RIWAYA: Isabel ndani ya mpango hasi

RIWAYA: Isabel ndani ya mpango hasi

ISABEL--ndani ya mpango basi

ilipoishia...
“Freeze, bastard” Gina alimuamuru Jomse
aliyekuwa akijaribu kujitutumua pale chini,
Jomse alijifanya asikii na kutaka kuichuku ile
short gun mara Makarov ya Gina ilicheua tena
na kuvunja mkono wa Jomse, yowe la maumivu
lilimtoka.
Mara polisi kadhaa waliingia ndani ya jengo lile
wakiongozwa na Inspekta Simbeye, walimfungua
kamanda Amata na kumchukua Isabel baada ya
kugundua kuwa bado alikuwa na uhai, haraka
sana wakamkimbiza Hospitali ya jeshi la
wananchi Lugalo.
“Naomba muhakikisehe huyu mtu anafika
makao makuu ya polisi leo kwa mahojiano
hata kama ana maumivu ya mkono sijali,
mimi naelekea uwanja wa ndege, kuna
muasi mmoja bado hajakamatwa na hayupo
hapa” kamanda Amata alitoa amri huku
akiingia katika gari ile iliyomleta, Toyota
Altezza na kuigeuza kwa kasi na kuondoka
eneo lile kuelekea uwanja wa ndege.
endelea..


Kwa maelekezo ya Amata, Inspekta Simbeye
alitoa amri kwa redio call maeneo muhimu yote yawekwe ulinzi ili kumnasa muasi huyo, kuanzia stendi ya Ubungo, Posta eneo zinaoondoke bot
za Zanzibar, Uwanja wandege wenyewe. Mji wa Dar es salaam ulijawa na askari kanzu kufanya
msako huo, mawasiliano ya redio za polisi muda
wote yaligubikwa na habari za wapi ameonekana au wapi kuna dalili. Maelekezo machache waliyoyapata jinsi alivyo yaliwafanya watu wa
mtindo huo kuishi kwa shida usiku huo
* * *
Tonton akiwa bado hajui kilichompata Jomse na Meno ya Mamba bado alikuwa katika harakati za kumsaka Madam S, ama awe hai au maiti, aliiangalia saa yake aliona inakaribia saa nne za usiku, akiwa amepaki gari yake katika njia panda ya uwanja wa ndege terminal one, bomu la mkono aina ya grunet lilikuwa juu ya kiti cha gari yake huku akijifanya anatengeneza tairi akisubiri
msafara ule wa wanausalama utoke kule uwanja wa ndege ili afanye yake. Alikuwa hakika amejizatiti kwa kila hali, walktalk yake iliita
akaichukua na kupata maelekezo Fulani kisha akairudisha kitini na kusubiri kidogo akiwa ndani ya overall. Akiwa katika kushangaashangaa mara mbele yake ilipita Toyota Altezza nyeusi
kwa kasi ya ajabu ikielekea uwanja wa ndege,Ton aliiangalia kwa makini akaingiza mkono mfukoni na kuinua simu yake na kubofya namba Fulani na kuiweka simu yake sikioni, lakini simu
ile haikujibiwa, aliipiga tena hali ilikuwa ileile,akachanganyikiwa afanyeje maana aliona Jomse
kaelekea airport na gari yake sasa akawa katika njia panda kama alipo, amfuate au asubiri pale kadiri ya maelekezo aliyoyapata, alizunguka huku
na huku akiwa kama mtu aliyechanganyikiwa.
* * *
Mabishano makali yalikuwa kati ya Madam S na waziri wa ulinzi, Madam S aling’ang’ani ndege ile ishuke haraka iwezekenavyo wakati waziri wa
ulinzi akisema kuwa hawana la kufanya ndege imeshakwenda hakuna jinsi ya kuiokoa.Akiangalia simu yake dakika thelathini zilikuwa zimekatika tangu ndege ile iache ardhi. Tairi za Toyota Altezza zililalamika katika lami
Amata alipokuwa akiingia uwanjani pale,
“Vipi Madam? Bado nimewaambia ndege ile
ina bomu itue hapa tufanye
kinachowezekana, ah!” Amata aliingia
kwenye gari yake na kuondoka kwa
kasi..............

********************************************
**********************************
Je; itawezekana kuiokoa ndege hiyo?
Ni nini kamanda Amata anategemea
kufanya?
kwa nini Madam S na waziri wa ulinzi Bw
Machura wanashindwa kuelewana?
SIMULIZI YA ISABEL-ndani ya mpango
hasi ......... inapatikana kwa Tsh 2000 tu,
tuma kwa m-pesa kupitia namba +255
767 152125.... weka email adress yako
kwa ufasaha kabisa na jina lako kamili
uteremshiwe mzigo wako.
 
wadau kama tangazo linavyojieleza mwisho wa story na mimi jitihada zangu zimeishia hapo kuwaletea pale Casuist alipoishia
 
Last edited by a moderator:
aisee bwana machura nae ni miongoni mwa waasi... bahati mbaya sina email.... ngoja niitafute
 
Weka tigo au airtel money tuyajenge fasta mkuu kidikudi
 
ISABEL--ndani ya mpango hasi

SIMULIZI YA ISABEL-ndani ya mpango
hasi ......... inapatikana kwa Tsh 2000 tu,
tuma kwa m-pesa kupitia namba
0767152125 weka email adress yako
kwa ufasaha kabisa na jina lako kamili
uteremshiwe mzigo wako.

poa wadau tuwaunge mkono waandishi wetu.
 
Watunzi WA Jf bana mna mambo yaani jukwaa hili mpewa bure nyie mnaleta ujasiriamali Alaf boa mbaya asee shame on you kidi a.k.a casuist
 
hiyo namba ukitumbukiza tu hela umeliwa. Jamaa hana ushirikiano kabisa kwanza muda wote ipo off line.
 
Watunzi WA Jf bana mna mambo yaani jukwaa hili mpewa bure nyie mnaleta ujasiriamali Alaf boa mbaya asee shame on you kidi a.k.a casuist

Mimi sio mtunzi wa hadithi mkuu, hujafanya vyema kusema kitu usichokijua. Nisamehe lakini naomba moderators waangalie kama ni ID moja na kama sio adhabu ikuhusu.

CC Rider
 
Last edited by a moderator:
kidi kudi mbona namba hiyo haipatikani.???? ukifanikiwa mwambie atume kwa waliotoa mpunga.
 
Last edited by a moderator:
Mbona wewe ulikuwa unatuletea hadithi mwanzo mwisho, inakuwaje tunaanza kuuziana hizi hadithi?


Mimi sio mtunzi wa hadithi mkuu, hujafanya vyema kusema kitu usichokijua. Nisamehe lakini naomba moderators waangalie kama ni ID moja na kama sio adhabu ikuhusu.

CC Rider
 
Last edited by a moderator:
ram

Sio mimi mpendwa, huwa siweki hadithi isiyo na mwisho, tatizo mtu anaingilia thread na anavyoiweka tofauti hivyo unaingia kazi ya ziada kuanza kuikata upya na kila siku anavuruga just huwa naamua kukaa pembeni na sometimes japo mara chache sana hawa waandishi ndo wazinguaji.

Attached ni PDF ya hadithi(Isabel) yenye mwisho



© richard MWAMBE ‘2013
≈ MWISHO ≈

mlyn mamaafacebook hawahamisi Jagarld Jullie Z Sangomwile Khantwe Mr Rocky Gunda66 Himidini VAN HEIST BPM ABUBAKAR SHEKAUNYIROmamsapkhan born again pagan princetx Ennie mcubic jonnie_vincy slim5 MAVUNO mp anoldamoneyazan
 

Attachments

Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom