Riwaya: Mkono Wa Chuma

Riwaya: Mkono Wa Chuma

Heshima yenu wakuu. Kwanza poleni na pia samahanini sana kwa kuwaacha kimya kimya kwa muda mrefu bila taarifa rasmi. Majukumu mengine yalinibana, na hivyo sikuweza kabisa kujumuika nanyi hapa jukwaani, ila sasa nimerejea.

Riwaya ambazo nakumbuka hatukufika nazo mwisho bila shaka ni mbili, yani 'Mkono wa Chuma' na 'Mtoto wa Baba Paroko'. Kwa upande wa mkono wa chuma nimeona mkuu SPYMATE ametoa taarifa hapo juu, na ni kweli hayo ndio maelezo ya huyo Alex Kileo mwenyewe. Kabla sijapotea jukwaani nakumbuka nliwahi kumcheki kwenye simu kumuuliza kama anaiuza sehemu iliyobakia, nkiwa na lengo la kuinunua na kuileta hapa, ila alisema 'haiuzwi' na akaahidi tena kua ni lazima ataiendeleza mpaka mwisho, pindi atakapomaliza changamoto zake 'personal' zinazomkabili. Baadae ndio akaleta hiyo taarifa kama ilivyowasilishwa hapo juu.

Kwa upande wa 'Mtoto wa Baba Paroko' nlifanya pia mawasiliano na mtunzi mwenyewe Lello, akasema hiyo itaendelea kama kawaida, na wala haitakua kwenye kitabu. Isipokua kwa sasa anabanwa na zoezi la kuandaa kitabu cha 'Mimi na Rais (the President and I)', na punde atakapomalizana na hilo zoezi atapata wasaa mzuri wa kuiendeleza 'Mtoto wa Baba Paroko'.

Hivyo kwanza niwape pole ya arosto ya muda mrefu, lakini pia niwaombe tuwe wavumilivu wakati tukiendelea kusubiri muendelezo wa hizo riwaya. Tuko pamoja wakuu
Ahsante kwa ufafanuzi Legend tutaendelea kufuta subra mpaka hapo itakapoendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom