RIWAYA: Isabel ndani ya mpango hasi

RIWAYA: Isabel ndani ya mpango hasi

Watu wamekufa balaa... maskini isabela pole sana kwa unayopitia
 
ISABEL-Ndani ya Mpango Hasi

Ilipoishia...
Dreva aliondoa gari na kuelekea alikoagizwa.
Walipofika central Suzan alishushwa na Gina
akafuata nyuma yake.
“Hifadhi huyu, naomba asihojiwe lolote mpaka
mpatapo amri nyingine” Gina aliwakabidhi Suzan
polisi waliopo kaunta na kisha yeye akaongoza
kuelekea ofisi ya Inspekta Simbeye.
“Kazi uliyonituma imekamilika afande” Gina
aliongea kwa ukakamavu mbele ya bosi wake
“Vizuri sana afande, waweza kwenda
nitawasiliana na wewe nitakapokuhitaji” Inspekta
Simbeye alimueleza Gina, Gina akaonesha
ukakamavu wake kwa kubana mikono yake
miwili kuonesha heshima, kisha akageuka na
kuondoka.
tiririka...
“Suzan, hebu kuwa mzalendo, tueleze, unajua
Isabel alipo?” Sergeant Bizibu alimuuliza kwa
upole
“Jamani mimi nina mhusiano gani na Isabel?
Mimi ni muhudumu wa afya, nimeingia kazini
nakuta hiyo habari, mbona mnanionea?” Suzan
alilalamika
“Sikia mrembo, hapa hatujaja kukufanyia
chochote kibaya, tunachotaka ni wewe kujibu
maswali yetu, usitufiche kitu. Tii sheria bila
shuruti, lakini ukikaidi utashurutishwa kuitii.
Tueleze Isabel ametoroka au ametekwa kwa
mawazo yako?”
Suzan alitulia kidogo aliziangalia pingu zile za
chuma mikononi mwake hakuamini, aliinua uso
wake na kumtazama polisi huyu mwenye cheo
cha sergeant aliyeketi mbele yake, aligeuka huku
na huku akaona kuwa kumbe wapo wawili tu mle
ndani, akajikohoza kidogo
“Sikia afande Isabel alikuwa anaumwa sana hasa
mbavu na mguu wake, lakini mimi simjui
kiundani anaweza akawa ametoroka au
ametekwa kwangu ni swala gumu kwa kuwa
sikuwepo kazini na aliyekuwepo ameuawa”
Suzan alijibu kisha akainamisha kichwa chake
kwenye kijimeza kile kidogo kilichotengenezwa
kwa chuma
“Kwa hiyo unatuambiaje?”
“Mi sijui kilichotokea”
Baada ya mahojiano marefu kati yao, sergeant
Bizibu alighairisha zoezi na kuamuru Suzan
apelekwe chumba cha pili akahifadhiwe kwa
muda.
Kilikuwa ni chumba chenye giza kilichojengwa
katika chini ya ardhi, Suzan aliingizwa na
kukalishwa kwenye kiti maalum mikono yake
ikiwa nyuma ya kiti hiko na kusikiliwa na kamba
maalum, Suzan hakuona chochote zaidi ya giza
nene lililokijaza chumba hicho.
“Jamani huku ni wapi?” aliuliza kwa sauti ya
kilio
“Huku ndiyo chumbani kwako kwa muda tu”
alijibiwa na WP mmojawapo aliyekuwa
akimfunga vizuri katika kiti hiko kisha wakatoka
na kumuacha wamemfungia mlango.
***
“Amekataa kutoa ushirikiano” Inspekta Simbeye
alimueleza Kamanda Amata aliyekuwa
akizungushazunguash akalamu yake vidoleni.
“Au tunamuonea?” aliuliza Amata
“Hapana haonewi mtu, huyu kwa vyovyote
anahusika”
“Inspekta, tusifanye mambo kwa hisia, anahusika
vipi? Hilo ndilo la msingi. Katika pekuzi zenu kitu
gani mmechukua kama kisaida polisi?”
“Ah, tumechukua simu yake ya mkononi.”
“Hapo umecheza, hebu lete hiyo simu tuangalie
namba zilizopigwa au zilizoipigia, tunaweza
kupata jibu” Amata alimaliza kwa maneno hayo.
“Kamanda, sikuwa na wazo kama hilo, mi
nilitaka kwenda kampuni ya simu kucheki rekodi
za simu na meseji zake”
“Huko mbali Inspekta, umeanza kuzeeka au?”
Kamanda Amata alimtania mzee huyo wa
makamu amabaye anamkumbuka sana kwa
kwata alilompigisha huko CCP Moshi.
Kamanda Amata aliifungua simu ile na sekunde
kadhaa ilitoa mlio mkali na kuonesha picha ya
bahasha juu ya kioo chake, akaufungua ujumbe
huo…
‘…umefika salama, kama utahitaji msaada
utuambie…’
Ujumbe ule uliisha hivyo na hakukuwa na namba
yoyote zaidi ya maandishi private number,
Amata alitikisa kichwa na kuendelea kuangalia
jumbe zingine, nyingi alizishuhudia za mapenzi
tu ambazo hazikuwa na maana sana kwake,
alipotaka kubadili kuangalia simu zilizoingia na
kutoka ndipo alipouona ujumbe wa mwisho
‘…Valley View hotel Na. 47…’
Amata hakuona umuhimu wake alijua itakuwa ni
sehemu ya kukutania na mpenzi wake, lakini
kengele za hatari ziligonga kichwani mwake,
akainua mkono kwa kidole chake cha shahada
akajikuna pua yake.
“Vipi Kamanda, umegundua kitu?” Inspekta
Simbeye aliuliza
“Aaa mapenzi na miadi tu”
Akampa ile simu Inspekta Simbeye aliitupia
macho ile meseji, jicho lake la kushoto
likamcheza, hatari! Alirudisha simu kwa Amata.
“Kamanda, Valley View.”
“Vipi umehisi kitu, Inspekta?”
“Kabisa, bila shaka”
“Ok, hiyo ni point namba moja, na hiyo itazaa
namba mbili. Naomba nikuache Inspekta”
“Hamna shida ukihitaji msaada usisite
kunitafuta”
Kamanda Amata alitoka na kuchukua tax
kuelekea ofisini kwake ambako alimkuta Gina
akiendelea na kazi hii na ile ilimradi siku
zilienda.
“Karibu” alimkaribisha
“Asante, hamna jipya?”
“Hamna”
Amata aliketi juu ya kiti chake na kuanza
kutafuna karanga zake moja baada ya nyingine
huku akiandika mambo Fulani katika kitabu
chake cha kumbukumbu.
***
“Kamwe hamtoweza kufisha juhudi za kimataifa,
mpango huu umesukwa na kusukika” Jomse
alimueleza Madam S maneno hayo huku akiwa
kamuelekezea domo la bastola kubwa aina ya
revolver iliyofungwa kiwambo cha sauti.
“Wewe ni nani?” Madam S aliuliza
“Mimi ni mwanamapinduzi halisi, nipo hapa kwa
kazi moja tu ya kuondoka na roho yako”
aliongea kwa dharau.
Ilikuwa ngumu kwa Madam S kujitetea mbele ya
bastola hiyo ambayo haikuonesha masikhara
hata kidogo, alishindwa kumtambua mtu huyu
kwa kuwa alikuwa amevaa soksi kichwani
kuuziba uso wake na kuruhusu macho tu kuona.
***Haya madam S mbele ya mdomo wa bastola,
atanusurika?
 
Mkuu Kid kudi tafadhari usituache saana, maana stori hii tamu mnoo... inanikumbusha akina Will Gamba
 
samahani casuist,unaweza kunitumia link ya hadithi ulizotuma nyuma? au yeyote anaeweza anitumie tafadhali.
 
ISABEL-ndani ya mpango hasi

ilipoishia...
“Kamwe hamtoweza kufisha juhudi za kimataifa,
mpango huu umesukwa na kusukika” Jomse
alimueleza Madam S maneno hayo huku akiwa
kamuelekezea domo la bastola kubwa aina ya
revolver iliyofungwa kiwambo cha sauti.
“Wewe ni nani?” Madam S aliuliza
“Mimi ni mwanamapinduzi halisi, nipo hapa kwa
kazi moja tu ya kuondoka na roho yako”
aliongea kwa dharau.
Ilikuwa ngumu kwa Madam S kujitetea mbele
ya bastola hiyo ambayo haikuonesha
masikhara hata kidogo, alishindwa
kumtambua mtu huyu kwa kuwa alikuwa
amevaa soksi kichwani kuuziba uso wake na
kuruhusu macho tu kuona.
endelea...


“Mimi ni mwanamapinduzi halisi, nipo hapa kwa
kazi moja tu ya kuondoka na roho yako”
aliongea kwa dharau.
Ilikuwa ngumu kwa Madam S kujitetea mbele ya
bastola hiyo ambayo haikuonesha masikhara
hata kidogo, alishindwa kumtambua mtu huyu
kwa kuwa alikuwa amevaa soksi kichwani
kuuziba uso wake na kuruhusu macho tu kuona.
“Umeingiaje ofisini mwangu hali milango yote
nimefunga?”
“Kama Yesu alivyoingia kwa wanafunzi wake
huku milango imefungwa” alijibiwa. Madam S
alipandwa na hasira kwa dharau alizozionesha
huyo bwana, alimkazia jicho na kumwangalia
kwa hasira.
“Usiniangalie kama unavyomwangalia paka
wako, nimeshakwambia nataka kuondoka na
roho yako ili mipango mingine iende, na hapa
ninavyoongea na wewe kijana wako anayejifanya
mtukutu Kamanda Amata yupo matatani,
tunataka tupindue nchi hii na hilo kwamwe
halipingiki.”
Madam S alishusha pumzi ndefu akimwangalia
mtu yule aliyekuwa akijiamini ndani ya ofisi ya
watu, akili ilimzunguka huku na huku hakujua
afanye nini. Kutoka pale alipoketi Jomse
alisimama taratibu, kitendo ambacho madam S
alikiona ni udhaifu mkubwa, kwa wepesi ambao
haukutegemewa madam S alijirusha mtindo wa
tick tack na kuipiga bastola ile kutoka mikononi
mwa Jomse, ilipaa juu na kugonga ceiling board,
Jomse akiwa bado anashangaa akitaka kuidaka
bastola, Madam S alikuwa tayari ameshatua
chini, pigo moja la karate lilitua sawia katika
mbavu za Jomse, maumivu yake yalimfanya
apoteze muelekeo, bila kuchelewa Jomse
aliachana na wazo la bastola na kumkabili
Madam, patamu! Jomse kwa haraka alimtazama
Madam S na kumuona jinsi alivyotulia kumkabili,
bila kuchelewa Jomse alicheza Ashi Barai,(Foot
sweep kick), kwa mguu wa kushoto aliupiga
mguu wa madam S ambao ulikuwa umetanguliza
mbele kwa kuufagia, madam S alipoteza stamina
na teke la nguvu lilitua sawia kwenya sikio la
madam S, mpepesuko wako ulimpeleka mpaka
kwenye kabati lililokuwa limejaa mafaili na kabati
lile lilishindwa kuvumilia na kuanguka palepale
alipoangukia madam S, kitendo bila kuchelewa
madam S alikuwa tayari kajirusha kiufundi na
kuondoka eneo lile ambapo kishindo cha kabati
kiliwashtua walinzi wa nje nao kwa haraka
wakakimbilia ndani kuona kunani, madam S
alijiviringa na kusimama karibu kabisa na kabati
lake dogo upande wa pili wa meza kubwa tayari
Colt 45 bastola hadimu ya kimarekani ikiwa
mkononi mwake, kidole kwenye trigger kilicheza
kidogo tu colt ikabanja lakini kwa haraka Jomse
alishatoka eneo lile kwa sentimeta kadhaa.
Mlango ulipigwa kikumbo na walinzi wawili
wakaingia.
“Mikono juu!” askari mmoja wa kampuni ya
ulinzi alimuamuru Jomse, kosa kubwa! Jomse
aliinua mikono juu wakati huo tayari
alishachomoa kisu chake kidogo katika mkanda
wake na kukirusha kwa ustadi wa hali ya juu,
moja kwa moja kilitua katika koromeo la askari
yule, kishindo kingine kilisikika cha bunduki
kubwa na kutawanya taa kubwa iliyokuwa
imesimamishwa kwenye kona, Jomse aliruka
back na miguu yake ikatua katika kioo kikubwa
cha dirisha na kudondoka nje, madam S na yule
mlinzi mwingine walitoka haraka na kukuta
tayari Jomse karuka wigo wa waya na kudandia
pikipiki lake kubwa Cagiva la Kirusi,
wamemkosa.
Madam S aliificha haraka bastola yake kwenye
mkanda wake maalum aliouvaa ndani ya koti
lake la suti, na kurudi kule ofisini kwake,
walimkuta yule mlinzi akikata roho, mauti
yakamfika.
Vitu vilikuwa shghalabaghala ofisini kwa madam
S.
“Bastard !!!” Madam S alifoka kwa hasira huku
kifua chake kikipanda na kushuka, akachukua
simu yake na kubofya namba za Kamanda
Amata, ‘mteja unayempigia kwa sasa hapatikani,
jaribu tena baadae’
“Shit !!” aling’aka madam S na kufungua droo
yake, akatoa magazine nyingine iliyojaa risasi,
akatoka nje akiwa anataka kuingia kwenye gari
yake, alishtushwa na sauti iliyomwita.
“Madam S” alikuwa ni Inspekta Simbeye.
“Hali ni tata Inspekta”
“Unaenda wapi madam?” Inspekta aliuliza
“Naenda kumsaka hayawani” alijibu huku
akiingia kwenye gari
“Hapana Madam subiri kidogo, akili yako itulie”
Simbeye alimbembeleza madam, maana
alimuona jinsi alivyopaniki na ule utu uzima,
“Nipe bastola” Inspekta Simbeye alimuomba
Madam bastola huku akimnyooshea mkono
ishara ya kuomba, madam S alitulia kidogo.
“Kwa kuwa ni kazi yako chukua unikabidhi
baadae” madam S alimwambia Inspekta
Simbeye.
Madam S alipiga tena simu ya Amata bado
ilikuwa haipatikani, kijasho kilimtiririka, hana la
kufanya, alishuka garini na kurudi ofisini kwake,
mlangoni alisipishana na mwili wa yule mlinzi
ukiwa ndani ya machela na kufunikwa kitambaa
cheupe, aliufunua na kumtazama kwa huruma,
akafanya ishara ya msalaba na kuufunika tena.
* * *
Kamanda Amata alifika katika kaunta ya Valley
View Hotel, mwanadada mrembo alimwangalia
kijana huyu mtanashati ambaye mwili wake
uliojengeka vizuri ulikuwa umetulia vyema
kwenye fulana yake nyeusi iliyombana na
kuonesha siha yake ya kimazoezi.
“Karibu nikusaidie tafadhali” muhudumu yule
alimkaribisha Amata
“Asante sana, nafika chumba namba 110
tafadhali” akili ya Amata ilikuwa inafanya kazi
haraka, katika kitabu cha wageni pale mezani
alishaona kuwa chumba namba 110
kimechukuliwa na mwanamke hivyo ingekuwa
rahisi kwa mhudumu huyo kumruhusu bila
shaka.
“Sawa, subiri mtu akusindikize.”
“Hapana, nitakwenda mwenyewe”
Kwa mwendo wa haraka haraka Amata alikwea
ngazi za jingo hilo mpaka ghorofa ya nne na siyo
chumba alichotamka, baada ya kuzimaliza ngazi
zile alifika kwenye korido ndefu iliyotandikwa
zuria mororo jekundu, alitembea mpaka mlango
namba 07, alisimama kidogo akaangalia huku na
huku na alipoona kuna utulivu alisikiliza kidogo
akagungua kuwa kuna utulivu wa hali ya juu,
akachukua moja ya funguo zake na kutumbukiza
kunako tundu husika, mizunguko miwili mitatu tu
mlango ulilegea na taratibu Amata aliufungua na
kuingia ndani kisha kuubana nyuma yake na
funguo kurudisha mfukoni. Kwa hatua za hadhari
akihakikisha hagongi kitu chochote alitembea
taratibu na bastola yake ndogo ikiwa tayari
mkononi, alisita kidogo na kurejesha akili yake
chumbani mle, alisikia maji yakitiririka bafuni,
aliuendea mlango wa bafuni taratibu bastola
ingali tayari mkononi, kwa mkono wa kushot
alitikisa kitasa cha mlango huo na mlango bila
ubishi ukajiachia, maji yalikuwa yakitiririka,
hakuna mtu bafuni. Amata aligundua hapo
kachezwa shere, akapuuzia na kurudisha bastola
yake kiunoni, lahaula! Kabla alipoiweka tu
bastola yake kabla hajageuka pigo moja la haja
la karate lilitua shingoni mwake, kigiza cha
sekunde kadhaa kilimtawala, alijihisi kukosa
nguvu lakini nuru ya mwanga ikamrejea tena,
hakuona haja ya kufanya mzaha katika hilo
akajiangusha chini, adui yake akaona huo ndiyo
mwanya wa kufanya yake alimuendea Kamanda
Amata pale chini kabla hajatahamaki, kamanda
Amata aliinua chupa ya whisky iliyokuwa hapo
chini na kumrushia adui yake usoni kwa nguvu
zote, wakati adui yake akiipangua kwa ufundi
chupa ile, Amata kwa mguu wake wa kulia bado
akiwa chini alikanyaga kwa nguvu sehemu za siri
za adui yake na kumfanya atoe mguno wa
maumivu. Kwa mruko wa kisarakasi, Amata
alijinyanyua na kuwa wima, ngumi nzito ilikuwa
ikiuelekea uso wa Amata nae kwa mchezo wa
kitoto akepa na kuudaka, bila ajizi akaukunja na
kuuvunjia begani kwake, yowe la nguvu lilimtoka
jamaa huyo baada ya kushuhudia mifupa ya
mkono wake ikiachana, Amata aliuvuta mguu
wake wa kulia na kumpita kidogo kisha
kumchota mtama a nyuma na jamaa alitua chini
kama mzigo na kuivunja meza ya kioo iliyokuwa
hapo vipande viwili, goti la kamanda likatua juu
ya tumbo la adui.
“Tulia! Shhhhhh” Amata alimuonya jamaa kutulia
huku akiwa kamshika mkono wake uliovunjika
kwa mkono mmoja na mwingine kashika kipande
cha chupa, “nani amekutuma?” alimsaili huku
akiuzungusha taratibu ule mkono uliovunjika.
“Aaaaaaaa, unaniumiza, ntasema ntasema..”
adui alitoa yowe la uchungu
“Sema!”
“Walionituma siwajui kwa undani” huku akilia
kwa uchungu “wapo wengi ila nawajua kwa
uchache”
“Wataje majina na wapo wapi?” Kamanda
aliuliza kwa hasira, “Hujibu ee?” aliuzungusha
mkono kwa nguvu.
“Wapo Burundi, wapo Burundi na wengine
Rwanda” alijibu
“Taja majina” Amata alilazimisha
“Aaaa nimeshakujibu tayari” alilalamika
“Bado, na hapa mko wangapi?” Amata aliuliza
nalipoona jamaa huyo hatoi ushirikiano,
aliuzungusha mkono kwa ghafla, yowe la nguvu
lilimtoka na Amata akubana mdomo wake kwa
kiganja cha kulia baada ya kukitupa kile kipande
cha chupa.
“Tupo wengi, na wengine miongoni mwenu…”
alijibu huku akianza kutupatupa miguu huku na
huko, Kamanda Amata alimwangalia kwa hasira.
“Shit!” povu lilimtoka mdomoni na macho yake
yakageuka kuashiria kuwa uhai haupo tena,
kimbebe.
‘Tupo wengi na wengine miongoni mwenu’
sentensi hii ilimjengea mwangwi Amata, hata
akajikuta nguvu zinamwishia, alisimama na
kumuacha huyo jamaa hapo chini, aliiendea
meza iliyokuwa na computer mpakato, akapekua
kwenye vidroo na kukuta business card
mbalimbali akakusanya zote na kutia mfukoni,
flash iliyokuwa ikining’inia katia laptop na kitabu
cha kumbukumbu akavitia katika kibegi chake
cha mgongoni na taratibu akauendea mlango,
alichukua funguo mezani na kufunga kwa nje
kisha kushuka ngazi taratibu. Alipita kaunta na
moja kwa moja alifika nje kabisa, alikatiza mtaa
wa kwanza wa pili na kuingia katika gari yake
akaketi.
“Uhhhhhhhh” akashusha pumzi kisha akawasha
gari na kuingia barabarani akatokomea mjini.
* * *
Tonton alifungua mlango wa chumba chake,
hakuamini alichokiona, Anaconda alikuwa
amelala chini chali damu zikiwa zimetapakaa na
kuanza kuganda huku chumba chote kikiwa na
hewa nzito. Tonton alitikisa kichwa, hakujua la
kufanya alipotupa jicho mezani laptop yake
ndogo (note book) haikuwepo, alichanganyikiwa,
alitazama huku na huku na kuichomoa bastola
yake kisha kwa mwendo wa minyato aliusogelea
mlango wa bafuni ambako bado maji yaliendelea
kumwagika, hakuna kitu, alirudi na kuangalia
kwenye kibaraza cha nje, bado hakuna mtu,
akasonya na kurudisha bastola yake kiunoni.
‘Hapa hapana usalama’ alijisemea na moja kwa
moja aliliendea begi lake chumbani na kukuta
lipo kama alivyoliacha, alichukua dokumenti zake
na hati za safari na kutoka chumbani mle. Akiwa
chini anatoka katika lifti alipishana na askari
polisi wane wakiingia kupandisha juu, moja kwa
moja akapita na kuondoka zake, njiani alikuwa
akiendesha gari huku akiwa na mawazo mengi,
kwanza aliona wazi kuwa bwawa limeingia luba,
hamna la kufanya, alifikiria tu kwanza kufika
chimbo ili akajipange upya na wenzake
waliosalia chimboni. Aliiacha barabara ya
Msimbazi na kuchukua ile ya Morogoro kuelekea
posta lakini katika makutano ya Umoja wa
vijana alikunja kulia na kuipita ile ya Lumumba
mpaka Nkurumah na kurudi mpaka mataa ya
Kamata na kukunja kushoto kuelekea Kurasini.
Honi za hatari zilipigwa na geti likajifungua
lenyewe, bila kuuliza aliingia ndani kumkuta
Jomse akiwa kajiinamia huku mkono mmoja
ukiwa unaminyaminya mbavu zake. Kelele ya
mlango ilimfanya kushtuka na kuikamata bastola
yake tayari kwa kazi.
“Oh Ton, bienvenue mon ami” Jomse
alimkaribisha kwa lugha yao ya kifaransa, “Ton,
kazi hii imeshatuelemea, yule bibi nimeshindwa
kummaliza, sijui itakuaje, sijui nimtafutie wapi,
amekuwa mbogo aliyejeruhiwa” Jomse alipigisha
mikono yake kwa ishara ya kukata tamaa na
kutikisa kichwa chake kushoto kulia.
“Jomse, Anaconda ameuawa, nahisi si mwingine
ni Amata aliyefanya kazi ile” Ton alifikisha
taarifa, Jomse alipatwa na mshtuko mkuu alibaki
midomo wazi na mikono ikimtetemeka, alipiga
ngumi mezani na meza ile ya kichina
iliyotengenezwa kwa cheapboard ailigawanyika
vipande viwili. Aliichukua bastola yake na
kuitazama kwa makini ‘Kisasi’ alijisemea, akiwa
kaukunja uso wake kwa hasira.
“Wangu Amata, wako Bibi, Meno ya Mamba
atabaki hapa kumlinda Isabel”

***** haya kumekucha....!
 
ISABEL-ndani ya mpango hasi

ilipoishia...
Honi za hatari zilipigwa na geti likajifungua
lenyewe, bila kuuliza aliingia ndani kumkuta
Jomse akiwa kajiinamia huku mkono mmoja
ukiwa unaminyaminya mbavu zake. Kelele ya
mlango ilimfanya kushtuka na kuikamata bastola
yake tayari kwa kazi.
“Oh Ton, bienvenue mon ami” Jomse
alimkaribisha kwa lugha yao ya kifaransa, “Ton,
kazi hii imeshatuelemea, yule bibi nimeshindwa
kummaliza, sijui itakuaje, sijui nimtafutie wapi,
amekuwa mbogo aliyejeruhiwa” Jomse alipigisha
viganja vya mikono yake kwa ishara ya kukata
tamaa na kutikisa kichwa chake kushoto kulia.
“Jomse, Anaconda ameuawa, nahisi si mwingine
ni Amata aliyefanya kazi ile” Ton alifikisha
taarifa, Jomse alipatwa na mshtuko mkuu alibaki
midomo wazi na mikono ikimtetemeka, alipiga
ngumi mezani na meza ile ya kichina
iliyotengenezwa kwa cheapboard ailigawanyika
vipande viwili. Aliichukua bastola yake na
kuitazama kwa makini ‘Kisasi’ alijisemea, akiwa
kaukunja uso wake kwa hasira.
“Wangu Amata, wako Bibi, Meno ya Mamba
atabaki hapa kumlinda Isabel”
endelea...


9
Kompyuta ya Kamanda Amata ilikuwa ikiisoma
flash aliyoichukua kule hotelini, siri nyingi na za
kutisha zilikuwa zikipita katika kioo cha
kompyuta ile, Amata alibaki kapigwa na butwaa,
akili ilimsimama na meno kumchezacheza, hapa
ndipo aligundua hatima ya mpango hasi ambayo
katika memory card aliyopewa na Isabel kipande
hiki hakikuwapo. Aliendelea kusoma na kupata
majina kadhaa ya madigala wa mpango huo
duniani, aligundua kuwa kumbe ni nchi za
Maghalibi ndizo zinazofadhili mapinduzi hayo
kwa faida yao wenyewe, Amata alizama katika
lindi la mawazo, akiwaza na kuwazua, akipanga
na kupangua.
Alipogeuka kuielekekea simu yake na ndipo
alipojikuta kuwa hayupo peke yake.
“Tulia hivyo hivyo!” sauti ilimkoromea kutoka
upande ule, Amata hakuwa na la kufanya
“Simama taratibu” aliamriwa na kutii bila shuruti
“Kwa mwendo wa taratibu ongoza nje ya
nyumba yako kupitia geti kubwa”, Amata
alifanya hivyo na kufika nje ambako aliikuta gari
ndogo aina ya Toyota Altezza ikiwa buti wazi
“Ingia kwenye buti, ukileta matata nafumua
ubongo wako sasa hivi”
Amata alitazama huku na huku “Usijaribu kuleta
shida ingia twende”, Kamanda Amata na ujanja
wake wote aliingia ndani ya buti ya gari hiyo,
Jomse aliruka kwa wepesi na kulifunga buti lile
Amata akiwa ndani, kisha akaingia garini na
kuondoka kwa kasi.
“Kamanda Amata nimemtia mkononi” Jomse
alikuwa akiongea kwa simu na mtu mwingine
“Vema, hakikisha unamhifadhi vizuri mpaka amri
nyingine itapotolewa” sauti ya kike kutoka
upande wa pili ilisikika
“Sawa Madam, nitahakikisha hilo, hawezi
kunitoroka huu ndiyo mkono wa Shetani” Jomse
alimalizia kauli yake.
Kamanda Amata akiwa ndani ya buti hakuweza
kujinyoosha kutokana na udogo wa buti lile,
aliuinua mkono wake wa kushoto uliokuwa na
saa kubwa ya kisasa akabofya kitu Fulani
pembeni mwa saa hiyo, kidoti chekundu kikawa
kinawakawaka juu ya kioo cha saa hiyo,
aliisogeza karibu na kinywa chake na kuongea
maneno Fulani, kisha akabofya tena sehemu
nyingine, sasa kidoti cha kijani kikawa
kinawakawaka, akatulia kimya butini akisubiri
hatima yake huku akihesabu kona ya kwanza
mpaka ya mwisho kulia ama kushoto.
Gari ilisimama, kamanda Amata alihisi geti
likifunguliwa na sauti zilizoongea kifaransa
zilimfikia masikioni mwake, alielewa yote
yaliyoongelewa, na baada ya sekunde kadhaa
gari ile iliingizwa ndani na geti kufungwa nyuma
yake, gari ikasimama
“Kuwa muangalifu, hajafungwa huyo” Jomse
alimuamuru Meno ya mamba ambaye alibaki
pale kuweka ulinzi kwa Isabel na jingo zima kwa
ujumla.
“Huyo msichana mpumbavu ameamka?” Jomse
aliuliza tena
“Hapana bado hajaamka, na sijui kama ataamka
maana hali yake ni mbaya sana” Meno ya
mambo alimjibu Jomse.
“Ah Muache afe tu, ijapokuwa Madam Rose
alikuwa anamuhitaji lakini hatuna la kufanya”
Jomse alimueleza Meno ya Mamba. Amata
aliposiki kauli hiyo aliumia sana kwa kuwa
aligundua kuwa Isabel lazima atakuwa
ametekwa na kuwekwa huku, na kwa vyovyote
atakuwa kwenye hali mbaya kutokana na mateso
makali.
“Suka taratibu, usilete makeke, la, hii SMG
itakufumua vibaya na mwili wako utakuwa
chakula cha samaki usiku huu” sauti kavu ya
Meno ya mamba ilisikika masikioni mwa Amata.
Kamanda Amata alishuka kutoka kwenye buti ya
gari ile na kusimama kwa miguu yake miwili,
mikono yake ikiwa juu aliona asifanye makeke
yoyote kwani alishajua kuwa Isabel yupo eneo
hilo, japokuwa kwake haingekuwa kazi ngumu
kuwadhibiti wote wawili.
“Geuka nyuma yako na uongoze njia unayoiona”
Amata alitii na kufuata kijia hiko huku mikono
yake ikiwa juu kama alivyoamuriwa. Hatua
chache alijikuta katika ubaraza mpana tu, ukiwa
na viti viwili na kighorofa kimoja, chini sakafuni
aliona mwili wa binadamu aliolala bila uhai,
Amata alipigwa na butwaa aliutazama mwili ule
kwa haraka haraka akagundua kuwa si
mwingine ni Isabel alikuwa amelala chini na
mwili wake kutupwa kama wa mbwa. Hasira kali
zilimshika Kamanda Amata hakujua afanye nini,
alitamani aukimbilie ule mwili kujua kama una
uhai au la, lakini alishindwa japo alikuwa
anaumia sana
* * *

Ikulu ya Dar es salaam

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
tayari katika suti yake ya kijivu na msafara wake
wa watu wa usalama, walijipangwa kwa safari
ya uwanja wa ndege, tayari kwa safari ya
Washington ambako alialikwa kwa mkutano
maalum na Rais wa Marekani Mheshimiwa
Barack Obama. Kila kitu kilikuwa
kimekwishapangwa, watu wa usalama tayari
walikuwa wameandaa kila kinachobidi kwa ajili
ya kutekeleza na kuhakikisha kuwa mheshimiwa
Rais anafika safari yake salama na kurudi
salama, ujumbe anaosafiri nao tayari ulikuwa
ndani ya ndege kule uwanja wa ndege terminal 1
wakiwa wanamsubiri tu mheshimiwa Rais.
“5H-ONE, Gulfsream Aerospace G-V SP G550,
ndege ya serikali ya jamhuri ya muungano wa
Tanzania, inaomba njia kuruka saa tatu na
dakika thelathini usiku huu” sauti ilisikika katika
chombo maalum cha muongoza ndege katika
mnara mkubwa wa kuongozea ndege ulio upande
wa kusini wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Kambarage Nyerere.
“5H-ONE, Gulfsream Aerospace G-V SP G550,
unaruhusiwa kuruka kupitia upande wa
mashariki” sauti ya muongoza ndege iliruhusu
kuondoka kwa ndege ya Rais baada ya
kuhakikisha anga yote ipo salama kabisa.
Wakiwa wameketi sawia na mheshimiwa Rais
katika kaofisi kake kadogo ndani ya ndege hiyo
tayari kwa sfari kuelekea DC Washington. Dakika
chache tayari ndege ile ilikuwa imeiacha ardhi ya
Tanzania na kupasua anga kwenda anga ya
kimataifa, ikiwa chini ya uangalizi wa Rubani
mzoefu Capt Maga Junior na wasaidizi wake
wawili.
Madam S, aliiangalia ndege ile inapopotelea
mawinguni upande wa Vingunguti, yeye na
wengine waliomsindikiza mheshimiwa Rais
walianza kuchukua magari yao tayari kwa kurudi
kwenye shughuli zao nyingine, mara alihisi saa
yake kubwa ya mkononi inamfinya kwa vijimeno
maalum vilivyo chini ya saa hiyo, alihisi kuna
kitu, akaingia haraka kwenye gari yake na
kubonyeza kitufe Fulani pembeni ya saa hiyo, mara ikaanza kupiga ukulele kwa sauti ya chini ikitoa kamkanda kembamba ka plastiki
kalikokuwa na maadishi Fulani.
‘Att:Hakikisha mheshimiwa Rais haondoki, hiyo ndege imetegwa bomu kwenye control box na italipuka akiwa angani, fanya hima, mimi nimetekwa na sijui nilipopelekwa, fanya hima Tena Sana Aisee’ , madam S alishuka kwenye gari akiwa kama aliyechanganyikiwa hakuwa anajua afanye nini, alichukua simu yake na kubofya namba Fulani.
“Hallo, naomba urudi uwanjani haraka sana kuna dharula” simu ilifika kwa waziri wa ulinzi aliyekuwa tayari amekwishaondoka lakini gari yake bado ilikuwa njia panda ya air port kuelekea mjini, dreva wa gari hiyo aina ya Toyota Land Cruiser V8 aliligeuza na kurudi uwanja wa ndege, mara gari zilizofuata nyuma, kwa kitendo kile nazo zilirudi hasa zile za usalama.
“Madam nini tena?” waziri wa ulinzi mheshimiwa Machura a,imuuliza Mdam S ambaye alimkuta nusu kachanganyikiwa akiongea peke yake. Akampa ule mkanda uliotoka katika saa yake, naye akausoma, akashika kichwa hakujua la kufanya. Walibaki wanahangaika akili zikiwa zimewaruka kwa kiasi Fulani, kizaazaa!
* * *
Kamanda Amata alisoma kipande cha mwisho cha mpango hasi katika flash disk aliyoichukua kule valley View Hotel, ikionesha kuwa baada ya mauaji ya watu muhimu, wa mwisho kabisa ni Rais wan chi ambaye atategewa bomu kwenye ndege yage yake itakayoruka tarehe 26 June 2013 saa tatu na nusu usiku, bomu hilo limepangwa kulipuka dakika arobaini na tano baada ya ndege kuruka, lilikuwa limetegwa kwenye control box inayosambaza umeme katika ndege hiyo ya kisasa kabisa ambayo hakuna nyingine kama hiyo Afrika, kwa jinsi walivyofunga bomu hilo ilikuwa ni pale rubani anaporuhusu magurudumu kurudi ndani ndipo nalo linajiwasha na kuanza kuhesabu dakika 45 tu na kulipuka.
“Simama apo hapo!” sauti ya Jomse ilimuamuru
Kamanda Amata. Meno ya mamba alimsogelea Amata ili amfunge katika kiti kilicho jirani hapo.
“Kaa chini usilete fujo, muda wetu umeisha wa kuwa nchini kwenu, dakika chache tutakuwa ndani ya nchi yetu” Jomse alimueleza Amata ambaye alishikwa na hasira kali, akihesabu dakika za bomu lile lililotegwa katika ndege ya Rais, hakujua kama itwezekana kuokoa janga hilo au la, alitamani kama yeye angekuwa pale uwanjani ahakikishe mwisho wake.
Alipohakikisha amemfunga barabara, Meno ya mamba aliirejesha bastola yake kiunoni na kutembea hatua chache na kumsukasuka Isabel kwa mguu wake, Isabel hakutikisika.
Mara simu ya Jomse iliita
“Mission clear, popo ameruka, subiri majibu”
Jomse alitoa cheko la dharau
“Kamanda Amata, sasa dunia itatikisika kwa hofu kuu kwa kusikia mlipuko mbaya wa ndege ya Rais wako, ha ha ha ha” alijigamba, “Sisi ndiyo wanamapinduzi, unakumbuka Rwanda na Burundi mwaka 1994, tulimtungua Rais
Abiyarimana na mwenzake Ndadaye!? Mliiona kama hadith ee! Ni sisi na sasa tuko hapa Tanzania, kamwe hamuwezi kukomesha juhudi,nakuwekea TV hapa uone dakika 40 zijazo breaking news” sauti hiyo ilimkosesha raha Amata alitamani amrukie na kumg’ata ama kumeza kabisa kiumbe huyo. Waziwazi Amata alifura kwa hasira, akaanza kuopumua kwa nguvu na kifua chake kipana kikipanda na kushuka, akiwatazama kwa macho ya hasira watu hawa wakati wanamuwekea TV mbele yake umbali wa mita kama saba hivi.
Jomse alichukua simu yake iliyokuwa mezani wakati huo na kubonyeza namba Fulani kisha akaweka sikioni.
“Yes. Hello, kutoka point A mission Clear, panga vikosi kuanza kazi mara moja pindi nikikupa taarifa” alikata simu na kuiweka mfukoni.
“Unasikia we mbwa, tayari majeshi ya waasi yameshakaa katima mapori ya Nyakanazi, na mengine yapo hapa Dar, tukitangaza tu nchi inapinduliwa dakika moja tu, na wewe ukishuhudia halafu utakuwa maiti, na yule bibi kizee wako muda si mrefu ataletwa hapa, na mtu wa kuwaua yuko Burundi anakuja, ha ha ha ha!” Jomse aliongea kwa daharau ya hali ya juu.
Kamanda Amata kwa nguvu zote alijinyanyua kitini na kukinyanyua kiti kwa miguu yake na kukirusha kwa kukipiga mbele, kumbe kiti kile kilikuwa hakijafungwa pamoja naye, kilinyanyuka kwa kasi na kutua kichwani kwa Meno ya mamba, akiwa sasa mikono yake iliyofungwa pamoja imebaki nyuma, alimuona Jomse akija kwa kazsi pale alipo, Kamanda Amata lijikunja kwa kuruka na kuipenyeza miguu yake ndani ya wigo wa mikono iliyofungwa kuelekea nyuma na sasa mikono ile ilikuwa mbele, alinyanuka kwa kazi na kupiga double kick iliyotua kifuani mwa Jomse na kumpepesua hata bunduki yake kumtoka mikononi na kudondokea mbali, alipotua tu sakafuni kwa miguu miwili alipigwa mtama wa nguvu ambao ulimnyanyua juu na kabla hajatua aliichanua miguu yake na kuwatandika wote wawili kila mmoja teke la nguvu la mguu wake. Meno ya mamba alitema meno kadhaa.
Kamanda Amata alijiviriga kutoka pale
alipokuwepo na kuiwahi bastola iliyokuwa chini,kabla hajafika alipigwa teke la sikio na kumfanya kupoteza uelekeo, alijigeuza chali na kumuona Jomse akiwa na shortgun mikononi mwake, Amata hakujali, akiwa bado yupo chini alimdiga Jomse teke la nguvu nyuma ya vivigino lililomfanya aanguke chali kama mzigo kabla hajatulia, mguu wa nguvu ulitu juu ya tumbo la Jomse, ukelele wa maumivu ulisikika, wakati Meno ya mamba akija kwa kasi kumkabili Kamanda Amata ambaye alikuwa amelala pale chini, alishuhudia kichwa cha Meno ya mamba kikitawanyika vibaya na mwili wake kurushwa mita kadhaa ukiwa hauna uhai. Gina akiwa bado hajasusha mkono wake wenye bastola aina ya Makarov, bastola ya kirussia iliyotengenezwa mwaka 1949 na bwana Nikolay Makarov na
kuanza kutumika rasmi mwaka 1951 ilishafanya kazi yake kama ilivyoamuriwa.
“Freeze, bastard” Gina alimuamuru Jomse
aliyekuwa akijaribu kujitutumua pale chini, Jomse alijifanya asikii na kutaka kuichuku ile short gun mara Makarov ya Gina ilicheua tena na kuvunja mkono wa Jomse, yowe la maumivu lilisikika.
Mara polisi kadhaa waliingia ndani ya jingo lile wakiongozwa na Inspekta Simbeye, walimfungua kamanda Amata na kumchukua Isabel baada ya kugundua kuwa bado alikuwa na uhai, haraka sana wakamkimbiza Hospitali ya jeshi la
wananchi Lugalo.
Naomba muhakikisehe huyu mtu anafika makao makuu ya polisi leo kwa mahojiano, mimi naelekea uwanja wa ndege kuna muasi mmoja bado hajakamatwa na hayupo hapa” kamanda Amata alitoa amri huku akiingia katika gari ile iliyomleta, Toyota Altezza na kuigeuza kwa kasi na kuondoka eneo lile kuelekea uwanja wa
ndege.

:::Shughuli imeamka, ndege ya Rais
imeshapaa... kuna bomu ndani yake...
:::Madama S atafanya nini kulinusuru janga
hilo?
:::Kamanda Amata atawahi uwanja wa ndege?
:::Nini hatima ya ISABEL, TONTON na kisa
kizima.
Kwa kujua hayo na mengine yote usikose
chapisho lijalo
 
Sawa mkuu tumekusoma
Subira yavuta heri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom