SLAVE SEX(Mtumwa wa ngono)……(27)
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY
Contact….+255718 862176
AGE….(18+)
ILIPOISHIA.
, akamshuhudia Mwanamke mtu mzima aliyekuwa
anashuka ndani ya gari aina ya ‘Jaguar,akiwa
kaukunja uso wake,akatembea mpaka kwenye kioo
upande wa Nickson na kugonga,kioo kikafunguliwa.
“Kaka hukuniona au?huku niona? naomba ushuke
tafadhali tuelewane,jamani mbona ivyo asubuhi
asubuhi kutafutiana mabalaaa,shuka kaka,shuka
upesi kwa usalama wako.Tena naomba ushuke
upesi usinipotezee muda”
SONGA NAYO.
“Pipiiiii piiiiiiiiiiii piii”
Honi za magari ndizo zilikuwa zikisikika kwa wakati
huo,ilikuwa ni asubuhi tu,kulikuwa kuna
msongamano wa magari,uliosababisha msululu
mrefu mno,Nickson ndiye alikuwa amesababisha
kitu hicho kitokee baada ya kuligonga gari la
mbele yake,tayari walikuwa wameshuka na
kutizama jinsi Jaquar la mwanamke huyo
lilivyoumia.
“Aa! Aah! unaona ulivyopasua hii hendiketa,hii
rangi imechubuka alafu ni metaliki hii,bei mbaya
sana”
Mama huyo alizidi kufoka huku akimuonesha
Nickson sehemu zilizopata matatizo.
“Mama naomba basi upaki pembeni ili tuepushe
huu msongamano,haya ni mambo ya magari cha
kufanya tuweke magari pembeni ili tuelewane
vizuri”
“Nani?sitoi gari hapa mpaka trafiki aje kupima”
“Mimi nimekubali kosa nitakulipa garama zote”
“Nimesema hapa sitoi gari”
“Oyaaa mazaaa eeh,Bi.Mkubwa.Wewe Maza si
muelewane tu hapo,mbona unakuwa sio mwelewa
angalia msongamano”
Dereva mmoja wa DCM aliropoka baada ya
kushuka ndani ya gari.
“Wewe hayakuhusu,hapa mpaka trafiki”
Ni kweli Mwanamke huyu aliweka mkazo
wake,hakutaka kulitoa gari eneo hilo,dakika
arobaini baadaye Trafiki alisogea eneo hilo na
kupima ajali.
“Nipatieni leseni zenu”
Trafiki aliomba na akapewa leseni ya kila mtu.
Baada ya ajali kupimwa Nickson ndiye
aliyeonekana ana makosa na alitakiwa kulipa faini
kwa sababu alisababisha ajali kizembe,hakuwa na
tatizo lolote akalipa kisha kuelewana na Mwanamke
huyo kwamba amtengenezee gari yake,akamkabidh
i kadi yake ya gari kisha kuondoka zake!
Bado alikuwa ana mawazo juu ya mke wake na
wala hayakumwisha!hakuna siku aliyoonesha
kuchanganyikiwa kama siku hiyo.Pesa nyingi
alizotumia kumpeleka Gloria nchini china
akitegemea kuwa amebadilika na wote kurudi
waendelee kuwa na furaha maishani,ikawa ni
shukrani ya punda.Alivyofika ofisini kwake
alisalimiwa na wafanyakazi wake.
“Shikamoo bosi”
Hakuitikia hata salamu moja akapita moja kwa
moja akapanda ngazi na kuingia ndani ya ofisi
yake,huko hakuna alichofanya aliweka kichwa
chake juu ya meza akazama kwenye mawazo.Bila
ya kutegemea alijikuta akilia machozi mwenyewe,
huku akilitaja jina la Gloria!
“Gl….oria ni ki..tu gani nilikufa..nya eeeh… mbona
una..nitesa hiv…i nimekufanya nini mke wa..ngu
au kwasababu ushajua kuwa na..kupenda sa..na”
Hayo ndiyo maneno aliyokuwa akiongea Nickson
huku akimwaga machozi,alihisi moyo wake
umepigwa na mkuki wenye moto,tena umechanika
chanika.Machozi yalimtoka yakadondoka mpaka
kwenye sakafu.Hata ivyo mawazo hayakumsaidia
sana, ukweli ulibaki kuwa palepale kwamba Gloria
yupo China na kivyovyote vile ana mahusiano ya
kimapenzi na Nyagogo, hilo alilielewa wazi
kutokana na kutokupatikana kwa Nyagogo.Alifuta
machozi haraka haraka baada ya kuhisi mlango
wake unagongwa.
“Ingia”
Alingia Wakili mwenzake aliyefahamika kwa jina la
Debora,huyu alikuwa msaidizi wake.Tangu Nickson
alivyopandishwa cheo na hapohapo akapewa mtu
wa kumsaidia baadhi ya kazi endapo atakwama.
“Karibu kiti Debora”
“Bosi,kuna kitu hapa nilitaka kukwambia,
Unamkumbuka Elizabeth Zackaria?Yule mama
mwenye migodi kule mererani?”
“Ndio namfahamu,aliyeleta kesi ya kudhurumiwa na
mume wake?”
“Ndio,basi alikuja hapa asubuhi akakusubiri sa….”
“Naomba uje baadaye,sasa hivi sipo sawa”
Nickson alimkatisha Debora ambaye alikuwa
anataka kuanzisha kesi nyingine,kwa siku hiyo
Nickson alijua kabisa kichwa chake kisingefanya
kazi sawasawa,na ndiyo maana akamtaka Debora
radhi.
“Bosi una tatizo gani?pia mbona macho yako
mekundu namna hiyo unaumwa au?”
“Hapana nipo sawa,jana sikulala usiku nilikuwa
napitia pitia baadhi ya kesi”
Nickson alidanganya ukweli ni kwamba hakukesha
kupitia kesi bali alikuwa akimlilia Gloria.
“Inakubidi sasa hivi ukapumzike bosi,ili upate
usingizi wa kutosha niachie mimi nitakusaidia kila
kitu, nitakupigia simu nikihitaji maelezo mengine”
“Kweli?”
“Ndio Bosi”
“Akifika Mkurugenzi mwambie kuwa nimetoka
kidogo”
“Nitajua cha kumwambia au nitakutetea mimi
wakili bwana Shayo,nitakukinga wewe nenda
nyumbani ukapumzike”
“Ha ha ha ha haaaaa,Dora una maneno wewe
mwanamke”
Debora,alikuwa ni msichana mwenye roho ya
ukarimu, alimuonea huruma Nickson akakubali
kuubeba msalaba wake,kila kitu alikifanya kwa
moyo mkunjufu.
Nickson akasimama huku akitoa shukrani
zisizokuwa na maelezo ya kutosha.Akaingia
kwenye gari akiwa na mawazo chungumzima!
***
Hakuna hata mmoja wapo aliyediriki kulitaja jina la
Nickson, sio Gloria wala Nyagogo,kila walilofanya
waliliona lipo sahihi,walijiachia wanavyotaka na
kufanya mapenzi muda wowote ule watakao
wao,mambo yaliyokuwa yanamtokea Gloria ni
dhahiri kwamba alihisi yupo ndotoni
anaota,mambo aliyokuwa anafanyiwa yalikuwa ni
makubwa mno,ambayo hakuwahi hata kuyafikiria.
Alikuwa akila bata kama aliambiwa kuwa atakufa
kesho,kufumba na kufumbua alikuwa kamsahau
tena Nickson akasahau alipotolewa kijijini.
Gloria alizidi kuwa mlevi kupita kiasi, alikunywa
pombe ikazidi kipimo.Mwanaume huyu
mfanyabiashara aliyeitwa Nyagogo ndiye aliyempa
kiburi.jiji la Beijing likamkoma akawa kiguu na njia
kutwa wapo kwenye kumbi za starehe.
“Pondaaa maliiii kufa kwajaaaaaaaa”
Ni Gloria ndiye alikuwa akiongea maneno hayo
huku mkononi akiwa ana chupa ya mzinga wa
pombe kali,walikuwa wapo ndani ya
Casino,wanawake wa kizungu wakichanganyika na
wachina walikuwa wakipita mbele yao wakiwa
wamevaa vichupi,huku mbele yao kukiwa na
wanawake wengine wakichezea machuma yaani
‘strippers’kwa kimombo. Nao walikuwa wamevaa
nusu uchi maziwa yao yapo wazi.walifanya
Kufuru.Ilikuwa ni club iliyokuwa nje kidogo ya mji
wa Beijing,
wafanyabiashara wengi walipenda kupumzika hapo
na kutoa ‘stress’ zao.Wengi wao walikuwa ni
matajiri na walizungukwa na wanawake warembo
wakiponda mali.
“Bebiiiiii”
Nyagogo alimuita Gloria kisha kumvuta upande
wake,akamvuta mdomo na kutoa ulimi wake ndimi
zao zikakutana wakaanza kulana denda,hakuna
hata mtu mmoja aliyewahangaikia,kila mtu alifanya
mambo yake.
“Mhhhhhhh”
Gloria alikuwa akiguna ndani kwa ndani huku
wakiendelea kubadilishana mate.
“Kesho inabidi turudi Tanzania”
“Eeeeeh,kwanini?”
Gloria akashtuka,hakutaka kuisikia kabisa nchi ya
Tanzania, yeye alitegemea kwamba angeishi nchini
China milele.
“Tubaki bwaaanaaaa huku huku,kwanini turudi
tena,kwani wewe si uliniambia tukakaa huku
mileleeee?”
“Ahhh,sasa biashara zangu nani ataziendesha?tu
rudi kidogo nikaweke mambo sawa kisha tutarudi
huku China”
“Kweli?”
“Niamini mimi Mke wangu,Mama watoto
bebiiii,Gloria hivi kwanini wewe ni mzuri kiasi
hichoooo?ujue sijawahi kuona mtoto mzuri kama
wewe,nitakuoa unajua mimi sijaoa kabisa,wala sina
mke”
Nyagogo alizidi kum-mwagia Gloria sifa
kedekede,ni wazi kwamba alitakiwa kurudi
Tanzania ili akaendelee na biashara zake,
alishaelewa kuendelea kubaki nchini humo akila
maisha,akaunti zake zingeyumba.
Nyagogo alikuwa ni mfanyabiashara mwenye
akili.Ilivyofika saa tisa ya usiku walibebana na
kutoka nje,huko walikodi Taxi iliyowapeleka mpaka
Hotel waliyofikia,kitendo cha kujitupa tu kitandani,
Nyagogo alimsogelea Gloria mdomoni na kuanza
kulana denda,huku taratibu wakianza kuvuana
nguo zao adoado,kiyoyozi kilichokuwa kinapuliza
kiliwaamsha hisia zao.
Haraka Nyagogo akatoa shati na Gloria akavuliwa
nguo zote kama umeme zikawekwa kando,kwa
maluweluwe ya ulevi,shikana haikuwa
sana.Nyagogo hakutaka kuchelewa aliipanua miguu
ya Gloria na kuingiza mjegeja wake kisha kuanza
kupeleka misumbwi.Kutokana na kunywa pombe
nyingi alichelewa kufunga goli la kwanza,
lilipopatikana alikuwa hoi akalala hapohapo kifuani
mwa Gloria!
***
“Nickson mwanangu,mbona unateseka sana
mshkaji wangu?..unakuwa kama sio mwanaume
kila siku unalia wewe,kwanini usimpige chini huyo
takataka,una mtoto sasa hivi,alafu ujue magonjwa
mengi,achana na huyo malaya.atakuuwa,pole kwa
mara nyingine..sasa usilie mwamba”
Nickson alikuwa akilia kwa uchungu sana,baada ya
kuumizwa tena kwa mara nyingine na
alipomwambia tena rafiki yake Tito ndiyo
kabisa,akawa kama amejitonesha kidonda
mwenyewe kilichoanza kukauka!
“Embu kwanza twende kwa Mushi tukale nyama
choma,nikupe ushauri”
Hapo Nickson hakuwa na tatizo,akaingia chumbani
kwake akabadili nguo na kumuachia Rukia pesa za
chakula kisha yeye kuondoka na swaiba wake Tito.
“Leo kwanza twende kwa Mzee Mushi
pale,tukalewe tupate akili mpya”
“Poa”
Wakaingia ndani ya landcruiser V8,Nickson
akawasha gari wakaenda mpaka Kigogo
Mburahati,kwenye Grocery ya mchaga
aliyefahamika kwa jina la Mushi na aliyesifika kuwa
na nyama nzuri za mbuzi za kuchoma.
Walivyofika tu Tito akaagiza mzinga wa Konyagi.
“Sasa mbona umeleta Moja dada,leta nyingine na
Glasi safi”
Tito aliagiza huku Nickson akiwa kimnya.
“Psiiii jikoni,psiiii pssiiiiiii wewe jikoni
wewe,unawaza nini?tengeneza ndizi kumi na
nyama choma ya mbuzi ya elfu thelathini
changanya mbavu na Mguu,weka na pilipili nyingi”
Tito alizidi kuagiza ilikuwa yapata jioni ya saa kumi
hivi.Mzinga wa konyagi ukaletwa wakaanza
kunywa taratibu bila kuongea zilivyofika nusu,
ndipo wakaanza maongezi.
“Uliniambia kuwa Gloria yupoooo china Mamaee
zake?”
Tito alianza kuongea kwa sauti ya kilevi,tayari
alikuwa amependeza!
“Ndiooo,yupo huko china,alienda na Yule Nyagogo”
“Sasaaaa,wewe kweli unampa mtu aende na mkeo
mbali,una akili sawa sawa?hapo ndipo ulifanya
mistake,yaani ulibugi mzee mwenzangu,wewe ni
ndugu yangu,tumetoka mbali sana mimi siwezi
kukuona una angamiaaaaa kisha nikabaki
kukuangalia,NOO nasema Noo Imposibleeee,swala
ni kwamba Gloria keshakuwa Malaya,anatomb****
na yoyote Yule,ananuka.Ptuuuuu”
Tito aliongea akatema mate chini akipigilia neno
lake msumari, kuwa Gloria ni kichefuchefu.
“Nishaurii nifanye nini ndugu yangu?”
“Hapo kuna ushauri teena,huyo piga chini wewe
sasa hivi muangalie mwanao Soniaaaaa,Gloria
keshaota pembe Yule,kibiritingoma,Kwani huyo
Nyagogo kwake unapafahamuuuuu?”
“Ndio,anaishi Mwanza”
“Mwanza eeeeh?”
“Ndio,kule Kilumba”
“Ana mkee?”
“Ndio, pia na watoto watano”
“Mimi ningekuwa weweee,ningepita na mkewe
kama mbwai mbwai tu,unagonga mke wake,kama
ana watoto wa kike unachafua chafua
tu,unatembeza dudu,sijalewa lakini nakupa
fact,Weweeee ni nduguuuu yaaaanguuuu wa
daaamuuuu,au nakosea?”
Tito alizidi kumshawishi Rafiki yake,akasisitiza
kwamba aachane na Gloria.Walizdi kunywa na
kulewa wakala wakashiba.Wakahama Grocery
wakawasha gari mpaka Magomeni,Ilikuwa teyari
saa nane ya usiku.
“Valuer zipo dadaaaaaa?”
Tito aliuliza hata kabla ya kukaa kwenye kiti.
“Ndioo”
“Leta lile lichupa likubwaaaaa”
“Pesa kaka”
“Wewe mpumbavuuu eeeh unagongwa
nini,unahisiii tutakudhurumu pesa zako au?embu
tuangalie vizuri tumekuja na V8,pumbavuuu
zako.Pumbavu tena….”
“Dadaaa shika hii”
Nickson akaingilia maongezi kati ili kuepusha
shali,alimuelewa rafiki yake Tito akilewa huwa ana
sifa ya ukorofi na ni lazima agombane na
mabaamedi.Pombe kali zikaletwa Nickson akawa
anakunywa nyingi bila kupumzika.
“Gloriiaaaaaaaaaa,popote ulipo naachana nawewe
rasmiiiiiiiii,naachanaa nawewe rasmi leoo
hiiii,umenitesa saaaanaaa”
Aliongea Nickson huku akisimama na kuyumba
yumba na kujipiga piga kifuani.Tito akasimama
nayeye, akawa anashangilia ushindi, akanyoosha
mikono hewani,akaanza kucheza mziki wa
Rumba,baada ya kupigwa wimbo wa Koffi
Olomide,akaanza kucheza katikati kwa furaha.
Nickson akazidi kunywa pombe,hazikupita hata
dakika kumi akazima,akaweka kichwa juu ya meza.
“Ehhh Umezimaaaaaaaa?sasa twenzetu,oyaaa
Nickson Nickiiii”
“Mhhh”
“Twenzetu”
“Niache nilale Gloriaaaa,nimechokaaaa kesho
asubuhi, leo nimechokaaaaa Mke wangu,Sasa
inabidii kesho twendee shambani tukalime,kuna
mboga mboga kule za matembele na
mchicha,tutaenda na Sonia nayeye apajue nataka
yeye ndiye awe mrithi kabla sijafa,nimuandike
kabisa mali zangu zoooooote,pia nina mpango wa
kununua kiwanja kingine Videte”
“Weweeeeee Nickson,wewe Shayooo”
Nickson aliongea vitu vya ajabu huku
akicheua,akavutwa na Tito wakaingia ndani ya
gari,kwa kasi ya ajabu Nickson alitoa gari,japokuwa
alikuwa amelewa chakali, lakini njia ya nyumbani
kwake aliifahamu fika!
Lakini kwa mwendo aliokuwa akitembea nao
ulitisha kupita kiasi,alikuwa ni kama yupo kwenye
mashindano,kutokana na kutokuwa na magari
barabarani baada ya dakika kumi na tano alipiga
breki nje ya nyumba yake,akashuka na Tito.
“Weee Dadaaaaaa”
Rukia alivyosikia mlio wa gari akaruka kutoka
kwenye shuka akafungua mlango,akamkaribisha
bosi wake!
“Dadaaaa niangalie,huyu ni rafiki yanguuuu hayuko
vizuri leo,asubuhi yaaa kesho umtengenezeee
supu,hakikisha analala salamaa,mimi mwambie
niliondoka na Taxi au bajaji,usiku mwema,Good
night,sawa?”
“Ndio nitafanya ivyo”Rukia akaitikia,hali ya watu
hao wawili ilimwogopesha.
Tito aliongea huku akipepesuka akaondoka Rukia
akafunga mlango lakini alivyoingia chumbani
kwake akashtuka kumkuta Nickson amelala.Moyo
ukamuenda mbio.
“Bosiii”
“Gloriaaaaa,njooo basi mpenzi panda kitandaani
tulaleee,Sonia amelala?”
Nickson aliongea huku akimtizama Msichana huyu
wa kazi aliyekuwa mrembo mbele ya macho
yake,akamvuta kama umeme kitandani kwake!
Katika hali ya kutokutegemea akampandia kwa juu
ya kuanza kulana denda,Nickson akili zake
zilimtuma kuwa huyu ndiyo Gloria mke wake na
hapo walipokuwa ni chumbani kwao.Rukia nayeye
akajikuta anatoa ushirikiano wakaanza
kubadilishana mate wakicheza na ndimi!
(BILA KUSAHAU KWAMBA HADITHI HII
INAPATIKANA YOTE WATSAP NA INBOX KWA
MALIPO YA TSHS 3000/- KWA MWEZI.mawasiliano
namba +255718 862176
Sasa unaweza kusoma hadithi za mtunzi kway
insta@storyzakway
ITAENDELEA.