Riwaya: Mke wa Rais

Naanza kukubaliana na shunie hii ni izidingo nyingine
 
Hii story iko poa, ila ni inaenda mwendo wa kobe
 
Na wewe ni muhusika( character) mmojawapo wa story

hebu tuhadithie bana nini kinandelea.
Ndugu, Mwanaharamu hawezi kujisimulia alivyo, anavyomwokoa MOA.... Ibra njoo Mkuu watu wanahitaji kuona mambo ya MOA huko alikopelekwa (Victoria base).
 
Hongera kaka
 
MKE WA RAIS

Na Ibrahim Masimba

*******
Lilikuwa faili ambalo hapo mwanzo hakujua linakitu gani. Kule kuambiwa usifungue kulimpa imani ya kupata kile ambacho alikihitaji ama kile ambacho alitaka kukijua. Alitaka kuijua victoria base, alitaka kukijua kile ambacho kimesababisha Rafiki yake kipenzi kuuawa. Baada ya kufungua faili lile cha kwanza kukutana nacho ni ramani kubwa huku pembeni kukiwa na mfano wa kisiwa ambacho kilionekana kuwa na majumba makubwa na chini kidogo kulikuwa na maandishi makubwa yalisomeka kama VICTORIA BASE. Hapo akahisi kitu kichwani kwake. Akahisi kuwa lazima eneo hili analoliona kwenye faili likawa ndio sehemu walipojificha watu wao. Katika Ramani ile hakuna sehemu ambayo palionyesha kuwepo kwa barabara zaidi ya bahari ambayo ililizunguka eneo lote. Hii ilionyesha kwamba kama mtu unahitaji kufika nilazima utumie bahari ama ndege kufika huko. Akazidi kuiangalia kwa umakini mkubwa. Alikuwa akisoma na akitizama kila kitu kwa umakini mkubwa. Alikiangalia huku akinukuu baadhi ya maandishi. Ni katika kutizama huko akagundua kitu, kitu ambacho hapo mwanzo hakuwa amegundua. Pembeni kabisa mwa fukwe za bahari ile akaliona jengo ambalo lilipakana kabisa na kisiwa kile. Licha ya kupakana lakini pia kulionekana kujengwa nje lakini likiingia mpaka nje ya kisiwa. Akatizama kwa muda mrefu sana akiangalia kama kuna kingine ambacho anaweza kugundua lakini hakuweza kugundua chochote. Bado alitaka kuipa kazi akili yake ya kugundua kile ambacho sohwa alitaka wao wa jue. Kwa nini anikabidhi hili disc huku yeye akihatarisha maisha yake? Kuna kitu gani kikubwa katika hiki kitu? Hapo akapata hamu ya kutizama zaidi. Akafungua kwenye faili jingine ambalo lilionekana sohwa kuhifadhi vitu vyake. Akalifungua kwa umakini.. akakutana na Maandishi makubwa yalioandikwa kwa wino mwekundu. NI MUHIMU KUFIKA. chini kulikuwa na maandishi mengine madogo. Yalikuwa maandishi ambayo yalimvutia na kumpa hamu Jenipher Dominic. Alikiona kile ambacho alikiandika Sohwa kabla ya kuuawa. Yalionekana ni maelezo jinsi ya kufika katika kisiwa kile. Kwa maelezo yale kulimpa nguvu na ari zaidi ya kuendekea kusoma. "Kuna sehemu moja tu kwa miguu ya kuingilia huko. Ni ndani ya jengo moja kubwa ambalo linaulizi mkali sana. Jengo hilo linaonekana kujengwa katikati ya bahari lakini likiunganishwa na Nchi kavu. Jengo hilo hulindwa kwa mitambo maalum, mitambo ambayo inauwezo wa kukuona kwa umbali mrefu. Ukiondoa mitambo hiyo pia, kuna ulinzi wa majasusi kutoka NSA na CIA hao utawakuta nje ya jengo hilo ambalo kwa upande wa nchi kavu limejengwa mfano wa jengo la kibiashara, lakini wauzaji wote ni majasusi wa washirika katika suala hili. Unapokwenda pale kuna mitambo maalum ambayo inauwezo wa kugundua chochote ambacho hakionekani kwa macho ama mikono ya majasusi hao. Unapoingia sehemu hiyo ni kama jengo la kibiashara lakini ndani ya jengo hilo ndipo kuna mlango na lifti sambamba na usafiri wa kukufikisha VICTORIA BASE. baada ya maelezo hayo chini kulikuwa na maelezo mengine jinsi ya kuingia humo ndani na kuupata usafiri wa kuwafikisha huko." Baada ya kumaliza kusoma maelezo yale. Jenipher aliinuka na kuelekea bafuni kujimwagia maji akisubiri muda wa kujiandaa sababu ya kufika katika Jengo hilo.

********

Lilikuwa giza ambalo liliyafunika macho yake, giza ambalo halikumuonyesha mwanga wowote hata pale alipo yafumbua macho yake. Mikono yake ilifungwa kwa minyororo sambamba na miguu yake huku akiwa amekarishwa kwenye kitu mfano wa kiti. Giza totoro ndicho kitu kilichomfanya asijaribu kufanya chochote kile. Hakujua waliomfunga pale waliweka na vitu gani vingine. Akailazimisha akili yake iifanye kazi kubwa ya kupanga jinsi ya kutoka hapo. Muda mwingi alikifikiria kile ambacho kilimtokea hapo mwanzo, lakini bado kichwa chake kilikataa kuifanya hiyo kazi. Hakukumbuka chochote, bado hakujua alifikaje pale. Sindano ya Sumu aliopigwa kabla ya kuondolewa na mwanaharamu, bado haikuurudisha mwili wake katika hali yake. Naam, Muddy alikuwa ametulia kwenye giza, ametulia akiwa amefungwa huku na kule. Mwili wake hakuonyesha kuwa na nguvu, haukuonyesha kumudu kufanya lolote katika eneo lile. Licha ya mwili kutokuwa tayari huku akili yake ikishindwa kufanyakazi, muddy alikuwa akiilazimisha akili yake kuwaza, alitaka kuirudisha katika utendaji kazi wake. Hilo likaonekana kuanza kufanikiwa, sura ya kichwa cha sohwa kikiwa hakina kiwiliwili ikamjia. Akakumbuka yote ambayo yalimtokea, akamkumbuka yule mwanamke. Hapo akaiona akili yake ikirudi huku mwili nao ukipata nguvu. Licha ya kutokuja wapi alipo halikumtisha hilo, aliuona uoga wa watu waliomteka. Uoga wa kumuacha hai bila hata kumdhuru. Huu ulikuwa woga wa hali ya juu. Woga kutoka kwa watu ambao waliaminika ndio wenye uwezo katika kazi hizi za kijasusi. Hilo likaendelea kumpa nguvu na kumfanya aivute subira. Sasa alikuwa tayari kukabiliana na lolote. Akaendelea kuuvuta muda, kuuvuta akisubiri wenyeji wake. Hakuwa na hofu tena.

*******
Alivaa miwani ya jua, chini akavaa suruali nyepesi ya kitambaa, miguuni alikuwa amevalia raba nyeupe sambamba na kuvaa tishrt nyeupe. Alikuwa akitembea akielekea kwenye jengo ambalo baada ya kuhangaika sana alifanikiwa kuliona. Lilikuwa Jengo kubwa sana, jengo ambalo liliwavutia watu wengi ambao walifika hapo kufanya manunuzi. Nje ya jengo palikuwepo na watu wengi ambao walionekana ni watu wakawaida hasa ukiwatizama kwa juu juu. Kuna ambao walionekana kubeba mizigo kupeleka sehemu ilimradi wafanikishe kile ambacho wamekipanga. Licha ya kubeba mizigo lakini Muonekana wa watu hawa haukumpa tabu ya kuwajua wao ni kina nani.

Akatembea pasipokuonyesha wasiwasi, akafikiwa kuingia ndani ya jengo hilo baada ya ukaguzi. Akatembea hatua kama tano kuelekea ndani kabisa ya jengo, hatua ya Sita akahisi akiguswa bega.
 
MKE WA RAIS

Mwandishi Ibrahim Masimba

Alitembea kwa hatua tano mbele, alipotaka kupiga hatua ya sita akahisi akiguswa bega. Jenipher akageuka nyuma kutizama. Macho yake yakakutana na mtu mmoja ambaye muonekano wake ulikuwa kama mmoja wa wasaidizi wa mle ndani ya jengo. Tabasamu likachanua mdomoni kwa mwanamume yule alieonyesha ucheshi. Halikuwa rabasamu la kumzuzua Jenipher. Hakuonyesha kutabasamu, bali akatulia akimuangalia mwanamume yule huku miwani ikiwa bado imeziba macho yake. Bado mwanaume yule aliendelea kusimama akitabasamu bila kuongea chochote. Hilo likampa wasiwasi, wasiwasi ambao hakuwa nao hapo mwanzo. Kwa nini anisimamishe harafu hazungumzi chochote? Au amenishtukia? Yalikuwa maswali ambayo hayakupata majibu na wala kukaa sana kichwani. Muda ule ule akaulizwa swali ambalo aliliona kama ni lakipumbavu.

"Unahitaji kitu gani nikusaidie?"

Hakumjibu kwa muda ule, alitulia kama sekunde kumi hivi. Baada ya kutafakari naye akauliza swali badala ya kujibu.

"Kumbe kuna utaratibu wa kuuliza wateja humu ndani? Mbona wenzangu niliongia nao hawakufuatwa na kuulizwa kama mimi? Ama kwa kuwa mimi ni mweusi? " aliongea Jenipher akionyesha kukasirika. Licha ya yeye kukasirika lakini bado yule mwanamume tabasamu lilikuwa usoni. Kuna kitu ambacho hakuwa amekitizama kwa umakini kutoka kwa mwanaume yule. Kitu ambacho kingemrahisishia kile ambacho alikizani. Kwa mara ya kwanza Jenipher alikuwa akikigundua kitu ambacho hakuwa amekigundua hapo mwanzo. Mtu aliembele yake nusura amfanye apige kelele. Alikuwa akitizamana na Mwanaharamu, alikuwa akitizamana na Nemisis the bastard, akiwa mtu mwingine kabisa, akionekana ni kama mwanaume wa kizungu. Wakatizamana tena na tena. Macho yakaongea ndani ya sekunde na hata sekunde ya pili ilipoingia kila mmoja alikuwa akielekea njia yake ndani ya jengo lile. Ulikuwa ni muda wa kuitafuta njia ndani ya jengo lile. Ulikuwa ni muda wa kuitafuta njia kuelekea ndani Victoria Base. Angeipataje njia wakati kila kona walisimama watu wa FSB, NSA, na MOSSAD. Wote hakuonyesha kama wapo hapo, wote hawakuonyesha kufuatilia kinachoendelea. Walionekana kama marofa wa kibeba hili na kuacha lile. Hilo halikumfanya Jenipher atishike kwa kuwa alishaaambiwa na Sohwa ulinzi ambao upo katika jengo lile. Akatembea macho yake yakitafuta maandishi alioelezwa na sohwa huku akiuliza hiki na kile. Hatua kumi mbele alikuwa akiliona lile ambalo alikuwa akikitafuta. Maandishi ambayo yalisomeka kama sehemu ile ni choo yakaonekana. Akatembea tena safari hii kwa uangalifu. Hakuufanya uso wake kuonyesha tofauti kwa kuwa alijua kuna sehemu alikuwa akitizamwa na watu fulani. Alipoifikia sehemu ile mkono wake ukapenya sehemu na kubonyeza kitu fulani, muda ule ule kamera za Jengo lile zote zikazima. Kilikuwa ni kitendo cha sekunde moja kutendeka lakini wakati akitaka kupiga hatua kuendelea mbele akausikia ubaridi ukigota shingoni kisha sauti nzito ikanguruma kutoka nyuma yake. "Tulia Hivyo hivyo!" Jenpher akatulia. Akatakiwa ageuke kuongoza. Kule ambapo alikuwa akielekea. Jane akatii.. Akatembea huku akiitafuta namna ya kujiondoa mikononi kwa mtu huyu alienyuma yake. Lakini hilo alitaka kulifanya watakapoingia sehemu sahihi. Lakini hilo halikufika popote, halikufika kwa kuwa Mwanaharamu alikuwepo na alilishuhudia. Hata pale wakati Jane akiongozwa kuelekea sehemu moja mle ndani, mlango wa mbele ukafunguliwa. Mbele ya Jane akatokea mtu yule yule ambaye hapo mwanzo alikuwa akitabasamu.

Mwanaharamu alikuwa akitokea chumba cha mbele akionekana kama mwenyeji katika viunga vile. Hilo likaonekana kumshangaza huyu aliyenyuma ya Jane. Kidole kikashuka kwenye Trigger. .lakini kabla hajafanya chochote akakisikia kitu kikipenya kwenye paji la Uso, akajiona akirushwa na kwenda kutupwa mbali. Hakuinuka tena kwa kuwa alikuwa maiti. Wakatizamana, bila kuongea chochote, kisha wakaianza safari ya kuitafuta njia ya kuifikia Victoria.

********

Bado hakujua wapi alipo na bado hakuwa amegundua yupo hapo kwa sababu zipi. Wazo kwamba alikuwa mateka ndilo pekee ambalo lilikuwa kichwani mwake. Akaivuta subira ya kumuona mwenyeji wake, mwenyeji ambaye hakuwa na adabu. Alitamani kumuona ama kuwaona watu waliomfikisha hapo. Alikaa hapo kwa muda bila kutokea kwa watu hao. Mikono pamoja na miguu iliuma kutokana na kuwekwa hapo kwa muda mrefu. Bado hakutaka kuthubutu kujitingisha, hakutaka kufanya hivyo kwa kuwa aliwajua majasusi wa kiisrael walivyo na Roho ngumu. Akaamua kutulia tena na tena. Punde akausikia mlango ukifunguliwa kisha taa kuwashwa. Chumba chote kikatoa mwanga. MUDY akajikuta akitizamana na sura ambazo hazikuionyesha utani. Walikuwa watu watatu ambao kwa kuwatizama tu.. ungehisi kitu kingine. Mudy akainua macho yake kuwatizama, hata macho yao yalivyokutana kila mmoja akaguna. Sio kuguna kwa woga ama chochote kingine, hawa waliguna kwa kumtambua na kumjua huyu aliembele yao. Hata Mudy naye aliwatambua watu hawa, watu ambao walikuwa marafiki kwenye mission fulani kule paris. Lakini hapa walikuwa wakikutana katika pande mbili tofauti. Pande hazikuwa zikifungamana. Wote wakatizamana kwa muda hakuna ambaye alitaka kuamua chochote, hakuna ambaye alithubutu kuongea. Chumba kizima kilikuwa kimya hata mlango wa kichumba kile ulipofunguliwa na sura mwanaume mwingine kutamalaki bado ukimya ulitanda. Lakini safari hii huyu alieingia akishindwa kunyamaza kabisaa na badala yake akaita Jina..

"MOA!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…