Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

[HASHTAG]#ibra78[/HASHTAG] neno THE END bado hatujaliona
 
Kumbe Ibra shabiki wa simba na alihusika kung'oa viti na sasa anatafutwa na Polisi
 
MKE WA RAIS

99

Giza likauteka uwezo wake na muda huo huo akahisi akipoteza uwezo wake wa kupambana. Akatulia tuli kama maji ya mtungini. Tabasamu likachanua kutoka katika nyuso za watu waliosimama pembeni kidogo ya ulipo mwili wa Jenipher. Mwili ambao haukuonyesha kuwa na fahamu. Bado jenifer alitulia hata pale mmoja wa watu wale alipokuwa anampapasa na kumpekua. Kila kitu kilikuwa kikifanyika katika kasi ya aina yake. Hawakutaka kuupoteza Muda. Muda huu walikuwa peke yao wakiupekua mwili wa Jenifer, lakini ndani ya Sekunde mbili wakashangaa kumuona mtu akiwa amesimama mbele yao. Amesimama huku tabasamu likitamalaki usoni Kwake, mkononi Alikuwa amekamatia Bastola aina Ya Revolver Colt 48 iliyotengenezwa Jamhuri ya Czech. Hakuonekana kuwa na wasiwasi katika kile ambacho alikuwa akikishuhudia. Ulikuwa ni uingiaji uliochomoza kama Juu la Asubuhi, juu ambalo huanza kuuona mwanga kabla yake. Macho ya mwanaume Huyu yalikuwa yakiwaangalia wazungu wale katika namna ambayo hata wao walijua huyu alikuwa mmoja kati ya watu ambao ni Hatari Duniani. Huyu hakuwa mwingine bali alikuwa Mohamedi, alikuwa amesimama mbele ya wakora wale.

Wote wakahamisha macho yao kutoka Ulipo mwili wa Jenifer wakaangalia mbele pale aliposimama Mohamed. Wakatizamana kwa muda na kutambuana tena na tena. Macho yalikuwa yakiongea, macho yalikuwa yakikiongea kile ambacho kipo ndani ya Wahusika. Mikono yao ilikuwa akishuka sehemu pasipokujua kuwa Mohamed alikuwa akitizama, hata mikono ilipokuwa akifika mahali ambapo palihifadhiwa bastola zao, walikuwa wameshachelewa, walichelewa kutokana na kutokuujua wapesi wa Mohamed. Wepesi ambao ulikuwa mara mia na wepesi wa vijana wale. Nukta mbili mbele kila mmoka alikuwa akivuja damu kwenye paji la Uso. Risasi zilifumua vichwa vya Wakora wale Wakatarajika Chini kama Magunia ya Viazi.. Punde Akamuona Sohwa akitokea kutoka Sehemu ya Ndani, mkononi Kwake alikuwa amemkamata Naibu Mkurugenzi Wa Usalama Wa Taifa. Bastola ilikuwa amekilenga kichwa chake akitakiwa atembee bila kugeuka Nyuma. Akapokelewa na Tabasamu, tabasamu ambalo alilitambua kwa kuwa hata yeye alikuwa ni Jasusi. Lakini ni ndani ya Tabasamu hilo kitu cha kushtua kikatokea. Taa zikazimwa kisha Risasi kunguruma ndani ya jengo kuelekezwa pale ambapo alisimama Muddy, Sohwa pamoja na na aliyekuwa naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara Ya Usalama wa Taifa. Zilikuwa risasi ziliozolenga kumnyamazisha mtu yule Muhimu, zilikuwa risasi ambazo zilipangwa kwa tukio lile na Zilikuwa Risasi ambazo zilikuwa Lazima Zifanyekazi ile. Na kweli ziliifanya kazi ile kisawasawa. Mwili Wa Naibu Mkuu wa Usalama wa Taifa ukaenda Chini Hukiwa umechakaa kwa risasi. Muddy na Sohwa wakikuwa wameshahama eneo lile pale tu taa zilipozimwa. Hata Risasi zilipoachiwa wao hawakuwa eneo hilo, walisharuka na Kuangukia pembeni kabisa. Wakishuhudia mwili wa mtu yule ukifumuliwa kwa Risasi. Hawakujibu chochote na hawakuta kulifanya Hivyo. Mbinu iliyotumika kumuua mtu yule ilikuwa mbinu ambayo hutumiwa sana na majasusi popote pale Duniani. Uwe wewe kuliko kutoa Siri ya kile unachokijua kuhusu mpango fulani. Huwezi kuachwa hai kama upo sehemu ambayo ni ngumu kwa wewe kujiokoa. Jambo kama hilo ndio maana kuna wakati huwa majasusi wanajiua kwa njia tofauti kutokana na hilo la kuuona Ugumu wa kujiokoa. Siku zote Jasusi aliefuzu mafunzo ya kila aina basi kwa hilo ni kitu Cha kawaida. Ni kama mfano wa komandoo anapokua kwenye uwanja wa kivita huwa anashauriwa Kubakiza Risasi Moja kwa Kwa Ajili ya Vitu vitatu. Kuitumia Katika Kuuwa Adui, Kuitumia katika msaada wa Kujiokoa na kitu Cha mwisho ni kuitumia mwenyewe katika Kujiua pale unapozidiwa.

Lilikuwa shambulizi lililopangwa hasa, shambulio ambalo lilitendeka ndani ya dakika mbili na kufanikiwa kufanya kile ambacho kilikusudiwa. Muda mfupi milio ya Risasi ilikoma na sehemu yote kurudi kwenye Ukimya ule ule Huku Giza likitamalaki. Bado Mudy na Sohwa walitulia wakiangalia Huku na Huko, bado hawakuamini kama Watu wale walishaondoka. Bado wakatulia tena na tena, Macho yao yalikuwa yakiangalia Sehemu ambayo ulikuwepo Mwili Wa Jenipher. Lakini kitu cha kushangaza Mwili haukuwepo. Haukuonekana pale na wala hapakuonyesha Dalili ya Kuwepo kwa mtu. JENIFER ALITOWEKA
 
MKE WA RAIS

100

Hapakuwa na Dalili ya Uwepo wa Jenifer. Jenifer alikuwa ametoweka. Hakuwepo pale wala hakuonekana. Kilikuwa kitu cha ajabu sana, kitu ambacho hakuna hata mmoja ambaye alikiamini. Atakuwa amekwenda wapi? Ametekwa ama ameondoka katika kujihami na Risasi zilizokuwa zikivulumishwa? Kama ameondoka, ameondoka vipi wakati hakuonyesha kuwa na fahamu. Wakaangaliana tena na tena bila kupata kile walichokuwa wakikiuliza. Wakainuka na kuanza kutoka nje huku kila mmoja akiwa hanajibu kuhusu wapi alipokwenda Jenifer.

*****.
Zilikuwa sauti za watu, sauti ambazo mwanzo alihisi labda ni wapita njia. Lakini Lugha iliyokuwa ikitumika na harafu ambayo ilikuwa ikipita katika matundu ya puani yake yalimfanya aliondoe wazo hiko haraka. Wazo la kwamba alikuwa sehemu jirani na barabarani. Harufu ya kinyesi na mikojo kilikuwa kitu pekee kilichomjulisha na kumtambulisha wapi alipo. Akafumbua macho yake kwa taratibu. Akakutana na kile ambacho hakukijua. Alikuwa amelazwa Chini ya sakafu katika Chumba ambacho kilikuwa kichafu sana. Chumba kilichotapakaa kinyesi na mikojo. Chumba ambacho hakikufaa kulazwa kwa mtoto nzuri kama Jenifer. Mwili wake wakike ulitakiwa kulazwa sehemu ya Gharama. Lakini leo alikuwa amelazwa Juu ya Kinyesi. Juu ya mikojo, alifungiwa ndani Ya Chumba kichafu kisichopendeza. Akaendelea kufumbua macho yake akiangaza huku na huko. Alikutana na vitu ambavyo vilimtisha. Alikuwa akitizamana na matone ya Damu. Matone ambayo kwa sehemu nyingine kulikuwa na mfano wa madimbwi. Kilikuwa ni chumba ambacho kilionyesha ni mahakama ya kifo. Akaendelea kutizama kila upande wa chumba kile. Bado kile alichokutana nacho kilimtisha. Akaamua kuinuka na kukaa kitako, mara akayahisi maumivu kichwani, hapo akaupeleka mkono wake sehemu hiyo akakutana na umajimaji, umajimaji ambao ulimpa majibu kuwa ni Damu. Kufikia hapo akavuta kumbukumbu, kumbukumbu ambayo ilishapotea baada ya kushambuliwa usiku uliopita. Hakufika popote katika kuirudisha kumbukumbu ya usiku wa Jana. Akakiona kitasa cha mlango kikitingishwa. Akarudi chini na kutulia kanakwamba Hakuwa yeye aliekuwa amekaa kitako. Akausikia mlango ukifunguliwa kisha hatua za watu zikasikika zikisogea pale alipo. Akaendelea kujikausha huku akiuandaa Mwili wake na mapambano iwapo itabidi kuwa hivyo. Ni kweli hatua zikasogea na kumfikia, mara akaihisi mikono ya kiume ikimtomasa hapa na pale katika mwili Wake. Mikono ambayo ilikosa adabu na kuingia mpaka ndani ya blauzi aliyovaa na kuanza kuchezea matiti yake mazuri. Bado Jenipher aliendelea kutulia, bado hakuonyesha kama Amesharudi katika fahamu. Mkono ukaendelea kushuka na kushuka, akahisi mkanda wa Suruali yake ukifunguliwa. Hapo hakutaka Kuruhusu hilo, hakutaka kulikubali kwa Gharama yoyote. Akakusanya nguvu zake na kuulegeza mwili wake. Punde alikuwa akiinuka sambamba na mapigo kadhaa mujarabu. Yalikuwa mapigo sahihi yaliokwenda sehemu Sahihi. Mapigo ambayo hayakutoa nafasi kwa yoyote mle ndani Kujitetea. Wote walikuwa wametambarajika wakiwa hawana uhai. Wote walitulia. Akaurudisha mkanda sehemu yake kisha kuokota bastola mbili ambazo zilikuwa pembeni yake. Baada ya hapo aliwapejuwa wale maiti na aliporidhika na alichokipata akaanza kupiga hatua kufuata mlango ili atoke na kupotea Eneo lile. Akaufungua mlango vizuri, akachungulia kwa Chati, hapo akakutana na Ukimya wa hali ya juu. Hapakuwa Dalili ya kuwepo kwa mtu. Lakini hakutaka kuuamini Ukimya ule. Hakutaka kuamini kwa kuwa alijua alikuwa akipambana na Watu ambao ni Zaidi Ya maneno. Bastola ikatangulia mbele, kikafuatia kichwa kisha kiwiliwili. Alikuwa akitembea mbele na Nyuma, alikuwa akiangalia katika pembe zote. Akafakiniwa kupita kizingiti, hata alipouanza mlango wa pili bado Ukimya ulizidi kutamalaki. Hakulijali hilo bado aliendelea kutembea, bado aliendelea kusonga mbele. Akaupita mlango wa pili, mbele yake kulikuwa na Korido ndefu ambayo ilikuwa ikielekea sehemu ambayo hakuijua. Mbele kidogo Akakutana na Neno CIA MISSIONS. Moyo ukamdunda na Umakini Ukaongezeka. Alikuwa Ndani Ya Jengo la Shirika la Kijasusi la Marekani. Alikuwa ndani Ya Shirika ambalo ni Hatari sana kwa Uchunguzi. Alipipiga hatua kama kumi hivi, Akajihisi hakuwa peke yake, akahisi uwepo wa mtu nyuma yake, mtu ambaye hakuwa akimuona.:. Naam hakukosea na hakuwa mbali na wazo lake, Jenifer akageuka
 
Asante sana Mkuu Ibra, kama IPO nyingine ongeza kaka.
 
Back
Top Bottom