RIWAYA: Mume Gaidi

SEHEMU YA 26


Tusa nae akaanguka chini na kupoteza fahamu.
Wote wakabaki wakistaajabu.
ANNA: Kwani vipi jamani! Huyu binti ana nini? Na wewe Deborah unalia nini?
DEBORAH: Nimemkumbuka mwanangu tu.
ANNA: Maana sijaelewa, wewe unalia na gafla huyu binti kazimia jamani loh!
PATRICK: Hata hivyo huyu binti ni mgonjwa.
DEBORAH: Basi tumpeleke hospitali jamani.
Wakasaidiana kumnyanyua na kutoka nae nje, kisha kumpakiza kwenye gari ya Patrick, na safari ya kwenda hospitali ikaanza.
Adamu bado hakuelewa namna ya kumpata mkewe, aliendelea kuwaza sana.
REHEMA: Punguza mawazo mwanangu, atarudi tu.
ADAMU: Kwakweli mama, simuelewi kabisa huyu mwanamke.
REHEMA: Ni vigumu kuelewa ila tambua yule ni mama, anauchungu na mwanae ndomana kamfuata.
ADAMU: Vipi wewe hukuwa na uchungu na mwanao ulipomuacha kwa mumeo? Na vipi huyo mtoto wako wa Mombasa, huna uchungu nae?
REHEMA: Laiti ungejua mwanangu, ungetambua ninavyojisikia. Nakumbuka watoto wangu mapacha wawili wa kiume tena wa kupendeza na kuvutia machoni, nikawapa majina yanayofanana na kuendana lakini wewe umebadili jina nililokupa, ilikuwa bado kidogo nikukose mwanangu.
ADAMU: Majina yapi hayo unayoyazungumzia mama?
REHEMA: Wewe nilikuita Jumanne na mwenzako nilimuita Juma.
ADAMU: Kumbe jina la Jumanne ulinipa wewe?
REHEMA: Ndio mwanangu, nilitamani siku moja ungekutana na nduguyo. Kwanini ulibadilisha jina mwanangu?
ADAMU: Nilipatwa na maswaibu, ikabidi nibadili jina. Sikutaka tena kuitwa Jumanne, nilitaka kuwa mtu mpya kabisa, mtu wa tofauti. Nikajipa jina Adamu, jina la marehemu babu.
REHEMA: Maswaibu gani yalikukumba?
ADAMU: Mama ni historia ndefu, ipo siku utajua ila yote ni kuhusiana na mke wangu wa kwanza.
Rehema nae akabaki na mawazo na kuona kuwa kuna vitu vingi sana anafichwa na mtoto wake.
Tusa alifikishwa hospitali na kuhudumiwa ipasavyo, kila kitu ni pesa na uzuri ni kuwa Patrick alikuwa na pesa.
Baada ya kuambiwa na daktari kilichomsibu mgonjwa wao, Deborah alimuita Patrick na kumsema.
DEBORAH: Mwanangu, inamaana muda wote unakuja na huyu binti ulikuwa hujui kama anavuja damu kiasi kile?
PATRICK: Mmh! Mama, nilikuwa sijui.
DEBORAH: Acha upumbavu Patrick, utaua mtoto wa watu wewe. Hujui kuwa ni khatari, mimba imetoka, damu inamwagika. Unajua mwanamke anapatwa na maumivu ya kiasi gani? Mwanangu kama ulikuwa unajua halafu ukamtizama tu hiyo ni roho mbaya tena iliyopitiliza.
PATRICK: Hapana mama, sipo hivyo. Nadhani unanijua vizuri.
Hali ya Tusa ilikuwa mbaya sana, ilionyesha kuwa alimwaga damu nyingi sana na aliishiwa damu kwahiyo ikabidi ajitolee mmoja kumchangia damu.
Deborah alijitoa ila damu yake haikuendana na Tusa, ila damu ya Patrick ndiyo damu iliyoendana nae. Ikabidi Patrick atoe damu kutokana na shinikizo la mama yake, na damu hiyo akaongezewa Tusa.
DEBORAH: Yani Patrick ulitaka kukataa kabisa kutoa damu?
PATRICK: Nilijua kuna madhara mama, hata hivyo kuna kitu kimejificha hapa.
DEBORAH: Kitu gani?
PATRICK: Nitakwambia tu mama.
Patrick hakuona sababu ya kumchangia Tusa damu, alitamani anunue damu awekewe kuliko kumchangia damu yake. Sababu kubwa ni kwavile anajua wazi kuwa hapendwi na Tusa, kwahiyo kumchangia damu aliona ni kazi bure.
Bi.Rehema nae akapatwa na maswali zaidi kwenye kichwa chake, ikabidi amuulize Fausta aliyekwenda kumuaga.
REHEMA: Unajua bado siwaelewi Pamela na mwenzie jamani!
FAUSTA: Huwaelewi nini mama?
REHEMA: Kwanini Adamu alimuacha mke wake wa kwanza? Na ilikuwaje hadi akamuoa Pamela?
FAUSTA: Mama, hata mimi namfahamu vizuri huyo mwanamke wa Adamu ila sijui walipatwa na nini hadi kuachana, ila ninachokumbuka alizaa nae mtoto mmoja.
REHEMA: Yuko wapi huyo mtoto?
FAUSTA: Kwakweli sijui chochote mama.
REHEMA: Mmh! Kazi ipo.
FAUSTA: Mama, nimekuja hapa kukuaga. Kesho alfajiri nasafiri naenda China kwenye biashara zangu.
REHEMA: Mbona mapema sana? Nitakukumbuka kweli.
FAUSTA: Usijari mama, safari hii sitakaa sana huko.
Fausta akamuaga bi.Rehema ili awahi kujiandaa na safari yake.
Pamela alipozinduka tena alikutana na macho ya Mashaka yakimtazama, Pamela akaongea kwa uoga huku akitetemeka.
PAMELA: Tafadhari naomba usinidhuru.
MASHAKA: Sina nia hiyo, ila unachotakiwa kufanya ni kuniambia dada yako Fausta yuko wapi?
PAMELA: Kwani mimi na Fausta tumefanyaje?
MASHAKA: Mama yako sikutaka kumuua ila ikatokea tu nimemuua, najutia ndio. Ila ninayemtaka ni Fausta, nikimpata kichwa chake kitakuwa mali yangu.
Pamela alihisi baridi na kutetemeka sana.
MASHAKA: Unachotakiwa kufanya Pamela ni kunitajia alipo dada yako, vijana wangu wakileta kichwa chake hapa ndipo na wewe utakuwa huru.
PAMELA: Kwani wewe ni nani? Na umetujuaje?
MASHAKA: Mimi ni ndugu wa mama yako, mimi na mama yako ni mtoto wa baba mkubwa na mdogo. Mimi ni Mashaka.
Aliposema hivyo moyo wa Pamela ulilia paaa, alihisi kuwa amesikia kitu cha ajabu ambacho hakuwahi kufikiria maishani mwake.
Tusa akasafishwa kizazi na hali yake kuwa na unafuu, Tusa alikuwa na maumivu tu moyoni mwake, tena maumivu yaliyopitiliza.
Wakaruhusiwa kurudi na mgonjwa wao nyumbani.
Deborah hakuacha kumuangalia Tusa, muda wote macho yake yalikuwa juu ya Tusa hata Tusa mwenyewe akajishtukia.
Hata walipokuwa nyumbani, Deborah aliendelea kumtazama Tusa kwa ukaribu zaidi. Deborah alijikuta akimuita Tusa.
DEBORAH: Binti!!
TUSA: Abee.
DEBORAH: Kuna kitu nataka nikwambie, kitu kilichonifanya nilie nilipokuona.
Tusa alibaki kushangaa kuwa anataka kuambiwa nini na mama yake Patrick.
 
SEHEMU YA 27

Tusa alibaki kushangaa kuwa anataka kuambiwa nini na mama yake Patrick.
DEBORAH: Unaitwa Tusa, si ndio?
TUSA: Ndio naitwa Tusa.
DEBORAH: Sawa sawa nilisikia hospitali ukitajwa na Patrick, hivi uliwezaje kuolewa na mwanaume ambaye hujui ndugu zake?
Tusa kabla hajajibu akaitwa na Patrick, Deborah akamruhusu Tusa kwenda kumsikiliza Patrick.
PATRICK: Ole wako umwambie mama kuhusu Maiko, hakuna kumwambia jambo lolote la ndoa yetu. Yote nitamwambia mwenyewe, umenielewa Tusa?
TUSA: Ndio nimekuelewa.
PATRICK: Haya nenda kaendelee kuzungumza nae.
Tusa alirudi kwa Deborah akiwa amenywea sana.
DEBORAH: Una umri gani Tusa?
TUSA: Nina miaka 23.
DEBORAH: Bado binti mdogo sana, kwakweli Tusa umefanana sana na mwanangu. Isingekuwa umri wako mdogo ningesema ni wewe, mwanangu alikuwa hivyo hivyo kama wewe. Ingawa ni sura ya utoto ila alikuwa kama wewe Tusa, nadhani hata wewe sura yako haijabadilika toka utotoni.
TUSA: Ni kweli, watu wengi huniambia kuwa sibadiliki sura. Ila huyo mwanao niliyefanana nae ni nani?
Deborah alijikuta akiinuka na kwenda chumbani kwake ambako alilia kwa uchungu sana, alijikuta akitembelewa na matukio ya nyuma kwenye akili yake. Machozi mengi yalimtoka.
Pamela akiwa kwenye himaya ya Mashaka, akaweza kugundua kuwa Mashaka alikuwa ndugu yao wa aina gani.
MASHAKA: Umenikumbuka vizuri Pamela?
PAMELA: Nimekukumbuka ndio, lakini hakuna baya nililowahi kukufanyia mjomba.
MASHAKA: Ni kweli, wewe ulikuwa mpole, mkarimu na mpenda watu tena mwenye moyo wa huruma. Ulinisaidia sana nilipotoka jela ila dada yako ndiye ninayemtaka hapa, anamajivuno na maringo nahitaji kichwa chake.
PAMELA: Ila hakukufanyia baya.
MASHAKA: Nadhani hujui kitu Pamela, nilipotoroka jela nilifikia kwenu, unadhani ni nani aliyeenda kutoa taarifa polisi kuwa mimi nipo pale?
PAMELA: Sijui.
MASHAKA: Ni Fausta, yule binti ni mbaya sana. Ana roho mbaya, alikuwa ananinyima chakula ananifanyia kebehi, alikuwa ananiona kama chizi.
PAMELA: Ila hata mama yetu hakukufanyia vibaya.
MASHAKA: Sina tatizo na mama yenu, alikataa kunitajia mlipo. Namuhitaji Fausta, nina mengi sana na yeye. Mimi ni Mashaka ila si Mashaka yule ambaye mlimzoea mwanzo na kumuita mjomba chizi. Kwasasa sina masikhara wala mzaa, huwa nikitaka kitu lazima nikitimize kupona kwako ni kumtaja alipo Fausta.
PAMELA: Sawa nitawatajia ila ingebidi kwanza mnipe simu ili nimpigie nijue alipo.
Mashaka akaenda kuichukua simu ya Pamela kwa Maiko na kuiwasha.
Safari hii Maiko nae hakumuelewa Mashaka ana mpango gani.
MAIKO: Tatizo ni nini Mashaka? Mbona tangu aje huyu mama yake Tusa umekuwa kama mtu usiyejielewa?
MASHAKA: Damu za watu zinatembea kwenye akili yangu, kwakweli hii kazi ni kama uchawi ukianza kuacha hutaki.
MAIKO: Kwani ulikuwa unataka kuacha?
MASHAKA: Labda nikimpata huyo Tusa.
MAIKO: Mara nyingi nakuona ukizungumza na mama yake Tusa, kwani ni ndugu?
MASHAKA: Hapana si ndugu ila kuna vitu nahitaji toka kwake.
MAIKO: Nikajua ni ndugu, kwakweli kwa mimi nitawatesa watu wote lakini si ndugu zangu.
MASHAKA: Vizuri sana, ila kuna muda hata ndugu unapaswa kumgeuka.
MAIKO: Mmh unamaana gani?
MASHAKA: Sina maana yoyote.
Maiko amekuwa na Mashaka kwa muda mrefu sana ila hakuelewa mambo baadhi anayofichwa na Mashaka.
Patrick alipoona mama yake amekaa kwa muda chumbani, ikabidi amfate na kumkuta akilia sana.
PATRICK: Jamani mama, una nini wewe?
DEBORAH: Mwanangu, alikufa kifo cha kutisha sana. Siwezi hisia ni maumivu gani alipata, je aliliaje? Roho inaniuma kila nikikumbuka. Siwezi kumsahau mwanangu Jasmine.
PATRICK: Khaaa mama, inamaana mimi nilikuwa na dada yangu?
DEBORAH: Tena amefanana kila kitu na huyu mwanamke uliyekuja nae, hadi nahisi kuwa amefufuka na kukua gafla.
PATRICK: Mama, usilie sana kumbuka mimi nipo kwaajili yako mama yangu.
Deborah alijikuta akiinuka na kumkumbatia Patrick kwa nguvu.
DEBORAH: Ni kweli upo kwaajili yangu Patrick, na umeyafuta machozi yangu.
Akajifuta machozi na kurudi tena alipo Tusa. Kwasasa Tusa aliogopa kumuuliza chochote Deborah kwani aliona kuwa ni kumpa mateso.
Tusa akamuomba Patrick ampigie baba yake simu kuwa yupo salama ila Patrick akaona kama vile ni kujitia mashakani ukizingatia hawajaijua bado hali ya mama yake Tusa. Ila Tusa aliendelea kumsisitiza ili aweze kuongea na baba yake, mwisho wa siku Patrick akakubali.
TUSA: Mimi Tusa baba, nakutaarifu kuwa nipo salama.
ADAMU: Na mama yake je? Maana alikufata huko Arusha.
TUSA: Mi siko Arusha baba, mi niko Mwanza.
ADAMU: Mwanza?
Simu ikakatika kabla ya Tusa kujibu.
Adamu akaamua kuijaribu tena simu ya mkewe kama inapatikana.
Akashangaa inaita, alitaka kujua alipo na aweze kumtaarifu habari ya mtoto wao.
ADAMU: Uko wapi Pamela?
PAMELA: Nipo Arusha, nimepatwa na......
Akazuiliwa kusema na Mashaka.
ADAMU: Umepatwa na nini mbona husemi? Nimezungumza na Tusa.
PAMELA: Aah sawa.
Halafu akakata simu, Mashaka akachukia kwani alitaka aambiwe huyo Tusa yuko wapi halafu Pamela kaishia kusema sawa.
Mashaka akamuangalia Pamela kwa macho makali na kumlazimisha ampigie simu tena mumewe na amuulize alipo Tusa. Tamaa ya viungo vya Tusa ilishamjaa Mashaka, alivihitaji sana viungo hivyo.
Patrick ndiye aliyempokonya Tusa simu.
PATRICK: Kwanini unakuwa na akili fupi Tusa? Unataja ulipo ili iweje? Ili waje? Unadhani akibanwa atashindwa kusema? Tumia akili wewe.
TUSA: Sawa nimekuelewa.
Tusa alikuwa hawezi kubishana na Patrick kwa kipindi hiki, alikuwa anakaa kimya tu.
Mara kuna mtu akawa anagonga mlango, Patrick akaenda kufungua na mtu huyo alikuwa ni Sele.
 
SEHEMU YA 28

Mara kuna mtu alikuwa anagonga mlango, Patrick akaenda kufungua na mtu huyo alikuwa ni Sele.
Patrick akafurahi sana kumuona Sele, wakakumbatiana na Patrick akamkaribisha Sele ndani, wakawa wanazungumza huku wanaingia ndani.
PATRICK: Dah ni siku nyingi sana, umerudi lini kaka?
SELE: Kitambo tu ndugu yangu, kuna matatizo yalinipata mjini mwenzio.
PATRICK: Yapi tena?
SELE: Nitakwambia tu ndugu yangu, vipi maisha maana na wewe umepotea sana.
PATRICK: Mi nipo mbona, sema niliweka maisha yangu pande za Arusha ila sasa nimerudi nyumbani.
SELE: Nimesikia umeoa kaka, vipi ndo umerudi moja kwa moja au utaenda tena Arusha?
PATRICK: Inategemea bhana, ila kweli nimeoa na nilimletea mama mke wangu ili nae amtambue. Tena alikuwa hapahapa, nadhani atakuwa chumbani sasa.
Patrick na Sele walikuwa sebleni wakizungumza, kwa kipindi hiki Tusa alikuwa anaogopa sana macho ya watu kwahiyo alipoona Patrick anaenda kufungua nae akainuka na kwenda chumbani, kwahiyo hawakumkuta pale sebleni.
SELE: Bora kaka umemleta tumjue shemeji yetu.
PATRICK: Ngoja nikamuite.
Patrick akainuka na kwenda chumbani kumuita Tusa na muda huo wakaingia ndani Deborah na Anna ambao walikuwa wametoka kidogo, nao wakafurahi kumuona Sele na wakasalimiana vizuri. Patrick nae akarudi,
PATRICK: Anakuja muda sio mrefu.
DEBORAH: Nani tena?
PATRICK: Mke wangu bhana, yupo chumbani ndo nimemuita aje amsalimie shemeji yake.
DEBORAH: Aah kumbe, loh! Umenishtua maana nilikuwa nawaza mengine hapa.
ANNA: Dada nawe mmh!!
Wakaendelea na maongezi ya hapa na pale.
Pamela akalazimishwa kumpigia simu mumewe tena na kumuuliza alipo Tusa, alipewa amri sasa na si ombi.
PAMELA: Ila mjomba bado sijaelewa, unamuhitaji mwanangu Tusa au dada yangu Fausta?
MASHAKA: nimekwambia mpigie mumeo sasa na umuulize.
PAMELA: Kwani mwanangu Tusa amekukosea nini jamani?
MASHAKA: Sihitaji mjadala, ninachotaka ni umpigie mumeo basi.
Pamela alikuwa anasita ila macho ya Mashaka yakamtisha, Pamela alitamani aongee na mumewe kwa njia ya mawazo ili asimtajie alipo Tusa.
Akapiga simu ambayo iliita bila kupokelewa, akajaribu tena na tena ila ikawa hivyohivyo, Mashaka akachukia sana.
MASHAKA: Mumeo nae ana kiburi eeh!
PAMELA: Hapana, hayupo hivyo unavyodhani.
MASHAKA: Na mbona hapokei simu?
PAMELA: Atakuwa mbali na simu.
MASHAKA: Unamtetea eeh! Haya mpigie Fausta sasa.
Pamela akashika simu na kumpigia Fausta ila hakupatikana.
PAMELA: Hapatikani.
MASHAKA: Tafuta mtu wa karibu yake umpigie na uulize alipo.
Ikabidi Pamela ampigie Tina na alifanya hivyo kwavile alijua wazi atapewa jibu kuwa Fausta kasafiri.
PAMELA: Tina, dada yangu yuko wapi?
TINA: Mamdogo, mama ameshasafiri. Vipi wewe uko wapi?
PAMELA: Nipo Arusha mwanangu, nahitaji maombi.
TINA: Vipi tena mamdogo?
Hiyo haikusikika kwani Pamela alishanyang'anywa simu na Mashaka.
PAMELA: Ila unanionea bure tu.
MASHAKA: Nitakuachia nikishajua Tusa alipo.
PAMELA: Ila Tusa ni mwanangu na mimi sijawahi kukufanyia lolote baya mjomba, unakumbuka ulipotoroka jela! Nani alikuhudumia? Nani alijua njaa yako kama sio mimi? Mbona wanipa malipo nisiyo stahili mjomba? Wewe ni ndugu yangu tu hata iweje itabaki kuwa hivyo, nihurumie basi, niache niwe huru. Mwanangu sijamuona na mateso nayapata, nionee huruma ndugu yangu.
MASHAKA: Maneno yako yananiingia vilivyo akilini mwangu, ila ngoja wakati wako bado.
Mashaka akainuka na kutoka nje huku akimuacha Pamela akiwa katika uchungu na lindi la mawazo.
Tusa akaamua kwenda huko sebleni alipoitwa, alipofika hakuamini macho yake kuiona sura ya Sele mbele yake.
Sele nae hakuamini kumuona Tusa, akajikuta akiinuka na kumfata Tusa alipo, alimshika mikono na kumuuliza,
"Tusa ni wewe"
Tusa aliitikia kwa kichwa tu, Sele alimkumbatia Tusa kwa nguvu huku akifurahi kumuona.
Wote pale sebleni walipigwa na bumbuwazi, Patrick akainuka na kuwafata.
PATRICK: Mbona sielewi? Kwani mnafahamiana?
Sele alijikuta akimuangalia Patrick kwa ghadhabu sana huku akikumbuka maneno aliyoambia na John kuwa itakuwa ni Patrick nduguye, Sele akamgeukia Patrick na kumwambia.
SELE: Huyu ni Tusa wangu.
PATRICK: Tusa wako? Wakati huyu ni mke wangu, vipi wewe?
SELE: Huyu ni wangu mimi na sio wewe Patrick.
Deborah na Anna wakausogelea mzozo.
DEBORAH: Mbona siwaelewi jamani, kwani nini Tatizo? Inamaana wote mmetembea na mwanamke mmoja au ni vipi?
Muda wote Tusa alikuwa akitokwa na machozi na baada ya dakika kadhaa akaanguka na kuzimia.
Ikabidi waache mzozo na kuanza kumuhudumia Tusa.
Maiko akaamua kumfata Pamela ili akamuhoji maswali mawili matatu kuhusu Mashaka.
MAIKO: Kwani Mashaka ni nani yako?
PAMELA: Mashaka ni mjomba angu.
MAIKO: Ni mjomba wako kabisa?
PAMELA: Ndio, yeye na mama yangu ni watoto wa baba mkubwa na mdogo kwahiyo ni kaka wa mama yetu.
MAIKO: Anataka nini kwako kwasasa?
PAMELA: Kaniambia anahitaji kichwa cha dada yangu, na kikubwa anataka nimwambie Tusa alipo.
MAIKO: Mmh! Mambo mengi ya kikatili nimefanya ila hili la sasa ni too much yani kwa ndugu kabisa duh!
PAMELA: Sasa utanisaidia?
MAIKO: Ngoja niongee na Mashaka ili nipime uzito wa maneno yako, ila dah! Ina maana Tusa nae ni ndugu?
PAMELA: Tusa ni mwanangu kwahiyo Mashaka atakuwa babu yake, hata nashangaa kwanini anamchukia mwanangu.
MAIKO: Nitakusaidia kitu dada, ila na wewe unatakiwa kunisaidia sawa?
PAMELA: Sawa niambie tu nami nitatekeleza.
MAIKO: Tulia kwanza, badae nitakufata kwaajili ya kunisaidia hicho kitu ila chunga sana usiseme Tusa alipo kabla sijakuruhusu mimi.
PAMELA: Nimekuelewa ndio.
Hata Pamela alishangaa kuongea vizuri na mtu katili kama Maiko, hakujua ni kitu gani Maiko anapanga kichwani mwake, na hakujua ataombwa kusaidia nini na Maiko ili nae apate kusaidiwa.
Tusa akiwa hospital, Deborah akaamua kumuita kwa pembeni Sele ili apate kuzungumza nae.
DEBORAH: Unajua Sele hali ya leo mmenishangaza sana, kwani na wewe huyu Tusa ni mkeo?
SELE: Hapana mamdogo ila mimi ndio nilistahili kumuoa Tusa na si Patrick.
DEBORAH: Mbona sielewi, kama wewe ndio ulipaswa kumuoa Tusa na mbona akaolewa na Patrick?
SELE: Mamdogo usitake kumtetea Patrick kwavile ni mwanao.
DEBORAH: Unanijua wazi mwanangu, huwa sina upendeleo wa namna hiyo. Hata wewe ni mwanangu pia, cha msingi unieleze ilivyokuwa na Patrick nae nitaongea nae ila kwasasa naomba nianze na wewe Sulemani.
Sele akaamua kumueleza Deborah kuanzia pale ambapo Tusa alienda Arusha kwa mara ya kwanza hadi yeye alipoteswa.
Kwakweli Deborah alihuzunika sana na hakufikiria kabisa kama Patrick anaweza kufanya kitu cha namna ile.
Mashaka alikuwa na simu ya Pamela na akaamua kujaribisha mwenyewe kumpigia mume wa Pamela.
Alipopiga sauti ya kike ikapokea, alikuwa ni bi.Rehema, alipokea kwavile ile simu iliita kwa muda mrefu na nia yake ni kutaka kuwaambia kuwa mwenye simu katoka na kuacha simu nyumbani, na alipoenda kupokea aliona ni Pamela anapiga kwahiyo hakuwa na wasiwasi wowote.
REHEMA: Hallow
MASHAKA: Mpe mwenye simu niongee nae.
Rehema alijikuta akiitikia kama mtu ambaye hajasikia vizuri na Mashaka aliendelea kumsisitiza kuwa ampe mwenye simu.
Ile sauti ilimtembelea kichwani na kugonga kama mwangwi, alijikuta akisema
"Mashaka!!"
 
SEHEMU YA 29

Ile sauti ilimtembelea kichwani na kugonga kama mwangwi, alijikuta akisema,
"Mashaka!!"
Mashaka nae alijikuta akikata simu baada ya jina lake kutajwa.
Rehema akaendelea kutafakari sauti ya Mashaka.
"Mashaka na simu ya Pamela? Amemkutia wapi? Sauti ile ni yake au ni mawazo yangu?"
Alijikuta akiwaza sana bila ya kupata jibu.
Tina alimkuta bibi yao huyo akiendelea kuwaza.
TINA: Bibi una nini?
Rehema akashtuka kutoka mawazoni na kumgeukia Tina.
REHEMA: Unajua sauti ya Mashaka naijua sana!
TINA: Mashaka yupi unayemuongelea?
REHEMA: Mashaka ni ndugu yangu kabisa, Pamela kampata wapi?
TINA: Mbona sikuelewi bibi?
REHEMA: Hata na mimi mwenyewe sielewi.
Tina akabaki akimshangaa tu bibi yao huyo aliyeonyesha kuchanganyikiwa kabisa.
Mashaka baada ya kukata ile siku akajikuta nae akijiuliza maswali mengi,
"ni nani huyu aliyeijua sauti yangu na kunitaja jina? Au atakuwa Fausta!"
Akaamua kumfata tena Pamela.
MASHAKA: Yani wewe Pamela unanidanganya kuwa dada yako hayupo kumbe yupo nyumbani kwako!
PAMELA: Nilichokwambia ni kweli, dada yangu hayupo nchini.
MASHAKA: Nani anayeweza kunitambua kwa sauti nyumbani kwako zaidi yake?
PAMELA: Hata yeye hawezi kukutambua kwa sauti, hatukukaa sana na wewe hata hivyo ulituacha tukiwa mabinti wadogo.
MASHAKA: Sasa nani anayeweza kunitambua mimi?
PAMELA: Sijui ni nani.
MASHAKA: Najua unanificha, nitaenda tu nyumbani kwako na kufyeka kicha cha dada yako.
PAMELA: Tafahari usifanye hivyo.
MASHAKA: Haina msamaha hii lazima Fausta aangamie.
Pamela alikuwa akitetemeka na kumuhofia dada yake.
Tusa akapata nafuu na kuweza kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Deborah hakutaka tena kusikia mabishano ya Sele na Patrick badala yake aliomba kukaa mwenyewe na Tusa, hakutaka tena kuona Tusa akiwa kama sehemu ya ugomvi baina ya Sele na Patrick.
Deborah akawaida dada zake ili waweze kuzungumzia mzozo uliokuwepo.
SELE: Mimi sina tatizo, ila kwakweli Patrick amenitesa sana jamani. Naumia moyoni, kaniibia Tusa wangu na pia akanipa mateso makubwa sana.
DEBORAH: Nasikia uchungu na masikitiko, yani Patrick unamdhuru nduguyo sababu ya mwanamke?
PATRICK: Hapana mama, sikutarajia iwe vile na wala sikufikiria kama Sulemani ndio Sele.
ANNA: Tofauti ya Sulemani na Sele ni nini Patrick? Mbona ni jina moja tu?
MARIUM: Hata hivyo jamani, ingawa amemtesa nduguye bila kujua ila kitendo alichofanya hakistahili kufanyiwa yeyote hata kama si ndugu.
Wote walikuwa wakimshambulia Patrick kwa maneno, ambaye alikuwa ameinama tu.
DEBORAH: Kikubwa kinachonisikitisha ni kuwa Patrick ametoa wapi ukatili wa namna hiyo? Ila najua muda ambao Tusa ataamua kusema basi ataeleza mengi tusiyoyajua.
SELE: Ila mngenipa Tusa wangu niende nae mamdogo.
DEBORAH: Huyu Tusa atabaki na mimi kwasasa, si wewe wala Patrick atakayeruhusiwa kumgusa.
Waliona ukatili wa Patrick ni ule wa kumtesa Sele tu, hawakujua kuwa Patrick kuna mambo mengi makubwa kayafanya.
Wakati yote yanaongelewa, hofu ya Patrick ilikuwa sehemu moja tu yani pale Tusa atakapoamua kusema ukweli wa mambo yote.
PATRICK: Naomba mnisamehe ndugu zangu, hasa wewe hapo Sulemani, nisamehe sana kaka. Ila hata hivyo Tusa ni mke wangu, mama unavyonifanyia sio fair.
DEBORAH: Hata kama Tusa ni mkeo, ila kwasasa nitakaa nae mimi. Atalala ninapolala na atakula ninapokula, Patrick unapaswa kuniheshimu kama mama yako, nafanya hivi kwa faida yako na ya wote hapa.
MARIUM: Kwakweli hawa watoto wametudhalilisha sana, wenzao wanatafuta maendeleo eti wao wanagombania mwanamke loh!
ANNA: Deborah endelea na msimamo huo huo hadi pale Tusa atakapoamua mwenyewe.
Deborah alijua lazima kuna kitu kinachomsumbua Tusa ndiomana aliamua kuwa nae karibu ili apate kusema, Tusa hakuweza kusema chochote tangu siku alipomuona Sele na kuzimia, alijikuta machozi yakimtoka muda wote, alikumbuka mambo yote mabaya aliyofanyiwa na Patrick. Machozi tu yalionyesha jinsi gani Tusa alivyo na maumivu moyoni kwakweli Deborah alimuhurumia sana.
Mashaka akamkaba sana Pamela ili ataje mahali ambako anaishi, wazo la Mashaka ni kuwa Fausta yuko nyumbani kwa Pamela.
MASHAKA: Yani usiponitajia kwako, nitaanza kukufyeka wewe.
PAMELA: Nihurumie jamani, kwangu kuna mume wangu na mama mkwe tu, utawaumiza bure hawahusiki na chochote.
MASHAKA: Nahitaji maelekezo ya nyumbani kwako, najua huko ndio nitampata na mumeo ambae atanipa maelekezo ya alipo Tusa.
Pamela alikuwa akikataa kutoa maelekezo ya nyumbani kwake, ila Mashaka akamkaba sana na mwisho wa siku Pamela akataja ilipo nyumba yao.
MASHAKA: Na ole wako maelekezo yasiwe sahihi, nitakufyeka kichwa chako mimi mwenyewe.
Pamela alikuwa akitetemeka tu.
Sele hakuridhishwa na maamuzi ya mamake mdogo wakati anajua wazi kuwa yeye na Tusa wanapendana, akajikuta akiwaza mambo mengi sana na kubwa zaidi ni kumrudisha Tusa kwenye himaya yake.
Alimuhurumia sana Tusa kwani hakuwa Tusa yule aliyemzoea, Tusa huyu alikuwa amekonda, amenyorodoka halafu alionekana kama kupungukiwa na akili, Sele alitambua kwamba yote yatakuwa ni sababu ya mateso aliyopewa na Patrick.
Sele alijisemea,
"Lazima nifanye kitu cha kumuondoa Tusa toka mikononi mwa Patrick, huyu Patrick si mtu mzuri kwasasa. Nitamkomboa Tusa wangu tu kwani bado nampenda"
Hali ya Tusa ilikuwa ni mbaya kwa mtu yeyote aliyemuona mwanzo, akimuangalia sasa anaweza kutokwa na machozi ndomana Sele aliumia sana.
Mashaka akamfata Maiko ili ampe maelekezo aende, safari hii Maiko akagoma ila baada ya kuombwa sana na Mashaka akaamua kukubali kwenda, ambapo alitakiwa kuondoka usiku wake na ndege.
Kabla ya kuondoka, Maiko alimfata Pamela na kumwambia.
MAIKO: Bado unahitaji msaada wangu?
PAMELA: Ndio, naomba unisaidie tafadhari.
MAIKO: Hakuna tatizo, mi ndio naenda nyumbani kwako hivi ila unatakiwa unifanyie kitu kimoja tu, ila ukishindwa nitafikiria cha kukufanya.
PAMELA: Kitu gani?
MAIKO: Nataka unitajie lilipo kaburi la mama yangu mzazi.
Pamela akashtuka na kujiuliza kuwa atalijulia wapi kaburi la mtu asiyemfahamu.
Kwakweli alijiona kushindwa mtihani wa ukombozi wake na hakujua hatma yake ni nini.
 
SEHEMU YA 30

Kwakweli alijiona kushindwa mtihani wa ukombozi wake na hakujua hatma yake ni nini.
Pamela akamwangalia tena Maiko na kumuuliza.
PAMELA: Nitalijulia wapi kaburi la mama yako mimi?
MAIKO: Wewe ni ndugu wa Mashaka au sio ndugu?
PAMELA: Mashaka ni ndugu yangu ndio.
MAIKO: Sasa utashindwa vipi kujua lilipo kaburi la mama yangu?
PAMELA: Siwezi kujua mimi, hata huyo mama yako simjui.
MAIKO: Mama yako wewe aliitwa nani na yuko wapi?
PAMELA: Mama yangu aliitwa Neema na ameshakufa, aliuwawa miaka ya nyuma huko.
MAIKO: Unajua kaburi lake lilipo?
PAMELA: Ndio najua.
MAIKO: Sasa kwanini hujui na kaburi la mama yangu lilipo? Nataka kuliona.
Pamela alimshangaa sana Maiko kwa kumsisitiza amwonyeshe vitu asivyovijua.
Adamu aliporudi kwake alimkuta mama yake akiwa na mawazo sana, akaamua kumuuliza.
Rehema akamueleza Adamu kuhusu sauti aliyoisikia wakati Pamela akipiga.
ADAMU: Mama, unauhakika?
REHEMA: Kabisa mwanangu nakwambia ukweli, nimeshangazwa sana na hata sielewi nini kinaendelea.
ADAMU: Au ni mawazo yako tu mama?
REHEMA: Si mawazo yangu ila ni ukweli mtupu.
Adamu akaamua kuchukua simu yake na kupiga ila iliita tu bila ya kupokelewa.
Adamu akabaki kushangaa kwanini simu haipokelewi.
ADAMU: Sasa mama hii inamaana gani?
REHEMA: Hata sielewi, tuseme Pamela kapatwa na matatizo Arusha au ni vipi? Na je huyo Mashaka amekutana nae wapi? Kama kweli ni Mashaka mbona akate simu aliposikia sauti yangu? Na je alikuwa anataka kusema nini? Inamaana nimechanganya sauti kweli? Mmh hata sielewi.
ADAMU: Sasa tutafanyaje mama?
REHEMA: Sijui mwanangu, inabidi tuchunguze na kufatilia. Mtafute tena mume wa Tusa labda tupate taarifa kidogo.
Adamu akaanza taratibu za kumtafuta Patrick hewani.
Sele hakuweza kutulia huku akijua Tusa anaumia, akaenda tena kwa mamake mdogo na safari hii akaamua tena kuishi hapo.
DEBORAH: Mbona nakuona na mabegi?
SELE: Kwani kuna ubaya mamdogo? Nimeamua kuishi tena hapa, siku ile niliondoka kwa hasira tu baada ya kurudi kwa bibi.
DEBORAH: Ila hapa hali si shwari, mbona mtanipa mawazo jamani!
SELE: Mamdogo usijari, moyo wangu umekubaliana na hali halisi kuwa Tusa kashaolewa na Patrick, ingawa nampenda Tusa ila sina la kufanya.
DEBORAH: Kama umeridhia hakuna tatizo, ila mimi bado sijaridhika hadi pale Tusa atakaposema.
SELE: Namjua Tusa mamdogo, ataongea tu ila naona sasa amechanganywa na mambo.
DEBORAH: Analia muda wote hadi huruma, sijui Patrick amemfanya nini mtoto wa watu. Amefika hapa akiwa hoi kwani mimba ilitoka.
SELE: Dah ilikuwa ni mimba yangu hiyo mamdogo.
Sele aliumia sana moyoni mwake alipogundua kuwa mimba aliyompa Tusa imetoka, laiti angejua ilitolewa na Patrick angeweza kumchukia maradufu.
Sele aliamua kuishi hapo ili aweze kufanya mpango wa kutoroka na Tusa, na safari hii alipanga kwenda nae mbali zaidi.
Mashaka hakutaka kupokea tena simu ya Pamela, kwani alijua kuwa akipokea atamshtua Fausta na kutoroka.
Mashaka akaendelea kumlazimisha Maiko aende kwenye tukio ila Maiko alionyesha kukawia kwavile alitaka apewe jibu na Pamela kwanza.
Mashaka akachukia na kuamua mwenyewe kupanga safari ya kwenda nyumbani kwa Pamela, nia yake kubwa ni kumkamata Fausta kwa mikono yake mwenyewe.
Maiko akaachiwa jukumu la kumpata Tusa, akamfata Pamela na kumuuliza.
MAIKO: Je unajua alipo binti yako?
PAMELA: Sijui chochote kwakweli.
MAIKO: Mi najua alipo.
Pamela akashtuka na kujua mwisho wa bintiye umefika.
MAIKO: Umekataa kunionyesha kaburi la mama, mimi naenda kukuonyesha binti yako halafu nitamchukua mbele ya macho yako.
PAMELA: Usinifanyie hivyo tafadhari.
MAIKO: Kesho wakati Mashaka anaenda Dar, mimi wewe na kundi langu tutakuwa Mwanza kwaajili ya Tusa.
Pamela akaogopa sana, roho ilimuua alijikuta akimlilia mtoto wake Tusa, na hakujua kwanini hawa makatili wanataka kumchukua Tusa, alijiuliza maswali mengi kuwa Tusa amewakosea nini.
PAMELA: Mwanangu hana hatia.
MAIKO: Mwanao ana tamaa ndio iliyomponza, hukusoma ile methali ya kuwa ukitaka uzuri sharti udhurike?
PAMELA: Hata kama, ila mwanangu inaonyesha ameshateseka sana.
MAIKO: Kiasi tu, hapa tunachomtakia Tusa kwa sasa ni kumuumiza moyo Patrick, ametulaghai, ametusaliti na kutudanganya kwaajili ya Tusa. Lazima Tusa arudi mikononi mwetu ili Patrick atambue umuhimu wetu, hata hivyo Tusa bado hajalipia gharama tulizotoa kama mahari yake, hata na wewe mama yake unahusika. Ila kwasasa tunayemtaka ni Tusa.
Pamela hakuelewa kitu kabisa, jioni yake Maiko na baadhi ya vijana wakajiandaa kwaajili ya safari ya kwenda Mwanza kumsaka Tusa.
Patrick nae alijikuta akijipanga kurudi Arusha ili akakabiliane na wakina Maiko na kuacha kazi rasmi kabla mama yake hajagundua chochote, muda wote Patrick alionekana yuko kwenye mihangaiko, nyumbani alionekana usiku kwa usiku, hakuna aliyejua Patrick anapanga mambo gani au anataka kufanya nini ila alijua yeye na nafsi yake tu.
Kutokana na Patrick kutokupatikana nyumbani ilimfanya Deborah kukosa muda wa kuzungumza nae na pia kuwa na mashaka na mtoto wake huyo kwani hakumuelewa kabisa anapanga vitu gani.
Patrick alikuwa na mawazo mengi kichwani ikiwemo na wazo la kumtoa Tusa mikononi mwa mama yake kwani hakuwa na uhuru nae tena ingawa alikuwa mkewe.
Mashaka aliingia ndani ya jiji akiwa na watu wake wawili aliofatana nao.
Akafata yale maelekezo aliyopewa na Pamela na kweli alifika kwenye nyumba hiyo, wale watu wawili walikaa pembeni kwanza.
Mashaka alienda yeye mwenyewe alitaka aonane macho kwa macho na Fausta.
Akagonga mlango, Rehema akiwa amebaki mwenyewe ndani akaenda kufungua.
Macho ya Mashaka yakagongana na macho ya Rehema.
 
SEHEMU YA 33

Fausta alivyofika nje alishtushwa sana kumuona mgongaji, alijikuta akisema kwa taharuki,
"Maiko!!!"
Maiko alikodoa macho kwani hakudhani kama angekutana na Fausta mahali hapo, na hakujua kuwa Fausta anayetafutwa na Mashaka ndio yuleyule anayemjua yeye.
FAUSTA: Ona ulivyokodoa macho kama fundi saa, katika wanaume ninao wachukia hapa duniani wewe unaongoza Maiko.
MAIKO: Ni haki yako kusema hayo yote uyasemayo, najua unavyoumia Fausta.
FAUSTA: Unajua maumivu ya mtoto wewe Maiko? Unajua mtoto anavyouma wakati wa kujifungua? Sikufikiria kama wewe ni gaidi kiasi kile na sikudhani kama ungenifanyia unyama ule Maiko.
MAIKO: Yote nakubali Fausta ila huu si muda muafaka wa kuzungumza hayo, napenda kukuokoa sasa.
FAUSTA: Kwenda zako huko, sipendi hata kukuona nahisi kichefuchefu. Na kama umepanga kuniua, nimalize tu sikuogopi wala nini.
Maiko akaanza kuondoka akiwa amenywea sana. Fausta aliendelea kubwabwaja maneno kama vile amemeza kanda, aliongea bila kumeza mate tena aliongea kwa hisia na hasira.
FAUSTA: Wewe Maiko sio binadamu kabisa, wewe ni mnyama tena shetani wa mashetani, narudia tena sikuogopi ukitaka kunimaliza njoo tu unimalize, wewe si gaidi bhana, njoo unimalize. Siwezi kusahau unyama uliofanya kwa mwanangu, Maiko sitakusahau wala kukusamehe hadi naingia kaburini najua ni Mungu tu ndiye atakayenilipia, mabaya uliyoyafanya kwangu hayatasahaulika kamwe. Shetani mkubwa wewe, hata sijui umetokea wapi leo.
Ingawa Maiko alikuwa ameshaondoka, Fausta hakuacha kuongea, aliongea sana na mwisho wa siku alijikuta akikaa chini na kuanza kulia, alikuwa akilia na kuomboleza.
Maiko aliondoka na Yuda, huku akiwa na mawazo mengi sana.
YUDA: Bosi, mbona siwaelewi jamani? Nilipokuja na Mashaka nae akakutana na mtu anayemfahau, leo tena na wewe, vipi tena kwani yule ni nani yako?
MAIKO: Kwakweli nilikuwa shetani sana si uongo wala utani, hata mimi maneno yake yameniingia sana. Ushetani wa Mashaka sasa ulikuwa ndani yangu, nimetesa watu wengi sana, nimeua sana, hadi sasa sina mtoto kabisa. Fausta aliwahi kuwa mwanamke wangu, ila nilimtenda vibaya sana sidhani kama anastahili adhabu ya Mashaka.
YUDA: Inamaana wakati Mashaka anakwambia kuwa anataka kumuua Fausta, wewe hukujua kama ni Fausta yule?
MAIKO: Kwakweli sikujua, na wala sikutambua kama leo ningekutana na yule mwanamke. Yuda, wewe ni mgeni kwenye kazi hizi, tukirudi Arusha nitakupeleka kwenye chumba changu maalum ukaone, hapo utaelewa kwanini yule mwanamke amesema vile.
YUDA: Sawa, na Mashaka je utamwambiaje?
MAIKO: Kuhusu Mashaka usijari, najua jinsi ya kufanya hawezi nisumbua kitu. Ila leo dah, nilikosa cha kusema mbele ya Fausta, sikujipanga kukutana nae, sikupanga kumuona dah!! Nimejikuta roho ikiniuma sana leo sijui kwanini jamani!! Siku zote huwa sijihisi kuwa na hatia, ila leo mmh!!
Maiko alionekana kuguswa sana na maneno aliyoongea Fausta.
Pamela naye alitafakari sana mambo aliyomfanyia mwenzie, alijiona kuwa na makosa makubwa sana.
PAMELA: Debo, nakubali makosa ila naomba unieleweshe kitu kimoja.
DEBORAH: Kitu gani?
PAMELA: Patrick umezaa na nani?
DEBORAH: Hayakuhusu.
PAMELA: Nauliza nikiwa na maana Debo, kama Patrick ni mtoto wa Jumanne basi Tusa atakuwa dada yake.
DEBORAH: Jumanne nilizaa nae mtoto mmoja tu ambaye ni yule Jasmine wangu aliyefanana kila kitu na Tusa, (akainama kidogo kufuta machozi), haya ya Patrick hayakuhusu, niachie mwenyewe na moyo wangu.
PAMELA: Mmh!! Kwani ulibakwa?
DEBORAH: Pamela usitake kuniudhi tafadhari, nishakwambia hayakuhusu sasa chokochoko za nini?
PAMELA: Nisamehe tafadhari, sitarudia tena.
DEBORAH: Sina sababu ya kutokukusamehe mtu kama wewe usiyejielewa, ila kumbuka kuwa chochote ulichomtendea mwingine, utarudishiwa kwa namna tofauti. Wengine husema, what goes around comes around. Mimi sikuhukumu wala nini, ila niliongea kwa hasira tu ukizingatia mapito niliyopitia ni mengi. Sina baya na wewe na wala sina sababu kubwa ya kukuchukia.
PAMELA: Asante Debo kwa msamaha wako.
DEBORAH: Ila kikubwa, nitapenda Jumanne aje kwa miguu yake mwenyewe huku Mwanza kukufata.
PAMELA: Hilo halina tatizo Debo, cha muhimu ni kuishi kwa amani.
Ingawa Deborah aliongea mengi ila kidonda chake moyoni bado kilimuuma sana.
Pamela nae hakumshangaa sana Deborah kuhusu Patrick kwani hata dada yake Fausta hakumjua mtu aliyezaa nae mtoto wake Tina.
Tina aliyekuwa ametoka kidogo, aliporudi pale kwa Adamu, akamshangaa mama yake aliyekuwa chini akilia sana, Tina akamsogelea na kumuita "mama"
Fausta aliinua macho yake na kumtazama Tina, akamkumbatia kwa nguvu huku akiendelea kububujikwa na machozi.
TINA: Una nini mama yangu?
FAUSTA: Tina mwanangu, dunia ni duara na binadamu wote hukutana humo. Leo nimetembelewa na shetani.
TINA: (Aliuliza kwa mshangao), shetani!!
FAUSTA: Ndio, shetani alikuja leo.
Tina alihisi mama yake ameanza kuchanganyikiwa kwani hakufikiria kama mtu unaweza kumuona shetani kwa macho ya kawaida.
TINA: Mama, mbona sikuelewi?
FAUSTA: Nimetembelewa na baba yako Tina, alimuua pacha wako mbele ya macho yangu. Unajua alimfanyaje?
TINA: Mmh!! Alimfanyaje mama?
FAUSTA: Alimuua, alimchukua akam....
Aliangusha kilio kikubwa kabla ya kumalizia kauli yake, alikuwa akilia sana, "mwanangu mimi, mwanangu jamani"
Tina alijikuta akilia na mama yake, alimuonea huruma sana.
Tusa alikuwa bado hajauelewa vizuri uhusiano wa mama yake na Deborah, alipokuwa akitafakari alifatwa na Sele.
SELE: Tusa, hapa ni swala moja tu.
TUSA: Swala gani?
SELE: Inatakiwa tutoroke hapa, sidhani kama hapa ni mahali sahihi pa kuishi.
TUSA: Na mama yangu je?
SELE: Mama yako hakuna tatizo Tusa, yeye yuko salama na mamdogo ila wewe hauko salama Tusa, sidhani kama Patrick ni mtu sahihi kwako.
TUSA: Kwanza futa hiyo kauli kuwa Patrick ni mtu, Patrick si mtu kabisa, Patrick hata sijui nimfananishe na mdudu gani hapa duniani. Amenifanyia mambo mabaya sana sijawahi kufikiria kama ningefanyiwa vile.
Tusa akainama na kuanza kulia, Sele akamsogelea karibu na kuanza kumbembeleza.
Patrick akarudi na kumkuta Sele akimbembeleza Tusa, Patrick akapatwa na hasira za ajabu.
Akaingia ndani bila kuwasemesha, wote wawili hawakujua ni kipi kingewapata Patrick atakapo toka nje, walichofanya ni Sele kuondoka na Tusa kwenda alipo Deborah kwani ndio mtu pekee anayesikilizwa na Patrick.
Walipofika Arusha, Maiko kama alivyomuahidi Yuda, akampatia funguo zake za chumba cha siri aende akatazame.
Yeye alienda kuzungumza na Mashaka ili aweze kuweka mambo sawa kabla Mashaka hajaamua kumdhuru Fausta.
Wakiwa katika maongezi mara Maiko alimuona Yuda akija na ghadhabu nyingi usoni.
Moja kwa moja Yuda alienda kumkaba Maiko huku akiwa na hasira kali.
 
SEHEMU YA 34

Moja kwa moja Yuda alienda kumkaba Maiko huku akiwa na hasira kali.
YUDA: Kwanini umemuua baba yangu Maiko?
Maiko kabla hajajibu, alishtukia akipigwa ngumi ya sura.
YUDA: Kwanini Maiko? Kwanini umemuua baba yangu?
Maiko akapigwa ngumi nyingine na kujishtukia akiwa chini, Mashaka akaenda kumshika Yuda, nae akashindiliwa ngumu. Mashaka akapatwa na hasira ilibidi awaite vijana wake wengine kuja kumkamata Yuda, wakafanikiwa kumfunga kamba kwavile walikuwa wengi kwahiyo wakamzidi nguvu.
Mashaka alimfata Maiko pale chini,
MASHAKA: Dah! Pole sana mwanangu, hujaumia kweli?
MAIKO: Nadhani alitaka kuniua huyu.
MASHAKA: Ila imekuwaje kwani?
MAIKO: Sijui, labda kuna kitu kakiona kwenye kile chumba changu cha siri maana nilimpa funguo.
MASHAKA: Hilo ni kosa kubwa sana Maiko, unadhani tufanyeje na mtu huyu?
MAIKO: Ilimradi mmemfunga, hata msiangaike nae, niachieni mwenyewe nitajua namna ya kutatua hili tatizo.
Maiko akajua sasa ameingia kwenye matatizo mengine, ukiachana na yale ya Patrick na Tusa.
Bi.Rehema aliamua kurudi jijini baada ya kuona ukimya toka kwa Fausta.
Alipofika alimkuta Fausta akiwa amenyong'onyea sana, wakasalimiana na kuongea mawili matatu.
REHEMA: Mwanangu nini tatizo kwani?
FAUSTA: Wakati haupo mama, alikuja hapa mwanaume. Mwanaume ambaye ni gaidi, mwanaume ambaye ni shetani, mwanaume ambaye hastahili kuwepo katika jamii.
REHEMA: Mwanaume gani huyo?
FAUSTA: Mwanaume aitwaye Maiko, aliua mwanangu mbele ya macho yangu mama. Siwezi kumsahau mwanaume huyu.
Fausta alianza kulia, Rehema alimbembeleza huku akiwaza moyoni kuwa huenda akawa Mashaka ila jina la Maiko lilamchanganya kwani aliona kuwa atakuwa mtu mwingine na si Mashaka.
REHEMA: Yukoje huyo mwanaume?
FAUSTA: Ukimuona unaweza sema ni mtu mstaarabu na mwenye heshima zake ila kiukweli ni shetani.
REHEMA: Au ni Mashaka?
FAUSTA: Mashaka? Hapana anaitwa Maiko, kwani Mashaka ndio nani?
REHEMA: Mashaka ni kaka yangu, ila nae ni shetani kama huyo mwanaume uliyemtaja. Kanipotezea wanangu wawili, hafai hata kuonekana. Ila yeye ukimuona unaweza kuhisi tu kuwa ana roho mbaya, msura wake kama alidumbukizwa kwenye tindi kali, macho yake kama ya mmbwa mwizi kiukweli hafai kabisa. Naye alikuja hapa wakati nyie wote hampo.
FAUSTA: Mama, basi hapa hapafai inabidi tujihadhari jamani. Kama watu wa ajabu kiasi hiki wanafika hapa basi maisha yetu yapo hatarini hasa ya mtoto wangu Tina.
REHEMA: Tufanyeje sasa?
FAUSTA: Tuhamie kwangu, nyumba hii ifungwe tu hadi pale kaka ataporudi.
REHEMA: Mmh!! Tumngoje basi siku mbili hizi arudi ndio tuhame.
Rehema nae akaanza kuingiwa na hofu mahali hapo.
Tusa akiwa mikononi mwa Deborah, Patrick alimfata mahali hapo.
PATRICK: Mama, hivi hii ni haki kweli? Yani mke wangu anakataziwa kukaa na mimi ila Sulemani anakaa nae, anambembeleza na kila kitu.
DEBORAH: Mmh! Acha jazba mwanangu, Tusa ni mkeo usiwe na hasira hivyo.
PATRICK: Mama, sipendi kumdhuru mtu ila msitake nifanye hivyo. Mwambie Sulemani acheze na vyote lakini asicheze na mke wangu, nitamuumiza.
Deborah alikuwa na wakati mgumu sana juu ya kusuluhisha hili swala.
Kwavile Tusa alikuwa kawaida sasa ikabidi amuulize,
DEBORAH: Niambie maisha ya Arusha Tusa.
TUSA: Yalikuwa kawaida tu mama.
DEBORAH: Kawaida! Kweli? Mbona unamuogopa sana Patrick? Nakuona kila muda anapokuja huwa unakosa raha, kwanini?
TUSA: Hakuna tatizo mama.
DEBORAH: Hutaki kusema sio! Mmh! Mficha maradhi kifo humuumbua, unaijua hiyo methali?
TUSA: Ndio naijua.
DEBORAH: Kwanini unanificha Tusa? Niambie ukweli, mi namjua sana Patrick, ukiniambia nitajua cha kufanya, niambie mama. Acha kuficha ficha.
Tusa aliinama na kuanza kulia, Deborah akafanya kazi ya kumbembeleza.
DEBORAH: Niambie ukweli nikusaidie mwanangu.
TUSA: Ni mambo ya aibu sana, hayafai hata kueleza.
DEBORAH: Mmh! Mambo gani hayo? Niambie tafadhari.
TUSA: Nitakwambia mama.
Akaendelea kulia tu, Deborah akatambua kuwa ni kitu kizito sana kilichomsibu Tusa, ila Deborah alitaka kujua kwa haraka ili kama ataweza kudhibiti basi adhibiti swala hilo.
Maiko akamfata Yuda kuzungumza nae.
MAIKO: Yuda Yuda, hii ni himaya ya watu wengi tena wenye uwezo mkubwa. Huwezi fanya chochote hapa, kama una roho nyepesi ni bora usingeenda kwenye kile chumba.
YUDA: Sikia Maiko, hata ingekuwa ni wewe ungeumia tu, yani kuona baba yako alichinjwa dah! Nyumbani tulizika mwili kumbe kichwa unacho wewe Maiko!! Dah, sikujua kama kazi zenu zipo hivi jamani.
MAIKO: Sikia Yuda, maji yakishamwagika hayazoleki cha msingi ni kukubaliana na matokeo na kusonga mbele.
YUDA: Poa bhana, mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Sawa bhana.
MAIKO: Unatakiwa kuwa mpole tu bwana Yuda.
Ikabidi Yuda awe mpole kweli ili aweze kufunguliwa na kwenda kupanga plan zingine.
YUDA: Nifungueni basi.
MAIKO: Nitakufungua endapo utaahidi kutoleta fujo tena.
YUDA: Ilikuwa hasira tu zile, haitajirudia bosi.
Vijana wa Maiko wakamfungua Yuda kama walivyoamriwa na Maiko.
Kwakweli Yuda aliumia sana na kujiapiza moyoni kuwa lazima alipe kisasi.
Adamu aliporudi nyumbani kwake akasimuliwa mikasa yote iliyowakumba mahali hapo.
ADAMU: Duh hii khatari, lazima tumdhibiti huyo Maiko jamani.
REHEMA: Na Mashaka mwanangu nae anatakiwa adhibitiwe.
ADAMU: Mama, usijali nitatuma wapelelezi waweze kuchunguza hao watu.
REHEMA: Utawezaje mwanangu?
ADAMU: Mama usijari, mimi ni khatari ila watu hawanijui tu. Nitawapata hao mabwege nazi.
FAUSTA: Itakuwa vizuri kaka, hayo majitu yatakuwa mashetani tu.
Fausta alichukizwa sana na Maiko, alitamani hata ampate amchinjilie mbali.
Mpango wa Yuda ilikuwa ni kumteketeza Maiko pamoja na Mashaka ila akajua peke yake hawezi kitu, akaamua kusafiri ili arudi kwao amuombe ndugu yake ambaye aliambiwa kuwa amesharudi, wakashirikiane kumtokomeza Maiko, Yuda alikuwa na hasira sana.
"Haiwezekani, yani tumekazana kumjua aliyemuua baba kumbe ni huyu baladhuri!! Sisi tunazika mwili halafu kichwa anacho yeye!! Lazima nimfunze adabu Maiko, na lazima nae afe tu, kama asipokufa yeye safari hii basi nitakufa mimi, dah! Maiko ni shetani sana jamani"
Yuda alijikuta akimchukia sana Maiko, alimchukia kupita maelezo.
Sele aliandaa mipango yake vizuri na moja kwa moja wazo lake lilikuwa ni kumtorosha Tusa.
Siku hiyo alilala nyumbani kwa Deborah na kama alivyopanga na Tusa, usiku wakati watu wote wamelala, Tusa akatoka na kumuacha Deborah na mama yake wakiwa wamelala na kumkuta Sele akiwa anamngoja sebleni.
Wakautumia muda huo kutoka pale ndani, wakiwa wanatokomea gizani machale yakamcheza Patrick na kujikuta akishtuka kwa nguvu.
Patrick akatoka nje na kuona watu wawili wakipotelea gizani, Patrick akapatwa na wasiwasi. Hapohapo akaamua kuwafatilia kwa nyuma ili kujua ni wakina nani.
 
SEHEMU YA 35

Hapo hapo akaamua kuwafatilia kwa nyuma ili kujua ni wakina nani.
Patrick alipowanyatia karibu, moja kwa moja akagundua kuwa ni Sele na Tusa.
Jambo la kwanza alilofanya ni kumkaba Sele kwa nyuma, alipomgeuzia mbele akampiga ngumi ya sura iliyompeleka Sele hadi chini.
Sele akainuka na kupewa ngumi nyingine na hapo kuanza kupambana na Patrick.
Tusa akaona hiyo ni vita kubwa, ikabidi akimbie kuwaamsha Deborah na mama yake, kwakweli nao walishangaa kuwa imekuwaje, wakakimbilia eneo la tukio na kumkuta Patrick akimshambulia Sele kwa ngumi zisizo na idadi.
Debora alijikuta akiweka mikono kichwani,
DEBORAH: Wee Patrick wewe utamuua mwenzako.
Akawasogelea kuweza kuwaamulia, Sele nae hakukubali akampiga ngumi Patrick wakati ameshikwa na Deborah, kitendo hicho kilimkera Patrick na kutaka kuchomoka mikononi mwa mama yake huku Pamela akimuondoa Sele.
PATRICK: Niache mama, niache nimfunze adabu huyu.
DEBORAH: Sikuachi Patrick, ukitaka nipige mimi. Naomba hasira zako zote umalizie kwangu maana nadhani ndio malipo ulioamua kunipa kwa kukulea mwanangu. Nipige baba.
Patrick akajisikia vibaya kwa kilio na maneno ya mama yake, ikabidi atulie na wote wakarudi nyumbani.
Kwavile Patrick alikuwa na nguvu sana, alijikuta amemuumiza sana Sele aliyekuwa akivuja damu.
Patrick alipomuangalia nduguye huruma ilimshika akaamua kumfata na kumuomba msamaha.
PATRICK: Nisamehe ndugu yangu.
Sele alimuangalia tu Patrick bila kusema chochote, humo ndani hawakuweza kulala tena hadi kunakucha wakijadili yaliyotokea, aliyerudi kulala ni Patrick tu baada ya kumuomba msamaha Sele, ila hawakujua kama huyo Patrick amelala kweli au anapanga mipango yake.
Maiko akiwa amefatwa na Mashaka kuhusu Fausta.
MASHAKA: Unajua sikukuelewa mwanangu, umesema Fausta kafanyaje?
MAIKO: Unapenda niendelee kuwa mshirika wako?
MASHAKA: Ndio napenda tena sana Maiko.
MAIKO: Basi achana na Fausta, nakuomba swala la Fausta niachie mimi.
MASHAKA: Kivipi wakati mi nahitaji kichwa chake?
MAIKO: Unaniamini au huniamini?
MASHAKA: Nakuamini mwanangu.
MAIKO: Basi swala la Fausta niachie mimi halafu utaona.
MASHAKA: Hivi yule Yuda alipatwa na nini?
MAIKO: Jinga lile, eti aliona kichwa cha baba yake ndo linaleta fujo zake hapa. Ila lishapotezea kwa sasa.
MASHAKA: Kweli ni jinga, nadhani alikuwa hajui kazi vizuri yule. Sasa vipi kuhusu Tusa.
MAIKO: Dah! Sasa hayo ndio mambo ya kujadili bhana.
Maiko akamueleza Mashaka na jinsi walivyompoteza mama yake na Tusa.
MASHAKA: Dah! Hilo ni kosa ila sio kubwa sana. Tatizo langu sasa ni kuwa, huyu Patrick ni mtu wa aina gani hadi anaweza kucheza na hisia zetu kiasi hiki? Mwanzoni katulaghai wote akatoroka na Tusa, na sasa katoroka na Pamela. Hivi huyu Patrick ni nani haswa!!
MAIKO: Hata na mimi namshangaa.
MASHAKA: Nadhani tufanye operesheni ya kumsaka yeye kwanza, na tukimpata kichwa chake tutakitunza kama kumbukumbu.
Mashaka na Maiko wakaanza kufanya harakati za kumpata Patrick.
Kulipokucha Patrick akamfata mama yake na kuongea nae.
PATRICK: Yote haya mama umeyataka wewe, ungeniachia mke wangu isingekuwa hivi.
DEBORAH: Nitakuachia mwanangu, ila hukupaswa kumpiga mwenzio sababu ya mwanamke.
PATRICK: Yani ulitaka nimuangalie tu wakati anatoroka na mke wangu? Mama, mke anauma sana.
DEBORAH: Hata kama, ila ulichofanya hakistahili kabisa.
Patrick akamuaga mama yake na kutoka, ikabidi Deborah amuulize vizuri Tusa juu ya kilichosibu.
Tusa hakuwa na jinsi zaidi ya kusimulia yaliyotokea usiku uliopita.
DEBORAH: Niambie ukweli Tusa, unampenda Sele au Patrick?
TUSA: Kwakweli mama nampenda Sele.
DEBORAH: Sasa mbona ukaolewa na Patrick? Hukujua madhara ya kuolewa na mtu usiyempenda?
TUSA: Patrick alinilazimisha tu, kwakweli simpendi Patrick mama.
DEBORAH: Unajua sheria za ndoa Tusa? Tatizo mnaolewa mkiwa wadogo jamani, hapo ulipo hata huelewi haki yako ni ipi. Unatakiwa umuheshimu mumeo, umpende na kumjali. Sasa kama wewe humpendi Patrick, siku zote hizo umeishi nae vipi?
TUSA: Mmh! Mama ni aibu.
DEBORAH: Hata kitendo cha kutoroka na mwanaume mwingine wakati mumeo yupo ndani ni kitendo cha aibu, ni bora kuniambia ukweli wa mambo yote.
TUSA: Ila mama, niahidi kuwa utanilinda.
DEBORAH: Usijali Tusa, cha muhimu ni kuniambia ukweli tu na siku zote ukweli huweka huru.
Mara Pamela akawafata Deborah na Tusa kwenye mazungumzo yao, nia ya Pamela ni kupata mawasiliano ya nyumbani kwake ili wasiwe na hofu tena.
Adamu akiwa na familia yake wakijadili.
ADAMU: Na bora haya mambo yametokea wakati watoto wangu wale wadogo wanasoma bording, maana tungepata shida dah!
TINA: Bora kabisa mjomba walivyoenda shule za bweni maana wanavyompenda mama yao sidhani kama wangevumilia kuona hata hakuna habari kuhusu yeye.
ADAMU: Na nimefanya vizuri kweli, maana likizo wanaenda kwa shangazi yao kulekule hadi nikawachukue.
Mara simu ya Adamu ikaanza kuita, kuangalia ni namba ngeni.
PAMELA: Mimi ni Pamela mume wangu.
ADAMU: Pamela! Uko wapi wewe?
PAMELA: Nipo Mwanza na Tusa.
ADAMU: Sasa mbona hamrudi nyumbani.
PAMELA: Kuna matatizo kidogo Adamu, itabidi uje kutufata.
ADAMU: Matatizo gani tena?
PAMELA: Ukija utajua tu, ila unatakiwa uje Adamu.
ADAMU: Sawa, utanipa maelekezo basi.
PAMELA: Hakuna tatizo, ni wewe tu kunitajia kuwa lini utakuja.
Simu ilipokatika kila mmoja ndani alikuwa na hamu ya kugundua ni kitu gani kinaendelea, ikabidi Adamu awaeleze vile alivyozungumza na Pamela.
REHEMA: Inamaana utaenda mwenyewe?
ADAMU: Ndio mama.
REHEMA: Tutaenda wote mwanangu, sitaweza kukungoja hapa. Twende wote hukohuko.
TINA: Hata na mimi mjomba nataka twende wote, nimemkumbuka sana Tusa.
FAUSTA: Halafu hapa mmuache nani? Hata na mimi nitaenda huko Mwanza.
ADAMU: Hebu acheni kunichekesha jamani, mmekuwa kama watoto wadogo bhana. Kwani mama tatizo ni nini? Mi si ninaenda na kurudi nao jamani! Na wewe Tina vipi? Kama Tusa si nitarudi nae! Na wewe Fausta, huko China kwako huendi tena?
FAUSTA: Siwezi kwenda hadi nimpate Pamela, ndomana nataka twende wote huko ili niondokee huko huko.
TINA: Mjomba, mi ndo hata sibaki tutaenda wote tu.
ADAMU: Mmh!! Haya majaribu, na kule tutafikia wapi sasa?
FAUSTA: Hotelini, ila kama huwezi waambie waje wao.
ADAMU: Wamesema wana matatizo jamani, ila nitajaribu kumuelewesha Pamela kama ataelewa.
Rehema ndio hakutaka kabisa kubaki mahali hapo mwenyewe kwani alihisi Mashaka anaweza kurudi tena, na jinsi alivyokuwa na hasira nae anaweza hata akamchoma kisu na kujitafutia kesi ya mauaji bure.
Mashaka na Maiko wakaanza kuandaa vijana kwaajili ya kwenda nao kumshambulia Patrick.
MASHAKA: Patrick anaonekana kuwa ni kijana mjanja sana, inabidi tutumie ujuzi na uzoefu kwa sana kumshika.
MAIKO: Tumepata vijana wa kutosha, sidhani kama atatushinda na kipindi hiki.
MASHAKA: Mazoezi ya kutosha kwa vijana hao, hakuna kumkosa Patrick.
Wakaendelea kupanga mpango kabambe wa kumkamata Patrick, ila hawakujua kuwa Patrick nae ana mipango yake jijini Mwanza.
Yuda akarudi kwao na kumkuta ndugu yake akiwa ameumizwa sana.
YUDA: Vipi kaka, nani amekutenda hivi?
SELE: Ni Patrick bhana, eti kisa mwanamke tena mwanamke mwenyewe kamuiba toka kwangu.
YUDA: Dah! Pole sana, nadhani Patrick amekuwa na nguvu sana kwasasa.
SELE: Patrick ni jambazi, ila watu wengi hawajui.
YUDA: Dah! Kuna kitu kaka ilitakiwa tukakifanyie kazi, ila kwavile umeumia sitakwambia nitangoja upone. Umesema Patrick ni jambazi?
SELE: Patrick ni jambazi ndio, ila nitapambana nae tu. Siachi kupambana nae hadi nipate haki yangu. Hivi na wewe Yuda, kipindi chote hiki ulikuwa Arusha? Ulikuwa unafanya nini huko?
YUDA: Mambo makubwa kaka, ila sikuwa Arusha kipindi chote. Nilikuwa Mombasa nafanya biashara na baadae nikapata kazi Arusha, ila niliyoyakuta huko!! Mmh nitakusimulia ukikauka vidonda.
Yuda aliendelea kutafakari kauli ya Sele kuwa Patrick ni jambazi, Yuda akaona kuwa anaweza kufanya ushirika mzuri na Patrick ukizingatia baba yao alihusika pia na wakina Patrick.
Patrick hakuwa na baba ila baba yao na wakina Sele ndio alikuwa kama baba yake kwahiyo uchungu wa Yuda na Sele juu ya mzee huyo utakuwa sawa na kwa Patrick, Yuda alifikiria hilo jambo akaona ni vyema akamshirikishe huyo Patrick.
Yuda akaenda kuonana na Patrick sasa ili amueleze kuhusu mzee wao.
Alipofika nje akamkuta Deborah na Pamela wakiongea, akawasalimia na kuongea mawili matatu na Deborah, halafu Deborah akamuelekeza Pamela kuwa Yuda pia ni mtoto wa Mariam yaani mdogo wake Sele.
Baada ya hapo, Yuda akamuulizia Patrick.
DEBORAH: Yupo chumbani kwake, nenda tu utamkuta.
Yuda akaenda chumbani kwa Patrick.
Jambo alilolikuta humo lilimfanya Yuda ashtuke na kutetemeka.
 
SEHEMU YA 36


Yuda akaenda chumbani kwa Patrick. Jambo alilolikuta humo lilimfanya ashtuke na kutetemeka.
Alimkuta Patrick ameshika bastola na kuielekezea mlangoni, na kwavile yeye ndo alikuwa anaingia ikawa kama vile amenyooshewa yeye.
Yuda akatetemeka na kuishiwa cha kusema, akajilaumu kwa kitendo cha kuingia bila hodi. Patrick akaishusha ile bastora na kuiweka kwenye mkoba pembeni,
PATRICK: Aaah Yuda, karibu sana.
Yuda alikuwa bado anatetemeka na kuamini maneno ya Sele kuwa Patrick ni jambazi. Akashindwa kumjibu Patrick kwani alikuwa na hofu bado.
PATRICK: Usijali Yuda, acha kufikiria ulichokiona bhana. Mambo ya kawaida tu yale.
YUDA: Mamdogo anajua?
PATRICK: Wee, usithubutu kumwambia.
YUDA: Na kama ni yeye je ndie angekuwa kaingia na kukuta kama mimi nilivyokuta?
PATRICK: Hawezi ingia bila hodi, hata hivyo angeongea ongea hapo kabla ya kuingia. Na wewe jifunze adabu usipende kuparamia sehemu bila hodi.
YUDA: Nimekusoma kaka, nisamehe kwa hilo.
PATRICK: Poa, za siku nyingi?
Yuda alipiga stori mbili tatu na Patrick huku akijaribu kumsoma kwanza kabla ya kumueleza.
Fausta alimuita Tina ili aelezwe kuhusu mume wa Tusa.
FAUSTA: Hivi Tusa yule mwanaume alimtolea wapi?
TINA: Facebook mama.
FAUSTA: Facebook? Mmh! Hata kama ni huko kulikuwa na umuhimu wa kuwajua ndugu zake.
REHEMA: Sema wewe Fausta, mi niliuliza hapa hadi nikachoka. Mwanaume hujui anapokaa, huwajui ndugu zake unamuozesha mtoto wako huko, hivi unampenda kweli mwanao?
FAUSTA: Kwakweli Pamela na Adamu wamefanya kosa ambalo watajutia maisha yao yote. Unajua tulipogundua kuwa Adamu ni ndugu yetu, baba yetu mzee Ayubu alipinga vikali ndoa yao lakini kwavile walishazaa haikuwa na jinsi. Na alitupa onyo kuwa tusiozeshe mtoto bila kujua ukweli wa upande wa pili, licha ya undugu unaweza pia kukuta yule si mtu.
TINA: Mmh! Mama, Patrick ni mtu bhana, acha zako hizo.
FAUSTA: Mi nasemea tu wala sina tatizo.
Fausta aliendelea kuwaza vitu mbalimbali kuhusu huko alipo Pamela.
Deborah akizungumza na Pamela kuhusu Tusa.
DEBORAH: Pamela, jaribu kumuweka sawa binti yako. Alishakosea kuolewa na mtu asiyempenda, asitake kufanya kosa lingine hapa, akitaka apange na Patrick na kuachana kiustaarabu, akilazimisha ataumiza wengine.
PAMELA: Ni kweli mwanangu hayupo sawa, na tatizo lake hataki kusema ukweli. Amekonda sana mwanangu, mwanao anamtesa sana Tusa.
DEBORAH: Kila mwamba ngoma huvutia kwake, utamtetea mwanao na mimi nitamtetea mwanangu. Tusa wako ni mpumbavu, atakuwa vipi na mahusiano na wanaume wawili kwa wakati mmoja tena ni ndugu!
PAMELA: Tusa si mpumbavu ila alipumbazwa na Patrick, Deborah huyajui yaliyojificha kwa mwanao, siwezi kumponda kwani ameniokoa toka kwenye mikono ya simba watu.
DEBORAH: Ndio wakina nani hao?
PAMELA: Ni majangili flani watu wa Arusha, hata tunaishi hapa sijui kama tuko salama.
DEBORAH: Majangili? Kivipi na wanafanya kazi gani?
PAMELA: Nadhani wanafanya kazi za kigaidi, nahisi hata mwanao Patrick ni mwenzao, naye atakuwa jangili tu.
DEBORAH: Ugaidi kama wa kuteka watu?
PAMELA: Ndio, na mengineyo ambayo magaidi hufanya. Hata Patrick alimuoa mwanangu kigaidi tu.
Deborah akaanza kuchezesha akili yake baada ya kusikia Arusha na kazi za ugaidi, wazo lake likaenda moja kwa moja kwa Maiko.
Fausta akiwa nyumbani kwa Adamu alijikuta akiwaza vitu vingi sana.
FAUSTA: Mama, mbona mimi kama najawa na mashaka moyoni juu ya huko Mwanza.
REHEMA: Mashaka gani tena?
FAUSTA: Labda Pamela na Tusa wametekwa, hivi ni kitu gani kinachoweza kuwazuia kurudi.?
REHEMA: Sijui maana wamedai wana matatizo tu.
FAUSTA: Nadhani huyo mtu nia yake itakuwa ni kaka Adamu tu.
REHEMA: Kwanini Fausta? Mbona sisi hatuna maadui kabisa?
FAUSTA: Mama, tusikubali kabisa Adamu kwenda mwenyewe. Lazima tumsindikize wote kwa usalama wake.
REHEMA: Mmh! Unanitisha Fausta. Kwanini unawaza hivyo?
FAUSTA: Mama, yule mke wa kwanza wa Adamu kwao ni Mwanza. Unajua kitendo alichofanya kabla ya kuondoka Dar?
REHEMA: Kitendo gani?
FAUSTA: Huyo mwanamke anaitwa Deborah, ukimuona ni mpole sana na mkarimu. Hata mimi sikuamini kama ni yeye alifanya kitendo cha kikatili kiasi kile.
REHEMA: Mmh! Alifanyaje?
FAUSTA: Alichukua upanga na kumkata binti flani hivi miguu na yule binti ni mlemavu hadi leo hana miguu kabisa. Mmh huyo Deborah ni mkatili mama.
REHEMA: Una uhakika alifanya yeye hicho kitendo? Mbona huo ni ukatili mkubwa jamani, loh anataka kufanana na kaka yangu Mashaka.
FAUSTA: Hata mimi namfananisha na Maiko, mama kuna wanawake makatili sana na yule Deborah ni mmoja wao. Nina hofu kama akawa yeye amewateka Pamela na Tusa na sasa anamtaka Adamu akalipe kisasi.
REHEMA: Mbona unanichanganya sasa, Adamu alifanyaje hadi alipe kisasi?
FAUSTA: Adamu alimsaliti Deborah na kuwa na Pamela kipindi hicho hatukujua kama Adamu ni ndugu. Ila mama hizi ni hisia zangu tu maana hakuna ajuaye kama huyo Deborah bado yupo hai au alikufa.
REHEMA: Ila hata Adamu aliniambia anajutia kitendo cha kumsaliti huyo mkewe, ila nadhani kama alifanya ukatili huo basi alikuwa na sababu maana Adamu kuna siku alinieleza kuwa mwanamke huyo alikuwa mpole sana. Mmh ila kama ndio hivyo alikuwa katili sana.
FAUSTA: Hata nashangaa leo nimemkumbuka mama, ila sitaki kumuwazia mabaya ila pia sidhani kama huko Mwanza ni kwema Adamu kwenda peke yake.
Ikabidi wapange mipango ya wote kwenda huko Mwanza.
Maiko na Mashaka waliendelea kunoa vijana wao kwaajili ya kuwapeleka kupambana na Patrick.
MAIKO: Ila kuna haja kweli ya kwenda na vijana wengi?
MASHAKA: Wengine tutaenda nao kwaajili ya madili mengine tu huko Mwanza.
MAIKO: Hapo sawa, maana Tukiwa wengi sana atatupotea yule. Ila tutachek na madili mengine pia, hiyo nzuri sana.
Wakapanga kusafiri na vijana wanne kwaajili ya madili mengine watakayo yapata huko Mwanza, vijana wawili wa kuwasaidia na wawili wa madili.
Yuda akaamua kumueleza ukweli Patrick baada ya kumsoma.
YUDA: Kaka, hivi unajua mzee wetu yule sisi huku tulizika mwili ila kichwa chake hadi leo kuna mahali kipo.
PATRICK: Kipo? Kipo wapi?
Yuda akaanza kumueleza Patrick jinsi alivyogundua jambo hilo.
Akamkuta Patrick akitikisa tikisa kichwa.
PATRICK: Umesema ni Arusha?
YUDA: Ndio ni Arusha kaka.
PATRICK: Huyo jamaa anaitwa Maiko na mwenzake Mashaka?
YUDA: Ndio hao hao kaka.
Patrick akapatwa na hasira sana, akajikuta akifumba macho kwa dakika kadhaa huku akitafakari hilo jambo.
PATRICK: Unataka tufanyaje Yuda?
YUDA: Nataka tukalipize kisasi, hiyo ndio shida yangu.
PATRICK: Hakuna tatizo, cha msingi tujipange twende huko Arusha.
YUDA: Ila tutaweza kaka?
PATRICK: Kujiamini ni ishara ya ushindi wewe jiamini tu.
YUDA: Sawa, hakuna tatizo basi.
Yuda akaondoka huku akitegemea kuanza kujipanga na Patrick kwaajili ya kwenda kulipa kisasi Arusha.
Yuda aliaga na kuondoka zake, Patrick akamsindikiza kidogo Yuda.
Nje kwao alimuona mama yake na Pamela wamelala kwenye mkeka, Patrick akaingia ndani, kuna kitu kikaanza kujichora katika hisia zake, akasimama mlangoni kwake mara Tusa akapita akiwa anatokea chumbani akitaka aende sebleni na kutoka nje walipo mama zake.
Alipokuwa anapita kwenye mlango wa Patrick, alishtukia akivutwa chumbani na Patrick, Tusa hakuweza kupiga kelele kwani alizibwa mdomo na Patrick.
Tusa hakuelewa ni kitu gani atafanywa na Patrick humo ndani, alijikuta machozi yakimtoka tu.
 
SEHEMU YA 37


Tusa hakuelewa ni kitu gani atafanywa na Patrick humo ndani, alijikuta machozi yakimtoka tu.
Patrick akiwa kamziba mdomo Tusa, akaanza kumwambia.
PATRICK: Hivi kwanini hutaki kunipa haki yangu Tusa? Leo nahitaji, hii ni haki yangu kama mumeo kwahiyo utake usitake utanipa tu.
Tusa akaendelea kuhangaika, Patrick akajua kwa vyovyote vile Tusa atapiga kelele tu, akachukua kitambaa alichokuwa amepulizia dawa na kumfunika nacho Tusa usoni, kitu hicho kilichofanya Tusa alale.
Patrick akatumia muda huo kumuingilia Tusa kimwili bila ya Tusa kujitambua.
Kitu hicho kilikuwa ni ushindi sana kwa Patrick, aliendelea kufanya mambo yake mengine kwa uhuru, huku akijisemea "Anataka nisimfaidi wakati naondoka, aje yule mjinga Sulemani kumfaidi wakati mi ndo nimemgharamikia mtoto aah!"
Deborah na Pamela wakiwa nje wakashangaa hadi jioni Tusa hajatoka ndani, Deborah akaingia ndani kumuangalia Tusa ila hakuwepo ndani, akashangaa na kujiuliza alipo Tusa.
Mara Patrick akatoka chumbani kwake, ndipo Deborah alipomuuliza.
DEBORAH: Umemuona Tusa?
PATRICK: Ndio, yupo chumbani kwangu.
DEBORAH: Chumbani kwako!! Anafanya nini?
PATRICK: Mama, Tusa ni mke wangu sasa unapouliza anafanya nini chumbani kwangu nakushangaa sana. Kwasasa amelala.
DEBORAH: Mmh makubwa haya.
Deborah akatoka nje na kumfata Pamela alipo.
DEBORAH: Eti Tusa yupo chumbani kwa Patrick, mbona mambo!!
PAMELA: Hata hivyo ni mumewe yule, hatutakiwi kuhoji sana.
DEBORAH: Pamela unakuwa kama vile hujui kumuangalia mwanao, hivi unavyomuona Tusa hapa unafikiri anafurahia ndoa yake na Patrick?
PAMELA: Sijui, ila Tusa angekuwa hafurahii angesema. Mbona anakaa kimya muda wote! Anashindwa hata kunieleza mama yake! Kwa upande wangu namuona Patrick ni mume bora kwa Tusa.
DEBORAH: Kwanini?
PAMELA: Anajua kumlinda mkewe, si unaone hata Sele ameshindwa kutoroka na Tusa kwasababu ya Patrick. Na pia Patrick ameniokoa.
DEBORAH: Binti yako nae hana msimamo, yani mi namtetea yeye anatoroka na Sele na leo je kilichompeleka chumbani kwa Patrick ni nini? Dah hata simuelewi kwakweli, eti kalala na kulala loh!
PAMELA: Kwa upande wangu sina shaka sana sababu najua Patrick ni mtu mzuri, mwanzo nilikuwa na mashaka nae, ila sasa nimemuona Patrick anafaa kwakweli.
Pamela alijivunia kitu kimoja kwa Patrick, ni kile kitendo cha kuokolewa nae toka mikononi mwa wakina Maiko, kwahiyo alimuona Patrick kuwa mtu mzuri kwake, hakujua kama kuna mambo maovu yanayofanywa na Patrick.
Tina alipoona safari ya kwenda Mwanza imenoga ikambidi aende kumuaga rafiki yake Vene.
TINA: Kesho ndo tunaenda kwenye ile safari yetu ya Mwanza. Nimefurahi kweli maana itakuwa ni mara yangu ya kwanza kufika huko.
VENE: Mmh Tina, Mwanza kuna mapedeshee huko balaa. Na nikujuavyo wewe lazima utawapagawisha tu.
TINA: Mapedeshee siwataki Vene, mdogo wangu Tusa tangu ameolewa na lile pedeshee la Arusha sijawasiliana nae hadi leo. Ndio wanasema yuko huko Mwanza.
VENE: Itakuwa amepatwa na mambo mazuri, yani Arusha na Mwanza ni hatari shoga yani, halafu wana hela hao balaa.
TINA: Ila siwataki hao mapedeshee bhana Vene.
Tina alikuwa akiuwaza mji wa Mwanza kwani akienda ndio itakuwa mara yake ya kwanza kufika Mwanza.
Wakiwa wanajiandaa nyumbani kwao,
TINA: Eti mama wanaume wa Mwanza wana pesa eeh!
FAUSTA: Nani kakwambia mwanangu? Mnapenda kuongopeana sana wewe na mwenzio.
TINA: Nambie ukweli bhana mama.
FAUSTA: Wapo Kawaida tu hawana lolote. Ngoja tujiandae hapa kwa hiyo safari ya kesho.
Wakaendelea kufanya maandalizi ya hapa kwaajili ya safari yao.
Tusa alipozinduka na kutazama huku na kule ndipo alipokumbuka kitu kilichotokea, akaamua kushuka pale kitandani ili aweze kutoka nje. Wakati akifanya hayo, mara Patrick akaingia chumbani.
PATRICK: Khee, umeamka mke wangu!
Tusa alimtazama tu kusema chuchote.
PATRICK: Usiwe na hasira Tusa, mimi ni mumeo.
TUSA: Hata kama ni mume, hutakiwi kunifanyia hivi.
PATRICK: Ni haki yangu Tusa, unategemea mimi niende wapi wakati wewe upo?
TUSA: Niachie nitoke basi.
Patrick akawa anamzuia Tusa nae aliendelea kuonyesha kiburi cha kutaka kutoka nje, na hapo hapo akashikwa kwa nguvu zaidi na Patrick.
PATRICK: Sasa ole wako umwambie mtu kitu chochote. Hakuna kusema, hutakiwi kusema kitu.
TUSA: Unanionea sana Patrick, laiti watu wangekujua ulivyo wangekuponda na mawe wewe.
PATRICK: Nimekwambia hakuna kusema Tusa.
TUSA: Bhana eeh nishakuelewa, wewe ni mbabe nani atakuweza bhana. Acha niendelee kuteseka ila siku watapoosha maiti yangu watajua ni vitu gani nimepitia. Niachie Patrick sitasema chochote.
Patrick akamuachia na Tusa akatoka mule ndani akiwa amenyong'onyea sana hakuwa na raha yoyote. Aliwaza vitu vingi moyoni mwake haswa mateso anayopewa na Patrick, mateso anayoyajua yeye mwenyewe.
Mashaka na Maiko walikuwa wameshakamilisha safari yao ya kwenda Mwanza.
MAIKO: Lazima tufanikishe safari hii.
MASHAKA: Tutaonekana wajinga kama tukiwakosa.
MAIKO: Vipi Tusa, nae bado tunamuhitaji?
MASHAKA: Tena sana, si unajua kazi zetu karibia zote zimesimama kwaajili yao, dah wametupatia hasara sana hawa watu jamani.
MAIKO: Yule Patrick anajiamini sana na hilo ndo tatizo, safari hii ni kimya kimya hadi tumpate.
MASHAKA: Ndio, nataka kujua jeuri ya Patrick itaishia wapi. Kijana mdogo lakini anajifanya kucheza na akili zetu, ngoja tumpate firauni yule.
MAIKO: Ametusumbua sana Patrick, hata sikufikiria kweli mapenzi hayafai kazini maana mapenzi ndo yamemponza yule hadi kutoroka na Tusa.
MASHAKA: Ila tuache utani bhana, kabinti kanavutia sana kale.
Wakawa wanacheka huku wakiendelea kuweka mambo sawa na kuianza safari ya kwenda Mwanza wakitumai kumpata Patrick na Tusa.
Patrick alienda kwa Yuda na kupanga mpango wa kuondoka mahali hapo kwenda kwenye ile himaya ya kina Maiko.
PATRICK: Jiandae kesho safari, twende huko kupambana.
YUDA: Dah umeishtukiza kaka.
PATRICK: Kushtukiza ni jambo jema kwani inamfanya adui asijipange kwa muda.
YUDA: Poa poa kaka, ila vipi silaha tutakuwa nazo?
PATRICK: Ondoa shaka, kila kitu kipo kwenye mstari.
YUDA: Poa, nami niko tayari tu.
PATRICK: Na Unapoaga nyumbani hapa usiwaage moja kwa moja ya tuendapo, wadanganye vyovyote ili kuokoa safari yetu.
YUDA: Hakuna shaka, lazima tutafanikisha tu.
PATRICK: Ndio hivyo, kuwa makini sana Yuda. Ikiwezekana usiage kabisa.
YUDA: Sawa, nimekuelewa hapo kaka yangu.
Wakaenda kujiandaa na kesho yake safari ya kwenda Arusha ikaanza.
Tusa alijiinamia huku akitokwa machozi.
DEBORAH: Hivi unaliaga nini wewe? Unatutisha sana kwa kilio chako ila husemi.
TUSA: Muda ukifika nitasema tu.
DEBORAH: Mmh! Haya bhana. Huo muda sijui utakuwa ni lini, ila usipende kuficha mambo Tusa utajitesa bure wakati msaada upo.
Deborah alikuwa akimshangaa sana Tusa kwani binti huyu alijua kuficha mateso yake, machozi tu ndo yalionyesha kuwa anateseka.
Muda mwingi Tusa alijilaumu kwa upumbavu wake, alijiona mjinga sana kukubali kuolewa na mwanaume asiyempenda.
Adamu na familia yake walikuwa ndani ya jiji la Mwanza, waliingia Mwanza usiku na kufikia kwenye hoteli wakalala hapo hotelini.
Kesho yake, Adamu akamtafuta Pamela kwa ile namba ila hakumpata hewani kwahiyo akangoja pale watakapofungua simu hiyo.
Tina baada ya kukaa pale kwa muda kidogo.
TINA: Mama, acha nishuke chini nikatembee kidogo.
FAUSTA: Mwanangu, miguu ishakuwasha tayari. Usiende mbali maana hapa tunangoja jibu la mjomba ako.
TINA: Siendi mbali mama, nitakuwa maeneo haya haya ya hotelini tu.
FAUSTA: Sawa mwanangu.
Tina akashuka na kwenda kutembea tembea kidogo pale karibu ili kuiona Mwanza ilivyo.
Muda ulipita sana bila ya Tina kurejea, wote wakaingiwa na wasiwasi kuwa Tina yuko wapi.
 
SEHEMU YA 38

Muda ulipita sana bila ya Tina kurejea, wote wakaingiwa na wasiwasi kuwa Tina yuko wapi.
Fausta akaamua kushuka chini kwenda kumuangalia ila hakuwepo kabisa katika maeneo yale, akarudi juu akiwa hata haelewi pa kuanzia.
FAUSTA: Kwakweli huyu mtoto ananieleleza leo mama.
REHEMA: Jaribu kupiga simu yake.
FAUSTA: Simu yake haipatikani, sijui hata yuko wapi na mjomba wake akirudi hapa tutamueleza nini jamani dah.
REHEMA: Ila Tina nae, alienda kutafuta nini nje?
FAUSTA: Mama, Tina huwa kama vile anawashwa miguu, alinambia anaenda tu hapo chini kuangalia mazingira ila hadi sasa hajarudi, na hata hapo chini hayupo.
REHEMA: Mmh hebu tuwe na subira kidogo.
FAUSTA: Mama, ingekuwa Dar nisingekuwa na mashaka, sasa huku Mwanza Tina hata hapajui, nahofia atapotea jamani.
REHEMA: Tina ni mtu mzima, hawezi kupotea kizembe. Shughuli akirudi huyo Adam kabla ya Tina.
FAUSTA: Hapo ndio pagumu, sijui kama atanielewa jamani.
Fausta hakuwa na raha kabisa, alipatwa na mawazo tofauti tofauti kichwani.
Tina akiwa hajitambui, akashtuka na kujiona yupo kwenye chumba na vijana wawili. Kumbukumbu zikamjia kuwa alipotoka nje ya hoteli ili kuangalia mazingira akakutana na baba mmoja asiye mfahamu, akasalimiana nae, yule baba alimuomba Tina wakae mahali na kupata bia mbili tatu kwa maongezi, Tina hakuona tatizo akaenda kukaa na huyo baba, anachombuka Tina ni kuwa alikunywa bia mbili tu halafu akapatwa na usingizi wa ajabu, ndipo hapo aliposhtuka na kujiona yupo kwenye chumba.
Tina akawaangalia wale vijana na kuwauliza
"Nipo wapi hapa?"
Wale vijana hawakumjibu kitu, ila mmoja wapo akatoka na kurudi na yule baba aliyekutana nae Tina, ile Tina alipomuona tu.
"umenileta wapi huku? Kwanini umeniweka humu?"
Yule baba alikuwa ni Maiko, alimuangalia Tina kwa jicho la hamasa na kumwambia.
MAIKO: Wow, umeamka mrembo.
Tina alikuwa na alama ya kuuliza bado.
TINA: Kwani humu nimefikaje?
MAIKO: Swali rahisi sana, umefika kama ulivyotakiwa kufika.
TINA: Ok, naomba niondoke maana ndugu zangu hawajui nilipo.
MAIKO: Hapa ndio umefika, huna pa kwenda tena.
Halafu Maiko akatoka mule chumbani, Tina akajikuta kwenye mawazo.
Patrick na Yuda wakiwa ndani ya Arusha, Patrick akaamua kumtuma Yuda aende akaangalie mazingira kwanza kabla hawajaanza kufanya jambo lolote.
Yuda akaingia kwenye himaya ya Maiko ili akaangalie kuna nini na nini, akakutana na Tulo, akamsalimia na kujifanya kama vile amerudi kazini.
YUDA: Vipi, bosi Maiko yuko wapi?
TULO: Amesafiri yeye na Mashaka.
YUDA: duh! Wameenda wapi kwani?
TULO: Wameenda Mwanza bhana.
Hiyo kauli ikamchanganya sana Yuda, akaamua kumuaga Tulo na kwenda kwa Patrick kumwambia.
PATRICK: Dah! Wale wapuuzi watakuwa wameenda kunisaka mimi Mwanza wale.
YUDA: Unajuana nao? Sasa itakuwaje?
PATRICK: Itabidi turudi Mwanza, twende tukaokoe familia huko, yale majitu hayafai.
Ikabidi waanze harakati za kurudi Mwanza.
Adamu alirudi akiwa na mawazo.
ADAMU: Pamela hapatikani kabisa kwa ile simu aliyotumia kunipigia, sijui ndo nini sasa.
FAUSTA: Mmh! Haya majanga sasa.
Ikabidi amueleze na kupotea kwa Tina.
ADAMU: Huo ni upumbavu sasa, huyo Tina nae kitu gani kimempeleka kuzurura miji asiyoijua! Sasa tutaanzia wapi kumpata jamani!
FAUSTA: Hata sijui kwakweli, yani huyu Tina huyu dah!!
Wakakaa na kujadili namna ya kumpata Tina kwani hakurudi wala hawakupata taarifa yoyote ya alipo.
Maiko na Mashaka walifurahia sana kumpata mwanamke.
MAIKO: Yule nitamfanya mke wangu.
MASHAKA: Acha ujinga wewe, mke wa nini? Hawa huwa tunawatumia tu, tukiwachoka tunatupa kulee. Hata hivyo yule binti ni mrembo pia, atatufaa kwenye kazi zetu.
MAIKO: Yani wewe kila mwanamke wa kazi, sijui hata unataka nini. Yule ni demu wangu bhana.
MASHAKA: Acha zako bhana, ukiendekeza mademu, utajikuta unafanya mambo kama ya yule mjinga Patrick, cha msingi ni kuwaepuka hawa viumbe. Dawa yao ni kuwatumia tu na kuachana nao ila ukiona ana mvuto zaidi basi tunamchukua kwa kazi bhana.
MAIKO: Ngoja nikamshughulikie kidogo basi, ana mvuto kweli yule binti.
Tina akiwa mule chumbani amejibanza tu, akaingia Maiko na kuwaamuru wale vijana wampishe kidogo.
MAIKO: Mrembo, nataka huduma kidogo.
Tina akawa anakataa kwa kutikisa kichwa, ila kukataa kwake hakukumsaidia Maiko, akaanza kumlazimisha ndio hapo varangati lilipoanza, katika kuhangaika Tina akafanikiwa kumpiga Maiko teke la chini kitu kilichofanya Maiko augulie maumivu, Tina akataka kutumia mwanya huo kutoroka ila vijana wa mlangoni wakamkamata na kumrudisha tena ndani, hapo Maiko alikuwa na hasira sana na Tina.
Akampiga ngumi nyingi nyingi hadi Tina akazimia halafu akambaka.
Alipomaliza, akatoka nje huku akijisemea.
"Eti mtoto wa kike anishinde mimi!! Nitakushikisha adabu mpenda ofa wewe."
Deborah alikuwa akijiuliza kuhusu mwanae Patrick.
DEBORAH: Hivi Tusa, Patrick alikuaga kuwa anaenda wapi?
TUSA: Hapana hajaniaga.
DEBORAH: Hivi huyu mtoto ana kichaa! Kuchukua simu yangu na kuniachia yake ndio nini jamani.
Wakati Deborah akiongea hayo Tusa akawa anajisemea kimoyomoyo "Inamaana siku zote hakujua kama amezaa chizi mmh!!"
Akajikuta akiropoka kabisa.
TUSA: Mwanao ni kichaa ndio.
DEBORAH: Unasemaje Tusa?
Tusa akawa amejiinamia chini tu.
DEBORAH: Hivi Pamela huyu mwanao ana matatizo gani?
PAMELA: Hata na mimi sielewi, ila hebu tujadili mambo ya maana kwanza. Umesema Patrick ameondoka na simu yako na kukuachia yake? Sasa akija huyo babake Tusa atatupataje?
DEBORAH: Duh! Hapo ndipo pabaya, na ubaya ni kuwa simu yake yenyewe ameiacha bila hata line mmh mtoto huyu!!
Deborah alishindwa kabisa kumtafakari mwanae Patrick na matatizo yake.
Patrick na Yuda walishaingia tena Mwanza, walianza msako wa kuwatafuta wakina Maiko kabla ya kuonwa wao kwanza haswaa Patrick.
Hapo ndipo Patrick alipoamua kumtumia Yuda kama chambo.
Katika harakati za kutafutana, Patrick na Maiko wanakutana mjini kwa kugongana vikumbo.
Walipogeukiana na kuonana ana kwa ana, kila mmoja alikuwa na ghadhabu na mwenzie.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom