Riwaya: Chokoraa

Riwaya: Chokoraa

Jamani Casuist, mwanaidi si alifariki kwa ugonjwa wa pumu, na frida akajifungua mtoto ndio akapewa jina la mwanaidi au?
 
Last edited by a moderator:
Jamani Casuist, mwanaidi si alifariki kwa ugonjwa wa pumu, na frida akajifungua mtoto ndio akapewa jina la mwanaidi au?

Pole kwa mkanganyiko, Three episodes to go, utaielewa tu ram
 
Last edited by a moderator:
Mh hata sijaelewa sijui ndo flashback au inaendelea mbele
 
SEHEMU YA THELATHINI NA TANO

Makala maalumu ya Kasuku ilifanya vizuri sana katika magazeti mbalimbali.Watu walioisoma walibaki midomo wazi. Kwa wote waliomfahamu Dembele walibaki wakijiuliza? Maswali yasiyo na majibu. Hakuna aliyetegemea anaweza kuwa bwana mbaya namna ile.
Lakini ilibaki kuwa hivyo, kila aliyemsoma mwanadada jasiri, yatima na chokoraa aliyewapigania wenzake. Bila kuwa na mhimili wa kuegemea na kisha kuishinda vita hii, alitamani kumuona.
Umri wa Mwanaidi uliwashangaza wengi. Haukuendana na harakati alizokuwa anafanya.
Harakati zile zilihitaji mtu msomi, mwenye pesa na nguvu kimapambano. Mwanaidi hakuonekana na vyote hivyo.
Mwanaidi akasubiriwa anyanyuke kutoka kitandani aweze kupewa heshima yake. Lakini hakuamka mapema kama wanavyotaka wengi.

Hadi usiku fulani ambapo Frida alikuwa amelala. Alishtuliwa na ndoto mbaya. Ndoto ya maajabu. Alishtuka na kujikuta akiwa anatokwa jasho lakini jasho pekee halikuwa linamtia kero, kuna kitu alikuwa anahisi kinamtokea kwa mara ya kwanza katika maisha yake.
Maumivu !! maumivu makali sana. Frida akajikaza lakini yaliongezeka, akapiga kelele kubwa, kelele ikavuka mipaka ikawafikia walengwa waliopewa kazi ya kumtunza.
Wakafika na kugundua kuwa binti huyu alikuwa ameshikwa na uchungu.
Upesi zikachukuliwa hatua.
Baada ya masaa kadhaa Frida alikuwa hoi huku macho yake yaliyolegea yakimtazama mtoto wake. Mtoto asiyekuwa na baba.
Japokuwa alikuwa amechoka sana aliweza kuwasikia manesi wakimpa hongera ya kujifungua mtoto wa kike.
"Mwana….Mwanaiiiidi." alijitutumua akakiita kitoto kile jina hilo.
Kikalipuka kwa kilio cha kitoto.
Jina kubwa!! Mwanaidi.
Kisha Frida akapoteza fahamu….

Kwa sababu Frida alikuwa bado kitandani hata alipozinduka hakupewa taarifa yoyote mpya juu ya maendeleo ya Mwanaidi aliyekuwa anapumulia mipira.
Lakini ndoto yake ya kuota kuwa anajifungua mtoto anayefanana na Mwanaidi huenda ilikuwa sahihi. Alikuwa amejifungua Mwanaidi mpya na kumbatiza jina hilohilo.
Wakati akiota ndoto hiyo tayari simanzi ilikuwa imetanda kwa wale waliomjua ama kutomjua Mwanaidi, yule malaika mbaya anayesadikika kuwa na kazi moja tu duniani ya kutoa roho alikuwa ameshikilia msimamo wake, licha ya wananchi wengi kumsihi amwache hai walau atazame jinsi jamii ilivyompa heshima kuu…malaika akagoma. Akampa dakika ya mwisho kupumua Mwanaidi huku wakati huo huo akimpa ndoto Frida. Ndoto ya kuagana na kumpokea Mwanaidi mpya.
Yule msichana mashuhuri kabisa, mpambanaji wa kweli ambaye hakuwahi kukata tamaa, aliyewajali yatima na kuamini kuwa siku moja wataishi kwa umoja na furaha, yule mwanajeshi asiyekuwa na gwanda wala nyota begani. Akavuta pumzi kwa usongo wote ndani kisha akazitoa tena kwa nguvu na asiweze kuzivuta tena.
Madaktari wakatazamana na kukiri kuwa hatimaye jitihada zilikuwa zimegonga mwamba.
Mwanaidi akatoweka!!!
Wangeweza kusema amekufa kijasiri, wangeweza kumuita shujaa lakini hii haikupunguza uchungu wa kifo kile. Mwanaidi alikuwa amekufa!!!!
Yule shujaa wa mapambano, asiyeogopa kufa wala asiyehofu kuua, ugonjwa wa pumu ukatwaa uhai wake.
Alikufa akiwa anapambana, hakuwahi kupumzika kamwe.
Kwa kifo chake akawaokoa wengi!!

Frida alipopewa taarifa juu ya umauti uliomkumba Mwanaidi, alifanya tabasamu hafifu kisha akasema.
"Ili itimie ile ndoto. Ndoto ya Mwanaidi kuishi maisha mapya ya furaha akiwa na mzazi wake ambaye ni mimi. Ni muda wa kumtunza aliyenitunza na kuniokoa. Alinipigania muda wote wa maisha yake, rafiki wa kweli asiyekuwa na unafiki hata kidogo….rafiki anayetambua thamani halisi ya urafiki." Maneno yale yaliamsha hisia, George akawa wa kwanza kudondosha chozi. Frida akalipuka na kilio kisichozuilika. Alikuwa anamlilia Mwanaidi.
Kisha Frida akaomba aletewe kile kichanga mbele yake. Hakika kikaletwa. Akakitazama kisha akiwa amelala vile vile akaanza kuzungumza.
"Wewe ni shujaa ambaye hukufaidi utoto wala ujana wako, Mungu aliyekuleta wewe kwangu na kunionyesha njia ndiye huyu amekuleta tena kwangu nikuhudumie, uishi kwa raha na amani ukilipata joto la mama ambalo ulilikosa hapo awali. Kwa mkono wangu na uhai atakaonipa Mungu nitakupigania kama ulivyonipigania, nitakuweka mbali na watu wabaya walisababisha mauti haya. Mwanaidi unaishi katika moyo wangu, utaendelea kuishi milele katika moyo huu." Alimaliza kauli hii na hakufumbua macho yake tena. Akaamua kusinzia.
Hakuna aliyemsemesha. Kila mmoja alikuwa na uchungu wake, Isha katika wodi aliyokuwa amelazwa kwa uchunguzi zaidi baada ya kubakwa na watu wabaya naye alikuwa akisina huku kwikwi nazo zikimwandama. Alikuwa kwenye uchungu mkubwa baada ya kupata taarifa za kifo cha Mwanaidi.

****

Makala ya Kasuku ikazidi kupenya anga zote hatimaye kila jicho likaingoja serikali ifanye maamuzi juu ya wanaharakati wale vijana tena yatima.

Bwana Dembele akasomewa mashtaka kadhaa yakiwemo ya kuhusika na vifo vya askari wawili usiku ule jambo ambalo Dembele alilikataa kata kata. Lakini sheria ilimbana zaidi hatimaye hukumu ikatolewa.
Dembele alihukumiwa kifungo cha maisha jela. Mkewe na watoto wake nd'o viumbe pekee waliotokwa na machozi na kuumizwa na jambo lile lakini hawakuwa na la kubadilisha hali ile.

Mali haramu za bwana Dembele zilitaifishwa baada ya kuwa amehukumiwa kumalizia maisha yake yote jela huku akisindikizwa na diwani ambaye alivuliwa madaraka kutokana na kuficha siri kubwa kama ile baada ya kuuziwa na hayati Mwanaidi kisha kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela, mali zile zikawekwa mnadani. Zilikuwa mali nyingi sana. Mauzo yake yakawezesha kujengwa kituo kikubwa cha watoto yatima. Ili kuenzi harakati za mapambano yale ya siku nyingi. Kwa heshima ya yule mtoto aliyekufa akipigania watoto kituo kile kikaitwa jina lake ‘MWANA'. Jina hilo likisimama badala ya jina la hayati Mwanaidi ambaye alizikwa kwa heshima zote.

Ilikuwa huzuni wakati wa kukifungua kituo hicho. Hapakuwa na burudani ya muziki wala kelele za kushangilia tukio lile. Umati mkubwa sana ulihudhuria ufunguzi ule. George, Isha, Frida, Suzi na mama George wote walivaa nadhifu mavazi yaliyofanana huku fulana zao kwa nyuma zikiwa na na jina Mwanaidi Shupavu huku mbele ikipambwa picha ya Mwanaidi. Picha ambayo ilitolewa katika kituo cha watoto yatima. Kituo ambacho Frida alitendewa unyama na mkuu wa kituo hadi akapata mimba na kisha kuitoa. Alisaidiwa na Mwanaidi kuitoa mimba ile.
Katika picha ile Mwanaidi alikuwa katika hali ya kulazimisha tabasamu ilhali huzuni ikimtawala zaidi.
Hatua kwa hatua mkuu wa mkoa akiongoza msafara huu, kuelekea katika mlango wa kuingilia katika kituo kile kipya.
Binti aliyekuwa amejitanda kichwa chake alikuwa anatembea kwa kusuasua huku pembeni yake akiwepo binti mwingine aliyemshika mkono…….
Hatimaye akasimama alipotakiwa kusimama, pembeni yake akiwepo mkuu wa kituo.
Akaomba kipaza sauti, akapewa alihitaji kusema neon kwa jamii.
Kila kinywa kilikuwa kimya. Ni kama mahali pale ulipigwa wimbo wa taifa.
"Ni siku ambayo laiti kama angekuwa hai…kwa mara ya kwanza angecheza na kurukaruka…..kwa niaba yake popote alipo najua anatutazama….Mwanaidi huko ulipo huyu motto mikononi mwangu ni wewe, naamini ni wewe. Naye anaitwa Mwanaidi. Kwa upendo usiohesabika, kwa heshima zisizoandikika, nakusihi kifungue kituo hiki. Kwa ajili ya kutimiza zile harakati zako za muda mrefu….harakati za ukombozi."
Frida alizungumza kwa sauti ya kusihi kisha akakikabidhi kile kitoto kilichokuwa na takribani miezi minne kisu, akakisogeza katika ule utepe. Akakisaidia kukaza mkono….utepe ukakatika.
Makofi, vigelegele vikasikika kwa sauti ya juu sana.,
Hatimaye kile kitoto cha Frida kilichoitwa Mwanaidi kikacheka kwa furaha.
"Hakika Mwanaidi anaishi!!!" George na Isha walinong'onezana.
Sherehe zikaendelea kwa hotuba ya mkuu wa mkoa. Kisha zikamalizika kwa uongozi wa kituo kuchaguliwa….
George kutokana na kuwa na elimu ya juu sana kupita wote akapewa jukumu la kukiongoza kituo kile.
George akawa mkuu wa kituo……
Frida akamkimbilia na kumkumbatia huku akimnon'goneza, "Usiwe kama wale wakuu wengi hakika utalaaniwa ukifanya yale."
"Sitawaangusha!!" George alijibu kwa sauti hafifu.
Wakati wawili hawa wakipongezana kuna jicho lilikuwa likiwatazama kwa makini sana. Jicho ambalo lilikuwa na mashaka na kitu fulani lakini halikutaka mdomo useme chochote.
Jicho la ajabu, jicho ambalo halikuwa likipepesa huku na kule.
Hakuna hata mtu mmoja katika ya wanaomfahamu walioweza kumtambua kwa jinsi alivyokuwa amejiweka.
Jicho hili halikuishia kuangali hapa tu…..
Liliendelea zaidi na zaidi kwa umakini….

****

MIAKA ilikatika kituo cha Mwana kikiwa kituo bora na kimbilio sahihi kwa watoto wa mitaani na yatima. Kituo kilikuwa na huduma bora sana kimaadili na pia kimarazi.
George hakuisha kuchukua tunzo kadha wa kadha kutoka kwa washika dau jambo ambalo lilijenga jina lake Tanzania. Mzee Emmanuel kutoka gerezani aliamriwaq kutoa maelezo juu ya wapi vyeti vya Georege vinapatikana. Akatii…ile elimu ya George ikarejeshwa tena mikononi mwake.
Alipozipata sifa kwa mara ya kwanza za kuwa mwalimu mzuri wa somo la hisabati katika kituo cha masomo ya ziada cha Mchikichini, George alisukumwa na sifa mwishoe akajikuta katika mkondo asioujua na kuangukia dhambini. Sasa amekutana na sifa maradufu kuliko za awali, sifa zilizompelekea kuitwa Ikulu akala chakula cha jioni na familia ya raisi. Picha zikasambaa magazetini.
George akaanza kutafutwa. Ni jambo hili lilihofiwa na lile jicho. Yule mtazamaji wa siku ya ufunguzi wa kituo kile alijipongeza kwa jicho lake kumpa machale ya uhakika. Akafanya tabasamu japo moyoni alihofia sana uhakika ule, kwani aliamini kuwa kijana yule atatafutwa na watu wazuri na wabaya kitu ambacho kitaleta madhara makubwa iwapo atadanganyika. Na mbaya zaidi litazuka fukuto.
Lakin kwa siku ile ni kama vile hakuwa na la kufanya kuzuia hali ile.

Hakika muonja asali haonji mara moja. Akiwa safari za kikazi nje ya jiji la Dar es salaam George alijikuta majaribuni, akashiriki tendo la ngono na msichana kutoka Mwanza. Ile ladha ikaanza kuishi naye na kumtawala…..aliporejea jijini Dar es salaam akaanza pupa za awali akiwa chokoraa.
George Emmanuel. Alikuwa muonja asali, na ladha ya shubiri hakuitambua. Suluba walizopitia wenzake yeye alikuwa hajazipitia kwa kiasi kikubwa hivyo. Hakuwa mwanamke akumbuke kubakwa wala kutoa mimba. Alichokumbuka zaidi ni kulala bila kula, jambo ambalo husahaulika pindi chakula kinapokuwa kingi tena.
Starehe alizoendekeza baada ya kuwa amepata pesa za bwana Dembele enzi za uchokoraa akaendelea nazo tena baada ya kupata kazi katika kituo kile cha watoto yatima cha MWANA..
Starehe yake aliyoendekeza zaidi ilikuwa wanawake.
Ukiyaendekeza mapenzi lazima uupoteze uelekeo, George aliyaendekeza huku akiisaka ile ladha aliyoipata kwa yule binti wa kitanga aliyemuingiza katika ulimwengu huu. Na ile ya mrembo kutoka Mwanza,
Alijisahau kuwa aliwahi kuwa chokoraa, alisahau kila kitu akavimba kichwa kutokana na heshima aliyoipata katika jamii.
Machoni pa watu alijionyesha kuwa yu mwema sana tena mkarimu lakini ndani alificha mengi. Alikuwa zaidi ya mchafu.

Frida na Isha walijaribu kumshauri, aliwasikiliza kwa makini na kuahidi kubadilika lakini kamwe haikuwa hivyo.
Kila yatima aliyekuja katika kituo cha MWANA ilimradi alikuwa ni mrembo George alifanya juu chini ili aweze kushiriki naye mapenzi.
Yote haya yalifanyika kimyakimya. Bila mtu yeyote kutambua.
George alitumia pesa!!
Kweli pesa mwanaharamu.
George alijisahau kuwa aliyekifungua kituo kile ni Mwanaidi, askari makini bila gwanda mwilini mwake.

Tabia hii ilizidi kukomaa huku ikiwa siri ya watu wachache tu…siri iliyoendelea kumwacha akiwa na nguvu ya kuishawishi jamii yake, nguvu ya kusema neno na kuaminika kwa asilimia zote.
Tabia hii ingeweza kudumu kwa kipindi kirefu sana tena bila jamii kutambua iwapo tu usingefika usiku huu, usiku wa aina yake. Ulikuwa mrefu kuliko giza lolote lile ambalo George amewahi kuliishi.
USIKU huu George akapata mgeni wa maajabu mgeni ambaye hakuwa na ahadi ya kumtembelea lakini akafika usiku mnene….
Alikuwa na lake jambo…..jambo lililozua mjadala mkubwa kisha kubadilika na kuwa utata….

***NINI kimetokea? Huyu ni mgeni gani na atabadili nini katika simulizi hii.
**NINI hatma ya haya yote………maana bado hayajakwisha…..

ram Toplady Khantwe muuza ubuyu Samaya Lio 002 Jullie Z binti kiziwi culbby
 
attachment.php

Frida na Isha walijaribu kumshauri, aliwasikiliza kwa makini na kuahidi kubadilika lakini kamwe haikuwa hivyo.
Kila yatima aliyekuja katika kituo cha MWANA ilimradi alikuwa ni mrembo George alifanya juu chini ili aweze kushiriki naye mapenzi.
Yote haya yalifanyika kimyakimya. Bila mtu yeyote kutambua.
George alitumia pesa!!
Kweli pesa mwanaharamu.
George alijisahau kuwa aliyekifungua kituo kile ni Mwanaidi, askari makini bila gwanda mwilini mwake.

Tabia hii ilizidi kukomaa huku ikiwa siri ya watu wachache tu…siri iliyoendelea kumwacha akiwa na nguvu ya kuishawishi jamii yake, nguvu ya kusema neno na kuaminika kwa asilimia zote.
Tabia hii ingeweza kudumu kwa kipindi kirefu sana tena bila jamii kutambua iwapo tu usingefika usiku huu, usiku wa aina yake. Ulikuwa mrefu kuliko giza lolote lile ambalo George amewahi kuliishi.
USIKU huu George akapata mgeni wa maajabu mgeni ambaye hakuwa na ahadi ya kumtembelea lakini akafika usiku mnene….
Alikuwa na lake jambo…..jambo lililozua mjadala mkubwa kisha kubadilika na kuwa utata….

*****

George alijilazimisha kufumbua macho yake kwa ukubwa ambao hajawahi kufumbua ili aweze kubaini iwapo yu ndotoni ama la! Lakini aliona hali halisi, ile sura ni kama aliwahi kuiona mahali lakini hakujua yule mtu anaitwa nani. Alitaka kumuita lakini sauti haikutoka, na bila kukaribishwa yule mtu ama kiumbe akaketi katika upande mmoja wa kiti. Kisha akafanya mfano wa tabasamu….George akaduwaa.
"Haujambo mheshimiwa!!." Hatimaye yule mgeni alimsemesha. George akashindwa kujibu akabaki kuduwaa. Mgeni wake hakujishughulisha na mshangao uliomkumba bwana George, aliendelea na shughuli zake ambazo kwa utashi wake anaamini ndizo zilimleta pale ndani, alifunua huku na kule akiwa anatafuta anachojua yeye mwenyewe hatimaye akakipata kipande cha karatasi, akaipata na kalamu. Akaandika maneno fulani katika mweandiko mbovu kabisa kisha akampatia George aweze kuangusha saini yake. George akasita, yule mtu akamuangalia kwa macho makali sana. Macho yaliyosisitiza amri. George akaweka sahihi. Yule mgeni akatabasamu, kisha akafungua matambala aliyokuwa ameyabeba. Akatoa mzigo ambao ulionekana wazi kukusudiwa kuachwa nyumbani kwa George.

George akaendelea kushangaa lakini safari hii alijikuta akiuliza, "Wewe ni nani na…na unataka nini?" yule mgeni akasita alichokuwa anafanya, akamgeukia Georgekwa macho ya utulivu kabisa. Akafanya tabasamu kisha akajitambulisha kwa ufasaha.
Jina geni kabisa masikioni mwa George, alitaka kuuliza zaidi lakini yule mtu alikuwa na mzigo mkononi akamkabidhi George.
George akapokea pasina ubishi. Yule mgeni bila kuaga alifungua mlango akaondoka zake, mara kiza kikatanda baada ya George kubaini mzigo aliokuwa ameachiwa. Kiza kilekile ambacho George hakuwahi kukiishi kamwe. Kiza kizito tena kilichotanda ukimya wa hali ya juu.
Simu yake ya mkononi iliita ndipo aliposhtuka, akapapasa kisha akabofya hovyo bila kutambua iwapo alipokea au alikuwa ameikata. Akaendelea kuuchapa usingizi, mara ikaanza kuita tena.
"Aaargh mamtu mengine bwanaa…." Alilalama huku akifanya juhudi za kufumbua macho. Akaoitazama simu zilikuwa ni namba za Isha.i Aaaargh usumbufu tena Isha, si tumeshakubaliana kuwa hatuwezi kuwa wapenzi tena au? Nishamwambia kabisa dini haziruhusu…hanidai wala simdai. Aah mi sipokei…..alizidi kughafirika George. Simu ikakatika.
Akapiga kite cha ghadhabu, mara ikaanza kuita tena. Akataka kuipokea kwa pupa na kumjibu hovyo Isha, lakini akakutana na jina la Suzi.
"He! Inamaana wanaambizana kunipigia au?" alijiuliza George…..
Sasa sipokei zote pumbavu kabisa!!! Akasema kwa sauti ya juu. Usingizi ulikuwa umekatika tayari. Akasimama wima huku akiwalaani wasichana hao kwa kuukatisha usingizi wake mtamu kupita yote aliyowahi kulala.
Alipofika sebuleni akakuta ustaarabu ukiwa umevurugwa, alishangaa kidogo na kujilaani kwa kuanza kuwa na tabia ya uzembe wa kutopanga chumba chake kama ilivyokuwa zamani. Akajilaumu zaidi kwa kumwajiri yule msichana wa kazi.
"Monicaaaa!!!! Weee mwanahizayaaa!!" aliita kwa ghadhabu. Sauti ya msichana kutoka nje ikaitika kwa ustaarabu….
Simu yake ikaita tena kutoka chumbani.
Sasa naenda kutukana mtoto wa mtu haki ya nani!!! Alisema kwa sauti ya juu yenye kutawaliwa na kitetemeshi cha hasira.
Aliifikia simu akiamini kuwa ni aidha Isha ama mwenzake Suzi.
Wakati anafika chumbani, Monica naye alikuwa amefika sebuleni akishangaa ni kitu gani bosi wake anatafuta hadi afanye vurugu kubwa kiasi kile.
Mpiga simu alikuwa ni Frida wakati huu. Hapa George akatuliza akili na kufikiri mara mbili, akaamini palikuwa na tatizo huenda tofauti kabisa na mawazo yake.
Akaipokea simu ile.
Frida badala ya kuongea alikuwa analia….kwikwi ilisikika na kuonyesha kuwa yule mtu alikuwa amezidiwa na kilio.
"Vipi? Amepokea!!! Eeeh!!" ilisikika sauti ya Isha pembeni…..George alizidi kusema ‘halooo' bila kupata majibu. Mara ile simu ikahamia katika sikio jingine.
"Kaka George kuna tatizo huku, tafadhali njoo tupo hapa chumbani kwa Frida njoo tafadhali…."
"Tatizo? Tatizo gani?" alihoji.
Isha kutoka upande wa pili hakuwa tayari kusema tatizo ni nini akamsihi afike.
George hakukumbuka kusafisha mwili wala kinywa chake, alikwapua suruali yake kutoka katika kiambaza cha mlango, akajivika na fulana aliyovaa siku iliyopita….akashika viatu mkononi, akaanza kutimua mbio akimpita Monica akiduwaa pale sebuleni bila kumsemesha lolote hadi alipofika nje.
"We mwanamke wewe yaani unalipwa mshahara halafu naniii….ngoja nikirudi…" aliropokwa haya akiwa nje tayari.
Akaita taksi na kuamuru apelekwe Kinondoni Studio.
Upesi gari ikaondolewa, George alikuwa kimya kabisa. Baada ya nusu saa walikuwa eneo alilokuwa anahitaji kufika. Akafanya malipo upesi na kuendelea kutimua mbio kuifikia nyumba.
Hakika palikuwa na tatizo maana hata majirani walikuwa wapo katika mchanganyiko wa majonzi na hamaniko kama si mshangao.
Mungu wangu Mwanaidi!!! George alianza kuweka hisia zake kuwa mtoto wa Frida alikuwa matatani, ama la sivyo basi mama yake mzazi alikuwa matatizoni.
Jibu la kwanza lilikuwa sahihi. Mwanaidi alikuwa matatizoni. Na ingekuwa heri zaidi kama angekuwa matatizoni na anaonekana pale ili aweze kupatiwa huduma ya kuliondosha hilo tatizo. Ilishangaza kwamba mtoto Mwanaidi hakuwa mahali pale.
Mwanaidi alikuwa ametoweka katika mazingira ya kutatanisha sana. Alikuwa na miezi sita tu tangu azaliwe siku ambayo wajina wake alikuwa anaiaga dunia, sasa haonekani tena kama wajina wake.
"Nimelala saa sita na nusu, kuna tamthilia nilikuwa naangalia na mama Mwana, wakati huo Mwana alikuwa amesinzia tayari…..kwa kweli hadi sasa ni maajabu ninaamka mama Mwana ananiambia eti mtoto hayupo kitandani…." Mama mmoja ambaye alikuwa anaishi ujirani mwema na akina Frida alielezea. Mama George naye akadakia, "Na ni mimi niliyeenda kumlaza, Mama Mwana alikuwa amejikita katika tamthilia mimi nikamchukua mtoto nikamlaza kisha nikaenda kujilalia huko. Yaani mbona kazi?"
"nilimkuta mwanangu kitandani jamaniii….niliangusha kioo akashtuka na kuanza kulia jamanii….kwa mikono yangu nikambeba nikampa titi anyone, aliponyonya akanyamaza tukaanza kucheza na mwanangu jamaniii uuuuuwi…..mamaa weeeeee!! Asubuhi naamka naikuta midoli tu uwiiiii mwanangu jamaniiiii nisaidieni mimiii Mwananidi wangu weeee" Maneno ya Frida na kilio chake yakaamsha msiba wa ajabu msiba usiokuwa na maiti.
Mara Frida alipokaribia kunyamaza, vikasikika vilio vingine kutokea njea vilianza taratibu kisha vikazidi kuvuma na kufika ndani, walikuwa akina dada wawili. Isha na Suzi. Hawa walikuwa wameenda kutoa taarifa polisi juu ya tukio hilo, huko wakaambiwa hakuna taarifa yoyote juu ya mtoto kupotea.
E bwana ee!! Kuna watu hawanyamazishwi wakifungulia kilio. Isha na Suzi walikuwa wanaongoza.
Kila aliyejaribu kumtuliza kama asipoambulia tusi zito basi angeweza hata kung'atwa meno.
Frida naye akaanza kulia, mama George akafunga orodha sasa akimlilia mjukuu wake. Huyu alilia hadi akapoteza fahamu.
Ilikuwa imetimia saa tatu asubuhi.
George akaaga kuwa anatoka mara moja kuangalia kipi kinaweza kufanyika, aliongozana na Isha ambaye alikuwa amejituliza mwenyewe. Wakaingia ndani ya taksi. Safari ya kuelekea nyumbani kwa George.
George alipokumbuka juu ya wapi wanaelekea akakumbuka juu ya mpangilio mbovu aliouacha pale sebuleni. Alijiuliza iwapo Monica atakuwa ameuweka sawa ama la anaenda kuabika na wageni wake….
Kuukumbuka mpangilio ule mara George akakumbuka kuwa usiku uliopita ni yeye alikuwa wa mwisho kukaa pale sebuleni pakiwa katika mpangilio mzuri kabisa. Lakini akakumbuka kuwa kuna muda alirejea tena pale na kuna jambo alikuwa anafanya na akamwona yule mtu aliyevuruga sebule yake, hakuwa Monica alikuwa ni kiumbe mwingine kabisa. Tena alijitambulisha jina, na kuna jambo la ziada alifanya..kuna mzigo alimpa naye akaupokea…..
Ni kama kiumbe hai ….alipewa kiumbe hai. Akajaribu kuikumbuka sura yake lakini likatokea giza, hakika giza lilitokea hata kabla hajatabua sura ya kiumbe kile….
"Mungu wangu weeee!!" George alipayuka ghafla. Isha akamtazama kwa masikitiko bila kusema lolote.
George alitangulia mbele na Isha akafuata, wakaingia sebuleni. Monica alikuwa ameiweka sawa sebule na haikuonyesha dalili yoyote ya kashkash! Isha akaanza kuona mwenzake anakaribia kupandwa na wazimu, alimwona George akiishangaa sebule yake mwewnyewe.
"Ehee alikuwa hapa hivi amesimama."
"Nani tena?" Isha aliuliza ndipo George akagutuka kumbe mambo aliyokuwa anayawaza kichwani aliyasema kwa sauti.
"Aaah hapana basi tu kwani….nani…karibu Isha." Alijiumauma.
"Upo sawa G." Isha aliuliza kwa sauti ya kinyonge.
"Aaah mimi?" aliuliza swali la kipumbavu bila kutarajia.
Isha akamtazama bila kusema lolote. George akasimama na kuingia ndani chumbani mwake …Isha akamsindikiza kwa macho.
Macho yaliyomsanifu kijana yule kama kwamba anaukaribisha uchizi kichwani mwake bila kujua.
"Unadhani nina tatizo basi mimi…hamna basi tu ujue…yaani.." alitokwa na maneno hayo wakati anaingia chumbani huku akirusha mikono huku na kule na tabasamu la kujilazimisha midomoni.
Isha hakutia neno akabaki kumtazama tu. Hadi alipotokomea kabisa.
Kimya kilitanda kwa sekunde kadhaa Isha akiwa anatafakari jambo lilitokea alfajiri ya siku hiyo kama mkosi ambao unawafuata kwa nyuma.
Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kutoweka katika mazingira ya kutatanisha tena akiwa mikononi mwa mama yake. Ilistaajabisha hakika.
Mara mawazo yake yalikoma baada ya kusikia purukushani ikitokea katika chumba cha George, ni kama alikuwa akipambana na mdudu ama chochote kile ambacho kilikuwa chumbani mwake kimakosa. Isha aliendelea kuzisikiliza zile purukushani za uhakika, mara kianguke hiki mara kianguke kile.
"We ni nani..unataka nini hapa eeh….Sikujui toka…" sauti ya George iliyokuwa inasota ilisikika ikihangaika. Isha akastaajabu, akavamiwa na hisia kuwa George alikuwa ameanza kuishi katika uchizi rasmi. Alifanya tabasamu la karaha kisha akajisemea ‘mzimu wa majanga unaandamana nasi bado'.
Neno lake la mwisho ‘bado' liliambatana na kishindo kikubwa baada ya yowe kubwa kutoka chumbani kwa George. Hapa sasa hakuendelea kukaa. Akasimama wima akakimbilia chumbani kwa George.
Macho yake yakakutana na mwili wa George ukitiririkwa jasho chumba kikiwa katika hali ya utulivu sana lakini kilichovurugika sana.
George alikuwa hajitambui
Isha akapagawa, hakuamini kilichokuwa kinatokea mbele yake, ulikuwa muendelezo wa ile filamu ya alfajiri ya kutoweka mtoto wa Frida katika mazingira tatanishi na sasa ilikuwa zamu ya George kupoteza fahamu katika mazingira ya kutatanisha vilevile.
Upesi akaitwaa simu yake akampigia Suzi. Simu ikapokelewa akamwomba afanye upesi akiongoza na wanaume kadhaa wafike nyumbani kwa George.
"Vipi Mwanaidi ameonekana?" Suzi aliuliza kwa kihoro.
Isha akamsisitiza afike upesi.

****

George alikurupuka kutoka katika usingizi mzito uliozigandamiza fahamu zake na kujikuta akiwa katika kitanda cha hospitali ya Mazengo katikati ya jiji.
Alijitazama huku na kule na kujikuta amezungukwa na watu kadhaa. Pole mfululizo zikafuata baada ya kujitambua.
"George ni nani ulikuwa unajibizana naye ndani." Isha alimuuliza wakiwa wamekaa.
"Mimi? Mimi nikajibizana na mtu." George aliuliza huku akijielekezea kidole kifuani kwake. "Sijazungumza na mtu hata mmoja wala." Alimalizia sentensi ile.
"Niliwaambia jamani…." Isha aliwatazama Suzi na wale vijana wengine ambao aliwaambia kuwa ana mashaka kupotea kwa mtoto Mwanaidi kunaelekea kumpa wazimu George. Suzi akainama chini na kufanya ishara ya msalaba kuombea lisitokee hilo linalodhaniwa na Isha.
Ilikuwa tafrani hakika.

Wakati haya yakiendelea huku hospitali kuna jicho lilikuwa likiyatazama yote haya huku uso wake ukitabasamu kwa matumaini makubwa sana. Alikuwa analifanikisha lengo lake taratibu lakini kwa umakini mkubwa sana….hakuna aliyejua kuwa kuna jicho linawatazama kutokea katika kona moja ya kile chumba.

George alikuwa mtulivu sana, akitafakari juu ya tukio lililotokea chumbani kwake. Alitamani sana kuwashirikisha watu waliomzunguka lakini akayakumbuka masharti yaliyotajwa na mtu yule wa ajabu…..kingine kilichomtia uzito katika jambo hili ni ile hali ya kukumbuka kuwa kile kitu alichokabidhiwa katika ile hali aliyodhani kuwa ni ndoto sasa alitambua fika kuwa alikabidhiwa mtoto mdogo ambaye alikuwa anamjua kwa sura na historia pia.
Lakini hakulitambua jina lake kwa wakati ule.

George angeweza kuelezea juu ya ndoto hiyo lakini nani angeamini kama asingetimiza masharti aliyopewa na yule mtu wa ajabu ambaye hisia zake zinakiri kuwa hapo kabla aliwahi kumuona. Alipomuona ni wapi? Hilo lilikuwa swali gumu zaidi.
Kichwa kikawaka moto zaidi ya kawaida. Huu ulikuwa mtihani mkubwa sana kuupata maishani. Yale maneno ya mwisho ya yule kiumbe ndo yalimfadhaisha zaidi, kuna jambo zito alitakiwa kuliweka bayana mbele ya jamii. Jambo ambalo George alitaka libaki siri milele.
Lakini kama angesimamia msimamo wake basi kuna shauri jingine ambalo lilikuwa zito zaidi na iwapo lisipotimizwa basi kinazuka kizaazaa kisichokuwa na mfanowe.
Ni heri yale maisha ya uchokoraa ya kulala katika vichochoro bila kupata chakula. Ni heri kukimbizana na mgambo wa jiji kuliko kukumbana na kizaazaa. Na ilikuwa heri zaidi kuishi jela miaka yote kuliko kuishi katika dunia huru inayotawaliwa na kizaazaa.
Kizaazaa kinazuliwa na George bila chokoraa wale kufahamu, lakini kinasambaa na kuwakumba wote, lakini wakati huu anaongezeka mtu mwingine matata kabisa anayeondoka kwa jina la Suleiman Meja.

****

KITABU CHA PILI CHA CHOKORAA NI (KIZAAZAA)

ram Khantwe
 
Attachments

  • Chokoraa.jpg
    Chokoraa.jpg
    28.3 KB · Views: 2,000
Casuist asante mkuu, huu mkanyiko pengine ndio mwanzo wa Kizaazaa, unakileta kizaazaa hicho?
 
Last edited by a moderator:
attachment.php

Frida na Isha walijaribu kumshauri, aliwasikiliza kwa makini na kuahidi kubadilika lakini kamwe haikuwa hivyo.
Kila yatima aliyekuja katika kituo cha MWANA ilimradi alikuwa ni mrembo George alifanya juu chini ili aweze kushiriki naye mapenzi.
Yote haya yalifanyika kimyakimya. Bila mtu yeyote kutambua.
George alitumia pesa!!
Kweli pesa mwanaharamu.
George alijisahau kuwa aliyekifungua kituo kile ni Mwanaidi, askari makini bila gwanda mwilini mwake.

Tabia hii ilizidi kukomaa huku ikiwa siri ya watu wachache tu…siri iliyoendelea kumwacha akiwa na nguvu ya kuishawishi jamii yake, nguvu ya kusema neno na kuaminika kwa asilimia zote.
Tabia hii ingeweza kudumu kwa kipindi kirefu sana tena bila jamii kutambua iwapo tu usingefika usiku huu, usiku wa aina yake. Ulikuwa mrefu kuliko giza lolote lile ambalo George amewahi kuliishi.
USIKU huu George akapata mgeni wa maajabu mgeni ambaye hakuwa na ahadi ya kumtembelea lakini akafika usiku mnene….
Alikuwa na lake jambo…..jambo lililozua mjadala mkubwa kisha kubadilika na kuwa utata….

*****

George alijilazimisha kufumbua macho yake kwa ukubwa ambao hajawahi kufumbua ili aweze kubaini iwapo yu ndotoni ama la! Lakini aliona hali halisi, ile sura ni kama aliwahi kuiona mahali lakini hakujua yule mtu anaitwa nani. Alitaka kumuita lakini sauti haikutoka, na bila kukaribishwa yule mtu ama kiumbe akaketi katika upande mmoja wa kiti. Kisha akafanya mfano wa tabasamu….George akaduwaa.
“Haujambo mheshimiwa!!.” Hatimaye yule mgeni alimsemesha. George akashindwa kujibu akabaki kuduwaa. Mgeni wake hakujishughulisha na mshangao uliomkumba bwana George, aliendelea na shughuli zake ambazo kwa utashi wake anaamini ndizo zilimleta pale ndani, alifunua huku na kule akiwa anatafuta anachojua yeye mwenyewe hatimaye akakipata kipande cha karatasi, akaipata na kalamu. Akaandika maneno fulani katika mweandiko mbovu kabisa kisha akampatia George aweze kuangusha saini yake. George akasita, yule mtu akamuangalia kwa macho makali sana. Macho yaliyosisitiza amri. George akaweka sahihi. Yule mgeni akatabasamu, kisha akafungua matambala aliyokuwa ameyabeba. Akatoa mzigo ambao ulionekana wazi kukusudiwa kuachwa nyumbani kwa George.

George akaendelea kushangaa lakini safari hii alijikuta akiuliza, “Wewe ni nani na…na unataka nini?” yule mgeni akasita alichokuwa anafanya, akamgeukia Georgekwa macho ya utulivu kabisa. Akafanya tabasamu kisha akajitambulisha kwa ufasaha.
Jina geni kabisa masikioni mwa George, alitaka kuuliza zaidi lakini yule mtu alikuwa na mzigo mkononi akamkabidhi George.
George akapokea pasina ubishi. Yule mgeni bila kuaga alifungua mlango akaondoka zake, mara kiza kikatanda baada ya George kubaini mzigo aliokuwa ameachiwa. Kiza kilekile ambacho George hakuwahi kukiishi kamwe. Kiza kizito tena kilichotanda ukimya wa hali ya juu.
Simu yake ya mkononi iliita ndipo aliposhtuka, akapapasa kisha akabofya hovyo bila kutambua iwapo alipokea au alikuwa ameikata. Akaendelea kuuchapa usingizi, mara ikaanza kuita tena.
“Aaargh mamtu mengine bwanaa….” Alilalama huku akifanya juhudi za kufumbua macho. Akaoitazama simu zilikuwa ni namba za Isha.i Aaaargh usumbufu tena Isha, si tumeshakubaliana kuwa hatuwezi kuwa wapenzi tena au? Nishamwambia kabisa dini haziruhusu…hanidai wala simdai. Aah mi sipokei…..alizidi kughafirika George. Simu ikakatika.
Akapiga kite cha ghadhabu, mara ikaanza kuita tena. Akataka kuipokea kwa pupa na kumjibu hovyo Isha, lakini akakutana na jina la Suzi.
“He! Inamaana wanaambizana kunipigia au?” alijiuliza George…..
Sasa sipokei zote pumbavu kabisa!!! Akasema kwa sauti ya juu. Usingizi ulikuwa umekatika tayari. Akasimama wima huku akiwalaani wasichana hao kwa kuukatisha usingizi wake mtamu kupita yote aliyowahi kulala.
Alipofika sebuleni akakuta ustaarabu ukiwa umevurugwa, alishangaa kidogo na kujilaani kwa kuanza kuwa na tabia ya uzembe wa kutopanga chumba chake kama ilivyokuwa zamani. Akajilaumu zaidi kwa kumwajiri yule msichana wa kazi.
“Monicaaaa!!!! Weee mwanahizayaaa!!” aliita kwa ghadhabu. Sauti ya msichana kutoka nje ikaitika kwa ustaarabu….
Simu yake ikaita tena kutoka chumbani.
Sasa naenda kutukana mtoto wa mtu haki ya nani!!! Alisema kwa sauti ya juu yenye kutawaliwa na kitetemeshi cha hasira.
Aliifikia simu akiamini kuwa ni aidha Isha ama mwenzake Suzi.
Wakati anafika chumbani, Monica naye alikuwa amefika sebuleni akishangaa ni kitu gani bosi wake anatafuta hadi afanye vurugu kubwa kiasi kile.
Mpiga simu alikuwa ni Frida wakati huu. Hapa George akatuliza akili na kufikiri mara mbili, akaamini palikuwa na tatizo huenda tofauti kabisa na mawazo yake.
Akaipokea simu ile.
Frida badala ya kuongea alikuwa analia….kwikwi ilisikika na kuonyesha kuwa yule mtu alikuwa amezidiwa na kilio.
“Vipi? Amepokea!!! Eeeh!!” ilisikika sauti ya Isha pembeni…..George alizidi kusema ‘halooo’ bila kupata majibu. Mara ile simu ikahamia katika sikio jingine.
“Kaka George kuna tatizo huku, tafadhali njoo tupo hapa chumbani kwa Frida njoo tafadhali….”
“Tatizo? Tatizo gani?” alihoji.
Isha kutoka upande wa pili hakuwa tayari kusema tatizo ni nini akamsihi afike.
George hakukumbuka kusafisha mwili wala kinywa chake, alikwapua suruali yake kutoka katika kiambaza cha mlango, akajivika na fulana aliyovaa siku iliyopita….akashika viatu mkononi, akaanza kutimua mbio akimpita Monica akiduwaa pale sebuleni bila kumsemesha lolote hadi alipofika nje.
“We mwanamke wewe yaani unalipwa mshahara halafu naniii….ngoja nikirudi…” aliropokwa haya akiwa nje tayari.
Akaita taksi na kuamuru apelekwe Kinondoni Studio.
Upesi gari ikaondolewa, George alikuwa kimya kabisa. Baada ya nusu saa walikuwa eneo alilokuwa anahitaji kufika. Akafanya malipo upesi na kuendelea kutimua mbio kuifikia nyumba.
Hakika palikuwa na tatizo maana hata majirani walikuwa wapo katika mchanganyiko wa majonzi na hamaniko kama si mshangao.
Mungu wangu Mwanaidi!!! George alianza kuweka hisia zake kuwa mtoto wa Frida alikuwa matatani, ama la sivyo basi mama yake mzazi alikuwa matatizoni.
Jibu la kwanza lilikuwa sahihi. Mwanaidi alikuwa matatizoni. Na ingekuwa heri zaidi kama angekuwa matatizoni na anaonekana pale ili aweze kupatiwa huduma ya kuliondosha hilo tatizo. Ilishangaza kwamba mtoto Mwanaidi hakuwa mahali pale.
Mwanaidi alikuwa ametoweka katika mazingira ya kutatanisha sana. Alikuwa na miezi sita tu tangu azaliwe siku ambayo wajina wake alikuwa anaiaga dunia, sasa haonekani tena kama wajina wake.
“Nimelala saa sita na nusu, kuna tamthilia nilikuwa naangalia na mama Mwana, wakati huo Mwana alikuwa amesinzia tayari…..kwa kweli hadi sasa ni maajabu ninaamka mama Mwana ananiambia eti mtoto hayupo kitandani….” Mama mmoja ambaye alikuwa anaishi ujirani mwema na akina Frida alielezea. Mama George naye akadakia, “Na ni mimi niliyeenda kumlaza, Mama Mwana alikuwa amejikita katika tamthilia mimi nikamchukua mtoto nikamlaza kisha nikaenda kujilalia huko. Yaani mbona kazi?”
“nilimkuta mwanangu kitandani jamaniii….niliangusha kioo akashtuka na kuanza kulia jamanii….kwa mikono yangu nikambeba nikampa titi anyone, aliponyonya akanyamaza tukaanza kucheza na mwanangu jamaniii uuuuuwi…..mamaa weeeeee!! Asubuhi naamka naikuta midoli tu uwiiiii mwanangu jamaniiiii nisaidieni mimiii Mwananidi wangu weeee” Maneno ya Frida na kilio chake yakaamsha msiba wa ajabu msiba usiokuwa na maiti.
Mara Frida alipokaribia kunyamaza, vikasikika vilio vingine kutokea njea vilianza taratibu kisha vikazidi kuvuma na kufika ndani, walikuwa akina dada wawili. Isha na Suzi. Hawa walikuwa wameenda kutoa taarifa polisi juu ya tukio hilo, huko wakaambiwa hakuna taarifa yoyote juu ya mtoto kupotea.
E bwana ee!! Kuna watu hawanyamazishwi wakifungulia kilio. Isha na Suzi walikuwa wanaongoza.
Kila aliyejaribu kumtuliza kama asipoambulia tusi zito basi angeweza hata kung’atwa meno.
Frida naye akaanza kulia, mama George akafunga orodha sasa akimlilia mjukuu wake. Huyu alilia hadi akapoteza fahamu.
Ilikuwa imetimia saa tatu asubuhi.
George akaaga kuwa anatoka mara moja kuangalia kipi kinaweza kufanyika, aliongozana na Isha ambaye alikuwa amejituliza mwenyewe. Wakaingia ndani ya taksi. Safari ya kuelekea nyumbani kwa George.
George alipokumbuka juu ya wapi wanaelekea akakumbuka juu ya mpangilio mbovu aliouacha pale sebuleni. Alijiuliza iwapo Monica atakuwa ameuweka sawa ama la anaenda kuabika na wageni wake….
Kuukumbuka mpangilio ule mara George akakumbuka kuwa usiku uliopita ni yeye alikuwa wa mwisho kukaa pale sebuleni pakiwa katika mpangilio mzuri kabisa. Lakini akakumbuka kuwa kuna muda alirejea tena pale na kuna jambo alikuwa anafanya na akamwona yule mtu aliyevuruga sebule yake, hakuwa Monica alikuwa ni kiumbe mwingine kabisa. Tena alijitambulisha jina, na kuna jambo la ziada alifanya..kuna mzigo alimpa naye akaupokea…..
Ni kama kiumbe hai ….alipewa kiumbe hai. Akajaribu kuikumbuka sura yake lakini likatokea giza, hakika giza lilitokea hata kabla hajatabua sura ya kiumbe kile….
“Mungu wangu weeee!!” George alipayuka ghafla. Isha akamtazama kwa masikitiko bila kusema lolote.
George alitangulia mbele na Isha akafuata, wakaingia sebuleni. Monica alikuwa ameiweka sawa sebule na haikuonyesha dalili yoyote ya kashkash! Isha akaanza kuona mwenzake anakaribia kupandwa na wazimu, alimwona George akiishangaa sebule yake mwewnyewe.
“Ehee alikuwa hapa hivi amesimama.”
“Nani tena?” Isha aliuliza ndipo George akagutuka kumbe mambo aliyokuwa anayawaza kichwani aliyasema kwa sauti.
“Aaah hapana basi tu kwani….nani…karibu Isha.” Alijiumauma.
“Upo sawa G.” Isha aliuliza kwa sauti ya kinyonge.
“Aaah mimi?” aliuliza swali la kipumbavu bila kutarajia.
Isha akamtazama bila kusema lolote. George akasimama na kuingia ndani chumbani mwake …Isha akamsindikiza kwa macho.
Macho yaliyomsanifu kijana yule kama kwamba anaukaribisha uchizi kichwani mwake bila kujua.
“Unadhani nina tatizo basi mimi…hamna basi tu ujue…yaani..” alitokwa na maneno hayo wakati anaingia chumbani huku akirusha mikono huku na kule na tabasamu la kujilazimisha midomoni.
Isha hakutia neno akabaki kumtazama tu. Hadi alipotokomea kabisa.
Kimya kilitanda kwa sekunde kadhaa Isha akiwa anatafakari jambo lilitokea alfajiri ya siku hiyo kama mkosi ambao unawafuata kwa nyuma.
Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kutoweka katika mazingira ya kutatanisha tena akiwa mikononi mwa mama yake. Ilistaajabisha hakika.
Mara mawazo yake yalikoma baada ya kusikia purukushani ikitokea katika chumba cha George, ni kama alikuwa akipambana na mdudu ama chochote kile ambacho kilikuwa chumbani mwake kimakosa. Isha aliendelea kuzisikiliza zile purukushani za uhakika, mara kianguke hiki mara kianguke kile.
“We ni nani..unataka nini hapa eeh….Sikujui toka…” sauti ya George iliyokuwa inasota ilisikika ikihangaika. Isha akastaajabu, akavamiwa na hisia kuwa George alikuwa ameanza kuishi katika uchizi rasmi. Alifanya tabasamu la karaha kisha akajisemea ‘mzimu wa majanga unaandamana nasi bado’.
Neno lake la mwisho ‘bado’ liliambatana na kishindo kikubwa baada ya yowe kubwa kutoka chumbani kwa George. Hapa sasa hakuendelea kukaa. Akasimama wima akakimbilia chumbani kwa George.
Macho yake yakakutana na mwili wa George ukitiririkwa jasho chumba kikiwa katika hali ya utulivu sana lakini kilichovurugika sana.
George alikuwa hajitambui
Isha akapagawa, hakuamini kilichokuwa kinatokea mbele yake, ulikuwa muendelezo wa ile filamu ya alfajiri ya kutoweka mtoto wa Frida katika mazingira tatanishi na sasa ilikuwa zamu ya George kupoteza fahamu katika mazingira ya kutatanisha vilevile.
Upesi akaitwaa simu yake akampigia Suzi. Simu ikapokelewa akamwomba afanye upesi akiongoza na wanaume kadhaa wafike nyumbani kwa George.
“Vipi Mwanaidi ameonekana?” Suzi aliuliza kwa kihoro.
Isha akamsisitiza afike upesi.

****

George alikurupuka kutoka katika usingizi mzito uliozigandamiza fahamu zake na kujikuta akiwa katika kitanda cha hospitali ya Mazengo katikati ya jiji.
Alijitazama huku na kule na kujikuta amezungukwa na watu kadhaa. Pole mfululizo zikafuata baada ya kujitambua.
“George ni nani ulikuwa unajibizana naye ndani.” Isha alimuuliza wakiwa wamekaa.
“Mimi? Mimi nikajibizana na mtu.” George aliuliza huku akijielekezea kidole kifuani kwake. “Sijazungumza na mtu hata mmoja wala.” Alimalizia sentensi ile.
“Niliwaambia jamani….” Isha aliwatazama Suzi na wale vijana wengine ambao aliwaambia kuwa ana mashaka kupotea kwa mtoto Mwanaidi kunaelekea kumpa wazimu George. Suzi akainama chini na kufanya ishara ya msalaba kuombea lisitokee hilo linalodhaniwa na Isha.
Ilikuwa tafrani hakika.

Wakati haya yakiendelea huku hospitali kuna jicho lilikuwa likiyatazama yote haya huku uso wake ukitabasamu kwa matumaini makubwa sana. Alikuwa analifanikisha lengo lake taratibu lakini kwa umakini mkubwa sana….hakuna aliyejua kuwa kuna jicho linawatazama kutokea katika kona moja ya kile chumba.

George alikuwa mtulivu sana, akitafakari juu ya tukio lililotokea chumbani kwake. Alitamani sana kuwashirikisha watu waliomzunguka lakini akayakumbuka masharti yaliyotajwa na mtu yule wa ajabu…..kingine kilichomtia uzito katika jambo hili ni ile hali ya kukumbuka kuwa kile kitu alichokabidhiwa katika ile hali aliyodhani kuwa ni ndoto sasa alitambua fika kuwa alikabidhiwa mtoto mdogo ambaye alikuwa anamjua kwa sura na historia pia.
Lakini hakulitambua jina lake kwa wakati ule.

George angeweza kuelezea juu ya ndoto hiyo lakini nani angeamini kama asingetimiza masharti aliyopewa na yule mtu wa ajabu ambaye hisia zake zinakiri kuwa hapo kabla aliwahi kumuona. Alipomuona ni wapi? Hilo lilikuwa swali gumu zaidi.
Kichwa kikawaka moto zaidi ya kawaida. Huu ulikuwa mtihani mkubwa sana kuupata maishani. Yale maneno ya mwisho ya yule kiumbe ndo yalimfadhaisha zaidi, kuna jambo zito alitakiwa kuliweka bayana mbele ya jamii. Jambo ambalo George alitaka libaki siri milele.
Lakini kama angesimamia msimamo wake basi kuna shauri jingine ambalo lilikuwa zito zaidi na iwapo lisipotimizwa basi kinazuka kizaazaa kisichokuwa na mfanowe.
Ni heri yale maisha ya uchokoraa ya kulala katika vichochoro bila kupata chakula. Ni heri kukimbizana na mgambo wa jiji kuliko kukumbana na kizaazaa. Na ilikuwa heri zaidi kuishi jela miaka yote kuliko kuishi katika dunia huru inayotawaliwa na kizaazaa.
Kizaazaa kinazuliwa na George bila chokoraa wale kufahamu, lakini kinasambaa na kuwakumba wote, lakini wakati huu anaongezeka mtu mwingine matata kabisa anayeondoka kwa jina la Suleiman Meja.

****

KITABU CHA PILI CHA CHOKORAA NI (KIZAAZAA)

ram Khantwe

Mkuuu kwa hyo riwaya ya Chokoraa ndo imeishia hapo?
 
Back
Top Bottom