jonas amos
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 3,648
- 4,451
Brqzq hii sehem imamakal. Sana mpaka yanapunguza kitu flan hasa mandege sijui inamanisha mataifa yamekiweka wazi kuwa yapo vitan tayar ni vita dhidi yao sio uharifu tena uleeeeeMKE WA RAIS
Askari wenye silaha nzito walikuwa wamelizunguka Jengo lote na kuwatia nguvuni wajumbe wote wa mkutano Ule. Kila kitu kilikuwa wazi na kila mmoja alikuwa katika hofu kubwa sana. Hofu ambayo haikuwepo hapo mwanzo. Ni wakati huo wakiwa katika taharuki kukatokea kingine ambacho hakuna aliyekitegemea. Hakuna ambaye alikuwa anaamini kile kilichokuwa kikitokea kwa wakati ule. Ndege za kivita za kirusi zilikuwa angani zikivurumusha makombora mazito kuelekea katika ardhi ya Nchi. Makombora ambayo yaliyafanya majengo kuanguka na mengine kuwaka moto. Wanausalama wakauona ugumu wa kumuondoa Rais katikati ya Tukio lile, Ugumu ambao ulisababishwa na milipuko mizito. Hawakuona umuhimu wa kupambana Zaidi ya kumuondoa Rais sehemu ile. Mbele alisimama Jenipher na Nyuma alisimama Ummu. Wote walikuwa wakipiga huku wengine wakimuondoa Rais kwa kumkimbiza. Kilikuwa ni kitu kilichopendeza machoni, kitu ambacho kiliburudisha kutizama. Walikuwa watamu katika kupiga na kujilinda. Walifyatua pamoja na kujizuia kwa pamoja. Kila mmoja alikuwa akionyesha ujuzi Wake, kila mmoja alikuwa akionyesha kile ambacho alikipata huko mafunzoni. Wakamvusha Rais na kumuingiza katika Jengo moja ambalo waliliona ni kama Lenye Usalama mkubwa. Bado mapambano yaliendelea na bado wananchi waliendelea kuyakimbia makazi yao. Milipuko na moto kuwaka kilikuwa kitu cha kawaida. Nchi ilikuwa kama Iraq, Nchi ilikuwa kama Syria. Uroho wa Madaraka ulikuwa unasababisha Uharibifu mkubwa sana. Tamaa ya Rasilimali za Nchi kuingia mikononi mwao kulisababisha taifa kupoteza vitu vingi pamoja na Raia Wake. Tanzania Haikuwa inaangalika tena, Watoto wadogo walikuwa barabarani wakiwa bila wazazi. Maiti zilikuwa zimezagaa chini. Hakukuwa na Ile Amani Iliyohubiriwa. Hakukuwa na Umoja Tena wakitaifa. Ilikuwa ni lazima Rais akubali kuiachia Nchini. Lakini ataiachaje mikononi mwa Watu ambao hawapo kwa maslahi ya Taifa? Hilo lilikuwa Swali, swali ambalo lilikuwa likipita kichwani kwa Rais akiwa katika kificho ndani ya Jengo fulani katikati ya Jiji.
Hali bado ilikuwa tete na hapakuwa na msaada wa Haraka. Hapo ndipo watu watano wakaamua kufanya kitu, kitu ambacho kilikuwa ni Cha Hatari. Kitu ambacho kilikuwa ni kufa na kupona. Walikuwa tayari kulipigania Taifa, Walikuwa tayari kufa sababu ya kulinda Rasimali Za nchi, kila mtu akapiga magoti kwa Mara ya Mwisho. Kila mmoja akaomba kwa Imani Yake na Walipomaliza kila mmoja alimgeukia Rais na kutoa Heshima Ya Saluti, Kisha kuondoka kuelekea kwenye mapambano. Mapambano ambayo yanaweza kuwarudisha wakiwa hai ama wakiwa maiti. HAKIKA HALI ILITISHA.
******
MOHAMMED AKATULIA.
alikuwa akitizamana na Midomo minne ya Bastola kutoka kwa watu wawili. Watu ambao hawakuonyesha Utani. Hakutaka kufanya haraka katika kupambana nao, alihitaji kukamatwa kuujua Mtandao kuhusu watu hawa. Bado alikuwa akitizamana nao na bado kila mmoja alikuwa akimsoma mtu anayemuangalia. Hawa hawakuwa Raia Wa Tanzania na hawakuwa watu kutoka bara la Afrika. Hawa walikuwa watu kutoka bara la Amerika na Asia. Hapa Alikuwa akitizamana na Carl Jack Jasusi kutoka CIA na jasusi mwingine kutoka Asia. Hawakuonyesha utani machoni mwao. Kila mmoja macho yake yalizungumza yale matendo yake. Ukapita muda wa dakika kama mbili wakiendelea kutizamana, haikujulikana nini walichokuwa wakisubiri, lakini punde taa zikamwa na wakati huo huo watu wakiruka huku na huko katika aina ile ya kukwepa Risasi. Mohamed akatua sehemu yake na hata wale majasusi wakaangukia wanapopajua wao. Punde tena taa zikawashwa katika mtindo ule ule. Sehemu yote akang'aa, lakini kung'aa huko hakukuubadili ukimya uliopo hapo. Punde walikuwa wakisikia milipuko na kelele za watu kutokea Nje. Akaipata hamu yakuondoka ndani kwenda kushuhudia, lakini angeondoka vipi na kuwaacha viumbe hawa? Viumbe ambao wako hapa kwa mipa9go hatarishi? Wakati akiwaza hayo bado milipuko ilikuwa akisikika kutoka Nje, milipuko ambayo ilifuatiwa na milio ya ndege za kivita. Ingawa alikuwa ndani lakini hakuwa mgeni wa Milio hiyo, Hakuwa mgeni wa ndege za kivita. Muda huu hakutaka kujishauri, alijikuta akiinuka na Sekunde Iliyofuata alikuwa katika mlango wa kutokea nje na Dakika ya kwanza ikamkuta akiwa katika Tax akielekea kule ambapo kulionekana moto kuwaka Angani. Yeye ndiye alikuwa Dereva baada ya kumkuta mwanye gari akikoroma chini baada ya kulambwa Shaba. Akaliacha eneo la Ubungo likiwa katika hamaki. Ingawa ulikuwa Usiku lakini Watu walionekana wakikimbia. Hilo likampa Mohamed Hamu ya kuwahi sehemu Husika. Hakuwa amewasiliana na Ummu wala Jenipher, pia hakuwa anajua wapi wapi walipo mpaka muda huu. Akataka kujaribu kuwatafuta katika Muda ule ili kujua wapi walipo. Lakini Hakufanikiwa Hilo, punde akaisikia milio ya Risasi ikitokea karibu kabisa. Hakuona kama ni salama kuendelea Kuendesha ile gari. Akaipaki na kuufungua mlango kisha kushuka. Akapokewa na Milindimo na milipuko ya Mabomu na Risasi, akajipa jukumu la kutaka kujua nini kinaendelea. Mbele yake akamuona Mtu, mtu ambaye hakuamini kama ni yeye. Akaikamata bastola
Sijui kaama nipo sawwa