Riwaya: Hila

mzaramo

JF-Expert Member
Sep 4, 2006
6,371
5,183
RIWAYA: HILA
MTUNZI: George Iron mosenya

MWANZO WA SHUBIRI

Umri wao ulikuwa unakimbilia miaka ishirini na nane upande wa mwanaume na ishirini na tano kwa mwanamke, lakini sasa walikuwa wamegeuka kama watoto wadogo, walikuwa wanakimbizana katika chumba kile kikubwa cha haja huku wakipondana kwa kutumia mito na mashuka meupe sana yaliyojitangaza kuwa ni masafi huku yakiwaumbua na kuwafanya kunguni waone haya kukaa juu yake.

Katika hali ya kimahaba mwanaume alimponda mwanamke kwa kutumia shuka halafu naye mwanamke akitoa kilio cha uongo na kweli kilichokonga nyoyo za mpenzi wake. Mwanamke alikuwa amesalia na chupi peke yake huku chuchu zake zilizokuwa wima kabisa zikimtazama yule mwanaume aliyekuwa amebakiwa na kibukta pekee katika matamanio.

Ndio! Ilikuwa haki yake kumtamani kiumbe huyu ambaye alikuwa na uzuri wa asili kabisa na laiti kama angejiongezea kikolombwezo cha aina yoyote basi angechukiza.

Alitakiwa kubaki kama alivyo!!!

Baada ya kuchoshwa na mchezo huu wa kukimbizana na kupigana, mwanaume alimdaka mwanamke na kukimbia naye kuelekea bafuni, binti huyu alikuwa akirusharusha miguu yake kama vile alikuwa anakataa kufanya hicho alichokuwa anafanyiwa, hali hiyo ilimfanya afananie na katoto kadogo kanakogoma kuoga na mama anakalazimisha.

Walilifikia bafu, binti akatuliwa chini katika hali ya utaratibu kabisa, akajidai amezimia lakini alipoguswa na maji kidogo aligutuka na kumrukia mpenzi wake akamkumbatia. Maji kutoka katika bomba la juu yakaanza kuwalowanishana. Ukaanza mchezo mwingine wa kuogeshana. Waliporidhika wakakongojana hadi kitandani tena.

Saa ya ukutani ilisoma mshale katika namba mbili ikimaanisha kuwa ilikuwa ni saa nane usiku tayari.
Ni kama vile waliambizana kuiangalia saa kisha kwa pamoja wakaulizana, “Saa nane??” hakuna aliyemjibu mwenzake. Mwanaume akajitoa katika mapaja ya mkewe akasogea hatua kadhaa mbele akifuata meza ndogo iliyokuwa hapo ndani.

“Unaenda wapi Samwel??” aliuliza Christina katika hali ya utani, Sam hakujibu kitu. Tina akajidai kuwa amechukia, Sam akaunda tabasamu la kinafiki akaendelea na alichopanga kukifanya.

Aliichukua simu yake akiwa na lengo la kuangalia muda kama ni sahihi lakini alikutana na simu zisizojibiwa tatu kutoka kwa watu watatu tofauti. Mmoja hakumshangaza lakini hawa wawili walimvutia kutaka kujua kulikoni.

Tina akiwa mpweke kabisa amejibweteka katika kitanda kikubwa cha futi tano kwa sita akiwa ameuvuta mdomo wake akisubiri kwa hamu kuja kubembelezwa na Sam. Kupitia ncha za jicho lake alimwona Sam akinakiri vitu fulani kwa uangalifu mkubwa kisha akamwona tena akinukuu katika simu yake kisha akasafirisha simu hadi sikioni akasafisha koo lake kabla ya kuanza kuongea.

“Ndio ni Samweli hapa!!!”
“Yaah!! Ndio mimi”
“Labda asubuhi sana nikiwa natoka hapa hotelini”
“Magomeni hapa!! panaitwa ..panaitwa….New Travertine Hotel”
“Haya usiku mwema mkuu!!”

Alimaliza maongezi Sam kisha akaitazama simu yake kama anayemtegea mtu wa upande wa pili aweze kukata badala yake yeye aliyepiga. Baada ya kuhakikisha kuwa simu imekatwa upande wa pili aliirudisha ilipokuwa.

Alisahau kuangalia saa!!

Alitembea kwa kunyata akakifikia kitanda, alijaribu kumgusa Tina. Hakujibiwa kitu, ilikuwa ni kawaida ya Tina ambaye alikuwa na pete ya uchumba kidoleni kuwa mtumwa wa wivu, wakiwa na uhusiano wa kimapenzi kwa miaka mitano bado hakuwahi kulizoea shinikizo la wivu.

“Ni nani huyo usiku huu Sam!” aliuliza kwa kukaripia Tina. Sam akajibu kwa tabasamu aliloamini kuwa litamlainisha Tina ambaye alikuwa katika kuutumikia utumwa wake katika wivu. Tabasamu lile halikusaidia.

Sam akamsogelea Tina aliyekuwa amempa mgongo.

“Baby nilikuwa na maongezi fulani kikazi”
“Nimechoka Sam, mara ngapi nakwambia usitumie taaluma yako ya uandishi wa habari kunilaghai…kazi gani saa nane”??” alilalamika tena Tina kama vile aliwahi kumfumania Sam, akiwa na mwanamke mwingine jambo ambalo kamwe halikupata kutokea tangu wawe na uhusiano.

“Tina mamangu unawaza mabaya buree…ngoja nikuletee simu usikie tulichokuwa tunazungumza tena maksudi kabisa nimerekodi maana nilijua tu tabia zako za wivu.” Alizungumza kama anasemezana na nafsi yake kwa kuilaumu huku akiifuata iule simu. Alirejea nayo akamsihi Tina amsikilize lakini bado alikuwa kiburi.

Tina anapenda kubembelezwa!!!aliwaza Sam kisha akaiweka ile simu pembeni ili aweze kumbembeleza huyu mke wake mtarajiwa.

Ghalfa mlango ukagongwa zaidi ya mara tatu, Sam na Tina wakajikuta wamekaa kitako, Tina alikuwa na dalili zote za wasiwasi. Sam hakuwa na shaka aliamini sana ulinzi wa mali katika hoteli hii. Hivyo alimtazama Tina wakakutanisha macho, Tina akakwepesha, Sam akacheka kwa sauti ya juu kidogo kisha akaufuata mlango akaufungua.

“Bwana Samweli Mbaule, samahani kwa usumbufu, sisi ni askari kutoka kituo cha polisi Usalama, unahitajika kituoni haraka sana” alizungumza mmoja kati ya wageni wale waliokuwa na nguo za kiraia huku akitoa kitambulisho chake na wenzake walifanya kama alivyofanya yeye.

“Kituoni? Kuna nini?.” Aliuliza kwa utaratibu bila hofu Samwel.
“Bwana Mbaule umeanza usumbufu wako tena, hatuna mzaha leo na hatutahofia utakachoenda kuandika magazetini….fuata unachoambiwa!!.”

Alitoa karipio kali askari mwingine aliyekuwa na sigara mdomoni. Sam akatoa tabasamu hafifu kisha akacheka kwa dharau na kuwaonyesha vidole vitatu akimaanisha kuwa anaomba apewe dakika tatu.

“Sam kuna nini tena wamekufuata hapa usiku huu, na..”
“Kama kawaida yao wasumbufu tu ngoja nikawasilize.” Alijibu kwa utulivu huku akiiweka mwilini suruali yake.

Tina alikuwa ametulia tuli akiwa na wasiwasi mkubwa, licha ya kuzoea kashkashi alizokuwa anazipata Samwel kutokana na kuifanya kazi yake ipasavyo lakini siku hii Tina hakuwa akihofia juu ya ujio wa wale watu waliojitambulisha kama askari, Tina alikuwa ameathiriwa na wivu mkali sana hata hao askari hakuwaamini, alihisi ni kamchezo tu Sam amekacheza ili aweze kutoka ndani ya chumba kile bila bughuza ya maswali yanayokera na yasiyokuwa na tija.

“Baby ngoja nikawasikilize nadhani sitapoteza muda sana. nitakupigia simu kwa lolote lile litakalotokea tafadhali usizime simu.” Sam alinong’ona kisha akazibusu papi kavu za Tina lakini zilizovutia muda wote.

Tina hakuonyesha ushirikiano alikuwa ameathiriwa na hofu na wivu. Akawa amezizima!! Asijue kama amzuie Sama ama amuache aende!!
Samwel alitoka nje akapokewa na wale askari kisha wakaongozana hadi nje ambapo walikutana na gari ya kifahari aina ya VX, urafiki wa kutembea kama marafiki uliishia pale walipoikaribia ile gari, ghafla askari mmoja alimdaka Samwel mikono akaizungusha kwa nyuma akamtia pingu. Samwel alilalamika lakini hakusikilizwa, matukio haya yalimpa faraja sana kwani alijua kuwa hiyo ni makala ambayo itamvutia kila mtanzania anayependa kusoma makala zake ambazo hufichua maovu.

Ndani ya gari aliwekwa katikati na kupewa onyo kuwa asizungumze chochote kile. Sam akatii amri.
Usiku ule wa manane hapakuwa na msongamano wa magari hivyo walitumia dakika kadhaa kukifikia kituo cha polisi cha Usalama Magomeni.
“Bwana Samwel Mbaule upo na utaendeelea kuwa chini ya ulinzi mkali sio kwa nia mbaya bali kuisaidia polisi katika uchunguzi wa kifo cha Steven Marashi. Ambacho …”

“Steven Marashi!!.Steve amekufa…ni huyu ninayemjua mimi ama.” Alihoji kwa taharuki kubwa, suala la kuwasaidia polisi katika upelelezi halikumpa shida alikwishazizoea kauli hizo, lakini sasa alikuwa amesikia juu ya Steven Marashi, msanii maarufu kabisa wa filamu katika nchi ya Tanzania ambapo alijiwekea makazi yake katika jiji la Dar es salaam maeneo ya Mwananyamala na baada ya kuwa maarufu akajisogeza Kijitonyama.

“Unauliza swali wakati majibu unayo bwana Sam, unahusika kwa namna moja au nyingine”
“Nahusika? Kivipi?.”
“Hebu vua mkanda, saa….anyway wewe sio mgeni hapa toa visivyohitajika mwilini hapo ukalale kwanza maongezi asubuhi sana.” Alipewa maelekezo hayo, hakuleta ubishi ni kweli alikuwa mzoefu wa kulazwa selo walau kwa masaa ama siku moja. Mara zote ikiwa kwa sababu za usalama wake lakini sasa alikuwa na kesi ya kujibu. Kesi ya mauaji!!!

“Samahani hebu naomba nimwambie mke wangu kuwa sitarudi!” aliomba Sam, akapatiwa simu yake. Akapiga mara ya kwanza ikamjibu kuwa inatumika, akapiga mara ya pili na ya tatu hali ikawa hiyo hiyo. Sam akachukia kiasi fulani akapiga kite cha hasira akataka kuwarudishia simu ukaingia ujumbe akaufungua harakaharaka pasi na umakini.

“Wewe eti ni kweli Steve amekufa? Maana hata siamini hapa nilipo usingizi umekatika.” Ujumbe huo ukamshtua, namba ile iliandikwa kwa jina la Slm, akaificha hofu yake akaufuta ule ujumbe akawarudishia simu kisha akafanya kuvua vile, alivyoambiwa akaingizwa katika chumba kilichokuwa na watu wachache tofauti na kawaida yake.

Alijisikia mpweke tofauti na kawaida, taarifa ya kifo cha Steven Marashi ilikuwa imemshtua sana japo hakuuonyesha mshtuko huo hadharani.
“Na huyo Slm ni nani kwani..mbona sikumbuki ni lini nimehifadhi jina hili kwenye simu yangu.” Sam aliumiza kichwa chake na maswali kedekede. Hakuwepo wa kumjibu. Akajilegeza taratibu akajikunja sakafuni akaanza kupambana na mbu wakali wasio na huruma pale ndani huku wakisaidiwa na visisimizi vidogo lakini visumbufu vilivyokuwa katika kutafuta ridhiki.

Baadaye usingizi ukampitia!!! Akaja kushtuliwa na makelele ya mwananchi mwingine aliyekuwa anaingizwa katika chumba hicho kisichokuwa na uhuru.

Alipoingia tu, Samwel akawa ameamka, harufu ya pombe kiasi ikamtuma Sam kuhisia kuwa aidha jamaa alikuwa amekamatwa akiendesha gari huku amekunywa pombe ama alikuwa amekutwa akizurura usiku katika doria zao.

“Vipi mazee?” alisalimia lakini hakujibiwa na watu wote ila Sam tu!!
“Mazee dunia mapito aisee, Steve Marashi amededi jamani.” Yule mgeni ambaye hakujibiwa salamu yake sasa akageuka kivutio ghafla mahabusu takribani wote wakaamka kumsikiliza.
“Marashi huyu huyu au mwingine?” mahabusu mwingine akauliza.
“Huyo huyo unayemjua kaka….”
“Amepata ajali ama…?”
“yaani mambo bado magumu ila nasikia wametangaza kuwa washukiwa wawili wamekamatwa tayari eti mmoja ni mwandishi maarufu wa habari…sijui anaitwaje hata hawajasema bado.” Alijieleza yule mgeni ambaye ghafla alibatizwa jina la Biggy kutokana na unene wake.

“Biggy amefia wapi? Biggy alikuwa anaumwa? Biggy amekufa saa ngapi?.” Haya yote yalikuwa maswali aliyotakiwa kuyajibu Biggy lakini alishindwa kutokana na maswali hayo na majibu kugeuka kuwa kelele.

Samwel Mbaule alikuwa mkimya sana akisiliza kila neno analotoa Biggy kinywani mwake na kulifanyia kazi harakaharaka.

“Nipo matatani, kuna mtu amenichoma hapa.” Sam aliwaza hivyo huku akiwa na kumbukumbu ya kuzungumza na Steve masaa manne kabla ya kutembelewa na polisi pale walipokuwa na Tina wake.

“Washukiwa wawili, mimi pamoja na nani sasa?” alijiuliza Sam. Akakosa majibu.
______________
 
KISA CHA PILI

Tina kwa upande wake hakuweza kabisa kupambana na kitanda ili kimpe usingizi, alikuwa na wasiwasi uliosababishwa na kutoweka kwa Sam huku akiongozwa na maaskari, kila mara aliitazama simu yake kama vile muda wowote ule inaweza kutoa mlio wowote ambao utamaanisha kwa Sam anampigia simu kumjuza kuwa yu njiani anarudi mahala walipokuwa wameamua kujipumzisha siku hiyo. Alisubiri kwa dakika arobaini na tano bila majibu yoyote zikaongezeka nyingine kumi na tano likawa saa zima bila dalili zozote za simu ile kuita.
Uvumilivu ukaanza kutoweka wivu ukazidi kumtafuna na sasa akajihisi hasira kwa mbali. Akazibonyeza namba za Sam kama vile anayejaribu kujionyesha ni jinsi gani ana kipaji cha kukariri. Baada ya zoezi hilo akavutiwa na kitufe cha kijani ambacho kama akikibonyeza mwenye namba zilizopo mbele ya kioo cha simu yake atapokea simu yake.
“Simu unayopiga….inatumika kwa sasa…the number you are dialing is busy” Tina akasubiri sekunde kadhaa akapiga tena simu ya Samwel jibu likawa hilo hilo, akajisikia kama anakabwa kooni na kitu kutoka katika mwili wake.
Zilikuwa ni hasira.
Samwel anaongea na wanawake zake!!! Aliwaza kisha akaitupa simu yake kitandani. Akaitazama kwa jicho la hasira jinsi ilivyokuwa ikiviringika, lakini ghafla akaikodolea macho makali, akakitazama kishikio chake kisha akaikwapua kama vile alikuwa katika kunyang’anyana na mwenzake. Akatoa tabasamu la kujilazimisha kisha akapumua kwa nguvu. Lile donge la hasira likalegea kidogo.
Ile simu haikuwa ya kwake, kumbukumbu za kumbadilishia Samwel simu wakati akiwa mlangoni akizungumza na polisi walioondoka naye. Simu zao zilikuwa zinafanana kila kitu na zilinunuliwa siku moja, kama zisingekuwa na vishikio basi ilikuwa ngumu kuzitofautisha ni kishikio hiki kilimfanya Tina kugundua tendo alilolifanya tendo ambalo kwa namna yoyote lazima lingekuwa kero kwa Samwel iwapo ataligundua, na ilikuwa lazima aligundue.
Wakati wote Tina alipokuwa akimpigia Samwel kumbe alikuwa anajipigia mwenyewe na hata Samwel wakati anampigia Tina na yeye alikuwa anajipigia mwenyewe. Tina alirekebisha makosa yake na kubonyeza namba zake katika simu ile ili aweze kuzungumza na Sam lakini alikuwa amechelewa simu ilikuwa imezimwa tayari.
Tina akataharuki asijue la kufanya!!!
Alikuwa amefanya kosa moja kubwa sana.
Kosa ambalo lingeweza kumgharimu kwa muda mrefu.
Kosa lililosababishwa na wivu wa kimapenzi.
Ni wivu huu sasa unamwingiza matatani!!!
__________

Katika chumba cha mahojiano, chumba kilichokuwa na faragha kuu kuliko vyumba vingine ambavyo Samwel Mbaule aliwahi kufanyiwa mahojiano. Faragha hii ilimshangaza sana lakini bado hofu kwake ilikuwa ni ndoto ya kufikirika na kusadikika.
“Samwel Mbaule!! Mwandishi wa kujitegemea aliyebobea” sauti ya bwana aliyekuwa anamuhoji Sam ilikoroma katika hali ya ujivuni.
Sam akatoa tabasamu la kinafiki bila kutia neno juu yake.
“Mbona mmemuua bado mapema?” swali hilo likamshtua Sam lakini hakutaka kuutangaza mshtuko huo, akaendeleza tabasamu lake lile le kughushi lakini safari hii akauliza kidogo, “Nani huyo?”
Mpelelezi wa kesi hiyo akatoa kicheko cha kusanifu. Huenda alikuwa akilipiza karaha alizozipata kutokana na tabasamu la Sam.
“Bwana Samwel…hii ni simu yako sivyo!”
“Kama hakuna ujanja wowote uliofanyika hiyo ni simu yangu!”
“Ujanja gani wa kukufanyia wewe, kwa lipi ulilotukosea.”
“Lolote ambalo silijui.” Alijibu kwa kiburi kiasi.
“Kwa hiyo hii simu ni yako.”
“Nilikwishajibu swali lako.”
“Na tangu umuazime mtu ni masaa mangapi yamepita?.”
“Sina kumbukumbu ya kumuazima mtu yeyote yule.”
“Vizuri sana..aah!! umesema hujaazima mtu eeh!!”
“Hukunisikia nikikujibu??” alijibu kwa kukaripia
Bwana yule mwenye nywele nyingi zilizoota bila utaratibu maalum akashtushwa na jibu hilo, akamkodolea macho Sam.
Kiburi chako kimefikia tamati!!! Aliwaza huku akijikuna kwa kutumia kalamu yake isiyokuwa na wino wa kutosha.
“Hii ni simu yangu na hii ni simu yako uliyokiri kuitambua. Weka namba zako hapa na uipige simu yako.” Alitoa maelekezo hayo, Sam akayapokea kwa utulivu na kuyafanyia kazi. Aliingiza namba zake kwa utulivu. Akapiga na kisha akaweka katika sauti ya juu ili kila mmoja aweze kusikia.
Simu ikaanza kuita. Sam macho yakamtoka lakini hayakufikia kiwango cha yule mpelelezi ya kwake yalitoka mara mbili na kuwa kama panya mkubwa aliyenaswa katika mtego uliowekewa nyama yenye harufu ya kuvutia na yeye akategeka. Asubuhi mtegaji anakutana na macho yaliyokodolewa yakisaidia kuielezea mauti yake ilivyokuwa ya kuogofya na kushtukiza.
“Mbonaa….eeeh!! ina maana…hebu ngoja…” alizungumza huku akitweta mpelelezi wa kesi ile. Kisha akachomoka kama mshale akakifunga kile chumba cha mahojiano na kutimua mbio baada ya dakika mbili alirejea na askari wawili, Sam aliwakumbuka kuwa ni hao ambao walimweka mahabusu usiku uliopita, na hapo walikuja kumchukua tena akawa amerejeshwa mahabusu chini ya ulinzi mkali bila kufanyiwa mahojiano yoyote yale.
Samwel bado hakujiruhusu kuogopa chochote, aliamini hakuwa na hatia ya aina yoyote.

****


“Hii ni simu yangu na hii ni simu yako uliyokiri kuitambua. Weka namba zako hapa na uipige simu yako.” Alitoa maelekezo hayo, Sam akayapokea kwa utulivu na kuyafanyia kazi. Aliingiza namba zake kwa utulivu. Akapiga na kisha akaweka katika sauti ya juu ili kila mmoja aweze kusikia.
Simu ikaanza kuita. Sam macho yakamtoka lakini hayakufikia kiwango cha yule mpelelezi ya kwake yalitoka mara mbili na kuwa kama panya mkubwa aliyenaswa katika mtego uliowekewa nyama yenye harufu ya kuvutia na yeye akategeka. Asubuhi mtegaji anakutana na macho yaliyokodolewa yakisaidia kuielezea mauti yake ilivyokuwa ya kuogofya na kushtukiza.
“Mbonaa….eeeh!! ina maana…hebu ngoja…” alizungumza huku akitweta mpelelezi wa kesi ile. Kisha akachomoka kama mshale akakifunga kile chumba cha mahojiano na kutimua mbio baada ya dakika mbili alirejea na askari wawili, Sam aliwakumbuka kuwa ni hao ambao walimweka mahabusu usiku uliopita, na hapo walikuja kumchukua tena akawa amerejeshwa mahabusu chini ya ulinzi mkali bila kufanyiwa mahojiano yoyote yale.
Samwel bado hakujiruhusu kuogopa chochote, aliamini hakuwa na hatia ya aina yoyote.

****
Mkuu wa kituo cha polisi alikuwa amejiinamia huku akichokonoa meno yake kwa kutumia njiti ya kiberiti, mezani palikuwa na soda aina ya Sprite iliyokuwa ikitoka mfano wa jasho laini lenye kuvutia, hali iliyoonyesha kuwa ndani ya muda mfupi ilikuwa ikihangaika katika baridi kali kutoka katika jokofu. Aliitazama soda ile huku akiilani nyama iliyokuwa imejificha katika fizi zake na kumletea usumbufu.
Baada ya kufanikiwa kuchokonoa na kutoa alichotoa, aliusogeza mkono wake ukaitwaa ile soda na kukiondoa kizibio cha juu, akapiga funda mbili kubwa, kisha akatulia kusikilizia utamu, akataka kuongeza funda jingine simu yake ya mkononi ikaita.
Bwana Sabatho, alikuwa ni mtu anayependa sana kutilia maanani kila jambo linalokatiza mbele yake, hata kama litakuwa limeingiliana na chochote alichokuwa akifanya, tabia hii ilimfanya agombane sana na mkewe na hata watoto wake wangekuwa na uwezo wangemgomea asiwe anatoka hovyo nyumbani tena bila taarifa. Mkewe alihangaika na hatimaye akazoea.
Ilikuwa saa mbili na dakika kadhaa asubuhi, ilikuwa nadra sana mzee huyu kustafutahi pamoja na mkewe lakini siku hii waliifanya ya kukumbukwa. Baada ya mlo huu walikuwa na mazungumzo na mtoto wao wa kiume aliyekuwa anaingia kidato cha kwanza katika shule ya bweni, walihitaji kumpa nasaha za hapa na pale huku baba yake (Mzee Sabatho) akiwa ameahidi kumsindikiza kwa kutumia gari yake ya kazini hadi kituo cha mabasi ambapo alikuwa amekata tiketi.
Huku mkewe akiwa chumbani akijiandaa na mtoto akiwa anakaribia kumaliza kufunga mkanda wa nguo yake.
Simu ya mzee Sabatho iliita, akaahirisha kupiga funda la soda iliyokuwa mbele yake akapokea simu.
“Simu aliyonayo sio ile inayohusika katika tukio, kuna jambo jingine jipya!!” alipewa maelezo hayo mafupi lakini akaelewa kwa kirefu.
“Nakuja huko sasa hivi…fatilia ni wapi simu hiyo inapatikana na aliyenayo simu hiyo akamatwe mara moja!!!”
“Sawa!!” upande wa pili ukajibu.
“Na huyo Samwel asiachiwe huru kwanza mpaka afahamike aliyekuwa na simu hiyo.” Alitoa maelezo hayo kisha akakata simu.
Fikra kuhusu mke na mtoto wake, alizisahau mara moja na hata ule utamu wa ile soda ukaishia pale pale. Mzee Sabatho akatoweka haraka, akiwa katika kuondoka mtoto na mkewe waliishia kuisindikiza gari yake kwa macho.
Mama mtoto akazisikia dalili zote za kutoa machozi lakini alijikiza kwa kuwa alikuwa sambamba na mtoto wake.
“Allen nakuja kukupeleka achana na babako tushamzoea” mama Allen aliaga na kukimbilia chumbani mwake. Huko alilia kilio cha kwikwi hadi akajiridhisha mwenyewe ndipo akatoka ndani akiwa tayari ameunawa uso wake vyema.

****

Christina Elisha Prosper ama Tina kama alivyozoeshwa kuitwa tangu utotoni na sasa lilikuwa limezoeleka katika kila kinywa cha mwanadamu aliyemfahamu hata kwa muda mfupi, sasa alikuwa katika hofu kubwa sana simu ya Samwel ilikuwa mikononi mwake na hata ile ya kwake ambayo ilikuwa mikononi mwa Samwel sasa haikuwa ikipatikana, wivu haukuwa na nafasi tena bali uoga juu ya nini kimemsibu mpenzi wake huyo ambaye walikuwa katika hatua za kuitangaza siku yao ya kuutangazia umma kuwa wao ni mwili mmoja kikamilifu. Tina alikurupuka kitandani majira ya saa moja na nusu asubuhi. Mkononi alikuwa ameikamata kikamilifu simu ya Samwel, hakujua ni muda gani alipitiwa na usingizi lakini alitambua kuwa alisinzia.
Alikimbilia bafuni akanza kujiuliza endapo aoge au asioge, kwani ni masaa kadhaa yaliyopita alikuwa ameoga akiwa na Sam wake. Akiwa katika kujiuliza simu ya Sam iliita, akapokea baada ya kuona jina. Akamtaka radhi mpigaji kuwa mwenye simu ameisahau nyumbani.
Alidanganya!!!
Akaanza kuvua nguo zake ili aweze aidha kuoga ama kuyabadili mavazi yake kwani bado hakuwa na jibu muafaka.
Aliposalia kama alivyozaliwa alisikia simu ikiita tena kisha ikakatika. Aliiendea na kuitazama akakuta ni namba mpya, akaanza kuuhisi usumbufu atakaoupata kutokana na kuwa na simu ya Sam. Akiwa katika kufikiria hilo mara ikaita tena akaipokea.
“Samahani kaka naitwa ….”
“Samahani, mwenye simu ameisahau nyumbani.”
Akamkatisha. Mchezo huo ukaanza kumkera zaidi, akatamani kuizima simu ya Sam lakini uoga ukamwingia vipi kama Sam atampigia na amkose. Ama vipi kama ataiharibu miadi ya Sam. Aliamini atamkera mno. Akaiacha ilivyo akaamua kuingia kuoga.
Ni heri angechukua maamuzi ya kumkera Sam kuliko kuiacha simu ile ikiwa hewani ama ni bora asingeoga aondoke tu, huenda angejiokoa na janga hili.
Hakuzima simu na aliingia kuoga!!! Kosa kubwa lisiloonekana madhara yake mara moja!!!

Tina akiwa katika hali ile ya kutaharuki alioga kwa pupa huku akisahau kuzifunika nywele zake ndefu zisiweze kuingiliwa na maji, alikuwa katika hali ambayo hakuwahi kuwa nayo hapo kabla.
Hali ya hofu iliyopitiliza.
Hakujiremba kama ambavyo hufanya siku zote, hakutumia dakika kumi na tano kuzichana nywele zake katika mitindo ya kisasa huku akifurahia lawama za mpenzi wake Samwel kuwa anamchelewesha kazini. Leo hii Tina alichomoka mbio mbio akiwa hajazipanga nguo zao chache katika mabegi yao kwa mpangilio maalum hivyo mabegi yale mawili kuvimba sana.
Alifika mapokezi akiwa katika hali ile ile ya ajabu ajabu, laiti kama dada wa mapokezi asingepigiwa simu kutoka vyumbani huenda angemuhoji Christina kulikoni akawa vile. Bahati mbaya hakupata nafasi hiyo. Tina akawa ametoweka baada ya kulipia bili za chakula walichokula usiku uliopita.
Mwanga wa jua hafifu likiwa bado na rangi nyekundu nyekundu uliyasabahi macho yake makubwa mithili ya gololi ndogo.
Akiwa katika kuyalazimisha macho yake yaizoee hali ya pale nje alijikuta akigongana na mwanaume mkakamavu sana kwa bahati mbaya. Maumivu ya bega aliyoyapata yalimfanya amlaani kimya kimya huyo mtu ambaye hakupata hata nafasi ya kumwangalia mara ya pili.
Mabegi mawili moja kila mkono, jaketi moja pamoja na mkoba wake kwapani huku usoni akiwa hajiamini Tina alikuwa kama anayetoroka. Kelele za madereva teksi zikinadi biashara yao zilimchanganya sana dada huyu akajikuta akiwa njia panda, hata alipokwapuliwa begi lake na dereva mmoja kisha likaingizwa garini hakuwa na kipingamizi alijikuta amejitoma garini.
"Wapi bosi??" Dereva alimuuliza abiria wake. Abiria akawa bubu kwa muda hakusema lolote.
Dereva akamwacha afikiri. Hakuna alichokuwa anafikiri binti huyu.
"Ndio dada!!"
"Ehh!! unasema?" aliuliza Tina katika hali ya mshtuko.
"Tunaelekea wapi?" aliuliza kwa ukarimu dereva huku akiitia moto gari yake kwa mbwembwe.
"Mhhhh!!! ahaaa!! twende hapa nanii hapa.....Sinza Kamanyola" alijibu Tina baada ya kujiuma uma kwa sekunde kadhaa. Sinza Kamanyola palikuwa nyumbani kwa mama yake Tina, mama huyu licha ya kwamba hakuwa mama mzazi wa Tina ambaye alikuwa ni yatima, alikuwa anampenda Tina huenda kuliko mama yake mzazi aliyetangulia mbele ya haki. Ni eneo hili Tina aliamini lilikuwa sahihi kwa ajili ya pumziko na ushauri nasaha kutokana na jambo lililotokea. Mama huyu mpole aliyefahamika kwa jina la Mama Tina ama Naomi kwa waliyelingana naye umri alikuwa na historia ya kuwahi kuwasuluhisha Tina na Sam mara kadhaa walizokuwa katika mitafaruku. Hivyo Tina aliamini kuwa ulikuwa wakati muafaka kwa mkongwe huyu kutenda miujiza yake tena, kwani tayari Tina alikuwa na wasiwasi kuwa Sam atakuwa amekasirishwa sana na kitendo cha kubadilishiwa simu.
Dereva alitii amri akajifunga mkanda lakini hakumsisitiza Tina kujifunga kama yeye. Safari ikaanza. Dereva huyu ambaye mwanzoni Tina alitegemea kumpa heshima ya shkamoo ila akajikuta amesahau kutokana na taharuki alikuwa mkimya sana lakini baada ya safari kunoga ni kama alikuwa na yeye ananogesha kwanza mdomo wake. Alianza kupiga stori za hapa na pale Tina alikuwa kimya akimsikiliza bila kumuelewa. Dereva hakuchoka kumburudisha abiria wake huyo katika gari yake hii isiyokuwa na redio.
"Hatimaye wamemuua halafu mi nilijua tu!!! hafiki mbali huyu, hakujiwekea kinga tatizo.. yaani vijana wa siku hizi bwana"
"Nani tena?" kwa mara ya kwanza Tina akajikuta amevutiwa na hiyo mada akauliza swali.
"Si huyu muigizaji wenu huyu....nani wanamuita...nani watoto wangu wanampenda sana huyuu...Steve...ewalaaa Steve Marashi" alijibu dereva huku akijikuna ndevu zake kwa fujo kulitafuta jibu.
"Steven yupi??"
"Huyu Steve Marashi huyu we hujasikia?"
"Acha masihara wewe Steve amekufa lini?? mbona mi sijasikia wala..acha utani wewe!!!" Tina alibisha huku akihitaji maelezo zaidi.
"Ndo nakwambia sasa waemuua jana mbona..mi nilijua tu…" alielezea kwa manung’uniko.
Dereva akatoa tabasamu hafifu baada ya kuona sasa Tina anamuunga mkono maongezi yake.
"Babu wewe Steve huyu ninayemjua mimi.."
"Ndio huyo ameuliwa na huyu mtoto nani huyu.......", alitaka kuzungumza akakatisha maongezi yake kisha akaendelea, "Hiyo gari inatufata sisi au?? maana muda kweli" aliuliza yule dereva, Tina akageuka nyuma kutazama kwa ushahidi tu bila msaada.
"Kata hapo kulia..." alitoa maelezo hayo bila kuujali wasiwasi aliokuwanao dereva.
Dereva akatii amri, suala la gari kuwafuata kwa nyuma likaishia hapo.
Baada ya dakika tatu tangu wakate kona gari ikasimama, Tina akamwona mama yake walipotazamana wakajikuta wanatabasamu, tabasamu lililoutangaza upendo wao. Japo macho ya mama yalikuwa, mekundu na yamevimba hali hiyo haikumshtua sana Tina.
Tabasamu lile halikudumu sana, likayeyuka bila wao kujua kama limetoweka tayari na kuwa mshangao. Mshangao wao ukamezwa na vumbi kali lililotokana na breki kali za gari mbele ya nyumba ya mama yake huyo wa kufikia. Dereva aliyekuwa anasubiri malipo yake na yeye aliungana na wanawake hawa kushangaa lakini alikuwa ni Tina aliyezidi kushangaa zaidi baada ya wanaume waliojengeka miili kutoka katika ile gari aliyokuwa imehisiwa na dereva kuwa imewafungia mkia kumvamia na kumzingira.
"Askari....upo chini ya ulinzi!!!" alipewa maneno hayo mafupi kisha bila kuuliza swali wakamtia katika bangili zisizopendwa na jinsia zote bangili hizi za rangi ya shaba zilibatizwa jina la 'pingu'.
Kwa mara ya kwanza katika mikono ya Tina. Bila maelezo wala majibu ya maswali yake ya 'nimefanya nini' aliongozwa hadi katika gari waliyokujanayo. Mama, damu ikawa nzito kuliko maji akawakimbilia polisi wale na kuwavamia akiwa na maswali mengi, hakujibiwa hata moja zaidi ya kusukumwa na kubaki akigaa gaa chini akilia bila msaada wowote.
Dereva wa teksi hakukumbuka kama alikuwa anadai pesa ama la aliwasha gari lake akatokomea huku akiilani siku hii iliyoanza vibaya sana kwake.
Aliondoka huku akiacha msiba mkubwa. Majirani ambao waliamkia kuzungumza habari juu ya msiba wa Steve sasa waliweka hayo makubwa yasiyowahusu wakavalia njuga suala hili zito linalowahusu la mama Tina!!!!

******
 
KISA TATU

Baada ya dakika tatu tangu wakate kona gari ikasimama, Tina akamwona mama yake walipotazamana wakajikuta wanatabasamu, tabasamu lililoutangaza upendo wao. Japo macho ya mama yalikuwa, mekundu na yamevimba hali hiyo haikumshtua sana Tina.
Tabasamu lile halikudumu sana, likayeyuka bila wao kujua kama limetoweka tayari na kuwa mshangao. Mshangao wao ukamezwa na vumbi kali lililotokana na breki kali za gari mbele ya nyumba ya mama yake huyo wa kufikia. Dereva aliyekuwa anasubiri malipo yake na yeye aliungana na wanawake hawa kushangaa lakini alikuwa ni Tina aliyezidi kushangaa zaidi baada ya wanaume waliojengeka miili kutoka katika ile gari aliyokuwa imehisiwa na dereva kuwa imewafungia mkia kumvamia na kumzingira.
"Askari....upo chini ya ulinzi!!!" alipewa maneno hayo mafupi kisha bila kuuliza swali wakamtia katika bangili zisizopendwa na jinsia zote bangili hizi za rangi ya shaba zilibatizwa jina la 'pingu'. Kwa mara ya kwanza katika mikono ya Tina. Bila maelezo wala majibu ya maswali yake ya 'nimefanya nini' aliongozwa hadi katika gari waliyokujanayo. Mama damu ikawa nzito kuliko maji akawakimbilia polisi wale na kuwavamia akiwa na maswali mengi, hakujibiwa hata moja zaidi ya kusukumwa na kubaki akigaa gaa chini akilia bila msaada wowote.
Dereva wa teksi hakukumbuka kama alikuwa anadai pesa ama la aliwasha gari lake akatokomea huku akiilani siku hii iliyoanza vibaya sana kwake.
Aliondoka huku akiacha msiba mkubwa. Majirani ambao waliamkia kuzungumza habari juu ya msiba wa Steve sasa waliweka hayo makubwa yasiyowahusu wakavalia njuga suala hili zito linalowahusu la mama Tina!!!!

******

Kila aliyeingia mahabusu siku hiyo alikuwa na habari juu ya msiba wa Steve Marashi, kila mtu alikuwa na lake lakini kati ya hayo habari za mwandishi kuhusika zilikuwa zikitajwa. Bado Sam alijikaza asiweze kujiwazia mabaya aliamini alikuwa hausiki hivyo kwake yeye hiyo ni habari anayotakiwa kuiandikia makala na jamii iweze kusoma, mara moja moja alimlaani huyo mwandishi aliyehusika na mauaji hayo
"Acha papara Sam, tulia ukitoka ufanye uchambuzi wa kina" Alijionya Sam baada ya kugundua alikuwa akilalamika bila kuwa na uhakika na malalamiko yake.

Ile hali ya yeye kurudishwa rumande hata kabla ya kuandika maelezo ilimuacha katika kizungumkuti, awali aliwaza kuwa huenda muhusika amepatikana naye ataachiwa huru muda wowote lakini hadi kigiza kinaingia mambo yalikuwa magumu sana, aliendelea kusota mahabusu. Akiwa amekata tamaa kabisa Sam alijitafutia kikona kizuri kabisa ambacho aliamini kuwa kitamfaa kwa usingizi wake hadi asubuhi ambapo aliamini kuwa lazima apate muafaka wa kwa nini anakaa rumande siku zote hizo bila kuufahamu mustakabali wake, akiwa hajaandika maelezo wala kufafanuliwa kwa kina kosa lake.
Hakujua usingizi ulimpitia saa ngapi na hakujua hata huo muda aliamshwa ilikuwa saa ngapi. Alitolewa nje ya chumba cha mahabusu na kupelekwa sehemu nyingine kabisa ambayo haikuwa na mwanga wa kutosha. Huko aliwakuta watu wawili, mmoja akijitambulisha kama mfuasi wake wa siku nyingi katika habari huku mwingine akiwa ni mpelelezi wa kesi yake. Hapakuwa na mazungumzo marefu sana bali huyo mfuasi ambaye alikuwa mnene wa umbo alikuwa amekuja kumwekea dhamana Samwel, dhamana katika kosa ambalo halijui, dhamana hata kabla ya kuandika maelezo. Kidogo Sam aikatae dhamana ile lakini alijihisi kama anataka kufanya kosa la kuukataa uzima wa milele tena katika mtindo wa ofa. Pia maumivu ya mbu wakali wasiokuwa na huruma waliomshambulia akiwa mahabusu nao walikuwa sababu ya kujikuta anapokea dhamana isiyoeleweka eleweka.
"Kaka Sam," alinong'ona yule mfuasi huku akimuinamia Sam sikioni, baada ya kugundua anasikilizwa akaendelea, "Nimejitoa mhanga hapa kukusaidia rafiki yangu ili na wewe unisaidie na ujisaidie mwenyewe, kuwa makini!!!"
"Kivipi tena?'' alihoji Sam ambaye alikuwa peku huku nguo yake ikiwa imelegea kiunoni. Hakuwa na mkanda wala viatu.
"Ukitoka hapa utajua. Tafadhali kuwa makini!!!" alihitimisha yule bwana ambaye Sam alijaribu kumtambua bila mafanikio. Wakati huo mpelelezi wa ile kesi alikuwa mbali kidogo hakuweza kuyasikia maongezi haya.
Sam japo hakuridhika na lile jibu bado alihitaji sana kuwa huru hivyo alifanya kama ameelewa ili maongezi yasiwe marefu.
Usiku huo baada ya Sam kurudishiwa saa na vitu vyake vingine anagundua kuwa ilikuwa yapata saa nane na nusu usiku. Alikuwa na akiba ya pesa, pia alikuwa na kadi ya benki. Aliachiwa huru akatoweka pale bila kujua ni wapi aelekee. Akiwa nje ya kituo kile cha polisi akakumbuka mara ya mwisho kabla ya kufika hapo alikuwa mapumzikoni na mpenzi wake Tina. Tina ambaye walikuwa na ahadi ya kuoana katika siku za karibuni.
Sam akajenga tabasamu hafifu, akaona ni vyema ampigie simu Tina ili aweze kufahamu ni wapi alipo aweze kwenda. Alipopiga simu ikawa inatumika. Wivu ukapenya kama kisu kikali katika ngozi ya mwanadamu. Sam akauma meno, akaitazama saa yake Saa tisa usiku!!!! Anaongea na nani sasa hivi?? alijiuliza kwa sauti ya chini kisha kama vile aliyemkosea alikuwa mbele yake, Sam alipiga teke kopo tupu la maji lililokuwa limetelekezwa barabarani hapo. Kopo likapiga kelele za uchungu Sam akajikuta anashtuka mwenyewe alikuwa anataka kuingia katika hali ya kutaharuki akajiminya minya kichwa chake katika hali ya kuzuia taharuki hiyo.
Alipojaribu tena na tena hali ikiwa ile ile, aliamua kumtumia ujumbe Tina. Ujumbe ule sio tu ulikuwa ukielezea mchomo wa wivu ulivyompiga bali pia ulikuwa unaandamana na hasira na kero kwa kutopokelewa simu yake. Alipomaliza kuandika ujumbe ule akamkumbuka mama yake Tina wa kufikia. Akawaza kama ni sahihi kumpigia simu ama la kwa muda huo. Wivu ukamjibu kuwa ni sahihi, akatafuta jina kwenye simu kwa jinsi alivyohifadhi hakuliona, akatafuta tena hakufanikiwa kitu.
Akaamua kumtumia Tina ujumbe ule!!!
Ilikuwa kitendo cha sekunde kadhaa mlio ukajibu, Sam akahisi ni taarifa ya kupokelewa ujumbe alioutuma kwa Tina (deliver report). Akabaki kusubiri majibu bila mafanikio, akataka kupiga tena simu, akakutana na ujumbe kutoka katika simu yake, namba iliyotuma ujumbe ule ilifanana kwa kila kitu na namba ya Tina, Sam akayalalamikia masikio yake kwa uziwi wa kijinga. Aliyalaumu kwa kutousikia ujumbe ule ukiingia, taratibu Sam akaufungua na kuanza kuusoma, kama ujumbe ule haukuwa nakala ya ujumbe alioutuma yeye basi ulifanana kila kitu na maneno aliyomwandikia Tina.
"Tina ananirudishia meseji niliyomtumia????" alitahamaki Sam, alipoitazama tena simu aligundua kuwa alikuwa anatetemeka. Kusalitiwa ukawa wasiwasi wake wa kwanza, Tina alikuwa anamsaliti na ujumbe huo ameutuma bwana ambaye wako naye kitandani ama chumba kimoja muda huo.
Sasa hakujiuliza mara mbili mbili, akaamua kumpigia mama Tina simu kwa kuziandika namba zake ambazo alikuwa amezikariri, jina 'Mama' likatokea katika kioo cha simu, Sam akajiuliza neno mkwe lililokuwa mbele ameliondoa nani, lakini hakujali sana mama na mama mkwe wote ni mama tu!!. Simu iliita lakini haikupokelewa.
Sam akazimisha simu yake akachukua usafiri na kuelekea nyumbani kwake maeneo ya Yombo dovya wilaya ya Temeke. Kabla hawajafika mbali sana alimsishi dereva wa teksi asimamishe, akachukua bia mbili za kopo akaingia nazo garini akawa anagida taratibu huku akipiga miluzi isiyomaanisha wimbo wowote.
Alimlipa mwenye teksi ujira wake, akazunguka nyuma ya nyumba ambapo huweka funguo wake wa ziada. Akaingia ndani akavua nguo zile chafu akaingia maliwatoni akajisafisha vyema kisha akajirusha kitandani, uchovu wa kulalia sakafu akiwa rumande, pombe alizokunywa kwa fujo zilishirikiana katika kumtia mwandishi huyu katika kifo cha muda.
Usingizi wa pono!!!!

* * * * *

Saa nne asubuhi haja ndogo ndio ilimtoa kitandani Sam, alipomaliza haja zake alirejea tena chumbani alitamani kulala tena mara akaitamani na simu yake. Halafu ghafla usingizi ukakatika ghafla baada ya kuona santuli ya picha (VCD) ya moja kati ya filamu alizowahi kupewa na rafiki yake wa ukubwani waliotokea kushibana kiasi chake japo hawakuwa karibu karibu. Ilikuwa ni filamu ya 'MIUNGU SABA', iliyochezwa na kinara Steven Marashi. Ghafla kengele za dharula zikalia kichwani mwake, akakumbuka kuwa kuna habari za umauti kumkumba huyu swahiba wake, kitu ambacho hakukiamini mara moja lakini alikitilia maanani.
Kama mkuki akachomoka akaiendea simu yake, akaiwasha ili aweze kupiga namba za Steve aupate ukweli kama alichokisikia akiwa rumande ni kweli ama tetesi. Wakati simu inawaka alikuwa akizitafuta namba za Steven katika kijitabu alipozinukuu maana Steve alikuwa mahiri sana wa kubadilisha namba za simu kutokana na usumbufu aliokuwa akiupata chanzo kikiwa umaarufu.
Akiwa katika kutafuta simu ikaita, akaikimbilia kupokea akiamini kuwa ni Tina.
Hakuwa yeye alikuwa mama yake na Tina.
"Shkamoo mama!!" alisalimia Sam.
"Marahaba nani wewe?" upande wa pili ulihoji.
Mama naye ina maana amefuta namba yangu!!! alijiuliza Sam kabla ya kujibu. "Mimi Sam mama!!"
"Samwel mwenzako amefanya nini tena mbona hivyo? Na yuko wapi sasa hivi?"
"Mimi ndio nikuulize wewe mama..."
"Uniulize mimi tena wakati hajazungumza na mimi polisi wamemkamata tangu jana asubuhi!!"
"Polisi!!! wapi na saa ngapi?" Sam aliuliza akiwa ametaharuki tayari.
"Kwani wewe hiyo simu yake amekupa saa ngapi Sam....ujue unanitania wewe mtoto" Mama Tina akaanza kuwa mkali.
"Simu gani mama tena?"
"Sam mwanangu naomba uweke kando utani...Tina yupo wapi kama upo naye niambie nisije kufa kwa presha mimi"
"Mama sipo na Tina mimi..."
"Na hiyo simu!!!"
"Ni yangu....hii mama"
Mama Tina akatukana tusi la kikabila chao kisha akakata simu.
Sam akasahau yanayomuhusu Steven Marashi, sasa yakazuka ya mama.
Simu...simu mbona ni ........Mungu wangu!!!!! akashtuka Sam baada ya kuutazama ule mkanda wa ile simu haukuwa wa kwake. Ilikuwa ni simu ya Tina kumbe muda wote alikuwa anajipigia simu, alikuwa anajitumia ujumbe na kukasirika pasipo sababu!!!.
HILA!!!! akashtuka Sam.
Tina mikononi mwa polisi!!! kidogo afikirie kurudi kule polisi aulizie lakini maneno ya tahadhari kutoka kwa mtu asiyemfahamu yakamtia wasiwasi.
"Kuwa makini!!!! Kuwa makini!!!!"
Sam akaamua kutuliza akili yake akautafuta umakini alioambiwa!!!!




Akiwa katika kutafuta simu ikaita, akaikimbilia kupokea akiamini kuwa ni Tina.
Hakuwa yeye alikuwa mama yake na Tina.
"Shkamoo mama!!" alisalimia Sam.
"Marahaba nani wewe?" upande wa pili ulihoji.
Mama naye ina maana amefuta namba yangu!!! alijiuliza Sam kabla ya kujibu. "Mimi Sam mama!!"
"Samwel mwenzako amefanya nini tena mbona hivyo? Na yuko wapi sasa hivi?"
"Mimi ndio nikuulize wewe mama..."
"Uniulize mimi tena wakati hajazungumza na mimi polisi wamemkamata tangu jana asubuhi!!"
"Polisi!!! wapi na saa ngapi?" Sam aliuliza akiwa ametaharuki tayari.
"Kwani wewe hiyo simu amekupa saa ngapi Sam....ujue unanitania wewe mtoto" Mama Tina akaanza kuwa mkali.
"Simu gani mama tena?"
"Sam mwanangu naomba uweke kando utani...Tina yupo wapi kama upo naye niambie nisije kufa kwa presha mimi"
"Mama sipo na Tina mimi..."
"Na hiyo simu!!!"
"Ni yangu....hii mama"
Mama Tina akatukana tusi la kikabila chao kisha akakata simu.
Sam akasahau yanayomuhusu Steven Marashi, sasa yakazuka ya mama.
Simu...simu mbona ni ........Mungu wangu!!!!! akashtuka Sam baada ya kuutazama ule mkanda wa ile simu haukuwa wa kwake. Ilikuwa ni simu ya Tina kumbe muda wote alikuwa anajipigia simu, alikuwa anajitumia ujumbe na kukasirika pasipo sababu!!!.
HILA!!!! akashtuka Sam.
Tina mikononi mwa polisi!!! kidogo afikirie kurudi kule polisi aulizie lakini maneno ya tahadhari kutoka kwa mtu asiyemfahamu yakamtia wasiwasi.
"Kuwa makini!!!! Kuwa makini!!!!"
Sam akaamua kutuliza akili yake akautafuta umakini alioambiwa!!!!

******
 
KISA CHA 4

Kile kitendo cha kutambua kuwa simu iliyokuwa kiganjani mwake haikuwa ya kwake bali ya mchumba wake kilimfadhaisha sana Sam na hapo kengele ya hatari ikalia katika kichwa chake.
Ni kitu gani kinatokea hapa?? Akajiuliza bila kuyapata majibu sahihi.
Akili yake ikaiunda picha iliyotokea kituo cha polisi pindi alipokuwa anahojiwa, alikumbuka namna mpelelezi wa kesi yake alivyomuuliza juu ya uhalali wake katika kuimiliki simu ile, akakumbuka namna alivyojibu bila wasiwasi na hata alipoambiwa apige namba yake akajaribu lakini kinyume na matarajio ikaita upande wa pili.
Inamaana niliingia mahabusu na simu ya mke wangu ama?
Alijiuliza tena lakini safari hii akiishika tena ile simu na kisha kujaribu kupiga namba yake afahamu ni nanji huyo aliyekuwa na simu yake… japo kwa makisio alitambua kuwa Tina ndiye anayeweza kuwa na simu ile na si mwingine.
Alipopiga simu haikuwa ikipatikana!
Sam akaishiwa nguvu na ubaridi ukajipenyeza katika ngozi yake. Akaitambua kuwa ile ni dalili ya uoga jambo ambalo hata yeye mwenyewe alishangaa ni kwa nini anaogopa.
Kutopatikana kwa simu yake hewani kukamkumbusha namna yule mpelelezi wa kesi yake ambaye hakupata hata kumjua jina lake alivyoshtuka baada ya simu ile kuita upande wa pili.
Kuna nini? Alijiuliza.
Na wakati huohuo akatoka na mwayo mrefu na tumbo likaunguruma. Akakumbuka kuwa hakuwa ametia chochote mdomoni tangu aingizwe mahabusu na hata alipoachiwa bado hakukumbuka kutii haja za tumbo lake.
Sam akaituliza akili yake na kujaribu kupuuzia kila kitu kilichokuwa kimetokea huku akijiaminisha kuwa Tina wake yupo salama na kila kitu kilichotokea yawezekana ni makosa tu yaliyofanywa na jeshi la polisi.
Aliamua kujifariji hivyo ilimradi tu aweze kuiruhusu akili yake kuuongoza mwili wake kufanya mambo mengineyo.
Mojawapo likiwa ni kula!!
Alikuwa na njaa!!
Njaa ikamfanya amkumbuke Mama Lao…. Na hapo akafanya tabasamu la matumaini……
hakujua kama alikuwa akikifuata kizaazaa!!......

*****

MAMA LAO MGAHAWA, ulikuwa mgahawa maarufu sana wilayani Temeke. Hata kwa ambao hawajawahi kufika waliutambua kwa jina. Na hii ni kwa sababu ya huyo Mama lao mwenyewe… mmiliki wa mgahawa ule.
Kwa jinsi jina lilivyokuwa kubwa usingeamini macho yako pale ambapo ungefika eneo la tukio na kukutana na majamvi yasiyozidi sita yaliyozungushiwa katika miti kadhaa, turubai chakavu liliunda kivuli katika namna ya mapengo mapengo.
Maneno mengi ya mama lao, ucheshi na ukarimu kwa wateja wake ilikuwa ngao kuu ya kuwavutia watu wengi.
Hata Sam na Tina licha ya kuwa na kipato kikubwa kiasi bado waliweza kujumuika mara kadhaa katika mgahawa ule kujipatia vitafunwa, supu na mara moja waliwahi kukaa kwa ajili ya chakula cha mchana katika banda lile maarufu. Lakini umaarufu wake haukulipuka ghafla tu!!
Umaarufu wa banda lile ulikuzwa zaidi na kitendo cha Sam na Tina wake kujumuika na muigizaji maarufu Steven Marashi katika banda lile kwa ajili ya kula supu ya makongoro.
Si mama lao pekee aliyetokwa macho kumshangaa marashi bali kila mteja aliduwaa na asiamini kile alichokuwa akikiona. Steve naye hakuuacha ucheshi wake uishie runingani tu… aliuendeleza hadi pale.
Waandishi wa habari hawakuwa nyuma… baada ya kusikia habari za Steve Marashi kukutwa katika banda bovu la mama lishe walifanikiwa kunasa picha kadhaa, nyingi na maarufu zikiwa zile ambazo steve alikuwa ameshika kongoro akilipeleka mdomoni.
“AMINI USIAMINI STEVE MARASHI AMEFULIA AKUTWA KWA MAMA LISHE AKILA KWA MKOPO!!”
“STEVE MARASHI AISHIWA!”
Hivi vilikuwa vichwa vya habari katika magazeti mbalimbali ya udaku. Steve alipohojiwa katika vipindi mbalimbali alilipaisha kadri awezavyo banda la mama lao. Kama hiyo haitoshi Steven Marashi akarekodi filamu yake moja huku akilitumia banda lilelile la mama lao…. Na hapo sura ya mama lao ikatambulika kwa wengi.
Na hapo kila mtu akalitambua banda lile hata ambaye hajawahi kuliona.

KITENDO cha kuambatana na Steve Marashi kilimfanya Sam awe anatazamwa kwa jicho la tatu na watu mbalimbali huku wengi wao wakimuonea gele.

Tofauti na siku nyingine ambazo Sam huwa anafika kwa mama lao na utani wa hapa na pale huku mama lao akiulizia wapi alipo Steve Marashi…..siku hii ilikuwa tofauti.
Sam alikuwa mkimya na mama lao naye alikuwa mkimya zaidi. Kila mteja aliyeutambua urafiki wa Sam na Steve alikuwa akimtazama kwa jicho la huruma bila kusema neno lolote.
Alikuwa ni mama lao aliyezua kizaazaa!!.......
Ilianza kwa sauti ya chini!!
Mama lao akawa anasemasema peke yake huku akifunyanga vidole vyake, maneno haya hakuna aliyeyaelewa!!
Sauti ilipopanda juu kiasi ikaonekana alikuwa akizungumza kikabila ambacho pia hakuonekana aliyekuwa akikifahamu.
Na hatimaye kikafuata Kiswahili….
Mama lao akawa anaomboleza kifo cha Steven Marashi katika namna ya kulaumu. Mara amlaumu Mungu, mara amlaumu marehemu mwenyewe na hatimaye akapaza sauti akamlaumu Lilian.
Na hapo akaanza kujigalagaza chini, ikawa ni shughuli ya wateja kuhangaika naye.
“Uuuuuuuwi!! Lili weeeee, umeniulia mwanangu Lili weeeeee…… uuuwi Sam weeee wamekuuulia rafiki yako Sam weeeee….” Mama lao aliendelea kupiga mayowe bila kukoma.
Banda la jirani wakakisikia kilio cha mama lao, walikuwa akina mama… walipofika wakaungana katika kilio wakijua tayari mama lao amefiwa!
Walianza kulia wasijue amefiwa na nani… walilia tu!
Wanawake!!
Penye wengi hapakosi mengi, wakati wengine wakihangaika na mama lao, vijana wengine waliitumia fursa hiyo kutoroka bila kufanya malipo na wengine wakiiba vitu vichache vilivyokuwa katika banda lile.
Bila hawa vijana kutambua ni kitu gani wameiba…. Waliiba kitu kimoja cha muhimu sana!!
Hata mama lao alipotulia hapakuwa na uwezekano wa kuendelea tena na biashara kwa siku ile.
Sam alirejea nyumbani kwake huku picha ya Steve akiwa marehemu ikianza kumwingia vyema kichwani na kuamini kuwa ni kweli swahiba wengi alikuywa amekufa. Alitamani kuwapigia simu waandishi wenzake ili aweze kujua ni nini kimemuua Steve lakinio alihofia kupata majibu kadha wa kadha yasiyoshabihiana na mwishowe yamchanganye kabisa. lakini akapiga moyo konde na kuamua kumpigia mmoja wapo wa waandishi na pia rafiki yake wa karibu.
Alipoishika simu aweze kumpigia akakumbuka kuwa ile haikuwa simu yake, hivyo hata namba asingeweza kuipata.
Wakati akiitazama simu ile akakutana na ujumbe ambao hajui uliingia muda gani.
Akaufungua bila kusita.
“Shoga eti wanasema mimi nimemuua Steve jamani…. Shoga naenda kufia jela mimi.. najua ni wewe unayeweza kuniamini. Hata nikiwa jela tambua kuwa nisingeweza kumuua Steve hata kwa kulazimishwa….. I will miss u.”
Sam alirudia kuusoma ujumbe ule mara mbilimbili, mikono yake ikaanza kuvujwa jasho.
Huyu ni nani anayesadeikika kumuua Steve? Na anafahamiana vipio na Tina?
Alijiuliza huku akizitazama namba zile zilizohifadhiwa kwa jina la SLM.
Namaba zilezile zilizotuma ujumbe wakati akiingia mahabusu!!
Akili yake ikafyetuka ghafla, zile lawama kuwa polisi wanaweza kuwa walimbadilishia simu wakati yupo mahabusu zikateketea na kuamini kuwa alibadilishiwa simu mapema kabisa hata kabla hajaingia mahabusu.
Nani mwingine kama sio Tina….
Wivu wa kipuuzi kabisa!! alighafirika Sam.
Na kwa jinsi tukio lilivyokuwa zito akaona ni heri afike nyumbani kwa mama Tina aweze kumweleza anayoyafahamu juu ya tukio hilo ili wajue ni wapi wanaweza kuanzia kuutafuta utatuzi wa Tina kukamatwa na polisi.
Njaa ilikwishatokomea zake, akajiandaa upesi na kuchukua pikipiki maarufu kama bodaboda… ikamfikisha nyumbani kwa mama Tina.
Salamu yake ilijibiwa kinyonge sana, tena bila kutazamwa usoni kama alivyozoea mama yule kumtania kwa kumuita majina yanayowakilisha mapenzi mazito.
Sam akatambua kuwa mama mkwe wake alikuwa amenuna!!
Kukaa kimya kusingesaidia Sam akalazimika kuuliza maswali mawili matatu.
“Hao polisi walimkamatia wapi Tina…”
“Hapo nje!”
“Walikuwa wamevaa sare za kipolisi..”
“Sikumbuki!!” alikuwa akijibu kwa kiburi fulani….
Sam akaamua kuwa mkali kiasi …
“Mama, nina uchungu mkubwa sana kusikia kuwa….”
“Weee komea hapo..uwe na uchunmgu hadi dakika hii hujui mchumba wako alipo. Uchungu gani we mwana nauliza…eeh! Uchungu upi hujui kama mwenzako yupo anapigwa huko na hao maaskari we umelala tu…” mama mkwe aling’aka.
“Mama nimelala mahabusu jana. Nilikamatwa kama alivyokamatwa Tina bila kuijua sababu yangu…nimeachiwa usiku wa manane.. nikadhani kuwa Tina yupo hotelini. Nikapiga simu yake naambiwa inatumika. Lakini baadaye sana nikagundua kuwa Tina anayo simu yangu na mimi ninmayo yake, sijui kama alinibadilishia ama nilichanganya wakati naondoka. Si unafahamu kuwa zinafanana kila kitu simu zetu. Hadi hapa ninapozungumza na wewe sijui kinachoendelea…. Nd’o nimekuja hapa tujue nini kinatokea. Lakini kwa ufupi na ufinyu sana kuna mmoja wetu ama wote kwa pamoja tunahusishwa juu ya kifo cha Steven ‘Ven’ Marashi..” alizungumza kwa sauti ya kunong’ona lakini inayoonyesha msisitizo.
Macho yakamtoka mama Tina aliposikia mstari wa mwisho. Mwanaye kuhusishwa na kifo cha msanii yule maarufu. Akanyanyua mikono yake na kuiweka kichwani kisha akafumba macho kama anayekabiliana na hali fulani ya kuzuia kumbukumbu fulani isimpotee.
“Nilimkataza lakini Tina…”
“Ulimkataza nini mama….eeh!” Sam alihoji kwa shauku. Lakini mama hakujibu zaidi ya kuendelea kulalamika peke yake.
“Hawa watu maarufu kujifanya anawajuajua….ona sana..” alijisemea mwenyewe.
Sam akamtuliza na kumweleza kuwa kila jambo litaenda sawa. Na hapo akaaga kuwa anaelekea vituo kadhaa vya polisi kumtafuta Tina.

Alizurura siku nzima vituo vyote vikubwa akimuulizia Tina, lakini hakupata walau fununu juu ya wapi alipokuwa mpenzi wake huyo.
Kila kituo hawakutambua jina la Christina wala kutambua msichana yeyote aliyekamatwa katika mazingira ambayo Sam alijaribu kuyaeleza.
Hali hii ilimtia katika utata. Alitarajia kuwa litakuwa jambo jepesi tu kufanikiwa kumpata Tina lakini haikuwa hivyo.
Namba za makachero kadhaa alizokuwa anazifahamu zilikuwa katika simu yake ambayo hakuwa nayo tena. Jambo hili likamtesa sana.
Wakati akiendelea kuhangaika, majira ya saa mbili usiku simu ya Tina aliyokuwanayo ikaita. Haikuwa mara ya kwanza kuita, na mara zote hakuwa akipokea.
Akaitazama macho yakamtoka pima. Ilikuwa ni namba yake ikiwa inampigia.
Akatambua kuwa iwe isiwe lazima atakuwa ni Tina anayepiga maana ndiye ambaye alikuwa na simu ile.
“Sisi ni vibaka wastaarabu.. tumeokota simu hapa Koko Beach. Sisi hata shida ya hii laini hatuna, shida yetu ni simu tu. Kwa hiyo tunakuachieni laini yenu hapa katika mwamba huu uliopo ndani ya maji. Tunaiwekea kijiwe juu yake, ukiwahi asubuhi utaikuta lazima… hata ukirudi sasa hivi. Asante kwa simu bosi..” ilikuwa ni sauti ya kijana muathirika wa madawa ya kulevya (teja) ikikoroma upande wa pili. Na kabla hajajibu chochote simu ikakatika.
Alipojaribu kupiga haikuwa ikipatikana na kamwe hakuipata tena!!
Kengele za hatari zikaanza kupiga katika kichwa chake, kupatikana kwa simu yake maeneo ya fukwe za Koko kulimaanisha kuwa Tina hakuwa kituo cha polisi tena ama la kuna hila zinafanyika ambazo yeye binafsi hajui nini yaweza kuwa sababu.
Taarifa ya kupigiwa simu kwa namba yake hakuifikisha kwa mama mkwe wake mapema usiku ule. Alihofia kuwa mama yule anaweza kupagawa na labda shinikizo la damu linaweza kumhangaisha.
Akajiahidi kuwa siku inayofuata asubuhi ataenda kumweleza kila kitu alichofanikiwa kufanya kwa siku nzima.
Ni vile tu wanadamu hatujui lijalo… lakini laiti kama tungejua lijalo. Sam angemweleza tu mama mkwe wake…. Huenda angemwepusha na mengi!!
Ila hakujua…..

*****


Taarifa ya kupigiwa simu kwa namba yake hakuifikisha kwa mama mkwe wake mapema usiku ule. Alihofia kuwa mama yule anaweza kupagawa na labda shinikizo la damu linaweza kumhangaisha.
Akajiahidi kuwa siku inayofuata asubuhi ataenda kumweleza kila kitu alichofanikiwa kufanya kwa siku nzima.
Ni vile tu wanadamu hatujui lijalo… lakini laiti kama tungejua lijalo. Sam angemweleza tu mama mkwe wake…. Huenda angemwepusha na mengi!!
Ila hakujua…..

*****
 
KISA CHA 5

BODABODA ilisimama jirani na nyumba aliyokuwa akiishi Sam. Malipo aliyafanya awali kabisa walipokuwa kituo cha mafuta. Hivyo Sam hakuwa na la kupoteza zaidi ya kuagana na yule dereva bila kutilia maanani lile agano la usiku mwema alilopewa na yule bwana ambaye tayari alikuwa ameitia moto pikipiki yake.
Kichwa cha Sam kilikuwa katika maumivu makali sana kutokana na mawazo mengi na pia mizunguko mingi aliyokumbana nayo siku hiyo na mbaya zaidi hakuwa amepata mafanikio yoyote.
Tina wake hakujulikana alipo hadi wakati huo na simu yake iliyopigwa kutoka fukwe za koko hakujua ni nani aliifikisha huko na kwa sababu zipi.

Mwendo wa mita mia mbili aliouzoea kutoka barabarani hadi nyumbani kwake aliuona mrefu sana siku ile tofauti na siku nyingine. Alijivuta hivyohivyo akiambaa katika njia ndogo ambayo alizoea kupita kila siku…….
Hatimaye akaufikia mlango wake, akauchukua funguo mahali pake ambapo huwa anauhifadhi kila siku. Akafungua mlango na kuingia ndani. Akakiendea kitufe cha kuwashia taa.. akajaribu kuwasha lakini haikuwaka.
“Aaargh! Luku imeisha tena?” alisononeka Sam huku akitupa kibegi chake kidogo bila kujali ni wapi kitatua.
Akajipekua na kuitoa simu aliyokuwa nayo akaiwasha na kuanza kuangaza huku na kule. Chumba kilikuwa shaghalabaghala katika namna ambayo hakukiacha asubuhi alipoondoka kwenda kwa mama mkwe wake.
Alipoangaza dirishani akashangaa na akili yake ikafunguka kuwa nyumba ya jirani ambayo walikuwa wanatumia LUKU moja umeme ulikuwa unawaka.
“Hah! Mbona……. Mbona kwa mama Sarah unawake sasa….” Alijiuliza kwa sauti ya juu iliyoonyesha kukereka waziwazi.
“Au kuna shoti?.... lakini mbona nyumba nayo ipo hovyo…nani ameingia humu ndani……” alijiuliza tena lakini safari alikuwa anahisi kama anaishiwa nguvu katika mwili wake, akaisikia ile simu ikiwa nzito, ikaanguka chini kisha na yeye mwenyewe akalegea na kuanguka chini.
Sam akatambua kuwa alikuwa alikuwa amenusa madawa makali ya kuleta usingizi ndani ya kile chumba. Akajikaza asiweze kusinzia akapapasa na kuikamata simu yake, akabofya kitufe cha kupigia akakutana na namba ya mama mkwe wake. Akajaribu kubofya lakini mkono ukawa mzito akaishia tu kuitazama simu yake. Mwisho akasinzia……
Fahamu zikamtoka!!!

***

Katika mitaa flani nchini Tanzania, jopo la watu wanne lilikuwa katika chumba cha siri kwa siku nzima wakifuatilia kwa ukaribu kabisa kila neno ambalo vinasa sauti vilivyotegwa katika chumba cha Sam maeneo ya Yombo wilayani Temeke.
Usiku huu umakini uliongezeka zaidi baada ya kuanza kusikia purukushani za mlango kufunguliwa. Walitambua kuwa ulikuwa ni muda wa Sam kurejea nyumbani. Na huo nd’o huo wakati waliokuwa wakiusubiri kwa hamu kubwa ili watambue iwapo machale yao yamewacheza kwa mtu sahihi ama la!
Nyaya za umeme zilikuwa zimetibuliwa maksudi ili Sam akigundua kuwa nyumba yake imeingiliwa na watu basi aanze kuhaha kutafuta kitu ambacho hata wao walikuwa hawajawahi kukiona lakini waliamini kuwa anaweza kuwa anahusika ama anaweza kuwa nacho.
Ajabu Sam hakuonekana kushtushwa sana na wala hakutafuta chochote walichodhani kuwa anaweza kukitafuta.
Madawa ya kulevya yalikuwa yanaanza kufanya kazi dakika kumi na tano baada ya kuvutwa na muhusika. Muda huu kwa upande wao ulikuwa sahihi kabisa iwapo hatajihangaisha kukitafuta basi huenda atakuwanacho mfukoni ama popote ambapo anaweza kuwa alikihifadhi na kutembea nacho. Hivyo atakapopoteza fahamu zake basi wataingia na kumpekua huku na kule ili kujihakikishia.
Naam! Kama walivyokuwa wamepanga….. Sam akapoteza fahamu, vijana wawili wakakamavu wakaingia upesi ndani ya kile chumba na kumgeuza Sam wakiwa wamevaa mipira maalumu mikononi ili wasiweze kuacha alama zozote ndani ya chumba kile.
Tochi zao zikaangaza vyema wakati Sam asiyejitambua akiwa anapekuliwa kila kona. Kibegi chake nacho kikapekuliwa kwa umakini bila kufanikiwa kupata chochote ambacho kingeweza kuwasaidia katika upelelezi wao wa kitu wasichokuwa na uhakika nacho.
Hatimaye wakaambulia sifuri!!
Wakamuacha Sam pale chini wakaangaza chumba kwa makini tena. Kisha wakatoweka baada ya kurekebisha kile walichotengua!!

****

Baridi kali ya sakafu majira ya saa kumi na moja alfajiri ilimzindua Sam kutoka alipokuwa amelala. Taa zote zilikuwa zinawaka kuanzia sebuleni hadi chumbani.
Sam akainuka na kuketi kitako, akili yake ikaanza kufanya kazi akakumbuka mambo kadhaa yaliyotokea na kumfanya alale pale chini.
Sam akageuka na kuitazama simu yake, ilikuwa palepale pembeni yake, na jina lililokuwa katika kioo lilikuwa la mama mkwe wake. Akakumbuka kuwa kabla hajakumbwa na usingizi mzito alitaka kumpigia mama mkwe wake lakini hakufanikiwa.
Ni akina nani hawa na wanataka nini? Sam alijiuliza huku akisimama wima.
Wakaukata umeme na sasa wameurejesha!! Wapuuzi kweli na pia ni waoga wa kutupwa! Alijisemea Sam huku akifanya tabasamu hafifu la kejeli. Ule ubaradhuli na ubabe aliouvuna wakati anapitia mafunzo ya JKT ulijijenga katika mwili wake na akili yake. Akawapuuzia maadui zake na kuwaona kuwa walikuwa na mioyo ya kike.
“Kama kweli wanaume waje tena bila mbinu za kishamba kama hizi…” alimalizia kwa kutoa tusi zito la nguoni asijue amemtusi nani.
Kisha akaliendea jokofu na kunywa maji glasi mbili…..
Hakutaka kukaa akabaki amesimama vilevile akifikiria matukio hayo na kukosa maana yake.
“Halafu mama alimzuia Tina kufanya nini?... haiwezekani iwe kirahisi rahisi tu eti alimzuia kujhichanganya na watu maarufu ama vionginevyo… lazima kuja jambo la ziada ambalo amelificha….. asubuhi na mapema naamkia nyumbani kwake haya mambo ya wanawake kufichiana siri yanaweza kugharimu maisha ya Tina…..” alisita kidogo baada ya kutambua kuwa Tina anaweza kupoteza uhai kizembe, uzembe wa mama mkwe wake kuficha siri.
Hali ya kutambua kuwa Tina anaweza kupoteza uhai kizembe ilimtia katika uoga. Lakini mara akatishika zaidi baada ya kutanabai kwamba sio Tina pekee ambaye anaweza kupoteza uhai, bali hata yeye mwenyewe angeweza kuwa amekufa tayari kwa sababu walifanikiwa kumzimisha kwa masaa kadhaa akiwa hajitambui kabisa na hajui ni kitu gani wamefanya akiwa hajitambui.
Jamaa ni hatari hawa aisee!! Alijisemea Sam huku uoga ukimwingia na ule ukakamavu na kiburi cha awali kikipotelea mbali.
Hali ya hatari ikatawala, mbaya zaidi wanaomletea hatari hakuwa akiwafahamu na hakuijua sababu ya wao kumletea kashkashi hiyo.
Uwepo wake katika hali ya uhuru alitambua wazi ni kwa sababu wawindaji walikuwa wakitaka kuendelea kumtumia.
Sam akajiapiza kuwa makini katika kila hatua ambayo atakuwa anapitia.
Zilipita dakika zaidi ya arobaini Sam akiwa amesimama wima mbele ya jokofu lake akifikiri hili na lile.
Hatimaye akafikia hatua ya kuondoka wakati uleule kuelekea kwa mama mkwe wake, hakuiona haja ya kuendelea kupoteza muda. Akafanya maandalizi mepesi na kutwaa kibegi chake.
Akaufunga mlango na kutoweka kuelekea barabarani ambapo angeweza kupata pikipiki ya kumfikisha nyumbani kwa mama mkwe wake.
Hakupoteza muda sana barabarani kabla pikipiki haijapita, akapunga mkono nayo ikasimama. Akakwea huku akitoa maelekezo ya wapi alipokuwa anaelekea… akafanya malipo kabisa.
Baada ya dakika arobaini na tano alikuwa Kinondoni jirani kabisa na nyumba aliyokuwa akiishi mama mkwe wake. Utulivu uliokuwa eneo lile ulimshangaza na kumfanya afikirie kuwa yawezekana kuwa hapakuwa na umeme ama la kuna tatizo jingine jipya. Haikuwa kawaida hata kidogo katika eneo lile kuwa na utulivu mkubwa kiasi kile.
Hakutaka kujishughulisha na hisia zake binafsi bali aliamua kuufuata ukweli, na hapakuwa na namna nyingine zaidi ya kuonana na mama mkwe wake.
Aligonga mlango mara mbili, ukafunguliwa na mtoto mdogo ambaye alizoea kuitana naye kwa jina la ‘anko’.
“Bibi yupo?” alimuuliza moja kwa moja akimaanisha mama mkwe wake.
“Aliondoka na shangazi tangu jana….. na hawajarudi. Ila shangazi amerudi halafu ameondoka amesema anaenda polisi…” alijibu yule mtoto huku akijifinyanga macho yake kupambana na usingizi.
“Polisi? Kuna nini kwani anko….au…au ngoja….” Alijiumauma Sam akigundua ameuliza swali kwa mtoto ambaye hawezi kumjibu kiufasaha.
Akajongea nyumba ya pili akagonga mlango mara kadhaa, mlango ukafunguliwa na mama mtu mzima ambaye Sam alimfahamu pia. Hakuonekana aliyetoka kulala, manukato makali yalizisabahi pua za Sam
“Shkamoo mama mkwe…..” alimsalimia na kumwita jina walilozoeana naye… yule mama akabaki katika bumbuwazi kwa sekunde kadhaa kabla ya kuijibu ile salamu na kisha kuzungumza jambo ambalo lilishtua akili ya Sam.
“Bora hata angeugua tujue moja…… kweli mama Tina anakufa hata Tina hajajulikana alipo jamani…Mungu weee!! Mbona majanga mfululizo haya anatupatia waja wake sisi…..”
Sam alitaka kuuliza kitu palepale lakini mdomo ukawa mzito kabisa kufunguka.
Akabaki kukodoa macho yake akimtazama yule mwanamke mnene aliyesimama mlangoni.
“Sam!” yule mama alimuita. Na hapo akili ya Sam ikarejea katika ufahamu wa kawaida tena!!
“umesema mama amekufa?” Sam aliuliza kwa utulivu.
“He! Mi nikajua wamekupigia simu……”
Sam hakuweza kuhimili shinikizo lililomkumba ghafla. Akajikuta anaanguka chini na kisha akatulia tuli.
Yule mama akapiga mayowe ya kuomba msaada!!
Lakini kabla hajapiga kelele zaidi alinyamazishwa na wanaume wawili waliokuwa wameshika silaha za moto mikononi mwao.
Kila mmoja akiwa na bunduki yake!
Yule mama akatulia kimya huku akitetemeka!!
Ilikuwa ni kitendo cha sekunde kadhaa, wanaume wale wenye miili iliyojengeka kimazoezi walimwinua Sam na kisha wakatokomea naye kuelekea walipopajua wao.
Wanaume hawa ni walewale waliokuwa ndani ya chumba cha Sam usiku ule!! Wakikitafuta kitu ambacho hawana uhakika kama Sam anaweza kuwanacho ama hana……
Wakikitafuta kitu wasichokijua!
Utata!!!

*****

Asubuhi iling’ara katika namna ya kipekee!!

MAGAZETI ya udaku nay ale yasiyokuwa na udakju yalibebwa na vichwa vikubwa vya habari, huku kila gazeti likiwa na picha ya marehemu Steven Marashi.
Kila gazeti lilijaribu kuipamba habari hii aidha kidaku zaidi ama kwa utafiti hafifu, machache sana yaliweza kuelezea kiuyakinifu!!
Kama ingekuwepo takwimu ya jinsi magazeti yanavyouzika kwa siku moja basi hii ilikuwa asubuhi ya kukumbukwa kwa muda mrefu sana ikiipiku ile siku ambayo hayati baba wa Taifa alipoaga dunia.
Hata wale wavivu wa kusoma na wao walinunua magazeti huku kila mmoja akionekana kuupokea msiba ule katika namna ya msiba wa kitaifa.
Naam! Msiba wa kitaifa, Steven Marashi alijulikana kwa taifa zima.

Si kila mtanzania aliyeweza kuyasoma magazeti haya mapema ama kuisikiliza taarifa hiyo gazetini. Kuna wale ambao hawakuisoma kwa sababu walikuwa wamelala.
Mmoja wao alikuwa ni Samwel Mbaule ‘Sam’. Huyu alikuwa amelala usingizi nasaba ya kifo wakati wale jamaa wawili wakakamavu wakipitia magazeti lukuki waliyoyanunua.
“Shit! Ona hawa wajinga wanasema Lili nd’o amemuua kwa sababu za kishirikina….” Jamaa mmoja alilalamika huku akibamiza kiti upande wa nyuma wa kiti kilichokuwa mbele yake.
Mwenzake alicheka kabla hajamsomea na yeye alichokiona, “kuna hawa wapuuzi wameandika tena kuhusu Lili………oooh! My God!! Hii picha wameitoa wapi sasa?” alihamanika ghafla baada ya kukutana na picha.
Steven Marashi akiwa amekumbatiana na Lulu kimahaba…..
“KUMBE LILI ALIKUWA SHEMEJI NA WIFI WA TAIFA!”
Kichwa cha habari kilikejeli!!
Upesi baada ya kuiona picha ile walinyanyua simu na kupiga namba ambayo ilipokelewa katika kile chumba cha siri ambacho kipo mahali flani nchini Tanzania.
Aliyepokea taarifa ile alitweta kwa hofu, akakosa kauli akalazimika kukata simu bila kutoa muafaka wa nini kifanyike.
Simu yake iliita tena, akaitazama na kupokea. Alikuwa ni mtu yuleyule.
“Mkuu kuna kila dalili kuwa kuna kiumbe yupo hai na anafahamu siri nyingi sana za marehemu. Na kama akiendelea kuwa hai basi atatufikisha katika hatua mbaya sana ambayo hatutakiwi kufika…..”
“Atafutwe mara moja na ninamuhitaji ndani ya siku mbili, nasema namuhitaji kabla hatujaruhusu mwili wa Steve kuingizwa kaburini. Sipo tayari tudhalilike makaburini, ni heri tetesi za magazetini na pale msibani kuliko fedheha msibani….” Sauti kutoka upande wa pili ilizungumza kiamri na kisha simu ikakatwa bila kupokea majibu yoyote kutoka upande wa pili.
Jamaa alipokata simu ile, alimtazama Sam aliyekuwa amepoteza fahamu, akajiuliza wana haja gani naye mtu yule ambaye hakutakiwa kuuwawa kwa namna yoyote kabla hajawapa kitu wasichokitambua. Alipiga kite cha ghadhabu kisha akazungumza maneno machache kwa sauti ya chini kabla hajamnasa kofi kali Sam asiyejitambua. Akamtukania mama yake mzazi na matusi mengine kedekede!
Ni kama alikuwa anajitukana mwenyewe! Sam hakusikia lolote.

***
 
KISA 6

TATIZO moja kubwa ambalo huwagharimu wanawake pindi wawapo na ghadhabu ni kuamini kuwa kila kitu wanachofanya wanakuwa sahihi. Na wakiwa katika katika hali hii mara nyingi huwa wakubwa wa siri na wavivu wa kushirikisha mtu juu ya mambo yao. Labda mwanamke mwenzake tena walioshibana.
Ni hiki mkilimsibu mama Tina, akiwa kama mwanamke mwingine tena mwenye mapenzi ya dhati kwa mtoto wake aliyekuwa hajulikani alipo baada ya kukamatwa na polisi.
Alipokea simu ileile ambayo Sam alidai kuwa yawezekana ni Tina atakuwanayo, ajabu hakuzungumza Tina walizungumza wanaume na kumwelekeza mama Tina mahali ambapo Tina yupo, aende na pesa kwa ajili ya kumchukua.
Pesa yenyewe ya kukodi teksi tu! Ajabu.
Bila kuishirikisha akili yake vyema, mama Tina akamshirikisha mdogo wake wa kuishi naye, wakaondoka huku ndani ya teksi wakimnanga Sam kadri walivyoweza, wakafikia hatua ya kumwita mwanaume suruali asiyemjali mchumba wake.
Walipokelewa eneo husika maeneo ya Koko, majira ya usiku.. bado watu walikuwepo katika hoteli wakipata vinywaji na chakula.
Mama Tina akaombwa aingie peke yake ndani na yule mwanamke mwingine akabaki kumsubiri nje!! Akiahidiwa kuwa atarejea na Tina baada ya dakika chache, mama Tina akaingia kichwakichwa!!
Muda mchache ukawa muda mwingi, saa zima likazaa saa la pili na la tatu. Baridi likamzidia yule mwanamke na kujikuta akizidiwa na uvumilivu, akaamua kupiga simu….
Simu ya mama Tina ilikuwa inaita tu bila kupokelewa. Aliendelea kupiga bila mafanikio. Hatimaye akaamua kuingia ndani ya hoteli kumtafuta.
Bado hakufanikiwa kumuona, hadi pale aliposikia kelele za kuhamasishana juu ya jambo Fulani la hatari. Akavutika kwenda kupoteza muda katika tukio hilo wakati huo akimsubiri mama Tina.
Kama alidhani anaenda kupoteza muda haikuwa hivyo…..
Alikuwa anaenda kushuhudia mwili wa mama Tina ukiwa hauna uhai wowote ule.
Mwili ulikuwa sehemu ileile ambayo Sam aliagizwa kwenda kuchukua kadi ya simu na mtu ambaye aliamini kuwa alikuwa ni teja.
Utata ukaendelea!!!




UKUNGU uliyatawala macho yake na kumfanya aone maumbo kadhaa yakiambaa katika ukungu ule katika namna ya kukera, alijaribu kuyapikicha macho yake na hapo akasikia miungurumo ya ajabu ajabu.
Ule ukungu akajiaminisha kuwa ni mawingu na ile miungurumo basi akaona kuna kila dalili ya mvua.
Mvua inataka kunyesha halafu nimekaa nje? Alijiuliza katika nafsi yake, kisha akaulazimisha mwili wake uweze kunyayuka aweze kuondoka eneo lile kujiepusha na mvua kubwa iliyokuwa inataka kumwagika.
“Pumzika Sam, subiri usisimame!” sauti zilizokuwa za miungurumo zikazungumza na akasikia vyema.
“Mungu wangu? Mawingu yameniita jina langu….au malaika?” alijiuliza lakini safari hii kwa sauti ya kukwaruza kidogo. Wakati huohuo akiendelea kunyanyuka….
Mara akaguswa begani, akashtushwa na kitendo kile akajipapasa begani mara akakutana na kiganja cha mkono.
Sam akapagawa na kuanza kupiga kelele!!
Ni katika patashika hiyo alijikuta akiona vyema mbele na wala hapakuwa na mawingu bali umati wa watu ulikuwa umemzunguka.
Sura kadhaa alikuwa akizitambua lakini kuna sura moja aliitambua zaidi.
“Sam mwanangu ulipoteza fahamu hukoo mjini, kuna wasamaria wema wamekuleta hapa….. pole sana” ilikuwa sauti ya Mama Lao!!
“Nini? Nilianguka, hapana hakuna kitu kama hicho mama…hakuna kabisa nasema sijaanguka mimi…” alipinga Sam huku akijisikia fadhaa kuwa amekaa chini huku amezingirwa na umati.
“Dah! Maskini wee! Sijui hata kama ataelewa huyu….” Kijana mwingine alilalamika pembeni huku akimwonea huruma Sam.
Sam aliamua kuituliza akili yake bila kusema lolote, akayafumba macho yake na kujilazimisha kukumbuka mara ya mwisho alikuwa wapi kabla hajarejeshwa nyumbani kwake bila kujitambua. Akili ikafanya kazi yake ipasavyo, akakumbuka kila kitu.
“Nooo! Noooo! Sikuzimia, walinichoma na kitu kama pini hivi eheee! Nimekumbuka ni kitu kama sindano, hapa begani, mh! Hivi ilikuwa begani ama shingoni….. ni..be….aah! ilikuwa shingoni….. wajinga sana wale jamaa wameniteka wale, hata siwajui maskini nimewakosea nini mimi eeh! Nimewakosea nini sasa….wamemchukua Tina wangu….na mama na mama wame…. Whaaaat! Mama amekufa?” Sam alihangaika huku na kule akitoa maelezo ambayo yaliwathibitishia watu kiuhakika kabisa kuwa mtu aliyepoteza fahamu, akirejea katika fikra zake za awali huwa anaweweseka.
Wakadhani kuwa hata Sam alikuwa katika kuweweseka!!
“Anko Sam, ingia ndani upumzike, haupo sawa?”
“Nini? Sipo sawa, sipo sawa natambua kuwa huyu ni mama lao, mama anayelisha mtaa mzima kwa tusiokuwa na familia, huyu hapa mama Khadija na Khadija wake anasoma kidato cha kwanza hapo Makongo, huyu naye sio baba Hamadi, na huyo Hamadi wake si ndiyo yule anayetaka kuwa mtangazaji…. Mnataka nitaje mtaa mzima nd’o mfahamu kuwa nipo katika timamu zangu…..sijachanganyikiwa narudia kusema kuwa nilitekwa baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika bega langu la kuume, na wakati yanatokea haya nilikuwa nimepokea taarifa kuwa mama mkwe wangu amepoteza uhai. Naitwa Samwel Mbaule na nipo katika akili yangu….naomba niaminike!!” Sam aling’aka kwa ghadhabu na kwa kitendo chake cha kutambua watu waliokuwa mbele yake kiliwafanya wote waanze kuamini kile alichokuwa akikisema.
“Simu yako hii hapa… hao wasamaria wema walisema tukupatie ukizinduka…” jirani mmoja alizungumza huku akimkabidhi Sam ile simu.
Sam alicheka kwa kujilazimisha, cheko la karaha….
“Eti wasamaria wema, mabaradhuli wakubwa wale wananionea bure tu…wananionea tu…” alilalama huku akiichukua ile simu, akasimama na kuwashukuru wote waliompokea akiwa amepoteza fahamu, kisha akafungua mlango wake na kuingia ndani ya chumba asichokuwa na imani nacho.
“Mmeweka tena madawa ya kulevya nyie paka shume waonevu wa kukwapua samaki mdogo wa mama mjane maskini…wekeni tena nitavuta na kuzimia tena. Naona mna lengo la kunisababishia niwe na kifafa…endeleeni lakini Mungu aliye hai ananipigania…. Na wakati unakuja hamtaweza kunizimisha tena bastard!!” alikaripia Sam huku akiamini kuwa ujumbe ulikuwa unafika.

*****

Baada ya kujimwagia maji na kuuweka mwili wake katika uchangamfu tena, Sam aliitwaa simu aliyokuwanayo, lengo lake likiwa moja tu. Wazo ambalo alilipata akiwa bafuni, kuwa ukitambua kundi fulani linakushinda basi ungana nao ili wote muwe washindi!
Sam alijiuliza maswali mengi na kuamini kuwa lile kundi linalomwandama lilikuwa likishabihiana na kifo cha Steve Marashi. Hivyo wakimtambua muuaji wa Steve iwe isiwe wataachana naye na hata Tina atarejeshwa mikononi mwake.
“Nyie majamaa…..” alianza kuzungumza kwa sauti akiamini kuwa mle ndani kuna vinasa sauti na lazima watamsikia tu….
“Nyie majamaa mnadhani namjua muuaji ama mimi naweza kumuua rafiki yangu Steve….mnanikosea sana heshima kwa hilo….mnanitesea bure Tina wangu na mama mkwe wangu mmemuua amakweli mmeamua kunionea….sasa sikilizeni humu katika simu kuna mtu alijitambulisha kama muuaji wa Steve na hadi sasa sijajua ni nani…jina lake lilihifadhiwa kwa herufi tatu ‘SLM’….Sikieni sasa hii ni simu ya mchumba wangu….mimi nampigia huyu SLM ili mmsikie wenyewe ni kwanini anasema kuwa anasingiziwa kumuua Steve. Msikie kama atanitaja mimi sasa….” Sam alisita. Akaichukua simu na kuanza kupekua jina lililohifadhiwa kwa herufi zile ambazo zilikuwa zimenasa katika kichwa chake kutokana na zile meseji kadhaa alizotumiwa na kuzifuta.
Sam hakuamini macho yake alipotafuta namba zile pasi na kufanikiwa…alitafuta kwa jitihada zote lakini bado hakufanikiwa!
Jina SLM halikuwepo tena katika simu ile!
Sam akayahisi macho yake yakichonyota, akaamini kuwa wale watekaji walikuwa wanazidi kumwona muongo.
Hatimaye akaanza kulia kama mtoto mdogo!!
“Mmelifuta jina…ni nyie mmelifuta washenzi wakubwa nyie.. mnamjua aliyemuua rafiki yangu…mnamjua na bado mnaniandama…ok! Njooni mniue na mimi..mumuue na Tina..mkamuue kila mtu, wanadhambi wakubwa nyie…” Sam akaporomosha maneno makali makali, kisha akajirusha kitandani kwake.
Hakika alikuwa amepagawa!
Alitamani kulala lakini usingizi ukagoma….
Ili kujinusuru katika utata huu, Sam akaamua kutafuta chcohote cha kuweza kumfariji na kumsahaulisha. Alikuwa amepanga kuwa jioni aelekee katika msiba wa mama mkwe wake huku akijiahidi pia kwenda polisi kupata taarifa juu ya kifo hicho.
Katika kupepesa macho akakutana na kikaratasi cha kuhifadhia santuri ‘CD’… akakitazama kile kikaratasi na hapo akakumbuka kuwa aliyempatia alikuwa ni marehemu Steven Marashi. Alimpatia santuri ile siku moja walipokutana akamweleza kuwa ilikuwa ni filamu yake mpya ambayo anatarajia kuitoa.
Sam akawasha runinga yake, akatia ile santuri ili aweze kujiliwaza na kumuenzi rafiki yake kipenzi.
Kama kawaida alitegemea kukutana na matangazo kadhaa ya filamu kabla ya filamu yenyewe kuanza. Lakini ajabu haya yote yalikuja lakini sio katika mfumo na nembo iliyozoeleka kuwa inasambaza kazi zake Marashi.
“Ah! Alihamia kampuni mpya ama…. Mbona hata siijui hii… Black Entartainment… ya wapi hii….” Alijiuliza Sam….
Mara akatokea Lili.
“Wacha wee alicheza na Lili, si alikuwa anazuga kuwa hataki kucheza naye filamu yoyote….nd’o maana akanipa kama Sapraizi eeh” akakaa vyema aweze kuitazama vyema ile filamu.
Mara ghafla mshangao ukahamia katika mshtuko, Lili alikuwa amevaa katika namna ambayo ni sawasawa na kuwa uchi tu.
“Nd’o maana haya ma Bongo muvi yao siyapendi….sasa nd’o kuvaa gani huku si uchi kabisa yupo?” alihamanika Sam…
Lakini hamaniko hilo halikudumu sana , zaidi likahamia katika kustaajabu. Lili akayageuza makalio yake kuelekea katika kamera na mara likatokea jambo ambalo lilimfanya sam ajikute anaziba macho yake.
Lili alibetua kitufe fulani katika nguo yake ambayo ilikuwa ni sawa tu na mkaa uchi. Lakini baada ya kubetua akawa uchi wa mnyama.
“Mama yangu weee!!....huyu si Lili huyu jamani….” Alijiuliza mwenyewe kisha kaangalia kushoto na kulia kama kuna mtu ambaye anaweza kumjibu.
Hakuwepo!!
Na alipoyarudisha macho yake kwenye runinga akamwona mwanaume akiwa uchi.
Hapa ukawa mwisho wa labda labda sasa ukawa ni uhakika.
Ile ilikuwa ni video ya ngono, muigizaji akiwa ni Lili wa Tanzania, lakini ile sura ya mwanaume haikuwa maarufu na Sam hakumtambua mara moja.
“Ni kitu gani hiki ulinipa Steve Marashi…ulimaanisha nini wewe eeh! Steve ulimaanisha nini, hebu kama haujafa kweli njoo uniambie nini ilikuwa maana yako we rafiki!! Njoo Steve…. Au…aaah! Hapana…” Sam alighafirika kweli.
Lakini hapohapo akasikia sauti ikiwaamuru Lili na mwenzake kulianza tendo.
“Stand by……..ACTION!!!” iliamrisha sauti ile ya kiume.
Kijasho kikaanza kumtoka Sam, masikio yake yalikuwa yameiskia sauti ya STEVEM MARASHI ikitoa amri!!
Amri ya Lili kuanza kucheza ile filamu ya ngono.
Kilichotokea baada ya hapo… Sam alilazimika kuzima runinga yake mara moja!!
Alikuwa amepagawa.

Nafsi moja ilimtuma kuufikisha mkanda ule polisi ikiwa ni kigezo namba moja cha wao kuanza upelelezi juu ya kifo cha Steve Marashi, lakini nafsi nyingine ikamsihi kuwa mkanda ule awapatie wale watu wabaya wanaomsumbua kila kukicha huku wakimmiliki Tina wake.
Hakujua ni wapi angewapata lakini aliamini kuwa wapo karibu naye na wanamsikia!!
Kabla hajapitisha maamuzi yoyote yale, mlango wa sebuleni uligongwa…. Upesi akakimbilia deki na kuitoa mahali ilipokuwa, akaificha chini ya uvungu wa kitanda.
Alipoufungua mlango alikutana ana kwa ana na mwanamke wa kazi, mcheshi na anayemzoea mtu kwa sekunde kadhaa tu.
Alikuwa ni MAMA LAO!!
Hakuwa na tabasamu usoni na ni kama kuna mambo mazito alikuwa ameyabeba na ilikuwa ni lazima ayatue.
“Karibu…” Sam alimkaribisha huku akiachia nafasi mlangoni mama yule akapenya. Sam akaufunga mlango na kisha kumkaribisha mama lao katika mojawapo ya sofa pale sebuleni.
Baada ya salamu na pole za hapa na pale.
Mama lao akamueleza Sam jambo lililobadili kila kitu katika kichwa chake huku likimwacha katika namna ya kukosa maamuzi kabisa!!
Huo ukawa mwendelezo wa utata!!!
 
KISA CHA 7

Kabla hajapitisha maamuzi yoyote yale, mlango wa sebuleni uligongwa…. Upesi akakimbilia deki na kuitoa mahali ilipokuwa, akaificha chini ya uvungu wa kabati huku akiwa anatetemeka sana na jasho likizidi kumtiririka.
Kisha upesi akachukua kisu kidogo kilichokuwa mezani akakizamisha mfukoni, ili kama kuna hatari yoyote mbele yake akabiliane nayo.

Alipoufungua mlango alikutana ana kwa ana na mwanamke wa kazi, mcheshi na anayemzoea mtu kwa sekunde kadhaa tu baada ya kukutana kwao.
Alikuwa ni MAMA LAO!!
Hakuwa na tabasamu usoni na ni kama kuna mambo mazito alikuwa ameyabeba na ilikuwa ni lazima ayatue.
“Karibu…” Sam alimkaribisha huku akiachia nafasi mlangoni mama yule akapenya. Sam akaufunga mlango na kisha kumkaribisha mama lao katika mojawapo ya sofa pale sebuleni huku akilazimisha tabasamu hafifu midomoni.
Baada ya salamu na pole za hapa na pale. Mama lao akamueleza Sam jambo lililobadili kila kitu katika kichwa chake huku likimwacha katika namna ya kukosa maamuzi kabisa!!
Huo ukawa mwendelezo wa utata!!!

****

Baada ya kudumu kwa dakika takribani dakika mbili bila kuzungumza kilichomleta, hatimaye alishusha pumzi na kumweleza Sam madhumuni ya ujio ule.
“Vipi mama Lao! Na wewe ni mmoja kati ya watu wanaoamini kuwa nimerukwa akili? Umekuja kuhakikisha” Sam aliuliza katika namna ya kusanifu.
“Nilitaka kuamini awali….” Alijibu mama lao kisha akaketi vyema na kumtazama Sam moja kwa moja machoni.
“Ikawaje hata usiamini tena kama nimerukwa na akili mama…”
“Kwa sababu nahisi ni mimi ambaye nimerukwa akili….” Alijibu kwa kifupi mama lao kisha akamalizia, “Nilikutana na watekaji kabla ya tukio”.
Sam akajitoa katika kuegemea kochi na sasa akawa kama nusu anataka kusimama na nusu anataka kuendelea kukaa.
“Nini…unamaanisha nini mama lao..”
“Walifika katika mgahawa wangu kununua supu, nilizikariri sura zao kwa sababu walikuwa wanaongea kinyakyusa na walikuwa wakizungumzia jambo ambalo nimeupata mwanga wake sasa baada ya kuhakikisha kuwa haujarukwa na akili….. walikuwa wakikuzungumzia wewe na kwa mbali kama walimzungumzia marehemu Steven Marashi japokuwa hawakumtaja jina lake moja kwa moja….”
“Sijakuelewa mama, wewe uliwaelewaje wakati wewe mzaramo?”
“Wengi sana ukiwamo na wewe mnatambua hivyo lakini mimi ni mnyakyusa, nadhani zaidi ya mama lao hata jina langu haulifahamu naitwa Sekela Ambindwile, lakini mama yangu alizoea kuniita Atuganile. Mbeya wakanifupisha na kuniita Atu….. naitwa Atu. Lakini endelea kuamini kuwa mimi ni mzaramo, napenda iwe hivyo kwa sababu zangu binafsi….” Mama lao alivuta pumzi kisha akazishusha na kuendelea.
“Hivyo, nilielewa kila kitu…. Kumbukumbu zimenikaa sawa baada ya kuwaona leo wakirejea na mwili wako na kudai kuwa wao ni wasamaria wema wamekuokota mbali. Kilichonivuta zaidi ni kauli yao tata kuwa hata eneo lile ni mara yao ya kwanza kufika. Wameelekezwa tu nyumbani kwako kwa sababu wewe unafahamika……. Mashaka yangu yakaanzia hapo.” Mama lao alijiweka sawa, Sam naye akazidisha utulivu zaidi, hakuamini alichokuwa anakisikia.
“Sasa wanataka nini kwangu eeh! Ni nini wanataka… nieleze mama lao nieleze niwapatie”
“Siwezi kusema kuwa nafahamu moja kwa moja lakini kwa maneno niliyoyasikia, nahisi hata wao hawana uhakika kama wewe ni mtu sahihi kwao…. Wanachofanya ni kubashiri tu……na inaonekana wameagizwa” alijibu mama lao. Sam akawa mkimya tu akipokea maneno yale mapya na mazito.
“Kwani wanakudai kitu gani Sam…”
“Sura zao tu sijui, nitajua vipi wanachotaka kwangu mama” Sam alijibu katika namna ya kughafirika. Mama lao akaligundua hilo.
“Lakini ukiachana na hayo ya kutokuwa na uhakika na hicho walichokuwa wakihisia kwako….. wale jamaa ni watu wa serikalini ama la wanafahamiana na mtu serikalini, kupitia mazungumzo yao nilisikia wakimtaja waziri wa ulinzi na waziri mkuu….. bila shaka jambo hili sio dogo.”
“Whaat! Waziri mkuu…. Mungu wee ni kitu gani sasa hiki…”
“Usirukwe na akili Sam, tulia sana kuna jambo hapa. Hivi wewe unaamini kuwa Steve amekufa hivihivi??” mama lao alimuuliza Sam ambaye alikuwa ameanza kuizoea ile hali baada ya taarifa.
“Hivi unaweza kuamini kuwa hadi sasa ninavyozungumza na wewe sijui rafiki yangu amekufa kifo cha namna gani?”
Mama lao alishangaa kwanza kabla ya kumweleza Sam kuwa Steven Marashi anasemekana ameuwawa na sio kuwa tu amekufa kikawaida. Mama lao akamweleza zaidi kwa ushahidi wa magazetini kuwa Steven Marashi alikutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni ambayo inasemekana alikuwa amelala na mpenzi wake ambaye inasemekana ametoweka, awali ikasemekana huyu msichana alikuwa ni Lili, mara vyombo vya usalama vikakanusha na kusema hadi sasa haifahamiki huyo mwanamke alikuwa ni nani.
Sam akaduwaa na kuzidi kuuona utata waziwazi.
“Lili yeye amesemaje juu ya shutuma hizi?”
“Lili hajasema lolote lile, simu yake haipatikani…. Nd’o magazeti yanavyosema. Sijui tu hiyo kesho itakuwaje…”
“Kesho kuna nini?”
“Nd’o anazikwa marehemu….. na raia wanataka kupata mustakabali juu ya kifo hicho cha ghafla cha kipenzi chao. Aliyehusika aadabishwe….” Mama lao alijibu huku akionekana wazi kuingoja siku inayofuata kwa hamu.
Waliendelea kuzungumza mengi juu ya utata huo.
Hatimaye wakaagana kwa makubaliano ya kukutana msibani siku inayofuata!!
Amakweli hakuna aijuaye kesho, hata yule mtunzi wa kalenda!!
Haikuwa nyepesi kama walivyopanga!!

*****

KIKAO kizito kilikuwa kimehitishwa katika ile nyumba ya siri mahali fulani nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa amewaka kwa hasira kali, kitendo cha jopo lake kushindwa kuambulia lolote lile kulimfanya aone ni uzembe wa hali ya juu japokuwa hata yeye mwenyewe hakujua ni kitu gani wanakitafuta kutoka kwa Sam.
Hiyo ilikuwa ni siku ambayo vijana wake wa kazi walikuwa wameleta mrejesho juu ya walichokuwa wakifuatilia. Na ilikuwa ni siku hiyo ambayo walikuwa wametoa vinasa sauti na kila kitu kilichokuwa kinahusiana na upelelezi wao ndani ya nyumba ya Sam.
Ni kama walivitoa wakati usiokuwa muafaka, hawakufanikiwa kutambua iwapo Sam alipata mkanda wa picha za ngono, na pia hawakuweza kuyanasa maongezi ya mama lao na Sam. Huenda hayo yangeweza kuwaletea mwangaza mkubwa sana na hatimaye na wao wakijue kile wanachokitafuta.
Bahati mbaya hata wao hawakuijua kesho yao!!
Baada ya mwenyekiti wa kikao kile muhimu cha siri kung’aka sana, mwishowe aliwapa nafasi ya mwisho ya kufanya wawezavyo, siku iliyofuata yaani siku ya maziko, wafuatilie hatua kwa hatua kuanzia mwili unavyotolewa mochwari hadi mipangilio ya kuaga na hatimaye kuzika waangalie iwapo wataambulia lolote la kuwasaidia kujua wasichokijua.
Wakaagana huku wakiingoja siku inayofuata, vijana wawili wa kinyakyusa wakalikamata jukumu lile katika mlengo mwingine, safari hii wakataka kubadili mbinu zao.

****
ULIKUWA ni msafara mkubwa sana kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanzania. Wananchi walijaa barabarani, wengine wakiushangaa msafara wa kutokea Muhimbili na wengine wakiwa katika sura za majonzi kutokana na tukio la kumpoteza muigizaji wao mahiri.
Barabara ya Bagamoyo ilifungwa kwa muda ili kuruhusu magari yanayokwenda tu Magomeni na kuyazuia yale yanayoelekea Kariakoo yasifanye safari zake.
Ulinzi uliimarishwa pande zote za barabara, vilio vilisikika huku na kule na miale ya kamera ikiwaka bila kupokezana. Kila mmoja alitaka kupata picha ya tukio lile.
Ama kwa hakika lilikuwa tukio la kuteka fikra za yeyote yule!!
Msafara ulienda kwa mwendo wa taratibu huku gari kubwa la muziki likipiga nyimbo za kuwakumbusha wanadamu juu ya kujiweka tayari maana hawaijui siku wala saa.
Katika gari ndogo aina ya Corola, baba wa marehemu akiwa ameyaziba macho yake na miwani alikuwa katika tafakari nzito juu ya wimbi zito lililotanda katika kifo cha mwanaye. Alimini kabisa kuwa hakikuwa kifo cha kawaida bali cha kupangwa, na kuna sababu kadhaa alihisi zinaweza kuwa chanzo cha kifo kile.
Kubwa zaidi aliamini tangu siku ya kwanza ni kuwa kuna hila zimefanyika ili kuondoa uhai wa mwanaye.
Alitamani sana kuwa mkewe angekuwa muelewa tangu awali na kumzuia mtoto wao katika mambo kadhaa waliyodhani anaweza kuwa anajihusisha nayo, lakini mkewe akawa upande wa mtoto wake, akamuunga mkono kwa kila jambo hata yale ambayo yalionekana kuwa ya hatari kabisa.
“Yaani mama Steve ni mbishi huyu mwanamke!! Ona sasa mtoto amekufa anajifanya kugalagala na kuzimia kila mara anawasumbua tu watu, nilimwambia kabisa mapema kuwa tumkanye Steve….” Alilalama mzee Marashi kimyakimya huku akiwa amekamata gazeti mkononi mwake na asilisome.
Alipolitazama lile gazeti na kukutana na picha ya Lili alikumbuka mengi sana, akamkumbuka msichana yule na mengi waliyokuwa wamezungumza awali na hapo akawa amepata wazo la awali kabisa juu ya kifo cha mtoto wake.
Lili lazima kuna mambo kadhaa anayafahamu tu!!
Baada ya maziko nitamtafuta…..
Baada ya kauli ile alitoa miwani yake na kujifuta machozi kiasi machoni pake. Alipotaka kurejesha miwani machoni alishangaa kumuona dereva akiwa anahangaika na usukani, na hapo akasikia makelele mengi kutokea nje. Ile anageuka kutazama ni kitu gani kinatokea katika msafara wao akakutana na mpasuko mkubwa wa kioo ukiambatana na mlio mkubwa sana. Hakuweza kusikia jambo lolote tena.

*****

Edson Mayagi ‘Ninja’, alikuwa akimalizia kipande cha sigara yake wakati macho yake yalipokutana na namba za gari ambazo alielezwa kuwa gari mbili nyuma yake ndipo alipanda baba mzazi wa Steven Marashi. Upesi akakitupa kile kipande cha sigara, akajiweka tayari katika kutimiza alichokuwa ameagizwa kwa malipo makubwa.
Mapigo yake ya moyo yalikuwa juu sana, hakuamini kama ataweza kutoka salama ama ndo atakuwa amefanya kwa ajili ya familia yake ambayo ilikuwa imejazwa pesa nyingi sana kwa ajili yake. Hawakujua ni pesa kwa ajili gani bali walijazwa pesa tu!!
Ni Edson pekee aliyekuwa akilitambua hilo.
Palepale akafanya maombi kwa Mungu wake aweze kufanikisha alichopanga kukifanhya.
Na hapo akaliachia ghafla lori lililokuwa katika mteremko wa kuelekea Kariakoo, moja kwa moja likawa linaelekea katika gari aliyopanda mzee Marashi. Baada ya kuhakikisha kuwa lazima lori lile litajikita katika gari alilopanda Marashi, upesi akaruka na kujichanganya katika umati uliokuwa umetaharuki.
Amakweli Mungu wetu ni wa ajabu sana…. Sala za Edson zikasikilizwa akatoka salama, na mzee Marashi akaupoteza uhai palepale.
Kizaazaa kikaendelea!!

***

KIFO cha mzee Marashi kilizagaa upesi sana hata kabla mwili wa mwanaye haujaingizwa katika nyumba ya milele…… pande kadhaa zikakijadili kifo hiki katika namna wazijuazo. Huku wakisahau kabisa juu ya vifo vya raia wema wengine ndani ya ile gari.
Lakini tabasamu zito kabisa lilikuwa katika midomo ya mzee Matata, tajiri maarufu kabisa nchini Tanzania mwenye asili ya kiasia lakini aliyekifahamu Kiswahili vyema na aliyeijua Tanzania.
Tabasamu lile lilikuwa la mafanikio makubwa mno kutokana na kunyamazishwa kwa mzee Marashi kabla hajaropoka lolote lile.
Amani ikatawala moyo wake!!

Kwa upande wa wale vijana wawili wa kinyakyusa, walipagawa kutokana na tukio lile ambalo halikuhitaji jicho la tatu kutambua kuwa limepangwa maksudi kabisa kwa nia flani.
Nia gani? Hilo likawa swali zito kabisa ambalo lilizua utata mpya!!

UPANDE wa tatu ulikuwa na faida ya ziada, huyu alikuwa ni Sam. Ambaye alikuwa amejichanganya pia katika umati akifuatilia kwa ukaribu zaidi tukio hili ili aweze kupata mwangaza wa kitu gani kinachotokea katika ukungu huu.
Kama ilivyo kawaida ya waandishi, Sam alikuwa na kamera yake akirekodi vitu kadhaa bila kujua ni kwa nini alikuwa anarekodi.
Ni kawaida ya waandishi wa habari!!
Kamera ya sam ilivutika kumrekodi kijana ambaye alikuwa akivuta sigara kwa fujo, mara aimalize mara asiimalize, mara aizime mara aiwashe.
Sam akatambua kuwa mtu yule alikuwa na hofu kuu…..
Ana hofu ya nini sasa? Kuchelewa anapoenda, kukamatwa na trafiki ama? Sam alijiuliza peke yake huku akipendezwa kupata walau picha mbili tatu za yule bwana mfupi mwenye kichwa kikubwa kilichoongezewa ukubwa na nywele zake kichwani.
Macho yake hayakubanduka katika sura ya yule bwana, hata alipopanda garini alimshuhudia….
Awali alikuwa akipiga picha za mnato lakini wakati anabadili na kuamua kurekodi picha zinazotembea ndipo alipomshuhudia yule kijana akiliachia lori lake, Sam akazidisha umakini katika kamera yake akarekodi kila kitu na nzuri zaidi akainasa picha ya yule kijana akijirusha na kujichanganya kagtika umati wa watu.
Sam akaizima kamera yake na papo hapo akauhitaji msaada wa mtu katika kulifuatilia hili, hakutaka kujihangaisha na ile ajali, alitaka kumpata msababishaji wa ile ajali.
Angemuhitaji nani zaidi wa kuweza kumwelewa zaidi ya mama lao.
Kidogo aache klumshirikisha katika hili kwa kuhofia kuwa mama lao hawezi kuwa na msaada wowote ule. Lakini nafsi nyingine ikamweleza kuwa usikihukumu kitabu kwa kulitazama jalada lake tu…..ni heri kuzama ndani na kusoma kilichomo.
Sam akamvuta mama .lao kando na kumweleza kijuu juu kuhusu alichokiona, akamwelekeza mama lao ageuke nyuma aangalie chini ya mti fulani. Akafanya hivyo na kufanikiwa kumwona yule mtu mfupi mwenye kichwa kikubwa akiwa anavuta sigara na ,kupuliza moshi mwingi hewani.
“Una uhakika…..”
“Asilimia zote na nimemrekodi…”
“Twende…” mama lao akamwambia Sam na kwa mwendo wa kawaida kabisa wakalifikia eneo ambalo yule kijana alikuwa pale Sam alitangulia mbele kabisa na mama lao akabaki kwa mbali. Sam akahisi kuwa mama yule ni muoga kwa kitendo chake kile cha kusimama mbali.
Sam hakujua…na hakumjua mama lao….

Wakati akidhani kuwa ni jambo jepesi kufika na kumhoji yule kijana alikumbana na mshtuko baada ya kijana yule kufyatuka ghafla akitimua mbio baada ya Sam kufanya kosa kubwa kwa kujitambulisha kuwa yeye ni mwandishi wa habari.
Bahati ilikuwa mbaya kwa yule kijana kwani alikimbilia upande ambao mama lao alikuwa ametanda.
Ni huko alikutana na shubiri…..
Sam hakuamini macho yake……..
 
KISA CHA 8

MAMA LAO ni kama alimchezea shere mhanga wake kwa kujifanya kuwa hamtazami na wala hana muda naye hivyo alikuja kwa pupa na alipompita sekunde kadhaa tu upesi Yule mama akafyatuka na kumnasa Ninja mguu wake wa nyuma. Ninja asiyetarajia lile jambo akapepesuka na kisha akatua chini kama mzigo.
Alipojaribu kusimama, Mama lao akawahi kumwamsha vyema kisha akiwa amemkwida shati lake vyema akampa shambulizi la kushtukiza. Akambamiza kichwa chenye uzito wa haja na palepale akapasuka vibaya sana.
Yule bwana akiwa amepagawa alijaribu kujitoa mikononi mwa mama lao lakini haikuwa kwa wepesi kama alivyoweza kudhani.
Mama lao alikuwa imara sana! Akamkata gwala akaanguka chini.
“Wewe ni nani na aliyekutuma ni nani? Jibu mara moja ama napasua makende yako” Mama lao alifoka huku mkono wake ukiwa ukiwa umezikama sehemu za siri za Ninja.
Yule mwanaume hakutegemea kujikuta katika suluba kubwa namna ile tena kutoka kwa mwanamke.
Sam alikuwa amepigwa na bumbuwazi, akili ilikuwa imesimama akishuhudia undava wa yule mwanamke, miguu ilikuwa mizito sana na akili ilikuwa imesimama.
Alikuja kushtushwa na watu ambao walikuwa wakishangilia ugomvi ule na yeye akaanza kupiga hatua kusogea alipokuwa mama lao.
Lakini kabla hajafika likatokea jambo ambalo lilizua kizaazaa kilichoitikisa Magomeni na kufunga barabara kwa muda mrefu sana.
Ukasikika mlio mkali sana wa bunduki, kikasikika kilio cha mama lao. Kisha damu ikatapakaa katika miili miwili iliyokuwa katika ugomvi.
Polisi waliokuwa eneo la ajali walitoa bunduki zao upesi na kuanza kuangaza huku na kule waweze kutambua ni wapi shambulio lile lilitoka. Lakini hawakuambulia kitu chochote…
Sam alipigwa butwaa miguu ikaishiwa nguvu, mwili ukamsisimka alivyotazamana ana kwa ana na lile dimbwi la damu. Huku mama lao na Ninja wakiwa wametulia tuli wakiwa wamekumbatiana.
Kwa jicho la harakaharaka la kibinadamu ungetambua kuwa hawakuwa na chembe ya uhai.
Sam, alitaka kuiruhusu akili yake ipagawe lakini akajionya na kulikumbuka lile angalizo alilopewa na yule bwana ambaye alimuwekea dhamana ya kimaajabu usiku wa manane.
Akakumbuka alielezwa kuwa awe makini!
Sam akajitoa ufahamu na kujifanya hamjui mama lao. Alijisikia vibaya kumsaliti yule mama lakini alitambua kuwa lile halikuwa tukio la kawaida na laiti kama angejiweka mbele lazima angejiingiza matatani, hasahasa akiikumbuka kamera yake ambayo ilikuwa na tukio la bwana Ninja kuunda kwa maksudi kabisa ajali ambayo sasa ilikuwa imeondoka na uhai wa mzee Marashi, baba mzazi wa Steven Marashi.


***

MAJIRA yaa saa mbili usiku simu ya mkononi ilitoa mwanga kumaanisha kuwa kuna ujumbe ama simu inaingia, bwana Robert Massawe, mkaribu mkuu msaidizi wa jeshi la polisi aliitazama Katina namna ya kuvizia kana kwamba akiitazama upesi itazimika.
Hiyo ilikuwa ni simu yake ya dharula sana ambayo walikuwa wakiifahamu watu wachache mno. Ilikuwa kawaida ya bwana huyu ambaye alikuwa na miaka arobaini na tano kuzima simu zake na kutafakari kwa kina kila linapotokea tukio ambalo linatatanisha.
Alikuwa akiiacha wazi simu yake moja tu kwa ajili ya watu maalumu.
“Goddamn! Shit!!” alifoka baada ya kutambua mpigaji wa ile simu. Alijua kuwa mpigaji alikuwa na kawaida ya usumbufu, na usumbufu huu ulikuwa na chanzo chake. Alitamani sana asiipokee simu yake, lakini ilikuwa lazima aipokee.
“Naam! Mheshimiwa sana Matata…” alizungumza bwana Robert kwa nidhamu na sauti ya chini.
“Pole sana nimekusumbua ulikuwa umelala… niwie radhi bwana…” sauti ya mzee Matata ilizungumza na kisha akashusha pumzi kumsikiliza bwana Robbert.
“Usijali mkuu.. nilikuwa sijalala bado.” Alijibu kwa kuchangamka, changamko la kujilazimisha.
“Pole sana kwa matukio mfululizo yanayolitokea jeshi la polisi, hakika mnapitia kipindi kigumu sana katika hili….” Akavuta pumzi kisha akaendelea.
“Ehe! Nambie vipi nasikia leo kuna ajali imetokea na risasi zimerushwa huku watu wakipoteza uhai…”
Kauli hii ilimkera Robert, lakini ilikuwa lazima ajieleze kitu ambacho alijua wazi kabisa kuwa alikuwa anaukiuka utaratibu
wake wa kazi lakini angefanya nini mbele ya mzee Matata, tajiri ambaye analifadhili jeshi la polisi mara kwa mara.
Robert akamueleza mzee Matata kuwa kijana asiyefahamika jina lake amepigwa risasi kifuani na kufa palepale huku yule mwanamke ambaye alikuwa akipambana naye bila kujulikana chanzo akiwa amepoteza fahamu.
Mzee Matata akakata simu bila kuaga.
Ilikuwa kawaida yake!!

KILE kitendo cha mzee Matata kutawala baadhi ya mazingira katika idara mbalimbali serikalini ilimkwaza sana mzee Robert na kwa namna moja ama nyingine alihisi kuwa si jambo salama kabisa na linaweza kuzua madhara makubwa kwa serikali.
Mzee Robert alitamani sana kurudisha siku nyuma ili arekebishe yaliyotokea hapo zamani kidogo lakini haikuwezekana.
****

Mzee Matata alishusha pumzi zake kwa juhudi huku akiketi katika kiti chake cha kuzunguka. Akafanya mfano wa tabasamu na kisha akampigia kijana aliyeagizwa maalumu kabisa kwa ajili ya kufuatilia nyendo za Ninja aliyeagizwa kumuua mzee Marashi kwa ajali ya kukusudia.
Tabasamu lake lilinoga zaidi alipoifikiria shabaha ambayo kijana yule aliwahi kumfyatua Ninja baada ya kuingia katika mtafaruku usiojulikana. Ni hivyo alikuwa amemuagiza afanye iwapo Ninja atasukwasukwa na jambo lolote.
Mzee Matata alikikuna kipara chake, kisha akatoa cheko la dharau huku akiitazama picha ya mtukufu raisi iliyokuwa imebandikwa katika ofisi yake.
“Congratulation Mr President….” Akaisemesha ile picha iliyokuwa inatabasamu wakati wote.
Hakumkumbuka mama lao…..
Labda kwa sababu hakujua nini kilitokea!!!
****

Samwel Mbaule alitoweka eneo lile akiwa ametaharuki, mapigo ya moyo yalikuwa juu sana na alijihisi yu katika matatizo zaidi. Hakugeuka nyuma licha ya watu kadhaa ambao ambao awali walimuona akiwa na mama lao kumuita.
Sam aliingia katika bajaji na ghafla akajikuta akimwamrisha mwenye Bajaji ampeleke ofisi za gazeti la HAKI, ofisi ambazo alikuwa akifanya kazi pale.
Hakujua ni kwanini alifikiria kwenda huko lakini hakubadili maamuzi. Akaendelea kuamini kuna kitu huko ambacho kinaweza kumpa nafuu ya kimaamuzi.
Majira ya saa sita mchana alikuwa amesimama nje ya ofisi za gazeti lao. Mlinzi ambaye alikuwa amezoeana naye sana leo hii alionekana mwenye wasiwasi. Hata wakati anaandika jina lake kuwa ameingia ndani ya ofisi hizo, mlinzi yule alikuwa mkimya sana.
Hilo hakushtushwa nalo, akaingia mapokezi… ile anaonekana kwa yule dada wa mapokezi, macho yakamtoka pima yule dada na kujikuta akiliita jina la Sam zaidi ya mara mbili hovyohovyo. Sam akawa wa kushangaa tu….
Akamsalimia na kumpita, akafika ofisi kuu.
Wafanyakazi walisimama kufanya kazi wakabaki kumtazama yeye….. alifadhaika sana na kujikuta akishindwa walau kutoa salamu. Alijitazama iwapo alikuwa na mapungufu yoyote lakini hakuambulia kitu chochote kile katika mwili wake.
“Jamani, kwema?” alijikaza akasalimia. Lakini ni wafanyakazi wachache sana waliojibu tena kwa sauti ya chini mno.
Akataka kupuuzia na hapa ili aweze kukiendea kiti chake. Jicho likawa la kwanza kuwa shuhuda, hapakuwa na kompyuta katika meza yake. Kiti kilikuwepo lakini pia lilikosekana koti lake ambalo alikuwa analiacha ofisini kila siku.
Sam akapigwa bumbuwazi asijue ni kitu gani kinaendelea hadi ofisini.
“Jamani mbona… eeh! Mbona kiti changu sikielewielewi ndugu zanguni…” alihoji lakini hakupata jibu.
Kila mmoja alikuwa akimtegea mwenzake aweze kumjibu Sam, lakini hakuna aliyesema kitu. Walionekana kuwa waoga.
Sam, akaona kwamba kuendelea kushangaana haisaidii kitu, akaufungua mlango wa mwanamke wa makamo kabisa ambaye alikuwa akiwazidi wafanyakazi wote wa gazeti la HAKI na hivyo wakazoea kumuita bibi, hata jina lake halisi lilisahaulika.
“Shkamoo bibi…” Sam alimsalimia mwanamke yule ambaye alikuwa amejikita katika kompyuta akifanya kazi yake ya uchapishaji.
“Marahaba….” Alijibu bila kunyanyua uso wake.
“Bibi… ni nini kinatokea hapa… maana sielewi kitu.” Sam alihoji, na mara hiyo yule bibi akanyanyua uso.
“Astakha Firullah” yule mama alibinuka na kiti chake kurudi nyuma huku neno lile likimtoka kwa sauti yenye kitetemeshi. Sam akamsogelea zaidi na kumuuliza nini kinasababisha yote hayo.
Yule mama mtu mzima bado hakuweza kusema bali alikuwa anatetemeka tu.
Wazo la upesi limkamvamia Sam, akauendea mlango na kuufunga kwa funguo, hakutabasamu tena badala yake macho yake makali yakamtazama yule mama.
“Usiniue Sam usiniue” yule mama akajitetea huku hofu ikiwa imetanda waziwazi. Kauli ile ikamshtua Sam, lakini hakutaka kutetereka akaendelea kukazia.
Hatimaye yule mama akatoa maelezo huku akitetemeka. Akamweleza Sam jambo ambalo lilizidi kumshangaza.
Yule mama akamweleza Sam kuwa mkurugenzi wa kampuni yao aliwaeleza kwa kifupi kabisa kuwa wasijiweke karibu na Sam kwa sababu ni muuaji wa kutisha na anajihusisha na watu hatarishi sana. Pia amemuua Steve Marashi.
Sam alibaki mdomo wazi, akarudi kinyumenyume akaufungua mlango na kutoka nje, hatua kwa hatua akaufikia mlango na kutoweka bila kuaga.
Alipofika nje alijikuta asiyekuwa na uelekeo, aliyoyasikia ofisini yalikuwa yamemvuruga kupindukia.
“Sasa kama mimi muuaji mbona sikamatwi tena, mbona hata taarifa zangu sizisikii kwenye vyombo vya habari… hawa watu ni akina nani wanaotaka kunichafulia jina namna hii jamani….” Alijiuliza kisha akajiona yu yatima haswa.
Hatua kadhaa mbele akakutana na Bajaji, akapiga mluzi kumuita dereva mara akasikia mtu akiita jina lake. Akageuka na kumwona mtu akijaribu kumkimbilia, Sam akatambua kuwa atakuwa ni mfanyakazi mwenzake anataka kumuuliza maswali ya kipumbavu ambayo yanaweza kumkoroga zaidi. Akaingia ndani ya Bajaji upesi na kumuamuru dereva aondoe hakutaka kuzungumza na huyo bwana aliyekuwa akimuita, safari hii hakutaka kurejea nyumbani kwake moja kwa moja, bali alienda moja kwa moja nyumba ya kulala wageni. Akachukua chumba na kujipumzisha akiitafakari siku ilivyokuwa na mshikemshike na ni kwa namna gani ilikuwa inamalizika.
Hakumkumbuka mtu aliyekuwa akimuita!!
Amkumbuke ili iweje?
Alibaki kumuwaza Tina wake pamoja na ule mkanda wa ngono ambao hakuwa amemshirikisha mtu yeyote.

***

MAMA LAO ASAKWE AUWAWE!

KOSA kubwa walilolifanya polisi waliowekwa kumlinda Mama lao akiwa hospitali ni ile hali ya kumchukulia kuwa yeye ni mwanamke. Na pia kwa ile hali ya kuchafuka na damu waliamini kuwa alikuwa amejeruhiwa na walikuwa wakitimiza wajibu tu huku wakiamini kuwa yule mwanamke hawezi kuupata uhai wake tena. Hawakujua kuwa hakuwa amejeruhiwa na ile risasi bali ililengwa katika kifua cha yule kijana na kukipasulia mbali.
Kilichomzimisha mama lao ni ule uoga tu!!
Polisi hawakumfunga pingu, walimwacha huru wakati dripu zikipishana katika mishipa yake ya damu.
Majira ya saa nane usiku mama lao alirejewa na fahamu zake. Akatulia kwa muda bila kuweweseka, ikawa kama bahati kumbukumbu zake hazikuwa mbali sana. Akayafumba macho yake! Akabaki katika namna ileile ya kupoteza fahamu lakini akizivuta vyeama pumzi zake.
Alifanya vile ili kupata uhakika wa usalama wa eneo lile.
Ni bila kujua kuwa ile ilikuwa siku yake ya kuingia katika utata mkubwa zaidi maishani mwake. Baada ya takribani dakika thelathini tangu azinduke alisikia hatua za watu zikijongea katika chumba alichokuwa amelazwa.
Aliisikia sauti ikiwaelekeza kwa mbali juu ya kitanda ambacho amelazwa. Walikuwa wanaume wane.
Mama lao akafunua jicho lake kwa upenyo mdogo sana, akatazama kushoto kwa na hatimaye akaziona sura.
Mkojo ukapenya katika nguo yake, tumbo likaanza kumkata.
Alikuwa anaonana moja kwa moja na wanyakyusa ambao walimteka Sam na kisha kumrejesha akiwa amezimia, walikuwa ni walewale walio katika mtandao wa mawaziri kwa jinsi alivyowasikia siku walipoenda kula katika banda lake.
Akiwa hajalifumba jicho lake bado, aliwaona wanyakyusa wale wawili wakisemezana kikabila. Walikuwa wakipanga mpango wa papo kwa hapo na mara kila mmoja akagawana mtu wake, wakawatia kabali wale askari wawili na kisha kuwadunga sindano.
Waliendelea kuwadhibiti hadi walipolainika kabisa. Wakawachukua na kuwasukumia uvunguni mwa vitanda.
Kisha wakasemezana kinyakyusa tena, wakakumbushana juu ya maelekezo ya mkuu wao wa kazi. Kuwa kama yule mama yupo hai aondolewe pale hospitali na kisha auwawe na kama amekufa tayari basi mzoga uachwe hospitali.
Kijana mmoja akainama na kuyasikiliza mapigo ya moyo ya mama lao ambaye alikuwa akiendelea kujikojolea.
“Mzima huyu… si tumdunge na yeye sindano afe hapahapa au?” alimwomba ushauri mwenzake….
Kusikia hivyo mama lao akahisia anazikosa pumzi zake, mapigo ya moyo yakazidi kwenda kasi lakini hakutaka ajulikane kuwa amezinduka, lakini akajiapia kuwa wakitaka kumdunga sindano lazima aanzishe timbwili.
“Kaka eeh! Tufuate tulichoagizwa, hujui bosi ana maana gani aisee… je kama hizi sindano haziui mapema… hebu acha bwana mambo yako….” Mwenzake alimpinga.
Mama lao akaipata nafuu kidogo….
Mara mirija ikatolewa na yeye akabebwa mzegamzega. Akaendelea kujikaza asionyeshe dalili zozote za kuzinduka. Kwa sababu alijua kosa lolote lile litayagharimu maisha yake kabla hajaonana na Sam.
Ndani ya sekunde kadhaa akajikuta hewani kisha akatua katika kitu katika kochi, kwa ule mshtuko akajikuta amefumbua macho, bahati ilikuwa upande wake taa ilikuwa imezimwa katika ile gari ambayo ilionekana kama ya kubebea wagonjwa.
Na mara milango ikafungwa na gari likatoweka kuelekea mahali ambapo mama lao hakujua ni wapi.
Harufu ya kifo ikaziandama pua zake na waziwazi akatambua kuwa yupo katika dakika za mwisho za uhai wake.
Alijaribu kufikiri ni kitu gani atafanya kujiepusha na kikombe hicho lakini akili haikufanya kazi kabisa….
Akaamua kufanya sala zake za mwisho huku akijilaumu kwa kujiingiza katika mchezo asioujua sheria zake!!

****

MAJIRA ya saa mbili na dakika kadhaa Sam alikuwa akitembea kinyonge kuelekea katika nyumba ambayo alikuwa akiichukia. Ilikuwa ni nyumba ambayo aliishi kwa furaha sana wakati akiwa na Tina wake lakini ndani ya juma moja tu ilikuwa imegeuka chungu sana.
Alifika na kufungua mlango, mara akashtuka kuwa mlango ule haukuwa umefungwa na funguo.
Sam akajaribu kukumbuka iwapo wakati anaondoka alifunga mlango, hakulipata jibu, akili yake ilikuwa imechoka haswa na hakujali iwapo ni kweli hakuufunga mlango ama aliufunga kwa kutumia funguo.
Akaingia kichwakichwa akiwa ametawaliwa na uchovu. Akajitupa katika kochi sebuleni, akatazama huku na kule kisha akaingia chumbani. Akaondoa nguo zake kisha akaingia bafuni, akaanza kujimwagia maji.
Maji yale baridi kabisa yakampa uhai kidogo kiakili.
Alipojipaka sabuni akayafumba macho yake, ghafla shingo yake akahisi mlango wa bafuni ukifunguliwa, akataka kufungua macho ilihali ana sabuni usoni sabuni ikapenya machoni, akalazimika kufumba macho.
Na hapo ghafla shingo yake ikakabwa kabla hajapiga kelele za aina yoyote ile.
Sam alitapatapa huku na kule lakini shingo yake haikuachiwa.
“Sam….tulia….” sauti ilimnong’oneza kwa chini sana. Sam hakutulia badala yake alizidisha kutapatapa…. Ule mkono nao ukaendelea kumkamata.
“Sam ni mimi…. Tulia…” ile sauti ikanong’ona tena. Sam akaigundua kuwa amewahi kuisikia mahali.
Akatulia mara akainamishwa chini.
“Nawa!”
Sam akatii akanawa uso, sabuni ikamtoka.
Na hapo akajikuta yu bafuni, ana kwa ana na mama lao.
Sam akapigwa butwaa la mwaka kwa kimbwanga hicho.
“Usiongee…” Mama lao akatoa sauti ya chini sana. Sam akaukumbuka umakini alioonywa na mdhamini mtata wa usiku wa manane.
“Kwani..” akataka kuzungumza, mama lao akamziba mdomo.
Sam akajipa utulivu zaidi!
Mama lao akashusha macho yake chini, Sam naye akayashusha!
Ama! Alikuwa yu uchi wa mnyama… upesi akalirukia taulo lake na kujifunga.
Mama lao akatabasamu!! Kisha akamsogelea Sam na kumnong’oneza.
“Maisha yangu yapo hatarini sana, nimewatoroka wauaji, na walikuja hapa kwako pia…”
“Sielewi Mama lao…” alijibu kwa kunong’ona Sam.
“Wametega vinasa sauti…. Usiruhusu kabisa kuongea sauti ya juu! Wamekuja mara mbili ndani ya chumba chako…”
Mama lao akamsimulia Sam mkasa mzima juu ya tukio la hospitali, na namna ambavyo wauaji walijisahau baada ya kupata wanawake na kwenda kufanya nao uzinzi wakiamini mama lao amezimia.
Mama lao akaitumia nafasi hiyo kukimbia mahali asipopajua, hadi alipopata pikipiki iliyomfikisha nyumbani kwa Sam.
“Sam sijui kama nitadumu sana katika kujificha lakini sikiliza kitu kimoja cha msingi, kuna mtu anaitwa BVB huyu ndiye aliyewaagiza wale wanyakyusa kukukamata wewe, na pia ni huyo BVB aliyemwagiza yule mwendawazimu kuiunda ajali na kumuua baba wa Steven Marashi.
Sam, amani na maisha yangu yapo mikononi mwako, mimi nitaenda Mbeya kwetu nitajificha huko lakini ni wewe wa kunifanya niwe huru tena. Tafadhali mtafute huyu BVB mfikishe mbele ya sheria. Simjui hata kwa sura lakini tafadhali kuwa makini kuanzia sasa… una jukumu zito sana nahisi hata Tina watakuwa wanamshikiria wao… halafu nimewasikia wakizungumza juu ya mkanda sijui ni mkanda upi” mama Lao aliongea katika sikio la Sam kwa hisia kali. Kisha akamkumbatia kwa nguvu.
Sam akayasikia mapigo ya moyo ya yule mama jinsi yalivyokuwa juu!!
Vita imeanza rasmi!! Sam akajisemea kisha akamwachia Mama lao na kupiga ngumi ukutani. Hasira ikachemka katika moyo wake, ule uoga akauweka kando na kuuvaa ujasiri.
Mama lao akamtia moyo kuwa ni yeye aliyeushika uhai wa Tina na kubwa zaidi alikuwa mwenye uwezo wa kuifichua siri iliyofichika.
Safari tatanishi ikaanzia pale!!
*****
ALFAJIRI sana Sam akafanikisha kumfikisha mama lao kituo cha mabasi, akapanda na gari na kuliacha jiji la Dar es salaam. Sam alisubiri hadi alipohakikisha basi limeondoka ndipo na yeye taratibu alianza kujivutavuta ili aweze kurejea maskani yake ya Temeke.
Kwa sababu ilikuwa ni asubuhi sana hapakuwa na foleni ambazo huleta kero ya kuishi katika jiji la Dar es salaam, hivyo ndani ya dakika zisizozidi arobaini tayari Sam alikuwa maeneo ya Tandika.
Aliposhuka akavutiwa na muuza magazeti ambaye nd’o kwanza alikuwa anakifungua kibanda chake. Sam akazuga kuwa kuna kitu ama mtu anamngojea pale, lakini nia yake ilikuwa kusoma vichwa vya habari vya magazeti ya siku ile.
Hatimaye yule bwana akaanza kuyatandaza magazeti katika meza yake.
Jicho la Sam likakutana na kichwa cha habari kikubwa kikifuatiwa na vingine vidogovidogo.
“Muuaji wa Steven Marashi aua askari wawili, amlevya daktari na kisha kutoroka mikononi mwa polisi”
Sam hakuwa na subira tena, upesi akamwomba yule bwana ampatie lile gazeti, akafanya malipo na bila kusubiri akafunua na kuisoma ile habari ambayo iliandikwa na mwandishi ambaye jina lake halikuwekwa wazi.
Habari ile ikawa inamzungumzia mama lao….
Kuwa ameua askari wawili na kisha kutoroka mikononi mwa polisi.
Sam akashusha pumzi kubwa sana akalikunja lile gazeti, wakati anaondoka akaliona gazeti jingine na kichwa cha habari, “GAIDI LA KIKE LAUA POLISI NA KUTOROKA”
Sam akafanya tabasamu la karaha na kisha akatoweka.
Akiwa njiani alikumbuka kuwa tayari alikuwa ametangaza vita rasmi tangu alipoambiwa na mama lao juu ya BVB. Japo hakujua hata hilo jina ni la nani lakini aliamini kuwa iwe isiwe atashinda hiyo vita.
Wazo la wapi pa kuanzia kumsaka huyo mtishia amani anayeitwa BVB lilikuja baada ya kutambua wazi kuwa kuna watu wenye nguvu serikali ama popote pale watakuwa nyuma ya kifo cha Steven Marashi, na kama wapo nyuma ya jambo hilo basi lazima kuna kitu watakuwa wanafahamu ama wanakihitaji.
Mkanda wa ngono! Sam akajaribu kuweka hili kama jibu lake sahihi…..
Mkanda huu unahusiana vipi sasa na Tina wangu, na kwanza yupo wapi? Maswali yaliendelea kumiminika katika kichwa chake.
Na alipomkumbuka Tina akazikumbuka siku njema za mapenzi yao, akazikumbuka ahadi tele walizopeana za kulindana. Sam akasimama kando ya barabara na kuegemea mti akayafumba macho yake. Akaikumbuka ile siku walipokutana ndani ya daladala, Sam akiwa anaumwa kichwa na bahati mbaya akawa amekosa siti ndani ya gari, mara akahisi mguso katika bega lake, alipogeuka macho yake yakakutana na sura ya Tina.
“Kaa hapa kaka yangu!” sauti ya Tina ikamweleza Sam wakati huo akimpisha kiti. Sam hakuamini kilichotokea, kupishwa siti na dada tena wa Dar es salaam?
Mara wakajikuta wanashuka kituo kimoja, Tina hakuwa mwenyeji eneo lile hivyo akajikuta akimuuliza Sam.
Ikawa zamu ya Sam kutenda wema, akampeleka hadi mahali alipokuwa anahitaji.
Safari yao ikaanzia hapo, urafiki hatimaye mapenzi. Walipotangaziana ndoa, yakatokea hayo ambayo sasa yamewatenganisha!!!
“Eeh! Mungu wangu mlinde Tina wangu huko alipo…” Sam akafanya dua fupi, kisha akaendelea kutembea huku akiwa amejipanga pa kuanzia.

Naam! Ilikuwa kama alivyopanga na ilikuwa hivyo.
Sam akiwa anatambua vyema kwa ushahidi wa Mama lao kuwa mle ndani kuna vinasa sauti vimetegwa, aliamua kuanza kucheza na akili ya adui yake.
Alipofika akajibwaga kwenye kochi, na baada ya dakika kadhaa akasikika akizungumza kwenye simu.
“Masu eeh! Usiuweke usiku, tukutane Sinza mida ya saa mbili nikupatie ule mzigo. Wao si wamemchukua Tina ngoja na mimi nilipue tu kila mmoja aumie kivyake, wajinga wananichukulia poa. Sasa wewe usipoteze muda tukutane Sinza Hotel, chumba namba kumi na nane….. jitahidi kujali muda, nazima simu.”
Sam akayamaliza mazungumzo hewa huku akitambua wazi kuwa alikuwa ananaswa sauti na wabaya wake.
Simu hii feki ikazua kizaazaa!!

****
 
KISA CHA 9



WAKATI Sam anapiga simu ile hewa kuna makundi mawili sehemu mbili tofauti yalikuwa yametulia tuli kusikiliza anachokizungumza Sam, kila kundi lilipagawa katika namna ya kipekee.

Kundi moja lilikuwa katika ofisi isiyokuwa rasmi iliyokuwa imejazwa na wanausalama wa taifa wanne. Simu ile iliwapa tumaini na kisha kuwapa swali tena juu ya huyo Tina. Tina ni nani na amechukuliwa na nani, mwanausalama mmoja akamtambua Tina kama mchumba wa Sam. Na pia akazitambua taarifa za kupotea kwake ambazo zilikuwa vituo kadhaa vya polisi.
Hilo wakalipuuzia na kutilia maanani juu ya mzigo ambao Sam alikuwa akitarajia kumpa mtu wa kuitwa Masu, kwa jinsi walivyolinasa jina lake katika vinasa sauti.
Mkuu wa usalama wa taifa akampendekeza kijana wake mahiri kabisa katika kufuatilia kimyakimya, asiyeogopa kufa na asiyetambua nini maana ya kusamehe!
Yakubu Gama akapewa jukumu hili .
Na ni huyu ambaye aliagizwa kutega vinasa sauti katika nyumba ya Sam awali.
Gama alifikishiwa taarifa hii akiwa anajiandaa kuandika barua ya kuomba likizo, hivyo wazo la likizo likaishia palepale.

KUNDI la pili lilikuwa kundi la Mzee Matata, hawa waliipokea taarifa ile kwa shangwe hasahasa baada ya kusikia juu ya mzigo ambao Sam alikuwa akiumiliki.
Ni hili walikuwa wakilitafuta siku zote, na hata uamuzi wa kurudisha vinasa sauti katika nyumba ya Sam ulikuja baada ya kukosekana mtu mwingine wa kumhisi juu ya umiliki wa mzigo ambao walikuwa na mashaka nao tangu awali.
Mzee Matata akafanya tabasamu la ushindi baada ya kupokea taarifa zile, safari hii alikuwa na vijana wapya baada ya wale waliotorokwa na mama lao kuambulia kupigwa risasi na kupoteza maisha.
Akawapendekeza vijana wake wawili aliokuwa akiwaamini sana katika suala zima la kupeleleza.
John na Johnson ama walivyozoea kuitana ‘PACHA’.
Na hakika walikuwa pacha, wote walikuwa na roho mbaya, wote walikuwa wartefu waliojaa miili yao kimazoezi na kubwa zaidi wote walikuwa hawachoki kuua, inapobidi na wakati mwingine hata isipobidi.
Kwao kuua ilikuwa mojawapo ya burudani!!
Na ni hawa waliofyatua risasi kuwasambaratisha wale wanyakyusa wawili baada ya kutorokwa na mwanamke wa shoka MAMA LAO.

****

HAIKUWA saa mbili usiku kama Sam alivyoongea katika simu hewa. Badala yake ilikuwa saa tano asubuhi, akalipia chumba namba kumi na nane, akaingia katika kile chumba kisha akatoka baada ya kufanya alilopanga kufanya kwa umakini.
Alirejea majira ya saa kumi jioni akiwa amevaa miwani na kofia ya pama huku miguuni akiwa amevaa viatu maarufu kwa jina yeboyebo.
Ilikuwa ngumu sana kutambua kuwa yule alikuwa ni Samwel Mbaule.
Akajiweka mahali ambapo angeweza kumwona kila mtu aliyekuwa akiingia na kutoka ndani ya hoteli ile ambayo ilikuwa imejitenga mita kadhaa kutoka barabarani.
Nia yake ikiwa kumtambua adui yake ni nani aweze kuanza vita ya kimyakimya.
Vita ya kumwokoa Tina iwapo yu hai, na pia kumweka huru mama lao dhidi ya hila aliyofanyiwa na kisha kutangazwa kuwa ni muuaji.
Akiwa anakunywa soda yake taratibu, jicho lake liliendelea kuwa makini kabisa kutazama yeyote ambaye ataingia pale na kutoka walau atazame iwapo kuna sura anaweza kuifananisha.
Muda ulizidi kusogea lakini hakuambulia sura yoyote. Akaanza kukata tama huku akihisi mama lao hakuwa na uhakika wowote juu ya watu kuingia katika awamu mbili na kuweka vinasa sauti katika nyumba yake.
“Huenda mama lao alikuwa ameghafirika tu!!” Sam alijisemea huku akiimalizia soda yake ili aweze kuondoka na kuingia katika chumba kile alichokilipia.
Sam alisimama kinyonge kabisa huku kichwa kikimuuma, alijiona kuwa hana mbinu mbadala za kumjua adui yake kama ambavyo mama lao alimpamba kuwa anaweza kuwa.
Taratibu kabisa akafika mapokezi na kuchukua funguo za chumba chake. Akajiondokea huku akili ikimchemka vibaya mno.
Alipoifikia lifti alibaki akijiuliza ni kipi sahihi, kupanda ngazi ili apoteze muda ama apande lifti awahi chumbani bila kuwa na sababu yoyote ya kuwahi?
Wakati anajiuliza mara lifti ikafunguka na mtu mmoja akatoka, Sam akafikia maamuzi ya kuingia ndani ya lifti. Akaiamuru imfikishe ghorofa iliyokuwa na chumba chake.
Ndani ya sekunde kadhaa mlango ukafunguka kumaanisha kuwa alikuwa amefika eneo stahiki.
Taratibu Sam akaanza kuambaa katika korido ili aweze kukifikia chumba chake. Na mara akapatwa mshtuko mkubwa sana baada ya kusikia mlipuko mkubwa, si yeye tu bali wateja takribani wote waliokuwa vyumbani walikurupuka, wengine wakiwa uchi na wengine wakiwa na mavazi ya kulalia. Wanawake kama kawaida yao walikuwa wanalia kwa sauti za bila kujua ni kitu gani kimejiri…..

****

Alikuwa ni Yakubu Gama ambaye alikuwa wa kwanza kuingia katika chumba ambacho Sam alikuwa amekilipia kwa ajili ya kukutana na mtu hewa waliyezungumza naye kwenye simu.
aliingia katika chumba kile hata kabla Sam hajaingia na kutoka baada ya kukilipia. Hivyo wakati Sam anaingia hakuwa peke yake, Gama alikuwa yu ndani tayari.

Waliofuata kuingia katika kile chumba walikuwa ni PACHA kutoka kwa mzee Matata. Alitangulia John kisha Johnson, wakati huo Gama akiwa uvunguni. Nia yake ikiwa ni kutoka katika ficho lile punde baada ya wawili hao walioingia kukabidhiana huo mzigo, aliiweka sawa bastola yake vyema katika kiwambo cha kuzuia sauti. Kisha akaendelea kutulia.
Wawili wale ambao aliamini kuwa ni Sam na mwenzake (Masu) hawakuzungumza lolote badala yake walianza kupekua huku na kule kisha mmoja akaingia bafuni na hakutoka huko.
Gama akiwa uvunguni akabaki katika mshangao lakini hakupoteza umakini wake, akayakaza macho yake vyema bila kuruhusu mtikisiko wa aina yoyote.
Mara yule bwana mmoja aliyebakia akaingiza mikono yake uvunguni na kuanza kupapasa. Gama akawahi kuuondoa mguu wake ambao ungeweza kuguswa na yule bwana…..
Baada ya kupapasa mara yule bwana akainama uvunguni.
Ebwana! Macho kwa macho na Gama. Gama hakumwachia upenyo maana alijua tayari mambo yameharibika. Gama akafyatua teke, lakini kama ilivyo maaajabu… yule bwana akauondoa uso wake ndani ya nukta chache, Gama akajikuta amebutua teke kitanda.
Na palepale akawahi kujitoa uvunguni, lakini kabla hajasimama imara akajikuta akipokea teke kali sana usoni, akayumba lakini hakuanguka akajiweka imara akasimama wima.
Ana kwa ana na kipande cha mtu!!!
Gama hakuonekana kuwa na mwili wa kimazoezi, alikuwa mnene kiasi na anayeonyesha kuwa legelege, jambo hili lilimzubaisha Johnson. Akamchukulia Gama kuwa ni dhaifu, akamsogelea ili amkwide, lakini akakutana na pigo kali la karate katika shingo yake na kisha ngumi kali katika korodani zake.
Yule bwana mkakamavu akajikuta amelainika, hakika alikuwa amekutana na mtu kati ya watu!
“Pachaaa…” akapiga kelele za hofu baada ya kuona amezidiwa, na hizi zilikuwa kelele zake za mwisho kabla Gama hajafyatua ngumi kali iliyojikita katika shingo yake na kumtupa chini ambapo hakuwahi kuamka tena milele.
Wakati akipambana kuvuta pumzi za mwisho mara chumba kikavamiwa na Johnson, yule pacha ambaye alikuwa bafuni, hakuuliza swali akamvamia Gama kwa papara akamnyuka ngumi mbili tatu za harakaharaka. Gama akajituliza kwa umakini zaidi akamuhesabia hatua Johnson alipojisogeza tena Gama naye akafyatuka na kuanguka naye chini mzimamzima.
Akamkaba shingo kwa uimara kisha akamuuliza juu ya wapi ulipo mkanda.
Johnson hakujibu chochote kwa sababu alikuwa amepigwa kabali, Gama akalitambua hilo, upesi akamwachia na katika nukta iliyofuata akampiga ngumi nzito kwenye taya.
Johnson akajiharishia!!
Na hapo akakiri kuwa alikuwa anapambana na kiumbe wa ajabu kupita wote aliowahi kukutana nao katika maisha yake.
“Ni nani alimuua Steven?, Tina ni nani?, na mkanda upo wapi… “
“Sijui lolote mkuu, nimeagizwa tu…” alijibu huku akigumia kwa maumivu makali.
“Jina la aliyekuagiza.. upesi kabla sijainyonga shingo yako bwana mdogo…..” akatoa karipio kali Gama. Macho yake yakiwa mekundu na mikono ikiwa na tamaa kali ya kuua!!
“BVB”
“BVB ni nini maana yake.. upesi….” Alihoji huku akiikaza shingo ya yule bwana.
Hilo likawa swali la mwisho kabisa kuuliza kabla yule bwana hajafanya kitendo cha ajabu, akaanza kujinyonga nyonga kama anayeugulia tumbo. Na mara mlipuko mkubwa ukasikika.
Hapo ndipo kilipozuka kizaazaa!!
Gama akarushwa mbali kabisa na mlipuko ule.
Mlipuko ambao hakuutegemea katika mazingira yale!

Mlipuko ule ukawavuta watu waliokuwa nje na ndani ya hoteli ile akiwamo Sam.
Na hakuwa Sam pekee bali askari kanzu wapatao kumi waliomsindikiza Yakubu Gama wakaingia kazini.
Kwa papara kama kawaida yao!!
Utawajua tu kwa amri zao.
Wakatapakaa huku na kule, raia nao wakakimbilia eneo la tukio, Sam akaongoza mbio hizo akawa mmoja kati ya watu waliowahi kuwasili eneo la tukio.
Macho yake yakakutana na mwili wa Yakubu Gama katika chumba chake.
Sura na umbo havikuwa vigeni kabisa katika macho yake. Sam alijiuliza ni wapi aliwahi kumwona kiumbe yule, akaituliza akili na kujikuta akimkumbuka.
Alikuwa ni yule mwanaume aliyekuja kumwekea dhamana na kisha kumsihi awe makini. Dhamana ya maajabu ya usiku mnene sana.
Inakuwaje bwana huyo katika chumba chake? Ilistaajabisha. Na hapo akajipongeza kwa kujisajili kwa jina lisilokuwa lake wakati anaingia hotelini hapo. Kwani kwa tukio lile tayari ni kizaazaa kipya.
Sam akazidi kutambua kuwa lipo jambo ambalo limetanda katika mkasa wa kifo cha Steven Marashi na hata baba yake mzazi. Kichwani akajiwekea picha kuwa kuna pande zaidi ya moja zinawania mkanda ambao alikuwa anaumiliki!
Pande hizo ni zipi? Alijiuliza bila kupata jawabu!!
Katika purukushani za hapa na pale kabla polisi hawajaweka utando wao wa kuzuia raia kuingia ndani ya kile chumba, Sam alifanikiwa kukitoa kinasa sauti chake ambacho alikiweka baada ya kuingia katika chumba kile na kutoka majira ya saa tano. Kilikuwa kimewekwa katika godoro ambalo alikuwa amelichana na kisha kukitandika kitanda vyema.
Sam alizuga kuwa amesukumwa, akaangukia pale na kwa sekunde chache akaondoka na kile kifaa.
Wakati anaondoka alipishana na yule mwanadada aliyemwandikisha kuingia katika chumba kile. Yule dada bado hakuwa na uhakika kama yu sahihi ama la. Sam mwenye hofu akajikaza akaongeza mwendo.
“We kaka…” yule dada akajaribu kuita. Sam hakugeuka.
“Ni yeye jamani…” sauti ikasikika kama akiwaambia watu fulani.
Sam akawa ameifikia kona, akaanza kukimbia, akakata mitaa hapa na pale hadi akatokea Ubungo.
Jasho lilikuwa linamtoka haswa.

***
 
Kuanzia mpango wa kando, ripoti kamili na hii.. Mtunzi amejipanga. Amejipanga zaidi ya Gama wa kwenye hii hila...
 
KISA CHA 10

Taarifa za vifo vya mapacha wawili tegemeo kabisa katika ngome ya mzee Matata ilipokelewa katika namna ngeni kabisa na mzee yule, alikuwa amepagawa na hakutarajia hata kidogo jambo kama lile lingeweza kutokea.
Hakuamini hata kidogo kama Sam angeweza kukabilia na vijana wale machachari na kisha yeye akaibuka bingwa. Tena sio bingwa wa kawaida tu, bingwa aliyeua.
Upesi akachukua simu yake na kumpigia mzee Robert, mrakibu mkuu wa polisi.
Simu ilipokelewa kwa utulivu! Harakaraka na kwa papara kubwa Matata alianza kumuhoji Robert juu ya tukio lililojitokeza Sinza hotelini.
“Kwani kuna tatizo gani mzee Matata ya nini kuuliza kila kitu kinachohusu usalama wa raia na hasahasa siri za jeshi la polisi. Samahani lakini kwa namna moja ama nyingine nashindwa kukuelewa mkuu….”
Bila kujibu chochote mzee Matata akakata simu.
Robert akabaki kutetemeka asijue mzee yule alichukulia vipi maelezo yale aliyompa. Lakini alifanya vile kwa sababu alilazimika kufanya, kwanza alikuwa amevurugwa sana. Matukio yalikuwa yanapangana, kabla hili halijaisha anasikia jingine likipanda juu yake.
Ilikuwa lazima achanganyikiwe na matukio yale yaliyozungukwa na utata.
Akiwa anaanza kusahau juu ya simu aliyozungumza na mzee Matata, mara simu yake ya mkononi ikaita.
Alikuwa ni IGP…..
Robert akaomba dua zote kabla ya kuipokea simu ile kwa sababu alimjua vilivyo mkuu wake wa kazi.
“Robby, hivi ungemjibu mzee Matata vizuri ni kitu gani kingekupungukia labda…… Robby, mzee Matata akiongea na mkuu wan chi ujue utaingia matatani.
Nisikilize Robby, wewe na mimi tunafahamu ni pesa kiasi gani mzee Matata ametoa ili kufadhili kampeni za chama. Unajua ni jinsi gani mzee Matata na raisi ni marafiki, chunga sana mdomo wako Robby, chunga sana inaweza kukugharimu, nimekusihi haya kwa sababu wewe ni mzazi na una familia kubwa… sitaki familia yako iteseke.
Nadhani unanielewa, sasa mpigie simu mzee Matata tena ni muda huu na umwombe msamaha….” Alihitimisha IGP.
“What? Ni nini hiki IGP… Msamaha kwa kuficha siri za jeshi letu mkuu…”
“Nimesema mwombe msamaha. Nimemaliza…” akakata simu IGP.
Robert Massawe akabaki kuitazama simu ile kana kwamba ina lolote la kumshauri ama inaweza kushiriki naye katika mshangao mkubwa aliokuwanao… lakini haikuwa hivyo. Simu nayo iliendelea kumtazama.
“Si bure…..” Robert alijisemea huku akiichukua simu yake na kubofya jina la mzee Matata.
Funika kombe mwanaharamu apite!! Alijisemea huku akiungoja upande wa pili uweze kupokea simu. Simu iliendelea kuita bila kupokelewa!!

*****
WAKATI simu ya mzee Matata ikiita, mzee huyu alikuwa ameenda mahali kujipooza hasira zake. Kitendo cha kukatiwa simu ya Robert alichukulia kama dharau kubwa sana kwake na tena ikiwa imefanywa na mtoto mdogo asiyekuwa na uwezo wa kutoa kauli yoyote mbele yake.
Mzee Matata alikifikia chumba alichokusudia akakifungua na kukabilia na sura iliyokuwa ikisihi huruma. Sura ya kike iliyopauka haswa na kuchubuka kutokana na kipigo.
Macho yake makubwa yalikuwa yamedumbukia ndani na midomo yake ilikuwa mikavu.
“Bitch! Huyo hawara wako anashirikia na watu gani?” Matata alitupa swali. Yule binti aliyezidi kusihi huruma kwa yale macho yake tu alijitahidi aseme lolote lakini akashindwa. Akabaki kulishika koo lake na hapo sauti ya kukoroma ikamtoka.
“Nina kiuuu…”
Hakika alikuwa ana kiu, kiu kikalikausha koo na kuondoka na ile sauti yake nzuri. Sauti iliyompagawisha Sam na kujikuta akiamua kutangaza ndoa kabisa.
Alikuwa ni Christina Elisha Prosper ama alivyozoeleka kwa wengi kama Tina!
Ile hali ya Tina kulalamika kiu badala ya kujibu swali aliloulizwa ilimghafirisha tena mzee Matata, akahisi anazidi kudharauliwa na watu wasiostahili hata kupita njia anayokanyaga yeye.
Mzee Matata akaondoka, sura yake ikiwa nyekundu akaingia bafuni na kutoka na ndoo iliyojaa maji. Akaifikisha katika chumba alichokuwa amehifadhiwa Tina.
“Inama unywe maji kisha unijibu…” mzee Matata akamweleza Tina kwa sauti iliyojaa upole. Tina akajisogeza kwenye ndoo na kuinama kama mbuzi. Akaanza kunywa maji.
Mzee Matata akamvamia pale pale kwenye ndoo na kukishika kisogo chake na kumzamisha kichwa kizima katika ile ndoo.
Tina alitapatapa akirusha miguu huku na kule, alivuta maji kwa pua na midomo. Akazikosa pumzi zake.
Baada ya dakika mbili mzee Matata akamwachia.
Tina akabaki kutapika huku na kule, akizisaka pumzi kwa jitihada kubwa, katika kuruka huku na kule mara akamtapikia mzee Matata katika mguu wake.
Yule mzee asiyekuwa na huruma akamnasa kibao kisha akamfyatua teke kali tumboni huku akimsindikiza na matusi.
Tina akatua katika kingo ya ukuta, uso ukabaki kutambaa sakafuni na maneno yasiyoelewekaeleweka yakimtoka.
“Sam anashirikiana na nani katika kikundi chake cha kijasusi??” alihoji mzee Matata.
“Sijui lolote…. Najua ni mwandishi tu…..” alilalamika Tina.
Mzee Matata akataka kumrushia adhabu nyingine ya teke lakini safari hii akaisikia simu yake ikiita.
Akaufunga mlango na kutoweka.
Akaipokea simu na kuupokea msamaha kutoka kwa Robert. Mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi!!
Ile hali ya kuombwa msamaha ikampunguzia ghadhabu kidogo na kujiona mtukufu sana mbele ya watu wenye madaraka.
“Haya kijana…. Ni nani wale waliopambana na kuuana katika hoteli ya Sinza…” akamuhoji Robert kifedhuli.
“Wawili hawajajulikana majina lakini mmoja ni kijana wetu…” alijibu Robert huku akiuma meno yake kwa hasira.
“Na kijana wenu naye amekufa?” aliuliza.
“Haijathibitishwa bado lakini yupo mahututi hospitali ya jeshi Lugalo…”
“Ok! Vizuri ntakupigia baadaye nikihitaji kujua juu ya hali yake. Poleni na muwe na siku njema…” akaaga na kukata simu.
“https://jamii.app/JFUserGuide!” alifoka Robert huku akiibamiza meza iliyokuwa pale ofisini, akaituliza akili yake na kujiuliza juu ya yule mzee ambaye anatambulika nchini kwa biashara zake kubwa anazomiliki. Sasa kulikoni mambo hayo ya jeshi awe anayafuatilia kwa ukaribu kiasi hicho.
Lazima kuna kitu hapa!! Alijishauri, na kisha akajiapiza kutothubutu kufuatilia nyendo za mzee Matata. Hakutaka kuyapata matata!!
Akakumbuka maneno kadhaa ya IGP alipokumbushwa juu ya familia yake, hapo uoga ukamwingia.
Lakini hakuwa amejitoa katika vita na mzee Matata kama alivyodhania!!
Nd’o kwanza alikuwa anaikaribia.

***

SIMU yake iliyokuwa katika mfumo wa mtetemo iliunguruma mara tatu kabla mkewe hajamgutusha kutoka usingizini.
Robert Masawe alijinyoosha kidogo kabla ya kutazama kwenye kioo na kukutana na namba mpya. Hilo halikumshtua ilikuwa kawaida kupewa taarifa kadha wa kadha kutoka kwa wakuu wake ama wadogo zake kikazi kwa kutumia namba mpya.
“Jambo afande, CW00JT Lugalo hospitali..” alijitambulisha kwa namba yake na Robert akatambua kuwa kuna ujumbe anatakiwa kupokea.
“Endelea afande.”
“Kuna vijana watatu wanahitaji kumwona Inspekta Yakubu Gama….”
“Vijana? Vijana kutoka wapi?”
“Madaktari wameagizwa na mzee Matata!”
“Whaat? Madaktari, madaktari kivipi?”
“Sina nijualo zaidi ya kukupa hii taarifa afande..”
“Usiwaruhusu kwanza!” akaagiza na kukata simu.
Akatulia kitandani kwa sekunde kadhaa, mkewe naye akaketi kitako kuungana na mumewe. Hakutaka kumuuliza lolote, zaidi alibaki kumminyaminya begani kama namna ya kumfariji.
Robert Masawe, mrakibu msaidizi wa polisi aliitwaa tena simu yake wakati anataka kupiga mara ikaingia simu kutoka kwa mzee Matata. Robert akaruka sentimita chache kutoka katika kitanda, ni kama alikuwa ameona mdudu wa hatari.
Hakuipokea simu ile akaiacha iite hadi pale ilipokatika.
Na hapo Robert akampigia IGP.
“Jambo afande!” akasalimia. IGP hakujibu akaendelea kumsikiliza.
“Mkuu, Mzee Matata ameagiza madaktari kwa ajili ya Inspekta Yakubu Gama! Unayo taarifa hiyo?”
“Unawezaje kupata taarifa nzito kama hiyo kabla mimi sijaipata?” IGP akajibu katika mfumo wa swali kwa swali. Jibu ambalo lilimkera Robert lakini hakuwa na la kufanya.
“Lakini mkuu ulipaswa kunieleza kwa sababu vijana walio katika lindo wanatoa taarifa kwangu kama ulivyoagiza mkuu…”
“Kwa hiyo unamaanisha waanze kuripoti kwangu moja kwa moja?”
“Hapana afande!!”
“Waruhusu waingie nimezungumza naye, ametusaidia madaktari kutoka India wanusuru uhai wa Gama…. Wakati mwingine tabia yako ya kupenda kuuliza kila kitu siku ya siku utasababisha tukose misaada….” Akamaliza na kukata simu.
Super retendant Robert Masawe akapagawa!
Na hapo mkewe akaamua kuhoji kulikoni, Robert Masawe alijaribu kumkwepa mkewe lakini mwanamke yule hakukubali kabisa. Akakazia hadi Robert akasalimu amri akaketi kitako na kuanzia kumsimulia mkewe juu ya mkasa mzima unaoendelea.
Mkewe alikuwa makini sana kumsikiliza na baada ya maelezo yale, mkewe akatokwa na kauli ambayo bwana Robert hakuitegemea.
“Ukilala usingizi basi Gama atalala usingizi wa milele leo, pindi utakapoamka utakutana na lile neno kwamba jitihada za madaktari zilishindikana…. Hakuna madaktari hapo mume wangu, hao ni watu wabaya na hapo wanataka kumzimisha Gama ili asiseme ambacho amekigundua huko alipotoka…”
“Heh! Mke wangu umeyajuaje haya yote?”
“Nasoma sana riwaya mume wangu hasahasa za kipelelezi, wewe hupendi riwaya lakini zile za wakongwe zina mambo mengi ya kujifunza, mfano Mhanga wa ikulu ya Beka Mfaume, Mkimbizi ya Hussein Tuwa na Msako wa Hayawani ya Eddie Ganzel…. Naona wanayoyaandika nd’o kisa kama hiki, ukitaka kuamini we lala halafu asubuhi tutasimuliana…. Lakini uhai hautakuwepo tena. Gama atakuwa mfu!!”
Maneno ya mkewe yakamsisimua Robert licha ya kutokuwa na undugu wowote na Gama lakini alitambua kuwa nchi ilikuwa ikimuhitaji sana kijana shupavu kama yeye ili amani iendelee kuwepo huku waovu wakifikishwa mbele ya sheria.
Uzalendo ukajikita katika moyo wake, ujasiri ukajiunga naye upya. Akaona si sawa kumpoteza Gama katika namna nyepesi hivyo.
Alitambua kuwa vijana waliokuwa wameweka ulinzi kwa Gama wasingeweza kuwaruhusu wale madaktari kuingia katika chumba cha mgonjwa bila idhini yake yeye.
Pale pale akachukua simu ya mkewe akabofya namba za mmojawapo wa askari katika lindo la hospitali ya Lugalo ambayo alikuwa amehifadhiwa Gama.
Akamwambia asogee kando kabisa waweze kuzungumza.
“Naomba uende katika chumba alicholazwa Gama, kamtazame hali yake na ukiwa humo chumbani nipigie simu.”
Akamaliza na kukata!!
Yule kijana kama alivyoamrishwa akawapita wale madaktari ambao walikuwa wakingoja ruhusa, akaingia katika chumba alichokuwa amelazwa Gama.
“Hali yake bado si salama amepoteza fahamu bado..”
“Afande! Sina imani hata kidogo na hao madaktari, ni mimi nakueleza wewe tu na ujue wewe tu kwa sababu kanuni za jeshi kumtilia mtu mashaka ni nguzo kuu katika upelelezi. Hivyo nakuomba ufanye kitu kimoja…… ni cha hatari lakini nd’o inaweza kuwa salama yetu…. Wasiliana na daktari mmoja anaitwa Haji. Ni rafiki yangu sana kisha nipe nizungumze naye. Mengineyo nitakujuza.
“Sawa afande!” alijibu yule kijana kisha akatoweka.
Akafanya kama alivyoamriwa!

****
 
KISA CHA 11

JOPO la madaktari wenye asili ya kihindi liliingia katika chumba cha ambacho Yakubu Gama alikuwa amelazwa. Walikuwa wameng’ara katika sare zao rangi ya bluu. Waliweza kuongea maneno machache tu ya kiingereza, asili yao ilikuwa uhindini.
Baada ya kuingia katika kile chumba milango ilifungwa huku wakitoa agizo kuwa haruhusiwi mtu yeyote kuingia katika chumba kile.
Askari wakabaki kufanya ulinzi!

Baada ya milango kufungwa, daktari mmoja alitwaa simu yake na kupiga namba kadhaa, sekunde chache mbele simu ikapokelewa.
“Tupo ndani ya chumba tayari!” alizungumza kwa kiingereza kibovu.
“Kumbuka kufanya upesi na kwa usahihi kama nilivyowaeleza….”
“Hakuna mashaka!”
Akakata simu na kuwafanyia wale wenzake kama ishara!
Wakakizunguka kitanda kama wakizungukavyo kitanda cha mgonjwa mahututi.
Mgonjwa alikuwa ana majeraha makubwa ya kuunguzwa na moto na pia alikuwa amevunjika mkono na mguu.
Naam! Gama aliyejeruhiwa katika mlipuko wa bomu.
Wakamtundika mipira mingine katika mishipa yake na kisha kuruhusu dawa zimwingie kwa kasi. Wakati huohuo daktari mwingine akiuamsha moyo wa mgonjwa kwa kutumia mashine.
Hatimaye akakohoa, wakaendelea na jitihada zao hadi fahamu zikamrejea.
Wale madaktari wakafanya kama walivyoagizwa wakaanza kumuhoji mgonjwa kitandani. Maswali yao yote yalikuwa juu ya tukio lililopita na kumfanya awe pale kitandani hoi.
Walimuuliza alichokuwa anakumbuka lakini hapakuwa na majibu, yule bwana hakuonekana kukumbuka jambo lolote lile. Walimuuliza jina lake akajitambulisha kuwa yeye ni Hasani Hasani.
Madaktari waliyarekodi majibu yote hayo, kama walivyoagizwa kuwa kwa majibu yoyote atakayoyatoa yule bwana ambaye walimtambua kwa jina la Gama Yakubu.
Baada ya kurekodi kilichokuwa kinafuata ni kuuondoa uhai wa mtu yule aliyesadikika kuwa na lolote ajualo kuhusiana na mkakati mahususi wa siri!!
Naam! Wakamwondoa uhai wake kwa kumchoma sindano yenye sumu kali.
Kisha wakatoka ndani ya kile chumba huku wakitikisa vichwa vyao.
Wakasikitika na kutoa majibu kuwa haikuwezekana kuokoa uhai wa Gama kwani damu ilivilia katika ubongo wake.
Pia wakasisitiza zaidi kuwa mwili wa marehemu umeharibika vibaya hivyo ni vyema uzikwe mapema.
Taarifa za Yakubu Gama kupoteza uhai zikamfikia IGP na mrakibu msaidizi Robert.
Kila mmoja akaipokea katika namna aijuayo mwenyewe.
IGP akampigia simu mzee Matata na kumshukuru kwa jitihada kubwa alizoonyesha, akamsifu kwa uzalendo wake katika nchi isiyokuwa yake. Lakini hakusahau kumkandia bwana Robert kuwa kwa kuchelewa kwake kuwaruhusu madaktari basi amechangia kifo cha Yakubu Gama. Mwisho akamweleza Mzee Matata kuwa raisi atasimamia safari nzima ya madaktari wale kurejea nchini India.
Mzee Matata akashukuru na kisha simu ikakatwa.
Gama akahesabika kuwa kijana wa pili muhimu kabisa katika usalama wa taifa kupoteza uhai katika kipindi cha mwezi mmoja..

Mzee Robert alipewa taarifa ile ya kifo na mkewe kama ushuhuda juu ya alichomweleza usiku juu ya madaktari hao feki.
Bwana Robert alimkumbatia mkewe na kumshukuru kwa ushauri wake lakini akabaki kusikitika kuwa yeye hakuwa juu ya IGP hivyo asingeweza kuwazuia madaktari wale kuingia katika kile chumba alichokuwa amelazwa Gama.
Mke akatoa pole na kumtia moyo mume wake.
Mzee Robert akashukuru! Na baada ya hapo akamuaga mkewe na kuelekea hospitali ya Lugalo.
Huko akaenda kukutana na Daktari Macho.
Bwana ambaye walisoma naye shule moja ya msingi hadi chuo kikuu, na hapo wakatengana mmoja akisomea udaktari na mwingine akisomea uhasibu!
Taaluma zikawatenganisha lakini baadaye zikawakutanisha tena, Dokta Macho akiwa anafanya kazi katika hospitali ya jeshi na Robert akiwa na cheo cha Mrakibu mkuu wa polisi.
Usiku ule thamani ya urafiki wao iliendelea kuonekana huku wakiwa wanaaminiana kwa silimia kubwa.
Dokta Macho aliyasikiliza mashaka ya Robert na kuamua kutii alichosisitizwa, akamuhamisha chumba Yakubu Gama kisha katika kile kitanda akawekwa bwana aliyeshukiwa kuwa ni mwizi, wananchi wakachukua sheria mikononi na kumchoma moto. Lakini kabla mambo hayajawa mabaya sana akaponea chupuchupu na kuwahishwa hospitali.
Majeraha katika mwili wake na yale ya Yakubu Gama baada ya mlipuko yalifanana sana maana yote yalikuwa majeraha ya moto.
Wale madaktari kutoka India wakakutana na mchezo ndani ya mchezo waliopanga kuucheza. Wakachezewa shere na mwisho wa siku wakaumalizia uhai wa yule kibaka.
Wakajisifu kuwa wamemuua Yakubu Gama.
***
Kwa kitendo kile cha kuwarubuni madaktari, bwana Robert alitambua vyema kuwa amejiingiza katika vita na IGP pamoja na mkuu wan chi maana hawa walikuwa hawaambiliki kwa lolote juu ya mtu wa kuitwa mzee Matata.
Hofu kubwa aliyokuwanayo Robert ni juu ya usalama wake na daktari aliyeshiriki katika tukio lile.
Na hapo akatambua kuwa hatakiwi kulala kitandani na kupeleka mambo taratibu taratibu.
Badala yake alitakiwa kufanya mambo kwa kasi ya ajabu ili hata siku wakimlaza usingizi wa milele basi neno lake liendelee kuishi huku likiwaumbua wote waliokuwa wakijificha huku kiuhalisia walikuwa wauaji.
Kwa kufikiria ni namna gani anaweza kuchakarika kwa kasi bila uoga. Robert akaamua kuyahamishia mambo yaliyokuwa katika kichwa chake akayaweka katika maandishi.
Neno kwa neno kuanzia mashaka yake juu ya mzee Matata, pia lawama zake juu ya IGP na kisha akagusa mamlaka kuu ndani ya nchi akapagusa Ikulu. Akapataja kuwa panahusika kumficha mzee Matata.
Baada ya kuandika kurasa nyingi sana akautuma ujumbe ule mahali ambapo aliamini kuwa ni sahihi kabisa na wala hatakuwa amepotea kufanya vile.
Hakujitambulisha yeye ni nani wala cheo chake katika uongozi wa jeshi la polisi.
Harakati zikazidi kupamba moto!!

*****

MOROGORO MJINI

AKILI za kuzaliwa za Atuganile ama maarufu kama mama lao zilimfaa mara nyingi sana. Hata katika maisha yake ambapo alikuwa ameishia darasa la saba hakubabaika na kuyaogopa maisha. Alipambana kwa mafanikio jijini Mbeya na kisha kuingia jijini Dar es salaam huku akiwa hana mwenyeji hata mmoja. Lakini licha ya hayo bado aliweza kupambana bila kuwa ombaomba.
Kilichokuwa kinambeba katika maisha yake ni siri zake kwa jambo ambalo anatarajia kulifanya. Kila wakati alikuwa akihofia kuwaambia watu mipango yake kwa kuhofia kukatishwa tama. Hivyo aliiongoza serikali ya maisha yake kwa kutumia kichwa chake mwenyewe.
Tabia hiyo iliendelea hata siku ile ambapo alipandishwa gari na Sam kwa ajili ya kwenda Mbeya.
Naam! Alihitaji Sam atambue kuwa yupo Mbeya, ili ikitokea siku moja Sam amekamatwa na kubananishwa ipasavyo ajikute akiisaidia ;polisi upelelezi wa kumtafuta mama lao Mbeya.
Msako ambao ungewachukua miaka zaidi ya kumi bila mafanikio yoyote.
Wangedumu wakimsaka mama lao jijini Mbeya wakati mipango yake ilikuwa tofauti kabisa.
Mama lao kwa utashi wake mkubwa gari lilipofika Morogoro akashuka, bila kutoa taarifa.
Gari likaondoka huku siti yake ikibaki wazi, kondakta akajisikia vibaya sana kuwa amemuacha abiria wa kwenda Mbeya stendi ya Msamvu Morogoro.
Wakati kondakta akifadhaika na kumuuliza jirani yake juu ya yule abiria wa Mbeya aliyeachwa njiani. Mama lao alikuwa ameshikilia gazeti ambalo lilikuwa likimtangaza kuwa anasakwa kwa mauaji.
Alitabasamu kisha akacheka kwa nguvu!
Hakuwa na wasiwasi hata kidogo.
Hakika alikuwa na jina kubwa lakini bahati nzuri iliyoje hakuwa na kumbukumbu ya kuwahi kupiga picha jijini Dar es salaam. Mazingira aliyofanyia kazi hayakuwa mepesi kupiga picha, alikuwa ni mtu wa kutingwa masaa yote.
Nani angekuja kumpiga picha!!
Ungekuwa mgahawa wa watu wa kifahari walau wangepata huo muda wa kuchukua kumbukumbu. Lakini waliohudhuria mgahawa ule wengi wao walikuwa mafukara tu ambao msongo wa mawazo ni kipande kimoja katika maisha yao ya kila siku.
“Wali nyama, niwekee wa kushiba!” hizi nd’o zilikuwa lugha zao. Baada ya hapo ni malipo na kukutana tena ni kesho yake.
Magazeti yakabaki kuandika jina la mama lao tu!
Bila picha wala jina halisi hawakulijua.
Tanzania nzima kuna akina mama lao wangapi??
Bahati iliyoje kwa mama lao Atuganile kuonyesha makucha yake pasipo kujulikana.

*****

KATIKA Mji ambao aliishi mama lao kwa wakati ule, ulikuwa ni mji wa maficho pia kwa kijana Yakubu Gama ambaye alikuwa amehifadhiwa kwa ajili ya matibabu.
Fahamu zilikuwa zimerejea tayari na damu yake ilikuwa inachemka haswa kwa ajili ya mapambano. Alikuwa na kiu ya kujua kunani hadi mambo haya yote yanatokea.
Na kubwa zaidi alitamani kumjua muuaji wa Steven Marashi ambaye alikuwa pacha wake katika kazi kabla hajahamishiwa kazi maalumu ya upelelezi, kazi ambayo ilimfanya ajikute katika sanaa ya maigizo na hatimaye kuanza kucheza katika filamu.
Hakuna hata muigizaji mmoja aliyetambua kuwa Steven Marashi alikuwa kijana wa usalama wa taifa.
Kwa tukio lile la kulipukiwa na bomu ambalo lilikuwa katika mwili wa kijana aliyeagizwa na BVB kulizidi kumtamanisha kutambua kuwa ni kitu gani ambacho kinafichwa.
Hisia zake kubwa zikajijenga juu ya upelelezi ambao Steven Marashi alikuwa akiufanya kimyakimya dhidi ya kigogo wa serikali. Upelelezi alioubatiza jina oparesheni tokomeza. Alichotaka kukitokomeza alifahamu yeye mwenyewe.. jambo la muhimu alimsihi Gama kuwa mtulivu ayangoje majibu.
Hivyo kama Steve ameuwawa bila shaka ule upepelezi wake ambao alikuwa hajaukabidhi ofisi kuu ulikuwa katika mikono ya mtu mwingine ambaye amezing’amua siri nzito za usalama wa taifa.
Kitendo cha kutaka kuuwawa akiwa hospitali kilimsababisha apigie mstari mashaka yake na kuamini kuwa anatakiwa apambane upesi ili kuupata ukweli.
Na aliamini hilo linawezekana sana kwa sababu tayari alitambulika kuwa amekufa. Na vile mwili wake haukuagwa kwa sababu kuwa ulikuwa umeharibika sana.
Akabaki kujulikana yu hai kwa watu wasiozidi wanne!
Hakuna hata mmoja kutoka katika familia yake aliyetambua kama yu hai mjini Morogoro.

Gama alijaribu kutembea kwa kujivutavuta hadi akakifikia kioo. Akajitazama!
Lahaula! Hakuwa yeye, sura yake iliunda mfano wa mapunye na ngozi yake ilikuwa imechubuliwa vibaya sana na lile bomu. Akajaribu tena na tena kujitazama hakuwa yeye!
Hasira zikamjaa kifuani akaubamiza ukuta kwa ngumi nzito!
Na hapo mwenyeji wake ambaye ni daktari akaingia na kumsihi ajipumzishe kwani hakutakiwa kujihangaisha kwa lolote hadi pale atakapopona!
Gama alirejea kitandani akajilaza lakini ni kwa kupumzisha mwili tu na sio akili. Akili ilikuwa inapanga mikakati kabambe!
Akamfikiria sana hayati Steven Marashi, akakifikiria kifo chake kilivyokuwa cha upesi, na tetesi zake ambazo hazikuwa zinaeleweka. Mara ameuliwa kishirikia na mpenzi wake, mara amejiua.
Gama akaufikiria ukakamavu wa Steve, akafikiria ni jinsi gani alikuwa na uwezo wa kupambana na maadui zake, akaitambua misimamo yake.
Hapa zile tetesi za kujiua akazifutilia mbali.
Akamkumbuka tena namna alivyokuwa bingwa wa mapambano ya ana kwa ana. Pia alivyoweza kupambana na mtu mwenye silaha…. Hakika Steven alikuwa mwiba!
Kuhusu mtu yeyote kuweza kumuua kirahisi vile labda kwa kumnyonga ama kumpa sumu. Hili nalo akalifutilia mbali!
Angeweza kufa mtu mwingine kizembe namna ile lakini sio Steve!!
Gama alipingana kabisa na hisia za Steve kuuwawa kizembe.

Mara ghafla akayafikiria MAPENZI.
Na hapo akaketi kitako. Akajenga picha ya mfanyakazi mwenzake huyo ambaye tayari ni marehemu.
Akamkumbuka jinsi alivyokuwa anakosa raha pale anapokerwa ama anapomkosea mpenzi wake. Alikuwa anashindwa kufanya kazi kabisa na wakati mwingine hata kufanya chini ya kiwango!
Yawezekana mapenzi yamemuua Steven!! Gama alijisemea huku akitikisa kichwa chake kuuunga mkono hoja ile.
“Lakini mapenzi kivipi?” akajiuliza….
Akawafikiria baadhi ya wasichana ambao walikuwa wakijihusisha kimapenzi na Steve.
Mariam, Subira, Recho…..
Akayamaliza majina yote yale aliyokuwa akiyafahamu, akampa kipaumbele Mariam. Huyu ndiye alikuwa akitumia naye muda mwingi mara kwa mara kwa sababu Subira na Recho hawa walikuwa wake za watu hivyo ndoa zao ziliwakosesha muda wa kuwa na Steve mara kwa mara.
Lakini Mariam hakuwa ameolewa na mpenzi pekee aliyekuwanaye kiuwazi alikuwa ni Steve, penzi lilianza kwa kasi kubwa lakini baadaye penzi likashuka thamani, ikawa linapita hadi juma moja bila Steve kutoka na kwenda mahali na Mariam, lawama zikaanza na mwisho zikapoa. Mariam akawa hawezi tena kumwendesha Steve!
Sasa nani alikuwa akimwendesha?? Akajiuliza!
Huyu nd’o anayetakikana nijue nini kimemuua Steven Marashi!
Hapa kama si mapenzi basi kuna HILA zimefanyika, aidha Mariam alimuua kulipiza kisasi ama.. ama…..
Gama akakosa lolote la kutabiri!
Akajipa siku tatu za ziada mbele ili aweze kuanza rasmi kazi nzito kupita zote alizowahi kufanya. Kujua ni kipi kimemuua rafiki yake na kuna njama gani zinaendelea asizozijua!!
Kubwa zaidi kuhusu ripoti ya hujuma ambayo anaamini Steve alikuwa ama ameikamilisha ama alikuwa amekaribia kuikamilisha.
Gama akatabasamu kisha akajilaza tena. Wakati huu ni mwili na akili.
Akasinzia huku fikra ya mwisho kabisa akiwa amemfikiria mtu wa kufanya naye hiyo kazi.

*****

MIAKA MINNE ILIYOPITA

ILIKUWA imebaki miaka minne kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika tena. Chama tawala kilitarajiwa kusimamisha mgombea mpya baada ya yule wa awali kuwa anaelekea kumaliza miaka yake kumi kama katiba isemavyo hawezi tena kugombea. Anatakiwa kuwaachia wenzake.
Tofauti na miaka mingine ambapo mgombea anaandaliwa mapema kabisa. Lakini hii ya wakati huu ilikuwa kinyume kabisa. Wagombea wenye sifa walionekana kuwa wawili na wote walikuwa wenye nguvu sana hivyo likawa ni jukumu la chama tawala kufanya uchaguzi sahihi ili nchi iendelee kuwa chini ya utawala wao.
John Masele, waziri wa mambo ya ndani na nje ya Tanzania alikuwa ameitangaza nia yake mapema kabisa kuwa anataka kuingia ikulu. Wafuasi wake wakaanza kumuita raisi mtarajiwa, jina likazoeleka huku akionekana kukosa kabisa dosari yoyote ya kupata nafasi hiyo.
John Masele alikuwa akikubalika hata kwa wapinzani, alikuwa na sera za peke yake ambazo zililenga katika kumkomboa mtanzania kiuchumi, kiutamaduni na kifikra.
Raisi aliyekuwa madarakani hakufanana misimamo na Masele, hivyo alitambua wazi kuwa hataishi kwa raha tena wakati akiitwa raisi mstaafu. Alihofia bwana Masele anaweza kutumia utawala wake kumsababisha yeye aonekane hakuna lolote alilofanya wakati akiwa ikulu. Jambo ambalo kwake lilikuwa fedheha kuu.
Raisi akamshawishi, Mathias Obhare, waziri wa nishati na madini atangaze nia ya kugombea pia. Huku akimsisitiza kuwa asimuhofie Masele na siasa zake kwani yeye ana watu wenye ushawishi mkubwa na pia wenye pesa nyingi, hivyo watashinda.
Na hapo akamwambia kuwa mzee Matata atakuwa nyuma yake kuanzia hatua ya kwanza hadi ya mwisho watakapokuwa wakipongezana wakiwa ikulu huku yeye akiwa ni raisi.
Kumsikia mzee Matata pekee haikutosha kumshawishi Mathias kukubaliana na wazo la raisi. Kitu kikubwa kilichokuwa kinamkwamisha katika hilo ni ukaribu aliokuwanao kwa John Masele kuanzia chuo kikuu walipokutana, John akawa raisi wa chuo huku Mathias akiwa makamu wake. Ukaribu huu ukaunda kama undugu, na hatimaye wakajiunga na chama tawala.
Sasa John ni waziri wa mambo ya ndani na nje wakati yeye ni waziri wa nishati na madini.
Raisi anataka kuwafanya maadui kwa mara ya kwanza!!!
Mathias hatimaye anashawishika, waandishi wa habari wanaitwa katika mkutano.
Mathias Obhare anatangaza nia ya kuwania nafasi ambayo John Masele alikuwa anawania.
Kujitangaza kwa Mathias Obhare kulimshtua sana Masele, akajiuliza ni lini Obhare akawaza upinzani kama ule. Kwanza ni yeye alikuwa wa kwanza kumshawishi atangaze nia, in akuwaje sasa na yeye atangaze nia.
Si bure kuna kitu hapa! akajisemea
Na hapo akatambua wazi kuwa kuna hila imefanyika dhidi yake ili asiweze kuleta mapinduzi kwani alikuwa na misimamo tofauti kabisa na chama tawala japo naye alikuwa ndani yake.
Kwa utulivu kabisa akaamua kukutana na Obhare na kumshawishi asigombee nafasi ile kwa sababu kwa namna moja ama nyingine ingeweza kuwaingiza katika malumbano makubwa na kuutia doa urafiki wao. Akamsihi kuwa iwapo ataachia nafasi ile basi atamchagua kuwa makamu wa raisi kama walivyofanya wakati wakiwa chuo kikuu
Obhare hakutoa jibu palepale, akayafikisha yale yote kwa raisi.
Mtukufu Raisi akatumia huo mwanya kuanza kumchafua Masele mbele ya wananchi.
Akasambaza maneno makali kwa wajumbe juu ya uoga wa kushindwa alionao Masele pia akaelezea juu ya tamaa ya madaraka aliyokuwa nayo bwana yule.
Na hapo baraza la chama tawala likatangaza rasmi kuliondoa jina la waziri wa mambo ya ndani na nje katika kinyang’anyiro kile.
Fukuto likaanzia hapo!

Baada ya juma moja, jambo jingine kubwa likazuka.
Mathias Obhare akatekwa na kuibiwa gari lake kisha akapigwa sana. Kipigo kilichosababisha akimbizwe Afrika kusini upesi kwa ajili ya matibabu.
Zikasemekana ni hila za Masele baada ya kuzidiwa kete na mpinzani wake kisiasa.
Baraza likaketi tena na kumweka kitimoto Masele ambaye alikataa kata kata kujihusisha na tukio lile, huku akisisitiza kuwa amebariki bwana Obhare kuwania kiti kile.
Lakini maneno yake hayakutosha kutengua kilichokuwa kimepangwa tayari.
Akiwa ameketi nyumbani na familia yake, mara akaisikia taarifa ya habari kuwa Raisi amemvua nyadhifa za uwaziri wa mambo ya ndani na nje….. huku sababu kuu ya kufanya vile ikisemekana ni kwa maslahi ya wananchi na sio chama.
Jina la Masele likazidi kuchafuka huku Mathias Obhare akianza kukaa katika damu za raia wema.
Wachache wenye kujitambua walihisi kuna jambo linatokea hapo katikakati. Lakini hawakuwa na pa kusemea.
Lakini mtanzania mmoja ambaye alikuwa masomoni nchini uingereza alitamani sana amalize masomo yake ili aweze kuingia katika upelelezi juu ya kipi kinachotokea maana naye alitilia mashaka matukio yale mfululizo.
Huyu alikuwa ni Steven Marashi, mwanausalama wa taifa aliyekuwa ameenda kuongeza elimu yake nchini uingereza.
Akiwa huko akajiunga katika vikundi vya kiafrika vya kucheza ngoma na kufanya michezo ya majukwaani, fani aliyokuwa akiipenda tangu utoto wake alipokuwa shuleni.
Fani ikanoga na kung’ara zaidi katika ukubwa wake.
Aliporejea nchini Tanzania, akaingia rasmi katika sanaa ya maigizo.
Ungeanza vipi kujua yule bwana alikuwa mwanausalama wa taifa na mpelelezi aliyekubuhu?
Safari ikaanzia hapo!!!
Alipojiunga na sanaa mtu mmoja tu ndiye aliyejua ni kwanini anajiunga katika sanaa, huyu alikuwa ni rafiki yake kikazi na hatimaye hadi mtaani wakawa marafiki na kushirikishana mambo yao mengine.
Alikuwa ni Yakubu Gama, zao la usalama wa taifa lenye asili ya Naijeria lakini mwenye uraia halisi kabisa wa Tanzania kwa kuzaliwa.
Na baada ya miaka minne Steven anakufa katika mazingira ya kutatanisha!!!
Na baada ya kifo chake mambo mengi yanajitokeza hapo katikati, Gama hakupata hata fursa ya kuonana na Sam yule mwandishi ambaye alikuwa rafiki wa karibu sana wa Steve!
Hadi usiku ule aliokwenda kumwekea dhamana.
Dhamana iliyotoka wa mtukufu raisi moja kwa moja, kupitia amri ya IGP.
Dhamana iliyokuwa na makusudi ndani yake!
Kuna kitu kilikuwa kinatafutwa na Sam alidhaniwa kuwa anaweza kuwanacho ama kuwezesha kupatikana kwacho!
Ni kitu gani hicho?
Hili swali linabaki katika kichwa cha Yakubu Gama ambaye yu hai sasa lakini akiwa amejeruhiwa!
Yakubu Gama anaapa kuwa atapeleleza hatua kwa hatua hadi ajue ni kitu gani kilimuua Steve! Huenda katika utafiti huo akatambua pia ni nani anayeitwa BVB.

****
 
Back
Top Bottom