SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010
SEHEMU YA TISINI NA SABA
"Hahaha Daniel Mwaseba, una bahati mbaya sana. Umejiingiza mwenyewe katika mdomo wa mamba. Umekifata kifo chako hapa! Huwezi toka salama mahali hapa, tunakuuwa Daniel na tunakutoa moyo!" Don Genge alisema kwa kujigamba sana. Daniel Mwaseba hakujibu kitu, alikuwa anawaangalia tu kwa zamu watu wale watano.
"Daniel Mwaseba, mpelelezi mahiri nchini Tanzania..." Sauti kutoka kule mlangoni ilisikika. Nayo ikitaja jina la Daniel. Daniel Mwaseba alinyanyua sura yake na kumwangalia mtu aliyotoa kauli hiyo, alimtambua vizuri sana. Alikuwa ni yule jamaa aliyepambana nae kule Kimbilio lodge, yule jamaa aliyejirusha katika gari la polisi likiwa katika mwendo mkali. Mhalifu mwenye roho ngumu ya paka!
Alikuwa anaitwa Tano!
Sasa kundi zima la Six killers lilitimia. Alikuwepo Moja, Mbili, Tatu, Nne, Tano na kiongozi wao Don Genge.
Kiukweli Daniel Mwaseba alikuwa katika balaa kubwa sana!
"Hahaha eti mpelelezi mahiri nchini Tanzania, mpelelezi mahiri anaingia kichwakichwa kwenye moto namna hii. Ulikuwa unajiona makini sana Daniel Mwaseba, eti Taifa la Tanzania linakutegemea hahaha, Tano ni mahiri zaidi yako. Kwa taarifa yako alikuwa anakuona ulivyokuwa unamfata. Huwezi kumfikia Tano wewe kiakili hata siku moja. Tumekushudia jinsi ulivyojirusha toka mtini. Huna akili za kutuzidi Six killers, huna hata kidogo" Don Genge aliongea kwa kujigamba na kumsifu kijana wake Tano.
Daniel Mwaseba aliwaangalia wale watu makatili sana. Aliudhika pia na majigambo yao, lakini kimoyomoyo Daniel Mwaseba alijisemea.
'Mtajuta'
"Tummalize sahivi Bosi, tusimcheleweshe" Moja alishauri.
"Hatuwezi kumuua haraka namna hiyo Moja, lazima afe kwa mateso makali sana!" Don Genge aliyasema maneno hayo huku akiachia teke kali lililonasa vizuri katika shavu la Daniel Mwaseba. Damu ziliruka hovyo! Daniel alipata maumivu makali sana, lakini hakutaka kuonesha mbele ya maadui zake. Alijikomaza na kwa bahati nzuri Daniel Mwaseba alikuwa mwalimu katika fani ya kuvumilia maumivu....
ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA