Skythelimit
Member
- Jul 19, 2023
- 27
- 53
SEHEMU 1
Hapo zamani za kale enzi za akina nabii mfalme Daud huku Israel kulikuwepo na nabii mmoja kwenye himaya ya Uingereza aliyekuwa akijulikana kwa jina la nabii Johnson Petersburg (45) alimaarufu kama “sababu ya kifo” au jina lingine alikuwa akitambulika kama “mpasua vichwa”. Hii ni historia yake kabla hajawa nabii na namna alivyokuja kuwa nabii mkubwa kwenye zama zake hapo Uingereza.
Johnson Petersburg akiwa juu ya farasi amesimama alikuwa akitafakali ni kwa namna gani ataenda kukiteketeza kijiji cha West Norwich. Sababu ilikuwa kusemekana kijiji hicho kulea vijana chokoraa sana ambao hugeuka kusumbua watu wanapopita mtaani hapo. “Hivi hawa vijana wa huu mtaa wananifahamu kweli!? Dah… watajuta!” Mpasua vichwa alijisemesha hayo akiwa anaweka shoka yake vizuri kiunoni na kuamuru farasi yake kuondoka kuelekea kijiji cha west Norwich.
Mitaani west Norwich kulionekana vijana wasumbufu zaidi ya kumi wakileta fujo sokoni kwa wateja waliokuwa wakinunua mahitaji. Skatel “ we dada leta hiyo burger hapa unajua matumizi yake!” Skatel aliekuwa miongoni mwa makundi ya vijana hao akamunyanganya hiyo burger Jennie. Vijana wengine wakawa wanawapiga baba mmoja na mke wake na wakamnyanganga kikapu chake, akawaambia “Lakini vijana jambo hili mnalofanya jueni sio vizuri”
“utatufanya nini?”
“fanyeni yote ila msimuguse mke wangu”
Ahaa!.....ahaaa! Vijana hao wakacheka kwa kebehi huku wakimsukuma mke wa bwana huyo huko chini na kuaendelea kupiga huyo bwana huku wakichukua mikufu na mikate aliyokuwa nayo. “unaleta ujuaji hapa kula hiyo” maneno hayo aliyasema Raul huku akimsindikiza bwana huyo kwa buti kali la tumboni.
“haaa! Hu si uhungwana kutupigia wateja wetu”
“Jacob embu tulia ndugu yangu hawa vijana wana fujo sana” wauzaji wa sokoni walikuwa wanasemezana pembeni ya akina Jacob.
Jacob akawasikia na kuwafata “nyie wapumbavu mnasemajee!” kabla Jacob hajawarushia ngumi, malangoni kwa soko hilo akaanza kuona vijana wenzake watukutu wakishushiwa kipigo kizito. Mpasua vichwa Johnson alikuwa ameshaingia eneo hilo na anashusha kipigo kizito kwa hao vijana.
“kwenchi ninyi ebu kujeni hapa!” Johnson aliwaita hilo kundi la hao vijana likiongozwa na Skatel. “ hoya embu chomoa hizo panga” amri kutoka kwa Skatel akimuamuru Rogers kufungua mkeka uliokuwa na siraha zao za majambia. “hoya shika hilo” Rogers aliwarushia majambia kila mwanachama wake ambapo walikuwepo vijana kama kumi na tano. Johnson akachomoa kishoka chake kutoka kiunoni ili awaponde vichwa vyao. Haikupita dakika tano Johnson kuwa amewamaliza hao vijana kwa kipigo kizito kama kumsukuma mlevi, huku akipasua vichwa vyao kwa mikono na kishoka chake.
“Nini sasa huyu mpuuzi anafanya ndugu zangu anaua vijana wetu angali sisi tunamuungalia” baba yake Skatel uvumilivu ukamshinda alipoona mwanae kauwawa na Johnson. “Haiwezekani hao ndo vijana wanautulinda eneo hili kwa nini kawafanyia unyama huu!?” mfanyabiashara mwenzake na baba Skatel akarukia mada na wauzaji ndani ya soko hilo wakacharuka “hili haliwezekani” “hili haliwezekani” wafanyabiashara hapo sokoni hasa wanaume wakachukua visu ili wakapambane na bwana Johnson Petersburg.
Johnson akasema “sawa damu za mapuku yenu zinawita… uhh! Kujeni hapa”
Inaendelea.......