mtzmweusi
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 8,596
- 8,878
- Thread starter
- #21
HEKAHEKA - 12
Bob nilikuambia kuwa Jacob Matata si mtu wa kumchukulia mzaha hata kidogo. Ona sasa inaonesha ameshafanya upelelezi wa kutosha hapa kwenye kambi aliyokuwepo bila nyie kujua. Siju watu wako walikuwa wanafanya nini. Sasa ni lazima muongeze ulinzi kwenye ukanda huu, nami nitaongea na marafiki zangu walioko kwenye vyombo vya usalama ili wanisaidie kulinda upande huu” Mzee Harken Kalm aliongea kwa hasira huku ngozi yake ikiwa imebadilika na kuwa nyekundu utadhani nini. Muda huu mzee huyu anaongea na Bob Sepeto mkuu wa walinzi wake, ilikuwa ni saa saba usiku. Hali ndani ya kambi hiyo ilikuwa shwari kabisa. Lakini si kwa upande wa walinzi na wana usalama wote wa kambi hiyo. Kwani dakika chache zilikuwa zimepita tangu pale yule mtu aliyekuwa ameuawa na Jacob na maiti yake kuwekwa kwenye mtumbwi ufukweni mwa bahari ilikuwa imeonekana. Hali hii iliwafanya watu hao wawe katika kutafuta wakidhani Jacob bado alikuwa maeneo hayo. Kilichowatia kiwewe zaidi ni ile salamu waliyoikuta imeandikwa kwenye mwili wa marehemu. Maandishi hayo yalisomeka hivi; ‘Jacob anasema siku zenu zinahesabika’ Kwa kumbukumbu alizokuwa nazo mzee Harken Kalm, hakuwahi kutishiwa na yeyote na wala hakuwa anapenda hiyo itokee. Leo ilikuwa ni mara ya kwaza, tena la kutia aibu ni kutoka kwa mwafrika mwenye umri mdogo, Jacob Matata.
Amri ya kutafutwa Jacob popote pale ilitolewa, huku yeyote ambaye angafanikiwa kumuua iliahidiwa kuwa angezawadiwa kiasi kikubwa cha pesa na mzee Harken Kalm.
*****
Dakika arobaini na tano zilipokatika ilikuwa kama wiki moja kwa Kalm, yalipokatika masaa mawili ilikuwa kama mwaka. Tayari alikuwa ameshakunywa mvinyo kiasi kikubwa. Muda ulikatika lakini pamoja na mzee Harken Kalm kusambaza vijana wake kila kona ya jiji hakuna aliyefanikiwa kumtia Jacob Matata machoni. Jitihada zilifanyika na maharamia hawa ili kujua yalipo makazi ya Jacob na nyendo zake. Wakuu mbalimbali wa usalama walitumika ili kujaribu kumuhujumu, lakini haikujulikana Jacob alikuwa akiishi wapi.
Kwake yeye maisha yalikuwa yakiendeshwa kama kawaida tena bila ugumu wowote. Alikuwa akiishi kwenye nyumba iliyokuwa ikilindwa masaa ishirini na nne na vijana wauaji wa mzee Harken Kalm. Walikuwa wameshajua nyumbani kwake na kwa hivyo muda wote walikuwa wakipalinda wakitegemea kumuona Jacob akija hapo.
Ni kweli Jacob alikuwa akilala ndani ya nyumba hiyo siku zote kwani ndiye aliyewapokea siku ya kwanza walipokuja. Walipokuja nyumbani hapo siku ya kwanza, vijana hao katili walimkuta mzee mmoja aliyekuwa amevaa miwani myeusi. Pasipo kujua kuwa ndiye Jacob Matata, walimuuliza yeye ni nani katika jumba hilo. Kwa vile Jacob alitegemea kuwa jamaa hao wangefika hapo alikuwa ameshawaandalia jibu la kuwaridhisha na kuwafanya wasione umuhimu wake na kumwacha kama mzee aliyekuwa amepewa hifadhi katika nyumba hiyo.
Jamaa hao hawakuwa wakiacha nyumba hiyo ibaki bila kuwa na mtu wa kuhakikisha kuwa Jacob asingeingia bila wao kuwa na taarifa. Mara zote alipouliza kama Jacob alikuwa ametokea, Bob Sepeto alipata jibu la kuwa “ ….hapana, isipokuwa yule mzee mwenye miwani myeusi ndiye ameingia kulala…” Hivyo alikuwa akiwadhihaki mara zote ambazo walikuwa wakikutana nae bila wao kumtambua.
Baada ya muda fulani Jacob akawa amefanikiwa kujenga urafiki na mmoja wa vijana wa mzee Harken Kalm. Kijana huyu alijulikana kama Ikwagama Zulu, mwenye asili ya Afrika ya kusini. Jacob alifuatilia na kugundua kuwa Zulu na wenzie walikuwa wakipenda kula kwenye mgahawa wa Jeff Inc fast food. Hivyo Jacob akionekana katika sura yake ya kizee akawa anapenda kwenda pale. Mara kwa mara gari la akina Zulu na wenzake ilipokuwa ikiegesha aliifuata na kujifanya kuomba msaada. Zulu akawa ni mwenye huruma kuliko wenzake kwa kuwa anapenda kuongea na mzee huyu ombaomba. Kwa tabia hii wakajikuta wakawa wameshajenga urafiki wa muombaji na mtoa msaada, huku wakiwa wamepeana majina ya babu na mjukuu.
Jacob alipoona ameshazoea sauti na matendo kadhaa muhimu ya Zulu, siku moja alijifanya kumtaka chemba ili ampe habari muhimu. Walitoka ndani ya mgahawa na kuelekea upande wa nyuma kwenye kichohoro. Ghafla Zulu alishangaa kumuona mzee huyu akiwa kabadilika na kuanza kumpa mapigo makali ambayo hayakuchelewa kuuchukua uhai wake. Baada ya kumuua zulu, Jacob alimvuta mpaka sehemu fulani ambapo alitoa kizibo cha tanki moja la kuhifadhi taka za chooni toka nyumba fulani ya jirani. Hapo aliuvuta mwili wa Zulu na kuutumbukiza humo. Alifunika tanki hilo na kuingia kwenye kona moja ambapo alitoa kikoba chake na kuvaa sura fulani aliyokuwa ameshaiandaa usiku uliopita. Alibadilisha nguo na kuvaa zile alizokuwa amemvua Zulu kabla hajamtumbukiza kwenye tanki. Hapo akawa ameshabadilika toka sura ya mzee ombaomba na kuwa Zulu mlinzi wa mzee Harken Kalm. Alifungua kikoba alichokuwa nacho, humo hakuhitaji chochote kikubwa zaidi ya vikasha kadhaa vilivyokuwa na ngozi za sura za bandia. Alivifutika vitu hivyo sehemu aliyijua yeye katika mwili wake. Kisha akachukua silaha alizokuwa amempora Zulu na vitambulisho vyake. Huyo akarudi pale alipokuwa amewaacha wenzie na Zulu. Mambo yote hayo yalifanywa na Jacob Matata kwa kasi na umakini mkubwa na hivyo kumchukua dakika chache tu.
Kwa Jacob aliona ametumia dakika chache, lakini haikuwa hivyo kwa wafanyakazi wenzie na Zulu. Kwa masharti ya kazi yao, mnapokuwa sehemu kwa kazi maalum hairuhusiwi kuwa mbali na wenzio bila sababu maalum. Hii ilifanyika hivyo ili kuondoa uwezekano wa kuhujumiana au mtu kutekwa pasipo wenzake kujua. Hivyo kiongozi wao hapo tayari alikuwa amewasiliana na Bob Sepeto mkuu wao na kumtaarifu juu ya lile lililokuwa limefanywa na Zulu siku hiyo.
Hivyo wakati Jacob alipokuwa anafika ili kujiunga tena na walinzi hao akiwa katika sura ya Zulu, ni wakati huo huo ambao watu wanne toka kwa Bob Sepeto walikuwa wameshawasili eneo hilo kumchukua Zulu. Kitendo cha Zulu kutokuwa na nidhamu na kutoweka bila taarifa katika wakati mgumu kama huu kilimchukiza sana Bob Sepeto. Kwa kuzingatia sifa za Jacob na utaalamu aliokuwa ameusikia hakumuamini tena Zulu. Hivyo alikuwa ameshatuma watu wake ambao ni maalum kwa kuua wafanyakazi wasio waaminifu. Hivyo wakati Jacob anafika kwa lengo la kwenda kuwahadaa wale watu na kujifanya kuwa ndiye Zulu, tayari wauaji toka kwa Bob Sepeto walikuwa wakimngojea tayari kwa kumuua.
Jacob alipoingia kwenye mgahawa alielekea pale walipokuwa wamekaa wenzie na Zulu, alipoangalia hakuona mtu. Kwa haraka sana alizungusha macho hapa na pale bila kuona yeyote kati ya wale jamaa. Ndio hakuona yeyote kati ya wale, lakini aliona kitu. Aliona macho ambayo kwa utaalamu aliokuwa nao aligundua kuwa yalikuwa na kila dalili ya hatari. Mbaya zaidi ni pale Jacob alipogundua kuwa macho hayo yalikuwa yakimfuatilia yeye kwa usiri mkubwa.
Ili kuhakikisha kuwa watu hao walikuwa mahali hapo kwa sababu yake, Jacob aligeuka na kujifanya kama vile anaelekea nje. Alitembea kwa hadhali kubwa huku mkono wake akiwa anaupeleka tayari kwa kutumia bastola yake.
Hawa ni nani tena, na wamejuaje kuwa ni mimi? Jacob alijiuliza huku akiwa tayari ameshafika mlangoni. Hakuwa na hakika kama watu hao walikuwa wanamtafuta kama Jacob au kama Zulu ambaye sura yake ilionesha hivyo. Alikuwa ameshatoka nje na kutaka kuvuka barabara, mara akasikia vishindo vya mtu aliyeonekana alikuwa akija kwa haraka. Alipotaka kugeuka akaona gari moja ikija kwa kasi upande ule aliokuwa amesimama. Hapo akajua kuna jambo na mambo yameiva.
Alikuwa na uwezo wa kuruka mapema lakini hakufanya hivyo kwa sababu moja kubwa, alitaka kuwafundisha hao jamaa. Gari ilikuja kwa kasi pale alipokuwa amesimama. Nusu sekunde baadaye eneo hilo lilindima kwa mlio wa breki ya gari hilo huku watu wakipiga kelele za hofu.
Wakati gari inafika miguuni Jacob alishahisi kuwa kulikuwa na mtu nyuma yake. Kwa wepesi wa ajabu alijipindua na kuruka hewani kwa kurudi nyuma. Wakati anatua tayari alikuwa upande wa nyuma wa yule mtu aliyekuwa ameinama nyuma yake, alimsukumia kwenye taili za gari ambalo taili zake zililalamika kwa kitendo cha dereva kujaribu kumkwepa mwenzie. Wao walitegemea Jacob ndiye angekuwa akisubiri taili imsage, lakini dereva alichanganyikiwa kuona kuwa mtu waliyetegemea kummaliza alikuwa ameruka kwa staili ambayo alikuwa hajawahi kuona na wakati huohuo akamsukumia jamaa yao kwenye mataili.
“Mmalizeni!!! Dereva wa gari lililokusudia kumgonga Jacob alipiga kelele. Wakati ukulele huo ukiishia hewani, risasi zilimiminika kuelekea pale alipokuwa amesimama Jacob. Kwa mshangao zilikuta hewa, kwani Jacob alikuwa amewahi na kujiviringisha chini. Bado akiwa anaviringika chini Jacob aliachilia risasi mfululizo ambazo ziliwamaliza jamaa wote.
Itaendelea kesho ama baadae inategemea tu.