Riwaya: Mke wa Rais

Brqzq hii sehem imamakal. Sana mpaka yanapunguza kitu flan hasa mandege sijui inamanisha mataifa yamekiweka wazi kuwa yapo vitan tayar ni vita dhidi yao sio uharifu tena uleeeee


Sijui kaama nipo sawwa
 
Mkuu endelea pleeease...!!
 
Huu uzi bora uondolewe tu inaonekana mtunzi pumzi imekata
 
Huu uzi bora uondolewe tu inaonekana mtunzi pumzi imekata
Inaonekana tutasubiri sana. Unajua Mwandishi alijichomeka vibaya. Kama mashirika ya kijasusi ya Marekani, Ulaya na Urusi yamejiunga pamoja halafu vita inapiganiwa Canada na lengo ni kurudisha wahalifu washtakiwe! Utaandika mistari gani hapo?

Wahaini wakikimbilia nje, kunakuwa na mawili; aidha uwaache tu au uwavizie uwaulie huko huko siyo kuwakamata na kuwarudisha nyumbani. Otherwise mashirika ya kijasusi ya nje upo nayo timu moja.

Kwa mwelekeo alioupeleka ni ngumu kuendeleza hapo alipoishia.
 
mkuu sijawahi kushindwa katika kitu chochote.. Hizi kauli zako zitaisha muda mfupi ujao. Hii ni Riwaya ya kutumia akili nyingi kuliko maelezo. Ni vipi wahaini watarudi, kipi kitaendelea kati ya muuangano wa mashirika ya kijasusi, na nini hatima ya hili suala? Mimi pekee ndiye nina majibu. Acha niendelea kuandaa ili ikitua hapa nisipate maswali. KUWA NA SUBIRA
 
Kilichotokea ni Muingiliano wa kimajukumu kikazi so nadhani haya maneno yataisha muda mfupi ujao.
 
Sawa sawa kiongozi, hayo ndiyo maneno.
 
MKE WA RAIS

***************

Hakuwa mbali na mawazo yake, hakuwa mbali na kile alichokifikiria. alichokifikiria wakati alipokuwa akitembea katika korido ile. Alihisi uwepo wa mtu nyuma yake, akageuka katika aina ambayo aliijua na kutambua kuwa kugeuka huku ni silaha na kujikinga tosha. Ni kweli hakukosea katika hilo, ni kweli hakukosea kuwepo kwa mtu nyuma yake. akamuona mtu akiwa hewani akija kwa mapigo mazito. Mapigo ambayo bila kuzuia na kuruhusu kuingia mwilini basi usingekuwa hai tena. Jenipher akanesa na kuruka pembeni, mapigo ya mtu yule yakapita. Akauruhusu mwili wake kukabiliana na mtu yule. Yalikuwa mapigano ya kiwango cha juu, mapigano ambayo kila mmoja alionekana ni fundi. Walikuwa wakinesa na kuinuka wote, walikuwa wakiendeana kana kwamba walikuwa ni watu kutoka kitengo kimoja. Haukuwa muda wa kupoteza, muda ambao ungetakiwa kumkuta jenifer akiwa nje ya Jumba lile. Lakini angetokaje wakati alikuwa kwenye mapigano na mtu hatari? Muda mfupi alikuwa akiikumbuka bastola ilioificha maungoni mwake, bastola ambayo kuifikia kunahitaji ufundi wa hali ya juu. ni wakati akiwaza hilo ndipo alipokiona kitu, kitu ambacho kilimshtua, kitu ambacho hakutaka kukiamini. Muda mfupi uliopita alikuwa akifikiria namna ya kuitoa bastola yake na muda huu alikuwa akimuona mtu aliekuwa akipambana naye akivuja Damu kwenye paji la USO. Alikuwa amepigwa risasi. Risasi ambayo hakuona wapi ilipotokea kutokana na sehemu husika kutokuwa na upenyo wa kuruhusu risasi. Akaduwaa kwa sekunde moja, sekunde ya pili alikuwa akiuona mlango ukifunguliwa, ukifunguliwa kisha kuruhusu mwanadada mrembo Kuingia. Alikuwa Sohwa Richardson. Alikuwa Sohwa akiingia sambamba na mwanaume mmoja, mwanaume ambaye hakumtambua, hakuwahi kumuona wala kuiona sura yake. Alipotaka kuuliza hakuupata Muda Huo. Aliambiwa ni wakati wa kuondoka ndani ya Jengo hilo. Ni kweli walitoka.

**************

Hali ya wasiwasi na kutiliana shaka ilikuwa imetawala miongoni mwao. kila mmoja alikuwa ameshtuliwa na taarifa ya kutekwa kwa mtu mmoja muhimu sana katika mpango wao maalum wa kuipindua serikali ya Tanzania MR COSMASS DERICK aliyekuwa gavana wa benki ya Tanzania. Kutoweka kwa mtu huyu lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo kamwe hawakutakiwa kulifanya. Kosa ambalo wangelijutia katika maisha yao yote yaliobaki. Majasusi wa CIA, KGB NA MOSSAD walikuwa wamemwaga katika mji wote wa VANCOUVER wakinusa hapa na kunusa pale kuhakikisha mtu huyo na watu wale wanaofanya mauaji wapatikane. ilikuwa amri ya kupiga risasi kwa yoyote ambaye angehisiwa au kuzuia kutendeka kwa jambo fulani. kila hoteli ilikuwa akipekuliwa kwa usiri mkubwa, usiri ambao hapakuwa na mhudumu wala mteja yoyote yule ambaye anaweza kugundua upekuzi huo.Usiku kucha ulikuwa ukifanyika msako. Shinikizo kutoka kwa wakuu wa nchi zao kuliwasukuma wakuu wa mashirika manne ya kujasusi wafanyekazi Usiku kucha. walitakiwa kumrudisha mateka ndani ya masaa ishirini na nne tena akiwa hai. Hilo lilikuwa shinikizo ambalo halikuwahi kutolewa katika taasisi nyeti kamahizo. wakurugenzi walikuwa wakipokea taarifa kutoka huku na huko. Taarifa ambazo bado hazikuwapa tumaini la kumpata Cosmass Derick.

********

alikuwa Akitembea kwa miguu akitokea sehemu moja kwenda sehemu nyingine. hakuonekana kuwa na wasiwasi wowote, kila hatua yake ilienda sambamba na macho yake. Kila ulipokuwa ukitua mguu wake jicho lake lilikuwa likienda mbali zaidi ya pale. Kichwa chake kilikuwa kikifiikiria na kuwaza wapi alipo Jenipher. Alishatembea maeneo mengi usiku huo lakini hakuwa amepata fununu ya pale alipo Jenifer. Kila sehemu ambayo alitegemea kumuona Jenifer hakufanikiwa katika hilo. Huyu alikuwa Muddy. Alikuwa akitembea kutoka Sehemu fulani kurudi hotelini kwake. hakutaka kuamini kama ilikuwa kweli Jenifer ameuawa bali mawazo yake yamwambia Jane yupo sehemu sahihi na salama. Aliikaribia hotel anayoishi pasipo kutokewa na jambo lolote, lakini hatua wakati akielekea mlango wa kuingilia ndani ya hoteli akashangazwa na wingi na aina ya watu ambao walionekana wakizagaa pale mbele ya hotel. Sio kwamba hakujua kama pale ni hotelini, sio kwamba hakujua kwamba kuwepo kwa watu ni jambo la ajabu! la hasha alilijua hilo na kulitambua hilo,lakini kilichomshangaza ni aina yenyewe ya watu waliokuwepo. Walionekana ni watu ambao wapo kwa sababu ya kitu. kuanzia sura, muonekana wa mavazi na tembea yao walikuwa ni watu kutoka sehemu moja na ni watu ambao hawakuwa pale kwa bahati mbaya. walikuwa pale kwa mission, mission ambayo kwa Mudy aliigundua mapema sana.

akaendelea kutembea kuelekea ndani ya hoteli, macho yake ya hila yalikuwa yakizunguka katika namna ambayo haikuwa rahisi kugundulika. Kile alichokiwaza kabla kikatokea, watu karibia wote walikuwa wakimuangalia katika namna ile ile. Namna ambayo wengi waliipenda, wengi waliihusudu na kuitamani. mlio wa hatari ukatamalaki katikati ngoma za masikio yake. Mikono yake mepesi ilikuwa tayari kwa tukio.Tukio ambalo lingetokea pale tu atakapoamua.. HAIKUWA HIVYO BALI ILIKUWA HIVI.
 
MKE WA RAIS

*********

Haikuwa vile bali ilikuwa hivi. Macho ya watu walikuwa wakimtizama kama hawakumuhutaji yeye. Licha ya kuonyesha hivyo lakini bado hakutaka hilo liwe sababu ya kutokuwa makini. Mikono yake ikawa tayari kwa kitu, kitu ambacho kilikuwa kikienda kutokea. Haikuwa vita rahisi, haikuwa vita rahisi. Hii ilikuwa vita ya kufa na kupona. Ni vipi watapambana na mashirika manne ya kijasusi, Tena mashirika yenye uwezo na nguvu kubwa katika dunia hii. ilikuwa mfano wa Mkasa wa kikosi cha kisasi. Mkasa ambao uliandikiwa kitabu na mtunzi mahiri africa Hayati ELVIS MUSIBA. Mkasa ambao uliifanya mikono ya wapiganaji wale kuvuja damu. wapiganaji ambao walikuwa chini ya Mpelelezi mashuhuri WILLY GAMBA. hili halikumpa hofu, halikumpa hofu kwa kuwa alijua hakuwa mwenyewe kwa kila hatua. akatembea kwa mwendo wa kawaida, akatembea bila kupatwa na hofu wala wasiwasi. bado macho yalikuwa yakimtizama kwa hila, bado macho ya watu walionyesha kuvutika katika kule kuingia kwake. akawapita watu wale kwa kawaida. Akaingia ndani ya ukumbi wa hoteli na kupitiliza kuelekea ndani kabisa ya vyumba. Hapakuwa katika ukawaida na hapakuwa na usalama wa kueleweka. wahudumu karibia wote walikuwa wapya. Hata wateja walionekana kama wamoja katika umoja wa medani za kimapigano. likamsisimua na kuamsha morali ya mapambano. Hakujali tena wala kugeuka tena, Akaendelea kuingia kwa ndani zaidi. Punde akawaona watu wawili wakitokea kwa mbele yake. hawa hawakuwa watu wageni machoni mwake. Kuanzia Mwendo, maumbile, na hata muonekano viliamsha tabasamu ambalo ni nadra sana kuonekana mdomoni kwa MUDY. mbele yake walikuwa wakitokea Watu wawili, lakini katika watu wawili hao mmoja hakutegemea kumuona pale. Alikuwa Jenifer, Jenifer pamoja na Sohwa. Hilo hakutaka kuuliza na hata walipopita wote walipitana kama watu wasiofahamiana. Ulikuwa mchezo hatari, mchezo wa kifo, mchezo ambao haukuwahi kutokea popote pale. MOSSAD, KGB, CIA na M16 kuungana katika mission moja, Mission inayohusu nchi moja tena masikini kupindukia. Nchi yenye rasilimali nyingi ambazo haziwasaidii wananchi wake. kwa nini hivi? kwa nini muuangano huu? hicho ndicho kitu pekee ambacho walikuwa wanahitaji kukipigania.

Alipopishana na Sohwa pamoja na Jenipher, Akaongoza bila wasiwasi. kuendelea kwake kutembea huku macho yakitizama huku na huko akamuona mtu. Huyu alikuwa ni yule yule mtu ambaye alikuwa akikutana naye katika mazingira tatanishi. Alikuwa mbele yake tena akitasamu. Safari hii hakuondoka kama mwanzo. Alionekana kuhitaji kuongea au kufanyakitu. Hata Mohammed hilo akaliona machoni kwa mwanaume yule. Hakuchelewa kugundua kile ambacho alitakiwa kugundua. Ramani ya Afrika ilikuwa ishara ya kwanza kuiona kwa mtu yule. Cha pili kukigundua ilikuwa kiswahili kutoka kwa mtu yule. Kiswahili ambacho kilimfanya atabasamu. atabasamu akiamini huyu alikuwa mmoja katika watu ambao wapo hapa katika suala hili. NI NANI HUYU? Lilikuwa swali ambalo liligonga kichwani kwa Mohamed.

"Kuwa makini MOA." ilikuwa sauti iliomtambulisha kuwa aliembele alikuwa mmoja kati yao. Mmoja katika mission hii ya kurudi na wahaini katika ardhi ya Tanzania. Lakini atakuwa ni nani huyu? hakupata jibu na hata alipohitaji kujua hakufanikiwa kwa kuwa hapakuwa na mtu tena mbele yake. Alikuwa Ameshaondoka machoni mwake.
alifanikiwa kuingia katika chumba alichokuwa akikitumia kwa siri kubwa sana pasipokuonekana na mtu. akaurudisha mlango taratibu na kuiruhusu miguu yake kupiga hatua kuliendea kabati ambalo lilikuwa pembeni kidogo ya kitand Akaonekana akiinua mkono na kupapasa juu kidogo pundekikaonekana kimkoba kikishuka taratibu hadi kweny mkono wa MUDDY, akakipokea na kugeuka kisha kutoka ndani ya chumba.

NAIROBI, KENYA

Marais takribani wote wa nchi za afrika walikuwa wamekutana jijini nairobi kwa mkutano wa siku tatu kujadili masuala kadha wa kadha yaliotokea afrika kubwa haswa likiwa ni lile lililoikumba nchi ya Tanzania. Mwenyekitu wa Umoja huo ambaye alikuwa ni ROBERT MUGABE rais wa Zimbabwe alikaa katika kiti chake tayari kwa Mkutano huo. Ulikuwa ni mkutano mkubwa kuwahi kufanyika afrika. mkutano ambao pia ulihudhuriwa na nchi marafiki wa afrika kama vile China, japan, korea kaskazini pamoja na nchi nyingine nyingi. Ulikuwa mkutano uliofanyika kwa siri kwa mara ya kwanza, lakini mara hii ulikuwa wawazi na hata kualikwa kwa baadhi ya mabalozi ambao nchi zao zilikuwa zikituhumiwa kuwepi nyuma katika mpango hovyo juu ya kupindua serikali ya Tanzania.

Ulikuwa mkutano uliovuta watu wa mataifa mbalimbali, mkutano ambao licha ya kufanyika afrika lakini moja kwa moja ulikuwa ukisikilizwa na viongozi wote wa mashirika ya kijasusi ambayo yalikuwa nyuma ya huu mpango ovu juu ya Nchi Ya Tanzania.

"tunajua wote tupo hapa kwa kitu gani. tunajua wote tuko hapa kwa kuwa tunaipenda afrika yetu. tupo hapa kukemea kile kilichofanywa na Mataifa ya Ulaya pamoja na Amerika. Ni ukweli usiofichika kwamba kile kilichotokea Tanzania, Marekani na nchi za ulaya zinahusika. Zina husika kwa kuandaa hili kwa sababu ya faida na maslahi yao. Wapo wakihitaji kuchukua kitu kutoka katika Ardhi ya Tanzania. tunalaani na kukemea kwa nguvu zote katika hili. Afrika tuachwe tufanye maamuzi bilq kuingiliwa na mataifa ya nje ambayo kazi zao ni kuifilisi Africa. HATUTAKII
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…