Riwaya: HOFU

SEHEMU YA TISA
Kisembe baada ya kufanikiwa kuidhibiti ile damu
kidogo, akavaa nguo zake hovyohovyo. Akatoka
nje na kuingia ndani ya gari lake, nia yake ikiwa
kuwahi huduma hospitali yoyote ile…
Haikuwa nyepesi kama alivyoweza kudhani!!
Asubuhi ya siku iliyofuata taarifa za kustua nchi
zikatapakaa.
Inspekta Juma Kisembe amekutwa amekufa
baada ya kuvuja damu nyingi akiwa ndani ya gari
lake kando kando ya barabara ya Mandela jijini.
Inspekta alikuwa akivuja damu katika sehemu
zake za siri!!
Kifo kama cha mume mwenzake wa siri kwa binti
Maria, Dennis!!
***
MWANDISHI AJIINGIZA KWENYE UTATA WA
HOFU!!
EBOLA….. watafiti wakatoa taarifa kuwa Inspekta
Kisembe amekufa kutokana na ugonjwa huo.
Ebola? Vyombo vya habari vikahoji!!
Ebola gani hiyo iliyomtoa damu sehemu moja tu
katika mwili wake!! Ebola humfanya mgonjwa
avuje damu katika kila tundu lililopo katika mwili
wake.
Hii Ebola ya Inspekta mbona ya aina yake!!
“Kwa hiyo tuwatangazie wananchi kuwa kuna
mlipuko wa gonjwa hilo hatari!!” mwandishi wa
habari akamchimba msemaji wa jeshi la polisi.
“Kutokana na taarifa ya daktari amesema
yawezekana ni Ebola maana ugonjwa mwingine
haujaonekana…”
“Lakini hata Gonorea nayo humtoa mtu damu
mkuu, huoni taarifa ya gonjwa la ebola bila
kuthibitishwa ni sawasawa na kuwajengea
wananchi hofu makusudi!!” mwandishi
akamchimba zaidi, kisha bila kumpa muda wa
kujibu akaongezea jingine, “ Na hawa wenzetu
akiwemo bwana Patrick Masawe na wao
wamekufa vifo vya aina hii… na hadi sasa maiti
hazijakabidhiwa kwa ndugu na kilichowaua
hamjakisema wazi, mbona hiki kifo cha mzee
Kisembe ufumbuzi wake umepatikana upesi sana
mheshimiwa?” mara simu ikakatwa!!
Mwandishi hakujisumbua kupiga tena maana
alijua imekatwa maksudi na hata mpata hewani
tena msemaji huyo aliyezidiwa na mzigo wa
maswali ya kuthibitisha uhakika wa kifo cha
inspekta Kisembe.
Hiyo ilikuwa kawaida ya wakubwa wakiulizwa
maswali magumu!!
Mwandishi yule akajinyoosha katika kochi
alilokuwa amekaa, kisha kitu kikamkuna ghafla
kuwa asipuuzie tukio hilo la inspekta kufa katika
hali ya kustaajabisha.
Akautazama ukuta kisha akafumba macho baada
ya kuiona picha kubwa ya msichana mrembo
kiasi ambaye amepauka haswa. Mwandishi
akamkumbuka Nadia, akaukumbuka mkasa wa
Usilie Nadia ulivyokuwa wa kusisimua, kitabu
chake ambacho kilimpeleka Musoma na kisha
kuishia Mwanza.
Akageuka upande mwingine akakutana na picha
nyingine iliyobuniwa haswa na kupendeza,
maandishi yakasomeka ‘Anti Ezekiel.’
Akalikumbuka tukio hili katika hekaheka zake za
uandishi.
Tukio ambalo almanusura liondoke na uhai wake,
badala yake mkewe na mama yake mzazi
wakapotelea katika tukio hilo.
Tukio hilo la kugundua mkakati kabambe wa
kuusambaza ushoga katika nchi ya Tanzania kwa
kuwateka watoto wadogo wa kiume kisha
kuwahifadhi katika ngome iliyojengwa ardhini na
kuwafundisha tabia za kishoga.
Ufumbuzi huu ulimfanya kuwa mtu maarufu na
wa kuheshimiwa!!
Akainama chini na kuzidi kuwashwa kufuatilia
tukio la kifo cha inspekta wa polisi na watu zaidi
ya kumi na tano. Wote kwa kutokwa damu
nyingi!!
Lazima kuna kitu hapa!! Aliwaza Gerlad Getonga,
mtunzi wa vitabu vya Usilie Nadia na kisha
akaandika kitabu cha kihistoria kile cha Anti
Ezekiel, mkasa wa kweli kabisa uliotaka
kuondoka na roho yake huko Iringa.
Alitamani sana kumshirikisha mkewe Anitha,
lakini akatambua kuwa lazima atakutana na
vikwazo vikali, kwa sababu tukio la Michigan
ambapo mkasa wa Anti Ezekiel ulimalizia wote
waliponea chupuchupu.
Getonga akaitazama picha ya Eva mtoto wake,
machozi yakamlenga lenga alipofikiria kuwa
atamuacha kwa muda wakati akilifuatilia kwa
ukaribu tukio hilo.
“Hapa hakuna hatari yoyote bila shaka ni katukio
kadogo tu..” alijipa moyo huku akipita maamuzi
ya kufuatilia mkasa huu tofauti na waandishi
wengine!!
Getonga akaondoka bila kuaga, tayari alikuwa na
vifaa vyake muhimu kwa ajili ya kazi hiyo.
Laiti kama angejua kuwa tukio lile sio dogo kama
adhaniavyo ni heri angejiepusha nalo!!!
Hakujua kuwa madhara yake ni ya papo kwa
hapo zaidi ya yaliyomkuta wakati akifuatilia
mkasa wa Anti Ezekiel.
Akajiingiza kichwakichwa pasi na hofu yoyote!!
****
Alikuwa amejitahidi na kuachana na matumizi ya
sigara, lakini pombe hakuweza kuiacha. Angalau
kwa siku chupa mbili kwa ajili ya kuichangamsha
akili yake kisha anaendelea na mambo mengine
halafu jioni anajumuika katika vijiwe vya kahawa.
Jioni hii akiwa amemaliza mizunguko ya siku
hiyo akitumia usafiri wa pikipiki binafsi alikuwa
amevuna mambo kadhaa ambayo yalimpa
mwanga juu ya wapi anaweza kuanzia.
Katika daftari lake dogo akaandika mambo hayo
kwa ufupi sana. Ambapo yeyote hata mkewe
akilikwapua daftari lile hakuna ambalo angeweza
kuambulia.
Kindo- Mwendawazimu anayetamka neno moja
tu! =Rensho. Huyu SIMJUI
Maria- inasemekana alikuwa hawara yake
Inspekta. =SIMJUI
Sarah- Rafiki kipenzi wa Maria. =SIMJUI
Kijana- alionekana katika nyumba ya Maria usiku.
=SIMJUI
“Kila mtu simjui! Duh pagumu hapa” Alijikuta
akisema kwa sauti ya juu.
“Unataka kumjua nani?” sauti ya Anitha
ikamkurupua kutoka katika mawazo yake.
“Baba naye kwa kuongea mwenyewe loooh!!”
sauti ya kitoto ya Eva ikapeperusha swali la
Anitha, wakajikuta wakicheka huku wakimtazama
Eva akijifinyafinya uso wake.
Getonga akarejea katika mawazo yake tena!!
Akalitazama daftari lake na kuendelea kusoma.
Deniss- alikuwa hawara wa Maria. =AMEKUFA!!
Inspekta Kisembe- alikuwa hawara wa Maria. =
AMEKUFA
“Mahawara nao wote wamekufa!! ” akajiuliza
safari hii hakutoa sauti nje.
Kuna kitu hapa!! Akamaliza kwa kujipigia makofi,
Eva na Anitha wasijue lolote linaloendelea.
Usiku huu ukapita Getonga akijipongeza kwa
kujua mambo kadhaa ambayo hakuyajua.
Asubuhi alichelewa kuamka!! Na alipoamka
alikutana na mkewe akiwa anacheka.
“Nini tena wewe kucheka asubuhi asubuhi..”
“Waandishi mna mambo nyie dah siwawezi. Ila
nashukuru hata ulivyojiweka mbali na mambo
hayo.”
“tumefanya kituko gani tena.”
“Si mwili wa Inspekta huyu aliyekufa kwa
ugonjwa wa Ebola….”
“Nani, Inspekta Kisembe ama…”
“Ehee huyohuyo… eti nimesikia magazetini kuwa
kuna raia wanadai kuwa marehemu amekutwa na
maneno gani sijui kwa hiyo inasemekana ni u-
freemanson umemuua dah!! Maiti hana la
kujitetea kwa kweli…” alisema haya huku akiwa
bado anatabasamu.
“Maneno tena? Wapi” Getonga aliendelea kuhoji
kwa shauku.
“Rensho sijui Renshi…ila wamesema ni jina lenye
herufi sita kwa hiyo ni Freemason…. Kweli
hamna dogo waandishi…”
Gerlad Getonga akauficha mshtuko wake,
akaguna na kuendelea na shughuli za kusafisha
kinywa chake.
Rensho!! Hilo neno nimewahi kulisikia wapi?
Akajiuliza kimya kimya huku akitamani kujiandaa
upesi akanunue hilo gazeti linalodai kuwa
Inspekta alikutwa na alama.
Baada ya kuoga alirejea chumbani, akachukua
kidaftari chake kidogo
Mstari wa kwanza kabisa wa harakati zake
akakutana na neno.
Kindo- chizi anayetamka neno Rensho pekee.
Upesi akaongezea maneno chini yake.
Rensho ni nani? Kisha akakihifadhi tena.
****
Gari dogo aina ya Toyota Carina lilisimama katika
maegesho ya magari yasiyokuwa rasmi maeneo
ya Kariakoo mtaa wa gerezani. Vioo vikashushwa
na aliyekuwa anaendesha gari hilo.
Akaangaza huku na kule akiwa ameinyoosha
shingo yake akaona alichohitaji kukiona, kisha
akairudisha gari nyuma kidogo akaiingiza
barabarani. Akaendesha kwa muda mfupi akafikia
sehemu ya kuosha magari!!
Akaliacha gari likiwa linaoshwa pale, akaingia
mtaa wa tatu kutoka pale. Akaifikia nyumba
ambayo siku iliyopita alielekezwa kuwa Maria
alikuwa anaishi pale. Akiwa na kofia yake ya
pama kichwani akajiundia uenyeji, hakutaka
kumuuliza mtu yeyote yule juu ya mahali
anapoelekea.
Akaufikia mlango na kuanza kugonga! Hakupata
majibu na bado hakukata tamaa akaendelea
kugonga kama yu mwenyeji sana wa eneo lile.
Baada ya kujihakikishia kuwa hakuna mtu wa
kuufungua ule mlango, mwandishi huyu
mashuhuri Gerlad Getonga akaamua kukishusha
kitasa ili ahakikishe kuwa Maria aliufunga kabla
hajaondoka. Mlango ukafunguka, akatazama
kushoto na kulia. Hapakuwa nna mtu
anayemtazama, akaanza kuita jina la Maria huku
akiingiza kichwa chake ndani katika mfumo wa
kuchungulia.
Chumba hakikuwa na mwanga sana, lakini kile
kitendo cha kuufungua mlango tu na kuangaza
huku na huko akakutana na kitambulisho. Upesi
akainama na kukikwapua kisha akauegesha
mlango tena na kutoweka akiwa anajiamini
kabisa ili kuleta imani kwa yeyote yule ambaye
atakuwa amemtazama.
Hakujua kwa nini amechukua kile kitambulisho na
hakujua ni cha nani lakini huo ukawa mwanzo wa
hekaheka ya ajabu kabisa!! Lakini hakujua kuwa
alichelewa sana kugundua.
****
HAKIKA alionekana kama mwendawazimu!
Jinsi alivyovaa, jinsi alivyokuwa akihangahika
kuchorachora huku na huko. Mwanamama mtu
mzima alikuwa jirani na kijana huyo.
Gerlad Getonga akawasalimia wote wawili. Kabla
mama hajajibu, yule mwendawazimu kimtazamo
akaropoka maneno ambayo yalikuwa muhimu
sana kwa Getonga.
“Rensho….Rensho!!”
Getonga akatikisa kichwa kisha akamsalimia
mama tena, mama akajibu kwa upole kabisa
akiwa na dalili zote za kukata tamaa.
“We nawe unataka unisumbue na maswali kama
wenzako halafu upotee usirudi tena… hamna la
kunisaidia nyie watu sijui waandishi” alilalama
baada ya Getonga kujitambulisha kuwa ni
mwandishi wa kujitegemea na anataka
wazungumze naye juu ya tukio lilomsibu
mwanaye.
Jibu lile lilimkwaza lakini alitumia utashi wa hali
ya juu kumshawishi yule mama mzazi wa kijana
aitwaye Kindo kuzungumza naye.
Ukumbi ukabaki kuwa wa mama Kindo
“Najuta kuitwa mama, lakini mbaya zaidi najuta
kuzaa kisichokuwa chema!” akasita kisha akakaa
sawa na kuendelea, “Kindo hakutaka kunisikiliza
mimi, kaamua kufunga ndoa na huyo Rebeka
sijui. Nikamkataza katakata na kumweleza wazi
kuwa binafsi sijaridhia suala lake la kumuoa huyo
binti na kuachana na Salome. …..” mama akasita
tena na kumgeukia mwanaye aliyekuwa
akitazama kitu asichokijua.
Kindo asiyesema neno zaidi ya ‘Rensho’ alikuwa
anatetemeka huku akiwa amekodoa macho yake,
Getonga naye akafuatisha macho ya mama ana
wote kusaidiana kumtazama Kindo.
Amekuwaje huyu naye!! Mama mtu alijiuliza.
Na hapo likatokea tukio la ajabu kabisa
liliwaduwaza wawili hawa. Kindo akaanza
kuzungumza!!
“Mpe….mpe… mpe upesi…mama mpeni…mpeni
mama.. kaka mpe upesi.” aliyasema haya huku
akimtazama Getonga…. Badala ya kushtuka
Getonga alifanya tabasamu, kwani aliamini kuwa
Kindo ameanza kurejewa na fahamu zake tena,
hivyo atanufaika naye hasahasa kwa kufanya
mahojiano na mwanadamu pekee aliyetoka akiwa
hai katika tukio la kustaajabisha na wanadamu
zaidi ya kumi na nne kuuwawa kinyama na
kilichowaua kisijulikane popote.
“Mama, wakija waandishi wengine usiwaruhusu
kuongea na Kindo sawa.. watamvuruga akili
yake. Mimi kama nilivyokwambia nina nia ya
kukusaidia.
“Sawa mwanangu… nita…” mama akakatishwa na
kelele za Kindo tena, “Mpe upesi nasema.. mpe
kama kipo.. mpe..” alitoa karipio Kindo, Getonga
akatabasamu huku akizidi kuamini kuwa ni
fahamu zinamrejea Kindo.
Na hekaheka za kukata na shoka zikaanzia
hapa!!
Kindo akamvagaa na kumwangusha chini huku
akimkaba kwa nguvu sana shingo yake huku
akimsihi kwa maneno hayohayo kuwa ampe
kama kipo.
Getonga akakakamaa na kujitoa katika mikono ya
ya Kindo kwa juhudi zote, akahema juu juu huku
akimtazama Kindo na kutoamini kitu kilichotokea.
Kabla hajapumua vizuri na kujiweka sawa tena
mara alimwona Kindo akizidi kuyakodoa macho,
halafu akaanza kukifuatilia kitu ambacho Getonga
hakukiona.
Na wakati huo alimuona mama yake akiingia
ndani!!
“Mpe kaka.. mpe …mpe anaomba …mpe…”
aliyasema haya kwa sauti ya chini, Getonga
hakuelewa kitu. Lakini sasa alikuwa ameanza
kuingiwa na hofu!!
Wakati huohuo zikasikika kelele ndani ya nyumba
ya mama yake Kindo, alikuwa akilia kuomba
msaada. Getonga akatoka mbiombio mpaka
ndani kutazama kulikoni. Hapakuwa na kelele
tena.
Akakutana na sebule isiyotamanika kuitazama,
hata kama ni filamu ya kutisha lakini hii ilikuwa
maradufu.
Kichwa katika stuli, mguu mmoja ukining’inia
darini, paja likiwa sakafuni, na..na…….
Ilitisha kutazama vinginevyo. Damu mbichi
ilikuwa imetapakaa!!
Mama Kindo alikuwa ameuwawa kinyama ndani
ya sekunde kadhaa!!
Riadha aliyotimka Getonga mwenye kitambi cha
pesa hakuwahi kukimbia namna ile, alijikwaa
akaanguka akasimama, akaongeza mwendo.
Akapotea njia na kujirekebisha tena, akajitapikia
lakini hakujali!!
Kila aliyemtazama alihisi kuwa yawezekana ni
kibaka ama anayerukwa na akili. Lakini hakuna
aliyemjali, kila mmoja alikuwa na shughuli zake.
Hii ikawa siku ambayo Getonga asingeweza
kuisahau aidha kwa kuishi ama kwa kuwa
kuzimu.
Ukawa mwanzo wa moyo kudunda kwa kasi kila
mara, mwanzo wa kuikosa amani ya nafsi na
mwanzo mwingine wa kuishi kama kivuli, kivuli
kinachoogopa na kuogopwa pia!!
Mwanzo wa kujutia maamuzi!!
***Ni kitu gani kimehusika katika kifo hiki cha
mama yake Kindo….
**Na nini alichokiona Kindo!!!
MWANDISHI KAJIINGIZA KATIKA
ASIYOYAJUA….NINI KITAMTOKEA!!
Je atatupatia jibu na kutuliza HOFU YETU!!!
 
SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA
GERLAD GETONGA amejiingiza katika mkasa
asioujua chimbuko lake. Anajiundia maswali yake
ambayo anahitaji kupata majibu yake!
Wakati anaanza kuyatafuta majibu anaanza
kukutana na mambo ya ajabu ajabu katika mkasa
huu…..
Anaanza kwa kumsaka mama yake Kindo, ili ajue
ni kipi kilimsibu mwanaye hadi kushindwa
kusema neno jingine zaidi ya Rensho!!...
Rensho ni nani?
ENDELEA!!!
Wakati huohuo zikasikika kelele ndani ya nyumba
ya mama yake Kindo. Getonga akatoka mbiombio
mpaka ndani kutazama kulikoni.
Akakutana na sebule isiyotamanika kuitazama,
hata kama ni filamu ya kutisha lakini hii ilikuwa
maradufu.
Kichwa katika stuli, mguu mmoja ukining’inia
darini, paja likiwa sakafuni, na..na…….
Ilitisha kutazama vinginevyo. Damu ilikuwa
imetapakaa!!
Mama Kindo alikuwa ameuwawa kinyama ndani
ya sekunde kadhaa!!
Riadha aliyotimka Getonga mwenye kitambi cha
pesa hakuwa kukimbia namna ile, alijikwaa
akaanguka akasimama, akaongeza mwendo.
Akapotea njia na kujirekebisha tena.
Kila aliyemtazama alihisi kuwa yawezekana ni
kibaka. Lakini hakuna aliyemjali, kila mmoja
alikuwa na shughuli zake.
Hii ikawa siku ambayo Getonga asingeweza
kuisahau aidha kwa kuishi ama kwa kuwa
kuzimu.
Ukawa mwanzo wa moyo kudunda kwa kasi kila
mara, mwanzo wa kuikosa amani ya nafsi na
mwanzo mwingine wa kuishi kama kivuli, kivuli
kinachoogopa na kuogopwa pia!!
Mwanzo wa kujutia maamuzi!!
***
MBIO kali za Getonga ziliishia katika teksi
ambayo ilimpeleka nyumbani kwa Maria. Safari
hiii hakujali iwapo kuna watu wanamtazama ama
la! Aliufikia mlango moja kwa moja na kugonga
kwa fujo ili aweze kufunguliwa.
Badala ya mlango kufunguliwa alishangaa kusikia
kitasa kikifungwa.
Yumo! Alijisemea na hapo hapo akausukuma kwa
nguvu mpaka ndani. Akamkuta Maria akiwa
ametaharuki na akiwa ameanguka chini baada ya
kusukumwa ghafla bila kutarajia, alikuwqa
amenyanyua mikono yake juu kama anayesihi na
kuomba msamaha.
Kwa mawazo yake aliamini kabisa kuwa mbele
yake alikuwa ni askari.
“Maria…..” Getonga akamwita huku akiwa
anaurudishia mlango vyema. Maria hakuitika na
badala yake aliendelea kutetemeka tu .
“Nini kinatokea hapa Maria….mimi ni mtu mwema
huna haja ya kuogopa.. nahitaji kuzungumza na
wewe Maria…” Getonga aliendelea kusihi huku
akiwa anamkazia macho Maria ambaye alikuwa
akitazama beseni, macho ya Getonga yakahama
na kulifikia lile beseni.
Macho yakaongezeka ukubwa wake kwa sababu
ya kukodoa.
“Maria, damu za nini hizo ndani ya chumba
chako…. Maria ni wewe unaye… ni wewe
Maria…..” Getonga alisema kama anayesuta….
Maria akapata nguvu ya kuzungumza.
“Sijui lolote kaka yangu… sijui nd’o nimeingia
hapa ndani… sijui kitu..” alijitetea huku
akisimama na kuketi kitandani….. kisha
akaendelea, “Kama utaamua kunikamata,
utakuwa tu umeamua kakangu, yaani mimi sijui
lolote lile nimeingia humu ndani na kuikuta hali
hii, haki ya Mungu naapa.” Alijitetea huku sauti
yake ikitetemeka.
“Maria, sijaelewa kitu hebu niambie ni kitu gani
kimetokea hapa kwa ufupi maana mchana
nimeukuta mlango huu ukiwa wazi. Ni nani
alikuwa humu ndani? Ukweli wako utakuweka
huru..”
Maria akajikuta katika kilio cha kimya kimya
kisha akajikaza na kuzungumza, aliamua
kuzungumza ukweli kwa sababu alikuwa matatani
tayari katika jambo asilolijua hata kidogo.
Akauelezea ujio wa inspekta Kisembe nyumbani
kwake pia akaielezea hali yake ya kuvuja damu
bila kikomo na maajabu yaliyotokea baada ya
kukutana na Kisembe.
“Yaani ilikuwa ajabu, wakati natarajia kuaibika
mbele ya Kisembe na kisha kuchafua mashuka
nikajikuta nipo sawa kabisa bila hata tone la
damu……” akaendelea kujieleza hadi jinsi
alivyoondoka na kumwacha Kisembe mle ndani
na hapo aliporejea nd’o anakutana na hali hiyo ya
damu kuwa katika beseni lake la kuogea.
Getonga alimsikiliza kwa makini huku mapigo
yake ya moyoi yakiongeza kasi na wakati
mwingine kupungua, hasahasa alipokikumbuka
kifo cha kutisha kupita vyote alivyowahi
kuvishuhudia.
Kifo cha mama Kindo!!
“Na unamfahamu vipi Samson? Na mara yake ya
mwisho kuja hapa ni lini..”
“Sam ni mpenzi wangu pia, ana majuma matatu
tangu aje hapa mara ya mwisho…angeweza kuja
siku za hivi karibuni lakini alipata janga la
kuwapoteza rafiki zake wawili, afande huwezi
amini kuwa na hao rafiki zake wamekufa kwa
kupoteza damu….”
“Unamaanisha wamekufa kama Inspekta
Kisembe sivyo?” Getonga akakolezea.
“Nini? Inspekta amekufa? Lini? Wapi eeh!! Mungu
weee!!” Maria alitaharuki kusikia taarifa hiyo kwa
mara ya kwanza katika masikio yake. Akahaha
huku na kule, Getonga akamtuliza na kisha
kumpa hali halisi juu ya tukio hilo la maajabu.
“Maria, nahitaji kuonana na Sam usiku huu huu…
hii hali si ya kawaida na ni lazima jibu lipatikane
upesi kabla mauaji hayajaendelea. Ninauhitaji
sana ushirikiano wako” Getonga akamsihi Maria
kwa upole sana.
Wakaelewana nna kuondoka wakiiacha ile damu
ikiwa palepale. Wakaufunga mlango kwa kitasa.
****
CHUMBA kilionekana kidogo na godoro alilozoea
kuliita mke wake wa pili lilionekana kumkera siku
hiyo, halikuwa laini kama siku zote na
halikunesanesa.
Alijigeuza huku na kule ili aupate usingizi lakini
hali ilikuwa tete. Hakuupata usingizi.
Kila alipofumba macho alikutana na picha ya
ajabu sana mnachoni mwake, damu nzito katika
beseni!! Chumbani kwa mpenzi wake wa siku
nyingi.
Na kwa jinsi alivyozizoea damu, alitambua mara
moja kuwa ile ilikuwa damu ya mwanadamu.
Swali moja likabaki kumuumiza kichwa, ni mpenzi
wake ameuwawa ama ni yeye ameua. Wakati
anataka kulipuuzia hili inakuja picha ya yule dada
wa kubakwa na akina hayati Don na Deniss.
Sam akaukosa utulivu, akasimama na kuliendea
jokofu akachukua maji ya baridi, akaketi katika
sofa na kuamua kuwasha luninga aweze
kutazamna mawili matatu.
Mlango wake ukagongwa!!
Askari! Akajiweka katika tahadhari kubwa na
kisha kujutia maamuzi yake ya kuamua kulala
nyumbani kwake siku hiyo. Upesi akaupeleka
mkono wake kiunoni na kuitoa bastola yake.
“Sam…..” sauti ya kike ikaita. Akaitambua mara
moja kuwa ilikuwa ya Maria!! Lakini hakufanya
papara kufungua mlango, akaendelea kuvuta
subira. Alitambua fika kama ni Maria kweli basi
atajua la kufanya ili aingie ndani. Hakika ndani ya
sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa.
Maria alikuwa na funguo za ziada!!
Sam kutokea katika eneo la uficho akatambua
kuwa Maria hakuwa peke yake. Jambo ambalo
lilimtatiza, na ghafla akakurupuka akiwa na
bunduki yake mkononi akawaelekezea wawili
wale.
Maria akazungumza kwa niaba ya Getonga,
akaelezea kwa ufupi juu ya ujio wao. Sam
akaridhika na mazungumzo yake akaitua bastola
yake na kuungana katika mazungumzo yenye
amani tele.
Sam akasimulia tukio la kubakwa kwa binti
wakiwa katika shughuli zao za kinyang’anyi,
akaelezea matukio yaliyofuata baada ya hapo
kwa rafiki zake kupoteza uhai katika namna ya
kustaajabisha.
“Mbaya zaidi hata mzee Yakuza naye alikutwa
amekufa..”
“Yakuza nd’o nani?”
“Huyo nd’o aliyetuagiza tumuue yule binti…”
Ni kwanini aliwaagiza mfanye vile labda..”
“Hakika hatukumuuliza maana kazi yetu sio kujua
bali kutenda tu!!”
“Getongaaaa!! Getongaaaa!!!........” sauti kali
kutoka nje ikasikika, Sam akagutuka kwa kudhani
wamezingirwa na maaskari. Akaikwapua bunduki
yake na kumwelekezea Getonga. Upesi
akanyanyua mikono juu kwa usalama wake.,
Maria aliduwaa asijue nini kinaendelea.
Na mara ukaanza kuvuma upepo wa maajabu,
upepo unaoleta kero ya joto badala ya kuleta
ahueni ya ubaridi.
“Mpatie anachotaka!!” sauti ikasikika tena. Wote
mle ndani wakatazamana.
“Sam, huna haja ya kutumia bunduki yako, si
mimi, wewe wala Maria anayejua nini
kinaendelea hapa…..” Getonga akamuonya Sam.
Akaishusha bunduki yake.
Mara vikasikika vishindo kutoka chumbani,
wakastaajabu tena. Sam akaiweka sawa bunduki
yake na kuelekezea katika korido inayotokea
chumbani.
Maajabu ya mwaka!!
Akatokea mtoto mdogo ambaye ni Getonga
pekee alikuwa anamtambua.
“Babaaaa…. Mpatie aniache mi sipapendi huko
baba. Babab mi nataka kwenda shule sitaki
hukooo anaponipeleka baba…” sauti ya kitoto ya
Eva ilizungumza na baba yake ambaye alikuwa
amekodoa macho tu.
“Babaa…” Eva alisihi tena.
“Anataka nini… na ni nani? Eeh nani….” Aliuliza
kwa pupa.
Badala ya kupata jibu, upepo ukaanza tena
kuvuma, ukalifunua gauni la Eva na kisha
ukavuma zaidi na kumwangusha Eva chini!!
“Mamaaa!!” sauti ya Eva ikasikika kwa mara ya
mwisho katika masikio ya Getonga!!
Upepo ukakoma, na hapo ukaanza msako wa
kumtafuta Eva ndani ya kile chumba.
Walimtafuta hadi katika kabati la vyombo na chini
ya viti lakini hakuwa Eva, sauti yake wala gauni
lake.
Getonga alipagawa haswa!
Ndani ya muda mfupi aliojiingiza katika tukio
asilolijua anakumbana na mambo mazito ya
kutisha.
Simu yake yta mkononi iliita na kumrejeshea
fahamu kuwa alikuwa hajaishika kwa muda
mrefu.
Alikuwa ni mkewe!!
Akaipokea upesi upesi!!
“Nikimpiga mwanao usinilaumu!!” sauti ya Anitha
mkewe ilisema kwa kiburi.
“Amefanya nini tena….”
“Mimi naandaa chakula mezani yeye ameenda
sijui wapi kucheza na hadi sasa hajarudi. Mi leo
namchapa kwa kweli…”
“Alikuaga na kukwambia anaenda wapi…”
“Kaondoka na watoto wenzake hapa na hajasema
hata anapoenda..” alizidi kulalamika Anitha, kisha
akasita na kugeuza mazungumzo, “we nawe
mbona unahema juu juu kwani ukwapi hadi muda
huu…”
“Nipo hapa wapi hapa….najiandaa kuja
nyumbani…” alijiumauma. Anitha akakata simu!!
Getonga akaketi chini kama zoba, jasho likiwa
linamtoka kwa wingi!! Eva wake alikuwa matatani
huku akimsihi kitu asichokijua!! Ile sauti ya Eva
kulalamika kuwa anataka kusoma hataki kwenda
huko kwingine ilizidi kumpagawisha!!
Majuto yakaanza kujengeka katika fikra zake.
Akajuta kuwa kiherehere!!
“Sam, kesho nitakuja na gari langu twende
pamoja hadi huko lilipotokea hilo tukio labda japo
sidhani lakini twende labda itasaidia. Kumbuka
hili ni kwa ajili yetu sote, wewe unasakwa na
polisi na pia kusumbuliwa na sura ya huyo binti
katika fikra zako, pia Maria unavuja damu bila
kikomo. Halafu mimi kama mlivyoona kwa macho
yenu waziwazi nimempoteza mtoto wangu wa
pekee. Eva! Kwa hiyo hili sio jambo la kupuuzia
hata kidogo.” Getonga alisihi kisha akaaga.
Maria akataka kuondoka naye, Sam akamzuia na
kumsihi walale wote maana anaogopa sana.
Maria akakubali!!
Lakini wakakubaliana kuwa hawatalala katika
nyumba ile bali nyumba ya kulala wageni. Hii ni
kutokana na tukio la mauzauza lililojitokeza.
Hawakuwa wapenzi bali mtu na shemeji yake
lakini hawakujali kuhusu hilo
Wakakubaliana kukutana siku iliyofuata saa tatu
asubuhi kwa ajili ya safari!!
***
WANGEUPATA vipi usingizi wakati mtoto wao
haonekani? Anitha alimlaumu Getonga kuwa kwa
kuchelewa kwake basi mtoto akawa huru sana na
kwenda anapotaka, Getonga hakutaka kujitetea
maana alimjua vyema mkewe.
Walihangaika huko na huko bila mafanikio,
Getonga hakusema lolote juu ya yale mauzauza
kwa kuhofia kumpoteza mkewe kwa shinikizo la
damu. Hata katika kituo cha polisi hakusema
lolote juu ya yale mauzauza.
Kitandani Anitha alimgeuzia mgongo mumewe na
hakutaka kuguswa hata kidogo, aliendelea
kulalama huku akimmwagia lawama Getonga,
sasa akaenda mbali zaidi na kudai mumewe ana
hawara huko nje na hii nd’o mikosi.
Getonga alijisikia hasira kali sana lakini hakutaka
kujibu mapigo kwa kuhofia kuipoteza amani
kidogo iliyobaki kwa ukimya wake.
Usingizi ukampitia Anitha na kuleta amani kidogo
kwa Getonga! Akabaki na maswali mawili tu,
asubuhi kuendelewa kumsaka Eva kwa kuzuga
ama aandamane na Sam kuelekea eneo la tukio.
Usingizi ukampitia bila jibu!!
Asubuhi akawahi kuamka ili kumkimbia Anitha
kitandani. Akaenda sebuleni na kywasha runinga.
Hakuwa na la kuangalia kwa muda ule lakini
alifanya kama geresha tu.
Anitha aliamka na kiburi chake kama kawaida,
akamsalimia mumewe huku ameuvuta mdomo na
masikioni akiwa amepachika ‘earphone’!! Getonga
akatabasamu bila kujibu chochote.
Anitha akiwa chumbani akajisikia vibaya
kuipoteza amani ndani ya nyumba. Akaona
hakuna maana kumkasirikia mumewe kwa tukio
la kupotea mtoto.
Ataanza vipi kuzungumza naye sasa?
Akakumbuka taarifa aliyotoka kuisikia katika redio
yake aliyokuwa nayo masikioni muda wote.
Akakiendea kioo na kuunda tabasamu lake
mwanana, kisha akaenda sebuleni huku mapigo
ya moyo yakimwenda mbio.
“Waandishi yawezekana mpo sahihi eeh!”
akaanzia hapo, Getonga akamtazama,
akaendelea. “Kafa mwingine na chata ya
Inspekta, mwaka huu freemason lazima
watumalize….”
Getonga akavuta umakini. Anitha akajisogeza
karibu yake na kumsimulia tukio jingine la mtu
kufa kimaajabu kwa kuvuja damu.
“Hebu ngoja umesema ni redio Tumaini ndo
wametangaza… ngoja hebu..” Getonga akachukua
simu yake na kumpigia rafiki yake aliyekuwa
anafanya kazi katika kituo hicho cha redio.
Akamuuliza juu ya ukweli wa habari hiyo.
“Taarifa imeletwa na muhudumu wa hoteli fulani
hivi na kisha kuthibitishwa na polisi juu ya tukio
hilo. Maajabu zaidi aliingia na mwanamke lakini
amekutwa akiwa peke yake. Ni balaa kaka..”
alijieleza wakati huo simu ikiwa katika spika za
nje. Wakisikiliza wote wawili.
“Wamekuta kitambulisho cha mwanamke huyo
ambaye sasa ndo anatafutwa… anaitwa Maria
Paul…”
“Whaat!!!” akashtuka Getonga.
“Unamfahamu ama?” Anitha akauliza.
“Ahhmm! Jina sio geni hilo….” Akajibu kwa hofu
Getonga.
Wivu!! Wivu ukajitundika katika moyo wa Anitha.
Akaondoka bila kuaga, amani ikatoweka tena!!
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
“Hebu ngoja umesema ni redio Tumaini ndo
wametangaza… ngoja hebu..” Getonga akachukua
simu yake na kumpigia rafiki yake aliyekuwa
anafanya kazi katika kituo hicho cha redio.
Akamuuliza juu ya ukweli wa habari hiyo.
“Taarifa imeletwa na muhudumu wa hoteli fulani
hivi na kisha kuthibitishwa na polisi juu ya tukio
hilo. Maajabu zaidi aliingia na mwanamke lakini
amekutwa akiwa peke yake. Ni balaa kaka..”
alijieleza wakati huo simu ikiwa katika spika za
nje. Wakisikiliza wote wawili.
“Wamekuta kitambulisho cha mwanamke huyo
ambaye sasa ndo anatafutwa… anaitwa Maria
Paul…”
“Whaat!!!” akashtuka Getonga.
“Unamfahamu ama?” Anitha akauliza.
“Ahhmm! Jina sio geni hilo….” Akajibu kwa hofu
Getonga.
Wivu!! Wivu ukajitundika katika moyo wa Anitha.
Akaondoka bila kuaga, amani ikatoweka tena!!
Halafu akarejea ghafla akiwa ameukunja uso
wake haswa!!
“Jana uliondoka na gari na umerudi bila kuwa
nalo.. umeliacha wapi G… eeh.. umeacha wapi
gari?” Anitha akahoji huku akiwa ameshika kiuno.
Macho yake makali yasiyokuwa na chembe
yoyote ya mzaha yakiwa yanatazama uso wa
Getonga unavyopigwa butwaa baada ya kusikia
swali lile ambalo hakulitarajia.
Mungu wangu wee!! Akasimama na kushika
kichwa chake. Anitha akayahamisha macho yake
kumfuata Getonga. Kisha akasonya na
kuendeleza malalamiko.
“Baba Eva…. Gari umemwachia nani yako leo…
nangoja jibu”
“Yaani huwezi amini…”
“Siwezi amini kuwa umelisahau kwa hawara
wako mpya…Eeh! kipi hicho ambacho siwezi
kukiamini sasa” Anitha akamalizia kauli.
“Mama Eva… ni nini hicho sasa unaleta hapa….”
“Sikuelewi hata kidogo, jana umechelewa kurudi
usiku, sikulalamika, umenikumbatia unanukia
marashi ya kike mi nakutazama tu…unaniona
mjinga, sasa na gari halipo… baba Eva ni nini
hiki…ni nini lakini?” Anitha akashindwa kuendelea
kulalamika akaanza kulia kwa kusina akiwa
amejiinamia kwenye kochi.
Nafsi ikamsuta Getonga akakumbuka kuwa
alikuwa jirani sana na Maria usiku uliopita na pia
wakati maluweluwe ya Eva kujitokeza Maria
alimkumbatia kwa nguvu. Bila shaka nd’o wakati
aliomuachia marashi.
Je? ajishushe na kuanza kuelezea mkasa juu ya
Maria? Ili aweze kuelezea juu ya kusahau gari
lake likioshwa mahali!! Lakini kwa kusema yote
haya bila shaka atalazimika kusema juu ya Eva
kuonekana na kisha kutoweka na kama hii
haitoshi lazima autaje mkasa wa Kindo na mama
yake kuuwawa kinyama.
Eva hatanielewa hata kidogo!! Getonga alisalimu
amri kimya kimya.
Akapiga hatua kadhaa na kumfikia Anitha kisha
akamshika bega, ghafla Anitha akakipangua
kiganja chake na kukitupilia mbali.
“Nenda ukawashike hawara zako ambao
unawahonga magari….. ndio hao unaowahonga
magari nenda ukawashike…. Gerlad Getonga…
wanaume wanaumee… pete ya ndoa kidoleni
unaenda kwa mahawara, unawahonga na…”
“Stooop Anitha!! Nyamaza…. Hujui usemalo. Eva
ametoweka tunatakiwa kujiandaa na kwenda
kutafuta ufumbuzi huu sio muda wa
kugombana….”
“Niache nizungumze mume wangu, Eva alipotea
ukiwa na hawara zako, kupotea kwake ni pigo
kwa ajili ya usaliti wako… oooh Eva mwanangu
weee… Eva weeee..” akashindwa kuendelea na
kuanza kuangua kilio. Getonga akamkabili na
kuanza kumbembeleza.
“Gari lipo car wash… nililiacha huko…
tunaongozana wote tunalichukua na kisha
tunaenda polisi. Sina hawara mke wangu!!
Nakupenda.” Getonga akajitetea. Anitha
akamkumbatia kwa nguvu huku akishusha
maneno kadhaa ya kumsihi Getonga asimsaliti.
****
HABARI mbili zikazidi kukichanganya kichwa cha
Getonga. Akashindwa aanze na lipi kwanza na
lipi lifuate baada ya.
Anitha alikuwa amegeuka mbogo, hakutaka
kushaurika na upuuzi kuwa gari lilikuwa
linaoshwa likasahaulika na kisha kupotea
hazikumwingia akilini hata kidogo. Akapigia
mstari majibu yake ya awali kuwa mumewe
amelitoa lile gari kwa ajili ya hawara wake.
Getonga alijaribu kusihi lakini hakusikilizwa tena,
Anitha akapanda taksi na kutoweka.
Getonga akabaki kuduwaa huku akilikumbuka
vyema tukio la kuacha gari likioshwa kisha
akaenda katika chumba cha Maria ambapo
hakumkuta. Baada ya pale akafanya safari ya
kwenda kwa mama yake Kindo ambapo mabalaa
rasmi yalianzia.
Gari aliloliacha likioshwa halikuwepo tena na
mkewe hataki kusikia habari hiyo.
Habari ya pili ilikuwa juu ya kifo cha Sam, kifo
cha aina ileile ya kuvuja damu. Hili lilimvuruga
kabisa Getonga na kuona mipango yake yote
ikienda mlama. Akafikiria kwenda kutoa taarifa
polisi juu ya gari lake kuibiwa katika mazingira
yale ya kuoshwa, lakini akaamini kuwa polisi
wanaweza kumpotezea muda zaidi bila kujali
mwanaye wa pekee Eva yu katika mikono ya
watu wabaya.
Asa aanzie wapi? Hilo likawa swali zito zaidi.
Akataka kwenda mahali ambapo tukio la kifo cha
Sam limetokea, lakini akasita baada ya kutembea
hatua kadhaa, akakumbuka jambo la muhimu
zaidi kwa muda ule.
Wanawake? Wanawake na wivu wao!!! Kengere
ya hatari ikalia katika kichwa chake. Akamuwaza
Anitha na kuhisi kuwa anaweza kufikia hatua
mbaya ya kujiua kutokana na hisia zake potofu!!
Upesi akapanda taksi na kuamuru apelekwe
maeneo ya nyumbani kwake kwa mwendo mkali
kabisa. Dereva akabuni njia zake za panya na
safari ikaanza!!
Baada ya dakika thelathini Getonga alikuwa
anatelemka garini baada ya kuwa amelipa pesa
iliyotakiwa.
Kichwani mwake alikuwa amepitisha maamuzi ya
kumweleza Anitha kila kitu juu ya mauzauza
yanayoendelea, aliamua hivi kwa kuamini kabisa
Anitha angeweza kuathirika kisaikolojia iwapo hali
itaendelea kuwa vilevile.
Nyumba ilikuwa tulivu sana, na milango ilikuwa
imefungwa kwa ndani.
Wanawake!! Sasa hapa hataki niingie ama?
Akajiuliza huku akiangaza huku na kule namna ya
ziada ya kuweza kuingia ndani.
Hapakuwa na namna!!
“Anitha… Anitha mama yangu…..” alianza kusihi
Getonga huku akijaribu kuchungulia huku na kule
bila mafanikio ya kumwona mkewe. Akazunguka
upande wa jikoni, akachungulia hakuona kitu,
akazunguka upande wa stoo, bado hakuona kitu,
bado aliendelea kuita kwa bidii huku akiomba
msamaha, moyo wake ulishatawaliwa na hofu juu
ya mkewe kujiua. Jambo ambalo aliliwaza awali
na kisha kuchukua maamuzi ya kurejea
nyumbani.
“Bwana Gerlad Getonga!!” sauti nzito ilimshtua
kutoka upande wake wa kushoto. Akageuka upesi
akiwa ametaharuki akakutana na sura ya
mwenyekiti wa mtaa.
“Mzee Magesa, kuna taarifa zozote juu ya
mwanangu.” Akamuuliza huku akijua kabisa
hapakuwa na uwezekano wa mwanaye
kupatikana kwa njia za kipolisi ama kipelelezi.
“Hapana Getonga, na si hilo lililonileta hapa.
Nimejaribu kupiga simu yako haikupatikana na
namba ya mkeo haipokelewi sijui kwanini..”
“Kuna tatizo gani mkuu….”
“Mkeo alipiga kelele za kutisha sana huku akiwa
amejifungia ndani ya nyumba, hakijulikani ni nini
kinaendelea…nimepewa taarifa na jirani yenu
nami nikajaribu kuwasiliana nawe bila
mafanikio..” sauti nzito iliendelea kuporomoka.
Kengere ya hatari ikalia kwa mara nyingine tena
katika kichwa cha Getonga. Akaondoka bila
kuaga hadi katika dirisha linaloelekeza chumbani
kwake na mkewe. Alijaribu kuchungulia pasi na
mafanikio, pazia zito lilikuwa limeziba kabisa.
Alitapatapa huku na kule bila mafanikio, na
mwisho wakakubaliana kuuvunja mlango.
Mwenyekiti akisikiliza uamuzi wa Getonga
akawaruhusu vijana waliokuwa wanashirikiana
katika kutafuta namna ya kuingia ndani ya
nyumba ile kuuvunja mlango.
Zoezi likamalizika, mbiombio Getonga akiwa
anahema juu juu na hofu ikiishi katika damu yake
akamsaka mkewe huku na kule.
Hatimaye akakifikia chumba chao!! Akausukuma
mlango, ukafunguka kidogo sana kisha ukawa
mzito kama kwamba kuna kitu kimewekwa
maksudi kiweze kuuzuia, akaendelea kuusukuma
ukawa unasogea kidogo kidogo. Waliposhirikiana
wakaufungua.
Getonga akaingia ndani, kitu cha kwanza
akatazama upande wa kushoto aweze kujua ni
kitu gani kilichokuwa kinauzuia mlango
usifunguke.
Macho yakaongezeka ukubwa ghafla, kiganja
kikawahi kuuziba mdomo usipige kelele.
Ushuhuda wa ajabu, pua ya mkewe ilikuwa
imepasuka vibaya na damu zilikuwa zimetapakaa
katika marumaru pale chumbani.
Mikono ilikuwa imesambaa kushoto na kulia,
mguu mmoja ukiwa na kiatu na mwingine ukiwa
peku.
Amekuwaje huyu jamani eeeh!! Getonga alianza
kulalamika peke yake.
“Gerlad Getonga…” sauti nzito ya mwenyekiti wa
mtaa ilimuita. Akageuka kumtazama, lakini sauti
nzito hakuwa na habari naye bali macho yake
yalikuwa yamekodoa kutazama kitanda cha
Getonga.,
Getonga akajisogeza kwa kusuasua hadi
akakifikia kitanda.
Hapa uvumilivu haukuwepo tena kwa alichokiona,
alipiga kelele moja kisha akalainika na kudondoka
chini. Ile pua iliyovunjika ya mkewe haikuwa
inatisha kama hali iliyokuwa pale kitandani.
Akajikongoja na kuinuka tena, kwa kutumia
magoti akajivutavuta hadi akakifikia kitanda,
akazidi kutumbua macho yake katika kitanda
chake kilichovikwa shuka jeupe.
Kipande cha gauni kilikuwa kimefunuliwa na
kilikuwa kimebeba vitu vya kutisha na kuduwaza
huku vikileta mateso ya nafsi. Pembeni yake
kulikuwa na karatasi.
“Eva…..Eva….” akaanza kuita huku akitetemeka,
mwenyekiti wake hakuwa amepata la kusema
bali kuungana na Getonga katika mshangao ule.
Getonga, akanyoosha mkono wake uliokuwa
unatetemeka ili aweze kushika kile kilichokuwa
katika kipande kidogo cha gauni ili aweze
kujihakikishia kabisa kama hofu yake ni sahihi
ama la!!
Naam!! Hayakuwa mauzauza bali hali halisi
kabisa, vidole viwili vilivyokuwa vimetapakaza
damu katika kile kipande cha gauni vilikuwa vya
mtoto wake wa pekee. Eva!
Kama mtoto mdogo, Getonga alianza kuomboleza
kwa sauti ya juu huku akijirusha huku na kule.
Mwenyekiti akasaidiana na majirani kumdhibiti
Getonga asije akajidhuru.
Na wakati huo simu ilikuwa imepigwa polisi
tayari.
Getonga akajilaumu kwa kusita kumweleza
mkewe ukweli juu ya kilichotokea usiku wa siku
iliyopita, sasa mambo yanazidi kuongezeka na
stori inazidi kuwa ndefu ya kuelezea…..
Getonga akajikuta kwa wakati mmoja akipoteza
vitu vingi; mtoto wake, amani, uaminifu kwa
mkewe na kubwa zaidi akajikuta amenunua hofu
bila kulazimishwa!!
Polisi walifika baada ya muda mfupi kutoka
katika kituo kilichokuwa jirani. Anitha akakatiwa
PF3 na kukimbizwa hospitali upesi, Getonga
akaandamana na msafara ule. Polisi
wakaimarisha ulinzi pale chumbani pasipo kugusa
kitu chochote kile.
***
“Gerlad Getonga, kuna mtu yeyote anakudai kaka,
ama umekosana naye siku za karibuni?”
mwenyekiti alimuuliza wakati wakiwa nje ya
hospitali wakisubiri muda wa kwenda kusalimia
wagonjwa.
“Hapana, sina madeni na sijagombana na
mtu….kwani nini?” alijibu na kupandishia swali
jingine huku akionekana kuvutiwa na swali lile.
“Getonga wewe ni rafiki yangu sana ujue…siwezi
kusikia jambo nisikueleze. Umeniunga mkono
sana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa,
nakumbuka kila kitu….” Akasita kidogo akakohoa
kulainisha koo kisha akaendelea, “Kwa tetesi ni
kwamba yale maandishi yaliyoachwa kitandani
yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya kiarabu, na
kwa wale wanaoielewa lugha wanadai kuwa yale
maneno kwa Kiswahili ni “UNANICHELEWESH
EA”…..sasa ni kitu gani unamcheleweshea huyu
shetwain hadi afanye unyama ule… eeh!”
alimaliza mwenyekiti.
Getonga akashusha pumzi kwa nguvu, akajishika
kiuno.
“Hawa watu wa hivi ni wabaya sana anaweza
kufanya mambo mabaya zaidi kwa mtoto wako…
kama lipo ambalo hujawatimizia tafadhali bwana
we fanya kutimiza….usibishane nao we wape.”
Mwenyekiti alizidi kutilia mkazo kauli yake.
***Hali tete kwa Gerlad Getonga….. Ameinunua
hofu bila kujua… sasa anaandamwa!!
SIMULIZI ND’O IMEANZA SASA!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
“Getonga wewe ni rafiki yangu sana ujue…siwezi
kusikia jambo nisikueleze. Umeniunga mkono
sana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa,
nakumbuka kila kitu….” Akasita kidogo akakohoa
kulainisha koo kisha akaendelea, “Kwa tetesi ni
kwamba yale maandishi yaliyoachwa kitandani
yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya kiarabu, na
kwa wale wanaoielewa lugha wanadai kuwa yale
maneno kwa Kiswahili ni “UNANICHELEWESH
EA”…..sasa ni kitu gani unamcheleweshea huyu
shetwain hadi afanye unyama ule… eeh!”
alimaliza mwenyekiti.
Getonga akashusha pumzi kwa nguvu, akajishika
kiuno.
“Hawa watu wa hivi ni wabaya sana anaweza
kufanya mambo mabaya zaidi kwa mtoto wako…
kama lipo ambalo hujawatimizia tafadhali bwana
we fanya kutimiza….usibishane nao we wape.”
Mwenyekiti alizidi kutilia mkazo kauli yake.
ASUBUHI waliyoingoja kwa ajili ya Anitha
kuruhusiwa kutoka hospitali haikukucha vyema,
wakati Getonga akijipa matumaini kuwa
atazungumza na mkewe kinagaubaga hadi
amuelewe na kisha wawe kitu kimoja waungane
katika kumsaka Eva. Kuna kundi la watu wanne
lilikuwa linamsaka kwa udi na uvumba kwa ajili
ya mahojiano, baada ya kumkosa nyumbani
kwake walipata taarifa kuwa anaweza kuwa yu
hospitali ambapo mkewe alikuwa anapata
matibabu.
Wakaandamana kuelekea maeneo hayo ya
hospitali!!
Mwenyekiti wa mtaa alikuwa amesinzia lakini
Getonga angali macho akitafakari juu ya kipindi
hicho kigumu cha mpito anachopitia. Taswira
ikanasa katika vidole viwili kutoka katika mkono
wa mwanaye, akauma meno kwa hasira huku
akijipiga piga miguu yake sakafuni kukabiliana na
uchungu mkubwa.
Ule uchungu wa mwana.....
"Nani huyu anayenifuatilia lakini kwa mara
nyingine?" Alijiuliza asiwepo hata mtu mmoja wa
kumjibu.
Mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita, kwa
sababu alikuwa amezuia sauti basi ilitoa mwanga
pekee kumpa taarifa hiyo. Akaitazama na
kugundua ilikuwa namba mpya.
Wanataka kunipa pole hawa!! Aliwaza kisha
akairejesha mfukoni bila kuipokea.
“Gerlad Getonga…….” Sauti laini ya kike ilimuita,
akageuka upesi akakutana na watu wanne
wakiwa wamemzunguka.
“Uumh! Naam…” akaitika.
“Upo chini ya ulinzi na unahitajika kituo cha polisi
Chang’ombe muda huu…” sauti ya kiume
ikaamuru. Na hapo akachomoa kitambulisho
chake na kumpatia Getonga ikiwa anahitaji
kuthibitisha.
Hakikupokelewa!
Sauti hii ikamtoa mwenyekiti katika usingizi,
akayapikicha macho yake kisha akapiga mwayo.
“Kuna nini hapa…” akauliza. Getonga hakuwa na
la kujibu, hata wale viumbe wanne ambao
walitambulika kuwa maaskari na wao hawakuwa
na la kumjibu.
Mmoja akachomoa pingu na kuikamata mikono
ya Getonga ambaye alijaribu kuikwepesha na
hapo akajihalalisha kupokea kofi zito mgongoni.
Hata kabla maumivu hayajamwisha tayari mikono
yake ilikuwa imeunganishwa katika pingu.
“Kituo cha polisi Chang’ombe…. Unaweza kufika
kesho maana kwa muda huu hauna la kusaidia..”
polisi wa kike akamwonya mwenyekiti wa mtaa
ambaye alitaka kuandamana na Getonga ajue
kulikoni.
****
Bunduki? Mauaji? Ujambazi?.... haya yalikuwa
maswali yaliyokisumbua kichwa cha Getonga
wakati yupo nyuma ya vyuma vya selo. Katika
makosa makubwa aliyowahi kufanya maishani
mwake basi hili alilolifanya lilikuwa kubwa lakini
la kizembe kupita yote aliyowahi kufanya.
Uzembe katika kutoa taarifa!
Alitambua fika kuwa gari lake limetoweka katika
mazingira ya kutatanisha, hakuna mtu yeyote
aliyetambua wapi lilipo. Lakini bado hakutoa
taarifa polisi. Hadi polisi wamekuja kumkamata
kwa kesi mbaya ya kukutwa na bunduki katika
gari lake ambalo limefanya ujambazi huku roho
nne za wananchi wasiokuwa na hatia zikipotea.
Kwa sababu gari ni lake na leseni pamoja na
kadi vimelithibitisha hilo basi aidha muuaji ni
yeye ama anawafahamu walioua!!
ASUBUHI majira ya saa nne mpelelezi wa kesi
iliyomuhusu Getonga tayari alikuwa amewasili.
Getonga akatolewa kwa ajili ya kuchukuliwa
maelezo, kila swali aliloulizwa aliliona kama jipya
sana kwake.
Umiliki wa bunduki?
Kushirikiana na majambazi?
Alichoweza kujibu ni kwamba mara ya mwisho
kulitumia gari lake ni pale ambapo alilipeleka
kituo cha kuosha magari. Zaidi ya hapo
hakulitumia tena. Mpelelezi akamrudisha
mahabusu huku akimwonya kuwa kama
hatakuwa mkweli basi hukumu yake itakuwa
mbaya sana.
Getonga akabaki katika kustaajabu, Eva, Anitha
na sasa yeye muhimili mkuu wa familia yu
matatani na hana namna ya kujinasua.
MAJIRA ya saa mbili usiku baada ya mahabusu
kuhesabiwa Getonga alijibanza katika kona moja
ya chumba kile. Alikuwa mtulivu kabisa akijaribu
kushtuka kutoka usingizini huenda alikuwa katika
ndoto mbaya, lakini kila alivyoyafumbua macho
alijikuta yupo rumande.
Akatoa tabasamu la karaha!!
Milango ikafunguliwa kisha matusi ya hapa na
pale kutoka kwa maaskari yakamsindikiza
mtuhumiwa mwingine mgeni katika rumande ile.
Mahabusu wazoefu wakaanza kumsumbua na
kumzongazonga hapa na pale, wengine
wakimwomba sigara wengine wakitaka awape
pesa na wakorofi zaidi walimlazimisha aende
kulala jirani na choo.
Getonga aliyatazama yote haya katika mwanga
hafifu!! Akangoja majibu ya yule mtu
anayesumbuliwa lakini la! Hakujibu lolote.
Akajipenyeza hapa na pale ili apate mahali sahihi
pa kuketi.
“Unaenda wapi wewe? Nimesema utalala chooni
huko?” alikoroma mahabusu mbabe. Yule mtu
mgeni hakuyajali maneno yake, akazidi
kujipenyeza tu bila kujali lolote.
“Unanikanyaga we bwege…” akabwatuka
mwingine, bado yule bwana hakujali na hata
hakuomba radhi. Hii ilistaajabisha mno..
Hakusema neno lolote lile. Getonga naye akawa
anamshangaa sasa!
“Nyie mnamchelewesha naona, mapombe yake
anakuja kutusumbua sisi….” Mtuhumiwa
mwingine akayasema haya huku akiruka hatua
kadhaa kisha akamgusa yule mgeni begani. Na
hapo hapo akamfyatua teke kiunoni.
Yule bwana akajikunja kwa maumivu
watuhumiwa wengine wakashangilia. Na hapo
akageuka upesi akarusha mkono wake ngumi
ikampata yule mbabe usoni, akapepesuka na
kuanguka chini huku akigumia kwa maumivu.
Miguno ikasikika kutoka kwa watuhumiwa!! Yule
bwana hakujali, hatimaye akaketi pembezoni
mwa Getonga ambaye naye alikuwa anamuhofia
huyo bwana asiyesema neno lolote lile. Ni kama
alikuwa hasikii na pia hana uwezo wa kuongea.
lakini hakuwa mnyonge!
“Bro….” Getonga alijaribu kumwita yule mgeni
baada ya kuwa ameukalia mkono wake kwa
muda mrefu bila kujua na sasa ganzi ilikuwa
inamshika.
Mgeni hakugeuka!!
Getonga akajaribu kujitoa kwa nguvu ndipo yule
bwana akajitikisa kidogo, Getonga kwa sababu
alikuwa ametumia nguvu kujitoa basi kile kitendo
cha kuachiwa akajikuta akimpiga kichwa
mwenzake wa pembeni ambaye alitaka kumjia
juu kisharishari kabla mgeni hajamnasa kofi zito
katika paji la uso na kumwacha akibung’aa
badala ya kuugulia maumivu.
“Oya wanakuja…wanakuja mwana!!” kwa mara ya
kwanza yule mgeni akaanza kuzungumza huku
akiwaaminisha watu wote mle ndani kuwa makini
na kile anachokisema.
“Mnasikia…hao wamekaribia hao hapo…” alizidi
kusihi!!
Watuhumiwa wengine waliokuwa mahabusu
wakabaki kumshangaa yule bwana ambaye sura
yake haikuwa inaonekana kutokana na giza.
Alipoona hakuna anayemuelewa aliruka hovyo
hovyo huku akiwakanyaga wenzake akakimbilia
katika matundu ya milango ya chuma ambayo
ikifunguliwa basi mtuhumiwa anaweza kutoka nje,
mlango huu upo jirani na mapokezi.
“Afandee…nyie maafande acheni kulala,
anaku….wanakuja hao…eeeh!! Wanakuja….”
Alipiga makelele hovyohovyo na alikuwa kama
anayetaka aeleweke.
“We bwege ulijifanya hujui kuongea sasa unapiga
makelele huko eeeh!! Kesho utanieleza fala
wewe…” afande alifoka baada ya kugundua kuwa
mtu ambaye aligoma kutaja majina yake baada
ya kukamatwa akizurura usiku akiwa na panga
sasa anazungumza.
“Afande….wanakuja niamini mimi….” Akasihi yule
bwana huku sauti yake ikiwa kama anayetaka
kulia.
Alipomaliza kauli hii kila mmoja aliweza kuusikia
upepo ulioanza kuvuma.
“We fala unaita mvua eeeh!!” afande akabwatuka
bila kufanya jitihada zozote za kuyafanyia kazi
maneno ya kijana yule mahabusu.
Upepo huu ukamshtua Getonga, aliwahi
kuushuhudia mahali. Siku ambayo Eva
anajitokeza na kisha kupotea, pia siku ambayo
mama yake Kindo aliuwawa.
Getonga akasimama upesi aweze kwenda
kumwona huyo mtu anayelalamika ni nani…..
Akaruka hovyohovyo na yeye.
Ana kwa ana wakagonganisha macho na Kindo!!
“Wamefika tayari…. Na we hutaki kuwapa vitu
vyao ona sasa…ona…..” alilalamika Kindo.
Getonga akabaki kuduwaa!!
Mara likafuata tukio jingine la kustaajabisha!!
Mapokezi zikaanza kusikika kelele zisizo na
kifani, vishindo vikubwa vikubwa vya mianguko
ya kabati navyo vikasheheni.
Watuhumiwa wote kila mmoja alikuwa
anang’ang’ania kuwa pale mlangoni ili aweze
kuona nini kinatokea. Lakini ghafla wote
wakauogopa ule mlango na kuanza kukimbia huku
na kule baada ya mkono wa mwanadamu
kupenya pale mlangoni huku ukiwa unavuja
damu. Kisha mwili wa askari ukajibamiza pale
mlangoni ukatoka na kurudi tena kwa kasi huku
ukizidi kupondeka pondeka.
Ilikuwa ni kama kuna mtu alikuwa anambamiza
pale lakini ajabu mtu huyo hakuonekana!!
Taharuki ikatanda kila kona, Getonga akamvaa
Kindo na kumhoji ni kitu gani kinatokea.
Kindo akarejea kuwa Kindo yuleyule asiyeweza
kusema maneno mengi zaidi akaendelea
kujiongelea akisema.
“Rensho…Rensho!!”
Kila swali liloulizwa alijibu Rensho!!
Hakuwa mkorofi tena, hakuwa msemaji tena!!
Utata!!
****
MWENYEKITI wa mtaa hakutaka kumshtua
Anitha kwa kumpa taarifa juu ya Getonga
kushikiliwa na polisi kwa makosa makubwa
makubwa likiwemo la mauaji. Alitulia tuli
akimweleza kuwa Getonga yu katika harakati za
kumsaka mtoto wao, Anitha aliyekuwa mnyonge
muda wote alikubaliana na yule mwenyekiti kuwa
alitakiwa kutulia nyumbani ale vizuri sana ili
mwisho aweze kurejea katika afya yake murua.
Kitu kikubwa alichofanya mwenyekiti ni kumpa
Anitha binti yake mkubwa ili aweze kuishi naye
kwa kipindi hicho alichotakiwa kuwa chini ya
uangalizi. Alifanya hivi ili kumweka mbali Anitha
na maneno ya majirani ambayo yanaweza
kumsababisha akaipoteza amani tena.
Anitha alikuwa mtu wa simanzi muda wote,
hakumuwaza Getonga bali Eva mwanaye. Kila
alipovikumbuka vile vidole viwili alijikuta akiangua
kilio huku Bertha binti wa mwenyekiti wa mtaa
akifanya jitihada za kumbembeleza.
Siku ya pili baada ya kutoka hospitali, Bertha
akiwa jikoni anapika na yeye akiwa sebuleni
anatazama filamu alipata ugeni wa ghafla.
Mgeni mwanamke ambaye hakukumbuka kuwa ni
ustaarabu kubisha hodi kabla ya kuingia ndani.
Yeye akaingia bila hodi!!
Tabasamu tele mdomoni mwake!
Hakusalimia, akaketi!!
Hawara wake Getonga!! Anitha akawaza kisha
akauficha uso wake usionekane kuwa katika
hasira.
“Kuna mzigo wangu mumeo alikuachia hapa…
maana mi hata si mkaaji nataka kuondoka
zangu…” aliuliza binti yule huku akiukunja mguu
wake na kuacha mapaja meupe nje. Anitha
akajihisi hasira, akatamani kutukana lakini
akasita.
“Hee dada kwani we bubu ama?”
“Sijaelewa swali lako ujue…” Anitha akaweza
kujiongoza akili yake akauliza kwa utaratibu.
“Mume wako…Gerlad Getonga amekuachia mzigo
wangu kabla hajaenda huko polisi?”
“Sijaonana naye na hakuniambia kama kuna
mgeni atakuja hapa…” akajibu Anitha. Yule mgeni
akaanza kucheka kwa sauti ya chini, vishimo
katika mashavu yake vikaonekana, na mzigo wa
matiti kifuani mwake ukawa unarukaruka wakati
anacheka. Anitha akajisahau kuwa alikuwa
amekereka macho yake yakaitazama shingo ya
yule dada, akayatamani madini aghali aliyovaa
shingoni.
“Mna visa kweli, yaani mumeo bwana daah!! Kwa
hiyo hamshirikishani madeni yenu eeh!!”
“Dada sikuelewi kabisa, mambo ya mimi
kushirikishana naye ama kutoshirikishana naye
wewe yanakuhusu nini..nimesema hakuna mzigo
wowote alioacha hapa…” akajibu kwa ukali.
Yule dada akashtuka kisha akasimama wima na
yeye akiwa amechukia. Midomo ikimtetemeka!!
“Pete si umeona haina umuhimu eeeh!!”
akasema, huku akimtazama anitha. Anitha naye
akajitazama kidoleni.
Maajabu!! Hakuwa na pete kweli, akaduwaa.
“Kama pete haina umuhimu, nitachukua na hicho
kidole chake ndo utajua umuhimu wake nyau
wewe!!” alifoka huku sura yake ikiwa nyekundu
kwa hasira.
Anitha akaanza kutetemeka huku macho yakiwa
yamemtoka pima!!
“Akija mwambie Rebeca wa Nshomile alikuja
kufuata mambo zake….” Akatoa kauli hiyo huku
akitoka nje na kuubamiza mlango kwa nguvu
mno.
Anitha akapiga mayowe, Bertha akakurupuka
kutoka jikoni mbiombio mpaka sebuleni.
Akamkuta Anitha akiwa katika taharuki kali.
ITAENDELEA!!
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU
“Pete si umeona haina umuhimu eeeh!!”
akasema, huku akimtazama anitha. Anitha naye
akajitazama kidoleni.
Maajabu!! Hakuwa na pete kweli, akaduwaa.
“Kama pete haina umuhimu, nitachukua na hicho
kidole chake ndo utajua umuhimu wake nyau
wewe!!” alifoka huku sura yake ikiwa nyekundu
kwa hasira.
Anitha akaanza kutetemeka huku macho yakiwa
yamemtoka pima!!
“Akija mwambie Rebeca wa Nshomile alikuja
kufuata mambo zake….” Akatoa kauli hiyo huku
akitoka nje na kuubamiza mlango kwa nguvu
mno.
Anitha akapiga mayowe, Bertha akakurupuka
kutoka jikoni mbiombio mpaka sebuleni.
Akamkuta Anitha akiwa katika taharuki kali.
“Wifi…… kuna nini eeeh!!” Bertha alimuuliza huku
akiangaza huku na huko huenda kuna kitu
ambacho kinamtisha Anitha, na kama kipo na
yeye aweze kujihadhari mapema.
Hakuna chochote alichofanikiwa kukiona!!!
“Atanikata kidole….atanikata kidole…amechukua
pete…” alibwatuka Anitha huku hofu ikizidi
kutanda na Bertha asielewe ni kitu gani
kinachozungumziwa.
“Nani eeh!! Nani…”
“Mwanamke…Rebeka anaitwa Rebeka…”
“Rebeca gani? Tuliza akili yako tulia kabisa
hakuna kitu kama hicho lakini….” Akasita Bertha
huku macho yake yakikitazama kidole
kisichokuwa na pete kidoleni.
Imeenda wapi sasa? Akajiuliza….
“Amechukua Rebeca ….amechukua..”
“Ni nani yako huyo Rebeca?”
“Simjui na sijui alichukua muda gani….” Anitha
aliendelea kujibu huku akitetemeka waziwazi.
****
KIINI MACHO CHA AJABU!!
ASKARI waliokuwa lindoni nd’o walikuwa wa
kwanza kugundua hali hii ya sintofahamu.
Hapakuwa na mtu yeyote mapokezi na
makaratasi yalikuwa shaghalabaghala, jambo
ambalo si la kawaida hata kidogo taarifa ya
dharula ikatolewa upesi. Namba za maaskari
wawili waliokuwa mapokezi zikatajwa na mara
moja ukaanza msako usiokuwa na mafanikio ya
haraka.
Ulinzi wa dharula ukawekwa kwa umakini kabisa
kabla selo hazijakaguliwa na kukutwa zikiwa
salama kabisa bila purukushani yoyote ile
ambayo ingeweza kuleta mashaka kuwa kuna
mahabusu aliyejaribu kutoroka.
Makaratasi yaliyosambaa huku na kule
yalikusanywa pamoja na daftari kubwa kabisa
ambalo ni maalumu kwa ajili ya kuandikishia
orodha ya mahabusu wanaoingia kila siku.
Wakati upelelezi wa kipi kilichotokea pale
ukiendelea C.I.D mpelelezi Gasto aligundua
jambo jingine. Ilikuwa baada ya kuhitaji
kuendelea kuchukua maelezo kutoka kwa
mtuhumiwa wa mauaji na ujambazi kwa kutumia
silaha.
Aliifikia milango ya chuma ya mahabusu ile na
kuita mara moja jina la mtuhumiwa.
“Gerlad Getonga!!” alirudia kwa sauti ya juu zaidi.
Kimya!
Hakuna aliyejibu huku mahabusu wakitazamana
wao kwa wao na kuulizana kuwa ni nani mwenye
jina hilo.
Baada ya kuita mara nne bila kupata mrejesho
wowote, afande Gasto akiongozwa na askari
mwenye dhamana ya kufunga na kufungua
mahabusu kwa siku ile aliingia ndani na
kumtazama mahabusu mmoja baada ya
mwingine.
Gerlad Getonga hakuwa ndani!!
Ametoka vipi kwenye vile vyuma? Ama
ameshirikiana na hao maaskari waliotoweka?
Haya yalikuwa baadhi ya maswali
yaliyowachanganya askari wote waliopewa
taarifa hii akiwemo inspekta Mujuni mkuu wa
kituo kile.
“Ita majina mahabusu wote huenda ni wengi
hawamo!” alitoa amri inspekta.
Majina yakaitwa kwa kufuata orodha iliyokuwa
katika lile daftari kubwa.
Tofauti na Gerlad Getonga ikafahamika kuwa
mahabusu mwingine ambaye hakuandikwa jina
lake na sababu za kutoandikwa jina zikaainishwa
kuwa aligoma kusema chochote
“Alikamatwa kwa kosa gani?”
“Uzururaji… uzururaji afande!!” askari mmoja
alijibu huku akisoma katika lile daftari.
Ukimya ukatanda kwa sekunde kadhaa, Inspekta
Mujuni akijikuna kichwa kwa kutumia kalamu
yake maaskari wengine wakitazamana bila
kusema neno lolote.
Mlango wa ofisi ya mkuu wa kituo ulipogongwa
ndipo fahamu zilimkaa sawa na kuuliza kwa shari
aliyepo mlangoni anataka nini? Badala ya kujibu,
aliyekuwa mlangoni akaendelea kuugonga
mlango!
Inspekta akampa ishara askari mmoja kuwa
aufungue mlango. Upesi akatii.
Alipoufungua akakutana na filamu ya kutisha,
sura moja ya kutisha sana na laiti kama
yasingekuwa mavazi yake basi asingeweza
kujulikana yeye ni nani zaidi ya mzimu uliokuja
kuwatisha maaskari.
Namba yake ya utambulisho begani
ikamtambulisha kuwa ndiye mmoja wa maaskari
waliokuwa wakisakwa ili waelezee ni kitu gani
kimetokea usiku pale kituoni.
Uso wake mweupe ulikuwa umegeuka
mwekundu, mashavu yalikuwa yamevimba huku
yakiwa yamekwanguliwa na kuacha michirizi
mizito ya damu, macho yalimvimba kana kwamba
amepigwa ngumi kali za usoni. Mikono yake
mwembamba ilikuwa imevimba huku na yenyewe
ikiwa imekwanguliwa haswa. Udenda ulimtoka
hovyo mdomoni huku ukiambatana na damu
nzito.
“Jenny…..umekuwaje eeh!!” Askari mmoja wa
kiume alimuuliza, lakini hakujibiwa kitu zaidi ya
kutumbuliwa macho tu.
“We Jenny wewe…” Inspekta Mujuni naye
alijaribu bahati yake kwa sauti iliyojaa uoga.
Jenny hakujibu kitu na huyu naye akaishiwa
kuangaliwa tu na macho yaliyokodolewa.
“Mwenzako yupo wapi… eeh afande Kassim
yukwapi?” Inspekta akapandishia swali jingine
zito.
Jenny akainama na kuruhusu damu izidi kumtoka
kinywani.
“Piga simu upesi huduma ya kwanza… tunatakiwa
kufanya jambo hapa…” amri ikatoka.
Wakati askari akibofya namba kadhaa kupiga
simu. Jenny aliyekuwa ameinama alinyanyua
kichwa chake hakutambua kama tabasamu lake
alilojaribu kutoa lilionekana kama kilio cha
kukera, yeye pekee ndiye aliyejua kuwa alikuwa
katika kutabasamu.
Kwa mara ya kwanza akafunua kinywa chake,
huku damu ikimtoka kwa wingi akajilazimisha
kuzungumza hivyohivyo.
“Anataka mali yake aondoke zake….” Akaitoa
kauli ile kisha akalegea askari wakawahi
kumdaka kabla hajaanguka chini. Wakamweka
chini taratibu.
Na hapo ndipo alipoichafua ofisi nzima.
Akaanza kukohoa kila akikohoa anarusha damu!!
Jitihada za kumsaidia ziligonga mwamba.
Walifuta damu kwa leso lakini ilikuwa sawa na
kazi bure tu!!
Huku mapokezi askari mwingine wa kike alikuwa
katika tatizo jingine mwanadada ambaye hata
jina alikuwa hajajitambulisha alikuwa ameenda
kituoni pale kuelezea shida yake katika namna ya
kupayuka bila kueleweka anasema nini, kwa jinsi
askari yule alivyokuwa amechanganyikiwa na hali
iliyomkumba askari mwenzao hakuweza hata
kumsikiliza. Yule dada hakukoma kuzungumza
aliendelea kusema huku akirukaruka huku na kule
kudhihirisha jinsi alivyotishwa na taarifa ile.
Wakati wakiendelea kutoelewana, mlango wa
mkuu wa kituo ukafunguliwa na maaskari kadhaa
walikuwa wameubeba mwili wa Jenny.
Mwili huu ulipoonwa na yule mlalamikaji pale
mapokezi mayowe yakaanza upya.
“N’do huyu…..mamaaaa nakufaaaa…” alipiga
mayowe makubwa. Askari mmoja akawahi
kumdhibiti na kumlazimisha atulie.
“Wewe ni nani?”
“Naitwa Anitha ……huyu amekuja kunitishia amani
nyumbani kwangu, ananitishia kuniua
mimi….anataka nimpe kitu nisichokijua…” Anitha
akajibu huku akiwa bado ametaharuki na asiamini
kile alichokuwa anakiona.
“Amekuja saa ngapi?”
“Kama dakika arobaini na tano zimepita…. Ni
huyu sijamfananisha hata namba zake begani
nilizikariri, na niliziandika hapa..” akaonyesha
mkono wake.
Kweli kabisa, namba za Jenny zilikuwa katika
mkono wa Anitha.
Maajabu haya!! Jenny alienda vipi kwa Anitha na
kisha akafika kituo cha polisi bila kuonwa na
watu wengine nje!!
Ilistaajabisha.
“Kwa nini umekimbilia kituo hiki?”
“Nahitaji kuzungumza na mume wangu, kama
kuna lolote linaendelea anifahamishe siwezi
maisha haya ya mashaka…”
“Mume wako? Mume wako anakuwaje hapa. We
ni mke wa askari..”
“Hapana mume wangu yupo mahabusu hapa
hapa nimeambiwa.”
“Jina nani?”
“Mimi?”
“Hapana yeye?” askari akajibu…
“Gerlad Getonga!!” Anitha akatoa utambulisho.
Kimya kikubwa kikatanda, Inspekta akabaki
mdomo wazi. Maaskari wengine wakabaki
kuguna.,
“We ndo mke wa Gerlad Getonga?” aliuliza huku
akiwa haamini.
“Ndio afande!”
Askari mmoja mwenye papara akajikuta
akiropoka kuwa Getonga ametoroka na
anatafutwa na jeshi la polisi.
Anitha akatumbua macho kisha akalegea na
kuanguka chini huku akipoteza fahamu papo
hapo.
Na hakuzinduka katika dunia ya kawaida hadi
aliposafiri kwenda nchi asiyoijua… nchi iliyojaa
mauzauza ya aina yake!!
***
Milango haikufunguka lakini mwanadada mrembo
kupindukia aliingia katikati ya kundi la mahabusu.
Macho yake makali yakamtazama mahabusuy
mmoja baada ya mwingine. Wakasalimu amri na
kuketi chini kisha kusinzia kabisa.
Kasoro watu wawili tu nd’o waliobaki na fahamu
zao.
“Rebeca…. Rebeca ulikufa Rebeca…” Kindo
alizungumza kwa kitetemeshi cha uoga. Yule
mwanadada akaanza kucheka huku akimkaribia
na kumkaba koo. Kindo akakodoa macho yake
asijue nini cha kufanya. Hata Gerlad naye
hakuwa na la kumsaidia alikuwa ametingwa na
hofu huku akishuhudia maajabu makubwa kupita
yote aliyowahi kuyaona katika ujana wake.
“Wewe na wewe….” Yule dada alisema kwa sauti
ya chini lakini yenye amri akasita kisha
akaendelea, “Leo ninaondoka na nyie, naondoka
nanyi usiku huu, hilo sio ombi hii ni amri yangu
na hakuna wa kuitengua!! Wanadamu huwa
mnajifanya mnajua sana kutengua amri, hii yangu
haitenguki na kama ukiitengua basi elewa kuwa
kuna gharama utalipa….wewe (akimtazama
Gerlad Getonga), ukiitengua amri hii kwa namna
yoyote ile basi mkeo na mtoto wako watakuwa
sadaka yangu, nitawang’oa macho kucha, na
masikio yao. Na utayala kama chakula chochote
kile kiliwavyo!!!” akasita na kumwacha Getonga
aingiwe na maneno yale.
“Halafu wewe dogo (akimtazama Kindo),
nitang’oa kichwa chako na kisha kumpelekea
mama yako makaburini huko akione kilivyokuwa
kibaya. Halafu kiwiliwili chako nitakisaga katika
mashine ya kusagia nyama na kisha huyu
mwenzako atakunywa kama mtoli… si unaujua
mtoli nyau wewe!!” alitoa karipio. Hakuna
aliyejibu chochote.
“Ooooh!! Nimeukumbuka mtoli jamani… dah!”
akasema kwa utulivu kisha akafanya tabasamu
na kumalizia tena kauli yake, “Nitakusaga na
kukufanya mtoli”
“Tunaondoka sasa hivi… dakika hii hii…”
alimalizia hiyo kauli huku akiwa amewakamata
mikono Kindo na Getonga. Wakalisogelea lile geti
ambalo hata mtoto mdogo hawezi kupita.
Rebeca alizidi kulikaribia.
Getonga akatarajia kuwa watakwama pale, lakini
haikuwa sahihi. Wakapenya kana kwamba hakuna
geti pale. Wakaongozana huku wakiipita ile maiti
iliyopondeka vibaya ya askari wa kiume.
Wakamfikia askari wa kike ambaye alikuwa hoi
kabisa.
Rensho akamnyanyua kwa mkono mmoja huku
akimwachia Kindo huru, akamsogeza hadi nje na
kisha akampa maagizo.
“Unaenda nyumbani kwa Anitha muda huu huu,
mwambie kuwa nitafuata kidole changu kama
hayupo tayari kunipa mzigo alioachiwa na
mumewe. Msalimie sana…” alimaliza kutoa
maelekezo. Yule askari akiwa anatokwa damu
sura imemvimba alipiga hatua kama msukule
akienda sehemu ambayo hajawahi kufika, akienda
kufanya jambo asilolijua.
Rensho na akina Kindo wakapita katika
vichochoro kadhaa na kutokea katika jumba
kubwa la kifahari!!! Wakaingia ndani na mageti
yakajifunga!!
Rensho akatoa kicheko!!
Akazidi kuwaongoza hadi katika vyumba viwili
tofauti, kila mmoja akiingizwa katika chumba
chake.
Milango ikafungwa!!
ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Getonga akatarajia kuwa watakwama pale, lakini
haikuwa sahihi. Wakapenya kana kwamba hakuna
geti pale. Wakaongozana huku wakiipita ile maiti
iliyopondeka vibaya ya askari wa kiume.
Wakamfikia askari wa kike ambaye alikuwa hoi
kabisa.
Rensho akamnyanyua kwa mkono mmoja huku
akimwachia Kindo huru, akamsogeza hadi nje na
kisha akampa maagizo.
“Unaenda nyumbani kwa Anitha muda huu huu,
mwambie kuwa nitafuata kidole changu kama
hayupo tayari kunipa mzigo alioachiwa na
mumewe. Msalimie sana…” alimaliza kutoa
maelekezo. Yule askari akiwa anatokwa damu
sura imemvimba alipiga hatua kama msukule
akienda sehemu ambayo hajawahi kufika, akienda
kufanya jambo asilolijua.
Rensho na akina Kindo wakapita katika
vichochoro kadhaa na kutokea katika jumba
kubwa la kifahari!!! Wakaingia ndani na mageti
yakajifunga!!
Rensho akatoa kicheko!!
Akazidi kuwaongoza hadi katika vyumba viwili
tofauti, kila mmoja akifungiwa katika chumba
chake. Milango ikafungwa!!
“Mwanadamu…..we mwanadamu…” sauti
inayokoroma ilimshtua Getonga kutoka katika
dimbwi la usingizi uliokuwa umemtwaa.
Akapikicha macho yake na kukutana na sura
ambayo hakuelewa kama ni ya mwanaume ama
mwanamke. Akayashusha macho yake chini
kidogo akabaini kuwa kiumbe kilichokuwa mbele
yake kilikuwa na mguu mmoja tu, na mwingine
ulikuwa umekatika kabisa.
“Amka ule!!” sauti ile ikaamrisha kwa kukoroma
vilevile.
“Sijisikii kula…” akajikuta ametokwa na jibu lile
huku akijaribu kujizuia asitaharuki zaidi..
Kile kiumbe kikaanza kucheka kwa sauti ileile
inayokoroma kisha kikazungumza, “Ukikitaa kula
sasa utaishia kula masikio yako ana vidole vya
mikono yako….mwanadamu ewe mwanadamu!!
Bora ule”
Getonga akashtushwa na kauli ile kutoka kwa
kiumbe kile. Lakini kabla hajaendelea kile kiumbe
kilitoweka na kurejea baada ya dakika tano.
“Tazama…tazama kisha nikueleze jambo..”
kiumbe kilirusha picha kadhaa katika chumba
alichokuwa amefungiwa Getonga.
“Nini hiki?” aliuliza baada ya kutazama. Zilikuwa
picha za msichana akiwa katika mikao tofauti
tofauti. Alikuwa anavutia sana kumtazama.
“Niliwahi kuwa mrembo sana, mrembo kupita
wasichana wengi sana. Nilipoletwa huku
nikauthamini urembo wangu, nikasusia chakula.
Nilichoambulia ni kula sikio langu….” Akasita na
kugeuka upande wa kuume, Getonga
akashuhudia tundu dogo bila kuwa na sikio, mwili
ukamsisimka akauma meno yake.
Yule kiumbe akaendelea, “nilikula vidole vya
miguu yangu, na hatimaye nikala mguu wangu……
kufikia pale nilijuta lakini nilikuwa nimechelewa
tayari… je mtanashati kama wewe unataka
yakutokee kama yaliyonitokea mimi…mwanadamu
eeh mwanadamu!!” akamaliza huku akiwa
amemkazia macho Getonga.
“Na hata jina langu lilikuwa zuri sana, niliitwa
Queen nilipokuwa mwanadamu…”
“Ulipokuwa mwanadamu? Kwani sasa wewe ni
nani?” hatimaye Getonga aliuliza.
“Mimi si mwanadamu tena bali mnyonyadamu…”
alijibu kwa ujasiri kisha akacheka kidogo.
Getonga akashindwa kuuzuia mkojo uliokuja
ghafla.
Akajikuta anajikojolea!!
“Nakufananisha ama nimewahi kukuona mahali?”
kile kiumbe kilisema hayo huku macho yake
yakiwa yamekaza kuutazama uso wa Getonga.
“Wewe ulikuwa nani duniani kwani?”
“Mwandishi…nilikuwa mwandishi..”
“Hapana sijakutana nawe katika uandishi lakini
mimi na magazeti wapi na wapi, ni sehemu gani
labda pengine umewahi kuishi…..”
“Dar, Mwanza, Iringa, Mbeya, Kigoma, Musoma
na Pwani….” Alijibu Getonga kwa umakini kabisa
akitarajia kuwa kiumbe yule anaweza kuwa
msaada.
“Sijaishi mkoa hata mmoja kati ya hiyo.
Yawezekana mnafanana tu… lakini haya macho
haya….haya macho yamewahi kunitazama…. Na
sio mara moja….tumewahi kukutana hakika”
Alizidi kuvuta hisia, Getonga akifanya juhudi za
kumwomba Mungu amkumbushe kiumbe yule ni
wapi wamewahi kukutana….
Haikuwa hivyo, kiumbe akatoweka akiamini kuwa
amemfananisha.
Getonga akabaki mwenyewe tena akijiuliza ni kitu
gani yule mwanadada wa kujiita Rensho alikuwa
akikitaka kutoka kwake.
Wanyonya damu?? Ana maana gani huyu kiumbe
***
Milango ilifunguliwa chumba kingine, yule kiumbe
aliyedai kuwa aliitwa Queen akiwa duniani
alikuwa anaendelea kusambaza chakula kwa
watu kadhaa waliokuwa katika jumba hilo.
Hapakuwa na chakula cha ziada zaidi ya nyama
na mboga za majani na matunda mchanganyiko.
Haikujulikana ni nyama ya mnyama yupi.
Katika chumba alichoingia ndipo alipopata jibu na
upesi aliufunga ule mlango na kuanza kurukaruka
na magongo yake hadi akakifikia chumba
alichokuwa amefungiwa Getonga!!
“Mwanadamu…eeh mwanadamu….” Akaita.
Getonga akajongea mlangoni.
“Sasa nimejua ni wapi tumewahi
kukutana…..tumewahi kukutana katika macho
yako ya pili duniani..”
“Macho yangu ya pili duniani? Sikuelewi?” alihoji
huku akiwa anatetemeka.
“Ukiogopa unazidi kufanana naye…”
“Nani sasa?”
“Eva…. Unamjua Eva wewe?”
“Eva mtoto wangu…Eva, yupo wapi mwanangu??
Namtaka mwanabgu!”
“Yupo katika maandalizi ya mwisho ya
kunyonywa damu, amenawiri vya kutosha na
malikia ana kiu kubwa sana… na ana hasira
wanadamu wanamkera sana” alijibu kiumbe yule.
Getonga akalegea na kuketi chini.
“Mwanadamu…njoo hapa njoo…” kiumbe sasa
alinong’ona, Getonga akiwa hajui la kufanya
alijisogeza karibu. Na hapo akatambua bayana
kuwa yule kiumbe alikuwa ananuka sana na
aliponyanyua kinywa azungumze ndipo harufu
ilizidi kuwa mbaya.
“Mshukuru Mungu wako kuwa ni mimi niliyefyeka
vile vidole vyake viwili….nikafanikiwa kuyaona
macho yake vizuri..na sasa nimeyaona hayo
macho kwako na kukutambua kuwa ni baba wa
kiumbe kile. Mwanadamu!! Mwanadamu, kwani
upo tayari kufa na kuiacha familia yako
ikiteseka? Ama unafurahia kuona mwanao asiye
na hatia anateseka namna hii katika ulimwengu
mchafu kama huu?” alihoji yule kiumbe huku
macho yakiwa maangavu kabisa.
“Sitaki, nisaidie nitoke humu ndani!! Na kwanini
mmekata vidole vya mwanangu eeh!!”
“Kila mmoja anataka kutoka humu ndani lakini
hajui cha kufanya ili atoke…lakini wewe unalo la
kufanya ili utoke…”
“Lolote nitafanya nisaidie!!” alijibu Getonga huku
hofu ikiwa inazidi kumtawala.
“Hautatoka kwa utanashati wako, lakini kama
ukifanikiwa kutoka basi ni kwa sababu moja tu…
nimempenda sana mtoto wako na siko tayari
kushirikisha macho yangu kumtazama akiuwawa
mbele yangu.. kama ukikamatwa akauwawa
ukiwa naye wewe ni sawa juu yako, lakini
sitakuwa tayari kushiriki walau kuiona maiti yake.
Mtoto wako anakupenda sana lakini wewe
humpendi mwanao, licha ya wakati mgumu kama
huu anakupendeni sana wewe na mama yake….
Yeye si kama watoto wengine akilia alilie mama
tu, huyu analilia baba na mama…. Ni wa pekee
sana.” Kwa sauti ya chini kabisa yule kiumbe
alinena na Getonga.
“Ni usiku wa kesho kutwa nd’o unaweza kutoka
lakini unatakiwa uniahidi kama utaweza kutimiza
masharti yangu na kisha nikupe masharti yako.
Kwanza jibu maswali yangu mawili….” Akaweka
kituo kisha akavuta pumzi na kuendelea.
“Unapafahamu Kahama?”
“Ndio napafahamu!!”
“Umepafahamu vipi?”
“Niliwahi kuishi kule…” akajibu Getonga.
“Ahaa kumbe, hebu sogea karibu yangu zaidi..”
kiumbe kikamsihi Getonga kwa utulivu, naye
akatii huku akitetemeka. Lakini safari hii haikuwa
kwa amani. Kiumbe kikapitisha mkono wake
upesi katika tundu lililokuwa kila baada ya nondo
moja. Mkono uliokomaa ukalichapa shavu la
Getonga na kumbamiza ukutani, akatokwa na
yowe kubwa sana la hofu na maumivu.
“Pumbavu sana wewe, unadhani hapa tupo
duniani unanidanganya mimi kama wasichana
wenu mnaowadanganya huko kila kukicha?
Dakika tano zilizopita umejibu kiufasaha sehemu
ambazo umewahi kuishi Tanzania, Kahama
haikuwa katika orodha, sasa nakuuliza juu ya
Kahama unasema umewahi kuishi huko.
Mwanaume mwongo sana wewe, huenda hata
humpendi mtoto wako shenzi kabisa…tena …”
akakoma kidogo, akarudi nyuma na kuchukua
ufunguo mkubwa akaufungua ule mlango.
Akamkuta Getonga bado yupo chini,
akamnyanyua na kumweka vyema kisha
akamtandika kofi kali katika paji la uso kisha
akamziba mdomo asiweze kupiga kelele.
Maumivu yakasambaa kwa kasi huku
akitetemeka.
“Yaani unanidanganya mimi wakati nataka
kukusaidia…”
Akambamiza ukutani huku akiwa amemziba
mdomo, sasa akiwa hana magongo bali
amesimamia mguu mmoja tu, akampiga kichwa
kifuani, Getonga akalainika na kuketi chini huku
akishindwa kusema neno nisamehe…likaishia
hewani!!
“Tena ngoja niwahishe tarehe yenu ya
kunyonywa damu shenzi wewe!!! Kumbe malikia
yupo sawa kuwachukia wanadamu” Kiumbe
kikatoweka kwa ghadhabu!!
Getonga aliyasikia maumivu yakitambaa mwili
mzima, hakuamini kama kiumbe yule alikuwa na
nguvu na maamuzi ya kikatili namna ile. Getonga
akajutia uongo wake, huku akipata fursa ya
kukumbuka maisha halisi ya duniani. Hadi wakati
huo alikuwa anajiuliza kama uongo mdogo kiasi
kile ameambulia adhabu ile, vipi ule uongo wa
usaliti!!
“Laiti kama wanawake mia kama hawa
wamwagwe duniani..wanaume tutaacha uongo
kwa kweli…” kisha akatabasamu baada ya wazo
hilo.
“Kisa umejua kuwa nakupenda wewe na mwanao
ndo unaanza kuninyanyasa wewe mwanadamu
kwa kunionyesha uongo wako mapema, ama kwa
sababu si mrembo tena….” Getonga akashtuka
kuisikia sauti ya kukoroma pale mlangoni!!
“Naomba usinidanganye tena tafadhali, sijisikii
kufanya nilichotaraji kufanya, nahitaji urejee kwa
mkeo, nahitaji umtunze mwanao…… ni kweli
unapafahamu Kahama?”
“Napafahamu kwa jina tu lakini sijawahi kuishi…
nisamehe”
“Nimekusamehe…na je unamfahamu mwanadada
anayeitwa Salome??”
“Nimekutana na Salome wengi sana, sijui ni yupi
unayemuulizia?” alijibu kwa nidhamu huku akiwa
palepale chini.
“Salome mtoto wa mzee Wilbard… Salome
Wilbard umewahi kusikia jina hilo”
“Hapana sijawahi lakini nawajua akina Salome
wengi…”
“Salome mjamzito….ujauzito wake una miezi
miwili sasa ama mitatu!! Je unamfahamu Salome
mjamzito?”
“Aaah!! Naweza kuwa namfahamu lakini nisijue
kama ni mjamzito, nawajua akina Salome
kadhaa…” alijibu kwa umakini Getonga.
“Salome ndiye atakayekuweka huru kwa sababu
Salome ndiye aliyekuingiza katika matatizo haya
wewe na mwenzako huyo bwege ambaye hawezi
kuzungumza.” Sauti ya kukoroma ilitoa
maelekezo yale.
“Salome? Salome ameniingiza mi matatizoni…
Salome gani huyo?” Getonga alijiuliza huku akili
yake ikifanya kazi kwa mwendokasi mkubwa
mno.
“Nampata wapi huyo Salome nimtie adabu zake!!”
akauliza huku akiwa ametaharuki.
“Yupo Kahama sasa…. Mnapajua nyie wenyewe
wanadamu… hata malikia wetu anamtafuta,
alikuwa anakutafuta wewe amekupata sasa
amebaki Salome ili aweze kutimiza mambo
yake.”
“Mambo yake? Na ananitakia mimi nini? Na
mtoto wangu je?” alizidi kuuliza Getonga.
“We unamwekea kauzibe kuna mambo zake
unazificha na kumsababishia ashindwe
kutambulika, na huyo Salome naye anamweka
matatani sana na kumfanya akose amani!!” alijibu
kwa utulivu.
“Maskini weee mimi nina nini chake sasa kama
sio uonevu huu jamani eeh na Eva wangu mie..”
akaanza kulia.
“Acha kuwa bwege kama mwenzako unalialia tu…
ulipokichukua kitambulisho chake anachokitumia
katika safari zake na mikutano uliona sifa eeh
sasa unalia lia nini? Mtoto hadi anakatwa vidole
we umekomalia tu kitu usichokijua” kiumbe
akamgombeza Getonga, na hapo akili ya Getonga
ikafyatuka na kuwa kama mwendawazimu.
Akakumbuka kuwa aliwahi kuwa na kitambulisho
ambacho hakuwahi kutazama jina limeandikwa
nani na picha ni ipi. Mbaya zaidi hakumbuki ni
wapi aliwahi kukihifadhi.
“Ukipate kitambulisho, umpate Salome mwenye
ujauzito wa miezi miwili Kahama, na kubwa la
mwisho unatakiwa kuhakikisha humu tumboni
mwangu unaniachia mtoto pia, hata mimi ni
mwanamke nahitaji kuwa na katoto kazuri kama
Eva!! Baada ya hayo utakuwa huru. Kwaheri!!”
kiumbe kikamaliza na kutoweka zake!!
Getonga akabaki katika mtihani mgumu kupita
yote maishani mwake.
Hajui kitambulisho kilipo, hamjui Salome wa
Kahama. Halafu anatakiwa kumjaza ujauzito
kiumbe yule wa maajabu, mwenye mguu mmoja,
asiyekuwa na sikio moja, sura mbaya, na mwenye
harufu mbaya.
Getonga akajisikia kichefuchefu alipojenga
taswira juu ya kifua cha kiumbe yule na harufu
yake chafu….akajizuia asitapike.
**HOFU imefikia mahali pake sasa mahali pa
kuchukua maamuzi kwa ajili ya familia………
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO
“Ukipate kitambulisho, umpate Salome mwenye
ujauzito wa miezi miwili Kahama, na kubwa la
mwisho unatakiwa kuhakikisha humu tumboni
mwangu unaniachia mtoto pia, hata mimi ni
mwanamke nahitaji kuwa na katoto kazuri kama
Eva!! Baada ya hayo utakuwa huru. Kwaheri!!”
kiumbe kikamaliza na kutoweka zake!!
Getonga akabaki katika mtihani mgumu kupita
yote maishani mwake.
Hajui kitambulisho kilipo, hamjui Salome wa
Kahama. Halafu anatakiwa kumjaza ujauzito
kiumbe yule wa maajabu, mwenye mguu mmoja,
asiyekuwa na sikio moja, sura mbaya, na mwenye
harufu mbaya.
Getonga akajisikia kichefuchefu alipojenga
taswira juu ya kifua cha kiumbe yule na harufu
yake chafu….akajizuia asitapike.
WAKATI Getonga akijiuliza iwapo afanye mapenzi
na kiumbe yule wa ajabu ajiitaye mnyonya damu
ama aache litokee janga la kuipoteza familia
yake. Katika kijiji kimoja maeneo ya Ushirombo
nje ya wilaya ya kahama kulikuwa na kikao
kikubwa sana kilichoshirikisha watu watatu,
mmoja akiwa mwanamke.
Mzozo ulikuwa mkubwa sana, wanaume wawili
ambao walikuwa wakimzidi umri yule mwanamke
waliongea kwa amri baada ya lugha ya awali ya
hiari kuonekana kugonga mwamba.
“Magdalena acha ubishi mdogo wangu… tambua
mimi ni kaka yako niliyekuachia titi na wewe
ukanyonya na kunenepa hivi. Mimi ni wa kwanza
kuona jua… na nilishaona hapa hatari ambayo
itatokea. Sawa sijasoma lakini mimba gani ile ya
kuvuja damu kila siku. Mtu hajui alipotoka hajui
hata jina lake we umeng’ang’ania tu na huo
ulokole wako. Mbona huyo mchungaji kama ana
moyo mzuri kwanini yeye asimchukue akae naye
kwake…. Wakati mwingine hii mikosi ya kukosa
mume unajileteaga mwenyewe” alitema maneno
lafudhi ya kisukuma ikishika kasi yake.
“Kaka nakuheshimu sana, nawe niheshimu kama
mdogo wako na kubwa zaidi niheshimu kama
mwanamke!!!” alikemea yule mwanamke yeye
hakutawaliwa na ile lafudhi.
Mwanaume aliyekuwa kando alikohoa kidogo
kisha naye akaingia katika maongezi.
“Vielimu hivi… yaani jasho lilitutoka sisi tukalima
mpunga wewe ukaenda shule lakini leo hii elimu
yako inakufanya ujione wewe nd’o wewe. Laiti
kama baba na mama wangekuwepo
wangekukataa na kukupa radhi nasema…. Hutaki
kytusikiliza kaka zako. Mchungaji anakudanganya
kila siku kuwa ni wema kutunza watu usiowajua,
haya umemtunza huu mwezi wa tatu sijui, mara
hospitali mara mavazi. Yote juu yako, mchungaji
hakusaidii mbona. Haya utasema hizo pesa ni za
kwako…. Sisi hazituhusu. Lakini usalama wa ukoo
wetu. Wewe unafuga mtu huko Kahama majanga
yanatupata sisi.
Magdalena yaani elimu yako haijakusaidia lolote
hadi leo dada yangu….” Alisema kwa upole yule
mwanaume huku akitikisa kichwa.
“Kwani kaka.. nyie mlitaka nifanye nini
labda….maana sijaelewa nia yenu.”
“Umwondoe nyumbani kwako….. aende mbali
kabisa na ukoo wetu.”
“Haya nitamuondoa..”
“Kila mara unasema hivyo… kama anakushinda
twende tutamuondoa kistaarabu tu!!”
“Nitamuondoa mwenyewe!! Kwaherini na
asanteni kwa ushauri, kuhusu lile shamba la
mpunga, nitatuma pesa mnunue yale madawa…”
alitoa kauli hiyo ikiwa ya mwisho kisha
akasimama na kutoweka hadi katika gari lake.
Safari ya kurejea Kahama mjini!!
Ilikuwa yapata saa kumi na moja za jioni!!!
******
Muda huo huo mjini Kahama!!!
Katika jumba bovu ambalo lilijengwa likaishia kati
ujenzi ukakoma baada ya mwenye nyuma hiyo
kuuwawa migodini. Kulikuwa na jambo……
wanaume wawili walikuwa wakihangaika kumtua
mwanamke ambaye alikuwa amepoteza fahamu.
Waliyakumbuka vyema masharti waliyopewa na
mganga wa jadi juu ya utajiri waliokuwa
wakiuhitaji.
Mganga aliwatuma ngozi ya mwanadamu! Wawili
hawa ambao madawa ya kulevya na ugumu wa
maisha ulikuwa umewachanganya walijadiliana
kisha kura yao ikaanguka kwa binti ambaye
alikuwa amezoeana nao. Binti ambaye ni kama
hakuwa timamu sana kiakili na hakujulikana ni
wapi anatokea. Wengine walisema ni msukule
unaishi katika nyumba ya mtu kwa masilahi
binafsi wengine wakadai nd’o dawa ya utajiri ya
mwanamama aliyekuwa akiishi naye.
Vijana hawa wakaona kuwa huyu alikuwa mtu
sahihi wa kumchuna ngozi kwa masilahi yao.
Wakamwekea dawa za usingizi katika pipi,
akauvaa mkenge wakamtorosha hadi katika
jumba lile kubwa.
Sasa hakuwa na fahamu kabisa walimngoja
mtaalamu wa kuchuna ngozi aweze kulifanya
zoezi lao likamilike. Hawakuzungumza chochote
kile kila mmoja alikuwa ana hofu juu ya hili
walilotaka kulifanya.
Wakati wakimngoja mchunaji, mwanaume mmoja
akaanza kuupapasa mwili ule usiokuwa na
fahamu!!!
“Maskini ana mimba halafu!!” akajisemea huku
akimpapasa bado, mara masikio mara mapaja,
mwisho akamfunua nguo yake.
Titi zilizosimama wima zikamdhihaki, akazibinya
kidogo. Yule aliyekuwa ametulia akaingiza mkono
wake maungoni na kujiweka sawa, tayari alikuwa
ameingiwa na matamanio.
Mwisho wakashirikiana na kumvua nguo zote
kisha wakakubaliana kumuingilia zamu kwa zamu
hadi mchunaji afike.
Mwili usiokuwa na fahamu ulikuwa umetulia
vilevile ukiwa umefumba macho!!!
****
KENGELE ya hatari ikagonga katika kichwa cha
Rebeca wa Nshomile akiwa katika kitanda chake
chenye thamani kubwa sana, alijihisi kuwashwa
washwa na mapigo yake ya moyo yakaanza
kwenda mbio. Alijaribu kuinuka akae vyema lakini
usingizi nao ukazidi kumsisitiza arejee kitandani.
“Amka Renshooo hatari!!!” akajikaza na kusema
kwa nguvu, kisha akaketi kitako.
“Amka Renshooo!!” akasema kwa sauti ya juu
tena.
Ndani ya mji wa Kahama mwili wa msichana
aliyetaka kubakwa ukatikisika kidogo. Yule
mbakaji akasita kubaka akamtazama iwapo
atafumbua macho na kuwatambua.
“Suka…Suka.. anataka kuamka, mdunge sindano
atazijua sura zetu huyu…” mbakaji akamwambie
mwenzake ambaye alichukua sindano na kuvuta
maji katika kichupa walichokuwa wameambatana
nacho. Akavuta ya kutosha. Kisha akamuinamia
yule binti.
Akamgeuza.
“Mh! Ana kalio la maana duuh!!” akajisemea huku
akimsuguasugua tayari kwa kumdunga sindano.
“I love KINDO…..sijui nd’o bwanake huyu…duh!!
Jina la bwana linaandikwa hadi takoni aisee!
Huyu demu noma aisee…..halafu hapo unakuta
bwana’ke ndo alimgeuza akamchora huu ujinga…
halafu wakaachana bora hata tumchune tu hii
ngozi maana hawezi kuolewa na mtu mwingine
huyu. Eti? Nani mpumbavu wa kukubali kuoa
mwanamke amechorwa jina la mtu”
“Oya acha maneno mengi choma sindano mi
nipande bwana mizuka inapanda sana.” Alisihi
bwana aliyekuwa uchi.
Jamaa mwenye sindano akainama tena
akampapasa yule binti.
Jijini Dar es salaam katika jumba lisilojulikana
lilipo Rensho akatetemeka tena na kisha akapiga
kelele kuu.
“Amkaaaa Rebecaaaaa…..amkaaaaa”
Wakati huohuo yule binti aliyekuwa amepoteza
fahamu mjini Kahama akanyanyuka kwa nguvu
sana na kumpiga kichwa yule bwana mwenye
sindano kisha akaikwapua ile sindano upesi na
kumdunga nayo uumeni yule aliyekuwa uchi.
Mshikemshike!! Jamaa akatoa mayowe makubwa,
binti akiwa uchi akasimama wima tena akarusha
teke kali katika korodani za yule aliyekuwa uchi
akapoteza fahamu palepale huku akigumia kwa
maumivu makali. Yule aliyebaki akataka
kukimbia, msichana akamdaka na kuikamata
shingo yake akaizungusha kwenda katika upande
usiokuwa wa kawaida.
Kilichofuata hapo ni kile ambacho wawili hao
walipanga kufanya kwa yule msichana.
Binti akazichuna ngozi zao katika mwendo wa
haraka kuliko kawaida bila kusema neno lolote.
Baada ya hapo akatoweka akitembea kwenda
sehemu asiyoijua, hakuwa na hofu yoyote ile na
alikuwa hajitambui, alizidi kwenda mbele tu hadi
aliposimama katikati ya barabara akitetemeka
baada ya kushtuliwa na honi kali za gari na breki.
“Mungu wangu…..” dereva mwanamke akapiga
kelele huku akishika breki kwa wepesi aweze
kumnusuru yule binti.
“Mungu wangu nini hiki….” Akataharuki baada ya
kukutanisha macho na mwanamke akiwa uchi wa
mnyama katikati ya barabara huku nguo zake
zikiwa begani.
Ile sura ni kama aliifananisha lakini alipofumba
na kufumbua tena yule aliyetaka kugongwa
hakuwepo barabarani.
“Mamaweeeeee!!” alipiga kelele huku akiendesha
gari hovyohovyo huku akilitaja jina la Mungu….
“Mh! Ni mtu kweli ama nilikuwa nawaza tu
mimi….” Alijiuliza Magdalena baada ya kupata
utulivu kiasi, mapigo ya moyo yakiwa hayajerejea
bado katika hali yake ya kawaida.
“Sio Martha yule?” alijiuliza kwa sauti,
akimfananisha yule binti barabarani uchi kama
binti ambaye kaka zake walikuwa wakimsihi
amwondoshe pale nyumbani kwake kwa sababu
ni mikosi. Jina Marha ni yeye aliyempatia baada
ya binti yule kushindwa kukumbuka lolote juu ya
historia yake
Magdalena akajiaminisha kuwa ni yale maneno
makali ya ndugu zake yaliyomletea picha ile ya
ajabu.
“Ningeweza kuangusha gari kijinga tu kumbe
hakuna lolote hata!!” aliwaza kisha akapuuza yote
yaliyotokea.
“Na haya ni maono kabisa, yule binti simwondoi
nyumbani kwangu, akina kaka wakichukia wao
wachukie tu!! Tena wasipende kufuatilia maisha
yangu, yaani watu wasiosoma bwana ni shida…
imani mbovumbovu zimejaa kichwani mwao”
alilaani Magdalena huku akiendelea kuendesha
gari lile.
Hakujua kuwa huo ulikuwa mwanzo kizungumkuti,
utata na hofu kuu!!
Laiti angejua!!!!.........
****
Jijini Dar es salaam ndani ya ficho lisilofahamika
wapi linapatikanika, baada ya kutulia Rensho
alisimama akapiga hatua kadhaa mwisho
akakifikia chumba alichokuwa amehifadhiwa
Gerlad Getonga. Kichwani mwake alijua kabisa
kuwa alisafiri maili kadhaa na alipigana na kundi
la watu ili kuusalimisha uhai wake, lakini hakujua
ni wapi uhai wake umehifadhiwa. Jambo ambalo
lilimkera kuishi kwa mashaka na hofu.
Nani huyu anayeshiriki katika uhai wangu!!!
Nataka kuishi shenzi zake. Halafu hayo mabazazi
yalitaka kumfanya nini yale maana kama
yalimlewesha hivi. Sijui mwannaume sijui
mwanamke huyo….
Maswali lukuki yakakighafirisha kichwa chake.
Akapandwa na hasira
“We fala Salome yupo wapi na kitambulisho
changu kipo wapi….” Aliuliza kwa shari kuu huku
akimtazama Getonga.
Getonga akajivika ujasiri hakujibu lolote
akatabasamu.
“Nakuuliza wewe….Salome yupo wapi, nahitaji
kujua alipo na pia kitambulisho changu. Hivi
wanadamu mbona wabishi nahitaji kuondoka
hapa… bado mnaning’ang’ania tu….” Alifoka kwa
sauti ya juu sana.
“Simjui salome na wala kitambulisho sikijui…”
alijibu kwa utulivu. Rensho akatoweka bila
kusema neno lolote.
Na baada ya muda geti likafunguliwa, Gerlad
akashikwa mkono na watu asiowajua na
kuongozwa kuelekea mahali.
Giza likatawala kisha akaufikia mwanga….
“Jibu moja la kipumbavu naondoa hii pua ya
mkeo!!” alikuwa ni Rensho akiwa amemning’iniza
Anitha mke wa Gerlad Getonga katika mbao nne
imara akiwa amefungwa kamba.
Getonga akapigwa na butwaa!!
“Kitambulisho, pili Salome anapatikana wapi…
hakuna jibu nachinja. Huwa sionyi mara mbili!!!”
Rensho akazungumza kwa sauti ya chini!! Na
wakati huo akahamishia kisu kuelekea katika
shingo ya Salome.
Getonga akatamani kusema lolote ajuala lakini
bahati mbaya hakuwa akijua lolote!!!
Mshikemshike!!!
**GETONGA hajui lolote na bado natakiwa kujibu
maswali.. kama hana majibu haipo nafasi ya
kujitetea ni mkewe kuuwawa kwa kuchinjwa!!
ITAENDELEA!!!
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA
Na baada ya kuda geti likafunguliwa, Gerlad
akashikwa mkono na watu asiowajua na
kuongozwa kuelekea mahali.
Giza likatawala kisha akaufikia mwanga….
“Jibu moja la kipumbavu naondoa hii pua ya
mkeo!!” alikuwa ni Rensho akiwa amemning’iniza
Anitha mke wa Gerlad Getonga katika mbao nne
imara akiwa amefungwa kamba.
Getonga akapigwa na butwaa!!
“Kitambulisho, pili Salome anapatikana wapi…
hakuna jibu nachinja. Huwa sionyi mara mbili!!!”
Rensho akazungumza kwa sauti ya chini!! Na
wakati huo akahamishia kisu kuelekea katika
shingo ya Salome.
Getonga akatamani kusema lolote ajualo lakini
bahati mbaya hakuwa akijua lolote!!!
Mshikemshike!!!
Zilikuwa ni sekunde takribani thelathini zilibaki ili
Getonga ashuhudie kifo cha mkewe na hakujua
iwapo Eva mtoto wake naye atauwawa kwa
mtindo huohuo.
“Rebeka….” Getonga aliita kwa sauti ya juu kiasi.
Rensho akageuka kumtazama.
“Huyo mama ukishamuua na kitambulisho
kisipatikane utakuwa umesaidia nini?”
“Gerlad Getonga na siasa zako tangu utotoni
nikikuruhusu kuzungumza utanishinda tu…. I need
my ID” Rensho aling’aka. Kisha akaongezea “Na
nahitaji pia kujua Salome yupo wapi….”
“Kuhusu kitambulisho kiukweli sikijui lakini
ukinielekeza kilivyo naweza kukusaidia kutafuta,
na kuhusu Salome yupo Kahama ukiniruhusu
vilevile naweza kukusaidia kumsaka….”
Maneno yale yakamtuliza Rensho kidogo,
akashusha kisu na kisha kumkaribia Getonga
waweze kuzungumza kiurafiki.
Rensho akaamua kuwa mpole zaidi na hatimaye
akaamua kumweleza Getonga mambo kadha wa
kadha juu ya utata uliotanda.
Getonga alikuwa msikivu sana akisikiliza historia
ya maajabu ya mtoto aliyesemekana kuwa
alikufa ulimwenguni na kuzikwa ilhali alikuwa
mzima katika ulimwengu mwingine.
“Wanadamu ni wabaya sana..watazame na
uwaache hivihivi na siwapendi kabisa. hata wewe
wasingekuwa mke na mtoto wako ningekuua siku
ile ulipokwenda kwa mama yake Kindo kufuatilia
jambo hili, hakuna kitu sipendi kama kufuatiliwa!!”
akasita kidogo kisha akamtazama Getonga
machoni kwa sekunde kadhaa. Macho yake
yakaanza kujaa hofu ghafla, akakosa amani na
mara akaanza kutokwa na kauli za ajabu ajabu.
“Shit!!!” ghafla Rensho alishtuka huku kile kisu
kikimtoka na kuanguka chini, aliyumba kama
anayesukumwa na mtu asiyeonekana, aliwahi na
kuushika mti uliokuwa jirani naye.
“Amkaaaa Renshoooo!!!” alipiga kelele huku
akitapatapa huku na kule.
“Amka watashtukiaa!!” alitokwa na ukelele tena.
Getonga akabaki kushangaa.
Hakujua kuwa Rensho yu katika mapambano
makali sana.
****
MAGDALENA aliegesha gari eneo maalumu
ambalo huwa analitumia kila siku kutokana na
ufinyu wa eno katika nyumba aliyokuwa akiishi.
Kisha akautwaa mkoba wake na kujizoazoa hadi
nyumbani kwake.
Tofauti na siku zote kukuta Martha amepika
chakula ama la yupo jikoni katika hatua za
mwishomwisho. Siku hii palikuwa kimya sana.
“Martha weee!!” akaita kwa sauti yake iliyojaa
upole.
Kimya!!
Akaita tena kwa sauti iliyoanza kupanda juu.
Lakini bado ukimya ulitanda. Magdalena akautua
mkoba chini na kwenda kutazama nini kimemsibu
Martha chumbani kwake.
Alifika na kukigonga chumba lakini hapakuwa na
jibu, akaelekeza jicho lake katika kitundu cha
kuingizia ufunguo.
Kitanda kilikuwa tupu, akataka kuufungua mlango
lakini upepo wa ghafla uliobamiza milango na
madirisha ukamfanya aghairi na kwenda
kupambana katika kufunga mlango mkuu na
madirisha.
Upepo huu ulikuwa wa ajabu sana, ni kama
ulikuwa ukipambana naye asiweze kufunga
mlango, alijaribu kusukuma bila mafanikio, upepo
ule wenye baridi na vumbi ukamzidi nguvu kama
masihara, upepo ukaingia na kutokea dirishani.
Kisha hali ikawa shwari……
Magdalena akatoka nje kutazama ni madhara
gani yamejiri kwa jirani zake, lakini akastaajabu
kuwa wengine walikuwa wameketi nje
wanasukana. Na wengine walikuwa wametingwa
jikoni wakipika.
Mh!! Upepo gani huu Mungu!! Alijiuliza huku
akirejea tena ndani, akajitupa kwenye kochi,
akawza juu ya hayo mambo mawili yaliyomtokea
kwa kipindi kifupi sana.
Kwanza kumkosakosa msichana barabarani
akiwa uchi, kisha upepo mkali uliopoa ghafla.
Hapohapo jicho lake likatua mlangoni, akaona
kiatu cha Martha, akakumbuka kuwa kabla ya
upepo kuvuma alikuwa chumbani kwake akifanya
jitihada za kumtazama nini kinamjiri, hakumuona
kitandani na alipotaka kufungua mlango ndipo
upepo ukaanza kuvuma.
Magdalena akasimama kiunyongeunyonge
akakiendea chumba tena, akafika na kukifungua
moja kwa moja.
“Oh! My God…” akatokwa na mshtuko. Alikuwa
anatazamana na Marha akiwa amelala uchi wa
mnyama kitandani, na alikuwa hoi kweli.
Dakika kadhaa zilizopita hakuwa kitandani, sasa
amelala hoi bin taabani.
“Mshenzi atakuwa ameingiza mwanaume humu
ndani…. Walikuwa wanafanya mapenzi
amemficha sasa anajifanya amelala..” akawaza
Magdalena kisha akakisogelea kitanda na kuanza
kumtikisa yule binti ambaye alimbatiza jina la
Martha.
“I love KINDO” Magdalena aliyaona maneno yale
katika makalio ya Martha. Akaendelea kumtikisa.
“Kindo jina kutoka Iringa hili… Kindole…” alipitisha
wazo hilo katika kichwa chake kilichokuwa
kimevurugwa haswa.
“We Martha wewe…..” aliita huku akiangaza huku
na huko kama upo uwepo wa mtu mwingine
ndani ya kile chumba.
Dakika tatu baada ya jitihada za kumuita bila
mafanikio, Magdalena aliamua kulifikisha jambo
lile kwa mjumbe!!
Wakaongozana hadi nyumbani ili waweze kujua ni
kitu gani kimemsibu Martha.
Wakati Magdalena anafika kwa mjumbe na
kumweleza juu ya hali ya mwanaye kitandani. Ni
wakati huohuo jijini Dar es salaam, mwanadada
mrembo wa kuitwa Rensho alikuwa amefumba
macho akihaha kupiga kelele za kumuamsha
Martha kwa namna yoyote ile. Aliita kwa nguvu
sana huku kila anayemtazama akiduwaa.
Mjumbe na Magdalena waliporejea wakamkuta
Magdalena akiwa sebuleni ameketi akiwa na
mavazi yake, mkononi akiwa na dawa za kutuliza
maumivu.
“Shkamoo mama…shkamoo mjumbe.” Alitoa
salamu ile kwa kujiamini lakini akionekana kuwa
hayupo sawa.
“Marahaba Martha….. we mama na huyu hapa?
Wanawake mbona mnatutia presha hivi sisi,
nimezeeka jamani mimi” alilalamika mjumbe.
Magdalena alikuwa amekodoa macho tu
akimtazama Martha hakuamini hata kidogo kuwa
ndiye huyu ambaye hakuwepo kitandani kisha
akaonekana kitandani akiwa hoi usingizini na
sasa yupo sebuleni.
Hofu ikatanda waziwazi!!
Mjumbe aliondoka akiwa amejaa ghadhabu
kubwa. Akamlaani Magdalena kwa kumpotezea
wakati na kumtia hofu pasipo na sababu.
“Martha umekuaje mama…eeh!” alimuuliza
walipokuwa wamebaki wawili.
“Kichwa kinaniuma mama…..”
“Pole mwanangu. Tangu muda gani una hali hii.”
“Yaani tangu nilale mchana sijaamka hadi sasa
hivi.”
Mh! Tangu mchana wakati sijamkuta kitandani
huyu…..
“Martha hakuna kitu sipendi kama kudanganywa
katika maisha yangu..” alionya Magdalena huku
akitetemeka kwa hasira, wazo lake lilikuwa
palepale kuwa Martha ni muongo. Na siku hiyo
atakuwa aliingiza mwanaume ndani ama la
alienda kwa mwanaume mahali.
“Sikudanganyi mama..nililala tu na sijatoka
nyumbani.” Martha alijibu kwa upole.
Magdalena alisimama na kuzunguka huku na kule
kisha akamvaa Matha tena.
“Niambie ukweli jioni hii kabla hujaigiza kuwa
umesinzia kitandani uchi, ulikuwa unafanya nini?”
“Mama sijawa sehemu yoyote na sijatoka
kabisa….. kichwa kimeniuma sana.”
“Ok! Hebu ngoja….” Alisema na kuiacha ile kauli
ikielea hewani akaingia chumbani ili aweze
kuhakikisha ni kitu gani Martha anamficha.
Alipokifungua chumba tu… kitu cha kwanza
kugundua kilikuwa ni kiatu cha kiume.
“Mwanaharamu mkubwa huyu!!” akatokwa na
kauli nzito huku akikibeba kile kiatu.
“Nahesabu hadi tatu..wewe kidume uliyejileta
ndani ya nyumba hii kuzini na binti yangu kama
hujajitokeza. Naita polisi na utajuta kwa kitendo
ulichokifanya.” Alitoa karipio kwa sauti ya juu
sana iliyojaa kitetemeshi.
Martha akiwa sebuleni akaiona dalili ya mama
yake huyo wa kufikia kurukwa na akili.
Mwanaume gani ndani ya chumba chake. Ni
jambo ambalo halikumuingia akilini kabisa.
Akaona isiwe tabu, akasimama na kuelekea
chumbani kwake.
“Mama….”
“Nani mama yako mshenzi wewe… Martha
kukupenda kote kule leo hii unaniletea
mwanaume ndani ya nyumba yangu. Ulitaka
nikupendeje wewe. Matha nimekuokota huna hili
wala lile wewe eeer” alizungumza kwa uchungu
mkubwa.
“Mama mimi na wanaume wapi na wapi?”
“Hiki kiatu cha kwako eeh!! Cha kwako
nakuuliza?” Magdalena alimwonyesha kile kiatu
kwa kumsuta. Matha alipokana kuwa hakijui
akawa ametibua hasira za Magdalena.
Kipigo kikachukua nafasi!!
Magdalena alipiga kama mwizi!!
Jijini Dar es salaam, Rensho akaanza kuingiwa
na hofu ya usalama wake.
“Renshooo atakuuua…. Pigana wewe….” Alipiga
kelele huku akianguka chini na kugaagaa.
Alikuwa akiunguruma kama mbwa aliyejeruhiwa
ama mwenye hasira.
Mjini Kahama, Martha ambaye ni Salome.
Akaudaka mkono wa mama yake wa kufikia,
akaanza kuuviringisha, yule mama hakuamini.
Akaanza kujitoa lakini hakuweza, Martha
akarusha mkono na kumnasa kibao kikali yule
mama.
“Martha unanipiga mimi…” aliliza na asiamini
kinachotokea. Martha hakumjibu, akauzungusha
mkono kwa nguvu zaidi mama akapiga mayowe
yalkiyoambatana na mlio wa mkono kuvunjika.
Teke zito likamtoka Martha na kusambaratisha
mbavu kadhaa katika ubavu wa yule mama na
palepale akapoteza fahamu.
****
KESI mbili zikapata muunganiko na kushabihiana.
Wanaume wawili wamekutwa wamechunwa ngozi
nje kidogo ya mji wa Kahama. Katika eneo la
tukio vimekutwa viatu vitatu, viwili vikiwa
vinafanana na kimoja kikikosa mwenzake.
Kiatu kilichokosa mwenzake kimekutwa maeneo
ya kahama mjini katika nyumba ya mwanamke
anayedai kujeruhiwa na binti yake wa kufikia, na
kiatu hicho kilikuwa chumbani mwake.
Mwanamke huyo aliyejeruhiwa vibaya huku
akivunjwa mkono wa mbavu mbili alifahamika
kwa jina la Magdalena na anadai anayeweza
kujua wapi kile kiatu kimetoka anakwenda kwa
jina la Martha.
Mama yule akaongeza kuwa katika makalio ya
yule binti kuna jina KINDO hivyo kwa namna
moja ama nyingine anaweza kuwa anahusika
kufahamu huyu binti ni nani na anapatikana wapi.
Mahakama ya wilaya haikuwa na uwezo wa
kusikiliza kesi ile ya mauaji. Kesi ikahamishiwa
jijini Dar es salaam
Martha akaanza kusakwa kwa kesi ya mauaji na
kisha kuchuna ngozi za mwanadamu.
Kindo akahusishwa katika kusaidia upelelezi!!
Wakati kesi hii ikishika kasi.
Getonga na Rensho walikuwa wasafiri katika basi
la abiria kutoka Dar es salaam kwenda Kahama
kwa sababu moja tu ya kumsaka Salome ili
Rensho aweze kuuchukua uhai wake na kurejea
katika maisha yake bila kumsumbua mtu tena.
KIZAAZAA kikubwa kikaanzia hapa!!!.
ITAENDELEA!!
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA
Mama yule akaongeza kuwa katika makalio ya
yule binti kuna jina KINDO hivyo kwa namna
moja ama nyingine anaweza kuwa anahusika
kufahamu huyu binti ni nani na anapatikana wapi.
Mahakama ya wilaya haikuwa na uwezo wa
kusikiliza kesi ile ya mauaji. Kesi ikahamishiwa
jijini Dar es salaam
Martha akaanza kusakwa kwa kesi ya mauaji na
kisha kuchuna ngozi za mwanadamu.
Kindo akahusishwa katika kusaidia upelelezi!!
Wakati kesi hii ikishika kasi.
Getonga na Rensho walikuwa wasafiri katika basi
la abiria kutoka Dar es salaam kwenda Kahama
kwa sababu moja tu ya kumsaka Salome ili
Rensho aweze kuuchukua uhai wake na kurejea
katika maisha yake bila kumsumbua mtu tena.
Rensho alikuwa gumzo punde tu baada ya kupiga
hatua na kuingia ndani ya basi lile. Mavazi yake
na manukato aliyopulizia yalimfanya awe wa
kipekee katika safari ile.
Wanaume walimtamani pasi na kujua kuwa
hakuwa wa ulimwengu huu!!
Getonga pekee ndiye aliyefahamu fika kuwa
alikuwa ameongozana na mwanamke ambaye
alizikwa akiwa na miaka kumi tu, akasahaulika na
matanga yakakaa. Lakini ajabu yu hai tena.
Kichwani mwake Rensho yalipita maswali mengi
sana juu ya namna ya kukabiliana na huyo dada
wa kuitwa Salome mjini Kahama. Hamu yake
ilikuwa kurejea alipotoka.
“Ulisema kitambulisho umekihifadhi wapi?”
Rensho alimuuliza Getonga kwa sauti ya chini
kabisa.
“Kitakuwa nyumbani katika nguo zangu, sikuwahi
kukitazama hata siku moja. Na hata ukiniuliza
kipo vipi sina la kujibu.”
Rensho akafanya tabasamu hafifu na kisha
kuendelea kuuchapa usingizi katika siti aliyokuwa
ameketi. Getonga yeye alikuwa anasoma gazeti
alilonunua.
Robo saa baadaye mwanaume mwenye sauti ya
juu ya kukoroma aliwasalimia abiria kwa ujumla
na asijali iuwapo wamemjibu ama la. Kisha
akakohoa kuweka koo sawa.
Na hapo akaanza kuhubiri neno Mungu,
akakemea mambo kadha wa kadha akawasihi
watu kumtukuza Mungu maana ufalme wake
umekaribia. Asilimia hamsini ya abiria
walimsikiliza na kumtilia maanani huku wale
wengine wanaoamini kuwa dini imegeukia
biashara hawakujishughulisha naye hata kidogo.
“Wengine wamelala kabisa, mwanadamu
unaweza vipi kulala bila kumtukuza Mungu.
Imeandikwa kesheni mkiomba maana ufalme wa
mbingu unakaribia…..” sauti ile ikapaa zaidi na
kupasua ngome za Rensho. Kutoka katika
usingizi wake akaitambua ama kuifananisha ile
sauti.
“Getonga na huyu ni mmoja wao….” Alimweleza
huku akiwa amefumba macho.
“Mh! Unaota mapema yote hii…” Getonga alijibu
huku akitabasamu na akilini akijisemea “Hadi
majini nayo yanaota….balaa!!”
“Gerlad Getonga, sioti nimefumba macho, na
huyu ni mmoja wao..anataka kutoa kafara watu
wote katika basi hili. Washenzi sana hawa….
Washenzi G…..mimi si mkorofi ila sitaki
kushirikiana na watu hawa nataka kurudi
nyumbani….” Rensho akasema huku bado akiwa
amefdumba macho. Kwa maongezi yake Getonga
akagutuka kuwa yule binti hakuwa katika ndoto.
Akamtilia maanani!!
“Ni nani unayemzungumzia…”
“Huyu anayepiga hizo kelele katika lugha ya
maajabu…” alijibu kwa utulivu. Kisha akaongezea,
“Atawasimulia wenzake kitakachomtokea.
Akisema fumbeni macho tuombe nishike bega
unitikise kwa nguvu, usiipoteze nafasi hiyo
maana hamtafika Kahama salama, wote
mtakufa!!” alizungumza kisha akatulia tuli.
Getonga akabaki katika kuduwaa asiamini kabisa
kama Rensho yupo sahihi, alimtazama yule
bwana aliyevalia suti ya bei ya kawaida tu
anayepiga kelele na kutokwa jasho.
Mbona kama mtu wa Mungu huyu!!! Alijisemea.
Na wakati huohuo yule bwana akawaomba abiria
wote wafumbe macho waweze kuomba.
Getonga hakutaka masuala ya majuto ni mjukuu,
akaamua kufanya Rensho alivyotaka na hapo
likazuka sekeseke maridhawa ndani ya basi.
Wakati huo walikuwa katikati ya Mlandizi na
Kibaha.
Baada ya kutikiswa bega, Rensho aliruka kama
mtu aliyeshtuka kisha akajirusha na kuikaba
shingo ya yule aliyejiita mtu wa Mungu. Yowe la
hofu likamtoka na kile kitabu cha dini kikamtoka
mkononi.
Rensho bila kuiachia koo ya yule muumini,
akaivuta suti yake kwa nguvu. Wakati huo abiria
wengine walikuwa wamemsogelea Rensho
wakiamini ana mapepo.
Lahaula!! Hirizi kubwa nyekundu ikaonekana
kifuani mwa yule jamaa. Wasafiri waliokuwa na
viherehere wakarudi nyuma na kukanyagana
walipoiona hirizi ile. Wanawake wakaanza kupiga
mayowe wanaume wakawa wanatetemeka.
Dereva naye akasimamisha basi.
“Ni nani aliyekuagiza humu??” hatimaye Rensho
akauliza swali lile akiwa na ghadhabu. Yule
bwana aliyekuwa amekodoa macho alijaribu
kufinya macho hapa na pale kama namna ya
kujitetea lakini Rensho alikuwa makini zaidi, kwa
zaidi ya miaka kumi alikuwa ameishi katika yale
maisha ya giza na bado alikuwa hajatoka.
Amakweli Rensho hakuwa mtu wa kuuliza mara
mbili!
Ghafla akamwachia yule jamaa na hapohapo
akamrukia teke kali kifuani mwake, jamaa
akajibamiza katika viti na kutua chini kwa nguvu
huku akipasuka vibaya mno.
“Nshomi….Nshomi…..” alijibu hatimaye huku
akivujwa damu.
Baada ya kupata jibu lile, Rensho mwenye
ghadhabu alimrukia tena kwa nguvu pale chini,
akamkaba koo kwa nguvu kisha likafuata tukio la
maajabu ambalo lilileta hofu zaidi.
Rensho huku akipiga kelele nyingi sana akaivuta
ile hirizi, na hapo ukatokea mlipuko mkali. Moshi
mweusi ukatanda katika ile basi.
Hakuna abiria aliyemuona mwenzake, moshi
ulikuwa unanuka vibaya sana.
Mayowe yakatanda kila kona na wakati huu hadi
wanaume nao walilia wakiita mama zao. Utata!
Getonga alikiri kuwa mkasa huu ni zaidi ya yote
aliyowahi kupitia katika uandishi wake. Maana
huu wa sasa ulimweka ye mwenyewe katika
mazingira ya kuishi kwa uoga wakati wote bila
kujua nini hatma ya yote haya.
Baada ya takribani dakika kumi, kila mmoja
alimtazama mwenzake kama kituko, alikuwa
mweusi tii!! Kwa sababu ya ule moshi.
Kasoro Rensho tu ndiye alibaki katika mng’ao
wake wa awali.
“G…” Rensho akamuita Getonga kisha akamshika
mkono. Wakatoka nje ya basi ambapo raia wema
walikuwa wamezunguka hapa na pale kufuatilia
kuna nini kinatokea.
“Nawatakia safari njema!!” Rensho alizungumza
huku akitoweka na Gerlad. Yule jamaa wa
kuhubiri hakuonekana tena, Rensho alikuwa
ametuma salamu zake huko ajuapo. Salamu kwa
njia ya kuua….
Abiria walikuwa kimya wakati Rensho na Getonga
wakitoweka.
Hatimaye wakaishia porini.
“Nishike kwa nguvu..muda umetuacha sana…”
Rensho alimuelekeza Getonga ambaye hakuwa
na kipingamizi akafanya kama anavyotakiwa.
Kufumba na kufumbua, walikuwa wanatazamana
na bango lililoandikwa KARIBU KAHAMA.
Getonga alianza kuyazoea haya mauzauza.
Msako ukaanza usiku uleule!!
****
Jijini Dar es salaam, kesi kutoka mjini Kahama
ilionekana kuoana vyema na tukio ambalo
limewahi kutokea jijini Dar es salaam takribani
mwezi mmoja na ukiwa umepita.
Mpelelezi wa kesi ile kutoka mjini Kahama
aliikabidhi kwa wapelelezi wa jijini Dar es salaam
kwa minajiri ya kushirikiana katika kulitatua hili.
Inspekta John Magege aliisoma vyema kesi ile
akahusisha na nyingine kadhaa ambazo
zimejitokeza jijini Dar es salaam.
Kindo! Hili ndilo jina ambalo lilitokea Kahama na
pia Dar es salaam.
Akalikumbuka tukio la mauaji makubwa katika
nyumba ya mheshimiwa mbunge mtarajiwa,
mauaji ambayo chanzo chake hakikujulikana zaidi
ya kupitishwa kuwa Ebola ndiyo imewaua.
Katika kesi hii Inspekta Magege alitakiwa
kushirikiana na mpelelezi wa kwanza kabisa wa
kesi iliyotokea jijini Dar es salaam. Inspekta
Kisembe.
Lakini bahati mbaya Kisembe naye alikufa hata
kabla kesi haijafika popote. Alikufa kwa kuvuja
damu!
Alipokumbuka hili mwili ukamsisimka.
Alikuwa anayo nafasi ya kujiingiza katika kesi hii
ama kuiacha kwa wapelelezi wapya kabisa. lakini
akachagua kuendelea na upelelezi huo. Upelelezi
wa kumsaka msichana aitwaye Matha ambaye
anajihusisha na kuchuna ngozi za wanadamu.
Inspekta John akiwa ndani ya gari lake binafsi
aliamua kuifanya kesi hii katika utaratibu wa hali
ya juu sana.
Wakati natoka kazini bila kumpa mtu taarifa
yoyote aliamua kufuatili ile nyumba ambayo
yalitokea mauaji ya kutisha huku akipona
mwanaume mmoja tu wa kuitwa Kindo huku
akisema neno moja tu… “RENSHO!” tena bila
kukoma.
Aliiendesha gari yake kwa umakini na utulivu
mkubwa hadi akaifikia ile nyumba ambayo
hakuna mtu alikuwa akiishi tena bali mlinzi wa
serikali aliwekwa pale kulinda hadi ufumbuzi
utakapopatikana.
“Inspekta John Magege…” alijitambulisha kwa
mlinzi ambaye alikuwa ananuka pombe za
kienyeji wakati ule. Mlinzi akamruhusu kuingia
ndani.
Kwanza akaikagua nyumba vyema kuanzia nje
kabla hajaufikia mlango na kuufungua…..
Nzi wakaruka wakipishana naye na wengine
kumzunguka.
“Mh! Nzi hadi leo…” alijiuliza wakati akiungua
mlango zaidi. Nia yake alitaka kufananisha ripoti
iliyoandikwa na marehemu Inspekta Kisembe na
mazingira halisi juu ya vifo vile vya kutatanisha.
Akapiga hatua ndani, nzi wakazidi kusikika
wakipiga miluzi kutokea katika chumba kingine.
Inspekta John akasita kuendelea mbele
akatamani kumuuliza mlinzi swali, akapiga hatua
mbele kisha nyuma tena.
Akatoka nje hadi kwa mlinzi!!
“Mpo makini na ulinzi wa jengo hili ama?”
“Makini sana afande!!”
“Hakuna watoto wanaruka humu ndani na kuacha
vinyesi. Not watoto peke yao hata watu
wazima….” Alihoji Inspekta.
“Hapana, kila dakika kila sekunde tupo hapa
kulinda. Na kwa uzio huu hawezi kiumbe kuruka
ili aje kumaliza haja zake humu. Haiwezekani
hata kidogo afande!!” alipinga mlinzi wakati huu
akiwa makini zaidi. John akalisaili eneo lile na
kukiri kuwa hakuna kiumbe awezaye kuruka ule
uzio kwa ajili ya kumaliza haja zake mle ndani.
“Kwani kuna nini afande!!?”
Akaondoka bila kujibu swali la mlinzi ambalo
lilikuwa muhimu. Muhimu sana.
“Badala anijibu na mimi nimwambie ninachokijua
katika jumba hili…. Aah! Shauri zake bwana na u-
inspekta wake. Yaani watu wakiwa na vyeo eti
hawataki kuulizwa maswali..” alilaani yule mlinzi
huku akiketi katika eneo lake tena. Gobole lake
akilifanya egemeo.
JOHN aliingia moja kwa moja ndani tena,
akapenya hadi kule ambapo awali alisikia nzi
wakivuma.
Safari hii alisikia na sauti zikiunguruma kwa chini
sana mle ndani.
“Pumbavu zao hawa walinzi wameipangisha hii
nyumba…” alijisemea huku akitembea kwa
kunyata.
Hatimaye akaanza kusikia neno moja moja…
“Ametuzidi ujanja……. Atatuua yule….” Moja
ilikuwa sauti ya kiume na nyingine ikiwa ya kike.
“Wamepangisha majambazi humu. Pumbavu
sana….” Akajipapasa mahali inapoishi bunduki
yake, akakumbuka kuwa aliiacha ndani nya gari
yake.
Sauti zikazidi kunong’ona, sasa alianza kuifahamu
sauti mojawapo. Na lile wazo lake kuwa kuna
watu wamepangishwa mle ndani likaanza
kuyoyoma.
“Tatizo hatuwezi tena kujua alipo…… atatuua
kimyakimya akitoka katika lile tumbo la Kahama.
Yaani akitoka kila mmoja aanze kuchimba kaburi
lake mapema… ila wewe nilikueleza kabisa kuwa
yule nani yule……”
“Shhhh!! Sio muda wa kulaumiana huu, yule nani
sijui nani sio wakati wake…ishu ni moja
tunafanya nini?? Limeshatokea hilo?” mwanamke
alihoji kwa hamasa.
“Hivi huyu kitambi naye ameendaje kwenye basi
bila kulikagua.. huenda angemjua na kumkamata
kabla hajauwawa.” Mwanaume bado alikuwa
katika kulalamika.
“Makamu anakuja muda gani maana hapa sio
salama, tunatakiwa kuuchukua huu mzoga
tuondoke.” Mwanamke aliulizia na hapohapo
upepo ukaanza kuvuma, upepo wenye ubaridi wa
hali ya juu. Upepo ule ukapenya ndani kama
kimbunga.
Inspekta John akashikwa na kigugumizi iwapo
atoke nje ama aendelee kubaki. Ujasiri
ukamsukuma kubaki, akapiga hatua moja na
kuchungulia, akakutana na migongo ya watu
wawili. Lakini chini ulikuwa mwili uliotokwa na
uhai. Bila shaka nzi walijileta kwa sababu ile.
Akina nani hawa? Mbona sauti kama…..hata
mwili nao kama wa…..oooh!! ni yeye huyu ni
yeye…anafanya nini humu jamani. Mungu
wangu…” alitaharuki Inspekta John. Mara ule
upepo ukakoma.
John akatoa simu yake mfukoni aweze kupiga
picha walau moja tu ya umuhimu sana.
Akaseti simu yake isitoe mwanga wakati wa
kupiga ile picha na wala isitoe mlio wowote.
Upesi akaitega vyema!! Akiwa makini kabisa.
Lakini kosa moja tu likamgharimu. Simu yake
haikuwa imewekwa katika ukimya na muda
huohuo mkewe alimpigia simu maana usiku
ulikuwa unaingia na hajarejea nyumbani!!
Simu ikapiga kelele.
KIZUNGUMKUTI!!!!
***ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom