[19:30, 12/02/2017] Ibrahim Masimba: MKE WA RAIS
Mwandishi
IBRAHIM MASIMBA
*****
Macho yake yalitua kwenye miili ya miili ya watu weusi iliotambarajika na kulitengeneza dimbwi kubwa la damu. Kila mmoja alionekana kutokuwa na uhai. Hawakuonekana kupumua na hata kujitingisha. Bado damu ilikuwa akitembea taratibu katika sakafu ya chumba kile. Chumba kilichokuwa kikinuka mauti, chumba kilichokuwa kikinuka damu. Harafu ya kifo ilikuwa puani kwa mudy na hata sauti ya Israil mtoa roho ilipenya masikioni mwake. Mudy akauruhusu mguu wake wa kwanza kusogea ndani, hata mguu wa pili uliposogea ndipo alipojihisi kuwa hakutakiwa kuingia katika chumba kile, hakutakiwa kwa kuwa hakujua nani alikuwepo ndani, hakujua kwamba ulikuwa mtego, hakujua kuwa hakutakiwa kuingia mle ndani. Kule kuruhusu mguu wake kupiga hatua ya pili na kuuruhusu mwili kuingia, huku nyuma mlango wa chumba kile ukajifunga. Kujifunga kuliko ambatana na hewa nzito kutamalaki. Mudy akajiona mjinga kwa kuiruhusu akili yake kufanyakazi tofauti, kuifanyakazi ambayo hapo mwanzo asingeifanya. Ameupeleka wapi uwezo wake wa utambuzi? Mbona kama sio mudy yeye? Yalikuwa maswali mawili mazito. Hewa nzito ikazidi ndani ya chumba kile. Mudy alikuwa amekwama akitizama huku na Huko kuona kama atapata msaada. Lakini hakuona chochote ambacho kingemuwezesha kutoka salama. Akaikusanya mikono yake na kuirudisha kifuani. Alikuwa akikisubiri kifo chake, licha ya kujua kuwa anakufa lakini usoni bado alikuwa akitabasamu. Alikuwa anakufa kwa kuipigania nchi yake, alikuwa anakufa kwasababu ya nchi yake. Akainua uso wake juu, hakukiogopa kifo lakini hakupenda kufa kabla ya kuimaliza kazi hii. Macho yake yakatoa machozi, lakini chozi lile halikufanikiwa kushuka na kudondoka chini. Akaiona ardhi ikifunguka kisha yeye kuvutwa kwa nguvu kisha ardhi kujifunga tena. Hilo lilifanyika katika muda wa sekunde mbili na nusu. Hata yeye hakuwa amekitarajia kitendo kile. Alikuwa ametua mbele ya watu watatu, mbele ya watu wenye ngozi nyeupe. Watu ambao hawakuwa wa rangi yake. Hawa walikuwa wale majasusi wa FSB. Wote walikuwa wakimuangalia mudy huku mmoja akidiliki kumpa mudy kidonge. Kilikuwa kidonge cha kuzuia athari ambazo husababishwa na mvuke ule.
******
Wakati hilo likiendelea kutendeka ndani ya kisiwa kile, tayari Mwanaharamu alishakutana na Jenipher. Tayari mwanaharamu alikuwa amekishuhudia kile ambacho hakuwahi kukishuhudia kwa miaka kadhaa. Alishangazwa na uwezo wa Jenipher, alishangazwa na utaalamu wa jenipher. Maiti zilitapakaa huku damu zikichuruzika mfano wa maji. Alikuwa akiwaangalia vipande wa watu walivyotambarajika. Hata pale macho yake yalipomshuhudia Jenipher akipambana kwa mikono, bado hakuamini kama huyu alikuwa ni mwanamke. Aliusuuza moyo na kuuburudisha mwili wake. Aliutamani upiganaji wa mwanamke huyu. Hakuweza kuufananisha na upiganaji wa mtu mwingine, hakufanana na Neema na Hakunaendana na Sohwa. Labda kidogo unaweza kumfananisha na Nuru, Nuru yule aliyekuwa mke wa mpelelezi nambari moja africa. Nuru Yule wa Joram Kiango. Nuru yule wa kwenye Roho ya paka na hata Malaika wa Shetani. Huyu alifanana na mwanadada huyo, mwanadada ambaye amekuwa katika misukosuko. Huyu na Joram Ndio waliomfanya nguli wa Kuandika Riwaya BEN MTOBWA kuinua kalamu yake kuandika kila heka heka waliopitia. Mwanaharamu leo alikuwa akiuangalia upambanaji ule, upambanaji alioupenda na kuuhusudu. Yalikuwa mapambano makali sana, yalikuwa mapambano ya kufa na kupona. Akajitizama akikilazimisha kitu, kitu ambacho ulikuwa ugonjwa kwake.. bastola mkononi akielekea mbele, bastola mkononi akikitafuta chumba, akikitafuta chumba cha mawasiliano. Alikuwa akikitafuta chumba kwa sababu alitaka kukata mawasiliano ya kisiwa kile na upande wa miji mingine. Alijua hilo lingewawezesha kufanya chochote kile bila mawasiliano kufika sehemu nyingine. Hicho ndicho kilichofanyika..
[11:53, 15/02/2017] Ibrahim Masimba: MKE WA RAIS
Mwandishi Ibrahim Masimba
Ndicho kilichofanyika katika muda ule, ndicho kilichofanyika hapo. Muda mfupi hapakuwa na mawasiliano tena. Bado hali haikuwa nzuri, bado hali haikuwa katika usalama. Damu, maiti zilizotapakaa na harufu ya baruti ndio kitu pekee kilichoonekana na kupenya kwenye matundu ya pua. Mwanaharamu akajiondoa ndani ya chumba kile bastola mkononi, akakivuta kitasa na kuufungua mlango tayari kwa safari ya damu, kifo na hata kupona. Akaifuata korido moja ambayo ilikuwa kimya sana. Hapakuonekana uwepo wa mtu, bado hakuuamini ukimya huo.. hata alipopiga hatua bado hakutaka kuamini kama hapakuwa na watu eneo lile. Alijuwa wapo sehemu na walikuwa wakimuangalia ama kumtega ili kufika usawa fulani. Hilo alilichukulia uhakika wa asilimia mia moja. Akatembea akiruhusu macho yatembee kila upande, macho yaangalie hapa na kuangalia pale, yatizame hiki na kukiangalia kile. Hakutaka kudharau kitu ambacho angekitilia mashaka. Alitaka kila kitu akifanye kwa uhakika wa isilimia zote. Muda mfupi alikuwa akiiangaliana na chumba kingine lakini kitupu, chumba ambacho hakikuwa na mtu. Chumba ambacho licha ya kutokuwa na mtu, lakini pia kilikuwa shaghalabaghala. Hilo likayavutia macho yake, kuyavutia macho yake ambayo yalikuwa yakitua kila sehemu. Hapo akaiona alama, alama ya soli ya kiatu. Soli kuonyesha kuwa palikuwa na mtu ndani ya chumba kile. Hilo likaongeza Umakini kwa mwanaharamu, umakini na utayari, utayari wa mapambano.. akairuhusu miguu yake kutembea huku mdomo wa bastola ukitangulia mbele yake. Akaingia zaidi na zaidi, kufika pembeni ya kitandana akakiona kitu kama remoti, remoti ambayo hakujua ilikuwa pale kwa nini. Alichokifanya nikuongeza umakini, akaangaza macho sehemu zote lakini hakuweza kukiona kitu chochote zaidi ya rimoti ambayo ilikuwa chini. Hilo likampa tafakuli, haikuwa pale kwa bahati mbaya, haikuwa pale kwa bahati mbaya, ilikuwa pale kwa makusudi, makusudi ambayo bado hakuyajua. Akairuka Rimoti na kuelekea ukutani, akagusa hiki na kuachia kile. Punde macho yake yakaziona namba ambazo zilikuwa zimefichwa kwa ustadi mkubwa kwa kufunikwa na vitu vingine.
Hakutaka kukurupuka kushika, bado aliendelea kuangalia kwa umakini kama kuna kingine cja hatari. Lakini haikuwa hivyo, hapakuwa na chochote. Wakati anaangalia hilo, akahisi mlango wa chumba kile ukifunguliwa taratibu, kisha akakiona kitu mfano wa kivuli kikiingia. Hakuwahi kupuuza hisia zake. Akageuka taratibu kama hakukuwa na chochote kile. Akajikuta akitizamana na mwanamume, mwanamume ambaye hakuonyesha kuwa na wasiwasi. Alikuwa akimuangalia Mwanaharamu Kanakwamba anakiangalia kitoto kidogo. Macho yake hayakuonyesha hofu, macho yake hayakuonyesha kumuogopa Mwanaharamu. Ndio kwanza aliendelea kumtizama, ndio kwanza hakujitingisha kabisa. Kitendo kile kilimburudisha Mwanaharamu. Aliwapenda sana watu wa aina hii. Aliwapenda sana watu wasio waoga. Aliwapenda watu ambao hawakuhofu chochote. Naye akawa anamtizama. Au tuseme walikuwa wakitizamana. Ulikuwa mtizamano wakiaina fulani. Mara wakaiona Nuru ikitamalaki ndani ya chumba kile. Nuru ilionyesha kumbabaisha mtu yule alieingia mfano wa kivuli, alionekana akishangazwa na mwanga ambao hakuujua wapi ulipotokea. Ni hapo alipogeuka na kuanza kurusha makonde. Yalikuwa makonde Yaliorushwa kwa uoga, makonde ambayo kwa mwanaharamu yalikuwa Makonde ya kawaida na yaliokuwa yakionekana kwa uwazi. Mwanaharamu akamuacha mwanamume yule ahangaike. Zikatumika dakika tano kila mmoja akijitahidi kufanya kile ambacho alijifunZA hapakuwa na urahisi, hapakuwa na urahisi wa ngumi kupenya na kuugusa mwili. Lakini niwakati huo huo likatokea tukio, likatokea tukio ambalo si mwanaharamu wala yule mtu alielitarajia. Lakini kwa Mwanaharamu ndio ilimuacha katika mshangao wa hali ya juu. Ni muda ule walikuwa wakipambana na mtu huyu, lakini cha ajabu muda huu, mtu huyu alikuwa ametambalajika chini tena damu ikianza kutengeneza mfereji.
TUKUTANE KESHO KATIKA TAMATI YA RIWAYA HII