Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

Mwandishi Ibrahim Masimba

******
Hakuwa kushindwa kwa njia yoyote, hata yeye hakuamini kama binti yule aliweza kuvumilia mateso yote bila kusema chochote. Alishakutana na watu wengi wenye roho ngumu lakini kwa mwanamke yule ilikuwa ni habari nyingine. Alitumia mbinu zote lakini bado hakuambulia kitu. Akamuacha akiwa amelala kama mfu, akiwa amelala kama maiti, damu zilikuwa zimeunda mfereji na kwenda kutengeneza dimbwi kubwa. Mwili wa mwanamke yule haukutamanika kutokana na majeraha.. alilala mfano wa mfu.. licha ya mateso makali aliopitia lakini kamwe hakuufungua mdomo wake kusema chochote. Kwao ilikuwa ni bora kufa kuliko kuongea chochote kile. Hata mlango ulipofunguliwa na mtu kutoka ndipo hapo Sylivia alikumbuka kuwa alikuwa na kidonge kimoja, kidonge ambacho ilikuwa silaha ya mwisho kwao katika kujiangamiza hasa pale wanahisi kushindwa kuvumilia. Mkono wake dhaifu ukatambaa taratibu kuelekea sehemu ambayo kilihifadhiwa kile kidonge. Hakujali maumivu makali aliokuwa akijisikia kwa wakati ule, hakujali jeraha kubwa la risasi ambalo lilikuwa begani. Mkono ukafika sehemu husika na kutoka na kile ambacho kilikusudiwa. Punde kidonge kikapelekwa mdomoni pasipo kuonwa na mtu yoyote. Baada ya hapo akatulia akikisikilizia kile ambacho alikitegemea. Sekunde kumi mbele shingo yake ikalegea na kugeuka huku macho yakiwa wazi. Mapovu yalikuwa yakitoka mdomoni.. alikuwa maiti. MUda ule ule mlango ukafunguliwa, akaingia Nemisis the bastard. Alikuwa amekatia vitu vya kutesea mikononi. Lakini alipousukuma mlango kisha kuruhusu macho yake yatembee juu ya mwili wa mwanamke yule akagundua kuwa hapakuwa na uhai kwa mateka wake. Akasogea zaidi na zaidi mpaka ulipolala mwili ule usio na uhai. Povu lililokuwa likishuka mdomoni lilikuwa limempa majibu, majibu ambayo hakuyapenda. Alimtegemea huyu mtu ampe japo kwa uchache kuhusu huko Victoria. Lakini kabla hajapata chochote tayari mateka wake ameshakufa. Mwanaharamu akamtiza kwa muda mrefu pasipokuongea kitu. Hakutakiwa kuwepo pale tena, hakutakiwa kuzubaa au kushangaa, alitakiwa kujua ni wapi huko victoria. Akauangalia tena mwili wa mwanamke yule, akainuka na kuufunga mlango wa chumba kile. Akaondoka eneo lile akiamua kuelekea huko, akielekea kwenye moto wenyewe. Alitaka kuifanyakazi kwa mikono yake, alitaka kuifanya kazi kwa wakati huu. Na haikuwa kazi yingine zaidi ya kuisambaratisha VICTORIA BASE.

********

Alionekana kama msichana mchafu na ombaomba, alikuwa amesimama nje ya hoteli kubwa ya kifahari akionekana kutetemeka kwa baridi. Mavazi yake chakavu hayakuwa sababu ya kuuficha uzuri wake. Mavazi yake chakavu haikuwa sababu ya kulificha umbo lake. Alikuwa mzuri, mrembo na kilakitu ambacho kilikuwa ndani yake kilikuwa kizuri. Macho yake yalikuwa yakitizama ndani ya hoteli na wakati mwingine Nje. Hakuna ambaye alimtilia manani kutokana na mavazi yake husika. Lakini haikuchukua muda msichana yule kutoweka katika namna ambay hakuna ambaye alimuona. Hakuondoka kwenda popote bali kile ambacho kilitokea muda mfupi ndani ya hotel ile ndicho kilichomuondoa. Hata pale alipowaona watu watano wakitoka ndani ya hoteli huku wamebeba mifuko maalumu ya kuwekea maiti, yeye tayari alikuwa upande wa pili wa barabara macho yake yakiangalia kitendo kilichokuwa kikitendeka. Huyu alikuwa Neema Habibu. Alikuja muda mrefu sana akitizama hiki na kile ambacho kilikuwa kikifanyika. Maneno ya mwanaharamu kuwa Muddy hakuwa na nguvu za kutosha kupambana ndiyo yaliomfanya Neema kufika hapo akiwa sambamba na Mwanaharamu. Baada ya kufika hapo, yeye alifanyakazi moja ya kuhakikisha macho yake hayabanduki kule alipokaa Muddy. Ni wakati akilifanya hilo ndipo alipowaona watu watano wakiingia, ikiwa ni baada ya kumuona Mudy akielekea mapokezi. Hata pale Muddy alipoondoka pale mapokezi na kuelekea chumbani bado alikuwa akikitizama kile kitendo. Muda mfupi baada ya Muddy kuondoka pale mapokezi, akawaona watu wale nao wakielekea mapokezi na baadae kuelekea kule ambapo alikuwa akielekea Muddy. Kengele ya Tahadhali akalia kichwani kwake. Akajua watu wale lazima wanamfuata Muddy. Akatamani kwenda huko ndani akamwambie Muddy kuwa anafuatwa. Lakini mavazi yake hayakuruhusu hilo. Wakati akifikiria kipi ambacho anaweza kufanya, akawaona watu walewale wakitoka lakini safari hii wakiwa wamebeba kitu mfano wa mtu. Hapo hisia kuwa Muddy alikuwa msambweni zilimjia. Hapo akaamua kufanya kitu, kitu ambacho kilikuwa cha hatari sana. Aliamua kuzifuatilia gari zile ili kujua ni wapi zinaelekea.

**********

Alipotoka pale kwenye chumba alichomuacha yule binti akiwa tayari na zana zake za kazi. Mwanaharamu alikuwa ndani ya tax akielekea kule ambako aliambiwa na Neema kuwa kuna kitu kinaendelea. Alikuwa na bastola tatu katika sehemu tofauti. Alikuwa na visu vitatu, magazine tatu za risasi. Gari ilikuwa akitembea katika mwendo wa kasi, muda mwingi Mwanaharamu alikuwa akiwasiliana na Neema kujua kile ambacho kilikuwa kikiendelea. Upande wa Neema hata yeye alikuwa kwenye gari akiendesha mwenyewe. Alikuwa nyuma kwa magari matano kuepuka kushtukiwa mapema. Aliiacha magari yale yatangulie kisha yeye akifuatilia kwa nyuma. Bado alihakikisha magari yale hayampotezi.. lakini mwendo wa dakika kama kumi mbele, akakiona kitu ambacho hakukitegemea. Magari matatu ambayo alitoka nayo sambamba kule hotelini yote yakasimama na magari mengine yakipita barabara nyingine. Hilo kwake hakulitegemea, hakulitegemea kwa kuwa muda ule ule akausikia mngurumo wa helkopta, sekunde tano baadae akaiona milango ya gari zile ikifunguliwa, wakashuka wale watu watano wakiwa sambamba na mfuko wao. Helkopta ikazidi kushuka. Neema akatamani kusimamisha gari lakini akaogopa kushtukiwa. Akapita akishuhudia mwili wa mtu ukipakiwa ndani ya helkopta na muda ule ule helkopta ikapaaa na kutokomea.
 
Mimi sio Shigongo na Hata Riwaya zetu Hazifanani.. unawezekana huzifahamu Riwaya za aina hii.. Nikuulize swali ushawahi kuona wapi Riwaya za Hayati BEN MTOBWA NA ELVIS MUSIBA ZIKIWA NA LUGHA TOFAUTI? TUTARUDI NA ROHO ZETU LICHA YA ASILIMIA 80 KUWA KATIKA NCHINI ZA MAGHARIBI UMEONA KUNA SEHEMU KULIKUWA NA LUGHA TOFAUTI NA KISWAHILI?

TUACHE UTUMWA WA KIFIKRA
mkuu, nadhani unapanic sana, kwa namna hii huwezi kujifunza, mimi napokuuliza unatakiwa kuunijibu, na sikusema UTUMWA WA FIKRA, Sidhani kama jibu lako umelifikiria sana, anyway asante sana
 
MKE WA RAIS

Na IBRAHIM MASIMBA

*******
Ulikuwa mchezo uliochezwa kwa dakika moja tu, mchezo ambao ulimuacha Neema katika bumbuwazi. Hata alipokuja kugutuka kutoka huko alikokuwa, aliishuhudia helkopta ikitokomea na kupotea katika upeo wa macho yake. Akahamanika kwa muda akitaka kurudi pale nyuma. Lakini alipokumbuka kuwa nyuma kuna gari za watu wale ikabidi atulie kwanza. Alichokifanya ni kushuka na kujifanya kama anaingalia gari yake kuonyesha kama imeharibika. Aliinama huku akigusa hiki na kugusa kile, macho yake yakitizama huku na huko kama mtu ambaye alikuwa akiusubiri msaada kutoka sehemu. Macho yake yalikuwa yakitizama kwa chati kule yalipokuwa yamesimama yale magari. Alikuwa akitamani kumuona Mwanaharamu akitokea pale pale, lakini muda ulisonga bila kuonekana kwake. Akatulia akiendelea huku na huko, magari yakaendelea kupita huku yale mengine yakiwa bado yamesimama. Akaivuta subira ili kukiona kile ambacho kinaendelea. Punde akaliona gari likipita, gari ambalo lilipoufikia usawa wake kioo kikashushwa, akatimazamana ma mtu ambaye alikuwa ndani ya gari ile. Tabasamu likatamaki, alikuwa akitizamana na Mwanaharamu. Licha ya kutizamana lakini hakusimama, alimpita akimpa ishara fulani. Wakati Neema akiifikiria ile Ishara akauona mlango wa gari moja kati ya magari yale ukifunguliwa. Akashuka mwanaume wa makamo, mfupi mweusi na mwenye mwili uliojengeka kimazoezi. Baada ya mwanaume yule kushuka alionekana akiangalia huku na huko huku muda mwingi akionekana kutizama pale aliposimama Neema. Kweli punde akaonekana akivuka barabara kisha kuongoza pale aliposimama Neema. Kila hatua Neema alikuwa akiitizama katika namna ya kipekee. Mkono wake mmoja ulikuwa tayari kushuka ilipo bastola, lakini bado alihitaji kuuona mwisho wa mwanaume yule. Alitembea huku mwili wake ukisadifu kilichopo ndani, ukisadifu ujuaji, ukatili na hata ufundi wa mapigano. Muda mfupi alikuwa amesimama pembeni mwa gari ya Neema huku tabasamu likitamalaki mdomoni. Neema hakumtizama na hakumjali, alimuacha kwanza ili aangalie kipi ambacho angefanya.

"Hellow bibie!" Akaita mwanaume yule huku akimkadhia macho.

"Yeah!, aliitika Neema huku akiendelea kutizama gari yake.

"Nimekuona umesimama hapa kwa muda mrefu. Vipi unatatizo?" Akauliza tena huku sasa akisogea karibu zaidi. Akili ya Neema ikachemka kwa haraka, usogeaji wa mwanaume yule hakuuamini, hakuuamini kwa kuwa alijua ni mmoja kati ambao walibeba kitu ambacho alihisi ulikuwa mwili wa Muddy. Akatafuta Jibu la kutoa, hakutaka kusema gari ilikuwa mbovu akihofia kugundulika mapema.

Baada ya kufikiria nini ajibu, kwa mara ya kwanza Neema akainuka na kugeuka kisha kumtizama mwanaume yule. Macho yao yakakutana, yakaangaliana kisha kutambuana. Wote walikuwa watu katika fani moja, watu kama fani ya mapigano na hata ujasusi. Kutizamwa na mwanamke yule kisha kugundua kile ambacho kilikuwa ndani ya macho ya binti yule, kilimpumbaza na kumduwaza, akapoteza umakini akihitaji kujiridhisha, mkono wake ukashuka, mkono wake ukaifikia bastola ndani ya nukta moja. Lakini hakutambua alikuwa na nani, hakutambua Neema alikuwa nani, na hata mkono wake ulipoifikia bastola yake, tayari Neema alikuwa ameshafyatuka mateke mfululizo ambayo yaliingia bila kipingamizi na kumtupa mwanaume yule chini. Lakini muda ule ule akamuona mtu yule akichupa na kusimama tena. Lakini alijikuta akitizamana na mdomo wa bastola aina ya Revolver colt 38 ikiwa imeshikiliwa sawa sawia na mtoto wa kike. Akatulia, akatulia akiinyoosha mikono juu kutii sheria bila shuruti. Hapakuwa na muda wa kusubiri, kidole chake kikashuka na kuiruhusu Risasi, punde mtuu yule akapaa na kuanguka katikati ya Barabarani. Kilikuwa kitendo kilichotendwa kwa muda mfupi sana. Ni macho ya watu wachache sana ndio walifanikiwa kukiona kile ambacho kimetokea pale. Wengi walikidharau wakidhani ni waigizaji wakifanya yao. Lakini baada ya kumuona mwanaume akianguka katikati ya barabara hapo ndipo walipotambua kuwa hapa kuwa na uigizaji. Hata pale walipohamisha macho yao kutizama kule alipokuwa amesimama yule mwanamke hawakumuona. Alikuwa amepotea kwenye macho yao mfano wa barufu kwenye jua. Hawakumuona alipopitia wala kule alikoelekea. Alikuwa kama kivuli, kivuli ambacho katu hakionekana gizani. Neema akatokomea akiiacha taharaki nyuma yake. Simu zikatembea kwa muda mfupi, magari ya polisi yakiwasili huku watu wa usalama wakizingira eneo lote.

Neema hakuwepo pale na hata gari yake haikuwepo, alikuwa ameondoka pasipo kuonekana.

********

Macho yake yalikuwa yamegandishwa yakiangalia ndani ya simu ya Mohammed. Alikuwa akitizama picha ya Sohwa, picha ya kusikitisha na kutisha. Picha ya kichwa pekee cha Sohwa kikiwa hakina kiwiliwili. Aliitizama picha kwa muda mrefu sana. Akaiweka simu pembeni kisha kuichukua cd ambayo aliichukua sehemu akiwa na Sohwa. Ilikuwa siku ya mwisho kumuona sohwa. Akaipachika tena na kuanza kutizama upya. Akili yake akaituliza kwwnye kitu kile, alitulia akiangalia na kuzingatia kila kitu. Aliandika hili na lile na kufanya hiki na kile. Punde likaja andishi ambalo hapo mwanzo hawakuwa wameliona. 'USIFUNGUE" Lilikuwa ni Neno ambalo lilisomeka katika moja ya mafaili yaliopo ndani ya laptop. Moyo wake ukapigaaa paaaa.. Akaongeza umakini, kisha akaanza kufungua....
 
thank you,
then ukiipeleka kwa aditor na kuchapwa kitabu kitauzika sana tena sana tu
 
Back
Top Bottom