RIWAYA: Isabel ndani ya mpango hasi

RIWAYA: Isabel ndani ya mpango hasi

Season 2

Episode 1

A mata ga Imba aliketi kwa utulivu kabisa juu
ya kiti chake cha kunesanesa akishikashika
magazeti ya siku hiyo ili aone chochote
kilichandikwa, kila gazeti liliandika habari hiyo
kwa manjonjo kweli kweli ili mradi kuvutia
wasomaji ‘Majambazi yavamia Treni’ mojawapo
liliandika, ‘Polisi auawa ndani ya Treni’ lingine
liliandika hivo ‘Treni yatekwa, wawili wauawa
akiwemo Polisi’. Amata alipitia yote hayo na
hakuona jipya lililokuwemo zaidi ya habari za
kubuni.
“Boss!” sauti ya kike ilimstua Amata akiwa
amezama katika moja yha magazeti hayo.
Alikuwa ni Gina aliyesimama kaegemea mlango
wa kuingia ofisini kwa Amata
“Unatamani kama ungekuwepo eti!?” Gina
alimtupia swali Amata. Amata alimuangalia na
kutoa tabasamu pana kisha akazama tena katika
gazeti hilo.
“Boss!” Gina aliita tena
“Nimekwambia mara nyingi usiniite Boss, we
husikii” Amata alimwambia Gina katibu muhtasi
wake
“Oh nilisahau, samahani Mr Amata” Gina
alijisahihisha na kusogea karibu na meza ile
huku akiwa na faili mkononi mwake, Amata
alikunja gazeti lile na kuliweka pembeni.
“Nipe ripoti mrembo” Amata alimwambia Gina.
Gina akiwa antazama dokumenti fulanifulani
katika faili lile alikuwa akimueleza Amata taarifa
mbalimbali za kazi alizomuachia lakini wakati
huo Amata mawazo yote yalikuwa hayapo hapo
alifikiri tu kama angekuwa ‘Mungu’ angemponya
Isabel ili ajue nini kilitokea katika mkasa ule wa
jana usiku.
“Mr Amata, inaonekana haupo kabisa hapa
kimawazo, au hiyo habari imeshakutia kiwewe,
tayari unatamani kuanza fujo zako” Gina
aliongea kwa hamaki kidogo.
“Ah Gina, unajuaje? Kama waniletee mzigo
niufaulishe” alimueleza Gina huku akiwa
anacheka kiutani, akatoa karanga zake mfukoni
na kula moja moja. Amata ga Imba alipenda
sana kutembea na karanga mfukoni tangu utoto
wake alipokuwa shule ya msingi Ukonga mpaka
ukubwani, tabia hii imepigiwa kelele na watu
wengi akiwemo marehemu mama yake lakini
alishindwa kuiacha.
6
MAMBO YA NDANI
Kikao cha watu wanne kiliendelea katika moja
ya ofisi za jengo la wizara ya mambo ya ndani
karibu kabisa na barabara ya Ohio, makubaliano
yalikuwa ni magumu kwa jinsi kila mtu
alivyofikiri juu ya tukio hilo.
“Hii ni kazi ya polisi tuwaachie wenyewe” IGP
Makabayo, alilieleza jopo hilo
“Hatukatai usemalo lakini linavyoonekana tatizo
lenyewe unafikiri polisi wataliweza?” Madam S
aling’aka kwa kuwa yeye anahusika na usalama
wa Taifa moja kwa moja.
“Tuna kitengo cha CID, kazi haiwezi kutushinda
hata kidogo” IGP aliongeza
“Ok! Nafikiri hii ni kazi yetu sote, kulinda
usalama wa nchi vinatuhusu sisi sote. Haina
haja ya kugombana. Tuwaachie jukumu hilo
vijana wetu wa polisi walishughulikie,
wakishindwa tutaona kwa pamoja tufanye nini”
Waziri wa mambo ya ndani alipitisha uamuzi
wake.
“Sikatai unalosema mheshimiwa lakini tangalie
tunachokifanya tusije kulaumiana baadae”
Madam S aliliambia jopo huku akiwa
amesimama. Madam S alishaliona swala lile
kuwa polisi kama wao peke yao hawaliwezi kwa
jinsi lilivyo katika mapana yake, na alishangazwa
jinsi ambavyo IGP alivyolitaka swala lile libaki
mikononi mwa polisi, Madam S alikubali kwa
shingo upande lakini atafanyeje, hakuna jinsi.
Kikao kiliendelea na kuona mipango ya hapa na
pale.
Maagizo yalitolewa kwa pande zote mbili jinsi ya
kufanya kazi hiyo.
“Ok sasa baada ya hapo, nitaomba mambo
yafuatayo yafuatwe, moja, hakikisheni yule binti
anawekwa chini ya ulinzi asiruhusiwe mtu awaye
yote kumuona kwa sasa bila kibali cha polisi,
pili, Madam S mueleze Kamanda Amata juu ya
hili na mueleze kwa sasa asijihusishe kabisa na
swala hili mpaka atakapopata taarifa tofauti.
Nafikiri tumeelewana, jinsi ya kufanya kazi IGP
unajua kuwapanga watu wako. Asanteni.” Waziri
alimaliza na kuagana na wajumbe.
Madam S alibeba faili lake na kutoka nje bila
kuaga, hakupenda wala kufurahia juu ya uamuzi
uliotolewa na wizara, kwake hakuingia hakilini
kabisa.
***
Kamanda Amata alipata taarifa yote ya kikao
kutoka kwa Madam S, hakuwa na la kufanya
isipokuwa ni kukubaliana na utaratibu uliotolewa
lakini moyoni mwake alikuwa na shauku sana ya
kutaka kujua hasa kiini na mpango mzima wa
mkasa huu. Alitulia juu ya kiti kile huku
akimwangalia Madam S kama mtu ambaye
hajawahi kumuona katika maisha yake
“Hii ndiyo shida ya polisi” Amata alimwambia
Madam S, ambaye wakati huo alikuwa anaperuzi
mambo Fulani katika kompyuta yake pale
mezani, sauti hiyo ya Amata ilimgutusha kidogo
maana alishasahau kama ofisini mle hakuwa
pekeyake.
“Usijali Kamanda, kwa kuwa mambo yenyewe
ndiyo yanaanza wakizidiwa watatutafuta”
Madam S alijibu huku akicheka kwa kebehi.
“Nina wasiwasi sana juu ya hili, na usalama wa
yule binti” Amata aliongeza huku akitikisa
kichwa chake na kupepesa macho kuzunguka
ukuta uliopambwa kwa kalenda nzuri na picha
moja kubwa ya Madam S alipokuwa chuoni huko
Canbella. Alipiga picha hiyo na wasichana
wenzake kutoka nchi mbalimbali, Amata
aliiendea na kuitoa pale ukutani
“Kamanda! Nini sasa unatoa picha za watu
ukutani bila kuomba?” Madam S aliongea huku
akinyanyuka na kumfuata Amata.
“Subiri bibi” Amata alipenda kumuita Madam S
bibi, kwa kuwa umri wake ulikuwa umekwenda
sana lakini bidii yake kazini iliishawishi serikali
kumuongezea muda kabla ya kustahafu.
“Hii picha imekaa vibaya au wewe hujagundua?”
Amata alimwambia madam S huku akikimbili
upande wa pili wa ofisi hiyo kubwa, kitu kidogo
mfano wa kifungo kikaanguka kutoka katika
picha hiyo, Amata alisimama na kukiangali
kidubwasha hiko, Madam S alikitazama na
kushika kichwa, akakiokota, kilikuwa ni kinasa
sauti, kifaa kilichona sauti na kupeleka sehemu
Fulani wasiyoijua, Madam S alirudi na kuketi
katika kiti chake akitazamana na Amata, hakuna
aliyemsemesha mwenzake, Amata akairudisha ile
picha pale ukutani na kumpa madam S kile
kidubwasha. Madam S akakichukua na
kukivunjavunja, kisha akajitupia kwenye kiti
chake, akamwangalia Amata na kumuona kuwa
ni mtu wa ajabu sana, alijiuliza kidubwasha hiko
kimekaa pale kwa muda gani, hakupata jibu,
kama waliweka ili kupata siri za ofisi je; hapo
alichanganyikiwa kabisa.
“Umejuaje kuwa hiyo picha ilikaa vibaya” Madam
S alimtupia swali Amata
“Nilipokuja wiki ikiyopita hii picha haikuwa hivi,
leo nimeona imeyumba kidogo” Amata alijibu
“Jesus!” Madam S alinong’ona, kwa jibu la
Amata aligundua kuwa kidubwasha hiko
kilipachikwa karibu wiki moja nzima hapo
ukutani.
“Haya! Nambie kilichokuleta, nilishakwambia
usije hapa bila kuniambia” Madam S alimueleza
Amata kwa utani wa mtu na mtoto wake
“Mama nina njaa nimekuja unipe lunch” Amata
alijibu kwa kudeka
“Gina yuko wapi?” Madam S alimuuliza Amata
“Nimempa kazi moja hivi ofisini, kuna mzigo wa
kuufaulisha kutoka bandari kavu ndiyo
anatengeneza mazingira” Amata alijibu.
Baada ya mazungumzo mafupi waliteremka
ngazi na kuliendea gari la Madam S,
walipolikaribia Amata alimshika mkono Madam S
kama ishara ya kutofungua mlango wa gari hiyo.
Walitoka na kuchukua tax mpaka mgahawa wa
Steers na kuketi, juice mbili zikawa mezani na
sambusa kadhaa.
Mara wateja walokuwa hapo walinyanyuka
mmoja mmoja na kuingia ndani ya mgahawa
huo wote walisimama mbele ya luninga kubwa
wakitazama habari fulani, Madam S na Amata
walibaki palepale lakini hawakujua kwa nini watu
wale wamevutiwa na habari hiyo, Amata alitaka
kunyanyuka kuelekea huko ili ajue kilichojiri,
Madam S akamvuta mkono na kumrudisha kitini.
“Tumia akili, sio unakurupuka tu!” alimwambia
Amata ambaye wakati huo alikuwa akitoa
kicheko cha kitoto. Madam S alitoa simu yake
kubwa mkobani na kuiwasha simu ile ilikuwa na
uwezo wa kukamata matangazo ya televisheni
ya kidigitali bila chenga, akabofya vitufe fulani
fulani kisha akatulia kuangalia
“What!? Jesus!!” Madam S alipata mshtuko na
kumpa simu ile Amata, wote walihamanika na
taarifa ile
“IGP?! Ameuawa!!” walijikuta wote wakinyanyuka
kwa pamoja na kuacha juice zao, lakini baada ya
hatua mbili tatu, Amata akarudi mezani na
kupiga tarumbeta juice zote mbili na kisha
kuondoka eneo lile.
***
Mwili wa IGP, Bw Makabayo, mkuu wa jeshi la
polisi Tanzania ulikuwa umelala juu ya machela,
ukiwa umefunikwa na kitambaa cheupe mpaka
kifuani na kuruhusu sehemu ya juu kuonekana.
Madam S, akiwa anafuta machozi alishikwa bega
na Kamanda Amata na kumuegemeza kwake
akimbembeleza. Viongozi mbali mbali walifika
mchana huo katika chumba cha kuhifadhia maiti
cha hospitali ya rufaa ya Muhimbili kushuhudia
walichokisikia, hawakuamini lakini ukweli ulikuwa
ndiyo huo.
HALI ILIVYOKUWA
IGP alikuwa katika safari ya kikazi akitoka
makao makuu ya jeshi la polisi, jingo la wizara
ya mambo ya ndani na kuelekea Lumo Kigilagila
kufungua kituo kidogo cha polisi katika mtaa
huo, msafara wake ulikuwa na gari mbili tu,
mbele ilitangulia golf na yeye mwenyewe alikuwa
katika Toyota Prado iliyokuja nyuma, walipoiacha
barabra ya Nyerere na kuingia barabara ya Jet,
kwa mwendo wa kawaida walivipita viwanda
eneo hilo kuuzunguka uwanja wa ndege, wakiwa
katika kona ya mwisho walipishana na gari
nyingine ailiyokuwa ikiyumba njia nzima kiasi
kwamba ilibidi gari zingine zisimame. Msafara
wa IGP haukusimama bali ulipikwa upande wa
kulia hapondipo iliposhuhudiwa kioo cha Prado
kikitawanyika nakumwagika kama chumvi, gari
iliacha njia na kuingia kwenye mtaro wa maji
uliojengwa pembeni mwa barabara hiyo. Polisi
waliokuwa kwenye golf walishuka haraka na
bunduki mkononi walipofika hapo tayari walikuta
IGP hana uhai tena, bila kuchelewa waliwabeba
katika golf na kurudi mjini.
Watu watatu waliokuwa katika Land Rover 110
waliifanya kazi yao kwa umakini na kasi kama
walivyoelekezwa, kwa kutumia bastola maalum
ya kizamani PSS silent pistol , bastola ya kirussia
iliyotengenezwa 1983, inaonekana mtumiaji
alifuzu mafunzo maalum ya kuitumia bastola
hiyo inayofanya kazi yake kwa ukimya wa hali ya
juu.
***Nani kamuua IGP? kwa nini...?
 
ISABEL - MPANGO HASI

seaso 2 -MPANGO HASI
ilipoishia ...
Jeshi la polisi linahaha kutafuta sababu au
chanzo cha kifo cha IGP.
kamanda Amata katakiwa kutojihusisha na
sakata hili la ISABEL.
Isabel bado hajazinduka hospitalini.
Unafikiri ni nini kitatokea hapo?
Je ni nini hatima ya Mpango Hasi?
endelea .....
***
H akuna aliyeamini kilichotokea kila mmoja
alijiuliza kwa nini IGP Makabayo kukumbwa na
umauti katika jinsi ile, kama ilivyo ada kwa jeshi
la polisi, mara moja walianza kufanya uchunguzi
wa tukio lile, walifuatilia nyendo za gari lile
ambalo si mpita njia wala aliye dukani aliiona
namba yake kwa jinsi lilivyokuwa mwendo wa
kasi, walijaribu kulifukuzia lakini walichoambulia
ni kulikuta Tazara karibu na kampuni ya Azam
likiwa limeegeshwa pembeni na hakuna mtu
ndani yake. Baada ya kufanya yote ambayo
kanuni zao zinawataka walilivuta na kulipeleka
kituo cha polisi kati na msako wa kuwasaka
wauaji ulianza.
Walijaribu kuangalia gari ile ni mali ya nani
baada ya kuwasiliana na wakala husika wa
magari hayo CMC, jibu walilolipata liliwaridhisha
kidogo, lilikuwa ni mali ya mburushi mmoja
aliyekuwa akiishi huko Mbalali kwenye
mashamba ya mpunga, lakini jambo moja
likawachanganya, katika kadi kivuli ya gari hiyo
kulikuwa na jina la mtu mwingine kabisa,
walipowasiliana na TRA wakapata jibu kuwa hilo
gari lilishauzwa na mmiliki alishabadilishwa
katika kadi, kadi ilionesha gari ni ya Bw.
Costantino Chawala. Baada ya kuchunguza kwa
kina hata huyo Costantino Chawala alishafariki
siku nyingi nyuma.
6
Bujumbura – Burundi
Kikao cha watu wachache kilifanyika katika
moja ya vyumba maalum ndani ya mgahawa wa
Amahoro (Amahoro Cafe), uliopo katikati ya
viunga vya jiji la Bujumbura. Maelewano
yalikuwa tete. Msemaji mkuu wa kikao hicho,
Madam Rose alionekana wazi kukasirishwa na
yaliyotokea katika mission yao hiyo, Mpango
Hasi.
“Kweli kabisa, niliwaamini sana lakini inaonekana
mna uzembe wa hali ya juu sana” Madam Rose
aliongea kwa hasira huku akipigapiga meza yake,
akawatazama vijana wale waliokaa viti vya
mbele tu ya meza yake, “Hamjui kazi? Au
uzembe tu?” aliwatupia maswali ya haraka
haraka. Wote walionekana kushindwa maswali
hayo machache lakini yenye fedheha.
“Jomse!” Madam aliita “Hata wewe
ninayekuamini na kukuweka mstari wa mbele, leo
umeniangusha namna hii!”
“Hapana Madam Rose” Jomse alisema
“Hapana nini; wakati hali yenyewe
inajidhihirisha?” Madam Rose aliendelea kuongea
kwa hasira. Ukumbi wote ulikuwa kimya kabisa,
hamna aliyethubutu kufungua kinywa chake
maana walijua moto utakaomuwakia kutoka kwa
Madam Rose.
“Tupo hapa, hata hatujui Mandi yuko wapi, kama
kakamatwa; na kupata mateso si atatoa siri
yote! Hilo la kwanza, la pili, Memory Card,
wanaume wapumbavu nyie” Madam Rose
aliongea huku akitembea kutoka kona moja
kwenda nyingine “Mmepoteza siri yote, eti
msichana! Msichana mdogo, anawashinda piga
risasi moja ya kichwa mengine yatafuata”
alinyamaza kidogo na kuinua bilauri yake iliyojaa
maji na kuoiga mafunda kadhaa kisha akaitua
mezani. Frank Sabatie akamwangalia mwanamke
yule jasiri mwenye maamuzi yasiyopingwa jinsi
alivyotingwa kwa mawazo na hofu, mwanamke
mwanajeshi aliyekuwa kiongozi wa battalion
moja ya katika vita vya msituni, alivuta faili lake
na kulifungua kurasa kadhaa.
“Ok! Madama tulia kitini,” alimweleza Madama
Rose ambaye alionekana kutokujua nini
champasa kutenda katika hili.
“Tuna wasiwasi kuwa siri yetu imeshavuja katika
serikali ya Tanzania” Frank alizungumza kwa
upole huku akiwa kaikutanisha mikono yake
pamoja na kuiegemeza juu ya meza hiyo “ Tuko
matatani, Watanzania hawana mchezo hata siku
moja, kila raia anailinda nchi yake, kutokana na
hili kutukia tunapaswa kutumia nguvu
kurekebisha makosa.” Jomse na Tonton
walikuwa wameketi kimya wakiwasikiliza mabosi
wao, hakuna aliyeongea lolote.
“Sasa hivi, plan B, maandalizi ya mpango hasi
yameshaanza matekelezo, kwa kuwa ninyi
mlivyoleta uzembe tuliunda kikosi kazi kingine
cha watu wanne kutoka nchi za Magharibi, kazi
ya kwanza tayari imekamilika siku nne zilizopita,
na ya pili si muda mrefu itakuwa tayari. Sasa
ninyi tunawageuzia kibao, lazima muende
Tanzania mkahakikishe yule msichana anauawa
kabla hajatamka chochote, fanyeni kila hila,
sistoshe hakikisheni mnarudi hapa na ile memory
card hapa” Frank aliongea kwa msisitizo swala
hilo. Tonton na Jomse walibaki kumwangalia tu
wakisubiri amri kutoka kwa wakuu hao, wakuu
wa kikosi kazi.
Kila mtu alikuwa kachanganyikiwa kwa jinsi
yake, Madam Rose alitakiwa kupeleka taarifa ya
mission yote baada ya siku chache kwenye kikao
cha ma top, huko Geneva alishindwa afanyeje
baada ya vijana hao kuvuruga katika utendaji,
missing in action!.
***
J omse aliishusha sigara yake kutoka kinywani
na kuikandamiza katika kidubwasha maalumu
kwa kazi hiyo kilichowekwa mezani hapo,
akachukua bilauri yake iliyojaa pombe aina ya
Primus na kujimiminia tumboni kabla hajashusha
bilauri ile kwa nguvu hata kupasua kitako chake
na kufuatiwa na sonyo kali ambalo lilimfanya
kila mtu kati mgahawa huo kugeuka.
Alinyanyuka na kuchukua suitcase yake, kisha
taratibu aliivuta kuelekea barabarani ambako
alichukua tax na kupotelea mjini.
Dakika kadhaa, Jomse alikuwa ameingia katika
uwanja wa ndege wa kimataifa Bujumbura, tayari
kwa safari yake ya kuelekea kunako bandari
salama ‘Dar es salaam’ . Safari hii walijua kabisa
kuwa wanaweza kushtukiwa hivyo Frank
aliwapanga kuondoka kila mmoja kwa staili yake
na kuingia Dar es salaam kwa staili yake ili
wasijulikane. Walishapewa tahadhari kuwa
makini na makachero wa Tanzania na
Watanzania wenyewe ‘trust no one’ , mara kwa
mara sentensi hii ilijirudia kinywani mwa Jomse.
Jomse alikuwa na uchungu uliochanganyika na
hasira hasa kwa kulaumiwa na Madam Rose juu
ya makosa waliyoyafanya, lakini kilichomuumiza
kichwa zaidi ni kuhusu Mandi na Isabel, hakujua
kabisa kuwa swahiba wao Mandi alikwishakuwa
marehemu.
Akiwa ameketi sawia na kujifunga mkanda katika
ndege hiyo ya shirika la ndege la Afrika ya Kusini
‘SA Airline’ , alikuwa akijisomea gazeti lililopo
kwenye kijimeza kidogo karibu yake, ‘Tanzania’s
Inspector General of Police died on car
accident’ , habari iliyokuwa juu katika kurasa ya
habari za kimataifa, Jomse aliisoma kwa umakini
mkubwa sana na akaelewa kuwa kazi imeanza.
***
‘Valley View Hotel, chumba namba 47’ , Tonton
aliikunja karatasi ile mara baada ya kuisoma,
kisha kuitia mfukoni. Aliishusa miwani yake
myeusi na kuifuta vumbi kidogo, kisha
akairudisha tena usoni pake. Mtu mmoja alipita
nyuma yake na kumpiga kibega kisha kumuomba
samahani kwa tukio lile, Tonton alinyanyua
briefcase yake na kuelekea kule alikoelekea yule
kijana.
“Kila kitu kipo katika mstari” Kijana mmoja
alimueleza Ton wakiwa ndani ya Tax, Ton
hakujibu kitu alinyamaza tu.
Tax ailifika mitaa ya Jangwani, Ton alilipia Tax
hiyo na kuisogelea hotel iliyokuwa akitazamana
nayo, juu ya mlango kenye canopy kulikuwa na
maandishi makubwa yaliyosomaeka Valley View
Hotel, alipiga hatua chache na kuifikia meza ya
mapokezi.
****Haya Jomse na Ton mchezon tena kumsaka
Isabel \na kuipata hiyo memory card, je unafikiri
kazi itawezekana au?
tiririka na riwaya hii ya kusisimua mpaka ujue
hatima yake.
 
ilipoishia...
***Mandi amekufa pindi alipojirusha katika
treni.
***Jomse na Ton wamerudi Burundi, madam
Rose anawatupia lawama kwa kushindwa
kutekeleza kazi yao kwa uzembe.
***Swala hilo linawafanya kuumia sana hasa
kudharauliwa kama watoto
***Mpango hasi umeanza cheche zake, IGP
amekwishauawa, Jomse na Ton wanatumwa
Tanzania kutekeleza azma ya mpango hasi,
lakini pia kuhakikisha wanampata Isabel ili
asitoe ukweli wa mpango huo. Je watafanikiwa
kuipata ile memory card?
endelea na riwaya hii...
Akiwa ameketi sawia na kujifunga mkanda katika
ndege hiyo ya shirika la ndege la Afrika ya Kusini
‘SA Airline’ , alikuwa akijisomea gazeti la Daily
Mail alilolikuta kwenye kijimeza kidogo karibu
yake, ‘Tanzania’s Inspector General of Police
died on car accident’ , habari iliyokuwa juu katika
kurasa ya habari za kimataifa, Jomse aliisoma
kwa umakini mkubwa sana na akaelewa kuwa
kazi imeanza.
Masaa sita baadae
Dar es salaam
‘Valley View Hotel, chumba namba 47’ , Tonton
aliikunja karatasi ile mara baada ya kuisoma,
kisha kuitia mfukoni. Aliishusa miwani yake
myeusi na kuifuta vumbi kidogo, kisha
akairudisha tena usoni pake. Mtu mmoja alipita
nyuma yake na kumpiga kibega kisha kumuomba
samahani kwa tukio lile, Tonton alinyanyua
briefcase yake na kuelekea kule alikoelekea yule
kijana. Ilikuwa ni trick ya utambulisho kati yao.
“Kila kitu kipo katika mstari” Kijana mmoja
alimueleza Ton wakiwa ndani ya Tax, Ton
hakujibu kitu alinyamaza tu.
Tax ailifika mitaa ya Jangwani, Ton alilipia Tax
hiyo na kuisogelea hotel iliyokuwa akitazamana
nayo, juu ya lango kuu kwenye canopy kulikuwa
na maandishi makubwa yaliyosomaeka Valley
View Hotel, alipiga hatua chache na kuifikia
meza ya mapokezi.
“Tonton, bila shaka!” mdada wa mapokezi
alimwambia Ton. Ton alitikisa kichwa kuonesha
ishara ya kukubali. Alipewa funguo zake, na
msaidizi akamsaidia suitcase yake kuelekea
chumbani. Ton aliweka vitu vyake sawa
chumbani humo, akajimwagia maji na kujilaza
akisubiri muda ufike ili awasiliane na swahiba
wake tayri kuanza kazi waliyotumwa.
***
Polisi katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere walikuwa makini kuchunguza kila
ashukae na kuingia nchini, ukaguzi wa kina
ulifanyika hasa baada ya kupata tetesi ya
mpango hasi uliopangwa na vikundi vya waasi
kutoka nchi jirani. Waliamuriwa kumkamata
yeyote atakayedhaniwa ili kumhoji kwa kina,
haikuwa kazi rahisi maana watu wengi kutoka
nchi mbalimbali walifikia uwanja huo.
Majira ya saa kumi na moja na nusu jioni ndege
ya shirika la ndege la Tanzania iliikanyaga ardhi
yake ya Dar es salaam na kujiegesha sawia
kabisa katika ngazi za kuteremkia abiria. Watu
walianza kuteremka mmoja baada ya mwingine,
vyombo vya usalama vilikuwa makini kuangalia
wote washukao katika ndege hiyo. Dakika
chache walikuwa wamekwisha na ndipo
aliposhuka mkuu wa upelelezi wa makosa ya
jinai DCI Salila, akiwa na katibu wake pamoja na
watu watatu waliomsindikiza, waliteremka ngazi
za ndege hiyo kwa umakini, alipoikanyaga ardhi
tu kitu kisichotegemewa kilitokea, DCI Salila
alionekana kujishika kifua kwa mikono yake
miwili na kuanguka chini, wasaidizi wake
walimuwahi kumdaka lakini walichelewa.
Walipomuinua tayari alikuwa marehemu Salila,
risasi iliyopita upande wa kushoto wa kifua
chake iliutoa uhai wake kwa wepesi sana. Damu
ilichafua suti yake hasa upande wa pili ilipotokea
risasi hiyo. Gari ya wagonjwa iliingia haraka
uwanjani hapo na kutoa huduma iliyostahili.
Tafrani kubwa ilizuka uwanjani hapo, polisi
walitanda haraka eneo la uwanja wa ndege
kuhakikisha wanamtia nguvuni aliyetenda hayo.
Lakini uwingi wa watu haikuwa rahisi
kufanikisha hilo.
Joseph Msengiyumva au ‘Jomse’ kwa jina la
kificho, akiwa ndani ya mavazi ya shirika la
Dahaco alisitazama tukio zima baada ya
kuanguka kwa DCI Salila, huku bastola yake
maalum ya kijasusi akiwa ameifutika vizuri
uvunguni mwa gari maalumu ya kuvutia ngazi
ambazo hutumika kwa kushukia abiria katika
ndege kubwa kama ile, bastola tulivu isiyotoa
kelele, ndogo inayotosha kukaa kwenye kiganja
cha mkono. Hakuna aliyemdhania, kama ni yeye
aliyetekeleza mauaji yale. Alisimama mara moja
kutoka pale alipojifanya anaangalia kitu Fulani
kwenye gurudumu ya gari hiyo na kwa muda
huo ndipo alipotekeleza kazi hiyo kwa ufundi wa
hali ya juu kabisa. Alitoka pale alipo na kusogea
jirani na tukio kwa ajili ya kutoa msaada.
“Kijana, tunaomba msaada wa haraka.”
Wasaidizi wa Salila waliomba msaada kutoka
kwa vijana wa Dahaco akiwemo Jomse, baada
ya kumaliza kutoa msaada huo na kuhakikisha
kuwa mtu yule tayari ni marehemu alirudi na
kuchukua kale kagari akaondoka na kuelekea
upande wa pili, balaa!
***
Inspekta Simbeye alijikuna kichwa chake kana
kwamba kulikuwa na chawa anayemsumbua.
Lakini la, ni katika kuchanganyikiwa tu na
mambo yanayomzunguka katika siku hizo.
Taarifa juu ya kifo cha DCI Salila, kilizidi
kumzeesha kitini hapo, alijikuta akiongea
mwenyewe ofisini huku kaishika bastola yake
akiitazama tazama. Hakujua hasa ni kitu gani
anataka kufanya. Wakati bado machungu ya kifo
cha IGP Makabayo hayajafutika katika mioyo ya
watu, sasa wanapokea kifo kingine cha mtu wa
juu katika medani ya usalama hapa nchini.
‘Lazima kuna mchezo unaofanyika’ alijiwazia
huku akiwa kasimama dirishani na kuangalia nje,
kijasho chembamba kilimvuja makwapani na
kumfanya kutota kiasi Fulani.
Aliinua simu iliyopo mezani hapo na kuzungusha
namba fulanifulani kisha kuweka sikioni
kidubwasha hiko cha kusikilizia.
“Nini kinaendelea hapo?” aliuliza
“hatujafanikiwa kumkamata muuaji, lakini watu
kadhaa tunao kwa mahojiano” sauti ya upande
wa pili ilijibu.
“Muwe makini na kazi yenu, msipoangalia huyo
muuaji atawatoroka na nyi mkiwa hapo hapo”
Simbeye alitoa maagizo.
“Sawa mkuu, tumekupata” ilijibu sauti ya upande
wa pili.
Inspekta Simbeye alishusha pumzi na kutoka nje
ya ofisi yake, shughuli za watu ziliendelea kama
kawaida kana kwamba hakuna lolote lililotokea
la kuhatarisha amani ya nchi. Akiwa na karatasi
mkononi lililomtaka kwa muda mfupi awe
amefika katika makao makuu ya polisi pale jingo
la wizara ya mambo ya ndani, Simbeye alijikuta
anzidi kupata wakati mgumu, ukizingatia
dhamana ya ulinzi wa mji huu ipo mikononi
mwake. Alirudi ofini na baada yta muda mfupi
alielekea kuitikia wito.
7
Isabel aliamka kutoka katika usingizi mzito
uliojalizwa ndoto mbaya na nzuri. Macho yake
yalijaribu kupambana na nuru ya taa kubwa
nyeupe iliyokuwa kiwaka juu tu ya uso wake,
alifumbafumba macho na kujaribu kujikinga kwa
mikono yake.
Muuguzi wa zamu alifika moja kwa moja na
kufungua pazia lile la plastiki na kuingia ndani,
kwanza alizimisha lile taa na kumuacha kwa
muda. Baada ya dakika kadhaa alimsaidia kukaa
vizuri, Isabel alikuwa akijishika ubavuni mwake
mara kwa mara kutokana na mvunjiko wa mbavu
zake kadhaa. Alijaribu kujinyanyua lakini ilikuwa
ni ngumu sana kwake.
“Endelea kupumzika Isabel” muuguzi alimueleza
kwa sauti ya upole kabisa.
“Samahani, nesi, nipo wapi?” Isabel aliuliza kwa
tabu kidogo
“Hapa ni Hospitali ya Muhimbili” Nesi alimjibu
“Muhimbili! Nimefikaje hapa na lini?” Isabel
alizidi kuchanganyikiwa na kumtupia maswali
muuguzi yule.
“Uliletwa hapa wiki mbili zilizopita, ulipata
matatizo ulipokuwa safarini kwa treni” Muuguzi
alijibu huku akiwa ameketi katika kitanda kilekile
alicholalia Isabel. Isabel aliposikia juu ya treni
picha ilirudi na kumbukumbu zikaanza kujirejesha
ubongoni taratibu.
“Mandi!” alianza kujisemea taratibu huku
aking’ata kidole kimoja cha mkono wake. Mara
nyingi alitamka jina hilo ‘Mandi’ .
“Njaa!” alimwambia Muuguzi. Mara tu uji
uliletwa na akaanza kuubugia kwa fujo sana.
Baada ya kuufakamia uji ule kwa fujo, hali yake
ya tumbo haikuwa nzuri alisikia kichefuchefu cha
hali ya juu, aliomba msaada ka muuguzi na moja
kwa moja aliongozwa maliwato.
Kitu kidogo cheusi kilionekana katika matapishi
ya Isabel, alikitazama kwa makini hakujua mara
moja ni kitu gani, baada ya kuvuta kumbukumbu
ndipo akakumbuka ile memory card aliyoimeza
kule kwenye treni ‘Nilijua washaichukua!’
aliipekua na kuisafisha bombani kisha
akaihifadhi vizuri.
Kamanda Amata aliingia katika wodi aliyolazwa
Isabel kwa kificho, kwa kuwa alishaambiwa
asijihusishe na lolote katika sakata hilo;
awaachie polisi, lakini alijiapiza moyoni kuwa ni
lazima ahakikishe anapata maelezo yote kutoka
kwa Isabel kabla hajayatoa kwa mtu mwingine.
Mara ya mwisho kuja hapo alimuaomba muuguzi
kuwa endapo Isabel ataamka tu basi amjulishe
mara moja kabla ya mtu mwingine, na ndivyo
ilivyokuwa. Akiwa ndani ya kanzu na
barakhashea, miguuni kajitupia makubanzi
aliingia bila tabu katika wodi hiyo akiwapita
polisi waliopo zamu, maana kila aliyeingia katika
wodi hiyo ilipaswa kufanyiwa upekuzi wa kina.
“Dakika tano tu tafadhali” WP aliyekuwa jirani ya
kitanda cha Isabel alimueleza Amata, ambaye
aliingia hapo kama mmoja wa ndugu. Alisimama
kando ya kitanda na kumtazama Isabel, Isabel
alimtazama Amata lakini hakumtambua kabisa
ukizingatia hawajawahi kuonana hata siku moja,
walibaki wakitazamana, Amata alitabasamu,
hakuweza kuongea chochote kwani yule WP
alikuwa pale, na Amata hakupenda mtu yeyote
ajue juu ya mazungumzo yao.
“Hujambo Isabel?” alimsabahi huku akimuinamia
pale kitandani
“Sijambo, shikamoo,”
“Marhaba, wajisikiaje sasa?”
“Mungu anasaidia nimeamka. Mbona mi
sikufahamu, we ni nani?”
“Huwezi kufahamu wote wanaokuja kukuona. Ila
mi ni mgeni uliyemtegemea sana kuonana nae
japokuwa humjui hata kwa sura” Amata
alimueleza Isabel, lakini ilikuwa ngumu kwake
kujitambulisha kwa uwazi kwa kuwa yule WP
angeweza kusikia kwa ukaribu na picha
ingeungua. Lakini Amata alipenda kusikia juu ya
tukio lile kutoka kwa Isabel, hakujua mbinu gani
atumie katika kulifanikisha, aliumiza kichwa kwa
kuwa alijua wazi kuwa asipopata habari hiyo
muda huo basi polisi wakija wataondoka na
Isabel ili akapate hifadhi na kwa mahojiano.
Mungu si Athumani, yule WP alinyanyuka na
kuelekea ofisini kwa wauguzi, ni muda huo mfupi
ulitosha kwa Amata kutekeleza azma yake.
Aliingiza mkono ndani ya kanzu yake na kutoa
kitambulisho kidogo ambacho daima huwa
hakioneshi hovyo kutokana na unyeti wa kazi
yake, akanong’ona.
“Mimi Amata, nilitaka kuongea na wewe lakini
naona haiwezekani. Nitashindwa kukusaidia
Isabel” alirudisha kile kitambulisho mahali pake
kwa haraka. Isabel alishasoma kwa haraka na
kuwa na uhakika juu ya mtu huyo. Isabel
alitikisa kichwa kuashiria kuwa alimuamini.
“Niitie nesi tafadhali!” Isabel alimuomba Amata,
na Amata akafanya hivyo haraka, nesi alifika
pale pamoja na yule WP.
“Nini Isabel?” nesi aliuliza
“Najisikia kutapika.”
Yule nesi alimshika mkono Isabel na
kumsindikiza maliwato, kwa kuwa Isabel alikuwa
hana nguvu za kutosha kutembea mwenyewe,
WP alikuwa nyuma yao kuhakikisha usalama wa
binti huyo.
Baada ya muda kidogo alikuwa akirudishwa
kitandani na kabla hajakifikia kitandani
alisimama na kujishikia kwenye nguzo iliyo
katikati ya wodi hiyo, akihema kwa shida huku
kajishika mbavu zake.
“Kaka, tunaomba utusaidie kidogo” WP alimwita
Amata kutoa msaada wa kumfikisha Isabel
kitandani. Amata alinyanyuka na kwenda kutoa
msaada, alitaka amnyanyue Isabel, lakini Isabel
alikataa akampa mkono amshike, na hapo ndipo
Amata alipogundua hila ya Isabel. Kamanda
Amata alihisi kama kitu kidogo kigumu
kikikandamiza kiganja chake kutoka kile cha
Isabel, alimsaidia Isabel kutembea mpaka
kitandani na ye kubakia na kile kitu mkononi
mwake.
Akiwa kitandani Isabel, alimwangalia kijana huyu
na kutoa tabasamu pana.
“Naomba nipumzike, sitaki kuongea na mtu”
Isabel alimueleza nesi, na Amata aliombwa
kutoka nje ya wodi ile maalum.
Kwa hatua za haraka haraka Amata aliiendea
gari yake Toyota Altezza na kujitoma
ndani. Memory card ndogo ilikuwa kiganjani
mwake, aliitazama na kuigeuzageuza kisha
akaihifadhi vizuri katika wallet yake, na
kuondoka kuelekea nyumbani kwake moja
kwa moja, ili kwanza akajue nini kilichoma
ndani ya card ile.
***Memory card imetuwa mikononi mwa
Kamanda Amata...
***DCI Salila ameuawa, je kifo hicho ni moja
ya matekelezo ya mpango hasi?
usikose kusoma chapisho lijalo ili kujua hasa
nini kilichopo katika mpango huo...
 
Hadithi ni nzuri ....ila ongeza font size kidogo kama mkuu Casuist.
 
Asante sana kidi kudi kwa episode hizi. Waiting for the next episodes.
 
Last edited by a moderator:
ISABEL- ndani ya MPANGO HASI

ilipoishia...
Yule nesi alimshika mkono Isabel na
kumsindikiza maliwato, kwa kuwa Isabel alikuwa
hana nguvu za kutosha kutembea mwenyewe,
WP alikuwa nyuma yao kuhakikisha usalama wa
binti huyo.
Baada ya muda kidogo alikuwa akirudishwa
kitandani na kabla hajakifikia kitandani
alisimama na kujishikia kwenye nguzo iliyo
katikati ya wodi hiyo, akihema kwa shida huku
kajishika mbavu zake.
“Kaka, tunaomba utusaidie kidogo” WP alimwita
Amata kutoa msaada wa kumfikisha Isabel
kitandani. Amata alinyanyuka na kwenda kutoa
msaada, alitaka amnyanyue Isabel, lakini Isabel
alikataa akampa mkono amshike, na hapo ndipo
Amata alipogundua hila ya Isabel. Kamanda
Amata alihisi kama kitu kidogo kigumu
kikikandamiza kiganja chake kutoka kile cha
Isabel, alimsaidia Isabel kutembea mpaka
kitandani na ye kubakia na kile kitu mkononi
mwake.
Akiwa kitandani Isabel, alimwangalia kijana huyu
na kutoa tabasamu pana.
“Naomba nipumzike, sitaki kuongea na mtu”
Isabel alimueleza muuguzi, na Amata aliombwa
kutoka nje ya wodi ile maalum.
Kwa hatua za haraka haraka Amata aliiendea
gari yake Toyota Altezza na kujitoma
ndani. Memory card ndogo ilikuwa kiganjani
mwake, aliitazama na kuigeuzageuza kisha
akaihifadhi vizuri katika wallet yake, na
kuondoka kuelekea nyumbani kwake moja
kwa moja, ili kwanza akajue nini kilichomo
ndani ya card ile.
Endelea....
mpango hasi hadharani
***
Ton aliketi kwenye moja ya viti vilivyopo
chumbani kwake, akisubiri maelekezo mengine
kutoka kwa asiyemjua. Mara kwa mara
aliangalia saa yake na kuona muda ulivyokuwa
ukikimbia alinyanyuka na kuangalia dirishani
lakini hakuna aliyemuona kuja wala kumjua
aliketi na kuwasha televisheni ndogo chumbani
hapo. Mara simu iliita aliinyakuwa na kubofya
kidude cha kusikilizia.
“Halo” aliita
“Ok nakuja” aliijibu hiyo sauti ya upande wa pili,
akaliendea kabati na kufungua, aktupa jicho lake
hapa na pale na kuivuta bastola yake
anayoiamini aina ya Winchester 73, akaitia kotini
na kufunga mlango nyuma yake, alishuka
taratibu ngazi za jingo hilo na kutokea
barabarani moja kwa moja akaiende marcedec
benz nyeusi iliyokuwa imesimama eneo hilo.
Ton alikutana na watu wawili asiyowajua garini
mle aliwaangalia kwa hadhari kubwa, aliyekuwa
nyuma ya usukani akageuka.
“Ton Ton, kutana na meno ya Mamba”
alimueleza Ton huku akimuoneshea kijana
mwingine aliyeketi kushoto kwake “ na
Anaconda” alimalizia kwa kumuonesha mtu wa
kiti cha nyuma. Ton alitikisa kichwa kuonesha
amekubaliana nao, akawapa mikono.
“Swahiba huyu ni Ton, mtakuwa naye katika ile
opereshen, mnatakiwa muifanye kwa umakini na
haraka iwezekanavyo,mambo mawili tu
apatikane mzima au ikishindikana auawe”
alimaliza kauli yake na kuondoa gari, Ton aliitoa
bastola yake na kuiweka tayari kwa kazi na
wenzake walifanya vivyo hivyo. Gari ile kwa
mwendo wa kawaida ilipita mtaa wa Swahili na
kuelekea taa za faya kabla ya kupita njia panda
hiyo kuchukua barabara ya Umoja wa mataifa
mpaka Muhimbili.
“Yupo wodi maalum, ndani ya chumba hicho ni
yeye, muuguzi na msaidizi mmoja,” sauti
nyembamba ya kike ilisikika katika kidubwasha
maalum ndani ya gari hiyo, ikatulia kidogo kisha
ikaendelea “nje mlangoni kuna polisi wawili
wenye bunduki, muwe makini sana wasilete
matatizo, muda mzuri ni jioni ya saa moja mimi
nitakuwa nimetoka zamu ataingia mwingine”
kisha sauti ile ilikatika.
“Mmesikia vijana?” yule dereva aliwauliza, wote
wakaitikia kwa vichwa kukubali. Yule dereva
aliinua mkono wake kuangalia saa ilikuwa saa
kumi na mbili jioni, walipopaki gari katika
maegesho ya wageni, Ton na wale wawili
wakashuka na ile gari ikaondoka.
“Mmoja ataingia kwa muuguzi kwanza wakati
wawili watasubiri nje, kisha ataingia mtekaji
baadaye wa mwisho atakuwa makinina askari,
tutatofautisha dakika mbili kwa mtu wa kwanza
na wa pili, halafu sekunde thelathini kwa mtu wa
pili na wa tatu” Ton alitoa maelekezo kwa
wenzake na kuonekana wako pamoja kisha
wakatawanyika na kukubaliana kuanza kazi
baada ya kupeana signal Fulani.
***
“Surprise!” Amata alimwambia Madam S
“Surprise ya nini?” madam S alimjibu huku
akifunga faili alilokuwa akilipitia.
“Nilishakwambia Kamanda, ukiwa unakuja ofisini
kwangu uwe unanipa taarifa” Madam S
alimueleza Amata huku akimnyooshea Amata
kalamu aliyoishika mkononi.
“Hapana, nimekuja tu kwa dharula, lakini kuna
jambo zito sana nataka tuliongee, tukichelewa
itakuwa balaa” Amata alimueleza madam S huku
akivuta kiti na kuketi, kisha akaendelea “Kuna
mpango mchafu, mpango hasi, kutoka nchi jirani
kwa ajili yetu”, Madam S aliduwaa kumsikiliza
Amata.
“Unasema nini kamanda!?” aliuliza kwa
mshangao
“Watu wanataka kufanya mapinduzi, kama
ilivyotokea huko nchi za jirani mwaka 1994 ndiyo
mpango uliopo unaosukwa na haohao kwa ajili
ya Tanzania” Amata alinyamaza na kumwangalia
Madam S usoni.
“Mh! Mbona unanitisha na hizo habari, we
umepata wapi?” madam S alimtupia swali
Amata.
“Isabel” alimjibu
“Isabel?” madam S aliuliza kwa sauti
“Ndiyo, Isabel kanipa taarifa hii” Madam S
aliposikia taarifa hiyo alinyanyuka kitini na
kuiacha meza yake kisha akampa ishara Amata
ya kumfuata. Walitoka nje na kuingia kwenye
gari na kuondoka eneo hilo. Breki ilikuwa katika
uwanja wa shule ya msingi ya jirani, wakashuka.
“Umenileta huku kufanya nini?” Amata alimuuliza
Madam S
“nataka kukunulia karanga za kukaanga,
hupendi?” alimjibu na kumuuliza.
“Ha ha ha ha!” Amata alicheka kwa jibu hilo.
Wakiwa wamesimama katikati ya uwanja wa
shule kamanda Amata na Madam S
waliabadilishana mawazo.
“Nafikiri hapa ni sehemu salama zaidi kwa
maongezi” Madam S alimueleza Amata
“Ndiyo.”
“Ok, niambiye hiyo habari na mpango wenyewe
ulivyo”
“Kuna kikundi cha watu wachache wanaoongoza
mapinduzi katika Africa, na nchi zinazoendelea,
na ndiyo hao waliotekeleza mapinduzi na mauaji
ya kimbali katika Rwanda na Burundi, sasa
wamesuka mpango huohuo kwa ajili ya
Tanzania” alijikohoza kidogo na kuendelea “Sasa
kabla ya kutekeleza mpango huo kuna mambo ya
kuandaa mazingira, Madam hivi tunavyoongea
kuna watu wameshaingia nchini na si mmoja ni
kikundi kutekeleza kazi hiyo”.
“Amata!” madam S aliita, akamshika bega
Amata, “Isabel, anahusika.”
“Hapana, sina uhakika kama anahusika.” Amata
alimjibu Madam S
“Yeye amejuaje yote haya? Hata akueleze wewe,
na wewe mmeongea saa ngapi? Maana
ulishaambiwa usijiingize katika sakata la Isabel”
“Swali zuri Madam, nilikwenda kumtembelea jana
jioni…”
“Hawakukuona?” madam S alimkatisha
“Hakuna aliyeniona, nilikwenda kikazi” Amata
alijibu, madam S akacheka kidogo
“Mbona unacheka?” Amata alimuuliza
“Umenikumbusha siku ulipojifanya wewe ni padri
ukavaa kanzu na stola tulipokuwa Nairobi
kwenye lile sakata la ‘mauaji ya kasisi’ ” Amata
alirudisha kicheko.
“Nakusikiliza” Madam S akaendelea
“Sasa nilipokuwa pale nilimuonesha kitambulisho
changu Isabel, akanifahamu na akafanya ujanja
Fulani akanipatia memory card bila mtu kujua,
ndani ya memory card hiyo ndiyo kuna huo
mpango wa mapinduzi, Mpango Hasi wameuita
hivyo”, Amata akashusha pumzi kidogo na
kuendelea, “Madam utakelezaji wake umeanza,
kaa tayari, kifo kinachokuja ni cha kwako baada
ya kile cha IGP na DCI”, alimaliza. Madam S
alibaki mdomo wazi.
“Amata, una hiyo memory hapo?”
“Yes, Madam” Amata akatoa kijifuko kidogo cha
plastiki na kumkabidhi Madam S.
“Twende” madam alimuamuru Amata na wote
wakarudi garini. Ndani ya gari madam S
alifungua kijikompyuta kidogo kilichotengenezwa
maalum katika dashboard ya gari hiyo,
akatumbukiza memory ile na ikaanza kusoma.
Baada ya kumaliza kuisoma, Madam S alishusha
pumzi nzito na kujiweka vizuri kitini, hakuamini
anachokisoma mbele yake, machozi machanga
yalianza kumtoka, kwa kitambaa chake akajifuta
machozi.
“Madam,” kamanda Amata aliita
“Kamanda” Madam aliitikia, akatikisa kichwa na
kuendelea “Asante Kamanda, kwa kunijulisha kifo
changu, tatizo sijui watanitafutia wapi, na sijui
adui yangu ni nani. Ningekufa kama kuku
mwenye kideli, lakini sasa nitakufa kishujaa, ama
zao ama zangu” Madam alimaliza kusema kwa
masikitiko, akaitoa memory ile na kuirudisha
katika kile kiplastiki.
“Isabel, akachukuliwe jioni hii awekwe hospitali
ya jeshi kwa mahojiano” Madam alimwambia
Amata, “Na hapo yeye atatueleza kila kitu, kisha
tutajua tunaanzia wapi. Sasa twende kwa waziri
mwenye dhamana”, alimalizia. Kamanda Amata
alikaa nyuma ya usukani wa gari ya Madam S,
alipotaka kuwasha gari ile, Madam S akamshika
mkono Amata.
“Nakupenda Amata, nakupenda sana”
“Oya, pancha hiyo!” kijana wa pembeni
barabarani hapo aliwatahadharisha kwa ukulele.
Amata na Madam S walishuka na kuangalia
kweli tairi lilikuwa flat , wakatafuta uwezekano
wa kulirekebisha ili waendelee na safari. Vijana
walichangamkia tenda haraka haraka, lo.
Mlipuko mkubwa ulitokea, gari ya Madam S
ilipaishwa juu huku ikiwaka moto, hali ilikuwa ya
taharuki eneo lote hilo, watu walikimbia huku na
huku vilio vilisikika kila kona. Madam S
alichanganyikiwa, alitaka kukimbilia kwenye gari
lakini Amata alimshika na kumzuia alimvuta
pembeni palipokuwa na tax na kumuingiza katika
moja ya tax hizo.
“Shit!” madam S alitamka kwa hasira, “Walitaka
wanimalize namna hii, saa ngapi wameweka
bomu kwenye gari yangu, saa ngapi? Nani
kafanya hivi, ntamtia mkononi tu.” Madam S
alishikwa na hasira kali iliyoshindwa kujificha,
Amata alijaribu kumpoza kidogo.
“Madam, tulia Madam, tuendelee na ratiba yetu
kama ilivyo maada m tumepona maana kwenye
orodha si umeona hata mimi nipo, wangefurahi
kutumaliza pamoja” Amata alizungumza hayo
huku akitoka na Madam S. Moja kwa moja safari
iliishia kwa katika ofisi ya waziri wa ulinzi na
jeshi la kujenga taifa. Madam S alioneka
kuchanganyikiwa kabisa.
“Vipi mbona ghafla hivyo?” aliuliza Mheshimiwa.
“Tumenusurika kifo mheshimiwa,” Amata
alimueleza waziri wa ulinzi kila kitu kama
kilivyokuwa.
“Hali imekuwa mbaya, tukicheza tutakufa wote
huku tunajiona. Hatua za haraka inabidi
zichukuliwe, na hii memory ifike kwa
Mheshimiwa Rais haraka iwezekanavyo, hakuna
jinsi.”
Waziri wa ulinzi aliitisha kikao cha dharula ofisini
kwake cha wakuu waote wa vyombi vya ulinzi na
usalama mchana huo. Punde tu wote walifika,
Amata aliondoka kupisha kikao hicho na kurejea
ofisini kwake ambako alimkuta Gina anasoma
gazeti la alasiri ya siku hiyo. Amata aliingia na
kuketi juu ya kiti chake, akamtazama Gina na
kutikisa kichwa.
“Tungekuwa tumekufa mimi na Madam S leo”
“Kwa nini?” Gina aliuliza huku akimpa juice
kwenye bilauri. Amata alimueleza Gina tukio hilo,
Gina alionekana na kuchoka kwa habari hiyo.
“Gina, sina la kufanya hapa lazima niingie kazini
bila ruhusa” Amata alimueleza Gina huku akivuta
kitabu chake cha kumbukumbu na kupekua
kurasa kadhaa, na kuandika vitu Fulani.
“Gina, nashindwa nianzie wapi, naomba hata
wewe uwe makini na usitembee kizembe kama
kawaida yako, hakikisha muda wote unakuwa na
mawasiliano na mimi ili kujua nilipo na ulipo,
kimenuka mama” alipokuwa kimaliza maneno
hayo, saa yake ilimfinya mkono kuashiri kuna
ujumbe uliokuwa ukiingia, aliinua mkono na
kubonyeza namba Fulani mara mkanda maalum
ukawa unatoka ndani ya saa hiyo ukiwa na
maadishi ‘tukutane shamba haraka
iwezekanavyo mama anataka msaada Tena Sana
Aisee’ mkanda ule uliishia hapo na kukatika,
Amata alijiweka tayari.
“Gina natoka, signal yetu iwe ileile, sawa?”
“Yes Sir!” Gina alijibu kwa utani kama kawaida
yake. Amata alitoka na kuelekea shamba…
*** Haya kimenuka, Madam S na Kamanda
Amata wanusurika kifo,
***Nini hatima ya Isabel?
 
Dah had simanzi maskin isabel sijui atapona kweli😕
 
ISABEL

ndani ya mpango hasi
ilipoishia...
“Tungekuwa tumekufa mimi na Madam S leo”
“Kwa nini?” Gina aliuliza huku akimpa juice
kwenye bilauri. Amata alimueleza Gina tukio hilo,
Gina alionekana kuchoka kwa habari hiyo.
“Gina, sina la kufanya hapa lazima niingie kazini
bila ruhusa” Amata alimueleza Gina huku akivuta
kitabu chake cha kumbukumbu na kupekua
kurasa kadhaa, na kuandika vitu Fulani.
“Gina, nashindwa nianzie wapi, naomba hata
wewe uwe makini na usitembee kizembe kama
kawaida yako, hakikisha muda wote unakuwa na
mawasiliano na mimi ili kujua nilipo na ulipo,
kimenuka mama” alipokuwa akimaliza maneno
hayo, saa yake ilimfinya mkono kuashiri kuna
ujumbe uliokuwa ukiingia, aliinua mkono na
kubonyeza namba Fulani mara mkanda maalum
ukawa unatoka ndani ya saa hiyo ukiwa na
maadishi ‘tukutane shamba haraka
iwezekanavyo mama anataka msaada Tena Sana
Aisee’ mkanda ule uliishia hapo na kukatika,
Amata alijiweka tayari.
“Gina natoka, signal yetu iwe ileile, sawa?”
“Yes Sir!” Gina alijibu kwa utani kama
kawaida yake. Amata alitoka na kuelekea
shamba.
endelea...
***
Gari ya wagonjwa ya Jeshi kutoka hospitali ya
Lugalo ilifunga breki mbele ya wodi ya mifupa
(MOI), vijana wawili waliovalia kombati za jeshi
na msichana mmoja waliteremka na kuielekea
wodi hiyo, jambo la kushtua! Polisi aliyekuwa
lindo alionekana kwenye kiti chake akiwa hana
uhai, yule kijana wa jeshi alimtazama yule polisi
mwenye bunduki mkononi, kisha akapitiliza ndani
akifuatiwa na mwenzake walipoingia ndani
walimkuta muuguzi akiwa chali juu ya meza
yake, tundu la risasi lilionekana wazi kifuani
mwake. Chumba hakikuwa na mtu,
walitazamana hawakujua la kufanya walitoka
ndani ya chumba hicho kwa kasi na kuripoti
haraka kambini, Isabel ametekwa.
Haraka gari za polisi zilifika eneo hilo lakini
habari hazikubadilika, Isabel alikuwa ametekwa.
Inspekta Simbeye alijishika kiuno, hakujua nini la
kufanya, aliusogelea ule mwili wa yule askari na
kuuangalia kwa makini, kisha akaingia ndani
ambako vijana wake walikuwa wakifanya mambo
mbalimbali ya kiusalama.
“Ina maana we hukuona yeyote aliyekuja?”
Inspekta Simbeye alimuuliza daktari wa zamu
jioni hiyo.
“Hapana, mi nimetoka hapa niliacha kila kitu
sawa. Nashangaa hawa jamaa wameingia saa
ngapi”
“Uhhhhhh” Inspekta Simbeye alishusha pumzi,
kisha akausogelea mwili wa yule muuguzi,
ilionekana wazi kuwa hata tukio lenyewe bado ni
bichi kwa kuwa jeraha lile la risasi lilikuwa bado
linavuja damu taratibu. Kazi ilikamilika na miili
yote ilihifadhiwa katika chumba cha kuifadhia
maiti.
Inspekta Simbeye alikuwa kwenye lindi la
mawazo ‘Isabel anaweza kufanya hili?’ alijiuliza
sana kwa kuwa aliamini kuwa ulinzi aliouweka
wodini hapo ulikuwa makini lakini nini kimejiri
katika utekaji huo, lilikuwa swali gumu sana.
Simbeye aliuangalia ule mlango mkubwa wa
wodi hiyo, bado alikuwa haamini kilichotokea,
mbele yake aliiona kazi jinsi itavyomuia ngumu,
aliingia kwenye land cruiser ya Polisi na
kuondoka.
***
Kamanda Amata aliketi juu ya kochi kubwa na
upande wa pili kulikuwa na Madam S, pamoja
nao kulikuwa na watu wengine wawili.
“Kamanda, mi nakwambia kwenye hili sakata
Isabel lazima anahusika” Madam S alimsisitizia
Amata juu ya uhusika wake katika mpango hasi,.
“Hapana Madam, mi nafikiri ngoja aondolewe
pale kisha tutaenda kuongea nae vizuri”
“Ok! Kamanda…” Madam S alikatishwa na mlio
wa simu, akainua mkono wake na kuelekeza
sikioni.
“Yes, nakusikia…” Madam S alijibishana na sauti
ya upande wa pili
“Eee? What?” aliuliza kana kwamba kuna kitu
ambacho hajakielewa katika simu hiyo. Alishusha
mkono wa simu taratibu na kuupachika kwenye
kikalio chake, kisha akainua bilauri ya maji na
kujimiminia kinywani, alikunywa kama mtu
aliyekuwa na kiu ya jangwani, kisha macho yake
mawili yaliyofunikwa kwa miwani yalitua kwa
wale vijana wawili na kisha kwa Amata, akatikisa
kichwa kuonesha masikitiko yake.
“Isabel” alitamka.
“Isabel? Kafanya nini?” Amata aliuliza
“Isabel katoroka, na isitoshe ameuwa muuguzi
na askari wa mlangoni”.
Amata alishtushwa na habari hiyo ambayo
kwake ilikuwa ngeni sana na ya kutoaminiwa,
alisimama kitini na kuliendea dirisha kubwa
lililopo hapo, uso wake ulianza kushikwa na
taswira ya gadhabu, ‘Madam yuko sahihi,
inaonekana Isabel ni mmoja wao’, kamanda
Amata aligeuka na kumtazama Madam.
“Lazima apatikane” Kamanda alijikuta akitamka
maneno hayo bila mwenyewe kujua.
“Kamanda, kazi imerudi mikononi mwetu kwa
ushirikiano na jeshi la polisi, ila wao watafuata
maelekezo kutoka kwetu, kazi njema vijana”
Madam S alimaliza na kuelekea kwenye vyumba
vya kulala.
Kamanda Amata alitoka katika jumba lile kubwa
‘shamba’ akaingia kwenye gari yake na
kutokomea.
Tairi zake zilisimama moja kwa moja katika wodi
ya mifupa, kwa mwendo wa haraka alizivuta
hatua zake na kuingia kwenye lango kuu kisha
moja kwa moja akingia kwenye kijivhumba cha
wauguzi akawakuta watatu wameketi hapo.
“Habari zenu wadada? Mimi ni afisa usalama”
Amata alijitambulisha moja kwa moja bila
kujizungusha, “poleni kwa msiba. Lakini naomba
mnisaidie kitu kimoja ili kukabiliana na jambo
hili”
“Karibu sana” mmoja wa wauguzi hao
alimkaribisha
“Ningependa kuona daftari la zamu zenu, hasa
wale waliokuwa wanamhudumia Isabel”
Bila kusita muuguzi yule alivuta daftari kubwa na
kuliweka mezani, Amata aliangalia orodha ya
majina yale na akalifikia jina la muuguzi
aliyebadilishana zamu na marehemu ‘ Suzan
Crispin’ , alifunga lile daftari na kuwarudishia
“Asanteni warembo” alijibu
“Kaka tutoe hata soda basi” mmoja wa wauguzi
alitamka
Amata alitoa wallet yake na kutoa noti ya ya sh
elfu kumi nma kuwapatia, kisha akaondoka zake.
8
Madam S, alibaki akihangaika mawazoni mwake,
moyo wake ulijawa hasira, kila mara aliapa
kumsaka aliyeweka bomu kwenye gari yake,
lakini alimshukuru Mungu kwa kuwa amemuokoa
katika hilo. Alitafakari kwa muda mrefu akipanga
na kupangua lakini picha haikuja sawa sawa.
Polepole alianza kupata hisia na kujua wapi ni pa
kuanzia kazi, akiwa katika mawazo hayo
alipitiwa na usingizi.
Asubuhi ya siku iliyofuata
Madam S, aliliendea geti kubwa la gereji hiyo,
akasukuma kijimlango kidogo, hakikuleta matata
akaingia na moja kwa moja akafika ofisini.
“samahani kuna kijana mmoja, jana asubuhi
alinitengenezea gari yangu, nina shida nae, ile
gari imekorofisha nataka akaiangalie” madam
Limueleza fundi mkuu
“Unamjua kwa jina?”
“Hapana ila nikimuona nitamjua kwa sura”
Madam S pamoja na yule fundi walitoka na
kuingia eneo la kazi, haikuchukua muda
alimtambua kijana yule, baada ya mazungumzo
yote waliondoka pamoja. Madam S alipita
taratibu eneo la uwanja wa Taifa.
“Unaijua ile gari iliyochakaa pale?” alimuuliza
“Hapana, ntaijuaje gari iliyoungua vile?”
“Ok, umejibu vizuri. Gari yangu jana imelipuliwa
kwa bomu kama umesikia kwenye redio au TV”,
Madam akameza mate na kuendelea “Sasa nina
wasiwasi mkubwa wewe ndiye uliyefanya kazi
hii, ya kuweka bomu na kutaka kuniua siyo?”
Yule kijana akaonekana kuchanganyikiwa, alikaa
kimya kwa muda bila kujibu chochote.
“Usiponipa ushirikiano, utalala pabaya leo”
“Mama, utanionea tu, labda gari imelipuka
kutokana na mfumo wa umeme”
“Hapana, mimi najua aina za milipuko, lile ni
bomu” Madam S alitulia kisha akaendelea “Najua
si wewe, ila nambie nani unamuhisi”
Yule kijana alibaki kimya moyo ulimuenda mbio
hakujua nini cha kufanya katika hali hiyo.
Alijaribu kuvuta kumbukumbu ya siku ile ili
angalau ajue ni nani labda alifanya hivyo, ‘Bro
Jose’ , alijiwazia mwenyewe.
“Nafikiri nimekumbuka kitu mama, kama ni yeye
kuna bro mmoja tunamwita Bro Jose , mara
nyingi huwa anakuja pale gereji”
Madam S akatikisa kichwa kuashiria kuwa
amekubaliana na kijana huyo.
“Ok, uliona anafanya nini?”
“Alikuja pale, akawa anaisifia gari yako, mi
nikiwa narekebisa tairi, ye akawa mara anaingia
ndani ya gari mara anaagalia engine ”
“Ok, zaidi ya hapo, hamna kingine?”
“Hapana”
“Sawa, sasa nitampataje huyo Jose?”
“Huyu Bro Jose ni ndugu na mwenye gereji yule
uliyekwenda ofisini kwake”
Madam S, aligeuza gari na kurudi mjini, kisha
alichukua simu yake ya upepo na kuongea na
watu Fulani, alisimama mahali na mara land
cruise yenye vioo vyeusi ilikaribiana nao, vijana
wawili walishuka na kumchukua fundi gereji
kutoka katika gari ya Madam S na kumuingiza
kwenye ile Cruiser
“Sikia, sikufanyii hivi kwa nia mbaya ila utajua
baadae, utaenda kupumzika sehemu mpaka
nitakavyokuachia” Madam S alimueleza yule
kijana, na baada ya hayo “Panda kwenye gari”
alimuamuru kupanda kwenye ile cruiser, akiwa
ndani wale vijana walimvalisha kofia kubwa ya
sox ambayo ilimfunika uso wote , na hakuona
chochote kilichoendelea zaidi ya kupitiwa na
usingizi mzito.
***
“Umejiingiza kwenye jambo lisilokuhusu
msichana!” Jomse alimueleza Isabel ambaye
alikuwa hoi kwa kipigo kutoka kwa jamaa huyo.
“Hata mkiniua, nina uhakika hamtafanikiwa,
taarifa tayari zipo kwenye vyombo vya usalama
na nijivunia kwa kufanya hilo, heri mimi nife
lakini niwaokoe maelfu wanaotarajiwa kufa hapo
mbeleni” Isabel alizungumza kwa sauti ya
kwikwi huku damu zikimtoka mdomoni, mguu
wake uliokuwa umeanza kupona sasa
ulitoneshwa tena kiasi kwamba hata hakuweza
kusimama. Jomse alichukizwa na jibu la Isabel,
alimpiga mateke mengi na mikanda ya kijeshi
mpaka Isabel akapoteza fahamu kwa mara
nyingine.
“Jomse, acha hasira utamuua bure tu huyu na
haitatusaidia lolote” Tonton alimwambia Jomse.
“Na we usiwe kama Mandi, badala ya kufanya
kazi uliyotumwa unaanzisha mambo mengine,
hata nikimuuua huyu mimi napata faida gani, afe
tu tutatupa maiti yake porini iliwe na mbwa”
Jomse aliongea kwa hasira huku akirusha
mikono yake hewani na kuondoka hapo
“Muacheni afe apo hapo” aliwaeleza wengine na
wote wakaondoka katika chumba hicho na
kumuacha Isabel peke yake akiwa hana fahamu.
“Ok! Tuzungumze yajayo, kazi karibu inakamilika
plan A, japo kuwa jana tumemkosa yule bibi
kizee (Madam S), kweli ni tukio baya kwa
upande wetu. Tunapofanya kosa moja
tunajiharibia wenyewe” Jomse aliwaambia vijana
wake akiwemo Tonton, akawatupia macho
mmoja mmoja kisha akaendelea “Jamaa wapo
tayari mipakani, wanasubiri tukamilishe plan A, ili
wao wamalize plan B, lakini kumkosa yule bibi
jana, naomba muwe makini sana” Jomse
alimaliza na kujimiminia wine yake kinywani.
Kabla hajasusha bilauri yake simu iliita mfukoni,
akaitoa na kuiweka sikioni,
“Yeah man” aliitikia
“Eh! Unasema?(...), kama atarudi ni wa
kumpoteza tu. We njoo huku watarudi hao”
Jomse akashusha simu yake.
“Jamaa wamemkusanya dogo kule gereji” taarifa
hiyo iliwashtua wote, kila mtu alionekana
kuchanganyikiwa na hilo.
“Du! Eee sasa hapo patamu, tukamilishe mpango
huu haraka iwezekanavyo” Ton alitoa rai.
Walivunja kikao na kurudi kule walikomuacha
Isabel, wakamkuta bado amezirai, Jomse
akachuku maji ya baridi kwenye ndoo na
kummwagia.
“Amka mpumbavu wewe, na wewe lazima
ukutane na Madam Rose akutie adabu” Jomse
alifoka na kumuacha Isabel akijivutavuta pale
chini.
Ton alikuwa kimya sana, fikra zake zilimfanya
akose raha kabisa, aliingia kwenye gari yake
tayari kuondoka
“Ngoja nikaonane na Suzan nimpe mzigo wake
narudi baadae” Tona alimuaga Jomse
“No. Ton usiende peke yako, uko uendeko
hakutabiriki,nenda na Anaconda akulinde” Jomse
alitoa amri na ikafuatwa.
Punde si punde walifika katika hotel ya Valley
View, Anaconda akasuka kwanza na kuangali uku
na huko kisha akagonga kioo cha dirisha la
nyuma kuashiria kitu, Ton akashuka na moja
kwa moja akongoza kuelekea hotelini na
Anaconda akamfuata nyuma yake.
Tax nyeupe ilisimama nyuma kidogo ya gari ya
akina Ton, mwanadada mrefu kiasi, mwenye
mwili wa kawaida, aliteremka na baada ya
kuiweka miwani yake vizuri, alivuta hatua
taratibu kuielekea hoteli hiyo, alichukua lifti
kupanda ghorofa ya nne kisha akaelekea chumba
namba saba akagonga mlango kwa staili
aliyoelekezwa, na mlango ukafunguliwa.
“Karibu Suzan” Anaconda Limkaribisha
“Upo peke yako?” Ton alidakia kwa swali
Suzan alisita kidogo kujibu “Ee nipo peke yangu”
“Ok haina haja kuchelewa, tunashukuru kwa kazi
uliyotufanyia. Na ujira wako huu hapa dola za
kimarekani elf moja” Ton alipomaliza kuongea
hayo alimkabidhi kitita hiko Suzan, nae
akakisunda katika mkoba wake. Suzan
hakuamini kabisa anachokishuhudia, pesa zote
hizo kwa kazi ndogo, kazi ya kumsaliti Isabel.
“Ok. Mi naomba niende” Suzan aliaga na
kusimama tayari kuondoka
“Ok Suzan, be carefull ” Ton alijibu na kumruhusu
Suzan kuondoka.
Suzan aliiendea tax iliyomleta na kuingia mlango
wa nyuma wa gari hiyo.
“Ingia! Ukileta fujo nakumaliza” Suzan
alitazamana na domo la bastola kutoka kwa
Gina, Gina hakuonesha uso wa masihara hata
kidogo
“Ingia” alirudia tena na Suzana akaingia ndani,
Gina alichukua mkoba wa Suzana huku mkono
mmoja ukiwa bado umeshikilia bastola ile,
aliupekua na kutoa na alipoiona simu yake
aliichukua kwa kutumia kitambaa maalum kisha
akaitia kwenye mkoba wake. Suzan akatiwa
pingu mikononi.
“Haya endesha gari”
“Tunaelekea wapi?”
“Central police ”
Dreva aliondoa gari na kuelekea alikoagizwa.
Walipofika central Suzan alishushwa na Gina
akafuata nyuma yake.
“Hifadhi huyu, naomba asihojiwe lolote mpaka
mpatapo amri nyingine” Gina aliwakabidhi Suzan
polisi waliopo kaunta na kisha yeye akaongoza
kuelekea ofisi ya Inspekta Simbeye.
“Kazi uliyonituma imekamilika afande” Gina
aliongea kwa ukakamavu mbele ya bosi wake
“Vizuri sana afande, waweza kwenda
nitawasiliana na wewe nitakapokuhitaji” Inspekta
Simbeye alimueleza Gina, Gina akaonesha
ukakamavu wake kwa kubana mikono yake
miwili kuonesha heshima, kisha akageuka na
kuondoka.


***Haya kazi imeanza.... mpango hasi
matatani...
****Nini hatima ya Isabel?
 
Leo mapumziko kama vipi shusha hii hadi mwisho mana imeanza kitambo
 
Kidi kudi shusha vitu basi kama ni hii au uchu angalau tujiliwaze na hii mana hela zishatutoka watoto wamekwenda shule
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom