SEHEMU YA MWISHO PART ONE
Baada ya udhibiti huo, wakazifunua nyuso zao.
Alikuwa ni waziri mkuu mstaafu na aliyemdhibiti
Kindo alikuwa ni baba yake mzazi na Rensho.
Mzee Nshomile!!
Rensho ana kwa ana na baba yake!!! Rensho
alimtazama kwa hasira lakini pale alipo goti
lilikuwa halifanyi kazi na mwili ulikuwa dhaifu.
Hasira pekee nd’o ilimuongoza na kuamini kuwa
anaweza kumdhibiti yule mzee.
Lakini alikuwa na maadui watatu, waziri, baba
yake pamoja na mtumwa aliyesaliti utumwa
Queen!!
HATARI!!!
Nianze na nani sasa? Alijiuliza Rensho huku
akimlaani Queen kwa lile pigo ambalo lilitawanya
goti lake na kumfanya ashindwe kusimama.
Akapiga kite cha ghadhabu kuhu akiangaza
macho huku na kule kama kuna namna ya
kuweza kujinyofoa kutoka katika mikono ya watu
wabaya.
“Laiti kama mguu ungekuwa unafanya kazi
ningeweza hata kukimbia……lakini aah!! Huyu
kaka na familia yake wangekufa vibaya.” Alizidi
kuwaza na kuwazua.
Akiwa hajapata jibu sahihi, mara mzee Nshomile
alimpiga Kindo kwa kutumia kiganja chake
maeneo ya shingoni, akalainika na kupoteza
fahamu. Kisha akamfuata Rensho na kusimama
mbele yake.
Ili kuthibitisha hasira kali aliyonayo mbele ya yule
binti akamuuliza swali moja.
“Mimi nani yako?” akahoji kwa hasira.
“Sikufahamu.” Rensho alijibu kwa jeuri huku
akijua fika kuwa yule ni baba yake.
Mzee Nshomile bila kusogeza hatua nyuma
akanyanyua mguu wa kulia akamtishia kama
anamchabanga usoni. Rensho kwa kutumia
mikono akajaribu kuzuia lakini ghafla ule mguu
ukatua katika goti lililosambaratishwa na Queen.
Rensho akapiga mayowe makali ya kutangaza
maumivu.
Tendo lile la yule mzee kumsaga Rensho gotini
likamtia hasira Getonga akafanya kujitingisha
kidogo ili kutetea usalama wa Rensho lakini pale
pale alikatwa kofi kali ya usoni, uso ukawaka
moto na sekunde kadhaa mbele akaanza kutokwa
damu puani.
“Mwanadamu mpumbavu wewe hauna la kutuzuia
sisi…dunia hii ni yetu!” Waziri mstaafu ambaye
alikuwa amemdhibiti Queen alisema kwa kejeli.
Getonga akanyanyua macho yake
wakagonganisha na yule waziri mstaafu.
“Whaaat…Gerlad Getonga Mosenya….. son of the
bitch!!” akawaka kwa hasira yule mzee, Getonga
naye akaduwaa hakutegemea kuwa yulew
angeweza kuwa waziri mkuu mstaafu. Waziri
ambaye aliwahi kuingia katika mzozo na gazeti
ambalo Getonga alikuwa akiandikia makala.
Makala iliyomponda sana kuwa ni mbadhlifu wa
fedha na maamuzi yake hayajanyooka, makala
ambayo iliwapa nafasi wapinzani kukidhoofisha
chama tawala.
Mafahari hawa wanakutana katika dunia nyingine.
Ni aidha Getonga atoke hai na kwenda kuandika
makala kuwa raisi mtarajiwa ni mshirikina
amaafe ili kila kitu kiende salama.
“Njoo umshike huyu…mdhibiti kabisa” Waziri
alimwamuru Nshomile naye akatenda vile mara
moja.
Waziri akawa huru, akamsogelea Getonga
ambaye alikuwa akivuja damu bado.
“Ulikuja huku pia kuchukua habari eeh!” Waziri
alimdhihaki, kisha akaendelea, “ulinichafua
magazetini enzi nikiwa waziri…nasikitika kuwa
licha ya kukutanishwa na kupatanishewa ni
kwamba hadi leo sijawahi kukusamehe nina
hasira na wewe na leo nitazimisha ndoto zako
zote ulizonazo mshenzi wewe.” Alizungumza kwa
ghadhabu huku akiwa ameikaba shingo ya
Getonga.
Na kwa kitendo cha sekunde chache tayari
alikuwa amemchapa makofiu mawili makali.
Damu ikazidi kuvuja huku Rensho akiishia kuumia
tu asiweze kumsaidia Getonga.
“Babaaaa!” sauti ya mtoto mdogo ilisikika ikiita,
matukio yote yakasimama.
Masikio ya Getonga yakatambua kuwa huyo ni
Anitha alikuwa amesikia kilio chake kikuu cha
maumivu.
“Nani huyo?” Waziri alimuhoji Nshomile.
“Kama ni mwanadamu nyonga mara moja…”
alitoa amri Waziri . nshomile akiwa amemkaba
Queen alikubali alichoelekezwa na wakaongozana
kwenda sauti ya mtoto ilipotokea.
Queen alikuwa akimchukia Getonga lakini
hakuwahi kumchukia mkewe na hasahasa yule
mtoto, alimpenda sana.
Ile amri ya ukikamata nyonga ilimshtua na hasira
zikampanda hakuwa tayari kushuhudia kifo cha
yule mtoto.
Nshomile asiyekuwa na taarifa kabisa wala
mategemeo katika lile tukio, alijikuta akimlegezea
ukabaji Queen na kumpuuzia akimchukulia kama
wanadamu wengine.
Hilo lilikuwa kosa kubwa sana kwa mzee huyu na
ambalo lilizua varangati.
Queen aliinama ghafla na kujitoa katika mikono
ya Nshomile, kisha upesi akakunjuka teke kali na
kumchabanga mgongo akajibamiza katika vyuma
vilivyokuwa mbele yake.
Hapohapo akamrukia tena na kumpiga ngumi ya
kisogo kali sana, mzee Nshomile akaishia kuona
maluweluwe na kuanguka chini.
Queen akamnyakua Eva (mtoto wa Getonga) na
kisha akatimua mbio….. ile anafika mlangoni
akatambua kuwa bado yeye si mwanadamu
kamili na bado anamhitaji Kindo ili aweze
kumrejesha tena katika ubinadamu. Akakata
tamaa.
“Eva mpenzi…..” akamuita yule mtoto kwa sauti
ya chini.
“Bee dada..” Eva akaitika kwa sauti ya kitoto.
“Naomba unisikie na ujaribu tu kunielewa sawa
mama eeh! Unauona ule mlango pale..”
akamnyanyua kichwa na kumuelekezea kule,
“Kimbia nenda ukaufungue na uingie ujifiche
pale, usilie wala usipige kelele hata kidogo…
naenda kumleta baba sawa eeeh!!...sawa
mamangu?” alimsihi kwa sauti tulivu ili aweze
kuelewa.
Japokuwa alikuwa mtoto yale maisha ya utata
yaliyokuwa yanaendelea katika jengo lile na kile
kilio alichokisikia kutoka kwa baba yake tyari
alitambua kuwa kuna hatari kubwa eneo lile.
Akafuata aliyoelekezwa!!
Eva akaanza kukimbia kuelekea ule mlango
ulipokuwa, Queen alimtazama vyema ili afike
kabisa na kujifungia nyuma ya ule mlango.
Tabasamu likamtoka kwa wepesi wa yule mtoto
mdogo, akaufungua mlango, ile anatak kuingia
ajifungie tu likatokea jambo ambalo lilivuruga
utaratibu.
Katoka paka katika ficho lile, Eva akapiga kelele
za uoga.
Queen akabaki kukodoa macho akimtazama jinsi
Eva alivyokuwa anatapatapa.
Kelele za Eva zikamkurupua na mzee Nshomile
kutoka pale chini, kabla Queen hajajua afanye
nini alivisikia vishindo vya mwanadamu kusogea
katika eneo lile. Akajipanga kumkabili…..
Ila mwenzake alikuwa amejipanga zaidi,
mawenge yakamkumba baada ya kupondwa na
kitu kizito kisogoni. Ile anaugulia maumivu
akashtuka akiwa amebanwa mbavu zake mbili za
chini kwa nguvu mno. Alijaribu kufyatuka lakini
hakufanikiwa…maumivu yalikuwa makali mno.
Queen akaanza kulia kama mtoto mdogo. Lakini
kama ile haitoshi akapigwa ngumi kali kiunoni,
ngumi iliyopigwa kitaalamu kwa ajili ya kuvunja
tu!
Queen akalainika na kumwangukia yule bwana
huku akiendelea kuugulia.
Mzee Nshomile akamchukua begani kama mzigo
tu usiokuwa na thamani yoyote, kisha akamfuata
Eva pale alipo akamvuta mkono kwa nguvu sana
Eva akaanza kulia.
“Mwache mtoto wangu nasema?” sauti kutoka
katika ficho jingine ikatoka, Nshomile akaifuata
kwa tahadhari akamkuta mama yake Eva
(Anitha) akiwa amefungwa kamba mikono
yake….. akamfungua na kumpa pigo moja la
kulainisha.
Baada ya dakika kadhaa kwenye ukumbi wa
mapambano alikuwepo Nshomile na mwenzake
Waziri mstaafu huku mateka wao wakiwa
wameongezeka idadi.
Rensho, Getonga, Kindo, Queen, Anitha (mke wa
Getonga), Eva (mtoto wa Getonga). Ukumbi
ulikuwa umechafuka damu. Ni Eva pekee ambaye
alikuwa havuji damu.
*****
FAMILIA nzima ilikuwa ikimtazama Getonga, naye
hakuwa na la kufanya zaidi ya kujisikia vibaya
kukaidi ushauri aliopewa na mkewe kuwa ajiweke
mbali kabisa na mambo ya uandishi wa habari za
kipelelezi kwani ni hatari kwa maisha yake.
Alimtazama Anitha mkewe akamtazama na Eva.
Machozi yakamtiririka kwa uchungu mkuu,
uchungu wa kuamini kuwa baada ya vifo vyao
kama kweli kuna mahali watakutana basi
watamlaumu bila kumsamehe kamwe.
Ni heri wakutane duniani wakiwa hai, ataomba
msamaha na maisha yao ya ndoa yataendelea.
“We kinyamkera ulidhani kuwaua wenzeti nd’o
utatoka na wewe ukiwa hai ili ukatuaibishe dunia
sivyo?” Waziri alimuhoji Rensho aliyekuwa hoi.
“Sasa utashuhudia vifo vya hawa rafiki zako
mmoja baada ya mwingine halafu wewe utake
usitake utatimiza ulichotakiwa kutimiza….na
ukileta ubishi ni kifo cha moja kwa moja…wewe
ni mtoto na utabaki kuwa mtoto tu..” Nshomile
akaongezea.
Rensho hakujibu kitu alikuwa akihema juu juu tu
kutokana na maumivu makali hasahasa ya goti
lililotawqanyika.
“Queen, tunafanyaje sasa…’ hatimaye
alimnong’oneza Queen, ambaye naye alikuwa hoi
akiwa amevunjika kiuno.
“Wangetuachia hata dakika kumi tungebusti ila
bila hivyo, naona tunateketea hapa…” alijibu
akiwa amekata tamaa.
Mzee Nshomile alimfuata Eva akamshika mkono
na kumvuta akasimama wima.
“Niue mimi umuache mwanangu hai…” Getonga
akajikaza na kusema maneno yale ya kijasiri….
Waziri mstaafu akamrukia na kumchapa ngumi
kali juu ya jicho, akachanika vibaya mno. Damu
ikaanza kuvuja. Eva akaanza kulia kwa hisia kali
za kuona baba yake akiteseka.
Waziri na mwenzake hawakujali hayo.
Na wakati haya yakitokea ilikuwa yapata saa
kumi na mbili alfajiri.
Rensho aliwatazama kwa uchungu mkubwa
majeruhi waliomzunguka, alimuonea huruma hadi
Queen ambaye alihusika katika kulisambaratisha
goti lake wakiwa katika mapambano. Alijua kuwa
wote hawana nguvu za kuwadhibiti watu wale
lakini hata yeye alikuwa dhaifu sana…..
Rensho akajaribu bahati ya mwisho kabisa huku
akijisemea nafsini mwake, iwapo hiyo nayo
itashindikana basi tena atakuwa radhi kushuhudia
vifo vya mateso kwa watu wale.
“Muulize Kindo…. Salome jina lake la kikabila ni
nani…jibu muhimu na haraka” alimnong’oneza
Queen, Queen naye akamnong’oneza Anitha,
Anitha akamuuliza Kindo aliyekuwa hoi.
“Ndema” Kindo akamjibu kwa shida huku akiwa
na dakika takribani kumi tangu arejewe na
fahamu zake.
Jibu likamfikia Rensho!!
Akayafumba macho yake. Na kisha kuzua
mtafaruku baada ya kuanza kupiga makelele.
“Ndema weee….Ndema weeeee amka
Ndema….amka…mwili hauiwezi kuishi bila roho
na hata roho haiwezi kuishi bila mwili….Ndema
weeeee Ndema njoo sasa….. amka Ndema..”
“Pumbavu unasema nini wewe..” Waziri alimtusi
kwa ghadhabu huku akimwendea kwa kasi.
Nshomile alikuwa anajiandaa kukikata kichwa
cha Eva kwa kutumia kisu kikubwa.
Upepo haukuvuma sana hadi kusababisha
milango kuvunjika. Hilo liliwashangaza wote hadi
Rensho mwenyewe.
Lakini akaamini kuwa ukweli kabisa mwili
hauwezi kuishi bila roho.
Baada ya mlango ule kuvunja katikati ya ule
ukumbi akaingia mwanadada mwenye mimba…
macho yake yalitangaza hasira kali sana, ujumbe
ulikifikia kiumbe kilichokuwa katika tumbo lake.
“Salomeeee!!: Kindo alipiga kelele huku
akijitutumua ainuke lakini yule alikuwa salome
mwili tu, akili yake ilikuwa imevurugika vibaya
mno na alikuwa anachemkwa na hasira.
“Wewe ni nani mwanamke…” waziri mkuu
mstaafu alimuuliza. Lakini hakupata jibu badala
yake Salome aliendelea kuangaza huku na kule.
Waziri akamfuata kwa fujo akidhani kuwa itakuwa
rahisi kiasi kile.
Salome akajirudisha nyuma kidogo kisha
akafyatuka kichwa kikali sana katika kinywa cha
waziri, meno mawili ya mbele yakasalimu amri
akayatema huku akiugulia maumivu.
Mzee Nshomile akajirusha ili kumsaidia waziri,
Salome akajikunja kidogo lile teke kali likamkosa,
akajizungusha hewani na teke la mzunguko, mzee
Nsomile akainama likamkosa. Akataka kumpiga
Salome ngumi katikati ya mapaja lakini alikuwa
mwepesi sana akawahi kujirusha kisha kama
afanyavyo kondoo akamfuata hewani kwa
kutumia kichwa, ni heri aliwahi kukwepa kichwa
kile kisikutane na kifua chake maana angepasuka
pasuka kama ulivyopasuka ule mkono uliokutana
na dhahama ile. Nshomile akaugulia maumivu,
huku akisimama wina na kujaribu kumkabili
Salome huku akiwa na majeraha.
Salome alikuwa hajasema neno lolote lile….tangu
aingie katika kile chumba.
Waziri alijitutumua na kusimama akiwa nyuma ya
Salome akaandaa shambulizi kwa kutumia chuma
alichokiokota pale ndani.
Hakujua kama ni roho ipo katika utendaji na
inaona kila kona.
Akakitupa kile chuma kwa nguvu, nia ikiwa
kukitandika kisogo cha Salome….
Binti akainama chuma kikapita kwa kasi na
kumtandika Nshomile usoni akatokwa na yowe
kubwa kisha akaanguka chini.
Waziri akajirusha kwa kutanguliza miguu miwili
mzima mzima ili kumuwahi Salome lakini
haikuwa rahisi kama alivyodhani. Salome
akakwepa kidogo kisha baada ya waziri kutua
chini na yeye akajirusha hewani na kutua katika
magoti yake.
Hapo akatokwa na ukelele mkubwa wa huku
akiyasaga magoti ya waziri mkuu mstaafu.
Hali ikatulia huku Salome akiwa amefura kwa
hasira kali sana.
“Wamalize wamalizeee….” Rensho alimsihi
bSalome lakini akijua kuwa anazungumza na ile
roho ndani yake.
“Sitaua mtu …” Salome alijibu. Rensho akawa
mpole. Na wakati huohuo Salome alianguka chini
na kutokwa na ile hali aliyokuwanayo akabaki
kuwa Salome halisi.
Rensho alipogeuka kuangaza kushoto na kulia
akagundua kuwa kuna watu walikuwa
wamepungua…..
Kindo na Queen. Wako wapi hawa? Alijiuliza.
Na mara kindo na Queen wakaingia wakiwa
katika afya zao imara.
Walikuwa wamebusti tayari.
“Kindo..” Salome aliita baada ya kumuona Kindo
akiingia pale ndani.
Kindo akaingia katika mchecheto, ni kweli
alikuwa akimpenda sana Salome kwa dhati.
Lakini katika mazingira yale ili atoke salama
ilikuwa lazima ajihusishe na Queen.
“Ni nani huyu kwani?” Queen alihoji.
“Huyo ni mume wangu..” Salome alitoa jibu……
“Shhhh! Komea hapo hapo mwanamke.”
“Hey! Jamani tunatakiwa kuwa wamoja jamani,
ugomvi wa nini tena? Tunatakiwa kutoka humu
ndani..” Rensho aliyekuwa amekaa pale chini
alionya. Wakanyamza.
Lakini Queen alikuwa amefikiria jambo, hakuwa
tayari kutoka mle ndani huku akijua kuwa Kindo
si mali yake. Tayari alikuwa amekolea. Wivu wa
kimapenzi ukaanza kumshambulia.
Na hapo akafanya tendo la kipuuzi kuliko yote
aliyowahi kuyafanya.
BOFYA LIKE, TOA MAONI YAKO