Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

Giza likatanda usoni, kizunguzungu kikampata na muda mfupi alikuwa akianguka Chini. Akajitahidi kupambana na hali ile, haukuwa kazi rahisi. Muda mfupi alitulia na hakujua tena kinachoendelea. Ulikuwa ni kama muujiza au mchezo wa kuigiza, muda mfupi uliopita kabla walitoka wakiwa waarabu kuanzi muonekano, Nywele na ndefu. Lakini Muda huu walikuwa wakirudi kama wazungu tena tofauti na Carl pamoja na yule mwanamke. Hawa walikuwa Warusi kimuonekanma. Hawakuonyesha kuwa na wasiwasi pale walipokiendea Chumba chao. Hata walipoingia, waliingia kanakwamba hapa kuwa na mtu ndani. Hata walipouona mwili wa Jenifer ukiwa Chini umetambalajika bado hakuonyesha kujali. Bado waliuangalia mwili wa Jenipher huku wakitabasamu. Mwanamke akausogelea mwili wa Jenipher na kuupekuwa katika mavazi yake. Hapo wakakuta na bastola mbili za kirusi na magazine tatu za Risasi. Baada ya kuhakikisha hakuwa na kitu kingine walichukua kitu kama begi ambalo lilikuwa kubwa kupita kiasi. Muda mfupi baadae Jenipher alikuwa amewekwa ndani ya begi na kufungiwa humo ndani. Dakika mbili baadae watu wale walikuuwa wakiiacha hotel wakiwa na fuko lao begani. Dakika mbili tena gari moja ya kifahari Ilikuwa ikisimama mbele yao. Mlango wa nyuma ukafunguliwa kisha begi ambalo ndani yake alikuwepo Jenifer likaingizwa ndani kisha mlango kufungwa, hawakutaka kuupoteza muda, hawakutaka kuchelewa, walitakiwa kuondoka ndani ya Ardhi ya Tanzania wakiwa na mateka wao. Gari ilikuwa akikata mbuga kulitafuta Daraja la kigamboni, hawakutaka kupitia feri kuhofia kukaguliwa. Kila mmoja alikuwa makini kwa kila gari aliopita mbele yao. Bastola zao mikononi huku kila wakati wakiangalia nyuma pale walipoliweka begi. Hakuna ambaye alijiamini kirahisi katika kuondoka na mwanamke yule. Kila mmoja alikuwa akiondoka katika ardhi ya Tanzania kwa kushindwa. Muda mfupi walikuwa uhasibu wakiutafuta uwanja wa Taifa. Punde wakaibukia Tazara wakiutafuta Uwanja wa ndege. Kufikia hapo kila mmoja akatabasamu, yalikuwa matasamu ya Kufanikiwa kutoroka na mpiganaji mmoja. Hawakuuona Ugumu tena wakuondoka Tanzania kwa usalama.

Alikuwa akihisi kama yupo kwenye shimo refu sana. Akahisi ndani ya Shimo hilo kama alikuwa akirushwa na kuachiwa akijibamiza kitu ambacho alihisi ni kingo za shimo hilo. Akataka kufumbua macho yake ili kutizama na kuona wapi alipo. Hata alipofanikiwa kufumbua macho hakufanikiwa kuona chochote zaidi Ya Giza totoro. Akajaribu tena na tena katika kuangalia huko lakini ndio kwanza kiza kilitanda kila sehemu. Hakujua alipo na pia hakutambua kwa nini yuko pale. Akajituliza na kuipa Uhuru Akili yake, Uhuru wa kukumbuka ilikuwaje mpaka kufikia pale alipo. Akakumbuka walipoingia ndani ya kivuko kisha kufuatiwa na watu ambao waliwatambua kuwa ni majasusi. Akakumbuka waliposhuka upande wa pili na kuanza kuwafuatilia. Kufikia hapo akakumbuka kila kitu, alikumbuka mara ya mwisho alipoingia katika Chumba kile na kuchomwa na kitu kama sindano. Kufikia hapo hakujua tena kilichoendelea. Hapo ndipo akajua kuwa yupo mahala ambapo hapakuwa salama kwake. Kule kurushwa rushwa na kujigonga kwenye kitu kama kingo kulimpa ufahamu kuwa alikuwa akipelekwa sehemu. Sehemu ambayo aikuwa salama kwake. Akajaribu kuunyoosha mkono wake, akakutana na kitu kama Kitambaa. Hapo akagundua kuwa alikuwa ndani ya kitu kama begi. Akauruhusu mkono wake uelekee sehemu fulani ambayo alipendaga sana kuhifadhi Kisu chake. Ilikuwa sehemu ambayo haikuweza kufikiwa na mikono ya binadamu wakaida. Mkono Wake kufika pale ukakutana na kile ambacho alikuwa akikitafuta. Kisu yake ilikuwa imewekwa katika Sehemu yake. Akaichomoa kisha kuipeleka moja kwa moja katika kitambaa kile. Muda mfupi alikuwa akiona taa kupitia upenyo ambao ulitosha kumsaidia kuona alikuwa wapi. Hapo ndipo aliposhudia kuwa alikuwa ndani ya Gari na kwa muda ule walikuwa wakiipita Vingunguti. Akatambua kuwa alikuwa akisafirishwa. Akisafirishwa bila kujua wapi ambapo alikuwa akipelekwa.

Akajiondoa katika begi lile kisha kutulia akisubiri mpaka mwisho wa safari kuona wapi anapelekwa. Aliendelea kutulia mpaka pale alipoiona gari ikikatiza kushoto kuingia Uwanja wa Ndege wa mwalimu nyerere. Hapo akaamua kujiandaa kufanya kitu, kitu ambacho hakujua kitapokelewa vipi. Wakati wakiingia Eneo la uwanjani Kitu Cha ajabu kikatokea. Taa zote za uwanjani zikazimwa, Hilo likaleta mshangao kwa majasusi wale, muda mfupi walikuwa wakichupa kutoka garini na kuangukia pembeni. Kila mmoja alikuwa na bastola mkononi. Macho yao yakiwaka huku na huko, kila mmoja alikuwa akitizama katika aina fulani, aina ambayo husaidia kumuona hata sisimizi gizani. Bado hali ilikuwa ngumu na tete, wakiwa bado wamekaza macho kuangalia huku na huko, wakamuona mtu akitoka nyuma ya Gari huku akiwa kama kivuli. Ulikuwa Ushukaji thabiti, Ushukaji ambao ulipendeza lakini huku ukiogofya machoni kwa Majasusi wale. NGOMA BADO ILIKUWA MBICHI, TENA MBICHI KABISAAA
 
MKE WA RAIS

Ulikuwa ushukaji wenye kuburudisha machoni mwao, ushukaji ambao haukuwahi kufanywa na mtu katika namna ile. Licha ya kuburudisha machoni lakini ulikuwa ni ushukaji uliowatia hofu Moyoni. Kila mmoja alikuwa haamini kile kilichotendeka pale. Wakahisi labda hakuwa Jenifer, walihisi hivyo kwakuwa waliamini Jenipher hawezi kutoka kutokana na sehemu waliomuweka. Bado uwanjani palikuwa giza, bado uwanjani hapakuonyesha usalama wa upande wao. Punde tu mlio ukasikika katika ngoma za masikio, mlio ambao haukuwa mgeni masikioni mwao. Ulikuwa mlio wa risasi, Risasi kutoka kwenye bunduki kubwa ya kivita, Hii ilikuwa bunduki ambayo iliwakumbusha mbali, bunduki ambayo iliwaonyesha njia wakati walipokuwa katika mapambano Kule Mexico. Haikuwa Bunduki nyingine bali ilikuwa AK 47. Bunduki iliotengenezwa Nchini Urusi. Wote wakainuka kuitafuta Njia, Lakini hatua kumi mbele kabla hawavuka maegesho ya magari wakashuhudia mwanamke walienaye akirushwa hewani na kutupwa umbali mrefu. Hawakufanikiwa kumuona akisimama tena. Walijua alikuwa maiti, walijua alikuwa mfu. Kila mmoja aliitafuta njia huku wakifyatua Risasi Juu kujihami. Lilikuwa kosa kubwa katika mapambano kufanya kama kile walichokuwa wanakitenda. Walikuwa wakiipiga risasi kwa kila Wanachohisi ama kusikia. Hawakujua risasi zingewaishia, hawakujua kwamba wanacheza na watu hatari. Muda wote walikuwa wakionekana machoni kwa Jenipher, alikuwa na uwezo wa kuwaua, alikuwa na uwezo wa kuwafyeka, lakini hakutaka hilo litendeke. Bado walihitajika wakiwa hai, bado walihitajika wakiwa wanapumua. Bado aliwaangalia na kuzidi kuwaangalia, aliwatizama wakitembea na hata walipokuwa wakijificha. Umbali wa hatua kama sabini macho yake yakamshuhudia mwanaume akiingia, huyu alikuwa Mohamed akisogea katika Ile namna. Hapa ndipo alipokumbuka Kitabu Cha Mtunzi Mahiri Afrika mashariki na kati. Mtunzi ambaye alibeba sifa kedekede. Hapa alimkumbuka Hayati Ben Mtobwa. Mwandishi katika vitabu vilivyompa Ujasirikatika kupambana. Ulikumbuka mkasa Wa mikata ya kishetani, hata alipokumbuka salamu toka kuzimu aliamini kuwa yeye alikuwa ni kama Neema Idd. Aliamini alikuwa ni kama Nuru Katika Mkasa wa Je TUTARUDI NA ROHO ZETU? Akaruhusu macho yake yamtizame Mohamed pale alipokuwa akihama hapa na kuingia pale.

Alijisikia faraja, faraja ambayo iliongezeka zaidi pale alipomuona Mohamed akipaa angani na kuachia mapigo kadhaa, mapigo ambayo yalitolewa kwa umaridadi na mtu yule aliyekuwa tayari kwa mapambano. Alituliza macho yake akimuacha Mohamed katika pambano lile. Akashuhudia utaalam kutoka kwa mtu yule ambaye alionyesha kuleTa Upinzani. Zilimchukua Mohamed Dakika tano kumnyamazisha Yule mkora. Akamuona Mudy akiondoka pale kwa kuhama hama kama Chui. Jenipher akajiinua pale na kusogea naye. Muda wote bado giza lilikuwa totoro, bado hawakuonana wala kutizamana. Uwanjani palitulia huku abiria waliokuwepo wakitakiwa kutokutembea popote. Haikupita muda taa zikawashwa lakini muda ule ule zikazimwa tena. Kuwashwa kwa taa na kuzimwa ndani ya sekunde hakukuondoka pasipo kitu. Bali kuliambatana na milio ya Risasi na mayowe ya maumivu, kisha ukimya ukarudi Tena na giza kuendelea kushika hatamu. Ulikuwa mchezo wenye burudani, ulikuwa mchezo ambao ulikuwa ni wahatari. Majasusi wanne kati ya watano walikuwa chini wakiwa tayari maiti. Bado alikuwa akitafutwa Carl Jack, bado alikuwa akitafutwa uwanja mzima. Hakuweza kuonekana katika eneo hilo. Kila mmoja alikuwa macho kutizama huku na huko lakini bado Carl Jack hakuonekana machoni mwao. Umakini ukaongezeka zaidi, eneo lote lilikuwa chini ya Uangalizi wa kikosi kitiifu kwa Rais Wa Nchi. Likageuzwa nje ndani lakini bado hawakumuona Carl Jack. Tangazo likatolewa kutoruhusu ndege kupaa. Kikosi kikaongoza kuingia ndani ya Uwanja. Wakati wakikaribia kuufikia mlango wakausikia mlio wa Bunduki ukitokea Nyuma yao.. Wote Wakageuka Nyuma kuangalia...
 
Ibra, nina stress level leo, hata usingizi sina, plz naomba vipande hata vinne vinitolee uvivu.
Natanguliza Shukrani
 
MKE WA RAIS

Wote wakaangalia nyuma huku midomo ya bastola ikiwa imetangulia mbele. Kila mmoja kidole tayari kilishuka mpaka sehemu ya kitufe cha kuruhusu Risasi. Walikuwa tayari kulipua chochote. Hawakukuta kiummbe chochote kikiwa hai. Chini alilala Carl Jack damu ikisambaa kama maji. Kichwa chake hakikuwa kinatizamika kutokana na kufumuliwa kwa Risasi. Kila mmoja akamtizama mwenzake katika mtizama wa maswali, ni nani amemuua Carl? Ni nani ameruhusu Risasi kufumua kichwa cha Jasusi Huyu? Yalikuwa maswali yasio na majibu, maswali ambayo yalijibiwa pale walipousogelea mwili wake. Chini pembeni kidogo ya ulipo mwili wake ilikuwepo Bastola aina ya Revolver Colt 48. Jibu ni kwamba Jack alikuwa amejiua, hapakuwa na ujanja wa kuwatoroka kikosi kile kitiifu kwa Rais. Hii ni moja kati ya mbinu za kijasusi, mbinu ya kujiua pale ambapo utahisi kuzidiwa. Mohamedi na Jenipher wakautizama Mwili wa CARL kwa hasira, alitamani kumkata kichwa na kumpotezea mbali, alitamani kumkuta hai ili alipize kwa kile alichomtendea Ummu. Lakini hakufanikiwa Hilo, matokeo yake mwili wa Carl Jack ulikuwa mbele ya macho yake akiwa hata tena Uhai. Bado hawakujua kipi ambacho kinaendelea, lakini punde wote wakageuka kumtizama Mohammed pale simu ya mfukoni kwake ilipotoa mlio wa ajabu. Ulikuwa mlio tofauti sana katika milio yote wanayoifahamu.

Siku moja simu ilikuwa mikononi mwa kikosi cha usalama. Kila mmoja alikuwa akiusoma Ujumbe kutoka ndani ya Simu ile. Mtumaji akionyesha kutokujua kama Mmiliki wa Simu tayari ni Marehemu. Mtumaji alikuwa Yule yule Mwenye jina lenye Herufi Mbili VP, herufi ambazo bado ilikuwa ni kizungumkuti. Ujumbe Ulitumwa kwa lugha taalam ya kijasusi, Lugha ambayo haikuwa shida machoni na kichwani kwa Mohammed katika kuelewa. Baada ya kuusoma Ujumbe Akamuangalia Jenipher usoni. Macho yao yakaongea kitu, kitu ambacho kilionekana dhahiri Shahiri machoni kwa wapiganaji wengine. Mtumaji wa Ujumbe ule aliandika kitu ambacho kiliwapa wakati wa kufikiria. MKIFANIKIWA KUONDOKA SALAMA HAPO UWANJANI NJOONI MOJA KWA MOJA NCHINI CANADA. Ndivyo Ulivyosomeka Ujumbe. ''Ni wakati wakuwafuata huko huko na kurudi nao hapa Tanzania. Hawawezi kutuchezea kama watoto.'' ilikuwa sauti ya Mohammed akiongea mbele ya wanausalama wengine. Ilikuwa ni lazima waelekee Canada Sehemu ambayo ni hatari kuliko kilichotokea hapa Tanzania. Ni vigumu kwenda kuwachukua watu katika Nchi ya kigeni, watu ambao walikuwa Chini ya Ulinzi Wa majasusi wa MOSSAD, CIA, KGB. Ilikuwa ni kazi ngumu na ya hatari lakini ilikuwa nilazima kufanywa.

Muda mfupi baadae walikuwa masaki ndani ya Jengo moja ambalo Rais amehifadhiwa. Mohammed na Jenipher walikuwa mbele ya Rais Wa nchi Mheshimiwa Omary Ramadhan Mustapher. Rais alikuwa akiwatizama Huku Machozi Yakimtiririka na kushuka mashavuni. Hakuwa na neno sahihi la Kuongea, hakuwa na neno la Shukurani ambalo aliliona likifaa kuwapa vijana wale. Akabaki akiwatizama Huku akilia. Mwisho akatamka kuwa TANZANIA SI NCHI YANGU PEKE YANGU BALI NI NCHI YENU. KILA KILICHOPO NDANI YA ARDHI YA NCHI HII NI HAKI YA KILA MWANANCHI WA TANZANIA. NASIKITIKA MKE WANGU HAKULIANGALIA HILO. NAWASHUKURU SANA NI WAKATI WA KUIJENGA TANZANIA YETU. Baada ya kuongea hilo hapakuwa na Muda wa kupoteza. Walieleza dhamira Yao kuwafuata wale wote waliotoroka na Kuwa Rudisha nyumbani. Rais akaonyesha kupigwa na Butwaa, Mohammed na Jenifer hawakusubiri kauli kutoka kwa Rais. Waliondoka ndani ya Jengo lile Wakimuacha Rais akiwatizama. Aliujua Uhatari uliombele yao, lakini hakuwa na njia Ya kulizuia hilo.

********

ilikuwa yapata saa tano za usiku kwa sasa za america. Ndege kubwa ya Abiria ilikuwa ikishuka katika Uwanja wa Vancouver nchini canada. Baada ya ndege kutua na kuruhusu abiria kushuka. Kila mmoja alishuka na kuelekea chumba cha ukaguzi. Baada ya kila kitu kukamilika abiria walitoka ndani ya uwanja kuelekea nje. Kati ya Abiria walioshuka wawili walikuwa ni Mohammed na Jenipher. Ilikuwa ni vigumu kuwatambua kuwa walikuwa wao kutokana na Mavazi na jinsi walivyojibadilisha. Hawakuwa wale walioondoka Tanzania wakiwa katika uzuri wao, hapa walionekana ni watu wa miaka Hamsini mpaka sitini. Baada ya kufika Nje waliiendea tax moja Ambayo ilikuwa Jirani, muda mfupi walikuwa barabarani wakielekea katika mji Uitwao Victoria. Ulikuwa mji ulio pembezoni mwa Mji wa Vancouver, kila mmoja alikuwa macho akitizama na kuangalia huku na Huko, Haukuwa mji mgeni kwa Mohamed. Alishawahi kufika mara nne katika safari tofauti. Safari ambazo zilikuwa za kufa na kupona kama hii. Muda wote alikuwa akimuangalia Jenipher na walikuwa wakitizamana. Muda wote alikuwa akitamani kuongea na Jenipher lakini Hakupenda kufanya Hivyo kwa wakati Ule. Ni hapo wakati wakiwa kwenye Tax wakaiona Gari ikiwapita kwa kasi. Haikuwa kasi ya kawaida, ilikuwa kasi ya kuashiria kuwa Hapakuwa na Usalama. Lakini hawakujali hilo, Hawakujali kwa kuwa hawakujua kama wao ndio wanafuatwa. Muda mfupi baadae walikuwa ndani ya Hoteli Ya kifahari kila mmoja akiwa katika chumba tofauti. KAZI IMEANZAAAA
 
Back
Top Bottom