Riwaya: Mke wa Rais

Pole sana ibra Mungu akutie nguvu
 
Story nzur
 
Dah hii hadithi balaa

 
MKE WA RAIS

MWANDISHI IBRAHIM MASIMBA
*****
Kazi ambayo alitaka kuifanya tayari ilishafanywa na Sohwa. Hata pale alipomuona Sohwa akimburuza yule jasusi hakutaka kushangaa wala kusubiri. Akajitoa pale akiwa na bastola yake mkononi. Hawakuongea kitu zaidi ya kutizamana. Muda mfupi walikuwa wakiondoka eneo lile wakiwa sambamba na mtu yule ambaye alikuwa akiburuzwa na Sohwa. Hapo ndipo Jenipher akipotambua kuwa mtu huyu hakuwa maiti, mtu huyu hakuwa mfu bali alikuwa Amepotezwa fahamu kwa makusudi ilikusaidia kazi ambayo ilikuwa mbele yao. Alitakiwa kuwa chanzo cha kuwapata na kuwarudisha wahaini wote. Kwa kuwa ulikuwa usiku na hawakujua nani yupo ama alikuwepo eneo lile, walichoamua ni kutokutumia usafiri. Waliamua kutembea kwa miguu huku mateka wao akiwa begani kwa sohwa. Jenipher alikuwa nyuma akiwa amekamatia bastola mbili na Sohwa alikuwa mbele akiwa na mwili wa mtu yule begani. Kila mmoja alikuwa akimlinda mwenzake, kila mmoja alikuwa hapo akielekea katika kuhakikisha wanafika salama na mateka wao. SOHWA hakuwa katika wasiwasi, sohwa hakuwa katika kuamini kwamba mateka huyo angeweza kurudiwa na fahamu kwa muda ule kutokana na sindano aliomchoma. Wakazidi kutembea usiku huo bila kukutana na kizuizi chochote, lakini umbali kidogo wa hatua kama tano wakaanza kukutana na miili kadhaa ya binadamu ikiwa imelaliana. Miili ambayo haikuonekana kuwa na majeraha ama matundu ya risasi, miili ambayo haikuonyesha suluba. Bali ilikuwa miili ilioonyesha kuvunjwa shingo iwe kwa karate, judo ama martial combart. Hilo likamfanya sohwa amgeukie Jenipher na kumtizama kwa jicho la maswali, jicho lenye kutaka majibu kuhusu yule aliefanya mauaji yale ya kupendeza machoni mwake. Majibu kuhusu uuaji ambao kwa mara ya mwisho Sohwa aliuona akiwa katika Jiji la Monaco nchi ufaransa walipokwenda kwenye mission moja ya kumchukua Mtu mmoja ambaye alikuwa akitafutwa na idara zote za usalama katika nchi ya urusi kutokana na kuvujisha taarifa ambazo hazikuipendeza Urusi. Jennifer naye akamuangalia kwa jibu la sijui. Sio kwamba alikuwa anaujua, la hasha hakuwa anajua, hakuwa anamjua mtu huyo alieua kwa kuvunja shingo..

"Hii ni Kama Staili ya Willy Gamba ama Joram Kiango." Akanong'ona Jenipher kwa sauti ambayo ilitoka pasipo na uhakika.

"Willy Gamba ama Joram Kiango? Hapana Huyu ni mwanaharamu Mwingine. Huyu ni mwanaharamu mwingine kutoka Afrika.. lakini bado siamini kama bado yupo katika medani hii." Akajibu Sohwa kwa kirefu. Aliujua ufundi wa mtu huyu, aliutambua uuaji huu, uuaji ambao haukuwa mgeni katika kumbukumbu zake.

"Mwanaharamu? " akauliza Jenipher.

"Yeah! Mwanaharamu kutoka Afrika kusini." Akajibu Sohwa akianza kupiga hatua akiondoka eneo lile huku tabasamu likiupamba uso wake, tabasamu likichukua nafasi katika sura yake nzuri. Lilikuwa tabasamu la kukipenda kile, tabasamu la kujua kwamba mwanaharamu mwingine ameongezeka katika hili. Akazidi kutembea akicheka na kutabasamu kisha kwa sauti tamu na ya kujiamini akasema.

"Kazi imekwisha."

********
Mwanga wa Jua la asubuhi ndio kitu kilimshtua Mohamedi, kutoka kwenye usingizi wa kifo. Alikuwa bado amefumba macho wakati alipohisi kitu kama mwanga ukimmulika usoni. Akaanza kufumbua macho taratibu akiangaza huku na huko. Hapo akashangazwa na mazingira, mazingira ambayo kwanza yalikuwa mageni kwake. Alishangaa kujiona amelala juu ya kitanda tena akiwa amefunikwa shuka Jeupe. Akafumbua macho zaidi huku akiendelea kushangaa.. bado hakurudiwa na kumbukumbu kwamba ilikuwaje. Bado hakurudiwa na kumbukumbu ya kukumbuka wapi alikuwepo kabla ya kufika pale. Hilo likamfanya aitulize akili yake na kuanza kukumbuka kila kitu. Alitulia kwa muda akijaribu kuupa nafasi ubongo wake lakini hilo halikutendeka, alitaka kujiondoa kwanza pale. Alitaka kujua wapi alipo. Kitendo cha kujikuta yupo sehemu ngeni machoni mwake, kilimshangaza na kumpa wasiwasi. Wakati akiliwaza hilo, akaisikia michakato ya Viatu, michakato ambayo ilikuwa inakuja pale pale mlangoni mwa chumba alichokuwepo. Akajifunua shuka tayari kwa kuinuka kumkabiri mwenyeji wake. Lakini wakati akiianza kufunua shuka ndipo alipouona mlango ukifungukiwa kisha akamuona mtu akiingia, mtu ambaye alivalia koti kubwa huku akiwa ameachia mindevu. Licha ya mabadiliko hayo lakini Mudy hakuchelewa kumtambua, hakuchelewa kumjua mtu huyu, licha ya kumjua na kumuona hapa lakini alishakutana naye katika matukio kadha wa kadha.

"Bastard!? Akaita Mudy kwa mshangao.

"MOA!" Akaita yule mwanaharamu. Kisha akaendelea. "Pole sana kwa tukio la jana. Sindano waliokuchoma ilikuwa hatari sana kama usingepata tiba ya Haraka. Nashukuru huyu dada hapa amewahi kukufanyia huduma ya haraka kuitoa sumu mwilini. Anaitwa Neema Habibu (pumzika katika Amani Mama. Bado machozi Yangu Yanatoka Na hayajaacha tokea uliponiacha. I still loving u). Huyu ni Daktari pia ni mtu kama sisi katika fani hii." Aliongea mwanaharamu huku akinyoosha kidole sehemu ambayo alisimama Neema. Mudy akaigeuza shingo yake kutizama kule alipo. Akakutana na mwanamke mrembo kupindukia. Tabasamu halikubanduka mdomoni.

"Karibu MOA! Jisikie upo nyumbani. Tupo hapa kwa ajili ya africa na safari hii tumekuja hapa kwa ajili ya TANZANIA. Yalikuwa maneno matamu kutoka kwenye kinywa cha mwanamke Mrembo. MOA akatulia na kuendelea kumtizama huku akikumbuka kile ambacho kilimkuta kule mpaka kumfikisha pale. ALIHITAJI NA ALITAKA SANA KUJUA. LAKINI ANGEJUAJE?

TUSUBIRI TUONE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…