Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

Asante mkuu, unafanya Kazi nzuri sana, pia naomba nikukumbushe tu kwamba tumeanza weekend, tunakutegemea sana.
 
MKE WA RAIS

aliyaacha maji yashuke taratibu na kuulowesha mwili wake. Mikono yake migumu ilikuwa ikitembea mwilini kuusugua mwili wake laini. Mkono ambao ulikuwa ukipita kila sehemu kuhakikisha usafi wa mwili wake. Chuchu nzuri zilizochongoka mfano wa Mida ya michongoma yalikuwa yamening'inia kifuani kwake yakikifanya kionekana kwa uzuri zaidi. Bado aliendelea kutulia kanakwamba hakuwa na haraka. Mikono ikawa Juu ya chuchu ikisugua kwa utaratibu ule ambao ulitakiwa. Lakini punde akakisikia kitu, kitu ambacho kilimfanya atulie na kulitega sikio lake vizuri. Sikio ambalo lilikuwa na uwezo wa kusikia mchakato hata wa sisiminzi. Akasikia tena kile alichokisia mwanzo, hii ilikuwa michakato ya Hatua za miguu ya mtu. Hilo likamfanya aendelee kutulia huku akijipa muda zaidi wa kumsoma aliyeingia Chumbani kwake. Hata pale alipokiona kitasa cha bafuni kikizungushwa, Bado Jenifer hakuonyesha kuogopa. Bado alikuwa Uchi, bado hakuwa na kivazi Chochote mwilini. Akauona mlango ukifunguliwa kisha mdomo wa bastola ukachungulia. Hakulisubiri hilo, alichokifanya ni kujivuta na kukaa Nyuma ya mlango. Bado bastola alionekana kwa uzuri, tena safarii ukionekana na mkono wa mtu. Akajiandaa kwa Hilo, akajiandaa kwa kile ambacho alipanga kukifanya. Punde mlango wa bafuni ukasukumwa zaidi na Mwili wa Mtu kuingia. Hakusubiri ageuke upande alipo. Mapigo mawili mazito ya Karate Yalitosha kumnyamazisha Jamaa Yule.

Hakuchelewa pale bafuni, aliuvuta mwili wa mwanaume yule na kuungiza ndani kabisa. Mikono yake ikazama katika kila sehemu ya mavazi ya mwanaume Yule. Akakuta vitu vingi sana, Hasa vitambulisho. Kati ya Vyote Hivyo akavutiwa na kitu kimoja, kitu ambacho kilikuwa mfano wa Saa. Kitu ambacho ndani kilikuwa kikiwaka taa ya Kijani. Juu kuliandikwa maneno Fulani kwa Lugha tata, Lugha ya kijasusi, Lugha ambayo kwa Jenifer Haikuwa ngumu. Denis peterson jasusi kutoka M16 ndiye alikuwa Chini pale tena akiwa mfu. Baada ya kulisoma hilo Jina yakafuata majina ya Watu wengine ambayo kila jina lililoandikwa ndani ya kitu kile mfano wa saa pembeni yake yalikuwa yakitokea maandishi ya kuonyesha ni Wapi wanapatikana watu wale.
.
Baada ya Jenifer kuridhika na alichokiona kutoka kwa jasusi Yule, alitoka Haraka bafuni na kuyaendea mavazi Yake. Akayatupia mwilini na Muda mfupi alikuwa akiondoka Eneo la Hoteli Ile kuelekea Katika Mji mwingine kumfuata mtu mmoja ambaye kwa kile alichokisoma kilionyesha ni mmoja kati ya watu Muhimu wanaowahitaji Kurudi Nao Tanzania..

*****
ukimya ulikuwa umetanda eneo lote la mji ule uliopembezoni kabisa mwa Nchi ya Canada. Mbwa wachache na mingurumo ya magari ndicho kitu pekee ambacho kilisikika katika Eneo lile. Bastola Mkononi, macho yakiangaza namba za Majengo, Jenipher alikuwa hapo kwa kazi maalum. Kazi Ambayo iliwatoa Nchini Tanzania. Alikuwa akimfuatilia mtu ambaye alihisi ni aliekuwa Gavana Wa Benki Kuu Ya Tanzania Bwana Cosmas Derick, mmoja ya wala njama ya kuipindua Serikali Ya Tanzania. Alitembea akiwa makini kwa kila hatua, hata pale alipokuwa hapa na kuhamia pale bado alikuwa akihakikisha kuwa anabaki salama. Aliitambua Hatari Iliombele yao.

Macho yake yalikuwa yakiangaza kila pembe na kila kichochoro. Bado ukimya ulitawala Eneo lote. Macho yake yakaliona Jengo ambalo alikuwa akiishi Bwana Cosmass Derick. Tabasamu la Uhakika likaupamba uso wake, hasa pale alipokuwa akiuhama upande alipo ili kuufuata upande Ule ambao umepakana na Jengo hilo. Alikuwa makini kwa utimamu wake wote. Hukuuamini ukimya ule na hata siku moja hakutakiwa kuamini hilo. Hakuamini kama hapakuwa na Ulinzi bali alijua Kwamba Ulinzi ulikuwepo na kuna watu mahali fulani wakifuatilia kwa Ukaribu. Akaingia upande ule kisha kuongoza kurudi nyuma ili kuwapoteza watu ambao alihisi walikuwa wakimfuatilia. Baada ya kurudi na kutembea umbali wa hatua kumi akachepuka kushoto kisha kurudi nyuma kwa kupitia Nyuma ya Jengo hilo. Lilikuwa Jengo La ghorofa nane, Jengo ambalo lilikuwa limezungushiwa Ukuta mkubwa sana. Alitembea huku akilichunguza, alipofika Nyuma kabisa ya Jengo akauona mlango. Mbele ya Huo mlango Kulikuwa na Watu watatu. Wote walikuwa wamevalia makoti meusi na Mikononi walionekana kuwa na Bunduki kubwa za kivita. Jenifer akakitingisha kichwa Chake kuonyesha kuridhishwa na kitu ambacho alikuwa akikiona mbele ya Macho yake. Akaingiza mkono Mfukoni na kutoka na kiwambo cha kuzuia Mlio wa Risasi na kukipachika kwenye Bastola Kisha akaanza kunyata kuelekea pale walipo walinzi. Hakuwa Muoga na wala hakuwa anahofia chochote. Mavazi yake aliovaa yalikuwa yakifanana na mazingira Ya sehemu alipo. Alikuwa ni kama kivuli ama mzimu. Bado walinzi wale walikuwa wakiranda Eneo lote. Alichokifanya baada ya kuliona Hilo ni Kuirudisha Bastola Mahala pake. Alipohakikisha yupo sawa akaichana tishirt aliovaa Kisha kuyaacha matiti Yake nje, harafu Akajitokeza Mbele ya Walinzi...
 
MKE WA RAIS

98

Alikiacha kifua wazi , kifua ambacho kilibeba matiti mazuri. Akayaacha matiti yaonekane kwa uwazi. Akajitokeza na kusogea pale huku akihakikisha macho ya walinzi wale yanamuangalia yeye. Hatua ya kwanza ikapita akitembea, na hata alipipiga hatu ya pili bado ilikwenda kama alivyotaka, Hatua ya tatu hakufanikiwa kuifikia. Sauti nzito ya kiume ikasikika kutokea nyuma yake. Ilikuwa sauti nzito yenye mamlaka. ''Usijali kusogea, ukifanya hivyo tutakifumua kichwa chako kwa Risasi''; sauti ikaingia ndani ya ngoma za masikio ya Jenifer, akasita kuipiga hatua ile ya Tatu. Mbele yake walinzi Watatu walikuwa wanenyoosha silaha kwake, na hata alipoangalia Nyuma aliwaona watatu wengine wakiwa na silaha zao mikononi. Jenifer Hakuonyesha kujali, hakuonyesha kuogopa bunduki za walinzi wale. Ndio kwanza alikuwa akijizungusha mfano wa changidoa, changudoa wa kiwango cha juu kama wale wa Ohio amba Africasana Pale Sinza. Mkono wake mmoja ukijuwa ukiipandisha sketi yake juu hadi kufikia Usawa wa Ilipo chupi yake. Paja lake lilikuwa likionekana waziwazi. Bado majasasi wale walikuwa wakimtizama, bado hawakuamua chochote cha kufanya, macho yao yalikuwa kwenye mapaja na kifuani kwa Jenipher. Wakasogea tena kwa tahadhali, Hatua kwa hatua kwa walinzi wa mbele na Nyuma. Wakamfikia Jenipher, wakamfikia huku kila mmoja macho yake yakionyesha kutamani kile ambacho yalikuwa yakikishuhudia. Sekunde mbili tatu walikuwa wakimshikashika Jenipher maeneo katika maeneo tofauti mwilini.

Hawakulijua walilokuwa wakilitenda, hawakuwa wakijua kile ambacho kingewatokea. Muda mfupi kitu kama mlio wa Alam Ukasikika kutoka kwa mmoja kati yao. Wakaipoteza Dakika katika kushangaa hilo. Lilikuwa nikosa kwa jasusi kama Jenipher. Mkono wake ukashuka kwa wepesi na kuifikia bastola. Sekunde ya pili cheche zilikuwa zikionekana huku walinzi wa nne kati ya Sita wakianguka Chini kila mmoja akiwa na Tundu la risasi Utosini. Kilikuwa kitu kilichofanywa katika Muda ambao haukutegemewa na Walinzi wale. Hata pale wengine wawili waliobaki walipotaka kujitetea hawakufika popote. Risasi nyingine zikazama Vifuani na kuwatupa chini. Hakusubiri hapo, akasonga mbele akielekea ndani ya Jengo lile. Muda mfupi alikuwa akichupa na kuangukia upande wa ndani. Akatulia kwa muda kama angewaona watu wakielekea pale, lakini utulivu bado Ulibaki pale pale. Hapakuonekana mtu, wala kitu Chochote kile. Bado utulivu ulikuwa pale pale. Akajiinua hapo na kusogea sehemu Nyingine. Kila wakati alikuwa akisoma Jina La Cosmass Derick kujua wapi chumba chake kilipo. Akaufikia Mlango wa kuingilia ndani kabisa ya Jengo. Akakinyonga kitasa akashangaa kuuona mlango ukifunguka ''HATARI'' Llilikuwa neno la kwanza kugonga kichwani kwa Jenipher. Hakujali, akaingia taratibu kisha kuurudisha Mlango bila kutoa Sauti. Akageuka Kuendelea na Safari ya kuitafuta lifi. Alikuwa akitembea safari hii bastola mbili mkononi. Akaifikia lift na kujitumbukiza Humo ndani, Muda mfupi baadae alikuwa akipelekwa Ghorofa ya Saba ambayo ndipo alipokuwa Akiishi aliyekuwa Gavana. Lift ikafika sehemu yake na Muda ule ule mlango Wa Lifti ukafunguka Jenipher akashuka. Wakati akishuka na kunyoosha kwenda upande mwingine, akapishana na watu watatu nao wakiingia kwenye Lifti. Kati ya hao mmoja alikuwa Sohwa, wakatizamana kwa nukta mbili kisha Kila mmoja akaushika uelekeo wake. Wakati Sohwa akielekea ndani ya lifti, Jenipher alikuwa akielekea Sehemu yake. Hakushangaa kumuona Sohwa hapo, na Hakushangaa hilo kwa kuwa, alishatambua kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Sohwa Alikuwa mwenzao na Sohwa alikuwa kiunganishi katika Mpango wao wa kurudi na Wahaini. Akaendelea kutembea bila wasiwasi. Alijua alikuwa na Mtu, alikuwa na Jicho linalomtizama. Hakumuamini Mohamed Pale mwanzo alipomtambulisha kwa Sohwa lakini Kumuona Sohwa ndani ya Jengo Hili, kulimpa Imani, Nguvu na Uwezo wa kusonga mbele. Mbele katika kumchukua Yule mmoja, Mmoja ambaye atafuatiwa na Wengine kisha Wengine tena. Hilo ndilo wazo la Jenipher, Sohwa na Mohamed, Wazo la Tanzania kwanza na Wengine baadae. Aliufikia mlango wa chumba hicho kwa Urahisi Zaidi, akasimama Nje Ya Mlango kwa nukta kama kumi, Kisha akaushika Mlango na kunyonga kitasa. Mlango Ukamtii na Kumkaribisha Ndani, ndani ambapo alipokelewa na kile kilichofanya kengele ya Hatari Ilie kichwani Mwake. Kabla hajajua kipi cha kufanya, Akahisi kitu kizito kikitua Kichwani, kitu ambacho kilimpeleka Chini na kumpeleka katika giza, Giza ambalo lilimpoteza na kuhisi hakuwa katika Uso wa Dunia hii. JENIPHER AKATULIA TULIII
 
Back
Top Bottom