RIWAYA: Mtumwa wa Ngono

RIWAYA: Mtumwa wa Ngono

kitakachoendelea hapo Gloria atawekwa jela au atakufa, Nick atakuwa na house girl msukuma, Sonia atapata malezi mabaya sana. Atakuwa malaya kuliko mama yake na kuambukizwa HIV nk nk
 
Mzee Alex atakuwa mmoja kati ya wengi watakao ambukizwa HIV na ndipo mwisho wa Sonia, mwisho wa riwaya.

Ujinga wa Nick kujifanya malaika umegharimu maisha ya binti yake. So sad.
 
Mzee Alex atakuwa mmoja kati ya wengi watakao ambukizwa HIV na ndipo mwisho wa Sonia, mwisho wa riwaya.

Ujinga wa Nick kujifanya malaika umegharimu maisha ya binti yake. So sad.
prediction yako duh..
 
SLAVE SEX(mtumwa wa ngono)……..(24)
MTUNZI…..EMMANUEL F. KWAY
Contact…..+255718 862176
AGE….(18+)
ILIPOISHIA.
,wakabinuana mpaka jikoni, ambapo mafuta ya
chips yalikuwa jikoni yameiva.Katika kupigana
Gloria akasukumizwa mpaka kwenye jiko la gesi
ambapo alitingisha Sufuria kubwa lililokuwa na
mafuta ya chips likamwagikia Gloria usoni,Uso
wote ukababuka.
“Mamaaaaaaaaaaaa”
Gloria akaachia ukulele wa maumivu.
SONGA NAYO.
Mafuta ya chips yaliyokuwa juu ya jiko la gesi
teyari yalikuwa usoni mwa Gloria yakambabua
ngozi yote ya usoni,hakutofautishwa na mfupa wa
ng’ombe, ngozi yake ikawa kama imegeuzwa
ndani- nje.
Alilia kwa uchungu huku akikaa chini taratibu,
maumivu aliyoyasikia hakuweza kuyafananisha na
kitu chochote kile,akawa analia huku anataja jina la
Nickson,Wakati huo Esta alikuwa ameshakimbia
tayari, hakutaka kukutwa kabisa na kesi hiyo au
kwenda kuisaidia polisi.
“Nicksoooon nakufa mume waaanguu…nisaaa
idieee”
Nickson akiwa bafuni alisikia sauti kama ya mtu
anamuita,alijua sana ni ya mke wake Gloria, lakini
hakutaka kuliamini jibu hilo moja kwa
moja,akafunga bomba la mvua ili kusikiliza
vizuri,sauti ikawa inazidi kupaa na kuita jina lake.
“Gloria!Gloriaaa!Gloriaa”
Nickson aliita ili kulihakiki jibu lake,kwasababu
alimuacha Gloria chumbani muda wa dakika mbili
uliopita kabla ya kuingia bafuni kuoga,
isingewezakana kabisa akawa yeye,akajifunga taulo
na kutoka bafuni,alivyomkosa haraka akarukia
pensi yake kitandani na kuiweka mwilini, akatoka
nje kama mkuki na kufanya agongane kikumbo na
Rukia,hata yeye alikuwa njiani kugonga chumba
cha bosi wake kumpa taarifa juu ya Gloria,
kitendo cha Nickson kutoka alijua fika nayeye
aliisikia sauti ikitokea jirani ikiomba
msaada.Nickson hakuelewa mke wake amekumbwa
na nini, sauti ya kuomba msaada ilimshtua
zaidi,akatembea kwa hatua mbili mbili.
“Gloriaaaa,Gloria”
Aliita huku akifungua mlango taratibu, ambao
ulikuwa umesindikwa tu,akatembea mpaka sauti ya
Gloria ilipo,Moyo wa Nickson ukapiga paaa!
alishtuka na majasho yakaanza kumtoka mwilini
baada ya kumuona mke wake amebabuka uso,
ngozi yake ikiwa inaning’inia.Alikuwa ni kama mtu
aliyechanganyikiwa,alishindwa ni kitu gani akifanye
kwa wakati huo.
Haraka haraka alirudi kwake na kuomba msaada
wa watu kumsaidia ili kumuingiza Gloria ndani ya
gari.Gari likasogezwa na Nickson karibu kabisa na
mlango, Gloria akapakiwa.Kwa spidi aliyotoka nayo
Nickson ilitisha, kila mtu alilishangaa gari lake
likiwa linatimua mavumbi,wengine wakadhani
wenda ni gari la majambazi limetoka kuvamia
benki.
Nickson alikanyaga mafuta na Landcrusier V8
likazidi kuchanja mbuga.
“Gloria,nini kimekupata mke wangu,ilikuwaje tena?”
Nickosn aliuliza huku akiwa katika kasi ya ajabu.
“Nicksoooon, Ngipfyaaa,Ngipfyaaaaa
Nickson”(NICKSON nakufaa nakufaa Nickson”
Gloria akawa anaongea kwa kichaga,maumivu
aliyokuwa akihisi yalimtisha,wasamalia waliokuwa
pembeni yake walimuonea huruma.Kutokana na
siku hiyo hakukuwa na msongamano wa magari
waliweza kufika hospitali ya madona ndani ya
dakika kumi.
Nickson akaweka mguu kati haraka akaruka kama
mwanajeshi akiwa na kipensi,akiomba msaada kwa
wauguzi.
“Kaka vipi imekuaje?”
Nesi mmoja aliuliza baada ya kumshusha Gloria
kwenye gari.
“Sielewi, tafadhali naombeni huduma ya kwanza”
“Sawa,twendeni huku nadhani mafuta ndiyo
yamemuunguza,pole dada”
Nesi alitoa pole lakini Gloria aliendelea kulia kwa
sauti kubwa.
Nickson alichanganyikiwa kupita kiasi,maumivu
aliyoyapata moyoni mwake yalizidi hata ya
Gloria,walikaa hospitali takribani masaa matatu
wakiwasubiri wauguzi wawape majibu.
“Vipi imekuaje,vipi hali ya mke wangu?”
Nickson akamuuliza Muuguzi mmoja aliyetoka
wodini.
“Usiwe na presha anaendelea vizuri,tumemchoma
sindano ya maumivu sasa hivi anaendelea tu vizuri
na tumpaka dawa ambazo zitamsaidia”
“Naweza nikamuona?”
“Sawa,nifuate”
Dokta Mbele Nickson akawa nyuma yake mpaka
chumba alicholazwa Gloria,ambapo kwa wakati huo
alikuwa ana bandeji usoni mwake,alivyomuona
Nickson, alilia tena.
“Gloria usilie sasa,kwani nini kimetokea?”
“Nickson,naomba unisamehee”
“Mimi nishakusamehee,niambie imekuwaje na
unaendeleaje?bado unasikia maumivu?”
“Wamenichoma sindano ya maumivu,sasa hivi
sisikii maumivu tena Nickson”
“Pole mke wangu utapona,sawa Mungu yupo”
“Ahsante”
Gloria alilia sana na kuanza kuhadithia kila kitu
kilichotokea tangu walivyokutana na Pedeshee
kway na Esta kumkuwadia,alijilaumu sana na
alimuomba sana Mme wake msamaha,ni kweli
alikiri makosa yake na alijiona mkosaji mbele za
Mungu.Wakati mwingine aliona kama Nickson ana
mdhiaki tu kwani hakuna binadamu ambaye
angesamehewa makosa kama hayo,yalikuwa ni
mapenzi mazito kutoka kwa Nickson.Hilo alilijua
siku hiyo na tangu walivyorudiana.
“Nickson naomba unisamehee,sitorudia tena”
Gloria alisisitiza.
“Mimi nilishakusamehe Gloria,nilikusamehe
kabisa,na ndiyo maana mpaka leo upo na
mimi,naomba tugange yajayo,yaliyopita si ndwele”
“Ninakuhaidi nitakupenda daima”
“Tuachanae na hayo,tutaongea siku nyingine
kwanza inabidi upatiwe matibabu kwanza”
Matitabu yaliendelea tangu siku hiyo,Gloria alikuwa
akiwekewa bandeji yenye dawa na kufungwa kila
siku,kila Nickson akitoka kazini ilikuwa ni lazima
apite hospitali kumjulia hali mke wake kisha arejee
nyumbani na wakati mwingine walikesha wote
hospitali,mpaka Gloria aliporuhusiwa kwenda
nyumbani baada ya siku saba kufika.
Nickson alimchukia Esta Vibaya sana lakini hakuwa
na la kufanya sababu alijua sheria ingembana.
“Ningemfunga Esta,lakini wewe ndiye uliyeenda
kwake kufanya fujo.kisheria hiyo unashtakiwa
Gloria, sina kifungu cha kumbana ila angekuja hapa
nyumbani na kuyafanya haya,ningemfunga kifungo
cha maisha,hakyanani”
Nickson alimuongelesha Gloria siku hiyo baada ya
kuulizwa kuhusu Esta kama alichukuliwa hatua
yoyote.
“Kwahiyo huwezi hata kumshtaki?”
“Siwezi hata kidogo,sheria itanibana
mimi,tumshukuru Mungu tu umepona na
keshokutwa unaenda kutolewa hiyo bandeji”
“Ahsante Nickson,nataka kwenda kulala”
“Hapana,Rukia anakutengenezea Uji,We Rukiiaaaaa”
“Abeee Baba”
Rukia aliitikia akiwa jikoni.
“Huo uji bado tu?”
“Ndio naweka sukari baba”
“Haya fanya haraka basi”
Baada ya dakika moja Rukia alitokea na
kumkabidhi Nickson kikombe cha uji,Nickson
akawa ana kazi ya kumnywesha mkewe mpaka
ulipoisha.
Siku zote Gloria aliomba Mungu sura yake isije
ikawa imeharibika na mafuta mabaya
yaliyomuunguza usoni,asilimia arobaini ya sura
yake aliamini kuwa ingekuwa imebabuka vibaya
mno.
********
Kama kuna siku ambayo Gloria hatoisahau
maishani mwake ni siku hiyo ambayo alifunguliwa
bandeji usoni,alishtuka na kuangua kilio baada ya
kuomba kioo ajitizame,hakujitofautisha na nyama
mbichi ya Nguruwe,uso wake uliharibika vibaya
sana.Hakukuwa na namna ya kubadilisha ukweli
huo,sura yake nzuri iliyokuwa nyeupe ya kung’aa
sasa iliharibika na kuwa ya kutisha,hakuna
mwanaume yoyote hata angekuwa kipofu
angempenda Gloria.Nickson aliyekuwa mbele yake
alishtuka hata yeye lakini hakutaka kujionesha
waziwazi kuhofia kuwa angemvunja moyo mke
wake.
“Yesu waaaaaanguuu,Nickson sura
yaaaangu….naomba sura yaaangu”
Gloria alizidi kulia.
“Dada usilie,utapona tu taratibu taratibu kuna
madawa tutakupa utatumia,mbona hali yako nzuri
kabisa”
Nesi alijaribu pia kumfariji.
****
HALI ALIYOKUWA NAYO Gloria ilimtesa sana
Nickson,moyoni aliumia sana kumuona mke wake
anateseka, sura yake ikiwa ina mabaka kama gari
la jeshi,ukapita mwezi mzima bila mafanikio
makovu hayakuweza kupotea.
“Duuu nimekumbuka,ngoja nimtafute
Nyagogo,aliniambia china kule alimpeleka mke
wake akafanyiwa surgery akapona”
Nickson akamkumbuka rafiki yake Nyagogo
mfanyabiashara anayemiliki maduka mengi
Musoma na jiji la Dar es salaam,huwa anaenda
china kupakua mizigo kisha kurudi.Akachukua
simu yake ili kujaribu kama yupo China au bado
Tanzania, hakuweka matumaini asilimia mia moja.
“Griii griiiii”
Bahati nzuri simu ikaita akafurahi na kukohoa
kidogo!
“Hallooo”
Upande wa pili ulisikika baada ya simu
kupokelewa.
“Naongea na Nyagogo?”
“Ndio,nani mwenzangu?”
“Nickson Shayo”
“Nickson Shayoo?,Nickson shayooo…aaaaaah
Mangiiiii aise vipi bwasheee?,unanitenga sana siku
izi nilikuwa naitafuta sana namba yako,ukawa
hupatikani”
“Ile namba nilibadilisha,ndiyo maana ukaona
kimnya,vipi biashara?”
Nickson alianza mzunguko kabla ya kusema jambo
lililomfanya apige simu.
“Ivyo ivyo tu,biashara bado ngumu,tunawajibika”
“Bado unafanya biashara zako china?”
“Ndio,naanzaje kuacha”
“Unaenda lini tena huko Mzee?”
“Baada ya wiki mbili”
“Sasa,kuna kitu naomba unisaidie Mzee,nina
matatizo kidogo nimepata”
“Nini tena?”
“Mke wangu ameungua na mafuta sasa nataka
kidogo,akapigwe sop sop huko China,wamuweke
sawa”
“Ahaaaaa,sasa hakuna tabu wewe weka mambo
sawa tu”
“Hilo ondoa shaka,nitawasiliana nawewe kesho
kutwa hapo tuanze taratibu inakubidi uje utokee
huku”
“Lazima nije kutokea huko Dar Nickson”
“Basi sawa Ahsante”
Simu ikakatwa.Nickson akawa na furaha ya
ajabu,ilivyofika jioni siku hiyo alivyorejea,habari ya
kwanza alimwambia mke wake juu ya yeye kwenda
nchini China.Gloria akafurahi kupita kiasi.
“Lakini utaenda peke yako,mimi nitabaki kazini pia
inabidi nimwangalie Sonia”
“Sawa Mme wangu”
Kwa kuwa Nickson alikuwa na pesa Benki alienda
kuchota na kuanza kufanya taratibu za visa na
tiketi,haikuchukua muda mrefu kupitia
kitambulisho chake cha serikali akizuga kuwa mke
wake anahitajika mahakamani kutoa ushahidi wa
kesi,visa ikawa imetoka baada ya wiki moja.Akawa
anasubiriwa Nyagogo afike Dar es salaam ili baada
ya siku mbili safari ya Kwenda china katika jiji la
Beijing ianze.
****
KILA KITU ALIPEWA KUANZIA PICHA YA GLORIA
MPAKA PESA ZA MATUMIZI, Gloria na Nyagogo
walikuwa wapo ndani ya shirika la ndege ya
Kichina,kila Nyagogo alipoitizama picha ya Gloria
alishtuka,uzuri wa msichana huyu ulimtisha kupita
kiasi,akaanza kumkagua akashusha macho yake
mpaka kwenye kifua cha msichana huyu ambayo
yalionekana kwa juu kidogo,weupe wa kifua cha
mke wa rafiki yake ukawa umevuruga akili yake.
“Huyu nikimfanyia Surgery namuoa huko
huko,Nickson hapa hana chake,huyu namkarabati
mpaka shepu,nampiga kalio la kichina lile, Nickson
Kushneiii”
Nickson ikawa kama amemkabizi fisi bucha la
nyama. ITAENDELEA
 
Km namuona gilo akimkibali nyagogo chaa! Kaka Nick imekula kwako
 
Back
Top Bottom