Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MATESO YANGU

Alikuwa Carl Jack jasusi kutoka CIA akiwa sambamba na binti ambaye hakufamika machoni mwake. Licha ya Carl kujibadilisha lakini bado hakuweza kumdanganya Mohamed. Bado alishindwa kuyadanganya macho ya mtu huyu, mtu ambaye ni nadra sana kudanganywa katika aina yoyote. Alikuwa na upeo wa hali ya juu mfano wa Willy Gamba. Willy ambaye aliondokea kuwa mpelelezi Bora afrika na Dunia kote. Alijiona kama ameweza machoni kwa wengine lakini sio machoni kwa huyu. Akawasindikiza kwa macho wakati wakiingia ndani ya kivuko. Wakiingia huku wakiwa wameshikana mikono kuonyesha kuwepo katika mapenzi. Mwendo wake pamoja na mwendo wa mwanamke Yule ulisadifu kile kilichopo akili kwa Mohamedi. Mwendo wa kikomandoo, mwendo wa mapigano na mwendo ulioonyesHa Roho mbaya. Kitu mauaji kilisomeka katika macho yao. Licha ya kuingia wote kivukoni lakini kila mtu alikuwa mbali, macho yake yalikuwa yakiangaza huku na huko. Walionyesha kukitafuta kitu, walionyesha kumuangalia ama kumtafuta mtu. Hawakutulia hata pale kivuko kilipoondoka bado hawakukiona walichokuwa wakikitafuta. Muddy Bado alikuwa ametulia, alikuwa akiwatizama kwa macho ya sitaki kuonekana.

Muda wote alikuwa amemlaza Jenipher miguuni huku uso wake akiuficha mgongoni kwa binti, Huku macho yake yakipata uhuru wa kutizama. Panmtoni likaufika upande wa pili na kuruhusu watu kutoka. Mohammed hakutoka wala hakumruhusu Jenipher kutoka. Bado walisimama Sehemu wakimtizama Carl Jack. Walikuwa wakiamini kuwa akuwa amewaona. Japo hakuwa amewaona lakini alikuwa akielekea wapi? Na kufanya nini? Yalikuwa maswali ambayo hakuweza kupata majibu. Wakati akijiuliza hayo akawaona Jack na mwanamke Yule wakishuka. Walikuwa mbele ya Mohamedi kwa Hatua kama Ishirini. Hajutaka kuwapoteza machoni, akaruhusu macho yake yatembee na kuangaza huku na Huko. Akamuona Carl Jack akiiendea bajaj na kujipakia sambamba na mwanamke Yule. Bado Mohamedi alikuwa akiangalia kila kitu ambacho kilikuwa kikitokea. Licha ya uwepo wa milipuko lakini bado watu walikuwa mtaani wakitembea usiku ule. Akaishuhudia bajaj iliowapakia watu wake ikiondoka. ''kazi imeanza Jenipher.' ilikuwa sauti ya kunong'ona kutoka kwa Mohamedi. Akategemea kupata majibu kutoka kwa Jane. Haikuwa hivyo na wala hakujibiwa. Bali alishtukia kumuona Jenipher Yupo juu ya pikipiki akiondoka kuelekea kule ilipoelekea Bajaj. Kila kitu kilifanyika ndani ya dakika moja kuruhusu mfuatano ule. Bajaj tatu zilikuwa mbele, pikipiki aliopanda Jenifer ilikuwa kati kisha zinafuata gari mbili kisha Pikipiki aliopanda Mohamedi. Muda Wote alikuwa akijipapasa na muda wote alikuwa akimtupia macho Jenipher. Mbele kidogo akashudia bajaj aliopanda Carl Jack Ikionyosha Ishara ya kuingia upande wa kushoto kuacha barabara Iendayo Mjimwea. Akamshuhudia Jenipher naye akionyesha kuingia upande ule. Kwa kuwa aliifahamu sana kigamboni Mohamed akawaacha waendelee yeye akaitafuta barabara ya mbele kidogo akakata kushoto kuendelea na Safari ile. Wakati akitokea katika barabara iendayo mahakama ya kigamboni akaishuhudia Bajaj aliopanda Carl na Yule mwanamke ikisimama Mbele ya Hotel Iitwayo Hope Country Iliopo maeneo ya Midizini Kigamboni. Licha ya kuiona bajaj lakini alishangaa kutokumuona Jenipher. Hilo nalo likaonyesha kumshangaza.

Lakini hakufanikiwa kuumaliza mshangao wake akamuona Jenipher naye akipaki pikipiki pembeni kidogo yaIliposimama Bajaj. Hakutaka kusubiri zaidi ya kushuka nakuongoza mpaka ndani ya hotel. Haukupita muda akatoka akionyesha kusahau kitu, kutoka kwake akajikuta akipishana na watu wengine wenye asili ya kiarabu wakiingia ndani ya Hotel. Hakuwaangalia Sana, alichokifanya ni kutoka nje mpaka alipoiacha pikipiki. Akasimama na kuchungulia kwa Chati ndani ya Bajaj, alichokutana nacho kiliufanya mkono wake ashuke pale ilipo bastola yake. Dereva Wa bajaj alikuwa amelala kiubavu huku matundu mawili ya Risasi yakionekana kifuani. Hakutaka kuonekana kama mzoefu katika kutambua kilichotokea. Akaona njia ya kuwazuga wauaji ni kupiga kelele kanakwamba ameshtushwa na kitu kile. Kweli muda mfupi watu wakazi wa midizini walikuwa wamejaa wakiushangaa Mwili wa dereva Yule wa bajaj. Alikuwa amekiegemea kiti akiwa maiti. Akautumia wakati Ule kuingia Ndani ya Hotel kwa kutumia mlango wa nyuma. Wakati akiendelea kuangalia jinsi ya kusonga mbele akawaona wale waarabu wakitoka Nje. Ulikuwa ni Muda huo huo Jenipher akachepuka na kuingia chumba walichotoka waarabu. Alipoingia akaurudisha mlango na kuamua kujibanza pembeni. Macho yake yakatua kitandani ambapo palikuwa na Bastola Mbili pamoja na Magazine. Wakati akishangaa hilo akahisi kitu kama Sindano kikipenya mwilini mwake. Haikumchukua Muda, akahisi nguvu kumuishia kisha kizunguzungu na kilichofuatia nikuanguka chini. HAKUJUA TENA KILICHOENDELEA
 
Kama isidingo. Kila ukifikiri inafika mwisho, ndo inaanza. Hapo Jenipher kadungwa sindano, nadhani moa atamwokoa
 
Kama isidingo. Kila ukifikiri inafika mwisho, ndo inaanza. Hapo Jenipher kadungwa sindano, nadhani moa atamwokoa
hii ngoma bado mbichi, wanamaliza masalia kabla hawajaelekea Marekani kurudi na wahaini waliotoroshwa. Twende taratibu mpaka tujue kama mke wa rais alikuwa ni mmoja kati ya wahaini hao
 
hii ngoma bado mbichi, wanamaliza masalia kabla hawajaelekea Marekani kurudi na wahaini waliotoroshwa. Twende taratibu mpaka tujue kama mke wa rais alikuwa ni mmoja kati ya wahaini hao
Shusha mzigo mkuu
 
hii ngoma bado mbichi, wanamaliza masalia kabla hawajaelekea Marekani kurudi na wahaini waliotoroshwa. Twende taratibu mpaka tujue kama mke wa rais alikuwa ni mmoja kati ya wahaini hao
Nilijua umeshusha mzigo, kuumbe....!!!!!!!
 
Back
Top Bottom