Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

******

alikuwa yule yule, yule aliepishana naye muda mfupi uliopita. Lakini safari hii akimuangalia na kutabasamu. Tabasamu halikumfanya Mohamedi ashindwe kugundua kile kilichopo nyuma yake. Nyuma ya tabasamu la urafiki, tabasamu linaloongea na kufikisha ujumbe sehemu nyingine. Licha ya tabasamu lote, lakini halikumyumbisha wala kumshtua Mohammed. Ndio kwanza alikuwa akiikwea Lifi kuelekea pale alipoambiwa afike. Pale alipotakiwa kwenda kuitafuta Zabibu. Yeah! Hilo ndilo ambalo lilipita katika kichwa cha Mohamedi. Lifti ikamuacha atelemke na kuambaa na korido moja matata sana. Alitembea kwa kujiamini, mikono yake ilikuwa tayari kuifikia bastola endapo angetakiwa hilo. Bado hapakuwa na upinzani wala hakumuona mtu wa kumtilia mashaka. Hapo akajipa imani ya kuamini, hatua nne kabla ya kuifikia sehemu Husika akahisi kitu, kitu ambacho hakikuwa cha kupuuzwa. Akagundua hakuwa peke yake, alikuwa akifuatiliwa na Mtu. Mkono ulikuwa ukishuka sekunde hii, sekunde ya pili Alikuwa akigeuka kwa Silika ya Aina yake. Lakini akakuta patupu. Koridoni hapakuwa na mtu wala paka. Kwa mara ya kwanza hisia zake zilimpoteza. Alichokifanya ni kupuuza, sasa alikuwa akielekea kwenye mlango wa Chumba kile alichoambiwa afike kwa mujibu wa kile kikaratasi alichokikuta pale Alipotoka.

Akauendea mlango na kuusukuma baada ya kunyonga kitasa, akaukuta ukiwa mgumu kuonyesha kuwa ulikuwa umefungwa kwa ndani. Nukta ya kwanza alikuwa iliukuta mkono wake ukiwa mfukoni, na Nukta ya pili ukatoka ukiwa umeshikilia Lundo la funguo. Akauchagua Mmoja na kuutumbukiza kwenye kitasa. Muda mfupi alikuwa ndani akitizamana na mwanamke alielala Chali kitandani akiwa Uchi wa nyama. Hakuonyesha kutingishika wala kugeuza shingo kuangalia mlangoni anapotokea Mohamed. Bado alionyesha kutulia kana kwamba hapakuwa na chochote kile. Hilo kidogo likampa hofu Mohammed. Kwa nini aonyeshe kutokujali ujaji wangu humu chumbani? Kwa nini haonyeshi kama kile alichokuwa anakionyesha kule club? Ana nini? Amefanywa nini? Yalikuwa maswali yaliokosa majibu wakati Mohamed akitizamana na Umbo la mwanamke Mrembo akiwa ametulia uchi juu ya kitanda. Mguu ulikuwa Huku na mwingine kule. Mohamed akakaza macho kutizama, Ghafla akaliona lile ambalo aliliwaza. Damu ilikuwa ikichuruzika kutoka pale kitandani kuelekea pembeni kabisa ya Kitanda. Mkono ulikuwa tayari umekamatia bastola yake katika utimamu. Akazipiga hatua kwa kuhesabu moja baada ya nyingine, macho yake yalikuwa yakiangaza chumba kizima yasimuone mtu. Akainua kichwa kulitizama Dali la Chumba kile. Akakiona kipande cha Sillingboard kikiwa kimewekwa pembeni. Upenyo mdogo wa kumpitisha Mtu ukionekana. Muddy akajua kuwa tayari mwanamke yule alikuwa ameuawa. Ameuawa na mtu aliyepita katika upenyo ule anaoutizama. Akatingisha kichwa huku akimsogelea mwanadada yule. Macho yakagota kwenye mpini wa kisu ubavuni kwa mwanadada yule. Hakutaka kusubiri, alirudi nyuma kisha kukiacha chumba kile huku mawazo mazito yakiwa kichwani. Alimtambua muuaji na alimtambua yeye alikuwa nani. Lakini kwa nini kila akiniona anatabasamu? Na kwa nini huwa anaua mtu ambaye alikuwa na miadi nami? Yeye anamsaidia nani? Kila kitu kilikuwa gizani, hakutaka kuamini kama mauaji yanayofanywa na Mtu yule ni vita ya kuwasaidiwa wao.

******

ukumbi ulikuwa kimya kila mmoja akiangalia mbele ya meza kuu. Waziri wa mambo ya Kigeni wa marekani na wenzake wa Urusi, Uingereza na Italia walikuwa wametulia wakiangaliana na wajumbe kutoka Tanzania wakiongozwa na Makamu Wa Rais Mzee Kilowoko. Waziri mkuu na mawaziri wengine wa Serikali ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania. Ukiwaondoa hao wengine waliokuwepo ni Mke wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania sambamba na watu wengine ambao hawakuwa wakijulikana. Kila mmoja alikuwa kimya akisikiliza maoni Juu Ya mpango mkakati wao waliouleta kuhusu kupewa nguvu ya kifedha na kiusalama kama maandalizi Ya kuipindua iliopo madarakani. Ulikuwa ni mkakati Uliosukwa kwa Muda Mrefu. Watu wengi walikuwa wamepandikizwa katika kufanikisha hilo. Ulikuwa ni Mkutano Uliofanywa kwa kificho Sana kwa Siri Nzito. Baada ya Muda wa majadiliano na mikakati ya kufanikisha mapinduzi Hayo, Nchi hizo nne zikaamua kutuma watu wao ambao kazi yao ilikuwa ni Kuratibu Mapinduzi na Kuhakikisha wanaua kila mtu ambaye angeonekana kuwazibia katika mpango huo. Ni katika Mkutano Huo uliozalisha mahusiano kati ya Mke wa Rais na mtu mmoja ajulikanae kwa Jina la Comrade Robert ambaye alikuwa ni Meja General Mstaafu katika jeshi la nchi. Uhusiano Huo Ulikuwa wa Siri sana, siri ambayo hata mheshimiwa Rais Hakuwa ameigundua. Uhusiano Huo Ukaanza kuleta mabadiliko makubwa kwa Mke Wa Rais, kila wakati alikuwa akiondoka Ikulu bila taarifa huku muda mwingi akimtumia Mkurugenzi Wa Idara ya Usala,a Wa Taifa kufanikisha hilo. Ni wasiwasi Huo Na mashaka kwa Mheshimiwa Rais ndipo alipoamua Kuwaajili Vijana Watatu ambao aliwaamini kwa kuwa walikuwa ni Watiifu kwa Rais. Hapo ndipo Alipowachagua captain George, Kanali Jamilah na Liutenant Sevenlee katika kufuatilia kilichopo nyuma ya safari hizo
 
MKE WA RAIS

Walikuwa vijana watatu, vijana waaminifu katika Idara nyeti ya Usalama wa nchi. Hawa walipewa kazi maalum, kazi ya kuifuatilia mieneno ya mke wa Rais. Ilikuwa kazi ngumu sana kwa kuwa walikabiliana na Upinzani kutoka kwa Mkuu wao wa kazi. Hilo likaifanyakazi yao kuwa ngumu. Ugumu ulikuwa pale ambapo mke wa Rais alikuwa akibadilishiwa walinzi kila wakati. Hilo likawafanya vijana wale watatu kubuni mbinu nyingine. Hii ilikuwa mbinu iliofanikiwa lakini ni mbinu hiyo iliosababisha Uhasama kati yao na kupelekea Captain George Kuuawa Kinyama. Wakati vijana wale wakimchunguza Mke Wa Rais, kwa upande mwingine majasusi wa Kutoka mashirika manne walikuwa wapo nchini Tanzania wakiisuka mipango Yote. Ulikuwa mpango mkakati uliokuwa ukielekea katika kufanikisha malengo yao. Lakini kuuawa kwa Meja jenerali Comrade Robert akiwa na mke wa rais kuliwashtua wote na kuhitaji kujua kile ambacho kilitokea. Walitaka kujua nini ambacho kilitokea hadi kufikia hapo. Kwa nini Robert auawe? Hapo ndipo vijana wa CIA na KGB walipoingia ndani katika Uchunguzi wa Suala hilo na kugundua kuwa Chanzo kilikuwa ni kupigwa picha kwa Mke wa Mheshimiwa akiwa Faragha na Meja Jenerali Robert. Na hata baada ya Tukio hilo la kuuawa kwa Comrade Robert, bado vijana wa CIA na KGB kwa kusaidiana na watu wa usalama wa Taifa wakaendelea na Uchunguzi. Katika Uchunguzi huo waligundua kile ambacho hawakukijua mwanzo. Cha kwanza kugundua ilikuwa ni Kitendo cha kuwepo kwa watu waliokuwa wakimfuatilia Mke wa Rais bila mwenyewe kujua. Cha pili ni tukio la kupigwa picha kwa camera za kutegwa kitendo ambacho iliwalazimu wawaondoe katika Uso Huu wa Dunia Walinzi wa Mke wa Rais pamoja na Yeye mwenyewe ili kuondoa Uwezekano wa kugundulika kwa mpango wao Wa Kuipindua Serikali hasa pale ambapo watachunguzwa na kugundulika mienendo.

******

alipoondoka ndani ya hotel baada ya kukutana na tukio la kuuawa kwa mwanadada yule, Mohamed akaamua kurudi chumbani kwake katika hoteli aliopanga huku kichwa chake kikimfikiria Mtu yule. Mtu ambaye mpaka wakati huo hakuujua ni upi upande wake kutokana na kuuwa watu ambao hata yeye alikuwa akiwahitaji. Alitembea usiku ule bila wasiwasi wowote. Alihitaji kukutana na Jenifer kwa usiku huo, lakini hakutaka kumfuata mpaka pale atakapo toka chumbani kwake akiwa amebadili mavazi. Alipokuwa akiikaribia Hoteli ile akawaona watu watatu wakiwa wamesimama wakiangalia huku na huko kanakwamba walikuwa wakikitizama kitu cha muhimu. Wakati akiendelea kuwaangalia watu wale mara akamuona mtu ambaye alimfahamu. Huyu Alikuwa Sohwa, alikuwa akitoka ndani ya hoteli kisha akaonekana kuongea na Vijana wale, harafu akarudi ndani ya Hoteli tena. Kengele ya Hatari ikalia kichwani mwake. Akaongeza mwendo na kuwapita vijana wale. Punde Akausikia Ujumbe ukiingia kwenye Simu, Hii ilikuwa ni Simu Ya Marehemu Neema Mtobwa. Hakuona Umuhimu wa kuitoa Simu na kuisoma. Hakuweza kufanya Hivyo kwa kuwa bado alikuwa akihisi kufuatiliwa. Aliingia ndani Ya hoteli bila kuonekana na vijana wale, akaongoza mpaka kwenye mlango Wa chumba chake. Hapo akasimama kwanza, alisimama akiwa anakiangalia kitu ambacho kilikuwa chini ya sakafu. Kikaratasi ambacho ulikuwa ujumbe mahususi. Hakutaka kuinama kufanya lolote, hakujua nani alikuwa amekitupa kikaratasi kle chini ya mlango wa chumba chake. Wakati akiwa bado hapo akauona Upenyo Mdogo kuonyesha kuwa mlango wake ulikuwa wazi. Hapo kengele za hatari zikaendelea kulindima. Mkono wake ulishaifikia Bastola yake katika Sehemu yake. Akaipiga hatua moja kuufikia mlango. Akaugusa kisha kuusukuma, mlango ukamtii na kufunguka wenyewe. Hakuingia kwanza kwa Urahisi, akachungulia kwa chati tayari kwa chochote. Chumba kilikuwa kitupu, haukuonekana Uwepo wa mtu ndani ya Chumba kile. Hilo halikumfanya aamini kwa Urahisi. Bado akaendelea kucheki Huku safari hii akiingia mwili mzima. Akapokewa na Marashi, Marashi matamu kuonyesha chumbani kwake aliingia mwanamke. Mwanamke ambaye alihisi ni Sohwa. Akiwa ameduwaa hapo akaisikia sauti ya kike ikimkaribisha Chumbani kwake. Ilikuwa Sauti iliotokea Nyuma yake.

Haikuwa sauti nyingine bali alikuwa sauti kutoka kwa Sohwa. Mohamed akageuka kule ilipotokea sauti. Akakutana na Mdomo wa Bastola, bastola ilioshukwa sawa sawia kutoka kwa mwanamke Tofauti na Yule aliemhisi. HUYU hakuwa Sohwa, hakuwa Jenipher, bali alikuwa Shunie. Bastola Mkononi Akiwa amekilenga kichwa cha Muddy. Kidole chake kilikuwa kikishuka Taratibu kwenye kitufe cha Kuruhusu risasi. Haikuwa Ngumu kumuua Mohamedi. Hakuwa Rahisi kwa kuwa Sekunde mbili kitu kama mlipuko kikatamalaki ndani ya Chumba kile, Damu ikaruka na Ubongo kusambaa. HALI IKABAKI TETE
 
ibra87 mkuu jicho kavu hapa nasubiri muendelezo sibanduki

Yaani hii story ni tamu kama kujikuna upele

Nimekumbuka tena aina Fulani ya uandishi wa zamani walipenda kuutumia


Kwamba nilijibwaga kitandani kwa uchovu na sikukumbuka hata kuvua viatu nilikuja kushtuliwa na kitu ambacho sikujua ni nini,miale ya jua la asubuhi ilipenya ndani
 
MKE WA RAIS

Mlipuko mdogo ukasikika. Damu ikaruka na Ubongo kusambaa Chini. Muddy alikuwa ameshachupa na kuangukia kando ya kiti kikubwa ndani ya Chumba kile. Bastola mkononi Huku macho yake yakitizama kile ambacho alikiona kama kitendo cha ajabu. Shunie alikuwa Chini akiwa amelala katikati ya dimbwi la damu, hakuonyesha uhai, wala hakuonyesha kama anapumua. Alikuwa maiti, maiti ambaye hakuwa anaonekana Sura yake kutokana na kusambaratishwa kwa Risasi. Bado hakuwa anajua kipi ambacho kimetendeka. Lakini mshangao huo haukudumu sana hasa pale alipomuona mwanamke akiingia pale. Alikuwa mwanamke anayemfahamu, mwanamke ambaye alimtambua kwa undani zaidi, lakini licha ya kumtambua Huko hakufikiria kama kilichotendwa pale kilitokana na mikono yake. Nikweli alionekana ameikamatia bastola, na pia ni kweli alionekana ni mtu ambaye hakuwa na wasiwasi. Aliingia pale ndani kanakwamba alikuwa akiingia chumbani kwake. Alikuwa ni Sohwa, Sohwa Richardson, Sohwa ambaye alikuwa ni Jasusi. Hilo halikumuingia Mohamed, akaipata hamu ya kukisikia kwa sauti kile alichokiona. Hakuhitaji vitendo kabla ya maneno. Alihitaji kuhakikishiwa, kuhakikishiwa na Mhusika mwenyewe kuwa kwa nini amelitenda lile.

Wakati akiendelea kushangazwa na hilo, akaliona jingine likitokea pale pale chumbani. Mlango ulikuwa ukifunguliwa taratibu bila Sohwa kuligundua hilo, kisha akauona Mdomo wa Bastola ukichungulia. Punde akamuona mtu akiingia taratibu kanakwamba alikuwa akiingia sehemu takatifu. Huyu alikuwa Jenifer, Hata Muddy aliposimama bado Jenipher hakuonyesha papara. Sohwa akamtizama Mohamed Usoni, akayaona macho yakimuonyesha kitu, kitu ambacho hakukijua. Akageuka nyuma kwa haraka, lakini akajikuta akiangaliana na macho ya mwanamke kama Yeye. Tena mkononi alikuwa amekamatia bastola. Alikuwa akitabasamu, tabasamu sahihi katika wakati sahihi na Muda sahihi. Sohwa akataka kufanya kitu, lakini kabla hajafanya lolote sauti Ya Muddy Ikasikika masikioni Mwao. Wote wakageuka kuelekea pale aliposimama.

*******

walisimamisha gari yao kisha wakashuka kuelekea ndani ya hoteli. Hawa walikuwa vijana wanne waliovalia kinadhifu, vijana ambao waliingia pale kanakwamba walikuwa wakienda kwenye kikao. Hawakuwa pale kwa sababu ya kikao wala mkutano. Walikuwa pale wakiifuatilia mawimbi ya mawasiliano kutoka kwenye Simu Ya Marehemu Neema. Mkononi kila mmoja alikuwa na kifaa kilichokuwa kikitambua kabisa ni wapi alipo mtu ambaye alikuwa akiitumia Simu Ya Marehemu Neema. Baada ya kuingia pale ndani kila mmoja akabana sehemu yake yenye kificho huku kila wakati macho yao yakielekezwa mlangoni. Zikapita dakika kama kumi pasipokuona kile walichokuwa wakikitafuta. Hawakuchoka kusubiri kwa kuwa walikuwa pale kwa kitu Muhimu sana. Kitu ambacho kimeleta presha na kimuhemuhe juu ya Ushiriki wa mataifa manne makubwa duniani katika mpango wa kufadhiLi Wahaini kutaka kuiondoa Serikali Madarakani. Kila sehemu katika Jiji la vancouver na Miji mingine ya Jirani, Majasusi wa MOSSAD, CIA,KGB NA M16 walikuwa wamezagaa kote katika msako huo. Msako ambao ulianzia pale watu wao kadhaa walipouawa katika Matukio mawili tofauti. Kila hoteli ilikuwa imetegwa kitu maalum, kitu ambacho kitajulisha pale mhusika anayesakwa akifika sehemu husika. Wanadada warembo walikuwa kwenye manight club wakijiachia Ukiwa ni mkakati wa kuwanasa wanaotumia simu ya Marehemu Neema. Walikuwa warembo wakuvutia hasa, kila mmoja alikuwa na kitu chake sehemu fulani katika mwili wake. Hapakuwa na Hoteli hata moja ambayo haikuwa Imewekwa chini ya Uangalizi wa majasusi wale. Kila kitu kilikuwa kikifantwa na ukaribu na viongozi wakuu wa Serikali.

*****

walikuwa watatu katika chumba kimoja cha Hoteli. Wote walikuwa wakiangalia kanakwamba walikuwa ndio wanaonana. Chini yao palikuwa na mwili wa mwanadada Shunie Ukiwa bado upo umelala kwenye Dimbwi kubwa la Damu. Muddy, Sohwa na JENIPHER walikuwa wakiangaliana. Wawili walionekana kujuana huku mmoja akionekana mgeni kwa mwingine na mwingine mgeni kwa mwenzake. ''Sohwa, Kutana Na Jenipher Dominick. Ni mwanausalama mwenzangu. Jenipher, Kutana na Sohwa Richardson ni Jasusi Kutoka shirika la Kijasusi la Urusi. Hatimaye Muddy aliongea huku akiwaacha wakisalimiana. Walipomaliza kupeana mikono, wakaamua kuondoka Eneo lile kwa kila Mmoja Kurudi Kwa Njia yake...

*****

Alikuwa Jenifer wa kwanza kufika hotelini kwake. Aliingia moja kwa moja kuelekea mapokezi kuchukua funguo yake. Alipotoka Hapo akaelekea chumbani kwake. Akaufungua mlango bila waswasi na kujitoma ndani. Akapokelewa na kitanda alichokiacha kikiwa katika utandikwaji ule ule lakini pakionekana sehemu ndogo kuwa tofauti kitu ambacho kilimpa picha kuwa alitembelewa na Mgeni chumbani kwake. AKATABASAMU kisha kuyavua mavazi yake Muda Mfupi alikuwa Bafuni akijimwagia maji
 
Back
Top Bottom