Riwaya: HOFU

Riwaya: HOFU

MKUU YAANI NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA NIKIMAANISHA WEWE NI NOOOOOMAAAAA SALUTE JF KUNA THINKERS KWELI NIMEAMINI YAANI THE HOME NDOGO NI THE WORLD OF THE GREAT THINKERS (SASA MUZEI TUPIA BASI NA HICHO KITU WATU HAPA MACHO YASHA TUTOKA)
 
SEHEMU YA MWISHO PART 2
Kindo akaingia katika mchecheto, ni kweli
alikuwa akimpenda sana Salome kwa dhati.
Lakini katika mazingira yale ili atoke salama
ilikuwa lazima ajihusishe na Queen.
“Ni nani huyu kwani?” Queen alihoji.
“Huyo ni mume wangu..” Salome alitoa jibu……
“Shhhh! Komea hapo hapo mwanamke.”
“Hey! Jamani tunatakiwa kuwa wamoja jamani,
ugomvi wa nini tena? Tunatakiwa kutoka humu
ndani..” Rensho aliyekuwa amekaa pale chini
alionya. Wakanyamza.
Lakini Queen alikuwa amefikiria jambo, hakuwa
tayari kutoka mle ndani huku akijua kuwa Kindo
si mali yake. Tayari alikuwa amekolea. Wivu wa
kimapenzi ukaanza kumshambulia
Na hapo akafanya tendo la kipuuzi kuliko yote
aliyowahi kuyafanya.
Tendo lililomgharimu ila hakuipata nafasi ya
kujuta.
Akawaza kumuua Salome ili abaki kuwa mmiliki
halali wa moyo wa Kindo. Tayari alishatambua
kuwa ile nguvu ambayo aliingia nayo mle ndani
hakuwa nayo tena. Alikuwa ni mwanadamu wa
kawaida tu.
Queen akitambua zaidi kuwa hakuna mwenye
uwezo wa kumnyamazisha mle ndani hata Kindo
mwenyewe hakuwa na sauti juu yake.
Akamvamia Salome si katika namna ya ugomvi
wa kike kike uliozoeleka. Huu ulikuwa wa aina
yake…
Mapigano ya kiume! Queen akajirusha na
kumtundika ngumi ya shavu salome, akatokwa na
ukelele mkubwa huku akianguka chini.
“Queen acha, acha Queen…” alitoa onyo Rensho
asiyekuwa na uwezo wa kusimama.
Lakini Queen badala ya kujibu akasimama na
kumvaa Rensho akamtandika teke kali kifuani….
Rensho akapoteza fahamu palepale. Kimya
kikatanda, Queen alikuwa ameiva kwa hasira.
Kindo akajaribu kumtuliza.
Akamgeukia na kumtazama na macho yake
mekundu yaliyokuwa yanang’ara kwa hasira.
“Ukae kimya Kindo…..hukuniambia kama una
mahusiano na msichana yeyote kumbuka. Nyie
wanadamu ni waongo lakini hapa ni mwisho wa
mambo nasemaje Kindo ni aidha ufanye muujiza
umeze maneno yako ama la nakinyonga hiki
kiuchafu kinachojiita mkeo.” Alitoa karipio kali,
Kindo akakumbuka kuwa hana wa kumlaumu
zaidi ya ulimi wake. Ulimi uliopanga maneno
matamu na kumjaza Queen.
Baada ya kuhakikisha kuwa kila mtu mle ndani
alikuwa anamuogopa na Rensho akiwa
amepoteza fahamu, akarejea kwa Salome. Lengo
likiwa moja tu kummaliza kabisa.
Bila huruma akamkwinda na kumnyanyua kisha
akamtupa kando, akaangukia tumbo huku
akitokwa na kelele kubwa ambayo ilimzindua
mzee Nshomile ambaye alikuwa amepotea
kifahamu. Akakohoa huku akipepesa macho huku
na kule. Hakuwa na nguvu tena.
Yowe la Salome lilimaanisha uchungu mkubwa
sana. Uchungu usiokuwa wa kawaida.
Kisha akatulia tuli…..ule mtupo ulikuwa umeleta
madhara makubwa sana. Lakini yawezekana
kabisa kuumia kwake nd’o ilikuwa ponapona yake
baadaye.
Damu ikaanza kumtoka kwa fujo kutoka sehemu
zake za siri.
Mimba ilikuwa imeharibika!!
Damu ikazidi kutiririka, Queen akatambua kuwa
amemuua Salome. Hakujua kuwa ile haikuwa
mimba ya kawaida bali ilikuwa ni roho ya Rensho
iliyohifadhiwa katika tumbo lile miezi kadhaa
iliyopita. Roho iliyokuwa maalumu kwa ajili ya
kumpa vyeo Rensho ambaye alikuwa
ameandaliwa kuwa mwenyekiti kwa siku za
usoni, roho ambayo Waziri na Nshomile walikuwa
wakiisaka kwa hali na mali. Roho ambayo
ingemuwezesha Rensho kuishi katika nafsi mbili,
mwanadamu wa kawaida na pia katika dunia ya
kimiujiza.
Damu ile ikavuja hatimaye ikamgusa Rensho!!
Bila mvua kunyesha radi kubwa ikapiga.
Kila mtu akaingiwa na hofu mle ndani, Rensho
akarejewa na fahamu huku akijisikia imara
maradufu. Na goti lake likiwa imara kabisa.
Alikuwa Rensho mpya, akalisikia lile joto la
uhai…..tayari alikuwa ameipata roho yake.
Akasimama wima akitazamana ana kwa ana na
Queen.
Queen akadhani Rensho aliyevunjika goti bado ni
yule yule akamvamia aweze kumdhibiti, lakini
yakawa maajabu ya mwisho aliyoweza kuyaona
kabla hajapoteza uhai wake na kuteketea vibaya.
Alikutana na ngumi kali kutoka kwa Rensho,
akapepesuka huku na kule kisha akaanguka chini
na kuzimika moja kwa moja.,
Queen akapotea katika ramani ya uzima….
“We mzee kitovu cha Kindo kipo wapi? Ni swali
moja na jibu moja tu….” Rensho akatupa swali
kwa mzee Nshomile ambaye ni baba yake mzazi.
Kindo akaduwaa kusikia kitovu chake kikiuliziwa.
“Sihitaji ujifikirie katika hili mzee, ulikichukua
kitovu chake akiwa na umri siku mbili tu. Na
ulikichukua kwa sababu zenu za kishirikina
ambazo leo zinawatokea puani. Natambua fitina
zako zote ulizomfanyia Kindo ili kumvuruga na
kuipoteza amani yake, kumuua mama yake
mzazi…..na hata ujauzito wa Salome nadhani
unajua nia yenu ilikuwa ipi. Washenzi kabisa,
Salome aliwakosea nini mkampa mzigo huu.
Mmemtesa Kindo mmemnyang’anya amani yake
na kumpotezea marafiki zake….. baba mbaya
kupita wote duniani, shetani mkubwa wewe. Na
nilikuapia tangu siku ya kwanza uliponiingiza
katika utawala huu kuwa ipo siku utalia na
kusaga meno na hiyo siku ni leo sasa…..
Upesi nahitaji jibu….. kitovu cha Kindo kipo
wapi?”
Mzee Nshomile alipatwa na aibu wakati Rensho
akizungumza kibabe. Alijiumauma na hakujibu
chochote kile. Kama kawaida ya Rensho haulizi
mara mbili na ule upendo wa baba hakuwa nao
tena.
Akajirusha na kumfikia akainama chini akaokota
kile kisu kilichoandaliwa kwa ajili ya kumchinja
Eva.
Ndani ya sekunde tano tu kilio kikubwa
kikasikika.
Nshomile hakuwa na mkono mmoja!!!
“Ndani ya dakika mbili nitaondoa huo mguu…”
akaonya Rensho huku mzee wake akiwa
anaugulia maumivu na damu ikiruka na kumfanya
Getonga aikwepe, Kindo akatokwa yowe la hofu.
“Katika jeneza lako mwanangu….”
“Komea hapo, usirudie kuniita mimi mtoto wako,
unaruhusiwa kuzaa mwingine ukamuite hivyo,
mnafiki mkubwa wewe. Mtoto wako na umetaka
kuniua wewe leo…nyang’au wewe. Kwanza mtoto
wako ulimzika zamani kabisa sio mimi ambaye
nipo hai tena” alifoka Rensho huku macho yake
yakiwa mekundu sana.
“Mwamshe huyo bwege mwenzako hapo chini
upesi” Rensho akakoroma, Nshomile akamtikisa
waziri mstaafu kwa kutumia mguu, yule jamaa
akagutuka kutoka katika usingizi wa kifo.
“Uliuwauwa wabunge wangapi waliopaswa
kushika nyadhifa ya uwaziri mkuu hadi
ukateuliwa wewe shetani mwenye miguu miwili….
Aah! Ni swali na njibu upesi. Ukichelewa
nakuondoa mkono kama mwenzako, kama
shetani mwenzako.”
“Wanne….” Alijibu huku akitetemeka.
“Ni wapi umeizika akili ya raisi wetu hadi
amekuwa wa kukuamini kiasi hicho katika
madaraka yake?”
“Kwenye kaburi la mama yangu..”
“Ambaye ulimtoa kafara sivyo?” Rensho akakazia.
Waziri akaona aibu kujibu.
“Getonga, hii ni makala nadhani sihitaji
kukukumbusha kuwa wewe ni mwandishi. Hivyo
usitazame kama mchezo wa kuigiza natambua
unao uwezo mkubwa wa kufikiri na kukariri
utajua namna ya kuandika.” Rensho alimgeukia
Getonga na kumweleza kisha akafanya tabasamu
kali. Tabasamu la ushindi.
“Mkatandaza HOFU mabaradhuli wakubwa nyie,
nazitumia hizi nguvu zenu kuwaadhibu sasa
shenzi nyie……sogea hapa wewe waziri mkuu,
upesi!!” amri ikatoka. Waziri akajizoazoa hadi
mbele ya miguu ya Rensho.
“Mkeo anajua kuwa wewe ni mshirikina?”
akamuuliza kwa upole.
“Hapana hapana sijamwambia….”
“Tazama na uone aibu….. mkeo hajui mambo
haya kwa sababu ni machafu. Anayajua diwani
wenu yule niliyemtoa roho Kahama. Sasa na nyie
nawatoa roho mnasemaje juu ya hili.” Aliuliza
akimtazama waziri kisha akamtazama mzee
Nshomile. Wote walikuwa wametepeta huku
wakitetemeka sana.
“G yaone haya…” alimuonyesha Getonga kisha
akatoa kicheko cha dharau kubwa.
Ilikuwa imetimia saa mbili na nusu asubuhi
wakati haya yakitokea.
__________
NYUMBANI KWA WAZIRI.
___________
Yale masaa waliyokuwa wamemzimisha mkewe
ambaye aliwafuma wakiwa uchi yalikuwa
yameisha tayari, yowe alilotoa yule mwanamke
liliwashtua watoto wake wakaimbilia eneo la
tukio, walivamia kile chumba na kila mmoja
akapigwa na butwaa kukutana na maiti ya diwani
ikiwa imeharibika vibaya mno.
Mama alikuwa anazimia na kuzinduka huku
akishindwa kusema neno lolote lile. Majirani
walipata nafasi ya kuingia katika baadhi ya
vyumba vya waziri huyo ambaye alisifika kwa
wema wake na ukarimu.
Baadaye mwanamke aliweza kutoa ushuhuda juu
ya kila kilichotokea hadi alipomuona mumewe
akiwa uchi wa mnyama pamoja na mzee
Nshomile.
Waandishi wa habari walizinasa picha na
maelezo ya yule mama kwa ufanisi wa hali ya
juu.
Ilikuwa patashika katika jumba lile, kila mmoja
aliamini kuwa waziri alikuwa mshirikina. Lakini
swali lilikuwa moja tu. Na ni nani aliyemuua
diwani.
Waswahili wakasema kuwa ametolewa kafara.
Polisi wakafika eneo la tukio, chumba
kikazungushiwa utepe wa kiusalama, hakuna
aliyeruhusiwa kuingia ndani ya kile chumba tena
hadi hatua za ziada zitakapochukuliwa.
Waziri na mzee Nshomile wako wapi? Hilo likawa
swali.
Msako ukaanza…… msako madhubuti wa
kuwatafuta watu hao.
Raisi wa jamuhuri alizipata taarifa hizi lakini bado
alikuwa upande wa waziri mstaafu. Alijaribu kwa
kila hali kuupinga ukweli. Akili yake ilizikwa muda
mrefu bila yeye kujua.
“Akipatikana aletwe kwangu moja kwa moja..”
alitoa amri hiyo. IGP akaipokea.
Msako ukaendelea!!
WAKATI MSAKO ukiendelea Rensho alikuwa
amewapa amri wawili wale kuwa walitakiwa
kutoka ndani ya nyumba ile na kukitafuta kituo
cha polisi kilichopo karibu waweze kujisalimisha
na kueleza bila kuficha maovu yao.
Akawafungulia mlango huku akiwa onyo kuwa
wakithubutu kudanganya atavipasua vichwa
vyao.
Walifahamu kuwa anaweza na hakuwa akitishia
hivyo walitii, mmoja akiwa hana mkono,
mwingine hana meno. Wakatembea kwa shida
huku wakianguka anguka.
Ndani ya dakika kumi walikuwa wamezingirwa na
umati na watu wengi walimtambua waziri yule
aliyewahi kuwa maarufu sana, kisha akafifia na
kisha kuibuka tena akitabiriwa kuwa raisi wan chi
mtarajiwa.
Simu zkapigwa katika vituo vya polisi juu ya
unyama waliotendewa wawili hawa!!
Waliotoa taarifa hawakujua kuwa hao
wanaoonekana kutendewa unyama, wenyewe
pekee ni wanyama tosha.
Polisi wakafika eneo la tukio na kuwasomba
mabazazi wale wasiokuwa na huruma. Moja kwa
moja katika kituo kikuu cha polisi ambapo taarifa
ya mauaji ya diwani mwanamke ilikuwa imefika
pale huku msako mkali ukiendelea juu nya
waliotenda mambo haya.
Ajabu kuu waliosadikika kutenda unyama ule
walikuwa hoi zaidi!!
Kulikoni? Hilo nd’o swali walilojiuliza.
Taarifa zikafikishwa kwa IGP akaamuru waziri
mkuu mstaafu afikishwe mbele yake upesi sana.
“Sawa afande!” mtoa taarifa akajibu kwa
heshima.
_______
UPANDE WA PILI
________
Rensho akawakusanya watu wake akiiacha maiti
ya Queen katika jumba lile, Salome alikuwa
amerejewa na fahamu tayari. Rensho akambeba
Eva ubavuni mwake. Safari ya kukitafuta kitovu
cha Kindo na kuusaka mwili wa Rensho!!! Bila
kusahau kuifukua akili ya raisi wa jamuhuri
ambayo ilikuwa imezikwa katika kaburi la mama
yake waziri mkuu mstaafu.
Utata wa mwisho kabisa ukazuka katika harakati
hizi!!
Raisi wa jamuhuri ya muungano akazua HOFU!!
UTATA gani tena?? RAISI naye vipi??
 
Aisee tangu nimeifuma hii story mpaka Sasa sikujaribu Ku coment chochote kwa hofu ya kupitwa Na point katika hili sakata la HOFU.

mwanzo hili picha lilianza kwa kujisokota sokota sana almanusura nikate tamaa kuendelea kulisoma, lakini kila hatua moja mbele ndivyo movie lilizidi kunibamba ajabu. Asante sana kaka kwa story la nguvu
 
Umetishaaaa. Cjawah soma hadith ya kusisimua na ischosha kama hii. Congratz:
 
Kaka tupo uwanjani tunasubiri hatima ya rensho
 
SEHEMU YA MWISHO PART 3
UPANDE WA PILI
Rensho akawakusanya watu wake akiiacha maiti
ya Queen katika jumba lile, Salome alikuwa
amerejewa na fahamu tayari. Rensho akambeba
Eva ubavuni mwake. Safari ya kukitafuta kitovu
cha Kindo na kuusaka mwili wa Rensho!!! Bila
kusahau kuifukua akili ya raisi wa jamuhuri
ambayo ilikuwa imezikwa katika kaburi la mama
yake waziri mkuu mstaafu.
Utata wa mwisho kabisa ukazuka katika harakati
hizi!!
RAISI wa jamuhuri ya muungano alikutana na
waziri mkuu mstaafu katika chumba cha siri
kabisa cha kijeshi.
Alimkuta akiwa amepewa huduma ya kwanza.
Waziri mkuu mstaafu alitamani kudanganya lakini
alipokumbuka kile kitisho kisichokuwa na
masihara kutoka kwa Rensho alilazimika kusema
ukweli mtupu.
Ukweli ambao raisi aliukataa kata kata akidai
kuwa yule bwana amerukwa na akili tu. Hawezi
kuwa amefanya kitu kama kile, eti aliua wabunge
wanne akamuua na mama yake.??
Hapana!! Raisi alikataa katakata. Alikataa huku
akitabasamu akimaanisha kuwa ule ni mzaha
mkubwa kabisa usiotakiwa kutiliwa maanani
kabisa.
“Lakini mkewe anadai kuwa amemuona kwa jicho
lake akiwa uchi?”
“Hapana usikae kuamini maneno ya wanawake
na wewe….hakuna kitu kama hicho….mambo ya
wanawake. Wanafiki wanaota ndoto usiku
wanasema waliona kitu na wanabisha hao.
Wanawake we huwajui wewe, nilikwambia uoe
ona sasa…hujui lolote kuhusu wanawake IGP”
Raisi alizungumza maneno mengi huku akizidi
kuegemea upande wa Waziri mstaafu.
“Hapana mkuu, nimeyafanya hayo yote na mke
wangu ni shahidi wa kweli kabisa, naiomba
serikali yako inihukumu.” Waziri alimsihi raisi wa
jamuhuri.
Kisha IGP naye akakazia.
“Haya mkewe alikuwa anaota, vipi kuhusu maiti
iliyokutwa ndani ya kile chumba mheshimiwa?”
“Waliiweka mahanithi waliomjeruhi, tena hili
jambo nitalisimamia ipasavyo hivi vyama pinzani
vinataka kutudhoofisha kiasi hiki. Na chanzo ni
kwamba anataka kuwania uraisi..shenzi kabisa.
siwezi kuyafumbia macho, kuna vyama
vinatakiwa kufutiwa usajili kabisa, nadhani
unaelewa ninachosema” Raisi alizidi kuwaka.
Kwa asilimia mia akiwa anamtetea waziri
mstaafu.
Siasa bwana!! IGP alijiwazia huku akitazama jinsi
gani waziri mstaafu alikuwa katika hatia ya
waziwazi.
“Waliohusika na tukio hili wanatakiwa wafikishwe
mbele ya sheria mara moja!!” alitoa amri, amiri
jeshi mkuu wa Tanzania.
IGP akatii!!
*****
RENSHO alimruhusu Eva, Anitha na Salome
kuondoka kuelekea nyumbani huku yeye, Kindo
na Getonga wakibaki kwa ajili ya zoezi la mwisho
kabisa.
“Nilisikia unasema kuwa wana kitovu changu,
mbona sielewi?” Kindo alimuuliza Rensho wakiwa
wametulia eneo fulani nje kidogo ya jiji wakisubiri
kigiza kiingine waweze kufukua makaburi mawili.
“Unapozaliwa kitovu kinakuwa kimeungana na
mama. Hivyo lazima kikatwe nd’o unabaki na
hicho kidogo. Basi kilipokatwa kile kitovu huyo
mzee Nshomile alikichukua, lengo lake likiwa
moja tu. Kukutengeneza na kisha kukutumia
katika shughuli zao. Hivyo walitulia kwa muda
mrefu wakiyafanya maisha yako kama yao,
hukuwa na akili darasani Kindo, maisha yako na
ya wazazi wako yamekuwa magumu tu..mwisho
wakaamua wakutumie wewe kunitoa mimi….yaani
kuirudisha tena roho yangu. Wakakuongoza
kufanya mapenzi na Salome kisha kumpa mimba
isiyokuwa mimba. Mimba ya kichawi…. Nia yao
ile mimba kabla haijakomaa waitoe kishirikina na
kisha kuniunganisha na yale mabonge ya damu
nizaliwe upya. Nilitakiwa kupewa cheo.
Waliowaagiza kumuua Salome wakafanya makosa
kwa kumbaka yule binti, na hapa nd’o siku ile
ambayo unakumbuka damu ilianza kuvuja
chumbani nikiwa pamoja na wewe…unakumbuka
?” alimuuliza, Kindo akaikumbuka hiyo siku.
“Basi nd’o mambo yalipowaharibikia hapo na
walikufa wengi, nilibahatika kubaki hai kutoka
katika tukio lile kwa sababu moja tu, sikuwa na
mwili wala roho. Sasa ningekufaje
unadhani….mwili ulizikwa miaka mingi iliyopita na
roho ilikuwa katika mwili wa salome kama mimba
ya ajabu. Hivyo wewe ulikuwa wa muhimu
sana…… wakakutia hofu maradufu. Wauaji wale
wakaishika akili yako ili usiweze kutoa ushahidi
wowote ule juu yao. Mshukuru Mungu wako kuwa
upo hai hadi sasa.” Alimaliza Rensho.
“Na wewe unataka kujua juu ya kitambulisho….h
akina maana tena kile kitambulisho. Nina roho
yangu tayari, kile kitambulisho kilikuwa kwa
sababu moja tu….iwapo mambo yakiwa magumu
kabisa niende kujisalimisha kwa mkuu wetu,
lakini sasa sitajisalimisha bali nitamuangamiza na
popote anaponisikia anajua kuwa nitamuua tu….”
Alisema kwa hasira.
Walizungumza mengi, wakapata chakula na
hatimaye kigiza kikaingia.
Rensho akawashika mikono na kisha wakatoweka
na kutokezea makaburini.
Kindo na Getonga walikuwa wanatetemeka
haswa kujikuta makaburini wakati ule.
“Alikuwa anaitwa Magreth Hossana, tafuta kaburi
lenye jina hilo haraka.” Rensho aliamrisha. Kwa
kihoro Kindo na Getonga wakaanza kuangaza
huku na kule wakilitafuta jina katika makaburi.
“Huyu hapaa…..” Rensho ambaye pia alikuwa
akilitafuta lile kaburi aliwapigia wenzake kelele.
“Hapo hapo mlipo simama kama mlivyo mikono
juu” sauti nzito ya kiume iliamrisha.
Kindo na Getonga wakasimama huku
wakitetemeka. Kutahamaki walikuwa
wamezingirwa mbele ya nyuma na kundi la
wanaume wakiwa wamebeba bunduki mikononi
mwao.
“Nyie ni akina nani?” jamaa mmoja mwenye
ndevu nyingi aliuliza.
Kabla hawajajibu lolote sauti ya Rensho ikasikika.
“Nipo nao kwani vipi?” alitokeza akiwa katika vazi
lake lilelile jepesi kabisa.
“Mnafanya nini hapa wakati huu?”
“Kwani nyinyi mnafanya nini hapa?” na yeye
aliwauliza kwa jeuri. Kisha akaongezea, “Halafu
hamjisikii vibaya wanaume wazima tena sita sijui
mmetushikia bunduki watu tusiokuwa na silaha
na hatuna neno baya na ninyi?” aliwachokonoa
maksudi.
“Kaa kimya mwanamke…tutapasua vichwa vyenu
sasa hivi mkileta dharau wachawi wakubwa
nyie….” Alifoka jamaa mwingine mwenye kipara.
“Ok! Kwani mnataka nini labda…”
“Tunataka kujua nyie ni akina nani?”
“Wachawi tumekuja kuwaroga hizo Bunduki zenu
zigeuke nyoka ikibidi……” Rensho alijibu kwa jeuri
huku akitoa tabasamu hafifu.
Jamaa mwenye kipara akataka kumvamia
Rensho, hapohapo akaifungua mikono yake na
kisha kuifunga.
Mayowe yakatanda pale wale majingili walijikuta
wakiwa wameshikilia nyoka mikononi mwao.
Walipiga mayowe huku kila mmoja akitupa chini
kitu ambacho hapo awali kilikuwa ni bunduki.
“Kuja hapa?” aliamuru walipokuwa wanakimbia.
Wakatii na kurejea huku kila mmoja akipigwa
butwaa tena. Zilikuwa ni bunduki.
Wakaziokota kwa uoga…..
“Sasa mtafanya kazi ndogo tu kisha mtaondoka…
mnifuate haraka” akaamuru wakamfuata.
Wakalifikia kaburi la mama yake waziri mkuu
mstaafu….
“Mtafukua na kutoa jeneza…” alitoa maelezo
mafupi.
“Haraka!!” akaamuru. Wanaume waogopa kufa
wakabaki kushangaa ni kwa namna gani
watafukua kaburi lililojengewa.
“Mnaduwaa….wapuuzi sana nyie…haya nalitoa
jeneza huko chini nikilitoa mmojawenu analifunua
na kutoa hirizi nyekundu katika mwili wa
marehemu.
Rensho hakuwapa nafasi ya kufikiri.
Kindo alikuwa amejikojolea tayari baada ya dada
yule wa ajabu kubadili bunduki kuwa nyoka.
Getonga yeye alikuwa akitokwa jasho kwa fujo.
Haikuwa sinema kweli jeneza likatoka na kuwa
hewani, jambazi mwenye kipara akalivaa jeneza
akafunua. Akaingiza mkono katika mifupa
iliyosalia akatoka na hirizi.
“Wewe ni baba lao….” Rensho akamsifia huku
akiichukua ile hirizi na kisha akaifungua, upepo
ukavuma kidogo, jeneza likatoweka na hirizi nayo
ikatoweka.
“Uwe huru raisi wa watu wema…..” Rensho
akasema hakuna aliyemuelewa moja kwa moja.
“Mnaweza kwenda majambazi nawatakia kazi
njema!” aliwaaga kiutani….
WAKATI HUOHUO!!
Raisi wa jamuhuri ya muungano alikurupuka
kutoka kitandani, akili yake ambayo ilikuwa
ngumu sana kukubali kuwa Waziri mstaafu si mtu
mzuri ilikuwa imefunguka akajiona mjinga sana.
Akampigia simu IGP na kumweleza kuwa waziri
mstaafu hastahili huduma wala uangalizi wowote
ule wa kiafya.
Na sheria ichukue mkondo wake!! Akaagiza.
Walau IGP aliweza kutabasamu.
Akili ya Raisi ilikuwa imefunguka hatimaye.
*****
Makaburi ya CITY katika wilaya ya Temeke,
jeneza la mtoto mdogo lilikuwa juu tayari. Rensho
alilifunua lile jeneza huku machozi yakimtiririka.
“Baba kumzika mwana, kiunafiki kalia
Kaujaza umati sana, mama yangu kazimia
Baba asiye maana, kaidanganya dunia.
Narudi kuangamiza, huruma ka mbali nami.
Waziri si muungwana, ushirikina watumia.
Ikulu wataka sana, bila huruma waua.
Yote sasa ni bayana, wafungwe miaka mia.
Narudi kuangamiza, huruma kaa mbali nami.
Rensho amka tena, Myaka kumi karibia.
U hai si mfu tena, najua unasikia.
Watu hawana maana, ukiwaona kimbia
Narudi kuangamiza, huruma kaa mbali nami.
Rensho aliimba lile shairi huku akibubujikwa na
machozi. Kisha akaingiza mkono wake na kutoka
na hirizi nyeusi. Akaifungua na kuitupa kwa
Kindo. Kindo akajirusha nyuma huku akipiga
kelele.
“Kitovu chako hicho unakikimbia tena….”
Alishangaa Rensho kisha akaingiza tena mkono
katika lile jeneza.
Akatulia kwa muda mrefu kisha akaliachia jeneza
likaanguka mle kaburini.
“Getonga!” alimuita huku akiwa ameinama
bado……Getonga akasogea kwa Rensho.
“Nifungue hirizi kiunoni mwangu…..” alimweleza,
Getonga ambaye uoga ulikuwa umepungua
alimfunua Rensho na kutoka na hirizi kubwa.
“Itupe kaburini, usiniulize niliivaa saa ngapi?”
Getonga akaitupa….
“MWISHO” alisema huku akitabasamu.
“Sasa ninalo joto la kike nina kila kitu cha kuitwa
mwanadamu na sina ulinzi tena wa kishetani.”
Alizungumza huku dhahiri akionekana kuwa na
furaha kubwa.
“Tunalala kwa nani leo..wengine nd’o tunaingia
kuyaanza maisha sasa…..vipi huku duniani
lakini?” aliuliza Rensho huku wakiifuata njia na
kutoka katika makaburi yale.
Getonga akashauri waende nyumbani kwake kwa
sababu sio mbali sana. Wakatembea kwa miguu
kufuata barabara. Kila kitu ambacho Rensho
alikuwa kikiona laikuwa anauliza ni kitu gani.
Kindo na Getonga wakafanya shughuli pevu ya
kumjibu kila swali.
Hakika Rensho alikuwa mpya katika dunia!
Walifika nyumbani kwa Getonga, hawakumkuta
Anitha lakini Salome alikuwepo nje ya nyuma.
Salome akamkimbilia Kindo na kumkumbatia.
“Anitha yupo wapi?”
“Ameenda kwao”
“Na wewe mbona upo hapa nje!!” Getonga
akahoji.
“Mwenyekiti anadai kuwa nyumba hii imefungwa
na serikali…”
“Yupo wapi mjumbe?” aliuliza, Salome
akanyoosha kwa kidole. Getonga akaelekea
nyumbani kwa mjumbe, wakasalimiana kwa
bashasha kubwa huku mjumbe akishangaa jinsi
Getonga alivyokuwa amechafuka.
“Ni simulizi ndefu?” alimjibu.
“Polisi wanakutafuta lakini?”
“Ukweli upo wazi usijali kila kitu kitaenda sawa
naomba unihifadhie hawa wageni wangu. Kwa
usiku wa leo tu, naamini kuwa kesho nyumba
yangu itafunguliwa na maisha yataendelea…”
alimweleza kwa kifupi. Mjumbe akakubali kutoa
msaada huo.
******
KIHITIMISHO!!!
SIKU iliyofuata mambo yalikuwa motomoto,
magazeti yalilipuka kwa habari juu ya waziri
mkuu mstaafu na maamuzi ya raisi juu yake.
Dar es salaam palikuwa na hekaheka, yule
mwandishi aliyetoroka mahabusu kimiujiza
alikuwa mtaani, na yule mshtakiwa mwenza
aliyetoroka pamoja naye alikuwa amepatikana..
Mwanadada anayesadikika kuchuna ngozi za
wanaume wawili alikuwa jijini Dar es salaam.
Mwanadada wa kuitwa Rensho huyu nd’o alitikisa
jiji zaidi. Kila mtu alitaka kujua Rensho ni kimbe
gani hadi akawa anatokea katika miili ya watu
wakifa baada ya kuvuja damu kwa muda mrefu.
Inspekta aliyerukwa akili alikuwa timamu kabisa
akizisikia habari hizi katika redio.
Wanawake waliokuwa wakivuja damu nao
zilikuwa zimekoma kabisa.
Kwa kifupi kila mkazi wa Dar alikuwa na jambo la
kuzungumza.
Maofisini kazi zilikuwa haziendi kila mmoja
alitaka kujua nini hatma ya haya yote.
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu, waziri
mstaafu na mzee Nshomile walikiri makosa yao
bila kupinga. Walikubali kuwa nyuma ya majanga
yote yaliyotokea.
BAADA ya siku kadhaa hukumu ya kunyongwa
hadi kufa ilikuwa halali yao.
Rensho na wenzake wakiachwa huru kabisa.
Anitha alirejea kwenye ndoa yake baada ya
wazazi wake kumsihi sana asidai talaka kwani
mumewe alikuwa kazini nd’o maana akajikuta
akiingia katika mkasa huo na hata kama hiyo
haitoshi kwa ushahidi wake mwenyewe ni kwa
kiasi kikubwa alijaribu kuipigania familia yake.
Salome na Kindo wakarejea kuwa wamoja huku
Rensho akiyaanza maisha yake kwa kuishi
nyumbani kwao Getonga.
JIONI moja katika fukwe za coco maeneo flani
nje kidogo ya jiji.
Kindo, Salome, Rensho, Anitha, Getonga na Eva
walikuwa wameamua kukutana kwa ajili ya
kusimuliana mawili matatu. Kila mmoja alisema
lake juu ya mkasa walioupitia.
Getonga ambaye alikuwa amekaa kimya muda
mrefu aliongea wa mwisho.
“Katika mikasa yote niliyowahi kupitia sijawahi
kupitia mkasa wenye kutia HOFU kama huu,
yaani kila nilipogusa ilikuwa ni hofu
tupu….nadhani hata nikiwaandikia makala
wasomaji na wao wataingiwa na hofu wakiwa
wanaisoma… kwa kifupi huu mkasa nitauita
HOFU”
“Amakweli HOFU” Salome alijazia na wengine
wote wakakubali kuwa ule mkasa ulijaa HOFU.
“Ila yote juu ya yote ashukuriwe Mungu maana
maisha yanaendelea!” Anitha alimalizia huku
akimuegemea Getonga begani kimahaba.
“Baba HOFU nd’o nini?” Eva naye akauliza kitoto
toto.
Kila mmoja akacheka kwa sauti ya juu.
Sauti zao za furaha zikamtoa katika hofu
mwandishi wa simulizi hii na kuamua kuitua
kalamu yake chini na kulifunika daftari ambalo
nyuma kabisa liliandikwa neno moja tu…….
“MWISHO”
NB: Tangu riwaya hii iandikwe mwaka 2013
haijawahi kufanyiwa uhakiki.... kumradhi kwa
makosa yoyote yaliyojitokeza.....
 
Kila chenye mwanzo hakikosi kua Na mwisho,
La muhimu ni kuwa Na mwisho mwema,huu umekuwa mwisho mwema
 
ASANTE SANA MKULU KWA RIWAYA YAKO SALUTE TO YOU HII NI HOFU KWELI
 
Back
Top Bottom