RIWAYA: Isabel ndani ya mpango hasi

RIWAYA: Isabel ndani ya mpango hasi

punguza kukosea maneno ndugu,unaharibu radha ya hadithi yenyewe,kuna sehemu umeandika "****" badala ya "kuna" uwe unakagua kabla ya kuituma kwetu
 
punguza kukosea maneno ndugu,unaharibu radha ya hadithi yenyewe,kuna sehemu umeandika "****" badala ya "kuna" uwe unakagua kabla ya kuituma kwetu

Amekusikia na amekusoma. Maana hata mimi kwa kukosea kwangu ID yako nikadhani imeandikwa porno.
 
ISABEL...
episode 6
ilipoishia...
“Freeze!” akiwa kamnyoshea SMG Ton, Jomse
alifyatua bastola yake Koplo Kibona alipaishwa
na kujigonga juu kabla ya kudondoka chini
akiwa mfu… kimenuka.
Hali ya hewa ika wa mbaya, polisi walirusha
risasi kuwashambulia Jomse na Ton lakini kazi
haikuwa rahisi kwani vijana hawa walikuwa
wana mafunzo maalum ya kijeshi, walitoweka
eneo hilo na kukimbilia kwenye mabehewa ya
watu wengine, polisi nao wakaliunga uko huko.
Endelea...
A mata Ga Imba, Tanzania Secret Agency
namba 1, alisikia kila kitu kilichoendele kwenye
treni ile kupitia simu ya Isabel. Alitamani muda
huo ajikute ndani ya treni hiyo baada ya kusikia
kilio cha uchungu cha Isabel kupitia simu ile,
afanyeje? Alinyanyu simu yake haraka na
kumpigia nkuu wake wa kazi
“Hello” Amata aliita
“Hello mbona usiku sana kuna nini wakati mimi
nimekwambia upumzike, Kamanda Amata”
Madam Suzan au kama wenyewe wanavyomwita
‘S’ aliinuka nakuketi kujibu simu hiyo
“Dharula, miss S, kuna habari nimepata sasa,
kwenye treni ya Kigoma Dar kuna mauaji
yanaendelea na huyu mtu kawasiliana na mimi
moja kwa moja, msaada wako” Amata alisubiri
jibu lakini akaona ukimya umetawala. Simu
ikakatika, Amata alikunja uso wa lawama kwa
mkuu wake wa kazi. Simu ya Amata iliita tena
“Kamanda Amata samahani nilimpigia RPC wa
Tabora na IGP kuhusu hilo nimepata taarifa,
kutokana na uzito wa shughuli yenyewe
nakuteua uende sasa hivi, helkopta ya polisi
inakusubiri airport.” Amata hakusubiri simu ya S
iendelee. Alikurupuka kitandani na kufungua
kabati lake akachukua bastola yake moja na
vikasha vya risasi kadhaa akatupia kenye kibegi
chake, akavaa jeans lake jeusi, fulana nyeusi,
boot ya kazi akapachika kisu chake kiunoni …
kamili! Alivaa kofia lake la puendeshea pikipiki.
Muda mchache alikuwa barabara ya Kawawa
akielekea Magomeni, usiku huo hakukuwa na
magari, ilimchukua muda wa dakika kumi tu
kuwasili uwanja wa ndege terminal one, alikuta
tayari rubani na msaidizi wamewasha injini
tayari kuondoka.
“Kamanda… twende!” rubani wa Helkopta
alimwita Amata na bila kuchelewa Amata
alijirusha ndani safari ikaanza.
Wakiwa hewani Kamanda Amata alijilaza kwenye
kijitanda cha kamba akitafakari hili na lile
akijiuliza imekuwa Isabel atumbukie katika tatizo
kama hilo alijipa moyo kuwa akifika atajua kila
kitu, moyoni alimsifu sana Isabel kwa kutumia
akili siyo tu ya kuzaliwa lakini naya shule pia.
Lakini mara nyingine alijiona mjinga sana akaona
ingekuwaje kama amewekewa mtego kwa mtindo
huo na ye kanasa kijinga namna hiyo, alijicheka
na kujiona kweli yeye mjinga, lakini bado
alijiuliza kwa nini usiku ule aliendelea kubaki
akicheza na mtandao labda Mungu ana alikuwa
na mpango wake katika hili.
“Kamanda, tukushushe Tabora stesheni au kituo
cha polisi kati Tabora, maana tumeambiwa
tukusikilize wewe” rubani wa helkopta
alimweleza Amata
“Itafute treni yenyewe, nataka kushuka kwenye
treni” Amata aliwajibu
Helkopta la polisi lilikata anga, kwa kuwa rubani
alikuwa analiongoza kuelekea katika makao
makuu ya polisi ya mkoa Tabora, ilibaidi abadili
uelekeo na kuitafuta treni ile ilipo kwa wakati
huo.
“Kpteni Scopa, Chopper namba PLS 12 H ova”
rubani yule aliongea kwenye chombo maalumu
cha kuongelea alichokivaa masikioni mwake
“Tunalipata Kepteni, tupe habari ova” sauti
kutoka makao makuu ilimjibu
“Tunabadili uelekeo, kadiri ya maelekezo ya
Kamanda ova”
“Uelekeo wapi Kepteni?”
“Ameomba tuelekee mahali treni ilipo ili kazi
ianze mara moja ova”
“Read and clear ova”
“Work in progress” mabadilishano ya taarifa hiyo
yalikamilika na kepteni Scopa alimpa ishara
msaidizi wake Baba Lao ageuze uelekeo.
Chopper lilibinuka upande upande kuelekea
magharibi mwa mji wa Tabora ilikuwa yapa saa
saba kasoro usiku giza nene lilikuwa limefunika
anga.
Kamanda Amata alitoa bastola yake ndogo na
kuijaza risasi na magazine iliyobaki aliihifadi
vizuri, aliweka vizuri kisu chake na kuvaa soksi
zake za mikono tayari kwa kazi, aliicheki saa
yake na kuibonyeza kuweka kitu Fulani vizuri,
alivaa kofia yake aina ya nyeusi aina ya mzula
akatia big G yake mdomoni.
Kepteni Scopa na msaidizi wake walikuwa bize
kuliongoza dude hilohuku wakisikiliza muziki wa
Les Wanyika walionekana wakiipenda sana kazi
yao. Kwa mbali walianza kuiona treni ile
ikiendelea kuikata reli kwa kasi ya ajabu ambayo
ilimfanya kepteni Scoba kuhofu,
“Kamanda” aliita
“Hii treni ya umeme au?mbona inakimbia namna
hii?” aliuliza
“**** itilafu kwenye Injini naenda kurekebisha”
Amata alijibu
“All the Best” Scopa alipokea jibu hilo na kutoa
saluti kwa Kamanda Amata
Tayari Chopper ya polisi ilikuwa ikienda
sambamba na treni hiyo
“Weka Chopper juu ya treni” Amata alitoa amri
huku tayari akiwa mlangoni, upepo mkali
ulimsumbua macho. Scopa aliipeleka Chopper ile
juu, na Kamanda Amata alivizia kuona kasi ile ya
treni kama inawiana na Chopper ili aweze
kurukia juu yake.
H ekaheka zilendelea katika stesheni ya treni ya
Tabora, polisi tayari walikuwa pale usiku ule
wakiwa na hasira dhidi ya majambazi hao kwa
kuwaumiza wenzao
“Ama zao ama zetu” walisikika wakitamka neno
hilo mara kwa mara. Stesheni masta alikaa tu
ofisini kwake haelewi kinachoendelea ni jinsi gain
ataikoa treni hiyo ambayo sasa ilikuwa
inakwenda kwa kasi isiyo ya kawaida tena bila
operetta, mara kwa mara alisimama na kukaa
chini, aliweka mikono kichwani na kuitoa kisha
kuiweka mfukoni, mara alikwenda haja ndogo na
kurudi, alishika hiki akashika kile ili mradi tu hali
ilikuwa ni mkanganyiko hasa alipofikiria kuwa
endapo treni hiyo itapata ajali katika mwendo
kama huo ni wangapi watabaki Yatima, wangapi
watabaki Wajane na walemavu ndiyo usipime,
aliteseka sana moyoni na kila alipopiga simu
katika treni hiyo simu haikujibiwa kabisa.
Alitoka nje ya ofisi na kuangalia hekaheka
zilizopo hapo nje, waandishi wa habari
walishafika, vijana wa msalaba mwekundu
walikuwa pale tayari kwa lolote, polisi walitanda
kila kona ya stesheni ile wenye mbwa, farasi,
acha wale wenye bunduki za aina mbalimbali.
Stesheni masta Bw Nimrod Msigwa alivuta hatua
ndogondogo kushuka ngazi za jingo lile la
stesheni huku akionekana wazi hajui ni wapi
anaenda.
Punde tu RPC wa mkoa wa Tabora aliingia eneo
hilo naye kushuhudia kinachotokea baada ya
kupata simu toka makao makuu ya Polisi huko
Dar es salaam. Alikutana na stesheni masta Bw
Nimrod na kusabahiana lakini wote walionekana
wakiwa na mawazo mengi walisimama pamoja
kimya wakiangalia hekaheka za hapa na pale
hakuna aliyemsemesha mwenzie. Mafundi nao
walijaribu kurekebisha reli huku wakiimba nyimbo
zao.
“Samahani, Bw Nimrod, kwa uzoefu wako
unafikiri treni hii itafika hapa saa ngapi?”
kamanda wa Polisi wa mkoa Tabora Bw.
Sylvester Matinde alimtupia swali Bw Nimrod ili
kuvunja ukimya ule
“Kawaida ingeingia hapa saa kumi na moja
alfajiri ndiyo ratiba ykae lakini kwa jinsi ya hali
ilivyo itafika mapema zaidi ila siwezi kujua ni
saa ngapi” alijibu
“Sasa kama watu wa reli mnachukua hatua gain
kuokoa vifo vitarajiwa?”
“Kama unavyoona mafundi wapo kazini,
wanatengeneza njia moja tu ya reli ili kama
ikifika hapa basi inyooshe njia na wao watafanya
utaratibu wa kuipunguza kasi, wenyewe wanajua
kazi yao, usiwaguse” Stesheni masta alimalizia
jibu lake.
Kamanda wa polisi aliendele kuongea machache
na watu wake na kuwapanga hapa na pale mara
nyingi aliwasiliana na vijana wake walioko ndani
ya treni hiyo japo kwa taabu kidogo lakini
waliendelea kuwasiliana.
4
Kigali
Rwanda
S imu ya mezani iliita usiku huo chumbani kwa
Madam Rose, kabla ya kupokea simu hiyo
aliangalia saa yake ya ukutani na kugundua
kuwa ilikuwa tayari ni saa saba za usiku,
alikunja sura kwa kuwa hakupenda kupokea
simu mida hiyo…
“Hello!” aliita kwa mapozi kama kawaida yake
“Madam, we are in trouble!” sauti ya upande wa
pili iliongea kwa kutweta kama mtu
aliyekimbizwa na mbwa wakali.
“What?” Madam Rose aliuliza kwa hasira huku
akitoka kitandani kwake na kusimama dirishani
akiangalia nje
“Vijana tuliyowapa kazi wameharibu kwa uzembe
wao” sauti ile iliendelea
“Khaaaa!” alinguruma Madam Rose na kuendelea
“Imekuwaje?” aliuliza
“Amenipigia simu Mandi kuwa wapo kwenye treni
ya kwenda Dar, lakini ile memory card imepotea
na wamuhisi msichana mmoja kuwa kaichukua,
sasa wameshaingia matatizoni na Polisi.
Tutapona?” sauti ile iliongea kwa kukata tama
“Come on!!! Ni wajinga sana, nimewapa tiketi za
ndege wawahi Dar, sasa wanapoteza muda,
mbona tutaonekana wote hopeless” Madam
aling’aka kwa hasira. Sauti ya upande wa pili
ilitulia bila kusema kitu
“Frank! Frank!” Madam Rose aliita kwa hasira
“Yes Madam, nakusikia” sauti ile ilijibu
“Unashauri nini katika hili?” Madam aliomba
ushauri kwa Frank maana alihisi wazi kuwa
endapo watakamatwa basi halihaitakuwa shwari
hata kidogo maana wanaijua serekali ya
Tanzania jinsi isivyotaka mzaha katika dulu za
usalama.
“Madam hakuna jinsi, inabidi tuwaokoe wenzetu
ili tuuokoe mpango wetu” Frank alijibu sasa kwa
kujiamini
“Ok Frank fanya hivyo halafu tuwasiliane, lakini
hawa jamaa ni wapumbavu kabisa. Na
ukiwaokoa uwalete hapa moja kwa moja”
Madam Rose aliendelea kufoka kwenye simu,
alipomaliza aliitupa simu hiyo na yeye
mwenyewe kujitupa kitandani kwa hasira.
F rank, alipiga simu kwa vijana wake walioko
huko msitu wa Nyakanazi ambao wao wapo
tayari kwa lolote na muda wowote, vijana
waliochoka maisha ambao kwao kuua haikuwa
shida ilikuwa kama chai ya asubuhi tu. Maisha
yao waliyajenga huko Biharamuro katika mapori
ya Nyakanazi kikubwa ni kuteka mabasi na
kupora mali za wasafiri, kila kukicha
walipambana na polisi katika shughuli zao hizo
lakini hawakukoma kabisa. Katika
kimbizanakimbizana hiyo wengine walikimbilia
mbali huko sehemu za Nguruk, Kazolamimba
mpaka Uvinza, kote wakijifanya wababe kupora
mali za wananchi, wengine waliishia jela,
wengine waliuawa kwa risasi za polisi au
wananchi wenye hasira, lakini wengine
walisalimika nakufanya makazi yao katika mapori
hayo, hakuna mtu aliyejua wanasubiri nini siku
zote hiko, hata wao hawakujua wanachokisubiri
ni kipi na kitatokea lini.
Simu ya mmoja wao ilinguruma katika mfuko wa
koti lake
“Nani tena usiku huu anapiga au ndiyo wanga
wenyewe” aliongea maneno hayo kwa sauti ya
kilevi, huku akijipapasa kuitoa mfukoni
“Eee lete maneno mdosi” alimwambia mtu wa
upande wa pili
“Ee nakupata mdosi”(…)“Vijana wapo gado kaka,
hawana kwere”(…)“Niambie kiongozi”(…) “ok
nimekupata, kuwaokoa tu, tunajua kazi yetu
vizuri, hii ndiyo rescue mission… tega sikio
utapata habari” yule kijana alikata simu na
kuwaamsha wenzake.
“Oya Masela, inabidi tufanye rescue, mabradha
wametaitiwa kwenye gogo, sasa tuhakikishe
tunawatoa hai mwana” aliwaeleza wenzake
ambao tayari muda huo walikuwa wameshaanza
kukoroma.
“Donge lipo? Sio tunafanya kazi ya kanisa”
mmoja wao alimuuliza
“Donge lipo we twende kazini” akampajibu.
Vijana wale walinyanyuka na kupotelea msituni,
mara walitoka na jeep ya kijeshi wakiwa na zana
mbali mbali tayari kutekeleza waliloagizwa, bangi
zilikuwa zikifanya kazi muda huo.
Kilometa mia moja na hamsini kabla ya stesheni
ya Tabora vijana wale walianza kufungua vyuma
vya reli ili kuipoteza njia, wao hawakujali kama
wangapi watapoteza maisha ila walichojali wao
ni kuwaokoa watu wao watatu tu waliotumwa.
Kazi iliendelea kwa nguvu zote kulfungua
mataruma hayo.
“Madogo fasta madogo, kaza kaza” kiongozi
wao aliwaelekeza vijana wake. Kisha akachukua
simu yake na kupiga namba ileile
“Ee mdosi, sasa waambie walengwa wasogee
behewa moja kutoka kwenye injini, kwa maana
kwenye ajali yoyote ya treni behewa la pili hua
halianguki, hapo tutawapata na kutokomea nao”
yule kijana alionghea kwenye simu na kutoa
hayo maelekezo. Kazi ilikamilika trauma mbili
moja ya kushoto na nyingine ya kulia
zilishaondolewa, vijana wale walijificha porini
umbali kama wa mita mia tano wakiangalia na
kusubiri kuona kitachotokea.
Gurudumu mia mbili za chuma ziliendelea
kusumbuana na vyuma vigumu vya reli ya
Mjerumani usiku ule, kasi ya treni ile haikuwa ya
kawaida, watu wote walitulia kimya wakiwa
hawajui watafanya nini kila mtu aliomba kwa
Mungu wake aepushe balaa hilo, wakati wengine
wakiwa katika maombi lakini wengine walikuwa
hoi bin taabani, afande Kirama alikuwa
ameshapoteza fahamu muda mrefu, Koplo
Kibona nae alikuwa tayari tayari ameshaitwa
jiona lingine ‘Marehemu’, Mzee kasimu nae
alikwisha iaga dunia baada ya kupigwa vibaya
na Mandi pale alipojifanya kuleta ubishi na mwili
wakati alipokuwa akianguka aliigonga kinobu cha
kuongezea mwendo kasi wa treni hiyo hivyo treni
iliendelea kuongeza kasi bila mpangilio. Kengele
za hatari zilianza kugonga ndani chumba cha
operetta wa treni hiyo, hakuna la kufanya, Polisi
aliyeachwa hapo hakujua chochote cha kufanya
alibaki aking’aa macho tu.
Nani atafaniki azma yake?
maharamia au Polisi?
Kamanda Amata ana plan gani? atafanikiwa
kumuokoa Isabel...
Isabel ... hakuna anayejua hali yake baada ya
kipigo kikali toka kwa Jomse
Endelea kuona simulizi hii...
 
ISABEL... an action story!
by: richard MWAMBE
episode 7
ilipoishia...
Mzee kasimu nae alikwisha iaga dunia baada ya
kupigwa vibaya na Mandi pale alipojifanya kuleta
ubishi na mwili wakati alipokuwa akianguka
aliigonga kinobu cha kuongezea mwendo kasi wa
treni hiyo hivyo treni iliendelea kuongeza kasi
bila mpangilio. Kengele za hatari zilianza
kugonga ndani chumba cha operetta wa treni
hiyo, hakuna la kufanya, Polisi aliyeachwa hapo
hakujua chochote cha kufanya alibaki aking’aa
macho tu.
endelea...
Mandi aliendelea kujibanza palepale katika moja
ya vijichumba vidogo vilivyopo katika injini hiyo,
aliendelea kuangalia nyendo zote za askari yule
hakuna alichokitaka zaidi ya bunduki yake aina
ya SMG. Askari yule alikuwa akitembea hukuna
huku na mara nyingi alikuwa akikaa kwenye kile
kiti kirefu cha operetta akitazama huko treni hiyo
iendako. Mandi alitoka katika maficho yake na
polepole alianza kunyata kumfuata askari yule
pale alipoketi, kwa kuwa viatu vyake vilikuwa na
soli ya mpira hakuweza kusikika katika sakafu ile
ya chuma. Yule askari aliketi vile vile kwa utulivu
akiwa ameshika bunduki yake lakini alishamuona
Mandi kupitia katika kioo cha mbele kilichokuwa
kikiangazwa na mwanga hafifu kutoka katika
moja ya balbu ndogo iliyopo katika kijichumba
fulania katika injini hiyo. Yule askari slijifanya
kama anainzia hivi lakini alokuwa akimwangalia
Mandi kwa kificho, Mandi alipojiandaa kumvamia
akiwa karibu kabisa alijikuta akipigwa kwa kitako
cha bunduki, maumivu yalimfanya mandi
kuyumba na kujishika paji lake la uso ambalo
mpaka hapo lilishavimba kutokana na pigo lile,
yule askari alitoka pale katika kile kiti na kurukia
chini, kabla Mandi hajatulia alipigwa mateke
mawili ya kuzunguka na alipotaka kujiweka sawa
alijikuta akipata ngumi za mfurulizo
zilizompelekea kwenda chini, damu zilimtoka
mdomoni na puani, kwa kasi ya umeme mandi
alijinyanyua kisarakasi na kupiga mapigo ya judo
yaliyompata yule askari kifuani na kumfanya
akohoe kidogo na kutema damu, Mandi alijirusha
kwa ufundi na kuzamilia kuuwa lakini askari yule
aliepa na migugu ya Mandi ikatua katika dash
board ya treni ile mguu mmoja uliinasa kamba
ya bunduki nayo ikaanguka chini, mandi
alipotaka kuichukua yule askari aliipiga teke
ikasogea mbali kidogo, Mandi akatua pale
ilipokuwa ile bunduki, alipofika chini tu yule
askari bila kuchelewa alimpiga teke lililotua usoni
na kumgeuza Mandi kuwa chali, mguu wa pili
wa yule askari haukufanya ajizi ulitua kwenye
koromeo kwa mtindo ‘kutimba’ Ma ndi aliushika
mguu ule na kujaribu kuutoa kutoka katika
koromeo lake, kutokana na misuli yenye nguvu
ya mikono ya Mandi aliweza kuuondoa mguu ule
na kuuzungusha , maumivu makali yalimpata
askari yule akapiga yowe la uchungu na
kudondokea upande wa pili. Mandi alijinyanyu na
kuifuata ile bunduki kabla hajafika alihisi kupigwa
na kitu kama chuma kisogoni, yule askari pale
alipodondokea kulikuwa na kasha la vifaa vya
ufundi ‘tool box’ alichukua spana na kumrushia
Mandi, Mandi aliyumba na kujigonga katika
bomba la chumba lililopo ndani ya cabin hiyo.
***
“Shusha zaidi! Tena, tena, tena. Apo hapo haya
ongeza kasi” Kamanda Amata alikuwa akitoa
maelekezo kwa kepteni Scoba aliyekuwa
akiliongoza chopper lile la kipolisi
“Kisha hakikisha unakuwa mbele ya treni,mbele
sana ili kuangalia usalama wa reli kisha nipe
taarifa” Kamanda Amata alimuelekeza kepteni
Scoba huku akimpa kidude Fulani cha kuongelea
‘walk talk’ na kumpatia nay eye moja akaibana
katika mkanda wake wa begi. Amata alitua vizuri
kabisa juu ya paa la moja ya mabehewa ya treni
hiyo ambayo ilikuwa ikienda kasi sana, alitulia
kidogo kuliacha chopper lile liende, na baada ya
hapo alianza kutembea kwa mtindo wa ‘jogging’
kuelekea kati ya behewa na behewa ili apate
nafasi ya kuingia ndani.
“Tutoke kwa nje tupande juu ya paa ili kama
jamaa wameshahujumu sisi tutapona kwa
kurushwa pembeni” Ton alimwambia Jomse
ambaye alionekana kutokubaliana na hilo.
“Hatuwezi kuondoka mpaka tuhakikishe tumeipa
ile memory card” Jomse alisisitiza
“Tutapata hata hatujui ilipo?” Ton aliuliza
“Anayo yule msichana, tumeshamzimisha twende
tukaubebe mwili tumpekue kwa utulivu” Jomse
alimwambia Ton, lakini Ton alionekana kutoafiki
wazo hilo.
“Mandi, hatuna information yoyote toka kwake”
Ton alimwambia Jomse
“yule nae -----, achana nae kama kakamatwa
atajua yeye” Jomse alijibu kwa mkato
“Sio hivo Jomse we unafikiri akikamatwa na sisi
tutapona? Sote tupo kwenye mission moja
lazima tumtafute, atatoa siri akibanwa na polisi.”
Ton alimueleza Jomse. Jomse aliona kweli
amekosea kutoa jibu lile, akakubaliana na Ton.
Mara simu ya Jomse ilipokea meseji ‘Rescue
mission imekamilika, nendeni behewa la pili
kutoka katika injin haraka’
“Twende” Jomse alimvuta Ton, na wote kwa
mwendo wa kunyata walitoka katika maficho yao
na kuelekea huko walikoagizwa kwa tahadhari
kubwa. Jomse alipendekeza wapite kwa nje, Ton
mara hii akaafiki, kwa kutumia dirisha moja
walifanikiwa kutoka na kupanda juu ya paa
wakiwa na nia ya kutembea juu ya paa mpaka
behewa la pili lakini pia ikiwa ni moja ya
kuwakwepa Polisi ambao bado walikuwa
wakipekua behewa moja baada ya jingine.
Amata ga Imba kwa kutumia upenyo kati ya
behewa la usalama na la abiria aliteremka
taratibu katika maungio hayo na kukanyaga
sawia panapotakiwa, moja kwa moja aliingia
behewa la polisi kwanza
“Simama apo hapo ulipo” Polisi mmoja mwenye
short gun mkononi alimuamuru Amata, bila
kupinga Amata alinyanyua mikono yake juu.
Kutokana na hali iliyogubika katika treni hiyo
Amata alijua wazi akileta mchezo atafyatuliwa
maana polisi walishaona kila mtu sasa ni adui
kwao.
“Samahani nimekuvamia” huku akitoa
kitambulisho ambacho mara nyingihuwa
akioneshi ovyo.
“Samahani Kamanda!” askari yule aliomba
msamaha na kutoa salute ya kiukakamavu.
Amata aliuangalia mwili wa afande Kibona
uliokuwa umelazwa kwenye machela na
kufunikwa kwa shuka maalum kwa kazi hiyo,
kisha akamwangali afande Kirama ambaye
alionekana kupoteza fahamu. Amata alitoa
bastola yake na kuiweka vizuri tayari kwa kazi.
Alianza kupita behewa moja na jingine akiwa na
bastola yake mkononi, mabehewa mawili ya
mwanzo yalikuwa tupu akafika behewa la mizigo
ambalo lilikuwa na giza, amata alitembea kwa
hadhari kubwa sana, taratibu akitazama huku na
huko aliweza kuona vizuri kutokana na mawani
yake aliyovaa ambayo inamuwezesha kuona
gizani. Aliona mtu kalala chini, alipomwangalia
vizuri ni msichana, damu nyingi zikimtoka
mdomoni na puani, uvimbe ulikuwa katika uso
wake, Amata alirudisha bastola yake katika
kikoba chake na kuufikia ule mwili kwa haraka,
pembeni aliona laptop iliyovunjika vipande, simu
iliyokosa betri na mfuniko.
“Isabel…” alijikuta akiita hata kama hakuwa na
uhakika kuwa ni yeye, alichukua begi alilolikuta
hapo na kutia vile vipande vya laptop na ile simu
kisha akjaribu kuangalia hapa na pale katika
begi hilo akakuta kitambulisho alipokisoma ndipo
alipohakikisha kuwa ni yeye. Akamyanyua kutoka
pale chini, haikuwa rahisi kwa maana Isabel
alikuwa kibonge kwelikweli, alipomuweka vizuri
katika mikono yake alitembea mpaka behewa la
usalama na kumuhifadhi vizuri, lile begi nao
aliliweka pazuri, akatoa walk talk yake
“Scoba, Scoba!” aliita
“Yes kamanda, tupo mbele sana hali ni shari
kamanda”
“Geuza chopper uje haraka behewa la usalama”
Amata alimuamuru Scoba
“Nimekusoma Kamanda”. Scoba aligeuza
chopper na kurudi, haikuchukua muda walikuwa
tayari wameifikia treni hiyo. Kupitia dirishani
alimuelekeza Scoba kushusha chopper ile mpaka
mlangoni, kwa kushirikiana na yule askari mmoja
walihamisha mwili wa koplo Kibona kuuweka
katika chopper, kisha afande Kirama na Isabel,
kazi haikuwa rahisi sana kwa kuwa vyombo
vyote vilikuwa katika kasi kubwa lakini kwa
kusaidiana walikamilisha zoezi hilo. Amata
alipiga salute kwa Scoba kuonesha shukrani na
Scoba aliondoa chopper kuwawahisha hospitalini
Tabora.
Amata pamoja na askari aliyebaki walianza
safari ya kwenda behewa na behewa, behewa
nne za mwanzo zilikuwa tupu, kwa sababu Koplo
Kibona marehemu aliwaamuru abiria kukaa
sehemu moja ili kuweza kufanya ukaguzi
kuwapata wauwaji.
Zoezi lilikamilika lakini hakuna aliyeshukiwa
kuwa na hatia hiyo, hata wale waliohisiwa nao
waliachiwa kutokana na kuwa hakukuwa na
ushahidi uliokamilika. Abiri waliruyhusiwa kurudi
mabehewa ya nyuma ili kutoa na nafasi kwa
operesheni hiyo kwenda mabehewa ya mbele.
Jomse na Ton walilala juu ya paa la behewa la
kwanza wakisubiri kitachotokea kama
walivyoamuriwa, walimtumia meseji Mandi ili
kama yupo hai afanye mchakato kama huo.
Mandi alikuwa hoi baada ya kupambana na
polisi yule ambaye sasa aliwekwa chini ya ulinzi
wake.
“Simama juu!” yule askari alimuamuru Mandi
kisha akaendelea
“Ongoza njia twende”
Mandi akiwa mikono kichwani aliongoza njia
kuelekea kwenye mabehewa mengine huku
nyuma yake akifuatiwa na yule askari baada ya
behewa moja kulipita walipofika behewa la pili
mbele yao kulikuwa na askari wawili wakija
upande huo. Mandi aliona sasa amekwisha hana
jinsi iliyobaki ni kujitetea awezavyo, alishusha
mikono na kugeuka kwa kasi, kwa pigo moja tu
alilompa yule askari alifanikiwa kuipata bunduki
ile na kuiweka sawa kwa mashambulizi, kabla
hajafanya lolote aliona kitu kama jinamizi likipita
juu kwa kukanyaga mabega ya askari wale, pigo
moja la usoni lilimpepesua Mandi na bunduki
ikamtoka mikononi, Mandi alijiinua kwa ustadi
na kusimama wima kumkabili Amata ambaye
alikuja hapo kama mzimu, Mandi alipiga kareti
ambazo Amata alizipangua kwa ufundi sana,
Mandi akaona hapa anapambana na mjuzi.
Alipiga pigo lilingine na Anata alimkata vizuri na
kumtwanga kichwa ambacho kilimtonesha ile
nundu yake Mandi alijitoa katika mikono ya
Amata akarusha ngumi ambayo Amata aliiona
na kuikwepa kisha kutumi viganja vya mikono
yake alimsukuma nyuma na kumrukia teke la
kichwani lililompepesua na kumpeleka chini,
alijigonga vibaya kwenye meza iliyopo hapo
“Mkamate tia pingu” Amata aliamuru
Kabla hawajamfikia Mandi alijinyanyua na
kujirusha nje kupitia dirishani, Amata alitikisa
kichwa na wote wakakimbilia dirishani kuangalia.
Mandi alinasa kidogo mguu na hivyo kupoteza
uwelekeo, alijipiga katika ubavu wa behewa na
alipochomoka tayari gurudumu za chuma
zilishadaka mikono kilichofuatia ni kifo kibaya
cha kukanyagwa na treni, mwili wake
ulisambaratika huku na huko.
“Amejichagulia kifo chake, muache aende” Amata
aliwaambia wale polisi.
Amata na wale polisi walifika kwenye injini lakini
hawakuweza kuona cha kufanya, Amata
alipojaribu kuchezea ile nobu ya kupunguza kasi
alikuta imejam haifanya kazi tena.
“Oya, mchuma umekufa huo hauwezi kusimama
wala kupungua kasi, cha kufanya tuokoe ndugu
zetu” Amata aliwaeleza wale polisi,
“Kivipi kamanda?” mmoja wa wale askari aliuliza
“Tutenganishe mabehewa kutoka katika injini”
Amata aliwapa mbinu
Kwa kuwa wao walikuwa behewa la pili kutoka
injini na behewa la kwanza halikuwa na mtu
hivyo wakaanza kusaidiana kutenganisha
behewa la pili kutoka injini, kazi haikuwa rahisi
maana wote hawakujua mabehewa hayo
yaliunganishwa vipi, walijitahidi kufyatua hiki na
kile wakianza na mipira ya upepo na nyanya za
umeme.
“Jamani hivi humu hakuna Tiitii?” Amata aliuliza
“Maana wao wangeweza kutusaidia” Amata
aliongeza kusema. Kazi iliendelea kutenganisha
kiungio kile, jasho liliwatoka wanaume wale lakini
walishindwa, wakiwa wamekaa upande wa
behewa la tatu, Amata alishikwa na hasira na
kukanyaga kwa nguvu chuma kimoja kilichokua
hapo katika maungio, mara aliona behewa lile
likijiachia, cheche za moto kidogo zikatawanyika
huku na huko lakini walishuhudia injini na
behewa moja vikienda peke yake, na mabehewa
yaliyobaki yalifuata kwa kasi ileile, Amata na wa
le polisi walibaki kuangalia nini kitachotokea…
je wataka kujua kilichotokea?
 
ISABEL
episode 8
ilipoishia
Kazi iliendelea kutenganisha kiungio kile, jasho
liliwatoka wanaume wale lakini walishindwa,
wakiwa wamekaa upande wa behewa la tatu,
Amata alishikwa na hasira na kukanyaga kwa
nguvu chuma kimoja kilichokua hapo katika
maungio, mara aliona behewa lile likijiachia,
cheche za moto kidogo zikatawanyika huku na
huko lakini walishuhudia injini na behewa moja
vikienda peke yake, na mabehewa yaliyobaki
yalifuata kwa kasi ileile, Amata na wa le polisi
walibaki kuangalia nini kitachotokea…
endelea...
Kikao cha dharula kiliitishwa katika ofisi ya
waziri wa ulinzi eneo la Msasani makao makuu
ya JKT. Kikao hicho kiliwakutanisha watu
wachache usiku ule, waziri wa ulinzi mwenyewe,
madam S akiwa ndiyo top wa idara ya TSA, na
IGP.
“Unajua tatizo lenyewe jinsi alivyoeleza Kamanda
Amata bado halijawa wazi, anasema aliyumiwa
ujumbe wa facebook na mwanamke usiku ule na
katika mabishano yao alifanikiwa kupata namba
ya simu na kumpigia ndipo aliposikia kilio cha
msichana na sauti iliyomlazimisha kutoa kitu
Fulani, kasha mirindimo ya risasi ikasikika.”
Madam S aliueleza mkutano huo
“Mi nilipiga simu kwa kamanda wa polisi Tabora
na akathibitisha kuwa kapokea simu toka
kwenye treni kuwa kuna mauaji yanaendelea na
kijana wetu mmoja ana hali mbaya baada ya
kupigwa risasi na hao majambazi.” IGP
aliongeza
“Sasa hao majambazi wanataka nini kwa huyo
mwanamke? Mi nafikiri hili swala tuwaachie
polisi washughulike kabla hatujaamua kuingiza
nguvu kubwa japokuwa tumeshaanza kufanya
hivyo” Waziri alitoa rai
“Hebu ngoja tupate mrejesho kutoka Tabora
baada ya Amata kukamilisha uchunguzi wake
halafu tutawasiliana” Madam S alishauri.
Mazungumzo mawili matatu yaliendelea juu ya
usalama wa nchi lakini bado walikuwa na
kitendawili cha ni nini kilichotoke katika treni
hiyo hata mawasiliano yaende kwa Amata moja
kwa moja, lilikuwa ni kama wingu zito kati yao
ambalo hakuna hata upepo wa kuliondoa. Waziri
wa ulinzi mara ashike hiki mara kile hakujua
afanye nini
“Sasa ni nini kinaendelea? Kwa nini treni hiyo
isizuiwe?” Waziri aliuliza
“Mheshimiwa, kwa taarifa tulizo nazo operetta
wa treni hiyo ameuawa kwa hiyo hakuna
anayeweza kulimudu, hivyo linakwenda tu” IGP
alimjibu Mh waziri.
“Ha! Endapo litapata ajali si mamia watakufa…
mama yangu!” Mh waziri alishtushwa na taarifa
hiyo na alionekana wazi kabisa kuchanganyikiwa
bila kuficha. Kimya kilitawala katika mkutano
huo na kila mmoja alikuwa anawaza lake na
hakujua nini mwenzake anachofikiria. Madam S
alikuwa wa kwanza kuvunja ukimya huo kwa
kujikohoza kidogo
“Kwa nini tusiwasiliane na mkuu wa polisi
Tabora kujua kinachoendelea?”
“Kwa ujumla amesema yupo pale stesheni
Tabora pamoja na stesheni masta hawana la
kufanya kwa sasa ila tu kuna wale mafundi wa
reli ndiyo wanatengeneza njia ili kama ikifika
hapo isilete maafa zaidi” IGP alitoa jibu
“Hiki ni kitendawili kikubwa, wananchi watakufa
mamia kwa mamia, Yesu wangu!” Mh waziri
alisikitikia hali hiyo na kutoa maagizo
“Hebu mwambie mkuu wa polisi Tabora
ahakikishe anafanya lolote kuokoa maisha ya
watu” Waziri alitoa ombi. Madam S katika kiti
chake cha kuzungukazunguka alikuwa hana
shaka sana
“Tusubiri kitachotokea, naamini Kamanda Amata
atafanya kazi, na roho za watu zitapona tu”
Madam S aliyasema hayo huku akichezea
kalamu yake kwa mikono yake miwili
“Madam S, una uhakika Kamanda atafanya
kitu?” Waziri aliliza
“Naamini kwa asilimia tisini na tisa mheshimiwa,
ndiyo maana sina wasiwasi na hilo” Madam S
alijibu kwa kujiamini kabisa.
“Ok basi fuatilieni tukio hilo hatua kwa hatua
mnijulishe, na asubuhi tuondoke wote kwenda
Tabora” Waziri alimaliza na kufunga kikao hiko
cha dharula.
***
K utoka ndani ya kichaka kile vijana wale
wavuta bangi walitulia tu, kwa mbali waliiona
treni ile ikija kwa kasi sana usiku ule.
“Oya jiandaeni sasa hivi kitu kinaitika, we Nyau
washa jeep hiyo tayari tayari” kiongozi wao
aliwapanga vijana wake, na wote wakakaa
tayari.
“Kwa hiyo hatpekui kidogo?” mwingine aliuliza
huku akivuta pafu la mwisho na kukitupa kipisi
kile cha bangi porini.
Kitu wasichokitegemea kilitokea, kishindo
kikubwa kilitokea, injini ya treni ile ilijipiga
kwenye mawe na mchanga na kutoka nje ya reli
na kusimama porini ikifuka moshi mweusi,
behewa moja liliokuwapamoja na injini hiyo
lilinyanyuka na kujikunja vibaya kasha likajipiga
ubavuni mwa injini ile na kubondeka vibaya.
Jomse na Ton walirushwa mbali na kudondoka
mchangani. Kutoroka porini vijana wale
walipigwa na butwaa maana wameona kipisi tu
ambacho kimekuja lakini treni iliyobaki
hawajaiona kabisa. Walimuona Jomse na Ton
wakigalagala mchangani waliwakimbilia na
kwaokota moja kwa moja waliwapakia katika
jeep
“Mbona mpo wawili?” yule kiongozi wa wale
vijana aliwauliza
“Hata hatuji mwingine yuko wapi, nyie twendeni
hayo tutayacheki kesho” Jomse aliwajibu na
wote wakapanda katika jeep moja na kutokomea
porini.
“Mandi mjinga sana, na yule ndiye atakaye ttia
matatizoni kwa ujinga wake” Ton alimueleza
Jomse wakati jeep ile ikikata mapori kuelekea
kusikojulikana.
“Na mi nilishalijua hilo, sasa sijui bwana twende
tutulie kwanza tutajua la kufanya” Jomse
alimjibu Ton.
Mabehewa yasiyo na kichwa yaliendelea kwenda
kwa kasi lakini yalionekana kukosa nguvu hasa
yalipopambana na miinuko, muinuko wa mwisho
ulikuwa mkubwa zaidi yalipanda mpaka katikati
yakasimama kasha yakaanza kurudi nyuma,
abiria wote walitulia kimya kabisa wakisubiri
mwisho wake, mchezo huo uliendelea na mwisho
mabehewa yale yakasimama bila kuleta shida
yoyote, abiria walipiga kelele za furaha kwa
kupona dhidi ya kifo ambacho hawakukitarajia,
wengi waliamini sala zao zimewaokoa,
waliokuwa mbele kabisa, polisi na Amata
waliamini ujanja wao umewaokoa. Amata
alikumbatiana na polisi wale kwa shangwe
hawakuyaamini macho yao kile wanachokiona.
Abiria walianza kuteremka kwa furaha japokuwa
trenin ile ilisimama porini sana na ilikuwa tayari
usiku mwingi, wote hawakuamini kama
wamepona walianza kuimba na kucheza kwa
furaha. Amata aliwatazama wananchi wale
machozi yakaanza kumtoka
“wengi wangekuwa marehemu, wengine
wangekuwa yatima na walemavu, asante Mungu,
Asante Isabel” Amata aliyasema hayo bila kujijua
akiwa kasimama kando ya mabehewa hayo
akitazama wananchi wale wakicheza na kuimba
“Tumesalimika, tunaomba msaada wa usafiri
kutoka hapa tulipo, ova” Polisi mmoja alikuwa
akiongea katika redio call kutoa taarifa makao
makuu ya polisi Tabora.
“Tumekupata na tunafanyia kazi, ova” sauti ya
upande wa pili ilijibu
“Nimekusoma” alijibu.
Furaha ililipuka katika viwanja vya stesheni ya
Tabora, hakuna aliyeamini walipopokea taarifa
hiyo kutoka kwenye chumba cha mawasiliano.
Mkuu wa polisi mkoa wa Tabora aliruka kwa
shangwe haikujalisha kama alikuwa na kitambi
kilichomzidi uzito, alimkumbatia stesheni masta
na kupongezana kwa furaha.
“Thank God, watu wetu wamepona” alisikika
stesheni masta akipiga kelele kwa furaha sana.
Madam S, IGP na waziri wa ulinzi hawakuamini
wanachosikia baada ya simu iliyopigwa na
Amata kumfikia Madam S kabla hajaondoka
katika eneo hilo la makao makuu ya JKT. Kila
mmoja alifurahi kwa furaha ya aina yake
“Well done Kamanda Amata” Madam S alisikika
akiyatamka hayo maneno.
“Ok, tunamshukuru Mungu, sasa kesho
asubuhi wote tukutane tuelekee Tabora kwa
ndege ya kukodi” waziri alimaliza na wote
wakaagana kuelekea walikotoka.
Je nini kitaendelea?
 
ISABEL an action story
ilipoishia...
Madam S, IGP na waziri wa ulinzi hawakuamini
wanachosikia baada ya simu iliyopigwa na
Amata kumfikia Madam S kabla hajaondoka
katika eneo hilo la makao makuu ya JKT. Kila
mmoja alifurahi kwa furaha ya aina yake
“Well done Kamanda Amata” Madam S alisikika
akiyatamka hayo maneno.
“Ok, tunamshukuru Mungu, sasa kesho asubuhi
wote tukutane tuelekee Tabora kwa ndege ya
kukodi” waziri alimaliza na wote wakaagana
kuelekea walikotoka.
endelea...
***
G ari za jeshi ziliondoka kutoka kambi ya Kaliua
KJ 320B kuelekea eneo la tukio ili kuwasaidia
abiria wale kuwafikisha mjini, usiku kwa usiku
amri ilitolewa na kiongozi wa kambi hiyo na kazi
ilianza mara moja bila hata kchelewa.
Watu walikuwa ni wengi sana kiasi kwamba
ilipelekea wengine kubaki ili gari zingine zije
kuwasaidia, vijana wa jeshi la wananchi wa
Tanzania walifanya kazi yao vizuri sana na kwa
moyo wa kizalendo kuwasaidia abiria wale japo
kuwasogeza karibu na stesheni au kuwafikisha
kabisa.
Steshen masta wa Tabora aliamuru vibelenge
kadhaa kufuatana ili kuona hali ilivyo na ndani
ya kimojawapo mlikuwa na mkuu wa polisi wa
Tabora, stesheni masta mwenyewe na viongozi
wachache wa chama na serikali, wote walitaka
kwenda kujionea wenyewe kile kilichotokea.
Wakiwa bado njiani kwa mwendo wa taratibu,
kwa mbali waliweza kuona kitu kikubwa
kimezuia reli, operetta aliongeza mwanga wa taa
yake kubwa na kupiga honi nyingi lakini hakuona
dalili ya kitu hicho kuondoka mahali pale,
alipunguza mwendo na walipokaribia walikuta ni
injini ya treni iliyokuwa ikitoka Kigoma kuja
Tabora
“Oh my God!” stesheni masta alisikika akisema
kwa sauti. Operetta alisimamisha chombo chake
na wote wakashuka kuangalia hali hiyo, walikuta
injini ile ikiwa imeacha reli na kusimama kando
katika mawe wakati lile behewa lilikuwa
limeanguka na kuharibika vibaya. Waliteremka,
kwa kusaidiwa na kurunzi walizonazo waliweza
kulikagua behewa lile na injini ile, hawakukuta
madhara katika injini ile ila tu behewa lilikuwa
limeharibika vibaya. Baadhi ya polisi waliingia
ndani ya injini hiyo kuangalia hiki na kile
wakisaidiana na mafundi, katika chumba
kimojawapo ndani ya injini hiyo ndimo
waligundua mwili wa mzee kasimu usio na uhai,
waliutoa na kuuhifadhi vizuri kasha kuupeleka
katika kibelenge kile
“Alikuwa operetta wetu mahili sana” stesheni
masta alijikuta akisema mwenyewe huku
akiuangalia mwili ule, machozi yalimlenga
“Kwa vyovyote atakuwa kafa kishujaa, kwani
mwili wake unaoneka umepigwa sana”
aliongezea mkuu wa polisi mkoa.
Waliupakia mwili ule katika kibelenge lakini
hawakuweza kuendelea na safari kwa kuwa reli
ilikuwa imeharibika vibaya. Kwa uchunguzi wa
haraka walioufanya waligundua kuwa reli ile
ilikuwa imefunguliwa
“Washenzi hawa walifungua reli!” mmoja wa
mafundi alisema kwa sauti
“Ha! Hawa walidhamilia, mpaka wamefungua reli,
no hii ni hujuma” Mkuu wa polisi alizungumza
hayo huku mkononi mwake akiwa ameshika
moja ya nati kubwa zinazotumika kufungia reli
hiyo ya kijerumani.
“Tungewapata hawa jamaa leo wangejuta
kuzaliwa” mkuu wa polisi alisema kwa hasira
“Unafikiri bado watakuwa kwenye treni
iliyobaki?” Stesheni masta aliuliza
“Sio rahisi, hii ni hujuma kabisa lazima walifanya
hivi ili kuwaokoa wenzao, lakini dunia ni ndogo
tutawatia mkononi” mkuu wa polisi alimjibu
stesheni masta. Vijana wa polisi walijaribu
kuangalia huku na kule japokuwa ilikuwa ni giza
lakini mwanga wa taa kutoka katika kibelenge
kile uliwawezesha kuona vizuri, polisi mmoja
alipiga hatua chache pale mbele akaona kitu
kama karatasi ndogo iliyokuwa ikisukwasukwa
na upepo mdogo uliokuwa ukivuma eneo hilo,
akakitazama akataka kukiokota lakini akaona ni
upuuzi akaamua kuondoka zake. Walirudi katika
kibelenge kile lakini askari wane walibaki kwa
ajili ya ulinzi lakini pia walijua wahujumu wale
wangeweza kurudi hasa kufuata mafuta.
***
Amata ga Imba, alisimama pembeni akiliangalia
zoezi zima linavyoendelea la kuwahamisha abiria
wale kwa kutumia magari ya jeshi,
“Kamanda, asante kwa kazi, wewe waweza
kwenda sisi tutamalizia, na ulinzi tutaimarisha”
polisi mmoja alimwambia Amata.
“Hamna shida, lakini nasikitika kuwakosa wale
washenzi japokuwa mmoja wao kajiua
mwenyewe, sasa hatujui walikuwa wangapi”
Amata alimjibu yule polisi
“Hawa jamaa hata mi sijui walikuwa wangapi,
nahisi ni yuleyule mmoja” yule polisi alitoa jibu
na hisia zake
“Kama ni yule peke yake basi! Lakini sidhani,
lazima wako wengine au lazima ana mtandao
mkubwa, usijali afande” Amata alimaliza na
kuondoka eneo lile mpaka kwenye gari
mojawapo la kijeshi aina ya MAN ililokuwa
limeegesha hapo likipakia baadhi ya abiria.
Kichwa kilimzunguka Amata, hakutaka
kukubaliana na wazo lake kuwa mle ndani
kulikuwa na jambazi mmoja tu, kwake kama
mzoefu wa kazi ile alijuwa wazi lazima watakua
kikundi ama ndaniya treni ile au nje yake,
alimfikiria sana Isabel ambaye muda huo
alikimbizwa hospitali ili kuokoa maisha yake kwa
kuwa alijua wazi kuwa ni yeye pekee anayeweza
kutoa mwanga wa tukio zima. Amata alitoa
karanga zake na kuanza kurushia mojamoja
kinywani mwake huku akiwaza ili na lile, moyoni
akiomba na kusali Isabel apone ili azungumze
naye machache ‘watakuwa washapata ile
memory card?’alijiuliza, mara kwa mara
alipofikiria juu ya Isabel alishtuka kwa kuwa
hakuwa na uhakika kama atamkuta mzima alijua
wazi kuwa kama wale majambazi wana mtandao
mkubwa haitakuwa kazi kugundu Isabel alipo
‘lakini wamfuate wa nini wakati washapata
wanachotaka’ alijiwazia ‘mh naomba asife’
alijiomba mwenyewe na hapo alijikuta anaingiwa
na shauku ya kumuona Isabel japo asikie neno
moja kutoka kwake labda lintampa muelekeo wa
nini cha kufanya.
“Walikuwa watatu bwana we hukuwaona vizuri”
baadhi ya vijana abiria walikuwa wakibishana,
Amata alijiunga nao katika mazungumzo yao.
“Yule tall sura yake sio ngeni kabisa, kama
namuonaona madukani pale Mwanga sokoni au
itakuwa namfananisha labda” mwingine
aliongezea. Amata alivutiwa na mazungumzo
hayo alitulia kimya akijifanya kuchocheachochea
vikuni kwenye ule moto uliokuwa ukiwaka
taratibu ili kuwapa joto usiku ule.
Baada ya mazungumzo yale marefu Amata
alikuwa amehifadhi vitu fulanifulani kichwani
mwake ili labda itakapobidi vitamsaidia katika
upelelezi wake. Kufumba na kufumbua abiria
wote walikuwa wameondoshwa eneo lile, askari
wachache walibaki kulinda mabehewa yale na
mizigo ya watu. Amata alitazama saa yake
tayari ilikuwa inakaribia saa kumi na moja
alfajiri, kichwa chake bado kilikuwa kinawazua
mengi kikitoa hili na kuweka lile, moyo wake
haukuridhika hasa alipomkumbuka Mandi jinsi
alivyojiua kwa mbinu ya kijinga namna ile, alijua
wazo kuwa wapo wenzake lakini aliumiza kichwa
jinsi gain ya kupata ukweli ‘mpango hasi’
alikumbuka neno hili alilotumiwa na Isabel
kupitia facebook, Amata alipenda ajue hasa
undani wa mpango huo ni nini. Alitamani kama
ni upelelezi basi akabidhiwe yeye hilo faili kwani
alitaka kulipa kisasi cha kuumizwa Isabel.
***
5
Mwili wa Koplo Kibona ulikuwa umehifadhiwa
vizuri kabisa katika sanduku la kisasa
liliofunikwa kwa bendera ya polisi, maafisa wa
jeshi hilo waliovalia nadhifu kabisa walikuwa
wamesimama kwa mstari ulionyooka vizuri na
upande mwingine kulikuwa na waombolezaji
wengine. Kasisi alipomaliza ibada ya marehemu,
vijana sita waliovaria nadhifu vazi la kipolisi
walisoge karibu na sanduku lile kwa ukakamavu
wa hali ya juu mara ilipigwa buluji maalumu ya
kazi hiyo kabla ya kushusha sanduku lile
kaburini. Jeshi la polisi liliamua kumzika
kiheshima kwa sababu amekufa akiwa katika
harakati za kulilinda taifa, baada ya buluji ile
kumalizika zilipigwa risasi kadhaa hewani kisha
sanduku lile lilishushwa taratibu kaburini.
Amata alisimama kwa mbali akiwa ndani ya suti
yake nyeusi iliyomkaa vizuri, pembeni yake
alikuwa na Madam S wakifuatilia kwa karibu
kabisa matukio yote ya mazishi hayo.
Muda si mrefu shughuli ilikamilika na watu
kuanza kutawanyika wengine wakienda kumpa
pole mjane wa marehemu.
Isabel alihifadhiwa katika chumba maalum
chenye mitambo tiba ya hali ya juu iliyomsaidia
kupumua na mingine ikisoma mapigo ya moyo
wake jinsi yanavyoendelea, Isabel alilala kimya
katika kitanda kile chenye shuka safi lenye
maandishi ya buluu yaliyosomeka MSD, hakuwa
hata anatikisa mkono wla kupepesa macho
alitulia kabisa, mara kwa mara muuguzi alikuja
kumuona maendeleo yake huku akiandika vitu
fulanifulani katika faili lililopo karibu kabisa na
kitanda hicho
“Mgonjwa anaendeleaje?”sauti ilimuuliza kutoka
nyuma ya kichwa chake, yule muuguzi alistuka
sana alijua labda ni mzuka. Amata ga Imba
alitabasamu hasa alipogundua kuwa muuguzi
yule kapata mshtuko kwa hilo.
“Anaendelea vizuri, ila bado hajarudiwa na
fahamu” Muuguzi alijibu kwa utulivu. Amata
alilisogelea faili na kulisoma harakaharaka
japokuwa watu huamini kuwa muandiko wa
daktari ni mgumu kusoma lakini kwa Amata
haikuwa hivyo. Alielewa moja kwa moja
yaliyoandikwa, Isabel alivunjika mbavu nne za
kulia inaonekana alipigwa sana kwa mateke na
kitu kigumu sehemu za mbavu, amekutikana na
majeraha ya kichwani, fuvu lake limepata shida
kidogo kadiri ya uchunguzi imeoneka Isabel
alijigonga vibaya kwa paji lake la uso hivyo
kusababisha majeraha eneo hilo, damu nyingi
imepotea hasa kutokana na majereha
aliyoyapata, mkono wake wa kulia umevunjika
hivyo alikuwa tayari amefungwa muogo ‘POP’.
Amata alimwangalia Isabel kwa uchungu sana
machozi yalitaka kumtoka lakini hakuruhusu hali
hiyo itokee. Mitambo mingi ya kidijitali
iliyomzunguka Isabel ilikuwa ikitoa ushirikiano
wa hali ya juu kuhakikisha mambo
hayataharibika, aliporidhika alimuaga yule
muuguzi na kuondoka zake.
***
Siku 3 nyuma
NYUMBANI
KWA
KINA ISABEL
Mama na Baba wa Isabel walikuwa shambani
kwao huko Kasulu wakiendelea kulima ili
kuhakikisha watoto wao hawalali njaa katika
msimu wote wa mwaka, redio ya mbao aina ya
National ilikuwa chini ya mchikichi ikiendelea
kuwaburudisha. Wazee hawa ambao bado
walishikilia falsafa za Mwalimu Nyerere kuwa
kilimo ni uti wa mgongo hawakuchoka na kilimo
japokuwa bado walikuwa wakitumi dhana duni
‘jembe la mkono’ lakini hawakukata tama kwani
walikumbuka ‘mkitaka mali mtaipita shambani’.
“Mama Isabel! Aaaah mama mi nimechoka
bwana napumzika” Baba wa Isabel alimwambia
mkewe huku akitupa jembe pembeni na kuiendea
redio ile ambayo ilikuwa imetulia hapo bila ya
wasiwasi.
“Ah Baba Isabel, unanitia uvivu mwenzio, na mi
naacha” Mama Isabel naye alitupia jembe
pembeni na kwenda chini ya migomba alipoficha
viazi vyake ili kutafuna atulize njaa ambayo
wakati huo ilikuwa ikimtafuna kwelikweli.
Ngoma maarufu iliyopigwa na marehemu Moriss
Nyunyusa ilirindima ndani ya redio ile kushiri
taarifa ya habari ilikuwa mbioni kuwa hewani,
baba wa Isabel alitazama saa yake ilikuwa saa
saba mchana.
‘Tabora,
Watu wawili wameuawa na wengine wawili
kujeruhiwa kwa risasi katika treni iliyokuwa
ikitoka Kigoma kuelekea Dar es salaam jana
usiku, dulu za kiusalama zimesema treni hiyo
ilivamiwa na majambazi ambao hawajajulikana
idadi yao na kusababisha vifo hivyo. Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora amethibitisha kutokea
tukio hilo na amesema waliouawa ni askari polisi
Koplo Kibona na operetta wa treni hiyo mzee
Kasimu, eitha mkuu wa polisi huyo amethibitisha
majeruhi wawili walioumizwa vibaya na
kukimbizwa Muhimbili kwa matibabu kuwa ni
askari polisi konstebo Kirama na msichana
mmoja mwanafunzi aliyetambulika kwa jina moja
tu la Isabel, mpaka sasa hakuna mtu yeyote
anayeshikiliwa na polisi ila uchunguzi
unaendelea…’
Taarifa ile ilimshtua baba wa Isabel, alianza
kuhema kwa haraka haraka akamuita mkewe,
hali haikuwa nzuri, kilimo kilisitishwa, mama wa
Isabel akaanza kuagua kilio kilichowafanya
majirani waanze kukusanyika uko huko
shambani.
“Mwanangu Isabel, jamani nifanyeje mimi, Oh
Mungu we …” kilio kilitawala mama wa Isabel
hakuweza kujizuia kulia, alilia sana hata
kupelekea kuzimia mara kwa mara.
“Mama nyamaza, si wamesema yupo hospitali…”
dada mkubwa wa Isabel alimbembeleza mama
yake
“Wanatudanganya, mwanagu mimi atakuwa
ameshakufa, nimlilie nani mimi” Mama wa Isabel
hakuweza kutulia kwa haraka, muda mfupi
nyumba ilikuwa imejaa watu kujua kulikoni, Baba
wa Isabel alishafikishwa katika hospitali ya
mission Kabanga maana BP ilipanda ghafla.
Taarifa za treni hiyo zilisambaa sana na kwa
haraka, watu wengi walisikitishwa kwa tukio hilo
“Yaani hawa ni wakutia moto tu!” mmoja wa
vijana aliyaongea maneno hayo kwa sauti
akionesha jinsi ambavyo angependa majambazi
hao waadhibiwe.
Siri imefichika, hakuna anayejua nini kipo nyuma
ya tukio hilo, mh kazi ipo...
Hali ya Isabel ni mbaya, unafikiri atapona?
je serekali ya Tanzania itaamua nini juu ya hili?
Usikise chapisho lijalo...
 
Mkuu #kidikudi unatisha...hongera sana
 
Basi sawa.... ngoja tusubiri kuona hali ya isabela itakavyokuwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom