakutana na mdomo wa bastola ukimtizama. "Tulia kama ulivyo.. Usipende kucheza na watu kama sisi." Aliongea teddy huku akimtaka asimame. Kweli mwanamke yule akatii, akasimama akiwa anavuja damu. Lakini akiwa amesimama akimuangalia Teddy, tukio la ajabu likatokea.. ni tukio ambalo lilimfanya Teddy achupe na kudondokea pembeni. Risasi mbili zilizokusudiwa zimmalize Teddy, zilitua kifuani kwa mwanamke yule wa kisomali na kumtupa hewani kabla ya kutua chini akiwa marehemu. Teddy hakukitegemea kabisa kitendo kile. Hata alipoinuka kumfuata mwanamke yule, tayari alikuwa maiti. BADO GIZA LIKAENDELEA.

*********

Alisimamisha pikipiki nje ya geti la jumba la mkurugenzi wa usalama wa taifa. Masimba akashuka na kutembea kuelekea ndani ya jengo hilo. Wakati huo ilikuwa yapata saa kumi na nusu usiku. Akapokelewa na walinzi wa Jumba lile. Akakaguliwa kama destuli na kuruhusiwa kuingia ndani. Alitembea akipanda ngazi mpaka juu kabisa sehemu ya mikutano. Wakati anaikaribia sehemu hiyo akashangazwa na kuwaona walinzi binafsi wa rais. Wakati mshangao wake ukiendelea, akashangazwa zaidi Baada ya kumuona Rais akitokea mbele yake akiwa sambamba na makamu wa Rais. Hilo hakuwa amelitegemea kwake. Kuwakuta viongozi wa nchi pale ilimpa kufahamu kuwa Ushahidi wake ulikuwa ukihitajika sana. Masimba akasogea mpaka karibu na waliposimama Viongozi wale wa nchi. Akawapa mkono na kusalimiana nao kwa muda. Baadaa ya hapo akafungua vifungo vya kote lake na kuchomoa bahasha ambayo aliikabidhi mikononi kwa rais, kisha hata bila kusubiri chochote akapiga hatua kuondoka pale akiwaacha wakimtizama katika namna ya kumshangaa.

Alipotoka pale safari yake haikuwa ya kurudi nyumbani, bali iliunganisha kuelekea nyumbani kwa Suresh. Ilikuwa zamu yake ya kusafirishwa

Ilikuwa ni lazima asafirishwe kupelekwa kuzimu katika usiku ule ule. Bado pikipiki aliyoichukua kwa dereva yule ilikuwa ikimsaidia kutoka hapa kuelekea pengine. Muda wote alikuwa akiitizama saa yake ya mkononi. Ilikuwa ni saa kumi na moja kasoro. Ndani ya jiji la dar es salaam ndio watu walikuwa wakiamka kujiandaa kwenda makazini. Alitaka kuutumia muda huo kukamilisha kile alichokipanga. Kile ambacho alitaka kifanyike katika muda ule. Alitaka kuipenyeza Risasi kichwani kwa suresh kabla ya Jua la Asubuhi kuchomoza. Pikipiki ikatembea barabarani ikiteleza. Sasa alikuwa akiipita mbagala kuelekea nje ya Jiji la Dar es salaam. Muda wote alikuwa akipishana na watu waliokuwa wakienda makazini. Bado muda haukuwa tatizo kwake kuwahi nyumbani kwa Suresh. Muda mfupi baadae pikipiki ilikuwa ikisimama kwenye kichochoro kimoja pembezoni mwa ukuta mkubwa uliozunguka jumba analoishi Suresh. Kwa kuwa ni nyumba ambayo aliifahamu. Hapakuwa na ugumu Masimba kuruka na kuangukia ndani. Baada ya kutua tu alijibingilisha mpaka pembeni. Wakati anatambaa kuelekea sehemu nyingine, akajikwaa kwenye bati na kuanguka chini. Wakati ametulia hapo akaliona jibwa likimjia kwa kasi.. huku likibweka. Wakati hajiweka tayari mbwa lile likamrukia na kumvaa. Haikuwa kazi ndogo.. Masimba akaanza kubingirishana na yule mbwa pale chini. Alitakiwa kupambana hasa kwani alijua endapo angechelewa basi walinzi wangetokea na kufanya mapambano yawe magumu. Bado alimgalagaza mbwa yule na alipofanikiwa kumuweka chini ili amtie shaba.. Akahisi kitu kizito kikitua kichwani kwake. Akamuachia mbwa na kwenda chini huku giza likiibeba nuru ya macho yake.

HAKUJUA TENA KILICHOENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom