Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,190
- 34,526
NYEMO CHILONGANI
DILI LA DOLA BILIONI 4
Sehemu ya Kumi na Mbili.
Hakukuwa na muda wa kukaa Mombasa na ndiyo maana Robinson na Robert waliondoka na kuelekea jijini Nairobi. Walikuwa na pesa hivyo walifanya kila liwezekanalo kupata ukumbi mdogo ambao waliifanya kama sehemu yao ambayo wangekuwa wanafanya mahojiano na watu mbalimbali nchini humo.
Walitengeneza logo kubwa ya Wazalendo TV na kuibandika ukutani, walitaka kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanafanikiwa kupata pesa kutoka kwa watu waliopanga kuwafanyia umafia na ndio maana hawakuona hatari kutumia pesa.
Humo, wakaweka kamera ndogo za CCTV zilizokuwa katika kila pembe ya chumba hicho kwa juu, hizo ndizo ambazo zingefanikisha zoezi lao na kuingia kwenye akaunti ya WhatsApp ya Jesca na kuchukua picha kutoka katika mafaili yake yaliyokuwa kwenye akaunti hiyo.
Kamera hizo ziliunganishwa mpaka katika kompyuta ya Robinson huku zikiwa na nguvu kubwa ya kuvuta kiasi cha kumvuta nzi kutoka chini kwa mbali alipokuwa na kumuweka karibu kabisa.
Wakanunua masofa mawili, wakayaweka humo na kupanga kila kitu kuwa cha hadhi kubwa. Mwenye nyumba ambaye aliwapangisha sehemu hiyo alishangaa baada ya kugundua kuwa wale waliopanga hapo walikuwa waandishi na walitaka kufanya kazi kabla ya kuelekea nchini Tanzania.
“Mimi nitakaa katika chumba kingine. Kwenye mahojiano yako, zungumza naye kwa kina halafu mtumie kitu kwenye WhatsApp halafu mwambie akisome, akifungua akaunti yake hiyo kwenye simu, nitaivuta kwa kutumia kompyuta yangu kupitia moja ya kamera katika upande atakaokuwa,” alisema Robinson huku akimwangalia Robert.
“Unajua mimi nashindwa kukuelewa, hivi hayo yatafanikiwa vipi?” aliuliza Robert.
“Hivi ushawahi kuiona WhatsApp ya kulipia? Achana na hii ya bure huku Afrika, ile ya kulipia kabisa, ushawahi kuiona?” aliuliza Robinson.
“Hapana!”
“Hiyo inakuwa na vitu vingi, kuna sehemu ya kuhifadhi mafaili yako, kwa mbele kabisa kuna sehemu ya WhatsApp Web, si lazima ubonyeze vile vitufe vitatu, hivyo ndiyo ambayo tutaitumia kuingia kwenye akaunti yake,” alisema Robinson.
Kwa Robert alishindwa kuelewa, hakuwa mtu wa kompyuta, kwake, kila kitu alichokizungumza Robinson kilionekana kama muujiza fulani.
Baada ya kukamilisha kila kitu, wakaanza kuitafuta namba ya mwenyekiti wa vyama vya upinzani, Bwana Timoth Oyoyo ambapo baada ya kuipata tu wakaanza kuzungumza naye.
Walimwambia kwamba walikuwa waandishi wa habari kutoka nchini Tanzania ambao walifika Kenya kwa lengo la kufanya mahojiano na Jesca kwa kile kilichokuwa kikiendelea.
Oyoyo alishtuka, hakuamini alichokisikia, moyo wake ulikuwa na furaha tele, aliamini kwamba endapo Jesca angefanya mahojiano na waandishi wa habari kutoka nchini Tanzania basi ingekuwa kazi nyepesi kulisambaza suala hilo na kupata nguvu kwa kila kitu ambacho wangetaka kupata hapo baadaye.
Walizungumza na kukubaliana, baada ya hapo Oyoyo akazungumza na Jesca ambaye hakuwa na wasiwsi wowote ule.
“Ila kuna umuhimu na kufanya mahojiano na waandishi kutoka Tanzania?” aliuliza Jesca huku akimwangalia Oyoyo.
“Ndiyo! Tena hii ndiyo nafasi nzuri! Jesca, kama kweli tutafanikiwa katika hili, nakuahidi tutashinda hii kesi kwa asilimia mia moja,” alisema Oyoyo.
Ilikuwa ni vigumu kwa Jesca kukubali, ni kama moyo wake ulikuwa na hofu lakini hakuwa na jinsi, akakubaliana naye na hatimaye kumwambia Robert kwamba walikubali kufanya mahojiano.
Siku hiyohiyo majira ya saa nane mchana, wakaonana ndani ya sehemu hiyo ambayo ilitengenezwa na kuonekana kama kituo kidogo cha waandishi wa habari ambapo walikuwa wakipatumia.
Hapo kulikuwa na kamera za kukodi, ilikuwa ni lazima watengeneze sehemu ambayo ingeonekana kwamba kweli ilikuwa ni ya waandishi wa habari kutokana na vifaa vya humo kuwa na gharama kubwa.
“Naitwa Robert kutoka Mzalendo Tv,” alijitambulisha Robert huku kamera ikiwa mbele yao ambapo kulikuwa na vijana wawili waliowakodisha kwa ajili ya kazi hiyo.
Robert alionyesha tabasamu, alimwangalia Jesca, alikuwa msichana mrembo ambaye hakutakiwa kabisa kupitia kile alichopitia. Akazungumza na Oyoyo na kujitambulisha na kumwambia kwamba lengo kubwa la kufanya mahojiano hayo ni kwa sababu walitaka kuisambaza habari hiyo Afrika nzima.
“Ni jambo zuri sana!” alisema Oyoyo.
Baada ya kukubaliana, Robert na Jesca wakakaa kwenye kochi na kuanza kumuhoji maswali kadhaa. Jesca hakuwa na hofu, aliamini kwamba kweli mwanaume huyo alikuwa mwandishi wa habari, kila alichoulizwa, alijibu pasipo kugundua kwamba upande wa pili kulikuwa na mwanaume aliyekuwa akiifanya kazi yake kikamilifu kupitia kamera zilizowekwa ndani ya chumba kile.
Mahojiano yalikuwa yakiendelea, ndani ya chumba hicho kulikuwa na watu wengi kutoka kwenye vyama vya upinzani, kipindi hicho huyo Jesca alikuwa akilindwa kuliko kitu chochote kile kwani walihisi kwamba ndiye angekuwa ushindi wao mkubwa na kumdhoofisha rais wa nchi hiyo, Bwana Kimoni.
“Nataka nikuulize maswali ya siri sana, ila sitokuuliza kwa mdomo, nitakuuliza kwa WhatsApp, kama utaliona linajibika, naomba unijibu kwa mdomo,” alisema Robert huku akimpa kikaratasi aandike namba yake, Jesca akafanya hivyo.
“Haina shida.”
Hiyo ndiyo nafasi iliyokuwa ikisubiriwa, kule alipokuwa, Robinson akaanza kuivuta simu ya msichana huyo, swali lilipoulizwa kwenye WhatsApp na kuifungua tu, haraka sana Robinson akaivuta, akaingiza program yake ya udukuaji na kuanza kwenda kwenye kipengele cha WhatsApp Web ambapo huko kulikuwa na Barcode alizoziscan kwenye kompyuta yake na hatimaye kukubali na kuingia kwenye akaunti ya msichana huyo.
“Bravo figlio,” (safi kijana) alisema Robinson kwa Lugha ya Kilatin.
Hakutaka kuchelewa, hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake pekee. Kitu alichokifanya ni kuingia kwenye mafaili ndani ya akaunti hiyo, humo akakutana na vitu vingi zikiwemo picha na video kuhusu kile kilichokuwa kimetokea.
Alichokifanya ni kuanza kuzikopi harakaharaka. Alizichukua zote ambazo kwa pamoja zilikuwa na ukubwa wa 1.6GB na alipomaliza tu, akaamua kuzifuta kwenye akaunti ya msichana huyo.
Hakuishia hapo, kwa sababu akaunti hiyo iliunganishwa na barua pepe, akaingia huko, akapekua kwenye mafolder yaliyohifadhiwa na kuanza kuzifuta picha na video fupifupi zilizokuwa humo ambazo zingetumika kama ushahidi kwenye kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili.
Alipohakikisha amemaliza kila kitu, akazifuta moja kwa moja na kupandikiza kirusi ambacho alikuwa na uhakika kusingekuwa na mtu ambaye angekitoa kwenye akaunti hiyo.
“Nimemaliza mzee baba!” aliandika ujumbe mfupi kwenda kwa Robert ambapo baada ya kuupokea tu, alichokifanya ni kumaliza mahojiano harakahara na kuwashukuru wote kwa ushirikiano waliowapa.
“Tunashukuru sana!” alisema mwanaume huyo, watu hao hawakutaka kupoteza muda, wakaondoka zao mahali hapo huku wakiwa na uhakika kwamba habari hiyo ingesambazwa zaidi na uozo wa Kimeta ungejulikana kila sehemu.
***
Jesca alishtuka, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, aliangalia simu yake kwenye Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp kwa lengo la kuangalia kama kulikuwa na zile picha na video alizokuwa ameziweka kwenye faili lake, alipopekua hakuona kitu jambo lililomfanya kushtuka.
Hakuangalia mara moja, aliangalia zaidi ya mara tatu, alifungua huku na kule lakini hakubahatika kuziona. Hilo likamchanganya, alichanganyikiwa, akaingia kwenye barua pepe ambapo huko pia alizihifadhi, alipofungua, akazikosa na mbaya zaidi akakutana na vitu ambavyo hakuvielewa.
Haraka sana akampigia simu Oyoyo na kumwambia kwamba alitaka kuonana naye, kwa jinsi alivyoongea tu mwanaume huyo akajua kabisa kulikuwa na kitu kilichoendelea hvyo haraka sana akaonana naye na kuanza kuzungumza.
Kwa jinsi msichana huyo alivyoongea na machozi kumtoka aliamini kabisa kulikuwa na jambo kubwa na zito. Alipomwambia tu kwamba zile picha na video hazikuwa zikionekana, akahisi mwili wake ukinyong’onyea na kukaa kwenye kochi.
“Unasemaje?” aliuliza mzee Oyoyo.
“Zimefutwa, kuna mtu aliingia kwenye akaunti na kuzifuta,” alisema Jesca.
Oyoyo alimwangalia Jesca, hakuamini alichokuwa akiambiwa, alihisi kama alitaniwa kwani miongoni mwa vitu ambavyo walitakiwa kuwa makini navyo ni hizo picha na video.
Aliambiwa kwamba zilifutwa kwenye simu yake na barua pepe, zilifutwaje? Nani aliingia na kufanya kazi hiyo? Alimuuliza kama simu yake aliwahi kumgawia mtu yeyote yule na kuitumia, alimwambia kwamba hakufanya hivyo, sasa kama simu hiyo haikuchukuliwa na mtu yeyote, ni nani alifanya kazi hiyo?
Hawakutaka kumwambia mtu yeyote yule, ilikuwa ni lazima wajue kilichotokea mpaka vitu hivyo kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Waliendelea na uchunguzi wa kimyakimya kwamba iilikuwa ni lazima mtu huyo agundulike kwani walikuwa na hofu kwamba inawezekana katika hoteli ambayo walimlaza kulikuwa na mtu aliyeingia na kuiiba simu hiyo.
“Jesca! Inawezekana vipi?” aliuliza Oyoyo huku kijasho kikimtoka.
“Hata mimi nashangaa!”
“Hawa watakuwa watu wa serikali! Ni lazima tufanye kila liwezekanalo kuhakikisha vitu hivyo vinarudishwa,” alisema Oyoyo.
Hicho ndicho walichokifanya, haraka sana wakawasiliana na vijana wao wa IT na kuwaambia kulikuwa na kazi iliyotakiwa kufanyika haraka sana na kama iliwezekana basi waonane kwenye hoteli hiyo.
Ni ndani ya nusu saa tu vijana hao wakafika hotelini hapo, wakachukuliwa na kupelekwa katika chumba hicho na Jesca kuanza kuelezea kilichokuwa kimetokea.
Vijana hao walimsikiliza kwa makini, tatizo walilokutana nalo siku hiyo lilikuwa kubwa, mbaya zaidi hata kuwahi kuitumia WhatsApp ya kulipia hawakuwahi hivyo walivyoambiwa kuhusu mambo hayo walibaki wakishangaa tu.
“Hakuna mtu anayeweza kudukua akaunti ya WhatsApp, labda kuna mtu alichukua simu yako,” alisema kijana mmoja, kila kitu alichombiwa aliona kabisa haikuwezekana hata kidogo.
“Ila hakuna mtu aliyeichukua!”
“Hata mtu aliyekutaka ufungue akaunti yako?”
“Hakuna...sijawah....hebu subiri! Nafikiri ni wale waandishi wa habari!” alisema Jesca.
“Waandishi gani?”
Jesca akaanza kuwaambia kuhusu watu hao, hapo ndiyo Oyoyo akakumbuka kila kitu, naye akahisi kwamba inawezekana waandishi wale wa habari ndiyo waliohusika katika kungia kwenye akaunti ya Jesca na kuzifuta picha hizo.
Haraka sana Oyoyo akachukua simu yake na kupiga nchini Tanzania katika Televisheni ya Wazalendo na kuomba kuzungumza na meneja mkuu. Hilo halikuwa tatizo, simu ikaunganishwa mpaka huko na kuzungumza naye.
Kwanza alimuelezea kila kitu, jinsi walivyokuwa wakipambana lakini mwishi wa siku waandishi kutoka nchini humo waliondoka na kuelekea Kenya ambapo walifanya mahojiano na Jesca, walihisi kulikuwa na kitu walichokifanya.
“Waandishi kutoka kwetu?” aliuliza mwanaume huyo huku akionekana kushangaa.
“Ndiyo!”
“Hapana! Hatukutuma mwandishi yeyote yule,” alisema meneja kwenye simu.
“Hamkutuma mwandishi yeyote?”
“Ndiyo! Hao ni waandishi gani?” aliuliza meneja.
Kwa kusema maneno hayo tu kukampa uhakika Oyoyo kwamba wale wanaume wawili ndiyo waliokuwa wamehusika katika jambo hilo hivyo ilikuwa ni lazima wapambane kuhakikisha wanawapata na kuchukua picha na video zile.
Hawakujua ni kwa jinsi gani wangeweza kuwapata, waliwaambia wenzao kuhusu watu hao na hivyo kuanza kuwatafuta kimyakimya, kwa kile kilichokuwa kimetokea, ilikuwa ni lazima iwe siri kwani kama isingekuwa hivyo, wangekosa kila kitu kwa sababu kama wangeulizwa kuhusu ushahidi wa picha na video hizo, wasingekuwa na lolote la kuionyeshea mahakama.
“Jamani naomba tupambane! Wale vijana ni muhimu sana, si mnawakumbuka?” aliuliza Oyoyo.
“Mimi nawakumbuka sana! Ila wamefanya nini bosi?” aliuliza kijana mmoja, hakukuwa na mtu aliyekuwa akifahamu zaidi ya Oyoyo na Jesca.
“Wamefanya jambo moja kubwa sana, kwanza tuwatafuteni, tukiwapata nadhani itakuwa fudisho kwa watu wengine,” alisema Oyoyo huku akijitahidi kila kitu kilichoendelea kuwa siri kubwa pasipo watu wengine kufahamu lolote lile.