Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

Pole Ibra na karibu sana, unajua kujitete kama Muddy vile.
 
Pole Ibra87 tulikumiss sana muda wote nachungulia
 
Mlango ukamtii, akajikuta akitizamana na mwanaume wa miraba minne, mwanaume ambaye ukatili ulionekana waziwazi machoni kwa mwanaume huyu. Jenifer hakuonyesha kuogopa bali alilegeza macho na kukmkaribisha mwaname Yule. Lakini huyu hakuwa kama Juma, huyu alikuwa jasusi kupindukia. Hakuonyesha kutekwa kirahisi na uvaaji wa Jenipher. Mkono wake ukashuka mpaka nyuma ya mgongo, sehemu ambayo aliihifadhi bastola ndogo,lakini hakufanikiwa kuifikia, hakufanikiwa kusogea hata kidogo. Muda mupi alikuwa akianguka chini damu zikivuja kifuani.Bastola ilikuwa imefanya kazi yake. Kilikuwa kitu ambacho hakikutegemewa na mohamedi hasa pale alipomuona Jenifer akimvuta mwanaume Yule kwa ndani. Kilichofuata pale nikumsachi na kuchukua kila kitu ambacho walikiona kinafaa. Muda mfupi walikuwa wakitoka ndani ya JENGO LILE WAKIWA TOFAUTI, tofauti na walipoingia walipoufikia mlango wa pili bado walikuwa wenyewe, bado walikuwa peke yao. Walipoingia kwenye tax ndipo walipohisi kuwa walikuwa wakifuatiliwa, wakifuatiliwa na gari ambayo ilikuwa nyuma ya magari mawili. Hilpo likaongeza umakini kwao, hilo likawafanya kila mmoja awe makini. Wakaendelea kutulia wakati tax ile ikiendelea kukata mbuga, hata tax iliposimama mtaa wa tatu kabla ya kuifikia hotel wanayoishi, waliona ile gari ikiwapita kasha kwenda kusimama hatua kama kumi mbele yao. Kusimama huka kwao kulifuatana na kitu, kitu ambacho walikiona ndani ya casino. Walikuwa juu ya boneti wakibusiana na kutomasana hapa na pale. MOUDY NA JENIPHER hawakuwa wajinga, hawakuwa wajinga kuamini kile kinachofanyika kwamba ni mchezo wa mapenzi. Walijua wale ni watu kama wao, watu ambao walikuwa wakiwafuatilia kutaka kuwachunguza. Wakaonyesha kutokujali kitu wakashuka wakitembea wakiingia hapa na kutokea pale, hatua zao zilikuwa sambamba na macho ya na mikono yao, kila mmoja alikuwa mbele akitizama huku na mingine kuangalia huku, wakaingia katika mtaa ambao kulikuwa na watu wengi sana, wakajichanganya na kusimama hapo, wote wakigeuka kuelekea waliptoka. Haukupita muda wakakiona kile ambacho walikihisi, kile ambacho walikitarajia. Watu wawili waliowaacha wakidendeka walikuwa wamesimama wakiangalia huku na kule. Muddy akaondoka akimuacha jenifer amesimama, alitaka kuwafuata, bado hakuwa Muddy katika asili yake, huyu alikuwa na na humpa imani kubwa katika kupambana. Akasogea kama mtu wakawaida, akawapita kidogo huku pale alipo akiamini kuwa alikuwa akitazamwa na macho ya jenifer. Alipowapita kikafuatiwa na kitendo cha sekunde moja na sekunde ya pili alikuwa akitizama na mitutu ya bunduki, bunduki zilizoshikwa sawa sawia na watu ambao walionyesha kuua ndio kazi yao

Mudy akatulia kanakwamba hakuwa anajua chochote, alionyesha kushangazwa na kilichotokea, haukuwa mshangao wa kutokujua, huu ulikuwa mshangao wa kuwapoteza maboya. Akaruhusu wa msogelee kwa karibu, wakaruhusu kusogea wakimuendea MUDDY, hawakujua alikuwa nani, hawakujua huyu ni mtu gani, iliruhusu wapige hatua ya kwanza na hatua ya pili, ile wanataka kusogea hatua ya tatu wakakutana na mapigo ya uwepesi, mapigo ambayo hakuna alieona zaidi ya mpigaji na mpigwaji. Vijana wale walikuwa chini huku shingo zao zikiwa zimevunjika. Akautumia muda wa sekunde mbili kuwapekuwa marehemu wale, akachukua vichache alivyoona vinafaa akaungana na Jenipher wakaondoka katika eneo la tukio bila kuonekana.

  1. Ilikuwa ni asubuhi na mapema kuitishwa kwa mkutano ndani za ofisi za kitengo cha ujasusi katika nchini ya canada
 
Back
Top Bottom