Riwaya: Hila

Riwaya: Hila

Mzaramo ukitupia nyngne, tufidie na za jana kaka... teh teh teh teh!
 
Jana nadhani alikwenda ngomani au alipewa mke wa bure kule msanga
 
KISA CHA 16

LICHA ya kuwa amepokea kipigo kikubwa sana ambacho kilikuwa ni sawa na kuua nyoka, bado John Masele alikataa kata kata kuwa hajawahi kukutana na mwandishi wa habari aitwaye Sam na wala hajui chochote kuhusiana na BvB.
Alipinga licha ya ukweli kuwa waliwahi kukutana na akazungumza naye na kumpatia nyaraka tata.
Masele alipinga kwa sababu alijua hata akisema bado mabaradhuli wale watamuua tu na kisha kumwahi Sam kabla hajatumia zile nyaraka kuwavumbua waovu. Ilikuwa heri afe lakini akiacha harakati zikiendelea nyuma yake.
Kitendo cha mzee Matata kuleta kiburi kilimkera sana raisi. Akaona kuwa ile ni dharau ya hali ya juu, alitambua kuwa anaweza kumpiga risasi na kumuua mara moja, lakini kwake yeye furaha isingekamilika. Badala yake akawasiliana na BvB na kumwomba huduma ya vijana wake kadhaa wanaojua nini maana ya kuua mwanadamu yeyote kwa mateso makali. Akamsihi tena kuwa hakuhitaji afe upesi, alihitaji afe kwa hatua. Ikiwezekana hata ndani ya siku kumi za mateso nd’o aruhusiwe kufa.
____

Raia wa kizungu wanne walipokelewa uwanja wa ndege wa kimataifa wea mwalimu Nyerere. Ugeni huu ulipokelewa na wafanyakazi kutoka ikulu, hivyo baada tu ya kuwasili walipelekwa hoteli ambayo ilikuwa imelipiwa kwa ajili yao.
Waliwasili majira ya saa nne asubuhi!
Muda uleule walipelekwa hotelini na hawakutoka tena hadi ilipotimu saa tisa usiku.
Kazi iliyowaleta kutoka huko walipotoka ni moja tu, kumbana John Masele ili aweze kusema iwapo aliwahi kukutana na Sam ama la!
Na ajieleze zaidi iwapo walikutana ni kitu gani alimpatia!
Hawa wazungu kutoka uholanzi waliaminika kwa kazi yao ya kuadabisha mateka wao. Walikuwa na roho mbaya sana zisizokuwa na huruma hata kidogo. Kuua kwao ilikuwa kama kichekesho tu, ni wazungu hawa ambao mzee Matata alikuwa na video zao na alimuwekea Tina ili kumtisha siku ile. Walikuwa wanatesa na kuua vibaya mno.
Wakiongozwa na dereva waliyekabidhiwa wakiwa kimya kabisa huku wakipuliza sigara kila mmoja. Hatimaye walifika magomeni.
Nyumba ambayo John Masele alikuwa amehifadhiwa.
Walifika na kubisha hodi lakini mfunguaji alichelewa. Wakabisha tena na hapo akafika na kuwafungulia geti haikuwa mara yao ya kwanza kufika katika ngome kadha wa kadha za namna ile.
Wakapita moja kwa moja hadi ndani, dereva akabaki nje na baada ya wao kuingia ndani na yeye akatoweka kwenda mahali alipopajua yeye kwa sababu tayari aliambiwa kuwa hawatatoka mapema. Na wanaweza wasitoke humo ndani kwa siku hiyohiyo. Hakujua hata walichokuwa wakikifuata mle ndani wanne wale.

Walipoingia ndani wakaenda moja kwa moja katika ule ukuta wakataka kupenya lakini wakashtushwa na utofauti wa maelezo waliyopewa awali juu ya mazingira ambayo yapo eneo lile.
Mzungu mmoja akatoa simu yake na kisha kutoka nje ili aweze kupiga.
Alipotoka nje akaenda kwa mlinzi ili aweze kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili na wale mabwana wahusika wa ile ngome.
“Hey! Do you speak English?” mzungu akamuuliza mlinzi.
Yule mlinzi akajibu kuwa anaweza.
Yule bwana akabofya namba kadhaa na kutaka kumpatia yule mlinzi simu. Mlinzi akanyoosha mkono wake kuipokea ile simu. Lakini hakuchukua simu pekee.
Akaufyetua ule mkono wa mzungu na kuuvunja huku mkono wake mwingine ukiuziba mdomo wa yule bwana. Kisha akamvutia nyuma ya nyumba.
Akaitoa kofia yake na kuanza kumuhoji yule bwana kwa kiingereza.
“Who the *** are you?” ilikuwa sauti ya Gama iliyo katika ghadhabu kuu.
Yule bwana hakujibu, Gama hakupoteza muda kuzungumza na bubu. Akatoa pigo kali la kareti katika mbavu za yule bwana, hata sauti hakuweza kutoa alibaki kugumia kwa maumivu.
“Who are you bastard!” akamuuliza tena huku akimwonyesha wazi kuwa anataka kutoa pigo jingine.
Mwanga hafifu wa taa ulimmulika mzungu yule ambaye alikuwa mwekundu huku sura ikiwa imemvimba.
“BvB” akatokwa na kauli ile. Kisha akatulia kimya!
Ni aidha alikuwa amepoteza fahamu ama kifo kabisa.
Upesi Gama akaondoka na kuelekea katika kile chumba ambacho walikuwa wamesalia wazungu watatu wakingoja maelekezo zaidi.
“Me, you zea” alizuga kuzungumza kiingereza kibovu Gama, hapa akiwa amevaa tena kofia yake na kufanana na mlinzi.
Mzungu mmoja akatoa kauli kuamriosha mmoja wao aende kutazama mwenzao anasema nini.
Naam! Ramani ya Gama ikaenda kama alivyokuwa anahitaji.
Akamwongoza hadi nje, na kumpeleka nyuma ya nyumba. Akafika na kumwonyesha mwili wa mwenzake.
Hakumpa muda wa kushtuka sana, akamvamia kwa kiwiko akaivunja pua yake.
Mzungu akataharuki na akataka kupiga kelele lakini alichelewa, Gama alifyatua kisu alichokuwanacho kikajikita katika shingo ya yule kaburu.
Kisu kilikuwa na sumu kali. Gama hakugeuka nyuma tena kutazama jinsi atakavyokata roho.
Sasa hakuvaa kofia bali aliingia tena moja kwa moja katika kile chumba.
“You bastard where are you from and who the hell is BvB” aliwauliza huku akiwa anawakabili machoni.
Wakamtazama kwa jicho la hofu wasijue ni kitu gani kinaendelea.
Mmoja akajaribu kumsogelea lakini hakufika mbali ukasikika mlio wa bunduki, alipogeuka alimshuhudia mwenzake akiangukia kichwa huku kisogo kikiwa kinavuja damu.
“Kombolela mzungu..” Sauti ikasikika kisha tena bunduki ikakohoa na kuvunja miguu ya yule bwana aliyebakia.
Na hapo John Masele akajitokeza huku akiwa anajivuta kwa magoti na tabasamu tele mdomoni mwake.
Mchezo walioupanga ukawa umekamilika!
Gama alikuwa amemshirikisha John Masele juu ya kombolela, na pale walikuwa wakilicheza.
“Utajibu maswali yote kwa hiari ama kwa lazima ikibidi?” Gama akamuanza yule mzungu pekee aliyebaki akiwa hai.
Yule mzungu hakujibu kitu Gama. Akatoka nje kisha baada ya dakika zipatazo kumi akarejea tena, mikono yake ikiwa imetapakaa damu na mkononi akiwa na vichwa viwili vya wazungu. Akavirusha mbele ya yule mzungu mbishi.
Hakika alipagawa!
“Do you love hell??” Gama akamuhoji. Na hapo hapo akanyanyua vidole vyake juu, kisha akavishusha katika kichwa kimojawapo katika pigo la ‘finga’ na hapo akachomoka na macho kutoka katika kile kichwa. Akayarusha mbele ya yule mzungu.
“I will chop your eyes while you are alive” akamkoromea huku akimsogelea. Kitete kikamkumbuka yule mzungu.
Mzungu akajibu kila alichoulizwa huku akiwasihi wasimuue kwa sababu yeye ni mjumbe tu.
Akamtaja BvB kuwa ndiye bosi wao na siku iliyokuwa inafuata alitarajiwa kuanza safari ya kuja nchini Tanzania kufuatilia maendeleo ya miradi yake na kubwa zaidi kuitazama ardhi kubwa yenye madini ambayo alipewa zawadi na raisi wa Tanzania kutokana na ukaribu wa kimisaada aliokuwa akimpatia.
Yule mzungu hakusubiri kuambiwa aseme nini maana ya BvB aliitafsiri mwenyewe na kisha akamtaja mzee Matata kama kijakazi wa BvB nchini Tanzania.
Gama alivyotaka kuujua muonekano wa BvB, mzungu yule aliapa kuwa hajawahi kumtia machoni bwana yule hata siku moja katika maisha yake.
“Imelaaniwa ardhi hii” John Masele alijisemea baada ya maelezo ya yule mzungu.
Gama akamkonyeza kwa jicho la kuume. Akatambua nini kinamaanishwa.
Na hapo akafyatua risasi, yule mzungu akabweka na kupoteza uhai. Gama akamchukua John Masele katika mgongo wake kisha akatoka naye nje kwa tahadhari kubwa.
Akampita yule mlinzi mlevi na kutokomea gizani zaidi!
_____

WAKATI Gama Yakubu akihangaika kupenya katika njia ambazo ni salama kwake pasipo kuonekana. Mama lao alikuwa akiichochea moto zaidi ile gari aina ya Noah ambayo aliichukua nyumbani kwa waziri usiku ule.
Wale mateka ambayo walikuwa wanaelekea kuwa huru walikuwa katika maombi mazito kila mmoja akimshukuru Mungu kwa namna yake ya kipekee. Lakini Lili alikuwa mtu wa kulia tu.
Mama lao akiwa ndani ya pensi aliendesha gari kuitafuta Kibaha kama ambavyo walikuwa wamekubaliana na Yakubu ambaye alibaki nyuma kwa ajili ya kuimalizia kombolera yake.
Mitaa ya Kimara na ubungo bado ilikuwa imechangamka changamka licha ya kuwa ulikuwa usiku mnene. Hapo alipita bila wasiwasi wowote.
Lakini shughuli ikawa pevu walipofika mlima wa kibamba kuelekea Kibaha.
Gari ya akina mama lao ilisimamishwa katika namna ya kipekee.
Mawe yalikuwa yamepangwa barabarani!
Watekaji! Mama lao alisema kwa sauti ya kuhamanika, na hapo kila mateka akazidisha maombi yake.

Mama lao alijua kwa namna yoyote ile hawezi kuvuka kikwazo kile na ilikuwa lazima asimame. Aliwaona watekaji wake wakiwa na mapanga na marungu.
Akapunguza mwendo na kusimama!!
Watekaji wakasogea hadi pale garini.
“Mwanamke… tunakupa dakika moja na sekunde mbili.. uwe chini na wote waliomo humu wawe chini na kisha mpotee mbele ya macho yetu… ubakishe funguo pekee humo ndani.” Amri ilitoka.
Mama lao akawageukia mateka wake akatazama namna wanavyomtazama kwa jicho la huruma na wengine wakiwa wamekata tamaa.
“Mnaijua kombolera…. Lili umewahi kucheza kombolera?” aliwauliza na kisha akamgeukia Lilian.
Lili akatikisa kichwa kumaanisha kuwa amewahi kucheza.
“Ili umuokoe mwenzako unatakiwa kufanyaje?”
“Mbona sikuelewi mama…..” alilalamika Lili.
“Sijakuuliza kama unanielewa jibu swali binti…”
“Unabutua….”
“Vizuri sana… unabutua…” mama lao akarudia jibu lile huku anacheka. Kisha akawaambia wasishuke garini anaenda kubutua.
Wakati mama lao anashuka kutoka garini alikuwa anajiona kama yu katika tukio ambalo aliwahi kuwa awali. Lakini tofauti ilikuwa moja tu tukio la awali lilitokea jijini Mwanza, ambapo katika utafutaji wake akiwa bado anatawaliwa na ujana aliangukia katika penzi la kijana mwenye pesa. Naam! Tangu akiwa mdogo alikuwa akitamani kuolewa na mtu mwenye pesa akidhani zile pesa hujileta zenyewe.
Baadaye kabisa penzi likiwa limekolea akajitambua kuwa amezama katika penzi la jambazi aliyekubuhu na hawezi kutoka tena.
Akakubaliana na hali, akafundishwa kushika bunduki na kuitumia, akafundishwa kuwa na roho mbaya inapobidi, akafundishwa kurusha mateke na kupiga ngumi!
Naam! Mama lao akawa mtu mwingine, na hatimaye akaanza kuandamana na mpenzi wake kwenda kuteka magari.
Wao walikuwa wakifanikiwa sana kutokana na mbinu walizokuwa wakizitumia, hii mbinu ya kuweka mawe barabarani mpenzi wake yule ambaye baadaye aliuwawa kwa risasi aliziita mbinu za kishamba. Na aliwahi kumweleza mama lao kwanini mbinu zile ni za kishamba na mama lao akazielewa.
Sasa mama lao naye ametekwa katika mbinu za kishamba hayupo pamoja na marehemu mpenzi wake sasa yu mwenyewe, kwanini asicheke, kwanini asitabasamu wakati anatambua kuwa washamba nd’o wanaojaribu kumteka.
Dhumuni kuu la mama lao kushuka chini peke yake ilikuwa ni kuhakikisha iwapo walimteka wana silaha ama vipi.
Macho yake makali yakapenya katika giza lile jepesi, kwa mbali akamuona mtu mwingine amesimama huku akivuta sigara, hakutazama mara mbili akawa katika marudio akatambua kuwa yule aliyesimama mbali ndiye ambaye huwa anakuwa na bunduki. Na mara zote ndiye huwa kiongozi wa msafara, mama lao akauchuna kama hajamuona lakini kichwani akikiri kuwa marehemu Swebe mpenzi wake alikuwa anajua mambo mengi sana.
Hapa akawa anaishi katika dunia mbili tofauti, kichwani alikuwa makini kuwatazama adui zake lakini kwa nje alionyesha ule uoga wa kike. Akawalaghai wale ‘washamba’ kuwa yeye ni mwanamke wa kawaida.
Wakawa wanamkemea huku wakicheka, walidhani ni mwanamke kweli.
Wakiwa bado wanamdharau mama yule aliyekuwa akiwaomba msamaha. Mara likatokea tukio ambalo huenda watasimulia kwa vizazi vyao vya majambazi ‘washamba’.
Kwa kushtukiza kabisa kama ilivyo katika filamu za mapigano kwa kutumia silaha. Mama lao akaangukia magoti kama anayeomba msamaha, upesi mkono wake mmoja ukaingia kiunoni, na sekunde iliyofuata akawa na bastola mkononi, akafyatua moja kwa moja kumwelekea yule aliye mbali akampata kifuani. Jamaa akarushwa mbali, mama lao hakutaka kujiuliza iwapo amekufa ama la.
Sekunde inayofuata bastola yake ikawa inawatazama wawili wale. Sas ikawa zamu yake kutabasamu na wale jamaa kuanza kubabaika.
“Wee! Thubutu kukimbia na uwe umekimbia milele mbwa nyie…” akawapia mkwara. Kisha akatoa amri upesi.
“Mnayatoa haya mawe kwanza ndani ya dakika moja na sekunde mbili kisha mnapotea machoni kwangu mara moja!! Upesi.”
Mara moja wawili wale wakaanza kuyaondoa mawe kama walivyoamrishwa, huku wakitetemeka. Ndani ya gari Lili ambaye muda wote alikuwa anachungulia kinachoendelea, akajikuta kwa mara ya kwanza akitabasamu.
Barabara ilivyokuwa safi. Mama lao akawatazama wawili wale ambao waliogopa kuondoka bila kuruhusiwa. Kisha akawarushia neno lililowashangaza.
“Kombolela majambazi!”
Akaruka garini na kuitia moto gari. Safari ikaendelea kwa amani kana kwamba hakuna kilichotokea!
Kila mmoja garini alibaki kujiuliza juu ya yule mwanamama.
Hawakupata majibu!!

****

ASUBUHI SANA eneo la magomeni lilijaa umati wa watu, kila mmoja alikuwa akiongea neno ajualo yeye juu ya kile alichokuwa akikiona.
Vichwa vinne vya wazungu vilikuwa nje ya geti la nyumba iliyosadikika kuwa ni ya mheshimiwa waziri wa nishati na madini.
Simu zilipigwa kituo cha polisi cha Usalama magomeni, na punde askari walifika na kujawa na mshangao juu ya jambo lile.
Simu za upepo zikafika makao makuu, na hatimaye mezani kwa Robert Masawe.
Alipigiwa simu na IGP kuelezwa kuhusiana na tukio lile la kutisha tena katika nyumba ya waziri.
Robert Masawe alitamani amweleze IGP juu ya uozo unaoendelea chinichini maana alimuona ni mtu anayetumikia kitu asichokijua. Lakini hakuwa radhi kujaribu kumweleza badala yake alichukua ile taarifa kama taarifa nyingine kisha aingie katika utendaji.
Wakati anakata simu alisimama akapiga saluti huku akiwa peke yake.
Kisha akajisemea “Umelaaniwa mkono wa GAMA….”
Kisha akafanya tabasamu hafifu la matumaini.

WAKATI tukio hili likiendelea, hali ya waziri wa nishati na madini, bwana Mathias Obhare ilikuwa mbaya sana, shinikizo la damu lilikuwa limepanda. Alikuwa amechanganyikiwa kabisa na hakujua ni nani aliyepenya na kuingia katika ngome ile na kufanya yale yote aliyoyafanya.
Taarifa ya maaskari ilitaja kukutwa pia miili ya waafrika wawili ikiwa haina uhai na mbwa aliyepigwa risasi pia akiwa hana uhai.

Si waziri peke yake aliyekuwa amepagawa bali raisi wa nchi alikuwa hajielewi kabisa. Alipiga simu uholanzi kutaka msaada lakini bahati mbaya simu ya Benson van Bronchost haikuwa ikipatikana.
Alisahau kabisa kuwa bwana yule alikuwa safarini kuja Tanzania.
Waandishi wa habari wakaanza kuandika mambo wanayohisi bila kuwa na uhakika nayo.
Wakaandika waziri ameua, wakaandika waziri anajihusisha na umafia na mengineyo mengi huku wengine wakienda mbali zaidi na kutaja kuwa ni vita ya kuelekea ikulu inaondoka na damu za watu.
Tamko la mkuu wa majeshi ya polisi likasubiriwa.
Na hilo lilikuja baada ya siku moja!
Akiwa ameagizwa na raisi kusema hivyo, IGP akazungumza nje kabisa ya utashi wake. Mmoja kati ya watu waliokuwa katika mkutano ule japokuwa kwa siri kubwa alikuwepo Sam ambaye alitoka katika maficho yake baada ya kusikia habari juu ya wazungu wanne na waafrika wawili kuuwawa katika nyumba ya waziri.
“Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani na nje ya nchi, bwana John Masele aliyekamatwa na silaha za moto, ametoroka mikononi mwa polisi wakati akihamishwa gereza la mahabusu. Serikali inamshuku kuhusika na mauaji yaliyotokea katika nyumba ya waziri Obhare. Msako mkali unaendelea dhidi yake.”
Taarifa ile ilipokewa kwa namna tofauti tofauti na waandishi wa habari. Wengi walinung’unika kuwa ilifanana na taarifa ya kupikwa lakini IGP hakujibu swali lolote lile.
Huo haukuwa mwisho wa utata!!
Sam akatabasamu huku akiitazama picha zilizokuwa mkononi mwake akazifananisha na vile vichwa vilivyopigwa picha na kuwekwa magazetini. Picha zilifanana kabisa na zile alizopewa kule kijijini na John Masele ambaye sasa anashutumiwa kuwa ni muuaji.
“Wajinga ndio waliwao… siku zenu zinahesabika!” Sam akasema kwa sauti ya chini huku akiondoka zake.

___
 
KISA CHA 17

Ili kuupaka umma mafuta kwa mgongo wa chupa serikali ikamwongezea ulinzi waziri yule. Huku nyumba ambayo yalitokea mauaji yale nayo ikilindwa na wanajeshi ambao walikuwa wakipishana kila baada ya masaa manne.
Mathias Obhare naye akawa mtu wa kulindwa kila sekunde.
Nafsi yake haikuwa na amani hata kidogo, alitamani kuubadilisha ukweli uliokuwa unamkabili lakini haikuwezekana kufanya vile tena. Mambo yalikuwa yanaanza kuwakaa kooni yeye na raisi kutokana na hila zao.

Upande wa raisi, yeye alibaki katika fumbo kuu akiwafikiria wazungu wale walivyouwawa. Akiachilia mbali wale wazungungu, akamfikiria Suzi yule mwanadada mashuhuri ambaye aliaminika kuwa na roho saba.
Ni nani aliyeuondoa uhai wake kirahisi namna ile tena pasipo kutumia silaha? Hili jambo lilimvuruga raisi na ile hali ya Benson kutopatikana hewani basi alivurugika kupita maelezo.
Alitamani kumweleza mkewe juu ya wakati aliokuwa akipitia lakini akashindwa ni wapi angeanzia kwa sababu hata siku moja hakuwahi kumweleza juu ya hila zake serikalini na ubadhilifu aliokuwa akiufanya kwa kuwaruhusu wanyonyaji kula matunda ya nchi kuliko wazawa.
Hatia ikamsulubu, akajaribu kupambana na hali ile lakini hakuweza.
Akachukua simu yake na kumpigia mtu maalumu na kukatisha kikao cha bunge alichopanga kwenda kuhutubia.
Na baada ya pale akampigia simu IGP.
“Mkuu… una uhakika kuwa hakuna vijana wanatusaliti katika kambi ya usalama wa taifa…”
“Sijaelewa unamaanisha nini mkuu..” IGP alijibu.
“Haya mauaji we unayachukulia ya kawaida haya…. Wale wazungu na yule Suzi..” alijieleza Rais.
“Mkuu kwani unawafahamu hao watu..” IGP akahoji. Na wakati ule akatambua kuwa raisi alikuwa anatetemeka. Alama ya kuuliza ikajiunda katika kichwa chake.
Hao ni akinanani kwa raisi na wana mstakabali gani hadi awe katika hali ile.
“Mhh! Hapana siwafahamu lakini Obhare anaweza kuwa anawafahamu naamini…” alijikanganya raisi kisha upesi akakata simu.
IGP akaanza kuingiwa na mashaka.
Na hapo akajaribu kuwasiliana na mrakibu mkuu Robert Masawe na kumweleza iwapo amepata fununu zozote juu ya mauaji yale.
Robert akapiga fumbo.
“Inasadikika wameuwawa na watanzania wa kawaida ambao wamechoka kunyonywa….”
“Una maana gani na nani amesema.”
“Mkuu nimesema inasadikika, hivyo ni sisi kusadiki ama la!” akajibu mrakibu.
IGP akakata simu huku akizidi kuchanganyikiwa!!
Akabaki kujiuliza juu ya maneno ya Mrakibu msaidizi, kisha akahusisha na hali ya raisi.
Kuna kitu!!! Akapigia mstari.

****

NGUVU YA PENZI!!

USIKU wa mang’amung’amu ulimwandama Sam. Alijitazama kama kijana mzembe sana licha ya makwazo kadhaa aliyopitia.
Alizikumbuka ahadi tele ambazo alizipanga na Tina. Alikumbuka namna ambavyo kila mmoja aliapa kuwa yupo tayari kufa kwa ajili ya mwenzake.

Ajabu yeye Sam alikuwa nyumba ya kulala wageni ya bei ya chini kabisa maeneo ya Machimbo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Alijiona yu mjinga kujificha ili asife wakati mtu ambaye walipanga naye ahadi kedekede alikuwa matatani. Na hakujua hata kama alikuwa yu hai ama amekufa tayari.
Wakati akiyafikiria hayo mara akamfikiria na mzee John Masele. Kuna maneno ambayo alimweleza na sasa akajiona kuwa ni msaliti muoga tena asiyejiamini.
Yale maneno yakajirudia kwa kasi kubwa kichwani mwake.
“Sam naona unatetemeka bila shaka kuna baridi sana huku kwetu..” John Masele alimuuliza Sam huku akiwa anatabasamu.
“Dah! Mzee huku ni tatizo kabisa hili baridi la Mafisa ni hatari sana, Iringa haioni ndani….” Sam alijibu.
“Sam unahisi ili baridi lipungue unahitaji nini…”
“Mzee hapa ni sweta zito kabisa nd’o linaweza kuleta nafuu” Sam akajibu, John Masele akacheka kidogo kisha akaendelea.
“Hivi umewahi hata siku moja kuzungumza na Sweta lako na kulishukuru kwa kukulinda kwa baridi?”
“Aaah! Mzee wangu lile sweta ni langu ya nini mimi kulishukuru sasa.. ule ni wajibu wake kunilinda mimi…” Sam akajibu huku akimshangaa John Masele.
“Safi sana Sam, ehe! Na vipi sweta lako likichakaa…”
“Naachana nalo nanunua jingine…”
“Ooh! Umejibu vizuri sana Sam. Ninachomaanisha hapa kijana wangu, wewe ni sweta kwa watanzania Sam, unatakiwa uwalinde watanzania pasipo kusubiri kupewa shukrani ama kupewa pesa kama wanavyotaka wengine. Au kupigiwa makofi kama ilivyo asili ya wapuuzi wengi, wewe sio mpuuzi Sam na usikubali kuwa mpuuzi ishi kama sweta. Kawasaidie watanzania, usisubiri watoe shukrani, na katika kuwasaidia huko utambue kuwa unaweza kuchakaa, unaweza kufa. Ukifa wewe utakuwa umetanua njia kwa masweta mengine mapya kuwalinda watanzania wasitetemeke kwa baridi, usiogope kufa Sam. Maana waliotupa uhuru wa bendera na wao walikufa sasa ni zamu yetu kuupata uhuru wetu…”
Haya yalikuwa maneno ya John Masele usiku ule alipozungumza na Sam. Sam akajikuta katika aibu, kwanza akamfikira mpenzi wake, pili akatii maneno ya John Masele.
Akakurupuka kutoka kitandani, akasimama wima na kujiuliza atalala na kujificha mpaka lini? Na ni nani ambaye atampigania ikiwa yeye hajaamua kujipigania.

Sam akavinyoosha viungo vyake kisha akajisemea.
“Mimi ni sweta na kesho naanza kazi rasmi.”
Akarejea kitandani na kusinzia.
Asubuhi akatazama kiasi cha pesa alichobaki nacho kilikuwa kinatosha kwa harakati alizokuwa amezipanga.
Majira ya saa nne asubuhi Sam alikuwa katika ‘stationary’ moja isiyokuwa na watu wengi. Alikuwa ameketi mwenyewe kwenye kompyuta akitengeneza kitambulisho ambacho alipanga kwenda kukitumia mahali.
Alitumia muda wa saa zima kukitengeneza kisha akakichapisha na kuondoka zake akiwa amelipia huduma ile.

Sam akiwa amevalia suti yake nyeusi, miwani myeusi ya jua na kofia pana kichwani alichukua pikipiki ambayo ilimpeleka moja kwa moja maeneo ya Kurasini. Akashukia mbali kidogo na eneo alilopanga kwenda. Akapokelewa na mlinzi akajiandikisha jina lake na kuruhusiwa kuingia ndani.
Kisha akatembea kwa miguu, akafanya dua fupi kisha akaingia katika ofisi za mkuu wa shule ya sekondari ya kimataifa iliyokuwa pale.
Akasalimia huku akiwa amesimama kisha akatoa kitambulisho chake na kukionyesha mara moja kisha akajitambulisha kwa jina.
“Inspekta Babu kutoka kituo cha kati, amri kutoka kwa IGP, Suzan anatakiwa kuwekwa mahali salama muda huu kwa usalama wake. Tafadhali namuhitaji sasa hivi, samahani kwa usumbufu ni amri kutoka kwa IGP…” Sam aliunguruma huku miwani yake ikiwa ipo bado machoni huku akiwa amekakamaa mithiri ya askari.
Ama! Mwandishi wa habari ni muigizaji pia!
Mkuu wa shule alitetemeshwa na ujio ule wa Sam ambaye mafunzo ya JKT aliyoyapitia yalikuwa yamemjengea uimara sana. Akafanana kabisa na askari.
Pasipo kupoteza muda, mkuu yule wa shule alimuita mwanafunzi mmoja na kumuamuru amuite Suzan upesi.

Punde msichana mrembo umri usiozidi miaka kumi na tano alikuwa mikononi mwa Sam. Sam alitembea kwa tahadhari kubwa huku akitazama kushoto na kulia kana kwamba kuna hatari yoyote anayojaribu kupambana nayo.
Mkuu wa shule alibaki kuduwaa asijue ni kitu gani kibaya alitaka kufanyiwa mtoto yule hadi amri ikatoka kwa IGP upesi kiasi kile. Akabaki kutikisa kichwa asijue la kufanya!
Sam akatokomea akiwa na yule binti mrembo!
Siku iliyofuata taarifa zikatapakaa katika vyombo vya habari juu ya kutekwa kwa mtoto wa IGP.
Mtekaji hakuwa akifahamika, zaidi ya kutumia jina feki, ‘Inspekta Babu’.
Nchi ikaingia katika kizunguzungu kipya!!
Na hapa ndipo mpasuko ulipoanzia!!
Mpasuko wa aina yake!!!

****

Kwa kushtukiza kabisa kama ilivyo katika filamu za mapigano kwa kutumia silaha. Mama lao akaangukia magoti kama akanyeomba msamaha, upesi mkono wake mmoja ukaingia kiunoni, na sekunde iliyofuata akawa na bastola mkononi, akafyatua moja kwa moja kumwelekea yule aliye mbali akampata mguu.
Sekunde inayofuata bastola yake ikawa inawatazama wawili wale.
“Wee! Thubutu kukimbia na uwe umekimbia milele…” akawapiga mkwara. Kisha akatoa amri.
“Mnayatoa haya mawe kwanza ndani ya dakika moja na sekunde mbili kisha mnapotea machoni kwangu mara moja!! Upesi.”
Mara moja wawili wale wakaanza kuyaondoa mawe kama walivyoamrishwa, huku wakitetemeka.
Barabara ilivyokuwa safi. Mama lao akawatazama wawili wale ambao waliogopa kuondoka bila kuruhusiwa. Kisha akawarushia neno lililowashangaza.
“Kombolera majambazi!”
Akaruka garini na kuitia moto gari. Safari ikaendelea kwa amani kana kwamba hakuna kilichotokea!
Kila mmoja garini alibaki kujiuliza juu ya yule mwanamama.
Hawakupata majibu!!

****

ASUBUHI SANA eneo la magomeni lilijaa umati wa watu, kila mmoja alikuwa akiongea neno ajualo yeye juu ya kile alichokuwa akikiona.
Vichwa vinne vya wazungu vilikuwa nje ya geti la nyumba iliyosadikika kuwa ni ya mheshimiwa waziri wa nishati na madini.
Simu zilipigwa kituo cha polisi cha Usalama magomeni, na punde askari walifika na kujawa na mshangao juu ya jambo lile.
Simu za upepo zikafika makao makuu, na hatimaye mezani kwa Robert Masawe.
Alipigiwa simu na IGP kuelezwa kuhusiana na tukio lile la kutisha tena katika nyumba ya waziri.
Robert Masawe alitamani amweleze IGP juu ya uozo unaoendelea chinichini maana alimuona ni mtu anayetumikia kitu asichokijua. Lakini hakuwa radhi kujaribu kumweleza badala yake alichukua ile taarifa kama taarifa nyingine kisha aingie katika utendaji.
Wakati anakata simu alisimama akapiga saluti huku akiwa peke yake.
Kisha akajisemea “Umelaaniwa mkono wa GAMA….”
Kisha akafanya tabasamu hafifu la matumaini.

WAKATI tukio hili likiendelea, hali ya waziri wa nishati na madini, bwana Mathias Obhare ilikuwa mbaya sana, shinikizo la damu lilikuwa limepanda. Alikuwa amechanganyikiwa kabisa na hakujua ni nani aliyepenya na kuingia katika ngome ile na kufanya yale yote aliyoyafanya.
Taarifa ya maaskari ilitaja kukutwa pia miili ya waafrika wawili ikiwa haina uhai na mbwa aliyepigwa risasi pia akiwa hana uhai.

Si waziri peke yake aliyekuwa amepagawa bali raisi wa nchi alikuwa hajielewi kabisa. Alipiga simu uholanzi kutaka msaada lakini bahati mbaya simu ya Benson van Bronchost haikuwa ikipatikana.
Alisahau kabisa kuwa bwana yule alikuwa safarini kuja Tanzania.
Waandishi wa habari wakaanza kuandika mambo wanayohisi bila kuwa na uhakika nayo.
Wakaandika waziri ameua, wakaandika waziri anajihusisha na umafia na mengineyo mengi huku wengine wakienda mbali zaidi na kutaja kuwa ni vita ya kuelekea ikulu inaondoka na damu za watu.
Tamko la mkuu wa majeshi ya polisi likasubiriwa.
Na hilo lilikuja baada ya siku moja!
Akiwa ameagizwa na raisi kusema hivyo, IGP akazungumza nje kabisa ya utashi wake. Mmoja kati ya watu waliokuwa katika mkutano ule japokuwa kwa siri kubwa alikuwepo Sam ambaye alitoka katika maficho yake baada ya kusikia habari juu ya wazungu wanne na waafrika wawili kuuwawa katika nyumba ya waziri.
“Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani na nje ya nchi, bwana John Masele aliyekamatwa na silaha za moto, ametoroka mikononi mwa polisi wakati akihamishwa gereza la mahabusu. Serikali inamshuku kuhusika na mauaji yaliyotokea katika nyumba ya waziri Obhare. Msako mkali unaendelea dhidi yake.”
Taarifa ile ilipokewa kwa namna tofauti tofauti na waandishi wa habari. Wengi walinung’unika kuwa ilifanana na taarifa ya kupikwa lakini IGP hakujibu swali lolote lile.
Huo haukuwa mwisho wa utata!!
Sam akatabasamu huku akiitazama picha zilizokuwa mkononi mwake akazifananisha na vile vichwa vilivyopigwa picha na kuwekwa magazetini. Picha zilifanana kabisa na zile alizopewa kule kijijini na John Masele ambaye sasa anashutumiwa kuwa ni muuaji.
“Wajinga ndio waliwao… siku zenu zinahesabika!” Sam akasema kwa sauti ya chini huku akiondoka zake.

___

Ili kuupaka umma mafuta kwa mgongo wa chupa serikali ikamwongezea ulinzi waziri yule. Huku nyumba ambayo yalitokea mauaji yale nayo ikilindwa na wanajeshi ambao walikuwa wakipishana kila baada ya masaa manne.
Mathias Obhare naye akawa mtu wa kulindwa kila sekunde.
Nafsi yake haikuwa na amani hata kidogo, alitamani kuubadilisha ukweli uliokuwa unamkabili lakini haikuwezekana kufanya vile tena. Mambo yalikuwa yanaanza kuwakaa kooni yeye na raisi kutokana na hila zao.

Upande wa raisi, yeye alibaki katika fumbo kuu akiwafikiria wazungu wale walivyouwawa. Akiachilia mbali wale wazungungu, akamfikiria Suzi yule mwanadada mashuhuri ambaye aliaminika kuwa na roho saba.
Ni nani aliyeuondoa uhai wake kirahisi namna ile tena pasipo kutumia silaha? Hili jambo lilimvuruga raisi na ile hali ya Benson kutopatikana hewani basi alivurugika kupita maelezo.
Alitamani kumweleza mkewe juu ya wakati aliokuwa akipitia lakini akashindwa ni wapi angeanzia kwa sababu hata siku moja hakuwahi kumweleza juu ya hila zake serikalini na ubadhilifu aliokuwa akiufanya kwa kuwaruhusu wanyonyaji kula matunda ya nchi kuliko wazawa.
Hatia ikamsulubu, akajaribu kupambana na hali ile lakini hakuweza.
Akachukua simu yake na kumpigia mtu maalumu na kukatisha kikao cha bunge alichopanga kwenda kuhutubia.
Na baada ya pale akampigia simu IGP.
“Mkuu… una uhakika kuwa hakuna vijana wanatusaliti katika kambi ya usalama wa taifa…”
“Sijaelewa unamaanisha nini mkuu..” IGP alijibu.
“Haya mauaji we unayachukulia ya kawaida haya…. Wale wazungu na yule Suzi..” alijieleza Rais.
“Mkuu kwani unawafahamu hao watu..” IGP akahoji. Na wakati ule akatambua kuwa raisi alikuwa anatetemeka. Alama ya kuuliza ikajiunda katika kichwa chake.
Hao ni akinanani kwa raisi na wana mstakabali gani hadi awe katika hali ile.
“Mhh! Hapana siwafahamu lakini Obhare anaweza kuwa anawafahamu naamini…” alijikanganya raisi kisha upesi akakata simu.
IGP akaanza kuingiwa na mashaka.
Na hapo akajaribu kuwasiliana na mrakibu mkuu Robert Masawe na kumweleza iwapo amepata fununu zozote juu ya mauaji yale.
Robert akapiga fumbo.
“Inasadikika wameuwawa na watanzania wa kawaida ambao wamechoka kunyonywa….”
“Una maana gani na nani amesema.”
“Mkuu nimesema inasadikika, hivyo ni sisi kusadiki ama la!” akajibu mrakibu.
IGP akakata simu huku akizidi kuchanganyikiwa!!
Akabaki kujiuliza juu ya maneno ya Mrakibu msaidizi, kisha akahusisha na hali ya raisi.
Kuna kitu!!! Akapigia mstari.

****
 
KISA CHA 18

USIKU wa mang’amung’amu ulimwandama Sam. Alijitazama kama kijana mzembe sana licha ya makwazo kadhaa aliyopitia.
Alizikumbuka ahadi tele ambazo alizipanga na Tina. Alikumbuka namna ambavyo kila mmoja aliapa kuwa yupo tayari kufa kwa amjili ya mwenzake.
Ajabu yeye Sam alikuwa nyumba ya kulala wageni ya bei ya chini kabisa maeneo ya Machimbo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Alijiona yu mjinga kujificha ili asife wakati mtu ambaye walipanga naye ahadi kedekede alikuwa matatani.
Wakati akiyafikiria hayo mara akamfikiria na mzee John Masele. Kuna maneno ambayo alimweleza na sasa akajiona kuwa ni msaliti muoga tena asiyejiamini.
Yale maneno yakajirudia kwa kasi kubwa kichwani mwake.
“Sam naona unatetemeka bila shaka kuna baridi sana huku kwetu..” John Masele alimuuliza Sam huku akiwa anatabasamu.
“Dah! Mzee huku ni tatizo kabisa hili baridi la Mafisa ni hatari sana, Iringa haioni ndani….” Sam alijibu.
“Sam unahisi ili baridi lipungue unahitaji nini…”
“Mzee hapa ni sweta zito kabisa nd’o linaweza kuleta nafuu” Sam akajibu, John Masele akacheka kidogo kisha akaendelea.
“Hivi umewahi hata siku moja kuzungumza na Sweta lako na kulishukuru kwa kukulinda kwa baridi?”
“Aaah! Mzee wangu lile sweta ni langu ya nini mimi kulishukuru sasa.. ule ni wajibu wake kunilinda mimi…” Sam akajibu huku akimshangaa John Masele.
“Safi sana Sam, ehe! Na vipi sweta lako likichakaa…”
“Naachana nalo nanunua jingine…”
“ooh! Umejibu vizuri sana Sam. Ninachomaanisha hapa kijana wangu, wewe ni sweta kwa watanzania Sam, unatakiwa uwalinde watanzania pasipo kusubiri kupewa shukrani ama kupewa pesa kama wanavyotaka wengine. Au kupigiwa makofi kama ilivyo asili ya wapuuzi wengi, wewe sio mpuuzi Sam na usikubali kuwa mpuuzi ishi kama sweta. Kawasaidie watanzania, usisubiri watoe shukrani, na katika kuwasaidia huko utambue kuwa unaweza kuchakaa, unaweza kufa. Ukifa wewe utakuwa umetanua njia kwa masweta mengine mapya kuwalinda watanzania wasitetemeke kwa baridi, usiogope kufa Sam. Maana waliotupa uhuru wa bendera na wao walikufa sasa ni zamu yetu kuupata uhuru wetu…”
Haya yalikuwa maneno ya John Masele usiku ule alipozungumza na Sam. Sam akajikuta katika aibu, kwanza akamfikira mpenzi wake, pili akatii maneno ya John Masele.
Akakurupuka kutoka kitandani, akasimama wima na kujiulizaatalala na kujificha mpaka lini? Na ni nani ambaye atampigania ikiwa yeye hajaamua kujipigania.
Sam akavinyoosha viungo vyake kisha akajisemea.
“Mimi ni sweta na kesho naanza kazi rasmi.”
Akarejea kitandani na kusinzia.
Asubuhi akatazama kiasi cha pesa alichobaki nacho kilikuwa kinatosha kwa harakati alizokuwa amezipanga.
Majira ya saa nne asubuhi Sam alikuwa katika ‘stationary’ moja isiyokuwa na watu wengi. Alikuwa ameketi mwenyewe kwenye kompyuta akitengeneza kitambulisho ambacho alipanga kwenda kukitumia mahali.
Alitumia muda wa saa zima kukitengeneza kisha akakichapisha na kuondoka zake akiwa amelipia huduma ile.
Sam akiwa amevalia suti yake nyeusi, miwani myeusi ya jua na kofia pana kichwani alichukua pikipiki ambayo ilimpeleka moja kwa moja maeneo ya Kurasini. Akashukia mbali kidogo na eneo alilopanga kwenda.
Kisha akatembea kwa miguu, akafanya dua fupi kisha akaingia katika ofisi za mkuu wa shule ya sekondari ya kulipia.
Akasalimia huku akiwa amesimama kisha akatoa kitambulisho chake na kukionyesha mara moja kisha akajitambulisha kwa jina.
“Inspekta Babu kutoka kituo cha kati, amri kutoka kwa IGP, Suzan anatakiwa kuwekwa mahali salama muda huu kwa usalama wake. Tafadhali namuhitaji sasa hivi, samahani kwa usumbufu ni amri kutoka kwa IGP…” Sam aliunguruma huku miwani yake ikiwa ipo bado machoni huku akiwa amekakamaa mithiri ya askari.
Ama! Mwandishi wa habari ni muigizaji pia!
Mkuu wa shule alitetemeshwa na ujio ule wa Sam ambaye mafunzo ya JKT aliyoyapitia yalikuwa yamemjengea uimara sana.
Pasipokupoteza muda, mkuu yule wa shule alimuita mwanafunzi mmoja na kumuamuru amuite Suzan.
Punde msichana mrembo umri usiozidi miaka kumi na tano alikuwa mikononi mwa Sam. Sam alitembea kwa tahadhari kubwa huku akitazama kushoto na kulia kana kwamba kuna hatari yoyote anayojaribu kupambana nayo.
Mkuu wa shule alibaki kuduwaa asijue ni kitu gani kibaya alitaka kufanyiwa mtoto yule.
Sam akatokomea akiwa na yule binti mrembo!
Siku iliyofuata taarifa zikatapakaa katika vyombo vya habari juu ya kutekwa kwa mtoto wa IGP.
Mtekaji hakuwa akifahamika.
Nchi ikaingia katika kizunguzungu kipya!!
Na hapa ndipo mpasuko ulipoanzia!!

****

Daladala ilisimama maeneo ya Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Sam akatelemka huku akiongozana na Sam pasi na kujua ni wapi alikuwa akipelekwa lakini hakuwa na mashaka yoyote kwa sababu ilikuwa kawaida kwa baba yake kuwaagiza mara kadhaa maaskari walio na vyeo vya chini yake kumchukua kutoka pale shuleni.
Hata siku hii hakushangazwa na ujio wa Sam lakini alishangazwa na mahali ambapo walikuwa wanaelekea. Na ili kuinunua akili ya Suzan mtoto wa IGP wakati konda anakuja kudai nauli Sam akakitoa maksudi kitambulisho chake kilichosomeka kuwa yeye ni askari.
Hilo likamwondolea hofu Suzan , Sam ambaye alikuwa amevaa miwani myeusi muda wote alikuwa ameikunja sura yake maksudi kabisa kama wafanyavyo askari watata.
Ama hakika JKT ilikuwa imemsaidia sana na hakujutia ile miezi mitatu aliyoitumia kwenye mafunzo ya lazima baada ya kumaliza kidato cha sita.
Baada ya kushuka Sam alimwamuru Suzan kusimama mahali amngojee huku akimsisitiza kuwa makini na mtu yeyote ambaye atajaribu kujiweka karibu naye.
Akaondoka lakini kabla hajafika mbali akageuza tena kisha akamnong’oneza Suzan mtoto wa IGP.
“Kuna maharamia wanataka kukulipua bomu… usipokee salamu ya mtu wala chochote kitu…”
Maneno yale yakamtisha Suzan!! Akaingiwa na uoga kiasi huku akitii kila aliloambiwa.
Na baada ya kama dakika kumi Sam alirejea na kumshikana mkono wakaongozana, wakazama bondeni na kisha kuibukia katika nyumba ya kulala wageni isiyokuwa na bango la kuitangaza.
“Jifanye hauna hofu yoyote… we tabasamu tu!” Sam akamsihi Suzani. Binti bila kutambua kuwa anaendeshwa kama mtambo tu
Suzan akatii!
Wakaingia hadi katika chumba kimojawapo katika ile nyumba ambayo ilikuwa imekaa katika mfumo wa ‘uswazi’.
Haikuwa na hadhi wala usalama!
“Suzan… amani yetu watanzania inawekwa mashakani na watu wachache lakini jeshi letu lipo makini kupambana na watu hao na tupo tayari kwa lolote lile ikibidi hata kufa kwa ajili yenu.” Sam alizungumza huku akizunguka chumba kile kidogo huku na kule.
Aliendelea kuzungumza bila kukoma, na baadaye akatoa pipi. Moja akamrushia Suzan wakati yeye alitupa moja kinywa na kuanza kumung’unya.
Baada ya pipi ile kutupwa mdomoni mwa Suzani mtoto wa IGP. Mazungumzo hayakuendelea tena, kiza kikatanda wakati akisinzia.

**
 
KISA CHA 20

SUZAN aliposhtuka kutoka katika usingizi asiojua alisinzia kwa muda gani alikutana na sura ambayo alikuwa akiifahamu vyema kabisa kutokana na kumwona baba yake akihangaika nayo mara kwa mara.
Alikutana ana kwa ana na mwanadamu anayetafutwa auwawe kisha kichwa chake kikatwe na kutumwa uholanzi kikaketi makumbusho ya BvB wakati anaunywa mvinyo wake anakitazama na kutabasamu.
Ana kwa ana na Samweli Mbaule.
Macho yalimtoka pima Suzan, akataka kupiga kelele lakini ghafla kijana aliyehitimu mafunzo ya JKT akamkaba koo lake kwa ustadi mkubwa.
“Bila shaka haujawahi kufa!! Sipendekezi leo iwe siku yako ya kwanza kufa, maana ukifa leo hutapata bahati ya kukutana name tena tukitabasamu….. kuwa mtulivu mtoto wa kike mimi si muuaji lakini najua kuua….” Sam alikoroma huku macho yake yakiwa mekundu.
Sam, kwa mara ya kwanza alikuwa ameamua kunywa pombe ili kujipa ujasiri wa jambo ambalo alikuwa ameamua kufanya.
Akamwachia binti yule kisha akajipekua na kutoka na simu mfukoni mwake.
Ni kama alitegemea kile ambacho binti yule alikuwa amepanga kufanya. Kwa ncha za macho yake akamtazama jinsi alivyokuwa na akili mbovu.
Mara ghafla binti akachomoka akaufikia mlango na kuanza kukimbia huku akipiga kelele.
Sam akaanza kwa kutabasamu kisha akacheka kidogo, halafu likaja cheko kubwa.
Naam! Alikuwa na kila sababu za kucheka kwa sababu binti yule hakujua kuwa mwandishi wa habari ni jasusi vilevile!
Anazijua mbinu!!
Sam akauendea mlango na kuufungua kisha bila papara akatoka nje. Akamkuta binti yule akihaha huku na kule. Hakujua wapi aende, Sam akawasha tochi yake na kummulika.
“Rudi ndani dogo, au nd’o unataka kwenda kuliwa na fisi huko.”
Suzan alibaki kuduwaa, mahali walipoingia mchana ambapo palikuwa jirani na barabara ya kwenda Morogoro. Hapakuwa mahali hapa alipokuwa wakati huu. Baridi kali iliyopenya katika ngozi yake baada ya kutoka nje nayo ilimduwaza zaidi na kukiri kuwa alikuwa eneo tofauti na Dar es salaam.
Ama kweli nipo mikononi mwa muuaji hatari! Binti yule akakiri huku akirejea taratibu alipotoka.
Sam akamfungulia mlango naye akaingia!
Kwa utulivu Sam akachukua simu na kupiga namba kadhaa na kuweka sauti ya juu katika spika.
“Nani mwenzangu?” ikasikika sauti upande wa pili. Suzan akaanza kulia baada ya kuiskia ile
sauti….. ilikuwa ya baba yake mzazi.
Sam alikuwa amempigia IGP.
“Samwel Mbaule nazungumza. Na anayelia ni mwanao wa mwisho na pekee wa kike kama sikosei.”
“Nini unasema wewe mwendawazimu, Sam nitakuua vibaya we kijana nitakatakata vipandevipande ujue. Namwomba huyo mtoto mara moja….. namwomba kabla sijauruhusu mkono wa dola ukushughulikie
“Kwani ulipowaruhusu wanikamate nikiwa Tanga walikupa jibu gani? Anyway, ni kweli utanikatakata lakini usiponisikiliza kwa makini nitakuomba kesho uwe tayari kulikuta sikio la mwanao Tanga mjini, Kichwa Ubungo stendi ya mabasi, mguu mmoja Mwanza, Macho yote mawili Arusha mjini, na utumbo utaukuta kituo cha mabasi yaendayo Mugumu Serengeti yakitokea Musoma. Aah! Vingine hautavipata maana nitakula, mfano ulimi wake, na ana makalio mazuri… nitakula yote. Ukishaniua utayakuta hayo tumboni mwangu…” Sam alizungumza kwa utulivu mkubwa lakini aliye katika hasira kuu.
Hasira ya ukombozi.
Wakati akitapika maneno yale, Suzan alizidi kulia kwa sauti ya juu.
Na mara ikasikika sauti ya mke wa IGP akimuuliza mumewe ni kitu gani kinaendelea.
Ama kwa hakika IGP alidata akawa mpole haswa na kutulia tuli huku akiamini kuwa Sam hakuwa akitania.
“Ni kitu gani unataka hadi umguse mwanangu, nitakuua Sam. Nitakuua kwa mateso.”
“Nahitaji wewe na raisi wako mkiri maovu yenu na kuisafisha Tanzania yetu…”
“Maovu? Maovu gani we mpuuzi?”
“Ukiendelea kutumia lugha za kipumbavupumbavu nitakata simu na siku nikipatikana nitakuwa nakupa pole ya kuzika kiungo kimojakimoja cha mwanao huku kifo chake kikiwa moja kati ya vifo vya kutisha vilivyowahi kutokea Tanzania.” Sam alikoroma tena.
IGP akakiri kimyakimya kuwa alikuwa amekutana na kichwa kibovu kupita vyote alivyowahi kukutana navyo, na mbaya zaidi mtoto wake alikuwa mikononi mwa kichwa kibovu.
“Ninakusikiliza ni kitu gani unataka, Sam unafikia hatua ya kumgusa hadi raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania….”
“Mmeigeuza Ikulu kama gesti mnaingia tu kizembezembe kufanya mambo yenu ya kiharamia. Mafisadi wakubwa nyi, mnawaacha askari polisi wakiishi katika nyumba za mabati zilizogawanywa kwa maboksi ndani yake, vyoo havitamaniki. Eti mnataka kwa maisha yale waache kula rushwa, mnavimbisha matumbo yenu na kuvaa suti za gharama ya juu. Naomba nikate simu nitakapopiga tena nitahitaji kujua msimamo wako.
Ole wako uzunguke na kuanza kuunda mpango wowote ule wa kumwokoa mtoto wako, IGP sina utani na sijawahi kutaniana na wewe… utaokota viungo katika mikoa niliyokutajia….. kuwa mtulivu na makini katika hili. Kumbuka huyu ni mtoto wako pekee wa kike na sio mtoto wenu wewe na huyo Saidi anayejiita raisi…..alamsiki IGP” Sam akamaliza na kukata simu kisha akaizima.
Akamtazama binti yule mrembo akiwa anabubujikwa na machozi. Akamwonea huruma lakini hakuonyesha jambo hilo machoni. Alitamani sana kumweleza kuwa yeye si muuaji wala mtu mbaya lakini alitambua kuwa ule haukuwa wakati muafaka kufanya vile.
“Nilichomwambia baba yako nitakifanya kwa vitendo, huenda ni mapema kuliko nilivyomwahidi.” Sam akamweleza yule binti kisha akafungua mlango na kutoka nje huku akiufunga mlango ambao alikuwemo yule binti.

*****
VURUMAI likakolea nyumbani kwa IGP, mkewe akawa mbogo akitaka kujua ni kitu gani kinaendelea kwa mwanawe pekee wa kike.
IGP alitamani kumweleza juu ya maelekezo ya Sam juu ya kinachoendelea lakini alilikumbuka onyo la Sam juu ya kuwa makini ili aisije kusababisha kifo kibaya kwa mwanaye.
IGP alitambua wazi kuwa kwa kumweleza mkewe kila kitu angekuwa amevujisha siri na hapo zingesambaa na kisha kumkera Sam ambaye angechukua maamuzi ya kumuua mtoto wake.
Mambo ya wanawake aliyajua!
Alipofikiria aina ya kifo ambacho Sam alikuwa amemwelezea alisisimka na kumweka Sam katika daraja la watu hatari sana wanaotakiwa kuogopwa.
Akataka kuwasiliana moja kwa moja na raisi, lakini akakumbuka kuwa Sam alimsisitiza kuwa mtoto ni wake yeye na si mtoto wake yeye na raisi kwa pamoja. IGP akakiri kuwa alikuwa amewekwa kikaangoni.
Kwa usiku ule asingeweza kuupata usingizi, kwa sababu mkewe alikuwa haishi kulia na kulalamika bila kukoma.
IGP akasimama na kuvaa suruali yake.
“Unaenda wapi baba Suzani…” Mkewe akamuhoji.
“Naenda kufuatilia hii simu iliyonipigia….” Alijibu IGP kinyonge kisha akaondoka.
Akawasha pikipiki yake na kuondoka, wazo la aende wapi lilikuja akiwa juu ya pikipiki yake. Akabadili uelekeo baada ya kupita mataa ya Magomeni akiwa anatokea Kimara akaamua kuunganisha moja kwa moja hadi feri. Akakiwahi kivuko akaingia yeye na pikipiki yake. Akavuka hadi upande wa pili.
Kisha akaendesha kwa kasi akafika mahali alipokuwa anahitaji.
Alipokelewa kwa mitutu ya bunduki na askari wanne waliokuwa wakiilinda nyumba ile. Lakini baada ya kuvua kofia ngumu aliyokuwa amevaa wote walishusha bunduki zao chini na kisha kumpigia saluti kikakamavu, yeye akajibu kizembe.
“Robert yupo ndani?” aliuliza huku akiegesha pikipiki yake kando. Askari mmoja akamsaidia. Na mwingine akamkimbia ndani kwenda kumwamsha mzee Robert Masawe mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi.
Baada ya dakika kumi wawili hawa walikuwa wamejitenga kando wakiwa katika mazungumzo mazito sana.
“Masawe.. Sam atamuua yule mtoto, we unajua Masawe nimehangaika sana hadi kupata mtoto wa kike, hivi nitaweza kuishi tena unadhani. Masawe nimekimbilia kwako naomba unishauri kabla sijaamua kumkabili raisi kama itabidi…” IGP alijieleza huku akiwa anaukosa utulivu wa akili yake.
Masawe alikuwa msikivu huku moyoni mwake akiwa anatabasamu pana sana. Aliamini kuwa ile barua pepe aliyoituma kwa Sam hatimaye alikuwa ameifanyia kazi.
Lakini kitu ambacho hakukitarajia ni Sam kumteka mtoto wa IGP. Hapo akakiri kuwa wapo vijana wanaoweza kupambana kwa ajili ya taifa lao.
“IGP hili jambo sio la kukurupukia hata kidogo, maana kosa moja litagharimu uhai wa mtoto. Raisi wetu unamjua vyema si mtu wa kutunza jambo kifuani mwake, ukimwambia atakurupuka na kupiga simu Marekani ili apate msaada wa CIA… atakapofanya hivyo na kisha Sam agundue kuwa anafuatiliwa na watu hao haki ya Mungu nakuapia tutamzika Suzan.” Masawe alimweleza IGP na kila alipokuwa akitaja neno ‘kifo’ IGP alikuwa akiukunja uso wake na kujipigapiga kifuani.
“Sasa mi nafanya nini… maana amedai kuwa tumfichue BvB mara mimi na raisi tuache ufisadi.. sielewi hata jambo moja Masawe naapa na ukweli mtupu kwa jina la mama yangu aliyetangulia mbele za haki. Masawe sijui lolote mimi….” Na hapo IGP kashindwa kuzungumza akaanza kutokwa machozi na kisha kilio cha kwikwi.
Amakweli penzi lina nguvu ya ajabu. Robert Masawe hakuamini hata kidogo kuwa IGP shupavu kama yule anaweza kulia kama mtoto mdogo. Lakini pia akapata mwanga kuwa yawezekana ni ukweli mtupu kuwa IGP hajui lolote bali anaishi tu kwa amri za raisi wa nchi.
Robert akampigapiga bega IGP na kumsihi awe mtulivu na anyamaze ili waweze kujua ni kitu gani wanatakiwa kufanya.
“Kwani wewe unamjua BvB huyo ambaye unatakiwa kumfichua.”
“Nimewahi kumsikia tu lakini siijui hata sura yake….”
“Kuna siri zozote raisi anafanya na wewe labda.”
“Hapana Masawe mimi ananiamuru na ninafanya atakavyo lakini sina siri naye.”
“Na vipi kuhusu Sam kusakwa auwawe, unajua lolote lililojificha hapo. Kwanini auwawe…. Unahisi hakuna uhusiano na jambo lolote unalolijua?” Masawe akamuhoji kwa utulivu.
“Masawe, kila kitu anajua raisi mimi naamrishwa tu na unajua sitakiwi kupinga hovyohovyo….” Alijibu huku akilalamika IGP. Masawe akatambua kuwa anachosema ni ukweli mtupu.
“IGP naomba nikueleze jambo ambalo nadhani litaweza kuleta majibu mawili, ni kifo cha mwanao ama uhai wake tena.”
“Aaah! Masawe usiniambie kuhusu Suzani kufa.. acha Masawe najisikia vibaya mno…” alilalamika IGP.
Na hapo mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi akamweleza Masawe juu ya kile anachojua ama kuhisi juu ya sintofahamu ya hila zinazoendeshwa kimyakimya na serikali. Ubadhilifu wa pesa na ufisadi uliokithiri.
“Steven Marashi kijana wetu yule unadhani amekufa kifo cha kawaida…. Si bure IGP. Unachotakiwa kufanya wewe kama wewe sasa kwa ajili ya mwanao, zungumza na Sam akikupigia simu zungumza naye kwa upole kabisa. Mwambie upo tayari kufanya atakavyo yeye na ikiwezekana hata kushirikiana naye.
“Sasa Masawe..” akasita kuzungumza aliisikia simu yake ikitetema, akajipekua akaitoa na kukutana na namba mpya.
“Nani mwenzangu….”
“Dady please! Please Dady, help me. Ataniua huyu, mpe anachotaka baba… nakuomba.” Sauti ya Suzan ikasikika ikilalamika.
IGP akataka kupasuka kwa hasira iliyochanganyikana na mshtuko.
“Upo wapi Suzan, anataka nini huyo eeh!”
“Anataka wewe na mheshimiwa raisi mseme ukweli na kisha kujivua madaraka ikiwezekana.”
“Nini anasema ukweli upi anataka, nieleze mwanangu nipo tayari kwa lolote ili wewe uwe na amani… nini anataka huyo.”
“Dady… amezungumza nami kwa kirefu sana, BvB ni nani baba, ni nani huyo? Na vipi kuhusu Masele….. ulichokitangaza juu yake una uhakika nacho baba. Tafadhali baba nisaidie nitakufa….” Suzan alijieleza upesiupesi, maneno ambayo yalimchanganya IGP vibaya mno.
“IGP natoweka kwa sasa lakini nitakayopiga kwako itakuwa simu ya mwisho. Ubia mlio nao na mtu wa kuitwa mzee Matata si sahihi kwa nchi yetu, na yeyote yule wa kujiita BvB hana nafasi katika nchi hii huru, kesho nitahitaji kujua nini hatma ya mchumba wangu Tina, maana kama si jeshi lenu kumziba mdomo basi najua unafahamu alipo. Ikiwa ataendelea kufichwa ili aisiseme ukweli basi na mimi nitaendelea kubaki na mwanao hadi siku nitaamua kumuua….” Akamaliza Sam na kukata simu.
IGP akataka kutia neno lakini hakubahatika!
Simu ikawa imezimwa!
IGP akazidi kuchanganyikiwa, Masawe akamtuliza na kisha akamweleza jambo ambalo lilikuwa na maana kubwa sana kwake kwa usiku ule.
Masawe akaelezea juu ya vile vichwa vine vya wazungu vilivyokutwa nje ya nyumba ya waziri wa nishati na madini, Mathias Obhare.
Akamueleza kuwa wale wanne ni watu walewale ambao waliagizwa hospitali ya Lugalo na mzee Matata kama madaktari kuokoa maisha ya Gama, kitu ambacho hakikuwa kweli hata kidogo. Taarifa hiyo Robert hakumweleza IGP kuwa alipewa na nani lakini dokta Mosha ndiye aliyemweleza kwani alikuwepo usiku ule wa mchezo ule.
IGP akashtushwa na taarifa ile lakini Robert akamsihi afanye mambo yake taratibu kichwani lakini kasi kimatendo ili aweze kujua kuna jambo gani linaendelea kati ya raisi na mzee Matata na baada ya hapo atapata jibu.
IGP akaagana na mrakibu msaidizi Robert Masawe huku akiahidi kuwa makini kwa kila hatua yake.

*****
Siku iliyofuata zikiwa ni siku mbili tangu vichwa vine vya wazungu vikutwe nje ya nyumba ya waziri wa nishati na madini.
IGP aliamua kuitumia siku hiyo kwa ajili ya kujua kuna nini kati ya mzee Matata na raisi wan chi. Alikusudia kufanya jambo lile la hatari kabisa kwa maslahi ya mtoto wake ambaye yupo mikononi mwa Mzee Matata. Kwa kuupata ukweli basi angeweza kumshawishi Sam aweze kumwacha huru mwanaye pasipo kumdhuru.
Alikuwa ameyapanga maswali yake vyema jinsi ya kumwingia mtu yule mzito. Akajipanga kumnyenyekea na kumwagia sifa za kutosha ili aweze kuuingia mkenge na kuyasema maneno ambayo alikuwa akiyahitaji.
Wakati huu hakuondoka na pikipiki bali gari yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom