Meja Jenerali Isamuhyo
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 3,477
- 10,339
Mchezo wa soka una mikasa mbalimbali sana. Kuna mikasa ya kusikitisha na kuna ya kufurahisha.
Leo nimemkumbuka Michael Ballack, kiungo fundi kabisa wa Kijerumani.
Ballack angeweza kucheza kiungo wa chini, wa kati na pia wa juu, yaani alikuwa Kiungo wa shoka na aliyekamilika. Aliubonda haswa akiwa Bayer Leverkusen, Bayern Munich na kisha Chelsea huku akiwa Captain wa muda mrefu katika team ya taifa ya Ujerumani.
Licha ya sifa zote hizo, upande wa pili wa Ballack ni wa kusikitisha sana. Hakuwa na bahati nzuri linapokuja suala la kutwaa mataji. Twende sawa tuone.
Msimu 1999/2000 katika siku ya mwisho wa msimu akiwa na Bayer Leverkusen, walihitaji tu droo ili watwae taji la Ligi Kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga lakini Ballack na Bayer Leverkusen wakafungwa goli 2-0 huku Ballack akijifunga goli moja na kupeleka kukosa ubingwa huo ulioenda Bayern Munich.
Msimu wa 2001/2002 akiwa anakipiga Bayer Leverkusen alikumbwa na gundu haswa.
Walifungwa katika fainali ya kombe la ligi. Wakapoteza ubingwa wa Bundesliga katika siku ya mwisho ya msimu baada ya kuongoza kwa muda mrefu sana ligi.
Wakafanikiwa kuingia fainali ya Uefa Champions League ambapo wakapoteza Fainali dhidi Real Madrid ile Galacticos ambapo kwenye fainali Zidane alifunga moja ya magoli bora sana ya muda wote. Michael Ballack na Bayer Leverkusen wakapoteza mataji matatu waliyokaribia kuyatwaa ndani ya msimu mmoja.
Waandishi wa habari wa Ujeruamani wakaishia kuibatiza team ya Bayer Leverkusen kwakuita “Neverkusen” kwa mkosi wao kushindwa kuokota taji lolote msimu huo.
Baada ya msimu huo kuisha, kukawa na Mashindano ya Kombe la Dunia la Mwaka 2002, Michael Ballack akiwa na Ujerumani yake wakafanikiwa kufika Fainal naa wakapoteza mbele ya Brazil ya Ronaldo na Rivaldo.
Ballack akamaliza msimu akiwa na bahati mbaya zaidi kupoteza fainali ya kombe la ligi, kupoteza ubingwa wa Bundesliga katika siku ya mwisho ya msimu, kupoteza Fainali ya Uefa na kupoteza Fainali ya Kombe la Dunia.
Mwaka 2008, Michael Ballack akiwa sasa anakipiga Chelsea akapoteza Fainali Carling Cup mbele ya Tottenham Hotspurs.
Wakapoteza Ubingwa wa EPL mbele ya Man Utd katika siku ya mwisho ya msimu huo.
Kama haitoshi pia akapoteza Fainali ya Uefa Champions League dhidi ya Man Utd pale jijini Moscow baada kufungwa katika mikwaju ya penati.
Mwaka huo huo, akiwa na team ya taifa ya Ujerumani, Ballack akiwa captain wakapoteza Fainali ya Mataifa ya Ulaya (Uefa Euro 2008) dhidi ya Spain ya akina Fernando Torres, Xavi Hernandez na Marco Senna.
Wengi wanasema huyu ndio Mchezaji pengine aliyekuwa na nuksi zaidi katika soka.
Wengine wakisema kupenda kwake kuvaa jezi namba 13 inaweza ikawa ni sehemu ya mikosi iliyomuandama.
Kwa msiofahamu, wataalam mbalimbali wa soka na mambo mengine wanachukulia namba 13 kama namba ya mkosi na ndio maana kwenye team nyingi namba 13 huwa inavaliwa na makipa.
Huyo ndio Michael Ballack, kiungo wa shoka wa Kijerumani ambaye career yake ya soka ilikumbwa na mikosi ya kutotwaa mataji mengi muhimu licha ya ukweli kwamba pia ana mataji amewahi kuyatwaa.
Adios Amigos