MKE WA RAIS
Walikuwa ndani ya Hoteli ndani Ya Jiji la Vancouver Nchini Canada. Kila mmoja alikuwa katika chumba Chake akijiogesha na kuutoa Uchovu wa Safari. Walikuwa katika safari na mission hatari sana, walikuwa wawili katika nchi ya kigeni. Sehemu ambayo ilikuwa hatari kwa maisha na hata kwa nchi yao. Kuwafuata watu wanaolindwa na majajusi Wa kimataifa hakikuwa kitu chepesi na Rahisi. Muda wote walitakiwa kuwa macho, muda wote walitakiwa kuwa makini. Mudi alikuwa ni Jicho la Jenifer na Hata Jenifer aligeuka kuwa Jicho la Mohamed. Wote walikuwa wakiangaliana na wote walikuwa wakilindana. Ilikuwa ni Safari ya kufa na kupona, ilikuwa safari ambayo haikuwa ya Mchezo. Wao hawakwenda kama Cover wala Spy, wao walikwenda kwa sababu ya Mission Moja, Mission ya kurudi na Wahaini Katika Ardhi ya Tanzania. Wahaini ambao walikuwa Chini Ya Mossad, KGB NA hata CIA. Walioga katika utulivu na kumaliza katika usalama. Muda mfupi walikuwa wakitoka wakiwa wengine kisura, kiumbe na hata kimwendo. Walionekana ni kama bibi na babu. Hawakutaka kubaki pale wakiamua kuingia mtaani kufuatilia mawasiliano ya Kijana aitwaye Juma Hassan Ambaye alikuwa ni mmoja kati ya Watu ambao walikuwa wakiwasiliana na Neema Mtobwa kwa kipindi kirefu sana. Waliiendea Tax wakiwa wameshikana mikono, waliachiana baada ya kuingia ndani ya tax.
Wote walikuwa wakiangalia huku na huko bastola zilikuwa sehemu sahihi. Gari iliendelea kutembea kwa mwendo wa kawaida kuelekea pale ambapo walihitaji kufika. Hawakutaka kuongea chochote kile kwa kuwa hawakutaka kumuamini mtu, hawakutaka kuharibu kazi Yao mapema. Walitambua Uhatari wa kazi ile, walitambua uhatari wa kuongea na Mtu, Hilo walilifahamu, Hivyo hawakutaka kwenda kinyume. Dakika kumi baadae tax ilikuwa ikisimama mbele ya Hoteli kubwa ya kifahari. Wakalipa kisha kushuka na kuongoza kuelekea ndani Ya Jengo hilo ambalo licha ya kuwa hotel lakini pia ndani yake kulikuwa na Cassino. Waliingia kama wapenzi wakiwapita machangudoa waliokuwa wamezagaa nJe ya Hoteli. Wakazama ndani kisha kuongoza upande ule ambao kulikuwa na Cassino. Kila walipokuwa wakipita walikuwa wakikutana na vitendo vya ajabu sana. Kila hatua wanaume kwa wanawake walikuwa wamegandiana huku wakifanya vitu vya chumbani Hadharani. Bado hawakujali na wala hawakutizama, walikuwa wakitembea huku macho yao yakiangaza huku na Huko. Muda mfupi Wakausikia Mlio wa Simu, Simu Ya Marehemu Neema Mtobwa. Hawakuwa wajinga kuitizama pale, bado waliipuuza mpaka walipopita Ile Sehemu. Baada ya kuhakikisha hapakuwa na watu wanaopita wala kuwatizama Mohamed Akaitoa Simu na kuitizama. Akakutana na Ujumbe kutoka kwa Juma Hassan akiwataarifu kuwa Yupo Ghorofa ya TatU Room namba kumi na mbili.
Mudy akamuangalia Jenipher kisha akacheka.. Muda Mfupi Jenifer alikuwa Ghorofa ya tatu akielekea Chumba alichomo Juma Hassan. Alitembea kama mzoefu na alitembea kana kwamba ni Changudoa. Bastola mbili zilikuwa sehemu tofauti mwilini mwake, tayari kwa kuusambaratisha Ubongo wa Mtu. Akaufikia mlango wa chumba kile na kuugonga kama mara mbili. Punde aliuona Mlango Ukifunguliwa na Kijana Mwembamba mwenye Mwili Uliojengeka kimazoezi. Jenipher akasimama kumuangalia kijana yule kabla hajapiga hatua kuingia Chumbani. Kwa kuwa kuwa kuna kitu ambacho alikifuata hakuwa na muda wa kupoteza. Alikuwa katika mavazi ambayo yalimvutia kila mwanaume. Kinguo ambacho kiliyaacha mapaja yake Nje. Alipoingia hakusubiri kuambiwa pakukaa bali alijitupa Juu ya Sofa huku aliruhusu mapaja yake mpaka Chupi aliovaa kuonekana. Ulikuwa mtego ambao ulimnasa kiulaini Juma Hassan. Ingawa hakuwa Amemjua Mgeni Huyu lakini pale kuingia katika Chumba chake kulimfanya ahisi kuwa Labda ni Changudoa. Akayatoa mavazi yake na kubaki kama alivyozaliwa. Akapiga hatua na kusimama mbele ya Jenifer akimuelekezea Uume wake. Jenipher akatulia akimtizama kwa Macho Ya kurembua. Jicho ambalo lilimpa Ujumbe Juma Hassan. Punde alikuwa akiuruhusu Mkono wake ushike Uume Wa Hassan. Akauchezea huku Akiendelea kurembua. Muda mfupi Juma Hassan Alikuwa Chini akihema huku Jenipher akiwa Juu yake.
Alikuwa kwenye kiwango Cha Juu cha Uhitaji. Hata pale Mdomo wa bastola ulipomgusa kichwani kwake bado aliona ni kama Utani. Aliona kama Jenifer ana mtania. Lakini alipokuja kuuona mlango Ukifunguliwa na Kumuona Mohamedi akiingia. Akataka kujiinua ili kumuwahi. Hakuwahi kujaribu wala hakufanikiwa kujitingisha, mapigo mawili ya Karate yalimzimisha na kumpoteza fahamu. Wote wakaangaliana. Mudy akacheka huku Jenipher akitabasamu. ''Vipi hajanidokolea Mali yangu''!!? Akauliza Mohamed Swali ambalo liliwafanya wote wacheke. Baada ya kuhakikisha Yule mtu amepoteza fahamu wakaanza kupekua ndani Ya Chumba. Walipekuwa Kila Sehemu lakini Hawakupata kitu. Wakiwa wamekata tamaa wakitaka kutoka wakausikia Mlango Ukigongwa. Mudy akachupa na kutua kando Ya Mlango huku akimpa Jenifer Ishara Ya kuufungua Mlango. Jenipher akasogea Kisha Kunyonga kitasa, mlango Ukatii.....