MKE WA RAIS
***
Ulikuwa Usiku tulivu, Usiku ambao ulimkuta Mohamed akiwa ametulia ndani ya Club Moja ya Usiku akipata kinywaji Chake huku akiangalia huku na huko. Alikuwa pale yapata dakika ishirini akisubiri kile ambacho aliahidiwa Na Jenifer. Kila wakati macho yake yalikuwa yakiburudishwa na kile alichokuwa akikiangalia. Wasichana waliovaa uchi hakushindwa kuwatupia macho katika aina ambayo Ilimvutia hata mwenyewe. Ukiondoa hilo lakini Jicho lake hakuliondoa sehemu. Sehemu ambayo alitarajia kumuona Jenifer akitokea pale. Lakini Haikuwa Hivyo, Muda uliendelea kupotea na Jenifer Hakuwa ametokea. Kitu kama wasiwasi kikaendelea kutanda Moyoni na hata mawazoni mwake, kuchelewa kurudi Kwa Jenifer kilikuwa kitu kilichomshangaza sana. Hakikuwahi wala Haikuwahi kutokea. Akajipa dakika zaidi Za kusubiri. Akatulia akiendelea kumimina kinywaji mdomoni, Punde akahisi kama mkono wa binadamu ukimgusa begani. Taratibu Mohamed Akageuza Shingo na kumtizama mtu huyo. Akakutana na tabasamu zuri, tabasamu ambalo humvutia kila Lijali. Mbele yake alikuwa amesimama binti alievaa kinguo kifupi, kinguo ambacho kiliiacha mikanda Ya Chupi aina Ya Bikini kuonekana kwa Urahisi. Mohamed hakukurupuka kuongea, bado alikuwa akilisanifu Umbo la mwanadada yule. Jicho lake lilikuwa likishuka na kupanda na kuishia kifuani. Kifuani paliposimama kitu mfano Wa Embe. Embe dodo. Hapo akatuliza macho na muda katika kutizama mahali hapo. Sio kwamba alivutiwa sana na Kifua cha binti yule. La hasha, kilichomfanya akazie macho Eneo lile ni kile kinguo alichovaa binti yule. Kinguo ambacho kilitengenezwa kwa kamba. Lakini ndani ya kamba hizo kulipitishwa waya mwembamba sana. Kengele ya hatari ikalia kichwani kwake. Akatambua na kugundua mwanamke aliembele yake ni Shushushu. Akarejesha Jicho lake chini na kukitizama kinguo kile usawa wa kiuno. Hapo akakiona kitu ambacho alitarajia kukiona. Kilikuwa Chombo cha mawasiliano, chombo kilichotengenezwa mfano wa kifungo. ''karibu Mrembo.'' hatimaye Mohamed akanena kwa sauti ndogo. Binti hakuuliza wala kuitikia bali alikivuta kiti na kusogea karibu na Mohamed kisha kukaa huku akiuruhusu Mwili wake ugusana na Mohammed. Hilo likafanikiwa. Muda mfupi mhudumu akafika na kupewa agizo la kuleta kile ambacho mrembo yule alihitaji. Hata kinywaji kilipoletwa mazungumzo yakaendelea Zaidi na Zaidi. Binti alikuwa mzungumzaji mzuri sana, alitokea kumvutia Mohamed kwa Uchangamfu wake. Licha ya kuvutiwa na maongezi ya mwanadada yule, lakini muda wote alikuwa akitizama mbele kama ataweza kumuona Jenifer.
Safari alimuona kweli, alimuona akitokea akiwa tofauti na alieondoka mwanzo. Huyu alikuwa Jenifer alievalia mavazi tofauti na yale aliondoka nayo Muda Mfupi Uliopita. Tabasamu likaupamba uso wake, tabasamu lenye Ujumbe ndani yake. Sekunde mbili mbele Mudy alikuwa akiinuka kuelekea msalani. Haukuwa msalani kama alivyoaga kwa mwanadada Yule, bali ilikuwa safari ya kuonana na Jenifer. Akatembea akikongoja kana kwamba alikuwa amelewa kwa kiwango cha Juu. Macjo yake yalikuwa yakiangaza mfano Wa bundi. Alikuwa akitizama kila upande, alijua wapo na walikuwa wakimuangalia. Alijua lazima atakuwa akifuatiliwa. Haukuwa Uongo, mbele Yake akatokea mtu anayemfahamu. Mtu ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa kitengo Cha kijasusi ndani Ya Idara Ya Usalama Wa Taifa. Huyu alijulikana kama Muuaji Asiye na Huruma. Kwa nini yuko Hapa? Naye ni mmoja kati yao? Yalikuwa maswali mawili ambayo hakuupata muda kutafuta majibu. Ndio kwanza wakapitana pasipokuangaliana. Kipara kilichotengenezwa kichwani kwa Muddy kilimfanya awe Tofauti Sana. Akakiendea Choo kimoja wapo kati ya Vyoo vingi ndani Ya club Ile. Akaufungua mlango Taratibu lakini kwa Tahadhali Kubwa. Akatanguliza Uso na Kuchungulia kwa ndani. Macho yake yakapokewa na kitu cha ajabu, kitu kilichomsisimua Mwili wake. Mwanaume mmoja alikuwa amelala katikati Ya Dimbwi la Damu. Mohamed akaurudisha mlango na kurudi pale alipomuacha Yule msichana, lakini safarii Hakuwepo. Alikuwa ameondoka akiacha kikaratasi Cha Sehemu ambayo anaishi. Muddy akakichukua kikaratasi kile na kukiweka mfukoni.
Dakika mbili baadae alikuwa akiondoka ndani ya Club kuelekea kule alipoelekezwa. Bastola Tatu Zilikuwa Mwilini katika Sehemu Tofauti. Umbali wa hatua Hamsini mbele akamuona Jenipher, hakumuangalia, hakutaka kuchelewa. Akaondoka akiacha Ishara, Ishara ambayo ilieleweka kwa Mlengwa. Akajipakia ndani ya Tax kisha safari Kuelekea anapoishi mwanamke Yule ikaanza. Muda Wote alikuwa akiangalia huku na huko kuangalia kama kuna Jambo lolote linaendelea. Naam, hakuwa mbali na hisia zake, Magari mawili kutoka Gari yao aliliona Gari jingine Likifuatia. Hili alikuwa akilitambua kwa kuwa hata mchana wa leo aliliona pale hotelini. Baada ya Dakika Tano Tax ikasimama mbele ya Hotel moja kubwa sana. Mohamed Akalipa, kisha akaongoza kuingia ndani ya Hoteli. Wakati Anaukaribia mlango Wa Chumba alichoelekezwa, akashangaa kumuona mtu yule yule akitoka. Lakini Safari hii hakupita Hivi hivi, bali aligeuka na Kumuangalia Muddy KisHa AKATABASAMUUU