MKE WA RAIS
kilikuwa kikao cha asubuhi, kikao ambacho hakuna mjumbe hata mmoja aliekitarajia. Kila mmoja alikuwa amelala akiamini kila kitu kimetulia, lakini taarifa ya kuuawa kwa watu wao wanne katika sehemu mbili tofauti iliwashtua na kuwafanya waitane asubuhi hii. Kila mmoja macho yake yalikuwa yakiongea, hakukuwa na hata mmoja ambaye hakushtushwa na taarifa ile. Chumba chote kilikuwa kimya kikifikiria hili na lile. Bado hawakutaka kuamini kama Kuna watu wanaweza kuwaua watu wao Bila wao kuuawa. Kingine ambacho kiliwashangaza na kuwaacha midomo wazi ni kule kuachwa hai kwa kijana Juma Hassan. Kwa nini wengine wauawe lakini huyu ameachwa hai? Kuna kitu gani hapa kati? Yalikuwa maswali mazito sana, Maswali ambayo hayakuwa na Majibu. Mara mlango Ukasukumwa wakaingia watu wengine wapatao sita, kila mmoja akaelekea na kuchukua sehemu yake kisha kukaa. Macho ya wajumbe wote wakageuka kutizama kule alipokaa kijana Juma Hassan. Kila mmoja alikuwa na maswali mazito, maswali ambayo yaliulizwa kwa macho badala ya Mdomo. Ishara za kijasusi Zikamfanya Juma Hassan kusimama na kuelekea mbele ya chumba kile ambacho kiligeuka kama ukumbi wa mkutano. Hakutaka kusita kuongea chochote, aliongea tokea pale alipoanza kufanya mawasiliano na mtu ambaye alidhani ni Neema Mtobwa kwa kuwa alikuwa akitumia akitumia namba yake. Akaeleza jinsi alivyogingewa mlango na mwaname na mwisho akamaliza pale alipomuona mwanaume akiingia na hakujua tena kilichoendelea baada ya kupigwa pigo ambalo hakulielewa lilipotokea.
Kumaliza maelezo kwa nyuma kulifuatiwa na Bumbuwazi, bumbuwazi na kengele za hatari kulia vichwani mwao. Maelezo ya Juma na kile walichokipata kutoka Tanzania juu ya kuawa kwa vijana wao, kitendo cha muuaji kuitumia namba ya Neema kukutana na vijana wao kisha kuwaua ni kitu ambacho kiliwatisha na kuwasisimua, kitu ambacho walikiona ni kama kuvuliwa nguo mbele za watu. Ilikuwa dharau gani mtu akuulie watu wako katika himaya yako? Huyu ni nani? Na anafanya hivi kwa kumpigania nani? Je Huyu ni Mohamed? Yote yalikuwa maswali ambayo hayakupatiwa majibu kwa wakati Ule. Muda mfupi baadae walikuwa ndani ya chumba cha wataalam wa IT ndani ya kitengo cha kijasusi Cha CIA. Wote walikuwa wamemzunguka mwanadada Shunie ambaye alikuwa akijaribu kuitafuta namba ya Marehemu Neema Mtobwa. Alitaka kujua ilitumika lini na ilitumiwa na nani. Kila mmoja alikuwa akihema kwa utulivu, macho yao yalikuwa mbele yakitizama kwenye computer. Punde kila mmoja alikuwa akihamaki baada ya Computer Kuleta majibu kuwa Namba hiyo Bado inatumika na mara ya mwisho kutumika ni Leo hii katikati ya Jiji la Vancouver kwenye Hotel Moja ya Nyota tano.
Wote wakaendelea kutizamana huku kila mmoja akifikiria kitu Cha kufanya. Ilikuwa ni ajabu sana Neema kufanya uasi wakati walimuamini sana. Kila mmoja alikuwa akiwaza lake na kila mmoja alikuwa akiwaza nini kifanyike. Kila mmoja alikuwa akihisi labda Neema ametekwa, kila mmoja alikuwa akihisi hivyo kwa kuwa hakuna anayeweza kuwagundua kiurahisi. Muda Mfupi baadae kiongozi wa mkutano ule akakumbuka kitu, kitu ambacho kilimpa Tabasamu la kushangaza mbele ya Wenzake. Akaichomoa Simu kutoka mfukoni mwake akaandika namba fulani kisha kuiruhusu simu moja kwa moja akaweKa Simu Sikioni.
''KGB MOSCOW RUSIA''. ilisikika sauti upande wa pili.
''Sohwa Richardson Anahitajika Canada Mchana wa leo. Ofisi imuandalie ndege''. Alijibu Yule Mjumbe wa kikao kile na kukata simu.
******
ulikuwa mchana wa saa nane, ndege ndogo ya kirusi ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndani wa polisi nchini Canada. Baada ya ndege kutua akashuka mwanadada Mrefu mweupe wa kawaida na kupokelewa na watu wasiopungua watano. Baada ya kumpokea mwanadada yule wakampakia ndani ya Gari na safari Ya kuelekea Hotelini ikaanza. Alionekana Muda Wote kama mtulivu, hakutaka kuongea kitu. Muda wote alikuwa kimya akiangalia hapa na pale. Alikuwa Mwanadada Sohwa Richardson, Jasusi kutoka kitendo cha Ujasusi ndani Ya KGB. Ukimuangalia alikuwa ni mwanamke mpole na mkimya lakini alikuwa ni mwanamke mbaya kuliko Hata Shetani. Alikuwa ameshafanya mission nyingi sana katika nchini mbali mbali. Mission kubwa ambayo nusura iondoke na maisha yake ni Ile ambayo ilifanyika katika Nchini ya Mexico. Bila utaalam wake wa kutumia silaha na mapigano ya mikono nadhani asingeweza kuwa hai mpaka Muda huu. Lakini Leo hii alikuwa Nchini Canada kwa wito kutoka kwa mkuu wake wa kitengo. Mkuu wake kikazi ambaye kauli yake ni kama Amri. Akaruhusu macho yake ya burudishwe na mandhari Nzuri ya Jiji la Vancouver, Mandhari Ambayo ilikuwa akivutia kutizamwa. Haikuchukua Muda Mrefu Gari ilikuwa Ikisimama Nje ya Hotel kubwa na Ya kifahari. Wakashuka wale wajumbe wakiwa sambamba na Sohwa. Wakawa wanaingia katika Hoteli ile. Wakati Watu wale Wakiingia, Mohamedi naye Alikuwa akitoka katika Jengo la Hotel ile. Macho Yake yakatizamana na Mwanamke Yule, Wakatambuana na Kujuana, lakini hawakusalimiana Bali wakapitana.
PATAMU HAPO