Riwaya:Hatia

Riwaya:Hatia

HATIA--06

Na George Iron

Geti dogo lilifunguliwa kidogo, baada ya kuhakikisha aliyetegemewa kuingia ndiye alikuwa mlangoni lilifunguliwa zaidi.
“Mheshimiwa Mapulu!!!! Karibu nyumbani…..kama ndoto vile” sauti nzito ya kiume ilimlaki John aliyejibu kwa tabasamu hafifu.
“Matha yupo au na yeye alikamatwa??” John aliuliza wakati huo ilikuwa yapata saa kumi adhuhuri.
“Matha yupo lakini anakamuliwa na mshkaji mwingine” Alijibiwa kwa njia ya utani akaling’amua hilo akatoa kicheko kidogo.

“Dogo langu hili, linaitwa Michael Msombe muite Dabo M,ukishindwa kabisa muite Dabo” John alimtambulisha Michael kama mtu ambaye anamfahamu siku nyingi sana. Jina lake likageuka na kuwa Dabo.
“Mambo vipi bro!!!” alisalimia Michael MsombePoa Dabo naitwa Bruno…karibu sana”

“Asante sana” alijibu na geti likafungwa.

Haikuwa nyumba iliyotangaza umasikini hata kidogo lakini ilionyesha matumizi mabaya ya pesa kwa samani zisizokuwa na shughuli maalumu kulundikana pale ndani, usiku ule hakuona mtu yeyote zaidi ya Bruno akahisi huenda wamelala wengine lakini haikuwa hivyo hadi panapambazuka hali ilikuwa hivyohivyo.
Michael alishangaa lakini hakuuliza. Asubuhi yule John wa selo aliyekuwa akishindia kapensi kafupi kalikochakaa na wakati mwingine kumwacha uchi wakati akigombania vyakula walivyoletewa mahabusu wengine hakuwa yule tena alikuwa ameng’ara ndani ya nguo ya kulalia rangi nyeupe kabisa mkononi alikuwa na kikombe kikubwa kilichoongezwa uzito na maziwa yaliyokuwa ndani yake. John alikuwa tofauti sana hata rangi yake ilikuwa si ile iliyochafuka na kukosa maji ya kuoga walipokuwa selo.

“Michael kuna mtu yeyote aliyekuwa anafahamu uwepo wako ndani ya selo??.”

“Mh!!!! Hapana sidhani” alijibu baada ya kujaribu kufikiri

“Una uhakika kuwa hujawahi kuja kusalimiwa???”

“Hakuwahi kuja mtu yeyote pale kaka, we ulikuwa shahidi” aliendelea kusisitiza. John alitikisa kichwa ishara ya kukubali kisha akaifuata rimoti na kuitazama luninga kuubwa bapa iliyokuwa inamtazama kisha akaminya kitufe ikawaka, hakujishughuisha kuangalia ni chaneli ipi iliyokuwa inaupiga mziki wa zook, akajiondokea.
“Michael!!! Una uhakika na unalosema???” aliuliza tena macho yake mekundu yakiwa yanautazama mdomo wa Michael.
Swali hilo likamshtua Michael kwa nini lilikuwa likiulizwa sana, safari hii akachelewa kidogo kujibu

“Siku ile nilimpa namba za msichana mmoja yule afande sijui kama alipiga ama la lakini hakuwahi hata kuja pale mahabusu.” alijibu kwa sauti iliyokuwa na hofu

“Nipe namba ya huyo msichana na kuwa makini sana wakati mwingine unapojibu swali sawa!!!” alifoka kidogo John na Michael akakubali bila kuzungumza chochote. Baada ya kumtajia akaondoka, jambo la kushangaza ni kwamba John akuuliza mara mbilimbili na wala hakuandika hiyo namba mahali popote pale, ni kama alikuwa ameipuuzia hata Michael aliamini hivyo.
Siku hiyo ilipita huku Michael akipewa nguo za kubadilisha ambazo zilimkaa sawa kwenye mwili wake, japokuwa alikuwa na mawazo sana hakusita kukiri kwamba aliifurahia hali ya kuwa huru.

****

Majibu ya askari aliyekuwa na wasiwasi mkubwa machoni mwake yalimkera na kumshangaza sana Joyce Keto, alishindwa kuelewa kwamba ni kweli aliyezungumza naye kwenye simu alikuwa ni askari ama ni mtu alimletea utani. Kwa ghadhabu aliondoka kituoni pale.
Kwa nini nisimpigie simu huyo aliyejifanya askari!!! Alijiuliza Joyce huku akitembea kwa ghadhabu hakuwa na uhakika kama alikuwa akiyumba yumba ama la alichotambua ni kuwa alikuwa akisonga mbele. Moja kwa moja katika duka lililokuwa linauza vocha.

“Nisaidie Tigo ya mia tano!!” alisema Joy na mwenye duka akampatia baada ya kuwa ameisugua. Bila ya kujua ni mara ngapi alikuwa ameingiza ile vocha bila kuwa na umakini aishtushwa na ujumbe uliomtaarifu kuwa namba yake ilikuwa imefungiwa kutokana na kuingiza namba zisizokuwa sahihi, Joy alitamani kulia, aliitazama simu yake kwa jicho la hasira kama ni yenyewe ilikuwa imefanya makosa hayo ili kumkomesha. Kwa mwendo wa kukata tamaa akaanza kuondoka lakini akasita tena na kurejea dukani.

“Makao makuu ya tigo ni wapi, samahani lakini!!!”

“Bila samahani malkia!!....” alizungumza kwa lafudhi ya kichaga na kisha akamuelekeza Joy wapi ambapo kampuni hiyo ya simu imeweka makao yake.

“Asante sana….kwaheeri!!!” aliaga. Mwanzoni wazo lake lilikuwa kuondoka moja kwa moja na kuelekea hapo alipoelekezwa lakini njaa ilimkatisha kufanya hivyo, jicho lake liliangaza huku na huko kisha akajifikiria kwa muda pesa aliyokuwa nayo ilimruhusu kula wapi jibu likapatikana kuwa alitakiwa kula chakula cha bei poa sana ili mambo yaende sawia. Mama Fredi mgahawa jipatie chakula safi hapa.
Maandishi hayo yaliyoandikwa kwa mkaa yalimfanya Joyce atabasamu kisha akajiambia “Mahali sahihi pa Joyce kupata chakula chake kwa siku ya leo.” akanyata na kuingia kwa mtindo wa kuinama hadi akapata nafasi yake. Bila hata kutaja ni chakula gani alikuwa anahitaji alishangaa mbele yake ukiwekwa wali uliochanganywa na maharage, nyama moja, mchicha na kipande kidogo cha bilinganya, hakutaka kuhoji aliamini huo ndio utaratibu wa mgahawa wa mama huyo aliyekuwa muongeaji sana. Huenda hata ndio sababu ya kuvuta wateja wengi sana katika genge lake.
Baada ya kujiridhisha nafsi yake na chakula hicho kilichomgharimu shilingi elfu moja Joyce Keto alinawa mikono yake na kuondoka.

“Ngoja niandae mahali pa kulala kwanza maana dalili zote zinaonyesha kuwa nitalala Mwanza, na huu ugeni nisije nikapata tabu baadaye.” alijishauri na kukubali ushauri huo akaanza kuhangaika huku na huko hadi alipopata nyumba ya kulala wageni iliyomgharimu shilingi elfu kumi ikiwa na choo na bafu ndani.
Hakudumu sana katika chumba hicho baada ya kukizoea kwa dakika kadhaa wazo la kurejea tena Tigo lilimrudia, lakini kabla ya yote alijiweka maliwatoni na kuupasha mwili wake kwa maji baridi nguvu zikamrejea na uchangamfu ukachukua nafasi yake. Kosa dogo alilofanya Joyce liligeuka kuwa kubwa, ni baada ya kujiegesha kitandani na usingizi kumpitia. Alikuja kushtuka jioni ya saa kumi na moja.
Tayari huduma alizotaraji kuzipata tigo hazikuwezekana palikuwa pamefungwa tayari.
“Hee!! Saa kumi na moja.” alipayuka kwa nguvu akiwa pale kitandani lakini hakuwepo wa kumjibu hoja yake iliyokuja kwa mtindo wa kushtukiza. Alisimama kama anayetaka kuondoka ili awahi kitu lakini alirejea kivivu pale kitandani hakuwa na pa kwenda. Alijilaza pale alipotoka na kumkaribisha tena jinamizi wa usingizi lakini kabla hajachukua kiti na kuketi simu yake ya mkononi iliita. Ilikuwa namba mpya!! Mh!! Atakuwa mama yake Michael ama…sasa kwa nini atumie namba mpya…au!!!” alijiuliza bila kupata majibu, simu ikakatika!! Mara ikaanza kuita tena
“Hallo!! Mambo vipi dada Joy” upande wa pili ulianza kubwabwaja
“Poa nani mwenzangu samahani nilipoteza….”
Mimi Fredrick, haunifahamu lakini” ilimkatisha sauti ile baada ya kueelewa kuwa alitaka kujitetea kwa kudanganya.
“Wa wapi wewe??”
“Mwanza nimepewa namba yako na Michael yupo matatizoni, umeenda kumwangalia polisi???” iliuliza sauti ile kwa utulivu
“Nimeenda lakini sijamkuta….”
“Wamekwambiaje kwani??”
“Wamesema tu hayupo mi nikaondoka zangu”
“Dah!! Hata sisi wametwambia hivyo..wewe upo wapi sasa maana sisi wenyewe wageni hapa Mwanza”
“Mimi pia mgeni lakini nipo hapa Mitimirefu sehemu inaitwa Resting house, ukishuka tu hapa kituoni unapaona nadhani panafahamika” alijieleza Joy huku akiwa na furaha ya kupata wenzake katika vita moja.
“Haya kama tukiweza tutafika, kwa lolote lile tufahamishane sawa!”
“Msijali nitapenda sana mkija” alisisitiza Joy. Simu ikakatwa.
Baada ya saa zima akiwa anafanya tafakari mbili tatu alishtushwa na mlango wa chumba chake kugongwa kwa utaratibu maalum.
“Nani tena muda huu!!!” alijiuliza huku akiuendea mlango na kuufungua.
“Una vitu vingine zaidi ya huo mkoba mezani??” lilikuwa swali kutoka kwa sura hizi mbili ngeni kabisa machoni mwa Joy.
“Nyie ni akina nani??” aliuliza lakini hakujibiwa.
“Tuondoke haraka eneo hili” aliambiwa
“Twende wapi…nyie ni akina nani???”
“Ndugu zake Michael, chukua vyako tuondoke”. Joyce akatii amri na kukusanya vilivyo vyake na kuanza kuondoka hadi kwenye gari ndogo aina ya corolla safari ya kuelekea asipopajua ikaanza.
“Shem ujue nini yaani hii hali inashangaza sana mh!! Kumbe kweli anayekwenda jela si lazima awe na hatia…” baada ya kimya alikuwa ni John ambaye alikwa anajulikana kwa jina la Fredrick aliyeuvunja ukimya pale ndani. Mh!! Nimekuwa shem tayari!! Alijiuliza Joyce na kumalizia kwa tabasamu la kulazimisha bila kusema lolote.

Baada ya mwendo kidogo John alitoa pipi na kuwagawia wote waliokuwa pale ndani, ni Joyce pekee aliyekurupuka na kuibugia pipi ile, baada ya sekunde kadhaa usingizi mkali ulianza kuyafumba macho yake alijaribu kupambana bila mafanikio kuidhibiti hali ile, dhahiri alionekana kutambua janja hiyo iliyokuwa imechezwa dhidi yake lakini haukuwepo ujanja wowote ule Joyce akapitiwa na jinamizi la usingizi mkali sana.
Alikuwa amewekewa dawa za usingizi katika pipi!!!.
Alikuja kushtuka masaa manne baadaye na kujikuta katika chumba kikubwa cha haja ambacho kilikuwa na hewa safi sana yenye ubaridi bila shaka palikuwa na kiyoyozi.
Joyce alijinyoosha nyoosha huku akiyapikicha macho yake ili kujiweka sawa. Hapa ni wapi?? Alijiuliza, lakini kabla ya kupata jibu alisikia mlango ukifunguliwa kisha akaingia John ambaye alijitambulisha kwa Joy kama Fredrick.
“Mambo vipi Joy naitwa John….jisikie huru upo nyumbani” John alijitambulisha kwa Joy ambaye bado alikuwa anashangaa.
“Nimefikaje hapa….hapa ni wapi??” aliuliza Joyce, John ambaye alikuwa amevaa pensi pamoja na fulana kubwa iliouzidi mwili wake huku miguuni mwake akiwa na raba nyeupe.
“Hapa ndio nyumbani kwetu karibu sana” alisema John huku akiachia tabasamu hafifu.

*****

Michael Msombe alikuwa ametekwa na sinema aliyokuwa anaangalia katika luninga kubwa iliyokuwa sebuleni, hakupatwa na ukiwa wowote kwa kuondoka John na Bruno. Mdadi ulikuwa umemshika pale jambazi kuu lilipokuwa likipigwa na nyota wa filamu hiyo ambaye alikuwa ni Jackie Chan, Michael alikuwa ni kama amezama na kuwa mmoja wa wahusika wa filamu hiyo hadi pale aliposhtuliwa na kikohozi cha kujilazimisha kutoka katika upande wa mlango wa kuingilia.
Macho yake yalihama kutoka katika luninga na kuelekea pale mlangoni.
Alikuwa ni msichana ambaye hakuna mwanaume ambaye angesita kumuita mrembo, nguo fupi aliyokuwa amevaa iliyaruhusu mapaja yake meupe kuchungulia nje, wepesi wa kitambaa cha nguo hiyo ulionyesha mchoro wa chupi aliyokuwa amevaa ikiwa katika mfumo wa bikini, kinguo cha juu saizi ya mtoto wa miaka minne kilihalalisha nusu ya tumbo lake kuwa nje. Matiti yake kifuani yalikuwa na uwezo wa kukinyanyua kinguo hicho kwa umbali mdogo sana huku ule mchomo wa mbele ukionekana kumaanisha kamwe hajawahi kunyonyesha.
Sauti ya Michael ilipotea kabisa akajaribu kuilazimisha irejee ili aweze kumsalimia huyu kiumbe lakini iligoma kabisa.
“Mambo!!!!” alisalimiwa Michael kwa sauti laini sana iliyopenya katika masikio yake kisha katika koo na kuilainisha sauti yake hatimaye akajibu
“Safiii….karibu!!!” yule binti akaanza kusogea mahali alipokuwa ameketi Michael akimaanisha ameitikia wito, sehemu zake za nyuma zilikuwa zinatikisika kila hatua aliyopiga. Bila kutambua Michael akajikuta ameingia katika hisia nyingine na maungo yake kujikuta yakiinyanyua suruali yake, kwa haraka sana alichukua kitambaa kilichokuwa mezani na kujifunika lakini alikuwa amechelewa sana. Tabasamu zito kutoka kwa yule binti lilimpumbaza akabaki kama zoba.
“Naitwa Matha….unanifahamu sijui???...lakini haunifahamu”
“Yeah!! Sikufahamu nadhani”
“Ni mchumba wa John..unamjua??”
“Ndio John namjua!!!”
“Wewe unaitwa Michael eeh!!!”
“Umenijuaje kwani???” badala ya kujibu Michael aliuliza huku macho yake yakiendelea kumchunguza kwa chati binti huyu.

Matha Mwakipesile alikuwa amepewa jukumu kubwa la kumfundisha Michael jinsi ya kutumia silaha mbalimbali, John alikuwa ameamua kumchukua rasmi Michael katika shughuli zake za ujambazi.
Matha alimueleza Michael kwa utaratibu kabisa jukumu alilopewa, hali ya Michael iligeuka kuwa ya uoga sana hakuamini kuwa binti mrembo kama Matha anaweza hata kuwa na uwezo wa kushika bunduki sembuse kisu na kuua mtu. Mh!!! Usione ukadhani. Alisema kimya kimya Michael. Somo alilopewa na Matha halikuwa limemuingia hata kidogo, aliamini sasa alikuwa anapelekwa njia asiyoitaka hata kidogo. Kutoroka!!! Ndio wazo kuu lililomjia lakini atatoroka na kuelekea wapi. Akiwa bado katika mawazo hayo mara aliingia Bruno alikuwa mwingi wa furaha iliyojionyesha waziwazi, alimsabahi Michael kisha akaingia chumbani na kurejea tena baada ya muda mfupi akiwa amebadilisha nguo zake.
“Bruno nahitaji sana kwenda nyumbani, nimekaa hapa imetosha nadhani mama atakuwa akinitafuta sana.” Michael alimwambia Bruno baada ya kuwa amekaa kitako.
“John anakuja muda si mrefu utamweleza nadhani itakuwa vyema zaidi mi sijui lolote kuhusu wewe na John” alijibu kwa sauti iliyokuwa na uulizi ndani yake, Michael akatambua kuwa Bruno ameshtuka.
Baada ya masaa kadhaa John alifika na baada ya kuzungumza pembeni na Bruno alimfuata Michael.
“Nimeambiwa ombi lako si baya sana, lakini kabla sijakuruhusu naomba nikukumbushe kitu, unakabiliwa na kesi ya kumuua askari pale kituoni, una kesi kubwa ya kutoroka mahabusu hivyo umehalalisha kuwa ni wewe uliyemuua binti uliyekuwa naye nyumba ya kulala wageni, hizo ni kesi chache za halali zinazokukabili sijui kama zipo za ubakaji na wizi kwa kutumia silaha…kwa ufupi unarudi mtaani kupambana na hukumu ya kunyongwa baada ya fedheha ya kufanywa mke wa mtu gerezani….kama unaamini unaweza kupambana na haya yote peke yako mimi nitakusaidia nauli kesho uende mdogo wangu hata usijali.” alieleza John huku macho yake yakiwa yameutazama uso wa Michael aliyekuwa anaukwepesha uso wake kila anapogundua kuwa John anamwangalia.
Baada ya kumaliza kuzungumza hayo John aliyanyuka na kuondoka zake akimwacha Michael akiwa ameduwaa. Neno alilokuwa akilirudia mara kwa mara John kuhusu kuolewa na wanaume wenzake ni hilo lilimsumbua akili Michael hakuwa tayari hata kidogo kwa hiyo fedheha. Macho yalikuwa yamemtoka pima, aliingiwa na hofu ya kutoroka kwa mara ya kwanza!!.
“John!!! Kaka John.” aliita Michael kwa nguvu wakati John akikaribia kutokomea.
“Sema dogo!!!”
“Naomba basi walau niwasiliane na mama najua ananitafuta sana mh!!.”
“Polisi sio wajinga kama unavyodhani…wewe unamuwazia mtu ambaye kwa sasa anawasaidia upelelezi wa kujua wewe ulipo??? Wewe kumuona mama yako haina tofauti na kuonana na polisi” alijibu John Mapulu kisha akacheka. Neno hilo nalo likamshtua Michael na kuamini kuwa lilikuwa na ukweli ndani yake na mama yake huenda anaweza kumsaliti.
“Kwa hiyo hata Joyce Keto anaweza kuwa anasaidiana na polisi?.” alijikuta akiuliza.
“Tena kwa ukaribu sana…nakutakia safari njema Michael” alifungua mlango na kuingia ndani.
Kesho yake hakuondoka!!!!!
Pabaya hapo!!
 
Kwahiyo hii ni episode 6 peke akee au 4 kwa 1 msitufanyie hivi jamani ebu zifupisheni

Asante sana jogoo. Ila Michael amejua kupatikana. Anafosiwa awe bad guy wakati hayupo hivyo
 
HATIA--07

Na George Iron

Moshi wa bangi na sigara vilianza kuizoea damu yake, sumu ya maneno aliyokuwa akilishwa na John Mapulu sasa ilikuwa imesambaa ndani ya damu yake, aliwaona watu wote wanaomzunguka kuwa ni maadui hasa hasa askari.

John alimwelezea Michael jinsi polisi wanavyoua raia wema hovyohovyo, alimpa mikasa mbalimbali ya kutisha hivyo kuikoleza hoja yake kuelekea kwenye ukweli. Taratibu Michael akaanza na sigara hatimaye akajiunga katika mkumbo wa wavuta bangi, kwa jitihada zote aliyapinga matumizi ya unga hilo pekee ndilo alilipigania hadi mwisho.

Mwanzoni alikuwa msindikizaji katika shughuli walizokuwa wakienda kufanya akina John sehemu mbalimbali katika jiji la Mwanza kila baada ya shughuli alipewa nafasi ya kuuliza maswali mawili matatu. Kwa kuwa Michael alikuwa mwingi wa maswali hii ilimuwezesha kuelewa mambo mengi sana katika kipindi kifupi mno.

Tayari alijua mbinu za kuvunja maduka, kuiba magari, na mbaya na kubwa somo la matumizi ya silaha lilikuwa limemkolea.

John Mapulu hakuwa mtu wa masihala linapokuja suala linalomuhusu moja kwa moja, jambo hili hata Michael alilitambua upesi sana kadri alivyokuwa akiishi naye karibu. Mahusiano yaliyokuwepo kati yake na Matha (mpenzi wa John) katika kufundishwa jinsi ya kutumia bunduki yalikuwa yameanza kuvuka kiwango, nafsi ya Michael baada ya kumtamani Joyce Keto bila mafanikio ya kumpata, Joyce mwingine aliyefariki bila kuwa ameelewa azma ya Michael, sasa Michael alikuwa anamtamani Matha japo pia alikuwa hajamwambia, kila siku alikuwa akijizuia na kuuonya mdomo wake usije ukamponza.

Aliamini kwa kumtamkia Matha kuwa anampenda ni sawa na kuanzisha vita na John Mapulu, vita kubwa ambayo wala hakuwa na ubavu wa kuicheza. Wakati fulani Michael aliamini Matha amewekwa karibu yake ili kumchunguza tabia zake hivyo alikuwa makini sana asiweze kuzionyesha hisia zake kwa mrembo huyu.

Matha hakuisha kumvalia nguo za mitego Michael kila wanapokuwa wawili katika chumba maalumu cha mafundisho hayo.

Siku hii jioni tulivu kabisa John na wenzake wakiwa wameingia katika tukio la kuiba pesa benki ambapo hawakutaka kuandamana na Michael kwa sababu ya uchanga wake katika masuala ya uharifu pia hawakuwa na mtaalamu wao wa kike Matha Mwakipesile aliyedai kwamba akili yake haikuwa barabara siku hiyo. Michael kama kawaida akiwa katika burudani yake ya kuangalia filamu, mwilini akiwa na pensi fupi na fulana iliyokatwa mikono alishtuliwa ghafla na ujio wa Matha pale ndani.

“He!! Mwalimu vipi….pole aisee nasikia unaumwa??.” Michael alimuanza Matha ambaye kwa sasa walikuwa wamezoeana sana.

“Mh!! Kakwambia nani??”

“Ah!! Nimesikia tu!!!” alijibu huku akisimamisha hiyo filamu kupisha maongezi yake na Matha.

“Ok!! Twende darasani” Matha alimwomba Michael naye akafuata bila ubishi, darasa alilokuwa akipewa na Matha lilimvutia kuipenda bunduki. Walipofika chumba hicho maalumu somo lilianza kama kawaida lakini hawakuchukua muda mrefu Matha akabadili hali ya hewa ya hapo ndani, ni wakati akimfundisha Michael jinsi ya kulenga shabaha akiwa kwa nyuma yake mkono wake wa kushoto ukiwa umekizunguka kiuno cha Michael, zoezi lilisimama ghafla baada ya wawili hawa kujikuta hawaitazami bunduki ila wanatazamana machoni wakiwa wametwaliwa na dalili zote za mahaba mazito.

Mapigo ya moyo ya kila mmoja yalikuwa juu sana, taratibu bunduki ikatuliwa chini, Matha kwa kuutambua uoga wa Michael yeye mwenyewe akajitoa muhanga kusogeza papi (lips) za mdomo wake hadi zikagusana na za Michael, akaupenyeza ulimi wake katikati ya papi za Michael na yeye akaupokea taratibu. Michael alikuwa anatetemeka sana lakini baada ya ndimi zao kukutana akauvaa ujasiri, hapakuwa na godoro pale ndani hivyo wakajikuta katika sakafu iliyokuwa na vigaye, kivazi alichovaa Matha ni kama alimaanisha kitu kwani baada ya kuanguka chini alikigusa nacho mara moja mikanda ikaachia wawili hawa wakawa katika ulimwengu wa mahaba mazito.

Matha yule ambaye ana uwezo wa kuua binadamu dakika yoyote ile katika mapambano sasa alikuwa amelala chali mshindi akiwa ni Michael katika kifua chake. Raha walizozipata waliweza kuzielezea wao peke yao maana hapakuwa na shahidi pale ndani zaidi ya mtutu wa bunduki. Hiyo ilikuwa ndiyo siku ambayo Michael kamwe hataisahau kwani ile hali ya kujiamni mbele ya John alihisi inapungua huku akihofia siri hiyo iwapo itavuja ni jinsi gani John atakisambaratisha kichwa chake.

Kwa upande wa Matha hakuonyesha mabadiliko yoyote, hakuwa na uoga hata chembe, na siku iliyofuata alifika hapo nyumbani kwa ajili ya kumfundisha Michael. Darasa likageuka ukumbi wa ngono, Michael alipewa onyo kali.

“Ukikataa tusiendelee kufanya nitamwambia John kuwa unanisumbua kimapenzi, usidhani kuwa atakuhoji kama ni kweli ama la…atakachofanya atachukua bunduki kama hivi na kukufyatua kichwa chako, kama akiwa na huruma sana atakuwekea sumu ufe usingizini….vipi upo tayari kufa??” Matha alimwambia Michael kwa sauti iliyojaa majivuno. Michael hakuwa tayari kufa hivyo akaingia rasmi katika utumwa wa ngono na mpenzi wa muuaji hatari, tena katika nyumba ya muuaji. Raha alizokuwa akizipata wakati wakipashana miili yao joto ilikuwa inayeyuka kila alipokuwa akimfikiria John siku akiugundua huo mchezo mchafu unaoendelea.

*****

“John leo nitampeleka huyu dogo kwa mafunzo ya shabaha kule pori!!! Usiku” Matha alimweleza John Mapulu ikiwa majira ya asubuhi baada ya kuwasili pale nyumbani kwa John.

“Vipi lakini uelewa wake anaweza kuingia mzigoni???” Badala ya kujibu naye aliuliza

“Kiaina lakini si wa kuingia mzigoni kwa sasa. Ni moto wa kuotea mbali akishaiva vizuri” Matha alimsifia Michael. Wakati huo na Michael naye alikuwepo pale sebuleni, hakutaka kumwangalia John wala Matha. John alianza kudhani Michael ameogopa sana kusikia habari za porini usiku, wakati Matha alijua kwa nini Michael hakutaka kuwatazama usoni.

Msichana gani huyu hana hata chembe ya aibu!!! Aliwaza Michael.

“Kwa hiyo twende wote ama utaenda na Bruno!!!” aliuliza John

“Mwenyewe ninatosha hata usijali hatutachukua wakati sana, isitoshe Michael si mkorofi” alipanga maneno yake Matha kama karata na yakakubaliwa bila chembe ya wasiwasi na John.

****

Joyce Keto, alikuwa haelewi hata nini kilichokuwa kinaendelea ndani ya nyumba ile ambayo alikuwa hajafahamu wapi mlango wa kuingilia na kutokea licha ya watu kufika humo ndani na kuondoka, mwanzoni aliamini yupo katika mikono salama ya ndugu zake Michael lakini kadri siku zilivyosonga mbele ndipo akagundua kuwa alikuwa katika mazingira hatarishi sana. Siku hii jioni akiwa amepata tayari chakula chake alichokula bila kujua ni wapi kimetoka alipatwa na muwasho wa kuzunguka zunguka katika nyumba hiyo ambayo hakuijua tofauti na sebule na chumba chake cha kulala. Kiza kilikuwa kimeanza kuingia tayari lakini kutokana na taa kuwashwa mapema katika jengo hilo ilikuwa vigumu sana kugundua kwamba ni usiku. Joyce alizunguka sehemu mbalimbali bila mwongozo wa mtu yeyote hadi akaufikia mlango ambao ulikuwa umefungwa kidogo na kuachwa wazi kidogo, bila wasiwasi aliamua kuchungulia ndani.

Macho yake makavu yalikutana na tukio lililoizibua akili yake. Mwanaume mmoja alikuwa amefungwa kamba mikononi na miguuni, damu zilikuwa zinavuja kutoka katika paji la uso wake.

Joyce aliweza kumuona John, katika kundi la waliokuwa mbele ya mtu huyu, mapigo ya moyo yalipiga kwa kasi kubwa. Majambazi!!!! Ndivyo akili yake ilimtuma harakaharaka, akaondoka kutoka alipokuwa na kuelekea chumbani kwake. Aliwaza kukimbia lakini mgogoro wa nafsi ukamtawala hakuelewa kama alionekana wakati akichungulia ama la!! Alihofia kukimbia pia kwani hakujua njia sahihi ya kutoka nje ni ipi, nyumba ilikuwa kubwa sana. Akiwa bado hajaamua chochote mlango wake uligongwa alikuwa msichana wa kazi na alikuwaa amemletea kahawa ya jioni kama ilivyo ada. Alitamani kumuuliza juu ya alichokiona lakini hakumuamini hata kidogo akaizuia nafsi yake kufanya hivyo.

*****

Pori kubwa na zito ambalo Michael aliyepelekwa huku akiwa amefunikwa kitambaa usoni, hakulitambua hata kama asingekuwa na kitambaa usoni kwani alikuwa mgeni Mwanza. Walifika porini Michael akiwa na wazo moja tu la kutoroka kabla mambo hayajawa mabaya kwa upande wake, azma ya kuchangia mwili mmoja na mtu mkatili kama John ilikuwa inamtafuna kwa fujo, mwili wake ulioanza kunawiri kutokana na mlo safi na kamili aliokuwa anaupata pale kwa John sasa ulikuwa unaanza kufifia tena.

Matha yeye ni kama raha hizo zilimkubali kwani alizidi kunawiri na kuongeza mvuto wake. Matha alisimamisha gari ndogo aina ya Cresta Michael akashuka na yeye akashuka, hakuwa na wasiwasi wowote juu ya Michael kwani alijiamini kupita maelezo katika suala la kujihami kwa kutumia viungo vya mwili mafunzo aliyoyapata kabla ya kuliasi jeshi la polisi miaka kadhaa nyuma. Nia ya Michael ilikuwa kutoroka lakini hakuona hata njia moja ya kuweza kumtoa pale katika lile pori.

Nitazua mengine hapa!! Aliwaza na kusubiri kuona kilichokuwa kinataka kuendelea.

“Michael!!!” Matha alimwita na kumtoa katika ndoto zake zisizo na mafanikio.

“Naam mama!!!” aliitika kwa nidhamu.

“Njoo huku mara moja!!!” Michael alitii amri, akamfuata Matha alipokuwa anaelekea, fikra zake ni kwamba alikuwa akienda kufundishwa huko kulenga shabaha. Alipokaribia aliamriwa kurudi kinyumenyume hivyo navyo akatii.

“Simama!!” Matha aliamrisha, Michael akatii. Matha akamsogelea Michael na kumtia kitambaa usoni.

“Vipi tena mama??.”

“Ndio masharti ya kujifunza shabaha” Matha alitoa sauti ya amri lakini isiyokuwa na kujiamini ndani yake. Kimya kilitanda kwa sekunde kadhaa kisha Michael bila kuwa amejiandaa alichotwa mtama na kujikuta yu katika fundo la majani lililokuwa katika mfumo wa kitanda, kisha akafunguliwa kitambaa usoni, kabla hajasema lolote ulimi wa matha ulipenya katikati ya papi za mdomo wake, ule ubaridi wa ulimi wa Matha ukaubembeleza uoga wa Michael hadi ukasinzia na ujasiri ukaamka. Matha alikuwa kama alivyozaliwa na baada ya dakika mbili Michael naye alikuwa hivyo hivyo. Hii siku ilikuwa ya kipekee kwao kwani walikaa porini masaa mengi sana huku bunduki zikiwa pembeni kama nguo zilivyosahaulika na miili yao ikiwa imenatana.

“Michael nataka uwe mpenzi wangu!!”

“Unasemaje Matha??” aliuliza kama vile hajalisikia swali. Matha hakusema tena aliamini Michael amesikia.

“Hivi unataka niuwawe ndio ufurahie???” Michael alisema kwa sauti iliyojaa hamaki.

“Hautakufa…akuue nani???”

“Matha unauliza aniue nani???...wewe umesema John anaua au sikukusikia??” alihoji Michael kwa ghadhabu, tayari alikuwa amejinasua kutoka mikononi mwa Matha.

“Kama nisipokulinda utauwawa, laini nitakulinda” alijitetea Matha kwa sauti iliyojaa uhitaji wa mahaba.

“Matha ujue unahatarisha maisha yangu, kwanini tusiuache mchezo huu, John hakupi nini kwani??” alilalamika Michael. Matha hakusema neno akaanza kulia, mwanga wa mbalamwezi ulimruhusu Michael kuishuhuda simanzi hii, hakuamini kama maneno yake ndo yamemkasirisha mrembo huyu, kosa kubwa!!! Alipojaribu kumbembeleza huku akisahau kuwa yu uchi alijikuta tena katika mahaba mazito ambayo baada ya hapo yalizaa tabia ya mara kwa mara kudanganya kuwa wanakuja kwa ajili ya mafunzo na kisha kuubadili uwanja wa mafunzo kuwa uwanja wa mahaba.

Nachezea sharubu za simba!!!! Aliwaza Michael.

******

Matha alikurupuka kutoka kitandani alipokuwa amelala na John kitandani, mbio mbio alikimbia kuelekea bafuni kuna jambo lilikuwa limemtatiza, lilikuwa jambo geni sana kwake. Alikuwa ana kichefuchefu cha ghafla, hakuwa anaumwa hapo kabla wala hakuwa amekula kitu kibaya usiku uliopita. Alifika na kutapika bafuni, kichefuchefu kikapungua hakutaka tena kurudi kitandani alioga kabisa na kuingia katika chumba kidogo cha mazoezi. Kichefuchefu kikamrudia tena safari hii hakutapika baada ya kukikabili kwa kulamba limao alilolitoa katika jokofu.

“Matha Mwakipesile ndo wewe eeh!!!.”

“Ndio ni mimi dokta vipi malaria nini??.” alifanya utabiri usiokuwa sahihi.

“Hapana hauna Malaria mwanangu..”

“Mh!! Nini sasa hichi Mungu wangu.”

“U mjamzito Matha!!!....mwezi mmoja.”

“Dokta!!! Be serious!!!”

“Ninamaanisha, vipi kwani hukutegemea au??.”

***MATHA ANA UJAUZITO......PABAYA HAPO

ITAENDELEA
 
Aseee ni nouma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom