Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

Mwandishi Ibrahim Masimba

******
"MOA. "

ilikuwa sauti kutoka kwa mtu yule wanne alieingia. Macho yake yalikuwa yamemtizama Muddy usoni, huku yakishindwa kuuficha mshangao. Alionyesha kuvitarajia vyote lakini hakutarajia kumuona Muddy katika Eneo hilo. Hata pale mudy alipoendelea kuwaangalia kila mmoja alionyesha kushangazwa. Ni huyu huyu mudy ambaye alisaidiana na FSB Kumrudisha nyumbani Carlos Mendes porkovinic, ni huyu huyu mudy aliesafiri umbali mrefu kutoka africa kuja kusaidia katika tukio lile, lakini leo alikuwa ndani ya kisiwa, ndani ya kambi hatari yenye watu wenyekutii kila amri. Watu wenye ujuzi wa kimapigano, watu wenye kila aina ya unyama na unyankuzi. Alitakiwa kuuawa kabla ya kuhojiwa, alihitaji kupotezwa hata kabla jua la asubuhi halijachomoza. Nani angemuua Mudy licha ya amri, nani angemuaa Mudy wakati kila mmoja aliufahamu msaada wa mudy? Hilo likawa gumu, hilo likawapa mzubao wa kama sekunde kila mmoja akifikiria nini akifanye. Haikuwa kutolewa kazi ikawa ngumu kwao kama hii ya kumpoteza Mudy. Bado ilikuwa ngumu kutii amri hiyo. Hakuna alienua wala kufungua kinywa, lakini Muda ule ule akamuona mwanamke akiingia, mwanamke mweusi wa asili. Alikuwa akitembea kana kwamba alikuwa juu ya jukwaa la uanamitindo, alikuwa akitembea kana kwanba alikuwa akiiogopa ardhi, na mwisho alitembea kana kwamba alikuwa akitizamwa na macho ya wanaume, macho yenye uchu kutokana na umbo mubashara la mwanadada huyu. Licha ya urembo na mwende wake wa modoido lakini usoni hakulionyesha lile ambalo lilionekana kwenye mwendo na hata umbile lake. Macho yalisadifu kifo, macho yaliongea mauaji. Akaendelea kutembea akielekea pale alipofungwa Mohamed. Kila mmoja akionekana kumuangalia, wakati anamkaribia Mudy akakichomoa kisu kikubwa mfano wa panga, akasogea zaidi huku mkono wake Ukianza kulinyanyua panga tayari kummaliza Mudy. Lakini hakulifikia lengo, hakulifikia na wala hakuweza kuipiga hatua nyingine. Akausikia mlango ukisukumwa tofauti na mwanzo, mlango uliofunguliwa ukiambatana na Risasi ambayo ilitua sawia kwenye bega la Mwanamke yule. Panga likaponyoka na kuanguka chini, hata pale alipoushusha mkono wake kuupeleka pale palipo na bastola alichelewa sana. Alichelewa kwa kuwa risasi mbili zilipenya kichwani na kukifumua kichwa chake. Kilikuwa kitendo ambacho hakikuzidi hata dakika mbili katika kuchezwa. Kitendo kilichowaacha katika mshangao, mshangao wakimuangalia huyu mtu alieingia hapa. Walikuwa wakitizama na Mwanaharamu, walikuwa wakitizamana na mtu mfano wa mzimu, hawakuwahi kulitambua hilo mapema. Hata pale alipopiga risasi minyororo aliofungwa Mudy Bado walikuwa wamepigwa na butwaaa.

Mudy akajiondoa pale na kuichukua bastola ambayo ilikuwa kiunoni kwa mwanamke yule ambaye alishakuwa marehemu.
Baada ya hilo wakawageukia watu wale ambao hapo mwanzo walikosa kufanya maamuzi, lakini alichokutana nacho safari hii kilikuwa kitu kingine kabisa, kilikuwa kitu ambacho hakukiwaza, hapakuwa na hata mmoja, hapakuwepo na mwingine zaidi yake na mwanaharamu. Hilo halikuwashtua hata kidogo, hilo halikuwatisha bali liliwafanya watoke katika kichumba kile wakiwa katikati utayari, wakiwa katika kuua, kujilinda ama kushambulia. Wakati wanamaliza kutoka katika chumba kile, wakausikia mlio wa bunduki, hii haikuwa bastola wala smg, hii haikuwa rifle wala shotgun. . Huu ulikuwa mlio mzito wa Ak 47, Bunduki kubwa ya kivita. Kusikika kwa Bunduki hiyo kulitoa tahadhali kwao kwamba tayari kumekucha. Walitakiwa kupambana katika muda na wakati sahihi, muda ambao ungewafanya waondoke katika usahihi. Walipofikia mbele kidogo wakajigawa kila mtu na upande wake, wakati mudy akielekea kaskazini, mwanaharamu alikuwa akielekea kusini. Bado milio ya risasi ilitamalaki kila kona ya kisiwa kile. Kila alipokuwa akipita Mudy na Hata mwanaharamu walikuwa wakikutana na maiti waliolala katikati ya madimbwi ya damu. Hilo likawapa hamu ya kupambana, hilo likawapa hamu ya kujua ninani ambao wanasaidia katika hili. Ingawa Mwanaharamu aliingia sambamba na Jenipher lakini hakuuamini kwamba kazi yote ile alikuwa akiifanya yeye. Alijua lazima kungekuwa na watu, alijua lazima ni watu zaidi ya mmoja au wawili wanaoifanyakazi ile. Hakumjua Jenipher, hakumjua kuwa alikuwa mtu hatari kuwahi kutokea.

Bado aliendelea kusongambele akiifuata milio ya risasi inapotokea. Mkononi alikuwa amekamatia bastola sambamba na kisu kikubwa mkono wa kushoto. Kila alipokuwa akipita alikuwa akioona mili ya watu ikiwa imelaliana. Damu zilinuka kila kona. Hakutaka kusimama bado ilielekea ndani kabisa ya majengo tayari kwa kuwatafuta watu wao. Alifanikiwa kuuvuka mlango na kuingia ndani, hapo akaikuta sebule pana yenye ukimya wa kutia shaka. Kila hatua yake ilikuwa ikienda sambamba na mdomo wa bastola, bado palikuwa kimya kuonyesha hapakuwa na mtu. Hata alipoimaliza ile sebule bado hapakutokea lolote. Akaufikia mlango wa pili akaufungua taratibu kisha akachungulia ndani. Macho yake yakavutwa na Tukio ambalo lilikuwa limetendeka pale. Miili ya watu weusi ilikuwa imelaliana na kutengeneza Dimbwi kubwa la damu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom